Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live

UCHAMBUZI WA HABARI ZA MAGAZETINI LEO.

$
0
0
Prof. Ndalichako awapiga kitanzi waliovurunda elimu, Serikali yadhibiti ulanguzi wa ardhi. Pata mengi yaliyojiri magazetini hapa.

Waziri Ummy Mwalimu atembelea jengo la zahanati ya Mpingi wilaya ya Songea.

$
0
0
images
Na Mwandishi Maalum.
WAZIRI WA AFYA Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu ametembelea jengo la zahanati ya Mpingi wilaya ya Songea Vijijini na kuzungumza na wanakijiji wa eneo hilo. 

Ziara hiyo ni moja kati ya kazi anazozifanya mkoani hapa kwa lengo la kuzungumza na wananchi, watoa huduma na watumishi wa sekta ya afya ili kuboresha huduma za matibabu na kuhamasisha wananchi kushiriki katikashughuli mbalimbali za afya ikiwemo uchangiaji katika mifuko ya afya Baada ya kufika kijijini hapo na kuona jitihada zilizofanywa na Halmashauri na wananchi, Waziri Ummy aliwaahidi wananchi hao mabati na misumari ili kuunga mkono ujenzi wa zahanati hiyo.

JESHI LA POLISI KITENGO CHA USALAMA BARABARANI YAENDESHA ZOEZI LA KUTOA ELIMU KWA MADEREVA KUTOKUTUMIA SIMU WAKATI WAKITUMIA VYOMBO VYA MOTO.

$
0
0
 Msaidizi Mkaguzi Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani wa Wilaya ya Mtwara(DTO) Ahmed Mutabuzi(wapili toka kushoto) akiwakiwaelimisha madereva wa mabasi yanayofanya safari za mikoani kuhusiana na mwendelezo wa kampeni ya”Wait to Send”inayotoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto,Zoezi hilo lilifanyika stendi kuu ya mabasi ya Mtwara mjini,Katikati pichani ni Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu ambao ni wadhamini wakuu wa kampeni hiyo.
 Madereva wa mabasi ya Mkoani Mtwara yanayofanya safari za mikoa mbalimbali wakimsikiliza Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu(wapili toka kushoto)akiwasomea ujumbe maalum ambao ni kauli mbiu ya kampeni ya”Wait to Send”inayotoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto,Zoezi hilo lilifanyika stendi kuu ya mabasi ya Mtwara mjini,Kushoto ni Msaidizi Mkaguzi Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani wa Wilaya ya Mtwara(DTO) Ahmed Mutabuzi.
 Msaidizi Mkaguzi Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani wa Wilaya ya Mtwara(DTO) Ahmed Mutabuzi pamoja na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu ambao ni wadhamini wakuu wa kampeni ya”Wait to Send” inayotoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto wakipandika stika yenye ujumbe maalum wa kampeni hiyo kwenye basi linalofanya safari za mikoani wakati wa zoezi hilo lililofanyika stendi kuu ya mabasi ya Mtwara mjini.
 Askari wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Mtwara SGT. Martin Muyomba(kushoto) akimpima kiwango cha pombe mwilini dereva wa basi la kwenda mikoani, Masoud Ramadhani ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya”Wait to Send” inayotoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto,Zoezi hilo lilifanyika stendi kuu ya mabasi ya Mtwara mjini,Katikati pichani ni Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu ambao ni wadhamini wakuu wa kampeni hiyo.
 Askari wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Mtwara SGT. Martin Muyomba(kushoto)akiandika maelezo ya Mohamed Rashid(kulia)ambaye ni dereva wa basi linalofanya safari za mikoani ili ampime kiwango cha pombe mwilini wakati wa zoezi la mwendelezo wa kampeni ya”Wait to Send” inayotoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto,Zoezi hilo lilifanyika stendi kuu ya mabasi ya Mtwara mjini,Katikati pichani ni Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu ambao ni wadhamini wakuu wa kampeni hiyo.

WAZIRI KITWANGA AKUTANA NA VIONGOZI WA WILAYA YA MISUNGWI, ACHANGIA MIRADI YA MAENDELEO.

