Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

Dkt. Kigwangalla afanya ziara ya kushtukiza hospitali za mikoa ya Lindi na Mtwara

$
0
0
kigw1
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sokoine ya Mkoa wa Lindi, Dkt. Evaristo Kasanga akimkaribisha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla alipotembelea wodi za hospitali hiyo wakati wa ziara ya kushtukiza aliyofanya leo mkoa wa Lindi.Katikati ni Mganga wa Meno na Kinywa katika hospitali hiyo, Dkt. Hussein Athumani.
………………………………………………………………………………..
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,  Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla amefanya ziara ya kushtukiza mwishoni mwa katika hospitali za Rufaa za Mikoa ya Lindi na Mtwara kwa lengo la kujifunza namna wanavyofanya kazi ili Serikali iweze kuboresha na kutoa wa huduma bora za afya nchini.

Akifanya majumuisho ya ziara hiyo Dkt. Kigwangalla amesema kuwa amefurahishwa na namna hospitali hizo zinavyofanyakazi ya kuwahudumia wananchi ya kuhakikisha wanapata tiba ya uhakika katika masuala ya afya.“Nimefurahishwa na namna Hospilali ya Rufaa ya Sokoine ya mkoa wa Lindi wanavyofanyakazi wanavyotoa huduma, kila ofisi niliyofika madaktari walikuwepo na wanafanyakazi” alisema Dkt. Kigwangalla.

Licha ya kufanya ziara ya kushtukiza katika hospitali hiyo, Dkt. Kigwangalla alisema kuwa amefurahishwa na kitendo cha kuwakuta madaktari wa zamu na watoa huduma wote wapo katika maeneo yao ya kazi katika hospitali ya Sokoine Lindi mkoani na Ligula ya Mtwara kitu ambacho kinawapa faraja wagonjwa pamoja na jamaa zao wanaohitaji kupata huduma za afya ikiwemo huduma ya dharura anayohitaji kupewa mgonjwa kulingana na tatizo lake.

“Ziara tunazozifanya katika hospiltali za rufaa, mikoa, wilaya, vituo vya afya na zahanati, lengo letu ni kujifunza namna zinavyotoa huduma za afya kwa wananchi wetu ili baadaye kuona ni maboresho gani yafanyike na hatimaye kutoa huduma bora zenye tija na kwa wakati kwa wananchi” alisema Dkt. Kigwangalla.

Katika hatua nyingine, Dkt. Kigwangalla ameziagiza hospitali zote za mikoa nchini kote waige kutoka mkoa wa Lindi namna hospitali hiyo inavyotoa huduma kwa haraka na kwa wakati kwa kutumia mfumo wa kielekroniki kuanzia mgonjwa anapopokelewa chumba cha mapokezi hadi anapomaliza kupata huduma na kuruhusiwa.


Faida ya kutumia mfumo huo wa kielekroniki ni pamoja na kuongeza makusanyo kupitia kwa wagonjwa wanaotumia huduma ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na wale wanajilipia wenyewe, makusanyo yanayopatikana yanatumika kuboresha utoaji wa huduma ikiwemo kununua dawa na vifaa tiba kwa wakati, kutoa motisha kwa wafanyakazi pamoja na kupunguza urasimu usiowa lazima kwa wagonjwa.

Licha ya mafanikio hayo katika hospitali za rufaa za mikoa ya Lindi na Mtwara, hospitali hizo zinakabiliwa na changamoto ya uhaba wa madaktari bingwa ambapo hadi sasa Hospitali ya Sokoine ina Daktari Bingwa mmoja na Hospitali ya Ligula mkoani Mtwara ina madaktari Bingwa wawili licha ya ukubwa wa mikoa hiyo pamoja na kuhudumia wagonjwa kutoka nchi jirani ya Msumbiji.

Katika kutatua changamoto hiyo, Dkt. Kigwangalla amewaagiza Makatibu Tawala wa mikoa (RAS) yote kuandaa vyumba vya kufanyia upasuaji pamoja na vifaa tiba na kuandaa nyumba watakapokaa madaktari bingwa ambapo ameahidi Serikali itaanza kuwapangia vituo madaktari hao kwa kuanzia na mikoa ambayo imejipanga ili waanze kutoa huduma mara moja.

Akizungumzia namna walivyofanikiwa kutoa huduma bora, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Sokoine ya mkoa wa Lindi Dkt. Evaristo Kasanga alisema kuwa wameboresha namna ya kukusanya mapato hospitalini hapo kwa kufunga mashine za kielekroniki zinazopelekea wakusanye sh.milioni 24 kwa mwezi tofauti na hali livyokuwa hapo awali ambapo zilikuwa zinakusanywa chini ya sh.milioni 10 kwa wateja wanaotumia mfuko wa bima ya afya.

Mafanikio ya Hospitali ya Rufaa ya Sokoine ya mkoa wa Lindi yamejengwa juu ya falsafa yao inayosema “Sisi watumishi wa Sokoine tunaamini kwamba monjwa ndiye tajiri yetu, tunaahidi kuwa tutatoa huduma bora kwa wagonjwa wetu bila ubaguzi, hatupokei wala kutoa rushwa”.
Kwa upande wa makusanyo ya kawaida, Dkt. Kasanga alisema kuwa yamefikia sh.milioni 40 pesa tasilimu ikilinganishwa na hali livyokuwa hapo awali ambapo zilikusanywa chini ya sh.milioni 8 kwa mwezi.

“Hatua hiyo imesaidia kuboresha utoaji wetu wa huduma kwa kuanzia na usafi wa mazingira, mifumo ya kisasa ya mawasiliano ndani ya hospitali ili kurahisisha mawasiliano kati ya wagonjwa na wafanyakazi, wagonjwa kwa wagonjwa, wafanyakazi kwa wafanyakazi pamoja na masuala yote ya dharura kama daktari anahitajika kutoa msaada” Dkt. Kasanga.

 Aidha, Dkt. Kasanga alisema kuwa hospitali hiyo imefanikiwa kuwa mshindi wa pili kwa utoaji wa huduma bora Tanzania kwa mwaka 2015 ambapo wamezawadiwa kikombe cha ushindi wa nafasi hiyo na wamejipanga kuanzia Januari 2016 kuachana na mfumo wa watumishi kusaini kwenye vitabu wanapofika kazini badala yake wataanza kutumia mfumo wa kusaini kwa kuweka alama za vidole kwenye mashine maalum (Biometric) ambayo imefungwa na Shirika la Miradi la Ujerumani la GIZ hatua itakayorahisisha usimamizi wa mahudhurio kazini, kutoa huduma sahihi kwa wagonjwa na kwa wakati.

Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa ambaye pia ni Daktari wa Kinywa na Meno Hospilali ya Rufaa ya Sokoine ya mkoa wa Lindi Dkt. Hussein Athuman akitoa taarifa ya ugonjwa wa kipindupindu alisema kuwa hali inaendelea vizuri na idadi ya wagojwa imepungua kwa hatua inayoridhisha.

“Hali ya ugonjwa wa kipindupindu hadi mwishoni mwa wiki ilikuwa ni nzuri na tunaendelea kuisimamia ipasavyo, wilaya ya Kilwa ilikuwa na kesi za wagojwa wapya watatu ambapo mmoja tayari amesharuhusiwa kurudi nyumbani, manispaa ya Lindi kulikuwa na mgonjwa mmoja ambaye naye amesharuhusiwa” alisema Dkt. Hussein.

Ugonjwa wa kipindupindu mkoani Lindi umeathiri wilaya tatu za Manispaa ya Lindi, Kilwa na Lindi Vijijini ambapo wilaya ya Kilwa ndiyo imeathiriwa zaidi kuliko wilaya nyingie kutokana na ukaribu wa wilaya hiyo na mkoa wa Dar es salaam ambapo ugonjwa huo uligundulika mapema mwezi Augosti mwaka huu.

Aidha, Dkt. Hussein alisema kuwa mkoa huo umefanikiwa kusimamia ipasavyo na kuzuia maambukizi ya mapya ya ugonjwa huo yasitokee na kusambaa kwa kufanya usafi mahali pote katika makazi ya watu, hospitali, vituo vya afya na zahanati kama desturi ya mkoa huo wakichagiwa na agizo la kufanya usafi Desemba 9, 2015 la Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Zaidi ya hayo, Dkt. Hussein alisema kuwa waliweka dawa katika visima vyote vya maji hatua ambayo imesaidia kupunguza kusambaa kwa ugonjwa wa kipindupindi mkoani humo.

Kwa niaba ya uongozi, wafanyakazi na wananchi wa mkoa wa Lindi, Dkt. Hussein amewashukuru wadau wa maendeleo kwa kuendelea kuwaunga mkono kwa kuboresha mazingira ya hospitali ya Sokoine wakiwemo wabunge, washirika wa maendeleo wakiongozwa na  Shirika la Miradi la Ujerumani la Giz kuendelea kuwaunga mkono katika kuwahudumia wananchi.

