Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

JIJI LA ARUSHA LAJIPANGA KUONDOA MAKAZI HOLELA

$
0
0

Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha,Calist Lazaro(kushoto)akiweka saini makubaliano kati ya Jiji la Arusha na kampuni ya Bondeni Seeds Limited yatakayowezesha eneo la Heka 750 kupimwa na kuwa kwenye mpango unaoendana mpango Mji wa Jiji katika eneo la Murieti wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Diwani wa Kata ya Ngarenaro,Isaya Doita,Mbunge wa Arusha Mjini,Goodbless Lema,Mwanasheria wa Jiji,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji,Juma Idd na Mwanasheria wa Bondeni Seeds Limited leo.

Meya wa Jiji la Arusha,Calist Lazaro(kushoto)akibadilishana hati za makubaliano na Mkurugenzi wa kampuni ya Bondeni Seeds Limited ,Rakesh Vohora ya kuendeleza eneo la Heka 750 eneo la Muriet linalomilikiwa na kampuni hiyo .

Meya wa Jiji la Arusha,Calist Lazaro akizungumza baada ya hafla kuweka saini makubaliano kati ya pande mbili.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Arusha,Juma Idd akifafanua umuhimu wa ushirikiano kati ya Jiji na kampuni hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Arusha,Juma Idd(kulia) akifafanua umuhimu wa ushirikiano kati ya Jiji na kampuni hiyo,kushoto ni Meya wa Jiji la Arusha,Calist Lazaro.

Diwani wa Kata ya Moshono ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango miji ya Jiji la Arusha,Metson Paul(kushoto) akiwa Mwanasheria na Mkurungezi wa kampuni ya Bondeni Seeds Limited.

Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini,Goodbless Lema akizungumza katika hafla hiyo.


…………………………………………………………………………………………………………….
Halmashauri ya Jiji la Arusha imesaini makubaliano na kampuni ya Bondeni Seeds Limited kupima eneo linalomilikiwa na kampuni hiyo lenye ukubwa wa Hekari 750 ili liwe sehemu ya Master Plan ya Jiji .

Meya wa Jiji la Arusha,Calist Lazaro amesema wameshawishika kuingia makubaliano hayo na mwekezaji huyo ili kuwezesha wananchi kuishi kwenye maeneo yaliyopimwa yanayoendana na hadhi ya Jiji na kulipatia mapato yanayotokana naupimaji huo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji,Juma Idd amesema wamekubaliana na mwenye eneo hilo kulipanga na kuliendeleza kama sheria ya makazi inavyotaka.

“Hatutaweza kuendelea na makazi ambayo hayajapimwa kama Unga Limited ,Ngarenaro na mengine ,Arusha ni eneo lenye umuhimu wake katika sekta ya utalii,madini na ukizingatia hapa ndio Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) na taasisi za kimataifa.

Amesema baada ya kusaini makubaliano utekelezaji unaanza mara moja ili kufikia malengo ya kuweka mji uliopangika.

Mbunge wa Arusha Mjini,Goodbless Lema amewataka wananchi wenye maeneo makubwa kushirikiana na uongozi wa Jiji ili maeneo yao yapimwe kuepusha makazi holela na kuwataka waliojenga maeneo ya mabondeni na kwenye vyanzo vya maji kubomoa nyumba zao.

Imeandaliwa na www.rweyemamuinfo.blogspot.com

KESI YA KUPINGA MATOKEO INAYOMKABILI MBUNGE WA JIMBO LA BUNDA MJINI MKOANI MARA YAAHILISHWA

$
0
0
Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza leo imeanza kusikiliza Kesi ya Kupinga Matokeo ya uchaguzi Mkuu uliofanyika Novemba 25 mwaka jana katika Jimbo la Bunda Mjini, Mkoani Mara ambapo Mgombea kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Esther Bulaya aliibuka mshindi.

Na:George Binagi-GB Pazzo
Jaji wa Mahakama hiyo Mhe.Mohamed Gwae ameahirisha kesi hiyo hadi jumatatu ijayo ya Januari 25 mwaka huu baada ya mawakili wa pande zote mbili kuchuana vikali kwa muda mrefu. 

Waleta maombi (Mlalamikaji) katika kesi hiyo wametajwa kuwa ni wapiga kura wa jimbo hilo la Bunda Mjini ambao walikuwa wakiiomba Mahakama kutengua matokeo ya uchaguzi huo katika jimbo hilo kutokana na uchaguzi huo kukumbwa na kasoro mbalimbali ikiwemo uchaguzi kutokuwa huru pamoja na idadi ya wapiga kura kutofautiana na idadi ya waliojiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.

Madai hayo yamepingwa na upande wa Mjibu Maombi (Walalamikiwa ambao ni Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini pamoja na Mwanzasheria wa Serikali) uliokuwa ukiongozwa na Wakili Tundu Lisu. Upande wa Mleta maombi ulikuwa ukiongozwa na Wakili Constantine Mutalemwa.

