Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

UNESCO yaahidi kuendelea kusaidia sekta za Habari na Utamaduni

$
0
0
BB2
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO Bibi. Zulmira Rodrigues alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
BB3
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO Bibi. Zulmira Rodrigues (kulia) alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
BB1
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akimsikiliza Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO Bibi. Zulmira Rodrigues (kulia) alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
BB4
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO Bibi. Zulmira Rodrigues (kushoto) alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam. Wengine ni Afisa Habari wa UNESCO Bi. Nancy Kaizirege (mwenye nguo ya dhambarau).PICHA NA FRANK SHIJA, WHUSM

THOMAS MUNIS AAHIDI MAKUBWA NDANI YA CCM ARUSHA

$
0
0
SAM_7218
Kada maarufu wa chama cha mapinduzi ccm na mfanyabiashara wa madini mkoani Aarusha Thomas Munis akichukua fomu ya kuwania nafasi ya uwenyekiti wa mkoa ndani ya chama hicho hivikaribuni,  huku akiahidi mabadiliko makubwa ikiwemo kurudisha uhai wa chama katika jimbo la Arusha,kulia ni katibu msaidizi mkuu Omary Billaly
SAM_7221
Mgombea wa nafasi ya uwenyekiti wa mkoa ndani ya chama cha mapinduzi Mkoani Arusha Thomas Munis akionyesha fomu alizochukua kwa waandishi wa habari katika ofisi hizo jijini Arusha
SAM_7250
Thomas Munis akiongea na vyombo vya habari kuhusu nia yake ya kuchukua fomu hiyo ya kuwania nafasi ya uwenyekiti mkoa wa Arusha ambapo amehaidi ushirikiano mkubwa kwa wananchama pamoja na viongozi walipo katika kuleta mabadiliko ndani ya chama.
……………………………………………………….
(Habari picha na Pamela wa jamiiblog)
OFISI ya chama cha mapinduzi, ccm, mkoa wa Arusha imetoa orodha ya wanachama 25,waliochukua fomu za kugombea uongozi ngazi ya mkoa kuziba nafasi ambazo ziko wazi ili kukamilisha safu ya uongozi ya Chama mkoa.
 
Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake hivi karibuni katibu msaidizi mkuu, Omary Billaly aliwataja waliochukua fomu na kurejesha nafasi ya mwenyekiti wa mkoa ndani ya ccm kuwa niJacob Meja Mollel, Juma Saidi Lossin,Victor Nicodemas Mollel, John Danielson Palangyo, Rabiel Fanuel Mbise,Hamis Saidi,Mussa Hamis Mkanga.Wengine ni Ally Jumbe, Metui Ailo ole Shaudo,MustafaPanju, Michael Lekule Laizer,Kenedy Danford Mpumilwa ,Raphael Long’idu Mollel, Karim Ephraim MushiGodson Loning’o,Thomas Munis,Emanuel Makongoro Lusenga.
 Wengine ni Henry Obed Mejooli,Veraikunda Zablon Urio,Babu Mohamed Kitume, Kisali Eliah, Bernadeth Silas Changulu,,Hafidhi Mwango Bakary,Agnes Gidion Mollel, na Ndewirwa Soori Mbise.Billaly aliongeza kuwa wanachama wawili ambao ni Shaaban Masawe na Rajab Mshana hawakurudisha fomu hizo.
 Walichukua fomu za kugombea ukatibu wa siasa na uenezi mkoa wa Arusha ni Peter Mathew Kasella, Veraikunda Zablon Urio,Gerald Eliaika Munisi, Lightness Ahadiel Mweteni,Japhet Zakaria Moirani, Anna Agatha Musuya,Jasper Augustino Kisumbua,Zam zam Ramadhan Abdalah, Emanuel Makongoro Lusenga,Amani Silanga Mollel, Victor Nicodemas Mollel, Ally Juma Mwinyimvua.
 Wengine ni Hamis Said Migire,Julius Laanyun Mollel,Cylius Daniel Mlekwa,Ahmed Mwita Chacha,Semmy Robson Kiondo,Revocutus Wiliam,Palapala ,Emanuel Abel Sirikwa,Loata Erasto Sanare,Joshua Hungura Mbwana,Njechele Eliakim Laizer.Godson Solomon Mollel, (Mzunguu).
 Wengine Shaaban Omar Mdoe, Wahabu Hemed MbagaaZIZI Abdalah Mfundo,Abel Smwel Kalama,Justus Enock Rwandezi,Sylevesta Kornen Meda, Lobora Petro Ndarapoi, na Victor Livingston Njau.

Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo kuendelea kushirikiana na wajasiriamali wa kazi za Sanaa

$
0
0
BST1
Kaimu Mkurugenzi Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi.Leah Kihimbi akiongea na wajasiriamali wa kazi za Sanaa wa Mikono Cultural Heritage Ltd walipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.Bi leah aliwahaidi wasanii hao kufanya nao kazi kwa karibu na kuwapa ushirikiano mkubwa katika kazi zao.
BST2
Mwenyekiti wa kikundi cha wajasiriamali wa kazi za Sanaa Bw.Henry  Clemens (kushoto) akimweleza jambo Kaimu Mkurugenzi wa Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi Leah Kihimbi (kulia).Bw.Clemens aliomba serikali kuwawezesha kupata wawekezaji, na pia shughuli za za Sanaa ziwe rasmi ili wajipate kipato na kutengeneza ajira kwani wazalishaji wa Sanaa wanafiki milioni 3 kwa sasa.
BST3
Mwenyekiti wa kikundi cha wajasiriamali wa kazi za Sanaa Bw.Henry  Clemens akiishukuru serikali kwa kuonyesha nia ya kuwasaidia kwa kuanzisha Idara ya Sanaa na ivyo wataitumia kuimarisha kazi zao ili ziwanufaishe.Pembeni yake ni makamu mwenyekiti wa Kikundi icho Bw.Chief Eliewaha Shogholo Challi.
BST4
Baadhi ya wajasiriamali wa kazi za Sanaa wa Mikono Cultural Heritage Ltd wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bi leah kihimbi (hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam
BST5
Picha ya pamoja.
Picha zote na Daudi Manongi-WHUSM

UZINDUZI WA STIKA MAALUM YENYE UJUMBE WA KUTOKOMEZA MAUAJI YA ALBINO

$
0
0
????????????????????????????????????
Na Nyakongo Manyama-MAELEZO
TAASISI ya  watu wenye ulemavu wa ngozi mkoa wa Dar es salaam inatarajia kufanya uzinduzi wa  ‘stika’ maalum yenye ujumbe wa kutokomeza mauaji ya watu wenye albinism utakaofanyika januari 26 mwaka huu.Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa taasisi hiyo Bw. Michael Lugendo amesema kuwa uzinduzi huo utafanyika katika kituo cha polisi kati jijini Dar es Salaam kuanzia saa tano asubuhi.

