Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

NSSF KUKABIDHI DARAJA LA KIGAMBONI JANUARI 2016

$
0
0

Meneja wa Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Mhandisi John Msemo akimuonesha Waziri muunganiko wa barabara zinazoingia katika daraja hilo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akizungumza na waandishi wa habari.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhani Dau akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni wakati waziri huyo alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo, ambapo ujenzi wake utakamilika mwishoni mwa mwezi Januari mwakani.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhani Dau (katikati) wakati alipofanya ziara ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Mradi ujenzi wa Daraja hilo. Mhandisi Kareem Mataka.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhani Dau (wa pili kulia), akitoa maelezo kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (kulia), alipofanya ziara ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo, ambalo ujenzi wake utakamilika Januari Mwakani.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau wakati alipofanya ziara ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo ambalo ujenzi wake utakamilika Januari Mwakani.

Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau wakati ziara yake Daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau akifafanua jambo.
Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akizungumza wakati alipofanya ziara katika Daraja la Kigamboni.
Sehemu ya Daraja la Kigamboni.
Waziri akipata maelezo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni.




WAZIRI wa Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama amelitaka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kuhakikisha linakabidhi daraja la Kigamboni ifikapo Januari, 2016.

Pia ametoa fursa kwa shirika hilo na mengine nchini kama yataweza kuja na mradi wa ujenzi wa daraja kutoka Dar es Salaam hadi Zanzibar.

Hayo alibainisha jana jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa daraja hilo, ambalo linatarajiwa kukamilika mwakani.

Alisema ujenzi wa daraja hilo, umegharimu kiasi cha Dola za Marekani 143.5, ambapo serikali imetoa asilimia 40, huku NSSF ikitoa asilimia 60 ya fedha zote.“Tunaliomba shirika hili, lihakikishe linaheshimu nha kuzingatia muda uliotoa katika kukabidhi daraja hilo mwakani licha ya kujitokeza ujenzi mwingine wa barabara ya Kilomita moja,”alisema.

Alisema shirika hilo linapaswa kulikabidhi daraja ifikapo Januari 30 au kabla ya muda huo, kwani ukamilifu wake utapunguza adha ya foleni na kukuza sekta ya uchumi inayotarajiwa kukuwa kwa kasi.

Katika hatua nyingine, Mhagama alisema endapo mradi ukiwa katika ubora na viwango vinavyotakiwa utadumu kwa muda mrefu na kuisaidia Seriali katika kukuza uchumi.

“Miradi ya namna itasaisdia kukuza uchumi wa ndani na nje ya nchi, pia inatufundisha kujifunza ili kujua kwamba tunaweza kuhimili miradi mingine mikubwa zaidi ya huu,”alisema.

Kuhusu daraja la kutoka Dar es Salaam hadi Zanzibar, alisema uwezekano wa kujengwa upo endapo mashirika yakijitokeza na mradi huo. “Kila kitu kinawezekana, hivyo kama Shirika litajitokeza serikali ipo tayari kwa kila kitu kuunga mkono mkakati watakao kuja nao,”alisema.

Naye Mkurungenzi wa NNSF, Dk.Ramadhan Dau alisema ujenzi wa daraja hilo umekuwa wa kasi licha ya matatizo yaliyojitokeza, hivyo Watanzania watarajie Januari mwakani kulitumia.

“Bado kuna sehemu nyingine ambazo tutamalizia ila hadi Januari litakuwa limekamilika kwa asilimia 100, hivyo tunaipongeza serikali kwa ushirikiano uliotuonyesha,”alisema.

AKINA MAMA NA VIJANA NI NGUZO KUBWA YA KULETA MABADILIKO KATIKA VIJIJI.

$
0
0
Bwana Bony Lukas akieleza jinsi anavyofanya uraghbishi hasa katika kuwasaidia vijana kujua haki zao na kujitambua.

Na Fredy Njeje wa Blogs za Mikoa. 
Ni suala ambalo lipo wazi kuhusu tofauti za kimaisha baina ya wakazi wa mijini na vijijini, ila changamoto nyingi zaidi zinaonekana kuwakabili zaidi wale wanaoishi vijijini. Huko wananchi wanakosa huduma ambazo kimsingi ni haki zao na hivyo kutokuwa na usawa baina yao na wale wa mijini.

Picha kubwa inayojionesha vijijini kwa upande wa wanawake ni hasi kwa kiasi Fulani ukilinganisha na ile ya wanaume. Usawa wa kijinsia na kielimu baina yao na wanaume ni mkubwa sana, kesi za unyanyasaji kwao ni nyingi zaidi. Pamoja na jihudi nyingi za kuwawezesha wanawake bado hawajapata nafasi ya kutoshwa kuweza kusikilizwa. Wanaume wameendelea kuwa watoa maamuzi na wanufaikaji wa kimfumo. 
Mmoja wa waraghbishi akiwa anaonesha ripoti ya wanafunzi watoro katika shule ya msingi ya Nyandekwa .

Takwimu zinaonesha kuwa hata idadi ya ufauru kwa wasichana kwa Shule za msingi imeongezeka ambapo mwaka 2013 wasichana waliofaulu ni 281,460 sawa na asilimia 50.20 ya wanafunzi 560,706 wakati wavulana waliofaulu ni 279,246 sawa na asilimia 49.80. Kabla ya ya matokeo wasichana waliofanya mtihani walikuwa 456,082 sawa na asilimia 52.68 na wavulana 409,745 sawa na asilimia 47.32. Mwaka 2014 jumla ya watahiniwa 808,085 wa shule za msingi Tanzania wasajiliwa kufanya mtihani huo wakiwemo wasichana 429,624 sawa na asilimia 53.17 na wavulana 378,461 sawa na asilimia 46.83. Jumla ya watahiniwa 451,392 kati ya 792,118 walifanya mtihani, wasichana waliofauru ni 226,483 ambao ni sawa na asilimia 53.59 na wavulana 224,909 sawa na asilimia 46.41. 
Mraghishi Mariam Stephano (katikati) akieleza jambo wakati wa kikao.

Katika nchi yetu ya Tanzania kuna makabila zaidi ya 100 na kila moja likiwa na mila na tamaduni zake. Ni vizuri ikaeleweka kwamba wazee wetu hawakuwa wakichangamana kimakabila hivyo ni watu wachache walikuwa wanahama toka sehemu moja kwenda nyingine. Aina hii ya maisha ilipelekea wengi wao kuoana wa kabila moja, tofauti ikiwa ni vijiji ama kata, ila wengi ilikuwa toka mkoa ama wilaya moja. 

Tofauti na sasa ambapo watu wanachanganyikana kutokana na shughuli za kiuchumi na kijamii. Hali hii ya kuchanganyikana baina ya makabila ndani ya mkoa ama wilaya ama kijiji kimoja imeleta tamaduni tofauti na zile ambazo zilikuwa zimezoeleka kiuchumi na kijamii.

Pamoja na mchanganyiko huo bado kumekuwa na changamoto nyingi sana zinazowakabili wakazi wa vijijini. Bado wanaishi kwenye lindi la umaskini na ukosefu mkubwa wa huduma za kijamii. Changamoto hizi zinasababisha baadhi yao kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanadai na kusimamia haki za msingi za kijamii; hawa wanaitwa waraghbishi.

