Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

KUTOKA UWANJA WA FURAHISHA JIJINI MWANZA KATIKA MAOMBI YA KUMUOMBEA RAIS MAGUFULI.

$
0
0
Januari 13,2016 Umoja wa Makanisa Jijini Mwanza unawakutanisha Watanzania katika Uwanja wa Furahisha uliopo katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza kwa ajili ya Maombi ya rasmi ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli pamoja na Wasaidizi wake ili kuliongoza Taifa vema.

Pia maombi hayo ni mahususi kwa ajili ya kuliombea Taifa kwa ajili ya kupata baraka mbalimbali. Kuanzia majira ya saa saba Wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo jirani wameanza kujongea kwa ajili ya kujumuika pamoja katika maombi hayo ambayo yatafikia tamati jioni.

Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo huku wageni mbalimbali wakiwemo Viongozi wa dini pamoja na waimbaji nyimbo za injili wakihudhuria katika maombi hayo.

Picha na George Binagi.

NAIBU WAZIRI WIZARA YA HABARI AKIWA KWENYE ZIARA RUFIJI.

$
0
0
 Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Anastazia Wambura akiongea na watumishi wa Wilaya ya Mkuranga wakati ya ziar ya kujionea shughuli za maendeleo ya sekta ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Wilayani humo, wa pili kutoka kulia na Mbunge wa jimbo la Mkuranga Mh. Abdala Ulege na wa pili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mh. Abdalla Kihato.
Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Anastazia Wambura wa pili kutoka kulia akipokea taarifa ya utekelezaji wa kikundi cha Sanaa za maigizo kilichopo wilaya ya Rufiji Bw. Bashiru Kibopo wakati ya ziara ya kujionea shughuli za maendeleo ya sekta ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Wilayani humo,wa pili kutoka kushoto ni Mbunge wa jimbo hilo Mh. Allyseif Ungando na wa kwanza kulia ni Katibu Tawala Wilaya ya Rufiji Bi. Maria Katemana. 
Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Anastazia Wambura aliyenyoosha mkono akiongea na baadhi ya wasanii waliojenga katika kijiji cha Wasanii na wanahabari kilichopo Wilayani Mkuranga wakati ya ziara aliyofanya ya kujionea shughuli za maendeleo ya sekta ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Wilayani humo. 

 Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Anastazia Wambura (mbele) akiongea na wakazi wa Wilaya ya Mkuranga katika uwanja wa wilaya hiyo uliojengwa kwa nguvu za Serikali ya mtaa na nguvu ya wananchi uliogharimu shilingi milioni sabini na mbili.
Mbunge wa jimbo la Mkuranga Mh. Abdalla Ulege akiongea na wakazi wa jimbo lake wakati wa ziara ya Naibu Waziri, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Anastazia Wambura ya kujionea shuguli za maendeleo ya sekta hiyo. 
Mwenyekiti wa mtandao wa wasanii (SHIWATA) Bw. Cassim Talib katikati akimuonyesha baadhi ya nyumba za wasanii na wanahabari zilizopo Wilayani humo Mh. Anastazia Wambura wa kwanza kushoto wakati ya ziara ya kujionea shughuli za maendeleo ya sekta ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Wilayani humo., kulia ni msanii wa sanaa za maigizo maarufu kama mzee Chilo. 
 Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Anastazia Wambura akisalimiana na Mbunge wa Rufiji Mh. Allyseifu Ungando wakati wa ziara ya kujionea maendeleo ya sekta ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wilayani humo.
 (Picha na Benjamin Sawe- WHUSM).

MAJALIWA AKUTANA NA BALOZI WA RWANDA HAPA NCHINI.

$
0
0



 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akizungumza na Balozi wa Rwanda nchini, Mhe. Eugene Kayihura walipokutana Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Januari 13, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Rwanda nchini, Mhe. Eugene Kayihura kabla ya mazungumzo yao, Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Januari 13, 2016.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Rwanda nchini, Mhe. Eugene Kayihura kabla ya mazungumzo yao, Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Januari 13, 2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO WA MIRADI YA UBIA KATIKA UJENZI WA MIUNDOMBINU KATI YA JAPAN NA TANZANIA.

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua mkutano wa miradi ya ubia katika ujenzi  wa Miundombinu kati ya Japan na Tanzania kwenye hoteli ya Hyatt Regency- Kilimanjaro jijini Dar es salaam Januari 14,2016. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Waziri wa Ardhi , Miundombinu, Uchukuzi, na Utalii wa Japan, Bw. Takatoshi Nishiwaki baada ya kufungua  mkutano wa miradi ya ubia katika ujenzi  wa Miundombinu kati ya Japan na Tanzania kwenye hoteli ya Hyatt Regency- Kilimanjaro jijini Dar es salaam Januari 14,2016. Kushoto ni Naibu Waziri wa Ujwnzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

DHANA YA USHIRIKIANO KUKABILIANA NA UHALIFU MTANDAO YALETA MAFANIKIO

$
0
0
Kukabiliana na uhalifu mtandao lazima papatikane mashirikiano "Collaboration"– Mashirikiano ya ndani pamoja na nje. Mara baada ya Hotuba yangu Nchini Afrika kusini ambapo niliibua dhana ya kuwekea mkazo kwenye kuimarisha ushirikiano kwani uhalifu mtandao hauna mipaka na uharibfu wake ni wa kupindukia. Mengi yameendelea kuonekana na dhana imeendelea kubeba uzito huku mataifa mengi yakihakiki yanazingatia hili kwa kuanzisha au kuunganisha vitengo vinavyosimamia dhana ya ushirikiano.

Aidha, Bado uhalifu mtandao umeendelea kukua maeneo mbali mbali ambapo imeonekana wahalifu mtandao wamejipanga upya na nguvu mpya – Huwenda ni baada ya Raisi wa Marekani Kuzuia kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwaka jana kukutana. Hatua aliyoichukua baada ya kuona mikutano yao ya kihalifu mtandao ilikua ikionyesha mafanikio kwa kukuza uhalifu mtandao maeneo mengi duniani hata Taifa hilo.



Tahadhari na maangalizo mbali mbali yameendelea kutolewa ili kuruhusu makampuni ,watu binafsi na Mataifa kujipanga zaidi na dhana ya kuzuia tatizo kabla halijatokea. Ambapo katika hotuba yangu Nchini Kenya mwishoni mwa mwaka jana hili nililiimiza zaidi.


