Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 745 | 746 | (Page 747) | 748 | 749 | .... | 1896 | newer

  0 0

  Msimamizi wa Mifumo wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Ami Mohamed (kulia), akimuonyesha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kushoto), jinsi taswira ya muombaji kitambulisho inavyohifadhiwa kwenye mfumo ili kuwezesha kuiweka kwenye kitambulisho. Naibu Katibu Mkuu alikuwa kwenye ziara ya kutembelea Mamlaka hiyo mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kulia),akiuliza swali baada ya kupata maelezo kutoka kwa Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Noel Chikwindo (kushoto), Naibu Katibu Mkuu alikuwa kwenye ziara ya kutembelea Mamlaka hiyo mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (aliyenyooshamkono), akifuatilia kwaumakini uhakiki wa taarifa za muombaji wa Kitambulisho cha Utaifa, wakati alipotembelea kitengo cha Uhakiki waTaarifa cha Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Kulia ni Mkurugenzi wa Uzalishaji Vitambulisho, Paul Bwathondi .Naibu Katibu Mkuu alikuwa kwenye ziara ya kutembelea Mamlaka hiyo mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Uzalishaji Vitambulisho wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Paul Bwathondi (kulia), akitoa ufafanuzi kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (watatu kutoka kulia waliosimama), Naibu Katibu Mkuu alikuwa kwenye ziara ya kutembelea Mamlaka hiyo mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kulia), akielezea jambo wakati alipotembelea Kitengo cha kudhibiti ubora wa Vitambulisho vya Taifa, kilichopo kwenye Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA),Katikati ni Mkurugenzi wa Uzalishaji Vitambulisho, Paul Bwathondi na kushoto ni Afisa Usajili anayeshughulikia ubora, Jemima Mulokozi. Naibu Katibu Mkuu alikuwa kwenye ziara ya kutembelea Mamlaka hiyo mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam.
  Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), anayeshughulikia ubora, Jemima Mulokozi (kushoto), akimuelezea Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kushoto), jinsi wanavyothibiti ubora wa Kitambulisho cha Utaifa kabla akijachapishwa.Naibu Katibu Mkuu alikuwa kwenye ziara ya kutembelea Mamlaka hiyo mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam.( (Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizaraya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (katikati), akiongozana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dickson Mwaimu (kulia), wakati alipotembelea kituo cha kumbukumbu cha Mamlaka hiyo, mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam. Kushotoni Mkurugenzi wa Uzalishaji Vitambulisho (NIDA), Paul Bwathondi.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dickson Mwaimu (kushoto),akimuongoza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya NdaniyaNchi, Balozi Simba Yahya (kulia),kutembelea ofisi za Mamlaka hiyo zilizopo Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, mwishonimwa wiki ,jijini Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu alikuwa kwenye ziara ya kuona jinsi shughuli zaUchapaji na Uzalishaji wa Vitambulisho vya Utaifa zinavyofanyika.

  0 0

  KIKAO maalum cha Wakuu wa Nchi na Serikali na Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Uchumi na Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC Double Troika) kimeiagiza Serikali ya Lesotho iwe imetangaza matokeo ya Tume iliyoundwa kuchunguza matatizo ya kisiasa nchini humo ifikapo Februari Mosi, mwaka huu.

  Agizo hilo lililotolewa kwa Waziri Mkuu wa Lesotho, Dk. Pakalitha Mosisili katika kikao cha SADC Double Troika kilichofanyika mapema wiki hii Gaberone, Botswana, chini ya Mwenyekiti wake, Luteni Jenerali Seretse Khama Ian Khama ambaye pia ni Rais wa nchi hiyo.

  SADC Double Troika ni kikao maalum cha Wakuu wa Nchi na Serikali (SADC Summit) na wakuu wa nchi wanaounda Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama (SADC Organ on Politics, Defense and Security Cooperation) kilichofanyika kwenye kituo cha mikutano ya kimataifa (GICC), jijini Gaborone, Botswana.

  Pamoja na kutaka Lesotho itangaze matokeo ya tume hiyo, SADC Double Troika iliitaka nchi hiyo iandae mchakato wa kueleza njia za utekelezaji wa mageuzi kama yalivyopendekezwa kwenye ripoti ya tume hiyo ifikapo Agosti, mwaka huu.

  “Vilevile, nchi ya Lesotho inatakiwa kuandaa mazingira wezeshi yatakayotoa nafasi kwa viongozi wa upinzani na baadhi ya maofisa wa kijeshi wanaoishi uhamishoni ambao walikimbia machafuko, waweze kurejea nyumbani,” ilisema sehemu ya taarifa iliyotolewa na sekretariati ya SADC siku moja baada ya kikao hicho kumalizika.

  Mkutano huo wa Botswana ulihudhuriwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye alikuwa akimwakilisha Rais Dk. John Pombe Magufuli; Rais wa Botswana, Luteni Jenerali Khama; Rais wa Afrika Kusini, Bw. Jacob Zuma; Rais wa Msumbiji, Bw. Filipe Jacinto Nyusi; Waziri Mkuu wa Swaziland, Dk. Barnabas Dlamini na Waziri wa Mambo wa Nje wa Zimbabwe, Bw. Simbarashe Mumbengegwi ambaye alimwakilisha Rais Robert Mugabe wa nchi hiyo. 

  SADC Double Troika ni mkutano unaohusisha viongozi wakuu watatu wanaoongoza chombo cha ushirikiano wa siasa, ulinzi na usalama na wengine watatu kutoka kwenye Mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa SADC. Hawa wanawakilisha mwenyekiti aliyepo madarakani, mwenyekiti aliyemaliza muda wake na mwenyekiti ajaye ambaye huwa ni makamu mwenyekiti.

  Kwa mujibu wa Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Balozi Radhia Msuya, chini ya muundo wa SADC, kuna mambo makuu mawili; la kwanza likiwa ni utangamano wa kikanda ambao unasimamiwa na mkutano wa wakuu wa nchi (SADC Summit) na la pili ni la siasa, ulinzi na usalama ambalo linasimamiwa na chombo maalum (SADC Organ).

  Akifafanua zaidi, Balozi Msuya alisema wajumbe wa mkutano wa SADC Organ ni Msumbiji (Mwenyekiti); Afrika Kusini (Mwenyekiti aliyemaliza muda wake) na Tanzania inayotarajia kuchukua uenyekiti wa chombo hiki ifikapo Agosti, 2016. Botswana, Zimbabwe na Swaziland ndizo zinaundaSADC Summit.

  Mapema, kikao hicho, kilipokea taarifa ya msuluhishi wa SADC kwenye mgogoro wa Lesotho ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Afrika Kusini, Dk. Cyril Ramaphosa ambayo iliainisha mambo kadhaa yakiwemo ya kikatiba na kiusalama ndani ya nchi hiyo.

  Dk. Ramaphosa alitakiwa kuhakikisha kuwa mgogoro huo uliovihusisha vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi ya Lesotho, unatatuliwa kwa njia ya mazungumzo kati ya wadau husika ili kuhakikisha kuwa nchi hiyo inarudi kwenye hali ya amani – kisiasa na kiusalama.

  Mgogoro wa Lesotho umehusisha kuuawa kwa aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ya Lesotho, Luteni. Jenerali Maaparankoe Mahao, mnamo Juni 25, 2015. Pia baadhi ya wananchi wanadaiwa kutiwa vizuizini na wengine kuwekwa ndani.

  0 0


  0 0

  DSC07284-2
  Mwenyekiti wa Taasisi wa MO Dewji, Mohammed Dewji
  Na Modewjiblog team

  Mwenyekiti wa Taasisi wa MO Dewji, Mohammed Dewji kwa kushirikiana na kampuni ya Darecha Limited leo (jumatatu) wamezindua shindano la Mo Mjasiriamali lenye lengo la kusaidia kukuza ujasiriamali miongoni mwa vijana.