Waraghbishi ni mtu mmoja mmoja ama kikundi cha watu ambao wamevutika kufanya uraghbishi aidha kwa kufundishwa ama kwa kuona matokeo ya matendo wanayofanywa na wanajamii wenzao. Hususani wale ambao wanachukua hatua katika kustawisha au kulinda haki za binadamu na kuwakumbusha wenzao majukumu yao kwa maslahi ya kijamii, kiuchumi ama kisiasa.
Matilda Peter(wa pili kushoto) aliyeanza Uraghbishi 2015 akieleza namna anavyofanya Uraghbishi kwa kuwapa elimu wasichana juu ya kujitambua, na kuepuka mimba za utotoni.


Moja ya haki hizo ni zile za wanawake ambao kwa muda mrefu wameonekana kuwa nyuma zaidi. Hali hii imewaondelea kujiamini na kujiona wao ni wa daraja la pili na hivyo kutokuwa na sauti katika jamii zao. 

Mmoja wa waraghbishi hao ni Bw. Bony Lukas toka kijiji cha Nyandekwa wilayani Kahama katika mkoa wa Shinyanga. Mraghbishi huyu ameweza kuelimisha watu wa kijiji chake. 

Akielezea jinsi anavyoraghbisha vijana katika kijiji chao, Lukasi anasema: 

“Vijana ndio wenye nguvu za kuweza kuleta maendeleo na ndio wenye mchango mkubwa ndani ya jamii zetu. Kwa hiyo ni lazima wawe ni watu wenye kujitambua katika nyanja zote. Ili waweze kupata nafasi mbalimbali za kuweza kutoa mchango wa mawazo ili yaweze kufanyiwa kazi” 

Hali inatokana na ukweli kwamba vijana wamekuwa nyuma kwa muda mrefu bila. Uraghbishi kwao ni mrejesho wa nafasi finyu ambazo vijana wa vijijini wamekuwa hawapewi nafasi ya kuweza kuchangia pindi wawapo katika mikutano ya kimaendeleo ndani ya vijiji. Hii ilitoa nafasi ya mraghbishi kupokea mawazo kutoka kwa vijana wa kike na wakiume kwani vijiji vilivyo vingi hupuuza mchango wa mawazo ya mtoto wa kike na kumuona hana thamani. 

Kwa mantiki hiyo mraghbishi Lukasi aliweza kuwatia ujasiri kwa kutoogopa kwani watakavyo kuwa na roho ya uoga ndio itakayo wafanya wabaki nyuma kimaendeleo. Kuna msemo unasema “woga wako ndio umaskini wako”. Hivyo alihakikisha anawawezesha vijana kujiamini na kushirikiana vyema na uongozi wa kijiji. 

Elimu ya jinsia pia ni tatizo katika vijiji vingi vya hapa Tanzania ambapo mraghbishi Miriam Stephano yeye aliweza kutumia nafasi hiyo kwa kuweza kuwaelimisha vijana kuhusu elimu ya jinsia. Akilielezea hilo anasema: 

“Hapa kijijini kuna vijana wa rika tofauti tofauti. Wapo wale ambao ndio wanabalehe na wale waliovuka hiyo ngazi ya kubalehe. Mabadiliko hayo ya kimaumbile hupelekea vijana wengi kuanza kuwa na muelekeo usio sahihi. Sababu ikiwa ni mihemko inayo wakumba pindi wawapo katika shughuli za kila siku hasa kwa wale wanao soma.” 
Mraghbishi Bujika Adam Joseph kutoka kijiji cha Guduba akitoa mchango wake wa namna alivyofanya uraghbishi kwa kuwahimiza vijana kuhudhuria mikutano ya vijiji ili nao wapate kushiriki katika kutoa mawazo na michango yao mbalimbali ya mawazo.

Vijana hawa katika kijiji hicho wanapata changamoto mbalimbali zinazotokana na mabadiliko ya kimaumbile. Hili linapeklekea kupata mimba za utotoni pamoja na maambukizi ya virusi vha Ukimwi. Hivyo kupitia waraghbishi vijana hawa wamekuwa wakipewa elimu ili waweze kujikinga na kujiepusha na hari zinakokuwa zikiendelea kuleta mabadiliko katika miili yao. 

Changamoto hii ndio iliyomplekea mraghbishi huyu mwanamke toka kijiji cha Nyendekwa, wilayani Kahama Bi. Mariam Stephano kuraghbisha kundi hili, kama anavyofafanua yeye mwenyewe: 

“Nikiwa kama mwanakijiji mraghbishi huwa ninapita katika mashule mbalimbali. Huko naomba ruhusa kwa mwalimu mkuu na kuweza kuzungumza na wanafunzi wa kike jinsi gani wanaweza kushughulika na mabadiliko ya miili yao. Nawaelekeza nini wafanye pindi wanapofikia umri wa kubalehe. Hapo ntawafundisha usafi wa mwili na namna ya kukwepa vishawishi vitakvyowapelekea aidha kupata maambukizi ya virusi vya Ukumwi ama mimba za utotoni”

Elimu hii ya jinsia inawasaidia watoto katika kijiji cha Nyandekwa, kwani wengi wao huanza kujitambua na kuwa na akili ya kutafakari yale yaliyo mema na mabaya. Na pia inawasaidia hata upande wa serikali katika dhana ya kupunguza maambukizi ya Ukimwi na magonjwa ya zinaa. 
Bi Anna Zengu aliyepata uwenyekiti wa Kitongoji cha Busolwa kutokana na Uraghbishi akielezea kwa kina jinsi alivyo wasaidia akina mama wenzake kujitambua na kujua umuhimu wa kupiga kura na kuchagua viongozi bora wanaofaa kuongoza Taifa.

Kwa upande wa mraghbishi Wilbert Michael kutoka kijiji cha Kakebe wilayani Kahama yeye alifanya utafiti usio rasmi juu ya tabia za uongozi wa kijiji chao. Hapo aliweza kugundua mambo kadhaa yaliyokuwa yakifanywa na viongozi wa kijiji hicho pasipo kuwashirikisha na wananchi. Na walifanya hivyo kwa maslahi binafsi. 

Akielezea hali hiyo, Michael anasema:
“Kupitia uraghbishi nilionao niliweza kufuatilia mambo mbalimbali katika ofisi ya kijiji pamoja na ile ya kata. Lengo ikiwa ni kubaini tatizo lililokuwa linakabili kijiji. Kubwa likiwa ni viongozi kujali maslahi binafsi, hapakuwa na uwazi kwenye mikataba ya kimaendeleo ya kijiji,”

Swali la kujiuliza yeye mraghbishi alijuaje habari hizo, akijibu swali hilo ansema:

“Nililigundua kupitia mbao za matangazo ambapo walibandika tangazo la kuingia kwa mkataba na watu wanao sambaza vyandarua vijijini na wao kuchukua kama ni mradi wa kujipatia kipato. Kupitia mradi vijana walitakiwa kugawa vyandarua hivyo, na hivyo ilikuwa ndio iwe ajira yao.”

Badala yake Mwenyekiti na Afisa Mtendaji wa kijiji wao wakawa wanawachangisha vijana fedha kiasi cha shilingi elfu kumi (10,000) kwa kila mmoja. Lengo lao likiwa ni kuwasajili kwa kuwa wasambazaji wa vyandarua hivyo kinyume cha dhana nzima ya kuleta maendeleo kijini. 

Na ndipo mraghbishi Michaeli alitumia uraghbishi wake kwa kuweza kuwataarifu wananchi na ndipo wananchi walipoamua kumwajibisha mwenyekiti huyo. Walichoamua ni kupeleka malalamiko katika ngazi mbalimbali za kata na wilaya ili waweze kumvua madaraka yake na kupendekeza jina la mweenyekiti mpya wanayemtaka na atakayeshirikiana na wanakijiji.