Kesi hiyo ilianza kusikilizwa majira ya saa tatu asubuhi na baadae kuahilishwa kwa ajili ya chakula cha mchana na kisha kuendelea kusikilizwa kuanzia majira ya saa nane mchana hadi majira ya saa kumi na moja jioni.
Wakili upande wa mjibu maombi Tundu Lisu (mwenye miwani) akizungumza baada ya Kesi hiyo kuahirishwa ambapo amesema hoja za waleta maombi hazina mashiko kwani katika hati yao ya madai hawajalalamika kuonesha kama haki yao imekiukwa hivyo ni vyema mahakama ikatupilia mbali maombi yao kwani yanaonyesha kuwa yanampigania Steven Wasira (aliekuwa mgombea ubunge kutoka CCM Steven Wasira) ambae hata hivyo hakuwemo mahakamani hapo.
Kushoto ni mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini Esther Bulaya.
Wakili Tundu Lisu (mwenye miwani) akizungumza baada ya Kesi hiyo kuahirishwa
Wakili upande wa mleta maombi, Constantine Mutalemwa (mwenye miwani) akizungumza baada ya kesi hiyo kuahilishwa ambapo amesema kuwa waleta maombi wanasubiri maamuzi yatakayotolewa na mahakama hiyo baada ya hii leo kuahirishwa.
Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini Esther Bulaya (Chadema)

CHINA YATOA MAPENDEKEZO YA 13 KUKUA KWA UCHUMI NA KIJAMII

$
0
0
 Mchambuzi  wa masuala ya Siasa   na Taluma  za Jamii  na Naibu Mkurugenzi  wa Kamati ya Maendeleo  ya Jamii katika Wizara  ya Elimu nchini China, Gu Hailiang,akihutubia wajumbe waliohudhuria mkutano ambao Chama cha Kikomunisti cha Watu wa China kilibainisha mapendekezo ya 13 ya mpango wa miaka 5 ya maendeleo ya uchumi na kijamii, kwenye hoteli ya Dar es Salaam Serena.
  Mchambuzi  wa masuala ya Siasa   na Taluma  za Jamii  na Naibu Mkurugenzi  wa Kamati ya Maendeleo  ya Jamii katika Wizara  ya Elimu nchini China, Gu Hailiang, akihutubia kwenye mkutano wa kuelezea mpango wa miaka mitano ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwenye hoteli ya Dar es Salaam Serena, wengine pichani  waliokaa meza kuu kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano Ubalozi wa China,Ndugu Zhang Biao ,Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Ramadhani Madabida, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kukuza Urafiki kati ya Tanzania na China  Ndugu Kahama.
 Sehemu ya wajumbe walioshiriki mkutano huo ambao ulihusisha Wahadhiri wa Vyuo vikuu na wanafunzi,shirikisho la vyuo vikuu pamoja na waandishi wa habari na ujumbe kutoka chama cha Kikomunisti cha China.


Waziri Nape afanya ziara katika Kituo cha Michezo cha Jakaya Mrisho Kikwete Sports Park

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (wa tatu kutoka kushoto) akimsikiliza kwa makini Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Alibino Tanzania Bw. Josephat Tomer wakati wa ziara maalumu ya kutembelea Kituo cha michezo cha Jakaya Kikwete Sports Park na kushiriki siku ya Albino Tanzania iliyoratibiwa na Kituo hicho kwa ushirikiana na Chama cha Albino Tanzania.Kutoka kushoto ni Mkuu wa Utawala na Uendeshaji wa Kituo hicho Bw. Richard Mtui, Afisa Mtendaji Mkuu wa Syjmbion Power Bw. Paul Hinks na Mkufunzi wa Michezo katika Kituo hicho Bw. Ray Power.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza wakati wa ziara maalumu ya kutembelea Kituo cha michezo cha Jakaya Kikwete Sports Park na kushiriki siku ya Albino Tanzania iliyoratibiwa na Kituo hicho kwa ushirikiana na Chama cha Albino Tanzania.Kutoka kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Symbion Power Bw. Paul Hinks, Mkufunzi wa Michezo katika Kituo hicho Bw. Ray Power na Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Alibino Tanzania Bw. Josephat Tomer.

Taarifa ya urejeshaji wa fomu za Tamko la rasilimali na madeni kwa viongozi wa umma na ahadi ya uadilifu

$
0
0


 
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS, SEKRETARIETI YA MAADILI YA
VIONGOZI WA UMMA
   

        
   
 TAARIFA KWA UMMA
 
 
        Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma inawafahamisha Viongozi wa Umma wanaowajibika na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya Mwaka 1995 kwamba tarehe ya mwisho wa urejeshaji wa Fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni ilikuwa ni tarehe 31 Desemba, 2015.

         Hadi kufikia Disemba 31,2015 jumla ya Viongozi                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                     11,428 tu wamerejesha matamko yao kwa Kamishna wa Maadili na Viongozi 3709 hawajatimiza wajibu huo wa kisheria na hivyo kukiuka Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya Mwaka 1995 yanayowataka viongozi kurejesha fomu hizo katika muda uliowekwa kwa mujibu wa sheria na hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mbele ya Baraza la Maadili, iwapo sababu za kuridhisha juu ya ukiukwaji huo wa sheria hazitatolewa kwa Kamishna wa Maadili.
 

        Serikali pia imeanzisha utaratibu wa kutia saini Fomu ya Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wote na Watumishi wote wa Umma ambao wako katika mihimili mitatu (3) inayounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yaani Serikali, Bunge na Mahakama.

        Viongozi wote wanaowajibika na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya Mwaka 1995 wanatakiwa kutia saini Tamko la Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma na kurejesha kwa Kamishna wa Maadili kabla ya tarehe ya mwisho  ambayo ni tarehe 28 Februari, 2016. Wakuu wa Wizara, Taasisi na Idara au sehemu husika wahakikishe Viongozi waliopo sehemu zao wanatia saini katika tamko hilo.

