Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

Uongozi wa Wizara yenye dhamana na Sanaa wakutana na Viongozi wa Mashirikisho ya Sanaa kujadili namna ya kuboresha tasnia ya Sanaa nchini

0
0
E51
: Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati) akizungumza na viongozi wa mashirikisho ya sanaa wakati wa kikao cha kuchanganua changamoto zilizopo katika tasnia ya sanaa jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Sanaa Bibi. Leah Kihimbi na kulia ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fisoo
E52
Rais wa Shirikisho la Sanaa za Maonyesho Bibi. Agnes Lukanga (wapili kulia) akichangia mada wakati wa kikao kilichoandaliwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuchanganua changamoto zilizopo katika tasnia ya sanaa jana Jijini Dar es Salaam.
E53
Rais wa Shirikisho la Filamu Bw. Simon Mwakifamba (wapili kushoto) akifafanua jambo wakati wa kikao kilichoandaliwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuchanganua changamoto zilizopo katika tasnia ya sanaa jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni msemaji wa Shirikisho la Filamu Bw. John Kallage.
E54
Baadhi ya viongozi wa mashirikisho ya sanaa wakifuatilia kwa makini mada zilizokua zikiendelea wakati wa kikao kilichoandaliwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuchanganua changamoto zilizopo katika tasnia ya sanaa jana Jijini Dar es Salaam.
E55
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (watatu kulia waliokaa) katika picha ya pamoja na viongozi wa mashirikisho ya sanaa baada ya kumaliza kikao cha kuchanganua changamoto zilizopo katika tasnia ya sanaa jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Sanaa Bibi. Leah Kihimbi, wapili kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fisoo na watatu kushoto ni Rais wa Shirikisho la Filamu Bw. Simon Mwakifamba.Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo

SIMBACHAWENE AAGIZA TAKA ZILIZOKUSANYWA WAKATI WA UHURU ZIZOLEWE

0
0

wafanyakazi wa wizara ya ofisi ya Rais Tamisemi,Utumishi na Utawala bora wakimsikiliza waziri wao George Simbachawene.
WAZIRI wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi,Utumishi na Utawala bora George Simbachawene akizungumza na wafanyakazi wa wizara hiyo mjini Dodoma.
WAZIRI wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi,Utumishi na Utawala bora George Simbachawene akipokelewa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Jumanne Sagini alipowasili makao makuu ya ofisi hizo mjini Dodoma.
Naibu waziri nchi ofisi ya Rais Tamisemi,Utumishi na Utawala bora, Selemani Jaffo akipokelewa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Jumanne Sagini alipowasili makao makuu ya ofisi hizo mjini Dodoma
WAZIRI wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi,Utumishi na Utawala bora George Simbachawene akisaini kitabu mara baada ya alipowasili makao makuu ya ofisi hizo mjini Dodoma.
 
WAZIRI wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi,Utumishi na Utawala bora George Simbachawene amewaagiza wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurungenzi wote wa halmashari nchini kuhakikisha wanazoa taka zote zilizokusanywa wakati wa siku ya uhuru kabla ya tarehe 20 mwezi huu.Kauli hiyo aliitoa wakati alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa Wizara hiyo wakati wa kikao cha kumkaribisha katika ofisi ya Tamisemi mjini Dodoma.

Alisema kuwa hataki kuona hadi ifikapo tarehe 20 ya mwezi huu kuwa uchafu wa siku ya uhuru bado unaendelea kulalamikiwa na watu kuwa bado haijaondolewa katika maeneo uliokusanywa.“Hadi ifikapo tarehe hiyo sitaki kusikia uchafu bado haujaondolewa katika maeneo ulipokusanywa toka siku ya uhuru lakini pia unapoondolewa huo kuna uchafu mwingine unakuja hivyo basi watendaji wanaohusika wa hakikishe kuwa wanaanda maeneo ya kuupeleka”alisema Simbachawene.

Aidha aliwataka watumishi wa Tamisemi kubadilika katika utendaji wa kazi zao na kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwani awamu ya tano ya haitaendelea kuwalea watendaji wavivu.Kwa upande wake,Naibu Waziri wa wizara hiyo Suleiman Jaffo, aliwataka watumishi wa Tamisemi kubadilika katika utendaji wao wa zamani ili waweze kuongeza ukusanyaji wa mapato na kuweza kuboresha maisha ya wananchi.

KAMPUNI YA TINGATINGA IMEINGIA MKATABA NA KAMPUNI YA BRICOLEUR HOLDINGS Co.LIMITED YA JAPAN.

0
0
Mkurugenzi wa Kampuni ya Bricoleur Holdings ya nchini Japan, Bi. Yu Shiran (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu kushirikiana kufanya kazi za sanaa na Kikundi cha Sanaa cha Tingatinga, leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO). Kulia ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Sanaa Tingatinga, Bwana Zachi Chimwanda na kushoto ni Mkurugenzi pia wa Kampuni ya Bricoleur Holdings ya nchini Japan, Bwana Shoji Tsuchiya.
Kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Bwana Godfrey Mngereza akiwa na wanakikundi cha Sanaa cha Tingatinga na wajapani wakonyesha vibao vilivyochorwa na kikundi cha Sanaa cha Tinga Tinga jijini Dar es Salaam leo.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Bwana Godfrey Mngereza (kushoto) akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kusaini Mkataba wa makubaliano kati ya Kikundi cha Sanaa cha Tingatinga na Kampuni ya Bricoleur Holdings ya nchini Japan. Katikati ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Bricoleur Holdings ya nchini Japan Bwana Shoji Tsuchiya pamoja na Bi. Yu Shiran. 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Bricoleur Holdings ya nchini Japan Bwana Shoji Tsuchiya (kulia) wakibadilishana mikataba na kupeana mikono na Mwenyekiti wa Kikundi cha Sanaa cha Tingatinga, mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam katika wa mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO). Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo ya Japan Bi. Yu Shiran. 
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwasikiliza na wakati wa kusaini wa Mkataba wa Makubaliano ya kufanya kazi na Kikundi cha Sanaa cha Tingatinga na Kampuni ya Bricoleur Holdings ya nchini Japan uliofanyika leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO)
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii..

