Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live

SERIKALI WILAYANI CHUNYA KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU WAJIPANGA KUTATUA KERO ZA MAJI WILAYANI HUMO

0
0
Inline image
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Elias John Tarimo akizindua Mradi wa Kisima cha Maji Kijiji cha Ngwala Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya kilicho jengwa na Kampuni ya utafiti wa madini yaPeak Resources Katika kata ya Ngwala Wilayani humo .
Inline image
Baadhi ya Wananchi wakishuhudia uzinduzi wa Mradi wa Maji Kijiji cha Ngwala Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya.

Na Ezekiel Kamanga ,Mbeya,Jamiimojablog 
Serikali WIlayani Chunya Mkoani Mbeya kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wameendelea na jitihada mbalimbali katika kuhakikisha wanatatua changamoto ya ukosefu wa maji wilayani humo.

Hatua hiyo  inakuja kufuataia  kampuni ya Peak Resource limited ambayo hujihusisha na utafiti wa madini adimu chini ya ardhi yanayopatikana katika kata  ya ngwala wilayanii chunya mkoani mbeya kuchimba visima viwili vya maji vyenye thamani ya shilingi milioni 16.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya visima hivyo Mkuu wa Wilaya ya Chunya Ndugu Elias Tarimo  amesema hatua ya kampuni huyo inayojihusisha na utafiti wa madini kuamua kuchimba visima hivyo kwa lengo la kuwasaidia wananchi ni jambo jema nalinalotakiwa kuungwa mkono na wananchi hao.

Amesema katika kuunga mkono jitihada hizo wananchi hao   hawana budi kutunza miundo mbinu hiyo waliojengewa kwani wakiiharibu watarudi katika adha ya shida ya maji walikuwanayo hapo awali na kwamba waendeleze ushirikiano bora na kampuni hiyo.

 Akisoma tarifa fupi ya ujenzi wa miradi mbalimbali waliojenga katika kata hiyo  meneja mradi wa Peak Resource limited Patrick Ochieng amesema miradi waliojenga ni visima viwili vilivyogharimu  milioni 16kila kimoja unjezi wa nyumba ya mwalimu iliyogharimu shilingi milioni 55 na ujenzi wa eneo la kupumzikia wagonjwa katika kituo cha Afya cha Ngwala iliyogharimu  shilingi milioni  7 vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 94.

Ochieng alindelea kueleza kuwa kwa sasa Kampuni yao ipo katika hatua za mwisho za utafiti na kwamba wanafwatilia leseni ya uchimbaji madini na kibali kutoka nemki ili kuanza uzalishaji na kwamba mgodi huo unauwezo wa kudumu kuchimbwa kwa miaka 40.

Aidha baadhi ya waliohudhuria katika sherehe za uzinduzi wa miradi ni pamoja na Mwenyekiti wa kijiji cha  Neston Simoni na Diwani wa Kata ya Ngwala Donard Maganga ambao walisema wamefurahishwa na kile kinachofanywa na kampuni hiyo kwani wanajenga miradi bora kwa kutumia gharama nafuu.

Maganga aliwataka wakazi wa Ngwala kuiga mfano wa kampuni hiyo kwani nalisema nyumba waliojenga ya shilingi milioni 55 ukiweka Mkandarasi wangeweza kujenga kwa shilingi milioni 100 hivyo alisema mfano wa kampuni hiyo unapaswa kuigwa ili kuondoa ufisadi katika jamii yetu.

Kwaupande wa wananchi waliokuwepo hapo walishukuru kampuni hiyo kwa kupunguza adha walizokuwa nazo katika Kata yao kwani kwasasa wamekuwa na matumaini wa kupata walimu ambao watafundisha watoto wao katika mazingira yalio bora kutokana na uwepo wa nyumba bora ya Mwalimu ukilinganisha na hapo awali walikuwa wanakosa eneo la kujihifadhi,alisema Raisoni George.

Vile vile Elizabeti Yusuph mkazi wa ngwala alisema wao kama wakinamama walikuwa wachelewa kufanya shughuli za shambani kutokana na kufwata maji umbali mrefu kwani kutokana na uwepo wa mrado huo wa maji utarahisisha shughuli nyingine.
Mwisho.

MEGATRADE INVESTMENT LTD YA JIJINI ARUSHA YATOA SIKU KUU KWA WATOTO WA KITUO CHA AMANI CENTER

0
0

Watoto waish7io katika mazing4ira mag4umu wanaolelewa katika kituo cha Amani Center wakifurahia zawadi zilizotolewa na kampuni ya Megatrade kwa ajili ya siku kuu za Christmas na Mwaka mpya.
Meneja mauzo wa kam-puni ya Megatrade Investment ya jijini Arusha,Edmund Rutaraka akiwa na wafanyakazi wenzake pamoja na wafanyakazi katika kituo cha kulelea watoto waishio katika mazingira mag4umu cha Aman Center wakati alipofika kituoni hapo kukabidhi zawadi kwa ajili ya siku kuu za Christmas na Mwaka mpya.
Baadhi ya zawadi zilizotolewa na kampuni ya Megatrade kwa watoto wao.


Watoto waishio katika mazingira magumu wanao lelewa katika kituo cha Amani Center wakiweka pozi la picha mara baada ya kukabidhiwa zawadi kutoka Megatrade Investment ya jijini Arusha.
Kituo cha watoto cha Amani Center.


Meneja Masoko wa kampuni ya Megatrade kanda ya Kaskazini,Edmnd Rutaraka akizung4umza kabla ya kukabidhi zawadi kwa watoto waishio katika mazingira magumu wanaolelewa katika kituo cha Amani cha mjini Moshi.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

Temeke yajipanga kuondoa Kero ya taka

0
0
Na Raymond Mushumbusi -Maelezo

Manispaa ya Temeke imeandaa utaratibu wa  kuondoa taka katika manispaa hiyo kwa kuongeza magari na vifaa ili kuyaweka mazingira katika hali ya usafi.

Hayo yamesemwa na Msemaji wa Manispaa ya Temeke Bi Joyce Msumba alipozungumza na Mwandishi Ofisini kwake wakati alipokuwa akijibu kuhusu  kulundikana kwa taka katika Kata ya Keko iliyopo katika Manispaa hiyo.

