Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live

TIMU YA WATAALAM KUTOKA WIZARA TATU ZATEMBELEA VYANZO VYA MAJI YA MABWAWA YA KUZALISHA UMEME

0
0
Baadhi ya wajumbe wa Timu ya kutoka Wizara ya Nishati na Madini,Wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi ,Wizara ya maji, na umwagiliaji , Shirika l Umeme Tanzania (Tanesco )pamoja na Watalamu wa bonde la mto Rufiji wakipata maelezo ya namna ambavyo umeme wa maji huzalishwa katika kituo cha Kihansi .

Timu ya wataalam  kutoka Wizara ya Nishati na Madini,Wizara ya kilimo, mifugo na Uvuvi ,Wizara ya maji, na Umwagiliaji , Shirika l Umeme Tanzania (Tanesco ) pamoja na Watalamu wa bonde la mto Rufiji waliotembelea  vyanzo vya maji vinavyotiririsha  maji katika mito inayomwaga maji  mabwawa ya kuzalisha umeme wa maji ikiwemo  Mtera, Kihansi na Kidatu ili kuunganisha nguvu ya pamoja na kurejesha vyanzo hivyo katika hali yake ya awali kutokana na kuathiriwa na shughuli za kibinadamu na hivyo kusababisha kukauka na upungufu wa maji katika mabwawa ya kuzalisha umeme wa maji ilivyokuwa katika miaka ya nyuma.
 Muonekano wa Bwawa la Kihansi kwa sasa ambalo pia limepunguza uzalishaji wa umeme wa maji kutokana na kupungua kwa kina cha maji.
 Timu ya wataalamu  kutoka Wizara ya Nishati na Madini,Wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi ,Wizara ya maji, na umwagiliaji , Shirika l Umeme Tanzania (Tanesco )pamoja na Watalamu wa bonde la mto Rufiji waliotembelea  vyanzo vya maji vinavyotiririsha  maji katika Mabwawa ya kuzalisha umeme .
 Eneo lenye  chanzo cha cha maji pamoja na mto  mbalo hutumiwa kwa shughuli za kibinadamu na kusababisha upotevu wa maji yanayoingia katika mto unaomwaga maji katika mabwawa ya kuzalisha umeme wa maji
 Moja ya sehemu ya mashine ama mtambo inayotumika kuzalisha umeme wa maji katika vituo vya Kihansi, Kitadu na Mtera.
 Mashine inayotumika kuondoa  taka  kama vile magogo na nyingine zanamna hiyo katika mabwawa ya kuzalisha umeme wa maji.


WAZIRI MKUU KUANZA ZIARA MKOANI RUVUMA

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa   anatarajia kuanza ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Ruvuma, ambapo atawasili mkoani  hapo  leo saa tisa alasiri.

Baada ya Waziri Mkuu kuwasili Uwanja wa Ndege wa Songea, atapokelewa na viongozi wa Chama na Serikali, pia atakwenda Ikulu kupokea taarifa ya maendeleo ya mkoa wa Ruvuma.

Aidha, siku ya jumatatu  atakuwa na shughuli za kufungua  tawi la Benki ya Posta mjini Songea, kukagua  maghala ya Wakala wa Taifa wa  Hifadhi ya chakula  (NFRA) kanda ya Songea na kukagua  makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea.

Siku inafuata atatembelea na kukagua Hospitali ya Rufaa ya mkoa, na baadaye kuzungumza na watumishi wa hospitali  hiyo.

Siku ya nne ya ziara yaani jumatano, Waziri Mkuu atafanya majumuisho ya ziara mkoani humo, kabla ya kuagana na viongozi wa Chama na Serikali na kurejea Dar es Salaam.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMAPILI, JANUARI 3, 2016.

UCHAMBUZI WA MAGAZETI YA LEO

0
0



AZAM TV: Arsenal yapaa, Man united yashinda, Azam na Simba vitani Zanzibar, Liverpool chali, Chacharito ang’ara, Niyonzima atoa ya moyoni. Tazama uchambuzi wa magazeti ya leo. https://youtu.be/7l4a3gY8ngM  

TBC: Kingunge ampa siku 100 Magufuli, Wananchi wavamia shamba la Sumaye, Basi lenye abiria 42 latumbukia mtoni, Mwigulu acharuka; Pata dondoo za magazeti ya leo. https://youtu.be/0gFnivfZUfc  

STAR TV: Mchungaji Rwakatare aivimbia serikali, Wingu zito lazidi kutanda Zanzibar, Panga la Magufuli lawanyemelea Mabalozi. Furahia uchambuzi wa magazeti. https://youtu.be/CviaHbXdM_o

CH10: Lowassa amemponza, Ubadhilifu wa kutisha mnadani, Mawaziri wakuu wamjadili Magufuli, Bomoa bomoa yahamia kwa Vigogo. Tazama habari zilizopewa uzito wa juu magazetini. https://youtu.be/ADpPuEdXzeA

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI SONGEA

0
0
e92a2ca8-1b8e-49f8-a0bc-fa4646427e30
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary   (kushoto kwake )  wakielekea kwenye Chumba cha mapumziko baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Songea na kupokelewa na wanachi na viongozi wa mkoa huo Januari 3, 2016.  Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma , Thabiti Mwambungu na kushoto ni Mbunge wa Songea Leonidas Gama. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

JUMUIYA YA KUKUSANYA ZAKA NA SADAKA ZANZIBAR (JUZASA) YAFANYA MKUTANO MKUU WAKE.

0
0
UD1
Mwenyekiti wa Jumuiya ya kukusanya Zaka na Sadaka Zanzibar (JUZASA) Shekh. Said Masoud (Gwiji) akitoa maelezo ya Jumuiya na kumkaribisha mgeni rasmi (kushoto) Katibu Mtendaji Kamisheni ya Wakfu na Mali ya amana Zanzibar Shekh. Abdalla Talib kufungua Mkutano wa Jumuiya hiyo uliofanyika katika ukumbi Sha-Ntimba Mombasa Zanzibar.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanziba
UD2
Baadhi ya wanachama wa Jumuiya na wageni walikwa wakisikiliza nasaha za Mwenyekiti wa Jumuiya ya kukusanya Zaka na Sadaka Zanzibar (JUZASA) Shekh. Said Masoud (Gwiji) hayupo pichani wakati wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya hiyo.
UD3
Mjumbe wa Bodi ya Jumuiya hiyo Dkt. Muh’d Hafidh akitoa neno la shukrani mara baada ya kumaliza kwa Mkutano. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.  
………………………………………….
Na Maelezo Zanzibar.

