Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 725 | 726 | (Page 727) | 728 | 729 | .... | 1896 | newer

  0 0

  Wazee waishio kata ya Kimandolu wilaya ya Arusha mkoani Arusha wamemuomba Rais John Pombe Magufuli awakumbuke wazee kwa kuhakikisha kuwa wanapata huduma bora za afya ,lishe bora na kupata mafao ya uzeeni kutokana na mchango wao katika ujenzi wa taifa kupitia sekta binafsi na za serikali tangu nchi ipate uhuru.

  Wazee hao ambao wanaishi katika hali ngumu za kimaisha na wengine kutokua na uhakika wa milo mitatu huku wakikabiliwa na jukumu la kulea familia zao pamoja na wajukuu licha ya uzee unaowakabili pamoja na kutokua na kipato cha uhakika na wengine kutokua na nguvu ya kufanya kazi.

  Amon Mwita ni mzee anayeishi kata ya Kimandolu alisema kuwa licha ya mchango wao katika uchumi wa nchi na maendeleo ya taifa tangu kipindi cha uhuru wamekua ni watu wa kusahaulika jambo ambalo linawafanya waiishi maisha ya shida.

  Mwita alisema kuwa kwa muda mrefu wamekua wakipigwa danadana juu ya kupatiwa matibabu bure hali ambayo imesababisha afya za wazee wengi kuzoroto kwani wengine hukosa fedha za matibabu na kujikuta wakipoteza maisha kwa kukosa matibabu.

  Navoneiwa Maeda ni mzee ameitaka Serikali iwathamini wazee kwani ni kundi linaloishi katika mazingira magumu na bado halijapewa kipaumbele na serikali jambo ambalo linawaumiza hivyo ameiomba serikali na jamii ichukue jukumu la kuwalea wazee na kuwatunza.

  Mwenyekiti wa Baraza la wazee mtaa wa kimandolu Emmanuel Mollel asema kuwa wazee wengi wamekua wakijificha majumbani ingali wagonjwa bila kupata matibabu na wengine kutopata mlo wa siku kutokana na hali ngumu za kiuchumi walizonazo hivyo ameiomba jamii ijitokeze kuwasaidia wazee.

  Mkurugenzi wa Jamii Media Group Pamela Mollel na Mdau wa wazee Amedeus Moshi waliofika kuwatembelea wazee hao na kutoa msaada wa kibinadamu wameitaka jamii itambue wajibu wake wa kuwalinda na kuwatunza wazee pamoja na kukemea mauaji ya vikongwe suala linalochafua taswira ya taifa na kuathiri ustawi wa wazee nchini.


  0 0

  WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye leo anazindua filamu ya Homecoming katika Ukumbi wa Century Cinema uliopo Mlimani City.
  Mwongozaji wa filamu hiyo, Seko Shamte.
  Mwigizaji Mkuu wa Filamu hiyo Daniel Kijo
  WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye leo anazindua filamu ya Homecoming katika Ukumbi wa Century Cinema uliopo Mlimani City.

  Uzinduzi huo pia utaoneshwa moja kwa moja na king’amuzi cha Azam kupitia Channel yake ya Sinema Zetu.

  Akizungumza kuhusiana na filamu hiyo mwogozaji wake Seko Shamte alisema kuwa filamu hiyo inahusiana na masuala ya rushwa na  imekuja wakati mwafaka ambapo jami imezinduka na kupambana na janga hilo.

  Alisema kuwa kwa sasa ni uzinduzi tu na kisha itaanza kuoneshwa kwa kulipia katika kumbi za Cinema kuanzia Januari 29 mwakani.

  Alisema kuwa wapenzi wa filamu wanaweza kufuatilia uzinduzi huo katika chanel ya Sinema Zetu ya King’amuzi cha Azam na kuongeza kuwa ni filamu ambayo inasisimua kuangalia.

  “ Hii filamu imeidhinishwa na bodi ya Filamu nchini na kupewa alama nzuri tu zinazoiwezesha kuoneshwa kwenye kumbi za sinema na hata kutumiwa na shule kama sehemu ya somo,” alisema Seko.

  Kwa upande wake Ofisa Uhusiano wa Azam Media, Maryam Elhaj alisema kuwa King'amuzi cha Azam kupitia Chanel yake ya Sinema Zetu kimeamua kuonesha uzinduzi huo live ili kuwapa fursa wapenzi wa filamu kuburudika zaidi.

  "Najua king'amuzi cha Azam ni king'amuzi ambacho kimenuia kuwaendeleza wasanii na sanaa kwa ujumla sasa kama filamu nzuri kama hii ya Homecoming yenye viwango vya kimataifa imetuvutia na kuamua kuipa support ya kuionesha moja kwa moja uzinduzi wake na wapenzi wa filamu nao wanapata wasaa wa kuona shamrashamra ya uzinduzi wake," alisema Maryam.

  Kwa upande wake mwigizaji mkuu wa filamu hiyo Daniel Kijo alisema kuwa ana imani kuwa nafasi yake ya uhusika kama kijana alieathiriwa na rushwa inatoa fundisho kwa vijana wengine wengi.

  Filamu hiyo imehusisha waigizaji wengi wakubwa wa ndani na nje na kuandaliwa na kampuni ya Alkamest Media ambayo inahusika na utayarishaji wa filamu na vipindi vya runinga.

  Wengine katika filamu hiyo ni Susan Lewis maarufu kama Natasha, Uncle Mshindi, maarufu kama Hashim Kambi pamoja na Abby Plaatjes aliyewahi kuwa mshiriki wa Big Brother Afrika.