Bi Joyce Msumba amesema kuwa taka zinazonekana zimelundikwa katika maeneo ya Manispaa ya Temeke sio madampo ila ni vituo vya ukusanyaji wa taka vilivyoteuliwa kukusanya taka kwa ajili ya kupekeka katika madampo elekezi na kuongeza kuwa taka hizo zimetokana na ufanyaji wa usafi wa tarehe 9 Desemba mwaka huu.

“ Tulipata tatizo la vifaa hasa magari ya kuzoa taka na Manispaa imeshaandaa pesa kwa ajili ya kukodi magari yatakayo zoa taka katika Manispaa yetu” alisema Bi Msumba.

Aidha msemaji wa manispaa hiyo amebainisha kuwa kuanzia kesho magari yataanza kufanya kazi ya kuzoa taka katika maeneo ya Manispaa ya Temeke ili kudhibiti hali ya mlundikano wa taka na wanaendelea kutangaza tenda za kupata wakandarasi wenye uwezo zaidi ili kumaliza tatizo hilo.

Pia ameongeza kuwa elimu zaidi inahitajika kwa wananchi kuhusu usafi wa mazingira na uhifadhi wa taka sehemu husika na sio kulundika ovyo hali inayosababisha kuwepo kwa  mlipuko wa magonjwa kama Kipindupindu.

Mlundikano wa taka katika Manispaa ya Temeke umekuwa ni kero ya muda mrefu inayosababisha hatari ya kuweko kwa magonjwa ya mlipuko hivyo ni wajibu wa kila  mwananchi kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuondoa kero hiyo.

KUTOKA KWA MH KIGWANGALLA

0
0
Ndugu zangu,
Tunaweza kuibadilisha nchi yetu tukiamua. Wiki iliyopita nili-observe namba ya mahudhurio ofisini na namna watumishi wanavyowasili, nikashangazwa kwamba Waziri wangu, Mhe. Ummy Mwalimu (MB), Katibu Mkuu, CMO - Mganga Mkuu wa Serikali na mimi tunawahi kila siku. Wafanyakazi wenzetu wengi wanachelewa!

Nikamuomba ruhusa Mkuu wangu wa kazi, Mhe. Ummy, kuwa nichukue hatua. Akanisikiliza akanielewa. Akaniruhusu. Nikatazama sheria inasemaje kuhusu muda wa kuwasili kazini na utaratibu wake wa hatua za kinidhamu. Nikachukua hatua.Watu wengi walikasirika. Walikerwa. Kila mtu alisema yake. Najua wengine walichukia. Sawa tu. Lakini wajue ‪#‎HapaKaziTu‬

Suala hili limezua mjadala mkubwa sana. Wengi wakiitupia lawama serikali wakidai wanaishi maeneo ya mbali na miundombinu ya usafiri siyo mizuri kuwawezesha kuwahi ofisini. Si jambo la kudharau ama la kutokutazamwa, la hasha. Hii ni hoja ya msingi kabisa. Lakini niseme wazi hapa kuwa haishindikani. Ili mimi binafsi niwahi ofisini kwangu saa moja za asubuhi, huamka saa kumi na nusu asubuhi kutokea kule Kijijini kwangu, natakiwa kuvuka Pantoni, na mara nyingi tu hulazimika kuvuka bila gari. Nikifika ng'ambo natembea tu Kwa miguu nawahi ofisini. Namfahamu Mkurugenzi mwingine wa hapa Wizarani, naye hufanya hivyo. Nafahamu Katibu Mkuu wa Wizara naye anaishi Salasala, lakini sijawahi kufika ofisini kabla yake!

Nidhamu ni tabia. Usipokubali kujituma, mwili unazowea uvivu na uzembe. Na uvivu ni raha. Usipoukataa uvivu hautotoka mwilini. Watanzania wengi wanapenda kuzungumzia Mabadiliko lakini hawataki kubadilika. Tubadilike kwanza sisi wenyewe ndipo tutayaona Mabadiliko tunayoyatamani.
Kwenye zama za 'Hapa Kazi Tu' viongozi tutakuwa mfano wa Mabadiliko; kwanza, tutawapa wenzetu kwenye utumishi wa umma fursa ya kubadilika, wakishindwa tutawabadilisha!

Pamoja na hatua hizi za awali za ukaguzi wa kushtukiza, tumeagiza watendaji watazame namna bora zaidi ya kuweka mifumo ya kielektroniki, biometric systems (dole gumba) na kadi za elektroniki, kwenye taasisi zote za Wizara yetu ili kudhibiti mahudhurio ya watumishi na movement yao wakati wote wa kazi. Malengo ni kuboresha huduma kwa wateja wetu.

Muda wa mwajiri unaibiwa sana. Tutaziba mianya yote mikubwa ya wizi wa muda wa mwajiri.Sambamba na mifumo hii, tutaweka utaratibu wa kupima utendaji kazi wa kila mtumishi kwa kuwawekea malengo maalum na kuwapima. Na mfumo huu utakuja sambamba na mfumo wa kutoa motisha Kwa watumishi. Maana hauwezi kumkamua ng'ombe usiyemlisha ipasavyo!
Ninawapongeza wafanyakazi wote wa Wizara kwa kuwahi mapema leo hii. Mjue tu kuwa sintowaambia ni lini tena tutafunga geti!
Ahsanteni,
Dr. Hamisi Kigwangalla, MB.
NW-AMJW.

MBUNGE WA MLALO ATIMIZA AHADI YAKE KWA WANAMLALO

0
0
 Katika utekelezaji wa ahadi zake Mbunge wa jimbo la Mlalo Rashid Shangazi amekabidhi mabati 40 ya geji 28 kwa wanajimbo la Mlalo  kwaajili ya  kwa ajili ya jengo la Maabara shule ya Sekondari Mtae pamoja na Mifuko 10 ya sementi kwaajili ya kwa ajili ya ukarabati msikiti mkuu wa makose. Alikabidhi vitu hivyo mwishoni mwa wiki mkoani Tanga.
Wana Mlalo wakishusha Mifuko ya Sementi 10  kwa ajili ya ukarabati msikiti mkuu wa makose, kutoka kwenye gari pamoja na Mabati 40 kwa shule ya Mtae wishoni mwa wiki katika jimbo la Mlalo mkoani Tanga.
sambamba na hilo alikabidhi mifuko ya Sementi 30 kwa ajili ya kukarabati  jengo la maabara shule ya sekondari kalmere na mifuko ya  sementi 10 kwa ajili ya ukarabati msikiti mkuu wa makose,hii ni kupelekea kuhakikisha mlalo inasonga mbele katika maendeleo ya jamii.

