Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 716 | 717 | (Page 718) | 719 | 720 | .... | 1903 | newer

  0 0

  liw1
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubakar Zuberi, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Desemba 18, 2015.
  liw2
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubakar Zuberi, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Desemba 18, 2015. Kulia ni  Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhad Musa. (PIcha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Ni majira ya saa 10 na dakika 10 Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Mhongo ndipo alipofika katika mitambo ya kuzalisha umeme wa gesi ya Tegeta jijini Dar es Salaam kinachomilikiwa na Tanesco bila ya kutoa taarifa na kukuta wafanyakazi pamoja na wahandisi wa kituo hicho cha umeme wakiendelea na kazi katika mitambo hiyo. 

  Na kukagua mitambo hiyo leo  na kubaini kuwa umeme uniti moja inatengenezwa kwa gharama ya shilingi 90 na kuuzwa kwa wananchi kwa shilingi 180 ikiwa ni kiwango kikubwa kwa mwananchi wa kawaida.

  Pia Mhongo amesisitiza kuwa umeme unatakiwa kushuka bei ili kila mwananchi anufaike na umeme hapa nchini.
  Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Mhongo akipokea vifaa vya kuzuia kusikia sauti kuingia masikioni mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Mitambo ya Gesi ya Tegeta jijini Dar es Salaam leo.
  Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Mhongo akizungumza na Meneja wa Mitambo ya gesi ya Tegeta jijini Dar es Salaam, Mohamed Kisiwa mara baada waziri wa Nishati na Madini kutembelea mitambo ya umeme wa gesi wa Tegeta jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Mhongo akipewa maelekezo na Meneja wa Mitambo ya gesi ya Tegeta, Mohamed Kisiwa mara baada ya waziri huyo kutembelea mtambo huo bila kutoa taarifa na kuhoji baadhi ya matengenezo katika mtambo huo.
  Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Mhongo akitembezwa na Meneja wa Mitambo ya gesi ya Tegeta Mohamed Kisiwa mara baada ya kutembelea mitambo ya Tegeta jijini Dar es Salaam leo.
  Baadhi ya Mitambo ya Gesi iliyotembelewa na Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Mhongo leo jijini Dar es Salaam.


  Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Mhongo akipewa maelekezo na Meneja wa Mitambo ya gesi ya Tegeta, Mohamed Kisiwa jijini Dar es Salaam leo.


  Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

  0 0

  Madiwani wa Manispaa ya Kigoma ujiji wakiwa katika picha ya pamoja .
  Mwenyekiti wa uchaguzi wa Meya na Naibu meya mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe akitoa maelezo ya awali kabla ya uchaguzi.
   Meya wa Manispaa ya kigoma Ujiji Hussein Ruhavi akimweleza jambo makamu meya  Athuman Mussa wa manispaa hiyo kushoto ni mbunge wa Kigoma mjini ndiye alikuwa mwenyeti wa uchaguzi
   Mmoja wa Madiwani akipiga kura ya kumchagua meya wa manispaa ya Kigoma Ujiji

  Na Editha Karlo wa Globu ya Jamii,Kigoma

  BARAZA la madiwani la Halmashauri ya Kigoma Ujiji  limemchagua Diwani wa kata ya Bangwe Hussein Ruhavi kuwa meya wa Manispaa hiyo.

  Mbunge Zitto Zuberi Kabwe alikuwa mwenyekiti wa uchaguzi huo alimtangaza diwani Ruhavi kutoka chama cha ACT wazalendo kuwa mshindi wa kiti cha umeya kwa kupata kura 19 kati ya kura 21 zilizopigwa na akamshinda mpinzani wake Masudi Kassim kutoka chama cha mapinduzi(CCM).

  Pia Zitto alimtangaza diwani wa kata ya Buzebazeba Athumani Mussa kupitia chama cha ACT wazalendo kuwa naibu meya wa manispaa ya Kigoma Ujiji alimshinda Mussa Maulid wa CCM aliyepata kura moja.

  Baada ya kutangaza matokeo Zitto ambaye ni mbunge wa jimbo la kigoma mjini alisema kuwa watasimamia mipango ya kuwaletea wananchi maendeleo kwa usawa.

  "Diwani yeyote ambaye kwa makusudi ataamua kukwamisha michakato mbalimbalu ya maendeleo tutamshughulikia lwa namna tutakayojua sisi"alisema Zitto

  Naye meya Hussein Ruhavi akizungumza baada ya kuchaguliwa aliwashukuru madiwani kwa imani yao waliyoionyesha kwake kwa kumchagua kuwa Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji.

  Alisema atafanya kazi kwa kushirikuana na madiwani wote ili kuwaletea wananchi maendeleo,pia aliwataka madiwani kufanya kazi pamoja bila ya kujali itikadi zao

  0 0  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

  Simu: 255-22-2114512, 2116898
  E-mail: press@ikulu.go.tz
  Tovuti : www.ikulu.go.tz              

  Faksi: 255-22-2113425  OFISI YA RAIS,
        IKULU,
   1 BARABARA YA BARACK OBAMA,  
  11400 DAR ES SALAAM.
  Tanzania.
   
