Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

TANESCO YAAGIZWA KUKAMILISHA MIUNDO MBINU YA KUSAMBAZA UMEME JIJINI DAR ILI KUPUNGUZA TATIZO LA UMEME

$
0
0

NA  ALLY DAUD-MAELEZO

Serikali imeliagiza Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kukamilisha mradi wa kukuza miundo mbinu ya kusafirisha umeme unaosimamiwa na Kampuni ya kutengeneza vipozeo(Transformer) ya Italy (SAE) ili kusaidia upatikanaji wa umeme wa uhakika.

Agizo hilo limetolewa leo jijini Dar es salaam na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kaleman katika ziara yake ya kutembelea mradi huo katika vituo vya Mbagala, Kurasini , Gongo la Mboto na kipawa.

Amesema kuwa ni vema hadi kufikia Februari mwakani Tanesco wawe wamekamilisha mradi huo na wananchi waweze kupatiwa huduma ya umeme haraka iwezekanavyo.

Aidha Dkt. Kalemani aliagiza kuwa kutokana na kesi ya fidia  ya wananchi wote ambao wameondolewa kwenye maeneo yao ili kupisha  mradi huo  ni vema wawe wamelipwa kufika Januari 2016.

Akitoa maelezo kwa Naibu Waziri huyo ,Meneja Mradi wa Tanesco Mhandisi Frank Mashalo amesema kuwa kulingana na mkataba walioingia na Kampuni ya SAE mradi huo ulipaswa kukamilika kwa kipindi cha miezi 18 lakini bado haujakamilika kutokana na vikwazo mbalimbali ikiwemo sakata la fidia na kuchelewa kwa vipozeo vya umeme  kufika kwenye vituo hivyo.

Ameongeza kuwa jumla ya dola milioni 34.252 zinatarajiwa kutumika ili kukamilisha mradi huo ambapo kati ya hizo tayari Dola milioni 28 zimeshalipwa.

UWAJIBIKAJI WA VIONGOZI WA VIJIJI NI DHANA KUU YA KUTATUA KERO ZINAZOWAKABILI WANANCHI WANAO WAONGOZA.

$
0
0
Baadhi ya wenyeviti toka Halmashauri ya wilaya ya Kishapu wakimsikiliza mkufunzi (hayupo pichani) wakati wa mafunzo yao yaliyofanyika wilayani hapo. 

“Unakuja kwenye ofisi yangu na kutoa taarifa za ubadhirifu wa mtendaji wa kijiji. Nakuuliza, je umechukua hatua zipi kama kiongozi wa kijiji kabla kuja kwenye ofisi yangu? Unanijibu hapana, hii si sahihi,”  Hayo ni maneno ya mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Hashim Mgandilwa, aliyoyatoa wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya  wenyeviti wa vijiji, watendaji wa kata na vijiji kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Loliondo.
Alisema hayo kwa lengo la kufafanua dhana ya uwajibikaji kwa viongozi kama njia muhimu ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wa maeneo ya vijijini katika wilaya yake. Ni dhahiri kwamba viongozi wa ngazi za vijiji na kata wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za kiutendaji katika maeneo husika.  Kuna nafuu kwa watendaji wa kata na vijiji,  ambao ni waajiriwa wa serikali na hupewa kazi kutokana  na miongozo, lakini siyo kwa wenyeviti wa vijiji na madiwani, wakati mwingine hata wabunge.

Akielezea changamoto hiyo wakati wa mafunzo ya wenyeviti wa vijiji kupitia mradi wa Chukua Hatua yaliyofanyika Septemba mwaka huu na shirika mdau la CABUIPA, mwenyekiti wa kijiji cha Nyakafulu kilichopo wilaya ya Mbogwe, mkoani Geita, Salum Said amesema:  “Baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa kijiji hiki, hakika sikufahamu vya kutosha kuhusu majukumu yangu mapya kama kiongozi. Na hii ni changamoto kubwa kwa wenyeviti wa vijiji karibu vyote vya wilaya yetu.” 


Yeye ni mmoja kati ya wenyeviti 200 wanaopatiwa mafunzo katika mikoa ya Shinyanga, Geita na Simiyu. Wakati wananchi wakiwezeshwa kuwasimamia viongozi wao, viongozi hawakuwa wakiwezeshwa kutimiza majukumu yao kuwasikiliza na kuwahudumia wananchi wao.  Hivyo kuna haja ya kutoa mafunzo kwa viongozi hao ili waweze kutimiza majukumu yao kwa wananchi waliowachagua, ilikuwa lazima. 
Wanakijiji wa Kijiji cha Uchunga wilayani Kishapu wakiendelea na mkutano pamoja na viongozi wa kijiji na wazee Maarufu.

 
Akielezea umuhimu wa kuwawezesha wenyeviti wa vijiji  wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya wenyeviti na watendaji wa kata Julai 2015, mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri  ya Wilaya ya Kishapu, mkoani Shinyanga, Jane Mutagurwa alisema “Kwa muda mrefu wenyeviti mmekuwa mkilalamika kusahaulika kwenye programu zetu za mafunzo, fursa ndio hii imekuja. Tunafahamu kwamba wenyeviti wetu mnakutana na changamoto nyingi za kiutendaji zinazotokana na uwelewa mdogo katika majukumu yenu, hasa kwa wale wanaoingia madarakani kwa mara ya kwanza. Hivyo mtumie mafunzo haya vizuri.” 


Pamoja na umuhimu wa mafunzo hayo kwa viongozi wa ngazi  ya kijiji na kata, bado imekuwa ni changamoto kubwa kwa serikali kuwawezesha wenyeviti kujua majukumu yao. Na hii inatokana bajeti kuwa na vipaumbele vingine ambavyo halmashauri huwa wamejiwekea katika  kutimiza majukumu yao."