Kama ilivyo ada, katika kupitia mapitio kadhaa ya kihalifu mitandao na ukuaji wa matumizi ya TeknoHAMA tumeendelea kutoa taarifa ya mategemeo ya uhalifu mtandao katika mwaka huu ili pia kutoa fursa ya mataifa kujipanga kukabiliana nayo yatakapo jiri na hata kujitahidi kutengeneza njia rafiki ya kuzuia kabla hayajatokea.
MAFANIKIO
Mapema mwanzoni mwa mwaka huu hatimae wahusika wa uhalifu mtandao uliotikisa anga ya usalama mtandao ambapo pesa nyingi zilifanikiwa kuingia mikononi mwa wahalifu baada ya kufanikiwa kuingiza kirusi cha Tyupkin kwenye Mashine za kutolea fedha "ATM" na kusababisha pesa kutoka bila mpangilio wamefanikiwa kutiwa nguvuni. Taarifa ya Tyupkin ilipojiri niliitolea ufafanuzi kupitia andiko linalosomeka kwa “KUBOFYA HAPA”

Aidha, Kupitia dhana ya ushirikiano baina ya mataifa mbali mbali ambapo pia imekua chanzo cha kufanikisha upatikanaji wa wahusika wa Tyupkin, Watuhumiwa wengine wa wili waliohusika na kundi la “DD4BC DDOS extortion” wametiwa nguvuni.
Mpango kabambe ulipangwa kuhakiki kundi hili lililo umiza vichwa vya wanausalama mitandao linasambaratishwa ambapo mataifa mengi yaliunganisha nguvu kukabiliana nalo na hatimae wiki hii mwanzoni ndoto ikatimia. Inaaminika wawili waliotiwa nguvuni si mwisho wa tatizo na bado jitihada zaidi zinaendelea.


KASI YA UHALIFU MTANDAO
Wakati mafanikio kadhaa kutoka katika mataifa mbali mbali hasa barani Ulaya ambapo kwa hakika tayari wamekua na mpango madhubuti baina ya Nchi zao kukabiliana na uhalifu mtandao huku wakishirikiana kwa karibu na mataifa nje ya umoja wao kufikia malengo bado tumeendelea kuona matukio kadha ya kihalifu mtandao ndani ya mwaka huu katika maeneo mengi.


Nchi ya Ukraine, Wahalifu mtandao walifanikiwa kuzima umeme ambapo tukio hilo limetafsiria kama “Wakeup call” kwa mataifa mengine kwani tayari hili lilisha bashiriwa kua mataifa yajipange kwenye mifumo ya umeme kwani wahalifu walisha tengeneza mikakati ya kuidukua na kuleta madhara.


Taarifa za awali zinaeleza kua uhalifu huo chanzo kimeonekana kutokea Nchini Urusi. Marekani imeshasema itatoa ushirikiano wa dhati kujua mzizi wa tukio husika na ufumbuzi kupatikana. Wakati Marekani ikijipanga kutoa usaidizi kwenye hili- onyo limetoka kua huwenda nayo ikawa nchi itakayofatia kwenye uhalifu huu hivyo nayo ijiweke/ijipange vizuri mapema.


Nissan nayo haijabaki salama, Wahalifu mtandao wa kundi la “Anonymous” wamefanikiwa kuidukua na kuiangusha wakidai ni namna yao ya kuandamana dhidi ya Japan. Nissan kufuatia tukio hilo ililazimika kufunga tovuti zake mara moja ikiwa ni hatua za kuhimili vishindo vya uhalifu huu mtandao dhidi yake.           
Swala la Makampuni ya magari kudukuliwa sio geni na mwaka jana tulishuhudia magari aina ya "Jeep" kuingiliwa na wahalifu mtandao yaliyosababisha magari hayo kupata ajali zisizotegemewa baada ya wahalifu mtandao wakiwa mbali kuweza kuyasababishia ajali hizo.

Nigeria pia Hamkani si shwari , Jumatatu ya wikii hii, Wakati ufunguzi wa mafunzo maalum ya kiuslama mtandao – Waziri wa TEHAMA wa Nchi hiyo Mh. Adebayo Shittu aliainisha kupitia hutuba yake kua makundi ya kihalifu mtandao yameendelea kulitesa taifa hilo kwa kuathiri wizara, mashirika ya kiserikali, mashirika ya kifedha na penginepo ambapo uhalifu huo umeendelea kuigharimu nchi hiyo zaidi ya dola za kimarekani Milioni 400 kila mwaka.


Mafunzo hayo maalum ni katika utekelezaji wa azimio la kuongezea uwezo wataalam tulio nao – Azimio ambalo limeendelea kutekelezwa na mataifa kadhaa kitaifa. Binafsi nategemewa kuendelea kushiriki kwenye mpango huu kwa Nchi ya Kenya kufuatia mwaliko maalum. Nitumie fursa hii kutoa wito kwa taifa la Tanzania kuliangazia hili kwani ni moja ya njia sahihi za kukabiliana na uhalifu mtandao nchini.


Marekani nako wahalifu wame chachamaa, Nchi hiyo imetoa tamko  kua kufuatia uangalizi kwenye mitandao yake, imebaini wahalifu mtandao waki vamia zaidi mifumo ya makampuni yao na tayari wameaza kuimarisha namna ya kukabiliana na uvamizi huo huku ikitahadharisha kuonekana kwa uhalifu mtandao kutegemewa kutatikisa zaidi mataifa mengi mwaka huu.


ANGALIZO - TAHADHARI


Microsoft imetangaza kwamba imeacha kutoa usaidizi wa kiufundi kwa matoleo ya awali ya kisakuzi chake cha Internet Explorer na kuwaweka hatarini mamilioni ya watu wanaotumia matoleo hayo.


Mabadiliko hayo yataathiri matoleo nambari 8, 9 na 10 ya kisakuzi hicho.


Baadhi ya mashirika yanakadiria kwamba matoleo hayo hutumiwa na takribani asilimia 20 ya Computerworld inasema kati ya watu wanaotumia Internet Explorer, ni asilimia 55 pekee wanatumia matoleo ya majuzi zaidi.


Visakuzi hulengwa na wadukuzi na wataalamu hubashiri uwezekano wa mashambulio kutokea na kuweka kinga kupitia kutoa matoleo mapya.


"Kuanzia Januari 12, 2016, ni toleo la karibuni zaidi la Internet Explorer litapokea usaidizi wa kiufundi na maboresho ya kiusalama,” Microsoft wamesema.

"Microsoft inawahimiza wateja kuboresha na kutumia toleo la majuzi zaidi na ili kuchakura mtandaoni kwa njia salama zaidi.”


Kampuni hiyo inaendelea kutoa usaidizi kwa matoleo ya IE 11 na Edge, ambayo kimsingi ndiyo hutumiwa na Windows 10.


NetMarketShare inakadiria kwamba wanaotumia Internet Explorer mtandaoni ni 57% wakilinganishwa na 25% wanaotumia Chrome, 12% wanaotumia Firefox na 5% wanaotumia Safari.


Aidha, Uhalifu  unao sababisha kufunga kwa mfumo wa mtumiaji na kumtaka atoe kiasi cha pesa ili aweze kuendelea na huduma maarufu kama “Ramsomware” unashika kasi hivyo makampuni na watu binafsi hawanabudi kujipanga.


MATARAJIO 2016 YA KIHALIFU MTANDAO


Watu binafsi, Makampuni na mataifa yameaswa kujipanga zaidi kufuatia matarajio na ongezeko la uhalifu mtandao mwaka huu ambapo zaidi tunategemea kuona na baadhi tayari yameanza kuonekana uhalifu mtandao utatikisa zaidi maeneo yafuatayo.