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye amepatwa na msiba mzito wa kufiwa na Dada yake Mpendwa Bi. Tausi Khalfan Kikwete kilichotokea jana tarehe 17 Desemba, 2015 huko nchini India.

  Katika salamu hizo, Rais Magufuli amesema anaungana na familia ya Rais Mstaafu Kikwete katika kipindi hiki kigumu cha majonzi ya kuondokewa na mtu muhimu kwa familia."Kwa masikitiko makubwa nakupa pole nyingi Mheshimiwa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete kwa kufiwa na dada yako ambaye alikua nguzo muhimu katika familia" Amesema Rais Magufuli.

  Aidha Rais Magufuli amemuomba Rais Mstaafu Kikwete kumfikishia salamu nyingi za pole kwa familia nzima na amewaomba wawe na moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.Rais Magufuli amemuomba Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema aipumzishe roho ya marehemu Tausi Khalfan Kikwete mahali pema peponi, Amina.

  Imetolewa na;
  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  18 Desemba, 2015

  0 0

    Balozi wa China nchini Dk. Lu Youqing akiangalia baadhi ya vitanda ambavyo vimekabidhiwa kwa mkoa wa Lindi kwenye hafla fupi iliyofanyika kwenye hospitali ya mkoa wa Lindi Sokoine.
   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kulia) akiangalia vitanda hivyo vya kujifungulia wakina mama akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa Taasisi ya kukuza Urafiki wa Tanzania na China  Ndugu Joseph Kulwa Kahama.
   Bi. Ziada Maulid akitoa shukrani zake mbele ya Balozi wa China nchini  Dk. Lu Youqing mara baada ya ya Balozi huyo kukabidhi vitanda 60 vya kujifungulia wakina mama.
   Balozi wa China nchini Dk. Lu Youqing pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama wakiwasili katika kata ya Kiwalala, jimbo la Mtama tayari kwa kukabidhi vifaa vya matibabu katika Zahanati ya Mauhumbika.
   Wakazi wa kijiji cha Mahumbika wakiwa wamejitokeza kwa wingi kushuhudia makabidhiano ya vifaa vya matibabu katika Zahanati yao.
    Balozi wa China nchini Dk. Lu Youqing akihutubia wakazi wa Mahumbika ambapo pamoja na kuahidi misaada zaidi ikiwemo kwenye matatizo ya maji, Balozi pia aliahidi kusaidia vijana wanaomaliza Chuo Kikuu kwenda kujiendeleza nchini China.
   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akitoa salaam za shukrani kwa Serikali ya China kwa msaada wa vifaa vya tiba vilivyogharimu zaidi ya milioni 20.
   Balozi wa China nchini Dk. Lu Youqing akizungumza kabla ya kukabidhi vitanda 60 vya kujifungulia wakina mama katika mkoa wa Lindi, kushoto ni mkalimani wake Ndugu Mu Lin.
   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (MB) akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (MB) ambapo alisema Serikali ya China pamoja na watu wake wamekuwa marafiki wa kweli kwa Tanzania na wamekuwa wakitoa misaada mingi bila kutoa masharti.
   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (MB) akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (MB) ambapo aliishukuru  Serikali ya China pamoja na watu wake kwa msaada wa vitanda 60 vya kujifungulia ambavyo vitasaidia kuokoa maisha ya Mama na Mtoto katika mkoa wa .


  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

  Simu: 255-22-2114512, 2116898
  E-mail: press@ikulu.go.tz
  Tovuti : www.ikulu.go.tz              

  Faksi: 255-22-2113425  OFISI YA RAIS,
        IKULU,
   1 BARABARA YA BARACK OBAMA,  
  11400 DAR ES SALAAM.
  Tanzania.
   

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza kufuatia ajali ya basi la kampuni ya New Force kugongana na lori, na kusababisha vifo vya watu 12, na wengine 15 kulazwa Hospitali.

  Ajali hiyo imetokea tarehe 18 Desemba, 2015 Majira ya saa nane mchana katika Kijiji cha Mahenge, Wilaya ya Kilolo Mkoani IRINGA ambapo Basi la kampuni ya New Force lenye namba T 483 CTF lililokuwa limebeba abiria 49 limegongana na Lori la Kampuni ya Reign-ford Limited lenye namba T 616 BEF na Tela lake lenye namba T 320 DEF lililokuwa na shehena ya mbao .

  Rais Magufuli amemuomba Mkuu huyo wa mkoa kufikisha salamu za pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wote ambao wamepoteza ndugu zao katika ajali hiyo mbaya"Nimesikitishwa sana na kutokea kwa ajali hii, ninawapa pole nyingi wote waliopoteza ndugu zao na ninawaombea Majeruhi wote wapone haraka ili waungane na familia zao na kuendelea na shughuli zao za maendeleo" amesema Rais Magufuli.