Bw. Michael Lugendo amesema kuwa stika hiyo ina lengo la kuhamasisha jamii kuungana na Rais Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli na Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam ili kuyafanya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi yatokomezwe na yabaki kuwa historia.
Kwa upande mwingine Bw. Lugendo ameongeza kuwa kulingana na kasi ya mabadiliko tabia nchi, jamii isipochukua hatua za makusudi kuna uwezekano wa watu wenye ulemavu wa ngozi kuangamizwa na saratani ya ngozi.

Alisema watu wenye ulemavu wa ngozi wanaishi katika mazingira ya umaskini kiasi kwamba waliowengi hawana uwezo wa kupata fedha ya kununua mafuta ya kuzuia mionzi ya jua  ambayo husababisha saratani ya ngozi.“Sisi watu wenye ulemavu wa ngozi ni wahanga wakubwa sana na jamii isipochukua hatua za makusudi upo uwezekano wa kuangamizwa na saratani ya ngozi ukizingatia kwamba tunaishi katika mazingira ya umaskini na walio wengi hatuna uwezo wa kupata fedha ya kununua mafuta” alisema Bw. Lugendo.
 
Aidha Bw. Lugendo amesema kuwa  taasisi hiyo imemteua Bw. Mbwana Ally Samata kuwa balozi wa kudumu wa kusemea watu wenye ulemavu wa ngozi.
Alibainisha kuwa majukumu ya Nahodha huyo wa Timu ya Taifa ya Tanzania kwa ujumla ni kuhamasisha dunia kwa njia ya soka kuhakikisha  kwamba hakuna mlemavu wa ngozi anayefariki kwa kifo cha saratani ya ngozi au mauaji ya kukatwa viungo yanayotokana na Imani za kishirikina.

Bw. Lugendo aliwataka wadau mbalimbali, kampuni, balozi mbalimbali, Mashirika yasiyokuwa ya Serikali kujitokeza ili kuwezesha kutimiza lengo hilo kwa kutoa taarifa za uhalifu dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi kupitia vyombo vya habari pamoja na jeshi la polisi.

WAZIRI DKT.AUGUSTINE MAHIGA AKUTANA NA WABUNGE WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI, EALA KUTOKA TANZANIA

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dkt. Augustine Mahiga, (wanne kutoka kushoto), Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Susan Kolimba, (watatu kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, EALA, kutoka Tanzania, Mh. Shy-Rose Bhanji, 9wakwanza kushoto), Mh. Makongoro Nyerere (wapili kushoto), Mh. Angella Kizigha, (Wasita kutoka kushoto), naMh. Bernard Murunya). Wabunge hao walikwenda kumsalimia waziri Mahiga na kujitambuslisha ikiwa ni siku chache kabla ya kuanza vikao vya bunge hilo jijini Arusha Januari 24, 2016. (K-VIS MEDIA/Khalfan Said)

NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dkt. Augustine Mahiga, mapema leo Ijumaa Januari 15, 2016 amekutana na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, (EALA), kutoka Tanzania waliokwenda kujitambulisha na kubadilishana mawazo ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Wabunge hao waliongozwa na mwenyekiti wa wabunge wa Tanzania, Mh. Makongoro Nyerere, Mh. Shy-Rose Bhanji, Mh. Angella Kizigha, na Mh.Bernard Murunya.Naibu Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Susan Kolimbanaye alikuwepo wakatiwa kikao hicho kifupi cha kutambuana.
Akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kikao hicho, Mwenyekiti wa wabunge wa EALA kutoka Tanzania, Mh. Makongoro Nyerere, alisema, “Tumefika kujitambulisha kwa Mh. Waziri kama ujuavyo yeye ni mgeni kwenye wizara hiyo, tulikuwana Dkt. Mwakyembe na sasa tunaye Dk. Augustine Mhiga, kwa hivyo tuliona ni vyematukafika kujitambulisha na kutambuana.” 

AlisemaMh. Makongoro na kuongeza, “Lakini pia lazima utambue kuwa vikao vya EALA, vinaanza Januari 24 pale Arusha na Mh. Mahiga ndiye mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki, kwa hivyo sio busara tukakutanie kule ndio maana tumeona ni vema tukaja kumsalimia hapa atutambue na kubadilishana mawazo hapa na pale.” Alimaliza Mh. Makongoro.
Bunge la Afrika Mashariki, EALA, ni chombo cha kutunga sheria cha Juamuiya ya Afrika Mashariki na linaundwa na nchiwanachama wa Jumuiya hiyo ambaonipamoja na Tanzania, inayoshikilia uenyekiti kwa sasa, Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi.


 Dkt. Mahiga, akisaliamiana na mmoja wa wabunge hao, Mh. Shy-Rose Bhanji
 Mh. Shy-Rose Bhanji akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga, (wakwanza kushoto) na maafisa wengine wa wizara hiyo, mara baada ya kikao hicho
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dkt. Susan Kolimba, akisalimiana na Mh. Shy-Rose Bhanji
Mh. Makongoro Nyerere, akipena mikono na Bi. Mindi Kasiga

TAARIFA YA MSIBA

Tamko,Tiba ASILI NA TIBA MBADALA

$
0
0

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
NEMBO YA TAIFA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,
JINSIA, WAZEE NA WATOTO
MAELEZO YA WAZIRI KUHUSU TIBA ASILI NA TIBA MBADALA
 
Ndugu Wananchi,Katika nchi yoyote ile uhuru usio na mipaka ni jambo la hatari; lakini pia hakuna haki isiyo na wajibu. Vivyo hivyo, katika huduma za Tiba Asili na Tiba Mbadala hapa nchini kuna Sheria, Kanuni na Taratibu za Maadili zinazoweka masharti, uhuru na mipaka; pia haki na wajibu wa kila mdau. 