Na Zainabu Hamis,Globu ya Jamii. 
CHAMA Cha Wasanii wa uchoraji picha aina ya Tingatinga imeingia mkataba wa miaka tano (5) na kampuni ya Bricoleurholdings Co.Limited ya nchini Japan, kwa ajili ya kuwatafutia soko nchini Japan 

Makabidhiano ya Mkataba huo yamefanyika leo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. 

Mwakilishi wa Kampuni ya Bricoleurholdings Co.Limited, Shoji Tsuchiya amemkabidhi mkataba huo Mwenyekiti wa Chama Cha Tingatinga, Zack Chimwanda, amesema kuwa kazi hii ya uchoraji wa picha aina ya Tingatinga imeanza nchini Tanzania ikiwa na mwanzilishi wake Edward Said Tingatinga ambaye alifariki dunia mwaka 1970 na jina la hilondipo lilipopatikana kutokana na yeye. 

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Hakimiliki Nchini (Cosota) Doreen Sinane,amesema kuwa kampuni ya BricoleurholdingsCo,Limited itakuwa inafanya kazi ya kuuza na kutafuta soko la picha zinazotengenezwa na wanachama wa Tingatinga. 

Kwa upande wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Godfrey Ngereza, amesema kuwa sanaa ya uchoraji ni kazi kama kazi nyingine pia ni biashara inayomfanya msanii kupata kipato pamoja na kuliingizia taifa mapato.

WAZIRI UMMY MWALIMU AWATAKA WATUMISHI WA SEKTA YA AFYA KUTOFANYA KAZI KWA MAZOEA

0
0

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (aliyesimama) akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika leo (15.12.2015) Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Donald Mmbando na wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Hamis Kigwangalla.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (aliyesimama) akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika leo (15.12.2015) Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Donald Mmbando na kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Hamis Kigwangalla.

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika leo (15.12.2015) Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wa nne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii mara baada ya kulifungua Baraza hilo leo (15.12.2015) Jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Hamis Kigwangalla (wa tano kutoka kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Donald Mmbando.

PICHA NA ISMAIL NGAYONGA- MAELEZO 

Na Ismail Ngayonga
MAELEZO
Dar Es Salaam
15.12.2015
SERIKALI imewatakawatumishi wa sekta ya afya nchini kutofanya kazi kwa mazoea na badala yake kufanya kazi kwa bidii na uadilifu ili kufikia malengo yaliyowekwa.
Hatua hiyo inaelezwa itasiaidia kurahisisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wananchi kwa kutoa huduma bora na zinazofikiwa kwa wakati.
Akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema kila mtumishi wa umma anapaswa kutekeleza kwa bidii ilani ya Chama Tawala ya mwaka 2015.
“Sekta ya Afya imeingizwa kwenye mpango wa Tekeleza kwa Matokeo makubwa sasa, ili tuyakifia matokeo makubwa sasa pamoja na mambo mengine tunahitaji kubadilika sana katika utendaji wetu wa kazi” alisema Mwalimu.
  Aidha Waziri huyo alisema alisema pamoja na mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa katika sekta ya afya, Wizara hiyo hiyo hiyo haina budi kuakabiliana na chyangamoto mbalimbali zinazojitokeza ikiwemo vifo vya akina mama wajawazito wakati wa kujifungua.
Kwa mujibu wa Waziri Mwalimu aliwataka watumishi wa Wizara hiyo kutekeleza kwa vitendo maagizo yaliyotolewa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika hotuba yake ya kuzindua Bunge la 11, kwani hotuba yake ni dira ya maelekezo rasmi ya masuala muhimu yanayopaswa kutekelezwa na kusimamiwa katika kipindi cha miaka mitano.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Donald Mmbando alisema katika kutekeleza mpango wa tekeleza kwa matokeo makubwa sasa, Serikali imeanisha maeneo 4 ya utekelezaji ili kuboresha huduma bora za afya kwa wanachi.
Dkt. Mmbando alianisha maeneo hayo kuwa ni pamoja mgawanyo wa watumishi wa kada ya afya, upatikanaji wa dawa, vifaa,  vifaa tiba na vitendanishi, ubora wa huduma pamoja na kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto.
“Katika kutekeleza haya, wiki ijayo tutazindua mpango mkakati wa miaka 5 wa sekta ya afya (2016-20), ambapo tutahakikisha kuwa yote yaliyoanishwa katika Ilani ya Chama Tawala tunaweza kuyafikia na kuyatekeleza” alisema Dkt. Mmbando

MAWAKILI ZINGATIENI MAADILI YA TAALUMA YA SHERIA - JAJI MKUU

0
0
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande akizungumza na Mawakili 104 walioapishwa leo jijini Dar es salaam. Mhe. Chande amewataka Mawakili hao kufanya kazi zao kwa kuzingatia weledi na maadili ya taaluma yao.

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande (katikati) akiwa na Majaji na Watendaji wa Mahakama wakati wa zoezi la kuwaapisha Mawakili wapya 104 katika viwanja vya Karimjee leo jijini Dar es salaam.
Juu na Chini - Mawakili wakiwa wamesimama mbele ya Jaji Mkuu kabla ya kuapishwa.

