Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live

KENYA'S TOP RIB CRACKER COMING TO DAR

0
0


Mwanahabari wa ITV Bw. Spensor Lameck alamba nondo chuo cha Diplomasia

0
0
1
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Augustine Mahiga akihutubia jana wakati wa mahafali ya Chuo cha Diplomasia yaliyofanyika jana chuoni hapo Kurasini jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na wahitimu wa shahada mbalimbali, Wahadhiri na wageni waalikwa ambapo mmoja wa Mwanahabari kutoka kituo cha Televisheni cha ITV Bw. Spensor Lameck alikuwa ni mmoja wa wahitimu.
2
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Augustine Mahiga akiwa katika jukwaa kuu na viongozi mbalimbaliwa chuo hicho pamoja na wahadhiri wakati wa mahafali hayo.
6
Mwanahabari kutoka kituo cha Televisheni cha ITV Bw. Spensor Lameck akipata picha ya pamoja na wahitimu wenzake wakati wa mahafali hayo.
8
Mwigizaji wa filamu Christina Manongi maarufu kama Sinta kulia akiwa na mhitimu mwenzake wakati wa mahafali hayo.
10
Mwanahabari kutoka kituo cha Televisheni cha ITV Bw. Spensor Lameck akipata picha ya pamoja na Christina Manongi maarufu kama Sinta kulia na mhitimu mwenzao.

WATUMISHI WAISHITAKI OFISI YA MKUU WA MKOA YA IRINGA KWA SSRA

0
0
 Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya jamii, Sabato Kasuri akifafanua majukumu ya mamlaka hiyo kwa watumishi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa wakati wakitoa dukuduku lao kuhusu mifuko ya hifadhi ya jamii
 Baadhi ya watumishi katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa na idara zake wakifuatilia mjadala kuhusu mifuko ya hifadhi ya jamii ulioendeshwa na mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) mjini Iringa jana.

 WATUMISHI wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa na idara zake wameishtaki kwa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) baadhi ya mifuko ya hifadhi ya jamii wakiilalamikia kwa mambo makubwa matano ikiwemo ucheleweshaji wa mafao kwa wanachama wake wastaafu.

Katika kikao kilichofanyika juzi mjini hapa baina ya SSRA na watumishi hao; watumishi hao walisema uzoefu toka kwa baadhi ya wastaafu wengi unaonesha kwamba inawachukua muda mrefu kupata mafao yao.

Afisa Utumishi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa, Gasto Andongwisye alitoa mfano akisema; “baadhi ya watumishi waliostaafu kabla ya mwezi Julai mwaka jana hawajapata mafao yao hadi leo na imekuwa ni kilio kikubwa ofisini kwangu.”

Akijibu lalamiko hilo, Afisa Uhusiano wa SSRA, Sabato Kasuri alisema ucheleweshaji wa mafao ni changamoto ambayo tayari imefanyiwa kazi kwa kiasi kikubwa baada ya kubainika ilikuwa ikisababishwa na na ukosefu wa kumbukumbu sahihi za walengwa.


Alisema mamlaka yao imetoa miongozo mbalimbali ya kuboresha sekta ya hifadhi ya jamii na katika suala la kumbukumbu kuna miongozo ya utunzaji wa kumbukumbu na takwimu ambayo kama ikitumiwa ipasavyo hakuna mstaafu atakayecheleweshewa mafao yake kwasababu zilizondani ya uwezo wa mifuko.

Ili kuondokana na lalamiko hilo wanachama hao walitaka mifuko hiyo ilipie riba fedha za mafao zinazochelewa kulipwa kwa wahusika sawasawa na waajiri wanapochelewa kuwasilisha michango ya wanachama katika mifuko hiyo.

Malalamiko mengine yaliyotolewa na watumishi hao ni pamoja na uwepo wa taarifa kwamba baadhi ya mifuko hiyo haitaki kulipa mafao ya kabla ya mwaka 1999 na inataka mzigo huo ubebwe na serikali.

Mengine yanahusu baadhi ya mifuko hiyo kushindwa kuweka kumbukumbu zake vizuri pamoja na uwepo wa miongozi ya SSRA jambo linalowafanya baadhi ya wanachama wake wawe na akaunti zaidi ya moja na wakati huo huo taarifa za baadhi ya michango yao kutoonekana.

Huduma ya bima ya afya ni eneo lingine lilitajwa na wanachama hao kuwa na  changamoto kubwa kwani mbali na wanachama wake kuchangia michango yao lakini baadhi yao wameendelea kupata huduma hafifu.

Lingine linalolalamikiwa katika mifuko hiyo ni mikopo ya nyumba ambayo kwa maelezo ya wanachama ni mzigo mkubwa kwa wastaafu kwani zinauzwa zikiwa na riba wakati zimejengwa kwa fedha za wanachama.

Katika kukabiliana na changamoto za mifuko hiyo, Kasuri aliwaambia watumishi hao kwamba SSRA inaendelea kutoa elimu kwa wadau wake, inarejea miundo na kanuni zinazogongana katika sekta ya hifadhi ya jamii, inafanya tathmini za mifuko yote ya hifadhi ya jamii na inatoa miongozo ya uwekezaji.

Alisema mamlaka yao ina wajibu pia wa kupitia vikokotoo vya mafao na mafao yanayotolewa, kutathimini afya ya mifuko yote na kushauri ipasavyo, na imeielekeza mifuko yote ya hifadhi ya jamii kufanya mikutano ya wanachama.

Kwa kutambua umuhimu wa hifadhi ya jamiii kwa kila mwananchi, Kasuri alisema sheria iliyounda SSRA imeruhusu uandikishaji wa wanachama kutoka katika sekta isiyo rasmi jambo linalowanufaisha pia wakulima na wafanyabiashara wadogo.

Alisema mpaka sasa Tanzania Bara ina mifuko sita ya hifadhi ya jamii ambayo ni Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Mfuko wa Pensheni wa PPF, Mfuko wa Pensheni kwa Wafanyakazi wa Serikali (GEPF), Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa (LAPF), Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya (NHIF) huku Zanzibar ikiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF).

Katika kikao hicho ni mifuko miwili ya GEPF na mfuko mpya wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ilipata fursa ya kueleza majukumu yao.

CLOUDS TV YAINGIA RASMI KWENYE KING’AMUZI CHA DStv “CHANELI 294”

0
0
MultiChoice Africa inapenda kuwatangazia wateja wake na watanzania kwa ujumla  kuwa  Clouds TV sasa imeingia rasmi kwenye DStv.

Kile kilio cha muda mrefu cha watazamaji na wapenzi wa Clouds TV juu ya Clouds TV kukosekana kwenye king'amuzi cha DSTV kimesikika na sasa Clouds TV imeingia rasmi ndani ya DStv.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Meneja  Uendeshaji  MultiChoice Tanzania, Ndugu Ronald Baraka Shelukindo,  amesema baada ya mazungumzo ya muda mrefu kati ya Clouds TV na Multichoice Africa  kuhusu Clouds TV kuingia katika king'amuzi cha DStv, MultiChoice Africa na Clouds TV wamefikia muafaka ambapo watazamaji na wapenzi wa Clouds TV  wenye ving'amuzi vya DStv watapata uhondo wa Clouds TV ndani ya DStv.

Akiongezea, Meneja Mauzo wa MultiChoice Tanzania , Ndugu Salum Salum  ameelezea furaha ya kampuni yao na akasema,  wakati mwingine walikuwa wanashindwa kufikia lengo la kupata wateja wengi zaidi kutokana na kukosekana kwa  Clouds TV  “hivyo kuanzia sasa, tuna imani kuwa idadi ya wateja itaongezeka maradufu!”.