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akizungumza na Wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza mara baada ya kupokelewa wilayani hapo. Waziri Kitwanga aliwataka viongozi hao kuongeza nguvu kubwa ya kukusanya kodi kwa wafanyabiashara wenye mitaji mikubwa na si kuwasumbua wafanyabiashara wadogowadogo. Pia aliwataka viongozi hao wahakikishe hakuna mwanafunzi atakayekaa chini darasani ifikapo mwakani.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akiwauliza maswali viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza wakati alipokuwa anakagua ujenzi wa Maabara katika Shule ya Sekondari Aimee Milembe wilayani humo. 
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akiwauliza maswali viongozi wa Kata ya Mabuki wilayani Misungwi wakati alipokuwa anakagua ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kijiji cha Mhungwe katika kata hiyo. Waziri Kitwanga alichanga milioni moja kwa ajili ya ujenzi wa Kituo hicho cha afya. Wapili kulia ni Diwani wa Kata hiyo, Nicodemus Ihano, na wapili kushoto ni Mtendaji wa Kata hiyo, Angelina Nyanda.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (kushoto) akiangalia ufa katika moja ya madarasa ya Shule ya Msingi Lubuga iliyopo Kata ya Mabuki wilayani Misungwi. Waziri Kitwanga aliagiza darasa hilo livunjwe na ameahidi kuchangia matofali pamoja na mifuko ya saruji.

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (kulia) akimsalimia Diwani wa Kata ya Misungwi, Mwamba Makune, wakati Waziri huyo alipokuwa anawasili katika Shule ya Sekondari ya Aimee Milembe jimboni humo kwa ajili ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo pamoja na kuzungumza na viongozi wa Serikali ya vijiji katika Kata ya Misungwi. 
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Mwajuma Nyiruka akizungumza na Wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi (hawapo pichani) kabla ya kumkaribisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) ili azungumze na wakuu hao wa idara. Waziri Kitwanga aliwataka viongozi hao waongeze nguvu ya kukusanya kodi kwa wafanyabiashara wenye mitaji mikubwa na si kuwasumbua wafanyabiashara wadogowadogo. Pia aliwataka viongozi hao wahakikishe hakuna mwanafunzi atakayekaa chini darasani jimboni humo ifikapo mwakani. Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Nathan Mshana. 
Picha zote na Felix Mwagara.

UTT AMIS YATOA SEMINA KWA WAFANYAKAZI WA MAZNAT JUU YA UWEKEZAJI WA PAMOJA

$
0
0
Mkurugenzi wa Maznat Bridal akifungua semina kwa wafanyakazi wake juu ya huduma bora kwa wateja, ujasiriamali na Uwekezaji wa Pamoja iliyofanyika katika hoteli ya Kebbs jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa masoko na uhusioano UTT AMIS akihamasisha Uwekezaji wa Pamoja katika semina ya wafanyakazi wa Maznat Bridal and Beauty Services katika hoteli ya Kebbs jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko na Uhusioano UTT AMIS akihamasisha Uwekezaji wa Pamoja katika semina ya wafanyakazi wa Maznat Bridal and Beauty Services katika hoteli ya Kebbs jijini Dar es Salaam.

WAZIRI LUKUVI AWAONYA MADALALI WA ARDHI, AFANYA ZIARA KIBAHA ADHAMIRIA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI.

$
0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wiliam Lukuvi akisaini kitabu cha wageni alipowasili Ofisi ya mkoa wa Pwani kukagua utendaji wa kazi kuzungumza na wananchi pia kusikiliza malalamiko na kero zao kuhusu maswala ya ardhi alipokuwa kwenye ziara ya kikazi katika Wilaya ya Kibaha jana. 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wiliam Lukuvi akikagua mafaili ya hati za ardhi za wananchi yanayodaiwa kukaa kwenye shelvu kwa zaidi ya miaka mitatu pasipo kufikishwa kwa wahusika. Anayempa maelezo ni Afisa Ardhi Mteule, Majaliwa Jaffari. 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wiliam Lukuvi akikagua mafaili ya hati za ardhi za wananchi yanayodaiwa kukaa kwenye shelvu kwa zaidi ya miaka mitatu pasipo kufikishwa kwa wahusika. Anayempa maelezo ni Afisa Ardhi Mteule, Majaliwa Jaffari. 
Wantedanji na viongozi wakimsikiliza Waziri Lukuvi. 
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Bi. Halima Kiemba akimsomea muhtasari Waziri wakati wa kikao na viongozi pamoja na watendaji wa wilaya hiyo Mkoa wa Pwani jana. Kutoka (kulia) ni Mkubge wa Kibaha, Mhe. Koka Foka na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Mgeni Bauani. 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wiliam Lukuvi akiongea na wafanyakazi na watendaji wa Halmashauri ya Kibaha pamoja katika kikao nao kabla kuzungumza na wananchi na kusikiliza malalamiko na kero zao kuhusu maswala ya ardhi alipokuwa kwenye ziara ya kikazi katika Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani jana. 
Waziri Lukuvi akielekeza jambo alipotembelea eneo la Stendi ya mabasi eneo la Kibaha Maili moja na kujadili namna ya kufanikisha mradi wa ujenzi wa kituo hicho. Kushoto ni Mbunge wa Kibaha, Mhe. Koka Foka na Mkuu wa Wilaya hiyo Halima Kiemba. 
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wiliam Lukuvi akisikiliza kero za Bi. Zena Shabani kabla kupokea vielelezo vya malalamiko na kero za kuzulumiwa ardhi yenye hekari 50 kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemiah Mchechu kutoka kwa Zena Shaban (85) alipokuwa katika ziara ya kikazi kusikiliza malalamiko ya wananchi Kibaha Mkoa wa Pwani jana. 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wiliam Lukuvi akipokea vielelezo vya malalamiko na kero za kuzulumiwa ardhi yenye hekari 50 kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemiah Mchechu kutoka kwa Zena Shaban (85) alipokuwa katika ziara ya kikazi kusikiliza malalamiko ya wananchi Kibaha Mkoa wa Pwani jana. 
Mmoja wa wananchi waliohudhuria mkutano huo akitoa kero zake kwa Waziri. 