Taasisi za kiislamu nchini zimeshauriwa kushawishi kuwepo kwa mfumo wa pamoja wa ukusanyaji wa Zaka na Sadaka ili ziweze kuleta tija katika kundi kubwa la jamii ya Kislam.

Katibu mtendaji wa kamisheni ya mufti namali ya amana Zanzibar sheikh abdalla talib amesema Lengo la mfumo huo uliwekwa kwa mujibu wa sheria za kiislamu ni kusadia na kupunguza umasikini katika jamii lakini kwa sasa wengi wanaotaoa sadka hizo hazifikii lengo hilo kwa vile kumekosekana mfumo bora  unaowafikia watu wengi na kuleta mabadiliko makubwa.

Akifungua mkutano wa jumuiya ya zaka na sadaka Zanzibar ZASA ametolea mfano wan chi ya denmar amabyo ina waislamu kwa asilimi 3 tu imekuw ana utaratibu mzuri wa ukusanyaji wa sadka na zaka  hali iliyofanikisha kupatikana  misaada mingi iliyosaidia  katika nchi hiyo na hata nchi nyengine.

Amefahamisha kuwa  kwa kuwa  Zanzibar asilimia kubwa ya wanananchi wake ni waislamu ina nafasi ya kufikia malengo hayo kama pia itatoa elimu kwa wananchi hasa wenye uwezo  ili kufahamu  umuhimu wa Ibada hiyo pamoja na njia bora za kutoa zaka na sadaka katika jamii.
Nae mwenyekii wa jumuiy hiyo sheikh said masoud  amesema kwa sasa umekuwa na mwamko mdogo hasa kwa wafanyabiashara kutoa zaka na sadaka  kulingana na taratibu zinazotakiwa  kidini.

Nae katibu wa jumuiya hiyo ya jusaza omar abubakar Mohamed amesema jumuiya hiyo  imeshatoa zaka kwa watu 46 zikiwemo za fedha taslim, charahani, friza na wengine kujengewa nyumba. 

CHEKA KUPANDA ULINGONI FEB, 23 DAR ES SALAAM

0
0
Promota Juma Msangi kushoto akiwa na Rais wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO Yassin Abdallah ‘Ustadhi’ pamoja na Meneja msaidizi wa bondia  Fransic Cheka  wakitambulisha mpambano wa bondia Cheka mbele ya waandishi wa habari mpambano utakaofanyika Feb 27 katika uwanja wa Leaders Club .
 
 Promota Juma Msangi kushoto akiwa na Rais wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO Yassin Abdallah ‘Ustaadhi’ pamoja na Meneja msaidizi wa bondia  Fransic Cheka  wakitambulisha mpambano wa bondia huyo mbele ya waandishi wa habari mpambano huo utakaofanyika Feb 27 katika uwanja wa Leaders Club Picha naSUPER D BOXING NEWS

Hivi ndivyo Mawaziri watatu wa Rais Dkt JOHN MAGUFULI walivyotumbua Majipu Machinjio VINGUNGUTI

0
0

KIWANGO CHA UFAULU DARASA LA 7 CHAPANDA WILAYANI MUFINDI

0
0
Zaidi ya wanafunzi 5,100 wa shule za msingi Wilayani Mufindi Mkoani Iringa, wanatarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza baada ya kufaulu mtihani wa darasa la 07 ulifanyika mapema mwaka jana, huku ufaulu huo ukipanda na kufikia asilimia 80.39 ukilinganisha na asilimia 68.21 ya mwaka 2014.

 Taarifa ya kitengo cha habari na mawasiliano cha halmashauri ya wilaya ya mufindi kwa nyombo vya habari, imetanabaisha kuwa, wanafunzi waliokuwa wamesajiliwa   kufanya mtihani walikuwa 7,220 na miongoni mwao waliofaulu na kuchaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari ni 5,198.

Taarifa hiyo imeainisha mgawavyo wa wanafunzi hao kwa kuzingatia jinsi, ambapo kati ya waliofaulu, wasichana wameongoza kwa takwimu za ufaulu huo wakiwa elfu 2,831 wakifuatiwa na wavulana 2,367. Aidha, wanafunzi wote waliofaulu wamepangiwa shule ili kuendelea na elimu ya sekondari itakayokuwa ikitolewa bure hapa nchini.

Wilaya ya Mufindi yenye jumla ya shule za msingi 178 imeshika nafasi ya pili Mkoani Iringa kwa kufaulisha wanafunzi wengi kwaasilimia 80.39 ikitanguliwa na Manispaa ya Iringa iliyofaulisha kwaasilimia 80.55 ikiwa na jumla ya shule za msingi 50.

Mikoa yaanza kugombania Tamasha la Pasaka 2016

0
0

WANANCHI wa mikoa mbalimbali wamejitokeza kuiomba kkampuni ya Msama Promotions ianzie Tamasha la Pasaka mikoa kwao mwaka huu huku wakazi wa dare s salaam wakisisitiza libaki mkoani humo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama ameliambia Gazeti hili kuwa, tayari amepokea maombi toka kwa wananchi na mashabiki wa mikoa ya Morogoro, Mwanza, Mbeya, Dodoma na Dar es Salaam wakitaka tamasha hilo lianzie kwao mwaka huu.

“Kamati yangu  inafuata taratibu za Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambazo ni pamoja na kupata kibali cha kufanikisha kufanyika kwa Tamasha hilo linaloshirikisha waimbaji mbalimbali wa muziki wa Injili  wa ndani na nje ya Tanzania,” amesema Msama.

Salum Ismail Hamad ambaye ni mdau mkubwa wa Tamasha la Pasaka amesema anawaomba waandaaaji wa Tamasha hilo kutoliondoa jijini Dar es Salaam kwa sababu ni mkoa unaohusisha idadi kubwa ya mashabiki wa muziki wa Injili.

Rukia Joseph wa Kimara Dar es Salaam, alisema yeye anawapigia magoti waandaaji  kutoliondoa tamasha hilo jijini  Dar es Salaam hasaa kwa waimbaji wa nje ya Tanzania kama Solly Mahlangu na wengineo toka nje ya nchi.