Kwa upande wa Ngorongoro, mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya hiyo mkoani Arusha anaeleza:“Tangu tulipofanya uchaguzi mwaka jana hatujawahi kutoa mafunzo kwa wenyeviti. Kwa hiyo tunaunga mkono mafunzo haya yanayotolewa na PALISEP yatasaidia sana kwenye kuwawezesha viongozi hawa na watendaji wetu,”  Kutokana na hali hii, wenyeviti wamekuwa na changamoto za kuelewa mipaka ya majukumu yao, hivyo muda mwingine hujikuta kwenye mzozo na watendaji wa vijiji vyao.  Mwenyekiti anawajibika kwa mwananchi aliyemchagua, wakati mtendaji anawajibika kwa mkurugenzi aliyemwajiri. Kutokana na tofauti hizo, mafunzo ya sasa ya wenyeviti na watendaji yanaendeshwa kwa pamoja kuwafanya waelewe mipaka yao ya kiutendaji, hivyo kuboresha utendaji wao.


Afisa Programu wa CABUIPA, Michael Ikila anafafanua: “Tunawafundisha vitu sita muhimu; taratibu za uendeshaji serikali za mitaa, majukumu na haki za  wenyeviti wa vijiji, uwajibikaji na utawala bora,  mamlaka za vijiji, masuala ya fedha, ikiwamo uandaaji wa  bajeti na mawasiliano mazuri baina ya viongozi wa  vijiji.”  Mada hizi ni kwa mujibu wa mwongozo wa wizara ya Tawala za Mikoa and Serikali za Mitaa (TAMISEMI).  Majukumu mengine ya wenyeviti hawa ni pamoja na  kuhamasisha shughuli za maendeleo, utawala na  kuhakikisha usalama wa watu katika maeneo yao kwa kushirikiana na watendaji wa kata na vijiji.
Viongozi wa Kijiji cha Negezi wakiwa pamoja na wanakijiji kujadili mambo mbalimbali ya eneo lao.
Kwa upande wa Wilaya ya Ngorongoro, hii ni mara ya kwanza kwa wenyeviti kufundishwa majukumu yao. Mwanzoni mafunzo haya yaliwalenga madiwani ambao kimsingi hawakuyapenda kwa sababu ya kutokuwapo kwa posho. Hivyo mafunzo yao yakaamishiwa kwa wenyeviti wa vijiji ambao walipokea mwaliko kwa furaha pasipo kudai posho. “Mafunzo haya yatatusaidia kuboresha mahusiano na utendaji wetu.

 Mara kadhaa unakuta wenyeviti wanaingilia mipaka yetu ya kazi, hivyo kuathiri uhamasishaji wa shughuli za maendeleo. Na hii hutokea pale mwenyekiti mpya anapotaka kuwaonyesha wapigakura wake kwamba mwenzake aliyepita hakufanya kazi,” anaelezea mmoja wa watendaji wa kijiji aliyehudhuria mafunzo hayo.


Pamoja na changamoto hizo, bado washiriki ambao ni wenyeviti, watendaji wa kata na vijiji wamekiri kwamba mafunzo hayo yatakuwa chachu ya kumaliza tofauti zinazojitokeza baina yao. Lakini si hivyo tu, viongozi wa wilaya wameonyesha kuunga mkono mafunzo hayo kwa kuwa yanasaidia kuhamasisha wananchi kutimiza majukumu yao. Lakini pia viongozi hao walionyesha umuhimu wa kufikia wajumbe wengi zaidi ya halmashauri za serikali ya kijiji. Kwa mfano, wakati akizungumza na wakufunzi kwenye ofisi yake, mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu, alisema: Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu ina jumla ya vijiji 117 vyenye wajumbe 2,925. 

Katika mazingira hayo, mkurugenzi alitoa ombi maalumu la kusaidiwa kuwawezesha wakufunzi 25 wa wilaya watakaotoa mafunzo kwa wajumbe wa halmashauri za vijiji hivyo. Gharama za wakufunzi hawa kuwafikia wajumbe wengine zitakuwa ni za serikali.  Na huu ni ushirikiano unaotakiwa baina ya sekta ya umma na binafsi kwa kuwa ni jukumu letu sote kwa mustakabali wa maendeleo yetu.
 

DARAJA LA CHIKWALE LITAKAMILIKA - WAZIRI MKUU

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema darala la mto Mbwemkuru lililoko katika barabara ya kutoka Chikwale hadi Liwale litakamilika kwa sababu ni kiungo muhimu kwa wakazi wa eneo hilo.

Ametoa ahadi hiyo wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Nangurugai katika kata ya Mbwemkuru wilayani Ruangwa, mkoani Lindi ambako alikwenda kuwashukuru kwa kumchagua kuwa mbunge wao.

Waziri Mkuu alikuwa akijibu hoja za diwani wa Nangurugai, Bw. Selemani Likuche aliyetoa ombi la kutengenezwa kwa daraja hilo kwani limekata mawasiliano baina ya kijiji hicho na wilaya ya Liwale. Pia aliomba wapatiwe dawa na watumishi kwenye zahanati yao.

Akijibu hoja hizo, Waziri Mkuu alisema kazi ya ujenzi wa daraja hili itakamilishwa kwa sababu jukumu kubwa alilonalo ni kuhakikisha ujenzi wa daraja la mto Mbwemkuru unaisha.

Pia aliitaka Halmashauri ya Ruangwa isimamie uboreshaji wa barabara ya kutoka Nangurugai hadi Chikwale yenye urefu wa km. 35 kwa sababu ni muhimu kwa kusafirisha mazao ya eneo hilo. “Hili eneo ni maarufu kwa zao la ufuta, kwa maana hiyo linaongeza pia mapato ya Halmashauri, simamieni hii barabara ili wananchi wasisumbuke kuuza mazao yao,” alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Ruangwa, Bw. Nicholas Kombe alisema milingoti (pillars) ya daraja hilo ilikwishajengwa walikuwa wakisubiri kupokea vyuma vya kutandaza juu ya daraja. “Tulikwishapeleka maombi yetu TANROADS na TAMISEMI lakini bado hawajatujibu,” alisema.

