Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 736 | 737 | (Page 738) | 739 | 740 | .... | 1897 | newer

  0 0

  MSINUNE Taasisi ya Flaviana Matata ilizindua rasmi msimu wa "BACK TO SCHOOL" kwa kutoa vifaa vya shule kwa jumla ya watoto 270 wa Shule ya Msingi Msinune ambayo ipo chini ya ulezi wa mwanzilishi wa #FMF na mwanamitindo wa Kimataifa Flaviana Matata. Zaidi ya kutoa vifaa vya Shule Flaviana Matata Foundation kwa kushirikiana na wadau wamefanikiwa kujenga choo na waalimu na wanafunzi shuleni hapo. fmf msinune Flaviana Matata akikabidhi mabegi ya shule kwa watoto wa shule ya Msingi ya Msinune ambapo ameteuliwa kama mlezi wa shule hiyo kwa mwaka wa tatu sasa. fmf msinune primary school wanafunzi wa Shule ya Msinune wakikatiza na mabegi yao ambayo walikabidhiwa mwaka jana.     FmF  fmf msinune 1 
  Flaviana Matata akikagua Choo cha wanafunzi kilichojengwa na FMF kwa msaada wa wadau. fmf msaada choo

  0 0

  ????????????????????????????????????
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akizungumza na baadhi ya watendaji wa Mgodi wa Makaa ya Mawe ya Ngaka mara baada ya kuwasili katika mgodi huo wakati wa ziara yake ya kikazi mkoa wa Ruvuma. Wengine ni ujumbe aliofuatana nao   pamoja na Mbunge wa Mbinga vijijini, Martin Msuha, Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Senyi Ngaga, Kamishna Msaidizi wa Madini, anayeshughulikia Leseni John Nayopa, Watendaji toka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC), Ofisi ya Madini Kanda ya Ziwa Nyasa, baadhi ya Maafisa toka Wizara ya Nishati na Madini na EWURA.
  ????????????????????????????????????
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospter Muhongo, (kulia) akiwasikiliza wawakilishi wa wananchi wa Kijiji cha Mtundualo, Wilaya ya Mbinga ambao walimwomba waziri asikilize malalamiko yao  ikiwemo kuhusu suala la fidia kupisha mradi wa Makaa ya Mawe wa Ngaka na ombi la kijiji hicho kupatiwa umeme.  Kwa mujibu wa Meneja wa Tanesco Kanda ya Kusini, Joyce Ngahyoma, amewahakikishia kuwa ifikapo  mwezi Aprili mwaka huu kijiji hicho kitakuwa kimeunganishwa na nishati ya umeme.
  ????????????????????????????????????
  Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Senyi Ngaga, akijadiliana jambo na baadhi ya Watendaji wa Mgodi wa Ngaka kampuni ya TANCOAL, mara baada ya waziri kukagua shughuli za mgodi huo na kusikia malalamiko ya wananchi kuhusu fidia. Waziri Muhongo amezitaka pande mbili kati ya Kampuni, Halmashauri na wananchi kukutana ili kujadili na kukubaliana kuhusu masuala kadhaa yakiwemo fidia na uhifadhi wa mazingira.
  ????????????????????????????????????
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akimsikiliza Mwendeshaji Mitambo wa kituo cha kufua umeme cha Tulila kinachomilikiwa na Shirika la Wabenedictin wa Mtakatifu Agnes Chipole, Sister Maria Katani (OSB),. Wengine wanaofuatilia nia Meneja wa Tanesco Kanda ya Kusini, Joyce Ngahyoma na Afisa toka Wizara ya Nishati na Madini, Christopher Bitesirigwa.
  ????????????????????????????????????
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akisalimiana na Mfadhili wa Kituo cha Kufua umeme kinachomilikiwa na Watawa wa Shirika la Shirika la Wabenedictin wa Mtakatifu Agnes Chipole, Albert Cock (kushoto). Kituo hicho chenye uwezo wa kuzalisha kilowati 800 kipo Kata ya Magarura, wilaya ya Mbinga mkoa wa Ruvuma. Aidha, sehemu ya umeme unaozalishwa na kituo hicho unasambazwa Songea, JKT Mlale na Chuo cha Maendeleo ya Jamii Mlale. Vilevile, Kituo hicho kipo katika hatua za ujenzi wa kituo kitakachokuwa na uwezo wa kuzalisha megwati 7.5.
  Meneja wa Tanesco Kanda ya Kusini, Joyce Ngahyoma akimweleza jambo Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo wakati alipotembelea kituo cha mwekezaji binafsi cha Kufua umeme  kinachomilikiwa na Familia ya Andoya, Wilaya ya Mbinga. Mradi huo wa Mbangamao unazalisha megawati 0.2, huku malengo ni kufikia megawati 2. Anayemsikiliza nyuma yake ni Meneja wa Tanesco Mkoa wa Ruvuma, Patric Lwesya, wengine ni ujumbe uliofuatana na Waziri.
  ????????????????????????????????????
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo katika picha ya pamoja na Watawa wa Shirika la Shirika la Wabenedictin wa Mtakatifu Agnes Chipole, Mfadhili wa Kituo hicho cha kufua umeme Albert Cock, ujumbe aliofuatana nao wakiwemo Maafisa toka Wizara ya Nishati na Madini, EWURA, Shirika la Umeme Nchini, Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC), Uongozi wa Wilaya ya Mbinga, Mbunge wa Mbinga Vijijini Martin Msuha, Uongozi wa Kijiji, Wakandarasi wanaojenga kituo cha kuzalisha umeme cha megawati 7.5, na baadhi ya wananchi wanaozunguka eneo hilo.
  ????????????????????????????????????
  Baadhi ya Maafisa Kutoka Wizara ya Nishati na Madini (Mbele) na ujumbe uliofuatana na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (nyuma) kutembelea kituo cha Kufua umeme cha Tulila kinachomilikiwa na Watawa wa Shirika la Wabenedictin wa Mtakatifu Agnes Chipole,wakiangalia  maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Bwawa la kufua umeme. Imeelezwa kuwa, kukamilika kwake kutawezesha uzalishaji wa umeme wa kiasi cha megawati 7.5.
  ????????????????????????????????????Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, katika picha ya pamoja na Watawa Shirika la Wabenedictin wa Mtakatifu Agnes Chipole na Mfadhili wa Kituo hicho Albert Cock.
  ……………………………………………………………………………………………………………..
  Asteria Muhozya na Rhoda James, Mbinga
  Serikali imesema  itahakikisha  inafanya Makaa ya Mawe yanakuwa chanzo kingine kikubwa cha uzalishaji umeme Nchini
  Hayo yameelezwa na Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo alipotembelea  Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Ngaka unaomilikiwa kwa ubia Kati ya Kampuni ya  TANCOAL na Serikali kupitia shirika la NDC. Mgodi huo  upo katika Wilaya ya  Mbinga mkoani Ruvuma.