OFISI YA RAIS, TUME YA MIPANGO YAKAGUA MIRADI YA VITUO VYA KUZALISHA UMEME VYA KIDATU NA KIHANSI

$
0
0
SONY DSC
Bibi. Florence Mwanri, Kaimu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango (aliyekaa) akipata maelezo kuhusu namna Kituo cha Kihansi kinavyofanyakazi kwa kutumia teknolojia ya kisasa ambayo imeboresha utendaji kazi kwa wafanyakazi na mitambo ambayo inatumika kuzalisha nishati ya umeme. 
SONY DSC
Bibi. Florence Mwanri, Kaimu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango (aliyevaa nguo nyeusi) pamoja na maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakipata maelezo kutoka kwa Injinia kituo cha Kidatu Bw. Yonah Mwasajone (wa kwanza kushoto) kuhusu Sub Station  ambayo baada ya umeme kuzalishwa katika mitambo ya kufua umeme Kidatu hutumika kuuingiza katika Grid ya Taifa.
SONY DSC
Bibi. Florence Mwanri, Kaimu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango (aliyevaa nguo nyeusi) akiangalia na kupata maelezo kutoka kwa Injinia wa kituo Bw. Rajabu Kindunda (wa tatu kulia) kuhusu Bwawa la Kidatu ambalo maji hukusanywa kutoka mto Rufiji kabla ya kutumika kwa ajili ya kuzalisha umeme. Wengine pamoja nae ni wataalamu kutoka Tume ya Mipango na TANESCO.
SONY DSCBibi. Florence Mwanri, Kaimu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango (aliyevaa nguo nyeusi) akiangalia eneo la mradi wa kuzalisha umeme Kidatu na kupata maelezo kuhusu faida na changamoto za mradi kutoka kwa Injinia wa TANESCO kituo cha Kidatu Bw. Rajabu Kindunda (wa tatu kulia). Wengine ni wataalamu kutoka Tume ya Mipango na TANESCO.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AWAONYA WATUMISHI WA SERIKALI, AWASILI KIJIJINI KWAKE NANDAGLA RUANGWA

$
0
0

f3940726-a5ba-43fe-8d8a-66bdb6a1cb19
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akisalimiana na wapigakura wke baada ya kuwasili kijijini kwake Nndagala wilayni Luangwa kwa mapumziko mafupi Desemba 20, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
……………………………………………………………………..
*Asema wabadhirifu watang’olewa mara moja
*Asema wako wasomi wengi wanaotafuta ajira
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaonya watendaji wa halmashauri nchini kwamba atakayebainika ametumia vibaya fedha za Serikali atang’olewa kazini kwa sababu Serikali ya Awamu ya Tano haina mchezo na mtu.
 Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumapili, Desemba 20, 2015)  wakati akizungumza na mamia ya wananchi waliofika kumsikiliza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Ilulu uliopo Lindi mjini.
 “Natoa onyo kwa watendaji wote wa halmashauri. Fedha ya Serikali itakayotumwa kwenu halafu mtu aifanyie ubadhirifu,  ole wake. Yeyote atakayebainika kuzitumia kwa ubadhirifu fedha hizi tutamng’oa. Wako wasomi wengi huko nje tena wazuri tu, wanasubiri kupata ajira.”
 “Nataka watumishi wa umma watambue kwamba Serikali ya Awamu ya Tano inajielekeza kujali wananchi.  Wao wana dhamana ya kuwasilikiliza na kuwahudumia wananchi ili kuhakikisha wanatatua kero zinazowakabili, ” alisema huku akishangiliwa na wengine wakisema huyu sasa ni Sokoine wa pili. (Edward Moringe Sokoine alikuwa ni Waziri Mkuu katika Serikali ya Awamu ya Kwanza).
 Waziri Mkuu ambaye amewasili Lindi leo, aliwaeleza wakazi hao kwamba amekuja kuwashukuru wazee na wana Lindi kwa dua zao na kuwaahidi kwamba hatawaangusha Rais John Pombe Magufuli na Makamu wake Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumpa dhamana ya kuwatumikia Watanzania katika ngazi ya Uwaziri Mkuu.
 Waziri Mkuu pia alimpa kazi Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Jordan Rugimbana ya kuhakikisha anaufufua uwanja huo na kuurudisha kwenye enzi yake ulivyokuwa maarufu katika mikoa yote ya Kusini. “Uwanja huu lazima uboreshwe kwa sababu unanikumbusha mwaka 1984 wakati nachezea timu ya Amri Rangers.  Kulikuwa na ukoka wa nguvu hapa uwanjani. Kwa hiyo timu aliyoiunda Mkuu wa Mkoa itafanya kazi lakini pia iwajumuishe Meya na mbunge wa Lindi Mjini kwa sababu huu uwanja ni mali ya Halmashauri ya Lindi, ” alisema.

Akielezea kuhusu mipango ya Serikali kuendeleza sekta ya viwanda, Waziri Mkuu alisema hivi karibuni mkoa huo utapata wawekezaji kwenye sekta ya gesi baada ya kampuni ya BG kutoka Uingereza kupata umiliki wa eneo la Kikwetu ili wajenge mitambo ya kusafisha gesi.

Aliwataka wananchi wa mkoa huo wawekeze kwenye ujenzi wa hoteli na nyumba za kulala wageni ili ifikapo Agosti mwakani, watu wanaokuja kushiriki maonyesho ya NaneNane kitaifa mkoani humo wasipate taabu ya malazi kama ambavyo imekuwa ikitokea huko nyuma.

WAZIRI UMMY MWALIMU KATIKA ZIARA HOSPITALI YA RUFAA YA BOMBO MKOANI TANGA, KUKAGUA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA LEO

$
0
0
IMG-20151220-WA0012
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akizungumza na mmoja wa wakina mama anayemhudumia mwanae katika wodi ya watoto Hospitali ya rufaa ya Bombo mkoani Tanga alipofanya ziara ya kushtukiza leo mchana Disemba 20, 2015.
IMG-20151220-WA0019
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akimsikiliza mmoja wa akina mama aliyelazwa kwenye wodi ya wazazi wakati wa ziara ya kushtikiza aliyoifanya mchana wa leo Desemba 20, 2015 katika Hospitali ya rufaa ya Bombo mkoani Tanga.
IMG-20151220-WA0011
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akizungumza na mmoja wa wahudumu wa afya (jina lake halikuweza kupatikana kiurahisi) wa dirisha la dawa katika Hospitali ya rufaa ya Bombo mkoani Tanga alipofanya ziara ya kushtukiza mchana wa leo Disemba 20, 2015.
IMG-20151220-WA0017
Daktari aliyekuwa kwenye mafunzo, Dkt. Zuberi (Medical Intern) akitoa maelezo ya namna wanavyohudumia wananchi wanaofika hospitalini hapo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu (kulia) aliyefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya rufaa ya Bombo, mkoani Tanga mchana wa leo Desemba 20, 2015 ambapo Waziri huyo alikutana na changamoto utoro wa madktari wa zamu kutokuwepo kwenye kituo chao cha kazi katika Hospitali ya rufaa ya Bombo, mkoani Tanga.


IMG-20151220-WA0020
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga (RMO), Dkt. Clement Marceli akimwelezea changamoto wanazokabiliana nazo katika Hospitali ya rufaa ya Bombo mkoani Tanga Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu (hayupo pichani).

IMG-20151220-WA0019
Mratibu wa Hospitali ya Rufaa ya Bombo, mkoani Tanga kutoka Idara ya Tiba, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Ibrahimu Maduhu (mwenye tai) akitoa maelezo kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu namna wanavyokabiliana na changamoto ya kuzuia vifo vya mama na mtoto katika hospitali hiyo wakati wa ziara ya kushtukiza iliyofanywa na Mh. Ummy Mwalimu katika wodi ya wazazi leo mchana Disemba 20, 2015.
IMG-20151220-WA0014
Baadhi ya madaktari waliokuwa mafunzoni wakizungumza na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu  aliyefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Rufaa ya Bombo, mkoani Tanga mchana wa leo Disemba 20, 2015.
IMG-20151220-WA0023
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akipitia orodha ya mahudhurio ya zamu za Madaktari na Wauguzi ambao wengi hawakuwepo kazini wakati wa ziara yake ya kushtukiza katika Hospitali ya rufaa ya Bombo, mkoani Tanga aliyoifanya leo mchana Disemba 20, 2015.

