Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46371 articles
Browse latest View live

MWANANYAMALA HOSPITAL RECEIVES ASSISTANCE FROM AAR ON WORLD MALARIA DAY

$
0
0
 AAR Health Care Managing Director,Dr.Kandie Ng'ochoch handling bedsheets to the Mwanananyamala Acting Chief Doctor Kariamel John Wandi.
========  =======  =====

MWANANYAMALA HOSPITAL RECEIVES ASSISTANCE FROM AAR ON WORLD MALARIA DAY

AAR Tanzania Company Limited today has provided 92 mosquito nets and 42 Bed sheets worth 1.3 Million to Pediatric and Maternity block in Mwananyamala Hospital Dar-es-salaam as the way of showing support to the Society on World Malaria Day.

Speaking during the handling of the assistance, the AAR Insurance Marketing Manager, Tabia Massudi said “The Company is being operated with ethics and integrity. Being responsible to the community is one of the ethical activities that AAR Company would want to embrace. That is why AAR Insurance and Health Centers have collaborated and seen the need to provide this kind of assistance on this particular day”.

Malaria is one of the Major Challenges in the country and as one of the Major contributors in health services in Tanzania, it is our responsibility to show concern to infants and mothers who are mostly affected by the disease concluded Mrs. Massudi.

The assistance went along with the AAR Team, visiting Pediatric and Maternity Block in Mwananyamala hospital.

“We appreciate the concern AAR Company has shown today as the assistance has come at the right time when we are still facing a lot of challenges, one of them being insufficient equipments , I would like to urge other companies, organizations and the government as well  to continue support Mwanayamala hospital  as  we depend on them for sustainability of our operations”. Said the Acting Chief Doctor, Kariamel John Wandi when receiving the assistance.

 AAR Health Care Managing Director,Dr.Kandie Ng'ochoch handling mosquito nets to the Mwanananyamala Acting Chief Doctor Kariamel John Wandi
 AAR Insurance Marketing Manager Tabia Massudi expressing to the press why AAR has decided to Provide the assistance to Mwanananyamala hospital Acting
 AAR Insurance Marketing Manager Tabia Massudi handling the assistance to the Mwanananyamala Acting Chief Doctor Kariamel John Wandi.
 AAR Team having a group photo with Mwanananyamala Acting Chief Doctor Kariamel John Wandi during the provision of assitance on World Malaria Day
AR Insurance Marketing Manager Tabia Massudi on her right is AAR Health Care Managing Director Dr.Kandie Ng'ochoch showing support to the patients when visiting Mwanayamala Hospital on World Malaria Day.

walioteuliwa kwenye kinyang'anyiro cha tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013 hawa hapa.

$
0
0
Photo: Majina ya wasanii, waandaaji muziki na vikundi kwa ajili ya tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013   WIMBO BORA WA MWAKA    Dear God - Kala Jeremiah  Leka dutigite - Kigoma all star  Mapito - Mwasiti Feat Ally Nipishe  Me n U - Ommy Dimpoz Feat Vanessa Mdee  Pete- Ben pol   MSANII BORA WA KIUME   Ben Pol   Diamond   Linex   Mzee Yusuf   Ommy Dimpoz    MSANII BORA WA KIKE   Isha Mashauzi   Khadija Kopa   Lady Jaydee   Mwasiti   Recho        MSANII BORA WA KIKE - TAARAB   Isha Mashauzi   Khadija Kopa   Khadija Yusuph   Leila Rashid  MSANII BORA WA KIUME - TAARAB Ahmed Mgeni   Hashim Said   Mzee Yusuf    MSANII BORA WA KIUME - BONGO FLAVA     Ally Kiba   Ben Pol   Diamond   Linex   Ommy Dimpoz    MSANII BORA WA KIKE - BONGO FLAVA  Linah   Mwasiti   Recho   Shaa       MSANII BORA WA HIP HOP     Fid Q  Joh Makini Kala Jeremiah Profesa J Stamina  9. Msanii Bora wa Kiume - Bendi   Chalz Baba    Dogo Rama    Greyson Semsekwa    Jose Mara    Khaleed Chokoraa     Msanii Bora wa Kike - Bendi    Anneth Kushaba    Luiza Mbutu    Mary Lucos    Vumilia     Msanii Bora anayechipukia    Ali Nipishe    Angel    Bonge la Nyau    Mirror    Vanessa Mdee     Video Bora ya Wimbo ya Mwaka    Baadae - Ommy Dimpoz  Kamili gado - Professor J Feat Marco Chali  Marry Me - Rich Mavoko  Nichum - Bob Junior  Party Zone  - AY Feat Marco Chali  Mtunzi Bora wa Mashahiri - Taarab  Ahmed Mgeni   Hemed Omary   Khadija Kopa   Mzee Yusuf   Thabit Abdul    Mtunzi Bora wa Mashahiri - Bongo Flava  Ally Kiba   Barnaba   Ben Pol   Linex   Ommy Dimpoz    Mtunzi Bora wa Mashahiri - Hip Hop  Fid Q   Joh Makini   Kala Jeremiah   Mwana Fa   Stamina    Mtunzi Bora wa  Mashahiri - Bendi  Chalz Baba   Grayson Semsekwa   Jonico Flower   Jose Mara   Khaleed Chokoraa   Mtayarishaji Bora wa Mwaka - Muziki wa Kizazi Kipya  Bob Junior  Ima the boy  Man Water  Maneke  Marco chali  Mensen Selecta  Mtayarishaji wa Wimbo wa Mwaka - Taarab  Bakunde  Enrico   Mtayarishaji wa Wimbo wa Mwaka - Bendi  Allan Mapigo Amoroso  Mtayarishaji Chipukizi wa Mwaka  Imma the Boy Mensen Selecta Mr T Touch Sheddy Clever  Rappa Bora wa Bendi    Fagasoni    Greyson Semsekwa    J4    Jonico Flower    Sauti ya Radi         Wimbo wenye vionjo vya asili    Aambiwe - offside trick  Atatamani - AT  Boma la utete - Young D  Chocheeni kuni - Mrisho Mpoto Feat Ditto  Mdundiko - Momba Feat Juma Nature   Wimbo Bora wa Bendi    Chanzo ni sisi - Mapacha watatu  Jinamizi la Talaka - Mlimani Park Orchestra  Risasi kidole - Mashujaa band  Shamba la twanga - African Stars band       Wimbo Bora wa Reggae    Hii si ya waoga - Yuzzo  Kilimanjaro - Warriors from The East  NATAFUTA PARADISE  - Mac Malick Simba  Salvation - Delayla Princess  Tunda - Hardmad   Wimbo Bora wa Africa Mashariki   Fresh All Day - Camp Mulla  Make you dance - Keko Feat Madtrax  Maswali ya polisi - DNA  Still a Liar - Wahu  Valu Valu - Jose Chameleone   Wimbo Bora wa - Bongo Pop   Aifola - Linex Feat fundi Samweli  Baadae - Ommy Dimpoz Feat Angel  Chuki Bure - Sharo  Milionea Feat Dully Sykes  Marry Me - Rich Mavoko  Me and you - Ommy Dimpoz Feat Vanessa Mdee    Wimbo Bora wa Kushirikiana/kushirikishwa  Chuki Bure - Sharo Millionea Feat Dully Sykes  Mapito - Mwasiti Feat Ally Nipishe  Me and U - Ommy Dimpoz Feat Vanessa Mdee  Sihitaji marafiki - Fid Q Feat Yvonne  Single Boy - Alikiba Feat Lady Jaydee     Wimbo Bora wa Hip Hop    Alisema - Stamina Feat Jux  Bum kubam - Nikki wa Pili Feat G Nako  Dear God - Kala Jeremiah  Nasema Nao - Nay wa Mitego  Sihitaji Marafiki - FID Q Feat Yvonne  Wimbo Bora wa RnB  Amerudi - Belle 9 Kuwa na Subira - Rama Dee Feat Mapacha Maneno maneno  - Ben Pol Pete - Ben Pol   Wimbo Bora wa Ragga/ Dancehall   Je ni nani - Ras Six Muda upite - Susu Man Predator - Dabo Push Dem - Dr Jahson Take it down - Chibwa and Tanah  Wimbo Bora wa Taarab  Mjini chuo kikuu - Khadija Kopa Mpenzi chocolate - Jahazi [Mzee Yusuph] Si bure una mapungufu - Isha Mashauzi [Mashauzi Classic] Sina muda huo - Jahazi [Leila Rashid] Siwasujudii Viwavi jeshi -Isha Mashauzi [Mashauzi Classic]   Wimbo Bora wa Zouk/Rhumba   Gubegube -Barnaba Mapito - Mwasiti Feat Ally Nipishe Nashukuru umerudi - Recho Ni wewe - Amini Sorry  - Barnaba  Bendi Bora ya Mwaka CD1 African Stars Band  Mapacha wa tatu  Mashujaa Band Mlimani Park Orchestra [Sikinde]  Msondo Ngoma Music band  Kikundi Bora cha Taarab  Dar modern Taarab   Five stars modern Taarab   Jahazi Modern Taarab   Kings modern Taarab   Mashauzi Classic        Kikundi Bora cha Muziki wa Kizazi Kipya   Jambo squad Makomando Tip Top Connection Tmk wanaume family Weusi 