Samatta kupongezwa Dar Live leo

$
0
0
Mchezaji Bora wa Mwaka 2015 kwa Wachezaji wa Ndani, mchezaji wa Taifa Stars na Klabu ya TP Mazembe ya DRC Congo, Mbwana Samatta.

BAADA ya kushinda Tuzo ya Afrika kama Mchezaji Bora wa Mwaka 2015 kwa Wachezaji wa Ndani, mchezaji wa Taifa Stars na Klabu ya TP Mazembe ya DRC Congo, Mbwana Samatta anatarajiwa kupongezwa na kuagwa rasmi na mashabiki wake leo ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.  Akizungumza na Uwazi, Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alisema kuwa mapema kabla ya saa kumi na mbili jioni kutakuwa na matembezi sambamba na Samatta maeneo ya Temeke na baada ya hapo, saa kumi na mbili atatinga ndani ya Dar Live kuwaaga mashabiki wake. 


“Kutakuwa na red carpet ambapo mashabiki wote watapata fursa ya kupiga picha na Samatta sambamba na kuzungumza naye mawili matatu kisha burudani kabambe itafuatiwa kutoka kwa Khalid Chokoraa ambaye tayari amemtungia wimbo, Twanga Pepeta chini ya Ali Chocky pamoja na Msagasumu,” alisema Mbizo na kumalizia kuwa kiingilio kitakuwa ni 5,000 kwa wote.

WAZIRI UMMY MWALIMU ATEMBELEA HOSPITALI YA PERAMIHO SONGEA

$
0
0
 Waziri Ummy Mwalimu akisalimiana na Padri Lucius wa hospitali ya Peramiho Mheshimiwa Ummy Mwalimu akizungumza na Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Peramiho, Dr. Venance Mushi, alipotembelea hospitali hiyo asubuhi ya leo. Baadhi ya wanachama wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), wakiwa sehemu ya mapokezi, tayari kwa kupata huduma.

WAZIRI UMMY MWALIMU ATEMBELEA JENGO LA ZAHANATI YA MPINGI WILAYA YA SONGEA.

$
0
0
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu ametembelea jengo la zahanati ya Mpingi, wilaya ya Songea Vijijini na kuzungumza na wanakijiji wa eneo hilo.

 Ziara hiyo ni moja kati ya kazi anazozifanya mkoani hapa kwa lengo la kuzungumza na wananchi, watoa huduma na watumishi wa sekta ya afya ili kuboresha huduma za matibabu na kuhamasisha wananchi kushiriki katika shughuli mbalimbali za afya ikiwemo uchangiaji katika mfuko wa Bima ya Afya.

Baada ya kufika kijijini hapo na kuona jitihada zilizofanywa na
na wananchi katika kujenga zahanati ya kijiji, Waziri Ummy aliwaahidi wananchi hao mabati na misumari ili kuunga mkono ujenzi wa zahanati hiyo. 
Mheshimwa Ummy Mwalimu akisaini kitabu cha wagenii kijijini Mpingi .
Baadhi ya wananchi wa Mpingi waliohudhuria kumlaki Waziri Ummy Mwalimu alipotembelea majengo ya zahanati yao.
Waziri Ummy Mwalimu akiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Benson Mpesya, kutembelea majengo ya zahanati ya Kijiji cha Mpingi .
Mzee Mohamed Mussa, mkazi wa kijiji cha Mpingi akimshukuru Waziri Ummy Mwalimu kwa kutembelea kijiji chao na kutoa msaada wa bati na misumari ya kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kijiji .