  Amewaombea marehemu wote kwa Mwenyezi Mungu ili azipumzishe roho zao mahali pema peponi, Amina.Aidha Dkt. Magufuli ametoa wito kwa watuaji wote wa barabara hususani madereva kuwa waangalifu waendeshapo vyombo vya usafiri na amewakumbusha wananchi wanaotumia barabara kwa kusafiri ama kusafirisha mizigo kutoa ushirikiano kwa vyombo husika pale wanapobaini kuwepo vitendo ambavyo ni chanzo cha ajali.

  Imetolewa na;  Gerson Msigwa,
                          Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
                          18 Desemba, 2015

  0 0

   Magari matatu yamepata ajali mkoani Mbeya asubuhi ya leo iliyohusisha mabasi ya Hood ya Mbeya na Arusha na basi la Bestline linalofanya safari zake Mbeya na Mwanza pamoja na lori eneo la Inyala Mbeya
  Katika ajali hiyo mtu mmoja amejeruhiwa vibaya na wengine kupata majeraha madogo madogo.

  Kamanda wa polis Mkoani mbeya ACP AHMED MSANGI amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.  0 0

  MRADI wa Mabasi yaendayo haraka (BRT) kuanza Januari 10, 2016 hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa wakati akikagua  ujenzi wa miundo mbinu ya Mradi wa Mabasi yaendayo haraka leo jijini Dar es Salaam.

  Pia Majaliwa amewaagiza watendaji wizara ya Tamisemi ambao ni wamiliki wa mradi huo  kusimamia vyema ili uanze kufanya kazi  kama ilivyo pangwa kwa kuwa mabasi 120 yalishawasili jijini Dar es Salaam.

  Waziri Mkuu ameanza kwa kukagua vituo vya mradi huo kuanzia cha Feri, Jangwani, Kimara na kumalizia na Morocco na kuwapongeza kwa kumaliza kujenga vituo 15 kati ya 27 na amewaagiza kumalizia vituo vilivyo baki ili kufikia januari 10 mwakani mabasi yaanze kufanya kazi.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa akisalimiana na watendaqji mbalimbali wa mradi wa mabasi yaendayo haraka waliofika katika kituo cha Feri cha Mradi wa Mabasi yaendayo haraka (BRT) leo jijini Dar es Salaam. 
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa akitembelea maeneo mbalimbali ya kituo cha Feri jijini Dar es Salaam leo.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa akipanda basi la mwendo wa haraka mara baada ya kutembelea maeneo mbalimbali katika kituo cha feri leo jijini Dar es Salaam.

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa akiwa katika kituo cha Mradi wa mabasi cha Jangwani kukagua maendeleo ya ujenzi ya kituo hicho ikiwa ujenzi wa kituo hicho upo hatua za mwisho kukamilika.
  Kituo cha Mradi wa mabasi yaendayo haraka kikiwa kimekamilika na mabasi yakiwa nyuma ya kituo hiki kwaajili yakisubiri kumalizika kwa barabara ili ifikapo Januari 10, 2016 kuanza kufanya kazi.
  Mabasi ya mwendo wa haraka yakiwa kwenye maegesho. 
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kumalizia kukagua ujenzi wa barabara ya mradi wa mabasi yaendayo haraka katika kituo cha Morocco jijini Dar es Salaam.
  Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

  SHIRIKISHO la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), limesema  kuwa waliopewa wajibu wa kusimamia fedha za elimu  bure wanatakiwa uaminifu na uadilifu kutimiza suala hilo.

  Akizungumza na waandishi habari  Mwenyekiti wa Shirikisho hilo, Zainabu Abdallah amesema kuwa kwa wale ambao watakiuka matumizi ya fedha za elimu bure, wamemtaka Rais John Pembe Magufuli  kutokuwa na huruma kwa yeyote atakayefanya urasimu usio na tija kukwamisha utekelezaji wa  ahadi ya wananchi ya kupata elimu bure.

  Amesema maazimio hayo yametokana na kikao kilichofanyika hivi karibuni kilichojadili masuala mbalimbali ya serikali ya awamu ya tano na kulitathmini shirikisho na  hatimae kubaini kuwa wako nyuma ya kutokwenda na wakati.

  Zainabu amesema katika kwenda na kasi wameunda kamati mbalimbali za shirikisho,amesema mosi wameanzisha dawati la mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu  katika kuondoa vikwazo vya kutopata mikopo kwa wakati.

  Pili amesema kuwa wameunda kamati ya uwezeshaji ambayo itafanya kazi ya kuibua fursa za ajira katika midahalo na semina hali ambayo  itasaidia kuwafundisha wasomi juu ya kuanzisha biashara na kusimamia.

