Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 741 | 742 | (Page 743) | 744 | 745 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Wahariri wa Gazeti la Mawio wakijisalimisha makao makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam leo mara baada ya Jeshi la Polisi kutangaza kuwatafuta popote pale kwaajili ya kutoa maelezo kwa kuandika habari ya upotoshaji kwa jamii, wakiwa na Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri, Abalom Kibanda katika makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam.
  Wahariri wa gazeti la Mawio wakizungumza  leo walipokuwa wanajisalimisha makao makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam leo.
  Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri, Abalom Kibanda  akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya Jeshi la Polisi leo jijini Dar es Salaam. Kuhusiana na kufungiwa na Serikali gazeti la Mawio jana.
  Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

  0 0

  ETIHAD imetunukiwa tuzo ya kifahari ya “Uvumbuzi katika Usafiri” katika hafla iliyoandaliwa na jarida la Travel Weekly ya kuwatunza wadau wa sekta ya usafiri dunia nzima huko Uingereza maarufu kama “Globe Travel Awards”. Hafla hiyo ilifanyika katikati ya wiki kwenye hoteli maarufu ya Grosvenor House, iliyopo Jijini London.

  Kwa kawaida tuzo hii hupewa kampuni ambayo imevumbua bidhaa au huduma yenye kuleta wimbi la mabadiliko na maendeleo katika soko. Shirika la Etihad waliibuka washindi baada ya jopo la wataalamu kuamua kwamba Shirika linastahili tuzo hii kutokana na huduma yake ya “Makazi”- ambayo ni huduma binafsi ya kipekee duniani yenye kutoa vyumba vitatu kwenye ndege ya Etihad. Huduma hii, iliyoleta mapinduzi katika sekta ya usafiri wa anga,ni matokeo ya programu ya utafiti na maendeleo iliyoendeshwa kwa miaka saba na kusimamiwa na timu nzima ya ubunifu kutoka kituo cha Uvumbuzi, Jijini Abu Dhabi.

  “Makazi” yanayopatikana kwenye ndege za Etihad aina ya Airbus A380 yana ukubwa wa mita za mraba 11 na ndani yake kuna sebule, bafu la pembeni, chumba kikubwa cha kulala na mhudumu mmoja kwa kila chumba.

  Shane O’Hare, Makamu Rais wa Masoko wa Shirika la ndege la Etihad alisema: “Tunafurahishwa na uamuzi wa jopo la wataalamu wa tuzo za Globe Travel, ambao ndio walipiga kura ‘Makazi’ kuwa huduma bora iliyovumbuliwa katika sekta yetu. Vyumba hivi vimebadili mitazamo ya wengi, vikiwapa fursa watu wa kawaida kufurahia huduma zinazopatikana mara nyingi katika ndege binafsi tu.”

  “Etihad inathamini ushirikiano kati yake na soko la Uingereza, uhusiano ulioanza tulipozindua safari zetu kuelekea na kutoka uwanja wa ndege wa Heathrow uliopo jijini London mnamo mwaka 2004. Tumeinua hadhi ya usafiri ikiwa ni pamoja na kuzipa ndege zetu muonekano halisia wa makazi ya kuishi na kuwapa wasafiri viwango vya hali ya juu vya faragha na utulivu”.

  Huduma ya ‘Makazi’ inapatikana ndani ya ndege aina ya A380 zinazofanya safari zake kati ya Abu Dhabi na London, New York pamoja na Sydney. SHirika la Etihad linatazamia kuzindua huduma hii katika ndege ziendazo Mumbai na Melbourne mwaka huu.

  Etihad ina timu maalumu ambayo kazi yake pekee ni kuhakikisha wanaochagua kusafiri na ndege zao wanaweza kufuruahia vyumba ya ‘Makazi’ wapendavyo. Timu hii pia ipo karibu na watoa huduma maalum waliopo kwenye vyumba hivi. Wateja wanapewa fursa ya kufurahia huduma mbalimbali wakiwa wanasafiri na ndege hii ya Etihad zikiwemo; kuweka oda ya mahala pa kula, burudani ndani ya ndege, matukio maalum kama sherehe za kuzaliwa, maelezo kuhusu waendako na kadhalika. Watuapo, timu hiyo maalum (VIP) huwasaidia wageni katika kufanya taratibu za kuwasili na usalama.


  Ndege za Etihad zinafanya safari zake kwenda Uingereza kutwa mara sita, pamoja na kutoa huduma za safari za moja kwa moja kati ya uwanja wa ndege wa Heathrow uliopo jijini London na kuelekea Machester na Ediburgh, zilizoanzishwa Juni 8 mwaka jana. Uwanja wa ndege wa Heathrow ulipewa nafasi kuwa kiwanja cha kwanza ndege aina ya Airbus A380 za Etihad kutua kwa mara ya kwanza, na hivyo huduma hiyo ilianza mwishoni mwa mwaka 2014.

  0 0
 • 01/18/16--06:51: RAIS WA AFC AWASILI TANZANIA
 • Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Asia (AFC) na Makamu wa Rais wa FIFA, Sheikh Salman Bin Ebrahim Al Khalifa amewasili nchini leo mchana na kupokelewa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi.

  Sheikh Salman amekuja nchini kwa matembezi ya siku ya mbili na atakua na mwenyeji wake Rais wa TFF, Jamal Malinzi.


  Kesho Jumanne, Sheikh Salman Bin Ebrahim Ali Khalifa atamtembelea ofisini Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel.