MISA MAALUM YA MZEE AMOS KALUGENDO KUFANYIKA LEO NYUMBANI KWAKE SEGEREA

$
0
0

Familia ya Kalugendo inapenda kukuarika kushiriki nasi kwenye misa ya kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kifo cha baba yetu mpendwa Mzee Amos Kalugendo, misa itafanyika tarehe 12.01.2016 nyumbani Karakata Bondeni saa 11 jioni.

Pia katika misa hiyo kutakuwa na Sadaka maalumu ya shukrani makusanyo yatapelekwa kanisani kuchangia ujenzi wa Kanisa na baada ya misa kutakuwa na Chakula cha jioni kwa wote. Karibuni sana tujumuike pamoja katika kumuombea baba yetu. Asante.

SERIKALI KUKAMILISHA UKARABATI WA KITUO CHA AFYA CHIPOLE.

$
0
0
 Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen, Mbazi Msuya akisisitiza umuhimu wa kuwa na Kituo cha Afya chenye vifaa tiba, tarehe 12 Januari 2016, wakati alipokuwa akikagua ukarabati wa kituo cha Afya cha Chipole wilayani songea vijijini, baada ya kituo hicho kuungua mwaka 2013 na Ofisi hiyo kukikarabati. (wa kwanza kulia) ni Makamu wa Mama Mkubwa Chipole, Sista. Sairis Mkinga.
 Daktari wa Kituo cha Afya cha Chipole, Ismail Mzimya akieleza umuhimu wa kituo hicho kwa wananchi wa Kata ya Magagura wilayani Songea vijijini wakati Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen, Mbazi Msuya tarehe 12 Januari 2016, alipokuwa akikagua ukarabati wa kituo hicho baada ya kituo hicho kuungua mwaka 2013 na Ofisi hiyo kukikarabati. (wa kwanza kulia) ni Makamu wa Mama Mkubwa Chipole, Sista. Sairis Mkinga.
Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen, Mbazi Msuya akiwa katika picha aya pamoja na Viongozi , watumishi na wananchi wanao hudumiwa na Kituo cha Afya Chipole wilayani songea vijijini tarehe, 12 Januari, 2016, baada ya kukagua ukarabati wa kituo hicho , kilichoungua mwaka 2013 na Ofisi hiyo kukikarabati.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Na. Mwandishi Maalum. 
SERIKALI kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu maafa imeahidi kukamilisha ukarabati wa Kituo cha Afya cha Chipole Songea Vijijini kilichopata majanga ya moto baada ya kituo hicho kuungua mwaka 2013 na Ofisi hiyo kutoa fedha za kukikarabati. 

Akiongea wakati wa ziara ya kukagua ukarabati wa kituo hicho, tarehe 12 Januari, 2016, Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali Mbazi Msuya amebainisha kuwa kufuatia kuungua kwa hospitali hiyo Ofisi ya Waziri Mkuu ilitoa kiasi cha shilingi milioni 35 kwa ajili ya ukarabati wa kituo hicho. 

“Tumekagua ukarabati wa kituo hiki cha afya na tumeona pamoja na kuambiwa na uongozi wa hospitali hii kuwa pamoja na fedha tulizozitoa lakini bado kuna mahitaji ya msingi yanahitajika ili hospitali hii iweze kuwahudumia wanakijiji wanao izungunka hospitali hii. Tunaahidi kukamilisha ujenzi wa chumba cha kuhifadhi maiti pamoja na maabara” alisema Msuya. 

Awali akitoa maelezo ya maendeleo ya ukarabati wa kituo hicho cha afya , Makamu wa Mama Mkubwa wa Chipole, Sairis Mkinga, alifafanua kuwa pamoja na mapungufu ya chumba cha maabara lakini bado kituo hicho cha afya kinao upungufu wa vyumba vya kuhudumia wagonjwa. 

“Tunayo changamoto bado ya kuwa na sehemu maalum ya Mapokezi ya wagonjwa na wagonjwa kupokea dawa. Pia panahitajika mahali kwa akina mama wajawazito kujifungulia kwani kwa sasa vyumba hivi viko karibu sana na vyumba vya wanaume lakini tunahitaji chumba maalum kwa aijili ya kliniki ya watoto” alisisitiza Sista Mkinga. 