Huduma za tiba asili na tiba mbadala ni huduma zinazotambulika na Jamhuri yetu, watu wake na ina thamani kubwa. Aidha, ni huduma inayotambuliwa na sayansi ya tiba ya kisasa. Hata hivyo huduma hizo zimekumbwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa watoa huduma wasiozingatia Sheria, Kanuni na Miongozo mbalimbali. 

Kutokana na hali hiyo na kutokana na ziara ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamisi A. Kigwangalla (Mb) kwa Tabibu Juma Mwaka Juma tarehe 14/12/2015 na kufuatia uchambuzi uliofanywa na Wizara baada ya ziara hii, Wizara imebaini changamoto zifuatazo:-
 1. Huduma za tiba asili na au tiba mbadala zinatolewa na watoa huduma wasiosajiliwa na Mamlaka husika kwa mujibu wa Sheria.2. Uwepo wa vituo vinavyotoa huduma za Tiba Asili na au Tiba Mbadala bila kusajiliwa kwa mujibu wa Sheria.
 3. Kutolewa dawa kwa wagonjwa bila dawa hizo kusajiliwa na mamlaka husika.4. Uingizaji na matumizi ya vifaa vya uchunguzi ambavyo havijasajiliwa na mamlaka zinazohusika, na
 5. Utoaji wa matangazo bila ya kufuatwa kwa matakwa ya sheria, Kanuni na Miongozo iliyopo. Aidha baadhi ya matangazo hayo yamekuwa na taarifa zinazoweza kuleta madhara na kupotosha Umma wa Watanzania.
Ndugu Wananchi,


Kutokana na hali hiyo, Wizara itahakikisha kuwa huduma za tiba asili na tiba mbadala zinatolewa kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo iliyopo. Lengo ni kuwezesha huduma za tiba asili na tiba mbadala zinakuwa huduma rafiki na salama kwa watumiaji. Tunao wajibu wa kuwalinda wananchi, vile vile tunaowajibu wa kuweka mazingira mazuri kwa watoa huduma za tiba asili na tiba mbadala ili kufanya shughuli zao vizuri.

Hivyo kwa upande wetu Wizara itahakikisha kuwa:-1. Baraza na sehemu inayosimamia huduma za Tiba Asili na Tiba Mbadala inakuwa na watumishi wa kutosha kwa mujibu wa Ikama.2. Kunakuwa na Mpango Mkakati wa muda mrefu kuwezesha kufanikisha uboreshaji wa huduma za tiba asili na tiba mbadala nchini.3. Watoa huduma wote, vituo vyote vya kutolea huduma, dawa na vifaa na vifaa tiba vinavyotumika vinasajiliwa.4. Utaandaliwa mwongozo wa mafunzo kwa watoa huduma wote nchini, kuhusu namna ya kuweka kumbukumbu za wagonjwa, kutoa rufaa kwa wagonjwa na kutengeneza dawa zilizo bora.5. Kunakuwa na mawasiliano na Wizara zinazohusika na habari na mawasiliano ili kuboresha utoaji matangazo yanayohusu Tiba Asili na Tiba Mbadala.6. Kunakuwa na mawasiliano na Ofisi ya Rais TAMISEMI na Taasisi za Utafiti ili kuboresha huduma za tiba asili na tiba mbadala nchini.7. Tutafanya mabadiliko ya Sheria ili kuongeza kiwango cha adhabu kwa watakaokiuka, na pia tunakusudia kuondoa Kanuni inayoruhusu matangazo kwa idhini ya Baraza kwa sababu inaweka mianya ya matumizi mabaya ya fursa ndogo ya matangazo inayotolewa.
Ndugu Wananchi,Katika kufanikisha hayo, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inatoa maelekezo yafuatayo kwa watoa huduma na jamii:-1. Hairuhusiwi kwa mtu yeyote kutoa huduma za tiba asili na au tiba mbadala bila kusajiliwa. Ninalielekeza Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala kuhakikisha kuwa watoaji huduma wote wanasajiliwa kwa mujibu wa Sheria:(a) Mijini, (Majiji, Manispaa na Miji) – usajili wao ukamilike katika kipindi cha miezi mitatu; kuanzia Januari 15, 2016 na (b) Vijijini, Halmashauri zote zilizobaki – usajili wao ukamilike katika kipindi cha miezi sita kuanzia Januari 15, 2016.Hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakaye puuza kujisajili katika kipindi hicho2. Hairuhusiwi kuuza na au kugawa dawa yoyote ile ya tiba asili au tiba mbadala mpaka iwe imesajiliwa na Baraza baada ya kuchunguzwa na Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kuwa ni salama na kupewa kibali na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA).3. Hairuhusiwi kuendesha kituo cha kutolea huduma za tiba asili na au tiba mbadala bila kukisajili.4. Wizara inapiga marufuku kwa mtu binafsi au taasisi yoyote ile kutumia kifaa au kifaa tiba chochote bila kukisajili TFDA na kupewa kibali; na5. Matangazo yote yanayohusu Tiba Asili na Tiba Mbadala ambayo hayajapitishwa na Baraza yamezuiliwa kuanzia leo tarehe 15/1/2016. Wizara inavitaka vyombo vya Habari hasa Televisheni, Radio na Magazeti kuzingatia Sheria na Kanuni za Tiba Asili na Tiba Mbadala inayozuia matangazo ambayo hayajachunguzwa na Baraza. Ni wajibu wa vyombo vya habari kujiridhisha na Mamlaka husika yaani Baraza kabla ya kutoa tangazo lolote linalohusu Tiba Asili na Tiba Mbadala. Wizara itashirikiana na Mamlaka zinazohusika na habari na mawasiliano kutekeleza agizo hili. Vile vile, hairuhusiwi kutoa elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari na mikutano ya hadhara kuhusu tiba asili na tiba mbadala.
Ndugu Wananchi,Katika kuwezesha ulinzi wa afya za wananchi, kila mmoja wote alinde afya yake kwa kuhakikisha kuwa huduma anayopata ya tiba asili na tiba mbadala ni kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Miongozo inayotolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Ni uhakika uliowazi kuwa kwa pamoja tukiboresha huduma za tiba asili siyo tu tutaboresha afya zetu bali pia tutaweza kuuza dawa na huduma hizo nje ya nchi na kupata fedha za kigeni kupitia na hivyo kuboresha uchumi wa mtu mmoja mmoja, jamii na nchi kwa ujumla.
Kwa pamoja tushirikiane kuboresha huduma za tiba asili na tiba mbadala nchini. INAWEZEKANA.
Ummy A. Mwalimu (Mb)WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO15 Januari, 2016