        Kwa kuzingatia Misingi ya Maadili iliyoainishwa katika Ibara ya 132 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya mwaka 1995 Viongozi wa Umma wanapaswa kuzingatia viwango vya juu vya Maadili, uzingatiaji wa maadili utakuza  utu, uwazi, uadilifu, uwajibikaji, maendeleo ya nchi na kuimarisha imani ya wananchi kuhusu dhana ya Utawala Bora kwa ujumla.

Jaji (Mst.) Salome S. Kaganda
KAMISHNA WA MAADILI

BENKI YA WANAWAKE YATAKIWA KUWAWEZESHA KIUCHUMI NA KIELIMU WANAWAKE

$
0
0
Na.Catherine Sungura-WAMJW.
 
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu, ameitaka Bodi na Watendaji wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB), kuhakikisha kuwa inawawezesha wanawake kiuchumi kwa kufikisha huduma hiyo mbali zaidi ili kuifanya benki kuwa kimbilio la wanawake kweli . 
 
Akizungumza katika ziara yake ya mafunzo katika benki hiyo akifuatana na Naibu wake waziri Dakta HAMISI KIGWANGA, Katibu mkuu na watendaji wa Wizara hiyo UMMY alisema wanawake wa Tanzania wanajitoa sana katika kulea familia hivyo wakiwezeshwa watakuwa wamewezesha familia, vijana na Taifa kwa ujumla.
 
Waziri huyo alisema   watendaji wa benki hiyo ya wanapaswa kuweka utaratibu mzuri wa utoaji wa huduma ambazo zitaweka fikra za wanawake pale wanapotaka kuchukua mikopo au kuweka fedha zao katika benki kufikiria kwanza benki ya TWB.
 
“Mimi huwa naona uwezeshaji wa kweli wa wanawake ni kuhakikisha kuwa tunawawezesha kiuchumi na kielimu kwasababu mwanamke atashiriki kulima kupanda lakini ikifika kuvuna tu mazao sio yake hivyo endapo tutapata fedha zinazohusu mfuko wa wanawake Serikalini tutaomba zipitishwe kwenye Benki ya Wanawake na tutakwenda kila Halmashauri kuanzisha saccos za wanawake ili waweze kupata fedha za kukopeshwa na benki ya wanawake,’’alisema Ummy.
 
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Hamisi  Kigwangalla amesema benki nyingi zilizopo hapa nchini hivi sasa hazimilikiwi na Serikali hivyo, TWB inapaswa kuhakikisha kuwa inaweka mipango yake sawa ili iweze kubaki Serikalini kwani lengo la kuanzishwa kwa benki hiyo ni kuleta ukombozi wa kiuchumi wa wakinamama kwani mama ni mlezi mkubwa wa familia.
 
Awali Mwenyekiti wa bodi wa benki hiyo Mohamed  Nyasanaamesema tangu benki hiyo inakabiliwa na ukosefu wa umiliki wa jengo ambapo tangu kuanzishwa kwake mwaka 2009 wamelipa kodi ya pango shilingi bilioni mbili ambapo kila mwaka hulipa shilingi milioni 500 (mia tano).
 
Aliongeza kwamba pamoja na changamoto hiyo ya kodi kubwa ya pango benki hiyo imefanikiwa kukuza mtaji wake kutoka shilingi bilioni mbili nukta nane hadi shilingi bilioni nane nukta tano ikiwa na wanahisa 164 huku mwanahisa mkuu akiwa msajili wa hazina ambaye anamiliki asilimi 99 ya hisa.
 
Amebainisha kuwa hivi sasa inawateja elfu 56, asilimia 77 wakiwa wanawake na asilimia 23 wakiwa wanaume na wateja wa kampuni wakiwa asilimia tatu.Pia  benki hiyo ina matawi mawili Mkwepu na Kariakoo vituo vya huduma sita Dodoma, Mwanza, Njombe, Ruvuma na Iringa. 
 
Naye Mkurugenzi wa benki hiyo Magreth Chacha  ameiomba Serikali kuwasaidia kupata fedha maalum ili waweze kukopesha wanawake wengi zaidi kwani kwa hivi sasa TWB inauwezo wa kukusanya shilingi bilioni saba kila mwaka.

DIWANI AFARIKI DUNIA MUFINDI

$
0
0
Diwani wa kata ya Igombavanu iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa Mh. HABIBU KILONGE amefariki Dunia katika hospitali ya wilaya ya Mufindi usiku wa kuamkia leo ilikokuwa amelazwa kwa matibabu.

Taarifa ya mwenyekiti wa Halmsahauri ya Wilaya ya Mufindi Mh. FESTO MGINA kupitia kitengo cha habari na mawasiliano cha Halmashauri ya Wilaya, ameeleza kuwa, marehemu amefarikia baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa takribani mwezi mmoja na mara kadhaa alikuwa akitibiwa katika hospitali ya Wilaya na kurejea nyumbani.

Aidha, amebainisha ratiba ya shughuli za maziko kuwa marehemu atazikwa Jumapili ya Tarehe 17 ambapo mapema asubuhi ya saa mbili mwili wa marehemu utaondolewa katika Hospitali ya Wilaya Mafinga na kupekwa katika kata ya Igombavanu ambakoa utaagwa na wapiga kura wake na itakapofika saa tano asubuhi mwili huo utasafirishwa kwenda Kijiji cha kichiwa Mtwango Mkoani Njombe ambako ndiko mwili huo utazikwa.