Hii ni dhahiri kwamba bado wananchi wanaoishi vijijini wanahitaji elimu ya kiraia itakayowawezesha kuwasilisha matatizo yao kwenye ngazi husika. Ili nao waweze kuwasaidia wenzao wanapogundua yale yanayofanywa na viongozi wao hayaendani na dhana ya ukweli na uwazi. Na piakuwa na ujasiri wa kuweza kuongea sehemu mbalimbali. 
 Baadhi ya wakazi wa kata ya Nyandekwa wakiwa wanajadiliana jambo.

Pata punguzo la tiketi za Diamond Dar Live

$
0
0
mpya diamondMwandishi wetu KAMPUNI ya simu za mkononi, Airtel kupitia huduma yao ya kijanja kimawasiliano ya Airtel Money Tap Tap wanakuletea punguzo la bei za tiketi za kumshuhudia staa wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Krimasi (kesho) ndani ya Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem jijini Dar. Akizungumza na Amani, Meneja Huduma wa Airtel, Moses James alisema kuwa mteja anatakiwa kununua laini yake ya Airtel kisha kujiunga na huduma ya Airtel Money Tap Tap na baada ya hapo atakabidhiwa namba ya siri ambapo ili kuanza kutumia huduma hiyo rasmi ni lazima mteja aweke kiasi cha kuanzia shilingi 11,000. 

“Watoa huduma wetu wa Airtel wanatoa huduma hii katika matawi yetu yote na hata ukienda Dar Live utaipata. Siku ya shoo ya Krismasi unachotakiwa ni kuonesha kadi yako ya Airtel Money Tap Tap kisha utapunguziwa bei ya tiketi kuanzia VIP ambayo ni 30,000 utapata kwa 25,000, kawaida 15,000 utapata kwa 10,000,” alisema Moses.

Salaam za mwisho wa mwaka toka kwa Balozi Wilson Masilingi

Wachora vibonzo tujitokeze, tupaze sauti ili serikali awamu ya tano ijue matarajio yetu

$
0
0
Mchora vibonzo Nathan Mpangala akifundisha uchoraji baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Koboko, Moshi mwaka 2011. Ili tufanikiwe katika sanaa, uibuaji na ukuzaji vipaji kuanzia umri mdogo havikwepeki.
Hivi karibuni, Rais wa Jamhuri wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, ameteua Baraza la Mawaziri ikiwemo Wizara ya Habari, Michezo, Utamaduni na Wasanii (Sanaa) inayoongozwa na Mh. Nape Nnahuye. 

Binafsi kutajwa moja kwa moja  kwa wasanii (wa sanaa za ufundi, muziki, filamu na jukwaani) katika wizara naona ni hatua moja mbele. Sasa, natarajia wizara itajishughulikia maswala ya wasanii kwa mtazamo tofauti na miaka iliyopita ambapo wasanii tulijumuishwa kwenye kapu la utamaduni hali iliyosababisha kutokuwepo kwa njia rasmi za uibuaji na uendelezaji vipaji, kutokuwepo na ulinzi wa ubunifu, sanaa kutochukuliwa kama ajira rasmi nk. 

Nachukua nafasi hii kutoa wito kwa wachora vibonzo wote nchini, kama wafanyavyo wasanii wa sanaa za aina nyingine nasi tujitokeze, tupaze sauti, tusemee maono na matarajio yetu ili tuisaidie serikali ya awamu ya tano katika mipango yake inayohusiana habari na wasanii. 

Kwa kipindi kirefu sasa, wachora vibonzo nchini tumekuwa tukielimisha, kufundisha, kuburudisha na hata kuitangaza nchi kimataifa. Pia tumesaidia mauzo ya magazeti na kuvutia watazamaji kwenye luninga. 


Pamoja na mafanikio hayo, kumekuwa na changamoto mbalimbali ambazo zikikwamisha fani hii. Vikwazo hivo ni pamoja na kutokuwepo kwa njia rasmi ya uibuaji na ukuzaji vipaji mashuleni, wachora vibonzo wengi wao kutokuwa na mikataba ya kazi, kuwepo kwa mazingira ya kazi ambayo si rafiki, malipo duni na wakati mwingine hayana uhakika, kutokuwepo kwa mafunzo ya mara kwa mara, wachoraji vibonzo tumepuuzia vikundi/vyama vyetu vya kutetea stahiki zetu za jumla nk. 

Hali hii imefanya uchoraji vibonzo kutoshamiri ukilinganisha mataifa yaliyoendelea. Hatuna uhakika na kesho. Imeathiri ubunifu, mafunzo, vipato na haki miliki. Wachora vibonzo wanaochipukia wamekuwa wakikatishwa tamaa. 
Sasa ni wakati mwafaka wachora vibonzo tujitokeze, tuzisemee haki zetu ambazo tunaamini ni stahiki yetu. Tukifanya hivyo tutakuwa tunajiwekea mazingira mazuri ya kazi na pia tutakuwa tumekitendea haki kizazi kijacho. Uhakika wa uibuaji, ukuzaji na ulinzi wa ubunifu na haki zingine za wachoraji vibonzo wa kesho inategemea misingi imara tutakayoiweka leo.

Baadhi ya matarajio yetu toka kwa serikali ya awamu ya tano;

1.       Somo la sanaa lirudishwe mashuleni kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.
2.       Wakati huu Serikali inapopanga mikakati yake kuhusu wasanii ikumbuke kuwa kuna wachora vibonzo.
3.       Kwa kuwa tunafanya kazi katika vyombo vya habari, serikali inapokuwa ikishughulikia masuala ya habari isisahau kwamba wachora vibonzo nao ni sehemu na wana uzito sawa kama ilivyo kwa wanahabari wengine.
4.       Kwa kuwa hakuna njia rasmi za ukuzaji sanaa ya uchoraji vibonzo nchini, natoa wito kwa vyombo vya habari kugharama mafunzo ya wachora vibonzo mara moja moja.
5.       Wachora vibonzo, huu si wakati tena wa kunung’unika. Tuungane, tupaze sauti ya pamoja kuhusu stahiki zetu ili tuisaidie serikali ya awamu ya tano kujua maono na matarajio yetu. Tukiendelea kukumbatia ubinafsi, hakuna mtu atakayesimama kwa niaba yetu. Na ikitokea serikali kutusahau basi kabla hatujainyooshea kidole itabidi kwanza tujilaumu wenyewe. Sauti ya pamoja inahitajika katika hili tena sasa hivi.
6.       Tuimarishe vikundi/vyama vyetu ili tuvitumie kutetea stahiki zetu na kizazi kitakachokuja. Katika hili hakuna njia ya mkato.
7.       Kwa kuwa wengi wetu tunajitegemea, ni wakati mwafaka sasa wa kuwepo kwa mikataba baina ya wachora vibonzo na vyombo tunavyofanyia kazi. Pamoja na mambo mengine mikataba hiyo izingatie haki miliki na malipo ya kuridhisha.

Kwa kumalizia navishukuru vyombo vya habari kwa kutumia vibonzo kwa wingi. Pia, nazipongeza taasisi mbalimbali za serikali na binafsi kwa kutumia vibonzo kwenye machapisho yao. 
Mwisho lakini si kwa umuhimu, nazipongeza taasisi mbalimbali ambazo zimetambua na kuamua kutoa tuzo kwa wachoraji vibonzo. Hatua hii inatia moyo na tunaiunga mkono kwani inachochea ubunifu zaidi.

Asante. 

Imetolewa na:
Nathan Mpangala,
(Mchora vibonzo),

MUWSA YAWAPATIA MAJI WAKAZI WA ENEO LA SHABAHA WILAYA YA MOSHI VIJIJINI.