Kituo cha Afya cha Chipole kilichopo Kata ya Magagura wilayani Songea vijijini kinamilikiwa na Shirika la watawa wa Mtakatifu Agnesi Chipole na inahudumia takribani wakazi 7,434 wa kata hiyo, hivyo kukamilika kwa Hospitali hiyo kutawezesha kupunguza vifo vya mama na motto pamoja na uboresha hali za afya za wakazi hao.

Global yatoa mifuko 100 ya saruji ujenzi sekondari Kinondoni

$
0
0
4DC, Makonda (kulia) akipokea mfuko wa saruji kutoka wawakilishi wa Global, Elvan Stambuli (katikati) na David Mwaipaja (kushoto).
1Wanahabari wakichukua tukio katika hafla hiyo.
7Mifuko ya saruji ikiwa ndani ya gari la Global kabla ya makabidhiano.
6Elvan Stambuli (katikati) akionesha risiti ya makabidhiano hayo kutoka kwa Makonda (kulia), anayeshuhudia kushoto ni Ofisa Masoko wa Global, David Mwaipaja.5. Mkuu wa Wilaya, Makonda (kulia), akionekana kutumia nguvu kubeba saruji wakati wa makabidhiano hayo. 8Mwakilishi wa Osyter Bay Pharmacy, Kefa Kijo (kulia) akimkabidhi saruji Makonda.
2Mwakilishi wa Global, Mhariri Mwandamizi, Elvan Stambuli, akihojiwa na wanahabari mara baada ya makabidhiano hayo.
3.DC, Makonda (kulia) akipokea mfuko wa saruji kutoka wawakilishi wa Global, Elvan Stambuli na David Mwaipaja.

KAMPUNI ya Global Publishers Ltd inayozalisha magazeti ya Championi, Uwazi, Amani, Risasi, Ijumaa na Ijumaa Wikienda, mapema leo imechangia mifuko 100 ya saruji katika ujenzi wa shule za sekondari wilayani Kinondoni, Dar. Mifuko hiyo imekabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, na mwakilishi mwandamizi wa Global, Elvan Stambuli, katika ofisi yake iliyopo Magomeni jijini Dar es Salaam. 

“Nikiwa mwakilishi kutoka Global Publishers, ninakabidhi mifuko 100 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa sekondari kwa Wilaya ya Kinondoni kutokana na kuguswa na wito wa mkuu wa wilaya hii alioutoa kwa makampuni na taasisi mbalimbali kusaidia kuongeza shule saba za sekondari wilayani Kinondoni ili vijana waweze kupata elimu vizuri,’’ alisema Stambuli.  

 Wakati huohuo, naye mwakilishi kutoka kampuni ya Ubapa Limited, Wenceslaus Rwezahula, na mwakilishi wa Oyster Bay Pharmacy, Kefa Kijo, walitoa mifuko ya saruji kuchangia ujenzi huo. Hata hivyo mara baada ya makabidhiano hayo, Makonda aliishukuru Kampuni ya Global Publishers kwa kuchangia mifuko 100 akisema ni mfano wa kuigwa kwa makampuni mengine, huku akisisitiza kuwa bado taasisi na makampuni mengine yanayo fursa ya kuendelea kuchangia ujenzi huo.

PICHA/HABARI: DENIS MTIMA/GPL

MAADHIMISHO YA SIKU YA MAPINDUZI ZANZIBAR.

KILELE CHA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 52 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR.

$
0
0
 Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akisalimiana naRais Mstaafu wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo katika killele cha sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52,zilizofanyika katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja,ambapo mgeni rasmi  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
 Pichani kutoka kushoto Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi,Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein,Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange wakiwa katika kilele cha Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52 katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja zilizofanyika leo
 Baadhi ya Wananchi na Maafisa mbali mbali wa Serikali wakiwa katika sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52,zilizofanyika leo katika Uwanja wa Amaani Studium Mjini Unguja
  Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa akisalimiana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu wakati alipowasili katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja katika Kilele cha sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52,ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange katika kilele cha Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52 katika Uwanja wa Amaan Studium zilizofanyika leo.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akisalimiana na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein katika kilele cha Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52 katika Uwanja wa Amaan Studium zilizofanyika leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono wananchi walioshiriki katika kilele cha Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52 katika Uwanja wa Amaan Studium leo akiwa katika gari maalum.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiteremka katika gari maalum alilopanda wakati akiwasalimia wananchi katika kilele cha Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52 katika Uwanja wa Amaan Studium leo.
[Picha na Ikulu.]