  Shindano ya Mo Mjasiriamali litatoa fursa ya ukuzaji wa mitaji, ulezi wa wajasiriamali na mitandao ya biashara kuongeza mwanga, ujasiri na kuzalisha wajasiriamali Tanzania.“Mimi kama Mjasiriamali kijana na mzaliwa wa Singida vijijini, sikufikiria hata mara moja kama leo ningekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa moja ya makampuni yaliyofanikiwa sana katika nchi yetu na hata barani Afrika.” Inasema taarifa Mkurugenzi Mtendaji huyo wa MeTL kwa vyombo vya habari mwishoni mwa wiki.

  Aidha alisema Afrika ni moja ya bara linalokua kwa haraka na lenye ukuaji imara wa uchumi na amini vijana wa Tanzania wana nafasi kubwa ya kutumia fursa hizo ili kujiletea uchumi endelevu.

  Lakini pamoja na ukweli huo changamoto kama za ukosefu wa mitaji, ukuzaji ujasiriamali na mitandao ya biashara zimekatisha tamaa vijana wengi kukuza kwa mafanikio makampuni yao hapa Tanzania na hivyo kupunguza kasi ya ukuaji wa uchumi kwa watu wa kipato cha kati.
  Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Benki ya maendeleo ya Afrika (ADB), watu wenye kipato cha kati katika bara la Afrika wataongezeka na kufikia watu bilioni 1.1 ifikapo mwaka 2060.

  Watu wa kipato cha kati ndio wanaochagiza ukuaji wa uchumi kutokana na mahitaji yao na pia ari ya ujasirimali.Pamoja na ukweli huo kunachangamoto nyingi zinawakabili watu hao wa kipato cha kati. Mathalani nchini Tanzania changamoto kubwa kwa vijana wajasirimali ni gharama za kutafuta mtaji kwa kazi hizo.

  “Kuna haja kubwa ya kuhakikisha kwamba vijana hawa wanaondolewa tatizo la ujasirimali ili waweze kusukuma mbele uchumi wa Tanzania.” inafafanua taarifa hiyo.

  Aidha kwa kuwa Tanzania inaelezwa kuwa ni nchi ya 19 katika bara la Afrika kuhusiana na fursa na ujasirimali ipo haja ya kusaidia ili kuiondoa katika nafasi hiyo. Taarifa ya nafasi ya Tanzania imo katika ripoti yake ya mwaka 2014 ya Africa Prosperity Report.

  Taarifa ilifafanua zaidi kwamba kutokana na haja hiyo Taasisi ya Mo Dewji na Darecha Limited wameungana pamoja na kuanzisha shindano la Mo Entrepreneurs ili kutambua na kuuenzi mchango wa wajasirimali chipukizi na kufanikisha ndoto zao.

  Ili kufanikisha nia ya kuwa na wajasiriamali wengi, shindano hilo linatarajiwa kuwa daraja kwenda kwa Mkurugenzi Mtendaji, Mohammed Dewji (MeTL Group na Mwenyekiti wa Mo Dewji Foundation) ambapo vijana ambao wanaonekana wana kitu cha kufanya, lakini hawana msaada watashiriki kwa lengo la kupata msaada katika mfumo wa mtaji, mtandao na usimamizi wa ukuaji wa shughuli wanayofanya au kutaka kuifanya ili kuianzisha na kuikuza.

  Mambo hayo yatatekelezwa katika mfumo wa shindano litakalogusa wajasiriamali ambao wana ari na nia ya dhati ya kuendeleza shughuli walizofikiria na kuzianzisha kwa lengo la kuinua uchumi wao binafsi na wa taifa.

  Washindi watatu watakaotangazwa Aprili mwaka huu watapatiwa mtaji wa kuanzia au kuendeleza, pia watapatiwa maarifa ya kuendeleza shughuli zao na kuanzishwa mtandao wa kibiashara na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa MeTL Group na mwenyekiti wa Mo Dewji Foundation, Mohammed Dewji.

  Wakati akipewa tuzo ya Forbes ya mwaka 2015, Mohammed Dewji aliitoa kwa heshima ya vijana akiwatakia kila la heri waking’aa, kuvunja nira ya woga, kukabili changamoto na kuendelea katika ujasiriamali kwa lengo la kufanya dunia yetu mahali bora pa kuishi.

  0 0

  Mshindi wa Ubunifu mitindo Jocktan Cosmas Maluli A.k.a Makeke(aliyeshika cheti) akiwa katika picha ya pamoja na waratibu wa shindano hilo kuanzia kushoto ni Zamda George, Comfort Badaru, Martin Kadinda, Reuben Nabora na Stanley Kamana. 
  Mshindi wa kipengele cha The Best Photographer, Daniel Msirikale (mwenye miwani) akipokea tuzo yake. 
  Mlezi wa FASDO, Reuben Nabora akitoa salamu kutoka kwa mwasisi wa FASDO, Lilian Nabora aliyeko Ubelgiji.
  Mratibu wa FASDO nchini, Joyce Msigwa akitoa muhtasari wa shindano la Bongo Style.
  Mshereheshaji, Mario Mpingirwa akifafanua jambo. 
  Mtumbuizaji wa ngoma za asili akionesha uwezo wake wa kuchezea nyoka. 
  Baadhi ya viongozi wa wa FASDO wakifuatilia shindano hilo. 
  Majaji wa ubunifu mitindo wakitathmini kazi za washiriki wao. 


  Majaji wa upande wa wapiga picha wakitazama kazi za washiriki wao. 


  Mshindi wa ubunifu mitindo, Jocktan Maluli 

  akiwa katika picha ya pamoja na wanamitindo wanaoonesha mavazi yake.  Wanamitindo wakionesha mavazi yaliyobuniwa na washiriki.  Washiriki wa ubunifu wa mitindo wakitambulishwa mbele za watazamaji.   Mkurugenzi Mtendaji wa Entango, Emma Kawawa akitoa salamu zake na kuendesha harambee kwa ajili ya FASDO.  Mkurugenzi Mtendaji wa FASDO, Chande akizungumza jambo.   Mwenyekiti wa FASDO, Stanley Kamana akiongea jambo.   Mshindi wa kipengele cha Best Personality of The Year, Shahbaaz S. Yusuf akipokea tuzo kutoka kwa mlezi wa FASDO, Reuben Nabora.  Mshindi wa Peoples Choice Awards for Fashion Designer, Winfrida Touwa akipokea tuzo yake.
  Mshindi wa Peoples Choice Awards for Photograph, Rasheed Hamis akipokea tuzo.   Msanii Alvin Dullah 'DY' akitumbuiza baadhi ya nyimbo zake.
  Baadhi ya washiriki wakichukua vyeti vya ushiriki wa shindano hilo.  Baadhi ya watu wakijifotoa.  Baadhi ya wadau wakiongozwa na Mzee Nabora wakizitazama picha za washiriki.


  Umati wa watu waliohudhuria fainali hizo wakifutatilia shindano hilo kwa umakini.

  (Picha na Fredy Njeje) 


  WASHIRIKI wa shindano la Bongo Style linaloratibiwa na asasi isiyo ya kiserikali ya FASDO, Jocktan Cosmas Maluli (25) na Daniel Msirikale (24) wameibuka kidedea kwa kujinyakulia tuzo za shindano hilo katika fainali iliyofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar.


  Shindano hilo lililoanzishwa mtandaoni mwezi Septemba mwaka 2015, lilijumuisha washiriki wapatao mia tatu wenye vipaji vya upigaji picha na ubunifu wa mitindo huku washiriki kumi pekee wakiingia kwenye fainali baada ya michujo mbalimbali kabla ya washiriki hao wawili wakishinda tuzo hizo.


  Washiriki hao walishinda kutokana na kura za majaji waliobobea katika fani hizo ambapo kwa upande wa picha majaji hao walikuwa ni: Sameer Kermalli, Hanif Abdulrasul, Idd John na Angela Kilusungu huku kwenye ubunifu wa mavazi majaji hao wakiwa ni: Martin Kadinda, Rio Paul, Zamda George na Comfort Badaru.