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Amos Makala akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi w mradi wa maji katik eneo la Shbaha wilaya ya Moshi vijijini.
Mkuu w mkoa Makala akifungua maji ktika moja ya Kilula katka eneo la Shbh wilaya ya Moshi vijijini.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Amosi Makala akimbebesha ndoy maji mmoja wa wakazi katika eneo la Shabaha mara baada ya kuzindua mradi huo.


Mkuu wa wilaya y Moshi,Novatus Makunga akizungumza wkati wa uzinduzi huo.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjro,Amosi Makala akifurahia jambo wakati akitoa hotuba yake ya uzinduzi wa madi wa maji katika eneo la Shabaha.
Baadhi ya wafanykazi wa MUWSA.
Mwenyekiti wa Bodi ya MUWSA,Sharry Raymond akimkaribisha Mbunge wa Jimbo la Moshi mjini Jafary Michael ,
Mbunge wa Jibo la Moshi mjini,Jafary Michael akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya MUWSA ,Sharry Raymond akimkaribisha Mwenyekiti wa Halmashuri ya wilaya ya Moshi ,Michael Kilawila .
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawila akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo.



Mkuu wa mkoa wa Kilimajaro,Amos Makala akifurahia jambo na Mbunge wa jimbo la Moshi mjini Jafary Michael mara baada ya uzinduzi wa mradi w maji wa Shabaha.
Mkuu wa wilaya ya Moshii ,Novatus Makunga akifurahia jambo na Mbunge wa jimbo la Moshi mjini Jafary Michael mara baada ya uzinduzi wa mradi w maji wa Shabaha.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Amosi Makala akiwa katika picha ya pamoja na Bodi ya wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA).
Wafanyakazi wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira mjini Mosi,MUWSA,wakifurahi mara baada ya kukamilisha mradi wa maji katiika eneo la Shabaha.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kskazini. 






Mkuu wa mkoa wa Kilimnjaro ,Amos Makala akiwa ameongozana na Mwenyekiti wa Bodi ya wkurugenzi wa Mamlaka ya maji sfi na usfi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Sharry Raymond kwa ajili ya uzinduzi wa mradi wa usambazaji wa maji katika eneola Shabaha,wilaya ya Moshi vijjini.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na u safi wa mazingira mjini Moshi,MUWSA ,Joyce Msiru akiwasili katika eneo la mradi huo.
Baadhi ya viongozi walifika kwa ajili ya uzinduzi wa mradi huo,kutoka kushoto ni Mwenykiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawila,Mbunge wa Moshi mjini na mjumbe wa bodii ya Muwsa ,Jafary Michael wakiwana Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi MUWSA,Sharry Raymond.
Baadhi ya wajumbe wa Bodiya Wakuugenzi ya MUWSA,kutoka kulia ni Hajira Mmambe,Elizabeth Minde,na Mhandisi Alfedy Shayo.

Makamu Mwenykiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya MUWS,Profesa Faustine Bee akifanya utamburisho wa wageni mbalimbali waliofika katika eneo la Shabaha kwa ajili ya uzinduzi wa mradi wa maji.
Baadhi ya wafanyakazi wa MUWSA.
Diwani wa kata ya Mabogini ,Emnuel Mzava akizungumza wkati wa uzinduzi wa mradi wa maji katia eneola Shabaha lililopo katika kata yake.
Baadhi ya Viongozi wa MUWSA,kutoka kushoto ni Mkaguzi wa ndani wa MUWSA,Benson Maro,Meneja rasilimali watu Michael Konyaki na Meneja ufundi ,Mhandisi Patrick Kibasa.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjni Moshi,MUWSA,Joyce Msiru akitoa taarifa juu ya utekelezaji wa mradi wa maji katika eneo la Shabaha ambao umetumia siku 25 hadi kukamilika kwake.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjni Moshi,MUWSA,Joyce Msiru akikabidhi taarifa y utekelezaji wa mradi huo kwa Mkuu wa mkoa wa Kilimnjaro,Amosi Makala aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi huo wa maji.
Baadhi ya wafanyakazi wa MUWSA.
Kikundi cha Ngoma cha Msnja kikitumbuiza wakati wa uzinduzi huo.
Baadhi ya wananchi waliofika katika uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ,Shrry Raaymond akizungumza katika uzinduzi huo.
Badhi ya wfanyakazi wa Mamlka ya maji safi na usafi wa Mazingir mjini Moshi (MUWSA).

SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LAFUNGUA KITUO CHA AFYA CHENYE HADHI YA KIMATAIFA KWAAJILI YA WAFANYAKAZI WAKE ABUDHABI

$
0
0
Ukataji wa Utepe mwekundu (Kutoka kushoto kwenda kulia): Naser Al Mazroei, Mkurugenzi mtendaji kitengo cha huduma kwa wateja katika mamlaka ya vitambulisho Emirates; Ray Gammell, Afisa mkuu wa Utendaji na Watu kutoka Shirika la ndege la Etihad; Dk Nadia Bastaki, Makamu rais huduma za matibabu; Dk Mariam Buti Al Mazrouei, Kaimu afisa mtendaji wa Ambulatory Healthcare Services; and Dk. Mubarak Al Darmaki, Kaimu afisa mkuu wa kliniki kutoka Ambulatory Healthcare Services.

SSHIRIKA la ndege la Etihad ambalo ndio shirika rasmi la nchi ya Falme za kiarabu, leo hii imefungua milango ya kituo cha afya chenye hadhi ya kimataifa kwa ajili ya wafanyakazi wake Abu Dhabi. Kituo hiki ambacho ni kikubwa kwa mazingira kitatoa huduma za kliniki, huduma za kitabibu kwa wafanyakazi wenye visa pamoja na raia wenye vitambulisho toka falme za kiarabu. 
Kituo hicho kilichopo jengo la Etihad Plaza, mjini Khalifa, kitaruhusu wafanyakazi zaidi ya 23,800 wa shirika hili la ndege wenye makazi nchi ya Falme za kiarabu kupata huduma bora za kitabibu, katika mazingira ya kisasa karibu kabisa na makao makuu ya shirika hilo la ndege.

Afisa mkuu wa rasilimali watu na Utendaji, Ray Gammell, alisema “Kama muajiri bora zaidi duniani, tunajivunia kwa kutoa huduma kwa timu yetu kubwa ya wafanyakazi, wakiwemo wa nchi ya falme za kiarabu na wakigeni. Kituo hiki kipya kitaruhusu tuendelee kuboresha programu zetu zinazolenga kutunza afya za wafanyakazi wetu na hivyo kuongeza ufanisi wao wa kazi.

Upanuzi wa Kliniki mpya ya anga ni sehemu ya mkakati maalumu wa shirika la ndege la Etihad kuwa na kituo cha afya kinachoongoza katika kanda hiyo. Kituo kikiwa na wahudumu wa afya zaidi ya 30 waliobobea, wakiwemo madaktari bingwa 10, vyumba sita vya uchunguzi, vyumba tisa vya madaktari na vifaa vya kisasa kabisa kusaidia wafanyakazi, kliniki ina ahidi kutoa huduma bora kabisa ya kitatibu na afya kwa wafanyakazi wa shirika la ndege la Etihad.