LADY IN RED MWAKA HUU KUFANYIKA TANZANIA NA UINGEREZA

$
0
0
Miongoni mwa burudani maarufu duniani ni pamoja na "Fashion Industry' yaani mitupio inayowafanya watu kuwa katika good appearance Wanawake kwa Wanaume kuanzia miguuni mpaka kichwani. Wanamitindo kutoka hapa nchini Tanzania wamekuwa na utaratibu wa kuandaa Fashion Show ambazo zinatoa opportunity kwa Designers na Models.

Hivyo basi new update kutoka Mama wa mitindo maarufu kama Asya Idarous ambaye kila mwaka huandaa Fashion Show inayo wakutanisha Designers "Lady in Red" amesema kuwa "Mwezi huu nitahakikisha "Lady in Red" inafanyika Tanzania coz tarehe 17 January, 2016, nategemea kukutana na designers pale Regency Hotel Mikocheni saa 10:00 jioni kwa ajili ya maandalizi ya "Lady in Red" inayotegemea kufanyika 31/1/2016 katika ukumbi wa "Danken House'.

Pia Asya  Idorous aliongeza kuwa "2016  "Lady in Red" itaifanyika Tanzania na United_Kingdom (UK) Uingereza . So kwa wale wapenzi wa mitindo hapa ndio pake staytuned yaani kitu ni "Lady in Red" Cheers 2016.

KITUO CHA UTAFITI CHA RCRSDS KUZINDUA MFUMO WA KIELEKTRONIKI WA KUKUSANYA, KUHIFADHI NA KUWEKA ANGANI TAARIFA ZA KITAFITI ZA UWAJIBIKAJI WA TAASISI ZA BINAFSI NA UMMA

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Utafiti wa Shughuli za Maendeleo ya Jamii Tanzania (RCSDS),Abraham Shempemba (kulia) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo , kuhusu mafanikio ya tafiti zao walizozifanya zinazoonesha takwimu za misaada iliyotolewa kisekta, gharama zilizotumika, uwajibikaji wa jamii na jinsi ilivyonufaika. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa kituo hicho, Chrizostom Thadeo. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA).

Na Celina Mathew

KITUO cha Utafiti wa shughuli za maendeleo ya jamii Tanzania(RCSDS), kinatarajia kuzindua mfumo wa kielektroniki wa kukusanya, kuhifadhi na kuweka angani taarifa za kitafiti za uwajibikaji wa taasisi za binafsi, za umma na watu binafsi serikali kuu na za mitaa na hata mtu mmoja mmoja.

Mfumo huo unatarajiwa kuzinduliwa mwishoni mwa mwezi huu ambapo utapelekwa katika mikoa 30 Tanzania Bara pamoja na maeneo 100 yenye wananchi wenye uhitaji mkubwa.

Akizungunza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa kituo hicho, Abraham Shempemba alisema lengo la mwendelezo huo ni kutoa nafasi kwa walengwa kutambua mchango unaotolewa kwao na wadau mbalimbali pamoja na misaada kwa jamii zenye uhitaji mkubwa.

"Sisi kama RCSDS tunatambua uwepo wa makampuni, mashirika na taasisi mbalimbali za umma na binafsi zinazochangia kwa kiasi kikubwa mahitaji na hata majanga yanapotokea ili kunusuru na kuboresha maisha ya watanzania wenzetu na kuthamini michango na misaada yao,"alisema.

Alisema mfumo huo unaoaznishwa una lengo la kutambua michango na misaada mbalimbali inayotolewa na wadau kwa jamii pia wadau nao wapate fursa ya kuweka malengo yao ya uwajibikaji kwa jamii kwa kuona ni wapi wanaweza kuwekeza zaidi kiuwajibikaji na eneo lipo nani amewekeza.

Shempemba alisema utafiti walioufanya na kuutolea taarifa msimu ulipita kwa kushitikiana na taasisi ya ukaguzi ya Konsalt inayofanyika kila mwaka wapo waliosaidia jamii kwa sekta mbalimbali kama huduma za afya, maji, miundombinu, elimu, michezo, maafa na mambo mengine kwa asilimia tofauti.

Aliongeza kuwa tafiti hizo pia zimesaidia takwimu za misaada iliyotolewa kisekta, gharama zilizotumika, uwajibikaji jamii ulivyowekezwa, jamii ilivyonufaika na misaada hiyo na wadau walivyonufaika na uwekezaji wao kwa jamii hizo.