  Jocktan Maluli ambaye ameshinda katika kipengele cha Best Fashion Designer 2015 na Daniel Msirikale aliyeshinda katika kipengele cha Best Photographer 2015, wote pamoja wamepokea kitita cha dola 500 kila mmoja huku wakipata nafasi ya kwenda nchini Ubelgiji kwa ajili ya kuonesha ubunifu wao katika maonesho ya Africa Firm Festival Belgium kuonesha kazi zao pamoja na washiriki 18 walioshiriki shindano hilo, yatakayofanyika hivi karibuni nchini humo.


  Aidha washindi wa vipengele vingine ni: Shahbaaz Yusuf aliyeshinda kipengele cha Best Personality of the Year 2015, Winfrida Touwa aliyeshinda katika kipengele cha Peoples Choice Award for Fashion Designers na Rasheed Rasheed aliyeshinda kipengele cha Peoples Choice Awards for Photograph.


  Fainali hizo zilizohudhuriwa na wageni waalikwa na wadau mbalimbali wa kazi za sanaa na kupambwa na burudani mbalimbali kama vile nyimbo za asili, muziki na maonesho ya mavazi na kazi za sanaa kutoka kwa washiriki hao.


  0 0

  Vero Ignatus - Moshi Kilimanjaro.

  Chama cha Karate Mkoa wa Kilimanjaro wanaiomba serikali kutupia macho kwenye mchezo huo kwani imekuwa ikiwasahau ukizingatia mchezo huo ni michezo kama ulivyo mingine na kwamba mchezo huo umekuwa ukifundishwa pia katika majeshi mbalimbali hapa nchini. Hayo yamesemwa nakapteni wa timu na katibu msaidizi wa chama cha Katrate mkoa wa Kilimanjaro bwana Wembo Hamisi katika viwanja vya mazowezi mkoani hapo na amekusema kuwa wamekuwa wakikwama mara wanapohitajika kwenye mechi za kirafiki,ndani na nje ya nchi kwasababu hawana sapoti kutoka serikalini na wafadhili. 

   Aidha amesema kuwa Karate ni mchezo ambao mtu yeyote anaweza kuucheza na akatengeneza afya ya mwili,na mchezo huo ni wa kawaida kama ilivyo michezo mingine kama mpira wa miguu amewataka watu wote kujitokeza kwa wingi kujiunga katika mchezo huo wa Karate kwa sifa kuu ya karate ni nidhamu. Sambamba na hayo bwana Wembo amesema kuwa katika mchezo huo wapo wanawake na ameiomba jamii waondokane na ile dhana potofu kwamba mwanamke akicheza mchezo huo wa Karate hawezi kupata mtoto na kufanya shughuli nyingine za kijamii amesema huo ni upotoshaji kwani mwanamke anao uwezo wa kupata mtoto kama walivyo wengine na anatengeneza afaya nzuri kabisa. 

  Aidha amesesema kuwa mchezo huo wa Karate kwa historia umeanzishwa miaka mingi kwa mkoa wa Kilimanjaro chama cha karate kina takribani miaka saba sasa tangia kuanzishwa kwa chama hicho,na baadae wakaunda shirikisho la Karate nchini Tanzania ambapo inajumuisha michezo yote ya karate ,ambapo januari 30 watakuwa na tamasha la Karate la kuwatambulisha wachezaji wa timu litakalofanyika mkoani hapo katika ukumbi wa shule ya msingi Mwenge. 

  Katibu huyo ameinisha ratiba yao ndani ya miezi sita ambapo watafanya matamasha mbalimbali ikwemo februari 13/2016 watafanya tamasha wilayani Same katika ukumbi wa kimweli same mjini, machi 24-26, mashindano ya mchezo wa GOJUKAI KARATE ya Afrika Mashariki, Kampala Uganda , aprili 30 mashindano ya GOJUKAI Karate ya wazi ya kuuenzi mlima Kilimanjaro ambapo watashiriki watoto wenye umri wa kati na watu wazima yatafanyika Moshi.

  Mwisho ni Tamasha la shukrani litakalofanyika mei 16 hapo hapo Moshi Kilimanjaro. Kwa mkoa wa Kilimanjaro mchezo wa karate unaochezwa unajulikana kama Gojukai Stayle, ambayo ilianzishwa kutoka nchini Japan,na chama katika mkoa huo kinaundwa na vilabu mbalimbali ambavyo klabu mama ni Ralway club, Pasua Club, Mwenge Club, Ccp Club,Rau Club,na vilabu vingine vinaundwa na wanafunzi mbalimbali ambapo kila club ina zaidi ya wanafunzi 20-30.hivyo wanawaomba ,Taasisi mbalimbali ,wafanyabiashara,makampuni mbalimbali hata watu binafsi kujitokeza kuudhamini mchezo huo wa Karate.

  0 0

  Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania ,Anthony Mtaka akiwa na Mwe3nye3kiti wa Chama cha riadha mkoa wa Kilimanjaro,( KAA) Liston Methacha wakati wa uzinduzi rasmi wa mbio za Dodoma Hapa Kazi tu Half Marathoni 2016 zinzotarajia kufanyika January 30 mwaka huu mjini Dodoma. 
  Baadhi ya wadau wa Riadha wakifuatiia mkutano wa uzinduzi wa Mbio za Dodoma Hapa kazi tu Half Marathon 2016 uliofanyika katika Hotel ya Nyumbani mjini Moshi. 
  Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka akizungumza na wanahabari (hawako pichani ) wakati wa uzinduzi rasmi wa Mbio hizo. 
  Kocha wa timu ya taifa ya Riadha ,Francis John akiwa na wanariadha ,Alphonce Felix na Said Makula waliofuzu viwango vya kushiriki mashindano ya Olyipiki ,walipotamburishwa mbele ya wanahabari . 
  Raisi wa RT ,Mtaka kifanya mahojiano na Mwandishi wa habari ,Enos Masanja wa Azam TV.

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.


  SHIRIKISHO la Riadha Tanzania(RT) limeandaa mbio fupi kwa ajili ya kuhitimisha siku 100 za rais Dk.John Pombe Magufuli kuwa Ikulu zitakazotimua vumbi jumamosi hii januari 30 mwaka huu mjini Dodoma.

  Mbio hizo zimepewa jina maalumu la Dodoma ‘hapa kazi tu’ Half Marathon ambazo zitashirikisha washiriki mbali mbali wakiwamo waheshimiwa wabunge,mawaziri,wanafunzi,walemavu na wanariadha wakongwe nchini.

  Akizindua mbio hizo mjini Moshi mwishoni mwa wiki zinazodhaminiwa na Kampuni ya JSM,Rais wa shirikisho hilo,Anthony Mtaka alisema kuwa lengo la kuanzishwa kwa mbio hizo ambazo zimeandaliwa na kuendeshwa na shirikisho hilo ni kufufua michezo hapa nchini.

  Pia alisema mbio hizo zitatumika kwa ajili ya kumpongeza Rais Dk.John Pombe Magufuli kutimiza siku 100 tangu aingie maradakani ambazo zitakuwa februari 14 mwaka huu.Kwa mujibu wa rais huyo wa RT,mbio hizo zimegawanywa katika makundi matatu ambako mbio za kwanza ni za kilomita 2.5 ambazo zitashirikisha wabunge,mawaziri,walemavu,wanafunzi ,wazee na watu mbalimbali.

  Mbio za kilomita 5 ambazo ni za kujifurahisha zitashirikisha wakimbiaji wote na mbio za nusu marathon ambazo zitakuwa ni mbio za ushindani washindi watapata zawadi .Akitangaza zawadi kwa washindi,Mtaka alisema mshindi wa kwanza kwa upande wa wanaumme na 

  wanawake atapata zawadi ya piki piki yenye thamani ya sh,Milioni 2.8,mshindi wa pili akipata bati 100,wa tatu bati 40,mshindi wa nne akipata sh,200,000 huku mshindi wa tano akiondoka nash,100,000.