Naibu Katibu Mkuu Samataba Awaasa Walimu Kuwa Wazalendo

0
0
 Washiriki wa mafunzo ya ya kuwajengea uwezo Walimu na Wanafunzi katika Ufundishaji na Ujifunzaji kwa shule za sekondari (STEP)  wakifuatilia mafunzo hayo katika kituo cha Shule ya sekondari Kilangalanga iliyopo wilayani kibaha Vijijini  mkoani Pwani.

Walimu nchini wametakiwa kuwa wazalendo kwa kuhakikisha wanawafundisha watoto katika muda wa ziada ili kuwaongezea uwezo wa ufaulu katika mitihani yao.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Elimu Bw. Zuberi Samataba wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo Walimu na wanafunzi katika ufundishaji na Ujifunzaji kwa shule za sekondari ( STEP) yanayoendelea katika mikoa sita nchini.

Aidha, Bw. Samataba aliwataka walimu wasihangaike kutafuta michango kwa ajili ya uendeshaji wa shule na badala yake wajikite katika kufundisha na kuwasaidia wanafunzi kupata elimu na kufaulu kwakuwa serikali ndiyo itafanya kazi kubwa ya kuhakikisha fedha za uendeshaji wa shule na vifaa vinapatikana kwenye shule zote za Serikali.

Mafunzo hayo ni ya siku tano (5) yanashirikisha walimu wa shule za sekondari wapatao 2,528 yameanza kufanyika kuanzia tarehe 19 Desemba, 2015 na yanatarajia kumalizika tarehe 23 Desemba, 2015.

Mafunzo hayo yanayolenga kujenga uwezo wa walimu na  wanafunzi katika ufundishaji na ujifunzaji yanafanyika kwa awamu ambapo katika awamu hii ya pili yanafanyika katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Iringa, Singida na Katavi na hatimaye kufanyika katika mikoa yote nchini.

Awamu ya kwanza ya Programu ya STEP  ilifanyika mwezi  Juni, 2015 katika mikoa ya Mwanza, Dodoma, Geita, Mara Simiyu, Shinyanga na Tanga ambapo walimu wa sekondari wapatao 3,880 walipatiwa mafunzo hayo.Katika kila awamu, walimu wanne wa masomo ya Kiswahili, Hisabati, Biolojia na Kiingereza kutoka kwenye shule za sekondari katika Halmashauri na Mkoa husika wanashiriki katika mafunzo katika vituo mbalimbali vinavyoandaliwa na mikoa.


Katika mafunzo hayo, walimu wanajengewa uwezo wa kuwawezesha kuwatambua wanafunzi wenye uwezo mdogo kimasomo na walio katika hatari ya kufeli mitihani ya Taifa kwa kuwapatia mafunzo rekebishi kwa lengo la kuwawezesha kufaulu mitihani yao. 

Mafunzo yanayotolewa ni sehemu ya utoaji wa mafunzo ya walimu kazini ikiwa ni utekelezaji wa Programu ya kuboresha taaluma ya Walimu na Wanafunzi wa shule za Sekondari  ambayo ni mojawapo ya Mpango wa Tekeleza kwa Matokeo Makubwa  Sasa.

Programu ya STEP ilibuniwa na  Serikali kwa lengo la kubadilisha hali ya kushuka kwa ufaulu wa wanafunzi na kuboresha kiwango cha ufaulu kwa kuwawezesha walimu kujenga tabia ya kuwatambua wanafunzi wenye uwezo mdogo kimasomo na walio katika hatari ya kufeli Mtihani wa Taifa kwa kuwasaidia kufanya Mafunzo Rekebishi. 

Ili kuyafanya mafunzo yanayotolewa kufanyika kwa ufanisi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imeandaa miongozo ya masomo husika unaotumika kuwafundishia walimu hao.

Mafunzo ya STEP yanatekeleza azma ya serikali  chini ya Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) unaolenga kuweka mfumo thabiti wa kusimamia, kufuatilia na kutathmini mipango yake hususan Mpango wa Kupunguza na Kuondoa Umaskini Tanzania (MKUKUTA) na Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano.

BRN ni mfumo ambao umejikita katika kuweka vipaumbele, kufanya ufuatiliaji makini na uwajibikaji katika kuleta matokeo tarajiwa. Elimu ni mojawapo wa sekta za kipaumbele katika utekelezaji wa BRN nchini.

Sekta ya Elimu ina vipaumbele tisa (9) vilivyoainishwa ambavyo ni:- upangaji wa shule kwa ubora wa ufaulu katika matokeo ya mitihani ya kumaliza elimu ya msingi na sekondari kidato cha nne, utaratibu wa utoaji tuzo kwa shule zinazofanya vizuri ili kuzipa motisha wa kuendelea kufanya vizuri, kuandaa kiongozi cha kuimarisha utendaji wa shule na kutoa mafunzo kwa wakuu wa shule na kufanya upimaji wa stadi za Kuandika, Kusoma na Kuhesabu (KKK) kitaifa.

Maeneo mengine ya vipaumbele katika sekta ya elimu ni:- kutoa mafunzo ya Ufundishaji wa KKK kwa walimu wa darasa la Kwanza na Pili, kujengauwezo wa Walimu na swanafunzi katika Ufundishaji na Ujifunzaji, Ujenzi wa Miundo mbinu muhimu ya shule, Utoaji wa Ruzuku ya Uendeshaji na Motisha kwa walimu.