  Aidha, ili kufikia lengo hilo ,Prof. Muhongo amesema Serikali itahakikisha inafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na Mgodi huo ambao Serikali ina umiliki wa hisa  ya asilimia 30 kupitia Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) ili kuimarisha uchumi wa taifa kupitia Makaa ya Mawe.
  Ameongeza kuwa, ili  kuhakikisha kwamba Kampuni ya TANCOAL inaendelea kuzalisha makaa  na kutumiwa na viwanda vya ndani, Prof Muhongo amevitaka viwanda vilivyoingia Mkataba wa mauziano na mgodi huo kuacha kununua Makaa kutoka nje ikiwa makaa ya Ngaka yanakidhi viwango na ubora unaotakiwa.

  “Nimeelezwa Makaa ya Ngaka yana  ubora na kiwango cha hali ya juu na nimeelezwa  kwamba kuna baadhi ya viwanda vimeingia mkataba na Ngaka lakini  badala yake wananunua makaa kutoka nje. Hilo halikubaliki ikiwa makaa ya ndani ya nchi yana ubora lazima tutumie bidhaa za nyumbani,”amesisitiza Prof. Muhongo.

  Kutokana na malalamiko ya Mgodi kuhusu hali ya Mkataba ya kuuziana makaa kutoafikiana, Waziri Muhongo ameutaka mgodi huo,NDC,EWURA, Kampuni za Saruji za Dangote, Tanga Cement na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kukutana Makao Makuu ya Wizara tarehe 14 Januari,2016, ili kujadili  kuhusu suala hilo na pia kujadiliana juu ya  gharama za kuuziana umeme na TANESCO pindi mgodi huo utakapoanza kuzalisha umeme kwa kutumia makaa ya mawe.

  ” Umeme wa makaa ya mawe Tanzania ni lazima. Tutapigana kufa na kupona kuhakikisha tunazalisha umeme kwa kutumia makaa ya mawe kwa sababu gharama zake zitakuwa nafuu kwa wananchi na pia umeme huu utachochea ukuaji wa viwanda nchini,” amesisitiza Prof. Muhongo.

  Kadhalika Prof. Muhongo amerejea kauli yake ya kuwataka wazalishaji umeme hususan wa makaa ya mawe na vyanzo vingine kuhakikisha wanaiuzia TANESCO umeme wa bei ya chini na kuongeza “mauziano ya umeme wa makaa ya mawe lazima yafuate viwango vya kimataifa. Lazima yawe ya gharama nafuu.”

  Katika hatua nyingine, Prof. Muhongo amewataka EWURA kubadilika na kushiriki katika hatua za mwanzo za majadiliano ya gharama za kuuziana umeme katika utekelezaji wa miradi mbalimbali badala ya kusubiri kushiriki katika hatua za mwisho na kulieleza jambo hilo kuwa ushiriki wao katika hatua za awali unawezesha majadiliano na makubaliano kufanyika kwa haraka.

  Aidha, Prof. Muhongo amechukua fursa hiyo kuzitaka Mamlaka chini ya wizara kuzingatia suala la usawa na namna Serikali inavyonufaika na makubaliano ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kitaifa kwa kuzingatia kuwa rasilimali ni za nchi , hivyo taifa linapaswa kunufaika na uwekezaji husika.Kwa mujibu wa Mkuu wa Masoko wa mgodi wa Ngaka, Christopher Temba, mgodi huo unazalisha tani za makaa ya mawe Laki Tano kwa mwaka lakini lengo ni kufikia tani milioni moja.Tayari makaa hayo yanasafirishwa katika nchi za Kenya, Zambia, Malawi na vilevile katika viwanda kadhaa hapa nchini vikiwemo vya  Saruji Tanga Mohamed Enterprises na viwanda vingine

  0 0

  kt1
  Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Misasi, Ernest Msiba akikijaribu kimoja kati ya vitanda 20 kabla ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (watatu kushoto) kumkabidhi vifaa hivyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Nathan Mshana (wapili kushoto). Waziri Kitwanga alikabidhi vitanda (20), magodoro (20) pamoja na shuka (20) kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Misasi pamoja na vitanda sita kati ya hivyo walikabidhiwa Zanahati ya Nyamijundu iliyopo Kata ya Kasololo jimboni humo. Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika katika Kijiji cha Misasi. Kushoto kwa Waziri ni Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Kanda ya Ziwa, Meshack Bandawe, ambapo shirika lake pia lilitoa baadhi ya misaada katika kituo hicho cha afya. Picha zote na Felix Mwagara.
  kt2
  Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Kanda ya Ziwa, Meshack Bandawe (kushoto) akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga, magaodoro (20) na shuka (20) vyenye thamani ya shilingi milioni tatu na laki tano katika hafla iliyofanyika Viwanja vya Kituo cha Afya Misasi, wilayani Misungwi. Waziri Chikawe baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo alivikabidhi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, pamoja na vitanda (20) vyenye thamani ya Shilingi milioni 16 ili aweze kuvigawa kwa Kituo cha Afya cha Misasi pamoja na Zahanati ya Nyamijundu iliyopo Kata ya Kasololo jimboni humo.
  kt3
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akikata utepe wakati akifungua jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Msingi ya Ihelele iliyopo Kata ya Ilujamate, jimboni humo wakati alipofanya ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi wa eneo hilo. Waziri Chikawe katika hotuba yake, aliwaahidi wananchi wa eneo hilo upatikanaji wa maji hivi karibuni kwani eneo hilo linamradi mkubwa wa maji wa Mamlaka wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Kahama Shinyanga (KASHWASA), hivyo ni lazima maji yasambazwe kwa vijiji vyote vya jirani.
  kt4
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Shule ya Msingi ya Ihelele iliyopo Kata ya Ilujamate, Wilaya ya Misungwi. Shule hiyo inajengwa kwa nguvu ya wananchi pamoja na kuchangiwa na Mamlaka wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Kahama Shinyanga (KASHWASA) ambayo inamradi mkubwa wa maji katika Kijiji cha Ihelele ambapo shule hiyo inapojengwa.
  kt5
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akizungumza na wananchi wa Kata ya Misasi mara baada ya kukabidhi vitanda (20), magodoro (20) pamoja na shuka (20) katika Kituo cha Afya cha Misasi wilayani Misungwi. Waziri Chikawe katika hotuba yake aliwaahidi wananchi wa eneo hilo ujenzi wa barabara ya lami pamoja na upatikanaji wa maji.
  kt6
  Mkuu wa Polisi Wilaya ya Misungwi (OCD), Sylivester Ibrahim akijibu maswali ya wananchi wa Kata ya Misasi kuhusu usalama katika eneo lao. Ofisa huyo wa Polisi alipewa nafasi na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (kulia-aliyekaa) baada ya wananchi hao kutaka kujua masuala ya haki zao waendapo Kituo cha Polisi kuripoti matukio mbalimbali. 
  kt7
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi misaada mbalimbali ikiwemo vitanda (20), magodoro (20) pamoja na shuka (20) katika Kituo cha Afya cha Misasi wilayani Misungwi. Picha zote na Felix Mwagara.