Matarajio ni kua Sekta ya Umeme, Anga na Elimu (Vyuo) vitegemee kupata itilafu ya kiuhalifu mtandao. Bado Mabenki nayo kupitia aina tofauti kadhaa mpya za uhalifu ili kuiba pesa ni miongoni mwa vinavyo tajwa.


Sekta ya Umeme tayari tumeona Ukraine ikifungua dimba huku mataifa mengi yakiaswa kujipanga. Wakati huo huo sekta ya Anga mpango kabambe wa kuimarisha kujipanga umewekwa huku tamthilia ya “CSI Cyber” ikitoa episodi maalum kulizungumzia hili mapema mwaka huu.


Hili likijiri Umoja wan chi za Ulaya “EU” imeanzisha rasmi “Digital ‘SWAT’ Team for Aviation” ambapo wataalam wabobezi watapata ajira kukabiliana na kujipanga dhidi ya tishio hili la kihalifu katka sekta ya Anga.


Vyo Kadhaa tayari vimeingiliwa na wahalifu mtandao na baadhi wametiwa nguvuni huku mataifa kadhaa yakijipanga kwenye hili.



Matarajio haya ni kwa uchache – Ila jitihada za mwaka huu maangalizo na kutumia njia mbali mbali patakua na mpango kabambe ya kuyatolea ufafanuzi sanjari na kuainisha namna ya kujipanga kukabiliana na hali mbaya ya kihalifu mtandao.


Nichukue Fursa hii tena kutoa wito kwa taifa la Tanzania kua sikivu kwenye hili ili kuweza kujipanga mapema na hali ya kihalifu mtandao kabla ya mambo kuharibika na kuanza kukimbizana kutafuta suluhu ya changamoto. 

MFUKO WA PPF WASAIDIA KITUO CHA AFYA MISASI.

$
0
0
 Meneja wa Mfuko wa PPF Kanda ya Ziwa, Meshach Bandawe, kushoto akimkabidhi Mbunge wa Jimbo la Misungwi na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia),msaada wa magodoro 20 na mashuka 20 kwa ajili ya kituo cha Afya Misasi.Kulia ni Happness Manyenye, Ofisa Mwandamizi wa PPFHafla hiyo ilifanyika kituoni hapo jana.
 Meneja wa Mfuko wa PPF Kanda ya Ziwa, Meshach Bandawe, kushoto akimkabidhi Mbunge wa Jimbo la Misungwi na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia),msaada wa magodoro 20 na mashuka 20 kwa ajili ya kituo cha Afya Misasi.Hafla hiyo ilifanyika kituoni hapo jana.Kushoto kwa waziri ni Mkurugenzi wa Hlmahsuari ya Misungwi, Nathan Mshana.
PPF Meneja.Meneja wa mfuko PPF,Meshach Bandawe kushotoka akizungunmza na baadhi ya wananchi wa Misasi kabla ya kukabidhi msaada wa magodoro na mashuka kwenye kituo cha Afya Misasi wa pili kutoka kujlia waliokaa ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga ambaye ni Mbunge wa jimbo la Misungwi,kushoto ni Mkurugenzi wa halmashauri wa Misungwi, Nathan Mshana na wa pili ni Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Khalid Mbitiyaza.
Picha zote na Baltazar Mashaka.

Na Baltazar Mashaka,MWANZA
MFUKO wa Pensheni wa PPF umetatua moja ya changamoto za kituo cha Afya Misasi,Wilayani Misungwi mkoani Mwanza baada ya kutoa msaada wa magodoro 20 na mashuka 20,yenye thamani ya sh.3.5 .

Msaada huo ulikabidhiwa jana kwa Mbunge wa Jimbo hilo, Charles Kitwanga ambaye ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,hafka iliyofanyika katika kituo hicho na kuhudhuriwa an Mkurugenzi wa Halmashauri wa Wilaya ya Misungwi.

Akikabidhi msaada huo, Meneja wa PPF Kanda ya Ziwa, Meshach Bandawe,alisema mfuko huo umekuwa ukisaidia jitihada za serikali kuboresha afya za jamii kwa kutoa misaada mbalimbali katika sekta ay afya.

Alisema wanafanya hivyo ili kuwasaidia na kuwawezesha wanachama wa mfuko huo wawe na afya bora ili waweze kuchangia kwa muda mrefu ikiwa ni pamoja na kuwakinga na majanga wawapo kwenye ajira.

“Msaada huu wa magodoro 20 na mashuka 20 licha ya kuwa si mkubwa utapunguza changamoto za kituo hiki cha Afya Misasi,na ni sehemu ya kuisadia serikali yetu kuboresha afya za wananchi wake na uwekezaji wa mfuko,”alisema Bandawe

Alimwomba Waziri na Mbunge huyo kuwa, awasaidie kutoa elimu kwa jamii ijunge na mfuko huo ili wanufaike na mafao yanatolewa na PPF kwa kuwakinga na majanga,ili pindi wakistaafua wasipate taabu baada ya kuwa wamekosa nguvu ya kufanya uzalishaji.

“Walimu,Walikuma na Wafugaji wanaweza kujiunga na mfuko kwa ujtaratibu maalum wa kujichangia,hivyo tunakuomba Mbunge utusaidie kutoa elimu kwa wananchi na kuwahamasisha wajiunge na mfuko wetu,”alisema Bandawe.

Naye Kitwanga akipokea msaada huo,aliushukuru mfuko huo akisema umepunguza kero ya magodoro na mashuka lakini pia marafiki zake wa nchini Australia wamesaidia kituo hicho kinachohudumia wilaya tatu za Kwimba, Shinyanga na Misungwi yenyewe, vitanda vya kisasa 16 vyenye thamani ya sh.16 milioni.

Alisema vifaa vizito kulingana na mahitaji ya kituo hicho vinatokana na bajeti ya wilaya kwa kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha tiba bora kwa wananchi zinapatikana kwa karibu.


“Tunahitaji vituo vya Afya kila Kata,hata kituo cha Misasi kinachohudumia baadhi ya vijiji vya wilaya za Shinyanga, Kwimba na Misungwi, kikipanuliwa bado hakitakidhi mahitaji isipokua msongamano utapungua.”alisema

Alisema Serikali itaendelea kuajiri Madaktari na Wauguzi kulingana na bajeti ambapo kwa sasa kituo hicho kina madaktari 14 kutoka wawili wa awali tangu kilipoanzishwa mwaka 1968.

Awali Mganga Mfawidhi wa kituo hicho,Dk.Ernest Celestine alisema kuwa kituo hicho kinakabiliwa na ukosefu wa majengo ya wodi wagonjwa wanawake na wanaume wanaofanyiwa upasuaji,magodoro na vitanda,ongezeko la wagonjwa wa huduma za upasuaji,wagonjwa wa nje na wa kulazwa, wagonjwa wa Kifua Kikuu(TB) na Virusi vya Ukimwi (VVU) .


Alisema wanakabiliwa pia na ukosefu wa wodi ya kulala watoto,mashine ya Utra Sound,makazi duni ya watumishi,huduma endelevu za maabara,jengo na jokofu la kuhifadhi maiti,jengo la kuchoma taka hatarishi,jengo la utawala na jiko.