Clouds TV itaanza kupatikana rasmi ndani ya DStv tarehe 14 Januari 2015, kwenye Chaneli 294, katika  vifurushi  vyake vyote ikiwemo; Premium, Compact Plus, Compact , Family na kifurushi cha DStv Bomba.

KESI YA PINGAMIZI DHIDI YA BOMOABOMOA KUSOMWA TENA JANUARI 25 MWAKA HUU.

0
0
Mbunge wa jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia akizungumza na wandishi wa habari juu ya kuhairishwa kwa kesi dhidi ya bomoabomoa ambayo itasomwa tena Januari 25 mwaka huu.
 Kesi hiyoilifumguliwa ili kupinga agizo la wizara ya Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi ambapo walikuwa wanabomoa maeneo hatarishi na maeneo ya wazi yaliyovamiwa na wananchi. 
Kesi hiyo ya zuio la bomoabomoa imesomwa leo na Jaji Panterine Kente leo katika mahakama kuu kitengo cha ardhi jijini Dar es Salaam.
 Wananchi wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia leo katika Mahakama kuu kitengo cha ardhi jijini Dar es Salaam leo.
Wananchi wakiwa nje ya Mahakama kitengo cha Ardhi leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Emmanue Massaka wa Globu ya jamii.

MWAKA MWINGINE WA MAENDELEO MAKUBWA KWA SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD.

0
0
SHIRIKA la ndege la taifa la umoja wa falme za nchi za kiarabu la Etihad limefurahishwa na ufanisi na utendaji wa operesheni zake kwa mwaka wa 2015 zilizowafanikisha kufikia malengo yao ya ukuaji ambapo sasa wanabeba abiria wengi na mizigo mingi zaidi ya awali.
Mwaka jana Shirika lilibeba abiria milioni 17.4, sawa na asilimia 17 zaidi ya mwaka 2014, wakiendesha safari 97,400 za ndege zilizofikisha jumla ya kilomita milioni 467. 

 Hii ni dhahiri kwamba abiria walifurahia huduma hizi na hivyo uhitaji uliongezeka, jambo ambalo lilisisitiza nguvu ya mikakati ya ukuaji iliyowekwa na shirika la ndege la Etihad.

Kwa ujumla, ndege za Etihad pekee zimebeba zaidi ya asilimia 75 ya abiria waliosafiri kwenda na kuondokea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abu Dhabi katika mwaka wa 2015. Etihad pamoja na washirika wake walio na ndege zinazofika mji huo mkuu wa UAE wamefikisha jumla ya asilimia 84 ya abiria waliotua uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abu Dhabi.

James Hogan, Rais na Afisa Mkuu Mtendaji wa Etihad, alisema: “Katika mwaka 2015, tumeweza kuwapa mamilioni ya wasafiri chaguo lenye thamani ya fedha katika usafiri wa anga na tumeleta nguvu mpya ya ushindani katika sekta hii. Yote haya yametokana na huduma zetu zinazokidhi viwango vya kimataifa ambazo pia zimejizolea tuzo mbalimbali. Pamoja na hayo, mashirika mengi yanavutiwa kujiunga nasi na tunazidi kuongeza idadi ya washirika wetu, kukuza ukubwa wa mitandao yetu ili kufika sehemu nyingi zaidi duniani. 

Hamna shirika lingine lenye kuleta tija na ushindani wa viwango hivi katika sekta hii”. Katika mwaka 2015, Shirika la Etihad limezindua njia mpya kwenda Kolkata, Madrid, Edinburgh, Entebbe, Hong Kong na Dar es Salaam, pamoja na huduma ya moja kwa moja kwenda Brisbane.

Mwaka jana pia Etihad walianza kutumia ndege aina ya Boeing 787-9 Dreamliner, ambayo ilianza kutoa huduma za ndege za biashara kwenda Washington DC, Zurich, Singapore na Brisbane. Mtandao wa ndege aina ya Airbus A380 umeongeza huduma zake za kuelekea London Heathrow na kuanza safari mpya za kuelekea Sydney na New York.

Mwaka huu, Shirika litaongeza  safari zake za kwenda London Heathrow hadi kufikia safari tatu kwa siku hii ni pamoja na mwanzo wa safari mpya za ndege aina ya A380 kufika Mumbai na Melbourne, wakati Boeing 787 itaanza kupaa kwenda vituo vipya vya Düsseldorf, Perth, Shanghai, Istanbul na Johannesburg.

Etihad pia iliongeza mizunguko katika njia za kusafiria 16 zinazotumika hivi sasa ambazo hufika Bangkok, Chennai, Dammam, Delhi, Hong Kong, Hyderabad, Istanbul, Jeddah, Kochi, Kozhikode, Melbourne, Mumbai, Muscat, Seychelles, Tehran na Trivandrum.

Ili kukabiliana na kasi ya ukuaji wake, Shirika la ndege la Etihad liliongeza idadi ya washirika wake mwaka jana. Mkakati huu uliwapa fursa abiria zaidi ya milioni tano kutumia ndege za Etihad, iliyosababisha ongezeko la asilimia 43 ambayo ni abiria milioni 3.5 zaidi kuliko 2014.

Mkakati mwingine ni makubaliano waliyozindua na Shirika la kimataifa la ndege la Pakistan (PIA), wakati Etihad inaendelea kukuza na kuendeleza ushirika wake na mashirika ya  Air Serbia, American Airlines, flynas, Jet Airways, Korean Air, NIKI and S7.

Kutokana na hayo, Etihad sasa inawapa fursa abiria wake kuwa katika mtandao utakaowawezesha kusafiri na kusafirisha mizigo kwenda sehemu 600 kwa kuunganisha ndege na moja kati ya washirika wake 197 ama kusafiri na washirika wake wa “codeshare” 49.   
Mnamo mwezi wa nne wa mwaka 2015, Shirika la ndege la Etihad lilipata kibali kutoka kwa Ofisi ya Shirikisho la Usafiri wa Anga ya Uswisi (FOCA) kukamilisha asilimia 33.3 ya uwekezaji katika shirika la ndege la Darwin, ambazo ni ndege zinazoruka kanda za Uswisi.

Ndege za shirika la Etihad ziliripoti kubeba tani 592,090 sawa na ongezeko la asilimia 4 mwaka hadi mwaka. Mwaka jana, ndege hizi zimebeba asilimia 88 ya mizigo ya bidhaa kuingia na kutoka uwanja wa kimataifa wa ndege wa Abu Dhabi.

Katika mwaka 2015, Etihad imefikisha mizigo vituo vipya sita duniani na sasa huduma hii ya kusafirisha mizigo inapatikana katika jumla ya vituo 96 ambavyo hutumika na abiria wakati wa kusafiri. Shirika limepanua uwezo wake wa kusafirisha mizigo kufika masoko mapya yakiwemo Dakar, Nouakchott na Douala, ambapo imefanya jumla ya vituo vinavyosafirisha mizigo tu kuwa 20.

Kufikia mwisho wa mwaka 2015, Etihad ilifikisha jumla ya ndege 121 (ogezeko la asilimia 9 mwaka hadi mwaka) yenye wastani ya umri wa miaka 5.8- kulifanya kuwa shirika lenye ndege changa na zisizoharibu mazingira kati ya wapinzani katika sekta nzima. Mwaka 2015 Shirika lilipokea Airbus 11 (A380 nne, A321 sita na A320 moja) na Boeing 787-9 Dreamliner nne huku wakiongeza nafasi za kukodi pia.

Ili kuunga mkono mikakati iliyojiwekea ya kukuza mtandao wao duniani, shirika la Etihad litapokea ndege nyingine mwaka huu, zikiwemo Boeing 787-9 tano, A380 tatu na Boeing 777-200 Freighters mbili.

