Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 723 | 724 | (Page 725) | 726 | 727 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mshambuliaji wa Yanga, Deus Kaseke akichuana na beki wa Mbeya City, John Kabanda  katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga imeshinda 3-0. (Picha na Francis Dande).
   Mshambuliaji wa Yanga, Deus Kaseke akiwatoka mabeki wa Mbeya City.
   Wachezaji wa Mbeya City wakimzonga mwamuzi Jeonesia Rukyaa kutoka Kagera baada ya Yanga kupata bao la kwanza.
   Sio goli.............
   Kocha wa Yanga, Hans Pluijm akitoka wakati wa mapumziko.

  Mashabiki wa Mbeya City.
   Polisi wakituliza fujo zilizotokea katika jukwaa la Mbeya City.
   Donald Ngoma wa Yanga akichuana na Haruna Shamte.
   Amis Tambwe wa Yanga akishangilia bao la pili aliloifungia timu yake.
   Thaban Kamusoko (katikati) akishangilia na Deus Kaseke na Simon Msuva.
   Wakishangilia kwa staili ya aina yake.
   Deus Kaseke wa Yanga akiwania mpira na mchezaji wa Mbeya City.
   Hatari....
   Mashabiki wa Mbeya Cuty wakiwa wameduwaa wakishuhudia timu yao ikipata kipigo kutoka kwa Yanga.

  0 0


  Mraghabishi mwalimu Revocatus Renatus ( kulia ) wa kijiji cha Unyanyembe mkoani Shinyanga akihojiwa na mtangazaji wa Redio Free Africa Felista Kujirilwa wakati wa kuandaa moja ya vipindi vya redio vya Chukua Hatua.

  “Haijatokea hata siku moja mwandishi wa habari akaja huku kwa kweli. Hii ni mara yangu yakwanza kuona wanahabari katika kijiji chetu. Toka nimezaliwa sijawahi kumuona mwandishi wa habari kuja hapa na mimi nina miaka 70.” Hayo ni maneno ya Mzee Titus Ndugulile mraghabishi wa kijiji cha Mwamala-B kilichopo kata ya Mwamala wilaya ya Shinyanga vijijini.

  Kijiji hicho kina wakazi wanaokaribia 2,820 toka katika vitingoji vya Mwanundi, Igegu, Witasisa na Wela. Yeye ni mmoja kati ya waraghabishi 400 waliosambaa katika vijiji zaidi 180 vilivyopo katika mikoa ya Geita, Simiyu, na Shinyanga. Kundi hili la waraghabishi linawajumuisha wakulima, viongozi wa dini, madiwani, wenyeviti wa vijiji, walimu, wanafunzi, wanawake viongozi na wafugaji wanaofanya kazi na programu ya redio ya Chukua Hatua inayorushwa na redio Kahama FM, Faraja FM, na Radio Free Afrika.

  Redio hizi zimeanza kufanya kazi na Chukua Hatua kuanzia mwezi Novemba 2012 zikiwa nalengo la kutoa fursa na nafasi kwa waraghabishi kuwakilisha mawazo, shida na vipaumbele vyao kwa viongozi ili waweze kusikiliza kero zao na kuzifanyia kazi. Lakini pia kuongeza wigo wa vyanzo vipya vya habari kwa vyombo hivyo. Waandishi hawa walitambulishwa


  Kwa waraghabishi kupitia mafunzo, ziara za ufuatiliaji na uwezeshwaji wa wananchi katika


  kung’amua matatizo yao na kupendekeza njia ya kuyatatua. Mafunzo na ziara hizi zilikuwa zinafanywa mashirika ya ADLG na CABUIPA ambao ni washirika watekelezaji wa programu ya Chukua Hatua katika maana ya uwezeshaji wananchi. Matukio haya ya mafunzo na ZA `WWW3ziara ndio njia ya kwanza iliyotumika kuwatambulisha na kuwakutanisha waandishi na waraghabishi katika vijiji wanavyotoka. “ Huku ni l i k uwa si j awahi kufika ni mara yangu ya kwanza na kiukweli watu wamefunguka sana kuhusu matatizo yao.  Kila mtu anataka kuongea nasi mambo ni mengi na watu wanahamu ya kupaza sauti z a o n a wa n a t a k a k u s i k i k a , ”anafafanua mtangazaji wa Redio Free Afrika Felista Kujirilwa baada ya kutembelea kijiji cha Mwambasha mkoani Shinyanga. Waraghabishi hawa wamepatiwamafunzo yaliyowawezesha kutambua haki na majukumu yao katika kuleta mabadiliko ya kweli katika jamii zao. Wameweza pia kuchukua hatua mbalimbali kwa kushirikiana na wanajamii wengine katika maeneo wanayotoka ila walikuwa wanakosa sehemu ambayo wangeweza kupaza sauti zao zaidi tukiacha mikutano ya vijiji na kwenye midahalo wanayoiandaa. Hivyo redio hizi zimeweza kutoa nafasi kwa waraghabishi nasauti zao zinasikika na viongozi wao wanasikia na kuchukua hatua stahiki. Kama anavyoelezea mtangazaji wa Kahama FM William Bundala ambaye pia anajulikana kama Kijukuu na wasikilizaji wake. “Baada ya kutoa taarifa za nyumba kupata nyufa kubwa kutokana na milipuko ya baruti inayolipuliwa kwenye mgodi wa Buzwagi unaomilikiwa na kampuni ya Barrick, mkuu wa wilaya ya Kahama ameunda kamati maalumu ya kufuatilia suala hilo ili kuweza kulitolea maamuzi. Tunaendelea kufuatilia kujua nini kitatokea, kubwa ikiwa ni kulipwa fidia kwa wale ambao nyumba zao zimeharibika.”

  Lengo mojawapo la program ya redio ya Chukua Hatua ni kuhakikisha kwamba viongozi na wenye dhamana wanachukua hatua kwa kusikiliza matakwa ya wananchi. “Tunawashukuru sana waandishi wa Kahama FM na hasa Kijukuu kwa kazi nzuri wanayoifanya. Kama wasingekuja hapa sidhani hata kama mkuu wa wilaya angeweza kumtuma mwakilishi wake kuja zungumza nasi. Tutaendelea kuitumia redio hii mpaka pale haki itapotendeka kwa viongozi wetu,” anaelezea Halid Abdu mkazi wa kijiji cha Shenda wilaya ya Gombwe mkoani Geita. Hii ilikuwa baada ya redio Kahama FM kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mkutano wa kijiji ulioamua kuwatoa viongozi wa kijiji kwa tuhuma za kutumia vibaya fedha zinazotokana na vitega uchumi vya kijiji; ikiwamo makrasha, wachimbaji wadogo wadogo na malori yanayobeba mchanga katika mgodi mdogo unaomilikiwa na kiijiji hicho cha Shenda. Baada ya habari hiyo kurushwa redioni mkuu wa wilaya alilazimika kumtuma Mkurugenzi wake kwenda katika kijiji hicho ili kuongea na wananchi kuhusu kilio chao. Makutano haya baina ya waandishi wa habari na waraghabishi