WACHUUZI WA TANZANITE WALIA NA LESENI

$
0
0
 

Na Woinde Shizza.
WACHUUZI wa madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wameiomba Serikali kutowabana walipe leseni ya ununuzi, kwani uwezo wao ni mdogo na wao ni madalali siyo wanunuzi wa madini hayo.
Wakizungumza juzi wachuuzi hao walidai kuwa hawapingi kulipa mapato ya serikali ila zoezi la ulipaji wa leseni ya kununulia madini ya Tanzanite ingetakiwa kutekelezwa kwa wafanyabiashara peke yao na siyo kwa wachuuzi wadogo.
Mmoja kati ya wachuuzi hao Anturusia Chande alisema wengi wao wanapewa madini hayo na kuzunguka kwenye masoko ya Mirerani kwa lengo la kujikimu maisha yao ikiwemo kusomesha watoto, mavazi, chakula na matibabu. 
“Sisi hatuvuki na madini nje ya eneo la Mirerani na tunategemea kuendesha maisha yetu kupitia uchuuzi huu mdogo mdogo na pia hatuna mtaji kwani tumejiajiri wenyewe serikali ituangalie kwa kupitia hili,” alisema Chande.
Alisema wao wanachangia pato la Taifa kupitia sekta hiyo kwa kulipa kodi pindi wanaponunua bidhaa mbalimbali madukani ikiwemo sukari, mchele, mafuta ya kula, ya taa, sigara na nyinginezo ila bado wanasumbuliwa na serikali. 
Kaanael Minja alisema zoezi la kuwakamata wachuuzi ambao hawakulipa leseni lililoendeshwa wiki iliyopita, halikufanyika kwa haki kwani kuna baadhi yao waliporwa madini ambayo siyo yao na hawakurudishiwa hadi hivi sasa. 
“Kabla ya kuendesha kamata kamata hiyo wangetoa elimu kwanza kwa wachuuzi hao lakini kitendo cha kufika kijiweni na kuanza kuwakamata watu wasio na leseni siyo kizuri, wangepaswa kuwaelimisha kwanza,” alisema Minja. 
Hata hivyo, mkuu wa wilaya ya Simanjiro Mahmoud Kambona aliwataka wachuuzi hao kujipanga na kulipia leseni ya ununuzi wa madini hayo ili waongeze mapato kwa serikali ambayo inawaletea wananchi maendeleo.
“Wanatakiwa kutambua kuwa hiyo ni sheria ambayo imepitishwa na sasa kinachotakiwa ni utekelezaji kwani serikali zote hujiendesha kutokana na kodi ambazo zinalipwa na wananchi wake na siyo vinginevyo,” alisema Kambona.

WIMBO WA INJILI WA "MUNGU AMESEMA NDIO" KUZINDULIWA MWISHONI MWA MWEZI JANUARI MWAKA.

$
0
0
 WIMBO mpya wa Injili wa MUNGU AMESEMA NDIO kuzinduliwa mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huu wimbo wa  MUNGU AMESEMA NDIO umeimbwa na mwimbaji wa nyimbo za Injili ajulikanae kama Mhandisi Carlos Mkundi (Pichani).

Hayo yamesemwa na mwimbaji huyo wa nyimbo za Injili wakati akizungumza na mwandishi wa MICHUZI BLOG jijini Dar es Salaam leo.

Amesema kuwa baada ya kutoa wimbo wake wa MUNGU AMESEMA NDIO atatoa wimbo wa mwingine ambao ameupa jina la YOU ARE THE SAME YOU NEVER CHENGE ambao ataimba kwa lugha ya kiingereza ili watu mbalimbali waweze kuusikia.

Mhandisi Mkundi ameimba nyimbo za Injili mbalimbali zinazojulikana kama Nimetoka mbali, Wewe ni Mungu, Usinishike bega, Moyo wangu wakuabudu.

Aidha amewaomba wananchi na wadau wa nyimbo za Injili hapa nchini wamuunge mkono ili kutangaza neno la Mungu kwa mataifa yote kupitia nyimbo za Injili.

MAKAMU MWENYEKITI WA CCM (BARA) AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA CHINA LUMUMBA LEO

$
0
0
 Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Ndugu Philip  Mangula,  akizungumza na  Mchambuzi  wa masuala ya Siasa   na Taluma  za Jamii  na Naibu Mkurugenzi  wa Kamati ya Maendeleo  ya Jamii katika Wizara  ya Elimu nchini China, Gu Hailiang, aliyeongoza ujumbe wa watu sita kutoka nchini humo,  kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa NEC, Makao Makuu ya CCM Ofisi Ndogo Lumumba., Dar es Salaam,. Kushoto ni  Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya CCM (NEC)  ,Siasa na Ushirikiano wa Kimataifa,  Dk. Asha Rose Migiro pamoja na maofisa wengine wa Chama.
  MAKAMU Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip  Mangula,  akizungumza na  Mchambuzi wa masuala ya Siasa   na Taluma  za Jamii  na Naibu Mkurugenzi  wa Kamati ya Maendeleo  ya Jamii katika Wizara  ya Elimu nchini China, Gu  Hailiang, aliyeongoza ujumbe wa watu sita kutoka nchini humo,  kwenyemkutano uliofanyika katika ukumbi wa NEC, Makao Makuu ya CCM Ofisi Ndogo Lumumba., Dar es Salaam,. Kushoto ni  Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya CCM (NEC)  ,Siasa na Ushirikiano wa Kimataifa,  Dk. Asha-Rose Migiro.
 Mchambuzi wa masuala ya Siasa   na Taluma  za Jamii  na Naibu Mkurugenzi  wa Kamati ya Maendeleo  ya Jamii katika Wizara  ya Elimu nchini China, Gu Hailiang, aliyeongoza ujumbe wa watu sita kutoka nchini humo, akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara)  kwenye
mkutano uliofanyika katika ukumbi wa NEC, Makao Makuu ya CCM Ofisi Ndogo Lumumba., Dar es Salaam,. Kulia ni  Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya CCM (NEC)  ,Siasa na Ushirikiano wa Kimataifa,  Dk. Asha-Rose Migiro pamoja na maofisa wengine wa Chama,.
 Mchambuzi wa masuala ya Siasa   na Taluma  za Jamii  na Naibu Mkurugenzi  waKamati ya Maendeleo  ya Jamii katika Wizara  ya Elimu nchini China, Gu Hailiang, akimkabidhi zawadi Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Ndugu Philip Mangula mara baada ya kumaliza mazungumzo yenye nia ya kuimarisha uhusiano kati ya Serikali ya Watu wa Jamhuri ya China na Tanzania.
 Mchambuzi
wa masuala ya Siasa   na Taluma  za Jamii  na Naibu Mkurugenzi  wa
Kamati ya Maendeleo  ya Jamii katika Wizara  ya Elimu nchini China, Gu
Hailiang, akimkabidhi zawadi Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya CCM
(NEC)  ,Siasa na Ushirikiano wa Kimataifa,  Dk. Asha-Rose Migiro mara baada ya kumaliza mazungumzo yenye nia ya kuimarisha
uhusiano kati ya Serikali ya Watu wa Jamhuri ya China na Tanzania.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Ndugu Philip  Mangula,  akiwa kwenye picha ya pamoja nje ya Makao Makuu ya CCM, Ofisi Ndogo Lumumba na  Mchambuzi  wa masuala ya Siasa   na Taluma  za Jamii  na Naibu Mkurugenzi  wa Kamati ya Maendeleo  ya Jamii katika Wizara  ya Elimu nchini China, Gu Hailiang, na Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya CCM (NEC)  ,Siasa na Ushirikiano wa Kimataifa,  Dk. Asha Rose Migiro pamoja na wajumbe wengine kutoka China. BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