RAIS DKT MAGUFULI ASHIRIKI MAZISHI YA DADA YAKE RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE KIJIJINI MSOGA LEO

0
0
 Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya dada yake, Marehemu Tausi Khalfani Kikwete kijijini Msoga wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani leo Jumatatu Desemba 21, 2015
  Rais John Pombe Joseph Magufuli akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya dada yake Rais Mstaafu Dkt JAkaya Kkikwete, Marehemu Tausi Khalfani Kikwete kijijini Msoga wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani leo Jumatatu Desemba 21, 2015
 Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya dada yake Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kkikwete, Marehemu Tausi Khalfani Kikwete kijijini Msoga wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani leo Jumatatu Desemba 21, 2015
 Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli, Marais Wastaafu Alhaji Ali Hassan  Mwinyi na Dkt Jakaya Mrisho Kikwete wakishiriki katika dua wakati wa wa mazishi ya dada yake Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete, Marehemu Tausi Khalfani Kikwete kijijini Msoga wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani leo Jumatatu Desemba 21, 2015

Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli na Rais Mstaafu kt Jakaya Mrisho Kikwete wakiondoka makaburini baada ya mazishi ya dada yake Rais Mstaafu Dkt JAkaya Kikwete, Marehemu Tausi Khalfani Kikwete kijijini Msoga wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani leo Jumatatu Desemba 21, 2015

PICHA NA IKULU

Asilimia 49 kati ya asilimia 100 ya uchunguzi wa DNA yaonyesha baba si mzazi halali wa mtoto

0
0
Na Beatrice Lyimo-Maelezo

Asilimia 49 kati ya asilimia 100 ya matokeo ya uchunguzi wa makosa ya vinasaba (DNA)  yanayowasilishwa katika ofisi ya Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa mwaka yanaonyesha kuwa baba si mzazi halali wa mtoto katika kesi hizo.

Hayo yamesemwa na Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa wadau wa wakala wa afya ya mazingira leo jijini Dar es Salaam.

“Kesi zinazopokelewa katika maabara yetu zinazohusu sampuli ya Vinasaba kwa mwaka zinaonyesha kuwa asilimia 49% kati ya asilimia 100% ya matokeo hayo huonyesha mzazi mmoja ambaye ni baba kuwa si mzazi halali wa mtoto huyo”.

“Vinasaba ni utambulisho wa kipekee wa kila kiumbe ambao unabeba taarifa muhimu na inayorithisha tabia au umbile fulani la mhusika. Vinasaba ni kama vile kitabu cha kumbukumbu kinachohusu maisha binafsi”, aliongeza Prof. Manyele.

Profesa Manyele aliongeza kuwa mikoa ya kanda ya Ziwa, Arusha, Dar es Salaam na Mbeya ndio inayoongoza kwa matokeo ya uchanguzi huo wa makosa ya Vinasaba nchini.

Akizungumza kuhusu lengo la mkutano huo, Profesa Manyele amesema kuwa ni kuimarisha uhusiano uliopo kati ya wadau wa kemikali na wadau wa afya ya mazingira kutoka katika halmashauri tofauti nchini pamoja na ofisi ya Mazingira.

Aidha Profesa alibainisha baadhi ya majukumu yanayofanywa na wakala wa Mkemia Mkuu wa Serikali kuwa ni kufanya uchunguzi ili kuhakiki ubora na usalama wa vyakula, dawa, maji, maji machafu, bidhaa za viwanda na mashambani, sampuli za mazingira na sampuli zinazohusiana na makosa ya jinai.

“Matokeo ya uchunguzi wa makosa ya jinai na vinasaba (DNA) huviwezesha vyombo husika kufikia maamuzi stahili na kusaidia kutendeka kwa haki katika tuhuma za kesi za jinai ikiwemo ulevi, mauaji, ubakaji, wizi wa watoto, uhalali wa mtoto kwa mzazi, kwa kupitia vyombo husika” alifafanua Profesa.

Mbali na hayo, alisema  wakala  kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inatarajia kuwasilisha mapendekezo ya kutunga sheria ya kuunda maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na Sheria ya kusimamia taaluma ya Wakemia, kuimarisha upatikanaji wa mitambo na vifaa vya maabara kila teknologia inapobadilika pamoja na kuimarisha zaidi taratibu za uchunguzi ziwe za kisasa ili kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknologia.

WANAFUNZI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (UDSM) WAHAMASISHA UTALII WA NDANI KWA VITENDO

0
0

Mnyama Ngiri akiwa amejipumzisha kwenye tope kama alivyokutwa na kamera yetu

Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) wamefanya ziara ya siku mbili ya kitalii katika hifadhi ya taifa ya Saadani pamoja na sehemu ya kihistoria ya Kaole iliyopo Bagamoyo ikiwa ni sehemu ya kujifunza pamoja na kuhamasisha utalii wa ndani.

Wanafunzi hao kutoka katika "Collage" tofauti tofauti ikiwemo utalii , uchumi na biashara waliofanya ziara hiyo ikiwa chini ya mwamvuli wa University of Dar es Salaam Tourism Association (DUTA) ,walipata fursa ya kujifunza na kushuhudia wanyama pori pamoja na sehemu ya kihistoria ya Kaole na kuhamasisha jamii hasa ya wasomi kuwa mfano wa kuigwa kwa kuzuru hifadhi pamoja na makumbusho ili kuhimiza utalii wa ndani.
Hii ni tabia ya kipekee ya ngiri ambapo hula nyasi akiwa amepiga mfano wa magoti kwa kukunja miguu ya mbele .
Waterbucks kama wanavyojulikana wakiwa miongoni mwa wanyama walioonekana wakati wa ziara hiyo.Akizungumzia ziara hiyo aliyekuwa kiongozi wa msafara huo ambaye ni mwanafunzi wa kozi ya utalii ,Gabriel Lyimo alisema huu ni muendelezo wa ziara ambazo wamekuwa wakizifanya kama sehemu ya kujifunza pamoja na kuhamasisha watanzania na hasa wanafunzi pamoja na wasomi kujenga utamaduni wa kukuza pato la taifa kwa kufanya utalii wa ndani na sio kuona kama ni jukumu la wageni.
Picha ya pamoja