MAJALIWA AENDA MHUMBILI KUMSALIMIA SUMAYE NA BALOZI KIBELLOH

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Waziri Mkuu, Mstaafu Frederick Sumaye  ambaye amelazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa matibabu Januari 12, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (wapili kushoto) wakizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye amnaye amelazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa Matibabu Januari 12, 2016. Kushoto ni Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Mama Esther Sumaye. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Balozi Hassan Kibelloh ambaye amelazwa katik hospitali ya taifa y Muhimbili kwa Matibabu Januari 12, 2016.

 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI UMMY MWALIMU AFANYA ZIARA KATIKA DAWATI LA JINSIA NA WATOTO LA MKOA WA RUVUMA

$
0
0
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu (Mb.)akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa Maendeleo ya Mtoto, mbele ya Ofisi za Dawati la Jinsia na Watoto la Mkoa wa Ruvuma.
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu (Mb.) leo ametembelea Dawati la Polisi la Jinsia na Watoto la  Mkoa wa Ruvuma, kwa lengo la kufuatilia hali ya Ulinzi na Ustawi wa Mtoto Mkoani humo.

Wakati wa ziara hiyo Mhe. Ummy Mwalimu aliwapongeza Wadau mbalimbali wa Maendeleo ya Mtoto Mkoani Ruvuma kwa Ushirikiano waliouonyesha hadi kufanikisha Ujenzi wa Kituo hicho. 

Alieleza kuwa kwa Mkoa wa Ruvuma Wizara yake kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo ya Mtoto, itahakikisha inashughulikia kwa haraka tatizo la Usafirishwaji wa watoto kwenda nchi za jirani kutumikishwa katika kazi mbalimbali.

Pia aliagiza Uongozi wa Mkoa kuongeza jitihada zaidi katika kukabilina na Vitendo vya Ukatili wanavyofanyiwa Wanawake, kwakuwa Mkoa huo ni miongoni mwa mikoa mitatu yenye wastani mkubwa wa vitendo vya vipigo kwa wanawake.

Filamu ya Wema ni akiba yakamilika

$
0
0
 Filamu ya Wema ni akiba yake mwanamama Jennifer Mgendi imekamilika.
Akiongea na blogu hii Jennifer amesema filamu hiyo ambayo imewashirikisha wasanii na watumishi mbalimbali ni stori inayomhusu kijana Mawazo anayepambana na changamoto nyingi akijaribu kulipa deni la fadhila kwa Eli alizotendewa ujanani na baba yake Eli.
Fuatana naye katika filamu hii ili kupata undani wa mkasa huu.

KATIBU MWENEZI CCM MKOA WA MWANZA ATOA MAAGIZO KWA WAWAKILISHI WA WANANCHI.

$
0
0
Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Mwanza Simon Mangellepa akiongea na Wanahabari katika ofisi za Chama hicho Mkoa wa Mwanza.

Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG
Chama cha Mapinduzi CCM Mkoani Mwanza, kimewataka viongozi mbalimbali Mkoani Mwanza, kuwatumikia vema wananchi waliochagua na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mwenezi wa Chama hicho Simon Mangellepa mbele ya wanahabari, wakati akitoa shukrani kwa makundi mbalimbali ya wananchi ambayo ni pamoja na machinga, wakulima, wavuvi pamoja na wafanyabiashara kwa namna walivyojitoka kwa hali na mali kukisaidia chama hicho kuibuka na ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana.


Mangellepa amesema kuwa uchaguzi umemalizika hivyo ni vema viongozi wote ambao ni pamoja na Mabalozi, Wenyeviti wa Serikali za Mtaa na Vijiji, Madiwani pamoja na Wabunge wakaacha kuwatumikia wananchi kwa mazoea na badala yake wawakilishe vizuri katika ngazi za maamuzi katika kutatua matatizo yao.


“Hii kauli ya Hapa Kazi Tu haishii kwa Magufuli peke yake (Rais John Pombe Magufuli), mimi nasema inaanzia hata kwa mabalozi, wenyeviti wa vitongoji, mitaa, madiwani na wabunge. Chama cha Mapinduzi Mkoa kinawataka Madiwani na Wabunge warudi kwa wananchi ili wanapokwenda kuwawakilisha wananchi wawakilishe mawazo sahihi ya wananchi wao”. Alisema Mangellepa.