  Haya yamewezesha redio kupata vipindi mbalimbali nje ya mambo ya Chukua Hatua. “Hapa pana stori nyingi tofauti za kufanya, tumeongea na huyu binti, maskini kumbe ameambukizwa virusi vya ukimwi na ametueleza mambo mengi yanayotokea pale njia panda ya Tinde. Inabidi tufike hapo ili tufanye kipindi cha TV kuhusu tatizo la Ukimwi na jinsi mabinti wanavyojiuza,” anaelezea Regina Mwalekwa wa kituo cha TV cha Clouds alipotembelea kijiji cha Kitule. Si hivyo tu vipindi vingine vinatumika katika taarifa za habari na hasa mafunzo ya waraghabishihasa ya viongozi wa dini, lakini pia waandishi wa redio hizi wangeweza kurekodi sauti za wanawake pia kwa ajili ya vipindi vya wanaawake na maendeleo


  Lakini pia kuna taarifa ya habari baadhi ya matukio ambayo waraghabi shi wameweza kuyaelezea yametumika katika habari na zinasomwa redioni mfano tukio la wananchi wa kata ya Dutwa kuiomba serikali kupitia wizara ya Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi kutoa semina juu ya sheria za ardhi kwa mabaraza ya ardhi vijijini ili kupunguza migogoro ya ardhi inayosababisha vifo. Habari hiyo iliyotumika June 6 2013 saa kumi kamili jioni na saa tatu usiku iliandikwa na mwaandaaji wa vipindi vya Chukua Hatua wa redio Kahama FM William Bundala. Ambapo mmoja wa wanakijiji hao Masalu Lugodisha, wa mjini Bariadi amesema, kutokana Jumuia ya Afrika

  Mashariki kuungana, thamani ya ardhi itakuwa kubwa hivyo ni bora serikali ikalijua hilo mapema na kuanza kuepusha migogoro kwa wananchi. Mpaka jumla ya vipindi 53 vimerushwa na redio hii vikiwamo vipindi 5 vya TV katika kituo cha Clouds. Huku wasanii wa Chukua Hatua toka katika wilaya za Maswa, Kahama na Shinyanga vijijini wakijiandaa kuigiza vipindi vya redio baada ya kumaliza mafunzo yao mwezi wa Juni 2013. Lakini si hilo tu madiwani wa kata za wilaya ya Bariadi wamenufaika na vipindi hivi kwa kuelezea mambo waliyoyafanya katika maeneo yao ikiwamo kupata mrejesho toka wa wapiga kura wao ni kwa kiasi gani wameweza kutimiza ahadi zao na hivyo kujiwekea mazingira mazuri ya kuchaguliwa tena.

  Walimu waraghabishi nao wameweza kuelezea mikakati na jinsi wanavyofanya kazi na wanajamii katika kujikomboa na ujinga. Mfano mzuri ni waraghabishi walimu wa wilaya ya Kishapu na hasa kata ya Uchunga. Kwa sasa programu hii ina waraghabishi zaidi ya 350. Akishangaa jinsi program ya Chukua Hatua inavyozidi kukua mmoja Wa waraghabishi waanzilishi wa mwaka 2010, Titusi Ndugulile wa kijiji cha Mwamala B mkoani Shinyanga alisema,
  “Yaani siamini kama hiki kitu kimekuwa hivi aisee. Nakumbuka siku ile tulikutana pale kempasi ya Chuo Kikuu cha Ushirika tulikuwa watu 12 tu, lakini leo limekuwa dude kubwa kabisa. Na waandishi wa habari nao wanatutembelea wanatuhoji, wanaturekodi kwenye haya mashikolo mageni yao.


  0 0

  IMG_1255 
   Video Queen anayefanya pia filamu, Asha Salum ‘Kidoa’ akiwa na tuzo yake ya Ijumaa Sexiest Girl 2015 baada ya kuwafunika Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Vanessa Mdee ‘Vee ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala- Zakhem jijini Dar.IMG_1250 Kidoa (katikati) akiwasalimia mashabiki baada ya kutangazwa mshindi wa Ijumaa Sexiest Girl 2015.IMG_1252...Akilia kwa furaha.IMG_7945Kidoa akikabidhiwa tuzo na Mkurugenzi wa Hamadombe Distributor, Fatuma Makame.IMG_1232rt...Akibusu tuzo. IMG_1260Akiwa katika picha ya pamoja na mratibu wa shindano hilo lililodhaminiwa na kampuni ya uandaaji na usambazaji wa filamu ya Hamadombe Distributor, Amran Kaima (kulia).
  IMG_1266...Akiwa na tuzo na cheti baada ya kukabidhiwa.
  IMG_1232Amrani Kaima akiongea jambo.
  IMG_1311Mshindi wa Ijumaa Sexiest Girl 2015, Kidoa akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Gazeti hilo.

  Mwandishi wetu Fainali ya lile Shindano la Ijumaa Sexiest Girl 2015 ilifanyika jana ambapo Video Queen anayefanya pia filamu, Asha Salum ‘Kidoa’ aliibuka kidedea. Kidoa alitangazwa mshindi kufuatia kupigiwa kura nyingi na wasomaji wa Gazeti la Ijumaa hivyo kuwafunika wenzake, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Vanessa Mdee ‘Vee Money’. 

  Akizungumza na Risasi, mratibu wa shindano hilo lililodhaminiwa na kampuni ya uandaaji na usambazaji wa filamu ya Hamadombe Distributor, Amran Kaima alisema kuwa, ushindani ulikuwa mkubwa kwani wasanii wote walioshiriki walikuwa wakali ile mbaya. “Kidoa amefanikiwa kuibuka mshindi baada ya kupigiwa kura nyingi. Atapokea tuzo, cheti pia atapewa ofa ya kutengeneza nywele kwenye saluni ya Bulldozer iliyopo Kigamboni jijini Dar kwa miezi sita pamoja na kufanyiwa shopping ya nguvu,” alisema Amran.
  (PICHA NA RICHARD BUKOS NA MUSA MATEJA/GPL)

  0 0

  Mwana FA akiimbaKulikuwa na muziki poa kutoka kwa Dj
  Madam Ritha Paulsen akiwa na Mwana FA pamoja na Mmiliki wa Oasis Baa, Nuru mosha.


  Mheshimiwa Zitto pia alikuwapo
  Akiendelea kuimba huku akiwa na chupa yake ya Hennessy

  Wageni waliojumuika pamoja siku hiyo.

  MWANAMUZIKI mahiri wa muziki wa Hip Hop nchini, Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana Fa amezikonga nyoyo za mashabiki wake kwenye hafla ya kuadhimisha miaka 250 ya kinywaji cha Hennessy yaliyofanyika katika baa ya Oasis Masaki.

  Mwana Fa alianza kuimba majira ya saa nne ambapo alianza kwa kuimba nyimbo zake mbalimbali zilizowahi kutamba kama vile, Mimi na Mabinti pamoja na nyinginezo za zamani.

  Baada ya kumaliza nyimbo hizo za miaka ya nyuma akaanza kuimba nyimbo zake za sasa ukiwamo ule wa Mfalme na nyinginezo mpya.

  Watu wengi walihudhuria hafla hiyo ya maadhimisho ya kinywaji hicho iliyoenda sambamba na maonesho ya michoro mbalimbali kuhusianana historia ya kinywjai hicho ambacho asili yake ni Ufaransa.

  Pia watoa burudani mbalimbali kama vile kundi la Mosaic Collective pamoja na Mac Band walitoa burudani.

  Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa maadhimisho hayo, mratibu wa maadhimisho hayo ambae pia ni mmiliki wa baa ya Oasis Nuru Mosha alisema kuwa kinywaji hicho kimekuwa karibu zaidi na sanaa ya Tanzania kwa ujumla mbali na kufanya biashara.