Michael Deogratius alisema  ni ngependa Tamasha la Pasaka lihamie mikoani  kwa sababu ya ukubwa na umuhimu wa tamasha hilo ambalo linatimiza miaka 16 tangu kuasisiwa kwake.Msama alisema bado wanasubiri taratibu za kufanikisha tamasha hilo  kutoka Basata, hivyo nawaomba wakazi wa mikoani kuvuta subira wakati wakijiandaa.

1st East Africa Congress of Accountants in Arusha – Tanzania

0
0


Challenges for the East African Community”.
The 1stEast Africa Congress of Accountants (EACOA) will be held at  AICC Arusha – Tanzania from 2th to 4thMarch 2016.

The objective of the conference is to create a forum for professional accountants in the region to interact, seek opportunities and to discuss issues impacting the accounting profession in the region.

The conference is jointly organised by the Accounting Bodies in the Region: OPC Burundi; Institute of Certified Accountants Kenya (ICPAK); Institute of Certified Accountants of Rwanda (ICPAR); National Board of Accountants and Auditors –Tanzania (NBAA); Institute of Certified Accountants of Uganda (ICPAU).NBAA is the host of the conference.Members of the accountancy profession, academicians and all interested persons are invited to attend this important professional conference.

Registration and Conference Fee
Early registration start on 7th December,  2015 to 29th January 2016 conference fee is Tsh. 800,000 or USD 400.  Late registration is from 1st– 29th February 2016 conference fee  Tsh. 950,000 or USD 450.  The fee include 1 day trip to Ngoro Ngoro Crater.

Register online through eacoa.nbaa-tz.org or download the form through www.nbaa-tz.org scan and send toeacoaregistration@nbaa-tz.org

 FOR MORE INFORMATION CLICK HERE www.nbaa-tz.org

INTRODUCTION OF DIPLOMA IN INTERNATIONAL PUBLIC SESCTOR ACCOUNTING STANDARDS FROM 1ST FEBRUARY 2016.

0
0
PUBLIC NOTICE

(NBAA)
THE NATIONAL BOARD OF ACCOUNTANTS AND AUDITORS
TANZANIA
INTRODUCTION OF DIPLOMA IN INTERNATIONAL PUBLIC SESCTOR ACCOUNTING STANDARDS FROM 1ST FEBRUARY 2016.

Introduction 

Due to growing demand in public sector entities to prepare and present high quality transparent financial statements, the National Board of Accountants and Auditors has introduced Diploma in International Public Sector Accounting Standards to be known as “Diploma in IPSAs” which will start on 1st of February, 2016

The introduction of Diploma in IPSAS is in accordance with the mandate granted to the Board under Section 4 of the Accountants and Auditors (Registration) Act [Cap. 286 Revised in 2002], where the Board has been mandated to conduct examinations and grant diplomas, certificates and other awards in accountancy, auditing and allied subjects.

Course Objective
The Course principal objective is to provide an in-depth understanding of the practical application of the International Public Sector Accounting Standards. At the end of the course, the Board shall award Diploma in IPSAS for those who will be successful.
Targeted learners
Diploma in IPSAS will benefit anyone who requires an understanding and application of international accounting standards in the public sector. In particular, it is suitable for: 

· Accountants and finance staff at all levels who are involved in the preparation of financial statements 
· Trainers wishing to acquire advanced knowledge of the standards 
· IPSAS’s implementation and sustainability teams 
· Both internal and external auditors and consultants dealing with financial reporting 
· Officers responsible for public sector financial reporting and auditing
Entry Qualifications: Holders of Certified Public Accountant (CPA) Certificate or its equivalent or Holders of Postgraduate Studies in Accounting, Finance, Tax or related subject.

Venue: will be at NBAA Campus

Training hours per week: The time for classes will be from 5.00 PM to 7.00 PM
Duration of the Course: Duration of the course will be six months and examinations will be held in two sessions in a year that is February and August. Two hour classes will be held for three days per week on Monday, Wednesday and Friday. To begin with, classes and examinations centre will be in Dar Es Salaam only.

Fees and Registration: Application for admission in the February 2016 intake has commenced since 16th November, 2015 and deadline will be on 15th January, 2016.

Registration form can be downloaded from NBAA website (www.nbaa-tz.org) or collected at Mhasibu House Room No. 208. 

Total cost for the programme is Tshs.1,500,000/- which includes registration, tuition and examination fees.


For more Information contact:

EXECUTIVE DIRECTOR
NBAA MHASIBU HOUSE
BIBI TITI MOHAMED STREET
P.O. BOX 5128,
DAR ES SALAAM
TEL: 255 22 2211890 -9
FAX: 2151746 E-mail: info@nbaa-tz.org

Ikulu Yaagiza Mtumishi Atakayefanya Kosa Aadhibiwe Hapohapo Alipo Badala Ya Kuhamishiwa Sehemu Nyingine ya Kazi

0
0
 
MAKATIBU Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu walioteuliwa na kuapishwa juzi wamekutana katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya semina elekezi iliyoongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.

Akizungumza kabla ya kuanza kwa mada zilizoandaliwa katika semina hiyo  jana, Katibu Mkuu Kiongozi Sefue, alisema semina hiyo ni ya kikazi zaidi na kwamba lengo la serikali ni kuhakikisha viongozi hao waandamizi wanatekeleza wajibu wa kusimamia utendaji kazi wa serikali vizuri.

Balozi Sefue alisema kila Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu anapaswa kutambua kuwa nafasi yake ni ya maamuzi, hivyo serikali inatarajia kuona wanafanya maamuzi kwa usahihi na kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zinazomuongoza kila mmoja katika majukumu yake.

Alisema Serikali ya Awamu ya Tano inawatarajia viongozi hao kuwa wasimamizi wazuri wa fedha za umma na kwamba haitarajii kuwepo kwa hati za ukaguzi wa mahesabu zenye kasoro.

Balozi Sefue aliongeza kuwa Makatibu Wakuu hao na Naibu Makatibu Wakuu ni mamlaka ya nidhamu katika wizara zao, hivyo serikali haitarajii kuona wanakuwa na kigugumizi katika kuchukua hatua dhidi ya watumishi watakaokuwa na makosa.