Akizungumzia kuhusu upatikanaji wa dawa kwenye zahanati yao, Waziri Mkuu alisema ameshaongea na Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo ambaye amemhakikishia kuwa ameanza maboresho ya upatikanaji dawa katika zahanati zote. Kuhusu tatizo la watumishi wa sekta ya afya, Waziri Mkuu aliahidi kuwa watapatikana katika muda mfupi.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Dk. Japhet Simeo, alimweleza mwandishi wa habari hii kwamba ameanzisha mfumo wa ukaguzi na udhibiti wa dawa zinazoletwa kwa kutumia leja (ledger) tangu zinapoingia stoo hadi kwenye chumba cha kutolea dawa.

“Kosa la kitakwimu halina msamaha, mtumishi akikosea kuoanisha mahesabu (tallying) anapaswa kujaza commitment form na sisi tunachukua hatua kuanzia hapo,” alisema Dk. Simeo.

“Pia nimeunda Kamati ya Wilaya ya Ukaguzi wa Dawa ya Idara ya Afya kwa vituo vyote vya afya na zahanati ambayo hufanya ukaguzi mara moja kila baada ya miezi miwili. Hii inasaidia kufanya re-distribution ya dawa kwa zahanati zenye upungufu,” alisema.

Dk. Simeo alisema maboresho mengine anayofanya ni kudai taarifa za mwezi ambazo ametaka zimfikie tarehe 5 ya kila mwezi. “Nina zahanati 28, vituo vya afya vitatu na hospitali ya wilaya moja, hizi ni taarifa 32 ninazopokea kila mwezi na ninaipitia kila moja ili kujiridhisha licha ya kuwa zimetoka kwa wasaidizi wangu. Inanisaidia kupata picha halisi ya utendaji kazi,” alisema.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, DESEMBA 22, 2015.

BENDI YA FM ACADEMIA YAWAPAGAWISHA WAKAZI WA MKOA WA ARUSHA NA VITONGOJI VYAKE

$
0
0
Mwanamuziki wa Dansi Patcho Mwamba Akiwa anaimba mbele ya washabiki wake waliouthuria onyesho la bendi hiyo lililofanyika ndani ya ukumbi wa Triple A uliopo ndani ya jiji la Arusha
Wanenguaji wa bendi ya Fm Academia wakifanya mambo ndani ya ukumbi wa Triple A uliopo ndani ya jiji la Arusha.
Washabiki wa bendi ya Fm Academia wakiwa wanacheza nyimbo ya heshima kwa wanawake iliyokuwa ikipigwa bendi hiyo.
Washabiki wa fm wakiwa waangalia show ya nguvu iliyokuwa inadondoshwa na bendi hiyo 
Mwanamziki wa kingombe blaise akiwa na mmoja wamashabiki wake waliouthuria show hivyo.
Washabiki wa bendi ya fm Academia wakiwa wanaendelea kucheza sebene la nguvu lilokuwa likidondoshwa na bendi hiyo.

Picha zote na Woinde shizza wa libeneke la kaskazini blog.

C-SEMA , TAJOC WAJADILI ULINZI MTOTO

$
0
0
 Afisa Mtendaji Mkuu wa C-SEMA, Kiiya Kiiya akizungumza na Waandishi wa Habari za Watoto (TAJOC) na Wadau Watunga Sera katika kampeni Nijali Mtoto wa Tanzania iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Mshauri Mwandamizi wa Kituo cha Huduma ya Simu kwa Mtoto wa C-SEMA, Thelma Dhaje akizungumza na Waandishi wa Habari za Watoto (TAJOC) na Wadau Watunga Sera katika kampeni Nijali Mtoto wa Tanzania iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Wadau wa Watoto wakiwa katika picha ya pamoja jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
WATOTO  wametakiwa kupewa ulinzi katika jamii katika kuweza kuwa na kizazi kinachojiamini na kufanya watoto kuwa wanajiamni ni kuondokana na mila potofu ambazo zinawakandamiza ikiwemo ukeketaji kwa watoto wa kike.

Akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari za Watoto (TAJOC) na Wadau Watunga Sera katika kampeni Nijali Mtoto wa Tanzania, Mkurugenzi wa C-SEMA, Michael Kehongoh amesema ulinzi wa watoto unatakiwa kupewa kupaumbele ikiwemo kutenga bajeti ya watoto.

Kehongoh amesema katika mazingira yaliyopo mtoto anatakiwa ulinzi wa kumuwezeha kuishi ikiwa ni pamoja na serikali kuunda timu za ulinzi ambapo ni Halmashauri chache ambazo zimeweza kufanya hivyo.
Amesema maafisa ustawi wa jamii ni kiungo katika usimamizi wa watoto kwa serikali kuweka kipaumbele cha bajeti ya kuweza kutekeleza majukumu yao.

Kehongoh Maafisa ustawi wa jamii kwa nchi zilizoendelea zimeweka kipaumbele kutokana na kazi wanazozifanya zinahusiana moja kwa moja na jamii na watu wengine wanatakiwa kupata taarifa kwa watu hao.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa TAJOC, Edward Qorro amesema waandishi kuhabarisha masuala yanayohusu watoto ni jukumu letu hivyo kunahitaji ushirikiano katika kupeana taarifa juu ya ulinzi wa watoto.


Amesema kazi ambayo imekuwa kikwazo ni kuwafikia watoto pale inapotokea tatizo hapo hapo kutokana na changamoto ya rasilimali fedha.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AHUTUBIA- MANDAWA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akimtambulishasha diwani wa kata ya Mandawa kwa tiketi ya CUF, Said Abdallah `Nachinga na kuahidi kuwa atashirikiana nae kwa karibu katika kazi za kuwaletea maendeleo wananchi wa kata hiyo bila kujali tofauti za vyama. Alikuwa ktika mkutano wa hadhara kwenye kijiji cha Mandawa Desemba 22, 2015.   
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Mandawa wilayani Ruangwa kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara kijijini hapo desemba 22, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Dkt. Magufuli kuwa Mgeni Rasmi Mkesha wa kuiombea amani Tanzania.