Dk. Nadia Bastaki, makamu raisi wa huduma za afya, alisema “Kliniki mpya yenye viwango vya kisasa kabisa inaonyesha dhamira yetu kuendelea kutoa huduma za afya zenye viwango vya juu kabisa kwa ajili ya wafanyakazi wetu ikiwemo marubani na wahudumu wa ndani ya ndege. Kliniki hii inasimamiwa na mamlaka ya afya ya Abu Dhabi (HAAD) na mamlaka ya usafiri wa anga UAE (GCAA), tukiwa na furaha ya kutambulika kama moja ya kituo kinachoongoza katika huduma za utabibu na vifaa katika sekta ya anga.”

Wafanyakazi wa shirika la ndege la Etihad pamoja na wategemezi wao pia wataweza kupata huduma kutoka kituo hiki cha matibabu ili kusaidia mchakato wa maombi ya VISA. Kuna makubaliano yaliyosainiwa mwezi Februari 2015 na Ambulatory Healthcare Services – SEHA kuendesha kituo hicho na kutoa huduma za vipimo kwa ajiliya Visa kama X-Ray, vipimo vya damu na vipimo vya mwili.

Dk. Mariam Buti Al Mazrouei, Kaimu mtendaji mkuu wa Ambulatory Healthcare Services (AHS), alisema: “lengo letu kuu baina ya SEHA na AHS ni kuboresha upatikanaji wa huduma za kiafya na ufunguzi wa kituo cha vipimo kwa ajili ya mchakato wa VISA ni mfano wa jinsi gani lengo letu linaweza kufikiwa kupitia ushirikiano wa wadau kutoka sekta mbalimbali nchini. Kituo kipya kinaleta idadi ya vituo vinavyoendeshwa na AHS kufikia jumla ya vituo kumi na moja, na hivyo kuimarisha nafasi yetu kama vinara wakutoa huduma ya vipimo vya afya kwa ajili ya mchakato wa VISA kwa nchi ya Falme za kiarabu”

Aidha kituo cha mamlaka ya vitambulisho cha Emirate pia kikiwa kimejengwa eneo husika ili kutoa huduma kwa wafanyakazi takribani 200 kupata vitambulisho kila siku. Eneo husika litasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa msongamano na mchakato mzima wa kupata vitambulisho vya Emirates kwa wafanyakazi na wategemezi wao hapa nchi ya Falme za kiarabu

Hapo mbeleni kutakuwa na nafasi kwa raia wa Emirate kupata mafunzo na ujuzi wa unesi kupitia mpango wa chuo cha mafunzo ya unesi cha Fatima, kikilenga kuvutia manesi nchini humo kupata ajira katika sekta ya anga pia.

Kituo kipya kinafuatia utambulisho wa huduma ya ambulance kwa wafanyakazi, kliniki maalumu kwa wanaosafiri kikazi, vituo kadhaa vya afya na mazoezi huko Abu Dhabi pamoja na kituo mahususi kwa ajili ya kusaidia ustawi wa marubani pamoja na wahudumu wa ndani ya ndege.

Halotel kuandaa matamasha ya Christmass katika mikoa mitano nchini

$
0
0
Kampuni ya simu za mikononi ya Halotel inaandaa matamasha ya Christmass katika mikoa mitano nchini yenye lengo la kuwapa burudani watuamiaji wa mtandao huo pamoja na wale watakaohitaji kujiunga na mtandao huo.

Matamasha hayo ambayo yatafanyika wilaya za Tukuyu, Ruangwa, Moshi Vijijini, Chato pamoja na Mpwapwa, yatajumuisha wasanii wa bongo fleva pamoja na burudani nyingine kutoka kwa wasanii wa maeneo hayo.

Tamasha la Halo Christmass wilayani Tukuyu litafanyika katika uwanja wa Tandale na burudani itatolewa na wasanii Tundaman na Makomando.

Kwa upande wa Ruangwa, tamasha hilo litafanyika katika viwanja vya shule ya msingi Likangala, na kutumbuizwa na wasanii Amini pamoja na Matonya, wakati Mpwapwa tamasha litafanyika katika viwanja vya Mgambo likitumbuizwa na wasanii Madee na Malaika.

Tamasha hilo pia litafanyika wilayani Chato katika viwanja vya Stand ya Zamani huku burudani ikitolewa na msanii Shetta na Baraka Da Prince.

Wakazi wa Moshi vijijini pia watafurahia tamasha la Christmass kwa burudani Shilole na Msami zitakazofanyika katika viwanja vya Kae.

Akizungumzia matamasha hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Halotel bwana Nguyen Thanh Quang, amesema matamasha hayo ya Halotel yanalenga kuwaleta watumiaji wa Halotel pamoja na kuwapa burudani ya kufunga mwaka.

‘Hii ni zawadi kwa watumiaji wa mtandao wetu na wateja wapya wanaotaka kujiunga na familia yetu ya Halotel, na ndio maana tunawafata katika maeneo yao yalipo’ alisema Quang.

Matamasha hayo yatafanyika kuanzia saa sita mchana hadi saa kumi na mbili jioni, na kiingilio itakuwa ni laini ya mtandao wa Halotel kwa wateja wapya huku wale wenye laini za Halotel tayari wakiingia bure.

Quang pia amewaahidi wateja wa Halotel kuwa mtandao wake unatarajia kuleta mabadiliko katika sekta ya mawasiliano nchini kwa kuwapa wateja wake zaidi ya huduma za simu.

MTU MMOJA AKUMBANA NA KICHAPO KWA KUJIDAI AFISA WA TRA

$
0
0
Camera ya Globu ya Jamii imelinasa tukio la baadhi ya Raia wenye hasira waliokuwa wakilishambulia gari la mtu mmoja lenye namba za usajili T945 BYG,na pia kumpa kipigo mtu huyo aliyetuhumiwa kuwa ni tapeli .

Mtu huyo alijitambulisha kuwa ni Afisa wa TRA,lakini akatuhumiwa kuwa ni tapeli aliyetaka kufanya tukio la kiuhalifu kwenye moja ya Maduka yaonekayo mbele ya gari hilo,tukio hilo limetokea hivi punde maeneno ya Tabata Segerea. Mtuhumiwa huyo ambaye jina lake halikuweza kufahamika  mapema,amekamatwa na kupelekwa kituo cha Polisi Tabata Segerea kwa hatua zaidi za kisheria
 
 

Malawi yafanya ziara ya kujifunza katika sekta ya Habari na Mawasiliano

$
0
0
x71
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utalii na Elimu toka Malawi Justin Adack Saidi akiwa na ujumbe wake wakizungumza na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel walipomtembelea ofisi kwake leo.
x72
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel mwenye shati la batiki akizungumza na ujumbe toka Malawi walipomtembelea ofisini kwake leo.
x73
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel wa pili kutoka kushoto akizungumza na ugeni toka Malawi ofisi kwake leo kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utalii na Elimu toka Malawi Justin Adack Saidi.
x74
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiagana na ujumbe uliomtembelea toka Malawi leo ofisini kwake.
x75
Mkurugenzi Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene akifafanua jambo kwa ujumbe uliotembelea Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utalii na Elimu toka Malawi Justin Adack Saidi.

x76
Baadhi ya maofisa wakuu  walioambatana na  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utalii na Elimu toka Malawi wakifatilia mazungumzo yaliyofanyika Wizarani hapo Leo.
x77
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utalii na Elimu toka Malawi Justin Adack Saidi akifaafnua jambo kwa Mkurugenzi Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene walipokuwa wakizungumza kwenye mkutano uliofanyoka leo Jijini Dare s salaam.
x78
Mkurugenzi Msaidizi,sehemu ya Usajili wa Magezeti toka Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Raphael Hokororo akifafanua jambo kwa ujumbe toka Malawi uliotembela Wizarani hapo leo
x79
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utalii na Elimu toka Malawi Justin Adack Saidi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wake toka Malawi na na wakurugenzi wa Habari toka Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo kulia mwa Katibu mkuu huyo ni Mkurugenzi Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene
  picha Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
x64
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel Akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utalii na Elimu toka Malawi Justin Adack Saidi alimpomtembelea ofisini kwake Leo Jijini Dar es salaam.
x65x66x67x68x69
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel Akisalimiana na wageni toka Malawi walipomtembelea ofisini kwake leo Jijini Dar es salaam.
x70
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (Kushoto) Alizungumza na ujumbe toka Malawi (Hawapo pichani) walipomtembelea ofisi kwake leo Jijini Dar es salaam Kulia ni Mkurugenzi Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene.
 