Bwana Hogan alisema: “Tumeingia mwaka 2016 kwa kujiamini kwamba nguvu tulizoonesha awali zitaendelea na zitatumika kuitambulisha Abu Dhabi kama kitovu cha usafiri wa anga duniani.

“Tunaendelea kukabiliana na changamoto, ikiwemo suala la ulinzi wa urithi wa wasafirishaji wakubwa Marekani na Ulaya. Tunaendelea kuboresha huduma zetu ili kuwahakikishia wasafiri wetu kwamba wanachagua kilicho bora kati ya sisi na washindani wetu”.

Rais Dkt. Magufuli aongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri Ikulu jijini Dar leo

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 14, 2016. Kulia kwake ni Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na kushoto kwake ni Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa. Picha na IKULU.

Benki ya Exim yaibuka na ushindi katika mechi ya ligi ya mabenki

0
0

Kikosi cha timu ya soka ya Benki ya Exim Tanzania ambacho kiliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Benki ya Akiba katika mechi ya pili ya ligi ya mabenki iliyofanyika katika Viwanja vya Karume jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Klabu ya soka ya Benki ya Exim imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Benki ya Akiba katika mechi ya pili ya ligi ya mabenki iliyofanyika katika Viwanja vya Karume jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Wafanyakazi wa benki hizo na mamia ya mashabiki wa mpira walijitokeza uwanjani hapo kuzishangilia timu hizo katika mechi yenye ushindani ushindani mkali iliyoshuhudia dakika 90 zikimalizika huku Timu ya Benki ya Exim ikiibuka vinara katika mtanange huo.

Ligi hiyo, inayoshirikisha benki zaidi ya 16, inalenga kuimarisha urafiki na ushirikiano baina ya mabenki licha ya kuwa washindani kibiashara.

“Benki ya Exim iliona umuhimu wa kushiriki katika ligi hii kwani ni nafasi ya kipekee sana kutambua umuhimu wa jamii ya benki katika kuleta maendeleo kwenye taifa letu. Lakini pia michezo ni afya, na kwa kushiriki katika ligi hii tunawapa fursa wafanyakazi wetu kuimarisha afya zao kupitia mazoezi,” alisema Bw Greyson Malisa, Meneja Msaidizi rasilimali watu wa benki ya Exim.

Ligi ya mabenki ilizinduliwa mwishoni mwa mwezi Novemba 2015 na inatarajiwa kufikia tamati mwishoni mwa mwezi huu ambapo washindi wataibuka na zawadi mbalimbali zikiwemo medali.

“Shukrani za dhati ziwaendee wachezaji waliotoa muda wao na kuweka juhudi, ujuzi na nguvu zao ili kupata ushindi huu. Nawasihi wachezaji waendeleze juhudi hizi ili tuweze kuibuka washindi wa jumla katika mashindano haya,” alihitimisha.

Airtel yazindua Duka la kisasa jijini Dar es saalam

0
0
Afisa huduma kwa wateja wa Airtel, Deogratius Gerald,(wakwanza kulia) akimuonyesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na Mawailiano Eng, Edwin Ngonyani jinsi ya kupata taarifa kuhusu huduma mbalimbali za Airtel kupitia komputa zilizoweka katika duka jipya la Airtel Expo wakati wa uzinduzi rasmi wa duka hilo jana katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam. Akishuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwn Sunil Colaso (nyuma katikati) na Meneja huduma kwa wateja bi, Zakia Omary
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na Mawailiano Eng, Edwin Ngonyani akiongea wakati wa uzinduzi wa duka jipya la kisasa la Airtel Expo lililopo katika makao makuu ya Airtel Morocco, jijini Dar es Saalam. Pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwn Sunil Colaso akifatiwa na Mkurugenzi wa mawasilino wa Airtel Bi Beatrice Singano Mallya.
Afisa huduma kwa wateja wa Airtel, Deogratius Gerald (kulia) akitoa maelekezo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na Mawailiano Eng, Edwin Ngonyani juu ya huduma zinazopatikana katika duka jipya wakati wa uzinduzi wa duka hilo. wakishuhudia (kutoka kushoto)katibu mkuu wa wizara ya mawasiliano prof faustine Kamuzora, Naibu katibu mkuu Dr Mary Sasabo na Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwn Sunil Colaso.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na Mawailiano Eng, Edwin Ngonyani pamoja na mkurugenzi mkuu wa Airtel kwa pamoja wakibonyesha kitufe kuashiria uzinduzi wa duka la Airtel Expo lililopo makao makuu ya Airtel jijini Dar es salaam.
Shamrashamra za uzinduzi wa duka la Airtel Expo Morocco, jijini Dar es Saalam.
Afisa huduma kwa wateja wa Airtel, Deogratius Gerald,(kwanza kushoto) akimuonyesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, na Mawailiano Eng, Edwin Ngonyani vifaa na simu mbalimbali vinavyopatikana katika duka jipya la Airtel Expo wakati wa uzinduzi rasmi wa duka hilo jana katika ofisi za makao makuu ya Airtel Morocco, jijini Dar es Salaam. Akishuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwn Sunil Colaso (wa kwanza kulia) akifatiwa na Meneja huduma kwa wateja bi, Zakia Omary.

Wizara ya Nisahati na Madini yatoa ufafanuzi mradi wa umeme wa Kinyerezi II

0
0
Mkuu wa Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam, wakati alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu mradi wa umeme wa Kinyerezi Awamu ya Pili, akielezea kuhusu habari zilizoandikwa kimakosa katika moja ya magazeti ya kila siku nchini jijini leo. Kulia ni Ofisa Habari Mwandamizi wa Idara ya Habari-Maelezo, Magreth Kinabo. (Picha na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)

Na Nyakongo Manyama- MAELEZO
14/01/2016
WIZARA ya Nishati na Madini  imekanusha habari iliyopotosha umma kuhusu   mradi wa umeme wa Kinyerezi II kuwa bado haujaanza na gharama zilizoandikwa si za kweli.

Wizara hiyo imekanusha habari hiyo, iliyoandikwa katika gazeti la Mtanzania la leo Januari 14, mwaka huu toleo namba8063,  lenye kichwa cha habari “ Harufu ya Jibu Mradi wa Umeme.”

Habari hiyo  ambayo ilieleza kwamba mradi huo ulizinduliwa na Rais Mstaafu wa  Serikali ya Awamu ya Nne, Mhe. Dkt.Jakaya Kikwete uligharimu Sh. trilioni 1.6 na kwamba fedha za ujenzi wa mradi huo zimetokana ubia kati ya Serikali ya Tanzania na Japan,ambapo Serikali ya Tanzania itakuwa na hisa ya asilimia 40 na kampuni ya SUMITOMO ya Japan asilimia 60. 

 Aidha habari hiyo ilidai kuwa Serikali inachangia fedha za ndani kwa asilimia 12 na zilizobaki zikiwa na mkopo kutoka benki ya Japan na kwamba gharama za mradi huo ziko juu ikilinganishwa miradi mingine akitolea mfano Kampuni ya TALLAWARA Power Station ya nchini Australia anayodai ilitaka kujenga mradi huo kwa dola za Marekani milioni 350.

Hayo yamesemwa leo na  Mkuu wa Mawasiliano Serikali  wa wizara hiyo,  Badra  Masoud alipokuwa akizungumza  na waandishi wa habari kuhusu habari hiyo katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es Salaam. 

“Serikali  ya Tanzania  iliingia makubaliano na Serikali ya Japan  ya mkopo wa masharti nafuu  wa dola za Marekani  milioni 292  kwa ajili ya kutekeleza mradi wa  kuzalisha umeme wa Megawati 240 utakaojengwa na kampuni ya SUMITOMO kama mkandarasi wa “EPC contractor” na sio kama mbia wa Serikali yaTanzania kama ilivyodaiwa.