KAMPUNI YA ULINZI YA SGA YATOA MSAADA WA MASHINE YA KUPUMULIA NA MASHUKA WODI YA WATOTO MWANANYAMALA

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Ulinzi ya Security Group Africa (SGA), Eric Sambu (kulia) akimkabidhi mshine ya kupumulia na mashuka, Mratibu wa Tiba katika Hospitali ya Mwananyamala, Dk Daniel Nkungu. Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki. Katikati yao ni Meneja Mahusiano kwa wateja wa SGA, Sophia Luhikula.
 Vitu vilivyotolewa msaada Hosipitalini hapo.
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Ulinzi ya Security Group Africa (SGA), Eric Sambu (kulia) akimkabidhi mshine ya kupumulia na mashuka, Mratibu wa Tiba katika Hospitali ya Mwananyamala, Dk Daniel Nkungu. Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja Mahusiano kwa wateja wa SGA, Sophia Luhikula.
 Baadhi ya watumishi wa kitengo cha Ambulance cha SGA 
 Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Ulinzi ya Security Group Africa (SGA), Eric Sambu akizungumza wakati wa kutoa msaada huo.
 Wafanyakazi wa SGA wakibeba msaada huo.
Habari na picha: Father Kidevu Blog

KAMPUNI ya Ulinzi ya Security Group (T) imetoa msaada wa mashine moja ya kupumlia na mashuka 40 kwa wodi ya watoto katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam


Kampuni ya SGA ilikabidhi mashine hiyo ya kupumulia na mashuka vyote vikiwa na thamani ya Sh milioni tano kwa wodi ya watoto Hospitali ya hapo na kusema hiyo ni kuonyesha jinsi gani wana jali afya za watanzania ambao wanafanyakazi nao.


“Nifuraha yetu kuona familia zetu zipo katika afya njema, lakini pia ulinzi wa mali zetu unaenda vizuri, hivyo leo tumeona tujitoe kidogo kukumbuka jamii yetu hasa watoto ambao ndio taifa la kesho,” alisema Mkurugenzi Mkuu wa SGA, Eric Sambu.


Sambu alisema huo ni muendelezo wa kurejesha kile wanachopata kwa jamii ili kujenga mahusiano mazuri na wataendelea kufanya hivyo kila inapo wezekana.


Akipokea msaada huo, Mratibu wa tiba hospitalini hapo, Dk Daniel Nkungu wanaishukuru kampuni hiyo kuwakumbuka na kuweza kuwasaidia msaada huo ambao kwa kiasi kikubwa utasaidia ufanisi katika utendaji kazi wao na kupunguza vifo vya watoto wachanga.

Picha ya pamoja ilipigwa 
 Wafanyakazi wakiwa wameshika mashuka waliyokabidhi.
 Wafanyakazi wa SGA wakirejesha mashuka hayo katika boxi.
 Baada ya hapo wafanyakazi walishiriki katika tafrija fupi ya kufunga mwaka na kusherehekea mwaka 31 tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo nchini ambapo awali ilijulikana kama Group 4. 
 Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Ulinzi ya Security Group Africa (SGA), Eric Sambu akizungumza na wafanyakazi wakati wa tafrija.
 Wafanyakazi wakimsikiliza...
 Waliwasikiliza viongozi wao mbalimbali.
 Wakuu mbalimbali wa vitengo walizungumza...
 wafanyakazi walijumuika pamoja na kufurahi.
 Chakula kizuri kiliandaliwa na watu walikula vya kutosha na kupata vinywaji vya kila namna
Watu walikula chakula na kufurahi,

Rais Magufuli atuma salamu za Rambirambi kufuatia kifo cha Askofu Nkalanga

$
0
0


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU


Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz              

Faksi: 255-22-2113425



OFISI YA RAIS,
      IKULU,
 1 BARABARA YA BARACK OBAMA,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa kufuatia kifo cha Askofu Mstaafu Plasdus Gervas Nkalanga (OSB) kilichotokea Ijumaa tarehe 18 Desemba, 2015 katika hospitali ya Mtakatifu Joseph Peramiho, Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma.

Mhashamu Askofu Nkalanga aliyekua Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba alistaafu uaskofu mwaka 1974 na kujiunga na watawa wabenediktini wamonaki ambapo aliamua kwenda kuishi katika Abasia ya Hanga iliyopo katika Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma.  

Katika salamu zake Rais Magufuli amesema  Askofu Nkalanga aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 96 atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa alioutoa kuhimiza imani na uchapakazi kazi katika kipindi chote cha miaka 54 ya uaskofu wake na utawa wake akiwa katika Abasia ya Hanga.

Amesema Marehemu Askofu Nkalanga ambaye baada ya kustaafu aliamua kuingia katika utawa akianzia katika ngazi ya chini kabisa ya Unovisihadi alipofunga nadhili za milele za utawa mwaka 2009, ameacha mfano mzuri unaohimiza jamii kuishi kwa upendo, unyenyekevu na kutokata tamaa. 

"Kupitia kwako Baba Askofu Ngalalekumtwa napenda kuwapa pole nyingi Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Songea, Abate wa Abasia ya Hanga, watawa na waumini wote wa kanisa Katoliki kwa kupoteza mtu muhimu aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya kanisa na jamii kwa ujumla" amesema Rais Magufuli.

Rais John Pombe Magufuli amemuomba Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya Marehemu Mhashamu Askofu Mstaafu Plasdus Gervas Nkalanga mahali pema peponi, Amina.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
20 Desemba, 2015

Cosota, CMEA kuanza kulipa mirahaba kwa wanamuziki kuanza Januari mwakani

$
0
0
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama Cha Hakimiliki Tanzania (Cosota) Doreen Sinare akielezea umuhimu wa wanamuziki kujisajili kwao kupitia Kampuni iliyopewa jukumu la kuendesha zoezi usajili, Copyrights Management East Africa Limited (CMEA) ilikuweza kupata haki zao kutokana  na kazi zao.
 Mkuu wa Uendeshaji wa kampuni ya CMEA, Abdi Zagar akielezea jinsi ya mfumo wa kisasa wa ukusanyaji taarifa za wanamuziki kwenye vituo vya televisheni na redio kwa ajili ya kutumiwa na Cosota ili kufanya malipo sahihi kwa wanamuziki na wadau wake.
 Mwanamuziki, Barnaba akitoa maada katika semina hiyo iliyoandaliwa na Cosota na CMEA kwa ajili ya kuwapa elimu wanamuziki na wadau wake kuhusiana na malipo ya mirahaba.
 Mkurugenzi wa vipindi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba akijibu moja ya maswali katika semina hiyo. Mutahaba aliwahamasisha wanamuziki kujisajili CMEA kwa lengo la kupata haki  kutokana na kazi zao.
 Wanamuziki wa muziki wa dansi, Chalz Baba na Jonico Flower wakifuatilia semina hiyo ambayo iliwapa somo kuhusiana na umuhimu wa kujisajili kupitia kampuni ya CMEA na Cosota ili kufaidika na kazi zao.
Afisa Mtendaji Mkuu wa CMEA, Paul Matthysse akifafanua jambo kuhusiana na faida za wanamuziki na wadau wake mara baada ya kujisajili na kuanza kulipwa fedha zao.

Chama cha Hakimiliki Tanzania (Cosota) kwa kushirikiana na kampuni ya kusimamia kazi za wanamuziki nchini Copyrights Management East Africa Limited (CMEA) wataanza kulipa mirabaha ya wanamuziki na wadau wake kuanzia mwakani.

 Afisa Mtendaji Mkuu wa Cosota, Doreen Sinare alisema kuwa wanamuziki, watunzi na ma’producer’ watalipwa asilimia 60 kwa kila wimbo au video itakayochezwa katika redio na televisheni yoyote ndani na nje ya nchi kwa kutumia vifaa bora vilivyowekwa na kampuni ya CMEA.

Doreen alisema kuwa manamuziki, msanii alitakiwa kupata asilimia 70 ya kazi yake, lakini asimilia 10 itakatwa katika malipo hayo na kuingia katika mifuko ya jamii kwa mahitaji yake ya baadaye.

Alisema kuwa wanamuziki ni sawa na wafanyakazi wengine na asilimia 10 hiyo itamwezesha kujipatia kipato chake kama ilivyo kwa wafanyakazi wengine katika taasisi mbalimbali.

Kwa mujibu wa Sinare alisema kuwa ili kuhakikisha kila mwanamuziki  anafaidika na kazi yake, watashirikiana na vyama vingine vya Hakimiliki katika nchi mbali mbali kwa kutumia hati ya malipo zinazotokana na bei za matangazo kwa televisheni na vituo vya redio.

Alisema kuwa Cosota na CMEA pia watawapa ushirikiano vyama hivyo ili nao waweze kupata haki za malipo ya wanamuziki wao kwa vituo vya televisheni na redio vitakavyotumia kazi za wanamuziki wa nje.