  Pia wapo akina Isa Mbura, Magdalena Munisi, Godliver Gordian na  Michael Kauffmann na itaanza kuoneshwa kwenye kumbi za sinema kabla ya kuingia rasmi sokoni. Zaidi tembelea www.homecomingtz.com

  0 0  0 0

  Na Raymond Mushumbusi MAELEZO.

  Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) inaendelea na ujenzi wa Barabara itokayo Kamanga Ferry kuelekea Sengerema kwa kiwango cha lami ili kurahisisha  usafiri na usafirishaji katika eneo hilo.

  Hayo yamesemwa leo na Meneja wa TANROADS Mkoa wa  Mwanza Mhandisi Leonard Kadashi alipokuwa akizungumza na Mwandishi wa Habari ofisi kwake kutolea ufafanuzi suala la Barabara ya Kamanga Ferry mpaka Sengerema ambayo haipo katika hali nzuri na kusema mkandarasi yupo na ujenzi huo unaendelea.

  Pia amekanusha suala la kuwa Barabara hiyo imekuwa ikitumiwa na wanasiasa katika kampeni na kusema kuwa Barabara hiyo ipo katika mipango ya TANROADS na mkandarasi yupo katika ujenzi wake kwa kiwango cha  lami
  .
  “Barabara hii ya Kamanga Ferry tunaijua, tunaifanyia kazi na ipo katika matengenezo ila  ni mvua ndio zilikwamisha kwa muda ujenzi huu ila mkandarasi yupo katika ujenzi.” Alisema Mhandisi Kadashi.

  Mbali na Barabara ya toka Kamanga Ferry mpaka Sengerema kujengwa katika kiwango cha lami pia TANROADS inazishughulikia Barabara za Kamanga mpaka Katunguru,Katunguru mpaka Sengerema na Bukoba mpaka Nyehunge.

  Katika kurahisisha usafiri na usafirishaji nchini, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania  (TANROADS)  imefanikisha ujenzi wa Barabara nyingi nchini kwa kiwango cha lami na changarawe ambazo zimekuwa ni viungo vya nchi yetu na nchi jirani,Mikoa, Wilaya, Kata, Tarafa na vijiji katika kufanikisha usafiri na usafirishaji hasa katika sekta za kibiashara, na utalii pia kurahisisha mawasiliano hivyo kuleta maendeleo kwa wananchi na nchi kiujumla.

  0 0

  Mkurugenzi wa Huduma za mifungo Tanzania katika wizara ya Kilimo, mifugo na Uvuvi, Dkt. Abdu Hayghaimo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kusikitishwa kwao kama wizara kutokana na wanyama kuadhibiwa bila hatia yoyote kwenye migogoro kati ya wakulima na wafugaji hapa nchini. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano wa wizara ya kilimo, mifugo na Uvuvi, Judith Mliwa.
  Daktari wa Mifugo wa kurugenzi ya huduma za mifugo wizara ya kilimo, mifugo na Uvuvi, Dkt. Christine Bukuname akifafanua jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya waandishi wakiwasikiliza maafisa wa wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi jijini Dar es Salaam leo.
  Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.


  WIZARA ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, imekemea tabia ya kuadhibu wanyama kwenye maeneo ya migogoro baina ya wakulima na wafugaji.

  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Huduma za mifungo Tanzania katika wizara ya Kilimo, mifugo na Uvuvi, Dkt. Abdu Hayghaimo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

  Hayghaimo amesema kuwa wananchi wenye  tabia ya kuwadhuru wanyama waiache mara moja kwa kuwa wanyama hao wanaongozwa na binadamu kwenye maeneo yasiyowahusu wanayama. 

  Amesema kuwa kwa mujibu wa sheria ya ustawi wa wanyama wanahaki ya chakula, maji, mahali pazuri pakupumzika, kulindwa dhidi ya maumivu yeyote, magonjwa  na mateso ikiwa pamoja na kuwasaabishia kifo.

  Pia wizara imewatahadharisha wananchi wote wanaochukua sheria  mkononi na kusababisha madhara makubwa  yasiyokubalika kutokana na migogoro ya migogoro ya wakulima na wafugaji kuwa huwanyima wanyama haki zao ni uvunjifu wa amani.

  Jamii imeshauriwa kuwa itafute suruhu ya migogoro hiyo kupitia kamati zitakazo matumizi endelevuya ardhi kwa mujibu wa walaka unaoandaliwa na wizara.

  0 0

  Waziri wa Uchukuzi, Ujenzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa.
   Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
  BAADA ya  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  kufanya ziara  katika Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA) na kubaini uondoshwaji wa wa kontena 329  ambazo ziliondoshwa bila kulipa kodi zaidi ya sh.bilioni 12, baada ya ziara hiyo Mawakala wa Forodha walifanya ukaguzi  kuona kama kuna upotevu wa mapato  na kubaini jumla ya kontena 11,884 na magari 2019 yalitolewa bila malipo.


  Makontena hayoo yalitolewa katika bandari kavu ni MOFED 61,DICD 491, JEFAG 1, 450, AZAM 295, PMM  779, AMI 4384, TRH 4,424 ambazo kodi yake ni zaidi ya sh.bilioni 47.


  Magari 2019 yalitolewa bila kulipa kodi katika kampuni za  TALL 309, CHICASA 65, FARION 18, SLVER 97, MASS 171, HESU 1359 kodi yenye thamani zaidi y Tsh.bilioni moja (1) .