  0 0

  UMOJA wa wanamlalo, Wealfare Associastion waishio Dar es Salaam (MLAWA) wametoa msaada kwenye kituo cha watoto yatima cha Nyumba ya Furaha kilichopo mkoani Tanga wametoa shuka 20 vitene 8 na fedha taslimu shilingi laki tano (500,000).
  Mwakilishi wa UMOJA wa wanamlalo, Wealfare Associastion waishio Dar es Salaam (MLAWA), Rose Mbelwa akitoa zawadi mbalimbali kwa Sista Irene Kapuka ambaye ni mwakilishi wa kituo cha nyumba ya Furaha kilichopo mkoani Tanga.

  Watoto wakiwa katika picha ya pamoja na UMOJA wa wanamlalo, Wealfare Associastion waishio Dar es Salaam (MLAWA) katika makabidhiano yaliyofanyika mkoani Tanga Mwishoni mwa wiki.

  0 0

  Na ImmaMatukio

  BENKI ya Diamond Trust Tanzania, imedhamini shughuli ya upandaji miti katika Wilaya ya Iringa iliyopo mkoani Iringa kwa kuchangia sh. milioni tano. Wilaya ya Iringa imeanza rasmi kupanda miti katika maeneo yaliyotengwa na uongozi wa wilaya, ikiwa ni utekelezaji wa programu ya kitaifa ya kupanda na kutunza mazingira inayoanza mwezi huu.

  PICHA : Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akipanda miti jana wilayani humo ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa kampeni ya kupanda miti. Benki ya Diamond Trust Tanzania imedhamini shughuli hiyo kwa kuchangia sh. milioni tano. Picha kwa hisani ya DTB.

  Wilaya ya Iringa inategemea kupanda zaidi ya miti 5,000 ya mbao, mapambo, kivuli na matunda. Programu ya kupanda miti na kutunza mazingira ilizinduliwa rasmi na Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof. Jumanne Maghembe, wiki iliyopita.

  Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela wakati akizindua kampeni ya kupanda miti jana alieleza kuwa, Wilaya ya Iringa imetenga maeneo makubwa ya hifadhi ya misitu na mazingira ili kuhifadhi na kuongeza kiwango cha maji nchini katika tarafa za Mlolo, Ismani, Kalenga, Pawaga na Idodo.

  Pia alisisitiza umuhimu wa miti na misitu katika kuhifadhi maji na umuhimu wa maji kwa viumbe hai. Alisema, upandaji miti na utunzaji wake utasaidia kupata hewa nzuri, maji, mvua, kupunguza joto na kupambana na mabiliko ya tabianchi.

  Programu hiyo ya kitaifa ni ya aina yake nchini na inashirikisha serikali kuu, wananchi na sekta binafsi. Akizungumza na waandishi wa habari walioshiriki katika shughuli ya kupanda miti, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Diamond Trust Tanzania, Ndugu Viju Cherian, alisisitiza umuhimu wa programu ya kupanda miti.

  Kutunza mazingira ni moja ya nguzo kuu ya benki yetu katika maeneo tunakofanya biashara. Kwa kuzingatia hilo, tumeitikia wito wa Mkuu wa Wilaya na kuunga mkono programu hii kwa kuchangia shilingi milioni tano. Benki ya DTB ni mshirika mkubwa katika hifadhi ya mazingira nchini kote,ö alisema.

  Benki ya DTB ilifungua tawi katika mji wa Iringa mwaka 2014 na hadi sasa ina matawi 24, matawi 10 yakiwa katika jiji la Dar es Salaam (tawi kuu la Dar es Salaam Mtaa wa Jamaat, Masaki, Morocco,Magomeni, Mbezi, Mbagala,Barabara ya Nyerere, Kariakoo, Barabara ya Nelson Mandela karibu na njia kuu ya Tabata na Upanga katika Barabara ya Umoja wa Mataifa.

  Pia ina matawi katika miji ya Arusha, Mwanza, Zanzibar, Dodoma, Tanga, Mbeya, Moshi, Iringa, Morogoro, Tabora, Kahama na Mtwara. Aidha, DTB ni mshirika wa Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Aga Khan, ambao ni sehemu ya mtandao wa maendeleo wa Aga Khan (Aga Khan Development Network).

  Katika hatua nyingine, Benki ya Diamond Trust ina matawi zaidi ya 115 katika nchi za Afrika Mashariki ambayo inaundwa na Kenya, Tanzania, Uganda ikiwemo Burundi.  0 0

  Mkufunzi wa Maswala ya Biashara Ndugu Felix Maganjila  akiwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Shera Illusions Africa na Mkurugenzi wa Manjano Foundation Mama Shekha Nasser  Wakati wa Mafunzo hayo leo.

  Awamu ya pili washiriki watapatiwa elimu kuhusu matumizi sahihi ya Vipodozi hasa "Make-Up". Hapa washiriki watajua namna mbalimbali za kutumia vipodozi na namna ya kuwapamba maharusi na wakazi wa Mwanza na maeneo jirani kwa kutumia vipodozi.Mara baada ya mafunzo haya washiriki watapata fursa ya kukopeshwa mitaji kwa ajili ya biashara kwa lengo la kuwakwamua washiriki wote kuondokana na ukosefu wa ajira na kujikita katika kujiajiri. Mafunzo haya yanaratibiwa na Taasisi ya Manjano Foundation kwa kushirikiana na Kampuni ya Shear illusions kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano. Mafuzo kama haya tayari yamesha wanufaisha  wanawake 65 wa Jiji la Dar es Salaam.
  Picha ya Pamoja ya Washiriki  wa Mafunzo  ya Ujasiriamali kutoka Mkoa wa Mwanza.

   Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo kutoka Mkoa wa Mwanza wameishukuru Taasisi ya Manjano Foundation  kwa kuwapa nafasi hiyo na kuwaletea mrdai huu. Wakieleza zaidi wamesema walikuwa na hamasa sana tangu walipopata taarifa kwa wanawake wenzao wa mkoa  wa Dar es salaam kunufaika na mradi huu na walikuwa wanasubiri kwa hamu kubwa sana mafunzo hayo.Wakiendelea zaidi wamesema wapo tayari kupigana na kujikita vizuri kupitia mradi huu kwa lengo la kujikwamua na kujiongezea kipato
   Wanawake wa jiji la Mwanza walionufaika na Mradi wa Manjano Dream Makers wakikisikiliza kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zinatolewa kwenye Mafunzo hayo Yanayoendelea  Jijini mwanza..

  Mafunzo ya kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano yameanza mkoani Mwanza. Washiriki wa fursa hiyo wanajulikana kama Manjano Dream Makers kwa lengo la kuwawezesha wanawake kiuchumi. Mafunzo hayo yamegawanyika katika awamu mbili. Awamu ya kwanza wanawake 30 wa Jiji la Mwanza Watapatiwa elimu kuhusu biashara, namna ya kukuza na kuendesha biashara na nidhamu ya kutunza pesa na mahesabu yaani 'financial literacy'.Pia washiriki watanufaika namna ya kutoa huduma nzuri na bora kwa wateja na jinsi ya kujiwekea akiba. 

  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Hamad Yussuf Masauni akipata maelezo kutoka kwa Afisi wa Uhamiaji Zanzibar wakati wa ziara yake katika Idara ya Uhamiaji Zanzibar. 
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Tanzania Mhe Hamad Yussuf Masauni akitembelea Vitengo vya Idara ya Uhamiaji Zanzibar wakati wa ziara yake na kuangalia Utendaji wa Idara hiyo Zanzibar.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani akimsikiliza Afisa Uhamiaji Zanzibar akitowa maelezo ya jinsi ya kuweka kumbukumbu za Passport wakati wa ziara yake.


  Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar akitowa maelezo kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Hamad Yussuf Masauni, wakati wa ziara yake katika Idara hiyo Zanzibar. 

  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Tanzania Mhe Hamad Yussuf Masauni akizungumza na Maofisa wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar baada ya ziara yake ya kujitambulisha na kuangalia ufanisi wa kazi za Idara hiyo Zanzibar.
  Maofisa wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Eng Hamad Yussuf Masauni akizungumza na Maofisa hao baada ya ziara yake kutembelea Idara hiyo kuina ufanisi wa Kazi zake kwa Wananchi wanaofika kupata Passport.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Hamad Masauni, akisalimiana na Maofisa wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar wakati wa ziara yake kutembelea Idara hiyo ya Uhamiaji Zanzibar.kushoto Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar.

  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Hamad Masauni, akisalimiana na Maofisa wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar wakati wa ziara yake kutembelea Idara hiyo ya Uhamiaji Zanzibar.Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar.
  Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot
  Zanzinews.com   0 0

  Wazee wakimsimika James Katoro baada ya kuchaguliwa kuwa Diwani wa Kata ya Kayenze katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza.

  Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG 
  Katoro alichaguliwa kuwa diwani wa Kata hiyo katika uchaguzi uliofanyika Novemba 25,2015 kupitia Chama cha Mapinduzi CCM. Tukio hili limejiri jana katika Mkutano wa hadhara wa CCM kuwashukuru wakazi wa Kata hiyo kwa kumchagua Katoro kuwa diwani wa Kata hiyo.

  Wazee wakimsimika James Katoro baada ya kuchaguliwa kuwa Diwani wa Kata ya Kayenze katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza. 
  Mchungaji Elias Lutalamamila (wa pili kulia) kwa niaba ya viongozi wa dini akimsimika James Katoro baada ya kuchaguliwa kuwa Diwani wa Kata ya Kayenze katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza. 
  Diwani wa Kata ya Kayenze Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza James Katoro (CCM) akihutubia katika mkutano wa kuwashukuru wakazi wa Kata hiyo kwa kumchagua kuwa diwani wao. Aliahidi kushughulikia kero mbalimbali zilizo katika Kata hiyo ambazo ni pamoja na kero ya maji, ujenzi wa zahanati na vituo vya afya, miundombinu pamoja na ujenzi wa shule za msingi na Sekondari.
  Salum Abdallah Said ambae ni Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kayenze akizungumza katika mkutano wa chama hicho wa kuwashukuru wakazi wa Kata hiyo kwa ushindi waliokipa chama hicho katika uchaguzi uliofanyika Novemba 25,20515.
  Kulia ni Jeremiah Mtoni ambae ni Katibu wa CCM Kata ya Kayenze akizungumza katika mkutano wa chama hicho wa kuwashukuru wakazi wa Kata hiyo kwa ushindi waliokipa chama hicho katika uchaguzi uliofanyika Novemba 25,20515.
  Elias Makaranga (mwenye kinasa sauti) ambae alikuwa Meneja Kampeni wa Diwani Katoro katika uchaguzi uliopita akizungumza jambo katika mkutano wa kuwashukuru wananchi uliofanyika jana.
  Wakazi wa Kata ya Kayenze wakifuatilia Mkutano wa Chama cha Mapinduzi CCM katika Kata hiyo wa kuwashukuru kwa kukichagua chama hicho katika uchaguzi uliofanyika Novemba 25, mwaka jana.

  0 0

  Mh. Hassani Selemani Kaunje ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Lindi kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) leo hii ameweza kutekeleza ahadi yake aliyowaahidi kikundi cha wanawake wachuuzi wa samaki cha Mitwero ya kuwapatia msaada wa Majokofu mawili (2) ya kutunzia Samaki.