“Mradi huo unamilikiwa na Serikali kwa asilimia 100 kupitia TANESCO  na hakuna mwekezaji mwingine katika mradi huo.Hivyo si kweli kwamba Serikali ya Tanzania na kampuni ya SUMITOMO zinawekeza kwa ubia wa asilimia 40 (kwa Serikali ya Tanzania) na asilimia 60 kwa SUMITOMO. Kwa maana hiyo, hatutauziwa umeme utakaozalishwa na mradi huu kwani ni mali yetu na hakuna gharama yoyote ya ziada kama alivyodai mwandishi wa habari hiyo,” alisema Badra.

Aidha Badra alisema mwandishi huyo alidai kwamba mradi huo ulizinduliwa na Rais wa  Serikali ya Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete, wakati ni  kwamba mradi huo haujazinduliwa bado na sasa upo katika maandalizi ya kuwekwa katika jiwe la  msingi.

 Akizungumzia kuhusu gharama za mradi huo, alieleza kuwa unatekelezwa kwa dola za Marekani milioni 344 sawa na Sh. bilioni 740 zikiwa ni mkopo wa masharti nafuu wa asilimia 85 sawa  na dola za Marekani 292 na mchango wa Serikali ya Tanzania kwa asilimia 15 sawa na dola za Marekani milioni 52 na sio asilimia 12 kama ilivyodaiwa na mwandishi huyo. 
“Mwandishi wa habari hii amejaribu kufananisha uwekezaji huu na uwekezaji wa TALLAWARA Power Station ya Australia na kudai kwamba gharama yake ingekuwa ndogo kuliko gharama ya mradi huu. 

Taarifa hii haina ukweli wowote kwa sababu gharama ya dola milioni 344 zinazotarajiwa kutumika mkatika mradi huu iko chini kuliko dola milioni 350anazodai mwandishi kwamba zingetumiwa na kampuni TALLAWARA.

“Aidha, kampuni ya TALLAWARA haijawahi kuomba au kuonesha nia ya kuwekeza katika mradi wowote wa kufua mradi wa umeme nchini. Pia ni muhimu ifahamike kwamba makubaliano ya mkopo huu yalikuwa yanakwenda sambasamba na utekelezaji wa mradi wenyewe (EPC with Financing).  
   
Badra aliongeza kwamba pamoja na kwamba gharama za uwekezaji wa mradi huo wa kwanza wa aina ya “Combined Cycle” nchini zinawiana na gharama za miradi mingine ya aina hiyo duniani, gharama za uwekezaji zinaweza kutofautiana kutegemeana na mazingira ya nchi na nchi, teknolojia iliyotumika na aina ya mitambo.

Hivyo sio suala la kulinganisha gharama ya mradi mmoja na mwingine.

Wizara hiyo imeshauri waandishi wa habari kufuata miiko na maadili ya uandishi wa habari kwa kuandika habari  zenye ukweli na sahihi na zilizozingatia pande zote mbili kwa kuwa ipo na tayari kujibu maswali ya waandishi wakati wowote.

DKT. KIJAJI ATOA SIKU 3 KUPATA MIKAKATI YA NAMNA YA KUTATUA SUALA LA UBADILISHANAJI WA FEDHA UNAOFANYWA KIHOLELA (BLACK MARKET) TUNDUMA

0
0
va1
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (kushoto) akishauriana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Abbas Kandoro (kulia) namna ya kutatua changamoto ya usafirishaji mizingo katika forodha ya Tunduma.
va2
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Kijaji (kushoto) akiongea na watendaji wa TRA Mbeya alipowatembelea ofisini kwao kujua matarajio yao pamoja na changamoto wanazokumbana nazo katika utendaji kazi. Kulia kwake ni Bw. Lucas Mnabi Kaimu Meneja TRA Mbeya.
va3
Mkuu wa Hazina Ndogo Mbeya Bw. Siwale (aliyesimama) akitoa ufafanuzi kwa Mhe. Dkt. Kijaji namna wanavyowahudumia wastaafu. Na kushoto kwake ni wafanyakazi wa Hazina Ndogo Mbeya.
va4
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Kijaji (katikati) akiandika dondoo za ujio wake katika ofisi za Mhakikimali Mkoa wa Mbeya. Aliyesimama ni Katibu wa Naibu Waziri Fedha na Mipango na Mchumi Bw. Moses Dulle akitoa utangulizi kabla ya kuanza majadiliano. Kulia ni Mhakikimali Mkoa wa Mbeya Bw. Simon Njoka na pembeni yake ni Mkuu wa Hazina Ndogo Mbeya Bw. Siwale.

………………………………………
Akizungumza na Meneja wa  Oparesheni ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Benki Kuu Mbeya Bw. Ibrahim Malongo, Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji alisema kumekuwa na ubadilishanaji fedha isio halali unaofanyika kiholela hapa Tunduma unaopelekea Serikali kukosa mapato.

Mhe. Dkt. Kijaji alifanya ziara hiyo eneo la tukio huko Tunduma na kujionea namna vijana hao wanavyofanya biashara hiyo bila wasiwasi wowote huku wakiwa wameshika fedha nyingi sana mikononi.

“Nakupa siku tatu, nataka unijulishe hali hii (black market) iko vipi kwa sasa, mikakati gani ambayo mmeipanga kwa sasa, nini kimefanyika na hatua gani zimechukuliwa ili kuiwezesha Serikali kupata mapato.” Mhe. Dkt. Kijaji alimwambia na kumsisitiza Meneja wa Oparesheni ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Benki Kuu Mbeya Bw. Ibrahimu Malongo.
Katika ziara hiyo Mhe.  Dkt. Kijaji aliutaka uongozi wa Benki Kuu Mbeya kufuatilia wakopeshaji wanaojiendesha kinyume na taratibu kwa kuwakopesha wananchi tena kwa riba kubwa bila kulipa kodi.

Hivyo amemuagiza Kaimu Mkurugenzi Bw. Malongo na amempa siku saba kulifuatilia suala hilo kwa karibu, kujua wakopeshaji hao wako wangapi, na wana mikakati gani ya kuiweka kihalali biashara hiyo ili wakopeshaji hao waweze kusimamiwa kwa sheria kanuni na taratibu bila kumuumiza mwananchi na waweze kulipa kodi.Mhe. Dkt. Kijaji alishauri Taasisi zilizorasmi ambazo zinakopesha kupunguza masharti yasiyo na tija ili kuwasaidia wananchi waweze kukopesheka na waweze kulipa ili maisha yao yaweze kuendelea.

Katika ziara yake Mhe. Dkt. Kijaji alipata fursa ya kuonana na uongozi wa TRA, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Abbas Kandoro, Hazina Ndogo na alipata fursa ya kuongea na Mkuu wa Hazina Ndogo Bw. Siwale pamoja na Mhakikimali Mkoa wa Mbeya Bw. Simon Njoka. Aliwasisitiza kufanya kazi kwa bidii na kuwataka wawe jicho la Serikali ndani ya Mbeya kwa kuangalia hasa utendaji kazi na kusimamia maadili ya kazi.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano
Wizara ya Fedha

Mhe. Kassim Majaliwa awataka wadau wa Sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kushirikiana na wakezaji kutoka nchini Japan

0
0
k5
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa, akizungumza na Wadau wa Sekta ya Ujenzi kuhusu Kuungana na Kushirikiana katika kuboresha Miundombinu hapa nchini katika Hoteli ya Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.
k6
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Eng.Joseph Nyamhanga akizungumza kuhusu fursa za Uwekezaji katika Sekta ya Miundombinu hapa nchini katika Mkutano huo uliyohusisha sekta binafsi na Serikali kuhusu namna ya kuboresha sekta ya Miundombinu.
k7
Naibu Waziri wa Miundombinu wa Japan Koji Yonetani akizungumza katika Warsha hiyo na kusema nchi yake iko tayari kushirikiana na Tanzania katika kuboresha Miundombinu hapa nchini.
k9
Watendaji na Wadau wa Sekta ya Ujenzi wakifuatilia mada zilizowasilishwa katika Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Serikali na Binafsi kuhusu Ubora wa Miundombinu nchini.
k8
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa (Wa kwanza kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Miundombinu wa Japan Koji Yonetani(Wa pili kulia) pamoja na Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng.Edwin Ngonyani (Wa Pili kushoto).