Mawakili walioapishwa wakiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mkuu Mhe. Othman Chande na Watendaji wa Mahakama ya Tanzania.


Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande akiongoza maandamano ya Majaji na Watendaji wa Mahakama wakati wa hafla ya 53 ya kuwapokea na kuwaapisha Mawakili wapya 104 iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee leo jijini Dar es salaam.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju (kulia) akiwasili katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo wakati wa hafla ya 53 ya kuwapokea na kuwaapisha Mawakili wapya 104.


                                           (Na. Aron Msigwa - Dar es salaam).


Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande amewataka Mawakili kote nchini kufanya kazi zao kwa kuzingatia weledi na maadili ya taaluma ya Sheria na kwamba wasisite kuwaeleza ukweli wateja wao wanaopeleka mashauri Mahakamani ili kuepuka kupoteza muda na gharama katika masuala yanayoweza kupatiwa ufumbuzi nje ya Mahakama.


Akizungumza na Mawakili wapya 104 waliohitimu Shule ya Sheria  kwa mwaka 2015 wakati wa hafla ya 53 ya kuwapokea na kuwaapisha iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee leo jijini Dar es salaam amesema kuwa msingi mkubwa wa kazi yao umejengwa katika uzingatiaji wa maadili ya taaluma ya sheria.


Amewataka Mawakili hao kubadilika kifikra kwa kuwa Mawakili Bora ili kujenga imani na uaminifu kwa jamii wanayoihudumia na kuongeza kuwa sasa wameingia kwenye utaratibu wa kutambuliwa rasmi na Mahakama ya Tanzania kwa kuwezeshwa kufanya shughuli za uwakili kwenye mahakama ya Tanzania maeneo mbalimbali nchini.


Naomba mtambue kuwa kila Wakili ni Ofisa wa Mahakama hivyo mnao wajibu na jukumu la kusoma, kufuatilia mashauri mbalimbali ili kuwa na uhakika wa kesi mnazosimamia kuliko kuzitegemea Mahakama


Aidha, ameeleza kuwa yapo mambo ambayo yamekua yakifanywa na baadhi ya Mawakili wasio waaminifu yanayochafua sura ya Taaluma ya Sheria ikiwemo kutumia nyaraka za kughushi, kuvunja Kanuni na Maadili ya Taaluma huku baadhi yao wakijikuta wakiingia katika mgogoro na Mamlaka zinazosimamia kitaaluma taaluma hiyo.

Nawataka mzingatie sheria, kanuni na Maadili ya Uwakili, hata hivyo tuna chombo kinachosimamia maadili yenu, wapo takribani 176 waliokiuka maadili na hawa wanashughulikiwa kwa mujibu wa Sheria ili kulinda maadili na utendaji wa taluma yenu Amesisitiza Mhe. Othman.

Amewataka  watimize wajibu wao kwanza kwa wananchi watakaouhudumia pamoja na Mahakama ya Tanzania ambayo inawataka kufanya kazi zao kwa kuzingatia Sheria,  kanuni na taratibu zilizowekwa.

Mhe. Othman amefafanua kuwa Mahakama ya Tanzania inaendelea na Mkakati wa kupunguza mrundikano wa Kesi Mahakamani kwa kuhakikisha kuwa kesi zote zinazofikishwa Mahakamani  zinamalizika katika kipindi cha chini ya mwaka 1.

Ameeleza kuwa silimia 47 ya kesi zaidi ya 200 zilizokuwepo Mahakama Kuu katika kipindi cha miaka 4 iliyopita zimeendelea kusisikilizwa kwa ubora na sasa zimebaki asilimia 17 ya kesi hizo jambo linaonyesha kuongezeka kwa ufanisi wa Mahakama.

Kwa upande wake Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju akiwakaribisha Mawakili hao katika familia ya sheria Tanzania amesema kuwa katika jamii wanao mchango mkubwa katika kuhakikisha Haki na Usawa vinadumishwa nchini.

Amesema mawakili hao kabla ya kuapishwa na kuingizwa kwenye utaratibu wa kutambuliwa kuwa Mawakili wamepitia na kufauru vigezo vya kitaaluma vilivyowekwa ili kulinda heshima ya Taaluma ya sheria nchini.Amewaeleza kuwa mara baada ya kupokea viapo vyao wameingia kwenye utumishi wa umma kutekeleza majukumu yao ya kikatiba na kuongeza kwamba wao kama wanasheria wanatakiwa kuzingatia weledi wa taaluma yao. 

Amewataka kuwa makini katika utendaji wao kwa kuepuka kuwa sehemu ya migogoro na kuepuka kuegemea upande wowote watakapokuwa wakitimiza majukumu yao ili kuendelea kujenga jamii ya kistaarabu na ya kidemokrasia.

" Naomba mkumbuke kuwa mna wajibu mkubwa kwa watu mtakaokuwa mnawahudumia, zingatieni maadili maana ninyi sasa ni sehemu ya Mahakama ya Tanzania, fanyeni kazi kwa weledi na umakini mkubwa" Amesisitiza.Amesema utekelezaji wa majuku yao ya kila siku ni sehemu ya utumishi wao katika umma hivyo wasiruhusu aina yoyote ya ukiukwaji wa maadili yakitika kutimiza majukumu yao na kuwasaidia wananchi wasiokuwa na kipato/ wananchi masikini watakakao omba msaada wao wa kisheria.  

Aidha amewataka wawe wabunifu, kufanya kazi kwa bidii na kujiendeleza pale inapowezekana ili waweze kuwa msaada kwa wananchi walio na kiu ya kupata huduma kutoka kwao.Kwa upande wake Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Charles Rwechungura akizungumza wakati wa wa kuwakaribisha mawakili hao 134 amesema kuwa wao kama Chama cha Wanasheria wanayofuraha ya kuwakaribisha wanachama wapya kwenye uwanja wa Sheria nchini.