KITWANGA APOKELEWA KWA SHANGWE USAGARA, AMALIZA ZIARA YAKE MISUNGWI, WAMSHUKURU RAIS MAGUFULI KWA KUMTEUA KUWA WAZIRI

$
0
0
 Wananchi wa Kata ya Usagara, wilayani Misungwi wakimshangilia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga wakati alipokuwa akizungumza na wananchi hao katika Viwanja vya Gulio mjini Usagara. Wananchi hao walimwambia Waziri Kitwanga wanaikumbuka ahadi ya Rais John Magufuli wakati akiwa anamnadi Mbunge huyo kipindi cha kampeni, kuwa suala la maji atalishughulikia Rais mwenyewe. Hivyo wanamuomba Mbunge wao ashirikiane na Rais huyo ili maji yaweze kupatikana kwa haraka zaidi. 
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akizungumza na wananchi wa Kata ya Usagara kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo ya jimbo lake. Kitwanga aliwataka wananchi hao washirikiane katika kuchangia miradi ya maendeleo ili jimbo hilo liweze kupata mafanikio zaidi. Hata hivyo, wananchi hao walimuambia Waziri Kitwanga wanaikumbuka ahadi ya Rais John Magufuli wakati akiwa anamnadi Mbunge huyo kipindi cha kampeni, alisema suala la maji atalishughulikia Rais mwenyewe, hivyo wanamuomba Mbunge wao ashirikiane na Rais huyo ili maji yaweze kupatikana kwa haraka zaidi. Hata hivyo maandalizi ya upatikanaji maji zimeanza jimboni humo.
Msimamizi wa Mradi wa Maji Mwanza, Abbas Muslim akijibu maswali ya wananchi baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi, Charles Kitwanga (kulia) kumtaka ajibu maswali ya wananchi hao kuhusu lini maji yatapatikana jimboni humo pamoja na hatua walizozifikia mpaka sasa. Hata hivyo, Msimamizi huyo alitoa ufafanuazi kuhusu mradi huo na kuwafafanulia wananchi hao kuwa, mradi huo mkubwa wa maji unaojumuisha Misungwi, Magu, Lamadi, Musoma, Bukoba na Jiji la Mwanza unatarajiwa kumalizika mwaka 2018 lakini pia unaweza ukamalizika kabla ya muda huo uliopangwa na wananchi kuweza kupata maji. Picha zote na Felix Mwagara.

WAZO LA WAZIRI WA ARDHI WILLIAM LUKUVI KUHUSIANA NA UWANJA ULIOMTOA MBWANA SAMATA KUFANYIWA KAZI

$
0
0
Mkuu wa Mauzo wa Kanda ya Pwani wa Vodacom Tanzania Herieth Koka akimpongeza Mbwana Samata kwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka la kulipwa Afrika, Wakati wa hafla ya kumpongeza iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania na wadau wengine wa Soka na kufanyika katika hoteli ya Hyatty jijini Dar es Salaam

Waziri wa Habari ,Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Mnauye akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mauzo wa Kanda ya Pwani wa Vodacom Tanzania Herieth Koka, wakati walipokutana katika hafla ya kumpongeza Mbwana Samata aliyetwaa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ligi za Afrika. Kushoto ni Mchezaji bora wa Afrika 2015 Mbwana Samata.

Waziri wa Nyumba na Makazi William Lukuvi akisalimiana na Mkuu wa Mauzo Kanda ya Pwani wa Vodacom Tanzania Herieth Koka wakati wa hafla ya kumpongeza Mbwana Samata kwa kutwa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka la kulipwa afrika iliyofanyika katika hoteli ya Hyatty jijini Dar es Salaam.

KAMPUNI ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania ambayo ni mdhamini wa ligi kuu ya soka Tanzania bara imesema kuwa bado inaufanyia kazi ushauri wa serikali wa kuwa mmoja wa wafadhili wa ujenzi wa uwanja wa mpira wa Mbagala katika kumuenzi mwanasoka wa Tanzania Mbwana Samatta ambaye hivi karibuni alitunukiwa tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika.

Wakati wa hafla ya wadau wa soka ya kumpongeza mwanasoka huyo juzi iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt jijini Dar es Salaam,mgeni wa heshima kwenye hafla hiyo Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi,William Lukuvi aliwataka wadau wa kuendeleza soka nchini ikiwemo kampuni ya Vodacom inayofadhili ligi kuu kumuenzi Samatta kwa vitendo kutokana na heshima aliyoiletea Tanzania ikiwemo kujenga uwanja aliokuwa anachezea kabla ya kiwango chake kuwa kikubwa na kusajiliwa na vilabu vinavyoshiriki ligi ya daraja la kwanza.

Mkuu wa Mauzo wa Kanda ya Pwani wa Vodacom Tanzania,Herieth Koka amesema kuwa ushauri huo wa serikali ni mzuri katika kumuenzi mwanasoka Samatta na kampuni ya Vodacom itaufanyia kazi.

“Vodacom ikiwa ni mdhamini mkuu wa ligi ya soka nchini tumefurahishwa na mafanikio ya Samatta kwa kuwa moja ya dhamira ya kampuni yetu ni kusaidia michezo hususani mchezo wa soka wa kuwa tunaamini kuwa bado kuna fursa ya vijana wengi wa Tanzania maisha yao kuwa murua kupitia michezo”.

Alisema pia kuwa kampuni itaendelea kushirikiana na serikali na wadau wengine wa soka nchini kuhakikisha ligi kuu ya Vodacom inazidi kuwa bora ili wapatikane wachezaji wengine wa kuitangaza Tanzania katika ramani ya soka duniani kama alivyofanya Mbwana Samatta.

ZOEZI LA KUWASAKA WAHAMIAJI HARAMU LAPAMBA MOTO MKOANI MBEYA

$
0
0
Afisa Uhamiaji  Mkoa wa Mbeya Asumsyo Achacha akizungumza ofisni kwekwe juu ya zoezi linaloendelea la kuwasaka wahamiaji haramu mkoani humo.
Na jamiimojablogu, Mbeya

ZOEZI la kuwasaka wahamiaji haramu na wageni wanaofanya kazi bila kibali limeendelea kufanikiwa mkoani Mbeya ambapo jumla ya wageni 20 wamekamatwa mkoani humo kutokana na makosa mbalimbali likiwemo la kuingia nchini kinyume cha sheria.



Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwakwe Afisa uhamiaji Mkoa wa mbeya Ndugu Asumsyo Achacha amesema hatua hiyo imefanyika ikiwa ni kutekeleza majukumu yao ya kila siku sanjali na kutekeleza agizo la Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt Charles Kitwanga alilotoa hivi karibuni.



Aidha amesema hatua hiyo ni utekelezaji wa sheria mpya  ya kuratibu ajira za wageni ,Sherii Na.1 ya mwaka 2015 ambayo inawataka wageni wote walioajiliwa hapa nchini kuwa na vibali vya kazi na hati za ukaazi nchini.