  0 0

  RA7
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospter Muhongo (katikakati) akimsikiliza Mbunge Mteule wa Jimbo la Ludewa, Deo Ngalawa (kulia) wakati wa ziara ya waziri alipotembelea eneo la utafiti wa mradi wa Makaa ya Mawe Mchuchuma.
  RA8
  Kamishna Msaidizi wa Madini, anayeshughulikia Leseni, Mhandisi John Nayopa (kulia) akimweleza jambo Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo wakati alipotembelea eneo la utafiti wa Mradi wa Makaa ya Mawe Mchuchuma.
  RA9
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospter Muhongo akiongea jambo wakati akikagua sampuli za Makaa ya Mawe wakati alipotembelea Kampuni ya KATEWAKA Coal field, katika wilaya ya Ludewa, Mkoa wa Njombe. Wengine ni ujumbe aliombatana nao na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo. Mwenye Skafu ni Mbunge Mteule wa Jimbo la Ludewa, Deo Ngalawa.
  RA10
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Muhongo akimsikiliza Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wilaya ya Ludewa, Raeuben Sichone wakati waziri alipotembelea kituo cha Kufua umeme cha Mawengi, Ludewa k wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi ya umeme mkoani Njombe.

  RA11
  Padre Jordan Mwanjonde wa Parokia ya Lugalawa Jimbo la Mbeya, akimweleza jambo Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na ujumbe wake wakati waziri alipotembelea mradi wa kuzalisha umeme unaomilikiwa na Jimbo hilo wakati wa ziara ya Waziri utembelea miradi mbalimbali ya kuzalisha umeme.
  RA12
  Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Madaba wakizuia msafara wa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospter Muhongo wakati akipita katika kijiji hicho kutoka Wilaya ya Ludewa kuelekea Mkoani Ruvuma, wakati wa ziara yake ya kikazi kutembelea miradi ya umeme na maeneo ya Utafiti wa Makaa ya Mawe Mkoani Njombe. Wananchi hao walimuomba Waziri awasaidie kupata nishati ya umeme katika kijiji hicho.
  RA13
  Diwani wa Kata ya Mdindi, Wilaya ya Ludewa, Waisi Mgine, (wa pili kushoto mbele) akimweleza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) kuhusu ufafanuzi wa ulipwaji wa fidia kwa wananchi wa Kijiji cha Mdindi mara baada ya mradi wa Makaa ya Mawe utakapoanza baada ya maeneo ya wananchi hao kuingizwa katika eneo la mradi na mwekezaji Kampuni ya Tanzania International Resource Limited kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC).Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dkt. Rehema Nchimbi.
  …………………………………………………………….
  Asteria Muhozya na Rhoda James – Njombe
  Serikali imesema matarajio yake ni kuona kuwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) linajiendesha kibiashara kuhakikisha kuwa wazalishaji wanaliuzia shirika hilo umeme kwa bei ambayo haitawaumiza wananchi.Kauli hiyo imetolewa leo (Januari 11,) na Waziri wa Nishati na Madin, Profesa Sospeter Muhongo alipotembelea eneo la utafiti la Makaa ya Mawe Mchuchuma wilayani Ludewa mkoani Njombe. Profesa Muhongo alieleza kuwa, endapo Tanesco itanunua umeme kwa bei ya juu kutoka kwa wauzaji inamaanisha kuwa itaendelea kuwauzia wananchi umeme wa bei ya juu ambapo pia Serikali italazimika kutoa ruzuku kwa shirika hilo ili lijiendeshe.“Tunatoka huko sasa. Hatutaki tena kuendelea kuwapa Tanesco ruzuku, tunataka shirika hili lijiendeshe kibiashara lakini pia hatutaki kuwaumiza wananchi.”Kauli ya Waziri Muhongo imekuja kufuatia kutokukubaliana kwa gharama za kuuziana umeme mara baada ya mradi wa Makaa ya Mawe ya Mchuchuma utakapoanza kuzalisha umeme kwa kutumia Makaa ya Mawe, ambapo Kampuni ya Tanzania International Resource Limited ambayo ni mbia wa Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) katika mradi wa Makaa ya Mawe kupanga kuiuzia Tanesco umeme kwa bei ya kiasi cha senti za Marekeni 13 ambapo Tanesco wanataka kununua kwa nusu ya bei hiyo.Kufuatia hali hiyo Profesa Muhongo aliitaka kampuni hiyo ya NDC na TANESCO kukaa kikao chini ya Uenyekiti wa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Juliana Pallangyo siku ya Jumatano, Januari 13, 2016 ili kujadiliana kuhusu suala hilo na kufahamu mustakabali wa uendelezaji wa mradi huo ambao utakapokamilika, unatarajiwa kuwezesha uzalishaji wa megawati 600 za umeme ambazo kati yake megawati 350 zitaingizwa katika Gridi ya Taifa.“Tunataka mradi uiuzie Tanesco umeme kwa bei rahisi lakini pia tufike mwisho wa majadiliano na mradi uanze haraka. Endapo hatutaafikiana katika hili tutafute mwekezaji mwingine,” alisema Profesa Muhongo.Akizungumzia kuhusu suala la fidia kwa wananchi waliopisha mradi huo, Profesa ameitaka kampuni hiyo kuharakisha suala la fidia na kuwaruhusu wakulima kutumia ardhi kwa shughuli za kilimo cha mazao ya muda mfupi wakati makubaliano kati ya Tanesco na kampuni yanaendelea.Naye Mbunge Mteule wa Jimbo la Ludewa Deo Ngalawa amemshukuru Profesa Muhongo kwa kufika kwake na kuendesha majadiliano kuhusu mradi huo na kuongeza kuwa, jitihada za Profesa Muhongo katika kuongeza kiwango cha umeme nchini zinaonekana na kwamba wananchi wa Ludewa wanausubiri mradi huo kwa kuwa ni ajira na fursa kwao.Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Antony Choya amemuelezea Profesa Muhongo kuwa amekuwa ni zaidi ya Mwalimu katika kuwafahamisha kuhusu mradi huo na namna anavyosimamia masuala ya nishati na hususan kutafuta ufumbuzi juu ya mradi husika.“Nampongeza sana Mheshimiwa Rais kwa uteuzi wako kushika nafasi hii,” ameongeza Mkuu wa Wilaya.Kampuni hiyo inamiliki asilimia 80 ya hisa katika mradi huo ambapo NDC wanamiliki asilimia 20.