  Akizungumza na wafanyakazi wa Bandari leo Waziri wa Uchukuzi, Ujenzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa wataendelea kuchukua hatua kwa wale wote watakaohusika kukwepa kodi.


  Amesema kuwa wataendelea kuchukua hatua dhidi ya wale ambao wamehusika wakiwemo watumishi wanaoshiriki katika hujuma, Wafanyakazi saba wa TPA wanashikiriwa na polisi kuhusiana na upotevu wa kontena hizo na kusababisha serikali kukosa mapato.

  Wanashikiriwa na jeshi la polisi ambao wengine wamekamatwa leo ni John Elisante, Leticia Masaro, Christina Temu, Merina Chawala, Adnan Ally ,Masoud Seleman, Benadeta Sangawe.


  Wanaotafutwa kwa tuhuma za kusababisha upotevu wa kodi za serikali katika bandari ya Dar es Salaam ni Happygod Naftal, Nathan Edward, Aron Lusingu, Amani Kazumari, John Mushi, Valentine Sangawe, Benasweet Kamaina, Zainab Bwijo.

  0 0

  Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Hamad Masauni wa pili kushoto akipokelewa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Mbarak Abdulwakil wa watatu kulia mara baada ya Naibu waziri huyo kupokea Ua alilokabidhiwa na watumishi wa wizara hiyo ikiwa ni ishara ya kukaribishwa wizarani hapo baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli kumuapisha kushika wadhifa huo Ikulu jana jijini Dar es Salaam.
  Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Hamad Masauni wa kwanza kushoto akisalimiana na Kamisha wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja wa pili kulia muda mfupi baada ya Naibu waziri huyo kukaribishwa wizarani hapo baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli kumuapisha kushika wadhifa huo Ikulu jana jijini Dar es Salaam wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
  Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Hamad Masauni wa pili kushoto akisalimiana na Kamisha wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Magereza Gaston Sanga wa pili kulia muda mfupi baada ya Naibu waziri huyo kukaribishwa wizarani hapo mara tu baada ya kuapishwa Ikulu jana jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Lilian Mapfa watatu kulia akimkaribisha Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Hamad Masauni wa pili kushoto muda mfupi baada ya Naibu waziri huyo kukaribishwa wizarani hapo mara tu baada ya kuapishwa Ikulu jana jijini Dar es Salaam wa pili kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Huduma kwa Jamii.
  Sehemu ya watumishi wa wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kushoto wakimpokea Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Hamad Masauni wa tatu kulia muda mfupi baada ya Naibu waziri huyo kukaribishwa wizarani hapo mara tu baada ya kuapishwa Ikulu jana jijini Dar es Salaam.
  Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Hamad Masauni akisaini kitabu baada ya kupokelewa katika wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi muda mfupi baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. John Magufuli Ikulu jana jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi hiyo Mbarak Abdulwakil wa kwanza kulia akimfafanulia jambo Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Hamad Masauni baada ya Naibu waziri huyo kupokelewa na watumishi wa wizara hiyo mara tu baada ya kuapishwa Ikulu jana jijini Dar es Salaam.
  Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Hamad Masauni akisalimiana na baadhi ya Wakurugenzi na Wakurugenzi Wasaidizi wa wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumuapishwa jana kushika nafasi hiyo katika hafla iliyofanyika Ikulu jana jijini Dar es Salaam.

  0 0

   Mshambuliaji wa timu ya Mafunzo akijiandaa kupiga mpira huku beki wa timu ya KMKM akiwa tayari kumzuiya wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar timu hizo zimetoka sare ya bao 1--1.
   Beki wa Timu ya Mafunzo akiondoa mpira golini kwao, 
   Mshambuliajhi wa Timu ya KMKM na Beki wa Timu ya Mafunzo wakiwania mpira.
  Kipa wa timu ya Mafunzo akiokoa mpira ikiwa moja ya shgambulio golini kwake.
  Mshamuliaji wa Timu ya KMKM akimiliki mpira huku beki wa Timu ya Mafunzo akijiandaa kumzuiya wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zabnzibar uliofanyika uwanja wa amaan timu hizo zimetoka sare ya bao 1--1
  Beki wa timu ya Mafunzo akiondoa mpira golinin kwao, huku mshambuliaji wa timu ya KMKM akiwa tayari kuleta madhara. 
  Mshambuliaji wa Timu ya KMKM akipiga mpira golini kwa timu ya Mafunzo. 
  Kocha wa Timu ya Mafunzo Hemedi Moroko akitowa maelekezo kwa wachezaji wake wakati wa mchezo wao na  Timu ya KMKM uliofanyika uwanja wa Amaan Timu hizo zimetoka sare ya bao 
  1--1
  Mchezaji wa Timu ya Mafunzo na KMKM wakiwania mpira.
  Kipa wa Timu ya KMKM akidaka mpira wakati wa mchezo wao na timu ya Mafunzo uliofanyika uwanja wa Amaan timu hizo zimetoka sare ya bao 1--1
  Mshambuliaji wa timu ya Mafunzo akijiandaa kumpita beki wa timu ya KMKM wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika uwanja wa Amaan Timu hizo zimetoka 
  sare ya bao 1--1
  Mchezaji wa Timu ya KMKM na Mafunzo wakiwania mpira.