  Zainabu amesema kuwa iwapo wao ni wasomi,inawapasa lazima waendane na kasi ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa ajili ya fedha milioni 50 kwa vijana kuwa wabunifu wa miradi.

  Aidha wakati huo huo Shirikisho hilo limeitaka serikali kufanya uhakiki wa watumishi feki kutokana na kazi wanazozifanya sio zao na kusababisha watu wenye sifa kushindwa kupata kazi ili kuweza kuwatumikia wananchi.

  0 0

  IMG_9550
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na duka la dawa kwa wagonjwa wanaotumia huduma ya bima ya afya katika Hospitali ya Ligula ya mkoa wa Mtwara. Kulia ni Mganga Mkuu wa Hospitali ya Ligula ya mkoa wa Mtwara, Dkt. Shaibu Maarifa.
  IMG_9567
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akisikiliza maelezo kutoka kwa Daktari wa zamu kitengo cha dharura hospitalini hapo,Dkt. Ester Tumwanga (kulia) wakati wa ziara ya kushtukiza aliyofanya leo mkoani humo. Kushoto ni Mganga Mkuu wa Hospitali ya Ligula ya mkoa wa Mtwara, Dkt. Shaibu Maarifa.
  IMG_9602
  Muuguzi Kiongozi wa wodi ya wazazi katika Hospitali ya Ligula ya mkoa wa Mtwara, Getrude Mangosongo (wa kwanza kulia) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla (wa pili kushoto) alipotembelea wodi ya akinamama wakati wa ziara ya kushtukiza aliyofanya leo mkoani humo. Kushoto ni Daktari wa zamu kitengo cha dharura hospitalini hapo,Dkt. Ester Tumwanga na wa pili kulia ni Mganga Mkuu wa Hospitali ya Ligula ya mkoa wa Mtwara, Dkt. Shaibu Maarifa.
  IMG_9619
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla (kulia) akiwasili katika jengo jipya la Hospitali ya Kanda ya Kusini mkoani Mtwara ambalo linaendelea kujengwa na litahudumia mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma pamoja na nchi za jirani ikiwemo Msumbuji.

  IMG_9650
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla (kulia) akitembelea maeneo ya jengo jipya la Hospitali ya Kanda ya Kusini mkoani Mtwara ambalo linaendelea kujengwa na litahudumia mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma pamoja na nchi za jirani ikiwemo Msumbuji.
  IMG_9671
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akiwa ndani ya jengo jipya la Hospitali ya Kanda ya Kusini mkoani Mtwara ambalo linaendelea kujengwa na litahudumia mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma pamoja na nchi za jirani ikiwemo Msumbuji.
  IMG_9689
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akitoa maelekezo baada ya kutembelea jengo jipya la Hospitali ya Kanda ya Kusini mkoani Mtwara ambalo linaendelea kujengwa na litahudumia mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma pamoja na nchi za jirani ikiwemo Msumbuji.
  IMG_9315
  Kaimu Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Sokoine ya Mkoa wa Lindi, Damasiana Msalla akimuongoza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla kuelekea kwenye wodi za hospitali wakati wa ziara ya kushtukiza aliyofanya mkoa wa Lindi.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
  IMG_9342
  Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sokoine ya Mkoa wa Lindi, Dkt. Evaristo Kasanga akimkaribisha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla alipotembelea wodi za hospitali hiyo wakati wa ziara ya kushtukiza aliyofanya leo mkoa wa Lindi.Katikati ni Mganga wa Meno na Kinywa katika hospitali hiyo, Dkt. Hussein Athumani.
  IMG_9381
  Mtaalamu wa Tehama katika Hospitali ya Sokoine ya Mkoa wa Lindi, Abdallah Kivurugo akitoa maelekezo kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla (kulia) namna wanavyomsajili mgonjwa anapofika hospitalini hapo wakati wa ziara ya kushtukiza aliyofanya leo mkoa wa Lindi.
  IMG_9395
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla (kulia) akihoji jambo kwenye chumba cha mapokezi katika Hospitali ya Sokoine ya Mkoa wa Lindi, wakati wa ziara ya kushtukiza aliyofanya leo mkoani humo.
  IMG_9415
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sokoine ya Mkoa wa Lindi, Dkt. Evaristo Kasanga (kulia).
  IMG_9422
  Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sokoine ya Mkoa wa Lindi, Dkt. Evaristo Kasanga akionesha kombe la mshindi wa pili kwa utoaji wa huduma bora Tanzania kwa mwaka 2015 kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla.
  IMG_9501
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akipata maelekezo kwa wahudumu wa afya wa Hospitali ya Ligula ya mkoa wa Mtwara wakati wa ziara ya kushtukiza aliyofanya leo mkoani humo.
  IMG_9533
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Ligula ya mkoa wa Mtwara, Dkt. Shaibu Maarifa wakati wa ziara ya kushtukiza aliyofanya leo mkoani humo.
  IMG_9545
  Mganga Mkuu wa Hospitali ya Ligula ya mkoa wa Mtwara, Dkt. Shaibu Maarifa akimuongoza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla kuelekea wodi za wagonjwa wakati wa ziara ya kushtukiza aliyofanya leo mkoani humo. Kulia ni Daktari wa zamu kitengo cha dharura hospitalini hapo,Dkt. Ester Tumwanga.