  0 0

    Rais Mstaafu wa Tanzania, MzeeAli Hassani Mwinyi (katikati) akitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Sayansi ya Jamii ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afrika (IUA) na Rais wa Sudani ambaye pia ni mkuu wa chuo hicho, Omar al-Bashir (wa pili kulia) mjini Khartoum, Sudani  hivi karibuni.
   Rais Mstaafu, Ali Hassani Mwinyi (wa pili kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa zamani wa Mahakama Kuu ya Saudia, Abdulrahman Alsheikh Al Ashum alipotembelea Chuo Kikuu cha  Kimataifa cha Afrika (IUA) mjini Khartoum hivi karibuni na kutunukiwa Shahada ya Heshima (PHD) ya Sayansi ya Jamii ya chuo hicho na Mkuu wa chuo hicho ambaye pia ni Rais wa Sudani, Omar al-Bashir. Kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya   Munazzmat Al-Dawa wa Kanda ya Afrika Mashariki, Dk. Khalid A. Abdullah na kulia ni mke wa Mzee Mwinyi, Mama Khadija Mwinyi.
   Rais Mstaafu, Ali Hassani Mwinyi (katikati) akisalimiana na baadhi ya watanzania wanaosoma katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afrika (IUA) mjini Khartoum, Sudani  hivi karibuni ambapo pia alitunukiwa Shahada ya Heshima (PHD) ya Udaktari wa Sayansi ya Jamii ya chuo hicho na Mkuu wa chuo hicho ambaye pia ni Rais wa Sudani, Omar al-Bashir (hayupo pichani).
  Rais Mstaafu, Ali Hassani Mwinyi (wa pili kulia) akipokea nishati kutoka kwa Katibu Mkuu wa Taasisi ya  Munazzmat Al-Dawa, Abdulrahim Ali Ibrahim kutokana na mchango wa mzee Mwinyi katika kusaidia mipango na shughuli za taasisi hiyo barani Afrika hususani nchini Tanzania.  Rais mstaafu alitembelea nchini Sudani hivi karibuni ambapo akiwa huko alitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari (PHD) ya Sayansi ya Jamii ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afrika (IUA). Kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya   Munazzmat Al-Dawa wa Kanda ya Afrika Mashariki, Dk. Khalid A. Abdullah, Sheikh Athumani Kaburu wa Tanzania na waalikwa wengine. (Picha na Peter Mgongo)

   Rais Mstaafuwa Tanzania, Ali Hassani Mwinyi (katikati) akilakiwa na wenyeji wake baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Khartoum nchini Sudani hivi karibuni ambako pamoja na mambo mengine alitunukiwa shahada ya udaktari wa heshima ya sayansi ya jamii ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afrika (IUA) kutokana na mchango wake katika kusaidia maendeleo ya elimu nchini Tanzania na Afrika.

  0 0
 • 01/13/16--02:37: Article 15

 • Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Mahakama Kuu ya Tanzania Bw. Nurdin Ndimbe (kushoto) akimkabidhi Afisa Mfawidhi wa Mahabusu ya Watoto jijini Dar es salaam Bw. Ramadhan Yahaya (kulia) msaada wa vyakula na vitu mbalimbali vilivyotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania leo.
  Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Mahakama Kuu ya Tanzania Bw. Nurdin Ndimbe (kushoto) akishirikiana na Afisa Mfawidhi wa Mahabusu ya Watoto jijini Dar es salaam Bw. Ramadhan Yahaya (kulia) kupakua msaada wa vyakula na vitu mbalimbali vilivyotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania leo.
  Afisa Mfawidhi wa Mahabusu ya Watoto ya jijini Dar es salaam Bw. Ramadhan Yahaya (kulia) akipakua msaada wa vyakula na vitu mbalimbali vilivyotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania leo jijini Dar es salaam. Anayeshuhudia kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Mahakama Kuu ya Tanzania Bw. Nurdin Ndimbe
  Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Mahakama Kuu ya Tanzania Bw. Nurdin Ndimbe (kushoto) akiagana na Afisa Mfawidhi wa Mahabusu ya Watoto ya jijini Dar es salaam Bw. Ramadhan Yahaya (kulia) mara baada ya kutoa msaada wa vyakula na vitu mbalimbali. 

                             (Na. Aron Msigwa- Dar es salaam)

  Jamii imeaswa kujenga utamaduni wa kuwasaidia watu na makundi yenye mahitaji maalumu hususan wafungwa walio magerezani na wasiojiweza  ili kudumisha upendo na kuyafanya makundi hayo kujiona yanathaminiwa katika jamii.

  Wito huo umetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Mahakama Kuu ya Tanzania Bw. Nurdin Ndimbe wakati akikabidhi msaada wa vyakula na vitu mbalimbali kwa Mahabusu ya Watoto ya jijini Dar es salaam vilivyotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania kama zawadi yao ya mpya 2016.

  Bw. Ndimbe amesema Mahakama Kuu ya Tanzania imetoa msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo Mchele, Sabuni, Vinywaji, Chumvi, Unga wa Ngano, Unga wa Sembe, Mchele ,Sukari na Mafuta ya kupikia  kwa Mahabusu hao kuonyesha Upendo na namna Mahakama hiyo inavyowathamini watoto hao.

  Ameongeza kuwa Mahakama Kuu ya Tanzania imetoa msaada huo kwa lengo la kujenga mahusiano mema baina yake na watoto hao ili waendelee kuipenda na kuwa na mtazamo chanya juu ya utendaji wake.

  ‘ Nimekuja kukabidhi msaada huu kwa niaba ya Mahakama Kuu ya Tanzania kwa Mahabusu hii ya Watoto ikiwa ni zawadi yao ya mwaka mpya, lengo letu ni kujenga mahusiano mema kati yetu Mahakama na watoto hawa wajue kuwa tunasaidia jamii katika masuala mbalimbali’’ Amesema Bw. Ndimbe.

  Kwa upande wake Afisa Mfawidhi wa Mahabusu hiyo Bw. Ramadhan Yahaya akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo ameishukuru Mahakama Kuu ya Tanzania kwa uamuzi wake wa kuwakumbuka Mahabusu hao.

  Amesema kitendo cha Mahakama Kuu ya Tanzania kuwapatia msaada huo kimewapa faraja watoto hao na kuwafanya wajione wanathaminiwa na kupendwa na Mahakama hiyo.

  Ametoa wito kwa Taasisi na Mashirika mengine kuiga mfano huo ulioonyeshwa na  Mahakama  Kuu ya Tanzania ili kudumisha upendo miongoni mwa makundi ya watu wenye mahitaji maalum.