$
0
0
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Makanisa ya Kipentekoste (Tanzania Fellowship of Churches) Askofu Godfrey Malassy (kushoto) akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo 22 Desemba, katika Ukumbi wa Idara ya Habari jijini Dar es Salaam kuhusu maandalizi ya Mkesha Mkubwa wa Kitaifa wa kuliombea Taifa pamoja na dua maaum ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli ambaye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika dua hiyo. Kulia ni Mwanakamati wa Jumuiya hiyo, Mchungaji Olivia Mallonga.
Mwanakamati wa Jumuiya ya Makanisa ya Kipentekoste (Tanzania Fellowship of Churches) Mchungaji Mchungaji Olivia Mallonga (kulia) akichangia mada wakati wa mkutano na waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo 22 Desemba, katika Ukumbi wa Idara ya Habari jijini Dar es Salaam kuhusu maandalizi ya Mkesha Mkubwa wa Kitaifa wa kuliombea Taifa pamoja na dua maaum ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli ambaye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika dua hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Makanisa hayo Askofu Godfrey Malassy.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Makanisa ya Kipentekoste (Tanzania Fellowship of Churches) Askofu Godfrey Malassy akionyesha kitabu mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kilichozinduliwa na Jumuiya ya Makanisa hayo kinachohusu siri ya amani kwa taifa.



MAJALIWA AKUTANA NA ASKOFU NGONYANI WA LINDI

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu wa Jimbo Katoliki la LindI Mhashamu, Anthony Ngonyani kwenye Ikulu ndogo ya Ruangwa Desemba 22, 2015.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kizungumza na Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi Mhashamu Anthony Ngonyani kwenye Ikulu ndogo ya Ruangwa Dasemba 22, 2015.
(Picha na Ofisi ya Wazri Mkuu)

ABILIA WAKIWA STENDI KUU YA MABASI YA KWENDA MIKOANI (UBUNGO)

$
0
0
Abilia wakiwa katika Stendi Kuu ya mabasi ya kwenda mikoani Ubungo jijini Dar es Salaam wakisubilia usafili wa kuelekea Mikoa mbalimbali, leo.
Abilia wakiwa katika Stendi Kuu ya mabasi ya kwenda mikoani Ubungo jijini Dar es Salaam, wakiimalisha usalama wa malizao, leo.
Abilia wakiwa wamejipumzisha chini ya mti katika Stendi Kuu ya mabasi ya kwenda mikoani Ubungo jijini Dar es Salaam leo.

Picha na Emmanue Massaka wa Globu ya jamii.

RAIS MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA SPIKA WA BARAZA LA SENETI NA MJUMBE MAALUM WA RAIS WA JAMHURI YA BURUNDI,PIERRE NKURUNZINZA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Ndugu Reverien Ndikuriyo, Spika wa Seneti na Mjumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Burundi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Ndugu Reverien Ndikuriyo, Spika wa Seneti na Mjumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Burundi.

 PICHA NA IKULU.

Watendaji wa Tanesco Wazidi Kubanwa Watakiwa Kukamilisha Miradi Kabla Ya Februari Mwakani.

$
0
0
x28
Naibu Waziri Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani (wa kwanza kulia) akitoa maagizo ya kukamilika kwa mradi huo ifikapo february mwakani kwa Mkurugenzi Mwandamizi wa Miradi TANESCO Bw.Gregory Chegere (wa kwanza kushoto) alipofanya ziara yake leo katika mradi wa  Tanzania Energy Development Access Program (TEDAP) eneo la Mbagala Rangi Tatu,jijini Dar es Salaam,Mradi huo utasaidia kusambaza umeme wenye nguvu ya kutosha na unaotarajia kunufaisha zaidi ya wananchi elfu kumi wa eneo hilo,watatu kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Paul Masanja.
x29
Naibu Waziri Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani (kushoto) akitoa maagizo kwa Mkandarasi wa Kampuni ya SAE Power Lines Bw.Tahir Mehmood (wa kulia) anayejenga mradi wa TEDAP eneo la Kurasini jijini Dar es salaam kuhakikisha mpaka mwanzoni mwa mwakani awe amshafunga Transifoma katika eneo hilo la mradi ni baada ya kutoridhishwa na kasi ya utekelezaji wake katika mradi huo. 
x30
Mhandisi Mkuu wa Miradi TANESCO Bw. Frank Mashalo (wa kwanza kulia) akimweleza  Naibu Waziri Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani (wa pili kushoto)kuhusu maendeleo ya mradi  TEDAP uliyopo maeneo ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam na (wa kwanza kushoto) ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Paul Masanja.
x31
Naibu Waziri Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani (kushoto) akisikiliza malalamiko ya  mmoja wa wateja wa huduma za TANESCO  Bw.Michael Sedyan, Mkazi wa Sinza,hii ni baada ya Naibu waziri kufanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za Tanesco Magomeni leo jijini Dar es Salaam.
x32
Afisa Muendesha Mitambo kituo cha TANESCO Kipawa Bibi Zuhura Mmanyi (wa kwanza kulia)akimweleza Naibu Waziri Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani (wa kwanza kushoto) namna mitambo ya eneo hilo inavyofanya kazi na maeneo mitambo hiyo inayosambaza umeme ikiwemo eneo la Gongo la mboto,Kiwalani,Segerea,Chang’ombe na Buguruni leo jijiji Dar es Salaam Naibu waziri alipo fanya ziara yake katika ofisi hiyo (wapili kushoto ni Mkurugenzi Mwandamizi wa Miradi TANESCO Bw.Gregory Chegere na wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Paul Masanja.
x33
Naibu Waziri Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani (wa kwanza kushoto) akitoa maagizo kwa Mkandarasi wa Kampuni ya SAE Power Lines Bw.Stephen Joseph (wa kwanza kulia) anayejenga Mradi wa TEDAP eneo la Gongo la Mboto kuhakikisha umeme unaanza kuwaka katika mitambo hiyo ifikapo mwishoni mwa mwezi Desemba 2015 kwa kuwa kila kitu kimeshakamilika katika mradi huo na malipo yake tayari ameshamaliziwa kulipwa, (wapili kushoto) ni Mkurugenzi Mwandamizi wa Miradi TANESCO Bw.Gregory Chegere.
x34
Naibu Waziri Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani (kulia) akimsikiliza mmoja wa wateja wa Ofisi ya TANESCO Magomeni Bw.Mohamed Bago Mkazi wa Manzese alipokuwa akitoa kero yake kuhusu kusubiri zaidi ya masaa matatu kupatiwa huduma ya tatizo ya luku yake ambayo haiingizi umeme,hiyo ni baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za Tanesco Magomeni.Picha na Na Anitha Jonas –MAELEZO.