  Kocha Mkuu wa Timu ya KMKM Ali Bushiri (Bush) akiwakaripia wachezaji wake wakati wa mchezo wa ligi kuu ya Zanzibar uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar timu hizo zimetoka sare ya bao 1--1.
  Beki wa timu ya KMKM akimkata mtama mshambuliaji wa timu ya Mafunzo wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar timu hizo zimetoka sare ya bao 1--1
  Mchezaji wa Timu ya Mafunzo na Kmkm wakishindana nguvu wakiwania mpira wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar Timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1
  Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot.
  Zanzinews.com 

  0 0

  Na Zainabu Hamis,Globu ya Jamii.
  MAASKOFU na Wachungaji wa kamati ya maandalizi ya Mkesha wa mwaka mpya Kitaifa kufanyika katika viwanja vya Uhuru jijini Dar es salaam Desemba 31,Wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Askofu Godfrey Malassy, wamewaomba watanzania wote kujitokeza siku ya Desemba 31 katika kuliombea Amani na Utulivu wa Taifa letu.

  Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Jumuiya wa Makanisa ya Pentekoste , ambaye pia ni Askofu wa huduma ya Tanzania Fellowship Churches (TFC), Askofu Godfrey Malassy alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

  amesema kuwa lengo la Mkesha huu ni Kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuvusha mwaka 2015 na kuupokea mwaka 2016 ikiwa ni pamoja na mkumshukuru Mungu kwa kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu kwa amani na tuzidi Kumuombea Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.John Pombe Joseph Magufuli kwa kuongoza Taifa letu.

  "Mkesha huu ni kwa watu wote na wakumshukuru Mungu na kutoa sadaka ,ambazo zitakusanywa na kupelekwa kwa watu wenye mahitaji maalum" alisema Malassy.

  Askofu Malassy aliongeza kuwa anamshukuru Mungu kwa kuandika kitabu kinachoitwa IJUE SIRI YA AMANI KWA TAIFA,ambacho kinapatikana kwa shilingi 5000, kwa lengo la kufunua asili, thamani na jukumu letu katika kulinda Amani kwa kila Mtanzania bila kujali dini, itikadi, ukabila na hata utaifa.

  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kushoto) akikabidhiwa taarifa ya makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Lazaro Nyalandu (wa pili kulia) leo tarehe 29 Desemba 2015 ofisini kwake Mpingo House. Wanaoshuhudia makabidhiano hayo ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Adelhelm Meru (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Ndugu Selestine Gesimba (kulia).
  Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini Mhe. Lazaro Nyalandu (kushoto) akizungumza na Waziri wa sasa wa Wizara hiyo Mhe. Prof. Jumanne Maghembe na Katibu Mkuu Dkt. Adelhelm Meru (kulia) wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya ofisi yaliyofanyika leo tarehe 29 Desemba 2015 katika ofisi za Wizara hiyo Mpingo House. Katika salamu zake Mhe. Nyalandu amepongeza uteuzi wa Prof. Maghembe ambapo amesema Mhe. Rais amefanya chaguo sahihi kwani Prof. Maghembe anao uwezo wa kufanya kazi nzuri katika Wizara hiyo. 
  Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe akizingumza na aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini Mhe. Lazaro Nyalandu (kulia) muda mfupi baada ya makabidhiano ya ofisi yaliyofanyika ofisini kwake leo. Mhe. Prof. Maghembe amempongeza Mhe. Nyalandu kwa kazi nzrui aliyoifanya akiwa Waziri wa Wizara ya Malisili na kuahidi kuanzia alipoishia katika kuhakikisha Maliasili za nchi zinatunzwa ipasavyo ikiwemo kupambana na changamoto zilizopo za ujangili na uharibifu wa misitu na maliasili kwa ujumla.

  WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe amekabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Waziri kabla yake Mhe. Lazaro Nyalandu, Makabidhiano hayo yamefanyika leo Makao Mkuu ya Wizara hiyo, Mpingo House jijini Dar es Salaam.

  Katika makabidhiano hayo Mhe. Nyalandu amekabidhi taarifa rasmi ya makabidhiano kwa Mhe. Waziri Prof. Jumanne Maghembe kama ishara ya kukabidhi rasmi Ofisi ya Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii.

  Makabidhiano hayo ambayo ni utaratibu wa kiserikali wa kukabidhi ofisi umeshuhudiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Adelhelm Meru, Naibu Katibu Mkuu, Bw. Selestine Gesimba, baadhi ya watumishi wa Wizara hiyo na waandishi wa habari.


  Akizungumza baada ya makabidhiano hayo Mhe. Nyalandu amempongeza Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumteua Prof. Maghembe kuwa Waziri wa Wizara ya Maliasili kwa kuwa ana sifa stahiki za kuongoza Wizara hiyo nyeti.

  Aliongeza kwa kusema kuwa Prof. Maghembe ana sifa ya kuwa mhifadhi kwa kusomea na pia ni mhifadhi kwa asili yake hivyo Wizara imepata mtu makini kwenye masuala ya Uhifadhi.

  “Natambua umahiri wako katika masuala ya uhifadhi nina imani utapambana na ujangili pamoja na usafirishaji haramu wa magogo kwa kasi inayotarajiwa na wananchi”. Alisema Mhe. Nyalandu.

  Kwa upande wake, Waziri aliyechukua nafasi yake Prof. Jumanne Maghembe amempongeza Mhe. Nyalandu kwa kazi nzuri na juhudi aliozoonesha wakati akiwa Waziri wa Wizara hiyo katika kuhakikisha Maliasili zilizopo zinaendelea kuwepo kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho. 