Amesema mawakili hao wameingia katika wakati muafaka kuongeza nguvu katika kuwahudumia wananchi huku akieleza kuwa shule ya Wanasheria Tanzania itaendelea kutoa mafunzo na kusimamia viwango vya taaluma ya sheria nchini na kuwataka mawakili hao kulinda heshima ya taaluma ya sheria kwa kutoa huduma bora kwa umma.
 


TAFFA YAIBUA MAPYA YA UTOROSHAJI WA KONTENA

0
0
Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha (Taffa), Stephen Ngatunga (kulia), akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na njia zinazotumika kuiba mapato ya serikali bandarini na katika Idara ya Forodha, Jijini Dar es Salaam jana. kushoto ni maofisa waandamizi wa chama hicho. Picha na Mpigapicha Wetu

Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha (Taffa), Stephen Ngatunga (kushoto), akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na njia zinazotumika kuiba mapato ya serikali bandarini na katika Idara ya Forodha, Jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Ofisa Mwandamizi wa chama hicho, Ernest Kallaghe.


Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 
CHAMA cha Mawakala wa Forodha nchini (TAFFA) kimesema kuwa wizi wa kontena bandari ya Dar es Salaam na kusababisha serikali kukosa mapato ni tatizo la muda mrefu ambalo ni limekuwa likisababishwa na watumishi wa bandari.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Rais wa TAFFA, Steven Ngatunga amesema tatizo lilojitokeza ya uondoshaji wa kontena 329 katika bandari Kavu ya Azam ilitokana na baadhi ya watumishi wa baadhi ya benki na Bandari kuingilia taarifa katika mfumo na kusababisha serikali kukosa mapato. 

Ngatunga amesema kuwa tatizo la serikali kukosa mapato katika bandari ya Dar es Salaam walishagundua lakini serikali ilishindwa kuchukua hatua mpaka serikali ya awamu ya tano kugundua hilo na hatua zimechukuliwa kwa wale waliohusika.

Amesema TAFFA itatoa ushirikiano kwa kile ambacho wanakiona katika bandari ya Dar es Salaam juu ya watu wanaosababisha serikali kukosa mapato kwa maslahi yao binafsi.

Aidha amesema kuwa kuna kampuni zilionekana kuwa zipo kwa ajili ya kukwepa kodi ya serikali ambazo chama kiliona na kupeleka malalamiko ambayo mwisho wa siku kukawepo urasimu wa kukutana viongozi ambao wanaweza kushughilikia hilo.

Amesema baadhi ya mawakala walilipia kontena lakini wanaambiwa malipo hayakufanyika huku wakiwa na kumbukumbu za malipo na kusababisha kutilia shaka juu ya uadilifu wa watumishi wa benki pamoja na bandari.

TAFFA imesema haiko tayari kwenda na mawakala ambao wanaharibu taaluma hiyo na kusababishia serikali kukosa mapato ambayo ndio ya kufanyia maendeleo nchini.

Amesema kuwa kuna kampuni 73 zimefungwa wakati hawahusiki katika katika uondoshaji wa kontena katika bandari na bandari kavu kutokana na kampuni hizo kuwa kulipia kontena zinazodaiwa kukwepa kodi.

CHAMA CHA SANAA CHA TINGATINGA CHATILIANA SAINI MKATABA WA MIAKA MITANO WA KUFANYA KAZI NA KAMPUNI YA BRICOLEUR HOLDINGS YA NCHINI JAPAN

0
0
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Bricoleur Holdings ya nchini Japan, Bi. Yu Shiran (katikati) akiongea na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu kushirikiana kufanya kazi za sanaa na Kikundi cha Sanaa cha Tingatinga, leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO). Kulia ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Sanaa (Tingatinga), Bwana Zachi Chimwanda na kushoto ni Mkurugenzi pia wa Kampuni ya Bricoleur Holdings ya nchini Japan, Bwana Shoji Tsuchiya.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Bwana Godfrey Mngereza (kushoto) akifafanua jambo wakati wa utiaji saini wa Mkataba wa makubaliano kati ya Kikundi cha Sanaa cha Tingatinga na Kampuni ya Kampuni ya Bricoleur Holdings ya nchini Japan. Katikati ni Wakurugenzi wa Kampuni ya Bricoleur Holdings ya nchini Japan Bwana Shoji Tsuchiya pamoja na Bi. Yu Shiran.



Na Tupokigwe Marco na Mwanahamisi Matasi

Chama cha Sanaa cha uchoraji picha maarufu kama Tinga Tinga kimetiliana saini Mkataba wa Makubaliano wa miaka mitano wa kufanya kazi kwa pamoja na Kampuni ya  Bricoleur Holdings Co. Ltd ya nchini Japan utakaokiwezesha chama hicho kunufaika kwa kuuza kazi zake Kimataifa.

Akiongea leo wakati wa utiaji saini wa Mkataba huo, Mwenyekiti wa Chama cha Sanaa cha Tinga Tinga, Bwana Zachi Chimwanda ameeleza kuwa, utiaji saini wa Mkataba huo utakua chachu ya maendeleo katika kuwakomboa wasanii wachoraji katika kipato chao na kuboresha hali zao za kimaisha kwakuwa kazi zao sasa zitakuwa zikiuzwa ndani na nje ya nchi.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Wasanii la Taifa (BASATA), Bwana Godfrey Mngereza alieleza kuwa Mkataba waliosaini kati ya Tinga Tinga na watu wa Bricoleur Holdings Co. Ltd utaimarisha kazi za Wasanii katika fani ya uchoraji ikiwemo kuongeza vipato vyao.

