Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 722 | 723 | (Page 724) | 725 | 726 | .... | 1904 | newer

  0 0


  0 0

  Nesi Wangu
  Kilimanjaro Studio iliyopo Beltsville, Maryland inatoa salamu za kheri ya sikukuu ya Maulid, Christmas na mwaka mpya kwa wadau wote wa Vijimambo Blog, Kwanza Production na Nesi Wangu Blog. Sikukuu iwe ya upendo na amani na muweze kusherehekea kuuaga mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka 2016.

  Kama hukutimiza malengo mwaka 2015 usijali mwaka 2016 ni mwaka wa kujipanga upya na Kilimanjaro studio inakutakia kila la kheri kwa mwaka mpya 2016 uwe mwaka wa mafanikio makubwa kwako na kumwomba Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema palipokua na giza 2015 mwaka mpya apatie mwanga, palipokua na chuki 2015 mwaka mpya apaweke amani yote na tunaimani utafikia malengo na sisi kujipanga kwa mambo mapya kwa kuongeza vipindi kwenye Radio na kukuhabarisha kwenye Blogs zetu.

  SOTE KWA PAMOJA TUNASEMA KHERI YA SIKUKUU YA MAULID, CHRISTMAS NA MWAKA MPYA

  0 0

  Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli, mkewe Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakishiriki Ibada ya Krismas katika Kanisa la Mtakatifu Peter jijini Dar es salaam leo Desemba 25, 2015
  Sehemu ya waumini katika Ibada ya Krismas misa ya kwanza katika Kanisa la Mtakatifu Peter jijini Dar es salaam leo Desemba 25, 2015.
  Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli, mkewe Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakishiriki Ibada ya Krismas katika Kanisa la Mtakatifu Peter jijini Dar es salaam leo Desemba 25, 2015

  Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli, mkewe Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakishiriki Ibada ya Krismas katika Kanisa la Mtakatifu Peter jijini Dar es salaam leo Desemba 25, 2015


  Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Muadhama Askofu Mkuu Polycarp Kardinali Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam aliyemkaribisha kusalimia wananchi bada ya kumalizika kwa Ibada ya Krismas misa ya kwanza katika Kanisa la Mtakatifu Peter jijini Dar es salaam leo Desemba 25, 2015. 
  Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwasili kushiriki Ibada ya Krismas misa ya kwanza katika Kanisa la Mtakatifu Peter jijini Dar es salaam leo Desemba 25, 2015.
   
  Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akitoa salamu zake za heri ya Krismasi mara baada ya kumalizika Ibada ya Krismas misa ya kwanza katika Kanisa la Mtakatifu Peter jijini Dar es salaam leo Desemba 25, 2015.  0 0


  Askofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT( Dayosisi ya Iringa Dr OwdenBurg Mdegella akimpa baraka ya Christmas mtoto Monica Kasesela huku babake mkuu wa wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela na binti yake Cathelin Kasesela wakishuhudia baada ya kumalizika kwa ibada ya pili katika usharika wa kanisa kuu

  Askofu Dr Mdegela akitoa baraka

  Mwalimu wa kwaya ya vijana katika kanisa kuu Bw Lupyana Samweli akipokea baraka za Christmas kutoka kwa askofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Iringa Dr OwdenBurg Mdegela leo mara baada ya ibada.

  Askofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Iringa Dr OwdenBurg Mdegela akimpa baraka za Chritmas mlemavu ambae ni mwimbaji maarufu wa kwaya ya vijana kanisa kuu Gift Mwanuka 

  WAKATI waumini wa Dini ya kikristo hapa nchini leo wakiungana na wakristo wenzao kote ulimwenguni kusherekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo , Askofu wa Kanisa la Kilutheri (KKT) dayosisi ya Iringa Dkt. Owdenburg Mdegella amesifu amani iliyotawala nchini kutoka uchaguzi mkuu hadi sasa na kuwaomba watanzania kumwombea Rais Dr John Mapuguli kwa kuleta mabadiliko ya kweli ambayo hata wapinzani walikuwa wakiyataka.

  "Salamu zangu na maelezo yangu ni mafupi kila mmoja anafahamu Burundi na Kenya walifanya uchaguzi na hadi leo hii bado wanauana na maisha yanakuwa magumu......ninyi mnafahamu awamu ya kwanza kuja ya pili tumevuka salama ,awamu ya pili kuingia ya tatu pia salama na awamu ya nne kuingia ya tano ndio tumevuka salama salimini zaidi kuliko awamu nyingine zote.....kwa nilitaka kuasema hata wale waliotumia mabomu na kutumia gharama kubwa wakati wa uchaguzi nafikiri walikuwa wamekosa mazoezi kwa muda mrefu ya kutumia mabomu hayo bila sababu Watanzania ni wapenda amani"

  Askofu Dr Mdegella alitoa kauli hiyo wakati wa ibada hiyo ya christmas iliyofanyika katika kanisa kuu kuwa hadi hapa sasa Bwana Mungu ametusaidia na sio amesaidia uchaguzi tuo hata mambo mengine ambayo tulikuwa tunayataka kwa kuzungusha mikono kuwa mabadiliko sasa yamekuja.

  Alisema kuwa Mungu si kaibadilisha Tanzania na kuipa neema katika uchaguzi mkuu pekee kwani kila mtanzania kwa sasa anaona mabadiliko kawaida ukilinganisha na awali kwani wakati wa kampeni watu walikuwa wakizungusha mikono kama ishara ya kutaka mabadiliko na mabadiliko yameanza kuonekana kwani matajiri walikuwa wamejitajirisha mno na masikini walikuwa wamekumbatia umasikini wao .

  "Kulikuwepo pengo kubwa kati ya matajiri na masikini kwani matajiri walijitajirisha zaidi na masikini waliendelea kubaki masikini ila sasa kwa kipindi kifupi cha serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr Magufuli mabadiliko ya kweli yanaonekana "

  Askofu Dr Mdegella mbali ya kumpongeza Rais Dr Magufuli kwa utendaji mzuri na baraza lake la mawaziri bado alitaka uzi huu wa kutumbua majibu ambao unaendelea uzidi kukazwa zaidi ili kila mtanzania aweze kufaidi matunda ya nchi yake .