  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

  CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kinatarajia kuadhimisha miaka 39 ya kuzaliwa kwake na kumbukumbu hiyo itazinduliwa  Januari 31,Unguja –Zanzibar chini ya mgeni rasmi  Makamu Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein.

  Akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza maadhimisho ya chama hicho,Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa,Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema baada ya uzinduzi wa maadhimisho hayo Zanzibara,kilele chake kitakuwa mkoani Singida ambako zitafanyika kazi mbalimbali ikiwemo na ya kuingiza wanachama wapya, kufanya kazi za kujiletea maendeleo kwa kujenga madarasa,kupanda miti,pamoja na kufanya kazi za usafi .

  Amesema viongozi wa kitaifa na baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu watapangiwa shughuli za ujenzi wa chama na taifa kwa ujumla katika wilaya za Mkoa wa Singida siku tatu kabla ya kilele ya maadhimisho ambayo yatafanyika mkoani Singida.

  Nape amesema mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho hayo yatakayofanyika Februari 6 mkoani  Singida,anatarajiwa kuwa ni Mwenyekiti wa Chama hicho,Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne,Dk.Jakaya Kikwete.

  Kauli Mbiu ya maadhimisho kwa Chama hicho kwa mwaka huu kimetajwa kuwa ni “Sasa kazi,Kujenga Nchi na  Kukijenga Chama”.Maadhimisho ya CCM hufanyika kila Februari 5 ikiwa ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa CCM Februari 5 ,1977 iliyotokana kuungana kwa ASP na Tanu.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akizungumza na Baadhi ya Waandishi wa habari,mapema leo kuhusiana na uzinduzi wa maadhimisho ya sherehe za chama hicho pamoja na kilele chake ambacho kinatarajiwa kufanyika mkoani Singida,Mkutano huo umefanyika kwenye ofisi ndogo za chama hicho zilizopo mtaa wa Lumumba,jijini Dar .
   Mmoja wa Wanahabari akiuliza swali.
   Baadhi ya Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia mkutano huo. PICHA NA MICHUZI JR-MMG.

  0 0

  qa1

  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na balozi wa Qatar nchini, Mhe. Abdallah Jassim al Maadadi ofisini kwake jijini Dar es salaam Januari 13, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  qa2
   Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akisalimiana na  na balozi wa Qatar nchini, Mhe. Abdallah Jassim al Maadadi kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwake jijini Dar es salaam Januari 13, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  qa3
  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Balozi wa Kuwait nchini, Mhe. Jasem Al Najem, ofisini kwake jijini Dar es salaam , Januari 13, 2016. (Pichana Ofisi ya Waziri Mkuu)
  ……………………………………………………
  WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amekuatana na kufanya mazungumzo na mabalozi wawili kutoka nchi za Qatar na Kuwait.  

  Akizungumza kwa nyakati tofauti na mabalozi hao leo ,ofisini kwake ,Magogoni jijini Dar es salaam, Waziri Mkuu amewashukuru mabalozi hao kwa pongeza walizokuja kumpatia, pamoja na namna ambavyo nchi zao zimekua zikisaidia Tanzania, ambapo ameahidi  kuendeleza ushirikiano mzuri  baina ya Tanzania na nchi zao.

  Kwa upande wake, Balozi wa Qatar, Abdallah Jassim al Maadad amesema  Serikali yake itaendelea kuisaidia Tanzania katika maeneo yote ambayo Qatar imepiga hatua kubwa na inaweza kutoa msaada kwa Tanzania.

  Amesema Quwait iko tayari kuwekeza nchini katika sekta ya  kilimo, kwa vile ardhi ya Tanzania ni yenye rutuba na inafaa kwa shughuli za kilimo. Aidha, ametaja sekta nyingine  ambazo wangependa kuwekeza ni  pamoja na sekta ya uvuvi na viwanda. 

  Naye, Balozi wa Kuwait, Jasem Al Najem ambaye amekuja kujitambulisha kwa Waziri Mkuu, amesema nchi yake kupitia ‘Kuwait fund’ iko tayari kuendelea kuisaidia Tanzania katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

  Balozi  Najem, pia ameshauri vituo vya uwekezaji vya Tanzania na Kuwait kufanya kazi kwa ushirikiano zaidi ili kurahisisha utekelezaji wa miradi mbalimbali.

  0 0

   Mkurugenzi mtendaji wa TBC Clement mshana ambaye pia ni katibu wa bodi ya wakurugenzi ya TBC akimueleza jambo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo leo jijini Dar es Salaam walipokutana kuzungumzia changamoto mbali mbali za Shirika Hilo.
   Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) wakimskiliza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nnape Nnauye (hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam.  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akiongea na wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) leo hii jijini Dar es Salaam. Mhe. Nape alifanya kikao na Bodi hiyo ili kuzungumzia changamoto mbalimbali zinazolikabili shirika hilo na jinsi ya kuyapatia ufumbuzi.Kulia kwa waziri ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bi.Mwajabu Possi

  0 0


   Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Mh. Shy-Rose Bhanji, (kushoto), akipeana mikono na Balozi wa Rwanda hapa nchini, Mh.Eugene Kayihura ofisini kwa balozi Masaki jijini Dar es Salaam, Jumatano Januari 13, 2016. Mh. Bhanji alifika kumsalimia na kumtakia heri ya mwaka mpya balozi huyo ambaye nchi yake ni mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)
   Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania, Mh. Shy-Rose Bhanji, (kushoto), akiwa na mazungumzo na Balozi wa Rwanda hapa nchini, Mh. Eugen Kaihura kwenye ofisi ya Balozi, Masaki jijini Dar es Salaam Jumatamo Januari 13, 2016. Mh. Bhanji alifika kumsalimia na kumtakia heri ya mwaka mpya balozi huyo ambaye nchi yake ni mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

  NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
  MBUNGE wa Bunge la Afrika Mashariki, (EALA), tawi la Tanzania, Mh. Shy-Rose Bhanji, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Rwanda hapa nchini, Mh. Eugen Kaihura, ofisini kwa Balozi, Masaki jijini Dar es Salaam, leo Jumatano Januari 13, 2016.

  Wakizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mkutano wao, Mh. Bhanji alsiema, Rwanda ni nchi mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kama ilivyo kwa Tanzania, na Bunge la Afrika Mashariki linaundwa na wabunge kutoka nchi zote wanachama ambazo ni Tanzania, Rwanda, Burundi, Kenya na Uganda, hivyo aliona umuhimu wa kwenda kumtakia heri ya mwaka mpya balozi huyo wa Rwanda.