''Sanaa ni kazi lakini pia ni biashara, imefika wakati kwa wasanii kufaidika na jasho lao, kampuni hii watakua wakitafuta masoko kule Japan ili kazi hizi za wachoraji toka Tanzania ziweze kununuliwa hali ambayo itawaongezea kipato'', alisema Mngereza.

Aliongeza kuwa Mkataba uliosainiwa kati ya pande zote mbili umepitia taratibu zote za kiserikali na Taasisi zinazohusika na mambo ya sanaa na maslahi ya msanii na msanii yule aliyehusika katika kuchora picha fulani atanufaika na mkataba huo.

''Kwa msanii atakehusika binafsi na uchoraji picha mkataba utamwezesha kujua atanufaika vipi na kwa muda gani'', aliongeza Mngereza.Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Bricoleur Holdings Co. Ltd, Bi. Yu Shiran ameeleza kuwa mpango huo wa Mkataba kati yao na Tingatinga una lengo la kukitangaza Chama hicho cha wachoraji wa Tanzania Kimataifa.

‘’Kwa kutumia taarifa za kidijiti za Tingatinga tutaweza kushirikiana na watengenezaji mbalimbali wa bidhaa, na ili kulithibitisha hili, sisi na Tingatinga tumekuwa katika mjadala wa takriban mwaka mzima sasa’’, alisema Bi. Shiran.

Tinga Tinga Arts Group lilianzishwa nchini Tanzanja na Edward Saidi Tingatinga ambaye alifariki mwaka 1972 ambapo kwa sasa kundi hilo lipo maeneo ya Oysterbay jijini Dar es Salaam kikijihusisha na sanaa ya uchoraji.

MVUA ILIONYESHA LEO JIJINI DAR

0
0
 Mvua zilizonyesha asubuhi ya leo zimesabisha baadhi ya barabara kufunikiwa na maji na kusabisha adha ya usafiri  leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel  Massaka wa Globu ya Jamii)

BEI YA MADAFU LEO

0
0

WAZIRI NAPE NNAUYE AKUTANA NA UONGOZI WA CHAMA CHA WAFANYAKAZI WA TBC OFISINI KWAKE LEO

0
0
 Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na Viongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) walipimtembelea ofisini kwake.
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akiwasikiliza Viongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) walipimtembelea ofisini kwake.

 (Picha na Benjamin Sawe –WHUSM)

WAZIRI WA KILIMO ATOA SAA 48 KWA KAMPUNI YA SPARKWAY LTD KULIPA BILLION 3.4 KWA WAKULIMA WA KOROSHO

0
0
 Waziri wa Kilimo Uvuvi na Mifugo Mwigulu Lameck Nchemba akizungumza mbele ya Wanahabari mapema leo (hawapo pichani),ambapo Mh Nchemba ameiamuru kampuni ya Sparkway ltd ndani ya masaa 48 kuwalipa wakulima wa korosho wa Mkoa wa pwani, kiasi cha Bilioni 3.4 za mauzo ya korosho kufuatia agizo hilo,Wakulima waliouza Korosho  wataanza kulipwa jumatatu ya Desemba 21, mwaka huu.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Kilimo Uvuvi na Mifugo Mwigulu Lameck Nchemba wakati akizungumza mkoani Pwani leo.

MAKAMPUNI YA MAWASILINANO YA SIMU YATAKIWA KUBORESHA HUDUMA BORA KWA WATEJA WAO ILI KUONDOA MALALAMIKO

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya akifungua semina ya kuwaelimisha na kuwahamasisha watumiaji wa Huduma za Mawasiliano iliyoandaliwa na Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA-CCC) katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya Desemba 15 -2015 ).
Picha Emanuel Madafa 
Mwenyekiti Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA-CCC)Ndugu Stanley Mwabulambo (kulia) pamoja na Meneja wa Mawasiliano TCRA Kanda ya Nyanda za juu kusini Mhandisi Lilian Mwangoka wakimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro katika ufunguzi wa semina ya kuwaelimisha na kuhamasisha watumiaji wa huduma za Mawasiliano Mkoa wa Mbeya Desemba 15 katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya. 
Wananchi na baadhi ya watumishi wa serikali na mashirika binafsi wakisikiliza kwa Makini Hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro katika semina ya kuwaelimisha na kuwahamasisha watumiaji wa huduma za Mawasiliano Mkoa wa Mbeya Desemba 15 mwaka huu katika Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya. 
Watumiaji wa huduma za mawasiliano Mkoa wa Mbeya wakifatilia kwa makini hotuba ya mkuu wa mkoa wa mbeya Abbasi Kandoro. 
Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Ndugu Mariam Mtunguja akizungumza katika semina ya kuwaelimisha na kuhamasisha watumiaji wa wa huduma za Mawasiliano Mkoa wa Mbeya Desemba 15 Mwaka huu katika Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya. 
Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Ndugu Stanley Mwabulambo akitoa neo katika semina hiyo ya kuelimisha na kuhamasisha watumiaji wa Huduma za mawasiliano Mkoa Mbeya Desemba 15-2015 katika ukumbi wa Mkapa jijini mbeya. 
Wadau wakifuatilia mkutano 
Kaimu Katibu mtendaji Baraza la Ushauri watumiaji wa Huduma za Mawasiliano TCRA-CCC Ndugu Mary Msuya akiwasilisha maada kwa wanasemina juu ya haki na wajibu wa Mtumiaji wa huduma za Mawasilino katika semina hiyo yenye lengo la kuelimisha na kuhamsisha watumiaji wa huduma hizo Desemba 15 mwaka huu katika Ukumbi wa Mikutano Mkapa jijini Mbeya. 
Mhandisi toka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Kanda ya Nyanda za juu kusini Mbeya ( TCRA( Asajile Mwakisisile akitoa maada katika semina hiyo. 
Mmoja wa washiriki katika semina hiyo akichangia katika semina . 
Mjumbe wa Baraza la Huduma za Mawasiliano (TCRA-CCC) Ndgugu Nyanda Shuli akitoa Maada juu ya Muundo ,Kazi na Majukumu ya Baraza la watumiaji wa Huduma za Mawasiliano katika semina ya kuelimisha na kuhamasisha watumiaji wa huduma za mawasiliano Mkoa wa Mbeya Desemba 15 mwaka huu katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mkapa jijini Mbeya. 
Washiriki wa semina hiyo ya Uhamasishaji na uelimisha wa huduma za Mawasilino wakifuatilia kwa Makini semina hiyo. 
Picha ya pamoja na Meza Kuu. 
Na EmanuelMadafa,Mbeya(jamiimojablogu )
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro ameyaasa Makampuni ya huduma za Mawasiliano ya Simu Nchini kuhakikisha yanaboresha huduma zao kwa kuhakikisha yanaondoa kero zote anazo kutana nazo mtumiaji wa mawasilino hayo.