Marehemu Diwani HABIBU KILONGE alichaguliwa kwa mara ya kwanza na wananchi wa Kata ya Igombavanu kupiti atiketi ya chama cha Mapinduzi CCM katika uchaguzi Mkuu uliyofanyika mapema mwezi wa 10 mwaka jana kwa jumla ya kura Elfu 2 na 34 ikiwa ni ushindi mkubwa dhidi ya mpinzani wake wa karibu kutoka chama cha Chadema aliyepata kura 361 na mpaka mauti inakuta diwani huyo alikuwa amehudhuria kikao kimoja pekee, ambacho kilikuwa maalu kwa kuapishwa.

UKAWA WASHINDA KITI CHA UMEYA MANISPAA YA ILALA.

$
0
0
Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kwiyeko akizungumza na madiwa wa Manispaa ya Ilala leo mara bada ya kushinda  kwa Kura 31 katika uchaguzi wa meya wa manispaa hiyo katika ukumbi wa Karimjee leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Salum Kumbilamoto  akiwashukuru madiwani waliompigia kura leo mara ya kuibuka kidedea katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee leo jijini Dar es Salaam.




Baadhi ya  wapiga kura wakipiga kura za Meya na Naibu leo katika uchaguzi  wa kuwapata viongozi hao wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.

Matokeo ya Meya na Naibu Meya yakujumlishwa na baadhi ya wajumbe wa Meya,naibu Maya  wakiwa na Mwanasheria wao leo mara baada ya kumaliza kugika kura katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee leo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya viongozi wakiwa kwenye ukumbi wa Karimjee leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mgurumi akitangaza matokeo ya Umeya na Unaibu Meya katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
Wananchi wakishangilia ushindi wa Maya na Naibu Meya mara baada ya kutangazwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mgurumi jijini Dar es Salaam leo.
 Kutoka kushoto ni  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mgurumi wakiteta jambo na Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kwiyeko leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kushinda katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee. 
Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kwiyeko akizungumza na kuwashukuru madiwani leo jijinin Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

Article 1

WANAFUNZI 538 WATUNUKIWA VYETI VYAO KATIKA MAHAFALI YA NANE YA CHUO CHA TRA LEO JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
WANAFUNZI 538 wa chuo cha Mamlaka ya Mapato (TRA) wametunukiwa vyeti vyao leo katika mahafali ya nane ya chuo hicho yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.

Pia wahitimu hao wameaswa kuwa waadilifu katika kazi zao kwani taaluma yao ni ukusanyaji wa mapato ya sehemu zao za kazi.

Wameaswa hayo na  Naibu waziri wa Fedha na Mipamgo, Ashatu Kijaji wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa mahafali ya nane ya chuo cha Mamlaka ya Mapato (TRA) yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere.

amesema kuwa wahitimu wa chuo hicho wafanye kazi kwa weredi na uaminifu  kwani wasipofanya hiyo hawataweza kufanya kazi hayo vile inavyopaswa.

Chuo cha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kitajengwa kingine huko  kibaha mkoani pwani ili kuongeza wanafunzi kusoma katika mazingira mazuri kwani chuo kilichopo Mwenge kimezungukwa na viwanda.




 Naibu waziri wa Fedha na Mipamgo, Ashatu Kijaji akizumgumza na wahitimu wa chuo cha Mamlaka ya mapato Tanzania TRA leo katika mahafali ya nane ya chuo hicho yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere leo jijini Dar es Salaam




 Baadhi ya wahitimu wa chuo cha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakiwa katika mahafali ya nane ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Makamu Mkuu wa Chuo, Lewis Ishemoi akiwaita majina wanafunzi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) leo katika mahafali ya nane ya chuo hicho ikiwa wahitimu 538 wamehitimu mafunzo yao katika chuo hicho jijini Dar es Salaam leo.Wanafunzi wakivaa kofia zao mara baada ya kutunukiwa katika mahafali yaliyofanika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.


 Naibu waziri wa Fedha na Mipamgo, Ashatu Kijaji akiwatunukia vyeti wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yao katika mahafali yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.


 Wahadhiri wakiwitunukiwa vyeti pamoja na zawadi mbalimbali katika mahafali ya nane ya chuo cha mamlaka ya mapato (TRA) leo jijini Dar es Salaam. kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Alphayo Kidata na Makamu Mkuu wa Chuo, Lewis Ishemoi.

Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

WAZIRI NAPE AKUTANA NA BALOZI WA ISRAEL NCHINI NA KUKUBALIANA KUSHIRIKIANA KATIKA SEKTA ZA HABARI NA UTAMADUNI

$
0
0

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye(kulia) akifurahia jambo na Balozi wa Israel nchini Tanzania Bw.Yahel Vilan alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam.Katika maongezo yao wamekubaliana kuimarisha ushirikiano uliokuwepo na kuangalia sehemu zaidi za kushirikiana katika sekta za Habari na Utamaduni.
Balozi wa Israel nchini Tanzania Bw.Yahel Vilan(kushoto) akimpongeza Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe,Nape Nnauye(kulia) kwa kuchaguliwa kuwa Waziri pamoja na kumpatia zawadi ya kitabu na kikombe kutoka Israel alipomtembelea leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe,Nape Nnauye(kushoto) akimkaribisha ofisini kwake Balozi wa Israel nchini Tanzania Bw.Yahel Vilan(kulia) alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro wajipanga kuwatumikia wananchi waliowachagua

$
0
0
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Albert Msole akizungumza kwenye baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo kushoto ni Mkuu wa wilaya hiyo Mahmoud Kambona na kulia ni Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Jackson Lesikar Sipitieck.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Jackson Lesikar Sipitieck na Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Albert Msole wakifuatilia kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika mji mdogo wa Orkesumet
Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wakifuatilia kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika mji mdogo wa Orkesumet.Picha na Joseph Lyimo - Globu ya Jamii, Manyara.