Matokeo ya NBAA yatangazwa

$
0
0
Na Nyakongo Manyama-Maelezo
 
Jumla ya watahiniwa 813 ambao ni sawa na asilimia 14.3 wamefaulu mitihani ya Bodi ya Taifa ya Wasahibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) na uliofanyika Novemba 2015 kote nchini.
 
Katika matokeo hayo, wahitimu wengine 1867 ambao ni sawa na asilimia 32.9 wamefaulu baadhi ya masomo katika ngazi mbalimbali kati ya watahiniwa 6404 waliosajiliwa katika mitihani iliyofanyika novemba mwaka huu.
 
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji Bodi NBAA Bw. Pius Maneno katika kikao cha wakurugenzi wa bodi hiyo kilichokaa kuidhinisha matokeo hayo leo jijini Dar es salaam.
 
IMG_0256Bw. Pius amesema kuwa jumla ya watahiniwa 725 ambao ni sawa na asilimia 11.3 walishindwa kufanya mitihani kutokana na sababu mbalimbali hivyo kufanya jumla ya watahiniwa waliofanya mitihani hiyo kuwa 5,679 ambayo ni sawa na asilimia 88.7.
 
“Kati ya watahiniwa waliofanya mitihani hiyo, watahiniwa 236 ambao ni sawa na asilimia 4.2 wamefaulu mitihani katika mkao mmoja na wengine 258 sawa na asilimia 4.5 wamefaulu kwa kufaulu masomo waliyokuwa wameshindwa katika miaka ya nyuma na wengine 319 sawa na asilimia 5.6 wamefaulu katika masomo waliyokuwa wamebakiza” alisema Bw. Pius.
 
Aidha, Bw. Pius aliongeza kuwa katika mitihani ya Novemba 2014 na ya Novemba 2015 kiwango cha ufaulu kimeshuka kutoka asilimia 53.1 hadi kufikia asilimia 47.2 ikiwa ni pungufu ya asilimia 5.9 pia kuna upungufu wa watahiniwa 107 sawa na asilimia 1.8.
Bw. Pius aliwapongeza watahiniwa waliofuzu na kuwataka ambao hawajafuzu kutokata tamaa bali waongeze juhudi zaidi katika masomo yao ili waweze kufanya vizuri katika mitihani ijayo ya bodi.
 
Mitihani ya bodi ya Taifa ya wasahibu na wakaguzi wa hesabu Tanzania ni ya tatu chini ya mfumo mpya a elimu na mafunzo unaozingatia weledi ambayo ilifanyika katika vituo 11 vya mitihani vilivyopo Tanzania Bara na Visiwani na ilihusisha watahiniwa katika hatua ya kwanza na ya pili katika ngazi ya Cheti cha Utunzaji wa Hesabu, hatua ya awali, kati na hatua ya mwisho.

WAZIRI KITWANGA ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA NIDA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
571
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akiwasili Makao Makuu ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Kinondoni jijini Dar es Salaam na kupokewa na Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dickson Maimu (kushoto). Waziri Kitwanga alifanya ziara ya kikazi katika ofisi hizo kwa lengo la kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na mamlaka hiyo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
544
Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Brenda Joshua akimfafanulia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (aliyevaa tai), jinsi wanavyosajili taarifa mbalimbali za waombaji wa vitambulisho. Waziri Kitwanga alitembelea Kituo hicho cha Usajili na kujifunza kazi mbalimbali zinazofanywa na NIDA, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil na kulia kwa Abdulwakil ni Naibu Katibu Mkuu, John Mngodo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
572
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akiieleza jambo menejimenti ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wakati alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya NIDA, Kinondoni, jijini Dar es Salaam leo. Watatu kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abduwakil, wapili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, John Mngodo, na watatu kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dickson Maimu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
573
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dickson Maimu akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya NIDA, Kinondoni, jijini Dar es Salaam leo.  Watano kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abduwakil, wanne kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, John Mngodo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

HENNESSY'S 250 YEARS EXHIBITION AT OASIS BAR MASAKI

$
0
0
The owner of Oasis Bar and Lounge Nuru Mosha clarifying something to journalists at the The Hennessy 250's  Exhibitions.
Some pictures related to Hennessy
The Amazing Hennessy bottle
Some paints related to Hennessy 
The event was accompanied by live music
The Hennessy' s bar at Oasis Masaki
*************
By Staff Reporter
The four-day exhibition to mark the 250 years of Hennessy was launched in Dar es Salaam this Monday,  at Oasis Bar, Masaki and it has attracted many people including artists, socialites as well as other arts stakeholders.

The event was accompanied by a live music performance and involved artwork and limited edition bottles done by different artists, profiling the history and heritage of Hennessy.

Speaking with journalists at the Oasis Bar on Monday where the exhibition is taking place, the owner of Oasis Bar and Lounge Nuru Mosha clarified that, The Hennessy 250 Exhibitionis a multidisciplinary event in which the exhibition showcases the treasures of its heritage.