…………………………………………………………………………….
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amewataka wadau wa Sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kushirikiana na wakezaji kutoka nchini Japan katika kuendeleza miradi mbalimbali ya ujenzi, usafirishaji na mawasiliano nchini.
 Akizungumza jijini Dar es salaam katika mkutano uliowakutanisha wadau wa sekta hiyo kutoka nchini Japan na Tanzania, Waziri Mkuu Majaliwa amesema ushirikiano huo utaleta tija kwa taifa kwani wadau wa Sekta hiyo wataweza kujifunza masuala mengi kutoka kwa wataalam hao.
 “China na Japan ni moja ya nchi zenye Wakandarasi wengi na wazoefu katika sekta ya ujenzi, kushirikiana nao kutaongeza ushindani na kupelekea kupata fursa ya uwekezaji ndani na nje ya nchi, amesema Waziri Mkuu.Waziri Mkuu Majaliwa ameyataka Makampuni yote yenye miradi ya ujenzi nchini kufanya kazi vizuri na kumaliza kwa wakati katika kipindi hiki ili kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano.
 Amesema fursa ipo kwa Kampuni kutoka Nje ya nchi kufanya kazi na Kampuni za ndani kwa lengo la kupata Zabuni ndani na nje ya nchi, mara zinapotangazwa.“Kutokana na uchumi wa Tanzania kukua kwa kasi, hatuna budi Makandarasi wetu kuungana na kufanya kazi kwa ushirikiano na wenzenu kutoka nje ili kupata maendeleo katika Sekta hii”, alisisitiza Waziri Mkuu.
 Naye, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani kwa niaba ya Waziri, Prof. Makame Mbarawa amewaomba Wawekezaji, Wakandarasi na wadau wa Sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kutumia fursa hiyo, kuungana na kutengeneza kampuni za ubia baina ya nchi hizo mbili ili kuweza kujenga miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.
 “Tumieni fursa hii kupata elimu na uzoefu na hata kuunganisha Makampuni kwani wenzetu wa Japan wana uzoefu mkubwa na maendeleo katika Sekta hii, ukilinganisha na sisi”, alisema Naibu Waziri.
 Naibu Waziri huyo ameongeza kuwa kupitia mkutano huo Wakandarasi nchini wataweza kujifunza njia za kisasa ambazo zitasaidia katika kuboresha Sekta ya Miundombinu na Mawasiliano.
 Kwa upande wake Naibu Waziri wa Miundombinu kutoka Wizara ya Ardhi, Miundombinu, Usafirishaji na Utalii wa Japan, Bwana Takatoshi Nishiwaki, ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kukubali kushirikiana katika kuendesha mkutano huo na wadau wa sekta ya ujenzi wenye lengo la kubadilishana ujuzi na teknolojia kuhusu Miundombinu bora.Mkutano huo wa siku moja umewashirikisha Wawekezaji, Wakandarasi na na Wafanyabiashara kutoka nchini Japan na Tanzania walio katika Sekta ya Miundombinu na Mawasiliano.
 IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI, WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO.

KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI AKUTANA NA UJUMBE WA SERIKALI YA CHINA

0
0
el1
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel kulia akiongea na Kiongozi wa msafara kutoka Serikali ya China jimbo la Jiangxi Bw. Yao Yaping wa kwanza kushoto kuhusiana na uboreshaji wa sekta ya Utamaduni na Sanaa baina ya Serikali ya Tanzania na China, katikati ni Kaimu Mkurugenzi Sanaa Bi. Leah Kihimbi.(Picha na Benjamin Sawe- WHUSM)
el2
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel kulia akiongea na na Kiongozi wa msafara kutoka Serikali ya China jimbo la Jiangxi Bw. Yao Yaping wa kwanza kushoto kuhusiana na uboreshaji wa sekta ya Utamaduni na Sanaa baina ya Serikali Tanzania na China, katikati ni Kaimu Mkurugenzi Sanaa Bi. Leah Kihimbi.(Picha na Benjamin Sawe- WHUSM).
el4
Kiongozi wa msafara kutoka Serikali ya China jimbo la Jiangxi Bw. Yao Yaping wa kwanza kushoto akiongea na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel wa kwanza kulia kuhusiana na uboreshaji wa sekta ya Utamaduni na Sanaa baina ya Serikali Tanzania na China, katikati ni Kaimu Mkurugenzi Sanaa Bi. Leah Kihimbi.(Picha na Benjamin Sawe- WHUSM
el5
: Kiongozi wa msafara kutoka Serikali ya China jimbo la Jiangxi Bw. Yao Yaping wa kwanza kushoto akimpa zawadi Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel mara baada ya mazungumzo ya uboreshaji wa sekta ya Utamaduni na Sanaa baina ya Serikali Tanzania na China, katikati ni Kaimu Mkurugenzi Sanaa.(Picha na Benjamin Sawe- WHUSM)

Serikali yaokoa zaidi ya Bilioni 3 kwa kudhibiti utoroshaji na biashara haramu ya madini nchini.

0
0

UDHIBITI WA UTOROSHAJI NA BIASHARA HARAMU YA MADINI

Moja ya majukumu ya Wakala wa Ukaguzi wa madini Tanzania (TMAA) ni kufuatilia na kuzuia utoroshaji/magendo na biashara ya madini unaopelekea ukwepaji wa ulipaji mrabaha kwa kushirikiana na taasisi nyingine husika za Serikali zikiwemo Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Jeshi la Polisi, Idara ya Usalama wa Taifa, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Idara ya Uhamiaji.

Taarifa za matukio ya udhibiti wa utoroshaji na biashara haramu ya madini zilizopo zinaonesha kuwa katika kipindi cha kuanzia mwezi Julai 2015 mpaka Januari 13, 2016 kulikuwepo na jumla ya matukio 14 ya utoroshaji wa madini ambapo madini yenye thamani ya Dola za Marekani 1,474,194 milioni (zaidi ya Shilingi bilioni 3,235,856,181) yalikamatwa na wakaguzi wa Wakala kupitia Madawati ya Ukaguzi yaliyopo katika viwanja vya ndege vya Dar es Salaam (JNIA), Kilimanjaro (KIA) na Mwanza.

Katika matukio ya hivi karibuni ya ukamataji wa madini katika viwanja vya ndege, madini yenye thamani ya jumla ya Shilingi milioni 11,217,300 yalikamatwa na wakaguzi wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA) kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola.

Raia mmoja wa kigeni na mwingine wa Tanzania walikamatwa wakiwa na madini hayo bila kuwa na kibali chochote cha usafirishaji kulingana na Sheria ya Madini ya mwaka 2010. Raia wa kigeni (jina limehifadhiwa) ambaye alikuwa anasafiri kwenda Bangkok alikamatwa akiwa na madini aina mbalimbali ikiwemo almasi, aquamarine, sapphire, green tourmaline, quartz na rhodolite.

Tukio la pili, mtuhumiwa mwingine ambaye ni raia wa Tanzania aliyekuwa akisafiri kwenda Ujerumani alikamatwa akiwa na madini mbalimbali ikiwemo amethyst, moonstone cabochon, rulilated quartz (cabochon), rulilated quartz(faceted), chrysoprase, green tourmaline, ruby, red garnet, green quartz, zircon na rhodolite.