  " Sasa ombi langu kwenye watanzania najua Francis Godwin utaandika naomba kila mmoja wetu bila kujali ulimpa kura ama ulimnyima tuzame katika maombi kumwombea Rais wetu ili mabadiliko yaendelee na nchi iwe na amani na maendeleo pamoja na mafanikio ...kwa wale waombolezaji naomba leo kuombeleza kumshukuru Mungu na sisi wote kuungana kumwombea Rais wetu na tarehe 3 Januari 2016 wote kutoa shukurani ya pekee kumshukuru kwa kuvuka salama katika uchaguzi na kuendelea kuona neema hii ya utendaji wa Rais wetu pia kazi ya kutumbua majibu iwe endelevu kwa wakubwa na wadogo ....ukimkamanda mtu mwenye msokoto mmoja wa bangi na kumwacha mwenye gunia la bangi ikome japo sisemi mwenye msokoto mmoja asikamatwe wote washughulikiwi " 

  Alisema kuwa watanzania ni watu wanapenda amani na utulivu na ndio maana wamepata kupita katika wakati mgumu wa uchaguzi mkuu pasipo kutokea machafuko yoyote." Kati ya vipindi vigumu ambavyo watanzania tumepitia kwa amani na utulivu ni pamoja na kulinda amani wakati wa uchaguzi mkuu na kuingia katika sikukuu hii ya chritmas bila amani kuvurugika"

  Hata hivyo alisema kuwa amani hii watanzania tumeipata bure na kuwa kuzaliwa kwake Yesu Kristo kubisha hodi kwa kila mmoja wetu ili aweze kuingia ndani ya mioyo ya wote hivyo Kazi kubwa kumfungulia ili aweze kuingia ndani ya mioyo yetu.

  Alisema kuwa Yesu Kristo amekuja ili kufanana na wanadamu wote na kuwa njia pekee ni kumpokea pasipo kushindana na Mungu .Huku mkuu wa wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela ambae alipata kushiriki ibada hiyo alimpongeza askou huyu Dr Mdegella kwa kumpongeza Rais Dr Magufuli na serikali ya awamu ya tano na kuwa moyo huo wa viongozi wa dini unapaswa kuendelea zaidi kwani kauli zao zinasikilizwa zaidi.

  Bw Kasesela alisema amependezwa na askofu huyo kutenga muda wa kuiombea serikali na kudai kuwa kazi kubwa inayofanywa na viongozi wa serikali ya Dr Magufuli akiwemo waziri mkuu na baraza la mawaziri pamoja na watendaji wengine ni nzuri na kila mtanzania anaiona hivyo zawadi kubwa kwa watanzania ni sala na dua zao .
   

  Vijana wa kanisa kuu wakiwa katika maombi  Maombi maalumu kwa Taifa la Tanzania

  Kwaya kuu wakiimba

  Kwaya kuu wakiimba wimbo maalumu

  Mkuu wa wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela kulia akiungana na waumini wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) usharika wa kanisa kuu kuliombea Taifa na serikali ya Rais Dr John Magufuli  Waumini wa kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) usharika wa kanisa kuu wakiliombea Taifa wakati wa ibada ya Chritsmas

  Askofu Dr Mdegela akitoa salamu za Christmas leo


  Askofu Dr Mdegella akitoa baraka kwa waumini wa kanisa kuu leo
  Askofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT( Dayosisi ya Iringa Dr OwdenBurg Mdegella akimpa baraka ya Christmas mtoto Monica Kasesela huku babake mkuu wa wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela na binti yake Cathelin Kasesela wakishuhudia baada ya kumalizika kwa ibada ya pili katika usharika wa kanisa kuu

  Dereva maarufu wa Taxi eneo la Posta mjini Iringa Bw Sisico akiwa katika vazi la Christmas

  Na MatukiodaimaBlog
  0 0  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
  Simu: 255-22-2114512, 2116898
  E-mail: press@ikulu.go.tz
  Tovuti : www.ikulu.go.tz              

  Faksi: 255-22-2113425  OFISI YA RAIS,
        IKULU,
   1 BARABARA YA BARACK OBAMA,  
  11400 DAR ES SALAAM.
  Tanzania.
   

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameungana na watanzania wote kuadhimisha Sikukuu ya Krismasi ambayo wakristo wote duniani huadhimisha siku ya kuzaliwa Yesu Kristo, zaidi ya miaka 2000 iliyopita.

  Rais Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wamesali ibada ya Krismasi katika misa takatifu iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay Jijini Dar es salaam.

  Akitoa salamu za Krismasi baada ya kukaribishwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es salaam Mhadhama Kadinali Polycarp Pengo, Rais Magufuli amewatakia heri watanzania wote katika sikukuu hii ya Krismasi na kuwataka waishi kama ambayo Yesu Kristo aliishi, na kwa kutekeleza yote ambayo aliyafundisha.

  Ametoa wito kwa watanzania kuishi kwa amani, upendo na Mshikamano huku wakizingatia kufanya kazi, hasa wakati huu ambapo yeye mwenyewe anahamasisha uchapa kazi kupitia kauli mbiu ya "Hapa Kazi Tu"

  Rais Magufuli pia amewataka wakristo wote kuungana kuliombea taifa, kuwaombea viongozi na kuwaombea watanzania wote ili waweze kutimiza majukumu yanayowakabili.

  "Ndugu waumini wenzangu, mimi ni yuleyule, nipo vilevile na nimekuja hapa kama Mkristo wa kawaida, muendelee kuliombea taifa hili na mtuombee pia sisi viongozi wake" Amesisitiza Rais Magufuli

  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  25 Desemba, 2015  0 0

    Maofisa wa Jeshi la polisi kitengo cha Usalama barabarani pamoja na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu(wapili toka kushoto)wakimshuhudia dereva Frank Masawe wa basi lenye Namba za usajili T 798 DCT linalofanya safari za mikoa ya Dar es Salaam na Mtwara akisoma karatasi yenye majibu baada ya kupimwa kilevi,wakati wa zoezi lilioendeshwa na Jeshi la polisi kitengo hicho kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania kupitia kampeni ya”Wait to send”inayotoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto ikiwa ni mwendelezo wa kampeni hiyo iliyofanyika jana katika Vituo vya mabasi ya kwenda mikoani cha Ubungo na Mbagala jijini.
   Askari wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Dar es Salaam, SGT. John Jonas(kushoto)akimpima kiwango cha pombe mwilini dereva wa basi lenye namba za usajili T 798 DCT la Dar es Salaa na Mtwara ,Frank Masawe ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya”Wait to Send” inayotoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto ikiwa ni mwendelezo wa kampeni hiyo iliyofanyika jana katika Vituo vya mabasi ya kwenda mikoani cha Ubungo na Mbagala jijini,katikati katika picha ni Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu ambao ni wadhamini wakuu wa kampeni hiyo.
   Baadhi ya Madereva wa Mabasi yanayoenda mikoani na wadalala wa jijini Dar es Salaam,wakimsikiliza Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kulia)akitoa elimu kuhusiana na pete ya kidoleni yenye ujumbe maalumu wa “Wait to send” wakati wa zoezi la kukagua magari na kutoa elimu kwa madereva hao kuhusiana na kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto ikiwa ni mwendelezo wa kampeni hiyo iliyofanyika jana katika Vituo vya mabasi ya kwenda mikoani cha Ubungo na Mbagala jijini.
   Mkuu wa kitengo cha elimu kwa Umma kitengo cha Usalama barabarani makao makuu ya Polisi ASP,Abel Swai(katikati) akifafanua jambo kwa Madereva wa mabasi ya endayo mikoani na daladala za jijini Dar es Salaam pamoja na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, matina Nkurlu(kulia) wakati wa zoezi lililofanyika Stendi kuu ya Ubungo na Mbagala ya kutoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya”Wait to Send”inayoendeshwa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama Barabarani.