  Akikabidhi majokofu hayo leo hii Mh. Mbunge amewataka wachuuzi hao kutunza vitu hivyo kwani ni vyagharama na vitadumu kwa muda mrefu endapo wataviweka katika mazingira mazuri. Nao wanakikundi hicho cha akinamama wachuuzi wa samaki wameweza kupongeza hatua hiyo, wamemsifia kuwa ni mtu wa kutimiza ahadi kwani ametimiza kile alicho ahidi.
  Mh. Mbunge amekuwa mstari wa mbele kutekeleza ahadi zake kwa kipindi hiki kifupi tangu alipochaguliwa na wananchi wa jimbo la Lindi mjini kwani hivi karibuni aliweza kutoa msaada wa Matanki ya kutunzia maji katika kata ya Kineng’ene.

  0 0

  Mwanamitido wa Kimataifa, Flaviana Matata akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya ya Mazingira Bora kwa Elimu Bora yenye lengo la kufanikisha maendeleo ya elimu katika Jimbo la Segerea kwa kusaidia kununua madawati, kuchimba matundu ya vyoo, kuchimba visima vya maji na kujenga vyumba maalum vya watoto wa kike, chini ya uratibu wa Mfuko wa Udhamini wa Elimu wa Bonnah (BETF), jijini Dar es Salaam jana. Wengine pichani ni mwandaaji wa kampeni hiyo ambaye ni Mbunge wa Segerea, Bonnah Kaluwa na Mratibu wa Elimu Josephat Peter.
  BONA
  Mbunge wa jimbo la Segerea,Mhe: Bonnah M.Kaluwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya ya Mazingira Bora kwa Elimu Bora yenye lengo la kufanikisha maendeleo ya elimu katika Jimbo la Segerea kwa kusaidia kununua madawati, kuchimba matundu ya vyoo.BONA1BONA2
  Mkutano ukiendelea.

  ………………
  Alichozungumza Mbunge wa Segerea,Mhe Bonnah Kaluwa .

  Leo tarehe 17/01/2016,Mimi Bonnah M.Kaluwa ambaye ni mbunge wa jimbo la Segerea katika wilaya ya Ilala.
  Nimekuiteni Asubuhi ya leo ili kuwashirikisha katika uzinduzi wetu wa kampeni ya MAZINGIRA BORA KWA ELIMU BORA ndani ya jimbo la Segerea,kwakujua dhahiri kuwa ushiriki wa wana habari ni muhimu sana katika kufanikisha kampeni hii kwa ajili ya maendeleo ya elimu katika jimbo la Segerea na nchi kwa ujumla .
  MAZINGIRA BORA KWA ELIMU BORA ,ni kampeni isiyo na malengo ya kumnufaisha mtu binafsi bali inalenga kuisaidia jamii ndani ya jimbo la Segerea katika upatikanaji wa elimu bora kupitia maboresho ya miundombinu ya shule kama madarasa, vyoo, mifumo ya maji safi na salama, madawati na kadhalika.
  Ndugu zangu ninyi wote ni mashahidi kuwa zipo changamoto nyingi katika sekta ya elimu ndani ya nchi yetu zinazohusiana moja kwa moja na masuala niliyoyataja hapo juu.Huku tukilenga kupata;
  madawati 15,000,
  matundu ya vyoo vya kisasa 1335,
  visima vya maji 12, na
  vyumba maalum vya watoto wa kike 38.
  Kimsingi kampeni hii ni muendelezo wa kampeni iliyowahi kufanyika katika kata ya KIPAWA [ndani ya jimbo la Segerea] kwa kusimamiwa na mfuko wangu wa elimu uitwao BONNAH EDUCATION TRUST FUND mnamo mwaka 2011,kipindi nilipokuwa diwani wa kata hiyo.Kwakuzingatia mafanikio na matokeo chanya ya kampeni hii katika ngazi ya kata;
  Kwa moyo wa dhati kabisa, kwakuwa nimechaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Segerea ,nimedhamiria kupeleka mafanikio ya kampeni hii kwa kushirikiana na mfuko wangu wa BONNAH EDUCATION TRUST FUND katika ngazi ya jimbo ili basi kila mwananchi ndani ya jimbo la Segerea anufaike na kampeni hii.
  Ili kufanikisha kampeni hii, tutawashirikisha wadau mbalimbali wa elimu waliopo ndani na nje ya jimbo la Segerea kama vile Serikali, Makampuni, Mashirika na watu binafsi.
  Kampeni ya MAZINGIRA BORA KWA ELIMU BORA tunatarajia kuifanya kwa awamu mbili ambazo ni;
  Matembezi ya hiyari (Charity walk) na
  Chakula cha jioni (Gala dinner).
  MATEMBEZI YA HIYARI.
  Matembezi haya yatafanyika ndani ya jimbo kwa kushirikisha wananchi ,na wadau wote wa elimu tukiwa na lengo moja tu la kukusanya fedha za kuboresha miundombinu ya elimu katika jimbo letu la Segerea kwa shule za msingi katika kata zote kumi na tatu[13] za jimbo la Segerea.
  Matembezi haya yanatarajiwa kufanyika tarehe 25/02/2016, kuanzia saa 2 asubuhi mpaka saa 10 alasiri.
  CHAKULA CHA JIONI
  Awamu hii ya pili na ya mwisho ya kampeni yetu inatarajiwa kufanyika tarehe 03/06/2016 kuanzia saa 2 usiku na kuendelea.
  Katika awamu hii tunatarajia kuwa na chakula cha jioni cha pamoja ambapo wageni kutoka maeneo mbali mbali na nje ya nchi watashiriki nasi katika kuchangia na kuhamasisha upatikanaji wa fedha na mahitaji yote muhimu kuelekea ufanikishaji wa kampeni yetu.
  Tunawashukuru ninyi waandishi wa habari na wageni wote waalikwa kwa kushiriki nasi katika uzinduzi huu wa kampeni hii ya MAZINGIRA BORA KWA ELIMU BORA jimbo la Segerea.
  Hivyo natangaza rasmi kuwa kampeni hii imezinduliwa rasmi leo tarehe 17/01/2016.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi wa Botswana, Bw. Tshenolo Mabeo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sir Seretse Khama uliopo Gaborone Januari 17, 2016. Majaliwa amemwakilisha Rais John Magufuli katika Mkutano wa SADC.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Katibu Mtendaji wa SADC,Dkt, Srergomena Tax mjini Gaborone ambako Mheshimiwa Majaliwa anamwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano wa SADC Januari 17, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Lucas Mweri akizungumza juzi kwenye baraza la madiwani wa wilaya hiyo (katikati) ni Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Jackson Sipitieck na Makamu Mwenyekiti Albert Msole.  
  Diwani wa Kata ya Ruvu Remit Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Alamayani Ranga akisoma taarifa kwenye baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo juzi juu ya uboreshaji wa huduma za jamii

