Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 724 | 725 | (Page 726) | 727 | 728 | .... | 1898 | newer

  0 0


  Na Magreth  Kinabo- MAELEZO.
   
  Serikali imeanzisha utaratibu wa utoaji wa taarifa  ya ugonjwa wa kipindipindu kwa wiki  kwa nchi nzima  ili kuweza kuhabarisha umma wa Watanzania kwamba ni mkoa upi au wilaya ipi imejitahidi kukabiliana na ugonjwa huo.

   Utaratibu umeanza rasmi leo, tarehe 28. 12. 2015, hivyo kila Jumatatu  ya wiki  kama leo taarifa za ugonjwa huo zitakuwa zinatolewa.
  Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya ugonjwa huo nchini kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo jijini Dar es Salaam.

  ‘’Ninatoa rai kwa wakuu wa mikoa na wilaya kuhakikisha kwamba wanaleta  taarifa sahihi za watu waliathirika na mlipuko wa  ugonjwa wa kipindupindu kwani kuficha taarifa haitasaidia kwa kuwa ugonjwa huu unaendelea kusambaa katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu,’’ alisema Waziri huyo.

  Aidha Serikali imesema kwamba   wizara  hiyo kwa itashirikiana na wadau mbalimbali, ambao ni Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Wizara ya Elimu ya Sayansi, Teknolojia na Ufundi, DAWASCO, DAWASA na Sekretarieti ya Mkoa wa Draes Salaam, wakiwemo wadau   wa maendeleo ili kuweza  kukabiliana na ugonjwa huo.

  Akizungumzia kuhusu ugonjwa huo, Waziri Ummy alisema  tangu umeanza Agosti 15, mwaka 2015 jijini Dares Salaam,ambapo mpaka Desemba 27, mwaka huu umesambaa katika mikoa 21 ya Tanzania Bara.
   
  ‘’ Watu  walioathiriwa na ugonjwa huo tangu umeibuka ni 12,222 na jumla ya  watu  196 wamefariki  kutokana na  ugonjwa  huo, lakini mikoa ya Mtwara, Njombe na Ruvuma mpaka hakuna ripoti ya watu waliathiriwa na ugonjwa huo,’’ alisisitiza.

  Hata hivyo waziri huyo aliongeza kwamba  katika kipindi cha mwezi nzima mikoa ya Kilimanjaro na Iringa hakuna taarifa za ugonjwa huo, hivyo aliipongeza kwa juhudi walizofanya za kuudhibiti.

   Waziri huyo alifafanua kwamba kwa kipindi cha wiki kuanzia Desemba 21 hadi Desemba 27 mwaka huu jumla wagonjwa 493 wameripotiwa kuugua ugonjwa huo na vifo sita katika wilaya 46 zilizopo kwenye mikoa 18.

   Aliongeza kwamba mikoa inayoonesha kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa ni Morogoro(98),  Mara (83), Arusha(60)Singida(48) ,Mwanza (45) na Manyara 27 na mikoa ambayo katika kipindi cha wiki hiyo ambayo haijaathirika na ugonjwa huo ni Iringa, Shinyanga, Kilimanajaro, Pwani na Kagera.

   Aliwataka wananchi kutumia kanuni za afya za kunawa mikono kablaya ya kula, kunywa maji safi  na salama, kuepuka kula vyakula vilivyoandaliwa pasipo kuzingatia  mazingira safi na salama , kuchaemsha maji ya kunywa kuwa vyoo bora ili kuweza kukabiliana na ugonjwa huo. 

  Akizungumzia kuhusu suala la uzoaji wa taka kufuatia zoezi la kampeni ya usafi wa mazingira lililofanyika hivi karibuni kwa agizo la  Rais  wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, alisema watashirikiana na TAMISEMI ilikuhakikisha taka hizo zinazolewa. Hata hivyo alisema tayari Waziri husika ameshato siku 21 kukabiliana na tatizo hilo.

  0 0

   

  Waziri Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe (mbele kulia) akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Selestine Gesimba wakati wa mapokezi yake leo tarehe 28 Desemba 2015 katika ofisi yake mpya Mpingo House mara baada ya kuapishwa Ikulu mapema asubuhi ya leo. Nyuma yake kulia ni naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Eng. Ramo Makani na anaeongoza utambulisho katikati yao ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Adelhelm Meru.
   Waziri Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe akisaini kitabu cha wageni mara tu baada ya kuingia katika ofisi yake mpya iliyopo Mpingo House mapema leo tarehe 28 Desemba 2015 baada ya kuapishwa Ikulu na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli. Wanaoshuhudia kulia ni Naibu Wazari wa Wizara hiyo Mhe. Eng. Ramo Makani na Katibu Mkuu Dkt. Adelhelm Meru (kushoto).
  Waziri Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe akiongea na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Adelhelm Meru (kushoto) na Naibu Waziri Mhe. Eng. Ramo Makani (kulia) mara baada ya kusaini kitabu cha wageni ofisini kwake mapema leo tarehe 28 Desemba 2015.
  Picha ya pamoja kati ya Mhe. Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kulia) na Naibu Waziri wake Mhe. Eng. Ramo Makani (wa pili kushoto), Katibu Mkuu wa Wziara hiyo Dkt. Adelhelm Meru (wa kwanza kulia) na Naibu Katibu Mkuu Ndugu Selestine Gesimba(kushoto). 
  Sehemu ya wafanyakazi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakiwa tayari kwa mapokezi ya Waziri wao mpya Mhe. Prof. Jumanne Maghembe aliyeapishwa Ikulu leo na Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tazania Mhe. John Pombe Magufuli.(Picha na Hamza Temba - Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Maliasili na Utalii)

  0 0


  0 0

  Na Magreth  Kinabo- MAELEZO
   
  Serikali imesema kwamba tamko lake lilitolewa hivi karibuni kuhusu matangazo ya Tiba Asili na Tiba Mbadala palepale kwa kuwa lengo lake ni kuboresha huduma hiyo. Hivyo kama  kuna mtoa huduma ambaye amekwazika na tangazo hilo ipo tayari kuzungumza naye.
   
   Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tamko hilo kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo jijini Dar es Salaam.
   
  Tamko hilo ambalo lilitolewa Desemba 24, mwaka huu,ambapo limepiga marufuku  matangazo yote yanayohusu tiba asili na tiba mbadala kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
   Ambapo kwa wale wenye vibali wanatakiwa kuviwasilisha vibali na matangazo yao kwenye Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala ili vifanyiwe mapitio.
   
  Tamko hilo  liliendelea  kufafanua kwamba  utoaji wa elimu ya afya kwa umma unaofanywa na watoa huduma za tiba asili na tiba mbadala kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii umepigwa marufuku hadi hapo utaratibu mwingine utakapotangazwa.
   
  ‘Watoa huduma za tiba asili na tiba mbadala nchini kote wanaagizwa wawasilishe kwenye Baraza nyaraka zote muhimu ndani ya wiki mbili kuanzia leo Desemba 2015. Baadhi ya nyaraka hizo ni zile zinazohusu kuuza dawa za asili na tiba mbadala, nyaraka za kumiliki mashine zinazotumika katika kufanya uchunguzi katika tiba asili na tiba mbadala,’ lilieleza tamko hilo.
   
  Tamko hilo lilifafanua kwamba  Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala linaagizwa katika kipindi cha siku 14 kuanzia leo 24 Desemba 2015, lipitie nyaraka zote zikapowasilishwa zinazohusu usajili wa watoa huduma, usajili wa vituo vyao, ikiwa ni pamoja na maduka ya dawa za asili na dawa za tiba mbadala, usajili wa dawa zote zinazotumika katika huduma hizo na usajili wa mashine zote zinazotumika katika huduma za tiba asili na tiba mbadala.
   
  Aidha  akizungumzia kuhusu tangazo hilo, Waziri   Ummy alisema  ‘Mimi  niko tayari kuzungumza na mtoa huduma ambaye amikwazika na tangazo hili, ili aweze kueleza ni sababu zipi zinazomfanya asisajiliwe.  Tunafanya hivi kwa mujibu wa sheria ,kanuni na taratibu,’ alisisitiza.

  Aliongeza kwamba Sheria ya Tiba Asili na Tiba Mbadala  Namba 23 ya Mwaka 2002 inaeleza  wazi.

  Kwa mujibu wa Waziri huyo alitaja idadi ya watoa huduma hiyo kuwa ni  wako 75,000 kwa takwimu za nchi nzima.Naye Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili  na Tiba Mbadala, Dkt. Edmund Kayombo alisema hadi sasa hawajapokea mrejesho wa tamko la tamko  hilo la  Serikali.

  Kwa upande wake  Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama  Vya Tiba Asili Tanzania(SHIVYATIATA), Abdulrahaman  Lutenga alisema  hakuna mganga yoyote aliyepinga tamko hilo na Serikali, hivyo tamko lililotolewa  hivi karibuni la kupinga agizo hilo si halali kwa kuwa halikupitia katika shirikisho hilo.
   
  ‘ Hatutambui kampuni hii iliyotoa tamko la kupinga tangazo la Serikali kwani ya mtu binafsi yenye wanahisa 11,’ alisema Lutenga.Akizungumzia kuhusu hatima ya tamko hilo, Dkt. Kayombo alisema baada ya siku walizotoa  kumalizika  watatangaza hatua zipi zitachukuliwa kama vile kuwaondoa wasiofuata sheria.

  0 0

   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akisisitiza jambo wakati alipokutana na Menejimenti ya iliyokuwa Wizara ya Uchukuzi, na wakuu wa Taasisi zilizo chini yake, katika Ofisi za Wizara hiyo leo asubuhi. Waziri Mbarawa amewasisitiza Viongozi hao kuwa waadilifu na kufanya kazi kwa kasi.
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kutoka kulia) na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Eng. Edwin Ngonyani ( wa kwanza kutoka kulia), wakimsikiliza Bi. Mkami Chacha kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wakati alipokuwa akiwaleza namna mashine ya Kukagua makontena inavyofanya kazi, leo mchana wakati Mawaziri hao walipotembelea Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kuona kazi mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka hiyo.
   Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Eng. Aloyce Matei akimwonyesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu) eneo itakapojengwa gati 13 na 14, wakati Waziri huyo alipotembelea Mamlaka hiyo leo Mchana.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akisisitiza jambo kwa wafanyakazi wa Taasisi mbalimbali wanaofanya kazi katika kituo cha pamoja (one stop center) katika Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) wakati alipowatembelea leo Mchana. Waziri Mbarawa amewasisitiza watumishi hao kufanya kazi kwa uadilifu.


  0 0

  Siku chache baada ya kuachia video ya wimbo wake - ‘NINGEFANYAJE’, muimbaji wa R&B kutoka Tanzania, Bernard Paul  maarufu kama Ben Pol ameeleza sababu zilizopelekea muimbaji  Avril kutoka Kenya aliyeshirikishwa kwenye wimbo huo,  kutoonekana kwenye video hiyo anayoitaja kuwa kubwa kuliko video zote alizowahi kufanya.

  Katika video hiyo iliyoongozwa na Justin Campos wa Afrika Kusini, Ben Pol anaonekana akiimba na Rossie M  ambaye pia ameshirikishwa kwenye wimbo huo huku mashabiki wakiisikia sauti ya Avril bila kumuona mwimbaji huyo mrembo.

  Ben Pol amewaomba radhi mashabiki wake kwa kuwapa video ambayo haijakamilisha wahusika wote hususan kutokuonekana kwa Avril,  na kwamba sababu zilizopelekea hivyo zilikuwa nje ya uwezo wa pande zote katika utayarishaji wa video hiyo.