He added that it reflects the vision that Hennessy has always had of itself and the world around it, a taste for the avant-garde and the pull of distant horizons.

" This hybrid cultural event and exhibition at Oasis Wine Bar with accompanying music and live performances, is a reflection of the unique bond that Hennessy has always maintained with the art world" he added.

He also added that since the Hennessy family were early patrons of the arts and have always been close to artists themselves, the exhibition would of course involve the arts.

"This has given us reflections of the longevity and permanence of its products in limited editions with prestigious signatures and even here in Tanzania. Hennessy is very proud to support artistic activities" he said.

Diamond: Njooni Dar Live X-mas, sitawaangusha!

$
0
0
Funga Mwaka Concert 2015 (7)Funga Mwaka Concert 2015 (9)
Diamond Platnumz akiwasalimia mashabiki wake waliofurika katika eneo la Karume leo kwenye mkutano na wanahabari kuhusu shoo yake itakayofanyika Dar Live kwenye Sikukuu ya Krismasi.
Funga Mwaka Concert 2015 (10)
Diamond akiimba wimbo wake mpya wa Utanipenda sambamba na mashabiki waliofurika Karume leo.
Funga Mwaka Concert 2015 (8)
Mashabiki wakiwa wamepagawa wakati Diamond akiimba wimbo wake mpya wa Utanipenda.
Funga Mwaka Concert 2015 (1)
Meneja Masoko wa Global Publishers na Dar Live, Innocent Mafuru (mwenye tisheti nyeupe aliyesimama kulia) akiwakaribisha wanahabari, wasanii na mashabiki wa burudani katika mkutano na wanahabari kuelekea shoo ya Funga Mwaka itakayofanyika Dar Live kwenye Sikukuu ya Krismasi.
Funga Mwaka Concert 2015 (2)
Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho akielezea jinsi walivyojipanga kwa shoo hiyo ya Krismasi.
Funga Mwaka Concert 2015 (3)Meneja Uhusiano Msaidizi wa Airtel Tanzania, Jane Matinde akionyesha kadi ya Airtel Money Tap Tap inayomuwezesha mteja kufanya malipo mahali popote na watakaohudhuria shoo ya Diamond kununua tiketi kwa punguzo la shilingi 5000 kwa wateja 1000 wa kwanza.

Funga Mwaka Concert 2015 (4)
Mratibu wa Burudani Dar Live, Juma Mbizo akiongea na wanahabari pamoja na mashabiki (hawapo pichani) kuhusu walivyojipanga kuwapa burudani mashabiki siku ya Krismasi.
Funga Mwaka Concert 2015 (5)
Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Staric ambaye naye atapanda jukwaani siku hiyo akiongea na mashabiki.
Funga Mwaka Concert 2015 (6)
Diamond akizidi kuwapagawisha mashabiki wake.
Funga Mwaka Concert 2015 (18)Funga Mwaka Concert 2015 (19)
Baada ya kuongea na mashabiki wake Diamond aliamua kugawa CD na DVD za nyimbo zake kwa mashabiki waliohudhuria.
Funga Mwaka Concert 2015 (20)
Diamond akiwaaga mashabiki na kuwataka wakutane Dar Live katika Sikukuu ya Krismasi.
Funga Mwaka Concert 2015 (21)
Mashabiki wakiwa wamemzingira Diamond wakati akiondoka eneo la mkutano na wanahabari leo.
Funga Mwaka Concert 2015 (22)Funga Mwaka Concert 2015 (23)Mashabiki wakiwa wamezingira gari la Diamond wakati akiondoka.
STAA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amewaahidi shoo ya nguvu mashabiki wake na kuwataka waje kwa wingi katika shoo kali ya kufunga mwaka itakayopigwa Dar Live, Mbagala Zakhem, Dar katika Sikukuu ya X-mas na kuwa hatawaangusha. Diamond anayetamba na ngoma ya Utanipenda ameyaongea hayo leo kwenye mkutano maalum uliofanyika Karume, Dar ambao ulihusisha waandishi wa habari na wapenzi wa muziki kwa ajili ya kuzungumzia shoo hiyo kubwa kuliko inayojulikana kama Funga Mwaka Concert. “Itakuwa ni Sikukuu ya Krismasi, sasa kwa nini tusifurahi pamoja, kama MTV wameamua kunipa tuzo ya Mtumbuizaji Bora Afrika kwa hiyo sihitaji kuongea sana shoo itakuwaje siku hiyo, naomba mje kwa wingi kwa kweli sipendi kuwaudhi, nawaahidi sitawaangusha,” alisema Diamond au Baba Tiffah. Pia waandaji wakuu wa shoo hiyo, Global Publishers Ltd, kupitia kwa Meneja Mkuu, Abdallah Mrisho, naye alizungumza machache pamoja na kutambulisha listi ya wasanii wengine watakaoambatana na Diamond siku hiyo. “Mbali na Diamond pia kutakuwa na Msagasumu, Wakali Dancers, Staric pamoja na burudani nyingine nyingi. Haitakuwa shoo ndogo, Diamond ameamua kufurahi na mashabiki wa muziki siku ya Krismasi kwa kufunga na kuukaribisha mwaka mpya. Shoo zitaanza asubuhi kwa watoto mpaka saa 12 jioni kisha baada ya hapo ni watu wazima mpaka alfajiri,” alisema Mrisho. Viingilio ni Sh 15,000 na kwa V.I.P ni Sh 30,000 lakini wadhamini wakuu wa shoo hiyo, Kampuni ya Mawasiliano ya Airtel wakaamua kutoa ofa ya punguzo la bei kwa tiketi 1,000 za awali kwa watakaokata kupitia kadi mpya za Airtel Money Tap Tap zenye mfumo mpya wa kulipia bili mbalimbali. “Kadi za Tap Tap zinazorahisisha kufanya malipo zaidi popote ulipo bila ya gharama yoyote tayari zipo zinapatikana maeneo ya Temeke na Ilala lakini kuwa nayo unapaswa kuwa na kadi ya Airtel na kwa wateja 1,000 wa kwanza wenye Tap Tap watakaokata tiketi kupitia kadi hiyo watakuwa na punguzo la Sh 5,000 yaani kwa 15,000 itakuwa 10,000 na 30,000 itakuwa 25,000,” alisema Meneja Uhusiano Msaidizi wa Airtel Tanzania, Jane Matinde. Habari: Hans Mloli, Picha: Musa Mateja