Aliwakumbusha pia kwamba haikubaliki kwa mtumishi aliyefanya makosa katika sehemu moja ya kazi, kuhamishiwa katika sehemu nyingine badala ya kuchukuliwa hatua palepale alipo.

SERIKALI KUNYANG’ANYA VITALU VYA MADINI VILIVYOHODHIWA.

0
0
Mmiliki wa kiwanda cha uongezaji thamani madini ya jasi kilichopo mkoani Singida, Emmanuel Shilla akimuonesha Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (wa kwanza kushoto) moja ya bidhaa za urembo wa ndani ya nyumba unaotengenezwa kutokana na madini ya jasi yanayopatikana mkoani Singida.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (wa kwanza kushoto) akitazama jinsi madini ya jasi yanavyotumika kutengeneza vitu mbalimbali ikiwemo urembo wa ndani ya nyumba mara baada ya kutembelea kiwanda cha uongezaji thamani madini ya jasi cha Singida Cornice.Aliyevaa shati jeupe ni mmiliki wa kiwanda, Emmanuel Shilla.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) akiangalia jinsi mtambo wa bayogesi ulivyomwezesha mmiliki wa mtambo huo, Habiba Sengasu (kulia) kupata faida mbalimbali ikiwemo nishati ya kupikia. Naibu Waziri aliutembelea mtambo huo akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya Nishati na Madini mkoani Singida.
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa kituo cha kupoozea umeme kilichopo mkoani Singida ambacho kinatarajiwa kuanza kazi mwezi Juni mwaka huu. Ujenzi wa kituo hicho ni sehemu ya utekelezaji mradi wa ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji umeme wa kilovolti 400 kutoka Iringa hadi Shinyanga unaotarajiwa kukamilika mwezi Aprili mwaka huu. Kituo kinajengwa na kampuni ya GSE&C na Hyosung kutoka Korea.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (kulia) akizungumza na wachimbaji wa madini ya jasi mkoani Singida wakati alipofika wilayani Manyoni mkoani Singida ili kukagua shughuli za uchimbaji wa madini hayo na kuzungumza na wachimbaji wadogo.Wa kwanza kushoto ni Yusuph Kibira na katikati ni Ismail Ivata
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (wa pili kushoto) akiangalia moja ya mitambo ya bayogesi inayomilikiwa na Habiba Sengasu (wa kwanza kushoto) mkoani Singida. Naibu Waziri aliutembelea mtambo huo akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya Nishati na Madini mkoani Singida.

Na Teresia Mhagama, Singida 
Serikali imesema kuwa itanyang’anya vitalu vya madini visivyoendelezwa na kuwapatia wachimbaji wadogo nchini ili waviendeleze. 

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani wakati akizungumza na Mkuu wa wilaya ya Manyoni Fatma Toufiq kabla ya kukagua miradi ya uchimbaji madini pamoja miradi ya umeme wilayani humo.

“Tutachukua maeneo yasiyoendelezwa na kuwagawia wachimbaji wadogo kama sheria ya madini ya mwaka 2010 inavyoelekeza hivyo Kamismhna Msaidizi wa Madini Kanda hii ya kati hakikisha hilo linatekelezwa,’’ alisema Dkt. Kalemani.

Naibu Waziri alitoa agizo hilo baada ya Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Fatma Toufiq kumueleza changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wachimbaji wadogo katika wilaya hiyo ikiwemo utumiaji wa zana duni za uchimbaji madini pamoja na ukosefu wa maeneo ya uchimbaji madini kutokana na watu wengi kuhodhi maeneo hayo kwa muda mrefu bila kuyafanyia kazi.

Aidha, Mkuu wa wilaya alimueleza Naibu Waziri kuwa licha ya changamoto za wachimbaji wadogo, wilaya hiyo pia inakabiliwa na changamoto ya umeme kukatika mara kwa mara jambo ambalo linaathiri shughuli za kiuchumi za wananchi katika wilaya hiyo.

Akifafanua suala hilo Naibu Waziri alimueleza kuwa umeme katika wilaya hiyo na mikoa ya Iringa, Singida, Dodoma na Kanda ya Ziwa utatengemaa mara baada ya ujenzi wa njia kuu ya umeme wa msongo wa kilovolti 400 kutoka Iringa hadi Shinyanga kukamilika mwezi Juni mwaka huu kwani mitambo hiyo itasafirisha umeme kwa kiwango kikubwa tofauti na miundombinu ya sasa ambayo inasafirisha umeme kwa msongo kilovolti 220.

Hata hivyo Naibu Waziri aliwataka watendaji wa Tanesco katika wilaya hiyo kuhakikisha kwamba umeme haukatiki kwa sababu ya uzembe wa kibinadamu kufanya au kutokufanya kitu fulani bali utokane na majanga ya kiasili ambayo hayazuiliki.

“ Watendaji wa Tanesco nileteeni taarifa kwa nini umeme unakatika mara kwa mara katika wilaya hii na kama ni uzembe wa mtu basi naye akatike hapohapo,” alisisitiza Dkt. Kalemani.

Wakati huohuo Naibu Waziri ameitaka kampuni ya spencon iliyopewa tenda ya kusambaza umeme katika vijiji 90 mkoani Singida kukamilisha kazi hiyo ifikapo mwezi Mei mwaka huu.

Naibu Waziri alitoa agizo hilo baada ya kampuni hiyo kusuasua katika kusambaza umeme vijiini kwani kazi ya kusambaza umeme katika vijiji hivyo ilipaswa kukamilika mwezi wa 11 mwaka jana lakini hadi sasa wamesambaza umeme katika vijiji 17 tu.


“Mradi huu unahusisha kilomita 188 lakini mpaka sasa nguzo zimefikia kilomita 48 tu, asipokamilisha kazi hii kwa muda huu tuliompa tutataifisha mali zake, na watendaji wa Tanesco mniletee taarifa ya kina sababu za mradi huu kuchelewa na hatua mlizochukua,” alisema Dkt. Kalemani.

MGODI WA DHAHABU WA BULYANHULU WAIPIGA JEKI ZAHANATI YA MWINGIRO GEITA

0
0

Maafisa wa kitengo cha Mahusiano ya Jamii katikamgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu, William Chungu (kulia) na Zuwena Senkondo (kushoto) wakikabidhi vifaa vinavyotumika wakati wakujifungulia kwa zahanati ya Mwingiro Wilayani Nyang’wale Mkoani Geita .