  0 0

   Mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. Magesa Mulongo akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Kamusi ya kiswahili huku akishuhudiwa na mwenyekiti wa TAHOSSA Taifa Bonus Ndimbo katika ghafla iliyofanyika kwemye mkutano mkuu wa TAHOSSA jijini Mwanza.
   Mgeni rasmi akiwaonyesha wakuu wa shule nchini (hawapo pichani) kamusi kuu ya kiswahili aliyoizindua, kushoto ni muhariri mkuu wa kamusi hiyo James Mwilaria
   Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. Masesa Mulongo akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la Longhorn Publishers Ltd.
   Meneja mauzo na msimamizi wa matangazo wa Longhorn Publishers Ltd Deisy Rono akimuonesha mgeni rasmi baadhi ya machaisho yao.
   Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. Magesa Mulongo akikagua moja ya kitabu cha civics kilichochapishwa na Longhorn Publishers Ltd mara baada ya
  kutembelea banda lao.
   Mkuu wa mkoa wa Mwanza  akipokea zawadi ya baadhi ya machapisho  kutoka kwa mwakilishi wa Longhorn Publishers Limited.
  Mgeni rasmi Mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo katika picha ya pamoja na wawakilishi kutoka BAKITA, Longhorn Publishers na TAHOSSA.

   Mwenyekiti wa TAHOSSA Taifa Bonus Ndimbo (kulia)pamoja na meneja mauzo na msimamizi wa matangazo wa Longhorn Publishers Deisy Rono (kushoto)wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani)katika ghafla ya uzinduzi wa kamusi ya kiswahili iliyofanyika katika mkutano mkuu
  wa kumi wa TAHOSSA jijini Mwanza.
   Meneja wa uhariri wa uhariri wa Longhorn Ltd James Mwilaria akitoa neno wakatiwa uzinduzi wa kamusi kuu ya kiswahili iliyoandaliwa na BAKITA.
   Mgeni rasmi Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. Magesa Mulongo akihutubia
  wakati wa uzinduzi huo uliofanyika jijini Mwanza.
   Baadhi ya wakuu wa shule za Sekondari nchini walioshuhudia uzinduzi huo watikamkutano mkuu wa TAHOSSA ulifanyika jijini Mwanza.


  0 0

  1010
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake katika sherehe ya  mahfali ya kumi na moja ya mwaka 2014/2015  yaliyofanyika leo  katika kampasi ya Chuo Tunguu wilaya ya kati Unguja leo.
  106
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA Dk.Ali Mohamed Shein (katikati)  akiwa na Viongozi wakuu wa  Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar  katika   mahfali ya kumi na moja ya mwaka 2014/2015 chuoni hapo  Tunguu wilaya ya kati Unguja leo.
  100
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA Dk.Ali Mohamed Shein akimtunuku Shahada ya Uzamili ya Sayansi katika kemia “Master of Science in Chemistry” ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar mhitimu Hadia Makame Juma wakati wa mahfali ya kumi na moja ya mwaka 2014/2015 Tunguu  wilaya ya kati Unguja leo.
  105
  Viongozi mbali mbali wakiwemo mabalozi wa Nchi za Nje wakiwa katika mahfali ya kumi na moja ya mwaka 2014/2015 Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA yaliyofanyika leo Tunguu wilaya ya kati Unguja,ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA Dk.Ali Mohamed Shein,
  107
  Viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar walioalikwa katika mahfali ya kumi na moja ya mwaka 2014/2015 Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA yaliyofanyika leo Tunguu wilaya ya kati Unguja,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA Dk.Ali Mohamed Shein wakati akiwatunuku wahitimu Shahada,Stashahada na Vyeti,
  108
  Wahitimu wa Shahada ya Kiswahili na Elimu wakiwa katika mahfali ya kumi na moja ya mwaka 2014/2015 Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA yaliyofanyika leo Tunguu Wilaya ya Kati Unguja,mgeni Rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA Dk.Ali Mohamed Shein.