  Mosha alisema kuwa kwa kuwa mwanzilishi wa kinywaji hicho alikuwa ni mtu mpenda sanaa hasa aiwa anajishughulisha na sanaa ya uchoraji na hivyo wageni wanaotembelea michoro hiyo wanapata kufahamu kiundani zaidi historia ya kinywaji pia.
  Chupa ya Hennessy 250 Collectors blend iliyotengenezwa maalum kusherekea miaka 250 ya kinywaji hicho.
  Kwa ndani kulikuwa na eneo lilikowekwa picha mbalimbali kuhusiana na historia ya kinywaji hicho

  0 0

   Wakazi wa Kahe wakifatilia tamasha la Halo Xmas katika Wilaya ya Kahe
   Msanii Msami akiburudisha wanakijiji wa Kahe katika tamasha la Halo Xmas
  Msanii Shilole akiimba wakati wa tamasha la Halo Xmas lililofanyika wilaya ya Kahe.
   Wakazi wa Ruangwa wakifuatilia burudani ya tamasha la Halo Xmas lililofanyika katika uwanja shule ya msingi Likangala.
   

  Matamasha ya Halotel yafunika nchi nzima

  Matamasha ya Halo Xmass yaliyoandaliwa na kampuni ya Halotel katika mikoa mitano nchini yamefunika kwa kutoa burudani nzuri na kupata mahudhurio makubwa ya mashabiki.

  Matamasha hayo ambayo yamefanyika wilaya za Tukuyu, Ruangwa, Moshi Vijijini, Chato pamoja na Mpwapwa, yamejumuisha wasanii wa bongo fleva pamoja na burudani nyingine kutoka kwa wasanii wa maeneo hayo.

  Tamasha la Halo Christmass wilayani Tukuyu limefanyika katika uwanja wa Tandale na burudani imetolewa na wasanii Tundaman na Makomando.

  Kwa upande wa Ruangwa, tamasha limefanyika katika viwanja vya shule ya msingi Likangala, na kutumbuizwa na wasanii Amini pamoja na Matonya, wakati Mpwapwa tamasha limefanyika katika viwanja vya Mgambo likitumbuizwa na wasanii Madee na Malaika.

  Wakazi wa Chato pia wamepata burudani ya kufunga mwaka katika viwanja vya Stand ya Zamani kutoka kwa msanii Shetta na Baraka Da Prince.

  Moshi vijijini pia wamefurahia tamasha la Christmass kwa burudani kutoka kwa Shilole na Msami zilzofanyika katika viwanja vya Kaye.

  Baadhi ya mashabiki waliohudhuria tamasha hilo Moshi wameipongeza Halotel kwa kuwaandalia tamasha hilo wakisema hii ni mara ya kwanza burudani kubwa imefika kijijini kwao.

  ‘Makampuni mengi hupenda kufanya matamasha ya aina hii mijini, lakini kwa Halotel ni tofauti, kama namna huduma zao zilivyo za kipekee’ alisema Bi Halima Sanare, mkazi wa kijiji cha Kaye.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Halotel bwana Nguyen Thanh Quang, amesema matamasha hayo ya Halotel yalilenga kuwaleta watumiaji wa Halotel pamoja na kuwapa burudani ya kufunga mwaka.

  ‘Hii ni zawadi kwa watumiaji wa mtandao wetu na wateja wapya wanaotaka kujiunga na familia yetu ya Halotel, na ndio maana tunawafata katika maeneo yao yalipo’ alisema Quang.

  Quang pia amewaahidi wateja wa Halotel kuwa mtandao wake unatarajia kuleta mabadiliko katika sekta ya mawasiliano nchini kwa kuwapa wateja wake zaidi ya huduma za simu.
  Msanii Sheta akiimba na mtoto katika tamasha la Halo Xmas lililofanyika uwanja wa stendi ya zamani Chato.
   Madee akiburudisha mashabiki wa Mpwapwa katika uwanja wa Mgambo
   Msanii Matonya akiimba katika uwanja wa Ruangwa wakati wa tamasha la Halo Xmas.
   Baraka Da Prince akiimba wakati wa tamasha la Halo Xmas mjini Chato


  0 0

  Mdau Edwini Mjwahuzi akimvisha pete Mkewe Bi. Hildegarda Mashauri, wakati wa Ibada ya Ndoa yao iliyofanyika kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph, Jijini Dar es salaam leo.
   Mdau Edwini Mjwahuzi na Mkewe Bi. Hildegarda Mashauri wakiwa ni wenye furaha tele mara baada ya kufunga pingu za maisha na kuwa mwili mmoja, kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph, Jijini Dar es salaam leo.
   Mdau Edwini Mjwahuzi ambaye ni Mpiga picha wa Magazeti ya Kampuni ya Mwananchi, jioni ya leo ameamua kuvunja kibanda cha Makapera na kukimbilia kwenye Mjengo wa wanandoa, kwa kufunga pingu za maisha na Bi. Hildegarda Mashauri kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph, Jijini Dar es salaam.
    Mdau Edwini Mjwahuzi na Mkewe Bi. Hildegarda Mashauri pamoja na Wasimamizi wao wakiwa kwenye ibada ya ndoa, iliyofanyika jioni ya leo kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph, Jijini Dar es salaam.  0 0

   Benchi la ufundi la timu ya Azam FC.
   Benchi la ufundi la Kagera Sugar.
   Wachezaji wa Azam FC wakishangilia bao la kwanza la timu yao katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar uliofanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex. Azam imeshinda 2-0. (Picha na Francis Dande)
   Kavumbagu akichuana na beki wa Kagera Sugar, Shaban Ibrahim.
   Didier Kavumbagu akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Kagera Sugar, Shaban Ibrahim.
   Shaban Ibrahim akimshika bukta Didier Kavumbagu.
   Uniwezi.....
   Kavumbagu akimtoka Shaban Ibrahim.
   Shaban Ibrahim akienda chini.
   Mshambuliaji wa Azam FC, Didier Kavumbagu akimtoka beki wa Kagera Sugar, Shaban Ibrahim.
  Mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco (kulia) akichuana na beki wa Kagera Sugar, Shaban Ibrahim katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam. Azam ilishinda 2-0.
  Golikipa wa Kagera Sugar, Agathony Antony akiokoa moja ya hatari langoni mwake.

  0 0

  Hashim Kambi ni msanii wa filamu nchini Tanzania.
  Alikuwa mkarimu sana kupita studio zetu za Kilimanjaro hapa Beltsville Maryland na kuzungumza nasi


  0 0

   Muda wa maanjumati ulifika na wateja pamoja na wafanyakazi wa Kupatana.com walijumuika katika mlo huo. 
   Wafanyakazi wa Kupatana.com na wateja wao walikula na kunywa
  Burudani ya mziki ilikuwepo ya kukata na shoka.
  **************
  Kupatana.com ni website ya matangazo madogo madogo ya bidhaa mbalimbali kutoka kwa wauzaji hapa Tanzania. Website hii ilianzishwa rasmi mnamo mwaka 2013 ambapo wakati wa kuanzishwa kwake ilikuwa ikitembelewa na watu takriban elfu tatu kila siku.


  Dhumuni la website ya Kupatana.com ni kuwezesha upatikanaji wa taarifa za bidhaa ambazo zinauzwa ikiwemo magari, samani, nyumba, vifaa vya umeme pamoja na nguo au bidhaa binafsi. Lengo ni kuwaunganisha wauzaji na wanunuzi wa bidhaa zao. Katika hili, hadi sasa Kupatana.com imefanikiwa kuwa soko kubwa kabisa la bidhaa mtandaoni. 