Afisa uhamiaji huyo amewataja raia hao waliokamatwa katika msako huo ni pamoja wakenya watatu (3)wamalawi 14 pamoja na wakongo watatu (3).



Aidha amesema kuwa mwaka 2015 jumla ya wahamiaji haramu 478 kutoka mataifa mbalimbali walikamatwa na kuchukuliwa hatua mbalimbali  ikiwemo kufikishwa mahakamani pamoja na kufukuzwa nchini.



Amesema mbali na changamoto zilizojitokeza ikiwemo upungufu wa vitendea kazi ,fedha pamoja na rasilimali  bado shughuli za uhamiaji mkoani humo ziliendelea kufanyika kama kawaida na kwa ufanisi mkubwa.



Pia Afisa Uhamiaji huyo amebainisha kuwa zoezi hilo ni endelevu hivyo ofisi yake itahakikisha kila mtu aliyevunja sheria anakamatwa hivyo ametoa wito kwa waajiri kuacha tabia ya kuwapa ajira wafanyakazi wa kigeni wasio na vibali vya kazi na ukaazi kwani msako huo utaendelea katika viwanda ,migodi mashuleni na hotelini.

BEI YA MADAFU LEO

MKE WA MAKAMU WA RAIS MSTAAFU, MAMA ASHA BILAL AHITIMU STASHAHADA YA UZAMILI KATIKA MENEJIMENTI YA KIMATAIFA

$
0
0
  Mke wa Makamu wa Rais mstaafu Mama Asha Bilal, (katikati) akiwa na wahitimu wenzake walipokuwa wakitunukiwa Stashahada ya Uzamili katika Menejimenti ya Kimataifa wakati wa Mahafali yao yaliyofanyika Chuo cha Diplomasia Kurasini jijini Dar es Salaam, jana Januari 13, 2016. Picha na Mafoto Media/Muhidin Sufiani
 Mke wa Makamu wa Rais mstaafu Mama Asha Bilal, (katikati) akiwa na wahitimu wenzake Janeth Nyoni (kushoto) na Hadija Hashim, baada ya kutunukiwa Stashahada ya Uzamili katika Menejimenti ya Kimataifa wakati wa Mahafali yao yaliyofanyika Chuo cha Diplomasia Kurasini jijini Dar es Salaam, jana.
 Mke wa Makamu wa Rais mstaafu Mama Asha Bilal, (wa pili kulia) akiwa na baadhi ya wageni waalikwa wakati wa sherehe ya maafali yake yaliyofanyika  Chuo cha Diplomasia Kurasini jijini Dar es Salaam, jana Januari 13, 2016. Mama Asha na wenzake walitunukiwa Stashahada ya Uzamili katika Menejimenti ya Kimataifa.
 Mke wa Makamu wa Rais mstaafu Mama Asha Bilal, (wa kwanza kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni waalikwa baada ya kutunukiwa Stashahada ya Uzamili katika Menejimenti ya Kimataifa wakati wa Mahafali yao yaliyofanyika Chuo cha Diplomasia Kurasini jijini Dar es Salaam, jana
 Mke wa Makamu wa Rais mstaafu Mama Asha Bilal, (kushoto) akiwa na Meneja Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele, baada ya kutunukiwa Stashahada ya Uzamili katika Menejimenti ya Kimataifa wakati wa Mahafali yao yaliyofanyika Chuo cha Diplomasia Kurasini jijini Dar es Salaam, jana Januari 13, 2016. Kulia ni mke wa Balozi wa Tanzania nchini Geneva, Rose Mero.
 Mke wa Makamu wa Rais mstaafu Mama Asha Bilal, (katikati) akiwa na baadhi ya wahitimu wenzake wa Chuo cha Diplomasia Kurasini jijini Dar es Salaam, jana Januari 13, 2016, baada ya kutunukiwa Stashahada ya Uzamili katika Menejimenti ya Kimataifa kwenye Mahafali yaliyofanyika Chuoni hapo.
 Baadhi ya Wahitimu wa Chuo hicho wakiwa katika mahafali hayo wakisubiri kutunukiwa Stashahada ya Uzamili katika Menejimenti ya Kimataifa, jana
 Baadhi ya Wahitimu wa Chuo hicho wakiwa katika mahafali hayo wakisubiri kutunukiwa Stashahada ya Uzamili katika Menejimenti ya Kimataifa, jana
 Baadhi ya Wahitimu wa Chuo hicho wakiwa katika mahafali hayo wakisubiri kutunukiwa Stashahada ya Uzamili katika Menejimenti ya Kimataifa, jana
 Baadhi ya Wahitimu wa Chuo hicho wakiwa katika mahafali hayo wakisubiri kutunukiwa Stashahada ya Uzamili katika Menejimenti ya Kimataifa, jana
Meneja Mfuko wa Pensheni wa PSF, Lulu Mengele (kulia) akipozi kwa picha na mke wa Balozi wa Tanzania Nchini Geneva, Rose Mero, baada ya kutunukiwa Stashahada yake.

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA NISHATI NA MADINI ATEMBELEA KITUO CHA JEMOLOJIA ARUSHA.

$
0
0
NAIBU Katibu Mkuu anayeshughulikia Madini katika Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe ametembelea kituo cha Jemolojia jijini Arusha ambacho hutoa mafunzo ya Jemolojia yanayojumuisha ukataji na uchongaji wa madini ya vito na kuyaweka katika maumbile ya kuvutia.

Naibu Katibu Mkuu alitembelea kituo hicho na Ofisi za Madini jijini Arusha ili kuona shughuli mbalimbali zinazofanyika pamoja na kuzungumza na watumishi.
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Madini katika Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe (wa Tatu kushoto) akiangalia mashine ya ukataji madini iliyopo katika kituo cha Jemolojia jijini Arusha.Aliyevaa shati jeupe ni Mratibu wa Kituo hicho, Mussa Shanyangi, wa kwanza kushoto ni Afisa Madini Mkazi Ofisi ya Madini ya Merelani, Mhandisi Henry Mditi na wa pili kushoto ni Kaimu Kamishna wa Madini nchini, Mhandisi Ally Samaje.
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Madini katika Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe (wa kwanza kulia) akiangalia mwamba uliochongwa, kunakshiwa na kuwa katika umbo la mjusi wakati alipotembelea Kituo cha Jemolojia jijini Arusha ambacho hutoa mafunzo yanayojumuisha ukataji na uchongaji wa madini ya vito na kuyaweka katika maumbile ya kuvutia. Wengine katika picha ni Afisa Madini Mkazi Ofisi ya Madini ya Merelani Mhandisi Henry Mditi, (wa kwanza kushoto), Kaimu Kamishna wa Madini nchini, Mhandisi Ally Samaje (wa pili kushoto) na wa pili kulia ni Kamishna Msaidizi wa Madini- Uchumi na Biashara, Salim Salim.

Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Madini katika Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe (kulia) akionyeshwa moja ya mashine zinazotumika katika Kituo cha Jemolojia jijini Arusha katika ukataji na uchongaji wa madini ya vito na kuyaweka katika maumbile ya kuvutia. Anayemwonyesha mashine hiyo ni Mratibu wa Kituo hicho, Mussa Shanyangi.