Sambamba na hilo wanafunzi hao walipata fursa ya kuweka kambi pembezoni mwa mwambao wa bahari ya hindi na kutumia fursa hiyo kupata upepo mwanana , kupumzika na kuogelea.
Saadani National Park ni Hifadhi ya Taifa ya 13 ya Tanzania yenye eneo la 1,062 km za mraba ambapo watalii wanaweza kuona wanyama pamoja mwambao Bahari ya Hindi.Mbuga hii ilikuwa rasmi katika gazeti la serikali mwaka 2005, Saadani National Park ni hifadhi pekee nchini Tanzania ambayo imepakana na bahari ya Hindi.
Mtembezi na muelekezi katika hifadhi ya Saadani Bw.Mollel akifafanua jambo wakati wa ziara ndani ya hifadhi .
Baadhi ya wanafunzi wakisikiliza historia kuhusu mji huu wa Saadani huku toka kwa mwenyeji na mkongwe wa eneo hilo mzee Mlelwa (mwenye shati la kijani) wakati wa jioni .
Mambo ya Msosi: baadhi ya wanafunzi wakiwa katika harakati za kuchoma kitoweo kwa ajili ya mlo wa usiku .
Hakika anapendeza!!
wanafunzi hao wakiwa karibu na eneo ambalo maji kutoka mto wami yanakutana na maji ya bahari ya hindi
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakichagua shanga na vito vya asili walipozuru Kaole Mamba Ranch iliyopo Bagamoyo
Moja kati ya mamba wanaopatikana katika eneo la Kaole Mamba Ranch
Kwa umakini na huku wakipewa fursa ya kuuliza maswali , wakisikilza historia ya eneo la Kaole na mfululizo wa matukio ya kihistoria kutoka kwa mtaalamu wa historia Bw.Ramadhani
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakiwa mbele ya msikiti wa kwanza uliojengwa katika pwani ya Afrika ya mashariki
Kulingana na historia ya eneo hili ,inasemekana kuwa mbuyu huu umeishi zaidi ya miaka mia tano na wengi wamekuwa wakiamini kuuzunguka mbuyu huu (kutoka upande wa kushoto kwenda kulia) kunaweza kumuongezea mtu miaka ya kuishi



Picha na Dickson Mulashani wa FUNGUKA LIVE MEDIA



ORODHA YA WAUZA DAWA ZA KULEVYA HAINISADII-KITWANGA

0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kumaliza mazungumzo na Viongozi Wakuu wa Jeshi la Polisi nchini. Waziri Kitwanga aliwaambia waandishi wa habari kuwa, wamekubaliana na Viongozi Wakuu wa jeshi hilo kuweka mikakati zaidi ya kukabiliana na uhalifu nchini. Wapili kushoto meza kuu ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu. Wapili kulia meza kuu ni Naibu IGP, Abdulharam Kaniki. Kulia ni Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi hilo, Paul Chagonja. Kushoto meza kuu ni Kamishna wa Polisi Jamii nchini, Mussa Ali Mussa. Kushoto ni Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
WAZIRI wa Mambo Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga amesema njia ya kudhibiti dawa za kulevya kuingia nchini ni kuweka mfumo wa kisasa wa kudhibiti uingiaji dawa hizo, kuwa na orodha ya waingizaji wa dawa ni kazi bure kutokana na kukosa mamlaka ya kisheria.

Kitwanga ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na Maafisa Wakuu wa Jeshi la Polisi, amesema katika kukabiliana na uingizaji wa dawa za kulevya ni kuweka mfumo imara na jeshi la polisi lazima lijipange katika udhibiti huo.

Kitwanga amesema kuwa mfumo wa kiteknolijia ukiwekwa hautabagua mtu yeyote au mkubwa katika madaraka awe mdogo wakishajulikana watachukuliwa hatua za kisheria bila kuangaliwa nafasi walizo nazo.

“Orodha ya wauza unga ukiwanayo haitasaidia na kufanya hivyo ni kuhisi, lakini huna sheria ya kuweza kuwabana katika orodha hiyo” amesema Kitwanga.

Kitwanga amesema kuwa katika mambo waliyojpanga nayo na jeshi la polis ni kuhakikisha wanaimarisha ulinzi katika bandari ili kuweza kudhibiti utoroshaji wa vitu mbalimbali ambavyo vinatoka bila utaratibu.

Hata hivyo amewataka polisi watu washitakiwe kwa kesi walizo nazo na sio kuwabambikia watu wasio na hatia kusababisha kufungwa kwa kesi zisizowahusu.

Kitwanga amesema utoroshaji wa madini,jeshi la polisi haliwahusu wakihitajika na Wizara ya Nishati na Madini watafanya hivyo katika kukabiliana na utoshaji huo.

Aidha amesema kati ya askari 45,000 ni askari 10,000 ndio wenye makazi hivyo wanatarajia kujenga nyumba 5000 ikiwa nia nia askari wote kukaa katika makambi ni rahisi kuweza kuhitajika kwa muda wowote.

RASI DK MAGUFULI AKUTANA NA MAALIM SEIF IKULU JIJINI DAR LEO

0
0

MWAKILISHI MKAZI WA UNHCR AMTEMBELEA WAZIRI KITWANGA OFISINI KWAKE, JIJINI DAR ES SALAAM LEO

0
0
742
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Joyce Mends-Cole (wapili kushoto) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati), kuhusu masuala mbalimbali ya Wakimbizi. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Kitwanga, jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke, na kushoto ni Naibu Mwakilishi Mkazi wa UNHCR, Robert Tibagwa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
741
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Joyce Mends-Cole, kuhusu masuala mbalimbali ya Wakimbizi. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Kitwanga, jijini Dar es Salaam leo.  Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
743
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akimkaribisha ofisini kwake Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Joyce Mends-Cole, kwa ajili ya kufanya naye mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya Wakimbizi nchini.  Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
744
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (wapili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Joyce Mends-Cole (wapili kushoto),  Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke (kulia) na Naibu Mwakilishi Mkazi wa UNHCR, Robert Tibagwa. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Dkt Magufuli Mgeni Rasmi Mkesha wa kuiombea amani Tanzania

0
0


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Makanisa ya Kipentekoste (Tanzania  Fellowship of Churches) Askofu Godfrey Malassy (kushoto) akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo 22 Desemba, katika Ukumbi wa Idara ya Habari jijini Dar es Salaam kuhusu maandalizi ya Mkesha Mkubwa wa Kitaifa wa kuliombea Taifa pamoja na dua maaum ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli ambaye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika dua hiyo. Kulia ni Mwanakamati wa Jumuiya hiyo, Mchungaji Olivia Mallonga.

………………………………………………………………………………………….
Na Shamimu Nyaki MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkesha mkubwa wa kuiombea amani Tanzania utakaofanyika Disemba 31 mwaka huu katika uwanja wa Taifa. 

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Makanisa ya Pentekoste (TFC) Godfrey Malassy alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijin Dar es Salaam, na kuthibitisha kuwa maandalizi yote yamekamilika ikiwemo kibali kutoka polisi, pamoja washiriki mbalimbali watakaoshiriki katika mkesha huo. 

Askofu Malassy ameongeza kuwa mkesha huo utakuwa ni kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa kuijalia nchi yetu kumaliza Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi Oktoba mwaka huu kwa amani na utulivu,pamoja na Dua maalum ya kumuombea Mhe. Rais afya njema na utendaji mzuri anaoendelea kuufanya kwa maendeleo ya Taifa letu kwa kuwa mara zote amesisitiza kufanyiwa maombi na watanzania. 