SHEREHE YA MAULIDI MAKUU YA MTUME MUHAMMAD (S.A.W)

$
0
0
x45
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad alipowasili katika sherehe za Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja.
x46
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji Khamis,Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad (kushoto) na Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh  Hassan Othman Ngwali wakiwa katika sherehe za Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja.
x47
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji Khamis, Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad (kushoto) na Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh  Hassan Othman Ngwali pamoja na Viongozi wengine wakiwa katika sherehe za Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja.
x48
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (katikati) akiangalia ratiba ya Maulidi ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja akiwa Viongozi mbali mbali na wananchi,
x49
Baadhi ya Akina Mama wa Kiisalmu wakiwa katika  sherehe za Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja ambayo hufanyika kila mwaka.
x50
Wanafunzi wa Madrasa mbali mbali za Zanzibar wakiwa katika sherehe za Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja,ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein.

x41
Wanamadrasa wakipiga dufu kukaribisha wageni na Viongozi wakati wa sherehe za Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja ambayo hufanyika kila mwaka.
[Picha zote na Ikulu.]
x42
Makamo wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt.Mohammed Gharib Bilali akisalimiana na Sheikh Kassim Haidar Jabir mjumbe wa Kamati ya Maandalizi alipowasili katika sherehe za Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja.
x43
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na viongozi mbali mbali alipowasili katika sherehe za Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja.
x44
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mwanasheria Mkuu Zanzibar Sheikh Said Hassan Said pamoja na viongozi mbali mbali alipowasili katika sherehe za Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja.

x51
Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji Khamis alipokuwa akitoa historia fupi wakati wa ufunguzi wa sherehe za Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja,ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akiwa ndio mgeni rasmi katika sherehe hiyo.
x52
Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji Khamis alipokuwa akitia ubani kama ishara ya kuyafungua Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W)  sherehe zilizofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman mjini Unguja jana na kuhudhuriwa na waislamu kutoka Mjini na Mashamba,(kushoto) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akishuhudia ufunguzi huo
x53
Ustadh  Juma Seif Said Hamad kutoka Mkoa wa Kaskazini Unguja akisoama Qur’aan Tukufu Surah Luqman Aya 33hadi 34 za  ufunguzi wa Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja.
x54
Wanafunzi wa Madrasat  Nurul Islamia ya Jang’ombe -Mkoa wa Mjini wakisoma Qasweeda baada ya mlango wa kwanza wa sherehe za Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja.
x55
Ustadh  Rashid Hamadi Bakari kutoka Muungoni Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja akisoma mlango wa kwanza wa  Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja.
x56
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na Viongozi mbali mbali wakisiamama kumswalia Mtume wakati wa Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwake Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja.
x57
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akitiliwa marashi pamoja na Viongozi mbali mbali wakati wa kumswalia Mtume katika sherehe za Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwake Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja.
x58
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (katikati) pamoja na Wake wa Viongozimbali mbali wakisimama kumswalia Mtume wakati wa Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwake Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika viwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja.
x59
Wanafunzi wa Madrasa mbali mbali na wananchi wakisiama wakati wa kumswalia Mtume (S.A.W) katika sherehe za Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwake zilizofanyika jana  katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja.
x60
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akipokea zawadi kutoka kwa Sheikh Sherali Champs Mshauri Mkuu wa kamati ya Maandalizi ya Maulidi Makuu ya Mtume Muhammad (S.A.W) wakati wa sherehe ya kusomwa maulidi hayo jana katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja.
x61
Wanafunzi wa Madressatul Mtendeni Mjini Zanzibar wakisoma Maulid ya Hom wakati wa sherehe za Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja.
x62
Ustadh Nassor Seif Rashid wa Kibanda hatari Mkoa wa Mjini akisoama Barazanj Mlango wa Nne wa  Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja.
x63
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Makamo Makamo wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt.Mohammed Gharib Bilali alipowasili katika sherehe za Maulidi Makuu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja,
[Picha na Ikulu.]

BREAKING NEWZZZZZ..Serikali yapiga marufuku matangazo yote yanayohusu tiba asili na tiba mbadala kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Mawaziri na Naibu Waziri Kuapishwa Jumatatu 28 Desemba 2015

$
0
0


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz              

Faksi: 255-22-2113425



OFISI YA RAIS,
      IKULU,
 1 BARABARA YA BARACK OBAMA,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 

Tarehe 23 Desemba, 2015 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliwateua Mawaziri wanne, Naibu Waziri mmoja na kumhamisha Wizara Waziri mmoja.

Walioteuliwa ni Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe, Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge,  Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Dkt. Joyce Ndalichako na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mheshimiwa Hamad Yusuf Masauni.

Rais Magufuli pia alifanya uhamisho wa Waziri mmoja ambaye ni Profesa Makame Mnyaa Mbarawa kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kwenda Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Kufuatia uteuzi huu, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue anawaarifu Mawaziri wote na Naibu Waziri walioteuliwa kuwa wataapishwa Jumatatu tarehe    28 Desemba, 2015 Saa tatu asubuhi, Ikulu Jijini Dar es salaam.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
24 Desemba, 2015

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AHUDHURIA SHREHE ZA MAULID ZANZIBAR

$
0
0
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Katibu Msaidizi Mkoa wa Magharibi Kichama Zanzibar Suleiman Mzee (CHARAS) alipowasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Karume Zanzibar leo Disemba 24,2015 kwa ajili ya kuhudhuria  Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W).
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Makamu wa Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alipowasili nyumbani kwake Migombani Zanzibar leo Disemba 24,2015 kwa ajili ya kuhudhuria Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) yanayofanyika kila mwaka.
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal katikati, akisalimiana na kumfahamisha wake zake Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kushoto alipowasili nyumbani kwake Migombani Zanzibar leo Disemba 24,2015 kwa ajili ya kuhudhuria  Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) yanayofanyika kila mwaka. Picha na OMR

REBECCA MALOPE AWASILI NCHINI TAYARI KWA KUWASHA MOTO TAMASHA LA XMASS DIAMOND JUBILEE KESHO

$
0
0
 Mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika ya Kusini,Rebecca Malope akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa JNIA jioni hii tayari kwa ajili ya kutumbuiza kaika tamasha la Krismass litakalofanyika ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam kesho likishirikisha waimbaji mbalimbali wakiwemo wa nchini Tanzania kama vile Rose Muhando, Upendo Nkone, Joshua Mlelwa na wengine wengi , kushoto katika picha anayefurahia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion iliyoandaa na kumleta mwimbaji huyo  Bw. Alex Msama.
  Rebecca Malope akiwasalimia baadhi ya mashabiki wake (hawapo pichani) waliokuja kumlaki mara baada ya kuwasilia uwanja wa ndege wa JNIA jioni hii tayari kwa ajili ya kutumbuiza tamasha la Krismass litakalofanyika ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam kesho
 Marope akikaribishwa kwa upendo na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Msama Promotions.
 Rebecca Malope Mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika ya Kusini akizungumza na mratibu wa tamasha hilo Bw. Hadson Kamoga mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa JNIA jijini Dar es salaam.
Rebecca Malope Mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika ya Kusini akisisitiza jambo huku akitabasamu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa JNIA.
 Rebecca Malope Mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika ya Kusini akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili nchini kwenye uwanja wa ndege wa JNIA jijini Dar es salaam, waliosimama nyuma Bw. Alex Msama na mmoja wa waratibu wa tamasha hilo Hadson Kamoga.