  Na Woinde Shizza,Arusha
  Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambona amewataka madiwani wa kata 18 za wilaya hiyo kushirikiana na maofisa watendaji wa vijiji vyao kuhakikisha migogoro inakwisha.
  Kambona aliyasema hayo juzi wakati akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo na kuagiza mipaka ya vijiji na vitongoji vya miji midogo ya Orkesumet na Mirerani izingatiwe kwa kupimwa.
  Alisema kila diwani akishirikiana na maofisa watendaji wa vijiji wataweza kumaliza migogoro hiyo na maeneo ya kilimo na mifugo yabainishwe na kuhakikisha suala la mifugo kuzagaa likomeshwe ikiwemo punda na ng’ombe.
  “Mifugo inazagaa ovyo na kuharibu mazao, lidhibitini hilo kwa kutumia kanuni ndogo zetu, kwani mifugo inaachiwa sana na ukitembelea sehemu nyingine unakuta punda wanaingia hadi kwenye madarasa ya shule,” alisema Kambona.
  Pia, Kambona amemuagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo Lucas Mweri kuwapangia wakuu wa idara, vitengo na watumishi wengine wawe walezi wa kata mbalimbali ili wawe wanazitembelea na kutoa ushauri.
  Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro Jackson Sipitieck alisema hivi sasa madiwani na watumishi kwa pamoja wanatakiwa kujipanga kikamilifu ili kuhakikisha wananchi wa kata za eneo hilo wanapatiwa maendeleo.
  “Tujipange kikamilifu kwa pamoja na kuhakikisha kuwa wananchi wetu wanapata huduma stahiki, kwani sisi tulichaguliwa kwa ajili ya kutumikia jamii ya Simanjiro ili wapate maendeleo kwenye sekta mbalimbali,” alisema Sipitieck.   0 0

  Aliyekuwa Mwenyekiti tawi la CCM DMV Bwn. George Sebo enzi za uhai wake

  George Sebo mwenyekiti wa CCM DMV amefariki Dunia muda si mrefu Katika hospitali ya Prince George taarifa zaidi zinakuijia hivi punde

  0 0

   Mwili ukiwasili katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazishi.
  Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa aliyekuwa Mkurungenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Mhandisi, Suleiman Suleiman kabla ya mazishi yake.
   Mwili wa aliyekuwa Mkurungenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Mhandisi, Suleiman Suleiman uwasili katika makaburi ya Kisutu leo.
  Mwili wa aliyekuwa Mkurungenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Mhandisi, Suleiman Suleiman ukihifadhiwa katika nyumba yake ya milele.
   Mwili wa aliyekuwa Mkurungenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Mhandisi, Suleiman Suleiman ukihifadhiwa katika nyumba yake ya milele.
   Waombolezaji.
  Baadhi ya waombolezaji wakiweka udongo katika kaburi la marehemu.
  Baadhi ya waombolezaji wakiweka udongo katika kaburi la marehemu.

   Wadau wa michezo wakibadilishana mawazo. Kutoka kushoto ni Rais wa Klabu ya Simba, Evance Aveva, Msemaji wa Simba, Haji Manara, Muhidin Issa Michuzi na Mpoki Bukuku wakibadilishana mawazo wakazi wa mazishi ya aliyekuwa Mkurungenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Mhandisi, Suleiman Suleiman. (Picha na Francis Dande)
  DAR ES SALAAM, TANZANIA

  SIMANZI, majonzi na vilio vimetawala nyumbani kwa aliyekuwa Mkurungenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Mhandisi, Suleiman Suleiman aliyefariki dunia leo wakati akiogelea katika bahari ya hindi.


  Suleiman alifariki dunia asubuhi akiwa njiani akipelekwa katika hospitali ya Aga Khan  mara baada ya misuli kukaza ghafla alipokuwa akiogelea.


  Ofisa Uhusiano wa TAA, Ramadhan Maleta alisema marehemu huwa anautaratibu wa kufanya mazoezi ya kuogelea kila siku asubuhi kutoka feri hadi Kigamboni.


  Alisema leo asubuhi kama kawaida yake alikwenda Feri kwa ajili ya kuogelea saa 12.00 ambapo aliogelea hadi Kigamboni na alipokuwa anarudi  alipata tatizo la kukaza kwa misuli na kuishiwa nguvu.


  Maleta alisema mwenzake aliyekuwa anaogelea nae alimuona na kujaribu kumuokoa na kuomba msaada kutoka boti za wavuvi ambao walifika na kumpeleka nchi kavu na kumpa huduma ya kwanza, ambapo alikuwa akiwa njiani kupelekwa hospitali.


  Alisema TAA imepata pigo kubwa kwa kupotea kiongozi mahiri ambaye alikuwa hana majigambo wala hakuweka matabaka baina na wafanyakazi na alishirikiana na wote bila kujali nyadhifa zao.