“Lengo la Cosota na CMEA ni kuona wasanii wanafaidika na kazi zao, mirabaha ya kwanza tutaanza kulipa Januari 2 na kwa sasa tupo katika hatua za mwisho kukamilisha jinsi tutavyolipa, ndiyo maana tumetoa semina kwa wanamuziki, lengo ni kuwahamasisha kujisajili,” alisema Sinare.

Afisa Mtendaji Mkuu wa CMEA, Paul Matthysse alisema kuwa mbali ya wanamuziki, kampuni yao itawawezeha pia watayarishaji wa muziki na wasanii wengine pamoja na vyombo vya habari kupata kufahami takwimu sahihi za nymbo zilizochezwa kwa siku, wiki, mwezi na kwa mwaka.

Matthysse alisema kuwa kampuni yao imewekeza mitambo ya kisasa inayowezesha kuchapisha na kuhakiki nyimbo pindi zinapochezwa hewani na televisheni na redio na kutoa ripoti za aina mbalimbali zinazohitajika kutumika kwa malengo maalum.

“Pia tunapokea na kuhifadhi nyimbo kwenye mitambo maalum kwa matumizi ya uhakiki, na kudhibiti kiasi cha mirabaha ambacho Cosota kupitia vyombo vya habari inatakiwa kuwalipa wasanii kulingana na idadi kamili ya urushwaji wa kazi zao,” alisema Matthysse.

Alisema kuwa wanamuziki na wasanii wengine ambao hawatakuwa na usajili, watakosa haki zao pamoja na CMEA kuendelea kurekodi kazi zao zinazochezwa katika redio na televisheni mbali mbali. “Ni muhimu kwao kujisajili, kutojisajili ni kupoteza haki zao zinazotokana na kazi yako,” alisisitiza.

SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LATANGAZA KUSAMBAZWA KWA BOEING 787S KWA SAFARI ZAKE MWAKA 2016

$
0
0
SHIRIKA la ndege la Etihad, ndege rasmi ya taifa kwa Falme za kiarabu limetangza kuanzisha mipango ya kurusha ndege aina ya boeing 787s kwa safari za kwenda Dusseldorf, Perth, Shanghai, Istanbul na Johannesburg kwa mwa mwaka 2016.

Matarajio ya kuwasili kwa ndege hizo mpya aina ya Boeing 787s ni ndani ya miezi saba ijayo, kuanzia Mei 2016, ndege hizo “Dreamliners” zenye uwezo wa kubeba abiria 299 zitaanza kutoa huduma kwenda Dusseldorf, Perth, Shanghai, Istanbul na Johannesburg kutoka Abu Dhabi zikichukua nafasi ya ndege zinazotumika sasa.

Kwa sasa Shirika la ndege la Etihad lina ndege tano tu aina ya 787s ambazo zinafanya safari zake kati ya Brisbane, Washington, Singapore na Zurich moja kwa moja kutoka Abu Dhabi. 

Matarajio ya Shirika hilo ni kuongeza zaidi ya Boeing 66 ndani ya miaka kadhaa ijayo ambapo ndege hizo aina ya “Dreamliners”zitakuwa ndege rasmi za shirika hilo kwa masafa marefu.

James Hogan, ambaye ni Rais na afisa mkuu wa shirika la ndege la Etihad alisema: “Tangu kuanzishwa kwa ndege aina ya 787 ya kwanza katika huduma za kibishara mnamo februari mwaka huu, tumekuwa tukipata maoni mazuri kutoka kwa abiria wetu  ambayo yamekuwa kama alama ya ubora wa hali ya juu katika kanda na dunia nzima.

“Kuanzia mwezi Mei mwakani, shirika la ndege la Etihad litazindua ndege mpya Boeing 787 aina ya dreamliners zitakazotumika rasmi badala ya hizi zilizopo kwa safari za masafa marefu ambapo zitatoa fursa kwa abiria wetu kupanda ndege za teknolojia mpya.

“Abiria na wateja wetu wa siku hizi wanapenda kusafiri bila kero wala pirika pirika kwenye usafiri wa viwango vya juu, wanataka chaguo zuri zaidi na bei nafuu. Hivi ndivyo vigezo vyao vikuu katika kuchagua na sisi hapa Etihad tunajitahidi kufikia matarajio hayo kwa tafiti na uvumbuzi wa aina mbalimbali kama vile kuleta ndege mpya na kuendelea kuboresha njia zetu za usafiri.


Ndege hizi mpya aina ya 787-S zitajumuisha ubunifu wa ndani ya kabini 28 za “business studios” na siti 271 za “economy smart” zikiwa na utulivu, burudani na uwezo wa kuunganishwa kwa mawasiliano zikiwa angani. 

Upambaji wa ndani na mwanga vimesukwa zaidi kwa ubunifu wa kiarabu zikiendana na ubunifu mpya wa kutoka “Abu dhabi” ulioletwa na shirika la ndege hili katika uzinduzi mpya mwaka jana.
Ratiba ya Boeing 787 kwenda DUSSELDORF, kuanzia Mei mosi 2016 (muda wa Abu Dhabi):
Ndege Na.
Inaanzia
Inaondoka
Itawasili
Muda wa kufika
Mizunguko
EY0023
Abu Dhabi (AUH)
02:15
Dusseldorf (DUS)
07:20
Kila siku
EY0024
Dusseldorf (DUS)
11:50
Abu Dhabi (AUH)
20:25
Kila siku

Ratiba ya Boeing 787 kwenda PERTH, kuanzia Juni Mosi 2016 (muda wa Abu Dhabi):
Ndege Na.
Inaanzia
Inaondoka
Itawasili
Muda wa kufika
Mizunguko
EY0486
Abu Dhabi (AUH)
22:25
Perth (PER)
13:50 siku inayofata
Kila siku
EY0487
Perth (PER)
15:40
Abu Dhabi (AUH)
23:10
Kila siku



Ratiba ya Boeing 787 kwenda SHANGHAI, kuanzia Agosti Mosi 2016 (muda wa Abu Dhabi):
Ndege Na.
Inaanzia
Inaondoka
Itawasili
Muda wa kufika
Mizunguko
EY0862
Abu Dhabi (AUH)
21:55
Shanghai (PVG)
11:10 siku inayofata
Kila siku
EY0867
Shanghai (PVG)
00:30
Abu Dhabi (AUH)
06:25
Kila siku
  
Ratiba ya Boeing 787 kwenda ISTANBUL, kuanzia Agosti 1 2016 (muda wa Abu dhabi): 
Ndege Na.
Inaanzia
Inaondoka
Itawasili
Muda wa kufika
Mizunguko
EY0097
Abu Dhabi (AUH)
09:05
Istanbul (IST)
13:10
Kila siku
EY0096
Istanbul (IST)
14:25
Abu Dhabi (AUH)
20:00
Kila siku
  
Ratiba ya Boeing 787 kwenda JOHANNESBURG, kuanzia Novemba Mosi 2016 (muda wa Abu Dhabi):
Ndege Na.
Inaanzia
Inaondoka
Itawasili
Muda wa kufika
Mizunguko
EY0604
Abu Dhabi (AUH)
10:00
Johannesburg (JNB)
16:40
Kila siku
EY0603
Johannesburg (JNB)
19:40
Abu Dhabi (AUH)
06:00 next day
Kila siku


MAITI ZALAZWA SAKAKFUNI HOSPITALI YA MAFINGA

$
0
0
Udogo wa chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Mafinga yalazimu wahudumu wa hospitali hiyo kulaza maiti sakafuni.

TSHABALALA AKABIDHIWA TUNZO YA MCHEZAJI BORA WA MWEZI SIMBA SPORT CLUB

$
0
0
Katika kuongeza morali na kuwazawadia wachezaji wanaofanya vizuri, Klabu ya Simba ilianzisha Tunzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi kuanzia mwezi wa Septemba 2015.
Mshindi wa mwezi wa Oktoba, 2015 ni Mohamed Hussein Tshabalala ambapo amepata kura nyingi zaidi zilizopigwa na mashabiki na wapenzi wa Simba na soka wa Tanzania kwa ujumla kupitia simu za mkononi ambao pia wamejiunga na huduma ya Simba News.
Akikabidhiwa tunzo pamoja na pesa taslim Tsh 500,000/= na Mwanachama na Shabiki wa Simba Mbunge wa Busega Simiyu Mh. Raphael Chegeni, beki wa kushoto Mohamed Tshabalala alisema “tangu nilipotata taarifa za kushinda tunzo ya mchezaji bora kwa mwezi wa 10 nilifurahi sana na leo furaha yangu inazidi zaidi, kwanza napenda kumshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuwa mchezaji na kuweza kushinda tunzo hii, pili kuushukuru Uongozi na wapenzi wa Simba walioona mchango wangu kwenye kikosi cha Simba na kunipigia kura kwa wingi na mwisho napenda kushukuru familia yangu pamoja na watu wangu wote wa karibu ambao wamekuwa mchango mkubwa kwenye mafanikio yangu ya soka”. Ninachoweza kuwaahidi ni kuwa kamwe sitowaangusha kwani tunzo hii itakuwa chahu katika mafanikio yangu aliongeza Tshabalala.