  ​​​Ben amesema kuwa baada ya yeye na Rossie M kuwasili Afrika Kusini ilikoshutiwa video hiyo, zilijitokeza changamoto muda mfupi kabla ya kuanza zoezi hilo. Ben Pol ameeleza kuwa pamoja na kuwa na maandalizi makubwa, video ya ‘Ningefanyaje’ ilikumbwa na changamoto nyingi tangu awali zilizopelekea kuahirishwa mara tatu.

  “Kwa kweli hii video tokea mwanzo ilikuwa na changamoto, kwanza tuliisogeza mbele karibu mara tatu tena tukiwa tayari tumeshafika Afrika Kusini mimi na Rossie,” alisema Ben Pol. “Mara ya kwanza ni kutokana na ‘delay’ ya viza upande wa Avril. Si unajua Wakenya wao wanaenda South kwa viza tofauti na sisi Tanzania hatuendi kwa viza so kwetu ni rahisi zaidi muda wowote tu ukiamua fasta unaenda,” aliongeza.

  Mkali huyo alieleza kuwa baada ya terehe mpya kupangwa na muongozaji aliyeshuti video hiyo, Justin Campos, siku moja kabla ya kushuti, AVRIL alipata tatizo lingine ambalo lilimzuia kusafiri kwa siku iliyofata kwenda Afrika Kusini.


  Wakati huo huo, Campos naye alimueleza Ben Pol kuwa  kwa jinsi ratiba yake ilivyo endapo ataahirisha tena kushuti video hiyo, ratiba yake isingemruhusu kushuti video hiyo hadi Januari au Februari 2016,  kitu ambacho Ben Pol amesema  kisingewezekana kwasababu ingeendelea kumgharimu zaidi kifedha na kuvuruga ‘timing’ yake.

  “Kutokana na hali hiyo, sikuwa na jinsi nyingine zaidi ya kukubali matokeo kwasababu  mwisho wa siku si mimi wala Avril wala director aliyekwamisha bali ni ‘situation’ ambayo ilikuwa nje ya uwezo wa kibinadamu.” Ben Pol anaeleza.

  Ameongezea kuwa pamoja na kwamba angeweza kuamua kushuti video kwa kutumia version nyingine ya wimbo huo isiyokuwa na sauti ya Avril ili video isionekane na upungufu wake, lakini hakupenda kufanya hivyo kwa kuwa lengo kuu la wimbo lilikuwa kumshirikisha mwimbaji huyo. Pia, mashabiki wangekosa ladha nzuri na kazi nzuri aliyoifanya Avril.  Hivyo, aliamua kufanya video hiyo bila Avril na kukusudia kuwaeleza mashabiki wake kilichosababisha hali hiyo kwa kuwa aliamini mashabiki wataelewa magumu aliyopitia katika kuwapa video hiyo waliyokuwa wakiisubiri.

  “Namshukuru sana Avril kwa kukubali kufanya kazi na mimi kwasababu imetimiza moja kati ya malengo yangu ya 2015, ambayo ilikuwa kuanza kufanya kazi na wasanii wa nje ya Tanzania na yeye ndiye alikuwa chaguo langu la kwanza. Ni imani yangu tutafanya tena project nyingine ya pamoja na kuikamilisha kama tulivyoikusudia,” alimaliza Ben Pol na kuwashukuru  mashabiki wake kwa kuupokea kwa mtazamo chanya wimbo na video yake.

  0 0

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na ugonjwa wa Kipindupindu ulivyoweza kupungua ikiwa kukiwa na vifo vya watu 493 kwa Tanzania Bara.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
  Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

  Na Zainabu Hamis wa Globu ya Jamii.
  JUMLA ya watu 493 wamefariki dunia kwa ugonjwa wa kipindupindu Tanzania bara tokea ulipoibuka jijini Dar es salaam.

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake leo, amesema kuwa jumla ya watu 12,222 wameugua ugonjwa huo tangu ugonjwa huo wa mlipuko kuaza hapa nchini.  “Ugonjwa wa Kipindupindu umeanza tokea tarehe Desemba 15, 2015 katika mkoa wa Dar es salaam na kusambaa katika mikoa 21 ya Tanzania” Mhe. Mwalimu amesema.  Hata hivyo,Waziri huyo,amesema waathirika wa kipindupindu wameanza kupungua katika mikoa ya 
  Mwanza, Arusha, Mbeya na Dar es salaam.

  Pia ameitaja Iringa na Kilimanjaro kuwa ni mikoa ambayo imeweza kuthibiti ugonjwa huo hatari.

  Mwalimu akitoa takwimu za ugonjwa huo, amesema hivi sasa kuna wagonjwa wapya 76, hivyo idadi ya wagonjwa wapya imefikia 493 na kifo kimoja.

  “Hadi sasa mkoa wa Morogoro vijijini unaongoza kwa wagonjwa 56, ukifuatiwa na Arusha (28), Rorya (22), Bunda (21) na Kigoma vijijini 17.” Mhe. Mwalimu amesema”

  Aidha Mhe.Mwalimu ametoa agizo kwa wakuu wa mikoa na wilaya kuwa ni marufuku kuuza matunda yaliyokatwa barabarani,kuuza vyakula katika mazingira yasiyo safi na salama,huku akitaka kuandaliwa kwa taarifa za kila wiki kuhusu ugonjwa huo.

  Akitoa rai kwa wakuu wa wilaya na mikoa, kuwa walete taarifa sahihi za mlipuko wa ugonjwa huo kwa ajili ya kuudhibiti. Na kwa kuwasisitiza watanzania kunywa maji safi na salama na kunawa mikono kwa maji safi na salama.

  0 0

  Mwanzilishi wa kikundi cha Tanzania Talents Organisation, Isaya  Msabila akizungumza na mwandishi wetu leo jijini Dar es Salaam katika eneo wanalofanyia mazoezi kata ya Kwembe jimbo la Kibamba. Kikundi hicho cha sanaa za maigizo na ngoma asilia hapa nchini ambapo wameungana vijana 26 ili kupunguza idadi ya vijana wasio na ajira wameona kujikusanya na kufanya maigizo na ngoma asilia ili kujikwamua kiuchumi.
  Vijana wa kikundi cha maigizo na ngoma asilia cha Tanzania Talents Organisation wakiwa katika picha ya moja leo jijini Dar es Salaam.