  Prof. Maghembe ameongeza kuwa kwa sasa vita kubwa iliyoko mbele yake ni vita dhidi ya ujangili na uharibifu wa misitu ikiwa ni pamoja na usafirishaji wa rasilimali za misitu kinyume cha sheria. Ameomba ushirikiano kwa wadau wote wa Maliasili nchini kumpa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha anafanikiwa katika vita hiyo.

  Pamoja na mambo mengine taarifa hiyo ya makabidhiano inaelezea kazi zilizokwisha kufanyika katika kipindi cha utawala uliopita, kazi zinazoendelea na zilizopo kwenye mpango wa utekelezaji pamoja na changamoto mbali mbali zinazoikabili sekta ya Maliasili na Utalii ikiwemo Ujangili na uvunaji pamoja na usafirishaji wa magogo. 
  (Na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Maliasili na Utalii)

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa zawadi ya khanga,blanket na ndoo kwenye wodi ya wazazi katika zahanati iliyopo kwenye kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu kwa Mama mkimbizi kutoka nchi ya Burundi aliyejifungua.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwajulia hali akina mama waliolazwa katika zahanati iliyopo ndani ya kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu Mkoani Kigoma wanaotoka nchi ya Kidemokrasia ya Congo.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongea na wakimbizi wa Congo na Burundi katika kambi ua Nyarugusu.
  Baadhi wa wakimbizi kutoka nchi ya Congo na Burundi waishio katika Kambi ya wakimbizi Nyalugusu Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma, wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (hayupo pichani) akiwahutubia.Picha na Editha Karlo wa Globu ya Jamii, Kigoma.

  MSIJE MAKAMBINI NA SILAHA – WAZIRI MKUU
  * Ataka walionazo wazisalimishe, asema watakaokiuka kukamatwa
  * Awaonya wakimbizi kuhusu ngono zembe, asema siyo jambo la dharura

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaasa raia wanaokimbia nchi zao na kupata hifadhi Tanzania kutobeba silaha wanapoingia nchini kuja kuishi kwenye kambi za wakimbizi.

  Ametoa onyo hilo leo mchana (Jumanne, Desemba 29, 2015) na wakati akizungumza na mamia ya wakimbizi wanaoishi kwenye kambi za Nyarugusu na Nduta zilizoko wilayani Kasulu na Kibondo, mkoani Kigoma waliofika kumsikiliza kwenye mikutano ya hadhara iliyofanyika kwenye kambi hizo.

  “Ninawasihi mjitambue kuwa mmehama kutoka DRC na Burundi, na mnapoingia hapa inabidi mbadilike muwe na tabia za hapa. Hatuhitaji mje na silaha au vifaa hatarishi kwa sababu tunataka mkae kwa usalama,” alisema.

  Alisema suala la usalama ni muhimu miongoni mwao, ni muhimu zaidi kwa majirani zao lakini pia ni muhimu sana kwa watoa huduma wanaowahangaikia. “Tunataka kila mmoja awe mlinzi wa mwenzake ili siku mkiondoka mrudi nyumbani mkiwa salama,” alisema.

  “Ninyi mko hapa mnatunzwa kwa hiyo hamruhusiwi kutoka kambini na kutembea hovyo huko nje. Hii ni kwa usalama wenu. Hatumruhusu kuingia na bunduki au mabomu na yeyote atakayemuona mwenzie ana silaha au ameificha mahali aje atuambie ili tumchukulie hatua na ninyi wengine mbakie salama,” alisisitiza.

  Kuhusu maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU), Waziri Mkuu aliwataka wakimbizi hao wajiepushe na ngono zembe kwa sababu kiwango cha maambukizi kimeongezeka kwa asilimia moja ikilinganishwa na mwaka jana. 
  “Nimetembelea hospitali yenu hapa kambini na kuelezwa kuwa maambukizi ya VVU hapa yapo na mwaka huu yamefikia asilimia mbili ya watu waliopimwa ikilinganishwa na mwaka ambapo ilikuwa ni asilimia moja tu,”

  “Kutokana na uwingi wenu, naomba niwasihi sana mjizuie kufanya ngono zembe na kama mtu atashindwa kabisa kujizuia ni vema atumie kinga. La sivyo mtaleta maambukizi ya juu sana na wote mtakwisha,” alisema.

  “Suala lenyewe siyo jambo la dharura, kawaida huwa kuna maandalizi baina ya wahusika, watu wanakubaliana juu ya muda na mahali pa kukutanandiyo maana nasema siyo jambo la dharura. Ndugu zangu tujihadhari sana kwa sababu kasi ya maambukizi mahali hapa iko juu sana,” alisisitiza. 
  Mapema, Mkuu wa kambi ya Nyarugusu, Bw. Sospeter Boyo alimweleza Waziri Mkuu kwamba kambi hiyo ilifunguliwa Novemba 1996 kwa lengo la kuwahifadhi wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo waliokuwa wakikimbia vita ya wenyewe kwa wenyewe.

  Alisema kambi hiyo yenye ukubwa wa kilometa za mraba 28, ina uwezo wa kuhifadhi wakimbizi 50,000 lakini kwa sasa inao wakimbizi 151,032 ambao ni mara tatu zaidi ya uwezo halisi wa kambi hiyo.

  “Tangu Aprili mwaka huu, idadi ya wakimbizi imeongezeka hadi kufikia 151,032 miongoni mwao ni wakongo 61,313, warundi 89,619, Wanyarwanda 75, Waganda 12, Wasudan kusini wane,Wakenya wane, Msomali mmoja, Mzimbabwe mmoja na raia wa Ivory Coast mmoja,” alisema Bw. Boyo.