Amesema moja ya changamoto inayowakwaza watumaiji wa mawasilino hayo ni pamoja na kuweka matangazo ya simu (Miito ya simu)ambapo hukatwa kiasi cha pesa pasipo makubalino.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro ametoa kauli hiyo jijini Mbeya wakati akifungua semina ya kuelimisha na kuhamasisha watumiaji wa huduma za mawasiliano iliyondesha na Baraza la Ushauri la watumiaji wa huduma za mawasilino TCRA-CCC katika ukumbi wa Mkapa jijini humo.

Amesema pamoja na kutambua mchango wa makampuni yanayotoa huduma hizo za mawasiliano katika kuleta maendeleo ,nivyema makampuni hayo yakahakikisha yanatoa huduma zenye ubora wa hali ya juu unaonekana na thamani inayolipwa na watumiaji wa huduma hizo sanjali na kutimiza majukumu yao kwa watumiaji kama yalivyo ainishwa katika sheria na kanuni za leseni.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya amewataka watumiaji huduma hizo za mawasiliano ya simu kujikita katika matumizi bora ya mitandao ya simu badala ya kujingiza katika matumizi yasiyo sahihi ambayo yamekuwa yakichangia kwa kiwango kikubwa kuondoa maadili katika jamii pamoja na uchochezi.

Amesema kuwa sheria ya makosa ya mitandao nchini namba 14 inaweka wazi juu ya adhabu atakayo weza kutolewa dhidi ya mtu au kikundi kitakacho husika na upotoshwaji wa aina yoyote .

Amesema sheria ya makosa ya mitandao inaanisha makosa na adhabu zinazohusiana na matumizi ya mfumo wa kompyuta na teknolojia ya habari na mawasilino.

Hata hivyo Mkuu huyo wa mkoa wa mbeya ametumia fursa hiyo kulitaka baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za mawasiliano TCRA- TCCC kuendelea kuhamasisha ,kuelimisha pamoja na kutambua na kuelewa kero na matalajio ya watumiaji wa huduma za mawasiliano nchi.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa huduma za mawasiliano Ndugu Stanley Mwabulambo ametoa wito kwa Makampuni yote yaliyojikita katika uwekezaji wa mawasiliano ya simu ,huduma za utangazaji na huduma za posta kuhakikisha wanaendelea kujenga mitandao ya huduma zao nchi nzima ili kuwawezesha wananchi kushiriki katika maendeleo.

Aidha Mwenyekiti huyo ameviomba vyombo vya habari nchini kusaidia kulitangaza Baraza hilo na shughuli zake ili wananchi wajue ni wapi pa kupata ushauri na kutatua matatizo yao yanayohusiana na huduma za mawasiliano.

Katika semina hiyo pamoja na kutoa elimu kwa watumiaji Baraza pia limeunda kamati ya watumiaji wa huduma za mawasililiano kwa mkoa wa mbeya ambapo wajumbe wa kamati hiyo walichaguliwa kutoka miongoni mwa wanasemina ambapo majukumu yao yatakuwa ni kuelimishajamii juu ya haki wajibu na utaratibu wa kuwasilisha malalamiko sanjali na kupokea toka kwa watumiaji na kuyawasilisha kwa baraza.

Wazee TAFF: Tuna imani na Mwakifwamba

0
0
Msemaji wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Ahmed Olotu (mzee Chilo) akisoma waraka  wa kupinga uamuzi wa Rais wa Shirikisho hilo Bwana Simon Mwakifwamba wa kutogombea tena nafasi ya Urais wa Shirikisho hilo katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO). Kushoto ni Mzee Ramadhani Ditopile.
Mmoja wa wazee wanaounda Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) mzee Hamisi Kagaye (kushoto) akichangia mada wakati wa kupinga uamuzi wa Rais wa Shirikisho hilo Bwana Simon Mwakifwamba wa kutogombea tena nafasi ya Urais wa Shirikisho hilo katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO). Kulia ni Mzee Ramadhani Ditopile.
Mmoja wa wazee wanaounda Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Bi. Salome Nonge (kulia) akichangia mada wakati wa kupinga uamuzi wa Rais wa Shirikisho hilo Bwana Simon Mwakifwamba wa kutogombea tena nafasi ya Urais wa Shirikisho hilo katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO). Kushoto ni Mzee Ramadhani Ditopile na anaemfutaia ni Mzee Ahmed Olotu.
Baadhi ya Waandishoi wa Habari wakifuatilia tamko la Wazee wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) lililohusu kupinga uamuzi wa Rais wa Shirikisho hilo Bwana Simon Mwakifwamba wa kutogombea tena nafasi ya Urais wa Shirikisho hilo katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO).