  VIJANA 26 wameunda kikundi cha maigizo na mgoma za asili kijulikanacho kama Tanzania Talents Organisation(T.T.O). ili kupunguza ongezeko la vija wasio na ajira hapa chini.

  Kikundi hiki cha maigizo na ngoma asilia kilichojichimbia katika kata ya Kwembe  jimbo la Kibamba jijini Dar es Salaam kikiwa na leongo la kutunza asili na tamaduni ya watanzania ili iweze kuigwa na mataifa mengine ulimwenguni kote.

  Hayo yamesemwa na Mwanzilishi wa kikundi cha Tanzania Talents Organisation, Isaya  Msabila wakati akizungumza na mwandishi wetu jijini Dar es Salaam leo.

   Pia Msabila amesema katika kikundi hicho wanachangamoto kadhaa baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na ukosefu wa vitendea kazi pamoja na huduma ya kwanza kwa vijana hao endapo kama kukitokea majeruhi katika harakati za kuigiza au kufanya mazoezi.

  Msabila aliwaomba wadau mbalimbali wanaoweza kusaidia kikundi hicho cha sanaa za uigizaji na ngoma asilia awasiliane na mwanzilishi wa T.T.O

  Isaya Msabila kwa namba 071449415 ili kuweza kukisaidia kikundi hicho kwa namna mbalimbali ili vijana waweze kujikwamua kiuchumi.

  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya Rais Dk John Magufuli kuwaapisha Mawaziri waliokuwa wamesalia Ikulu, Dar es Salaam leo.
  Ridhiwani pia alipata wasaa wa kujadiliana mambo mbalimbali na kiongozi huyo wa watumishi wa Serikali. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA.


  0 0


  0 0

  Mratibu wa Alliance For Social Education (ASE), Sunayritha Tawata akimkaribisha Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS, Daudi Mbaga (kushoto) katika semina ya Uwekezaji wa Pamoja iliyofanyika jijini Arusha.
  Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS, Daudi Mbaga akizungumza katika semina ya uwekezaji wa Pamoja uliofanyika jijini Arusha.
  Baadhi ya washiriki wa semina ya Uwekezaji wa Pamoja wakisikiliza mada.

  Ofisa Masoko Mkufunzi wa UTT AMIS, Waziri Ramadhan akitoa mada katika semina ya Uwekezaji wa Pamoja iliyofanyika jijini Arusha.

  0 0  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kushoto) akimuapisha Mhe. Dkt. Philip Mpango (kulia) kuwa Waziri wa Fedha na Mipango (Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge), leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kushoto) akimuapisha Mhe. Mhandisi Gerson Lwenge (kulia) kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji, leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kushoto) akimuapisha Mhe. Profesa Makame Mbarawa (kulia) (amehamishwa kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji) na kwenda Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. 

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kushoto) akimuapisha Mhe. Profesa Jumanne Maghembe (kulia) kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kushoto) akimuapisha Mhe. Dkt. Joyce Ndalichako (kulia) kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi. (Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge), leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.


  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  zit1
   Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizindua soko na Mwaro wa samaki wa Kibirizi mjini Kigoma Desemba 28 , 2015.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo Issa Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizindua soko na Mwaro wa samaki wa Kibirizi mjini Kigoma Desemba 28 , 2015.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo Issa Machibya. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)Machibya. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  zit2
  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua dagaa wanaokaushwa kitalaam kwa kutumia jua  wakati  alipozindua soko na mwaro wa kisasa wa samaki wa Kibirizi  mjini Kigoma Desemba 28, 2015. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
  zit5
  Mkazi wa Kigoma mjini akionyesha bango katika mkutano uliohutubiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye soko la samaki la Kibirizi mjini Kigoma Desemba 28, 2015.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  zit6
  Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa  akipata maelezo kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Kigoma, Issa Machibya kuhusu bunduki iliyokatwa ili kupunguzwa urefu ambayo ilikamatwa na polisi mkoani Kigoma wakati ilipotumika katika uhalifu. Mheshimiwa Majaliwa alikwenda kwenye Ofisi ya  Kamanda  wa polisi wa Mkoa wa Kigoma kukagua silaha mbalimbali zilizokamatwa na polisi  Desemba 28, 2015.. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  zit7
  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa  akitazama kifaa kinachotumiwa na wahalifu kutengeneza  risasi za bunduki aina ya goboli wakati alipokagua silaha mbalimbali zilizokamatwa na polisi  mkoani Kigoma na kuhifadhiwa kwenye Ofisi ya Kamanda wa polisi wa mkoa huo, Desemba 28, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  zit8
   Watumishi wa Serikali Kuu na Serikali za Mitaa  wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majliwa  wakati alipowahutubia  mjini Kigoma Desemba 28, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  zit9
   Watumishi wa Serikali Kuu na Serikali za Mitaa  wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majliwa  wakati alipowahutubia  mjini Kigoma Desemba 28, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  zit10
  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa  akizungumza na watumishi wa  serikari Kuu na Serikali za Mitaa mjini Kigoma Desema 28, 2015. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Photo Credits: govtech.com

  Kipindi hiki hukujia kila JUMATATU, kujadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu Tanzania ya sasa na ile tuitakayo. Wiki hii ni ya mwisho kwa mwaka 2015, hivyo kipindi hiki kimeangaza baadhi ya yaliyotokea katika siasa za Tanzania. Studioni alikuwepo Dj Luke Joe, Said Mwamende na Mama Jessica Mushala. Na kama kawaida, kwa njia ya simu tukaungana na wasikilizaji wengi ndani na nje ya Marekani KARIBU