Kauli ya Chama hicho imeungwa mkono na baadhi ya wananchi Jijini Mwanza ambao wamewakumbusha viongozi wao kuhakikisha kwamba wanatatua changamoto zinazowakabili ambazo ni pamoja na ukosefu wa ajira kwa vijana, ubovu wa miundombinu, kushughulikia kero ya upatikanaji wa maji safi na salama pamoja na huduma za afya katika ngazi za Kata ili kutimiza ahadi walizozitoa wakati wa kampeni zao.

Bonyeza PLAY Hapa Chini Kusikiliza

Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Mwanza Simon Mangellepa akiongea na Wanahabari katika ofisi za Chama hicho Mkoa wa Mwanza.
Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Mwanza Simon Mangellepa akiongea na Wanahabari katika ofisi za Chama hicho Mkoa wa Mwanza.
Wanahabari
Nikiripoti Kutoka Jijini Mwanza, Mimi ni George Binagi-GB Pazzo @BMG

Dua, maombi yake tumaini kwa wenye maradhi

$
0
0

 UMAARUFU wa Sheikh Chief Msopa maarufu kwa jina la Sharif Majini kwa sasa unazidi kushika kasi nchini Tanzania na nchi za Afrika Mashariki kwa ujumla. Sharif Majini ameamua kutumia Kituo cha Dua kilichopo Mabibo Mwisho Dar es Salaam, kwa ajili ya kufanya dua na maombi kwa kusaidia wenye shida mbalimbali. 

Kwa sehemu kubwa dua na maombi yake yamekuwa msaada mkubwa kwa wenye matatizo mbalimbali. Dua hizo kwa sehemu kubwa zinasaidia kwa wenye matatizo mbalimbali ya kiafya. Hivyo, wengi wanaofika kwenye kituo hicho ni kwa ajili ya kutatua shida hizo. 

Sharif Majini anatumia dua kwa ajili ya kusaidia wale ambao wana matatizo ya kupooza viungo vyote muhimu na kuwa na maumivu kama kuumwa kichwa.Pia kwa kutumia dua zake na maombi kwa ajili ya kusaidia wenye tatizo la mimba kuharibika mara kwa mara. Waliokosa kasi na wanaoandamwa na mikosi kwenye maeneo wanayoishi na wale wenye tatizo la kupata hedhi muda mrefu. 

Pamoja na hayo Sharif Majini kwa kutambua kuwa kuna umuhimu wa dua na maombi yake kusaidia watu wengi ameamua kuifanya siku ya Jumapili kuwa siku ya kufanya dua na maombi maalumu kwa wale ambao wanakosa nafasi ya kwenda kutokana na majukumu mengine yakiwamo ya ujenzi wa taifa.Hivyo, Sharif Majini kwa sehemu kubwa kupitia dua zake amefanikiwa kusaidia wananchi wengi hasa wa Dar es Salaam na mikoani ambao wamekuwa wakisumbuliwa na maradhi. Mbali ya wale wanaofika kwenye vituo hivyo, Sharif Majini amekuwa akitumia karama hiyo aliyopewa na Mungu kuitumia kwa ajili ya kuliombea Taifa lake liendelee kuwa na amani na utulivu ili maisha ya ujenzi wa nchi yaendelee. 

Mbali ya kufanya maombi kwa viongozi wa ngazi mbalimbali kwa kutenga siku maalumu kwa ajili ya kuwaombea kwa Mungu, pia Sharif Majini amekuwa akifanya dua na maombi kwa ajili ya viongozi wa nchi nyingine nyingi za Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla na hiyo inatokana na mialiko ambayo amekuwa akiipata. Siku za karibuni licha ya kufanya mambo kwa ajili ya wananchi wanaofika kwa wingi kwenye kituo kipya cha dua, aliamua kutumia uwezo wake ambao amejaliwa na Mungu kufanya dua maalumu ya kumuombea Rais, Dk. John Magufuli. Dua hiyo kwa sehemu kubwa ililenga kumuomba Mungu ampe nguvu na afya njema Rais ili kutimiza majukumu yake. Pia kumuomba Mungu kumuepusha na mabaya hasa kipindi hicho ambacho ameamua kupambana na ufisadi na kutumbua majipu