  Hadi sasa, tunatembelewa na watu wanaozidi 67,000 kwa siku. Kwa kutumia mtandao huu, muuzaji anaweza kupata mafanikio Zaidi kwa kufikisha taarifa ya bidhaa alizonazo nje ya eneo alilopo bila gharama yoyote.


  Hayo yalisemwa na Meneja Masoko wa mtandao wa Kupatana.com Bwana Makusaro Tesha katika hafla ya chakula cha jioni ambayo ilihudhuriwa na wafanyakazi na baadhi ya wateja wa Kupatana.com … Vilevile katika hafla hiyo Mr. Tesha alitoa wito kwa vijana na wajasiriamali kuchukua fursa na kuutumia vizuri mtandao wa Kupatana kwani hauna gharama na unawafikia wanunuzi wengi. Alisema, “jambo la kwanza ni kupakua (download) application ya kupatana kwa kupitia Google play store. Ukiwa na app ya Kupatana na kuitumia inavyopaswa ni sawa na kuwa na duka lako wakati wote”.  Vilevile baadhi ya wateja waliohudhuria hafla hiyo walisema kuwa wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuongeza mauzo kwa kutumia mtandao huu. Mmojawapo wa wateja hao Bwana Mohammed Waqas wa Jazmak Motors alisema toka waanze kutangaza magari yao kwenye mtandao wa Kupatana wamekuwa wakipata wateja wengi hata kutoka nchi za jirani ikiwemo Malawi na Zambia. 
  Makusaro Tesha akizungmza na wadau mbalimbali wa kupatana wa KUPATANA waliojumuika na watumishi katika tafrija ya kuuaga mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka mpya. Tafrija hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni. 

  Kupatana.com ni website ya matangazo madogo madogo ya bidhaa mbalimbali kutoka kwa wauzaji hapa Tanzania. Website hii ilianzishwa rasmi mnamo mwaka 2013 ambapo wakati wa kuanzishwa kwake ilikuwa ikitembelewa na watu takriban elfu tatu kila siku.
  Makusaro Tesha akizungmza na wadau mbalimbali wa kupatana wa KUPATANA waliojumuika na watumishi katika tafrija ya kuuaga mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka mpya. Tafrija hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni. 
  Makusaro Tesha akizungmza na wadau mbalimbali wa kupatana wa KUPATANA waliojumuika na watumishi katika tafrija ya kuuaga mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka mpya. Tafrija hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni. 
   Makusaro Tesha wa Kupatana wakizungumza na wadau wa KUPATANA
   Wafanyakazi wakiwa na furaha ya kuwa pamoja,
   Mama Kupatana akisalimiana na mmoja wa wadau wa KUPATANA.
   Wafanyakazi wa KUPATANA wakiwa katika tafrija hiyo ya kufunga mwaka 2015
   Msimamizi wa shughuli za Kupata, Ezekiel Alex akizungumza kuhusiana na jumuiko hilo. 
   Mkuu wa huduma kwa wateja, Neema Mwakalonge akizungumza.
   Msimamizi wa bidhaa za 'Real Estate' Liberator Wyson akizungumza.
   Msimamizi wa bidhaa mchanganyiko, Jesca Mathew nae akitoa salamu 

  0 0

  Unguja,zc4

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan(katikati) Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif Ali Iddi (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai wakiwa katika Mkutano wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Zanzibar uliofanyika leo  Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja,
  zc5
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiendesha Mkutano wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Zanzibar uliofanyika leo  Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja(kushoto) Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan naNaibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai,[Picha na Ikulu.]
  zc6
  Wajumbe wa Sekretarieti ya Kamati Maalum ya Halmashauri  Kuu ya CCM Zanzibar (NEC) wakifuatilia kwa makini Mkutano wa siku moja uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein.

  zc3
  Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa siku moja wa  Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Zanzibar wakiwa katika mkutano chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein uliofanyika leo  katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini

  zc7
  Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa siku moja wa  Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Zanzibar wakiwa katika mkutano chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein uliofanyika leo  katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]
  zc1
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi wa Chama wakati alipowasili Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja katika Mkutano wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Zanzibar leo,
  zc2
  Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Viongozi wa Chama wakati alipohudhuria katika  Mkutano wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Zanzibar uliofanyika leo  Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.


  0 0

  Baadhi ya Washiriki wa Mdahalao huo wakifuatilia mada iliyokuwa ikijadiliwa wakati wa mdahalo.

  Nchi mbalimbali duniani zimekuwa na sera mahususi kwa ajili ya kukaribisha wawekezaji mbalimbali kuja kuwekeza kwenye nchi zao ili kuweza kupata kipato kupitia kodi mbalimbali na faida nyingine kama ajira kwa wenyeji, uboreshwaji wa miundo mbinu n.k. Moja ya nchi hizoni pamoja naTanzania.  

   Tanzania ilibadilisha sera zake za kiuchumi mwanzoni mwa miaka ya 1990, kwa kutoa fursa kwa sekta binafsi kuweza kumiliki uchumi. Sera hii ilivutia wawekezaji wengi toka nje na ndani kuwekeza katika sekta mbalimbali, moja ya maeneo ambayo wakezaji wamejikita ni sekta ya madini.  Shinyanga ni moja kati ya mikoa yenye utajiri mkubwa wa madini nchini na hivyo kuvutia wawekezaji wakubwa katika sekta hiyo. Mfano mzuri ni kampuni ya Barrick inayomiliki mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliopo wilayani Kahama mkoani humo.

  Mgodi huo unazungukwa na vijiji vitatu ambavyo ni Mwendakulima, Mwime na Chapurwa.  Lakini kutokana na hali halisi kumekuwa na kelele nyingi za manung’uniko toka kwa jamii zinazoishi karibu na maeneo hayo kuachwa bila maendeleo yoyote wakati wageni wanachukua madini kwa kiwango ambacho hakijulikani.“Kitu kingine uwepo uwazi waweke uwazi katika haya masuala ya madini mapato wamepata kiasi gani wawekezaji na serikali yenyewe imepata kiasi gani, ikibidi hata kwa wale wananchi wanaozunguka mgodi huu au migodi mingine ya Tanzania. 

  Waweze kuwa  wanawabandikia kwamba mwezi huu mgodi umeingiza kipato hiki na serikali imepata hiki angalau kidogo inaweza kupunguza manung’uniko. Kwa watanzania wengine ambao wanaishi sehemu ambapo hapana madini wapeleke hata kwenye magazeti matangazo ya mapato,” anafafanua mkazi wa Mwime.Haya yamejiri kwenye mda- halo uliondaliwa na waraghabishi wa Chukua Hatua toka kijiji cha Mwime. 


  Ambapo wananchi walipata fursa yakuchangia mawazo kama madini ni laana ama neema. Katika mdahalo huo ambao ulifanyika katika shule ya sekondari ya Mwendakulima washiriki toka kada mbalimbali za kijamii Kama wachungaji, mashekhe, wakulima, walimu, watendaji wa vijiji, wanafunzi na waandishi wa habari walipatafursa ya kuchangia mawazo yao kama madini ni laana ama neema. 