  Alisema wanakabiliwa na changamoto za uhaba wa maji safi, ufinyu wa huduma za afya na elimu na uharibifu wa mazingira.

  Waziri Mkuu bado anatembelea pia kambi ya JKT ya Mtabila wilayani Kasulu na kesho asubuhi anatarajiwa kufanya majumuisho ya ziara yake.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMANNE, DESEMBA 29, 2015.


  0 0

   Baadhi ya wananchi wakiwa wamesha bomoa nyumba zao zilizo katika Bonde la mto Msimbazi, mtaa wa Magomeni Sunna jijini Dar es salaam, kabla ya serikali kuanza kuzibomoa nyumba hizo ifikapo tarehe 5 januari 2016


  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe akizungumza kwenye kikao cha pamoja kati yake na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mhe. Januari Makamba (kulia) leo tarehe 29 Desemba 2015 katika ukumbi wa Selous Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii  Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuipa majukumu Kamati Maalum ya Wataalam ya kutengeneza andiko maalum litakalotumika kuandaa Programu ya pamoja ya kitaifa ya upandaji miti nchi nzima kuanzia mijini hadi vijijini kwa lengo la kuhifadhi na kuendeleza mazingira ikiwemo misitu. Kwa mujibu wa Prof. Maghembe Kamati hiyo imepewa wiki mbili kukamilisha kazi. Mpango huo utashirikisha pia Wizara ya TAMISEMI.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mhe. Januari Makamba (kulia) akizungumza katika kikao hicho. Kushoto ni Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe.
  Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe akifafanua jambo katika kikao hicho.
   
  ……………………………………………………………………. 
  Wizara ya Maliasili na Utalii, Tamisemi
  na Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano
  inategemea kuanzisha programu ya pamoja wa upandaji miti nchini kwa ajili ya uhifadhi na undelezaji wa mazingira
  ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
  Akizungumza katika mkutano wa pamoja uliwakutanisha
  Mawaziri wa Wizara ya Maliasili, Utalii na Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na
  Muungano na jopo la wataalamu, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne
  Maghembe amesema Serikali ya awamu ya tano imekusudia kuboresha uhifadhi wa
  mazingira
  .
  Prof. Maghembe. Ameongeza kuwa Wizara
  ina maeneo makubwa yaliyotengwa kwa ajili ya kupanda miti ili kuzuia uharibifu
  wa Mazingira ikiwa ni pamoja na kuzuia ukataji miti hali inayotishia nchi kuwa
  jangwa kama hatua stahiki hazitachukuliwa mapema.
  ‘’Tupo tayari tumejiandaa na tunaweza
  ikiwa nia yetu ni kuhakikisha nchi nzima inapandwa miti kwa wingi na kwa
  usimamizi wa hali ya juu kwa kuwashirikisha wananchi’’ Prof. Maghembe
  alisisitiza.
  Mkutano huo ambao pia umehudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi
  ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mhe. January Makamba ulikuwa na lengo
  la kuipa kazi kamati maalum kwa ajili ya kuandaa andiko maalum litakalotumika
  kuandaa mpango mkakati huo.
  Kwa mujibu wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
  Mazingira na Muungano Mhe. January Makamba Kamati hiyo imepewa wiki mbili
  kuhakikisha inakamilisha kazi hiyo ambapo utekelezaji wake unategemewa kuanza
  mara moja ukiwa na mbinu mpya zaidi.
  ‘’Oparesheni panda miti ni lazima
  ibadilishwe kwa kuwa kumekuwa hakuna utaratibu mzuri ni lazima tuhakikishe
  idadi ya miti itakayopandwa inatunzwa ipasavyo’’ Mhe. Makamba alisisitiza.
  Alisema programu  ya kupanda miti hiyo  itahakikisha Wananchi wanashiriki kikamilifu
  kwani kwa sasa miti imekuwa ni biashara kubwa miongoni wa Wananchi hivyo
  itawasaidia pia kuwaongezea kipato.
  Kwa upande wake Naibu Waziri wa
  Maliasili na Utalii. Eng. Ramo Makani amewataka watalaamu hao wasiishie tu
  kwenye kuandika na badala yake wawe mstari wa mbele kuhakikisha malengo ya upandaji
  miti yanafikiwa kwa kuweka mipango hiyo katika vitendo.
  (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Maliasili na Utalii – www.wizarayamaliasilinautalii.blogspot.com)

  0 0

  ju3
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – UTUMISHI na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akiwahimiza watumishi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kufanya kazi kwa uadilifu alipoitembelea ofisi hiyo mapema leo.
  ju4
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – UTUMISHI na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) (kulia) akizungumza na watumishi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma alipoitembelea ofisi hiyo mapema leo.
  ju1
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – UTUMISHI na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akishuhudia mfumo wa maombi ya kazi (recruitment portal) unavyofanya kazi alipotembelea ofisi ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma mapema leo.
  ju2
  Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Daudi Xavier (kulia) akieleza majukumu ya ofisi yake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – UTUMISHI na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) alipoitembelea ofisi hiyo mapema leo.


  ……………………………………………………………………………………………………….
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) amesema kila Mtumishi wa Umma anatakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia taratibu na uadilifu bila kutoka nje ya mstari. Waziri Kairuki amesema hayo katika kikao kazi na Wafanyakazi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma mapema leo akisisitiza kufanya tathmini ya kazi na kuzaliwa upya katika utendaji kuwa ni jambo la msingi. “Hakuna kuruhusu chochote kinachoenda nje ya utaratibu, tufuate misingi ya kazi na kumbukumbu zitunzwe vizuri na ajira zipatikane kwa kuzingatia sifa na sio kujuana” Mhe. 