HATUA AMBAZO ZIMECHUKULIWA DHIDI YA STANBIC BANK TANZANIA LIMITED KUHUSU USHIRIKI WAKE KUWEZESHA MKOPO WA SERIKALI WA DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI 600

$
0
0

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Philip Mpango (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawamo pichani)jijini Dar es Salaam, kuhusu hatua zilizochukuliwa na Serikali dhidi ya Benki ya Stanbic Tanzania kutokana na ushiriki wake katika kuwezesha mkopo wa Serikali wa Dola za Kimarekani Milioni 600 na Kulia kwake ni Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania(BOT) Bw. Lila Mkila.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Philip Mpango (katikati) akitoa tamko kwa waandishi wa habari (hawamo pichani) jijini Dar es Salaam, kuhusiana na kusudio la kuitoza Benki ya Stanbic faini ya shilingi bilioni 3. Kulia kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servicius Likwelile na Kushoto kwake ni Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Bw. Lila Mkila.

………………

Utangulizi

Mwezi Julai 2013, Benki Kuu ya Tanzania kupitia ufuatiliaji wa kawaida wa shughuli za mabenki iligundua matatizo yaliyohusiana na hasara itokanayo na mikopo na pia kuacha na kuondolewa kazini kwa viongozi waandamizi wa Stanbic Bank Tanzania Limited (Stanbic) katika muda mfupi. Kutokana na hilo, Benki Kuu iliamua kufanya ukaguzi wa kulenga (Targeted Examination) katika benki hiyo. Ukaguzi huo ni kwa mujibu wa mamlaka iliyopewa Benki Kuu chini ya Kifungu 47 cha Sheria ya Benki Kuu ya mwaka 2006 na Kifungu 31 cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006.

Matokeo ya Ukaguzi wa Benki Kuu

Katika ukaguzi huo, wakaguzi wa Benki Kuu, pamoja na mambo mengine walibaini miamala ya kutia shaka iliyohusu malipo kwa kampuni ya kitanzania ya Enterprise Growth Market Advisors (EGMA). Kampuni ya EGMA ilihusika katika uwezeshaji wa upatikanaji wa Mkopo kwa Serikali ya Tanzania ambapo Standard Bank Plc (ambayo kwa sasa inajulikana kama ICBC Standard Bank) na Stanbic Bank Tanzania Limited kwa pamoja walikuwa “Mwezeshaji Mkuu” (Lead Arranger). Malipo hayo kwa kampuni ya EGMA yalikuwa yamefanyika kinyume na taratibu za kibenki na yalihusisha uongozi wa benki ya Stanbic. Jumla ya malipo yalikuwa ni kiasi cha dola za kimarekani milioni 6, na zililipwa katika akaunti ya EGMA na kutolewa kwa muda mfupi kwa njia ya fedha taslimu (cash) ambayo ni nje ya taratibu za kibenki.

Taarifa ya ukaguzi huo iliwasilishwa kwa benki ya Stanbic kwa mujibu wa taratibu, na Benki Kuu iliiagiza Bodi ya Wakurugenzi ya benki hiyo kuchukua hatua stahiki za kurekebisha kasoro zilizoonekana. Aidha, benki ya Stanbic iliagizwa kutoa taarifa kwa Kitengo cha Financial Intelligence Unit (FIU) kilichopo Wizara ya Fedha na Mipango kuhusiana na miamala hiyo yenye mashaka katika akaunti ya EGMA kama Sheria ya Kuzuia Utakatishaji wa Fedha Haramu ya mwaka 2006 (The Anti-Money Laundering Act, 2006) inavyoelekeza. Benki ya Stanbic ilitekeleza maagizo na kutoa taarifa FIU kuhusu miamala inayotiliwa shaka.

Mnamo 29 Septemba 2015, Benki Kuu ilipokea barua toka Idara ya Serikali ya Uingereza inayohusika na Upelelezi wa Makosa ya Kugushi na Rushwa (Serious Fraud Office – SFO) ikiiomba Benki Kuu ruhusa ya kutumia ripoti yake ya ukaguzi kama ushahidi katika kesi dhidi ya Standard Bank Plc ambayo ilikuwa ni mshirika wa Stanbic Bank Tanzania Limited katika kuwezesha mkopo wa dola za kimarekani milioni 600 kwa Serikali na kwamba ripoti hiyo ingekuwa wazi kwa umma. Benki Kuu iliijibu SFO kuwa kwa mujibu wa Sheria ripoti za Benki Kuu zinatolewa tu kwa benki au taasisi ya fedha inayohusika, hata hivyo, Benki Kuu haikuwa na pingamizi kwa SFO kutumia taarifa za ripoti hiyo kwa kuzingatia chanzo cha ripoti hiyo.

Hatimaye, Standard Bank Plc ilikubali makosa na ilitozwa faini ya jumla ya dola za kimarekani milioni 32.20, ambapo kiasi cha dola za kimarekani milioni 7 zinalipwa kwa Serikali ya Tanzania (dola za kimarekani milioni 6 zilikuwa ni fidia na dola za kimarekani milioni 1 ni riba).

Kwa kuzingatia mapungufu ya kufanya miamala iliyohusisha EGMA na pia kutokuweka taratibu madhubuti za udhibiti wa ndani, na kwa kuzingatia Kifungu 67 cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006, Benki Kuu imeiandikia benki ya Stanbic barua ya kusudio la kuitoza faini ya shilingi bilioni 3. Sheria inaitaka benki ya Stanbic kutoa utetezi katika kipindi cha siku ishirini (20) ambacho kitaisha tarehe 30 Januari 2016. Endapo Benki Kuu haitaridhika na utetezi, benki ya Stanbic italazimika kulipa faini hiyo.