  Baadhi ya abiria wa Mabasi yaendayo mikoani wakimsikiliza Mkuu wa kitengo cha elimu kwa Umma kitengo cha Usalama barabarani makao makuu ya Polisi ASP,Abel Swai,wakati alipokuwa anawaelimisha abiria hao ndani ya basi linalofanya safari zake mikoa ya Dar es Salaam na Mtwara ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya”Wait to Send”inayotoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto.Kampeni hiyo inaendeshwa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kitengo hicho ilifanyika jana katika Stendi kuu ya Ubungo na Mbagala jijini.

  0 0

   Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwan J. Kikwete.

  Ndugu zangu waandishi wa habari, nimeamua kuwaita ili kuzungumza nanyi kuhusu baadhi ya mambo yaliyokuwa yanasemwa katika vyombo vya habari kuhusu mimi.

  Awali ya yote napenda kusema kuwa habari hizo ni UONGO mtupu, ni mambo yanayozushwa na waandishi wa habari hizo kwa nia ya kuchafua jina langu kwa sababu wanazozijua wanaoandika. UKWELI ni kwamba haya ni mambo yenye kufanywa kwa nia na dhamira mbaya dhidi yangu na hata familia yangu.

  Hivi karibuni, kwa mfano, lipo gazeti moja liliandika na kutoa picha yangu na mtu mmoja waliyedai ni Mhe. Paul Makonda eti akinifunga kamba za viatu. Katika maelezo yake mwandishi akadai kuwa Mhe. Makonda alipata uteuzi kuwa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni kwa sababu hiyo. Huu ni uongo usiokuwa na hata chembe ya ukweli. 

  Napenda watanzania wajue kuwa hakuna wakati wowote Baba yangu alipokuwa Rais wa nchi yetu alinihusisha kwa namna yeyote ile katika uteuzi wa mtu yeyote katika Serikali. Hivyo basi kujaribu kunihusisha na uteuzi wa Mhe. Paul Makonda kuwa Mkuu wa Wilaya wa Kinondoni ni jambo lisilokuwa na ukweli wowote. 

  0 0


   Afisa Muuguzi Msaidizi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam Mwanne Satara  akimsaidia kumuelekeza Lulu Mohamed namna ya kumfunika nguo Mtoto aliyezaliwa usiku wa kuamkia Krismas Dar es Salaam ambapo akinamama 12 walipata watoto na Mmoja wa akinamama hao alipata mapacha 2 na  kufanya watoto wa kiume kufikia 6 na wakike 7, kati yao akinamama  waliofanyiwa upasuaji ni  akinamama 10 na kati ya hao  watoto njiti 2 na Hospitali ya Temeke akina mama waliojifungua hospitalini hapo kufikia idadi ya watoto 12, wakiume 4 na  wakike 8  (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA) Mmiliki wa UJIJIRAHAA BLOG
  Afisa Muuguzi wa Zamu wa Hospita ya Mkoa Amana Florensia Ndumbaro akizungumza na waandishi wa Habari  (pichani hawapo), Hospitalini hapo ambapo amesema  wamepokea idadi ya watoto waliozaliwa mkesha wa Krismas ni 33 kati yao 15 ni wakike na 18 ni wakiume na wote wapo katika hali nzuri na wananyonya vizuri pia mama zao wanaendelea vizuti

  0 0

  Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya The Ngoma Africa Band aka FFU-ughaibuni inayoongozwa na Kamanda  Ras Makunja yenye maskani nchini ujerumani inawatakieni kila la heri katika siku kuu ya Maulid el Nabii Muhammad(S.W.A) pia Heri ya siku kuu ya Krismasi kwa wadau wote iwena amani,upendo,furaha na mshikamano bila kusahau kupata muziki at www.ngoma-africa.com au www.reverbnation.com/ngomaafricaband

  0 0

  Mraghbishi Noorkiyengop Mbaima toka kijiji cha Enguserosambu akisimama mbele ya mifugo iliyokutwa msituni katika eneo lililoruhusiwa la msitu wa jamii wa Enguserosambu

  Ilikuwa ni siku ya shangwe na furaha kwa wananchi wa kata ya Enguserosambu wilayani Ngorongoro. Hii ni baada ya serikali kukubali ombi lao la kusimamia rasilimali ya msitu wa Loliondo namba 2 unaopakana na vijiji vinne vinavyokadiriwa kuwa na idadi ya wakazi wapatao 20,000 wanaotegemea mahitaji yao toka katika huo msitu.

  Huu ni msitu pekee ambao wananchi kwa kushirikiana na Mkuu wao wa wilaya, na mashirika rafiki, wamefanikiwa kuishawishi serikali kuukabidhi msitu huo kwao. Katika mchakato huo uliochukua miaka kadhaa wanawake toka katika vijiji vya Enguserosambu, Ng’arua, Orkiu na Naan wamekuwa mstari wa mbele katika kufanikisha azma hiyo ya kubakiza msitu wao wa enzi mikononi mwao. Akielezea furaha yake aliposikia msitu wa Loliondo namba 2 umekabidhiwa kwa wananchi, mraghbishi mwanamke Noorkiyengop Mbaima alisema 

  “Mimi mwenyewe nimefurahia, kwa sababu sisi akina mama tunategemea sana msitu huu kwa mahitaji yetu. Huu msitu kama ungeondoka katika mikono ya jamii basi tungeathirika sana sisi kina mama.” Umuhimu wa msitu huu kwa kina mama ndio uliowapelekea wao kutunga na kuimba nyimbo za hamasa na kutumbuiza, kushiriki kwa wingi katika vikao mbalimbali vya maamuzi wakati wote wa mchakato huo. 