Mwanachama na Shabiki wa Simba Mh. Chegeni alisema “kwanza kabisa nashukuru kwa Simba kunipa heshima ya kuweza kuwa mgeni rasmi katika kutoa tunzo hii kwa Tshabalala, napenda kumshauri Tshabalala na wachezaji wetu wengine kuendelea kujituma kwa bidii kwa ukiweka nidhamu, kujituma na kufanya kazi kwa bidii ni lazima mafanikio utayapata”.
Akizungumza leo jijini Dar es salaam Rais wa Simba Evans Aveva alisema “Uongozi, wanachama na wapenzi wa Simba wanathamini mno mchango wa wachezaji katika kuifanya timu yetu ifanye vizuri, hivyo tumeona ni jambo la busara kuwa klabu ya kwanza Nchini Tanzania kuwa na tunzo za mchezaji wake bora. Tunaamini kuwa Tunzo ya Mchezaji bora wa mwezi wa Simba itaongeza ari na kujituma kwa wachezaji wetu. Sisi tukiwa kama viongozi ni kazi yetu ya msingi kuhakikisha kuwa wachezaji wetu hasa wale wanaojituma zaidi wanatambuliwa na kuenziwa’’.
Akizungumza jinsi tunzo ya mchezaji bora itakavyoendeshwa, Mkurugenzi Mkuu wa EAG Group ambao ni washauri na watekelezaji wa Masoko na Biashara wa Simba, Imani Kajula alisema “Wanachama na wapenzi wa Simba na wapenda michezo ndio watakao kuwa wanachagua mchezaji bora wa mwezi kwa kutuma jina la mchezaji wanayempendekeza kwenda kwenye namba 15460, Ni wale tu ambao wamejiunga na Simba News kupitia mtandao wa Vodana Tigo wataweza kupiga kura kuchagua mchezaji bora wa mwezi wa Simba’’
Tukumbuke kuwa unaweza kumchagua mchezaji bora wa mwezi ukiwa umejiunganisha na huduma ya Simba News kwa kutuma jina la mchezaji kwenda namba 15460. Zoezi la kumchagua mchezaji bora wa mwezi wa October, 2015 linaanza tarehe October 10, 2015. Piga kura mara nyingi zaidi kuweza kumpata mchezaji wako bora wa Mwezi October, 2015.
Simba News ni huduma iliyoanzishwa na Simba ili kuwapa wapenzi wa Simba habari mbalimbali za Simba popote pale walipo ikiwemo matokeo, majina ya wachezaji wanaocheza mechi, usajili na habari nyingine za klabu ya Simba. Kujiunga na Simba News tuma neno Simba kwenda namba 15460 ni maalum kwa Tigo na Vodacom.

WAZIRI APIGA MARUFUKUWAHANDISI 'UCHWARA' KUPEWA TENDA ZA UJENZI WA BARABARA

$
0
0
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani (kushoto), akitoa maagizo mbalimbali kwa uongozi wa Bodi ya Mfuko wa Barabara nchini, alipotembelea bodi hiyo, Dar es Salaam juzi, kujua utendaji wake. Kulia ni Meneja wa bodi hiyo, Joseph Haule. (HABARI,PICHA NA RICHARD MWAIKENDA-KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
 .Mhandisi Edwin Ngonyani

Na Richard Mwaikenda
NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani, amepiga marufuku kwa Halmashauri zote nchini, kuwatumia wajenzi wa barabara wasiosajiliwa na Bodi ya Wahandisi nchini (ERB).

Mhandisi Ngonyaji alichukua hatua hiyo alipofanya ziara ya kujua utendaji wa Bodi ya Mfuko wa Barabara nchini, Dar es Salaam juzi, ambapo alielezwa na Meneja wa Bodi hiyo, Joseph Haule, kuwa barabara nyingi kwenye halmashauri zinajengwa chini ya viwango kwani wanaopewa tenda hawana utaalam wa ujenzi wa barabara. 

Alisema kuwa, kuanzia sasa halmashauri ziachane kabisa  kuwatumia mafundi wasio na utaalam, bali wawatumie wahandisi waliosajiliwa na Bodi ya Wahandisi nchini, ili barabara zijengwe kwa viwango vinavyotakiwa, na watakaokaidi agizo hilo wanyimwe fedha za mgao kutoka kwenye bodi hiyo.

Pia , Mhandisi Ngonyani, ameitaka bodi hiyo, kutokutuma fedha  za  ujenzi wa barabara kwa halmashauri yoyote ambayo imetumia fedha walizopelekewa na kuzitumia kinyume cha malengo yaliyokusudiwa.


Amemwagiza Meneja wa Bodi hiyo, kuzichukulia hatua halmashauri zote ambazo zimetumia fedha hizo tofauti na malengo yake ikiwa ni pamoja na kutopelekewa fedha  hadi hapo watakapoziresha walizozitumia.

"Ongezeni nguvu zaidi katika kusimamia matumizi ya fedha za mfuko wa barabara kwa halmashauri ambazo fedha hizo zinatumiwa kwa shuguli zisizo za barabara", alisisitiza Mhandisi Ngonyani.

Naye Meneja wa Bodi ya mfuko huo, Joseph Haule, alielezea mafanikio ya mfuko huo tangu ianzishwe  miaka  15 iliyopita kwamba kuwa mapato yameongezeka kutoka sh. bilioni 73 mwaka 2005 hadi sh bilioni 752.

"Kutokana na kupanda kwa mapato mtandao wa barabara umeboreshwa kwa kiwango kikubwa kwa kuwa barabara nyingi zimejengwa kutokana na kipato hicho", alisema Meneja Haule.


Aidha, Meneja wa Bodi ya mfuko huo, Haule, alisema kuwa  mfuko huo ambao chanzo chake kikubwa ni ukusanyaji wa fedha kutoka sehemu ya mauzo ya mafuta ya petroli na dizeli nchini, Bodi italitia mkazo katika ufuatiliaji wa matumizi ya mfuko kuhakikisha vyanzo vipya vya mapato vinapatikana.

Alisema kuwa, katika kuhakikisha ufuatiliaji wa usimamizi wa fedha hizo unatekelezwa, mfuko tayari umezichukulia hatua halmashauri tatu zikiwemo za Kinondoni, Songea Vijijini na Bukoba Vijinini ambazo zimetumia fedha za mfuko wa barabara kinyume na malengo yaliyokusudiwa.

Alisema Bodi ya Mfuko wa Barabara ilianzishwa kwa lengo la kukusanya mapato, kufuatilia matumizi ya fedha hizo na kugawa kwenye taasisi ambapo asilimia 63 zinapelekwa Wakala wa Barabara wa Serikali (Tanroads) kwa ajili ya matengezo barabar kuu na za mikoa, asilimia 30 katika halmashauri 166 kwa ajili ya ujenzi wa barabara za halmashauri na asilimia 7 zinapelekwa wizara ya ujenzi



 Meneja wa Bodi ya Mfuko wa Barabara, Joseph Haule akijibu baadhi ya hoja.
Naibu Waziri, Mhandisi Ngonyani akisisitiza jambo katika mkutano huo.

JAMII YETU IKO MIKONONI MWETU

$
0
0

Mratibu wa Vijana, Bahati Juma (wa kwanza kulia) akiwa na wanafunzi wa darasa la saba, shule ya Msingi Uchunga, kupitia pamoja somo la kiswahili kituoni hapo.
Mabadiliko katika jamii yoyote kwa kiasi kikubwa huchangiwa na ongezeo la mahitaji ya binadamu katika mambo mbalimbali. Kwamba, kadri dunia inavyopitia mabadiliko, kadiri ile ile changamoto, mahitaji na huduma katika jamii husika huongezeka. Ili kufikia malengo yanayotokana na misukumo na mageuzi yasiyokwepeka, binadamu amelazimika kubuni mikakati mbalimbali ya maendeleo. Si hivyo tu, mabadiliko haya yamemfungulia binadamu fursa ya uthubutu wa kujaribu mambo mbalimbali, siyo tu kwa faida yake, bali jamii nzima inayomzunguka.

"Sikutegemea kama siku moja katika maisha yangu nitapata wazo ambalo lingebadili na kushawishi watu kuchukua hatua kwa mustakabali wa jamii.” 