Mratibu wa tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013,kutoka BASATA Bwa.Luhala akitangaza majina ya walioteuliwa kuingia kwenye mchakato wa tuzo hizo zinazotarajiwa kufanyika Juni 8 2013,pale Mlimani City jijini Dar.

WIMBO BORA WA MWAKA 

Dear God - Kala Jeremiah 
Leka dutigite - Kigoma all star 
Mapito - Mwasiti Feat Ally Nipishe 
Me n U - Ommy Dimpoz Feat Vanessa Mdee 
Pete- Ben pol 

MSANII BORA WA KIUME 
Ben Pol 
Diamond 
Linex 
Mzee Yusuf 
Ommy Dimpoz 

MSANII BORA WA KIKE 
Isha Mashauzi 
Khadija Kopa 
Lady Jaydee 
Mwasiti 
Recho 

MSANII BORA WA KIKE - TAARAB 
Isha Mashauzi 
Khadija Kopa 
Khadija Yusuph 
Leila Rashid

MSANII BORA WA KIUME - TAARAB
Ahmed Mgeni 
Hashim Said 
Mzee Yusuf 

MSANII BORA WA KIUME - BONGO FLAVA 

Ally Kiba 
Ben Pol 
Diamond 
Linex 
Ommy Dimpoz 

MSANII BORA WA KIKE - BONGO FLAVA 
Linah 
Mwasiti 
Recho 
Shaa 

MSANII BORA WA HIP HOP 

Fid Q 
Joh Makini
Kala Jeremiah
Profesa J
Stamina


 Msanii Bora wa Kiume - Bendi 
Chalz Baba 
Dogo Rama 
Greyson Semsekwa 
Jose Mara 
Khaleed Chokoraa 

Msanii Bora wa Kike - Bendi 

Anneth Kushaba 
Luiza Mbutu 
Mary Lucos 
Vumilia 

Msanii Bora anayechipukia

Ali Nipishe 
Angel 
Bonge la Nyau 
Mirror 
Vanessa Mdee 

Video Bora ya Wimbo ya Mwaka 

Baadae - Ommy Dimpoz 
Kamili gado - Professor J Feat Marco Chali 
Marry Me - Rich Mavoko 
Nichum - Bob Junior 
Party Zone - AY Feat Marco Chali

Mtunzi Bora wa Mashahiri - Taarab

Ahmed Mgeni 
Hemed Omary 
Khadija Kopa 
Mzee Yusuf 
Thabit Abdul 

Mtunzi Bora wa Mashahiri - Bongo Flava

Ally Kiba 
Barnaba 
Ben Pol 
Linex 
Ommy Dimpoz 

Mtunzi Bora wa Mashahiri - Hip Hop

Fid Q 
Joh Makini 
Kala Jeremiah 
Mwana Fa 
Stamina

Mtunzi Bora wa Mashahiri - Bendi

Chalz Baba 
Grayson Semsekwa 
Jonico Flower 
Jose Mara 
Khaleed Chokoraa

Mtayarishaji Bora wa Mwaka - Muziki wa Kizazi Kipya

Bob Junior 
Ima the boy 
Man Water 
Maneke 
Marco chali 
Mensen Selecta

Mtayarishaji wa Wimbo wa Mwaka - Taarab

Bakunde 
Enrico 

Mtayarishaji wa Wimbo wa Mwaka - Bendi

Allan Mapigo
Amoroso

Mtayarishaji Chipukizi wa Mwaka

Imma the Boy
Mensen Selecta
Mr T Touch
Sheddy Clever

Rappa Bora wa Bendi 

Fagasoni 
Greyson Semsekwa 
J4 
Jonico Flower 
Sauti ya Radi 

Wimbo wenye vionjo vya asili

Aambiwe - offside trick 
Atatamani - AT 
Boma la utete - Young D 
Chocheeni kuni - Mrisho Mpoto Feat Ditto 
Mdundiko - Momba Feat Juma Nature

Wimbo Bora wa Bendi 

Chanzo ni sisi - Mapacha watatu 
Jinamizi la Talaka - Mlimani Park Orchestra 
Risasi kidole - Mashujaa band 
Shamba la twanga - African Stars band 

Wimbo Bora wa Reggae 

Hii si ya waoga - Yuzzo 
Kilimanjaro - Warriors from The East 
NATAFUTA PARADISE - Mac Malick Simba 
Salvation - Delayla Princess 
Tunda - Hardmad 

Wimbo Bora wa Africa Mashariki 

Fresh All Day - Camp Mulla 
Make you dance - Keko Feat Madtrax 
Maswali ya polisi - DNA 
Still a Liar - Wahu 
Valu Valu - Jose Chameleone 