  Mwanafunzi wa kike toka katika shule ya sekondari ya Mwendakulima yeye aliona kwamba madini yanaweza yakawa ni janga la mazingira pale aliposema kwamba, “Suluhisho jingine angalau wangebadilisha mfumo wa uchimbaji, kwa sababu mfumo wanaotumia ule yaani kadri siku zinavyokuja kutakuwa na janga kubwa sana, angalia udongo uliofika pale huku chini kuna nini.”   Ukiacha changamoto ya mazingira, suala jingine lililojitokeza ni athari zinazoletwa na kemikali mbalimbali ambapo mwalimu mraghabishi

  Paul Chui wa shule ya msingi Mwime alisema,  “Kwa kweli kutokana na sera  ya elimu, bado tunafundisha elimu kwa kuzingatia sera ya elimu. Hivyo kwa mimi kama mwalimu najitahidi sana kuwaelekeza wanafunzi kuhusu suala zima la athari za kemikali kama vile sunlight pamoja na mekyuri.”  Wakati washirki wengine waliojitokeza wao walielezea tatizo la kiungozi na mikataba mibaya. Katika kuelezea tatizo hilo walielezea usiri uliopo kwenye mikatabana hivyo kushauri wananchi kuhusisha siasa na mali zao  kwa kuhakikisha kwamba wakati wa kupiga kura ni wakati sahihi wa kudhibiti maliasili za umma kwa kuchagua viongozi wanaofaa.  Mapungufu katika sera pamoja na sheria za madini ni moja ya sababu zilizotajwa kufanya  madini yaonekane laana kwa wananchi wanaozunguka migodi hiyo. 
   Katika maelezo yake kwa washiriki, George Kingi ambaye ni mtendaji wa kijiji cha Mwime alisema, “Kuna mapungufu kwenye sheria zetu hata ungemweka leo mwingine hata kila siku kama sheria  hujaiboreshwa bado unarudi kulekule kwa hiyo suala la sheria lifanyiwe marekebisho. Kingine ni sera.  Sera kama haisemi Mwime waachiwe  asilimia fulani, hata ungemleta mwingine kesho na mwingine atakwamishwa na sera ambayo haisemi wanamwendakulima mbaki na nini.”  Katika hili ushauri uliotolewa ni wa kukaa vikao wananchi wanatakiwa kutoogopa na wanapokaa kwenye vikao kweli wasema.

  Kwa kuwa kama kuna watu wa kupiga  kelele kule juu sheria na sera zibadilishwe na zikabadilishwa basi kila kitu kitakuwa sawa. Kama anavyomalizia George,  “Ukishabadilisha sheria na sera hata maji Mwime unayapata hata gari unaletewa si sera inasema uletewe gari kama sera haisemiutaletewa gari?” Akitoa majumuisho ya mdahalo huo uliondaliwa na waraghabishi walimu na wakulima Toka kijiji cha Mwime, mwenyekiti Maimuna Said alisema  “Madini sio laana lakini viongozi wenyewe ni laana kwa sababu hawatendi haki ipasavyo kulingana na katiba ya jamhuri wa muungano wa Tanzania. Hii ni neema toka kwa Mungu.”   Suala jingine ambalo limejitokeza katika mdahalo huo ni wananchi kutokuwa na furaha jinsi ambavyo serikali haiwashirikishi katika  kufanya maamuzi muhimu yanayohusu mustakabali wa maeneo yao. Hivyo ili madini yasiwe laana ni muhimu sana kwa serikali kuwashirikisha wananch toka hatua za mwanzo.

  Lakini pia suala zima la kutoa elimu ya uraia kwa wananchi.  “Kuna haja kubwa ya kutolewa elimu hususani elimu ya uraia. Watu kwanza watambue haki zao, mtu akishatambua haki zake kuna kuwa na uwezekano wa yeye kuzidai, lakini kama watu bado hawatapata elimu hiyo ni kwamba watu watakuwa wananung’unika tu pembeni. Lakni hajui aanzie wapi na hajui aishie wapi,” anafafanua Maalim Daudi Athman Imamu wa Masjid Noor Nyandekwa.

  0 0


  Meneja Huduma kwa Jamii wa Tigo, Bi. May Thomas, akiongea na waandishi wa habari na kinamama wa wilayani Rufiji waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali na utunzaji wa mazingira programu ijulikanayo “Mradi wa Kuwaunganisha Wanawake”. Wengine kulia kwake ni John Kikomo Mkurugenzi wa chama cha waandishi wa mazingira(JET) na kushoto kwake ni Dkt. Flora Myamba Mkurugenzi Mtafiti Kinga Jamii toka REPOA.


  Meneja Huduma kwa Jamii wa Tigo, Bi. May Thomas akimkabidhi simu Bi.Mozza Salum kutoka kijiji cha Umwe wilayani Rufiji. Jumla ya simu 200 zilitolewa na Kampuni ya Tigo kwa Wanawake wasiokuwa na uwezo wa kununua simu wilayani humo kupitia mpango unaojulikana kama, “Mradi wa Kuwaunganisha Wanawake”
  Baadhi ya kinamama wa wilayani Rufiji Mkoani Pwani waliohuduria mkutano wa mradi wa Kuwaunganisha Wanawake wenye lengo la kujifunza ujasiriamali na kutunza mazingira wakifuatilia kwa makini, Kampuni ya Tigo ndio mdhamini wa mradi huo.
  Baadhi ya kinamama wa wilayani Rufiji Mkoani Pwani waliohuduria mkutano wa mradi wa Kuwaunganisha Wanawake wenye lengo la kujifunza ujasiriamali na kutunza mazingira wakifuatilia kwa makini, Kampuni ya Tigo ndio mdhamini wa mradi huo.


  Mkurugenzi Mtafiti Kinga Jamii toka REPOA, Dkt. Flora Myamba akiongea na waandishi wa habari na kinamama wa wilayani Rufiji waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali na utunzaji wa mazingira programu ijulikanayo “Mradi wa Kuwaunganisha Wanawake”. Wengine toka kushoto John Kikomo Mkurugenzi wa chama cha waandishi wa mazingira(JET) na Meneja Huduma kwa Jamii wa Tigo, Bi. May Thomas
  Meneja Huduma kwa Jamii wa Tigo, Bi. May Thomas akimkabidhi simu Bi.Habiba Mtigino kutoka kijiji cha Umwe wilayani Rufiji. Jumla ya simu 200 zilitolewa na Kampuni ya Tigo kwa Wanawake wasiokuwa na uwezo wa kununua simu wilayani humo kupitia mpango unaojulikana kama, “Mradi wa Kuwaunganisha Wanawake”
  Mkurugenzi wa chama cha waandishi wa mazingira(JET), John Kikomo akionyesha kimoja kati ya vyeti watakavyopewa kinamama walioshinda shindano la kutunza mazingira wilayani Rufiji. Mpango huo ulidhaminiwa na Tigo na asasi tatu zisizo za serikali za REPOA, KIDOGO KIDOGO na Care International.
   
  Itashirikana na REPOA, CARE INTERNATIONAL & KIDOGO KIDOGO 

  Rufiji, Desemba 23, 2015: Tigo imetoa simu za mkononi 200 ambazo zitasambazwa kwa wanawake maskini ambao hawana uwezo wa kununua simu katika wilaya ya Rufiji mkoani Pwani, lengo kuu likiwa ni kuziba pengo la kijinsia katika umiliki wa simu Tanzania.

  Usambazaji wa simu hizo upo chini ya programu inayojulikana, “Mradi wa Kuwaunganisha Wanawake” utafanyika kwa kushirikiana na asasi tatu zisizo za serikali za REPOA, KIDOGO KIDOGO na Care International.

  Akizungumzia zoezi hilo Meneja Huduma kwa Jamii wa Tigo, Bi. May Thomas, alisema kwamba mtazamo wa Tigo uko kwenye sera za kampuni ya kuwawezesha watu walio na kipato duni ndani ya jamii katika kuzipata simu za mkononi.