Zuwena Senkondo wkikabidhi vifaa vya kujifungulia kwa mmoja wa wauguzi katika zahanati ya Mwingiro Wilayani Nyang’wale Mkoani Geita

Kiongozi wa kitengo cha Mahusiano ya Jamii Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu Sara Ezra Teri akikabidhi Video Camera ya kisas kwa Mwenyekiti wa kikundi cha Vijana Thoams Mshilu kwa ajili ya kurekodia tamthiliya zao. 

Na Dixon Busagaga wa Globu ya jamii Kanda ya Kaskazini,aliyekuwa mkoani Geita.

Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu umekabidhi seti nane za vifaa vya kutolea huduma kwa akina mama wajawazito wanapojifungua, katika halmashauri ya wilaya ya Nyang’wale Mkoani Geita vyenye thamani ya shilingi Milioni Tatu.

Akipokea vifaa hivyo Mratibu wa Huduma ya Baba, Mama na Mtoto wa Halmashauri ya Nyang’wale Mkoani Geita Bi Neema Mhoja amesema, “Tunaushukuru Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu kwa kutupatia vifaa hivi muhimu kwa ajili ya kuokoa maisha ya mama na mtoto kwani awali upungufu wa vifaa hivyo umesababisha Wauguzi Wakunga katika zahanati wilayani humo kutoa huduma katika mazingira magumu.”

Naye Meneja wa Mahusiano ya Jamii wa Mgodi wa Bulyanhulu Bwana Elias Kasitila amesema, afya za akina mama ni nguzo ya msingi wa maendeleo katika jamii hivyo Mgodi kwa kutumia utaratibu wa kusikiliza kero za wananchi mwaka huu ulipata maombi ya vifaa hivyo kutoka kwa wananchi wa vijiji vya Iyenze na Mwasabuka katika kata ya Mwingiro wilaya ya Nyang’wale mkoani Geita na umeitikia ombi kwa kukabidhi vifaa hivyo kwa mratibu wa huduma za akina mama na watoto wa wilaya ya Nyang’wale.

Wauguzi katika zahanati ya kata Mwingiro wamekabidhiwa vifaa hivyo ili waweze kuvitumia na kuvitunza kwa ajili ya matumizi kwenye zahanati hiyo inayohudumia wakazi wapatao 12,000 wa kata ya Mwingiro.

Muuguzi Mkunga wa zahanati ya Mwingiro bwa Costantine Matata Bahebe, na Pendo Ntabudyo, na Elizabeth Lameck amesema, “ Sasa itakuwa rah asana ukipata mzazi maana vifaa vinatosha kwani kwa mwezi tunazalisha akina mama kati ya 20 na 25 hivyo kwa vifaa hivi tufanya kazi katika mazingira ya usafi, usalama na utulivu hata pale tutakapopata wazazi nane kwani kila mmoja atakuwa na kifaa chake kuliko kumsubirisha mzazi wakati unapochemsha vifaa baada ya kuvitumia.

Naye Afisa Mahusiano ya Jamii wa Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu Zuwena Senkondo amewaasa wakunga katika zahanati ya Mwingiro kutumia na kuvitunza vifaa hiyo vyenye thamani ya shilingi Milioni Tatu.

WIZARA TATU ZASHAURIWA KUSHIRIKIANA KUMALIZA TATIZO LA KUKAUKA NA KUPUNGU KWA MAJI MABWAWA YA KUZALISHA UMEME NCHINI

0
0
Picha za mitambo ya kuzalisha umeme na  wadau wa maji waliotembelea maeneo ya mito na kugundua baadhi ya njia za asili za  mito inayomwaga maji yake kwenye mabwawa ya kuzalisha umeme imezibwa.  kitendo hicho kinadaiwa kuathiri utiririshaji wa maji katika mabwawa ya kuzalisha umeme.

 pia wadau hao wameshauri taasisi zote ikiwemo wizara ya nishati na madini,wizara ya kilimo , mifugo na uvuvi, wizara ya maji na umwagiliaji pamoja na bonde la mto Rufiji  zinazotumia rasilimali maji katika shughuli zake kushirikiana ili kumaliza tatizo la kukauka na kupungua kwa maji katika mabwawa ya kuzalisha umeme.
 Cable wire za Umeme zikipitishwa katika moja ya njia zililizopo chini ya  mwamba wa mlima( tannel) ambapo ndipo zilizopo mashine za kuzalisha umeme wa maji na shughuli zote za uzalishaji.
 Mashine  za kuzalisha umeme wa maji katika vituo vya Kihansi, kidato na Mtera  vinanyonekana ambapo shughuli zote za uzalisha wa umeme wa maji na mashine hizo ziko chini ya mwamba wa mlima uliotombelea . 
 Sehemu iliyochepushwa maji kitaalamu kutoka katika moja ya mito inayomwaga maji kwenye mabwawa ya kuzalisha umeme wa maji ili maji hayo  yatumike kwa kilimo cha umwagiliaji.
 Sehemu iliyochepushwa maji kitaalamu kutoka katika moja ya mito inayomwaga maji kwenye mabwawa ya kuzalisha umeme wa maji ili maji hayo  yatumike kwa kilimo cha umwagiliaji.
Wataalam kutoka Wizara ya Nishati  na Madini , Wizara ya kilimo ,uvuvi na mifugo, Wizara ya maji na umwagiliaji pamoja na watalaam kutoka bonde la mto Rufiji wakipita eneo ambalo kumejengwa tuta ili kuzua njia ya asili ya moja ya mito inayomwaga maji katika mabwawa ya kuzalisha umeme wa maji kwa nia ya kupisha ujenzi wa mfereji wa maji yatakayotumika katika kilimo cha umwagiliaji, jambo ambalo  limedaiwa kuwa huathiri mazingira na utiririshaji wa maji katika mabwawa.