NAIBU WAZIRI WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA (NIDA)

$
0
0
NID1
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Hamad Masauni (kushoto), akiongozana  na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA),Dickson Maimu (kulia), wakati wa ziara ya kutembelea moja ya ofisi za mamlaka hiyo,iliyopo barabara ya Ali Hassani Mwinyi,jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri aliweza kupata fursa ya kuangalia jinsi utengenezaji wa kitambulisho cha Utaifa unavyofanyika.
NID2
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Hamad Masauni, akiwa katika kikao na viongozi mbalimbali wa Vitengo vya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA),wakati wa ziara iliyoanzia Makao Makuu ya Mamlaka hiyo,jijini Dar es Salaam.Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Dickson Maimu.
NID3
Afisa Msajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA), Emmanuel Joshua(kushoto), akitoa maelezo jinsi taarifa za muombaji wa kitambulisho cha Taifa zinavyohakikiwa kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Hamad Masauni(katikati),wakati wa ziara ya Naibu Waziri kwenye mamlaka hiyo,jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

SERIKALI YAWATAKA WANANCHI WALIOVAMIA ENEO LA KAMBI WA WAZEE NUNGE KUSITISHA UJENZI

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Dkt.Hamisi Kigwangalla (kulia)akitembelea jana Makazi ya Wazee walioathirika na ugonjwa wa ukoma yaliyopo kijiji cha Nunge eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam.mwenye shati la batiki Mkuu wa Makazi hayo Moses Gunza.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Dkt.Hamisi Kigwangalla akimsikiliza mmoja wa wazee aliyejulikana kwa jina la Salum Ubwabwa wakati alipotembelea jana Makazi ya Wazee walioathirika na ugonjwa wa ukoma yaliyopo kijiji cha Nunge eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam.Mzee huyo ambaye alimpatia historia ya eneo hilo, ambalo sasa limevamiwa na baadhi ya watu.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Dkt.Hamisi Kigwangalla akiangalia mazingira ya makazi hayo.

RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI AMPIGA CHINI KATIBU TAWALA MWANZA


MABADILIKO YA MUUNDO WA KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE

$
0
0
  ZZ3ZZ5
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai akiongoza kikao cha wajumbe wakamati ya kanuni Katika Ofisiza Bunge leo Jijini Dar es Salaam.
ZZ1
Spika waBunge la Jamhuri ya Muungano waTanzania Mh. Job Ndugai (Katikati) akiwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Tulia Ackson (kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Hai Mkoani Kilimanjaro (CHADEMA) Mh. Freeman Mbowe kabla ya kuanza kwa kikao kilicho wakutanisha wajumbe wakamati ya kanuni na Spika, Katika Ofisi za Bunge leo Jijini Dar es Salaam leo tarehe 15/01/2015.
ZZ2
Mbunge waJimbo la Hai Mkoani Kilimanjaro (CHADEMA) Mh. Freeman Mbowe akimueleza jambo Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Tulia Ackson kabla yakuanza kwa kikao cha wajumbe wa kamati ya kanuni na Spika, Katika Ofisi za Bungel eo Jijini Dar es Salaam.

…………………………………JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
imagesBUNGE LA TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MABADILIKO YA MUUNDO WA KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE
Kamati ya Kanuni ya Bunge iliyoundwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai hivi karibuni, leo imekutana Jijini Dar es Salaam na Kuridhia mapendekezo ya mabadiliko katika muundo wa kamati za Bunge yaliyowasilishwa na Mhe. Spika ili kuendana na mabadiliko ya Muundo wa Wizara katika Serikali ya awamu ya Tano.
Mabadiliko hayo ambayo yamefanywa chini ya kanuni ya 155 (3) ya kanuni za Kudumu za Bunge yamezingatia madaraka aliyonayo Spika kufanya marekebisho kwenye nyongeza za kanuni kwa kushauriana na kamati hiyo.
Akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo Mh. Ndugai ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati hiyo amesema amelazimika kufanya mabadiliko katika muundo wa kamati ili kuendana na mabadiliko ya Wizara na kwa kuzingatia kuwa muundo wa kamati umetajwa kwenye nyongeza ya nane.
Katika muundo huo Kamati mbili mpya zimeundwa ambazo ni kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo na kamati ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma.
Akifafanua kuhusu maamuzi ya Kikao hicho, katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah amesema kikao hicho kimekuwa na mafanikio makubwa na kuridhia mapendekezo ya Mhe. Spika kama yalivyowasilishwa.
Aidha Dkt. Kashililah aliongeza na kusema kuwa Kamati nyingine zimefanyiwa mabadiliko kwenye majina na nyingine mbili kuunganishwa na kufanya kamati mpya za Bunge kuwa kama ifuatavyo:
Kamati zilizounganishwa ni:
• Kamati ya Huduma na maendeleo ya Jamii – imeunganishwa kutoka iliyokuwa Kamati ya Maendeleo ya Jamii na kamati ya Huduma za Jamii
• Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama –imeunganishwa kutoka iliyokuwa Kamati ya Ulinzi na Usalama na kamati ya mambo ya Nje.
Kamati zilizofanyiwa Marekebisho madogo kwenye majina ni:
• Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira (awali ilikuwa Kamati ya Viwanda na Biashara)
• Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii (awali ilikuwa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira)
• Kamati ya Utawala na Serikali za Mitaa (awali ilikuwa Kamati ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa)
Kamati zilizobakia kama ilivyokuwa awali ni pamoja na:
•Kamati ya Uongozi,
•Kamati ya Kanuni za Bunge,
•Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge,
•Kamati ya Katiba na Sheria
•Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji,
•Kamati ya Miundombinu na
•Kamati ya Nishati na Madini.
Wabunge wote wanatakiwa kuwasili Dodoma tarehe 20 Januari, 2016 tayari kwa kuanza Vikao vya Kamati kabla ya Mkutano wa Bunge unaotarajiwa kuanza tarehe 26 Januari, 2016.
Imetolewa na,
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano.
Ofisi ya Bunge,
S.L.P 9133,DAR ES SALAAM
15 Januari, 2016.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Amos Makala- akemea uharibifu wa mazingira katika vyanzo vya Maji