  Kwa kuwa msitu huu ndio tegemeo lao katika kuendesha maisha ya kila siku. Hakuna chochote ambacho kiliamriwa bila ya wao kuchangia na kushirikishwa kuanzia utungaji wa sheria ndogongogo za usimamizi wa msitu hadi kukabidhiwa rasmi msitu huo. “Nikichukulia mfano katika mikutano yote ya vijiji. Kiukweli wanawake wamekuwa wanajitokeza kwa wingi, kuliko makundi mengine yoyote. Hata ile siku ya uzinduzi wa msitu walikuwa wengi zaidi,” anaelezea Jackson Nangiria 

  Ushiriki huu wa wanawake unatokana na ukweli kwamba wana uhusiano wa karibu na msitu huo wa enzi wa Enguserosambu.Si kwa ajili yao tu pamoja na watoto wao pia. Ni watoto hawa wa kike wenye majukumu ya kujenga nyumba kwa kutumia miti inayotoka ndani ya msitu huu, ndio wanaotembea na punda wakiwabebesha maguduria ya maji kwa umbali mrefu wakitafuta maji ambayo chanzo chake kipo kwenye msitu huu. Wanapopata watoto wanahitaji dawa za kuwaogeshea na dawa za uzazi ambazo zinatoka kwenye msitu huu. 

  Wao ndio wapishi katika familia zao hivyo wanahitaji kuni zinatokana na miti iliyoanguka na kukauka ambayo inapatikana kwenye msitu huu. “Kina mama wanafanya mitambiko ndani ya msitu huu wengine ambao hawakupata watoto wanapatia hapo baada ya kuomba ndani ya msitu huu. Si hivyo tu ndani ya msitu huu kuna dawa mbalimbali za asili kwa mfano mtoto akizaliwadawa ya kumwogesha na kumnawisha hupatikana humo humo na nyingine ni za kunywa kama maziwa na nyingine kwa ajili ya mama,” anaeleza mwanamama mraghbishi Noorkiyengop Mbaima. Uwepo wa wanawake hawa wa Kimasai katika kata ya Enguserosambu kiukweli unatokana na uwepo wa msitu huu. Huu ndio msitu wa enzi ambao serikali ilipendekeza uwe chini ya usimamizi wake kama ulivyokuwa msitnamba moja wa Loliondo. 

  Pendekezo hilo lilitolewa kupitia timu mbalimbali toka wizarani, ofisi za kanda na halmshauri ya wilaya, ambazo zilitembelea kijijini hapo kuomba kupatiwa muhtasari wa kikao cha kijiji kitakachopitisha ombi hilo la serikali. 

  Ombi hilo linakuja kwa kijiji kwa sababu msitu huo umekuwa chini ya usimamizi wa wananchi wa kata ya Enguserosambu kwa miaka mingi. Ni wananchi hao ndio ambao wameutunza msitu huo pasipo Kuombwa wala Kukabidhiwa na serikali. Na kwa kweli wameweza kuutunza kwa muda wote huo. Miti haijakatwa, wananchi wamejiwekea sheria ndogondogo na pia kuwakamata wale ambao wamekuwa wakiharibu msitu huo. Hivyo wananchi hawa wamewajibika katika kuhakikisha msitu unabaki katika hali yake ya asili pasipo kushurutishwa na mtu yeyote. 

  Kwa mantiki hiyo muhtsari uliokuwa unaombwa na serikali ya halmashauri yan wilaya ulihiitaji baraka za wananchi, ambao hawakuwa tayari kutoa sehemu ya uhai wao unaotegemea msitu huo. Hakuna mwanakijiji aliyekuwa tayari kukubali ombi hilo. Na jibu lilikuwa ni wazi kabisa kwamba ombi hilo lilitishia mustakabali wa jamii zinazozunguka msitu huo ambazo ni vijiji vya Enguserosambu, Ng’arua, Orkiu na Naan. Hivyo wakati serikali ikipendekeza kuusimamia 

  msitu huo wananchi kwa upande mwingine wakaanza kuiomba serikali iwaruhusu kuusimamia. Ni kama kichekesho pande zote zinaombana kuusimamia msitu huo. Serikalikupitia halmashauri ya wilaya inasema tunahitaji kuusimamia, na wananchi wanaiomba serikali hiyo hiyo kuusimamia msitu huo. “Kwa kweli sisi kama wananchi wa Enguserosambu tumeona kwamba huu msitu ukiondoka chini ya usimamizi wetu tutaathirika. Kwa sababu msitu huu ni uhai wa wananchi wa hapa. Tukikosa huu msitu, hatupati maji wala mvua, tutakosa chakula. Kwa kifupi tutakosa kitu muhimu cha uhai wa jamii,” anaelezea mraghbishi Noorkiyengop 
  Mbaima. 

  Ndani ya msitu huu kuna miti ambayo wazee wanaitumia kwa ajili ya shughuli za kimila pamoja na miti ya kiasili ambayo inatumika kwa shughuli mbalimbali. Baadhi ya miti hiyo ni pamoja na Oroilieni ambao unatumika kwenye shughuli za jadi, ujenzi na kiimani. Akifafanua kuhusu mti huo Robert Kamakia anaelezea, “Huwezi kuingia jando bila kuwa na mti Oroilieni. Kwa kuwa unatumika katika kufanya baadhi ya shughuli za kimila. Mti mwingine ni Orikienyi ambao unatumika kama dawa ya kutibia magonjwa ya aina mbalimbali kama homa, kifua, malaria na kadhalika. Mti mwingine ni Ostiani ambao hutumika kwa ajili ya kivuli na kutunza maji.”

   Hivyo msitu huu una maana kubwa sana kwa makundi mbalimbali yakiwemo ya wazee, wanawake na vijana. K wa upande wa vijana kwa mfano, mila na desturi za kimasai zinawataka kujitenga hasa pale wanapoingia ngazi ya Morani. Ambapo hutakiwa kuweka kambi kwa ajili ya kuchinja ng’ombe na kula nyama. Tukio hili huchukua mpaka mwezi mmoja wakati vijana hao, wanapoazimisha sherehe hizo. 

  Tukio hili linashirikisha matumizi ya miti mbalimbali kwa mujibu wa taratibu zao. Supu wanazokunywa huchanganywa na baadhi ya majani ya miti hiyo. Ni dhahiri ulaji wa nyama kwa mwezi mzima unahitaji pia matumizi ya dawa za asili. Na ndio maana wamasai hawasumbuliwi sana na magonjwa yanayotokana na ulaji mwingi wa nyamba. Si hivyo tu porini hamna vitanda hivyo baadhi ya majani hutumika kwa ajili ya zoezi hilo.