NEWZ ALERT;AJALI YA BASI LA LUWINZO NA LORI

0
0
Chumba cha habari cha GLOBU ya Jamii kimepata taarifa kuwa Basi la abiria  la kampuni ya Luwinzo (ambalo namba zake za usajili hazijafahimika mapema),lifanyalo safari zake Dar-Njombe inaelezwa kuwa limepata ajali asubuhi hii likitokea Njombe kuelekea Dar kwa kuligonga Lori (ambalo nalo namba zake za usajili hazikufahamika mapema), kwa taarifa za awali ambazo bado hazithibitishwa na jeshi la Polisi zinaeleza kuwa kuna vifo vya watu kadhaa,ambayo idadi yake haijajulikana mpaka sasa sambamba na majeruhi.

TUTAZIDI KUPEANA TAARIFA ZAIDI KADIRI YA ZITAKAVYOKUWA ZIKIPATIKANA.
 Baadhi ya Abiri na Wasamalia wema wakisaidia kuwaokoa baadhi ya abria waliokuwa wamenasa ndani ya basi hilo.
 Baadhi ya abiria wakiwa kwenye masikitiko makubwa.
 Kazi ya kuokoa baadhi ya abiria ikiendelea  
Namna basi hilo lilivyogonga Lori kwa nyuma.

WAZIRI MKUU AFURAHISHWA NA HALI YA CHAKULA MKOANI RUVUMA

0
0


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefurahishwa na hali ya chakula mkoani Ruvuma, ikiwa kati ya mikoa inayotegemewa kwa uzalishaji wa chakula kwa wingi nchini.

Akizungumza na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali jana jioni (Jumapili, Januari 3, 2016) katika ukumbi uliopo Ikulu ndogo Songea, Waziri Mkuu  ameutaka  uongozi wa mkoa kuhakikisha kuna  upatikanaji wa masoko kwa mazao mbalimbali pamoja na kuendelea kutoa msukumo kwa wananchi.

Pia, ameupongeza uongozi  wa mkoa huo kwa kutoa msukumo kwa wananchi na kufanyakazi, na kusema ni jambo linalosaidia kupanda kwa pato la mtu mmoja  mmoja, hata hivyo hakusita kuwashukuru kwa mapokezi makubwa aliyopata.

“Nawapongeza sana wana Ruvuma kwa kuongeza pato la ndani kutoka kutoka shilingi 654,227, hadi kufikia shilingi 1,800,000 kwa kipindi cha mika 4 tuendelee kujiweka vizuri kwa kuongeza pato la mtu mmoja mmoja” alisema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu Majaliwa pia amesisitiza  kilimo cha umwagiliaji katika maeneo yote yenye mabonde ili wakulima waweze kuvuna bila kutegemea sana kipindi cha masika. Amesema ni lazima kuimarisha huduma muhimu na kusisitiza matumizi mazuri ya fedha zinazopatikana katika mazao hayo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Thabit Mwambungu amesema  zaidi ya asilimia 90 ya wananchi wa Ruvuma hutegemea kilimo cha mazao  mbalimbali ya chakula na biashara  yakiwemo mahindi, mpunga ambao unalimwa sehemu za Tunduru na Songea vijijini, korosho  ambazo zinalimwa sehemu za Tunduru, Namtumbo, Nyasa, Mbinga na Songea vijijinina tumbaku  maeneo ya Namtumbo,Mbinga na Songea vijijini.

Alisema, Ruvuma imekua ikizalisha chakula kwa kiwango cha utoshelezi na ziada kwa kipindi cha mwaka 2012 - 2013, 2013 - 2014 hali hiyo imeendelea kuwa nzuri hadi kipindi cha mwaka 2015 - 2016. Mahitaji yakiwa ni tani 469,172 na ziada ikiwa tani 1,950,111, ametaja baadhi ya sababu za ongezeko hilo la tani  ni pamoja na matumizi ya dhana  bora za kilimo, matumizi ya pembejeo za kisasa na urahisi wa upatikanaji wa pembejeo, aliongeza Mkuu wa Mkoa.

Waziri Mkuu Majaliwa ambaye jana (Jumapili, Januari 3, 2016) ameanza ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Ruvuma, kesho  siku ya jumatatu  atakuwa na shughuli za kufungua  tawi la Benki ya Posta mjini Songea, kukagua  maghala ya Wakala wa Taifa wa  Hifadhi ya chakula  (NFRA) kanda ya Songea na kukagua  Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea.

 Kupitia ziara hii Serikali ina lengo la kuona hali halisi ya utendaji wa shughuli za maendeleo kutoka kwa watendaji mbalimbali, kuwatia moyo na kuweka msisitizo  katika maeneo yaliyopewa kipaumbele hasa katika sekta ya Afya.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMATATU, JANUARI 4, 2016.

SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LAPOKEA TUZO YA KIMATAIFA BAADA YA KUJIUNGA NA MPANGO WA KUPATA FEDHA.

0
0

MAKATABA wenya thamani ya dola za kimarekani milioni $700m uliosainiwa na washirika wa ndege ya Etihad kwa ajili ya upanuzi wa shirika hilo umetambuliwa na shirika lenye sifa duniani katika nyanja ya masuala ya kifedha na uchumi la “International Financing Review (IFR)” na hivyo kuitunuku shirika la ndege la Etihad na tuzo maalum. 

Mkataba huo wa miaka mitano ulitambulika kama dhamana kubwa kabisa ya mwaka iliyosainiwa kutoka barana ulaya, mashariki ya kati na Afrika, katika hafla iliyofanyika jijini London Januari 27

Mwezi Septemba , shirika la ndege la ndege la Etihad lilianza safari ya maonyesho, likiongozwa na mshauri mkuu, Goldman Sachs, katika bidi za kuongeza thamani ya hisa za Shirika hilo, kampuni yake tanzu ya huduma za viwanja vya ndege ya Etihad na washirika wengina wake watano wa huduma za angani – airberlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia na Jet Airways – wote wakiwa ndani ya shirika la ndege la Etihad.

Kupitia michango ya washirika wa ndege ya Etihad BV, kikundi kilifanikiwa kupata dola za kimarekani milioni 500, kiasi hicho kiliongezeka kwa kiasi cha dola za kimarekani milioni 200 ndani ya siku chache tu kufuatia kuongezeka kwa shauku kutoka jamii ya fedha ya kimataifa.

Ikiwa kama mkataba wakifedha wa kipekee katika sekta ya masuala ya anga, hii ni mara ya pili ndani ya wiki chache kwa shirika hili la ndege kutambulika na kupata tuzo kupitia mkataba wake huo. Washirika wa ndege la Etihad walipokea tuzo ya mkataba wa kifedha wa mwaka kutoka mashariki ya kati, katika hafla iliyofanyoka jijini London kupitia Makala ya Global Transport Finance ya nchini UK.