  Naye Balozi wa Rwanfa hapa nchini, Mh. Kaihura, alimsh
  ukuru mbunge huyo kwa kumtembelea ofisini kwake na kumtakia heri ya mwaka mpya, na kumuhakikishia Rwanda ambayo ni mwanachama wa Jumuiya itaendelea kushirikiana na nchi wanachama wa jumuiya hiyo ili kujenga Afrika Mashariki iliyo na ustawi wa hali ya juu na ushirikiano uliotukuka
   Mh. Bhanji akizungumza na waandishi wa habari
   Mh. Bhanji na balozi Mh. Kaihura wakiwa kwenye mazungumzo
   Mh. Balozi Kaihura akizungumza na waandishi wa habari
   Mh. Bhanji akiweka saini kitabu cha wageni ofisini kwa balozi Kaihura
   Mh. Balozi Kaihura akimsindikiza mgeni wake Mh. Bhanji
  Mh. Balozi Kaihura, akimuonyesha umbo la kitamaduni lililobuniwa nchini Rwanda likionyesha rangi za nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

  0 0


  Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari akiwa katika moja ya karakana ya kutengeneza vifaa tiba katika mji wa Guangzhou nchini China.

  Mheshimiwa Nassari akifanya mazungumzo na wahusika wa karakana hiyo kuona namna ya kuapata vifaa hivyo kwa ajili ya kusidia katika Hosptali ya wilaya ya Arumeru na vituo vya afya.
  Mh Nassari akiwa amelala kwenye moja ya vitanda vya wagonjwa alivyokuta katika karakana hiyo.
  Mh ,Nassari akipita katika karakana hiyo .  Mh Nassari akifanya mazungumzo na wahusika wa karakana hiyo ambako anatarajia kutumia fedha za mkopo wa gari la Ubunge kwa ajili ya kununua vitanda 200 ,viti vya magaurudumu pamoja na kabati ndogo za kuhifadhia dawa pamoja na vifaa vidogo vya matibabu.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya Kskazini.

  0 0
 • 01/13/16--04:29: Pato la Taifa lazidi kukua
 • dk1

  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi za Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa (katikati) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati akitoa takwimu za pato la Taifa kwa kipindi cha robo ya tatu ya mwaka 2015 (Julai – Septemba), kulia ni Mhadhiri Mwandamizi wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Haji Semboja na kushoto ni Mkurugenzi wa Sera na Utafiti toka Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) Bw. Hussein Kamote.
  dk2
  Mhadhiri mwandamizi wa uchumi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Haji Semboja (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati wakitoa takwimu za pato la Taifa kwa kipindi cha robo ya tatu ya mwaka 2015 (Julai – Septemba), kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi za Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa.
  dk3
  Mkurugenzi wa Sera na Utafiti toka Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania Bw. Hussein Kamote akieleza kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) juu ya mchango wa viwanda katika kuongeza pato la taifa wakati wakitoa takwimu za pato la Taifa kwa kipindi cha robo ya tatu ya mwaka 2015 (Julai – Septemba), kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi za Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa.
  dk4
  Baadhi ya watendaji wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt. Albina Chuwa (hayupo pichani) wakati akitoa takwimu za pato la Taifa kwa kipindi cha robo ya tatu ya mwaka 2015 (Julai – Septemba).
  dk5
  Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi za Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa (hayupo pichani) wakati akitoa takwimu za pato la Taifa kwa kipindi cha robo ya tatu ya mwaka 2015 (Julai – Septemba), mapema hii leo jijini Dar es Salaam.Picha zote na Eliphace Marwa – MAELEZO

  ……………………………………
  Na. Frank Shija
  Pato la Taifa katika kipindi cha Robo tatu ya mwaka 2015 limeendelea kukua kwa kasi ya asilimia 6.3 ikilinganishwa na kasi ya asilimia 5.4 katika kipindi cha mwaka 2014.

  Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa alipokuwa akiongea na waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam.Dkt. Albina amesema kuwa kutokana na ongezeko hilo Serikali imeendelea kutoa huduma za kijamii zikiwemo umeme, afya na maji

  “ Pato la Taifa kwa robo tatu ya mwaka 2015 limeendelea kukua kwa kasi ya asilimia 6.3 ukilinganisha na asilimia 5.4 katika robo tatu ya mwaka 2014” Alisema Dkt. Albina.

  Dkt. Albina ameongeza kuwa kuongezeka kwa Pato la Taifa kumeenda sanjari na kuongezeka kwa thamani ya bidhaa na huduma nje ya nchi kwa takribani asilimia 3.3 ambapo bidhaa na huduma zilizochangia ongezeko hilo ni pamoja na dhahabu, Almasi, madini mengine na Utalii.

  Aliongeza kuwa utangazwaji wa Takwimu za Pato la Taifa unazingatia matakwa ya Sheria ya Takwimu na 9 ya mwaka 2015 inayotoa mamlaka kwa Tume ya Taifa ya Takwimu kukusanya, kuchambua na kutangaza takwimu za Pato la Taifa.

  Aidha alitaja baadhi ya shughuli za kiuchumi zilizokua kwa kasi kubwa katika kipindi cha Julai hadi Septemba 2015 kuwa ni pamoja na Ujenzi (17.6%), Uchukuzi na Uhifadhi (10.6%), Uendeshaji Serikali na Ulinzi (10.6%) na Uchimbaji Madini na Kokoto (8.0%).

  Dkt. Albina amesema kuwa jumla ya thamani ya Pato la Taifa kwa bei za miaka husika katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Septemba 2015 ni takribani shilingi tilioni 71.7 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 6.9.

  0 0


  Naibu Waziri Fedha na Mipango Dkt,Ashatu Kijaji akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Mbeya ( hawapo pichani) mara baada ya kufanya ziara katika Mpaka wa Tunduma na Zambia .
  Baadhi ya waandishi wa Habari Mkoani Mbeya wakiwa makini kumsikiliza Naibu waziri wa Fedha na Mipango Dkt Kishatu Kijaji katika ofisi za Mamlaka ya Mapato TRA Mkoani humo kwa lengo la kutoa tathimini yake ya ziara aliyoifanya katika Mpaka wa Tunduma na Zambia .

  Na Jamiimojablogu,Mbeya

  Naibu waziri wa fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji ameitaka Mamlaka ya Mapato TRA Mkoa wa Mbeya kuhakikisha inaanda mpango maalumu kwa ajili kudhibiti mapato yanayopotea kutokana na kushamili kwa biashara ya ubadilishaji wa fedha kiholela katika mpaka wa Tunduma na Zambia.

  Naibu waziri huyo ametoa kauli hiyo Mkoani Mbeya mara baada ya kutembelea Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoani humo na kutoa tathimini ya ziara yake aliyoifanya katika Mpaka wa Tunduma na Zambia.

  Amesema serikali imekuwa ikipoteza mapato mengi hasa kutokana na kuwepo kwa biashara hiyo kiholela pasipo serikali kupata mapato yake hivyo ameitaka mamlaka hiyo kuhakikisha inaweka mpango kabambe utakao iwezesha serikali kupata mapato yake kutokana na biashara hiyo.