Wimbo Bora wa - Bongo Pop 

Aifola - Linex Feat fundi Samweli 
Baadae - Ommy Dimpoz Feat Angel 
Chuki Bure - Sharo Milionea Feat Dully Sykes 
Marry Me - Rich Mavoko 
Me and you - Ommy Dimpoz Feat Vanessa Mdee 

Wimbo Bora wa Kushirikiana/kushirikishwa

Chuki Bure - Sharo Millionea Feat Dully Sykes 
Mapito - Mwasiti Feat Ally Nipishe 
Me and U - Ommy Dimpoz Feat Vanessa Mdee 
Sihitaji marafiki - Fid Q Feat Yvonne 
Single Boy - Alikiba Feat Lady Jaydee 


Wimbo Bora wa Hip Hop

Alisema - Stamina Feat Jux 
Bum kubam - Nikki wa Pili Feat G Nako 
Dear God - Kala Jeremiah 
Nasema Nao - Nay wa Mitego 
Sihitaji Marafiki - FID Q Feat Yvonne

Wimbo Bora wa RnB

Amerudi - Belle 9
Kuwa na Subira - Rama Dee Feat Mapacha
Maneno maneno - Ben Pol
Pete - Ben Pol

Wimbo Bora wa Ragga/ Dancehall 

Je ni nani - Ras Six
Muda upite - Susu Man
Predator - Dabo
Push Dem - Dr Jahson
Take it down - Chibwa and Tanah

Wimbo Bora wa Taarab

Mjini chuo kikuu - Khadija Kopa
Mpenzi chocolate - Jahazi [Mzee Yusuph]
Si bure una mapungufu - Isha Mashauzi [Mashauzi Classic]
Sina muda huo - Jahazi [Leila Rashid]
Siwasujudii Viwavi jeshi -Isha Mashauzi [Mashauzi Classic]

Wimbo Bora wa Zouk/Rhumba 

Gubegube -Barnaba
Mapito - Mwasiti Feat Ally Nipishe
Nashukuru umerudi - Recho
Ni wewe - Amini
Sorry - Barnaba

Bendi Bora ya Mwaka CD1 African Stars Band

Mapacha wa tatu 
Mashujaa Band
Mlimani Park Orchestra [Sikinde] 
Msondo Ngoma Music band

Kikundi Bora cha Taarab

Dar modern Taarab 
Five stars modern Taarab 
Jahazi Modern Taarab 
Kings modern Taarab 
Mashauzi Classic 

Kikundi Bora cha Muziki wa Kizazi Kipya 

Jambo squad
Makomando
Tip Top Connection
Tmk wanaume family
Weusi

Watanzania Ujerumani kusherekea miaka 49 ya Muungano,Mjini Kolon

$
0
0

Mhe.Mfundo,mwenyekiti wa Umoja wa Tanzania Ujeruma

Watanzania Ujerumani wamepania !
kusherehekea miaka 49 ya Muungano,Mjini Kolon,
Siku ya Jumamosi 27.04.2013.

umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU)
kufanya sherehe za miaka 49 ya muungano
wa bara na visiwani,kama linavyoonekana
tangazo hapo.

Watanzania wote na marafiki wa tanzanzania
mnaoishi ndani na nje ujerumani mnakaribishwa.

"Umoja ni Nguvu ! Utengano Ni Udhaifu"
 Chereko Chereko na mwenye mwana
 Watanzania jitokezeni kwa wingi 

kwa mawasiliano zaidi at kamati.utu@googlemail.com

hafla ya Marketer's night out ilivyofana usiku huu ndani ya golden tulip jijini dar.

$
0
0
Ulifika wakati wa wageni waalikwa mbalimbali kuserebuka na muziki mzuri uliokuwa ukiporomoshwa na bendi ya B Band,kwenye hafla ya "Marketer's Night Out ",ambapo msemaji mkuu alikuwa ni Dkt.Wale Akinyemi kutoka nchini Nigeria.Usiku huo ulidhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake cha Tusker Lite.
Msemaji mkuu wa hafla ya "Marketer's Night Out " Dkt.Wale Akinyemi kutoka nchini Nigeria akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali (hawapo pichani) waliofika kwenye hafla hiyo iliyofana kwa kiasi kikubwa chini ya udhamini mkubwa wa kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake cha Tusker Lite.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), Steve Gannon akiwakaribisha wageni waalikwa mbalimbali kwenye hafla hiyo ya "Marketer's Night Out " ndani hotel ya Golden Tulip usiku huu jijini Dar.
Mkurugenzi Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), Ephrahim Mafuru akizungmza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla ya Usiku wa maafisa masoko (Marketer's Night Out),uliofanyika ndani ya hoteli Golden Tulip,Masaki jijin Dar.Usiku huo umedhaminiwa na kampuni ya  bia ya Serengeti kipitia kinywaji chake cha Tusker Lite.
 Mmoja wa watangazaji mahiri kutoka kituo cha redio, Eastafrica Radio atambulikae haswa kwa jina la Zembwela akijitambulisha mbele ya hafla maalum ya Usiku wa Maafisa Masoko kutoka makampuni mbalimbali,ndani ya Golden Tulip,Masaki jijin Dar.
 Pichani shoto ni Meneja Masoko wa Multchoice-Tanzania, Furaha Samalu akiwa na msemaji mkuu wa hafla ya  Marketer's Night Out,Dkt.Wale Akinyemi kutoka nchini Nigeria.
Pichani kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), Steve Gannon  akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Masoko,Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), Ephrahim Mafuru  kwenye hafla ya Usiku wa maafisa Masoko kutoka kampuni mbalimbali.
Pichani kulia ni Meneja wa Kinywaji cha Tusker Lite,Anitha Msangi akiwa na mdogo wake wakifurahia jambo.
 Mmoja wa waimbaji mahiri ndani ya bendi ya B Band,akiimba kwa hisia kwenye hafla ya Usiku wa Maafisa Masoko (Marketer's Night Out),iliyofanyika  kwenye moja ya ukumbi wa mikutano wa hotel ya Golden Tulip,Masaki jijini Dar.
Baadhi ya Wanamuziki wa bendi ya B Band inayoongozwa na Banana Zorro wakitumbuiza usiku huu wenye hafla fupi ya Usiku wa Maafisa Masoko (Marketer's Night Out),iliyofanyika  kwenye moja ya ukumbi wa mikutano wa hotel ya Golden Tulip,Masaki jijini Dar.Usiku huo umedhaminiwa na kampuni ya  bia ya Serengeti kipitia kinywaji chake cha Tusker Lite.

  Baadhi ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo usiku wa leo wakimsikiliza msemaji mkuu wa hafla hiyo Dkt.Wale Akinyemi kutoka nchini Nigeria.

MAONESHO YA NDEGE ZA KIJESHI KWENYE SHEREHE ZA MUUNGANO LEO

serikali ya zanzibar kuwachukulia hatua kisheria wale wote watakaobainika kufanya uvunjifu wa amani nchini.