  Alisema marehemu alikuwa miongoni mwa viongozi waanzilishi wa kwanza wa TAA mwaka 1999 na atakumbukwa kwa mchango mkubwa alioutoa na usimamizi wa ujenzi wa viwanja vya ndege vya Songwe na Mpanda.


  Pia ujenzi wa awamu ya tatu ta Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julkias Nyerere (JNIA) na viwanja vingine vya ndege vinavyoendelea na ujenzi katika mikoa mbalimbali nchini.


  Baadhi ya wafanyakazi wa mamlaka hiyo waliofika nyumbani kwa marehemu walisikika wakilia huku wakisema kuwa TAA wameacha yatima na kwamba pengo la Suleimani ni kubwa kwao na kwa taifa.
    

  Kaka wa marehemu, Farid Karamma alisema Suleima atakumbukwa kwa ukarimu wake na alikuwa mtu wa kupenda watu na asiyependa migogoro.


  Alisema marehemu ameacha mke mmoja na watoto watatu wa kiume ambao ni Mohammed, Said na Husam Suleima anayesoma katika shule ya sekondari Mzizima Dar es Salaam.


  Mwili wa marehemu uliwasili nyumbani kwake Upanda saa 7.25 mchana ukiwa katika gari la kubebea wagonjwa la msikiti wa Maamur ambapo saa 9.21 ulichukuliwa na kupelekwa msikitini hapo tena kwa ajili ya kuswaliwa, na kisha kwenda kus\zikwa katika makabiri ya Kisutu.

  0 0

  Madawa ya kulevya yaliyokamatwa mkoani Mbeya.

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
  WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
  JESHI LA POLISI TANZANIA.

  TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
  “PRESS RELEASE” TAREHE 19.01.2016.
  KATIKA TUKIO LA KWANZA, MWANAMKE MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA NURU ISMAIL [31] MFANYABIASHARA NA MKAZI WA JIJINI DAR ES SALAAM ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA MADAWA YA KULEVYA AINA YA BHANGI UZITO KILO 7 NA GRAMU 100 ZIKIWA ZIMEHIFADHIWA KWENYE MABEGI YA NGUO.

  MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 18.01.2016 MAJIRA YA SAA 05:30 ASUBUHI HUKO CUSTOM MPAKANI MWA TANZANIA NA ZAMBIA KATIKA MJI MDOGO WA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA.

  AIDHA MTUHUMIWA ALIKAMATWA AKIWA SAFARINI AKITOKEA SOUTH AFRIKA KUELEKEA JIJINI DSM AKIWA NA PASSPORT NO. AB.767234 ILIYOTOLEWA DSM TAREHE 21/10/2015 NA KUSAFIRI KWENYE BASI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.595 BPR MALI YA KAMPUNI YA FALCON IKITOKEA LUSAKA KUELEKEA DSM. 

  KATIKA TUKIO LA PILI, MTU MMOJA MKAZI WA BITIMANYANGA WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA AITWAYE HAMIS SELEMANI [30] ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI KETE 3 SAWA NA UZITO WA GRAMU 15 ZIKIWA ZIMEHIFADHIWA MFUKONI MWA SURUALI YAKE.

  MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 18.01.2016 MAJIRA YA SAA 15:30 JIONI HUKO KIJIJI CHA BITIMANYANGA, KATA YA MAFYEKO, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. 

  WATUHUMIWA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI MARA TU BAADA YA UPELELEZI KUKAMILIKA.

  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.

  Imesainiwa na:
  [EMANUEL G. LUKULA – ACP]

  Kny: KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
  NB: Kny – ina maana kwa niaba ya.

  0 0

   Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama, Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dr Rehema Nchimbi akiongea na askari wa Mkoa wa Njombe.
   Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama, Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dr. Rehema Nchimbi akiteta jambo na Kahimu RPC Njombe SSP JohnTemu kwenye sherehe ya Polisi Njombe kuukaribisha mwaka mpya 2016.
   Juu na chini Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama, Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dr Rehema Nchimbi akikabidhi zawadi kwa askari wa Mkoa wa njombe walio fanya vizuri zaidi kazi. 

  Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama, Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dr Rehema Nchimbi mwenye kilemba akionesha utaalam wa kulicheza Twist kwenye sherehe ya Mpolisi Njombe kuukaribisha mwaka mpya 2016, kulia ni Kahimu RPC Njombe SSP JohnTemu.

  POLISI Mkoa wa Njombe imeagizwa kuwa sehemu ya usimamizi wa fedha zilizo tolewa na Serikali kwa ajili ya maendeleo ya elimu Mkoa wa Njombe ili kuhakikisha pesa hizo zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ya kutoa elimu bure kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari kama alivyo agiza Mh Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.

  Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi katika sherehe zilizoandaliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe kusherekea mwaka mpya na kuwapongeza askari waliotimiza vyema majukumu yako ya kazi.

  Aidha Dr Nchimbi ameonesha imani kuwa polisi wanaweza kulinda matumizi ya pesa hizo baada ya jeshi hilo kuonesha uwezo mkubwa wakusimamia usalama wa raia na malizao kipindi chote cha uchaguzi na kuwafanya wananjombe kuendesha shughuli zao kwa amani na utulivu hivyo kudhibitisha dhana ya uwepo wa maisha baada ya uchaguzi.