$
0
0
 2
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makala, akiweka jiwe la msingi ujenzi wa Maabara Shule ya sekondari Dr chami.
1
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makala akizungumza na watendaji wa Vijiji, waratibu wa Elimu kata, madiwani, wakuu wa idara na Kamati ya Ulinzi na usalama wakati alipofanya ziara ya halmashauri ya Moshi.
3
Watendaji wa Vijiji, waratibu wa Elimu kata, madiwani, wakuu wa idara na Kamati ya Ulinzi na usalama wakimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makala wakati alipofanya ziara ya halmashauri ya Moshi.

4
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makala (kulia), akiwa kwenye ziara ya halmashauri ya Moshi.
5
7
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makala akiwa ameongiozana na viongozi wa mbalimbali wakati wa ziara hiyo.
……………………………………………………. 
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Amos Makala amefanya ziara halmashauri ya Moshi kwa kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Maabara Shule ya sekondari Dr chami, na kukagua mradi mkubwa wa Maji unaojengwa kutoka chanzo cha mto Gona utakaohudumia wananchi wa kata ya njiapanda wapatao 25,000. Mradi unagharimu Fedha sh 800 milioni smbao unafadhiliwa na ujerumani kupitia shirika la TPP trust na serikali ya TanzaniaAidha amefanya kikao na watendaji wa Vijiji, waratibu wa Elimu kata, madiwani, wakuu wa idara na Kamati ya Ulinzi na usalama .Pia amewataka viongozi watendaji kuthibiti ulevi , uuuzaji wa pombe haramu na unywaji pombe wakati wa KAZI Na amekemea uharibifu wa mazingira katika vyanzo vya Maji na ukataji miti na uharibifu wa msitu wa mlima Kilimanjaro kwa kulinda msitu huo theluji ya mlima kilimanjaro imeanza kuongezeka. 

MGODI WA BUZWAGI WAPONGEZWA KWA KUZINGATIA SHERIA ZA MAZINGIRA.

$
0
0

Meneja wa kinu cha kuchenjua dhahabu wa Mgodi wa Buzwagi Festo Shayo (wa kwanza kulia) akitoa maelezo kwa Naibu waziri ofisi ya makamu wa rais anaeshughulikia mazingira na Muungano, Luhaga Mpina namna mgodi wake unavyohifadhi maji yaliyotumika kusafishia dhahabu.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira na Muungano Luaga Mpina (wa kwanza kushoto), akisikiliza maelezo ya Afisa Mazingira wa Mgodi wa Buzwagi bwana Frank Ngoroma (wa kwanza mkono wa kulia), aliyesimama katikati ni meneja mkuu wa mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo.
Mh Luhaga Mpina akisisitiza jambo wakati wa ziara hiyo katika eneo la kituo cha Uthibiti wa taka mbalimbali mgodini hapo.
Naibu Waziri pamoja na wataalamu wake wakikagua moja ya maeneo ambayo NEMC yalitoa ushauri kuwa yafanyiwe kazi katika ziara zao, ambapo wakati wa ziara hii utekelezwaji wake ulikutwa umeisha kamilika kama walivyokuwa wameelekezwa.


Mmoja wa maafisa wa mazingira aliyekuwa ameandamana na naibu Waziri akiuliza jambo wakati wa ziara hiyo.

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo akifafanua jambo wakati wa ugeni wa naibu Waziri wa mazingira.


Baadhi ya maofisa wa Mgodi wa Buzwagi wakitoa maelezo mbele ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira na Muungano Luaga Mpina
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Shinyanga.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Luhaga Mpina, ameupongeza Uongozi na wafanyakazi wa Mgodi wa Buzwagi kwa kuzingatia sheria za mazingira Mgodini hapo.
Pongezi hizo alizitoa wakati alipofanya ziara ya kushitukiza katika Mgodi huo kwa lengo la kujionea namna mwekezaji huyo anavyozingatia maelekezo ya wataalamu wa wizara yake juu ya utunzaji wa mazingira.

Akiwa katika ziara hiyo Naibu Waziri huyo alitembelea bwawa maalumu kwa ajili ya kuhifadhia maji yalitumika kuchenjulia dhahabu na kujionea namna ambavyo mgodi huo unavyochukua tahadhari ya hali ya juu katika kuhakikisha maji yanayohifadhiwa ndani ya bwawa hilo hayawezi kuwa na madhara kwa Jamii, pia naibu Waziri huyo alitembelea kituo cha udhibiti taka, Uwanda wa kuvuna maji ya mvua mgodini hapo pamoja na karakana ya mgodi huo.
“Bwawa hili kama unavyoliona usanifu wake, umezingatia tahadhari zote kuhakikisha hakuna maji yoyote yanatoka nje na hasa ukizingatia maji yanayopatikana hapa ni yenye mchanganyiko wa madawa yanayotumika kuchenjua dhahabu” Alisema Meneja wa Kituo cha Uchenjuaji dhahabu bwana Festo Shayo, wakati alipokuwa akitoa maelezo juu bwawa hilo.

Kwa upande wake naibu Waziri Mpina amesema licha ya kufanya ziara katika Migodi mingi bwawa la kuhifadhia maji yanayotoka katika kinu cha kuchenjulia dhahabu la Buzwagi ni la kiwango cha juu na ameitaka Migodi mingine pia kutembelea kwa lengo la kujifunza usanifu wake.