“Tutatumia nafasi hiyo kumuombea Mhe.Rais katika kutekeleza jukumu kubwa alilokabidhiwa na watanzania kuongoza Taifa letu ili aweze kufanikiwa katika hilo.”Alisema Askofu Malassy. Aidha Mwenyekiti huyo amewataka wananchi wote kutumia siku hiyo kumuomba na kumshukuru Mungu kwa amani iliyopo nchini kwa vile ndio msingi mkubwa wa shughuli za kila siku zinazosaidia kupata kipato na maendeleo ya Taifa kwa ujumla. 

Naye Mch.Olivia Mallonga ambaye ni mjumbe katika kamati ya maandalizi ya Mkesha huo amesema kwamba wao kama wadau wanaendeleza desturi ya kuliombea Taifa amani ili lisije kutumbukia kwenye machafuko kama nchi nyingine . 

“Watanzania wana dini ndio maana wanatumia imani zao kufanya maombi ili Mungu awalinde na maovu au machafuko yanayoweza kutokea kutokana na sababu yoyote.”Aliongeza Mch. Olivia. Mkesha huo ni wa 17 tangu ulipoanza kufanyika Tanzania na umeleta mafanikio makubwa ikiwemo kuunganisha watanzania bila kujali imani zao.

Malkia wa Kombe la Muungano Timu ya Uhamiaji Yaifunga JKU Kwa 38-- 25

0
0
    
 Mrajisi wa Vyama vya Michezo Zanzibar akimkabidhi Kombe la Ubingwa wa Michuano ya Muungano Kepteni wa Timu ya Uhamiaji Sofia Komba Baada ya Timu yao kulinyakuwa Kombe hilo Mwaka huu katika Uwanja wa Gmykhana Zanzibar kwa kuifunga Timu ya JKU ya Zanzibar kwa mabao 38---25 












Kipindi cha Jukwaa Langu Dec 21 2015 (FULL)

0
0
Kipindi hiki hukujia kila jumatatu kuanzia saa 11 jioni kwa saa za Marekani ya Mashariki kuijadili Tanzania ya sasa na ile tuitakayo.
Kuna mengi tuliyogusia pamoja na wasikilizaji wetu
KARIBU
 

WAHITIMU WA VYUO VIKUU NCHINI WATAKIWA KUMSAIDIA RAIS DOKTA MAGUFULI KUPAMBANA NA UFISADI-DR.WALUKANI.

0
0
wal1
Proffessa,John Adamson Mwakilima akitunuku Shahadaya Udaktari na Uzamivu wa Falsafa katika Maswala ya Uongozi kutoka Chuo cha New Life Bible College and Seminary USA chenye tawi lake Kata ya Mlandizi mkoani hapa mhitimu Walukani Luhamba ambaye ni Ofisa Mfawidhi wa Sumatra Mkoa wa Tanga juzi.
wal2
Dr.Walukani Luhamba akipongezwa na Familia yake marabaada ya kutunukiwa Shahada ya Udaktari na Uzamivu wa Falsafa katikamaswala ya Uongozi kutoka Chuo cha New Life Bible College and SeminaryUSA chenye tawi lake Kata ya Mlandizi Mkoani Pwani juzi.

………………………………………………………………………………….
NA MWANDISHI WETU,PWANI.
 WAHITIMU wanaomaliza vyuo vikuu hapa nchini wametakiwa kumsaidia RaisJohn Magufuli kupambana na rushwa, ufisadi uliokithiri kwa kuhakikishahawajihusishi na masuala hayo katika maisha yao ikiwemo kutumiataalumu walizozipata kujipatia maendeleo wao na jamii zinazowazunguka.

Ushauri huo ulitolewa juzi na Mhitimu wa Shahada ya Udaktari naUzamivu wa Falsafa katika Maswala ya Uongozi kutoka Chuo cha New LifeBible College and Seminary USA chenye tawi lake Kata ya Mlandizimkoani hapa Walukani Luhamba mara baada ya kutunikiwa cheti chakuhitimu kwenye mafalali iliyofanyika mjini hapa.

Alisema kuwa wahitimu hao wanaweza kutumia vizuri taaluma zaowalizozipata kuhakikisha wanazitumikia jamii zao ikiwemo kuwa wabunikatika kujipatia vipato halali ambavyo vinaweza kuwasaidia kwenyekukabiliana na maisha badala ya kusubiriwa kuajiriwa.

Dokta Luhamba  alisema wahitimu hao wanapaswa kutambua wao wanafursakubwa ya kuibadilisha jamii ili waweze kuondokana na masuala ya jamiitegemezi badala yake watumia nafasi walizonazo katika kujileteamaendeleo.

 “Nchi yetu ina rasilimali nyingi sana ambazo zinaweza kutumika vizurikatika kuhakikisha wanajiletea maendeleo hivyo viongozi waliopewadhamana na wananchi waangalie alama za nyakati na wafanya kazi kwauadilifu mkubwa kama serikali ya sasa inavyofanya shughuli zake chiniya Rais Dr. Magufuli “Alisema Luhamba

Aidha aliwataka kuwa mabalozi wazuri kwa kufanya kazi zao kwa uadilifuna hekima kubwa ili kuchochea kazi ya ukuaji wa uchumi kwao na nchikwa ujumla sambamba na kusaidia serikali kukabiliana na wabadhirifu wamali za umma.

   “Lakini pia tuhakikisha tunakuwa mstari wa mbele kupiga vita rushwana kumuombea Rais wetu Magufuli ili mungu aweze kumtia nguvu za kuwezakutekeleza kazi zake nzuri alizozianza kwa ueledi mkubwa na ufanisikatika kulipatia maendeleo Taifa letu “Alisema Walukani.

Katika mahafali hayo zadi ya  wahitimu 30 walitunukiwa vyeti na mgenirasmi ambaye alikuwa ni Proffesa John Adamson Mwakilima lakini kwaupande wa Shahada ya Udaktari na Uzamivu wa Falsafa katika Maswala yaUongozi walikuwa wahitimu wawili akiwemo Ofisa Mfawidhi wa Mamlaka yaUsimamizi wa Usafiri wa nchi kavu na Majini (Sumatra) Mkoa,Dr.WalukaniLuhamba.