  Dkt Nchimbi amesema kwa kuwa Jeshi la Polisi ni Sikio na Jicho la serikali hivyo alinabudi kujua ni kiasi gani cha pesa kilicho ingia Mkoa wa Njombe na kuhakikisha usalama wa pesa hizo na usalama wa walengwa wa pesa hizo ili kuepusha matumizi yasio sahihii, na ametoa onyo kali kwa walimu watakao ficha taharifa za pesa hizo.  “Pesa zilizoinginzwa Mkoa wa Njombe na Serikali kwa ajili ya maendeleo ya elimu ni Nyingi, na zitakuwa zikiingizwa kila mwezi, hivyo tusipo zisimamia vizuri pesa hizi madhara yake yatakuwa ni makubwa, hivyo naliagiza Jeshi la Polisi Njombe, kupita pita na kutafuta taarifa sahii za mwenendo wa matumizi wa pesa hizi maana ninyi ndio Jicho na Sikio la Serilika, ili kama kunamwenendo mbaya wa matumizi tuchukue hatua kali kwa wahusika”, aliongeza Dr Nchimbi.

  Aidha Dr Nchimbi ameonesha imani kuwa polisi wanaweza kulinda matumizi ya pesa hizo baada ya jeshi hilo kuonesha uwezo mkubwa wakusimamia usalama wa raia na malizao kipindi chote cha uchaguzi na kuwafanya wananjombe kuendesha shughuli zao kwa amani na utulivu hivyo kudhibitisha dhana ya uwepo wa maisha baada ya uchaguzi.

  Nae Imamu wa msikiti Njombe Shehe UPETE katika kumtanguliza Mungu kwenye sherehiyo, amewaombea Askari wote wa mkoa huo ili mwenyezi Mungu awazidishie hekma na kuwapa afya njema ili wapate kuwatumikia vyema wakazi wa Njombe, Viongozi wa Juu serikalini na wananchi wote wa Tanzania kwa Ujuma.

  Akimshukuru Mkuu wa koa kwa uzalendo aliouonesha kwa jeshi la Polisi Njombe, Kahimu Mkuu wa Polisi Njombe SSP JOHN TEMU ameahidi kufanyia kazi maagizo hayo na pia amewataka askari wote wa Jeshi la Polisi mkoani humu kufanya kazi kwa weledi ili kudumisha amani na upendo kwa wakazi wa Mkoa huo.


  0 0

  JESHI la Polisi mkoani Mwanza imekanusha kuhusika na uhalifu kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini.

  Hayo yamesemwa leo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Justus Kamugisha alipokuwa akizungumza ofisini kwake kuhusu tuhuma zilizotolewa juu ya Jeshi la Polisi mkoani humo kuhusika na Uhalifu.

  Kamanda Justus Kamugisha amesema kuwa kuna taarifa zimekuwa zikitolewa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa Jeshi la polisi mkoani humo linajihusisha na masuala ya uhalifu ikiwemo baadhi ya maofisa wao kushirikiana na wahalifu katika uuzaji wa dawa za kulevya pamoja na kushirikiana na majambazi kupora mali za wananchi .

  “Ni habari za uongo na za kulichafua Jeshi la Polisi na mimi kama Kamanda wa Polisi nimelipokea suala hili kwa masikitiko na natoa onyo kwa vyombo vya habari na jamii kwa ujumla kuacha tabia ya kueneza habari sizizokuwa za kweli” Amesema Kamanda Kamugisha.

  Aidha Kamanda Kamugisha amesema kuna malalamiko yanayotolewa kuhusu Jeshi la Polisi mkoani hapo kujihusisha na ulanguzi wa bidhaa zinazouzwa kwenye kanteeni za Polisi, taarifa hizo ni za uongo kwani Serikali imeshafuta msamaha wa kodi katika bidhaa hizo ambazo zilikuwa na bei tofauti na zile zilizopo katika maduka ya kiraia.


  Jeshi la Polisi ni chombo cha ulinzi na usalama wa raia na mali zake hivyo wananchi wanatakiwa kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kupamabana na uhalifu uliopo.

  0 0

  Na Benedict Liwenga-MAELEZO.
  SHIRIKA la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) limetolea ufafanuzi kuhusu malalamiko ya Wakazi wa kijiji cha Seseko Kata ya Mwamalili mkoani Shinyanga.

  Ufafanuzi huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Afisa Uhusiano wa Shirika hilo, Bw. Lusajo Mwakabuku wakati akiongea na Idara ya Habari mara baada ya kuhojiwa kuhusu madai ya wakazi wa kijiji hicho kuhusu kufyekwa kwa mazao yao bila ya kulipwa fidia na Shirika hilo. 

  Mwakabuku amefafanua kuwa madai ya wakazi wa eneo hilo yamekuwa yakijirudia mara kwa mara licha ya TANESCO kuwalipa fidia kwa wakazi hao tangu mwaka 1999.

  Mwakabuku amefafanua kuwa, Madai hayo yanatokana na njia ya msongo wa Umeme wa kilovoti 220 ambayo ni njia inayotokea Shinyanga kuelekea Mwanza na inaonekana hawa wanaolalamika kufyekewa mazao yao ni wale ambao wamevamia ama wameweka makazi yao hivi karibuni katika maeneo hayo kwasababu Shirika la TANESCO lilishawalipa wakazi ambao walipitiwa na nguzo hizo tangu mwaka 1999.

  Aidha, Bwana Mwakabuku aliongeza kuwa, TANESCO kabla ya kupitisha nguzo katika maeneo ya makazi ama mashamba ya wananchi huwa wanawasiliana na uongozi wa eneo husika na kukubaliana na wananchi wenyewe ili waruhusiwe kupitisha ama kutopitisha nguzo za umeme, na ilipotokea wanakubaliwa basi fidia inalipwa kwa wakati na kwa kufuata utaratibu ikiwemo kufanya tathmini ya kutosha na kisha kuwalipa kwa wakati kulingana na matakwa ya Sheria.