  109
  Wahitimu wa Shahada ya Sanaa na Elimu wakiwa katika mahfali ya kumi na moja ya mwaka 2014/2015 Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA yaliyofanyika leo Tunguu Wilaya ya Kati Unguja,mgeni Rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA Dk.Ali Mohamed Shein.
  103104    
    Baadhi ya Wazee na Ndugu wa wanafunzi waliohitimu masomo mbali mbali ya Shahada,Stashahada na Vyeti wakiwa katika mahfali ya kumi na moja ya mwaka 2014/2015 Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA yaliyofanyika leo Tunguu wilaya ya kati Unguja,ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA Dk.Ali Mohamed Shein
   101
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatama na Viongozi wakuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar katika maandamano  wakati wa mahfali ya kumi na moja ya mwaka 2014/2015 yaliyofanyika leo chuoni hapo Tunguu  wilaya ya kati Unguja,
  [Picha na Ikulu.]
  102
  Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar  na Viongozi wengune wakiwa katika maandamano  wakati wa mahfali ya kumi na moja ya mwaka 2014/2015 yaliyofanyika leo chuoni hapo Tunguu  wilaya ya kati Unguja mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA Dk.Ali Mohamed Shein,


  0 0

  kitw4
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (watatu kushoto) na Waziri wa Sheria na Katiba, Dkt. Harrison Mwakyembe (wapili kushoto) wakikagua  jiko linalotumia gesi asilia kupikia vyakula vya wafungwa katika Gereza la Mahabusu Keko, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, CGP John Minja.
  kitw5
  Msafara wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga ukiwasili katika lango Kuu la Gereza Kuu Segerea, jijini Dar es Salaam kwa ziara ya kikazi kujifunza shughuli mbalimbali za uendeshaji wa Magereza.
  kitw6
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (wapili kushoto) na Waziri wa Sheria na Katiba, Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) wakitoka Gereza la Wanawake Segerea baada ya kuzungumza na Mahabusu na Wafungwa wa Gereza hilo lililopo jijini Dar es Salaam.
  kitw7
  Waziri wa Sheria na Katiba, Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akiangalia bidhaa zinazotengenezwa na wafungwa wa kike wa Gereza la Wanawake Segerea ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa program ya urekebishaji magerezani. Pembeni yake ni Mkuu wa Gereza Kuu Segerea, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Abdalah Kiangi. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga.
  kitw8
  Waziri wa Sheria na Katiba, Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto aliyevaa suti) akipokea heshima kutoka gadi maalumu iliyoandaliwa na Maafisa na Askari wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji cha Jeshi la  Magereza mara baada ya kumaliza kufanya ziara ya kikazi ya kutembelea Magereza Makuu ya Mkoa wa Dar es Salaam.
  kitw9
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akitoa majumuisho kwa waandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara ya kutembelea Magereza ya Mkoa wa Dar es Salaam. Katika ziara yake hiyo Waziri Kitwanga aliambatana na Waziri wa Sheria na Katiba, Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati). Kulia ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, CGP John Minja. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  kitw1
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akisalimiana na Kamshina Jenerali wa Jeshi la Magereza,. John Minja wakati alipokuwa anawasili Gereza la Mahabusu Keko kwa ziara ya kikazi. Mwenye mawani ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu, John Mngodo.
  kitw2
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga  akikagua gadi maalumu iliyoandaliwa na Maafisa na Askari wa Gereza Keko alipofanya ziara ya kikazi ya kutembelea Magereza Makuu ya Mkoa wa Dar es Salaam.
  kitw3
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akizungumza na mahabusu na wafungwa waliopo Gereza la Wanawake Segerea, jijini Dar es Salaam alipofanya ziara katika Gereza hilo kujifunza shughuli mbalimbali za uendeshaji wa Magereza. Kulia kwake ni Waziri wa Sheria na Katiba, Dkt. Harrison Mwakyembe. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil, Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba, Maimuna Tarishi. Wapili kulia ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, CGP John Minja.