  Kairuki alisema na kusisitiza lazima Watumishi wa Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma wafanye kazi kwa misingi ya weledi. Mhe. Kairuki alielekeza malalamiko yanapotokea yafanyiwe kazi mapema ili kila mtu apate haki anayostahili kwa kuzingatia malengo ya kuanzishwa kwa Sekretarieti hiyo. Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ilianzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29 (1). Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
  Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora

  0 0

  gad1
  Mwenyekiti  wa Jumuiya  wa Makanisa ya Pentekoste,(Katikati)  ambaye pia ni Askofu wa Huduma ya Tanzania Fellowship Churches (TFC), Askofu  Godfrey  Malassy  alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam.
  gadi2
  Wachungaji mbalimbali wa Makanisa ya Pentekoste wakiwa katika mkutano na Waandishi wa Habari kwaajili ya kuzungumzia mkesha utakaofanyika Desemba 31
  ………………………………………………………………………………..
  Na  Skolastika Tweneshe-Maelezo
  Fedha zitakazopatikana katika Tamasha la mkesha wa kuombea amani  nchini zitatumika kuwasaidia watu wenye mahitaji  hasa afya ya mama na mtoto.

  Hayo yamesemwa na Mwenyekiti  wa Jumuiya  wa Makanisa ya Pentekoste , ambaye pia ni Askofu wa huduma ya Tanzania Fellowship Churches (TFC), Ask0fu  Godfrey  Malassy  alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

  Malassy alisema kwamba, fedha zitakazopatikana katika tamasha hilo zitanunua vifaa vinavyotumia nishati ya jua (solar Panels) ili kuwasaidi wamama wajawazito na watoto wanaozaliwa.“Kina mama wajawazito na watoto wanakufa mahospitalini kutokana  na kukosa umeme hasa vijijini,  hivyo tumeamua fedha zitakazopatikana mkesha huu tutanunua solar” alisema Malassy.

  Aidha Askofu Malassy  amewaomba wananchi   kuzidi kumuombea Rais John Magufuli katika kuliongoza Taifa la Tanzania ili aendelee kufanya kazi yake kwa ufanisi ambayo tayari imekubalika ndani na nje ya nchi.  Mwenyekiti huyo alitambulisha kitabu  kiitwacho IJUE  SIRI YA AMANI  KWA  TAIFA ambacho  kinauzwa Sh.5000 amesema kuwa  kitabu hicho kina lengo la kuelimisha thamani na jukumu la watanzania kuilinda Amani  bila kujali itikadi za  dini, siasa wala ukabila.

  Pia ameomba kwa atakaeguswa na  matatizo yanayowakumba wamama wajawazito anaweza kutuma mchango wake kwa namba zifuatazo 0755202204,0719202204,0684202204.

  Mkesha huo  ni wa 18 tangu uanze kufanyika  na mwaka huu utafanyika  katika Uwanja wa Uhuru usiku wa tarehe 31 ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais wa Awamu ya Tano Mhe.  John Pombe Magufuli.

  0 0

   Naibu Waziri, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Angelline Mabula (Mb), akiangalia mafaili ya kesi mbalimbali katika Baraza la Ardhi na Nyumba la Kinondoni, jijini Dar es salaam, alipofanya ziara ya kushtukiza katika Baraza hilo, kulia kwake ni karani wa baraza hilo, Bahati Rashidi.
   Naibu Waziri, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Angelline Mabula (Mb), akitazama utunzwaji wa mafaili katika masijala alipofanya ziara ya kushtukiza katika Baraza la Ardhi na Nyumba la Kinondoni, pembeni yake ni karani wa baraza hilo; Bahati Rashidi
  Naibu Waziri, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Angelline Mabula (Mb), akiongea na Wananchi wa King’azi Juu A, alipofika katika eneo hilo ambalo limekuwa na mgogoro wa ardhi kati ya wilaya ya Kinondoni, Kisarawe na Ilala.  0 0

   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akihojiwa na mtangazaji mashuhuri wa Azam TV Taji Liundi muda mfupi kabla ya kuzindua filamu mpya ya Home Coming kwenye ukumbi wa Century Cinema ,Mlimani City jijini Dar es Salaam.
   Wadau wa Sanaa na Utamaduni wakisubiri kushuhudia uzinduzi wa filamu mpya ya Home Coming.
   Mmoja wa washiriki wa Filamu hiyo ya Home Coming ,Susan Lewis maarufu kama Natasha
   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye na Ayo TV muda mfupi kabla ya kuzindua Cinema ya Home Coming.
  Muigizaji mkuu wa filamu ya Home Coming Daniel Kijo (kushoto) akisalimana na mgeni rasmi katika uzinduzi wa filamu hiyo Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye mara baada ya uzinduzi wa filamu hiyo kufanyika kwenye ukumbi wa Century Cinema, Mlimani City jijini Dar es Salaam.
  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI.