$
0
0

MAKAMO Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein amesema serikali itawachukulia hatua za kisheria wale wote ambao watabainika wanafanya vitendo vya uvunjifu wa amani nchini.

Kauli hiyo  ameitoa jana wakati alipokuwa akiwahutubia wanachama wa Chama cha Mapinduzi katika ziara yake ya kichama Mkoa wa Mjini  Magharibi.

Amesema kuwa kuna baadhi ya wafuasi wa vyama vya siasa wanafanya vitendo viovu na fujo na kupelekea kusababisha uvunjifu wa amani.

“Hakuna sera za kufanya fujo, CCM ina fanya sera za kistaarab huu ni mfumo wa siasa za kistaarab sio kufanya fujo na vurugu”, alieleza Dr. Shein.

Alieleza kuwa CCM ina uwezo mkubwa sana katika medali za siasa hivyo imejiandaa katika kukabiliana na ushindani wa kisiasa kwa kushindana kwa sera sio kutumia fujo.

Aidha amesema kuwa CCM ni chama imara kipo makini katika uongozi wake ambacho kina wanachama walio makini na kinafuata  maadili  na sera za kistaarab sio zenye kubabaisha watu.

“Lazima watu wajuwe kama CCM wenyewe wapo hawajalala wala hawajachukua likizo tupo makini na huu ni mwanzo wa safari ya kuingia katika vuguvugu la siasa”, alifahamisha Makamo huyo.
  
Dr Shein aliwataka wanachama hao kutokubali kuhadaiwa na kubabaishwa na wale ambao hawana sera za msingi za kutaka kuvunja muungano kwa kisingizio cha kuwa hauna manufaa nchini.

“Tuna kila sababu ya kukiimarisha Chama cha Mapinduzi  na kukipa heshima kwani wakati ndio  huu wa kuongeza nguvu na kujiandaa bila ya kusita”, alieleza Makamo huyo.

Aidha aliwasisitiza kuongeza kasi ya kushikamana katika kukiimarisha na kudumisha chama ili kiweze kushinda katika uchaguzi ujao pamoja na kulinda na kuyaenzi Mpainduzi ya Zanzibar.

Akizungumzia huduma ya maji nchini Makamo huyo amesema Serikali ipo makini katika kuhakikisha kuwa wananchi wake  wanapata  huduma hiyo  kwa kiwango cha kutosha na  kuongeza kuchimba visima katika maeneo mbali mbali na taasisi husika inaendelea kulishughulikia tatizo hilo.

Katika ziara yake Makamo Mwenyekiti aliweka jiwe la msingi katika tawi la CCM Fumba , kutoa kadi kwa wanachama wapya pamoja na kukabidhi hati ya Utumishi bora kwa viongozi wa mashina.

Na Miza Kona   
 IDARA YA  HABARI MAELEZO ZANZIBAR   

IBF/AFRICA SUPER MIDDLEWEIGHT ON THE LINE AS MASHALI ATTEMPTS TO GRAB THE CROWN

$
0
0

FOR IMMEDIATE RELEASE – FRIDAY 26, 2013 - Dar Es Salaam - Reeling from the recent defeat in the hands of the German strongman Uensal Arik , TEAM Francis Cheka is back on the drawing board as it attempts to defuse negative impact of the loss in their forthcoming rumble against the man of the people and dreadlock Thomas Mashali. The duo is competing for the “IBF Continental Africa Super Middleweight Title” as optional defense for Cheka.
  
The tournament slated for 1st May, 2013 (May Day) has elicited a lot of excitements from thousands of boxing stakeholders in Tanzania and the whole of East African region. Thomas Mashali is the East & Central African Middleweight Champion and the biggest crowd puller in the region todate. 
                                                                      Francis Cheka (right) and Uensal Arik (left)
  
Cheka’s recent defeat was kind of embarrassment as he took the fight as a warm up but alas, things turned bitter as the Germany strongman Uensal Arik sent him reeling to the floor before Thomas Mtua threw out the towel as SOS for the Tanzanian slugger! It was a defeat from “Manna”as this kind of taught Cheka a lesson or two about taking boxing serious as there is nothing as a small fight in boxing.
  
Adam Tanaka of Mumask Investment and Gebby Presure LTD, the man of the hour promoting this fight has been working over drive to have all the details finalized. Of the top priority is the arrival of the ring officials (all coming outside Tanzania) who have been summoned to preside over the rumble. This is so because Adam want to avoid complaints from either boxer should the decision goes against their expectations.

"The poster in Kiswahili language tells it all"


The man who has been charged with the responsibility to stand in as “the third man in the ring” is no other than the Zambian Army Officer, John Shipanuka who himself looks like a heavyweight boxer in refereeing uniform. Shipanuka’s body language and impatiality with boxers in the ring has illuminated his CV and make him one of the most sort-out ring officials in Sub Sahara Africa.

To assist him would be two Sedentary Generals of; Uganda Professional Boxing Commission (UPBC), master Simon Katogole and Daudi Chikwanje of Malawi Boxing Association (MBA). These two gentlemen would be in the company of one of the most experienced judges in East Africa Alhaj Ismail Sekisambu alsofrom Uganda.


So, “the chickens have finally come home to roost" as any of the two has to face the consequences of his mistakes in the ring on that particular day.
  
So, as the clock ticks to the morning hours of May Day 2013, Dar Es Salaam landscape may turn into a “quicksand” for the two gladiators as fans from all walks of life jams the PTS Social Hall to witness yet another rumble of the year!
  
 Nothing has been left to chances as the World's premier professional boxing “top dog” the IBF has already given its blessing by sanctioning for the title!
 
Arusha Mayor (left) and IBF/AFRICA' Onesmo Ngowi
(right) crowing Cheka after his last defense 12/26/12

SHEREHE ZA MIAKA 49 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR ZAFANA SANA UWANJA WA UHURU JIJINI DAR LEO

$
0
0
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiingia uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam leo kuongoza Watanzania kusherehekea miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliozaa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Pamoja naye kwenye gari hilo la wazi ni Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange
 Nyomi si ya kawaida hata pa kutema mate hakuna
 Msafara wa Rais Kikwete ukizunguka uwanja wa Uhuru
Nyomi ya leo. Taswira zingine na kumwaga baadaye.

uwekaji saini mkataba wa ujenzi wa kivuko cha dsm- bagamoyo

$
0
0
 Picha ya mchoro ya kivuko cha  Dar es Salaam – Bagamoyo kitakavyokuwa.

 Mtendaji Mkuu wa TEMESA Mhandisi Marceline Magesa (mwanamke) , na mwakilishi wa kampuni ya  JOHS GRAM HANSSEN A/S ya  Denmark  Andreas Gottrup wakiweka  saini mkataba wa ujenzi wa Kivuko  cha Dar es Salaam- Bagamoyo leo jijini Dar es Salaam, katika hafla iliyoshuhudiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (aliesimama katikati) Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mecky Sadick(alie vaa  shati la kitenge) Balozi wa Denmark nchini Tanzania  Mh, Johnny Flinto (mzungu aliesimama  mstari wa nyuma). Pamoja na watendaji wakuu wa  Wizara ya Ujenzi. 
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Sadick Mecky (kulia) akizungumza wakati wa  hafla ya uwekaji saini mkataba wa ujenzi wa  Kivuko cha Dar es salaam – Bagamoyo. Kivuko hicho kitagharimu shilingi 7.91 bilioni za kitanzania. Mwengine ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli. 