  Amesema serikali lazima ijiendeshe yenyewe kwa kuongeza ukusanyaji wa mapato sanjali na kuzuia mianya yote ya ukwepaji wa kodi pamoja na watu wote kuhakikisha wanalipa kodi.Amebainisha kuwa nchi inategemea mapato kwa ajili ya kutoa huduma muhimu kwa wananchi na hivyo kuwaongezea wananchi matumaini kwa kuwafikishia huduma muhimu.

  Sehemu nyingine ambayo ameiagiza mamlaka hiyo kuishughulikia mara moja ili serikali iweze kupata mapato yake ni pamoja kuibuka kwa Saccos pamoja vikundi mbalimbali ambavyo vimekuwa vikijihusisha na ukopeshaji wa fedha kwa liba kubwa hali ambayo pia imekuwa ikiwapa mzigo mkubwa wananchi .

  Katika hatua nyingine Naibu waziri huyo ameuagiza uongozi wa mamlaka ya mapato (TRA) Katika mpaka wa Tunduma na Zambia kuhakikisha kuwa mizigo yote inayosafilishwa kupitia mpaka huo inafanyiwa tathimini na kulipiwa kwa muda wa usio zidi siku moja tayari kuendelea na safari kwa inayoingia na kutoka nje ya Tanzania.Ziara ya Naibu Waziri Dr. Kijaji ni ya kwanza Mkoani Mbeya tangu alipoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 11 Desemba 2015 kushika wadhifa huo.

  0 0

   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah  Kairuki (Mb) (kushoto)  akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) Bi. Haighat Kitala (kulia) alipotembelea ofisi hiyo mapema leo.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah  Kairuki (Mb)(kulia)  akizungumza na vyombo vya habari alipotembelea Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) mapema leo.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah  Kairuki (Mb) akizungumza na watumishi wa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) alipotembelea ofisi hiyo mapema leo.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah  Kairuki (Mb) akipokea Nyaraka kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) Bi. Haighat Kitala (kulia) alipotembelea ofisi za Mfuko huo mapema leo.

  0 0

   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kushoto) akizungumza na Mshauri wa Masuala ya Utamaduni kutoka Kituo cha Utamaduni wa Iran  hapa nchini Bw. Ali Bagheri alipomtembelea ofisni kwake leo jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kushoto) akifurahia jambo na Mshauri wa Masuala ya Utamaduni kutoka Kituo cha Utamaduni wa Iran  hapa nchini Bw. Ali Bagheri alipomtembelea ofisni kwake leo jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kushoto) akikabidhiwa zawadi ya Kitabu cha mashairi ya Iran na Mshauri wa Masuala ya Utamaduni kutoka Kituo cha Utamaduni wa Iran  hapa nchini Bw. Ali Bagheri alipomtembelea ofisni kwake leo jijini Dar es Salaam.
  Picha na Frank Shija,WHUSM

  0 0
 • 01/13/16--04:58: TAARIFA KWA UMMA


 • 0 0

  BOFYA LINK HAPO CHINI KUSIKILIZA

  0 0

  Na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
  WAMILIKI wa Taasisi za Kifedha wanatakiwa kujiridhisha kama waajiliwa katika taasisi hizo kama wanahusika kwa njia moja ama nyingine katika uharifu unaohatarisha maisha ya wakazi wa jijini la Dar es Salaam.

  Hayo yamesemwa na  Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam leo.

  Kamanda Sirro amesema kuwa hatua za makusudi zimechukuliwa katika maeneo mbalimbali hasa ya eneo la Kibiashara la Mlimani City kutokana na matukio mengi ya uporaji  wa fedha kwa kutumia pikipiki.

  Pia amesema kuwa pamoja na sheria hizo kuchukuliwa watafanya operasheni maalumu katika eneo hilo na kutafuta namna nzuri ya kuondoa pikipiki katika maeneo hayo.

  Katika Operasheni zilizofanywa na Jeshi hilo wamefanikiwa kuwakamata majambazi nane pamoja na kumamata Bunduki mbili aina ya Pump Action ambazo namba zake zilifutwa na kukatwa Mtutu.

  Aidha Kamanda Sirro amesema kuwa katika Operasheni hiyo wamemkamata jambazi aliyekuwa akitafutwa kwa muda mrefu anayejulikana kama Mkama Hassan mkazi wa Gomgolamboto jijini Dar es Salaam na alipopekuliwa alikutwa na Bastola aina ya Chinese iliyofutwa namba ikiwa na magazine yenye risasi saba. 
  Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Operasheni kali inayoendelea jijini Dar es Salaam.
  Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro akionyesha Siraha zilizokamatwa katika Oparasheni ya kutokomeza uharifu jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro leo wakati akizungumuza nao
  Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

  0 0

   Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kushoto) akibadilishana hati ya makubaliano ya mkopo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Uwekezaji (TIB), Jaffer Machano mara baada ya kutiliana saini. TTCL na TIB zimesaini mkataba wa makubaliano ya dhamana ya Benki na Mkopo wa Dola za Marekani milioni 22 ikiwa ni awamu ya kwanza ya mkopo wa Dola za Marekani milioni 329 zitakazotolewa kwa kampuni ya TTCL.  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kushoto) akibadilishana hati ya makubaliano ya mkopo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Uwekezaji (TIB), Jaffer Machano mara baada ya kutiliana saini. TTCL na TIB zimesaini mkataba wa makubaliano ya dhamana ya Benki na Mkopo wa Dola za Marekani milioni 22 ikiwa ni awamu ya kwanza ya mkopo wa Dola za Marekani milioni 329 zitakazotolewa kwa kampuni ya TTCL. Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Uwekezaji (TIB), Jaffer Machano (kulia) akizungumza na wanahabari katika hafla fupi ya kutiliana saini na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) juu ya makubaliano ya dhamana ya Benki na mkopo wa Dola za Marekani milioni 22 ikiwa ni awamu ya kwanza ya mkopo wa Dola za Marekani milioni 329 zitakazotolewa kwa TTCL. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kushoto) akizungumza na wanahabari kabla ya kusaini hati ya makubaliano ya mkopo wa TTCL uliyotolewa na TIB. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Uwekezaji (TIB), Jaffer Machano akifuatilia. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Uwekezaji (TIB), Jaffer Machano (kulia) wakisaini hati ya makubaliano ya mkopo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. TTCL na Benki ya TIB zimesaini makubaliano ya dhamana ya Benki na Mkopo wa Dola za Marekani milioni 22 ikiwa ni awamu ya kwanza ya mkopo wa Dola za Marekani milioni 329 zitakazotolewa kwa kampuni ya TTCL. Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.