Kufuatia Matukio hayo wahusika wote wamechukuliwa hatua za kisheria ikiwamo kufunguliwa kesi mahakamani.

Wakala unatoa rai kwa Umma kujiepusha na shughuli za utoroshaji/magendo na biashara haramu ya madini, kwani hatua kali zitaendelea kuchukuliwa kwa yeyote atakayebainika/kukamatwa akijihusisha na shughuli hizo. Aidha, madini yatakayokamatwa yakisafirishwa kinyume cha sheria na taratibu zilizopo yatatafishwa na Serikali.

Aidha, Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini inatoa wito kwa yeyote atakayetoa taarifa za utoroshaji/magendo na biashara haramu ya madini kwa Kamishna wa Madini au Wakala ambazo zitawezesha ukamataji wa madini, atazawadiwa fedha taslimu ambazo ni sawa na asilimia 5 ya thamani ya madini yatakayokamatwa na kunadiwa. Kwa mawasiliano ya haraka, wananchi watumie barua pepe info@tmaa.go.tz na simu 022-2137142 au 022-2601819.

IMETOLEWA NA
DOMINIC RWEKAZA
MTENDAJI MKUU
WAKALA WA UKAGUZI WA MADINI TANZANIA
15 JANUARI, 2016

PROF. MUHONGO ASIMAMISHA SHUGHULI ZA KAMPUNI YA OFF - ROUTE TECHNOLOGY ILIYOPO KYELA

0
0
Serikali imesimamisha  shughuli za uchimbaji wa Makaa ya Mawe ya Kampuni ya Off Route Technology  iliyopo Kyela ikiwemo kukamata vifaa vya uchimbaji na kuhakikisha kuwa  vinakuwa chini ya uangalizi wa  Mkoa wa Mbeya hadi hapo  uchunguzi dhidi ya uhalali wa kampuni hiyo kuchimba makaa utakapokamilika.Hatua hiyo inafuatia ziara ya Waziri wa Nishati na Madini, Prof Sospeter Muhongo kutembelea mgodini hapo na kubaini kuwa, kampuni hiyo inachimba makaa bila kuwa na leseni halali ya uchimbaji madini.

Aidha, Prof. Muhongo ameitaka kampuni hiyo kulipa kodi zote za Serikali ikiwemo inazodaiwa na Halmashuri tangu ianze kufanya shughuli za kuchimba.Aidha, ili kujua undani wa suala hilo, Prof. Muhongo ameitisha kikao kifanyike kati ya mgodi huo ,  Wizara ya Nishati na Madini,  Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania ( TMAA), Ofisi ya Madini Kanda ya Kusini Magharibi,  Katibu Tawala wa Wilaya ya Kyela, tarehe 18 Januari, 2016 chini ya uenyekiti wa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini.

"Hawa  watu wamechimba makaa, wameuza bila kuwa na Leseni na tunawadai kodi zetu. Uongozi hakikisheni katika kikao hicho  mnakuja na madai yenu,TMAA pia mje na madai yenu", ameongeza Prof. Muhongo.

Prof. Muhongo pia amezitaka pande zote kuwasilisha nyaraka muhimu kuhusu suala hilo, ili  iamuliwe kwa kufuata sheria na taratibu stahili, "hakuna mtu atakayeonewa, kila upande uje na nyaraka zote na sisi wizarani huko ndani kwetu tutaulizana wenyewe kuhusu jambo hili halafu tutalitolea taarifa" ,amesema. Prof. Muhongo.

Akifafanua kuhusu suala hilo , Afisa Mfawidhi  wa TMAA ,Mhandisi Jumanne Mohamed amesema kuwa, awali Wakala huo ilifanya ukaguzi na kubaini kuwa kampuni hiyo hailipi kodi na kuwa yapo  malimbikizo ya madai ambayo  yalipaswa kulipwa na kuongeza kuwa baada ya mawasiliano  juu ya suala hilo, kampuni  iliahidi kulipa kwa awamu jambo ambalo halijafanywa hadi sasa.Kampuni ya Off Route Technology,  ipo katika Kijiji cha Ngana Wilaya ya Kyela mkoa wa Mbeya.

WAHITIMU 67 WA MAFUNZO YASIYO RASMI WA CHUO CHA VETA WAPATA VYETI LEO JIJINI DAR ESALAAM.

0
0
Na Chalila Kibuda wa Globu ya Jamii.
WAHITIMU 67 wasio katika Mfumo Rasmi watunukiwa vyeti katika kuwarasimisha katika ujuzi waliopata  katika maeneo yao ya kazi.

Akizungumza katika mahafali hayo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mafunzo na Ufundi Stadi (VETA),Geofrey Sabuni amesema kuwa wataendelea kutoa mafunzo hayo ili kuwatambua mafundi wa mitaani ambao wamekuwa hatambuliki kutokana na kukosa mafanzo katika taasisi zinazotambulika.

Amesema kuwa nia ya kuwafikia watu 5000 katika kurasimisha kazi wanazozifanya kutokana na mchango mkubwa wa taifa huku wakiwa hawatambuliki.

Sabuni amesema kuwa VETA itahakikisha inaendelea kutoa mafunzo kwa vijana katika ujuzi mbalimbali pamoja na wale ambao hawako katika mfumo rasmi kuwatambua.

Aidha amesema kuwa katika jitihada zote kuna changamoto hivyo kwa wahitimu lazima waendelee kuongeza ujunzi wa mafunzo ya muda mrefu  katika kuwa wabobezi huku wakiwa na vyeti vinavyoonyesha ujuzi.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Veta Dar es Salaam,Violet Fumbo amesema katika mafunzo wanayotoa wanatambulika sehemu zote kutokana na mafunzo hayo kuingizwa katika mitaala.

Violet amesema katika mambo wanayoyafanya ni kutaka vijana kujituma katika ujuzi waliofanya kazi hiyo 



 Afisa mitihani wa chuo cha ufundi cha VETA kilichopo Temeke,Elishawake Lema akifungua sherehe za Mhafari kwa wanafunzi waliojiunga kozi ya muda mfupi ambayo Veta wameshirikiana na na shilika la kazi Duniani (ILO) kwa kutoa mafunzo hayo. mafunzo hayo ni Upishi, ufundi uwashi, ufundi wa magari na upambaji.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Chuo cha ufundi stadi cha Veta, Geofrey Sabuni akizungumza na wahitimu wa mafunzo ya muda mfupi katika chuo hicho leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkuu wa  Chuo cha ufundi stadi cha Veta, Violet Fumbo kulia akisoma lisala  mbele ya wahhitimu na mgeni rasmi katika mahafari ya muda mfupi ya chuo cha ufundi cha Veta leo jijini Dar es Salaam. waliokaa kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya mafunzo ya ufundi stadi (VETA), Geofrey Sabuni  Mwakilishi wa Shirika la Kazi (ILO), Albert Okal na Afisa mitihani wa chuo cha ufundi cha VETA kilichopo Temeke,Elishawake Lema.

Mwakilishi wa Shirika la Kazi (ILO), Albert Okal akizungumza na wahitimu wa chuo cha mafunzo stadi ya ufundi cha Veta jinsi walivyo shirikiana na chuo hicho ili kuondoa okosefu wa ajira kwa baadhi ya vijana walioweza kufanikiwa kujiunga na kozi ya muda mfupi katika chuo hicho.
Walimu waliofanikisha mafunzo kwa wanafunzi na wahitimu wa leo katika chuo hicho.




Wahitimu wakisimsikiliza mgeni rasm katika mahafari hayo leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wakiongalia matisheti yao yakiwa na nembo ya shirika la kazi duniani (ILO) leo katika mahafari ya mafunzo hayo.