Proffesa Mwakilima aliwataka wahitimu hao kuhakikisha wanakuwamabalozi wazuri katika jamii zao kwa kutumia vizuri taalumawalizozipata katika kuinua uchumi wao na wananchi wanaowazunguka.

KOMBE LA FA KUENDELEA LEO

0
0
Michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) mzunguko wa pili unaendelea leo kwa mchezo mmoja kuchezwa mmoja katika uwanja wa Majimaji mjini Songea kati ya JKT Mlale dhidi ya Mighty Elephant.

Kesho Jumatano kutakua na michezo miwili, Kariakoo ya Lindi watawakaribisha Mshikamano FC katika uwanja wa Ilulu – Lindi, Disemba 24 Njombe Mji watakua wenyeji wa Green Warriors katika uwanja wa Sabasaba mjini Njombe, na Pamba FC watacheza dhidi ya Alliance uwanja wa CCM Kirumba.

Ijumaa siku ya sikukuu ya Krisamsi Lipuli FC watawakaribisha Kurugenzi katika uwanja wa Wambi Mafinga.

Mzunguko huo wa pili unatarajiwa kumalizika Disemba 29 mwaka huu kwa michezo minne, Wenda FC v Kimondo (Sokoine), Mji Mkuu (CDA) v Singida United (Jamhuri), Mvuvuma v JKT Kanembwa (Tanganyika), Abajalo FC v Villa Squad (Karume)

Timu saba za Ashanti United, Burkinafaso, Geita Gold, Friends Rangers, Madini FCM, Panone na Rhino Rangers zimeshakata tiketi ya kucheza mzunguko wa tatu wa Kombe la FA mwezi Januari 2016, pamoja na timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom.


Bingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) ataiwakilisha Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF CC) mwaka 2017.

VYAKULA VINAVYOONGOZA KUONGEZA AKILI KWENYE UBONGO

0
0
Samaki na Mafuta ya samaki ambayo ni muhimu katika mwili

Pilipili kali 

Brokali

Nyanya 
‪#‎AfyaYako‬ Vyakula Vinavyoongoza kuongeza AKILI kwenye ubongo
Ifuatayo ni orodha ya vyakula ambavyo vinaongoza kwa kuimarisha utendaji kazi mzuri wa ubongo:

1.MAFUTA YA SAMAKI

Samaki na Mafuta ya samaki ambayo ni muhimu katika mwili

Mafuta ya samaki ni muhimu kwa ubongo na mfumo wa ufahamu. Ulaji wa samaki wenye minofu kama samoni (salmon) na dagaa, utaweza kupata faida hizo kwa sababu aina hii ya samaki ina kiasi kingi cha mafuta ya Omega 3 ambayo huimarisha utendaji kazi na mawasiliano kati ya ubongo na seli za mwili moja kwa moja.
2.PILIPILI KALI
Pilipili kali 

Pilipili kali nayo huwa ni chakula kikubwa cha ubongo kwa sababu ina kiwango kingi cha Vitamin C ambayo huhitajika zaidi kwenye ubongo, pilipili inaaminika kuwa na kiwango kingi cha vitamin hiyo kuliko hata machungwa.
3.MBEGU ZA MABOGA
Mbegu za maboga zina kiwango kingi cha madini ya ‘Zinc’ ambayo husadia kuongeza kumbukumbu (memory). Kuna njia nyingi za kula mbegu za maboga, moja wapo ni kuzikaanga na kula kama karanga, ukila kiasi cha kiganja kimoja kwa siku, inakuwa poa.
4.NYANYA
Nyanya 
Nyanya ni muhimu sana kwa sababu huzuia magonjwa ya ubongo (brain disease) kutokana na kuwa na kirutubisho aina ya ‘Lycopene’ chenye uwezo wa kuzuia magonjwa nyemelezi yanayoweza kutokea. Hivyo ulaji wa nyanya utakusaidia kukupa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali, yakiwemo ya akili.
5. BROKOLI
Brokali



#‎AfyaYako‬ Vyakula Vinavyoongoza kuongeza AKILI kwenye ubongo
Ifuatayo ni orodha ya vyakula ambavyo vinaongoza kwa kuimarisha utendaji kazi mzuri wa ubongo:
1.MAFUTA YA SAMAKI
Mafuta ya samaki ni muhimu kwa ubongo na mfumo wa ufahamu. Ulaji wa samaki wenye minofu kama samoni (salmon) na dagaa, utaweza kupata faida hizo kwa sababu aina hii ya samaki ina kiasi kingi cha mafuta ya Omega 3 ambayo huimarisha utendaji kazi na mawasiliano kati ya ubongo na seli za mwili moja kwa moja.
2.PILIPILI KALI.
Pilipili kali nayo huwa ni chakula kikubwa cha ubongo kwa sababu ina kiwango kingi cha Vitamin C ambayo huhitajika zaidi kwenye ubongo, pilipili inaaminika kuwa na kiwango kingi cha vitamin hiyo kuliko hata machungwa.
3.MBEGU ZA MABOGA
Mbegu za maboga zina kiwango kingi cha madini ya ‘Zinc’ ambayo husadia kuongeza kumbukumbu (memory). Kuna njia nyingi za kula mbegu za maboga, moja wapo ni kuzikaanga na kula kama karanga, ukila kiasi cha kiganja kimoja kwa siku, inakuwa poa.
4.NYANYA
Nyanya ni muhimu sana kwa sababu huzuia magonjwa ya ubongo (brain disease) kutokana na kuwa na kirutubisho aina ya ‘Lycopene’ chenye uwezo wa kuzuia magonjwa nyemelezi yanayoweza kutokea. Hivyo ulaji wa nyanya utakusaidia kukupa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali, yakiwemo ya akili.
5. BROKOLI
Brokoli ni mboga ya majani aina fulani kama maua ya maboga, ambayo nayo inafaida sana kwenye ubongo, ina vitamin K, C na inatoa kinga ya mwili. Vitamin K inahusika moja kwa moja na utendaji kazi mzuri wa ubongo na husaidia kuzuia magonjwa yatokanayo na uzee.
6.KARANGA
Aina zote za karanga zina vitamin E, ambayo huzuia tatizo la upotevu wa kumbukumbu na pia zina mafuta yenye afya yanayohitajika mwilini.
7.MAYAI
Mwisho ni mayai ya kuku, ambayo yana kirutubisho aina ya Choline. Kirutubisho hiki huzalishwa mwilini kwa kiwango kidogo tu, hivyo kwa kula mayai (ya kienyeji) utaweza kuongeza kiwango cha kirutubisho hicho mwilini kwa kiwango kikubwa na hivyo kuimarisha afya ya ubongo.CHANZO CRI SWAHILI
Brokoli ni mboga ya majani aina fulani kama maua ya maboga, ambayo nayo inafaida sana kwenye ubongo, ina vitamin K, C na inatoa kinga ya mwili. Vitamin K inahusika moja kwa moja na utendaji kazi mzuri wa ubongo na husaidia kuzuia magonjwa yatokanayo na uzee.
6.KARANGA
Aina zote za karanga zina vitamin E, ambayo huzuia tatizo la upotevu wa kumbukumbu na pia zina mafuta yenye afya yanayohitajika mwilini.
7.MAYAI
Mwisho ni mayai ya kuku, ambayo yana kirutubisho aina ya Choline. Kirutubisho hiki huzalishwa mwilini kwa kiwango kidogo tu, hivyo kwa kula mayai (ya kienyeji) utaweza kuongeza kiwango cha kirutubisho hicho mwilini kwa kiwango kikubwa na hivyo kuimarisha afya ya ubongo.CHANZO CRI SWAHILI.