Hiyo ni kauli ya mraghbishi Revocatus Richard ambaye pia, kitaaluma ni mwalimu katika shule ya msingi Uchunga. Richard alitoa kauli hiyo baada ya kupitia mafunzo ya uraghbishi na mwalimu mwenzake, Restusta Katobesi, ambao  baadaye kwa pamoja, walianzisha Kituo cha KIMAJU (Kituo cha Maendeleo cha Jamii ya Uchunga) kwa kushirikiana na uongozi wa kijiji na wananchi. Na hilo ndiyo lilifanya achaguliwe kuwa Mkurugenzi wa kituo hicho. 

 Hivi ni baadhi ya vitabu na majarida ambayo yapo katika maktaba ya kituo hicho.
Walimu hao walikuwa miongoni mwa waraghbishi 30 walioshiriki mafunzo ya uraghbishi yaliyotolewa mwezi Machi, mwaka 2012 wilayani Kishapu katika mkoa wa Shinyanga. Kutokana na faida na maarifa waliyoyapata kwenye mafunzo hayo, walimu hao waliamua kuunda umoja uliokuwa chachu ya kuanzishwa kituo hicho cha maendeleo.

Mwanazuoni Sarah Earl, aliwahi kusema: "Maendeleo ni watu na mazingira yao. Kwamba, kusingekuwa na maana iwapo barabara, hospitali, shule na miradi mingine ya  maendeleo inayojengwa kwa ajili ya watu isingetumika." Mraghbishi ni mwananchi anayeleta uhai mpya ndani ya jamii kwa kutambua matatizo na kupendekeza njia sahihi za kuyatatua. 

Kulikuwa na uraghbishi katika kijiji cha Uchunga ambapo baada ya kupatiwa mafunzo ya uraghbishi, walimu hawa walirudi kijijini kwao wakiwa na jukumu moja la kutambua changamoto zinazoikabili jamii yao na kupendekeza nini kifanyike wakitumia nafasi na uwezo walio nao. Kikubwa walichoangalia ni mustakabali wa mtoto wa Kijiji cha Uchunga, kwa maana ya nafasi ya mtoto, ikiwamo ya kufahamu huduma anazopata. Katika kufikiria sehemu ya kuanzia na ili kumpa mtoto wa kike nafasi katika jamii, hasa ya kuongoza, walianza na wanafunzi wa shule wanayofundisha, Uchunga.



Baadhi ya wananchi na wajumbe wa Kituo cha Maendeleo cha Uchunga wakiwa mbele ya kituo kabla hakijaezekwa na mabati.
“Nimepata bahati ya kuwa mwalimu mkuu msaidizi mara kadhaa na nimetumia fursa hiyo kuleta mabadiliko, nikianzia kubadilisha utaratibu wa kuchagua viongozi wa wanafunzi katika shule yetu," alisema Richard na kuongeza: "Kwanza tulibadilisha wazo la Kaka Mkuu na badala yake tukasema tutakuwa na Kiranja Mkuu, ili kutoa fursa kwa wanafunzi wa kike kushika nafasi za uongozi wa wanafunzi." Hadi sasa chaguzi mbili za kidemokrasia za kuchagua viongozi wa wanafunzi zimefanyika shuleni Uchunga Julai 2012 na Mei 2013. Katika kuhakikisha wanaendeleza mawazo hayo, waraghbishi hao walikuja na wazo la kujenga kituo cha kujisomea. Walianza kuwatembelea wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Uchunga wanaoishi katika kijijini hapo.  

Ili kufikia malengo yao, waliomba ushirikiano, siyo tu kwa walengwa ambao ni wanafunzi, bali kutoka kada zingine ndani ya jamii.

 Haya ndio mazingira ya kituo cha maendeleo ya jamii kilichopo Kijiji cha Unyeyembe kata ya Uchunga wilayani Kishapu mkoani Shinyanga
Akielezea jinsi walivyoanza, mraghbishi Katobesi alisema: “Tulikutana na wanafunzi na kuunda umoja wa kikundi wa Wanafunzi wa Sekondari Uchunga (UWASU).  Kikundi hiki kiliamsha hamasa kwa wanafunzi waliokukubali kujitolea kufanya kazi.”Na baadhi ya wanafunzi hao wametembelea shule nyingine na kuhamasisha wenzao kujitolea kusaidia kazi mbalimbali kama  kuchota maji na kuokota mawe kwa ajili ya ujenzi wa  jengo la kituo hicho cha kujisomea.  Ndani ya jamii yoyote kuna mamlaka, hivyo ili malengo yao yatimie kuliwalazimu waraghbishaji hao kupata ruhusa kutoka kwa walimu na aliyekuwa mwenyekiti wa kijiji wakati huo, Mahona Punguja.

“Baada ya kutoka kwenye mafunzo yao, walikuja kuzungumza na mimi kuhusiana na mambo waliyojifunza na jinsi watakavyoleta mabadiliko. Nilikubaliana nao na kuweka utaratibu wa kuwashirikisha wazazi kama wadau muhimu na makundi mengine maalumu,” alisema Punguja. Makundi maalumu ni pamoja na watumishi wa uma, kwa maana ya walimu na mtendaji wa kijiji na kata, wazee maarufu, viongozi wa dini, vijana na wajumbe wa halmashauri ya serikali ya kijiji. Waraghbishi hawa kwa ushirikiano na uliokuwa uongozi wa serikali ya kijiji waliweza kukutana na makundi hayo ili kuwaelimisha kuhusu wazo la kituo cha kujisomea. Baada ya kila kundi kukutana na waraghbishi, uliitishwa mkutano wa pamoja wa kujadili jambo hilo na kamati  ikaundwa ya kusimamia mchakato mzima. Kamati hii ilichaguliwa kwa kila kundi kuwa na mwakilishi wake. 
 Mmoja wa wanafunzi wa kijiji cha Unyenyembe akiwa anasoma gazeti ili kujua yaliyojili kutoka sehemu mbalimbali Tanzania na Dunia kwa ujumla.

“Njia ya kwanza ilikuwa ni kukusanya fedha, kisha kuwaomba wananchi kuchangia nguvu zao. Kila mmoja kwa nafasi yake alijitolea. Wengine tulisomba mawe na kuchimba msingi.  Wanawake walileta vyakula kwa ajili ya mafundi ambao nao walijitolea pia utaalamu wao bure”, anaelezea Michael Butu, Mwenyekiti wa Kituo cha KIMAJU. Wanajamii waliohamasika waliombwa kuchangia kila mmoja Shilingi 10,000 za Kitanzania, ingawa baadhi walitoa nusu ya mchango huo. Kila kitongoji kiliombwa kuchangia Shilingi 60,000. Michango hii ilikusanywa baada ya kuundwa kwa nguvu ya pamoja na wenyeviti wa vitongoji. Kati ya vitongoji vitatu, viwili vilikamilisha ahadi zao.

Harakati hizi ziliwezesha wanajamii kujenga kituo hadi ngazi ya linta, kabla ya mlezi wa kituo hicho, Charles  Dida kutoa shilingi 355,000 kama mkopo kwa ajili ya  kununua mabati na mbao. “Nilipoona jengo letu linasuasua, niliamua kujitolea kufanikisha ujenzi. Niliamua kumshirikisha mke wangu, ambaye aliunga mkono uamuzi wangu kwa kujua mafanikio yatakayopatikana ni ya jamii nzima,” alisema Charles Dida. Katika hili tumejifunza mahusiano yaliyopo baina ya baba na mama katika kufanya maamuzi ya pamoja. Ni tofauti na mfumo dume uliozoeleka katika jamiii ya kisukuma. Na mpaka sasa kituo kimeweza kulipa kiasi cha Shilingi 110,000 na hivyo bado kinadaiwa Shilingi 245,000. 

Baadhi ya wanakijiji wakiwa katika mkutano wa pamoja eneo la kituo cha maendeleo cha Jamii katika kijiji cha Unyenyembe.

Ili kuhakikisha kituo kinaendelea kutoa huduma kwa watoto wa Uchunga wajumbe wa kamati tendaji wanafanyakazi kwa kujitolea kwa kuwa wao kuwa sehemu ya jamii ya wananchi wa kijiji cha Uchunga. “Nilihamasika baada ya kupendezwa na wazo la kuanzishwa kwa kituo hiki. Na siku nilipoombwa kuwa sehemu ya kuleta mafanikio, nilikubali mara moja na kushiriki mikutano na ratiba nyingine,” alifafanua katibu wa vijana, Bahati Juma. Moja ya majukumu aliyokabidhiwa ni huhakikisha kituo kinafunguliwa saa mbili asubuhi na kufungwa saa 10 jioni. Kwa wastani, kituo kinahudumia wanafunzi 20 kwa siku.  Mbali na katibu huyo, watendaji wengine ni pamoja na mkurugenzi, katibu, mhasibu, na kamati tendaji chini ya mwenyekiti na mlezi wa Kituo. Nafasi hizi zote zina wasaidizi isipokuwa ya mkurugenzi na mlezi.
Watendaji wa Kituo cha Maendeleo cha Jamii ya Uchunga wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi mbele ya jengo la kituo hicho likiwa limekamilika kutokana na michango yao ya fedha na nguvu kazi.