  KAMPUNI ya Simu Tanzania TTCL na Benki ya TIB leo zimetiliana saini Mkataba wa makubaliano ya dhamana ya Benki na Mkopo wa Dola za Marekani Milioni 22 ikiwa ni awamu ya kwanza ya mkopo wa Dola za Marekani milioni 329 itakazopewa TTCL. 

  Akizungumza katika hafla ya kusaini hati ya makubaliano ya mkopo huo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura alisema mkopo huo ni mahususi kwa ajili ya kuiwezesha TTCL kusimika mitambo mipya na ya kisasa kuboresha huduma zake kwa kujenga na kusambaza huduma za Mitandao ya 3G na 4G LTE nchini kote.

  Dk. Kazaura alisema hatua hiyo ni habari njema kwa Watanzania, hasa wateja na wadau wa huduma za kampuni ya TTCL. “…TTCL inaishukuru sana Benki ya TIB kwa kutuamini na kukubali kushirikiana nasi baada ya kujiridhisha kuwa tunao uwezo na nia thabiti ya kufanya mageuzi makubwa ya kibiashara ili kuboresha huduma zetu,” alisema Dk. Kazaura akizungumza.

  “Kupatikana kwa mkopo na dhamana hizi kutapunguza tatizo la ukosefu wa fedha lililokuwa linatukabili na sasa tutaweza kutekeleza kwa kasi mpango wetu wa mageuzi ya Ki biashara ikiwa ni pamoja na kujenga miundombinu, kuleta mitambo na vifaa vya kisasa vitakavyoongeza ufanisi katika huduma zinazotolewa na TTCL kwa Wateja wa ndani na nje ya nchi. Natoa wito kwa Watanzania na Wateja wetu wote kwa ujumla waendelee kutegemea huduma na bidhaa zenye viwango vya juu kabisa vya ubora, uhakika na gharama nafuu kutoka TTCL.” Amesema Dk. Kazaura. 

  Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIB, Jaffer Machano amesema katika kutimiza wajibu wa TIB kama benki ya maendeleo, ujenzi wa miundombinu umepewa kipaumbele na hii ni pamoja na miundombinu ya sekta ya Mawasiliano.

  “Kama alivyosema Dk. Kazaura, lengo la mpango mzima ni kuwapatia Dola milioni 329 na TIB ipo tayari kuhakikisha mradi huu unafanikiwa kwa kushirikisha kampuni zote za TIB group. Mfano mzuri ni mradi huu wa kwanza ambao umefanywa na kampuni tanzu ya TIB group- TIB Corporate Bank, amesema Jaffer Machano.”

  Baadhi ya huduma za TTCL zitakazoimarika baada ya uwezeshaji huu ni pamoja huduma za simu na intaneti yenye kasi kubwa inayowezesha huduma za kijamii kufanyika kwa urahisi kwa njia ya mtandao. Huduma kama vile za Elimu kwa njia ya mtandao (E education), Afya kwa njia ya mtandao (E health) na huduma katika Sekta nyingine za kiuchumi kama vile Biashara, Viwanda na Kilimo nazo zitanufaika sana ambapo wafanyabiashara na wazalishaji wa bidhaa mbalimbali watapata Mawasiliano ya uhakika katika kufanikisha shughuli zao.

  Kampuni ya Simu Tanzania TTCL ipo mbioni kuanzisha huduma ya kusafirisha fedha kwa njia ya Mtandao ifikapo robo ya pili ya mwaka huu ili kutekeleza ombi la muda mrefu la Wateja wake wanaohitaji sana kuanzishwa kwa huduma hii kutokana na Mtandao mpana wa Kampuni uliosambaa ndani na nje ya nchi na unafuu wa gharama.

  0 0

  Meno ya Tembo vipande 8 vyenye uzito wa kilo 50 ya thamani ya milioni 120 ambayo ni sawa na Tembo hai wane aliyokamatwa nayo hivi karibuni mtuhumiwa Nzuri Ndizu Mkazi wa Kijiji cha Mbede Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi
  Mtuhumiwa Nzuri Ndizu Mkazi wa Kijiji cha Mbende Wilaya ya Mlele akiwa katika ofisi ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi baada ya kukamatwa na meno ya Tembo vipande nane yenye thamani ya shilingi milioni 120 hapo juzi .
  Kamanda wa Polisi wa Mkoa Katavi Dhahiri Kidavashari akiwa ameshika meno ya Tembo aliyokamatwa nayo mtuhumiwa Nzuri Ndizu mkazi wa Kijiji cha Mbede Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi ambae alikamatwa juzi akiwa na vipande 8 yenye thamani ya milioni 120 .

  Picha na Walter Mguluchuma Katavi yetu blog

  Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Nzuri Ndizu (44) Mkazi wa Kijiji cha Mbede Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi amekamatwa akiwa na meno ya Tembo nane yenye uzito wa kilogramu 50 yakiwa na thamani ya shilingi milioni 120 ambapo ni sawa na Tembo wanne waliuwawa.Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari aliwaambia waandishi wa Habari kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa mida ya saa tatu na nusu .

  Kidavashari alisema mtuhumiwa Ndizu alikamatwa kufuatia misako na uparesheni mbalimbali zinazoendelea kufanywa na Jeshi la Polisi ikiwa ni kuhakikisha wahalifu wa makosa mbalimbali wakimemo wawindaji haramu wa wanyama pori wanakamatwa.Siku hiyo ya tukio jeshi la polisi lilipata taarifa toka kwa Raia wema kuwa katika pori la akiba la Lwafe kuna watu wanajihusisha na biashara haramu ya meno ya Tembo .

  Kidavashari aliendelea kuwaambia waandishi wa Habari baada ya taarifa hizo kupokelewa ufuatiliaji ulifanyika kwa polisi kufika kwenye eneo hilo na kuweka mtego .Na walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo Nzuri Ndizu akiwa na meno ya Tembo vipande nane akiwa ameyaficha kwenye pori kwa ajiri ya kusubilia wateja .

  Kamanda Kidavashari alisema mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa na jeshi la Polisi kwa hatua za upelelezi zaidi ilikuendelea kubaini mitandao yote inayojihusisha na biashara hiyo haramu ya meno ya Tembo na kufikishwa Mahakamani baada ya upelelezi kukamilika .

  Hivi karibuni watu watatu walikamatwa katika mtaa wa Aiter Mjini hapa wakiwa na vipande kumi na mbili vya meno ya Tembo yenye thamani ya shilingi milioni 120 hari hiyo inaonyesha kuwa kuna kasi kubwa ya biashara haramu ya meno ya Tembo Mkoani Katavi .Na Katavi yetu blog/Blogs za Mikoa

older | 1 | .... | 736 | 737 | (Page 738) | 739 | 740 | .... | 1897 | newer