Hitimisho

Benki Kuu imechukua hatua hizo kama onyo kwa benki ya Stanbic na ili iweze kuwa makini katika kuhakikisha kuwa shughuli zake zinaendeshwa kwa mujibu wa taratibu za kibenki na kuzingatia Sheria.

Aidha, hatua hii ni onyo kwa mabenki na taasisi za fedha zisijihusishe na makosa ya aina hii ambayo ni kinyume cha taratibu za kibenki na ni uvunjaji wa Sheria za nchi. Hatua kali zitaendelea kuchukuliwa kwa benki au taasisi ya fedha yoyote itakayobainika kwenda kinyume na taratibu za kibenki na Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006.

DAWASCO YABAINI WIZI WA MAJI KIWANDA CHA BAHARI CHEMICALS LTD

$
0
0

Moja ya kisima kinachodaiwa kutumika kuhifadhi maji yanayodaiwa kuibwa kutoka katika mtandao wa maji wa Dawasco.
Madumu ya Maji ambayo yame3kuwa yakitumika katka utengezaji wa maji ya Betri katika kiwanda cha Bahari Chemicals Ltd .
Sehemu ya wizi wa maji kutoka katika mtandao wa DAWASCO unavyoone3kana kufanywa katika kiwanda cha kutengenezea Betri cha Bahari Chemicals Ltd.

……………………………………………..
Ikiwa siku chache tu zimepita baada ya shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (Dawasco) kubaini wizi mkubwa wa Maji kutumika katika shamba la mboga mboga na matunda katika chuo cha Islamic kilichopo Boko ununio jijini Dar es salaam. Dawasco imebaini wizi mwingine wa Maji katika kiwanda cha kutengeneza Maji ya betri cha Bahari Chemicals Ltd kilichopo kurasini wilaya ya Temeke jijini Dar
es salaam.

Akizungumzia tukio hilo meneja wa Dawasco Temeke, Bw. Deogratius Rwegasira, amethibitisha kutokea kwa wizi huo ambapo kiwanda hicho kilikuwa kimejiunganishia Maji bila kibali cha Dawasco na kwamba hawakuwa na mita wala akaunti namba inayoonyesha
kiasi cha Maji kinachopita katika system ya Maji iliyopo, na baada ya kufanya mawasiliano na Mkurugenzi wa kiwanda hicho Bw.Devendra Singh Parmar amekiri kutumia Maji hayo kinyume na taratibu .

“Baada ya kufanya uchunguzi tumebaini kuwa kiwanda hiki kimekuwa kikituibia Maji yetu kwa muda mrefu, mmiliki wa kiwanda amekubali kosa,lakini akisema kwamba wenyewe ni wageni hapa hawana zaidi ya mwaka mmoja tangu waanze kazi.hivyo hawakujua
taratibu za kufuata”. Alisema Bw. Rwegasira.

Aidha meneja wa kiwanda hicho, Bw. Abdul Gulam, amekiri kuihujumu Dawasco kwa kuiibia Maji, lakini amesema kuwa wao ni wapangaji tu wamepanga katika eneo hilo na wana muda wa miezi saba tangu wahamie kiwandani hapo, walikuta wizi huo wa Maji ukifanyika katika kiwanda hicho na hawakujua taratibu husika za kufuata ili wapate huduma ya Maji kihalali.

“Sisi tumekubali kuwa tulikuwa tunatumia Maji ya DAWASCO bila kuyalipia, lakini sio sisi ambao tuliounganisha bomba hili, wapangaji waliopita walijiunganishia Maji haya hivyo tunaomba tulimalize hili, ili tuanze kuwa wateja wenu rasmi” alisema Bw.Gulam.

Aidha bwn Gulam ameainisha kuwa wao kama wamiliki wa kiwanda wamekubali kulipa faini iliyotolewa na DAWASCO ya Shiling million 3.5 ili warudishiwe huduma kama wateja wengine na waweze kuendelea na biashara.Vitendo vya uhujumu wa Miundombinu ya Maji hususani wizi wa Maji unaendelea kuwa changamoto kwa DAWASCO licha ya kampeni na elimu inayotolewa kila siku juu ya uhalali na utaratibu wa kuungiwa huduma ya Maji inayotolewa na DAWASCO.

Imeandaliwa na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii.

HAKUNA ATAKAYEBOMOLEWA NYUMBA ALIYEJENGA KATIKA UMBALI UNAORUHUSIWA KISHERIA -KALUA

$
0
0
Na Skolastika Tweneshe-MAELEZO
Mbunge wa Jimbo la Segerea kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Mh. Bonna Kalua amesema kuwa hakuna nyumba ya mwananchi itakayobomolewa ambayo imejengwa katika umbali unaohitaji
kisheria wa mita 60 kutoka mtoni.

Mh.Kalua alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es salaam wakati akizungumza na wananchi wa Karakata kwenye mkutano wa hadhara.Aidha alitoa wito kwa wale ambao wamejenga ndani ya mita 60 na nyumba zao zimewekewa X kujiorodhesha majina yao kwa wenyeviti wa mitaa ili wamfikishiea Ofisi kwake kwa ajili ya kulifuatilia jambo hilo kwa ukaribu na hatimaye wapate haki zao.