Uongozi huu ulipatikana kidemokrasia kwa kuchaguliwa kwenye mkutano mkuu wa kijiji. Baada ya kupata uongozi walitengeneza katiba na kukisajili kituo chao. Kwa mujibu wa katiba ya kituo hicho, uongozi unachaguliwa kila baada ya miaka mitatu.  “Waasisi wa kituo ndio waliopendekeza mfumo wa uongozi na baada ya hapo wakauwakilisha kwenye mkutano mkuu wa kijiji. Kwa hiyo walioweza walishiriki. Na kila mtu aliyeona anafaa kuwa sehemu ya uongozi wa kituo hicho alipendekeza jina lake ama la mwenzake. Baada ya majina hayo kupatikana ndipo yalipigiwa kura na kupata viongozi,” anafafanua mwenyekiti wa kituo, Michael Butu.  Tukiachilia suala la uongozi, kuna utaratibu maalumu wa kuendesha kituo hicho. Kuna vijana wanaohusika na kuhakikissha ofisi inafunguliwa ili kutoa huduma za kujisoma bure, ikiwa ni mkakati wa kuhamasisha watu na kukifahamu kituo.

Taasisi hii ya kijamii kwa kiasi kikubwa imelenga kwenye uzalishaji maarifa kwa kutoa huduma ya maktaba, ambayo wanafunzi wanaoishi kijiji cha Uchunga hutumia kusoma na kufanya kazi za nyumbani baada ya masomo shuleni. Katika ziara za ufuatiliaji na uwezeshaji, wafanyakazi wa shirika mtendaji la TAMASHA katika mradi huo wa Chukua Hatua, walishauri kituo kupanua wigo wa huduma zake, kama anavyoelezea Afisa Mradi Winston Churchill.

“Tuliwashauri kuwalenga pia vijana walio nje ya shule ili kuwawezesha vijana wote kutumia kituo hicho vizuri kijijini hapo.” Watu wazima pia wanatumia kituo hicho kujisomea magazeti, ambayo huwa ni ya siku nyingi na hii ndio sababu ya umuhimu wa kutafuta redio ili watu wasikilize taarifa za habari.  Hali hii imehamasisha wanafunzi wa shule za sekondari na msingi kuja kujisomea, kama anavyoelezea mwanafunzi wa darasa la saba Leticia Isaka kutoka Shule ya Msingi Uchunga.

“Kituo kinanisaidia kutambua mambo mbalimbali, kwa mfano kupitia mafunzo ya hapa, napata malezi bora ya kuniandaa niwe mwalimu au daktari. Lakini si hivyo tu, wakati wa mapumziko ya saa sita huwa tunakuja kujisomea hapa baada ya kupatiwa mazoezi na walimu shuleni,”  "Mbali na mafanikio haya, kituo kina changamoto kadhaa ikiwamo ukosefu wa meza, viti na makabati ya kuhifadhia vitabu," anasema mkurugenzi wa kituo, Richard na kuongeza: “Haya mabenchi na meza tumeazima kanisani na tukimaliza tunarudisha sehemu husika. Hatuna vitabu vya mitaala kwa ajili ya wanafunzi wetu, ingawa eneo la kujisomea lipo vizuri, nishati ya umeme nayo ni shida.” 
Kimsingi, wanajamii wa Uchunga kwa kushirikiana na waraghbishi na uongozi kwa kijiji wamefanikiwa kufikia malengo. Ni dhahiri kwamba wana safari ndefu, lakini itoshe kusema kwamba kituo kinaweza kutimiza dhamira yake ya kuzalisha fedha za kujiendesha chenyewe. Tuendelee kuwaunga mkono katika hizi harakati zao.

WAZIRI MKUU AONYA KUHUSU CHAKULA CHA MSAADA

$
0
0
KOMONI
*Apiga marufuku mahindi ya msaada kutengenezea pombe
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepiga marufuku chakula cha msaada kutumiwa kutengeneza pombe za kienyeji na kwamba atakayekamatwa atachukuliwa hatua za kinidhamu.
 Ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwa nyakati tofauti kwenye mikutano ya hadhara iliyofanyika leo (Jumatatu, Desemba 21, 2015) kwenye vijiji vya Nangurugai, Machang’anja na Narungombe katika kata za Mbwemkuru na Narungombe wilayani Ruangwa, mkoani Lindi.

Waziri Mkuu alikuwa akijibu hoja za diwani wa Narungombe, Bw. Rashid Nakumbya aliyetoa ombi la kuongezewa chakula cha msaada kwa sababu wana hali mbaya. Alisema msimu uliopita haukuwa mzuri kiuzalishaji kutokana na hali mbaya ya hewa. Pia aliomba wasaidiwe kuboreshewa huduma za maji safi na salama.“Natambua kuwa kuna tani 2,000 za chakula zimeletwa katika mkoa wetu lakini hizo hazitoshi kwa sababu mahitaji yetu ni zaidi ya tani 5,000. Chakula hiki hakitoshi kwa sasa lakini kitasaidia kupunguza makali ya njaa,” aliwaeleza wakazi hao.

“Tumepiga marufuku kutumia chakula cha msaada kupikia pombe. Mwananchi atakayekutwa akitumia chakula hicho, atachukuliwa hatua za kinidhamu,” alisisitiza. Alitumia fursa hiyo kuwahakikishia kauli ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kwamba hakuna mwananchi atakayekufa kwa njaa. “Mheshimiwa Rais ameahidi kuwa hakuna Mtanzania atakayekufa kwa njaa. Tuna mahindi ya kutosha kwenye maghala ya Songea, Dodoma na Makambako lakini changamoto ni namna ya kuyasafirisha kutoka huko hadi kuyafikisha huku. Tunaendelea pia kupeleka misaada kwenye mikoa mingine,” alisema Waziri Mkuu.

Akijibu hoja nyingine zilizotolewa, Waziri Mkuu ambaye pia ni mbunge wa jimbo hilo alisema anatambua changamoto walizonazo za ukosefu wa maji safi, ubovu wa barabara, zahanati na nyumba za waganga na kwamba ameanza kuzishughulikia.“Hivi sasa nimeanza kushughulikia suala la uwekaji wa nishati ya umeme wa jua kwenye shule za msingi na zahanati. Mtaalam ameshafika hapa wilayani kwetu na ameanza hiyo kazi, na hivi karibuni mtamuona akifika maeneo ya huku,” alisema.

Kuhusu maji safi na salama, Waziri Mkuu aliwaeleza wakazi hao kwamba tatizo la maji analijua na kwamba changamoto kubwa waliyonayo ni upatikanaji wa chanzo cha maji baridi kwani kiasi kikubwa eneo hilo lina vyanzo vya maji yenye chumvi. “Wataalamu wanakuja kutafuta chanzo cha maji baridi kwa sababu asilimia kubwa ya eneo hili maji yake yana chumvi,” alisema.

Aliwataka wakazi hao waendelee kuwaombea yeye pamoja na Rais Magufuli na Makamu wake, Samia Suluhu Hassan ili waweze kutimiza malengo waliyoahidi kwa Watanzania wakati wa kampeni.

WAZIRI KITWANGA AKUTANA NA VIONGOZI WAKUU WA JESHI LA POLISI, WAWEKA MKAKATI WA KUKABILIANA NA UHALIFU NCHINI

$
0
0
NGA2
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akitoa taarifa mbalimbali za shughuli zinazofanywa na jeshi hilo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati), wakati Waziri huyo alipofanya ziara Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuzungumza na Viongozi Wakuu wa jeshi hilo, ambapo walikubaliana kuweka mikakati zaidi ya kukabiliana na uhalifu nchini.
NGA3
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kumaliza mazungumzo na Viongozi Wakuu wa Jeshi la Polisi nchini. Waziri Kitwanga aliwaambia waandishi wa habari kuwa, wamekubaliana na Viongozi Wakuu wa jeshi hilo kuweka mikakati zaidi ya kukabiliana na uhalifu nchini. Wapili kushoto meza kuu ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu.