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (kulia) akiongea na Balozi wa Denmark nchini Tanzania Mh. Johnny Flinto,katika  sherehe ya uwekaji  saini mkataba wa ujenzi wa kivuko cha Dar es Salaa- Bagamoyo (April 25, 2013).
 baadhi ya viongozi wakiwa katika meza kuu
Mwenyekiti wa Bodi ya ushauri ya TEMESA, Prof. Idrisa Mshoro (kulia) akimueleza  jambo  Mwakilishi wa  kampuni ya JOHS GRAM HANSSEN A/S ya Danmark , Andreas Gottrup wakati wa sherehe za uwekaji saini mkataba wa ujenzi wa kivuko cha Dar es Salaam- Bagamoyo jijini Dar es  Salaam(April,25,2013). 
 baadhi ya wadau wa wizara ya ujenzi wakishuhudia tukio hilo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Marceline Magesa (kulia) akizungumza  katika hafla ya uwekaji saini  mkataba wa ujenzi wa kivuko cha Dar es Salaam- Bagamoyo leo jijini . Kivuko hicho  kitakuwa na uwezo wa  kubeba watu 300 , kitagharimu  shilingi7.91 bilioni.(bilioni7.91 za tz).Pichani  kutoka kulia ni Waziri wa Uchukuzi Dkt,John Magufuli,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam  Mecky Sadick, na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi , Balozi Herbert Mrango. Picha zote na Mwanakombo Jumaa.

ASNATH NDIYE REDD'S MISS HIGHER LEARNING MOROGORO 2013

$
0
0
Mshindi wa Shindano la Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro, Anitha Mwakitwange kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe akipunga mkono mara baada ya kuvikwa taji hilo usiku wa kuamkia jana katika shindano lililofanyika Mjini Morogoro. Anitha aliwashinda warembo wenzake 10 aliokuwa akiwania nao taji hilo.
 
Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro, Anitha Mwakitwange(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili Rosemary Aloyce (kulia) na Mshindi wa Tatu Tarchisic Mtui mara baada ya warembo hao kutawazwa kuwa ndio washindi wa Shindano hilo usiku wa kuamkia jana katika shindano lililofanyika Mjini Morogoro. Anitha ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe aliwashinda warembo wenzake 10 aliokuwa akiwania nao taji hilo. KUONA PICHA ZAIDI>>> FATHER KIDEVU BLOG

Warembo 16 watemwa Miss Tabata

$
0
0

Washiriki wa Miss Tabata wakipozi mazoezini Da West Park, Tabata
 ========  =======  ======
Jumla ya warembo 16 wametemwa katika kinyang’anyiro cha kumtafuta Redds Miss Tabata ambao utafanyika Mei 31 Dar West Park. Mratibu wa shindano hilo, Godfrey Kalinga, alisema jana kuwa warembo hao wametemwa kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo utoro, kukosa sifa za kushiriki na utovu wa nidhamu.

Kalinga aliwataja warembo waliyotemwa kuwa ni Sophia Claud (21), Lilian Mpakani (19), Lilian Msanchu (19), Rita Frank (20), Pasilida Mandali (21), Rachel Mussa (19), Jasmin Damian (18), Angelina Mkinga (19), Mercy Mwakasungu (20), Tunu Hamis (19), Ray Issa (22), Shamim Abass (22), Shan Abass (22), Amina Ally (18), Magdalena Bhoke (21)  na Zilpha Christopher (19).

Kalinga aliwataja warembo wanoendelea na mazoezi katika umbumbi wa Dar West Park, Tabata kila siku kuwa ni Hidaya David (22), Aneth Ndumbalo (19), Dorice Mollel (22), Eunice Nkoha (19), Kazunde Kitereja (19),  Angela Fradius (19), Domina Soka (21), Rehema Kihinja (20) and  Glory Jigge (18). Wengine ni Rachel Mushi (20), Caroline Sadiki (20), Kabula Juma Kibogoti (20), Blath Chambia (23), Suzzane Daniel Gingo (18), Upendo Lema (22), Pasilida Mandari (21) na Martha Gewe (19).

Washindi watano kutoka Tabata watafuzu kushiriki Redds Miss Ilala baadaye mwaka huu.
Anayeshikilia taji la Miss Tabata ni Noela Michael ambaye pia ni Miss Ilala.  Redds Miss Tabata inaandaliwa na  Bob Entertainment na Keen Arts na chini ya Udhamini wa Redds, CXC Africa, Fredito Entertainment, Brake Points na Saluti5.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI HARAMBEE YA KUCHANGIA UJENZI WA KANISA LA TZ METHODIST MSASANI NA KUZINDUA CD YA KWAYA YA WATOTO WANAOFADHILIWA NA COMPASSION INTERNATIONAL TZ.

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya maua kutoka kwa watoto wa Kituo cha Kanisa la Tanzania Methodist la Msasani, wakati alipowasili katika kituo hicho leo kwa ajili ya kuhudhuria harambee ya kuchangia ujenzi wa Kituo cha Kanisa hilo iliyofanyika sambamba na Ibada maalum ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya Shirika la Compassion International Tanzania kwa kuingia Ushirika wenza na Makanisa ya Mkoa wa Dar es Salaam na kuzindua Cd ya Kwaya ya Watoto wanaofadhiliwa na Shirika hilo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili katika Kituo cha Kanisa la Tanzania Methodist la Msasani, leo kwa ajili ya kuhudhuria harambee ya kuchangia ujenzi wa Kituo cha Kanisa hilo iliyofanyika sambamba na Ibada maalum ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya Shirika la Compassion International Tanzania kwa kuingia Ushirika wenza na Makanisa ya Mkoa wa Dar es Salaam na kuzindua Cd ya Kwaya ya Watoto wanaofadhiliwa na Shirika hilo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya kutoka kwa Mkurugenzi wa Kituo cha Kanisa la Tanzania Methodist la Msasani, Joseph Mayala, leo  wakati wa hafla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa Kituo cha Kanisa hilo iliyofanyika sambamba na Ibada maalum ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya Shirika la Compassion International Tanzania kwa kuingia Ushirika wenza na Makanisa ya Mkoa wa Dar es Salaam na kuzindua Cd ya Kwaya ya Watoto wanaofadhiliwa na Shirika hilo. Kulia ni Askofu wa Kanisa hilo, Dkt. Mathew Byamungu. 