Mh.Bonna aliwatahadharisha wananchi kutodanganywa na watu wanaowachangisha fedha kwa kigezo cha kufungua kesi mahakamani kuwa ni uongo na hawana nia nzuri kwa wananchi kwa sababu kesi ya bomoa bomoa tayari ilishafunguliwa kwa niaba ya nchi nzima.Aliwataka wananchi kuwa wavumilivu mpaka hapo shauri lilipo mahakamani litakapotolewa tamko .

SHEREHE YA WAFANYAKAZI WA GAZETI LA JAMBO LEO YA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA 2016

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jambo Concepts, Juma Pinto  (kushoto), akimuelezea Mpiga Picha Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, Richard Mwaikenda kuwa wakati gazeti la Jambo Leo lilipoanzishwa 2009, alikuwa mfanyakazi wa kwanza kujiunga na gazeti hilo akitokea Kampuni ya Business Times.
 Baadhi ya wafanyakazi wa  Gazeti la Jambo Leo na familia zao, wakigongeana glasi zenye vinywaji ikiwa ni ishara ya kutakiana heri wakati wa hafla ya kuuaga mwaka 2015 na kuukaribisha ya Mwaka Mpya 2016, katika Mgahawa wa City Sports Lounge, Dar es Salaam
 Wafanyakazi wa Jambo Leo na familia zao pamoja na wageni waalikwa wakiburudika kwa muziki uliokuwa ukiporomoshwa wakati wa hafla hiyo iliyofanyika kwenye Mgahawa wa kisasa wa City Sports Lounge, katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

SERIKALI YALIFUTA GAZETI LA MAWIO

$
0
0



Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (mwenye suti ya kijivu) akiwaeleza Waandishi wa Habari (hawapo pichani) juu ya Uamuzi wa Serikali wa kulifuta Gazeti la MAWIO katika Daftari la Msajili wa Magazeti mara alipokutana na waandishi hao 17 Januari 2016 katika Ukumbi wa Idara ya Habari uliopo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Bw. Assah Mwambene, wa pili kulia ni Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia usajili wa Magazeti, Bw. Raphael Hokororo.

Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia taarifa ya Serikali toka kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (hayupo pichani) juu ya Uamuzi wa Serikali wa kulifuta Gazeti la MAWIO katika Daftari la Msajili wa Magazeti mara alipokutana na waandishi hao 17 Januari 2016 katika Ukumbi wa Idara ya Habari uliopo jijini Dar es Salaam.PICHA NA MICHUZI JR-MMG.



SERIKALI  YALIFUTA GAZETI LA MAWIO

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeamua kulifuta kutoka katika Daftari la usajili wa magazeti, gazeti lijulikanalo kama “MAWIO”. Amri ya kulifuta Gazeti hilo imetolewa kwa Tangazo la Serikali Na. 55 lililotolewa tarehe 15 Januari, 2016. Uamuzi huo umetolewa kwa mjibu wa Sheria ya Magazeti Sura ya 229, kifungu 25(1).


Hatua hii pia inazuia gazeti la Mawio kuchapishwa katika njia nyingine yoyote ikiwa ni pamoja na mitandao (Online publication) kwa mujibu wa Sheria ya Mawasiliano ya Kieletroniki na Posta Sura ya 306.



Serikali kwa masikitiko makubwa, imechukua uamuzi huu kutokana na mwenendo wa uandishi wa gazeti hilo usioridhisha wa kuandika na kuchapisha habari zenye mwelekeo wa uchochezi na kuhatarisha amani, utulivu na usalama wa nchi yetu.


Aidha, hatua hii ya kulifuta gazeti hilo imechukuliwa baada ya Msajili wa Magazeti kufanya juhudi kubwa za muda mrefu kuanzia Juni, 2013 hadi Januari,  2016  kumtaka Mhariri wa gazeti hilo kubadili aina ya uandishi wa habari na makala katika gazeti lake, bila mafanikio.


Msajili wa magazeti kwa juhudi zake alifanya mawasiliano na mhariri wa gazeti hilo mara nane kwa lengo la kutaka afanye marekebisho ya  mtindo wa kutoa habari zake lakini mhariri wa gazeti hilo hakuzingatia ushauri mzuri aliopewa na Msajili wa Magazeti.


Ninatoa wito kwa wamiliki, wahariri, waandishi na watangazaji wa habari kuzingatia sheria, Kanuni na taratibu za taaluma ya uandishi wa habari ambazo zikizingatiwa hakutakuwa na migogoro yoyote. Aidha Serikali inasisitiza kwamba inaheshimu uhuru wa vyombo vya habari unaozingatia maadili, weledi na Sheria za nchi na kwamba Serikali itaendelea kushirikiana navyo


Kwa upande mwingine ninatoa pongezi kwa vyombo vyote vya habari nchini vinavyozingatia maadili, weledi na Sheria zinazosimamia taaluma ya habari na sheria nyingine za nchi.  Kwa namna ya pekee Serikali inawapongeza wamiliki na wahariri wa vyombo vya habari ambavyo vinapofanya makosa vikielekezwa hujirekebisha na kutoa ushirikiano kwa Serikali na pia kubadili mwenendo wao; hawa ni pamoja  na wahariri wa magazeti ya;

·        Mwananchi Tanzania

·        Mtanzania

·        The East African

·        Magazeti ya Daily News na Habari Leo

·        Uhuru na mengineyo


Ninapenda  kusisitiza kwamba Serikali inapenda kujenga uhusiano mzuri na wa kirafiki kati yake na wadau wa sekta ya habari. Aidha ninasisitiza tena wadau wa sekta hii kuzingatia Sheria ili kujenga heshima ya tasnia ya habari na kulinda amani ya nchi yetu.