 Wapili kulia meza kuu ni Naibu IGP, Abdulharam Kaniki. Kulia ni Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi hilo, Paul Chagonja. Kushoto meza kuu ni Kamishna wa Polisi Jamii nchini, Mussa Ali Mussa. Kushoto ni Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova.
NGA4
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati waliokaa), Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu (watatu kulia waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wakuu wa Jeshi la Polisi nchini mara baada ya kikao chao kilichofanya katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi hilo kumalizika. Waziri Kitwanga alifanya mazungumzo na Viongozi hao na kukubaliana kuweka mikakati ya kupambana na uhalifu.
NGA5
Msafara wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga ukiwasili katika lango Kuu la Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Viongozi Wakuu wa Jeshi hilo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
NGA1
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu wakati alipokuwa anawasili Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam kwa ziara ya kikazi. Waziri Kitwanga alifanya mazungumzo na Viongozi Wakuu wa jeshi hilo na kukubaliana kuweka mikakati zaidi ya kukabiliana na uhalifu nchini. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

JIPATIE TIKETI YA BURE SHOO YA DIAMOND KRISMASI

$
0
0
DIAMOND (4) Staa wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz.
UNATAKA kwenda shoo ya Diamond, Krismasi hii? Kama ndiyo, sasa unaweza kujipatia tiketi ya bure kwenda kwenye shoo hiyo kwa kujibu maswali katika Gazeti la Uwazi kesho Jumanne pamoja na Risasi Mchanganyiko siku ya Jumatano. DIAMOND (3) 
Jinsi ya kushiriki, nunua gazeti lako la Uwazi au Risasi Mchanganyiko kisha jibu maswali kiufasaha ndani ya magazeti hayo katika kuponi maalum na washindi watano kila gazeti watajishindia tiketi ya bure kwenda kwenye shoo ya Diamond itakayofanyika Krismasi katika Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar. Wanaoruhusiwa kushiriki ni wenye umri kuanzia miaka 18, shindano hili ni kwa watu waishio jijini Dar pekee.

MAJALIWA AKABIDHI JEZI NA MIPIRA

$
0
0
MJ1
Waziri kuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi seti moja ya jezi na mipira miwili nahodha wa timu ya mpira wa miguu ya  Super Mark ya kijiji cha Nabgulugai wilayani Ruagwa, Paulo Joseph baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara kijijini hapo Desemba 21, 2015.
MJ2
Waziri kuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi seti moja ya jezi na mipira miwili nahodha wa timu ya mpira wa miguu ya Super Mark ya kijiji cha Nabgulugai wilayani Ruagwa, Issa Ngele baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara kijijini hapo Desemba 21, 2015.
MJ3
 Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akizungumza katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye kijiji cha Narungombe wilayani  Ruangwa Desemba 21, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

NAIBU WAZIRI WA HABARI AFANYA ZIARA KATIKA VITENGO VYA WIZARA HIYO

$
0
0
kol3
: Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Assah Mwambene akimuelezea Naibu Waziri Mh. Anastazia Wambura juu ya utendaji kazi wa Idara yake wakati wa ziara ya Naibu Waziri aliyoifanya Wizarani hapo kujionea utendaji kazi wa Idara ya habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
kol1
Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Anastazia Wambura akipata maelezo juu ya mradi wa  jengo la kituo cha sanaa na utamaduni litakalojengwa Bagamoyo mkoani Pwani,kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko (Picha na Benjamin Sawe-WHUSM).

kol4
Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya lugha Bi Shani Kitogo kulia akimuelezea Naibu Waziri Mh. Anastazia Wambura juu ya utendaji kazi wa Idara hiyo wakati Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo alipofanya ziara kukagua utendaji kazi wa Idara za Wizara hiyo.
kol2

WANAOTAKIWA KUSTAAFU WASIPEWE MIKATABA YA KUENDELEA NA KAZI SERIKALINI

$
0
0
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akitoa maelekezo kwa watumishi wa Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu-Utumishi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (Mb) akizungumza na watumishi wa Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu-Utumishi.

RAIS AKUTANA NA VIONGOZI MBALIMBALI IKULU

$
0
0
maa1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha  Maalim Seif Sharif Hamad ,Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Ikulu jijini Dar es Salaam na kufanya  Mazungumzo kuhusu hali ya kisiasa ya  Zanzibar. Katika Mazungumzo hayo viongozi wote wamefurahishwa na hali ya usalama na utulivu inayoendelea.
maa2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Maalim Seif Sharif Hamad ,Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Ikulu jijini Dar es Salaam.Rais amemshukuru  Maalim Seif  na amemsihi waendelee na mazungumzo hadi suluhisho la muufaka lipatikane.
maa3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Maalim Seif Sharif Hamad ,Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Ikulu jijini Dar es Salaam, wakwanza kushoto ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan.
maa4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha  na Maalim Seif Sharif Hamad ,Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan.
maa5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Dkt. Tonia Kandiero Ikulu Jijini Dar es Salaam.
maa6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuelekeza jambo Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Dkt. Tonia Kandiero Ikulu Jijini Dar es Salaam.
maa8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Dkt. Tonia Kandiero Ikulu Jijini Dar es Salaam.
maa9
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Rwanda hapa nchini Eugene Kayihura aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
maa10
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Rwanda hapa nchini Eugene Kayihura aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo. Picha zote na IKULU

WASHINDI 16 WAPATIKANA KATIKA DROO YA AIRTEL MKWANJIKA

$
0
0
 Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando (katikati) akiongea na

moja ya  washindi kupitia simu ya mkononi wakati wa kuendesha droo ya
kwanza ya promosheni ya Airtel Mkawnjika ambapo washindi 16 kutoka
katika mikoa mbalimbali walipatikana.  Akishuhudia  Msimamizi wa bodi
ya michezo ya kubahatisha nchini , Bwana Abdallah Hemed  na Afisa
Masoko wa Airtel Bi Rebecca Mauma (kulia)

Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (katikati) akiongea na
waandishi wa habari wakati wa kuendesha droo ya kwanza ya promosheni
ya Airtel Mkawnjika ambapo washindi 16 kutoka katika mikoa mbalimbali
walipatikana.  Akishuhudia  Msimamizi wa bodi
ya michezo ya kubahatisha nchini , Bwana Abdallah Hemed  na Meneja
masoko wa Airtel bi Anethy Muga (kulia)


KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel leo imechezesha droo ya kwanza ya
promosheni ya Airtel Mkwanjika  na kuwapata washindi 16 wa  siku nne
za mwanzo
Promosheni ya Airtel Mkwanjika imezinduliwa na Airtel wiki iliyopita
ikiwa na lengo la kuwazawadia wateja wake katika msimu huu wa siku kuu
za mwisho wa mwaka na X-mass  ambapo jumla ya shilingi milioni 300
zimetengwa na kampuni hiyo kushindaniwa na wateja wake kama  zawadi.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa droo hiyo Meneja Uhusiano
wa Airtel Jackson Mmbando alisema “Airtel Mkwanjika leo tumewanyakuwa
washindi 16 wa siku nne za mwanzo ambapo kila siku ni washindi wanne
na kila mmoja ataweza kujizolea hadi shilingi milioni moja katika
boksi letu la Airtel Mkwanjika.

Mmbando aliwataja walioibuka washindi wa kuingia katika boksi la
Airtel Mkwanjika kuwa Mama Masisimba ,  Abdallah S Rashid, Amani
Maruma, Msafiri Saidi Ruwia , Hassani Hamis Suleyman na  Aida Asabwile
Mwafi wakazi wa mkoa wa Dar, es  salaam. 

Carston Magoah na Godfrey
Frank Kamota wakazi wa Morogoro, Hassan Ngakoma mkazi wa Manyara ,
Safari Aidaru mkazi wa Mbulu, Lupembe Massanja  kutoka Rufiji , Rachel
Obedi Muhumu mkazi wa Moshi na Rodrique kimei  mkazi wa Msumbiji.
Washindi hawa  watapigiwa simu na kupatiwa maelekezo zaidi jinsi ya
kupata na kupoke zawadi zao.

Nae Meneja Masoko wa Airtel Bi Anethy Muga alisema “Promosheni yetu
imeanza kufanikiwa kwa kuwa tayari tumewapata wateja wetu 16 na
tumeshaandaa jumla ya milioni 16 ilikila mmoja akishajizolea pesa
kwenye sanduku la pesa papo hapo tutampatia pesa yake aliyokusanya
kupitia Airtel Money ili akasherehekee sikukuu kwa furaha zaidi”
Promosheni ya “Airtel MKWANJIKA” itawawezesha wateja wote wanaojinga
na kifurushi chochote cha yatosha au kuongeza muda wa maongezi wa
kiwango chochote kwenye simu zao kuingia moja kwa moja kwenye droo ya
siku na kupata nafasi ya kujishindia pesa taslimu.

Hakuna gharama ya ziada wala  malipo yeyote unaongeza salio kwa
kutumia vocha, huduma ya Airtel money au kununua vifurushi vya yatosha



na kujishindia pesa kila siku” alisisitiza Muga.
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images