MRADI WA KUWAWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI WA MANJANO DREAM MAKERS WATUA MWANZA

$
0
0



Mradi wa Kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia Tasinia ya Urembo ujulikanao kama Manjano Dream Makers hatimaye umefika Mwanza.Wataalamu wa Maswala ya biashara na Urembo Wataendesha Mafunzo Wiki ijayo Traehe 18.01.2016 Kwenye Ukumbi wa Rock city Mall Jijini Mwanza,Wanawake 35 wa jiji la Mwanza Watanufaika na mafunzo ya ujasiriamali kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano.

Wanawake Wakazi wa jiji la Mwanza Mwanza Wanaopenda Kunufaika na Mradi huo Wanaombwa Kujitokeza Kwa wingi Kujiandikisha siku ya Kesho Tarehe 15.01.2016 kuanzia saa Mbili Asb kwenye Ukumbi wa Rock City Mall .

Mafunzo yana Lengo la kumsaidia mjasiriamali mwanamke kujikwamua.

Awamu ya kwanza ni kumfundisha maswala ya Biashara namna ya kuibua na kubuni miradi mbalimbali namna ya kuandika Mpangilio wa Biashara ikiwemo Matumizi sahihi ya Rasilimali Muda, Fedha, Muda na pia namna ya kujitunzia akiba itokanayo na Biashara yake.Baada ya Wanawake hawa kuhitimu Mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation inatoa Mikopo kwajili ya kuwawezesha Kuanzisha Biashara wakiwa chini ya Uangalizi Maalum wa taasisi hiyo kwa Lengo la Kuhakikisha kila Mhitimu wa Mafunzo haya anapiga hatua na kuweza Kujitegemea .

MKE WA MAKAMU WA RAIS MSTAAFU MAMA ASHA BILAL AHITIMU STASHAHADA YA UZAMILI KATIKA MENEJIMENTI YA KIMATAIFA

$
0
0
 Mke wa Makamu wa Rais mstaafu Mama Asha Bilal, (katikati) akiwa na wahitimu wenzake walipokuwa wakitunukiwa Stashahada ya Uzamili katika Menejimenti ya Kimataifa wakati wa Mahafali yao yaliyofanyika Chuo cha Diplomasia Kurasini jijini Dar es Salaam, jana Januari 13, 2016. 

Mke wa Makamu wa Rais mstaafu Mama Asha Bilal, (wa tano kutoka kulia) akiwa na wahitimu wenzake walipokuwa wakitunukiwa Stashahada ya Uzamili katika Menejimenti ya Kimataifa wakati wa Mahafali yao yaliyofanyika Chuo cha Diplomasia Kurasini jijini Dar es Salaam, jana Januari 13, 2016. 
 Mke wa Makamu wa Rais mstaafu Mama Asha Bilal, (katikati) akiwa na wahitimu wenzake Janeth Nyoni (kushoto) na Hadija Hashim, baada ya kutunukiwa Stashahada ya Uzamili katika Menejimenti ya Kimataifa wakati wa Mahafali yao yaliyofanyika Chuo cha Diplomasia Kurasini jijini Dar es Salaam, jana Januari 13, 2016.
Mke wa Makamu wa Rais mstaafu Mama Asha Bilal, (wa pili kulia) akiwa na baadhi ya wageni waalikwa wakati wa sherehe ya maafali yake yaliyofanyika Chuo cha Diplomasia Kurasini jijini Dar es Salaam, jana Januari 13, 2016. Mama Asha na wenzake walitunukiwa Stashahada ya Uzamili katika Menejimenti ya Kimataifa. 
 Mke wa Makamu wa Rais mstaafu Mama Asha Bilal, (wa kwanza kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni waalikwa baada ya kutunukiwa Stashahada ya Uzamili katika Menejimenti ya Kimataifa wakati wa Mahafali yao yaliyofanyika Chuo cha Diplomasia Kurasini jijini Dar es Salaam, jana Januari 13, 2016. 
 Mke wa Makamu wa Rais mstaafu Mama Asha Bilal, (kushoto) akiwa na Meneja Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Lulu Mengele, baada ya kutunukiwa Stashahada ya Uzamili katika Menejimenti ya Kimataifa wakati wa Mahafali yao yaliyofanyika Chuo cha Diplomasia Kurasini jijini Dar es Salaam, jana Januari 13, 2016. Kulia ni mke wa Balozi wa Tanzania nchini Geneva, Rose Mero.
 Mke wa Makamu wa Rais mstaafu Mama Asha Bilal, (katikati) akiwa na baadhi ya wahitimu wenzake wa Chuo cha Diplomasia Kurasini jijini Dar es Salaam, jana Januari 13, 2016, baada ya kutunukiwa Stashahada ya Uzamili katika Menejimenti ya Kimataifa kwenye Mahafali yaliyofanyika Chuoni hapo.




Baadhi ya Wahitimu wa Chuo hicho wakiwa katika mahafali hayo wakisubiri kutunukiwa Stashahada ya Uzamili katika Menejimenti ya Kimataifa, jana Januari 13, 2016. 
Picha na Mafoto Media/Muhidin Sufiani

Waziri Mahiga akutana kwa mazungumzo na Rais wa Mahakama ya Afrika.

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (kulia), akimsikiliza Rais wa Mahakama ya Afrika Jaji Mstaafu, Mhe. Augustino Ramadhani alipofika kumtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kumpongeza kwa kuteuliwa kuwa Waziri. Pia kuzungumzia masuala mbalimbali yanayoihusu Mahakama hiyo likiwemo suala la ujenzi wa Mahakama hiyo katika Jiji la Arusha. 
Afisa Mambo ya Nje, Bw. Elisha Suku naye akielezea jambo katika mazungumzo kati ya Waziri Dkt. Mahiga na Mhe. Ramadhani (hawapo pichani), wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Baraka Luvanda, na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali Wizarani, Bi. Mindi Kasiga. 
Mazungumzo yakiendelea.

Picha na Reginald Philip.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje akutana na Balozi wa Syria.

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dkt. Susan Kolimba akizungumza na Balozi wa Syria hapa nchini Mhe.Abdulmonem Annan, baada ya Balozi huyo kumtembelea Naibu Waziri kwa ajili ya kumpongeza na kuzungumzia namna ya kuimarisha mahusiano ya nchi hizi mbili.
Balozi wa Syria hapa nchini Mhe.Abdulmonem Annan, akizungumza jambo na Mhe. Naibu Waziri wakati wa mazungumzo hayo.
Msaidizi wa Naibu Waziri, Bw. Adam Isara (kulia), akifuatilia kwa makini mazungumzo hayo.

Picha na Reuben Mchome.

WIZARA YA NISHATI YATOA UFAFANUZI MRADI WA UMEME WA KINYEREZI II

$
0
0
Na Nyakongo Manyama- MAELEZO.
Wizara ya Nishati na Madini imekanusha habari iliyopotosha umma kuhusu mradi wa umeme wa Kinyerezi II kuwa bado haujaanza na gharama zilizoandikwa si za kweli.