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia waumini wa dini ya Kikristo wa Kituo cha Kanisa la Tanzania Methodist la Msasani, wakati alipowasili katika kituo hicho leo kwa ajili ya kuhudhuria harambee ya kuchangia ujenzi wa Kituo cha Kanisa hilo iliyofanyika sambamba na Ibada maalum ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya Shirika la Compassion International Tanzania kwa kuingia Ushirika wenza na Makanisa ya Mkoa wa Dar es Salaam na kuzindua Cd ya Kwaya ya Watoto wanaofadhiliwa na Shirika hilo.
 Baadhi ya waumini waliohudhuria harambee hiyo.
 Watoto wa Kwaya inayofadhiliwa na Shirika la Compassion International Tanzania, wakitoa burudani ya kuimba moja ya wimbo wao ulio katika Albam yao iliyozinduliwa katika hafla hiyo.
 Askofu wa Kanisa la Tanzania Methodist la Msasani, Dkt. Mathew Byamungu, akitoa neno la shukrani baada ya hafla hiyo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na watoto wanaounda kundi la Kwaya ya watoto, inayofadhiliwa na Shirika hilo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na Watoto wa Kituo hicho.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na baadhi ya wachungaji na watumishi wa Kanisa hilo.

mkoa wa njombe wadaiwa kuwa na maambukizi makubwa ya virusi vya Ukimwi.

$
0
0


=========  ======== ======
Na Edwin Moshi, Makete.

Pamoja na mkoa wa Njombe hii leo kuadhimisha miaka 49 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, imeelezwa kuwa mkoa huo ndiyo unaoongoza kitaifa kwa kuwa na maambukizi makubwa ya virusi vya Ukimwi ya asilimia 14.8

Kufuatia hali hiyo mkoa huo umejipanga ipasavyo kukabiliana na changamoto hiyo ambayo inaleta sifa mbaya kwa taifa, zoezi litakaloanza mwezi Juni mwaka huu

Hayo yamezungumzwa na Mkuu wa mkoa wa Njombe Kapteni mstaafu Aseri Msangi ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 49 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika kitaifa katika Kata ya Itundu wilayani Makete

Amezitaja sababu zinazopelekea maambukizi ya vvu kuwa juu kuwa ni pamoja na kurithi wajane, wanawake kutokuwa na amri juu ya miili yao hivyo kuogopa kumwambia wanamme kutumia kondomu wakati wa kufanya mapenzi, wanaume kutofanyiwa tohara pamoja na wanaume kuoa wake wengi

“Hata biblia yenyewe inaruhusu tohara, na kwa taarifa yako mwanaume aliyetahiriwa inampunguzia yeye kupata maambukizi ya vvu kwa asilimia 60, lakini bado inashangaza watu hawataki kutahiriwa, sasa unategemea utaponaje kwenye maambukizi” alisema Msangi

Amesema mkoa umejipanga ipasavyo kupunguza maambukizi hayo kwa kuelimisha wanaume kufanyiwa tohara ambapo mwezi Juni hadi Augusti mwaka huu zoezi la tohara litafanywa mkoa mzima huku mkuu huyo wa mkoa akiwa namba moja kuongoza zoezi hilo la uhamasishaji kwenye kila kata ya mkoa wake

Pamoja na hayo mkuu huyo amesisitizia watu kutambua historia ya wapi walipotoka, kutumia wataalamu katika shughuli zao ikiwemo kilimo na ufugaji, ambapo watu wengi hukosa mazao kama walivyokuwa wakitarajia kutokana na kutotumia pembejeo za kisasa za kilimo

“Mtu hadi leo unatumia mbegu za mababu zako halafu utegemee kuvuna gunia 30 kwenye heka moja, hilo suala halipo ng’o wewe fuata wataalamu wa kilimo wakuelekeze namna ya kupanda, kutumia mbolea na namana ya kupalizi na utumie mbegu gani halafu tuone kama hutavuna magunia ya kutosha” alisisitiza Msangi.

Zaidi inaweza kubofya kwenye uzi huu www.eddymoblaze.blogspot.com

DAYNA NYANGE, AMPIGIA SALUTI AFANDE

$
0
0

  
 Mwanamuziki  toka  mkoani  Morogoro  anayefanya  poa  kwa  sasa  na  wimbo  wake  wa  Leo  mwanadada  Dayna  Nyange  a.k.a  Mkali  wao,  amefunguka  na  kumpigia  saluti mwanamuziki  mkongwe toka  hapa  Morogoro Afande  Sele.

    Akiongea  na  ubalozini.blogspot.com   toka jijini Mwanza  aliko  sasa  katika  ziara  ya kimuziki  na  uzinduzi  wa  Albam  ya  Kala.  Dayna  amesema  huwa  anamkubali  afande kwa  tungo  zake

 '' kwa  kweli  siku  zote,  nimekuwa  nikimkubali  sana  Afande  sele  kwa  tungo  zake  zenye  ujumbe,  lakini  kwa  wimbo  huu wa  Dini tumeletewa,  nampigia  saluti. Afande  ni  bonge  la msanii  na  huwa naskiliza  nyimbo  zake kwani  najuwa  nikiskiliza  nyimbo  zake  kuna  madini  napata,  lakini  sasa kaka  mkubwa  kwa  hapa  alipofikia  na kufikilia  kwa  kina juu  ya  wimbo  huu,  anastahili  kuwa mfalme wa  Rhyme,  waliompa  tuzo  hawakukosea. 

Big  up  sana  Afande, saluti  kwake,  aendelee kuwa  mwalimu  wa  ujumbe  , huuwimbo  ni  zaidi  ya  Hotuba  ya  kitaifa Inayotolewa  na  Rais''
  Amesema Dayna

Mdau alex kusaga wa Clouds Media Group auaga rasmi ukapera jioni ya leo.

$
0
0


 Maharusi Alex Kusaga na Mkewe Evelyn wakilisha keki ya upendo usiku huu ndani ya moja ya ukumbi wa hotel ya Serena jijini dar. 
 Ulifika wakati wa kufungua shampeni.

Wasanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka THT,Recho,Lina,Barnaba na Amin wakitumbuiza usiku huu kwa pamoja kwenye mnuso wa mdau Alex Kusaga kutoka mjengoni,Clouds Media Group.
  Wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye mnuso huo wa nguvu.
 Bibi harusi,Evelyne Julla akitoa tabasamu la nguvu na lenye furaha mara baada ya kuikamilisha ndoto yake ya kumpta mwenza wake wa maisha,Bwa.Alex Kusaga wa Clouds Media Group.
 Maharusi wakizifurahia pete zao za ndoa mara baada ya mapumziko mafupi kabla ya kuingia mnusoni jioni ya leo ndani ya hotel ya Serena jijini dar.
 Wakishoo love na mdogo wake Alex Kusaga,ambaye ni wifi ya bibi harusi.
 Maharusi wakionesha   vyeti vyao vya ndoa mara baada ya kufunga harusi ndani ya kanisa la St.Immaculata,Upanga jijini Dar.
 Maharusi wakila kiapo cha ndoa 
Maharusi wakiwa katika sura za furaha kabisa wakitoka nje ya kanisa mara baada ya kutimiza ndoto yao ya kuishi pamoja,baada ya hapo usiku huu mnuso uko ndani ya Serena hotel.