  Mshindi wa sita hadi wa kumi watapata kifuta jasho cha sh,50,000 kila mmoja huku waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa ndiye atayakuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mbio hizo na atashiriki mbio za kilomita 2.5.

  Wanafunzi waatakaopenda kushiriki mbio hizo watasajiliwa kwa sh,500,huku vwasio wanafunzi wakisajiliwa kwa sh,1,000 na wingine ambao hawakutajwa ni kundi gani wakisajiliwa kwa sh,5,000 na fedha hizo kwa mujibu wa Mtaka zitasaidia kambi ya wanariadha watakaoshiriki michuano ya Olimpiki.

  Uzinduzi huo pia ulitumika kuwatambulisha wanariadha wawili ambao wamekidhi vigezo vya kushiriki michuano ya Olimpiki itakayofanyika nchini Brazil mapema mwezi Agosti mwaka huu ambako nchi zaidi ya 216 kutoka kila kona ya dunia zitashiriki.

  Wanariadha hao ni Alphonce Felix ambaye ana wastani wa muda wa kukimbia wa saa 2:12.01 na Said Makula ambaye muda wake wa kukimbia ni saa 2:13.27 na watatumia mbio hizo mjini Dodoma kama majaribio yao ya kitaifa kati ya majaribio sita ya kitaifa kabla ya kwenda Brazil.

  Julai 6 mwaka jana,Felix alishiriki mbio za Gold Coast Marathon nchini Australia na kumaliza nafasi ya sita huku Makula akishiriki mbio za Casablanca Marathon oktoba 25 mwaka jana na kumaliza katika nafasi ya nne.   0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  OFISI YA MAKAMU WA RAIS
  TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUIMARISHA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA BARAZA LA TAIFA LA HIFADHI NA  USIMAMIZI WA MAZINGIRA-NEMC


   Katika kikao kilichoitishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (Mb), tarehe 24 Januari 2016, mjini Dodoma kuhusu kuimarisha utendaji  ndani ya Baraza la Taifa la Hifadhi na  Usimamizi wa Mazingira-NEMC maamuzi yaliyofikiwa  ni kama ifuatavyo:

   1.     Kuhusu suala la kiwanda cha kusindika minofu ya punda Mkoani Dodoma, imegundulika kulikuwa na ukiukwaji  mkubwa, wa makusudi na wa wazi wa miiko ya kazi  kwa watumishi  wa NEMC  walioshughulika  na kiwanda hicho. Hivyo, Mhe. Makamba ameagiza  watumishi wa NEMC wafuatao wasimamishwe kazi mara moja:

  a.     Dkt. Eladius Makene -Afisa Mazingira Mwandamizi,  

  b.     Wakili  Heche Suguta Manchare - Mwanasheria  Daraja la  II

  c.      Mhandisi Boniface Benedict  Kyaruzi, Afisa Mazingira

  Hatua nyingine za kinidhamu na kisheria zitafuatia.

   2.     Vilevile, imebainika kwamba usimamizi wa watumishi wa NEMC siyo makini na thabiti na kusababisha malalamiko mengi kuhusu utendaji wa Baraza. Hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Mhandisi Bonaventura Baya apewe barua ya onyo kali la mwisho kwa udhaifu  katika usimamizi wa watumishi wa Baraza.


  3.     NEMC kama chombo muhimu nchini kilichopewa jukumu la kusimamia utekelezaji wa Sheria ya  Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira inatarajiwa kazi zake zifanyike kwa ufanisi wa kiwango cha juu kulingana na majukumu yaliyoko kwa mujibu wa Sheria. Hivyo, kwa mapungufu yanayojitokeza  Mhe.  Makamba, ndani ya wiki moja ataunda jopo la wataalamu wasiozidi watano ili kutathmini utendaji wa NEMC na changamoto mbali mbali katika usimamizi wa hifadhi ya mazingira na kuishauri Serikali ipasavyo.


  4.      Ili kuimarisha ufanisi na udhibiti wa utendaji wa NEMC, ndani ya wiki moja  litatolewa Tangazo litakalokuwa na mambo yafuatayo: Anwani ya barua pepe (email), Nukushi (fax), Namba ya simu, Namba ya Whatsapp ili mtu yeyote mwenye malalamiko au aliyewahi kuombwa rushwa ama chochote na watumishi wa NEMC ambacho ni kinyume na  maadili ya kazi yao atoe taarifa mara moja ili uchunguzi ufanyike na hatua zichukuliwe.


  5.     Kutokana na mapungufu yanayojitokeza katika utekelezaji wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira, ndani ya wiki moja,  NEMC ipitie upya orodha  ya wataalamu na taasisi elekezi zilizosajiliwa na kufuta wataalamu na taasisi zote ambazo zimekuwa zikikiuka maadili ya kazi zao likiwemo suala la kuwasilisha taarifa zilizo chini ya viwango, kuchelewesha kazi za wateja wao na kutowasiliana na wateja wao kuhusu hatua za utekelezaji wa maombi yao.


  6.     Ndani ya wiki tatu uitishwe mkutano wa dharura wa Bodi ya NEMC kujadili na kufanya maamuzi juu ya changamoto za utendaji katika Baraza.


  IMETOLEWA NA:

  OFISI YA MAKAMU WA RAIS

  08.01.2016

  0 0   Mhandisi George Sambali.


   WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Profesa Makame Mbarawa amemteua aliyekuwa Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Mhandisi George Sambali kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kufuatia kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo,  Mhandisi Suleiman S. Suleiman. 

  Mhandisi Suleiman alifariki dunia tarehe 18 Januari, 2016 wakati akipelekwa katika hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam baada ya kuishiwa nguvu ghafla akiwa  katika  mazoezi ya kuogelea katika eneo la  Feri, jijini Dar es Salaam.

  Akitangaza uteuzi huo kwa niaba ya Waziri  Mbarawa mbele ya Menejimenti ya TAA Jumatano tarehe 20 Januari, 2016 katika Ofisi za Makao Makuu ya Mamlaka hiyo kwa niaba ya Mh. Waziri,  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Sekta ya Uchukuzi,  Dkt. Leonard Chamuliho,alisema uteuzi wa Mhandisi Sambali umeanza rasmi tarehe 20 Januari, 2016.

  Mhandisi George Sambali alizaliwa mwaka 1965, mkoani Tabora na ana shahada ya Uzamili ya Sayansi Uhandisi Uchukuzi na Barabara (MSc. Transportation (Transport & Road) Engineering, aliyoipata mwaka 1999- 2001 nchini Uholanzi.

  Mhandisi Sambali alihitimu shahada ya Kwanza ya Sayansi ya Uhandisi Ujenzi  (BSc.Civil Engineering) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwaka 1995 .

  Mhandisi Sambali pia amepata mafunzo na kozi mbalimbali za masuala ya anga kutoka katika  vyuo vya hapa nchini na nje ya nchi, ikiwemo  Stashahada ya Uongozi wa Viwanja vya Ndege (Certificate in Airport Executive Leadership) mwaka 2014 huko Montreal, Canada.

  Pia mwaka 2015 alitunukiwa Stashahada ya Wataalamu wa Kimataifa wa Viwanja vya ndege (Post-Graduate Diploma in International Airports Professionals (AIP) chini ya AMPAP nchini Canada.Mhandisi Sambali aliajiriwa na TAA mwaka 2001 kama Meneja Mipango, Usanifu na Uthamini (Manager Design, Planning and Evaluation) na mwaka 2012 aliteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uhandisi na Ufundi.

   Mwaka 2013, Mhandisi Sambali aliteuliwa kuwa Mshauri Maalum wa Mkurugenzi Mkuu kabla ya mwishoni mwa mwaka jana kuteuliwa tena kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha  Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).