   “Kiukweli bila msitu vijana hawawezi kufanya chochote. Kwa kuwa kila kitu kinatoka katika huo msitu,” anafafanua Julius Long’oli. Lakini si hivyo tu, wakati wanaingizwa jando pia kuna miti inayotumika. Vivyo hivyo na katika sherehe za kumaliza jando. Hivyo msitu ni sehemu ya mila na utamaduni wa jamii hizi zinaouzunguka. Ni imani yao pia, ambayo kimsingi ni lazima iheshimiwe. Huu ni msitu wao wa enzi na enzi. “Huu ni msitu wa jamii kwa Kimasai unaitwa Elieteti yaani ndani ya jamii kwa maana ya jina hilo ni msitu unaosaidia jamii ya sasa na ya kizazi kijacho. Kwamba huu msitu unategemewa na kizazi cha sasa na kijacho,” anafafanua Yohana Tuluni mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya kusimamia msitu. Mtizamo huu wa wananchi wa kata hii, kwamba wao ndio wausimamie msitu huu, unatokana hali halisi ya msitu namba moja wa Loliondo unaosimamiwa na serikali kupitia halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro kuwa katika hali ya kutoridhisha. Miti mingi imekatwa kwa ajili ya matumizi ya ujenzi na hivyo kutishia uhai wa msitu huo. Kitu ambacho wana Enguserosambu hawakupenda kitokee kwa msitu namba mbili wa Loliondo ambao wanautegemea kwa mustakabali wa maisha yao. Msitu huu umekuwa ukitegemewa na jamii ya hapa kwa miaka mingi. Ni wao ndio ambao wamekuwa wakiutunza na kwa kweli wamefanikiwa kwa njia moja ama nyingine kuufanya uwe mzuri zaidi kuliko hata ule wa Liliondo moja unasimamiwa na serikali. 

  “Wazo la kutaka kumiliki msitu lilikuwa kama ndoto, ukiangalia na hali halisi ilivyokuwa. Ni maono ya mtu mmoja aliyewashirikisha wenzake. Mwishowe wazo likatolewa Kwa wanakijiji ambao waliungamkono wazo hilo. Na mwishowe tukamwandikia Mkuu wa Wilaya na kwa kweli alituunga mkono sana,” anafafanua mraghbishi na mjumbe wa Bodi ya Wadhamini Jackso Nangiria Mchakato wa kuomba hadi kukabidhiwa usimamizi wa msitu umewezesha wananchi wa Enguserosambu kuongeza ufahamu wa mambo mbalimbali juu ya usimamizi wa misitu lakini pia mahusiano baina ya wananchi na viongozi yameboreka zaidi.

   Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu, hivi ndivyo unavyoweza kusema Wanaenguserosambu wamekuwa wamoja zaidi. Mashirika rafiki yamesaidia sana katika kutoa elimu kwa wananchi na viongozi wao ambao maarifa hayo yamewezesha kujiwekea mikakati na hatimaye kufanikisha jamii kumiliki msitu wake wa enzi kwenye mikono yake. Wakati mchakato unaanza palikuwa na kijiji kimoja tu cha Enguserosambu kilichokuwa kinaundwa na vitongoji vinne vya Enguserosambu, Ng’arua, Orkiu na Naan ambavyo sasa vimepata hadhi ya kuwa vijiji. Kwa sasa sauti yao ni kubwa zaidi kuliko pale Mwanzo.
  Watendaji wa PALISEP wakiwa pamoja na wanajamii wakishikana mikono kuonesha ushirikiano baina yao. Kuanzia kushoto ni Sarah Saningo, Robert Kamakia, Jackson Nangiria, Norkiyengop Mbaima, Sunde Tutayo na Fredy Samberu 

  Hivyo Bodi ya Wadhamini ilichaguliwa na mkutano mkuu wa kijiji, ambacho sasa kina hadhi ya kata. Kwa hiyo usimamizi wa msitu huu kwa sasa umekabidhiwa kwa Kata ya Enguserosambu. Hivyo wananchi kutoka katika kila kijiji walichagua wawakilishi wao waliounda Bodi ya Wadhamini. Wawakilishi hawa jukumu lao kubwa ni kuratibu mchakato wote wa uombaji usimamizi wa msitu wa Loliondo 2. 

  Baada ya kuchaguliwa wajumbe walipatiwa mafunzo na shirika la PALISEP ambao pia walisaidia uandikishwaji wa bodi tarehe 12/09/2012. Bodi hiyo imeundwa na wajumbe 10 kati ya hao wanawake ni 4. Bodi hii ilipata mafunzo ya sheria mbalimbali za misitu, usimamizi wa misitu na bodi yenyewe pia kupitia video ya hali ya msitu wa Loliondo 1. Walipata pia ziara za mafunzo kwa kutembelea misitu inayosimamiwa na jamii kwa mfano msitu wa Suledo uliopo Manyara wilaya ya Kiteto. Bila jamii kujitoa kwa hali na mali isingewezekana kufanikiwa kwenye hili. Kwani bodi ya wadhamini imefanya kazi kubwa. Jamii imeshiriki katika kuandika katiba ya bodi na sheria ndogondogo ambazo zimepitishwa katika mikutano ya vijiji. 

  “Baada ya kuchaguliwa jukumu letu ilikuwa ni kutembelea msitu ili kujua hali yake. Lakini pia tuliweza kutoa elimu kwa wale waliokuwa wanaishi na kufanya shughuli za kilimo ndani ya msitu. Ili waweze kuondoka. Si kazi rahisi,” mjumbe wa Kamati ya Bodi ya Wadhamini Sunde Tutayo.

  Kwa sasa mpango ni kuboresha na kutunza vyanzo vya maji. Kupitia bodi hiyo, wananchi wamejiwekea malengo ya kuuongeza zaidi kwa kupanda miti zaidi. Hili linafanywa kwa uangalifu mkubwa kwa kuwa kuna baadhi ya miti si rafiki mzuri kwa vyanzo vya maji inayakausha. Lakini si hivyo tu Bodi ya Wadhamini inaangalia njia sahii ya kuhakikisha kwamba zinapatika fedha za kununulia miti mipya. Wazo lililopo ni kuwakilisha mtizamo huu kwa wanajamii ili waweze kutaarifiwa na kusikilizwa nini yatakuwa maamuzi yao kwenye uchangishaji huo wa fedha. Changamoto nyingine ni uboreshwaji wa sheria ndogondogo kwa kuwa hakuna mipaka ya majukumu baina ya Bodi ya Wadhamini na Halmashauri ya serikali za vijiji. Kuna umuhimu wa suala hili kuwekewa utaratibu mzuri wa kiuwajibikaji kwa sababu muda mwingine vyombo hivi vinaweza kugongana kimawazo na kiutendaji na nani anawajibika kwa nani. 