James Hogan, Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika la Ndege la Etihad, alisema: “Uvumbuzi ndio msingi wa uendeshaji wa biashara zetu katika shirika hili. Tuzo hii kutoka “International Financing Review” inaonyesha dhahiri ni jinsi gani taasisi za kifedha zina uamini juu ya mafanikio yetu pamoja na mifumo yetu ya kibiashara katika kuunganisha biashara zetu zite tulizo wekeza” 

Akiongezea Bw Hogan, alisema: “Katika sekta ya biashara yenye ushindani mkubwa, siri ni kukuza uzalishaji pamoja na kuongeza ufanisi ili kukuza biashara. Kwa upande wa wahirika, kila mmoja wao ni kujikuza kibiashara. Ila kwa pamoja, nguvu inajumuishwa kwa pamoja. Mfumo huu wa uelewano ndio unatambua na kuidhinisha nguvu ya shirika zima. 

“Ningependa kumshukuru na kumpongeza afisa wetu mkuu wa masuala ya kifedha, Bw James Rigney, na timu yake nzima kwa juhudi zao za hali ya juu katika kuunda mfumo thabiti uliokuwa kivuto katika masoko ya ndani na nje ya nchi. Walifanya kazi kwa bidii sana kuleta shauku kubwa juu ya mifumo yetu ya kibiashara na tunayo furaha kuona bidi zao zikizaa matunda na kupata tuzo hizi, hasahasa wakati huu ambapo masoko mengi duniani yamejaa mashaka na wasiswasi juu ya kuwekeza fedha kutokana na changamoto za kiuchumi duniani”. 

Mkurugenzi mtendaji wa Goldman Sachs, Bw. Martin Weber, alisema: “ Tunafuraha kubwa kufanya kazi pamoja na washirika wa ndege ya Etihad katika kuwapatia dhamana hii kubwa na tunapongeza timu iliyohusika katika ushindi wa tuzo ya IFR. Mafanikio haya yanatokana na uongozi wa shirika la ndege la Etihad kukutana na wawekezaji mbalimbali dunia nzima, na hivyo kufanikisha kukamilisha mkataba huu. Hii pia ni ishara ya jinsi gani mfumo wao wa kibiashara ua nguvu ya kufurahisha masoko hata katika kipindi hichi kigumu cha masoko ya dunia” 

Safari za kuchangia fedha zilifanyyika Abu Dhabi, Dubai na London zikiwa zinasimamiwa na washauri wakuu Goldman Sachs, kampuni kutoka Abu Dhabi ya ADS Securities na Anoa Capital. Fedha zilizopatikana ziligawanywa katika Nyanja saba tofauti, ikiwa mchanganyiko wa matumizi ya mtaji na uwekezaji katika ndege, pamoja na kujazia fedha kulingana na mahitaji ya vitengo mbalimbali vya shirika hili la ndege ya Etihad. 

International Financing Review ndio chombo kinachoongoza duniani katika kutoa uchambuzi wa kina juu ya masoko, ikitoa ushauri na uchambuzi wa kina juu ya uwekezaji wa masuala ya kibenki kwa kauu wa benki duniani, pia hutoa habari juu ya masoko ya kibiashara kupitia Makala zake za kila wiki ma ripoti zao za kila siku mtandaoni

Uongozi wa shirika la ndege la Etihad ulisifiwa na IFR kwa kukamilisha na kufanikisha uchangishaji fedha, huku wakijenga uaminifu na kuungwa mkono na wawekezaji. 


Tukio hilo kubwa kabisa katika kalenda ya wawekezaji masoko wa dunia kila mwaka, litavutia wawekezaji wakubwa na wenye mafanikio zaidi ya 1,000 mwezi ujao jijini London ili kusherekea tuzo za IFA za kila mwaka.

TIMU YA KILUVYA UNITED YAITUNGUA AFRICAN LYON KWA MABAO 2-1 LIGI DARAJA LA KWANZA

0
0
NA VICTOR MASANGU.
KIVUMBI cha ligi daraja la kwanza (FDL) kwa msimu wa mwaka 2015-2016 kinazidi kushika kasi ambapo timu ya Kiluvya United (Wabishi wa Pwani) jana iliweza kuifunga timu ya African Lyon kwa mabao 2-1 katika mchezo uliopingwa katika uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo wa Kundi 'A' ulikuwa na upinzani wa hali ya juu kutokana na kila timu kucheza kufa na kupona kwa lengo la kuweza kuibuka na ushindi na kujinyakulia pointi tatau muhimu ili iweze kujiwekea mazingira mazuri ya katika msimamo wa ligi hiyo ya daraja la kwanza ambayo imeonekana kuwa upinzani wa hali ya juu kwa timu zote hususan katika kundi 'A'.

Kipindi cha kwanza katika dakika za mwanzoni wachezaji wa pande zote mbili walionekana kuanza mchezo huo kwa kasi kwa kuanza kushambuliana kwa zamu ambapo timu ya Kiluvya united iliweza kuandika bao la kwanza kunako katika dakika ya 23 lililowekwa kimiani na mshambuliaji Kassim Kilungo.

Kuingia kwa bao hilo kulionekana kuwachanganya wachezaji wa Africa Lyon na kuonekana wamebaki wameduwaha huku mashabiki wa kiluvya united waliokwenda uwanjani hapo wakiendelea kushangilia kwa staili ya aina yake ambayo iliweza kuwafurahisha wadau na wapenzi wa soka waliofika kushuudia mpambano huo.

Dakika ya 32 ya kipindi cha kwanza timu ya African Lyon nayo iliweza kufanya shambulizi la kushitukiza ambalo liliweza kuzaa matunda kwa kuandika bao la kusawazisha lililofungwa na mchezaji Kasakala Ndela baada ya safu ya ulinzi ya Kiluvya united kujichanganya katika eneo la hatari.

Kikosi cha wachezaji wa kiluvya kiliweza kujipanga upya na kuyarekebisha madhambi yaliyotendeka na kuanza kuliskama lango la wapinzani wao na kufanikiwa kuandika bao la pili katika dakika ya 44 lililofungwa na mchezaji Ayoub Lipat baada ya kuunganisha mpira safi kwa njia ya kichwa.