Wizara hiyo imekanusha habari hiyo, iliyoandikwa katika gazeti la Mtanzania la leo Januari 14, mwaka huu toleo namba 8063, lenye kichwa cha habari “ Harufu ya Jibu Mradi wa Umeme.”

Habari hiyo ambayo ilieleza kwamba mradi huo ulizinduliwa na Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Mhe. Dkt.Jakaya Kikwete uligharimu Sh. trilioni 1.6 na kwamba fedha za ujenzi wa mradi huo zimetokana ubia kati ya Serikali ya Tanzania na Japan,ambapo Serikali ya Tanzania itakuwa na hisa ya asilimia 40 na kampuni ya SUMITOMO ya Japan asilimia 60. 

Aidha habari hiyo ilidai kuwa Serikali inachangia fedha za ndani kwa asilimia 12 na zilizobaki zikiwa na mkopo kutoka benki ya Japan na kwamba gharama za mradi huo ziko juu ikilinganishwa miradi mingine akitolea mfano Kampuni ya TALLAWARA Power Station ya nchini Australia anayodai ilitaka kujenga mradi huo kwa dola za Marekani milioni 350.
Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mawasiliano Serikali wa wizara hiyo, Badra Masoud alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu habari hiyo katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es Salaam. 

“Serikali ya Tanzania iliingia makubaliano na Serikali ya Japan ya mkopo wa masharti nafuu wa dola za Marekani milioni 292 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa kuzalisha umeme wa Megawati 240 utakaojengwa na kampuni ya SUMITOMO kama mkandarasi wa “EPC contractor” na sio kama mbia wa Serikali yaTanzania kama ilivyodaiwa.


“Mradi huo unamilikiwa na Serikali kwa asilimia 100 kupitia TANESCO na hakuna mwekezaji mwingine katika mradi huo.

Hivyo si kweli kwamba Serikali ya Tanzania na kampuni ya SUMITOMO zinawekeza kwa ubia wa asilimia 40 (kwa Serikali ya Tanzania) na asilimia 60 kwa SUMITOMO. Kwa maana hiyo hatutauziwa umeme utakaozalishwa na mradi huu kwani ni mali yetu na hakuna gharama yoyote ya ziada kama alivyodai mwandishi wa habari hiyo,” alisema Badra.

Aidha Badra alisema mwandishi huyo alidai kwamba mradi huo ulizinduliwa na Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete, wakati ni kwamba mradi huo haujazinduliwa bado na sasa upo katika maandalizi ya kuwekwa katika jiwe la msingi.

Akizungumzia kuhusu gharama za mradi huo, alieleza kuwa unatekelezwa kwa dola za Marekani milioni 344 sawa na Sh. bilioni 740 zikiwa ni mkopo wa masharti nafuu wa asilimia 85 sawa na dola za Marekani 292 na mchango wa Serikali ya Tanzania kwa asilimia 15 sawa na dola za Marekani milioni 52.( na sio asilimia 12 kama ilivyodaiwa na mwandishi huyo). 

“Mwandishi wa habari hii amejaribu kufananisha uwekezaji huu na uwekezaji wa TALLAWARA Power Station ya Australia na kudai kwamba gharama yake ingekuwa ndogo kuliko gharama ya mradi huu. Taarifa hii haina ukweli wowote kwa sababu gharama ya dola milioni 344 zinazotarajiwa kutumika mkatika mradi huu iko chini kuliko dola milioni 350anazodai mwandishi kwamba zingetumiwa na kampuni TALLAWARA.

“Aidha, kampuni ya TALLAWARA haijawahi kuomba au kuonesha nia ya kuwekeza katika mradi wowote wa kufua mradi wa umeme nchini. Pia ni muhimu ifahamike kwamba makubaliano ya mkopo huu yalikuwa yanakwenda sambasamba na utekelezaji wa mradi wenyewe (EPC with Financing). 

Badra aliongeza kwamba pamoja na kwamba gharama za uwekezaji wa mradi huo wa kwanza wa aina ya “Combined Cycle” nchini zinawiana na gharama za miradi mingine ya aina hiyo duniani, gharama za uwekezaji zinaweza kutofautiana kutegemeana na mazingira ya nchi na nchi, teknolojia iliyotumika na aina ya mitambo.

Hivyo sio suala la kulinganisha gharama ya mradi mmoja na mwingine .
Wizara hiyo imeshauri waandishi wa habari kufuata miiko na maadili ya uandishi wa habari kwa kuandika habari zenye ukweli na sahihi na zilizozingatia pande zote mbili kwa kuwa ipo na tayari kujibu maswali ya waandishi wakati wowote.

KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI.

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (hawapo pichani), katika ukumbi wa Chuo cha Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
 Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,Rogatius Kipali, akitoa shukrani kwa mgeni rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (hayupo pichani), baada ya kufungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Jeshi hilo uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wa tatu kutoka kulia), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi pamoja na washiriki wa mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, ulifanyika katika ukumbi wa Chuo cha Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam. Wa tatu kutoka kushoto ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,Injinia Pius Nyambacha na wa poli kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Utalawa na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Lilian Mapfa. 
(Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

WAZIRI MKUU MAJALIWA: TUJIKITE KUIMARISHA MIUNDOMBINU YETU ILI TUKUZE UCHUMI

$
0
0
BIA3 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua mkutano wa miradi ya ubia katika ujenzi  wa Miundombinu kati ya Japan na Tanzania kwenye hoteli ya Hyatt Regency- Kilimanjaro jijini Dar es salaam Januari 14,2016.
………………………………
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka watanzania  kujikita katika kuimarisha miundombinu  ili kukuza uchumi, kuimarika kwa miundombinu ya usafirishaji ni muhimu kwa shughuli mbalimbali mfano kilimo na biashara.

Akizungumza  na  wadau wakati akifungua  mkutano wa Miradi ya Ubia katika Ujenzi wa Miundombinu kati ya  Tanzania na Japan(TANZANIA -JAPAN PUBLIC -PRIVATE QUALITY INFRASTRURE CONFERENCE) uliofanyika leo,  katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam, amesema  sekta   binafsi  inasaidia katika ujenzi wa miundombinu  na sekta ya usafirishaji kwa ujumla, ambapo ni muhimu kwa vile inasaidia kuboresha maisha ya watu.

“Serikali kupitia Kituo cha uwekezaji nchini (TIC) imeandaa mazingira mazuri ya biashara inayosaidia wawekezaji kuja kuwekeza nchi, matumaini yetu ni kwamba kutokana na mkutano huu   wawekezaji wa ndani  mtapata  fursa ya kujifunza na kujiunga katika   kampuni ambazo zitawasaidia  kushirikiana na kampuni za kijapani  na kuweza kupata ujuzi,  utaalamu wa kiutawala na uwezo wa kuwa wabunifu zaidi hasa katika masuala ya miundombinu.”  amesema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu Majaliwa ameendelea kwa kusema mkutano huu utaimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Japani, na kutoa fursa ya kubadilishana ujuzi kwa wakandarasi, washauri, kampuni za biashara na uhandisi kutoka Japani na Tanzania, vilevile utawawezesha kujenga mtandao kwa kushirikiana na makampuni ya nchi hizi mbili.