Katika mahafali hayo wametunukiwa vyeti vya kufuzu masomo yao katika chuo cha mafunzo ya ufundi Stadi (VETA) leo jijini Dar es Salaam.
Viongozi wa chuo wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wahitimu leo jijini Dar es Salaam.

MKUU WA WILAYA YA RUANGWA MKOA WA LINDI,MARIAM MTINA ATOA MACHOZI WAKATI WA KUPOKEA MSAADA MASHINE TOKA VODACOM FOUNDATION

0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mkoa wa Lindi,Mariam Mtina(wasita toka kushoto)akimsikiliza kwa umakini Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya hiyo, Omary Rajabu(kulia)alipokuwa akiwaelezea baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,Wauguzi wa hospitali hiyo na wananchi jinsi mashine inayofyonza uchafu(Electrical Suction machine) kwa watoto waliozaliwa kabla ya wakati”Njiti” Zaidi ya shilingi Milioni 6/- zilitumika katika kunua vifaa hivyo na kutolewa msaada na Vodacom Foundation kupitia taasisi inayojishughulisha na watoto hao ya Doris Mollel. 
 Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mkoa wa Lindi,Mariam Mtina(wapili toka kushoto)pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania, Wauguzi wa hospitali hiyo na wananchi wakimsikiliza Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa,Dkt Japhet Simeo(kushoto)akiwaelimisha jinsi mashine ya Oxygen inavyosaidia watoto waliozaliwa kabla ya wakati”Njiti” kupumua wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya msaada wa mashine hizo zilizogharimu zaidi ya shilingi milioni 6/- na kukabidhiwa na Vodacom Foundation kupitia taasisi inayojishughulisha na watoto hao ya Doris Mollel.
 Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mkoa wa Lindi,Mariam Mtina(katikati)akitoa shukurani kwa niaba ya wananchi wake kwa Meneja wa Vodacom Foundation,Sandra Oswald na Mwanzilishi wa taasisi ya Doris Mollel inayojishughulisha kusaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati”Njiti”,Doris Mollel(kulia)kuhusiana na msaada wa mashine ya kupumulia na vifaa mbalimbali uliotolewa na Vodacom Foundation kupitia taasisi ya Doris Mollel vya kuwasaidia watoto hao wanaozaliwa katika wilaya hiyo.Vifaaa hivyo viligharimu zaidi ya shilingi milioni 6/-
 Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mkoa wa Lindi,Mariam Mtina(watatu toka kushoto)akipokea msaada wa mashine inayofyonza uchafu kwa watoto waliozaliwa kabla ya wakati”Njiti”kwa niaba ya wananchi wa wilaya hiyo toka kwa Meneja wa Vodacom Foundation, Sandra Oswald.Msaada huo uliotolewa na Vodacom Foundation kupitia taasisi ya Doris Mollel,Uliogharimu zaidi ya shilingi milioni 6/-
Baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Ruangwa Mkoa wa Lindi,wakifurahia msaada wa mashine mbalimbali uliotolewa na Vodacom Foundation kupitia taasisi ya Doris Mollel inayojishughulisha kusaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati”Njiti”Msaada huo ulikabidhiwa hivi karibuni.

DC ATOA WIKI MBILI WANAFUNZI WAENDE SHULE

0
0
Na Woinde Shizza 
Mkuu wa Wilaya ya SimanjiroMkoani Manyara, Mahmoud Kambona ameagizawanafunzi wote waliofaulu kujiunga nashule za sekondari wilayani  humo wawe wamewasili kwenye shule zao na kuanzamasomo baada ya wiki mbili.

Kambona alitoa agizo hilo juzialipokuwa anakagua shule ya Sekondari Msitu wa Tembo na kuzungumza na watendajiwa vijiji, kata, madiwani na maofisa Tarafa, kuhusiana na wanafunzi waliofaulukujiunga na masomo ya sekondari. Alisema wanafunzi wote waliofaulukujiunga na Sekondari wanatakiwa wafike kwenye shule zao baada ya muda wa wikimbili kwa ajili ya masomo na endapo wasipotekeleza hilo atawachukulia hatuakali viongozi wa eneo husika.


 “Nitawachukulia hatua
kali viongoziwote wakiwemo madiwani, maofisa tarafa, watendaji wa
kata, vijiji na wenyevitiwa vijiji wa sehemu husika ambao wanafunzi wote waliofaulu watakuwa hawajafikashuleni,” alisema Kambona.

Pia,
aliwaagiza wakuu wa shule zasekondari za wilaya hiyo kuwaelekeza
wazazi na walezi wa watoto ambao wamefaulukujiunga na shule zao, juu ya majukumu yao na majukumu ya serikali kuhusiana naelimu bure.Baadhi
ya wazazi wa wanafunziwaliofaulu Joseph Odoyo na Mustafa Seif walisema
dhana ya elimu bure ya RaisJohn Magufuli bado hawajaielewa kwani iliondolewa ni ada pekee ila chakula na mahitajimengine
wanachangia.

“Ada ya sh20,000 ndiyo pekee iliyofutwaila tunachangia huduma nyingine za mpishi sh.15,000 kuni sh15,000 kusaga na
kukoboash15,000 kulima shamba la shule sh.15,000 na viungo sh10,000 kwa muhula mmoja,”alisema Odoyo. Alisema pia wazazi wanatakiwa
kuchangiakilo 80 za mahindi, kilo 35 za maharage, kilo tano za sukari,
kilo 12 za mchelena lita tano za mafuta ya kula kwa muhula mmoja ila sh5,000 ya muhuri wa nemboya shule imetolewa.

MBUNGE MWAMOTO ACHANGIA UJENZI WA DARASA LA CHEKECHEA , ASEMA RAIS DR MAGUFULI KAFUTA ADA NA MICHANGO SIO MICHANGO YA UJENZI WA SHULE

0
0
Mbunge  wa  jimbo la  Kilolo  Bw  Venance Mwamoto akikabidhi  fedha  akisi cha Tsh 500,000 kati ya Tsh milioni 1 alizoahidi kuchangia ukarabati    wa darasa la chekechea kijiji  cha Isele kata ya  Ilula 

........................................
Na MatukiodaimaBlog
MBUNGE  wa  jimbo la Kilolo  mkoani Iringa Bw  Venance  Mwamoto achangia  kiasi cha Tsh milioni 1 kwa ajili ya kuwaunga mkono  wananchi  wake kijiji  cha Isele kata ya Ilula  wilaya ya  Kilolo ambao  wamejitolea  kufanya ukarabati wa darasa la  chekechea kwa lengo la  kusogeza elimu kwa watoto  kijijini hapo.

Huku  akiwataka  wananchi  wote  kuendelea  kuchangia ujenzi  wa vyumba  vya madarasa ,shule na nyumba  za  walimu na kuwa serikali ya Rais Dr John Magufuli  imefuta ada na michango na  sio uchangiaji wa ujenzi .

Akikabidhi  kiasi cha Tsh  500,000 kati ya Tsh milioni 1  ambayo amepanga  kuwachangia wananchi hao leo  mbunge  huyo  alisema  kuwa baada ya  kufika kuhamasisha wananchi kuchangia  shughuli za  kimaendeleo zikiwemo  za  elimu  alikutana na changamoto ya ukosefu  wa darasa la awali katika  kijiji  hicho na  hivyo kuwahamasisha  wananchi  kuanza kutatua  tatizo  hilo.