  0 0

   x9
  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akiongea na Uongozi wa Mkoa wa Tanga,Waziri Ummy yupo mkoani Hapa kwenye ziara ya kikazi sehemu ya afya na wazee.
  x8
  Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora),Seleman Jaffo(Kulia) na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Salum Chime kwenye  ukumbi wa Mkuu wa Mkoa,
  x10
  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto akisaini kitabu cha wageni kwenye Ukumbi wa Mkuu wa mkoa.
  x11
  Waziri Ummy Mwalimu akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Tanga Abdullah Lutari (wa pili Kulia) na afisa toka wizara ya afya Dkt.Ibrahim Maduhu.
  ………………………………………………………..
  Na. Catherine Sungura,WAMJW-Tanga
  Halmashauri zote nchi zimetakiwa kujitahidi kudhibiti upoteaji wa dawa na vifaa tiba kwenye vituo vya afya ili wananchi waweze kupata tiba sahii na inayostahili Hayo yamesema leo na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati alipokutana na Uongozi wa Mkoani hapa.
    Ummy alisema kumekuwa na upoteaji dawa na vifaa tiba mara vifikapo kwenye vituo vya afya kwa kuzunguka na kupelekwa kuuzwa kwenye maduka ya dawa na hospitali binafsi.
    Alimtaka Mganga mkuu wa mkoa kudhibiti upoteaji wa dawa kwa kutoa elimu kwa kamati ya afya juu ya majukumu yao ili dawa zote zinazowafikia zisipotee mikononi mwa watu wachache.“Nimejifunza kuwa dawa zinapopokelewa kwenye vituo zinazunguka tena na kwenda kwa wauzaji binafsi hivyo hakuna udhibiti wa uingiaji na utokaji wa dawa na hivyo kufanya dawa nyingi kupotea kwenye maduka ya dawa binafsi
    Aidha alisema ataongea na Bohari ya dawa (MSD) ili kuanzisha utaratibu wa kila dawa zinazopelekwa kwenye kituo ziwe zinabandikwa kwenye ubao wa matangazo wa vituo vyote nchini ili wananchi wajue dawa zilizopo kwenye kituo chake nia aina gani.
    Hata hivyo amemuomba Naibu Waziri, Ofisi ya Rais(Tamisemi,Utumishi na Utawala Bora),Seleman Seleman Jaffo kuwachukulia hatua pamoja na kusisitiza suala la nidhamu,uwajibikaji na uadilifu kwa watendaji hususan kwenye sekta ya afya, kwakuwa yeye hana dhamana ya kuwasimamisha kazi moja kwa mojaWaganga wakuu wa mikoa na Wilaya kwakuwa yeye anasimamia sera na miongozo ya sekta ya afya.

  0 0

      x1
  Muuguzi wa Kituo cha Afya cha Miwani, Wilaya ya Kati Unguja Fatma Keisi Ali akimtembeza Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo  sehemu mbali mbali za Kituo hicho kuona changamoto zinazowakabili ikiwemo tatizo la umeme, maji na upungufu wa wafanyakazi kituoni hapo.
  x2
  Kituo cha Afya cha  Miwani ambacho Naibu Waziri ameahidi kukiboresha ikiwa pamoja na kuondosha tatizo la umeme, maji na kujenga nyumba ya wafanyakazi.
  x5
  Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na wananchi wa kijiji cha Miwani baada ya kusikiliza matatizo yanayokikabili kituo cha Afya cha Miwani.
  x4
  Naibu Waziri wa Afya Mhmoud Thabit Kombo akiwasilikiza wananchi wa Miwani wakati alipofanya viara ya kutembelea kituo cha Afya cha Kijiji hicho kujua matatizo yanayokikabili kituo hicho,  (kushoto) Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Mohammed Saleh Jidawi.
  x6
  Daktari dhamana Kanda ya Unguja Dkt. Fadhil Mohd Abdalla akitoa ufafanunuzi baadhi ya masuala yaliyoulizwa na wananchi wa kijiji cha Miwani wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Afya katika kituo hicho.
  x7
  Naibu Waziri wa Afya Mhmoud Thabit Kombo akiwasilikiza wananchi wa Miwani wakati alipofanya viara ya kutembelea kituo cha Afya cha Kijiji hicho kujua matatizo yanayokikabili kituo hicho,  (kushoto) Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Mohammed Saleh Jidawi.
  x3
  Mmoja ya wananchi wa kijiji cha Miwani akimueleza Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo (hayupo pichani) matatizo wanayoyapata kutokana na upungufu wa huduma muhimu katika kituo  hicho .

  Picha Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

  0 0

  90
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana  na Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mama Salma Kikwete wakati alipokwenda kuwapa pole wanafamilia kutokana na kifo cha dada yake Rais Mstaafu, Tausi Kikwete, Mikocheni jijini Dar es salaam Desemba 19, 2015.
  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  88
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mama Salma Kikwete wakati alipokwenda kuwapa pole wanafamilia kutokana na kifo cha dada yake Rais Mstaafu, Tausi Kikwete, Mikocheni jijini Dar es salaam Desemba 19, 2015.
  89
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na wanafamilia wa  Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya  Kikwete  wakati alipokwenda kuwapa pole wanafamilia kutokana na kifo cha dada yake Rais Mstaafu, Tausi Kikwete, Mikocheni jijini Dar es salaam Desemba 19, 2015.

  0 0  0 0

  2Nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ akitoa burudani usiku wa kuamkia leo katuka Uwanja wa Lugogo Cricket Oval, Kampala, Uganda.
  4 
  Diamond akiimba kwa hisia.5
  Madansa wa Diamond wakiendelea na makamuzi.
  index 
  ...Akiwauliza jambo mashabiki wake wa Uganda (hawapo pichani).
  9 ...Akicheza sambamba na madansa wake.rr 
  ...Akiimba wimbo wake mpya wa Utanipenda.
  uuDiamond akiwa amesimama na madansa wake baada ya shoo.
  USIKU wa kuamkia leo katika Uwanja wa Cricket wa Lugogo, Uganda, staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' alifunika kwa kupiga shoo kubwa na ya kihistoria. Diamond aliyekuwa ameongoza na madensa wake, muda mwingi aliwakosha mashabiki hao kwa kuwapigia nyimbo zake zote kali zinazotamba kama vile Kesho, Mdogomdogo, Nasema Nawe, Nana na nyingine kibao. Baada ya kufunika shoo hiyo.