Kwa upande wa  miundombinu na usafirishaji,  Tanzania ina ukubwa wa barabara zinazofikia kilomita 87,581, kutokana na sera na jitihada mbalimbali  kwa  kipindi cha miaka 10 (2005-2015) jumla ya kilomita 17,762  zimefikia hatua mbalimbali za ujenzi.

Waziri Mkuu ameendelea kwa kusema, Tanzania ina mifumo miwili ya reli, reli ya kati yenye kilomita 2,706 na reli ya ‘Tanzania Zambia Railway Authority’ (TAZARA) yenye kilomita 975. Pia, ina Bandari kuu za Dar es salaam, Tanga na  Mtwara .

Kwa upande wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), kupitia  Mkongo wa Mawasiliano wa Taifa (National ICT Broadband Backbone -NICTBB)  kwa kutumia mfumo wa baharini (SEACOM, July 2009) na (EASSY April,2010)  tayari nchi jirani za Rwanda, Zambia na Kenya zimeunganishwa na mkongo huo.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Edwin Ngonyani, amesema miundombinu ni kichocheo kikubwa cha maendeleo ya nchi yeyote ile duniani. Tanzania na Japani zimeshirikiana katika ujenzi na uboreshaji wa miundombinu mbalimbali, mfano barabara za Dodoma –Iringa, Namtumbo –Tunduru, Dodoma – Babati  inayoendelea  kujengwa, upanuzi wa barabara ya Gerezani  pamoja na   ‘fly over’ ya TAZARA. 

Naye, Waziri wa Ardhi, Miundombinu, Uchukuzi na Utalii wa Japani Takatoshi Nishiwake amesema, Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda alipotembelelea Japani alisema angependa kuona Japani na Tanzania zinashirikiana katika masuala ya ujenzi wa miundombinu.

 Ameendelea kwa kusema kuwa, Serikali ya Japani inapenda kubadilishana ujuzi na Tanzania katika masuala ya miundombinu, pia ni matumaini yake kuwa washiriki kutoka pande zote mbili wanapata fursa ya kubadilishana ujuzi na kujifunza zaidi. Vile vile kupitia mkutano huu mahusiano ya nchi hizi mbili yataimarika zaidi.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
  1. L. P 3021,
11410 DAR ES SALAAM
ALHAMISI, JANUARI 14, 2016.

Waziri Muhongo :Ahadi ya Jan 15 Iko pale pale

$
0
0
Asteria Muhozya  na Rhoda James, Mbeya

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesisitiza kauli yake kwamba tarehe iliyopangwa kati yake na Mameneja wa Tanesco nchi nzima ya kuhakikisha inawaunganishinia umeme wateja waliolipa kwa kipindi kirefu ikiwemo kukamilisha  matatizo ya  LUKU bado iko palepale.

imagesProfesa Muhongo ameyasema hayo  leo wakati wa kikao na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro na kuongeza kuwa  tarehe 15 Januari,2016, ndio tarehe ya mwisho ya kukamilisha shughuli hizo nchi nzima.

“Katika hili nasema kweli hakuna mzaha. Hatutanii. Wananchi wamechoka, wanataka umeme. Mtindo wa kuandikiana barua tena haupo. Ukishindwa , unajiondoa mwenyewe”,amesisitiza Prof. Muhongo.

Akijibu hoja za Kandoro kuhusu suala la Makaa ya mawe, amesema atahakikisha suala hilo linapata ufumbuzi wa haraka kuhakikisha rasilimali hiyo inatumika kama chanzo kingine cha kuzalisha umeme nchini.

“Mkuu wa Mkoa hili lazima tulishughulikie. Hatuwezi kuacha makaa ya mawe yakae tu kama mapambo wakati tunahitaji sana nishati ya umeme kwa ajili ya kuondoa matatizo ya umeme tuliyonayo”.
Prof. Muhongo ameongeza kuwa, tayari amewaagiza wawekezaji wote wa makaa ya mawe wenye leseni kukutana  nae katika ziara  ili kukubaliana kuhusu suala hilo.” Tayari nimewaambia wote tukutane huku huku site wanieleze wanafanya nini”, ameongeza.


Akieleza kuhusu suala la matatizo ya maji katika vyanzo vya uzalishaji umeme, Prof. Muhongo ameiagiza Tanesco Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, kuhakikisha wanaandaa  kikao cha wakuu wa mikoa ya Njombe, Iringa, Morogoro na Mbeya ili kufanya tathmini ya utumiaji maji bila kuathiri pande zote ikiwemo kutumika kwa ajili ya umeme na kilimo.

“Najua maji yanahitajika sana katika kilimo hususan kilimo cha umwagiliaji ambacho ndio cha kisasa. Lakini hata nishati inahitaji maji. Nawaomba kutaneni zungumzeni halaf tembeleeni maeneo ya mabonde na mashamba mpate data zote,  mkimaliza tuangalie suala la kisera linasemaje .  Suala hili ni muhimu sana kwa ustawi na maendeleo ya uzalishaji nishati na kilimo. Lakini pia tunahitaji kuwa na tamko la pamoja,” amesema Prof. Muhongo.
Aidha, Prof Muhongo ameagiza kuwa katika kikao hicho kiwakutanishe pia na Wakuu wa mabonde ili suala hilo liweze kujadiliwa na pande zote.

“Mkuu wa Mkoa nashauri na wakuu wa mabonde wawepo. Lakini pia wanatakiwa kuangalia suala la utoaji vibali kwa sababu kuna umwagiliaji mwingine sio mzuri”. Wazalishaji wadogo wanalia sana na suala la uharibifu wa vyanzo vya maji. Nimepita maeneo mengi wengi wanalia na wana hofu na maji. Wale wanatusaidia sana kuongeza kiwango cha uzalishaji umeme. Kwetu sisi  wazalishaji wadogo ni muhimu sana”, amesema Waziri Muhongo.

Awali Mkuu wa Mkoa alimweleza Prof. Muhongo kuhusu suala la Makaa ya mawe ya Kiwira na kumweleza umuhimu wa kuendeleza miradi hiyo kwa maendeleo ya nchi na katika kusaidia taifa kuwa na kiasi cha umeme wa kutosha.

” Prof. nashauri sana  wizara yako ifufue  mgodi wa Kiwira kutokana na umuhimu wake kwa taifa.” Awali mgodi huu ulikuwa  unasaidia kuingiza umeme kwenye gridi hii ni muhimu. Mkoa wetu umebarikiwa kuwa na madini na ni wa tatu katika kuchangia pato la Taifa. Tukiongeza na Kiwira taifa litanufaika zaidi,” ameongeza Kandoro.

Akiwa mkoani Mbeya Prof. Muhongo atatembelea mgodi wa Makaa ya Mawe Kiwira, Wachimbaji wadogo wa madini Chunya, maeneo yenye viashiria vya nishati ya jotoardhi Mbaka, Bonde la mto Songwe kwenye mradi wa kuzalisha umeme na maeneo mengine.
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images