  ‘’Wakati mwingine baadhi ya wananchi wamekuwa wasikivu kwa kukubali na kuruhusu kupitisha nguzo za umeme katika maeneo yao na tumekuwa tukiwalipa fidia, lakini kuna wengine wamekuwa wakifanya shughuli za kibinadamu ikiwemo ulimaji mazao chini ya laini za umeme kwa makusudi ili walipwe fidia pindi yakifyekwa, hawa wanakuwa wanavunja utaratibu ambao umewekwa na TANESCO kuwa, ndani ya mita thelathini kwa pande zote mbili ambazo laini zinapita hakutakiwi kufanyika shughuli yoyote ya makazi au maendeleo, hivyo katika ukaguzi wetu tunapofika na kukuta wamekiuka taratibu hizo tunazuia uendelezaji wa shughuli hizo na hasa kubwa likiwa ni suala la usalama wa mali na maisha yao wenyewe wananchi.’’, alisema Mwakabuku.

  Amewahasa wakazi nchini kote kuzingatia Sheria ya mita 60 kwa kutofanya shughuli zozote za kibinadamu chini ya nguzo za umeme kwa ajili ya usalama wa maisha yao kwani umeme upitao unakuwa ni wa msongo mkubwa hivyo unaweza kuhatarisha maisha yao endapo wanakaidi kufanya hivyo.


  ‘’Napenda kusisitiza kuwa, wananchi wazingatie na kuhakikisha kuwa hawafanyi shughuli zozote za kiuchumi au ujenzi wa makazi ndani ya eneo la mita 60 kutoka kilipo chanzo cha umeme ili kuondoa kero na madai kama haya’’, alisisitiza Mwakabuku.

  0 0

   Manamke ambaye jinalake halikupatikana mara moja akiwa amekaa juu ya paa la majengo ya Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es Salaam leo.
  Mwanamke huyo akizungumza na watu waliokusanyika ikiwa alikuwa hasikiki vizuri maneno aliyokua akiongea kutokana na wananchi waliokusanyika kumuuliza maswali mengi kwa wakati mmoja. 
  Polisi akiwa pembeni ya uzio wa majengo ya wizara ya fedha na mipango mara baada ya mwanamke huyo alipokuwa juu ya paa la nyumba hizo, ikiwa haikujulikana mwanamke huyo hatukujua anadhamira gani ya kupanda juu ya paa la majengo hayo. Baada ya muda wafanyakazi wa wizara hiyo kumwekea ngazi na kumshusha ili kumhoji zaidi nini kimemfanya apande juu ya paa la majengo hayo.

  0 0

  Meneja wa Mradi wa Kansa ya Shingo ya Kizazi wa UMMATI, Jeremiah Makula akizungumza wakati wa utoaji tuzo kwa wadau wa mradi wa kansa ya Shingo ya Kizazi iliyofanywa, PSI Tanzania, Marie Stopes pamoja na UMATI iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Kanda Kusini Mwa Afrika, Ulla Muller akizungumza wakati wa utoaji tuzo kwa wadau wa mradi wa kansa ya Shingo ya Kizazi iliyofanywa, PSI Tanzania, Marie Stopes pamoja na UMATI iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Kinga wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Neema Rusibamayilla akizungumza wakati wa utoaji tuzo kwa wadau wa mradi wa kansa ya Shingo ya Kizazi iliyofanywa, PSI Tanzania, Marie Stopes pamoja na UMATI iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Wakurugenzi wa Mashirika yaliyokuwa na Mradi wa Kansa ya Shingo ya Kizazi pamoja na wawakilishi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakifatilia maada wakati wa mkutano wa utoaji wa tunzo kwa wadau wa mradi iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya wadau wakifatilia maada wakati wa utoaji tunzo kwa mashirika yaliyokuwa katika mradi wa kansa ya Shingo ya Kizazi iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. 
  (Picha na Chalila Kibuda wa Globu ya Jamii). 

  Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii 
  WADAU wa wanaoshughulika na kansa ya shingo ya kizazi kwa wanawake ni wachache ikilinganishwa na mahitaji yaliyopo nchini kwa tatizo hilo. 

  Akizungumza katika mkutano wa wadau waliokuwa wakifanya Mradi wa Kansa ya Shingo ya Kizazi na Kinga kwa wanawake dhidi ya kansa hiyo, Mkurugenzi wa Kinga wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Neema Rusibamayilla amesema serikali inatambua juhudi za wadau ambao wamekuwa wakifanyia wanawake juu ya kinga ya kansa ya shingo ya kizazi. 

  Amesema serikali itaendelea kushirikiana wadau mbalimbali katika kukabili tatizo la kansa ya kizazi ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wanawake kujitokeza kupima afya zao na inapotokea na tatizo hilo kushughulikiwa kwa haraka. 

  Neema amesema serikali itaendelea kutoa ushirikiano zaidi kwa pale inapohitajika katika kukabili tatizo la kansa ya shingo ya kizazi kutokana na serikali peke yake haiwezi kushugulikia matatizo kwa wakati mmoja. 

  Nae Mkurugenzi Mtendaji wa UMATI, Lulu Ng’wanakilala amesema kansa ya kansa ya shingo ya kizazi inaua hivyo ni lazima wanawake kupima mara kwa mara kabla tatizo halijawa kuwa kubwa. 

  Amesema wadau wanaoshughulika na kansa hiyo ni wauchache ikilinanishwa na tatizo lilopo hasa katika maeneo ya vijijini ya kuwa na wanawake wengi ambao hawajafikiwa kwa kupima au kupata huduma hiyo. 

  Kwa upande wa Mkurugenzi Mkazi wa Marie Stopes ,Anil Tambay akiwakilisha wadau walikuwa katika mradi huo amesema mafanikio walioyapata katika mradi huo ni kwa kusaidia wanawake uhai katika utoaji wa tiba ya kansa ya shingo ya kizazi.

older | 1 | .... | 741 | 742 | (Page 743) | 744 | 745 | .... | 1897 | newer