   Diamond atarejea jijini na moja kwa moja kujiandaa na shoo nyingine kubwa na ya kihistoria itakayofanyika Sikukuu ya Krismasi (Desemba 25, mwaka huu) ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar. Kwa mara ya kwanza ndani ya Dar Live, Diamond atapiga live kwa kutumia vyombo nyimbo zake zote kali ikiwa ni pamoja na hii ya Utanipenda ambayo ni habari ya mjini kwa sasa. Mbali na Diamond katika shoo hiyo pia atakuwepo mkali wa nyimbo za Singeli, Msagasumu ambaye tagonga nyimbo zake zote kali zinazobamba kama vile Shemeji Unanitega, Huyu Mtoto, Naipenda Simba na nyingine nyingi. 

  Baada ya Msagasumu, Mashabiki pia wataburudika na shoo kutoka kwa wakali wa kucheza nyimbo Afrika Mashariki, Wakali Dancers ambapo watakinukisha mwanzo mwisho kwa kutoa burudani ya kucheza ngoma zote zinazobamba ndani na nje ya nchi kwa staili za kipekee. Imeandaliwa na Andrew Carlos/GPL

  0 0

   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akipungia mkono wakazi wa mkoa wa Lindi mara baada ya kuwasili mkoani humo ikiwa ndio ziara yake ya kwanza tangia kuteuliwa kwake.
   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama  Mhe.Nape Nnauye mara baada ya kuwasili mkoani Lindi.
   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Zamani wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe, anayewaangalia katikati ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye wakati wa mapokezi kwenye uwanja wa ndege wa mkoa wa Lindi.
   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa jeshi mkoani Lindi waliojitokeza kumpokea kwenye viwanja vya ndege mkoani Lindi.
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Halmashauri wilaya ya Lindi Vijijini Ndugu Matei B. Makwinya.BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa kigoma akiwaeleza wafanyabiashara(ambai hawapo pichani) wa Kigoma umuhimu wa kujiunga na mfuko wa bima ya afya(NHIF)
   Ofisa matekelezo kutoka mfuko wa bima ya afya Kigoma Evance Ndyamkama akiongea na wafanyabiashara wa Kigoma jinsi ya kujiunga na mfuko huo
   Makamu mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara Mkoa wa Kigima(TCCIA) Sethi Naftari akisona hotuba ya wafanyabiashara kwa Mgeni rasmi Issa Machibya na maofisa mfuko wa bima ya afya
   Baadhi ya wafanyabiashara wa Mkoa wa Kigima wakifuatilia mada mbalimbali katika mkutano huo

  =====  ====   ====    =======

  Na Editha Karlo wa Globu ya Jamii,Kigoma

  WAFANYABIASHARA Mkoani hapa wametakiwa kujiunga na mfuko wa bima ya afya(NHIF) ili waweze kuwa na uhakika wa matibabu pale wanapougua.

  Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali mstaafu Issa Machibya wakati akifungua mkutano wa wafanyabiashara na maofisa wa NHIF wa Mkoa wa Kigoma.

  Machibya alisema kuwa suala la kuugua ni la kila mtu na ugonjwa huwa unakuja bila ua taarifa,na magonjwa menfine gharama za matibabu zipo juu lakini kama mtu ana kadi ya bima atakuwa na uhakika wa matibabu.

  "Nina waomba wafanyabiashara mjiunge na mfuko huu wa bima ya afya kwani mtakuwa na uhakika wa matibabu kipindi cha mwaka mzima"alisema Machibya

  Aliwautaka mfuko huo kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kujiunga na bima ya afya ili kuongeza wigo mpana wa wananchi wanaonufaika na huduma zao.

  Naye ofisa matekelezo wa mfuko wa bima ya afya Mkoani Kigoma Evance Ndyamukama alisema kuwa kila mfanyabiashara anatakiwa kulipia shilingili elf 76000 itakayomwezesha kupata matibabu kwa kipindi cha mwaka mzima.

  Naye Makamu mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara mkoa wa Kigoma(TCCIA)Sethi Naftari aliuomba mfuko huo uwape kipaumbe cha kuweka na wategemezi wao wanne katika hiyo shilingi elf 76000 kama wafanyavyo watumishi na watu wa makundi mbali mbali.

  "Kama kweli NHIF mmelenga kutusaidia sisi wananchi wa kawaida tunaomba tuwaingize na sisi wategemezi wetu kwenye hayo malipo na yasiwe malipo ya mtu mmoja kwani sisi tumejiajiri"alisemaNaftari

older | 1 | .... | 716 | 717 | (Page 718) | 719 | 720 | .... | 1903 | newer