(Picha zote na Benedict Liwenga)



Na Skolastika Tweneshe na Tupokigwe Marco. ­­

Wazee wa shirikisho la filamu Tanzania (TAFF)  hawajakubaliana na  uamuzi wa Rais wa shirikisho hilo Bw. Simon Mwakifwamba  kutogombea  tena nafasi ya Uraisi katika shirikisho hilo.

Akizungumza  na waandishi wa  habari  leo  jijini  Dar es Salaam, Msemaji wa wazee wa Shirikisho hilo Bw. Ahmed Olotu  maarufu kama Mzee Chilo amesema kuwa wao kama Wazee wakongwe katika Shirikisho hilo wamemuomba Rais huyo agombee tena  wadhifa  huo kwa mara nyingine ili aweze kumalizia mambo muhimu ya maendeleo katika tasnia ya sanaa.

“Sisi  kama wasanii na Wazee wakongwe katika tasnia hii, bila kushurutishwa na mtu yeyote  tunapinga uamuzi wake wakutotaka kugombea tena nafafasi hiyo .” Alisema Olotu.

Aidha, ameongeza kuwa, miradi  kama TAFF Trust Fund, TAFF Creative Ltd na mingine mingi yenye kuhitaji umakini ambayo imehasisiwa chini uongozi wake inahitajika kumaliziwa kwani bado haijakamilika.

Kwa upande wake Bi. Salome Nonge (Mama Abdul)   ameeleza  kuwa, Bwana Mwakifwamba  ndiye aliyesaidia  kupatikana kwa Ofisi ya Wasanii pamoja na usafiri  katika  kazi  zao.

“Binadamu hakosi kasoro ila kwa Mwakifwamba ni  ndogo mno sasa  hatutaki mtu mwingine aje.”Bi Salome alisema.

Naye Bi. Salumu Ally (Mkasi)  ameeleza  kuwa uongozi  wa Mwakifwamba umesaidia wasanii kupata  haki zao kama hati miliki zilizowezesha kupata maendeleo ya kiuchumi kupitia sanaa wanaoifanya.

Hata hivyo sanaa ya filamu inakuwa kwa kasi nchini pamoja na changamoto zilizopo ambapo juhudi katika kutengeneza kazi zenye ubora zitakazoleta ushindani katika soko la kitaifa na kimataifa bado zinahitajika.

BENKI YA NMB YAZINDUA MFUMO WA KISASA WA UTUNZAJI WA TAARIFA ZA MIKOPO, WATEJA SASA KUPATA MIKOPO NDANI YA SIKU 4.

0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Plc Ineke Bussemaker akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu mfumo wa kisasa wa utunzaji wa taarifa za mikopo uliozinduliwa na Benki hiyo. Mfumo huo utatutumika kwenye kanzi data ya Mikopo ya Benki hiyo ( CRB's) na kuwawezesha wateja wakubwa na wadogo wa wanaoomba mikopo kutoka NMB kuipata ndani ya siku 1 hadi 4 kutokana na taarifa zao za mikopo kuendelea kuwepo kwenye mfumo wa Benki hiyo.

Afisa Mkuu Udhibiti wa Hasara wa Benki ya NMB Bw. Tom Borghols (wa pili kutoka kushoto) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) namna Benki ya NMB  inavyoongoza katika utoaji wa mikopo kwa makundi mbalimbali.


Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Wadogo wa Benki ya NMB Bw. Abbdulmajid Nsekela( kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu kuanzishwa kwa mfumo wa kisasa wa utunzaji wa taarifa za mikopo kwa wateja uliozinduliwa na Benki ya NMB na jinsi utakavyoongeza ufanisi kwa kuwawezesha wateja kupata mikopo kwa haraka. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Plc Ineke Bussemaker .

WAZIRI WA AFYA UMMY MWALIMU AKAGUA HUDUMA ZA AFYA MUHIMBILI

0
0

um3
Mtaalamu wa Mionzi kwenye chumba cha mashine ya MRI,  Job Joshua (kushoto) na Profesa Mseru (wa pili kulia) wakimpatia maelezo Waziri Ummy Mwalimu (katikati) wakati alipotembelea leo hospitali hiyo kukagua utengenezaji wa mashine hiyo. 
UM4
Mkuu wa Idara ya Mionzi, Dk Flora Lwakatare akitoa maelezo kwa Mheshimiwa Waziri kuhusu maendeleo ya utengenezaji wa mashine ya MRI leo asubuhi.
UM5
Mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu (katikati) akiwa na Profesa Mseru kuelekea kwenye chumba cha X-ray cha digitali.
UM6
Mkuu wa Idara ya Mionzi, Dk Flora Lwakatare (wa kwanza kulia) akimpatia maelezo mheshimiwa Waziri, Ummy Mwalimu (katikati) kuhusu utengenezaji wa mashine hiyo leo asubuhi.