  0 0

  ph1

  Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile (wa kwanza kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Philip Mpango (wa pili kulia) mara baada ya kuwasili Wizarani hapo leo jijini Dar es salaam. Wa kwanza kulia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji.
  ph2
  Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Sera Prof. Adolph Mkenda akifafanua jambo ofisini kwa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango mara baada ya kuwasili Wizarani hapo leo jijini Dar es salaam.
  ph3
  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akitoa taarifa fupi kwa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt. Philip Mpango (wa kwanza kulia) ikiwa ni sehemu ya ukaribisho kwa Waziri huyo Wizarani hapo.
  ph4
  Watendaji wa Wizara ya Fedha na Mipango wakielezea majukumu ya Idara na Vitengo katika mkutano na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt. Philip mara baada ya kuwasili Wizarani hapo leo jijini Dar es salaam.
  ph5
  ph6
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango akionesha kadi aliyoipokea kutoka kwa viongozi kwaniaba ya watumishi wa Wizara hiyo yenye lengo la kumpongeza kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo. Wa kwanza kulia ni Kaibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile na Mkurugenzi Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu Bi. Deodatha Makani (katikati). (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Fedha na Mipango)
  ph7

  Watumishi Wizara ya Fedha na Mipango wameaswa kufanya kazi kwa weledi   na kuwekeza nguvu zaidi katika ukusanyaji mapato ili kukuza uchumi wa nchi na kuifanya nchi iwe kitovu cha uchumi Barani Afrika.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango alipokuwa akiongea na watendaji wa Wizara hiyo alipowasili Wizarani hapo mara baada ya kuapishwa leo Ikulu jijini Dar es salaam.

  Katika mazungumzo yake na watendaji hao, Mhe. Dkt. Mpango, aliuagiza uongozi wa Wizara yake kuunda  na kisimamia sera za mfumo wa ukusanyaji  kodi ambao utabaki kuwa rafiki kwa wafanyabiashara ili kukuza biashara na uwekezaji nchini.

  “Ili kutekeleza kutekeleza ukusanyaji wa kodi kwa kutumia mfumo rafiki kwa wafanyabiashara na Serikali, Wizara inawajibu wa kusimamia na kukuza uchumi ambao utawanufaisha wananchi walio wengi, kwa kuhakikisha kodi zote ndogondogo ambazo ziko chini na nje ya Wizara, ambazo ni kero kwa wanachi wa hali ya chini zinapatiwa ufumbuzi kwani wananchi hao nao wanastahili maisha mazuri” Alisema Mhe. Dkt. Mpango.
  Waziri Dkt. Mpango aliwasisitiza watendaji kufanya kazi kwa bidii, maarifa na weledi ili nchi iweze kupiga hatua kwa kuzingatia nidhamu katika kufanya kazi ambayo ni dhamana walizokabidhiwa.

  Naye Naibu Waziri Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji aliwahimiza watendaji wa wizara hiyo kufanyakazi kwa umoja na mshikamano waliokuwa nao katika utendaji kazi ili kuleta maendeleo yenye tija huku akisisitiza kuwa wizara hiyo ndiyo msingi katika kukuza uchumi wa nchi.

  Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Servacius Likwelile aliwapongeza Viongozi hao wapya wa Wizara kwa kuteuliwa kwao kuiongoza Wizara ambayo ndiyo muhimili wa Serikali.

  Aidha, Dkt. Likwelile alitoa wito kwa watendaji wa wizara hiyo kuzingatia maagizo ya Mhe. Waziri kwa maendeleo ya nchi ili kulinda hadhi na heshima ya wizara.
  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano
  Wizara ya Fedha na Mipango
  28 Desemba, 2015

  0 0

  Harriet Shangarai, Stella Mpanda and Tausi Suedi
  "Pregnancy is not an illness or disease" say Childbirth Survival International (CSI) Co-founders - Stella Mpanda, CNM and Tausi Suedi, MPH.
  It is estimated at least 800 women die every day due to pregnancy, childbirth, and post-childbirth complications, most of which are preventable.

  Mama Mpanda and Tausi Suedi have an informative discussion with Harriet Shangarai of Nesiwangu show (click here) and leave no stone unturned as they passionately talked about the challenges, gaps, achievements, opportunities, and shared personal stories.
  This video will give you an in-depth picture of Childbirth Survival International, the amazing work the team is doing, and how you can partner to make a difference.
   For more information, visit www.childbirthsurvivalinternational.com

  0 0

  Harriet Shangarai, Stella Mpanda and Tausi Suedi
  "Pregnancy is not an illness or disease" say Childbirth Survival International (CSI) Co-founders - Stella Mpanda, CNM and Tausi Suedi, MPH.
  It is estimated at least 800 women die every day due to pregnancy, childbirth, and post-childbirth complications, most of which are preventable.

  Mama Mpanda and Tausi Suedi have an informative discussion with Harriet Shangarai of Nesiwangu show (click here) and leave no stone unturned as they passionately talked about the challenges, gaps, achievements, opportunities, and shared personal stories.

  This video will give you an in-depth picture of Childbirth Survival International, the amazing work the team is doing, and how you can partner to make a difference. For more information, visit www.childbirthsurvivalinternational.com

  0 0

   Waraghbishi toka vijiji vya Iponya, Nyakasumula, Bukandwe na Shenda wakiwa katika pichaya pamoja na mwenyekiti na mtendaji wa kijiji cha Shenda.

  Ni miaka mitatu na miezi nane toka mraghbishi Fedson Yaida na wenzake toka vijiji vya jirani kukutana na Chukua Hatua. Ni rafiki waliyekutana naye mwaka 2011 katika mazungumzo maalumu ambayo walitakiwa kuyafikisha kwa wananchi wenzao wa vijiji vya Shenda, Iponya, Nyakasumula na Bukandwe katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita. 