Red Carpet Swagga @ Bongo Black Ball - celebrating Tanzanian Music held at Mlimani City Dar.

$
0
0
Mbunifu wa Mavazi Khadija Mwanamboka (kushoto) ambaye pia ndio Mwandaaji wa Bongo Black Ball Party iliyobeba Theme " Celebrating Tanzania Music" wakati wa uzinduzi wa Kampuni ya Vitu vya Khadija Events & Clothing akiwa na wadau mbalimbali kwenye mnuso wa nguvu uliowakutanisha Masupastaa wa Bongo wadau waliopo kwenye Fashion Industry katika usiku uliopambwa na msanii Mkongwe wa muziki nchini King Kiki a.k.a mzee wa kitambaa cheupe pamoja na burudani kutoka kwa wasanii wa Bongo Flava Linex na Mwasiti. Pichani Bi. Khadija Mwanamboka akiwa na wageni mbalimbali kwenye Red Carpet ndani ya Ukumbi wa Mlimani City.
Designer Ally Rehmtullah ndani ya nyumba.
Blogger Missi Popular aliwakilisha kikazi zaidi.
Gyver Meena and Salma Msangi a.k.a Kimora Lee looking Gorgeous (I think these two Girls rock the night).
Mama Mia....Wow.....!
Kwa picha zaidi Bofya hapa

AFISA MTENDAJI MKUU WA PEPSI ATEMBELEA TANZANIA

$
0
0
Afisa Mtendaji Mkuu PepsiCo, Asia, Mashariki ya Kati na Africa Bw. Saad Abdul-Latif akiongea na Mkurugenzi Mkuu wa SBC Tanzania Bw. Ziad El Khalil.





Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, Bi. Joyce Mapunjo akifurahia jambo na Bw. Saad Adbul-Latif.

 *****    ******
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya vinywaji baridi ya PEPSI kwa Bara la Asia, Mashariki ya Kati na Afrika, Bw. Saad Abdul Latif, hivi karibuni alifanya ziara nchini Tanzania ikiwa ni sehemu ya ziara ya kuzitembelea nchi za ukanda wa Afrika Mashariki (Kenya, Tanzania na Uganda).

Katika ziara hiyo, Bw. Latif, aliambatana na Rais wa Kampuni hiyo ya PEPSI kwa bara la Asia, Mashariki ya Kati na Afrika, Bw. Sanjeev Chadha, ambapo waliweza kukutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, Bi. Joyce Mapunjo.

“Ni furaha kubwa kuwa hapa nchini Tanzania. Kubwa ninaomba muwe na uhaikika ya kwamba Kampuni ya PEPSI, imedhamiria kuhakikisha kwamba wateja wake wanafurahia bidhaa zenye ubora wa kimataifa katika bei nafuu zilizo za kirafiki,” alisema Bw. Latif.

Akizungumza kwa niaba ya Serikali, Bi. Mapunjo aliishukuru Kampuni hiyo ya PEPSI kutokana na ahadi yake iliyojiwekea ya kusaidia katika suala zima la maendeleo ya kiuchumi hasa katika juhudi zake za kuboresha viwanda, masoko, miundombinu na usambazaji.

“Kampuni ya PEPSI nchini (SBC Tanzania) inazalisha na kutengeneza nafasi za ajira nchini Tanzania,” aliongeza Bi. Mapunjo.

 Hivi karibuni Kampuni ya SBC imeanzisha kiwanda cha kisasa cha PEPSI katika jiji la Nairobi, ambapo matokeo yake yamekuwa mazuri naya kutia moyo kutoka kwa wateja. SBC si tu inatoa chaguo la ziada kwa wateja wake kwenye vinywaji vyake, lakini pia inatoa thamani ya ziada kwa fedha.

Vinywaji hivi vya PEPSI venye ujazo wa 350 ML kwenye glasi kinauzwa bei ya kawaida ambayo ni sawa na bei ya chupa yenye ujazo wa 300 ML. Ni pamoja na Pepsi, Mirinda, Mountain Dew na aina tofauti za Evervess Kampuni ya SBC Tanzania, ni kampuni pekee inayozalisha bidhaa mbalimbali za PEPSI nchini Tanzania.

IBF DOES IT AGAIN – AFTER FIGHTING AGAINST RACIAL DISCRIMINATION, NOW IT IS FIGHTING FOR PEACE IN AFRICA

$
0
0

When it was formed in 1963, after the few African countries gained independence from the colonial powers, the Organization of African Unity now African Union or AU was hosted at Addis Ababa , the capital city of Ethiopia, under the country’s then monarch King Haile Selassie.  This year 2013, the African Union (AU) is celebrating its 50th years anniversary

Mr. Sammy Retta, President & CEO, African Sport Promotion PLC
 Plan is underway to bring over most current “IBF Africa, Middle East and Persian Gulf” champions over to Addis Ababa, Ethiopia to take part in the African Union 50th years Anniversary  celebrations. This gesture by both the event's organizers led by Mr. Sammy Retta of the African Sport Promotion PLC and the AU to IBF/AFRICA, came about after major development initiatives in “African boxing fraternity" since IBF/AFRICA's inception in 2000”. The tournament is dubbed, “Campaign toraise awareness for peace in the horn of Africa" (Somalia, Sudan and Southern Sudan).
This event is happening exactly 33 years since “IBF” sanctioned the first black South African boxer Welcome Ncita in 1980 to vie for its "world featherweight title" making it “the first sanction body in the world to break the color ban” in the then“apartheid South Africa”. So, after fighting against racial discrimination, now “IBF” it is fighting for peace in the African continent" when it rallies all its Africa, Middle East and Persian Gulf champions in the biggest cause in history.
In order to make this event succesful, African Union (AU) has appointed its Director for Peace and Security Mr. El Ghassim Wane to supervise the implementation of this tournament and report to H.E Erastus Mwencha, Deputy Vice Chairperson of African Union Commission and Chair of the Organizing Committee of the 50th Anniversary Celebrations.
 “Boxing is a popular sport in Africa and the rest of the world, we have no doubt that the message of peace, solidarity and unity being conveyed throughout the continent in particular those countries emerging from conflicts such as Somalia, Sudan and Southern Sudan will find attentive audience in Africa and beyond through this event” said H.E. Erastus Mwencha, Deputy Vice Chairperson of African Union Commission, Chair of theOrganizing Committee of the 50th Anniversary Celebration in his letter of suppor.
African Union Chairperson, Nkosazana Dlamini-Zuma (left)
 A long list of IBF/AFRICA champions to feature in this colorful event will be announced during the “Press Conference”plannned to take place at the newly inaugurated “AU Headquarters” in Addis Ababa, Ethiopia 6 May, 2013. 
 Nothing is more “IMPORTANT” as Africans from all walks of life enjoy the fruits of their independence as this has largely been proven by development initiatives undertaken for the continent in the past 50 years.
 This event put IBF way ahead of the troop as it consolidates its grip on the African boxing fraternity and proves its “Top Dog”status as far as boxing as a professional sport is concern.  
 ISSUED BY
INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA)
DAR ES SALAAM, TANZANIA