  Mhandisi Sambali ni mwanachama kwenye vyama mbalimbali vya kitaaluma kikiwemo cha Wataalamu wa Kimataifa wa Viwanja vya Ndege chini ya Baraza la  Viwanja vya Ndege Duniani (ACI) na Shirika  la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO).

  Pia Mhandisi Sambali ni Mjumbe wa Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET); Mjumbe katika Jukwaa la Kimataifa la Uendeshaji wa Uchukuzi Vijijini (IFRTD); na Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB).

  IMETOLEWA NA KITENGO CHA SHERIA NA UHUSIANO –TAA Januari 25, 2016

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali Mstaafu, Issa Machibya Katikati akichimba mtaro kwa ajili ya kupitisha maji katika shule ya msingi Muungano iliyopo Mwanga mkoani Kigoma, anayechimba naye mtaro ni Diwani wa Mwanga Kusini (CCM), Mussa Maulid akishiriki katika uboreshaji huo wa miundombinu ya shule hiyo, hivi sasa mkoa wa Kigoma una mvua nyingi.
  Diwani wa Kata ya Mwanga Kusini, Mussa Maulid (mwenye suti ya michezo)akishiriki kuweka mazingira safi katika shule ya msingi Muungano iliyoko Mwanga mkoani Kigoma sambamba na wanafunzi wa shule hiyo.

  0 0

  Katapila likizikanyagakanyaga kwa lengo la kuziharibu bidhaa mbalimbali zikiwemo pampasi na dawa za meno zilizopitwa na wakati na zingine zisizo na ubora katika Dampo la Pugu Kinyamwezi, Dar es Salaam. Bidhaa hizo zenye thamani ya sh. mil. 20, kutoka Marekani na China zilikamatwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), katika Bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG).
  Na Charity James

  SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS), limeteketeza bidhaa hafifu na zilizokwisha muda wake zenye thamani ya sh. milioni 20 kutoka nchini Marekani na China.

  Akizungumza wakati wa uteketezaji wa bidhaa hizo,Dar es Salaam jana, Ofisa habari wa TBS, Roida Andusamile alizitaja bidhaa hizo kuwa ni dawa za meno, pampas, sabuni za kuogea na wipes.

  Alisema miongoni mwa bidhaa hizo zilikuwa ni kwaajili ya kutoa msaada katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime mkoani Mara huku nyingine zikiingizwa kwaajili ya biashara."Kazi ya kuteketeza bidhaa zenye ubora hafifu ni endelevu lengo letu ni kuhakikisha tunaepusha madhara kwa watumiaji ambao wanashindwa kutambua bidhaa hafifu," alisema.

  Alisema bidhaa zote zinazoingia nchini ziwe za biashara au misaada ni lazima zipimwe kwa lengo la kuondoa changamoto ya kuwauzia au kugawa zikiwa ni hafifu au kuisha muda wake.Kwa upande wake, Ofisa Mdhibiti Ubora wa TBS, Salome Emmanuel alitoa mwito kwa wafanyabiashara kuakikisha wanaingiza bidhaa zenye ubora na kuongeza wafanyabiashara ndio walinzi tosha wa kuhakikisha bidhaa hafifu haziingizwi nchini hivyo ni vizuri wakafuata sheria kukwepa tatizo hilo.


  0 0

  Na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
  KAMPUNI ya simu za mkononi ya Halotel ndio mtandao pekee unaotoa huduma za mawasiliano kwa njia ya Simu za mkononi katika kata ya Namayuni iliyopo Kilwa Masoko Mkoani Lindi.

  Mtandao huu ndio unawasaidia wakazi wa kata ya Namayuni kuweza kuwasiliana na ndugu na jamaa  wa maeneo hayo na sehemu nyingine kwa njia ya simu ya mkononi kwa kuwa wamejengewa mnara unao wawezesha kuwasiliana kwa njia simu za mkononi.

   Diwani wa Kata ya Namayuni iliyopo Kilwa Masoko Mkoani Lindi, Hussein Sungura amepongeza mtandao wa simu za mkononi wa Halotel na kusema kuwa umeisaidia sana jamii ya wakazi wa kata ya Namayuni mkoani humo kutokana na hapo awali kutokuwepo na mtandao wowote wa simu.

  " Tunawashukuru sana Kampuni ya simu za mkononi ya Halotel kukumbuka kama kunaviumbe huku na kutuwekea mnara katika kata yetu kwakua kabla ya mtandao huu tulisafiri na kupanda juu ya vilima ili kutafuta mtandao(network) ili tuweze kuwasiliana na watu wengine kwa njia ya simu."

  Nao wakazi wa Kijiji cha Namayuni wamesema kuwa Mtandao huu wa Halotel "umetusaidi sana katika huduma mbalimbali hasa kutufichia siri katika mawasiliano kwani tulikuwa tunaenda umbali mrefu kwenda kutafuta mtandao, kwa sasa tunakaa ndani tuu na tunawasiliana na ndugu na jamaa  bila mtu yoyote kujua kama tumewasilana na nani".

  Wafanyakazi wa mtandao wa Halotel wametembelea kata  ya Namayuni kwaajili ya Kampeni ya HALO MAISHA inayoendelea katika maeneo mbalimbali  yaliyofikiwa na mtandao huo nchi zima ili kila jamii ifaidike na spidi kubwa ya intaneti na upatikanaji wa huduma nzuri za mtandao huo.
   Wanafunzi wakisoma kupitia Kompyuta zilizounganishwa na intaneti ya spidi kubwa walizopewa  na kampuni ya Simu za mkononi ya Halotel katika shule ya sekondari ya Lugoba iliyopo Msata- Bagamoyo Mkoani Pwani.
  Mtaalamu wa masuala ya mtandao  wa kampuni ya Halotel, Kilwa Masoko Mkoani Lindi, Sebastian Inocent akifafanua changamoto mbalimbali zinazo wapata wakazi wa kijiji cha Namayuni.

  Afisa habari wa kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Halotel, Frank Mwakyoma akizungumza na wananchi wa kijiji cha Namayuni kilichopo kata ya Namayuni Kilwa Masoko Mkoani lindi mara baada ya wafanyakazi wa kampuni hiyo kuwatembelea katika kijijini hapo.

   Wakazi wa Kijiji cha Namayuni wakipata maelekezo walipo tembelea kibanda cha kusajili laini jijini  hapo.

   Kijana akipiga simu kwa ndugu na jamaa wakiwa kijijini hapo.

  Baadhi ya waandishi wa habari.
   Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Lugoba iliyopo Msata mkoani Pwani, Abdala Sakasa akizungumza wakati wafanyakazi wa kampuni ya Simu za Mkononi ya Halotel walipotembea katika shule hiyo kujionea jinsi wanafunzi wanavyotumia Kompyuta zilizounganishwa na intaneti yenye spidi ya kazi ili kusaidia wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Lugoba hasa wa kidato cha tano na cha sita kwa kusoma na kuongeza uwezo wao katika masoma kutokana na  wanafunzi hao kukosa baadhi ya vitabu. Wanafunzi wa shule hiyo wamefurahia uwepo wa mtandao wa Halotel kwani ndio mtandao pekee uliochelewa kufika hapa nchini na kuweza kutoa kompyuta 19 zilizounganishwa na intaneti katika shule hiyo.
  Mwalimu wa somo la Kompyuta na maswala ya mawasiliano(ICT), Emmanuel Mhizi akifafanua jambo mbele ya wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Halotel walipotembelea shuleni hapo mkoani Pwani. Mwalimu wa  Kulia ni Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya  Lugoba, Benjamini Nyamatwema.