“Ni seme tumepita maeneo mengi ila hapa mmejitahidi kuhakikisha wananchi wanaowazunguka wako salama, nafikiri kuna haja ya migodi mingine kuja kujifunza hapa, karakana yenu pia ni nzuri na inazingatia utunzaji wa mazingira. Alisema mh Mpina.

Aidha akiwa katika kituo maalumu cha udhibiti taka Mgodini hapo Naibu Waziri huyo ameutaka uongozi kujenga paa kwenye eneo la udhibiti wa taka za vyuma ili kuzuia maji ya mvua kugusa taka hizo.

“Mmejitahidi kuhakikisha taka zinawekwa katika utaratibu mzuri, ila kukosekana kwa paa hapa ni tatizo, hivyo nawaagiza ndani ya siku therathini eneo hili liwe na paa” alisema Naibu Waziri Mpina.

Awali akiukaribisha ugeni wa naibu Waziri huyo Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo alimueleza naibu Waziri huyo kuwa sekta ya madini kwa sasa duniani imekumbwa na changamoto ya kuporomoka kwa bei ya dhahabu, hali ambayo imepelekea wawekezaji wengi kujikuta wakijiendesha kwa hasara.

“Mheshimiwa naibu Waziri, Mgodi wa Buzwagi toka uanze shughuli zake umekuwa ukishirikiana na Jamii katika kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo na tunaendelea kufanya hivyo, Hata hivyo changamoto ni kubwa kwani kila siku bei ya dhahabu inashuka na hii inatufanya tushindwe kujiendesha kwa faida”alisema Mwaipopo.
“Tumeanza mchakato wa maandalizi ya kusitisha shughuli za uchimbali maana gharama zinazidi kuwa kubwa hata hivyo kama bei ya soko itabadilika tutafikiria vinginevyo” aliongeza Mwaipopo.

Akizungumzia hatua ya mgodi huo kutaka kusitisha shughuli za uchimbaji naibu Waziri Waziri ofisi ya makamu wa rais anaeshughulikia mazingira na muungano Luaga Mpina, amewaomba wawekezaji hao kuangalia namna ingine itakayowawezesha kuchimba kwa gharama ndogo inayoendana na bei ya dhahabu.

“kwa kweli serikali inawahitaji sana wawekezaji na tunaposikia mnaondoka kwetu sisi ni hasara kwa sababu kodi mbalimbali ambazo mmekuwa mkilipa kwa halmashauri ya mji wa Kahama hazitakuwepo tena na hii itafanya miradi mingi ya Maendeleo isitekelezeke baada ya ninyi kuondoka, tunawaombea bei ya dhahabu ipande ili muendelee kuwepo” Alisema Mpina.

Ziara hiyo ya kushitukiza ili lenga kujionea namna ambavyo mgodi wa Buzwagi unazingatia maelekezo mbalimbali ya wataalamu wa wizara yake.

MAOFISA UGANI WATAKIWA KUTOA ELIMU YA KILIMO

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Babati Crispine Meela

Na Woinde Shizza,Babati

Maofisa ugani na makampuni ya usambazaji wa pembejeo Wilayani Babati mkoani Manyara, wametakiwa kuwaelimisha wakulima aina ya mbegu na mbolea bora zinazofaa kulingana na udongo wa eneo husika na kuachana na kilimo cha mazoea.

Mkuu wa wilaya ya Babati Crispine Meela aliyasema hayo katika kikao cha kamati ya pembejeo kilichokuwa kikijadili utekelezaji wa mpango wa usambazaji wa pembejeo kwa mwaka 2015/2016 na changamoto za utekelezaji huo.

Alisema kumekuwepo na dhana potofu kwa baadhi ya wakulima ya matumizi   ya mbolea katika ardhi kuwa yanaharibu udongo na mbegu mpya zisizozoeleka kwa wakulima hazifai kutumika hivyo wataalamu wakitoa shamba darasa watawaelimisha wakulima ipasavyo.

“Suala la pembejeo ni suala nyeti kwani ni mpango wa serikali wa usambazaji wa ruzuku za vocha za pembejeo kwa wakulima na pia kilimo ni uti wa mgongo wa Taifa letu hivyo tunapaswa kuwa makini katika hilo,” alisema Meela.

Alisema wilaya hiyo imepokea vocha za sh1 milioni 1 ambapo makampuni ya usambazaji wa pembejeo hizo kwa kupitia mawakala wao watawasambazia wakulima wa maeneo husika na kuwawezesha kupata aina zote tatu za mbegu, mbolea ya kupandia na kukuzia kwa wakati mmoja.

Alikemea baadhi ya makampuni kupitia mawakala wa usambazaji wasio waaaminifu wanaoendelea kutoa aina moja ya mbegu na makampuni hayo yazingatie sheria na kanuni za mkataba waliowekeana na halmashauri, kabla ya hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi yao.

Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Babati Hassan Lugendo alitaka zoezi la usambazaji wa pembejeo kuharakishwa kuwafikia wakulima kwa wakati ili kuepuka malalamiko ya ucheleweshaji wa ruzuku za vocha hizo.

Ofisa kilimo, umwagiliaji na ushirika wa mji wa Babati, Daniel Luther alisema kati ya aina ya vocha 3,000 zilizotolewa ni vocha 821 pekee zimekwishapatiwa wakulima kutokana na changamoto za wakulima kupendelea kuchukua mbegu bila mbolea.

Luther alitaja sababu nyingine zilizosababisha kutochukuliwa vocha nyingi ni kuchelewa kuanza kwa msimu wa kilimo katika maeneo mengi na uelewa mdogo wa wakulima katika kutumia aina mpya ya mbegu na mbolea.

RAIS KIKWETE AKUTANA NA MWAKILISHI MAALUM WA MAREKANI

$
0
0
MWENYEKITI wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete akiwa na Mjumbe Maalum wa Marekani katika Ukanda wa Maziwa Makuu, Thomas Perriello, baada ya mazungumzo yao kuhusu hali ya Burundi, yaliyofanyika jana, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam. (Picha na Bashir Nkoromo).
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images