Rais Kikwete ahudhuria Ufunguzi wa Kikao cha EAC Arusha

$
0
0
Marais wa jumuiya ya Afrika Mashariki wakisimama kwa dakika moja kumkumbuka laiyekuwa Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Uganda Marehemu Eriya Kategaya wakati wa ufunguzi wa kikao cha kumi na moja cha Jumuiya hiyo jijini Arusha leo mchana. Katika Hoteli ya Ngurdoto.Kutoka kushoto Rais Wa Burundu Pierre Nkurunzinza,Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Wa Kenya Uhuru Kenyatta.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya wakati wa ufunguzi wa kikao cha juu cha kumi na moja cha Wakuu wa nchi wa jumuiya ya Afrika Mashariki kilichofaniyka jijini Arusha.
Marais wa jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa kwenye kikao cha kumi na moja cha Jumuiya hiyo jijini Arusha leo.
Baadhi wa ajumbe walioshiriki ufunguzi wa kikao cha Juu cha kumi na moja cha Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki(11th Extraordinary EAC Summit) kilichofanyika jijini Arusha(picha na Freddy Maro)

Mama Tunu Pinda azindua DVD mpya ya kwaya ya Imani leo

$
0
0
 Mama Tunu Pinda akiwa anasoma risala kwa waumini wa Kanisa la TAG kabla ya kuzindua DVD  yenye jina la .'Mungu Wetu Halinganishwi' ya  kwaya ya Kanisa  la Tanzania Assemblies of God TAG) Mwenge jijini Dar es salaam leo. 
 Mama Tunu Pinda akiwa anasoma risala kwa waumini wa Kanisa la TAG kabla ya kuzindua  DVD hiyo
 Mama Tunu Pinda akizindua rasmi  DVD yenye jina la .'Mungu Wetu Halinganishwi' ya  kwaya ya Imani ya Kanisa  la Tanzania Assemblies of God (TAG) Mwenge jijini Dar es salaam leo. Wanaoshuhudia kulia kwa Mama Pinda ni Mchungaji kiongozi Abdiel Mhini, kulia mwenye kilemba ni Mchungaji Grace Mainoya anayefuatia ni Askofu wa TAG jimbo la Mashariki Kaskazini  Spear Mwaipopo Mama Tunu Pinda alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Dvd hiyo Picha na Chris Mfinanga
Mfuniko wa DVD iliyozinduliwa leo


Mama Pinda Ataka Watanzania wajitolee kwa kazi za Mungu

 MKE WA WAZIRI MKUU Mama Tunu Pinda amewataka Watanzania wajenge tabia ya kuchagia kazi za Mungu ili kuwasaidia watu wengine wapate fursa ya kulisikia neno la Mungu bila vikwazo.

Ametoa wito huo leo mchana (Jumapili, Aprili 28, 2013) wakati wa ibada ya uzinduzi wa albamu ya“Mungu Wetu Halinganishwi” iliyofanyika kwenye Kanisa la TAG, Mwenge jijini Dar es Salaam.

“Mungu Wetu Halinganishwi” ni albamu za DVD, VCD na CD zilizotolewa na kwaya ya Imani ambayo ni kwaya kuu ya kanisa hilo. Albamu hiyo ina nyimbo nane. Zaidi ya sh. milioni 12 zilipatikana ikiwa ni ahadi na fedha taslimu kutokana na mnada wa DVD za albamu hiyo.

“Naomba kutoa changamoto kwa kila mmoja wetu aliyefika mahali hapa mchana huu, tujiulize ni kwa kiasi gani tumesaidia kupeleka Neno la Mungu kwa watu wenye uhitaji wa kulisikia Neno na hawana uwezo wa kulisikia Neno hilo? Ni kwa kiasi gani tumeshiriki kuchangia huduma ya Uinjilisti ili wenye kiu ya Neno waweze kuamini na hatimaye kuokoka?”, alisema.

Mama Pinda alisema Biblia Takatifu inawakumbusha wanadamu wote kwamba kuamini, kubatizwa na hatimaye kuokoka si hiari ya mwanadamu bali ni amri ya Mwenyezi Mungu, na akasisitiza kuwa ni wajibu wa kila mmoja kuwasaidia watu wenye kiu ya neno la Mungu ili kuhakikisha wanapokea neno la Mungu.

“Tujiulize ni jinsi gani tutawasaidia wapate kulisikia na kuliamini Neno la Mungu na hatimaye kuokoka.Tukumbuke kwamba hawa ndiyo majirani zetu ambao Biblia inatukumbusha kuwapenda kama tunavyojipenda sisi wenyewe,” alisisitiza.

Alisema umefika wakati wa Watanzania kuanza kuchangia huduma za kusambaza neno la Mungu iwe kwa nyimbo kama walivyofanya Imani Choir au kwa njia nyingine kwani watu wako radhi kuchangia harusi kuliko kuchangia kazi ya Mungu.

“Sisi sote tu mashahidi wa jinsi ambavyo tumekuwa mstari wa mbele katika kuchangia harusi lakini tukilegelega kuchangia kazi ya uenezaji injili. Nasi tunaweza kuwaunga mkono Kwaya ya Imani kwenye kazi hii kwa kutumia mali zetu. Naomba nitumie fursa hii kuwasihi sana wote mliopo hapa tujitoe kwa mali zetu ili tuwawezeshe Imani Choir kuifanya kazi hii kwa ukamilifu,” alisisitiza.

Mapema, akitoa mahubiri ya ibada hiyo ya kuweka wakfu ya kuzindua albamu ya “Mungu Wetu Halinganishwi”, Makamu wa Askofu wa Jimbo la Mashariki Kaskazini, Mch. Spear Mwaipopo, alisema mtu akifanya kazi ya Mungu kamwe haiendi bure ili mradi atambue kuwa anaifanya kazi ya Mungu.

Aliwasihi waumini na wageni waliohudhuria uzinduzi huo kutambua ukuu na mamlaka ya jina la Yesu.

Katika risala iliyosomwa na Katibu wa kwaya ya Imani, Bi. Janet Masaga, ilielezwa kwamba  jumla ya sh. milioni 25/- zinahitajika kwa ajili ya kununua basi aina ya Coaster kwa ajili ya kuwasaidia kubeba wanakwaya hao wenye nia ya kupeleka injili vijijini.

Naye Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo, Mch. Abdiel Meshack Mhini aliongoza maombi kwa ajili ya Taifa la Tanzania ambapo alitumia fursa hiyo pia kuwaombea viongozi wa Kitaifa, kuliombea Bunge la Tanzania na vikao vilivyosalia mbele yake.

Alimshukuru Mama Tunu Pinda kwa kutenga muda wake na kukubali kuizundia albamu ya kwaya kuu ya kanisa hilo.
Viewing all 46371 articles
Browse latest View live




Latest Images