  Mhizi amesema kuwa wanachangamoto kubwa katika kupanga zamu za wanafunzi wa shule hiyo kwani shule hiyo inawanafunzi 1391 na kompyuta zenye intaneti ni  19 tuu, kwa mujibu wa ratiba ya wanafunzi kuingia kwenye chumba hicho wanaingia wanafunzi 30 kwa kila kipindi ili kila mwanafunzi aweze kuingia katika chumba cha kompyuta.
  Wanafunzi wakiwa katika Darasa la kompyuta ambalo Kampuni ya Halotel walijitolea kwa kuwapa kompyuta hizo pamoja na kuwaunganishia Intaneti  spidi kubwa ya bure kwa miaka mitatu mfurulizo iki kuweza kuwasaidia wanafunzi hao katika kujisomea machapisho mbalimbali yaliyopo kwenye mitandao mbalimbali.
  Mwalimu wa somo la Kompyuta na maswala ya mawasiliano(ICT), Emmanuel Mhizi akiwakagua wanafunzi kwa uangalifu katika darasa hilo. 
  Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Lugoba akiendelea kujisomea somo alilolifungua  walipotembelewa na wafanyakazi wa Kampuni ya Halotel mkoani humo.
   Walimu wa Shule ya Sekondari ya Lugoba iliyopo Msata- Bagamoyo Mkoani Pwani wakijadiliana jambo wakati wanatembea.
   Diwani wa Kata ya Namayuni iliyopo Kilwa Masoko Mkoani Lindi, Hussein Sungura akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wakazi wa kijiji cha Namayuni mkoani humo walipotembelewa na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Halotel ambayo ndio mtandao pekee uliowafikia wananchi na wakazi wa kata hiyo. 
  Wakazi wa kata ya Namayuni na wanakijiji cha Namanyuni wakimsikiliza Diwani wa Kata ya Namayuni iliyopo Kilwa Masoko Mkoani Lindi, Hussein Sungura mara baada ya kutemelewa na wafanyakazi wa kampuni ya Simu za Mkononi yz Halotel mkoani humo.

  Mkazi wa Kijiji cha Namayuni akizungumza na simu wakati amekaa akitumia mtandao wa simu wa Halotel akiwasiliana na mtu aliyepo Zanzibar bila kwenda kupanda kwenye kilima kama zamani.
  Aidha mzee huyo alielezea furaha yake kwa ujio wa mtandao wa Halotel unavyowasaidia na kuwafichia siri zao, kwani mwanzoni kila mtu alijua kuwa ndio anaenda kuongea na simu na mpaka kusababisha kuaga na kwenda umbali furani kwaajili ya kutafuta netiweki ili aweze kuzungumza na mtu ambaye anamtafuta.
   Mwenyekiti wa Kijini cha Namayuni, Ally Mtumbwe akizungumza na waandishi wa habari Kilwa Masoko Mkoani Lindi kata ya ya Namayuni kijijini cha namayuni mara baada ya wafanyakazi wa mtandao wa Halotel kutembelea kijijini hapo. 
   Mkazi wa Kijiji cha Namayuni akielezea jinsi mtandao huo ulivyorahisisha biashara kutokana na kujengewa mtandao wa Halotel amesema kuwa mtandao huo umewasaidia kwa kuagiza bidhaa anazozihitaji ukitofautisha na zamani ambapo ilibidi kuzifuata hata kama hajui kama bidhaa anayoitaka ipo au haipo, hata hivyo amesema kuwa Halotel imewasaidia kuokoa muda sana.
   Mkazi wa kijiji cha Namayuni akiuliza swali kuhusiana na mtandao huo kuhusiana na kama unaweza kutuma pesa  au kupokea pesa.
  Watoto wa Kijijini cha Namayuni wakipata picha na mwandishi wa gazeti la The Citizen kijijini hapo.
   Afisa masoko wa kampuni ya Halotel , Charle anayepiga picha kwa simu akiwa na baadhi ya waandishi wa habari katika kijini cha Namayuni, Klwa Masoko mkoani Lindi.


  Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

  0 0

  TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUIMARISHA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA BARAZA LA TAIFA LA HIFADHI NA USIMAMIZI WA MAZINGIRA-NEMC

  Katika kikao kilichoitishwa na Mhe. January Makamba (Mb), Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira tarehe 24 January 2016, kuhusu kuimarisha utendaji ndani ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira-NEMC maamuzi yaliyofikiwa ni kama ifuatavyo:

  1. Kuhusu suala la kiwanda cha kusindika minofu ya punda mkoani Dodoma, imegundulika kulikuwa na ukiukwaji mkubwa, wa makusudi na wa wazi wa miiko ya kazi kwa watumishi wa NEMC walioshughulika na kiwanda hicho. Hivyo, Mhe. Makamba ameagiza watumishi wa NEMC wafuatao wasimamishwe kazi mara moja:

  a. Dkt. Eladius Makene -Afisa Mazingira Mwandamizi,

  b. Wakili Heche Suguta Manchare - Mwanasheria Daraja la II

  c. Mhandisi Boniface Benedict Kyaruzi, Afisa Mazingira

  Hatua nyingine za kinidhamu na kisheria zitafuatia

  2. Vilevile, imebainika kwamba usimamizi wa watumishi wa NEMC siyo makini na thabiti na kusababisha malalamiko mengi kuhusu utendaji wa Baraza. Hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Mhandisi Bonaventura Baya apewe barua ya onyo kalian la mwisho kwa udhaifu katika usimamizi wa watumishi wa Baraza.

  3. NEMC kama chombo muhimu nchini kilichopewa jukumu la kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira inatarajiwa kazi zake zifanyike kwa ufanisi wa kiwango cha juu kulingana na majukumu yaliyoko kwenye Sheria. Hivyo, kwa mapungufu yanayojitokeza Mhe. Makamba, ndani ya wiki moja ataunda jopo la wataalamu wasiozidi watano ili kutathmini utendaji wa NEMC na changamoto mbali mbali katika usimamizi wa hifadhi ya mazingira na kuishauri Serikali ipasavyo.

  4. Ili kuimarisha ufanisi na udhibiti wa utendaji wa NEMC, ndani ya wiki moja litatolewa Tangazo litakalokuwa na mambo yafuatayo: Anwani ya barua pepe (email), Nukushi (fax), Namba ya simu, Namba ya Whatsapp ili mtu yeyote mwenye malalamiko au aliyewahi kuombwa rushwa chochote na watumishi wa NEMC ambacho ni kinyume na maadili ya kazi yao atoe taarifa mara moja ili uchunguzi ufanyike na hatua zichukuliwe.

  5. Kutokana na mapungufu yanayojitokeza katika utekelezaji wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira, ndani ya wiki moja, NEMC ipitie upya orodha ya wataalamu na taasisi elekezi zilizosajiliwa na kufuta wataalamu na taasisi zote ambazo zimekuwa zikikiuka maadili ya kazi zao likiwemo suala la kuwasilisha taarifa zilizo chini ya viwango, kuchelewesha kazi za wateja wao na kutowasiliana na wateja wao kuhusu hatua za utekelezaji wa maombi yao.

  6. Ndani ya wiki tatu uitishwe mkutano wa dharura wa Bodi ya NEMC kujadili na kufanya maamuzi juu ya changamoto za utendaji katika Baraza.

  IMETOLEWA NA

  IDARA YA MAZINGIRA,

  OFISI YA MAKAMU WA RAIS

  TAREHE 24.01.2016

  0 0

  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam kuhusu uamuzi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli  kuwarejesha nyumbani mara moja Mabalozi wawili 


  2.0 Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa

  2.1 Aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwenye Serikali ya Awamu ya Nne, Mhe. Mahadhi Juma MAALIM ameteuliwa kuwa Balozi wa kwanza wa Tanzania nchini Kuwait, kufuatia uamuzi wa Serikali kufungua Ofisi ya Ubalozi katika nchi hiyo rafiki.