   Ni katika mazungumzo hayo ya siku tatu, ambayo Fedson toka kijiji cha Shenda alibadilishwa na kuwa mraghbishi wa aling’amua uwezo alio nao katika kusimamia rasilimali za kijiji chao, suala ni angezisimamiaje wakati yeye si  kiongozi na ni jukumu la wanakijiji wote. Katika mazungumzo hayo rafiki yao, Chukua Hatua aliwaambia, “Ni jukumu lako Fedson na waraghbishi wengine mliopo hapa, ni jukumu lenu la msingi kuj i t aj i r i sha kwa taarifa na maarifa.

   Kwa kufanya hivyo mtakuwa na uwezo wa kujenga hoja mkizithibithisha na vielelezo. Hivyo ni jukumu lenu kujua ni wapi na toka kwa nani mtapata taarifa na vielelezo vya hoja yenu. Uzito wa hoja na maelezo kwa uthibitisho ni silaha muhimu kama mnataka kushawishi wenz e n u  k u c h u k u a hatua.”    Baada ya maelezo hayo walitakiwa kwenda kutembelea halmashauri ya wilaya yao, wakati huo ikiitwa Bukombe. Na baadhi ya maeneo hayo ni ofisi za Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Halmashauri. Maelezo haya yalilenga katika haki ya kupata taarifa, kwa mujibu wa ibara ya 18 ya Katiba.

  “Kweli mazungumzo hayo yalinijengea uwezo mkubwa sana, Chukua Hatua alinipatia muongozo na akanipangia kwenda kwa mkuu wa wilaya. Moja kwa moja nikaonana na DC nikaanza kumuhoji mambo mbalimbali kuhusu pembejeo. Ingawa majibu aliyonipa sikuridhika nayo, lakini nilishukuru kupata nafasi ya kuongea naye. Na kwa kweli tokea siku hiyo nikawa na ujasiri mkubwa sana,” Fedson Yaida akitoa ushuhuda wa siku ambayo uoga ulimtoka.

  Ujasiri huo wenye msukumo wa ndani toka kwa mraghbishi mmoja kwenda kwa wenzake kwa njia ya kuwashirikisha aliyopatiwa na Chukua Hatua, ndio umekuwa chanzo kikubwa cha mafanikio ya pamoja ya wana Shenda katika kusimamia rasilimali zao. Safari ya mwandishi katika kijiji cha Shenda ilimtia moyo sana. Alikutana na waraghbishi toka vijiji vya Shenda, Ipoja, na Buluhe. Mkusanyiko huu ulikuwa na watu wa kada mbalimbali; walimu, wajumbe wa serikali ya kijiji, wazee, na wakulima. 

  Aliwakuta wakiwa pamoja na Mwenyekiti na Mtendaji wa kijiji chao. Na wote kwa pamoja walikuwa wanazungumzia mustakabali wa maendeleo ya kijiji chao. Na kwa haraka aligundua wote wamekuwa waraghabishi, akajiuliza aliyekutana na Chukua Hatua alikuwa mmoja, lakini sasa wapo kwa makundi na wote wanajitambulisha kama waraghbishi.  Hamu na shauku yao ya kutaka kusimamia rasilimali zao ndio imekuwa nguzo kubwa ya wao kuweza kufuatilia matumizi ya vyanzo vya mapato ya kijiji chao. 

  Ni miaka miwili imepita toka wananchi hao wautoe uongozi wa kijiji madarakani kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha. Kwa pamoja waliongozana na mwenyekiti wao pamoja na mtendaji wa kijiji na mpaka ofisi ya kata na kuwakabidhi kwa polisi. Ubadhirifu huo ulithibitishwa na taarifa ya ukaguzi, iliyoonyesha upotevu wa kiasi cha shilingi milioni mbili laki tisa na elfu hamsini (2,950,000/-). Taarifa hiyo ilisomwa katika mkutano wa hadhara na viongozi kutakiwa kulipa pesa hizo ambazo walizirudisha.

  Baada ya hapo walichagua uongozi mpya; mwenyekiti na halmashauri ya serikali ya kijiji na Mkurugenzi wa wilaya akawaletea mtendaji mpya wa kijiji. Na huo ndio ukawa mwanzo mpya wa safari ya uraghbishi katika kijiji hicho. Vuguvugu hilo la mapinduzi liliongozwa na waraghbishi wapya waliowezeshwa na Fedson wakisaidiana na rafiki yake wa karibu Abdu Haridi ambaye pia ni mraghbishi.  

   Habari ya kutolewa madarakani kwa uongozi wa kijiji hicho ilirushwa pia na redio ya Kahama FM na kupelekea mkuu wa wilaya kumtuma mwakilishi wake akaongee na wananchi wa kijiji cha Shenda. Uungwaji mkono huu na Mkuu waWilaya ni dalili kwamba yupo tayari kufanya
  kazi na wananchi wa kijiji cha Shenda. Yeye ni kiongozi wao na dhahiri anawajibika kwao kama ambavyo kiongozi yeyote anayejali watu wake angefanya.   Kwa sasa wanashirikiana kwa pamoja na uongozi mpya na mwandishi alithibitisha hivyo kwa kuwa alipata fursa ya   K a m a mwanzo mpya, wamekubal i ana kufanya ujenzi wa ofisi mpya ya kijiji. 

  K wa n z a  wa meanza na ujenzi wa zahanati kwa k u k a m i l i s h a msingi wake. Na wananchi wamekubali kuchangia, kila kaya matofali 50 na wengine w a m e c h a n g i a mawe. Uhai umerudi tena na kila mtu ana shauku ya kufanikisha ujenzi huo. Lakinisi hivyo tu wanataka kukamilisha pia na ujenzi wa zahanati ya kijiji. Haya yote yakiwa ni matunda ya ushirikiano kati ya uongozi wa kijiji na waraghbishi na  wanakijiji wote kwa ujumla.