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amsimamisha kazi Mkurugenzi wa (RAHCO),avunja mamlaka ya reli Tanzania (TRL)

$
0
0

magufuli1 (1)

Rais wa Jamhuri ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hodhi ya rasilimali za reli Tanzania (RAHCO) Mhandisi Benhadard Tito ili kupisha uchunguzi wa kina kufuatia ukiukwaji mkubwa wa taratibu za manunuzi uliobainika katika mchakato wa utoaji wa zabuni ya ujenzi wa reli ya kati.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema, Rais Magufuli amefikia uamuzi huo baada ya kuitisha kikao cha wataalamu kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za serikali ambazo zinahusika katika utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Reli ya kati kwa kiwango cha kisasa yaani “Standard Gauge”

Amesema pamoja na kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa RAHCO, Rais Magufuli ameivunja bodi ya RAHCO baada ya kujiridhisha kuwa haikutekeleza ipasavyo wajibu wake katika kusimamia mchakato wa zabuni hiyo na badala yake imeonekana kutetea kilichofanyika.

Aidha Rais Magufuli amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa RAHCO Mhandisi Benhadard Tito kutoa ushirikiano kwa vyombo vya serikali vitakavyofanya uchunguzi zaidi kuhusu mchakato wa Zabuni hiyo.

Pia ameiagiza Mamlaka ya udhibiti wa manunuzi ya umma (PPRA) kuchunguza na kuchukua hatua dhidi ya kampuni za ukandarasi zilizopewa zabuni ya ujenzi huo endapo itathibitika kuwa zimeshiriki katika ukiukwaji wa sheria.

Pamoja na kusimamishwa kazi kwa Mkurugenzi Mkuu wa RAHCO Mhandisi Tito na Kuvunjwa kwa Bodi ya RAHACO, Rais Magufuli pia amemuagiza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU kuanza uchunguzi wa kina mara moja kuhusiana na sakaata hilo la ukikwaji wa sheria ya manunuzi katika zabuni ya ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kisasa yaani "Standard Gauge".

Katika hatua nyingine Balozi Sefue amesema, Rais Magufuli amevunja bodi ya Mamlaka ya Reli Tanzania (TRL) kutokana na kutoridhishwa na jinsi bodi hiyo ilivyoshughulikia ripoti ya uchunguzi wa mchakato wa ununuzi wa mabehewa ya treni.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
22 Desemba, 2015

HEKA HEKA ZA SIKUKUU YA XMASS NA MWAKA MPYA NDANI YA SOKO LA KARIAKOO

$
0
0
 
 Wananchi kutoka ndani na nje ya jiji la Dar es Salaam wakiwa katika soko Kuu la Kariako,katika maandalinzi ya Sikukuuu ya X-mass na Mwaka mpya pichani kama walivyonaswa na Camera ya Globu ya Jamii mapema jana jioni.Picha na Emmanue Massaka wa Globu ya jamii.
 Sehemu ya Umati wa watu ndani ya soko la Kariakoo katika harakati za maandalizi ya sikukuu ya Xmass na Mwaka mpya.
 Kila mmoja na heka heka zake za maandalizi ya Sikukuu.

WATU SABA WAFARIKI DUNIA KWA KUUNGUA NA MOTO NA WENGINE KUMI WAJERUHIWA

$
0
0
 Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kigoma Ferdnand Mtui  akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) juu ya ajali ya moto iliyotokea Mkoani Kigoma.
 Majeruhi wakiendelea kupatiwa huduma katika wodi namba saba hospitali ya Mkoa wa Kigoma.
 Majeruhi wakiendelea kupatiwa huduma ya matibabu katika wodi namba saba hospitali ya Mkoa wa Kigoma.

                                               Na Editha Karlo wa blog wa jamii,Kigoma
WATU saba wamefariki duniani na wengine kumi wamejeruhiwa katika ajali ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka na kulipuka na kuwaka moto.

Akiongea na mtandao huu ofisini kwake Mganga Mkuu wa hospitali ya Mkoa wa Kigoma Maweni Dkt. Leonard Subi amesema kuwa jana majira ya saa 12 jioni walipokea miili ya marehemu 6 na majeruhi 11 ilipofika saa 6 usiku majeruhi mmoja alifariki duniana na kupelekea idadi ya vifo kuwa saba.

Aliwataja waliofariki katika ajali hiyo ni Ashura Mussa, Kadogo Yusuph, Kabwe Iddy, Mwamvua Juma na Peter Sungura,maremu wawili miili yao bado haijatambulika sababu ya kuungua vibaya.

Dkt. Subi aliwataja pia majeruhi wa ajali hiyo kuwa ni Andrew Peter, Amos Thomas, Mutta Hamis, Shabaan Fadhil, Hassan Kasa, Esau Elias, Asha Kassim na Riziki Jaah.

"Majeruhi wote wamelazwa wodi namba saba na hali zao siyo nzuri wanaendelea na matibabu, mtoto aitwaye Riziki Jaah mwenye umri wa miezi nane ndiye aliyenusurika katika ajali hiyo hajaumia popote mama yake alimtupa dirishani baada ya moto kuwaka ila mama yake alifariki kwa kuungua kwenye ajali hiyo"alisema Dkt. Subi.

Naye Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kigoma, Ferdnand Mtui amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ya gari aina ya Toyota Hiace lenye  namba T.700 ADK lililokuwa likitoka Kigoma mjini kwenda katika kijiji cha Subankala kata ya Ilagala Wilayani Uvinza kilichopo mwambao mwa ziwa Tanganyika.