  
  
Imetolewa na Nape M. Nnauye(Mb,)

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo



Dar es Salaam, leo tarehe 17 Januari, 2016

BREAKING NEWZZZZZZZ; Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) afariki dunia

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman Said amefariki dunia mapema leo asubuhi akiwa katika mazoezi ya kuogelea,taarifa zinaeleza kuwa baada ya tukio hilo Bwa.Suleiman alikimbizwa hospitali ya Agakhan kwa matibabu,na baadae ikaelezwa kuwa amekwishafariki na kuwa mazishi yanatarajiwa kufanyika leo. Marehemu alipata kuwa Katibu mkuu wa Simba alikopewa jina la Yelstin.Taarifa zaidi tutazidi kufahamishana kadiri ya zikavyokuwa zikiingia.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMEN.

JANET MWENDA NA MARAFIKI ZAKE WA "MENTORING AND NETWORKING" WATOA MSAADA KWA KITUO CHA WATOTO WETU TANZANIA

$
0
0
Bi. Janet Sosthenes Mwenda (wa pili kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi wa kituo cha Watoto Wetu Tanzania, Bw. Evans Tegete moja ya vitu vilivyowasilishwa kwenye kituo hicho ndoo ya sabuni ya unga. Kushoto ni Muhamasishaji na mchangishaji fedha wa “Mentoring and Networking”, Bi. Mary Sanga na wengine wanaoshuhudia ni watoto wa kituo hicho. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).


Mmiliki na Mwendeshaji wa kipindi cha ‘Ongea na Janet’ Bi. Janet Sosthenes Mwenda ambaye pia ni mmiliki wa programu maalum ya vipindi vya watoto katika kutoa elimu katika televisheni kiitwacho ‘Tuwalinde Watoto Wetu’ kwa kushirikiana na marafiki zake wa kundi la “Mentoring and Networking” kupitia mitandao ya kijamii wametoa misaada mbalimbali ya vyakula na vinywaji kwa kituo cha Watoto Wetu Tanzania.

Akizungumza wakati wa kutoa misaada hiyo mapema jana 17 Januari, wakati wa tukio hilo lililofanyika kwenye kituo hicho kilichopo Kimara jijini Dar es Salaam, Janet Mwenda ambaye aliambatana na baadhi ya marafiki zake hao wa “Mentoring and Networking” wameweza kutoa misaada hiyo ya vyakula, vinywaji ambavyo vitasaidia kituo hicho.

“Kwa kuja hapa kutoa msaada huu ni kutokana na kuguswa na hali ya watoto wanaolelewa hapa na kwingineko kote. Naamini msaada huu utasaidia watoto wetu hapa kituoni naamini kwa hiki kidogo kitasaidia kwa siku kadhaa” alieleza Janet Mwenda.

Janet Mwenda ameongeza kuwa, amekuwa akifikiria zaidi kutoa misaada hivyo kufika hapo ni kutokana na kuguswa kwake kwa muda mrefu na amekuwa pia akitembelea kituo hicho kipindi cha nyuma hivyo kuwa miongoni mwa wanafamilia.

WAWILI WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA UUZAJI WA MADAWA YA KULEVYA.

$
0
0
Na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
JESHI la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam yawafikisha mahakamani watuhumiwa wawili wanaotuhumiwa kwa uuzaji wa madawa ya kulevya hapa nchini na biashara haramu ya binadamu.

Watuhumiwa hao ni Mohamed Abdalla Omari miaka 37 mfanyabiashara na mkazi wa Tegeta Nyuki jijini Dar es Salaam, anatuhumiwa kwa kusafirisha madawa ya kulevya na usafirishaji haramu wa binadamu anatuhumiwa kwa kumsafirisha Mwinyi Mgobanya na kumweka rehani (Bond) huko Pakistani kisha kuchukua madawa ya kulevya kwa mali kauli na Nassoro Suleiman miaka 35 Meneja wa Tungwe Bureau De Change katika jengo la IPS jijini Dar es Salaam, anayetuhumiwa kwa kusa la kushiriki katika genge la wauza madawa ya kulevya na kusafirisha kiasi kikubwa cha pesa kwa njia ambazo si rasmi.

Hayo yamesemwa na Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi (DCP), Kamanda wa Polisi Kanda Maalum  ya Dar es Salaam, Simon Sirro
 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Makao makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam leo.

Pia Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam wamekamata magari na Pikipiki 24,068 na kutoza faini ya shilingi 722,040,000 katika Operesheni ya kukamata madereva wa magari na Pikipiki wanaovunja sheria za usalama barabarani, ikiwa  J
eshi  hilo halina lengo la kukusanya kiasi kikubwa cha fedha bali kuona watanzania wanatii sheria za usalama barabarani wakati wote wanapokuwa na vyombo vya moto.

Aidha Jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata waharifu sugu sita  kwa unyang'anyi wa kutumia silaha katika maeneo mbalimbali na walipohojiwa walikiri kufanya uharifu huo kwa kutumia siraha.
Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi (DCP), Kamanda wa Polisi Kanda Maalum  ya Dar esSalaam, Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo) Katika ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na watuhumia wa wizi na Madawa ya kulevya hapa nchini.
Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi (DCP), Kamanda wa Polisi Kanda Maalum  ya Dar esSalaam, Simon Sirro akionyesha magari yenye namba za usajili T593 DEL aina ya Prado na jingine lenye namba T 999 DDB nalo Prado.

Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live


Latest Images