    “Tumekaa muda mrefu sana bila zahanati hasa kwa ajili ya kina mama. Ni kilometa tano kutoka hapa mpaka zahanati ya jirani. Na kijiji chetu kama unavyokijua, hakina teksi, labda tumbebe kwa tela la ng’ombe au punda kama huna baiskeli. Tukajiuliza kwanini tusiiambie serikali yetu tujenge zahanati hapa karibu,”anafafanua Abdi Haridi.  Lakini si hivyo tu Mwenyekiti ameshahamasisha kila mwananchi achangie mawe, achangie matofali. Kwa sasa wameonela kumalizia kabisa ofisi yao ya kijiji. Ya sasa ipo katika hali mbaya harufu ya kinyesi cha popo na jengo lenyewe lina nyufa ikinyesha mvua kubwa itakuwa ni shida inaweza hata kuanguka na hapa ndio makao makuu ya kijiji.

   Kwa hiyo nguvu zao sasa ni kukamilisha hii ofisi afu ndio waendelee na zahanati ya kina mama.  Mazungumzo hayo na Chukua Hatua yalifanyika katika mfumo wa mafunzo  yaliwawezesha waraghbishi toka vijiji vya Ipoja, Shenda, Buluha na Nyakasaluma kuanza kufuatilia na kuhamasisha wengine kufanya hivyo pia.   Si kitu kirahisi sana kuwa mraghbishi, kunahitaji kujiamini, kujitambua na moyo wa kujitolea pia..  Katika kijiji cha Nyakasaluma wananchi walihamasishwa na uongozi wao kuchangia pesa kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati na kwa kweli walichangia kila kaya ilitoa kiasi cha shilingi za kitanzania elfu saba mia tano.

   Swali la kujiuliza michango ya maendeleo ya namna hii, inaamuliwaje? Wananchi wanahusishwaje? Je, wamefanya utambuzi wa watu/kaya/familia uwezo walio nao? Kwa mujibu wa mraghabishi Patrick Matagale ujenzi ulianza lakini ghafla ukasimama na walipofuatilia ikaonekana kwamba ujenzi hautaendelea kwa madai kwamba mwekezaji wa kijiji atamalizia na wananchi pesa wameshachangia.   “Sasa ilikuwa ni kuhoji tu kuhusu ile pesa iliyochangwa na wananchi”, anasimulia mraghbishi Patrick.   

  Uaminifu ni silaha kubwa ya uongozi imara, na mara watu wanaposhindwa kukuamini kama kiongozi, huamua kuchukua njia yao ya kutokukupa dhamana ya kuwaongoza,   “Hivyo tulichoamua kufanya kwa sasa ni kwamba hatutachangia tena pesa na badala yake tunahamasisha watu kuchangia vitu badala ya pesa, kama walivyofanya wenzetu wa Shenda. Mwenye mawe, matofali, mbao na chochote kile alete,” anafafanua mraghbishi Patrick Matagale toka kijiji cha Nyakasaluma.   Katika kijiji cha Iponya, suala
  lililoibuka ni michango wanayochangishwa wananchi. Ambapo kila kaya imetakiwa kuchangia kiasi cha shilingi za kitazania elfu sita (6,000/) kwa ajili ya mradi wa maji wa visima virefu. Mradi huu unafadhiliwa na benki ya dunia na una thamani ya shilingi za kitanzania milioni 221/-

  Hivyo wananchi nao wametakiwa kuunga mkono juhudi hizo kwa kuchangia pia gharama za ujenzi huo na wananchi walikubali bila kusita na kwa ujumla wao walichangia kiasi cha shilingi za kitanzania milioni tatu (3,000,000/-).  “Cha kushangaza wananchi wameshachanga hela zao, ila mpaka muda huu naongea hakuna ambacho kimeshafanyika. Lakini kwenye muhadhara tulidanganywa kwamba mradi ukishaanza Shenda na sisi pia tutaanza kufaidika, mpaka dakika hii hakuna maji,” anafafanua Thomas Mlekwa toka katika kijiji cha Iponya.  

   Wananchi wakawa wanataka kujua nini kimetokea baada ya wao kuchanga, kama anavyosimulia mwana mama Leornada Mathias toka kijiji cha Ipoja, “Ilikuwa mishe mishe kweli, kila siku mwenyekiti anapita katika kaya anahamasisha watu wachangie ili tuondokane na tatizo la maji. Ni kweli tuliitikia tukatoa michango na tuliambiwa tukichelewa tu huu mradi unatupita. Tukafungua akaunti na fedha zikawekwa. Baada ya hapo tukaona  kimya kabisa.”  Katika mikutano ya hadhara ya kijiji iliyofanyika hapo wananchi walitaka kujua nini kimetokea kwani fedha tayari kiasi cha shilingi za kitanzania milioni tatu zimeshawekwa benki. 

  “Kwenye mkutano watu wakataka kujua meza imekuwaje tuliambiwa Shenda wakipata  maji na sisi pia, mbona tayari kwa wenzetu yapo. Ndio tukaja kujua kwamba hakuna mradi wa maji. Na badala yake viongozi wanatuambia kwamba ile fedha wanaanza kuisoma kwenye mapato na matumizi,” anaendelea kufafanua Leornada.  Na katika muda huo wakaambiwa kwamba tayari laki nne zimeshatumika kutokana na makato ya gharama za kuendesha akaunti. Kwa hiyo uendeshaji wa akaunti umekula mpaka sasa kiasi cha milioni mbili na laki tatu zimebaki laki saba tu. Hapa pana kazi kubwa ya kufanya.  

   Pamoja na Shenda kuonekana kwamba kwao maji yameshaanza kutoka katika mabomba, bado kuna changamoto nyingi za kuwezesha kukamilika kwa mradi huo wa maji. Na waraghbishi wapo mstari wa mbele kufuatilia nini kinachoendelea kwenye mradi huo. Ni mradi ambao waliomba wapatiwe na utekelezaji wake umeshaanza ingawa baadhi ya maeneo bado hawapati maji.   “Mradi huu wa maji ni sawa na hakuna. Sisi wananchi wa Shenda tumechangia nguvu zetu. Tumechangia asilimia yetu tuliyoambiwa na serikali. Serikali ikachangia asilimia yake, ina maana kilikuwa ni kisima tu cha vitongoji vine vya kijiji chetu. Tuna tenki lile pale limeshakamilishwa.  Mashine ipo kule kwenye chanzo cha maji. Italike kule, lakini kijiji kizima kuna gati nane tu. Kuna vitongoji vingine havina gati. Kitongoji kizima kinapewa gati moja ebu niambie kitakidhi wangapi?” anauliza Abdi Haridi mraghbishi wa Shenda.