  “Tigo inadhamiria kuboresha muunganisho wa simu za mkononi nchini Tanzania hususani miongoni mwa wanawake ambao kimsingi wana uwezo mdogo wa kupata simu,” alisema Bi.Thomas na kuongeza, “Ni matumaini yetu kwamba kwa kusambaza simu hizi kwa wanawake maskini katika wilaya ya Rufiji, Tigo itakuwa imechangia kupunguza pengo la kijinsia katika umiliki wa simu nchini.”

  Thomas alisema kwamba Tigo imewekeza zaidi ya dola 30,000 ambazo zitatumika kusambaza pamoja na kuangalia tathmini ya matokeo ya mradi. Aliongeza kwamba washirika watatu REPOA, CARE International na KIDOGO KIDOGO kwa pamoja wataongoza utekelezaji huo wa usambazaji wa simu kwa kutoa laini ya simu pamoja na kufanya tathmini ya matokeo ya mradi.

  “Pengo lililopo la kijinsia katika kuifikia teknolojia ya simu linaweza kukwaza Tanzania katika mchakato wa kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia katika kukuza usawa kijinsia na kuwawezesha wanwake nchini na ndio maana Tigo inachukua hatua za kuunga mkono mradi huu,” alisema Bi.Thomas.

  Kwa mujibu wa Bi. Thomas mradi huo unalenga kuwanufaisha watu 500 katika kipindi cha mwaka 2015 na 2016 na inakuwa ni mara ya pili kwa Tigo kusambaza simu za mkononi kwenye mkoa huo kwani mara ya kwanza ilikuwa amwaka 2014.

  0 0


  Baadhi ya wenyeviti toka Halmashauri ya wilaya ya Kishapu wakimsikiliza mkufunzi (hayupo pichani) wakati wa mafunzo ya uraghabishi yaliyofanyika wilayani hapo

  Na Krantz Mwantepele

  “Unakuja kwenye ofisi yangu na kutoa taarifa za ubadhirifu wa mtendaji wa kijiji. Nakuuliza, je umechukua hatua zipi kama kiongozi wa kijiji kabla kuja kwenye ofisi yangu? Unanijibu hapana, hii si sahihi,”

  Hayo ni maneno ya mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Hashim Mgandilwa, aliyoyatoa wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya wenyeviti wa vijiji, watendaji wa kata na vijiji kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Loliondo, mwezi Agosti mwaka huu.

  Alisema hayo kwa lengo la kufafanua dhana ya uwajibikaji kwa viongozi kama njia muhimu ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wa maeneo ya vijijini katika wilaya yake.Ni dhahiri kwamba viongozi wa ngazi za vijiji na kata wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za kiutendaji katika maeneo husika.

  Kuna nafuu kwa watendaji wa kata na vijiji, ambao ni waajiriwa wa serikali na hupewa kazi kutokana na miongozo, lakini siyo kwa wenyeviti wa vijiji na madiwani, wakati mwingine hata wabunge.

  Akielezea changamoto hiyo wakati wa mafunzo ya wenyeviti wa vijiji kupitia mradi wa Chukua Hatua yaliyofanyika Septemba mwaka huu na shirika mdau la CABUIPA, mwenyekiti wa kijiji cha Nyakafulu kilichopo wilaya ya Mbogwe, mkoani Geita, Salum Said amesema:

  “Baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa kijiji hiki, hakika sikufahamu vya kutosha kuhusu majukumu yangu mapya kama kiongozi. Na hii ni changamoto kubwa kwa wenyeviti wa vijiji karibu vyote vya wilaya yetu.” Yeye ni mmoja kati ya wenyeviti 200 wanaopatiwa mafunzo katika mikoa ya Shinyanga, Geita na Simiyu.


  Hii ni kutokana na ukweli kwamba, katika awamu ya kwanza ya mradi wa Chukua Hatua, nguvu kubwa iliwekwa katika kuwawezesha wananchi kuwachukulia hatua watendaji na viongozi wabadhirifu wa mali za umma.

  Wakati wananchi wakiwezeshwa kuwasimamia viongozi wao, viongozi hawakuwa wakiwezeshwa kutimiza majukumu yao kuwasikiliza na kuwahudumia wananchi wao. Hivyo, haja ya kutoa mafunzo kwa viongozi hao ili waweze kutimiza majukumu yao kwa wananchi waliowachagua, ilikuwa lazima.

  Akielezea umuhimu wa kuwawezesha wenyeviti wa vijiji wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya wenyeviti na watendaji wa kata Julai 2015, mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, mkoani Shinyanga, Jane Mutagurwa alisema:

  “Kwa muda mrefu wenyeviti mmekuwa mkilalamika kusahaulika kwenye programu zetu za mafunzo, fursa ndio hii imekuja. Tunafahamu kwamba wenyeviti wetu mnakutana na changamoto nyingi za kiutendaji zinazotokana na uwelewa mdogo katika majukumu yenu, hasa kwa wale wanaoingia madarakani kwa mara ya kwanza. Hivyo mtumie mafunzo haya vizuri.” 


  Pamoja na umuhimu wa mafunzo hayo kwa viongozi wa ngazi ya kijiji na kata, bado imekuwa ni changamoto kubwa kwa serikali kuwawezesha wenyeviti kujua majukumu yao. Na hii inatokana bajeti kuwa na vipaumbele vingine ambavyo halmashauri huwa wamejiwekea katika kutimiza majukumu yao."


  Kwa upande wa Ngorongoro, mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya hiyo mkoani Arusha anaeleza:


  “Tangu tulipofanya uchaguzi mwaka jana hatujawahi kutoa mafunzo kwa wenyeviti. Kwa hiyo tunaunga mkono mafunzo haya yanayotolewa na PALISEP yatasaidia sana kwenye kuwawezesha viongozi hawa na watendaji wetu,”


  Kutokana na hali hii, wenyeviti wamekuwa na changamoto za kuelewa mipaka ya majukumu yao, hivyo muda mwingine hujikuta kwenye mzozo na watendaji wa vijiji vyao. Mwenyekiti anawajibika kwa mwananchi aliyemchagua, wakati mtendaji anawajibika kwa mkurugenzi aliyemwajiri.

  Kutokana na tofauti hizo, mafunzo ya sasa ya wenyeviti na watendaji yanaendeshwa kwa pamoja kuwafanya waelewe mipaka yao ya kiutendaji, hivyo kuboresha utendaji wao.


  Afisa Programu wa CABUIPA, Michael Ikila anafafanua: “Tunawafundisha vitu sita muhimu; taratibu za uendeshaji serikali za mitaa, majukumu na haki za wenyeviti wa vijiji, uwajibikaji na utawala bora, mamlaka za vijiji, masuala ya fedha, ikiwamo uandaaji wa bajeti na mawasiliano mazuri baina ya viongozi wa vijiji.”


  Mada hizi ni kwa mujibu wa mwongozo wa wizara ya Tawala za Mikoa and Serikali za Mitaa (TAMISEMI).


  Majukumu mengine ya wenyeviti hawa ni pamoja na kuhamasisha shughuli za maendeleo, utawala na kuhakikisha usalama wa watu katika maeneo yao kwa kushirikiana na watendaji wa kata na vijiji.