Bw  Mwamoto  alisema  kuwa baada ya   kufika katika  kijiji   hicho   uongozi  wa kijiji  ulimtembeza  eneo hilo ambalo  wananchi walikusudia  kufanya  ukarabati  wa darasa kwa ajili ya wanafunzi  wa  chekechea  na kuwa mahitaji yote pamoja na nguvu  za wananchi ilikuwa  ni Tsh milioni 2 na hivyo kulazimika  kuchukua  mzigo wa kuchangia pesa kiasi hicho  cha Tsh milioni 1

" Kimsingi hali ya  darasa  lile haikunifurahisha  hivyo  niliwataka  kufanya marekebisho  ili  watoto hao  kuweza  kusoma katika mazingira  bora  zaidi na hii  pesa nimetoa kwa ajili ya kuanza kazi hiyo na pindi  wakimaliza nitamalizia  pesa  iliyosalia "

Hata    hivyo mbunge  Mwamoto  aliwataka  wananchi  kuendelea  kuchangia shughuli za kimaendeleo hasa  elimu na  kuwa  serikali ya Rais Dr John Magufuli  imefuta michango na ada kwa elimu ya msingi na sekondari  na  sio kwamba imefuta michango ya ujenzi wa nyumba za walimu ama shule .

Hivyo  aliwataka  wananchi  kuendelea jitihada zao  za  kushiriki  kuchangia maendeleo ya  elimu kwa maana ya ujenzi  wakati  serikali  imechukua  jukumu la kuwalipia  watoto  hao ada na chakula kwa shule za  sekondari za bweni ambazo zipo chini ya  serikali.

Alisema  kuwa  yeye kama mbunge  wao kamwe hata  waacha yatima  katika shughuli  yoyote ya kimaendeleo atahakikisha anashirikiana na  wananchi hao  kikamilifu katika  kuitekeleza .

Afisa  mtendaji wa kata ya Ilulu  Bw  Chusi Ashrafu akimpongeza mbunge Mwamoto kwa kuunga mkono  nguvu za  wananchi hao alisema  kuwa hadi sasa mwitikio  wa wananchi katika shughuli za kimaendeleo ikiwemo ya umaliziaji wa madarasa  hayo  ni nzuri .

Alisema hadi sasa wananchi  wa  vitongiji  vyote  vitatu wameonyesha  ushirikiano mzuri zaidi kwa  kila kitongoji  kuchangia kiasi cha Tsh 200,000 na  wana jumla ya Tsh 600,000 kati ya Tsh milioni 1 ambayo wananchi  walipaswa  kuchangia wakati mbunge akiahidi kuchangia Tsh milioni 1 na kwa  sasa mwenyekiti wa Halmashauri ya  Kilolo pia ameahidi kumuunga mkono Mbunge Mwamoto kwa kuchangia Tsh 200,000 hivyo wanamatumaini  kasi ya  ujenzi  huo hadi  sasa imefikia pazuri  zaidi.

PROF. MUHONGO AITAKA KAMPUNI YA TANZU YA TANESCO (TGDC) KUHARAKISHA UZALISHAJI WA NISHATI YA JOTOARDHI KUTOKA ZIWA NGOZI.

0
0
Na Asteria Muhozya
WAZIRI wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo ameiaigiza  Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi  Tanzania (TGDC Ltd) kuwa ifikapo June 2016, iwe imeanza kuchoronga mashimo 3 katika eneo la Ziwa Ngozi ikiwa ni hatua ya mwisho inayohitajika kabla ya kuanza kujenga mitambo ya kuzalisha jotoardhi.

"Utafiti muhimu umekamilika. Joto la maji ni kubwa, 230-250C linalokidhi uzalishaji wa umeme. Hiki kitakuwa ni chanzo kipya muhimu cha umeme jadidifu" ,alisema Prof. Muhongo.

Ameongeza kuwa, jambo hilo haliwezi kuendelea kusubiri kutokana na mahitaji ya nishati hiyo nchini ikizingatiwa kuwa, Tanzania inapitiwa na  Bonde la Ufa kwa kiasi kikubwa.

"Tayari wenzetu Kenya na Ethiopia wamepiga hatua kubwa katika nishati hii lakni kwa upande wetu hatuna megawati hata moja kwa hili lazima tuchukue hatua tutoke hapa tulipo. Hakuna kusubiri anzeni na Ziwa Ngozi" amesema Muhongo.

Prof. Muhongo aliitaka Kampuni hiyo kuongeza nguvu katika eneo lenye viashiria vya jotoardhi la  Ziwa Ngozi kutokana na kuwepo maendeleo makubwa ya kitafiti ikilinganishwa na maeneo mengine yenye viashiria kama hivyo ikiwemo eneo la Mbaka lililopo Wilaya ya Rungwe.

"TGDC tunataka umeme wa jotoardhi, wananchi wanataka umeme, hawatakuwa kusikia maneno, ifikapo Mwezi juni na  mimi nitakwenda Ngozi kuangalia mmefikia wapi na kama hakuna maendeleo tutabadilisha timu ya wataalamu", alisisitiza Prof. Muhongo.

Akizungumzia kuhusu fedha za miradi, Prof. Muhongo alieleza kuwa, nchi nyingi duniani hazitegemei fedha za Serikali kutekeleza  miradi mikubwa ya nishati na ndiyo sababu hata Tanzania inatafuta fedha katika taasisi mbalimbali ikiwemo kukaribisha wawekezaji  ili kutekeleza miradi hiyo.

"Serikali kwa upande wake itasaidia kuwezesha upatikanaji wa fedha za kutekeleza miradi na ninyi kazi yenu ni kuhakikisha umeme wa jotoardhi unaanza kutumika Tanzania kwa kuanza na Ziwa Ngozi".

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro alisema kuwa amefarijika na maelekezo aliyoyatoa Prof. Muhongo na kuahidi kuweka nguvu kubwa katika kufuatilia suala hilo. " Ujio wako umetupa ari mpya katika kusimamia miradi hii kwa sababu rasilimali zipo lakini zimekaa tu nakuahidi kasi ya ufuatiliaji itaongezwa",alisema Kandoro

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Rugwe ,Mwalimu Zainabu Mbusi alieleza kuwa maagizo ya Prof. Muhongo yamekuwa faraja na kuongeza kuwa, kukamilika kwa mradi huo itaongeza kasi ya ukuaji uchumi na kuifanya Tanzania kufikia lengo lake la kuwa miongoni mwa nchi za uchumi wa Kati ifikapo 2025.

Kwa pande wake  Mbunge wa Jimbo la Busokelo, Fred Atupele alieleza kuwa, kukamilika kwa mradi huo kutachochea kasi ya uendelezaji wa viwanda vikubwa na vidogo na kueleza kuwa, kwa nafasi yake  watachukua jukumu la kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa vyanzo hivyo.

Awali akieleza akieleza Mikakati ya Taasisi hiyo, Mkurugenzi wa TGDC , Mhandisi Boniface Njombe alisema eneo la Mbaka ni miongoni mwa maeneo ya maji moto yenye viashiria vya nishati ya jotoardhi.

Vilevile, alieleza hivi sasa wataalam kadhaa wamesambaa wakifanya tafiti za mwisho katika  eneo la Mbaka ili kuanisha mipasuko na maeneo ya kuchimba nishati hiyo na kuongeza kuwa, TGDC imelenga kwa  kuanza kuzalisha umeme wa jotoradhi  wa kiasi cha  megawati 200 huku lengo ikiwa ni kufikia megawati 5000.

Aidha, alieleza kuwa, mbali na kuzalisha umeme , maji moto yanaweza kutumika viwandani na majumbani katika kukausha mazao ikiwemo kuwa kivutio cha utalii kuoga kwa kuwa inaelezwa kuwa maji hayo yanatajwa kuwa tiba ya magonjwa ya ngozi.

Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazopitiwa na Bonde la Ufa eneo ambalo linatajwa kuwa na viashiria vya nishati ya jotoardhi.
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live




Latest Images