  “Hapo nje kuna mikaratusi tumeikamata sisi kama Bodi ya Wadhamini. Mtu ameangusha mti mbichi ambao haujakauka. Na ameiyangusha bila idhini. Tumefanya hivi kwa kushirikiana na Mheshimiwa Diwani. Tunachosubili tukae na serikali ya kijiji ili tujue tunafanya nini,” anafafanua mraghbishi na Kaimu Katibu wa Bodi ya Wadhamini Jackson Nangiria. Kwenye kukabidhiwa msitu mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Wilaya na Diwani wa Kata ya Enguserosambu walikuwepo wakati wa kukabidhiwa kwa msitu huo pamoja na wenyeviti wa vijiji vyote vinavyounda kata ya Enguserosambu. Kwa hakika wenzetu wa Enguserosambu wameweza kujipanga na kuhakikisha kwamba msitu wao wa enzi unabaki mikononi mwao.

  0 0

  Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kigoma
  WAZIRI Mkuu Kassimu M Majaliwa(MB) (Pichani) kesho ataanza ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Kigoma.

  Akizungumza na waandishi wa habari juu ya ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya alisema kuwa Waziri Mkuu atawasili Mkoani hapa kesho majira ya saa tatu asubuhi.

  Alisema kuwa atapokelewa na viongozi mbalimbali wa serikali ya Mkoa na kisha atasomewa taarifa ya Mkoa.

  Baada ya hapo ataelekea katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyopo Wilayani Kasulu pamoja na kambi ya wakimbizi ya Nduta iliyopo Wilayani Kibondo.


  Na siku ya jumatatu atafungua mwalo wa kibirizi na kufanya majumuisho ya ziara yake katika ukumbi wa NSSF na kisha kurejea Dar es salaam

  0 0

  Afisa Muuguzi Msaidizi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam Mwanne Satara akimsaidia kumuelekeza Lulu Mohamed namna ya kumfunika nguo Mtoto aliyezaliwa usiku wa kuamkia Krismas Dar es Salaam ambapo akinamama 12 walipata watoto na Mmoja wa akinamama hao alipata mapacha 2 na kufanya watoto wa kiume kufikia 6 na wakike 7, kati yao akinamama waliofanyiwa upasuaji ni akinamama 10 na kati ya hao watoto njiti 2 na Hospitali ya Temeke akina mama waliojifungua hospitalini hapo kufikia idadi ya watoto 12, wakiume 4 na wakike 8 .
  (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA).

  Afisa Muuguzi wa Zamu wa Hospita ya Mkoa Amana Florensia Ndumbaro akizungumza na waandishi wa Habari (pichani hawapo), Hospitali tumepokea idadi ya watoto waliozaliwa mkesha wa Krismas ni 33 kati yao 15 ni wakike na 18 ni wakiume na wote wapo katika hali nzuri na wananyonya vizuri pia mama zao wanaendelea vizuri.

  0 0

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye aliyekuwa mgeni rasmi akimuwakilisha Makamu wa Rais Mh. Mama Samia Suluhu Hassan akizindua rasmi albam mbili za kwaya ya Wakorintho wa Pili kwenye tamasha la Krismas lililofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee leo, ambapo mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika ya Kusini Rebecca Malope amefanya onesho kubwa lililovuta hisia za mashabiki wengi waliohudhuria katika tamasha hili akishirikiana na waimbaji mbalimbali wa hapa nyu mbani na nchi jirani ya Kenya.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Nape Nnauye amewaomba watanzania kuzidi kumuombea Rais Dk . John Pombe Magufuli kwa kazi ya kutumbua majipu ambayo amekwishaianza kwani kazi hiyo ni ngumu na ina vikwazo vingi, lakini pia amewataka watanzania na waumini wa madhehebu mbalimbali kuwaombea wasaidizi wake ili waweze kuwa bega kwa bega na Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli ili kutekeleza kazi hii kwa ufanisi na kisha watanzania wafaidi matunda na rasilimali zao wenyewe.

  Waimbaji kutoka Kenya walikuwa ni Faustine Munishi na Sara K na Solomon Mukubwa kutoka jiji la Nairobi huku waimbaji wa hapa nyumbani wakiwa ni Rose Muhandom Upendo Nkone, Christine Shusho, Edson Mwasabwite, Joshua Mlelwa na wengine wengi, Tamasha hilo pia lilikuwa na lengo la kumshukuru mungu kwa nchi yetu ya Tanzania kufanya uchaguzi kwa amani, Kulia ni Akex Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion ambayo ndiyo imeandaa tamasha hilo.(PICHA NA JOHN BUKUKU- FULLSHANGWEBLOG-DAR ES SALAAM)
  Akex Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion ambayo ndiyo imeandaa tamasha hilo. akimkaribisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye ili kuzungumza na wananchi katika tamasha hilo kushoto ni Mbunge Martha Mlata na MC Mwakipesile mshereheshaji wa Tamasha hilo.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye akiwahutubia wananchi na mashabiki waliohudhuria katika tamasha hilo katikati ni Akex Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion ambayo ndiyo imeandaa tamasha hilo na kushoto ni MC Mwakipesile.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye akiimba moja ya mapambio na kuitikiwa na mashabiki wa nyimbo za injili waliohudhuria katika tamasha hilo.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye pamoja na maaskofu na viongozi mbalimbali wakishiriki katika sala maalum ya maombi iliyofanyika katika tamasha hilo,
  Wamumini na mashabiki mbalimbali wa muziki wa injili wakishiriki katika maombi maalum ya kumshukuru mungu yaliyofanyika kwenye tamasha hilo.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye na mkewe Mrs Rhobi Nape Nnauye wakicheza pamoja na mwimbaji Upendo Nkone kutoka kulia ni Mbunge Martha Mlata na Alex Msama wakishiriki kucheza.
   
  Mwimbaji Rebecca Malope akiimba katika tamasha hilo.
  Waimbaji wa mwimbaji Rebecca Malope akiimba katika tamasha hilo.
  Mwimbaji Rebecca Malope akiimba kwa hisia huku meza kuu pamoja na mashabiki wake wakiwa wamesimama.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye na mkewe Mrs Rhobi Nape Nnauye akicheza na mwimbaji Rebecca Malope wakati wa tamasha hilo. 
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye na mkewe Mrs Rhobi Nape Nnauye akicheza na mwimbaji Rebecca Malope wakati wa tamasha hilo kulia ni mbunge wa viti maalum mkoa wa mbeya Mary Majelwa na kulia ni Mbunge Martha Mlata.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye na mkewe Mrs Rhobi Nape Nnauye pamoja na maaskofu mbalimbali wakiwa wamesimama wakati mwimbaji Rebecca Malope akifanya vitu vyake katika tamasha hilo.
  Mwimbaji Christine Shusho na Mbunge Martha Mlata wakiimba pamoja wakati wa Tamasha hilo.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye na mkewe Mrs Rhobi Nape Nnauye,Alex Msama na Mkewe na baadhi ya wabunge kulia ni Martha Mlata na kushoto ni Mary Majelwa wakiwa katika picha ya pamoja.
  Mwimbaji Faustine Munishi kutoka nchini Kenya akiiimba katika tamasha hilo.
  Wanakwaya wa Wakorintho wa pili wakiimba wimbo wao mara baada ya kuzinduliwa kwa albam zao katika tamasha hilo.
  Mwimbaji kutoka nchini Kenya Solomon Mukubwa akiimba na mwimbaji mwenzake kutoka kushoto Sara K. huku mbunge Martha Mlata akishiriki kuimba nao.
  Mwimbaji Joshua Mlelwa naye amefanya mambo makubwa jukwaani katika tamasha hilo.