KIGWANGWALLA ATEMBELEA UJENZI WA HOSPITALI YA RUFAA KANDA YA KUSINI

0
0
01
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Ligula ya mkoa wa Mtwara, Dkt. Shaibu Maarifa (katikati) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla (kushoto) alipotembelea eneo la Mikindani inapojengwa hospitali ya mpya ya kanda ya kusini, mkoani Mtwara.
02
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akimuuliza swali Mganga Mkuu wa Hospitali ya Ligula ya mkoa wa Mtwara Dkt. Shaibu Maarifa (katikati) wakiwa eneo la Mikindani inapojengwa hospitali ya mpya ya kanda ya kusini, mkoani Mtwara.
IMG_9637
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Ligula ya mkoa wa Mtwara, Dkt. Shaibu Maarifa (kushoto) inapojengwa hospitali ya mpya ya kanda ya kusini inayojengwa eneo la Mikindani mkoani Mtwara.
03
05
Muonekano wa moja ya majengo ya Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini itakayohudumia mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma inayojengwa eneo la Mikindani mkoani Mtwara.(Picha na Eleuteri Mangi- MAELEZO).


Na Mwandishi wetu, Mtwara
UJENZI wa hospitali ya rufaa Kanda ya Kusini, unaofanyika mkoani Mtwara sasa upo katika majengo ya wagonjwa wa nje (OPD).

Ujenzi huo ulioanza mwaka 2009 kwa kusafishwa kwa eneo na kujengwa kwa uzio wa kilomita 2.7 mwaka 2011 kwa gharama ya shilingi milioni 840 na kuanza kujengwa kwa majengo ya OPD mwaka 2013 umelenga kuwezesha mikoa ya Kusini kuwa na hospitali kubwa yenye hadhi ya kisasa.

Akisoma taarifa ya maendeleo ya ujenzi kwa Naibu Waziri katika wWizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Dkt. Hamisi Kigwangalla, Mganga Mkuu wa mkoa wa Mtwara alisema kwamba ujenzi wa mapokezi umetarajiwa kutumia shbilioni 4.8 na hadi sasa wametumia bilioni 1.8
Mganga huyo alisema mradi mzima unatarajiwa kujengwa kwa bilioni 78.

Alisema kuchelewa kuendelea japo sasa wana ghorofa 2 zilizoezekwa na wanapiga ripu kunatokana na upatikanaji wa fedha kutoka serikali kuu.
Alisema hospitali hiyo ni muhimu sana kukamilika kutokana na kukua kwa uchumi wa Mtwara na mikoa jirani na pia kuwapo kwa uhitaji kwa mikoa ya kaskazini mwa nchi jirani.

Naye Naibu Waziri Kigwangwalla alisema kwamba ni matumaini yake kuwa hospitali hiyo itakamilika mapema na kubakiza changamoto za matumizi ya wananchi kutoka nchi jirani ambao kwa sasa wanafaidika sana na hospitali ya Ligula.

Alisema wataalamu wanatakiwa kuangalia hali hiyo ili kuwepo na matumizi sahihi ya miundombinu hiyo iliyolenga kufaidisha wananchi wa Tanzania.
Aidha akiwa Mtwara Naibu Waziri huyo aliendelea kusisitiza watumishi wote kuwajibika na kuwahi maeneo yao ya kazi.

Alisema watumishi wa umma wanaofikia laki nne wamepata nafasi adimu ya kuutumikia umma wa watu takribani milioni 50 na hivyo ni lazima waheshimu watanzania kwa kuwatumikia ipasavyo.Alisema wao waliomba nafasi ya kuhudumia watanzania kwa hiyo ni lazima wawahudumie watanzania na kila mmoja katika kitengo chake ni lazima kuhakikisha watumishi wanafanya kile walichoahidi katika mikataba yao.

IGWUTA WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA KAZI ZAKE

0
0
Na Zainabu Hamis wa Globu ya Jami.
CHAMA cha wafanyakazi wa viwanda na sekta mbalimbali(IGWUTA) champongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Joseph Magufuli (Pichani)kwa namna na jinsi anavyofanya kazi yake hasa ile ya kupambana na mafisadi na wanafiki.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Katibu Mkuu wa chama chama cha IGWUTA, Michael Kashamba amesema kuwa,Wamefurahishwa kwa  kumpata Rais Magufuli na wanatoa wito kwa Wafanyakazi wote hapa nchini kujitokeza na kumuunga mkono Rais wetu katika mapambano dhidi ya ufisadi.

Aidha Kashamba ametoa tamko la kumpongeza Magufuli kuwa ni kiongozi asiyekuwa wa kawaida, Hana ubinafsi na anaweka maslahi ya nchi mbele huku akimfananisha kwa utendaji wa kazi zake ni kama Rais wa awamu ya kwanza Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Pia Kashamba amesema kuwa, Chama chao kinatoa huduma ya kuelimisha na kuhamasisha wanachama kutimiza wajibu wao wa kufanya kazi kwa bidii, nidhamu na uaminifu mkubwa.

Pia IGWUTA inatoa Huduma za utetezi kwa Wanachama dhidi ya uonevu wowote uliofanywa na baadhi ya waajiri hapa nchini.
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live




Latest Images