  Gati zilizopo Shenda zinatokana na waraghbishi na wananchi kufuatilia suala hilo kwa karibu. Kwa sababu ni kitu walichokiomba wapatiwe na serikali. Baadhi ya vitongoji vya kijiji hicho vimetenganishwa na barabara. Hivyo wametaarifiwa kwamba gati haiwezi kuvuka barabara. Ili hali kwa baadhi ya viongozi wao gati imevuka barabara,” mraghbishi Abdi anauliza,  “Lakini ukienda pale makao makuu ya kata pale unakuta gati imewekwa kwa kiongozi. Nikauliza swali pale mbona kule Shenda tumeambiwa gati haiwezi kukata barabara ndio maana wananchi wa upande wa pili wa kijiji hawapati maji. Imekuwaje kwa kiongozi imekata barabara na kuingia mpaka mgongoni mwa nyumba yake? Barabara ile ile niliyoambiwa gati haiwezi kukatiza ndio hiyo hiyo imetumiwa kukatiza gati.” Kaloras Majura, mraghbishi kutoka kijiji cha Bukandwe kutoka kata yenye jina hilo hilo la Bukandwe, pamoja na kwamba yeye ni mraghbishi lakini pia alikuwa ni mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi ya kijiji chao.  

   “Changamoto niliyoanza nayo ilikuwa ni pale shule, nilipogundua kwamba mwalimu mkuu anaitisha michango, bila kuwashirikisha wazazi. Pamoja na nafasi niliyokuwa nayo lakini pia nilikuwa natoa elimu kwa wananchi. Nikajengewa kampeni na kufanyiwa uhasama na  mwisho wa siku nikaambiwa nafasi ya uenyekiti hainifai, kwa sababu natoa siri. Hivyo nimebaki mjumbe tu,” katika hali ya upole anaelezea mraghbishi Majura.   

  Suala lingine ambalo limejitokeza ni kuhusu mganga wa zahanati ya kijiji cha Bukandwe, ambaye alikuwa akiwachangisha wananchi kiasi cha shilingi za kitanzania elfu kumi (10,000/-) za mfuko wa afya. Alichokuwa akifanya wakati anawaandikia alikuwa akiweka kumbukumbu tofauti za mwaka.   

  “Kama mtu katoa hela mwaka huu yeye anamuandikia katoa mwaka 2012 na wengine mwaka 2013. Baada ya muda akawa amehamishwa sasa watu wanapokwenda pale zahanati wanaambiwa kwamba wewe muda umeshakwisha ulitoa mwaka juzi hivyo uanze upya,” anasimulia Majura  Kutokana na nafasi yake ya uraghbishi Majura ameweza kukaa na kamati ya kijiji ya afya. Na ameishawishi kamati kuwasiliana na watu waliolipa kuandaa vielelezo vyao na kufanya mawasiliano na mganga mkuu wa wilaya, ili waweze kujua wanachukua hatua gani kuhusu huyo mganga. Lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha kwamba wananchi wanarudishiwa fedha zao walizochanga.

  Si kitu kirahisi sana pia kufanya uraghbishi kwa sababu mara kadhaa waraghbishi wamekuwa wakitishiwa tishiwa ili wasiulize ulize maswali na kuhamasisha wananchi , lakini  bado mambo yameendelea.  “Sisi waraghbishi tunapata muda mgumu sana tunakutana na watu tofauti na viongozi tofauti. Tunatishiwa amani, ila na sisi tutapambana kama tulivyokwisha kupambana mpaka dakika ya mwisho ili haki yetu ipatikane. 

  Tukianza kuyatafuta mashirika ili tushirikiane nayo katika kuweka mambo sawa, kama hivi. Tayari tunaonekana siye wabaya kwa wale viongozi wa juu. Kwamba sisi tunawapondea wale. Basi sisi tunaomba waje wale wakubwa zaidi, waje watuulizie nini kinaendelea ili tuwaambie ukweli,” anaeleza kwa kujiamini mraghbishi Abdi Haridi wa Shenda.    

   Harakati hizi zinaungwa mkono na mwenyekiti wa kijiji cha Shenda, Masumbuko Kwileka, kama anavyosema kuhusu warghabishi,  “Kila siku waraghbishi tunao hapa. Fedson huwa anakujaga hapa wanazunguka huko na kijana wake huyu hapa Haridi. Wanapita vijiji hadi vijiji wanahamasisha.Hivyo waraghbishi wana hamasa hata mwenyekiti ajaye atakayekuja watakuwa msaada kwake. 

  Manake watamuuliza tu sasa mkuu unakwendaje hapa na itabidi uwaeleze mambo yanakwendaje. Hivyo mnapopata pesa ni lazima umuelezee mraghbishi zinavyokwenda.”  Ni mwaka sasa umepita toka shuguli za Chukua Hatua zisimame kwa muda, ila cha kufurahisha ni waraghbishi wameendelea na harakati za kujiletea maendeleo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali hasa wananchi wenzao. Na si hivyo tu wameendelea kuwatengeneza waraghbishi wengine ambao na wanaendeleza harakati za kuleta maendeleo.  0 0  0 0

  Zaidi ya nusu ya mama wajawazito waishio vijijini mkoani Tabora hukimbilia kwa waganga wa jadi na kuacha kuhudhuria kliniki.


older | 1 | .... | 724 | 725 | (Page 726) | 727 | 728 | .... | 1898 | newer