  Mwimbaji Rose Muhando pamoja na waimbaji wake wakifanya vuti vyao jukwaani.

  0 0


  Bondia Thomas Mashali kushoto akioneshana umwamba na Fransic Cheka wakati wa mpambano wao uliofanyika Morogoro. Mashali alishinda kwa point katika mpambambano huo wa raundi kumi.
  Bondia Thomas Mashali kushoto akikwepa konde kwa umahiri mkubwa lililorushwa na bondia Fransic Cheka wakati wa mpambano wao uliofanyika Morogoro. Mashali alishinda kwa point katika mpambambano huo wa raundi kumi.

  Mabondia wa kike Lulu Kayage kushoto na Mwanne Haji wakioneshana umwamba katika mpambano wao wa ubingwa wa raundi kumi ambapo Lulu Kayage alibuka bingwa wa TPBC kwa kumpiga Mwanne kwa point. Picha na SUPER D BOXING NEWS

  Bondia Lulu Kayage kushoto akimtwanga ngumi Mwanne Haji wakati wa mpambano wao wa ubingwa Lulu alishinda kwa point katika mpambano uho wa raundi kumi .

  Mabondia Mwanne Haji kushoto akipambana na Lulu Kayage wakati wa mpambano wao Lulu alishinda kwa point

  Bondia Vicent Mbilinyi kushoto akipambana na Deo Njiku wakati wa mpambano wao wa raundi sita Mbilinyi aslishinda kwa point mpambano huo.

  Bondia Vicent Mbilinyi kushoto akipambana na Deo Njiku wakati wa mpambano wao wa raundi sita Mbilinyi aslishinda kwa point mpambano huo.

  MABONDIA VICENT MBILINYI KUSHOTO SHABANI KAONEKA NA IMAN DAUDI MAPAMBANO WAKIMSHANGILIA USHINDI WA MBILINYI
   

  0 0

  IMG_7348Diamond Platnumz akisema na mashabiki wake waliofurika Dar Live usiku wa kuamkia leoIMG_7989Diamond akicheza na mashabiki wake waliofurika Dar Live.
  IMG_7359Akicheza na wacheza shoo wake wa kike.IMG_1416Nyomi ya kufa mtu ndani ya Dar Live wakiendelea kumshangilia Diamond.IMG_7371Wacheza shoo wa kike wa Diamond wakifanya yao.IMG_7324Diamond akiwachombeza mashabiki.IMG_7325Diamond akicheza na wacheza shoo wake wa kiume.IMG_7344Akiongea na mashabiki.IMG_7377
  IMG_7379IMG_7383Diamond akifanya yake na wacheza shoo wake.IMG_7390Diamond baada ya kuwakonga nyoyo mashabiki wake waliofurika Dar Live na wao kuridhika aliamua kupozi nao kwa picha hii.IMG_7432Nyomi ya kutisha ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live.IMG_7455
  IMG_7973Diamond akizidi kuwapa raha mashabiki wake wa Dar Live.IMG_7927Mashabiki baada ya kupagawa na shoo. IMG_7975...Akiongea na mashabiki wake.IMG_7991Akiwasalimia mashabiki.(PICHA: MUSA MATEJA, RICHARD BUKOS/GPL)

  0 0   Kampuni Ageco Energy & Construction Ltd ni kampuni ya kitanzania inayotoa huduma mbali mbali za ukandarasi ikiwemo ufungaji wa mitambo ya umeme wa jua (solar power) kwa watu binasfi, taasisi za umma, mashirika ya nje, na wateja wengine toka sekta binasfi.  Hivi majuzi Ageco ilikamilisha mradi wake wa mwisho wa mwaka kwa kufunga mtambo wa umeme wa sola ujulikanao kitaalamu kama solar hybrid backup system katika hospitali ya Mkoa wa Singida. 

   Mtambo huu wenye uwezo wa kuendesha vifaa vyenye jumla ya Kilowatt 15.7 utasaidia kutoa umeme kwa muda wa masaa 24 katika jingo la maabara la hospitali ya mkoa wa Singida hata kama umeme wa gridi ya taifa ukikatika. Mwezi wa Juni 2015, Ageco pia walifunga mtambo mwingine kama huu katika hospitali kuu ya mkoa wa Rukwa iliyoko Sumbawanga. Miradi hii imepewa ufadhili na Shirika la Misaada toka nchini Marekani linaloitwa Abbott Fund ambalo tayari limetoa misaada mingi katika kuimarisha sekta ya afya nchini Tanzania.

  Ageco ni kampuni ya kitanzania inayotoa huduma za ufungaji wa mitambo ya umeme wa kawaida, umeme wa jua, umeme unaotokana na mabaki ya takataka (biomass) pamoja na huduma za ukandarasi wa majengo/nyumba na barabara.  Bei zao ni nafuu na wanatoa huduma kwa ustadi na weledi mkubwa. Wanapatikana kwa njia ya simu kupitia namba 0758 733 333 au 062 222 064. Vile vile wanapatikana kwa email kupitia info@agecoenergy.com. Ofisi zao ziko barabara ya Bima, Mikocheni B, jijini Dar es Salaam. Unaweza pia kutembelea tovuti yao www.agecoenergy.com kwa maelezo zaidi kuhusiana na huduma zao.

  0 0

  SEM1
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimlaki Rais wa Zanzibar na  Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein  Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 26, 2015
  SEM2
  Rais Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika mazungumzo  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein  Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 26, 2015
  SEM3
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimsindikiza  Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein  baada ya mazungumzo  Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 26, 2015
  PICHA NA IKULU

  0 0  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
  Simu: 255-22-2114512, 2116898
   E-mail: press@ikulu.go.tz
  Tovuti : www.ikulu.go.tz              

  Faksi: 255-22-2113425
  OFISI YA RAIS,
        IKULU,
   1 BARABARA YA BARACK OBAMA,  
  11400 DAR ES SALAAM.
  Tanzania.
   

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Jumamosi 26 Desemba, 2015 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein Ikulu Jijini Dar es salaam.

  Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya mazungumzo hayo, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amesema  lengo la Mazungumzo hayo ilikuwa ni kumpa taarifa Rais Magufuli juu ya hali ya mazungumzo ya kisiasa yanayoendelea huko Tanzania Zanzibar baada ya uchaguzi Mkuu.

  Rais Shein amesema mazungumzo juu ya hali ya Zanzibar yanaendelea chini ya Kamati Maalum ambayo yeye ndiye Mwenyekiti na wengine wakiwa ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungo wa Tanzania Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa awamu sita wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume na Rais  Mstaafu wa awamu ya tano wa Zanzibar Dkt. Salmin Amour.

  Amesema tayari kamati hiyo imeanza mazungumzo tangu tarehe 09 Novemba, 2015 na kwamba mazungumzo hayo yamelenga kujadili hatma ya Zanzibar baada ya uchaguzi Mkuu.
  Rais Shein amebainisha kuwa mazungumzo hayo bado yanaendelea. 

  "Kwa hiyo nimekuja kumpa taarifa Mheshimiwa Rais Magufuli kuhusu maendeleo ya Mazungumzo yetu ili aweze kujua kinachoendelea akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo Zanzibar ni sehemu yake, na sisi ni jukumu letu kumpa taarifa hiyo" Alisema Rais Shein.
  Aidha Rais Shein ameongeza kuwa Mazungumzo hayo yatakapokamilika wananchi watajulishwa.

  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  26 Desemba, 2015


  0 0

  jo1
  Mkurugenzi wa  Kampuni ya Jambo Concerpt na Gazeti la  Jambo leo Bw. Juma Pinto akiwa katika picha ya pamoja na DJ John Peter Pantalakis kushoto na DJ Masoud Masoud kwenye uzinduzi wa kiwanja cha City Sports Lounge Posta maarufu kwa kuonyesha mipira ya ligi mbalimabli za ulaya, uzinduzi huo umefanyika alhamis wiki hii na kuhudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali. uzinduzi huo umefanyika kufuatia ukarabati na uboreshaji wa mambo mbalimbali katika klabu hiyo yaliyofanyika kwa muda wa mwezi mmoja.
  jo2
  Kutoka kulia ni Mwesa, Ally na Helman wakibadilishana mawazo huku wakishuhudia  zunduzi huo.
  jo3
  Chacha Maginga na wadau wenzake wakipozi kwa picha.
  jo4
  Wahudumu waliovalia sare nzuri wakwasikiliza  wageni waalikwa katika uzinduzi huo.
  jo5
  Wageni waalikwa mbalimbali walihudhuria katika uzinduzi huo
  jo6

  0 0
  Watendaji wa Kituo cha Maendeleo cha Jamii ya Uchunga wilayani Kishapu wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi mbele ya jengo la kituo hicho likiwa limekamilika kutokana na michango yao ya fedha na nguvu kazi.

  Na Krantz Mwantepele ,Kishapu

  Mabadiliko katika jamii yoyote kwa kiasi kikubwa huchangiwa na ongezeo la mahitaji ya
  binadamu katika mambo mbalimbali. Kwamba, kadri dunia inavyopitia mabadiliko,
  kadiri ile ile changamoto, mahitaji na huduma katika jamii husika huongezeka.
  Ili kufikia malengo yanayotokana na misukumo na mageuzi yasiyokwepeka, binadamu
  amelazimika kubuni mikakati mbalimbali ya maendeleo. Si hivyo tu, mabadiliko
  haya yamemfungulia binadamu fursa ya uthubutu wa kujaribu mambo mbalimbali,
  siyo tu kwa faida yake, bali jamii nzima inayomzunguka.  “Sikutegemea kama siku moja katika maisha yangu nitapata wazo ambalo lingebadili na kushawishi
  watu kuchukua hatua kwa mustakabali wa jamii.”
   
  Hiyo ni kauli ya mraghbishi Revocatus Richard ambaye pia, kitaaluma ni mwalimu katika shule ya msingi Uchunga. Richard alitoa kauli hiyo baada ya kupitia mafunzo ya uraghbishi na mwalimu mwenzake, Restusta Katobesi, ambao baadaye kwa pamoja, walianzisha Kituo cha KIMAJU (Kituo cha Maendeleo cha Jamii ya Uchunga) kwa kushirikiana na uongozi wa kijiji na wananchi. Na hilo ndiyo lilifanya achaguliwe kuwa Mkurugenzi wa kituo hicho.

  Walimu hao walikuwa miongoni mwa waraghbishi 30 walioshiriki mafunzo ya uraghbishi yaliyotolewa mwezi Machi, mwaka 2012 wilayani Kishapu katika mkoa wa Shinyanga. Kutokana na faida na maarifa waliyoyapata kwenye mafunzo hayo, walimu hao waliamua kuunda umoja uliokuwa chachu ya kuanzishwa kituo hicho cha maendeleo.

  Mwanazuoni Sarah Earl, aliwahi kusema: “Maendeleo ni watu na mazingira yao. Kwamba, kusingekuwa na maana iwapo barabara, hospitali, shule na miradi mingine ya maendeleo inayojengwa kwa ajili ya watu isingetumika.”

  Kwa mantiki hiyo, miradi yote ya maendeleo, ikiwamo Chukua Hatua ni kwa ajili ya ustawi wa maisha ya watu. Kwa kuwa kiini cha maendeleo ni watu. Shabaha kubwa ya mradi huu wa Chukua Hatua ni kuhakikisha wananchi (waraghbishi) wanajielewa na kujitambua katika kutimiza majukumu yao na kupata haki zao zikiwamo huduma bora za kijamii na kuhakikisha wananufaika na rasilimali zao. Pia unawasaidia kuwawajibisha viongozi wao ili watimize majukumu yao ya kuhamasisha maendeleo na kutatua shida za wananchi.

  Mraghbishi ni mwananchi anayeleta uhai mpya ndani ya jamii kwa kutambua matatizo na kupendekeza njia sahihi za kuyatatua.Katika kipindi cha miaka mitano ya mradi, zaidi ya waraghbishi 380 wameleta uhai katika jamii zao, hususani kwenye vijiji vya mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Geita na Arusha hasa katika wilaya ya Ngorongoro.


  Tafsiri
  ya uhai huu ni pamoja na kuwachukulia hatua viongozi wabadhirifu, watendaji
  wabovu, kuandaa midahalo, kudai huduma bora za kijamii, kuibua na kufuatilia matatizo
  mbalimbali katika vijiji vyao kama ambavyo waraghbishaji Richard na Katobesi
  wamefanya.

older | 1 | .... | 722 | 723 | (Page 724) | 725 | 726 | .... | 1904 | newer