Kamanda Mtui alisema kuwa ajali hiyo ilitokea katika kijiji cha Mwakizega na chanzo cha ajali hiyo ni dereva kuwakwepa watembea kwa miguu kisha kugonga gema iliyopelekea gari kupinduka na kuwaka moto.

SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LAZINDUA MFUMO MPYA WA KISASA WA USIMAMIZI WA MIZIGO KWENYE VIWANJA VYA NDEGE

$
0
0
SHIRIKA la ndege la Etihad ambalo ndio shirika rasmi la nchi ya Falme za kiarabu, leo hii limetangaza makubaliano na kampuni ya Luggage Logistics kuboresha mfumo mzima wa usimamizi wa mizigo katika viwanja vake vya ndege dunia nzima.


Kupitia mfumo wa kisasa wa Baggage Management System (BMS) unaosimamiwa na kampuni ya Luggage Logistics, shirika la ndege la Etihad litaweza kuboresha usimamizi ikiwemo kusafirisha mizigo ya wasafiri kwa wakati. Mfumo huo pia utawezesha kufuatilia kwa urahisi mizigo iliypotea njiani dunia nzima.

Mfumo wa BMS utahusisha ratiba za ndege, taarifa za wasafiri pamoja na mifumo ya udihibiti safari zote ka pamoja. Hii itasaidia kuongeza kasi taratibu za kutambua mizigo ya abiria na kisha kuhamisha mizigo toka kwenye ndege hadi uwanja wa ndege na hatimaye kwenda kwenye ndege ya kuunganisha safari husika, ikisaidia safari kutochelewa.

Mfumo huu umeunganishwa katika kituo kimoja cha udhibiti ambapo taarifa zote za mizigo kutoka vyanzo mbalimbali hutunzwa. Taarifa hizi zinaweza kusambazwa haraka na uwepesi baina ya vitengo husika dunia nzima.

Geert W. Boven, Makamu rais wa Huduma za viwanja vya ndege kutoka Etihad, alisema: “Ushirikiano na kampuni ya Luggage Logistics kutaongeza ufanisi zaidi katika kutambua, kusimamia na kusafirisha mizigo ya abiria duniani kote kwenye viwanja vyetu tukianzia na hapa Abu Dhabi. 

Mfumo mpya huu utasaidia kuboresha huduma kwa abiria kwa kupunguza upotevu wa mizigo, kupunguza idadi ya safari zinazochelewa juu ya kupotea kwa mizigo pamoja na kuongeza ufanisi wa huduma zetu za uwanja wa ndege”

Adam Dalby, Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Luggage Logistics, alisema “Tunayofuraha kushirikiana na shirika la ndege la Etihad, shirika ambalo tupo pamoja katika kutambua umuhimu wa uvumbuzi na huduma bora. Kupitia mfumo huu wa kisasa wa BMS, taarifa za papo hapo hupatikana na hutumika kuhakikisha mizigo ya abiria inasimamiwa kwa ufanisi zaidi safari nzima”


Shirika la ndege la Etihad lilichagua mfumo wa BMS kwani unakidhi mahitaji na vigezo vyote vya usimamizi mizigo, ikiwemo ICAO Annex 17 pamoja na maazimio ya IATA, mfumo huu unaweza kuunganishwa na mitambo ya shirika hili la ndege bila ugumu wowote pia. Suluhisho hili limewiana na uendeshaji na mahitaji ya miundombinu ya Shirika la ndege nay ale ya kituo cha Abu Dhabi.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli Atoa Mkono wa Krismas na Mwaka Mpya kwa Wazee wa Kijiji cha Welezo Zanzibar.

$
0
0
Mlukulu wa Ikulu Zanzibar Ndg Ameir Ali Khatib akimkabidhi Mbuzi Sister Mary Gemma wa kituo cha Wazee Welezo, hafla hiyo imefanyika katika makaazi ya Wazee hao Welezo Zanzibar, Vyakula hivyo vimetolewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli kwa ajili ya Wazee hao kujumuiika na Wananchi katika kusherehekea Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya. 
Mlukulu wa Ikulu Zanzibar Ndg Ameir Ali Khatib akimkabidhi Mafuta ya Kupikia Sister Mary Gemma wa kituo cha Wazee Welezo, hafla hiyo imefanyika katika makaazi ya Wazee hao Welezo Zanzibar, Vyakula hivyo vimetolewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli kwa ajili ya Wazee hao kujumuiika na Wananchi katika kusherehekea Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya. 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwezeshaji Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Zanzibar Ndg. Msham Abdalla akiozungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidha vyakula hivyo vilivyotolewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli. 
Wazee wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wakati wa hafla hiyo ya kukabidhiwa Vyakula kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya vilivyotolewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli kwa Wazee hao. kuweza kushiriki kwa vizuri katika sikukuu hizo.
Viongozi wa Kijiji cha Wazee wa Wasiojiweza Welezo Zanzibar wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwezeshaji Ustawi wa JamiiVijana Wanawake na Watoto Ndg Msham Abdalla wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi msaada wa vyakula kwa Wazee wa Welezo Zanzibar.
Msimamizi wa Kijiji hicho cha Wazee Welezo Zanzibar Sister Mary Gemma akitowa shukrani kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa msaada huo umefika wakati muafa na kutowa shukrani zake kwa Nioba ya Uongozi wa Kituo hicho kinachohudumia Wazee wasiojiweza Zanzibar.
Mzee wa Kijiji cha Wazee Wasiojiweza Welezo Zanzibar Mzee Shein Kombo akitowa shukrani kwa niaba ya Wazee wa Kijiji hicho kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli kwa msaada wake kwa Kuwakumbuka na kumtakia kazi njema katika uongozi wake na kumalizia.
Hapa Kazi Tu.
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot 
Zanzinews.com
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images