Hadi kipinga cha kipindi cha kwanza kinapulizwa timu ya Kiluvya United ilikwenda mapumziko ikiwa iko mbele ya mabao 2-1 dhidi ya wapinzani wao timu ya African Lyon ya Jijini Dar es Salaam, ambapo kipindi milango ya timu zote mbili ilikuwa migumu na kufanya hadi dakika 90 za mchezo huo zinamalizika Kiluvya kutoka kifua mbele kwa ushidi huo.


Kwa matokeo hayo Kiuvya United Wabishi wa Pwani kwa sasa wanashika nafasi ya pili wakiwa na pointi 16 huku nafasi ya kwanza ikikamatwa na timu ya Ashanti United ya Jijini Dar es Salaam yenyewe ikiwa na pointi 18.

WAFANYAKAZI 350 WA KIWANDA CHA SUKARI CHA MAHONDA WAKOHATARINI KUPOTEZA AJIRA ZAO.

0
0
 Baadhi ya Miwa iliyoteketea kwa moto kutokana na hujuma iliyofanywa na Watu wasiojuilikana huko kwenye mashamba ya Miwa ya Kiwanda cha Sukari Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimpa Pole Meneja wa Mradi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda Bwana Tushar Mehta kufuatia watu wasiojuilikana kutia tena moto mashamba ya Miwa Mahonda.
  Balozi Seif kati kati akifuatana na Uongozi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda akikagua baadhi ya sehemu ya shamba la Miwa la Eka 50 lililotiwa moto jana jioni na watu wasiojuilikana.Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Meja Mstaafu Juma Kassim Tindwa.

 Meneja wa Mradi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda Bwana Tushar Mehta akimueleza Balozi Seif hasara iliyopatikana kutokana na hujuma ya moto kwenye mashamba ya Miwa Mahonda.
Balozi Seif akielezea masikitiko yake kutokana na baadhi ya watu kufanya hujuma za makusudi kujaribu kuvuruga juhudi za Uongozi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda za kuimarisha Sekta ya Viwanda.


TISHIO la ajira za Wafanyakazi 350 wa Kiwanda cha Sukari Mahonda zinaendelea kuwa hatarini kufuatia hujuma zinazofanywa kwa makusudi na baadhi ya watu kuendelea kutia moto mashamba ya miwa huko Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Kitendo hicho cha hujuma kinaweza kuusababisha Uongozi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda kuwa na mawazo ya kufikiria kuzuia ajira mpya 450 za Wafanyakazi wa Kiwanda hicho katika malengo yake baada ya kukamilika kwa matengenezo makubwa na kuanza tena uzalishaji wa sukari.

Meneja wa Mradi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda Bwana Tushar Mehta alisema hayo wakati akimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyefika kuangalia hasara iliyosababishwa na moto uliotiwa kwa mara nyengine tena na Watu wasiojuilikana ndani ya shamba la Miwa katika kipindi cha siku Tano baada ya tukio kama hilo la Tarehe 30 mwezi uliopita.

Bwana Tushar alisema moto huo umetiwa kati kati ya shamba la Miwa jana jioni na wahalifu wenye dhamira ya makusudi ya kutoa usumbufu na kizuizi kwa wananchi na vikosi vya Ulinzi katika harakati za kukabiliana na moto huo. .

Alisema Eka zipatazo 50 za Miwa iliyopevuka imeteketea kwa moto hali ambayo imeisababishia Kiwanda hicho hasara ya Tani 200 za Sukari na Lita 2,300 za Spititi zilizokuwa zizalishwe kutokana na miwa hiyo ikiwa na hasara ya jumla ya dola za Kimarekani Laki 228,758.56 sawa na zaidi ya shilingi Milioni 494 za Kitanzania.

Meneja huyo wa Mradi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda alifahamisha kwamba hadi sasa Eka zipatazo 200 zimeteketea kwa moto kwenye matukio yote mawili katika kipindi cha siku Tano zilizopita na kusababisha hasara ya jumla ya Dola za Kimarekani Milioni 1,176,234.28 sawa na shilingi za Kitanzania Bilioni 2,326,818,500/-.

Akiupa pole Uongozi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda kutokana na hasara ya Mashamba iliyosababishwa na moto huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema hujuma hiyo ya makusudi haiitakii neema Zanzibar katika harakati zake za kustawisha uchumi wake.

Balozi Seif aliwanasihi watu wenye tabia hiyo kuachana nayo kwani mbali ya kujibebesha dhambi lakini pia inawavunja moyo wawekezaji walioamua kuja kuwekeza miradi yao ya kiuchumi Nchini kwa lengo la kuisaidia Serikali pamoja na Wananachi hapa Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alifahamisha kwamba juhudi za makusudi za Serikali kuu katika kukifufua tena Kiwanda cha Sukari na Manukato Mahonda baada ya kusita kwa miaka kadhaa zililenga kuimarisha  Uchumi kupitia sekta ya viwanda sambamba na kupanua soko la ajira kwa Vijana.

Alisema tabia ya baadhi ya watu kufikiria kwamba hujuma hiyo itatoa fursa kwao kutumia maeneo ya mashamba ya Miwa kuendeleza Kilimo na Mifugo inafaa kuachwa mara moja kwa vile mashamba hayo yataendelea kuwa katika mipango ya Serikali ya kuhudumia Sekta ya Viwanda.

“ Haya ni Mashamba ya Serikali yaliyotengwa maalum kwa shughuli za harakati za Viwanda. Hivyo ndoto za baadhi ya Watu kufikiria kwamba hujuma zao zitazaa matunda kwa kufanya wanavyotaka zinapaswa ziachwe mara moja ”. Alisema Balozi Seif.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliufahaisha Uongozi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda kwamba Serikali Kuu inaangalia mpango utakaowezesha Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kusaidia ulinzi kwenye Mashamba hayo ili kulinda hujuma zinazoonekana kushamiri siku hadi siku.

Hilo ni tukio la sita la hujuma za moto kwenye mashamba ya Miwa ya Kiwanda cha Sukari Mahonda tokea kianze tena uzalishaji wa sukari na Spiriti mapema mwaka uliopita wa 2015.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
4/1/2016.
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live




Latest Images