  0 0

  Mwenyikiti mpya wa shirikisho la wanafunzi wa elimu ya juu nchini Tanzania TAHLISO Ndugu STANSLAUS PETER akila kiapo kulitumikia shirikisho hilo mbele ya mwanasheria HAMZA JABIRI leo Jijini Dar es salaam kuanza kazi rasmi ya kuwatumikia wanafunzi wa elimu ya juu nchini Tanzania 

  Na Exaud Mtei (msaka habari) wa Habari24 blog

  Uongozi mpya wa shirikisho la elimu ya vyuo vikuu nchini Tanzania TAHLISO umesema kuwa upo tayari kumuunga mkono Rais wa Tanzania Dr John pombe magufuli kwa kasi aliyoanza nayo na kuhakikisha kuwa elimu ya Tanzania hasa elimu ya vyuo vikuu inakuwa ya ubora unaofaa na inaheshimika nchini Tanzania.
  Makamu Mwenyekiti mpya wa TAHLISO Ndugu JUMA ALLY OMARI akila kiapo leo jijini Dar es salaam 

  Akizungumza na wanahabari mapema leo jijini Dar es salaam katika hafla fupi ya kuwasimika viongozi wa shirikisho hilo wapya mwenyekiti mpya wa TAHLISO Tanzania Bw STANSLAUS PETER amesema kuwa kwa miaka mingi elimu ya juu nchini Tanzania imekuwa haina ubora unaotakiwa ikiwa ni pamoja na mitaala mibovu,ukosefu wa mokopo kwa wanafunzi wengi jambo linalowakatisha tamaa wengi kusoma,ambapo amesema uongozi wake umeona kasi nzuri ya serikali ya awamu ya tano na wapo tayari kushirikiana na serikali kutatua changamoto za wanafunzi nchini.
  Naibu katibu mkuu wa TAHLISO KHAMIS ELLY akiapa leo Jijini Dar es salaam 

  Mwenyekiti huyo amesema kuwa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa mwaka huu umeonyesha kuwa serikali ya Magufuli inawajali wanafunzi kwani asilimia kubwa ya wanafunzi walipata mikopo na wengine wanaendelea kupata mikopo huku akiwataka wanafunzi kutulia kwani neema kwao inakuja kutokana na kasi ya uongozi huo mpya pamoja na ule wa serikali ya awamu ya tano.
  Katibu mkuu Mtendaji mpya wa Shirikisho hilo SAGOLE WAMBURA akiapa leo 

  Viongozi wa TAHLISO wameapishwa leo rasmi Jijini Dar es salaam baada ya uchaguzi wa Kidemocrasia uliofanyika tarehe 23 mwezi huu na wataiongoza Taasisi hiyo kwa mwaka mmoja kwa mujibu wa katiba yao.
  JOSEPH SHABAN ambaye ni muazini mpya wa shirikisho hilo Akiapa leo 
  Omary Idd Naibu muazini akiapa leo tayari kulitumikia shirikisho hilo 
  Mwenyikiti mpya wa shirikisho la wanafunzi wa elimu ya juu nchini Tanzania TAHLISO Ndugu STANSLAUS PETER akizungumza na wanahabari mara baada ya kuapishwa rasmi kuwatumikia wanafunzi wa elimu ya juu nchini 
  Wanahabari waliokuwa katika hafla hiyo 
  Picha za pamoja baada ya kula kiapo kwa viongozi hao wapya wa TAHLISO leo Jijini Dar es salaam

  0 0


  0 0

  KAS1

  KAS2
  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na wanawake waliojifungua katika wodi ya wazazi ya hospitali ya wakimbizi katika kambi ya Nyarugusu wilayani Kaslu  akiwa katika ziara ya mkoa wa Kigoma Desemba 29, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  KAS3
  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na wanawake waliojifungua katika wodi ya wazazi ya hospitali ya wakimbizi katika kambi ya Nyarugusu wilayani Kaslu  akiwa katika ziara ya mkoa wa Kigoma Desemba 29, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  KAS4
  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akiwapungia wakimbizi kutoka  Burundi wakati alipotembelea kambi ya Nyarugusu akiwa katika ziara ya mkoa wa Kigoma Desemba 29, 2015.
  KAS5
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na watumishi  wa mashirika mbalimbali ya kimatifa wanaowahudumia wakimbizi wa Burundi kwenye kambi ya Nyarugusu wilyani Kasulu akiwa katika ziara ya mkoa wa Kigoma Desemba29, 2015.
  KAS6
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na watumishi  wa mashirika mbalimbali ya kimatifa wanaowahudumia wakimbizi wa Burundi kwenye kambi ya Nyarugusu wilyani Kasulu akiwa katika ziara ya mkoa wa Kigoma Desemba29, 2015.
  KAS7
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la Msingi la Shule ya Msingi inayojengwa kwenye kambi ya wakimbizi ya Nduta wilayani Kibondo  ambayo imepewa jina lake, Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Kigoma Desemba 29, 2015.  Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Ruth Msafiri.
  KAS8
  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akiwa amekalia dawati katika moja ya madarasa ya Shule ya Msingi inayojengwa kwenye kambi ya wakimbizi ya Nduta ambayo imepewa jina lake . Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Kigoma Desemba 29, 2015. Wapili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Ruth Msafiri.
  KAS10
  Watoto wa wakimbizi kutoka Burundi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye kambi ya wakimbizi ya Nduta wilayani Kibondo Desemba 29, 2015.
  KAS11
  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akimkabidhi Mkuu wa Kambi ya Wakimbizi ya Nduta, Bw. Frederick Nisajile shilingi milioni 2 zikiwa ni mchango wa kusaidia programu ya upandaji miti kwenye maeneo yanayozunguka kambi hiyo. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Kigoma Desemba 29, 2015. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Ruth Msafiri. (Picha na Ofisi a Waziri Mkuu)

older | 1 | .... | 725 | 726 | (Page 727) | 728 | 729 | .... | 1896 | newer