UM7
Mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu akizungumza leo asubuhi na wagonjwa wanaosubiri vipimo katika hospitali hiyo.
UM8
Mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu akiwa katika chumba cha CT-SCAN, huku Mkuu wa Idara ya Mionzi, Dk Flora Lwakatare akimpatia maelezo jinsi mashine hiyo inavyofanya kazi wakati ikiwa nzima.
UM9
Mheshimiwa Waziri Ummy Mwalimu akifafanua jambo baada ya kupewa maelezo jinsi mashine hiyo inavyofanya kazi.
UM10
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Lawrence Mseru (kulia), Mheshimiwa Waziri, Ummy Mwalimu (katikati) wakimsikiliza mgonjwa aliyefika katika hospitali hiyo kwa ajili ya kupatiwa matibabu leo asubuhi. 
um1
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Ummy Ally Mwalimu akiingia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) leo asubuhi kwa ajili ya kukagua utengenezaji wa mashine ya MRI na CT- Scan.
um2
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Ummy Mwalimu akiwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Lawrence Mseru leo asubuhi katika hospitali hiyo.


MAJALIWA AKUTANA NA KATIBU MTENDAJI WA SADC

0
0
1F1
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Katibu Mkuu Mtendaji wa  SADC, Dkt. Stergomena Tax, ofisini kwake jijini Dar es salaam Desemba 16, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
1F2

NAIBU SPIKA ATEMBELEWA NA BALOZI WA CUBA

0
0
 Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt Tulia Ackson akimshuhudia Balozi wa Cuba nchini Mheshimiwa Jorge Lopez Tormo akisaini kitabu cha wageni wakati alipomtembelea ofisini kwake jiiji Dar es salaam.
Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt Tulia Ackson akifafanua jambo wakati akizungumza na Balozi wa Cuba nchini Mheshimiwa Jorge Lopez Tormo aliyemtembelea leo ofisini kwake jijini Dar es salaam.
Balozi wa Cuba nchini Mheshimiwa Jorge Lopez Tormo akifafanua jambo wakati akizungumza na Naibu Spika Mhe. Dkt Tulia Ackson alipomtembelea leo ofisini kwake jijini Dar es salaam.
Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt Tulia Ackson akiagana na Balozi wa Cuba nchini Mheshimiwa Jorge Lopez Tormo mara baada ya kufanya mazungumzo naye ofisin kwake jijini Dar es Salaam.

 (Picha na Ofisi ya Bunge).

Profesa Mwansoko awaaga watumishi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni

0
0
 Mkurugenzi wa maendeleo ya Utamaduni Profesa. Hermas Mwansoko akipokea zawadi ya picha inayoonyesha maisha ya kijijini wakat wa hafla kumugaa jana jijini Dar es Salaam.anayemkabidhi zawadi hiyo niMkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Utamaduni sehemu ya Sanaa Bibi. Leaha Kihimbi . Mkurugenzi huyo anastaafu rasmi kuanzia tarehe 25 Desemba 2015.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Profesa. Hermas Mwansoko akiwa katika picha ya pamoja na baadhi watumishi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni wakati hafla ya kumuaga rasmi Mkurugenzi huyo anayemaliza muda wake jana ofisini kwake. 

 Mkurugenzi wa maendeleo ya Utamaduni Profesa. Hermas Mwansoko akizungumza na watumishi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni wakati akiwaaga rasmi jana ofisini kwake. Mkurugenzi huyo anastaafu rasmi kuanzia tarehe 25 Desemba 2015.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Utamaduni sehemu ya Sanaa Bibi. Leaha Kihimbi akielezea jambo wakati wa hafla ya kumuaga Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni anayemaliza muda wake Profesa Hermas Mwansoko (kulia) jana jijini Dar es Salaam.

 Afisa Utamaduni wa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Msami akitoa neno kwa niaba ya watumishi wa Idara ya Utamaduni wakati wa hafla ya kumuaga Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni anayemaliza muda wake katika utumishi wa umma Profesa. Hermas Mwansoko jana jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya watumishi wa Idara ya Utamaduni wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea wakati wa hafla ya kumuaga Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni anayemaliza muda wake katika utumishi wa umma Profesa. Hermas Mwansoko jana jijini Dar es Salaam.


Picha na Frank Shija,WHVUM

RAIS MAGUFULI APOKEA UJUMBE MAALUM KUTOKA KWA WAZIRI MKUU WA JAPAN

0
0

MUFINDI YASHIKA UKWANZA MKOANI IRINGA

0
0
Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi ya Mkoani Iringa imeibuka mshindi wa kwanza kimkoa na kushika nafasi za juu kikanda na kitaifa, kati ya Halmashauri tano za Mkoa wa Iringa, baada ya kufanya vizuri zaidi wakati wa mbio za mwenge wa uhuru ulipokimbishwa Mkoani Iringa mnamo mwezi Juni mwaka huu.
  
Taarifa ya kitengo cha habari na mawasiliano cha Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imevitaja baadhi ya vigezo kati ya vigezo 10 vilivyoshindanishwa, kuwa ni pamoja na miradi yenye maslahi kwa umma iliyozinduliwa wakati wa mbio za mwenge wa uhuru, uimarishaji wa vikundi vya uzalishaji mali kwa wanawake na vijana.

Vigezo vingine vinavyozingatiwa ni pamoja na mapambano dhidi ya Malaria, dawa za kulevya, michango ya Mwenge wa uhuru sanjari na mapokezi ya mwenge wenyewe ulipowasili wilayani Mufindi

Akizunguzia ushindi huo, Mkuuwa wilaya ya Mufindi JOWIKA KASUNGA amewashukuru wakazi wa Mufindi na wadau wa maendeleo kwa michango yao pamoja na kushiriki mbio za Mwenge wa uhuru na akatoa rai ya kundelea kuuenzi mwenge wa uhuru kama alama na utambulisho wa taifa.

Aidha, taarifa hiyo imezitaja nafasi ilizoshika kuwa ni ushindi wa kwanza kimkoa, ushindi wa 05 kwa kanda ya kiuchumi yenye zaidi Halmashauri 36 pamoja na nafasi ya 22 kitaifa ikijumuisha zaidi ya Halmashauri 140.
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images