MUUAJI WA AFISA WA INTELIJENSIA WA TANAPA AKAMATWA

$
0
0

ed6e0eca-61d5-4d32-9a22-85f328dd6ff9
Pichani  gari aina ya Nissan Mazda lenye namba za usajili T. 435 CSY lililokutwa na mwili wa marehemu Emily Kisamo ambaye ni Afisa wa Intelejensia TANAPA uliohifadhiwa kwenye buti mara baada ya kuuawa na Mfanyakazi wake wa ndani.
……………………………………………………

Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha.

Jeshi la Polisi Mkoani hapa limefanikiwa kumkamata mtu mmoja aitwaye Ismail Swalehe Sang’wa (20) ambaye ni mwenyeji wa kijiji cha Sepuka wilayani Ikungi katika Mkoa wa Singida kwa tuhuma za  kumuua Afisa wa Intelijensia wa TANAPA  aitwaye Emily Kisamo (52).

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake asubuhi ya leo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas alisema tukio hilo la mauaji ya Afisa huyo wa TANAPA lilitokea tarehe 18.12.2015 muda kati ya saa 2:30 asubuhi hadi saa 4:00 asubuhi mtaa uitwao Corridor Area Uzunguni jijini hapa.

Kamanda Sabas alisema kwamba, siku ya tukio hilo marehemu alikuwa nyumbani kwake sebuleni akiwa anakunywa uji ndipo mtuhumiwa ambaye ni mfanyakazi wake wa ndani na alimvizia na kumkata shingo na kitu kinachoaminika kuwa ni panga na kisha kuchukua mwili wake na kuuweka kwenye gari la marehemu aina ya Nissan Mazda lenye namba za usajili T. 435 CSY.

“Baada ya kuuweka mwili wa marehemu kwenye buti alilisafisha gari hilo kwa nje na kisha kuliendesha mpaka eneo la kikwakwaru “B” kata ya Lemara ambapo alilitelekeza hapo na kisha yeye kuondoka”. Alifafanua Kamanda Sabas.

“Mara baada ya gari hilo kukaa mpaka saa 2:00 usiku ndipo baadhi ya wananchi wa eneo hilo walitoa taarifa kwetu ambapo askari wa doria walikwenda na kulichukua gari hilo kwa kulivuta mpaka kituoni. Kwa kuwa mke wa marehemu aitwaye Caroline Lukumay (38) alikuwa anamtafuta mume wake kwa njia ya simu bila mafanikio ndipo alipoamua kuja kituoni kutoa taarifa ambapo tulimuonyesha gari lililotelekezwa ambalo alillitambua mara moja”. Alisema Kamanda Sabas.

Aliongeza kwa kusema kwamba askari walimuomba mke wa marehemu funguo za akiba za gari hilo ambapo baada ya kulifungua ndipo walipouona mwili wa marehemu kwenye buti akiwa na vitu mbalimbali kama vile simu mbili aina ya Sony na Panasonic, pesa taslimu Tsh 300,000, Laptop aina ya Asus na kadi za benki tofauti tofauti.

Mara baada ya mtuhumiwa huyo kukamatwa alikiri kuhusika na mauaji hayo na kusema siku hiyo walikuwa wawili tu yaani yeye na mrehemu na alifanya hivyo kwa kuwa alikuwa na tamaa za fedha alizokuwa nazo marehemu ndani ya nyumba hiyo kiasi cha Tsh. Mil.5.

Upekuzi zaidi wa Jeshi la Polisi ulibaini kuwepo kwa fedha taslimu Tsh. 4,294,000, simu tatu aina ya Sumsang na vocha za mtandao wa vodacom za sh. Elfu tano tano zenye thamani ya Tsh. 70,000 ambapo vyote vilifukiwa kwenye banda la kuku.

Mbali na vitu hivyo pia mtuhumiwa Ismail Swalehe Sang’wa aliweza kuonyesha panga lenye damu ambalo alilihifadhi stoo pamoja na taulo nne kubwa, kitambaa cha mezani na suruali yake ambazo zilikuwa na damu na alizitumia yeye mwenyewe kupigia deki sebuleni baada ya tukio na kisha kuzificha kwenye migomba karibu na mabanda ya kuku.

Kamanda Sabas alimalizia kwa kusema kwamba Jeshi hilo linawashikilia watuhumiwa watatu wengine mbali na Ismail Swalehe Sang’wa akiwemo mke wa marehemu, rafiki wa mke wa marehemu ambaye ni mwanamke na dereva wa nyumbani  wa marehemu kwa mahojiano zaidi.

Watanzania waaswa kuendeleza Amani iliyopo

$
0
0
Z4
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihutubia sherehe za Maulid zililofanyika katika viwanja vya Karim Jee.
Z6Z7
Baadhi ya waumini wa dini ya Kislamu wakifatilia hotuba na mawaidha mbalimbali wakati wa sherehe za Maulid zililofanyika katika viwanja vya Karim jee Jijini Dar es salaam.
Z8
Msanii wa sanaa ya maigizo Tanzania Ahmed Olutu maarufu kama Mzee Chilo akifatilia sherehe za Maulid  zililofanyika katika viwanja vya Karim jee Jijini Dar es salaam.
Z9
Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim akijadili jambo na baadhi ya wawakilishi wananchi mmbalimbali wakati wa sherehe za Maulid zililofanyika katika viwanja vya Karim jee Jijini Dar es salaam.

Z10Z11
vijana wa kislamu wakicheza kaswida katika kusherekea Sikukuu ya Maulid wakati wa Baraza la Maulid zililofanyika katika viwanja vya Karim jee Jijini Dar es salaam.
Z2
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwasili katika Viwanja vya Karim Jee jijini Dar es Salaam katika sherehe za Maulid.Picha na Raymond Mushumbusi Maelezo
Z3
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifurahi jambo, alipokuwa akishiriki katika sherehe za Maulid (Kushoto) Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Abubakari Bin Zuberi Bin Ali na kulia ni Rais Msataafu wa Awamu ya Pili Ali Hassan Mwinyi

……………………………………………………………………………..
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Watanzania wameaswa kuiendeleza amani na utulivu iliyopo kwa sasa nchini na kutoiacha ikapotea kwani ndio nguzo muhimu kwa watanzania na mstakabali wa maendeleo ya nchi yetu kiujumla.-
 
Hayo yamesemwa leo na Waziri Mkuu Mhe Kassimu Majaliwa alipokuwa akihutubi Baraza la Maulid lililofanyika katika viwanja vya karim Jee Jijini Dar es salaam na kuwaasa waislamu wote nchini na watanzania kiujumla kudumisha upendo amani na mshikamano uliopo.
 
Waziri mkuu Kassimu Majalimu ameongeza kuwa serikali itaendelea kushirikiana na Taasisi za kidini katika kulenda maendeleo na kutoa huduma kwa wananchi ikiwemo Elimu na Afya.
 