  2.2 Rais ameagiza Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kanda na Kimataifa kuwarejesha nyumbani mara moja Mabalozi wawili ambao mikataba yao imeisha. Leo hii Mabalozi hao wanatakiwa kukabidhi kazi kwa Afisa Mkuu au Mwandamizi aliye chini yao. Mabalozi hao ni:

  2.2.1 Bi Batilda Salha BURIANI, aliyeko Tokyo, Japan

  2. 2.2 Dkt. James Alex MSEKELA, aliyeko Rome, Italia.

  2.3 Rais amemrejesha nyumbani Balozi wa Tanzania aliyeko London, Uingereza, Bwana Peter Allan KALLAGHE. Anarejea Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa atakapopangiwa kazi nyingine.

  2.4 Kwa maana hiyo, vituo vya Ubalozi vifuatavyo viko wazi:

  2.4.1 London, kufuatia kurejea nchini kwa Balozi Peter A. KALLAGHE

  2.4.2 Brussels, kufuatia aliyekuwa Balozi, Dkt. Deodorous KAMALA kuchaguliwa kuwa Mbunge.

  2.4.3 Rome, Italia, kufuatia kuisha kwa mkataba wa Dkt. James Alex MSEKELA.

  2.4.4 Tokyo, Japan, kufuatia kuisha kwa mkataba wa Bibi Batilda BURIANI

  2.4.5 Kuala Lumpar, Malaysia, kufuatia aliyekuwa Balozi, Dkt. Aziz Ponray MLIMA, kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa.

  2.4.6 Brasilia, Brazil, kufuatia kustaafu kwa aliyekuwa Balozi, Bwana Francis MALAMBUGI.

  0 0

  Kikosi cha Amana FC ikiwa tayari kwa mchezo hapo juzi.
  Timu ya mpira wa miguu ya Amana Bank FC juzi iliichabanga timu ya Dar Community Bank mabao 8-1 katika mchezo wa mashindano ya mabenki yanayoendelea katika uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.

  Katika mchezo huo ambao Amana Fc iliutawala kwa vipindi vyote viwili, ikiongozwa na nahodha wao Muhsin Mohmed aliyefunga magoli matatu, huku kiungo mchezeshaji wa timu hiyo machachari  Ally Khamisi akiifungia mabao matatu pia kabla Anthony Mahimbali na Ally Abdul wakihitimisha karamu hiyo ya magoli. 

  Awali Amana Fc ilicheza na Access Bank Fc katika mcheko mkali na wa kusismua ambapo timu hizo zilitoka sare kwa kufungana mabao mawili kwa mawili, matokeo hayo yameifanya Amana Fc kuongoza msimamo wa ligi  hiyo ya mabenki ambayo inashiriki kwa mara ya kwanza mwaka huu ikiwa na pointi 7 na magoli 13. Amana Fc ipo katika kundi B ambalo lina timu za Mkombozi Fc, Access bank na wenyewe Amana Fc.

  Amana Fc imejikuta ikiingia robo fainali ya mashindano hayo baada ya kupewa ushindi wa pointi 3 na magoli matatu baada ya timu ya Mkombozi kutotokea uwanjani hivyo wakazawadiwa ushindi wa chee. Akiongea na mtandao huu meneja masoko wa benki hiyo Juma Msabaha Jr amesema vijana wao wapo vizuri na wana matarajio mazuri kushinda mechi yao ya robo fainali ambayo itachezwa baadae wiki hii katika uwanja wa Karume jijini Dar.


  0 0

   Jengo refu lilojengwa chini ya kiwango lililopo katika mtaa wa Indiraghandi jijini Dar,kama lionekanavyo pichani.
   Sehemu ya jengo ambayo inaonekana imepasuka.Picha na Emmanue Massaka wa Globu ya jamii
  Waziri wa Nyumba, Ardhi na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiwaagiza Watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na Shirika la Nyumba la Taifa kubomoa jengo refu lilojengwa chini ya kiwango lililopo katika mtaa wa Indiraghandi ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa.

  WAZIRI wa Nyumba, Ardhi na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amewaagiza watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na Shirika la Nyumba la Taifa kubomoa jengo refu lilojengwa chini ya kiwango lililopo katika mtaa wa Indiraghandi ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa.

  Lukuvi ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam kabla ya kuelekea kwenye ziara fupi katika Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani ambapo nako pia amebaini matatizo mbalimbali katika sekta  ya Ardhi.

  “Miezi sita iliyopita Rais Mstaafu alikuja hapa akaagiza jengo hili libomolewe na nyie mkajiridhisha kweli lafaa kubomolewa sasa inakuwaje mpaka leo linaendelea kuwepo, hivyo naagiza mfanye haraka jengo hili ndani ya mwezi mmoja taratibu za ubomoaji ziwe zimeanza ili kulinusuru taifa kuingia katika janga jingine.”alisema Waziri Lukuvi.

  Akiwa bagamoyo waziri Lukuvi alibaini katika Wilaya ya Bagamoyo upotevu wa viwanja  vya wanachi ambavyo walitakiwa kupewa katika eneo la ukuni ambapo vimetoweka 

  Mara baada ya kupata taaarifa hiyo mmoja wa wakaazi wa bagamoyo ambaye alitoa malalamiko juu ya viwanja hivyo mbele ya mkutano wa hadhara na kutaja kuwa Halmashauri ilichukua kiasi cha pesa kuanzia laki sita kwa kila mtu mwaka 2005 na kuahaidi kuwapatia viwanja lakini mpaka leo hawajapewa.

  Mara baada ya kupata taarifa hiyo waziri Lukuvi aliwagiza watendaji wa wilaya hiyo ndani ya miezi sita wawe wamewapatia wakazi hao viwanja hivyo.

  0 0

  Rais Dk. John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dickson Maimu (pichani) kuanzia leo.

  Aidha, baada ya utenguzi huo, Maimu amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi, pamoja na wafuatao. Mkurugenzi wa Tehama, Joseph Makani, Ofisa Ugavi Mkuu, Rahel Mapande, Mkurugenzi wa Sheria, Sabrina Nyoni na Ofisa Usafirishaji, George Ntalima.

  Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akifafanua moja ya swali lililoulizwa kutoka kwa mmoja Waandishi wa habari (hayupo pichani) kuhusiana na suala zima la kusimamishwa kwa Mkurugenzi wa NIDA,katika mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam mapema leo, kuhusu uamuzi wa Rais Magufuli kutengua uteuzi wa Mkurugenzi wa NIDA, Dickson Maimu.
  Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akizungmza katika mkutano na waandishi wa habari, Ikulu Dar es Salaam leo, kuhusu uamuzi wa Rais Magufuli kutengua uteuzi wa Mkurugenzi wa NIDA, Dickson Maimu.Picha Michuzi Jr-MMG 

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
  RAIS Dk.John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA),Dickson Mwaimu kwa ajili kupisha uchunguzi wa sh. Bilioni 179.6 zilizotolewa kwa ajili ya vitambulisho.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Katibu Mkuu Kiongozi , Balozi Ombeni Sefue amesema kutengua uteuzi huo ikiwa ni pamoja na baadhi ya watendaji wa vitambulisho vya taifa kusimamishwa kazi ambao ni Mkurugenzi wa Tehama ,Joseph Makani , Afisa Ugamvi Mkuu, Rahel Mapande ,Mkurugenzi wa Sheria, Sabrina Nyoni ,pamoja na Afisa Usafirishaji ,George Ntalima.

  Balozi Sefue,amesema kuwa kutengua uteuzi huo unatokana na kuwepo kwa malalamiko ambayo yamemfikia Rais juu ya wananchi kukosa vitambulisho vya taifa huku kukiwa na fedha ya Sh.Bilioni 179.6 zikiwa zimetumika .

  Rais Dkt Magufuli ameitaka Taasisi ya Kupambana na Rushwa (Takukuru) ifanye uchunguzi kama kuna vitendo vya rushwa vimefanywa ,amezitaka taasi ya Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),Mamlaka ya Manunuzi (PPRA) kufanya uchunguzi wa manunuzi yote yaliyofanywa na NIDA.