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

CHUO CHA KODI CHAIMARIKA KWA UMAHIRI WA MAFUNZO YA FORODHA NA KODI KIMATAIFA

$
0
0
Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Forodha na Kodi, Prof. Isaya Jairo akizungumza na wandishi wa habari (hawapo picha) jijini Dar es Salaam juu ya Mahafali ya nane yatakayofanyika katika Ukumbi wa Julius Nyerere tarehe 16 Januari mwaka huu, Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango. Kutoka kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Usimamizi wa Forodha na Kodi, Dkt. Lewis Ishemoi na  Bw. CharlesSabuni, Naibu mkuu wa Chuo (Mipango,Fedha na Utawala).
 Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini. Picha na Cathbert Kajuna. --- Na Chalila Kibuda, Globu ya jamii. CHUO cha Kodi kimeweza kupata hadhi kuwa kituo cha Umahiri wa Mafunzo ya Forodha na Kodi kimataifa. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa Chuo cha Kodi, Profesa Issaya Jairo amesema wakati wakielekea katika mahafali ya nane chuo kimeweza kufikia hadhi hiyo. 


Na Chalila Kibuda, Globu ya jamii.

CHUO cha Kodi kimeweza kupata  hadhi  kuwa kituo  cha Umahiri wa Mafunzo ya Forodha na Kodi kimataifa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa Chuo cha Kodi, Profesa Issaya Jairo amesema wakati wakielekea katika mahafali ya nane chuo kimeweza kufikia hadhi hiyo.

Amesema kuwa kwenda katika mahafali ya nane chuo kimeanzisha  ya shahada ya pili katika masuala ya kodi kufanya kutambulika kimataifa.

Wahitimu watakaotunukiwa vyeti, shahada na stashahada siku ya Jumamosi wamegawanyika katika kozi zifuatazo:-

1)    Cheti cha Uwakala wa Forodha Cha Afrika Mashariki yaani East African Customs Clearing and Freight Forwarding Practicing Certificate (CFFPC); wahitimu 125

2)    Cheti cha Usimamizi wa Forodha na Kodi yaani Basic Technician Certificate in Customs and Tax Management (CCTM); wahitimu 190

3)    Stashahada ya Usimamizi wa Forodha na Kodi yaani Ordinary Diploma in Customs and Tax Management (DCTM; wahitimu 131.

4)    Shahada ya kwanza ya usimamizi wa Forodha na Kodi yaani Bachelor of Customs and Tax Management (BCTM); wahitimu 68.

5)    Stashahada ya Uzamili katika Kodi yaani Postgraduate Diploma in Taxation; wahitimu 23.

Kati ya wahitimu 564, wahitimu 199 ni wanawake na wanaume ni 338. Wahitimu wa Mahafali haya watafanya idadi ya wahitimu wa Chuo cha Kodi tangu kiliposajiliwa mwaka 2007 kufikia ya 3541.

Pamoja na kutunuku vyeti, shahada na stashahada kwa wahitimu, Mgeni Rasmi pia atatoa tuzo kwa wahadhiri wa Chuo cha Kodi waliofanya tafiti mbalimbali  katika kipindi cha mwaka wa masomo wa 2014/2015. Tafiti hizi zimechapishwa katika majarida mbali mbali ya kitaaluma, ikiwa ni pamoja na Journal of the Institute of Tax Administration (JITA) linalochapishwa na Chuo cha Kodi (ITA).

Wahitimu waliofanya vizuri zaidi pamoja na wanafunzi wanaoendelea na masomo waliofanya vizuri zaidi nao pia watapata tuzo kutoka kwa wadau mbali mbali ili kuleta hamasa ya kujifunza kwa bidii zaidi miongoni mwa wanafunzi wanaoendelea na masomo.

Kwa sasa chuo kipo katika mwaka wa tatu wa utekelezaji wa Mpango – Mkakati wake wa tatu wa miaka mitano (SP3) kuanzia Julai 2013 hadi Juni 2018 ambapo  kinaendelea kubuni kozi mbalimbali na kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunza ili kukidhi mahitaji na matarajio ya Mamlaka ya Mapato Tanzania na wadau wengine.

Katika mahafali haya chuo kinatoa wahitimu wa awamu ya tatu wa shahada ya Usimamizi wa Forodha na Kodi (Bachelor of Customs and Tax Management-BCTM),  ambayo ni ya kipekee hapa nchini  na katika ukanda huu wa Afrika.

Mgeni rasmi anayetarajiwa katika mahafali ya nne ya chuo cha kodi yatakayofanyika Januri 16  ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango.
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live




Latest Images