Pia ameitaka jamii ya kislamu na watanzania wote kuzingatia maadili mema na kuwafundisha watoto maadili mazuri ili kupunguza wimbi la uvunjivu wa maadili nchini ambao unasababisha vijana wengi kupotea katika madawa ya kulevya na kupata mimba za utotoni.
 
“Sisi kama Serikali ya Awamu ya Tano tuko makini sana na tunatoa shukrani kwa Baraza la Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kwa kushirikiana na sisi katika maswala mbalimbali ya kimaendeleo na sisi tutashirikiana nanyi bega kwa bega” Alisema Waziri Mkuu Majaliwa.
 
Naye Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Abubakari Bin Zuberi Bin Ali amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano na kumpongeza pia kwa kumteuwa Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa na kuteuwa  mawaziri makini katika kuiletea maendeleo nchi yetu.
 
Waislamu wote Duniani leo wanaikumbuka siku ya kuzaliwa Mtume wao Mohamed SAW na kwa Tanzania maadhimisho hayo yamefanyika kitaifa katika viwanja vya Karim Jee Jijini dare s salaam nakuhudhuriwa na viongozi wa chini dini, na mabalozi mabalimbali waislamu na wanachi wa dini zote.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela Afungua mafunzo ya ulengaji Shabaha

$
0
0
S1
Mkuu wa Wilaya ya Iringa akipokea maelezo toka kwa Mshauri wa Mgambo wa Mkoa Luteni Kanali J. Kitita
S2
Mkuu wa Wilaya Bwana Richard Kasesela akiongea na wana Mgambo na kuwaasa kuwa waaminifu kwani wao ndio walinzi namba moja katika nchi kwani wao wako karibu sana na wananchi. pia Mkuu wa wilaya alisistiza suala la usafi kama nguzo moja wapo ya uadilifu.
S3
Mkuu wa wilaya akizindua mafunzo ya shabaha. alifanikiwa kulenga 10 kati ya 30 zilienda kwenye shabaha
S4
Mkufunzi wa mafunzo akihesabu shabaha.
S5
Mkuu wa wilaya akionyesha jinsi ya kutumia SMG

WANAKIJIJI WACHARUKA WAMTAKA MKURUGENZI MBOGWE AKAZOE TAKA ZILIZOTUPWA KIJIJINI KWAO SIKU YA USAFI DECEMBER 9

$
0
0
UCHAFU ULIOZOLEWA KATIKA KATA YA MASUMBWE NA KUTUPWA KATIKA MAKAZI YA WATU KATIKA KIJIJI CHA SHENDA.

Wanachi wa kijiji cha Shenda katika kata ya Masumbwe wilayani Mbogwe mkoani Geita Wameitaka ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri ya Mbogwe kuziondoa takataka zilizowekwa kijijini kwao kufuatia zoezi la usafi la December 9 Lililofanyika nchi nzima.

Wakiongea na waandishi wa habari za mtandaoni wananchi hao wanakijiji hao wamesema kuwa wanashangazwa na kitendo cha halmashauri ya wilaya kutuma takataka katika kijiji chao licha ya kwamba hakuna dampo la uchafu eneo hilo.

Wameongeza kuwa taka hizo ni hatari kwa afya zao kwani zimetupwa karibu na eneo la shule ya msingi,Makazi ya watu na vibanda vya mama ntilie hali inayozua hofu ya kuzuka kwa magonjwa ya mripuko kwani taka hizo zimeanza kuoza na kusambaa katika makazi ya watu kipindi hiki cha masika.

Sambamba na hayo wameshangazwa na maamuzi ya ofisi ya mkurugenzi kutupa taka hizo katika kijiji chao licha ya kuwa yapo maeneo mengi ya wazi ambayo yangeweza kutumika kutupa taka hizo ambazo kwa sasa zimekuwa kero katika kijiji chao hasa kutoa harufu mbaya na funza.


Kwa mujibu wa kaimu mtendaji wa kijiji cha Shenda Joseph Jaseda amesema sehemu zilizotupwa taka hizo ni makazi ya watu na kwamba walipouliza kuhusu hatua hiyo waliambiwa kuwa gari la kuzoa taka liliharibika sehemu hiyo na ndipo walipoamua kutupa taka hizo.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Masumbwe Shimo Kiyuyu amesema kuwa alifikisha malalamiko ya wananchi kwa mkurugenzi na Mkurugenzi akatoa gari ili uchafu uzolewe lakini juhudi hizo ziligonga mwamba kutokana na gari hiyo kwenda eneo la uchafu bila wazoaji wa taka hizo.
Kwa upande wake afisa afya wa halmashauri ya wilaya ya MbogweEdward Razalo amekiri uchafu huo kutupwa katika maeneo hayo na kuongeza kuwa baada ya wananchi kulalamika walienda kuweka dawa ya kuwa wadudu katika taka hizo na kwamba hawajaziamisha kutokana na taka hizo kutokuwa na madhara kwa wananchi.

Go for Zanzibar (GOZA) a German NGO supports the Welezo Old Age Home

$
0
0

Mwenyekiti wa NGOs ya Go For Zanzibar Antje Fleischer na Meneja Mradi Mussa Khamis Baucha , wakimkabidhi msaada Mwakilishi wa Wazee wa Kijiji cha Welezo Zanzibar Mzee Kombo Shein, vyakula kwa ajili ya wazee hao ili kuweza kujimuika na Wananchi katika kusherehekea Sikukuu ya Krismax na mwaka mpya kulia Msimamizi wa Kijiji hicho Sister Mary Gemma na Hassan Khamis hafla hiyo imefanyika katika makaazi ya wazee hao welezo jana

Mwenyekiti wa NGOs ya Go For Zanzibar Antje Fleischer na Meneja Mradi Mussa Khamis Baucha , wakimkabidhi msaada Mwakilishi wa  Wazee wa Kijiji cha Welezo Zanzibar Mzee Kombo Shein, vyakula kwa ajili ya wazee hao ili kuweza kujimuika na Wananchi katika kusherehekea Sikukuu ya Krismax na mwaka mpya kulia Msimamizi wa Kijiji hicho Sister Mary Gemma hafla hiyo imefanyika katika makaazi ya wazee hao welezo jana

Mwakilishi wa Wazee Welezo Mzee Shein, akimshukuru Mwenyekiti wa NGOs ya Go For Zanzibar Antje Fleische, kwa msaada wao na kumtaka kuwa Balozi wao huko Nje kuwawakilishi ili kuweza kupata misaada zaidi hasa gari kwa ajili ya kutembelea sehemu mbalimbali wakati wa sikukuu na kutumika kwa shughuli zao za kawaidi.

Mzee Shein akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhiwa Vyakula kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Krismax na Mwaka Mpya .


Sister Mary Gemma akitowa shukrani kwa Ngo’s GOZA kwa msaada wao kwa kuwajali Wazee hasa kwa wakati huu wa kusherehekea Sikukuu ya Krismax na Mwaka Mpya.

German help organization GOZA is celebrating Christmas 6 degrees south in Zanzibar together with the old people (Wazee) in Welezo Old Age Home
Since five years now the German help organization GO FOR ZANZIBAR (GOZA) NGO is supporting the Welezo Old Age Home.
Different charity offers have been done since the cooperation with the old age home in Welezo started in 2010.

The main offers in the last years were:

Renovation of two wards and improvement of the sanitary facilities
Establishing a regular medical support for the old people
Support of food, medecine, clothes, wheel chairs
Workshops in basic nursing for the nurse assistance

The donation amount in the last five years covers a budget of round 22,000,000 TSH (10,000 Euro).
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images