  Kwa upande wa Wilaya ya Ngorongoro, hii ni mara ya kwanza kwa wenyeviti kufundishwa majukumu yao. Mwanzoni mafunzo haya yaliwalenga madiwani ambao kimsingi hawakuyapenda kwa sababu ya kutokuwapo kwa posho. Hivyo mafunzo yao yakaamishiwa kwa wenyeviti wa vijiji ambao walipokea mwaliko kwa furaha pasipo kudai posho.

  “Mafunzo haya yatatusaidia kuboresha mahusiano na utendaji wetu. Mara kadhaa unakuta wenyeviti wanaingilia mipaka yetu ya kazi, hivyo kuathiri uhamasishaji wa shughuli za maendeleo. Na hii hutokea pale mwenyekiti mpya anapotaka kuwaonyesha wapigakura wake kwamba mwenzake aliyepita hakufanya kazi,” anaelezea mmoja wa watendaji wa kijiji aliyehudhuria mafunzo hayo.

  Pamoja na changamoto hizo, bado washiriki ambao ni wenyeviti, watendaji wa kata na vijiji wamekiri kwamba mafunzo hayo yatakuwa chachu ya kumaliza tofauti zinazojitokeza baina yao. Lakini si hivyo tu, viongozi wa wilaya wameonyesha kuunga mkono mafunzo hayo kwa kuwa yanasaidia kuhamasisha wananchi kutimiza majukumu yao.

  Lakini pia viongozi hao walionyesha umuhimu wa kufikia wajumbe wengi zaidi ya halmashauri za serikali ya kijiji. Kwa mfano, wakati akizungumza na wakufunzi kwenye ofisi yake, mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu, alisema:

  Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu ina jumla ya vijiji 117 vyenye wajumbe 2,925. Kwa mantiki hiyo, mafunzo haya yanayoendeshwa kupitia mradi wa Chukua Hatua yamefikia asilimia 4 tu ya wajumbe wanaounda uongozi wa serikali za vijiji, hivyo wengi bado wanahitaji mafunzo. Katika mazingira hayo, mkurugenzi alitoa ombi maalumu la kusaidiwa kuwawezesha wakufunzi 25 wa wilaya watakaotoa mafunzo kwa wajumbe wa halmashauri za vijiji hivyo. Gharama za wakufunzi hawa kuwafikia wajumbe wengine zitakuwa ni za serikali.

  Na huu ni ushirikiano unaotakiwa baina ya sekta ya umma na binafsi kwa kuwa ni jukumu letu sote kwa mustakabali wa maendeleo yetu.

  0 0

  Watoto wa Chuo waliowahi kuishi chuoni hapo wakiwa kwenye picha ya pamoja hakika hii ilikuwa ni party ya nguvu. 

  Watoto wa chuo waliokuwa wakiishi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wakati wazazi wao wakiwa ni wahadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Ili kuweka ukaribu watoto hao wamekutana na kufanya party ya nguvu hivi karibuni katika viwanja vya UDSM hii ikiwa ni kurudisha ukaribu pamoja na kufahamiana kwa wale waliopotezana miaka kadhaa chuoni hapo.


  Baadhi ya watoto walioishi Chuoni UDSM wakiangalia vitabu pamoja na kununua vitabu hii ikiwa ni kundeleza utamaduni wa kujisomea.
  Hakika ilikuwa shangwe kwa watoto walioishi chuoni hapo wakati wazazi wao ni wahadhiri chuoni hapo
  Hivi ni Baadhi ya vitabu vilivyokuwa vinauzwa wakati wa Party hiyo iliyofanyika chuoni hapo.

  Muda wa kuserebuka ulifika sasa kila mtu akaanza kuonesha umahiri wake kwenye kulisakata Rhumba.
  Watoto wa Chuo wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kumaliza party yao
   
  Hakika ilikuwa ni siku ya furaha maana watu walikuwa wanakumbushana mambo ya miaka ya 90 kwani kipindi hicho walikuwa wadogo.
  Watoto wakiendelea kucheza wakati wa party ya watoto walioishi chuoni hapo kipindi wazazi wao bado ni waalimu katika chuo cha UDSM
  Full Happy kwa kila tu aliyefika katika Party hiyo.
  Watoto wa wahadhiri wa UDSM wakibadilishana mawazo kwenye party ya kuwaunganisha pamoja kama wanafamilia wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
  Hakika watoto walikuwa waki-enjoy vya kutosha maana hakuna aliyeboreka kwani kulikuwa na kila aina ya michezo kwa watoto wa rika zote.

  Baadhi ya watoto wakiwa wametokelezea kwenye ukodak..

  0 0

  Afisa utalii wa tanapa fredy shirima akiwa anamkabidhi zawadi Mwanariadha Reginal Lucian baada ya kushinda kilometa 42,baada ya kukimbia kwa muda wa  1:00:05.
  Baadhi ya wanariadha walifanikiwa kupata zawadi katika shindano Arusha tourism Marathon wakiwa katika picha ya pamoja .  Na Woinde Shizza,Arusha 


  Mwanariadha Reginal Lucian alifanikiwa kushinda kwa upande wa
  wanaume,katika shindano la Arusha Tourism Marathon baada ya kutumia
  muda wa 1:00:05,akifatiliwa na mwanariadha wa kimataifa, Fabian Joseph
  1:00:14, nafasi ya tatu,Gabriel Gerald muda wa 1.00.37.

  katika mashindano hayo ya kilomita 42, yaliyoandaliwa na taasisi la
  Alfredo Shahanga na Mwanariadha kutoka Kenya, Evance Kiblanget
  alishika nafasi ya nne baada ya kutumia muda wa 1:07 huku nafasi ya
  tano ikishinda Wilbart Peter na nafasi ya sita akishinda mwanariadha
  wa kimataifa Dockson Marwa.

  Kwa upande wa wasichana Angelina Tsere alishinda kwa kutumia musa wa
  1:11:17, akifuatiwa na mwanariadha wa kimataifa Mary Naali muda wa
  1:11:23, nafasi ya tatu ulikwenda kwa Mkenya Ladis Shemayo aliyetumia
  muda wa 1:11:37 .

  Katika mashindano hayo, ambayo mgeni rasmi alikuwa ni ,Afisa Michezo
  wa Mkoa wa Arusha,Mwamvita Okeng'o mshindi wa kwanza hadi wa 10
  walipewa zawadi.

  Viongozi wengine waliotoa zawadi ni pamoja na Katibu Mkuu wa kamati ya
  Olimpic Tanzania(TOC), Filbert Bayi, Rais wa zamani wa chama cha
  riadha nchini(TAAA) Franis John na Afisa Utalii wa TANAPA Fred
  Shirika.

  Katika mashindano hayo, washindi wa kwanza walipoewa zawadi ta
  shilingi 500,000, washindi wa pili, 250,000,washindi wa tatu, 200,000,
  wanne 150,000 na wa tano 100,000 ambapo wa 6 hadi 10 pia walipewa
  zawadi.

  Wakizungumza wakati wa kutoa zawadi, Bayi na Okeng'o walipongeza
  wanariadha waliojitokeza kwa kuonesha upinzani mkubwa na kutoa wito
  mashindano haya yafanyike kila mwaka ili kusaidia kukuza utalii wa
  ndani.

  Mkurugenzi wa Alfredo Shahanga kwa upande wake, alisema lengo la
  mashindano hayo lilikuwa ni kuhamasisha utalii wa ndani, kuhamasisha
  amani mkoa wa Arusha na kutaka sasa riadha itumike kutangaza utalii.