  Amesema katika uchunguzi huo CAG ifanye uchunguzi na kuangalia vitambulisho vya taifa kama vinaendana na fedha iliyotumika ya sh.bilioni 179.6.

  0 0

  Wakili wa upande wa walalamikaji (waliobomolewa )Abubakari Salim akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya kuahirishwa kwa kesi ya Bomoabomoa kwa Wakazi wanaoishi maeneo ya mabondeni mpaka January 26 mwaka huu ambapo hukumu itatolewa rasmi.
  Wananchi wakimsikiliza Wakili wa upande wa walalamikaji (waliobomolewa )Abubakari Salim leo baaada ya kuahirishwa kwa kesi ya Bomoabomoa,katika Mahakama Kuu,Kitengo cha Ardhi jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanue Massaka wa Globu ya jamii

  0 0

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro (katikati) akifungua mafunzo kwa timu ya ukusanyaji taarifa za tathmini ya kazi (hawapo pichani) kwenye ukumbi wa jengo la Maendeleo ya Jamii Dar es Salaam mapema leo. Kulia kwake ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma Bibi Tamika Mwakahesya na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu wa Maendeleo ya Jamii, Bwana James Kibamba.
   Katibu Mtendaji wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma, Bibi Tamika Mwakahesya (kulia) akimkaribisha Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro (katikati) kufungua mafunzo kwa timu ya ukusanyaji taarifa za tathmini ya kazi kwenye ukumbi wa jengo la Maendeleo ya Jamii Dar es Salaam mapema leo.
   Timu ya washiriki wa ukusanyaji taarifa za tathmini ya kazi wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi, Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) alipokuwa akifungua mafunzo ya ukusanyaji taarifa za tathmini ya kazi kwenye ukumbi wa jengo la Maendeleo ya Jamii Dar es Salaam mapema leo.
  Picha ya pamoja

  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Dkt. Larean Ndumbaro amewataka Watumishi watakaoshiriki zoezi la ukusanyaji taarifa za tathmini ya kazi kufanya kazi hiyo kwa uadililifu mkubwa ili kuweza kupata tathmini sahihi ya mishahara ya watumishi wa umma nchini kulingana na majukumu waliyonayo. 

  Katibu Mkuu aliyasema hayo alipokuwa akifungua mafunzo ya ukusanyaji taarifa za tathmini ya kazi yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Maendeleo ya Jamii jijini Dar es Salaam.

  Dkt. Ndumbaro alisema kuwa kazi ya ukusanyaji taarifa za tathmini ya kazi ni kubwa hivyo inahitaji umakini wa hali ya juu.“kama nilivyoeleza hapo awali kwamba kazi hii itawahusu watumishi wa umma wote, ni dhahiri kwamba  mtakutana na watu wa kada, taaluma,uelewa na matarajio tofauti ambapo mtalazimika kutumia weledi wenu wa mahusiano na mawasiliano (interpersonal and communication skills) katika kufanikisha kazi hii kwa ufasaha,” Dkt. Ndumbaro alisisitiza.

  Amewataka washiriki kuwa wasikivu na wepesi wa kuelewa mafunzo haya kwani lengo si kuwapa ujuzi wa kufanya kazi hii peke yake bali kuwajengea uwezo katika kumudu mazoezi kama haya kwa siku za baadae. 

  “Nitafurahi endapo miongoni mwenu mtatokea wataalam wa kuendesha zoezi kubwa kama hili siku za usoni kama wataalam waelekezi (Consultants),” Dkt. Ndumbaro aliongeza.

  Aidha, amemtaka Mtalaam Mwelekezi kufuatilia kwa karibu utendaji wa kila mshiriki ili kuhakikisha kwamba ameelewa, ameshiriki kikamilifu na kuwa anaweza kuaminiwa siku za baadae kuwa sehemu ya kazi kubwa kama hii. 

  Zoezi hili ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Malipo ya Mishahara na Motisha katika Utumishi wa Umma ya mwaka 2010 ambayo imetokana na juhudi za Serikali za muda mrefu katika kuboresha mishahara na masilahi ya watumishi wa umma. 

  Zoezi la Tathmini ya Kazi sio zoezi jipya katika utumishi wa umma kwani zoezi la aina hii lilifanyika mwaka 1998 – 2000 ingawa halikuhusisha utumishi wa umma wote. Zoezi la sasa litapima uzito wa kazi katika utumishi wote wa umma kama ulivyoainishwa katika Hati maalum iliyoanzisha Bodi.Zoezi hili linajumuisha watumishi wa umma katika taaluma mbalimbali kutoka katika maeneo ya pembe zote za Tanzania.

  Akitoa maelezo ya awali, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma, Bibi Tamika Mwakahesya alisema katika mwaka 2013/14 Bodi ilifanya utafiti ili kubaini hali ya mishahara na masilahi katika utumishi wa umma.

  Katika utafiti huo, ilibainika kuwepo kwa tofauti kubwa sana za mishahara na masilahi katika utumishi wa umma hata kwa kazi zinazofanana. Baada ya utafiti huo ilionekana kuwepo umuhimu wa kuendesha zoezi la Tathmini ya Kazi kama njia ya kubaini uzito wa kazi ambalo maandalizi yake yalianza mwaka 2014/15.

  Zoezi hili, tofauti na zoezi lililokuwa limetangulia, linazishirikisha tumishi zote za umma kama zilivyoelezwa kwenye Hati ya kuanzishwa kwa Bodi na limekusudia kujenga uwezo wa watumishi wa umma. 

  Bodi itaendesha zoezi hili kwa kumtumia Mtaalam Mwelekezi, ambaye ni Kampuni ya Deloitte Consulting Ltd ambaye ametakiwa kufanya kazi na watumishi 70 kutoka kwenye utumishi wa umma ambao watapatiwa mafunzo ya nadharia na vitendo, atawasimamia kukusanya na kuchambua taarifa na mwisho kwa wale ambao watakuwa wametimiza wajibu wao ipasavyo, kwa kushirikiana na Bodi, watatunukiwa Hati Maalum za Ushiriki (Certificate of Participation) na kuingizwa kwenye kumbukumbu za Serikali. Zoezi hililinatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi 15 kuanzia mwezi Oktaba 2015. 
     

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU


  Simu: 255-22-2114512, 2116898

  E-mail: press@ikulu.go.tz

  Tovuti : www.ikulu.go.tz              

  Faksi: 255-22-2113425
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amempongeza Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mheshimiwa Ban Ki-moon kuunda jopo la watu mashuhuri watakaomshauri juu ya namna bora ya kuendeleza na kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu hususani katika afya ya uzazi ya Mama na mtoto.


  Jopo hilo la watu mashuhuri linaongozwa na wenyeviti wenza ambao ni Rais wa Chile Mheshimiwa Michelle Bachelet na Waziri Mkuu wa Ethiopia Mheshimiwa Hailemariam Desalegn, huku Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete na Rais Mstaafu wa Finland Mheshimiwa Tarja Halonen wakiteuliwa kuwa wenyeviti mbadala.


  Katika Pongezi hizo Rais Magufuli amesema kuteuliwa kwa Rais Kikwete kuwa miongoni mwa jopo la kumshauri Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kumeijengea heshima Tanzania na kumechochea matumaini ya mafanikio ya kukabiliana na changamoto za afya ya mama na mtoto hususani kwa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania.


  Rais Magufuli ameahidi kuwa serikali yake ya awamu ya tano itatoa ushirikiano katika kutimiza malengo ya maendeleo endelevu ambayo jopo hilo litamshauri Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ikiwemo katika kuimarisha afya ya uzazi wa mama na mtoto.


  Gerson Msigwa

  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

  Dar es salaam


  25 Januari, 2016


older | 1 | .... | 745 | 746 | (Page 747) | 748 | 749 | .... | 1896 | newer