  Mashindano hayo ambayo ni sehemu ya mashindano ya Arusha Tourism
  Festival ni mara ya kwanza kufanyika nchini, yalidhamiwa na shirika la
  hifadhi za Taifa(TANAPA), kampuni ya vinywaji ya SBC(T) Ltd,radio
  Sunrise,BiG Expedetion,Mega Trade Investment,Tanzania Breweris na
  Criative Solution.

  0 0


  0 0

  BELAKING of the Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’.

  KING of the Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’ anatarajiwa kufunga mwaka (Desemba 31) na wimbo alioufanya na mkongwe wa muziki kutoka Kongo (DRC), Koffi Olomide uitwao Acha Kabisa, ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar. Akizungumza na mtandao huu, Bella anayetamba na Wimbo wa Nashindwa alisema usiku huo mashabiki watafunga mwaka kwa kuimba na kucheza ngoma zake zote kali kama vile Nani Kama Mama, Nakuhitaji, Msaliti, Nashindwa, Amerudi na nyingine kibao. 

   “Usiku huo nitafunga mwaka na kufungua mwaka mwingine nikiwa na bendi yangu ya Malaika Music huku tukitoa sapraiz kwa mashabiki wetu wote, pia kwa mara ya kwanza nitawaonjesha Wimbo wa Acha Kabisa niliofanya na Koffi Olomide pamoja na kutambulisha wimbo wangu mpya mwingine,” alisema Bella. Mashabiki pia wategemee kupata sebene la aina yake kutoka kwa Malaika itakayokuwa na vichwa kama Adaya, Petit Mauzo, Pilu, Mico Bella, Chesco Vuvuzela, Yanick Soslo, Babu Bomba, Kadogoo Machine na wengine wengine wengi. 5_5
  Baada ya kufunga mwaka, katika Sikukuu ya Mwaka Mpya (Januari 1), bendi kongwe ya muziki wa Dansi, The African Stars ‘Twanga Pepeta’ ikiongozwa na Ali Chocky itakuwa na kazi moja ya kulishambulia jukwaa kwa kutoa sebene la kisasa. 

   Akizungumzia shoo ya kufungua mwaka, Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alisema kuwa siku hiyo pazia la burudani litafunguliwa mapema kuanzia asubuhi kwa kutoa nafasi kwa watoto wote kusherehekea kuukaribisha mwaka mpya. 

   “Tutakuwa na kundi linalotikisa kunako miondoko ya sarakasi na mazingaombwe kwa watoto la Masai Warriors ambapo watatoa burudani zote bila kusahau watoto wote wataburudika na michezo mingi kama vile kuogelea, kuteleza, kubembea pamoja na kucheza ndani ya ndege maalum,” alisema Mbizo.

  0 0
 • 12/28/15--01:09: WACHIMBAJI WADOGO KUANDAMANA • Mmoja kati ya wachimbaji wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Charles Mlay akizungumza juzi kwenye mkutano wa wachimbaji wadogo Marema kuhusiana na maandamano ya amani kupinga migodi yao 19 kusimamishwa kufanya kazi.
  WACHIMBAJI wadogo wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wanatarajia kuandamana hadi kwa mkuu wa mkoa huo, wakipinga kusimamishwa kazi migodi yao 19 inayopakana na TanzaniteOne.

  Wachimbaji hao wanatarajia kuandamana kwa amani mapema mwezi ujao na watamuandikia barua mkuu wa mkoa huo Dk Joel Bendera ili ayapokee maandamano hayo wakipinga kunyanyaswa na kusimamishwa migodi yao 19.

  Mmoja kati ya wachimbaji hao Charles Mlay akizungumza juzi kwenye mkutano wa chama cha wachimbaji wadogo wa madini ya Tanzanite Marema, alisema wachimbaji wamekuwa wananyimwa haki zao bila sababu ya msingi.

  “Hakuna mtu aliye juu ya sheria kila wakati wachimbaji wadogo wananyanyasika kwa kunyimwa haki zao wakati wanachimba kihalali hivyo ni bora kufanya maandamano ya amani yatakayoeleza hisia zetu,” alisema Mlay.

  Makamu Mwenyekiti wa Marema Wariamangi Sumari alisema maandamano hayo ya amani yatajumuisha wachimbaji wadogo, wafanyabiashara na wakazi wote wa Mirerani kwani maisha yao yanategemea madini ya Tanzanite.

  “Maandamano hayo yatakuwa ya halali kabisa kwani tutaomba kibali kwa mkuu wa polisi wa wilaya (OCD) na kumtaarifu mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa aje hapa Mirerani kwa ajili ya kupokea maandamano hayo,” alisema Sumari.

  Omary Mandari alisema kitendo cha migodi hiyo 19 kusimamishwa kufanya kazi kimewaathiri watu wengi kiuchumi, kwani familia nyingi za wachimbaji hao zinategemea kuishi ila kutokana na hali hiyo, sasa wanaishi kwa wakati mgumu.

  “Tutaandamana kwa amani kuanzia shamba la Maro na kuzungukia kwenye baadhi ya barabara za Mirerani hadi getini mnadani, kwa lengo la kuonyesha ulimwengu kuwa tunapinga migodi yetu 19 kusimamishwa,” alisema Mandari.

  Naye, katibu wa Marema Abubakari Madiwa alisema azimio hilo la kuandamana kwa wachimbaji hao wadogo linaandaliwa ipasavyo ikiwemo kamati ndogo itakayoratibu mpango wote hadi kufanikisha maandamano hayo ya amani.

  Zephania Joseph alisema haki ya wachimbaji wadogo haiombwi inadaiwa, hivyo huu ni wakati muafaka wa kuungana kwa wachimbaji hao kufanya maandamano ya amani ili kufikisha kilio cha kwa migodi yao 19 kusimamishwa.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa awasili kwenye Uwanja wa ndege wa Kigoma mchana huu, tayari kwa kuanza ziara ya kikazi Mkoani humo.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akivishwa skafu na vijana wa Chipukizi wa Chama cha Mapinduzi, Mkoani Kigoma mara baada ya kuwasili.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Kigoma iliyofika kwenye Uwanja wa Ndege kumlaki.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia kikundi cha ngoma cha akina mama wa ujiji Mkoani Kigoma.
  Kwaya ya vijana wa JKT Bulombora 821 wakitumbuiza kwenye uwanja wa ndege wakati wa mapokezo ya Waziri Mkuu.Picha na Editha Karlo, Globu ya Jamii, Kigoma.

  0 0

   Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando (wa pili kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuendesha droo ya pili ya promosheni ya Airtel Mkawnjika ambapo washindi 28 kutoka katika mikoa mbalimbali walipatikana. Akishuhudia ni balozi wa Airtel Mkwanjika na mtangazaji wa kipindi cha planet Bongo cha EATV Abdallah  Hamisi Ambua  (kushoto) akifuatiwa na  msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini , Mrisho Milao (wa pili kulia) na Afisa Masoko wa Airtel Bi Rebecca Mauma (kulia).
  Balozi wa Airtel Mkwanjika na mtangazaji wa kipindi cha planet Bongo cha EATV Abdallah  Hamisi Ambua (kulia)  akiongea na moja ya washindi kupitia simu ya mkononi wakati wa kuendesha droo ya pili ya promosheni ya Airtel Mkawnjika ambapo washindi 28 kutoka katika mikoa mbalimbali walipatikana. Akishuhudia Msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini , Bwana Mrisho Milao (kushoto) na Afisa Masoko wa Airtel Bi Rebecca Mauma (katikati).

older | 1 | .... | 723 | 724 | (Page 725) | 726 | 727 | .... | 1897 | newer