Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 708 | 709 | (Page 710) | 711 | 712 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya la Mufindi limemchagua  Diwani Festo Elia Mgina kutoka kata ya Mninga kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi na Diwani Ashery John Mtono kutoka kata ya Sadani kuwa Makamu Mwenyekiti.

  Akitangaza matokeo ya Uchaguzi wa baraza la madiwani, kwenyekiti wa uchaguzi huo ambaye pia ni Katibu tawala wa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi Bw. Allan Mwela, amesema jumla ya wapiga kula walikuwa 39 ambapo Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti walichaguliwa kwa kula 38 kwa kila mmoja huku mjumbe mmoja hakuweza kupiga kura.

   Akitoa sukran mara baada ya kutangazwa kwa matokeo Mh. Festo Mgina amewashukuru Madiwa wote kwa kumchangua na amewaomba wampe ushirikiano katika kutekeleza majukumu na ameahidi kuwatumikia wananchi wa mufindi kwa uwaminifu, kuzingata kanuni na taratibu ili kuleta maendeleo ya kweli kwa wanamufindi.

  Kwa upande wake Mkuuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Juma Masenza akizindua baraza hilo amewataka madiwani kuahakikisha watumishi wote waliopo katika kata zao hususani watendaji wa kata na vijiji wanafanya kazi kwa uwadilifu na kwa juhudi ili kutimiza dhana ya uwajibikaji na kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano ili kukomesha tabia ya kupokea mishahara inayotokana na kodi za umma pasipo kuwajibika.

  Ndimmyake MWAKAPISO
  Ofisa habari na Mawasiliano Mufindi DC.


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitangaza baraza lake la mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 10, 2015. Kulia kwake ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na kushoto ni Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitangaza baraza lake la mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 10, 2015. Kulia kwake ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na kushoto ni Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa. Kushoto kabisa ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.

  0 0


  Meya Mteule wa jiji la Mbeya Diwani wa Kata ya Nzovwe(CHADEMA) Ndugu David Mwasilindi ambaye aliibuka kidedea kwa kupata kura 34 dhidi ya Mpinzani wake wa CCM aliyepata kura 14 katika uchaguzi uliofanyika Desemba 10 katika ukumbi wa Mkapa jijini humo.
  Katibu Tawala Wilaya ya Mbeya Ndugu Quip Mbeyela ambaye ndiye aliyekuwa Mwenyekiti katika Kikao cha Baraza la Madiwani ambacho kiliketi kufanya uchaguzi wa kumpata Meya wa jiji hilo pamoja na Naibu Meya katika Halmashauri ya jiji la Mbeya .

  Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya jiji la Mbeya Dkt Samuel Lazaro akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani ambalo liliketi kwa ajili ya kumchagua Meya pamoja na Naibu Meya katika Ukumbi wa Mkapa jijini humo.

  Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Jiji la Mbeya Dkt Samuel Lazaro akiteta jambo na Meya Mteule wa jiji la Mbeya Mh.David Mwasilindi katika kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya jiji hilo.

  Wajumbe wa baraza la Madiwani Halmashauri ya jiji la Mbeya wakifuatilia kwa umakini majadiliano katika mkutano huo.


  Baadhi ya watumishi wa jiji la Mbeya wakiteta jambo katika mkutano huo wa baraza la Madiwani la Halmashauri ya jiji la Mbeya ambalo liliketi na kumchagua Meya na Naibu wa jiji hilo ambaye ni David Mwasilindi (CDM) baada ya kupata kura 34 dhidi ya mpinzani wake wa CCM aliyepata kura 14.

  Diwani akizungumza katika baraza hilo.

  Madiwani wakiimba wimbo wa taifa baada ya kukamiliza zoezi la uchaguzi katika baraza hilo la Madiwani halmashauri ya jiji la Mbeya .  Baadhi ya wananchi na wafuasi wa vyama mbalimbali jijini mbeya wakifuatilia kwa umakini uchaguzi wa kumpata Meya wa jiji la Mbeya na Naibu Meya wakiwa nje ya ukumbi wa Mkapa jijini humo .  Tukifuatilia Mkutano .


  Na EmanuelMadafa,Mbeya
  Hatimaye Halmashauri ya jiji la Mbeya limepata Meya wake mara baada
  ya kufanyika kwa uchaguzi wa kugombea
  nafasi ya Meya na Naibu Meya watakaoongoza halmashauri ya jiji la Mbeya katika
  kipindi cha miaka mitano ijayo.

  Meya huyo mpya wa jiji la mbeya ametokana na Chama cha Chadema Mch
  David Ponela Mwashilindi kutoka kata ya Nzovwe pamoja na Naibu wake Mch David Nelson Ngogo kutoka kata
  ya Nsalaga ambao wote wametokana na chama hicho.

  Katika uchaguzi huo uliofanyika Desemba 10 kwenye ukumbi wa Mkapa na kusimamiwa na Katibu
  tawala wa wilaya ya Mbeya Quip Mbeyela,alimtangaza mshindi wa Umeya kuwa ni
  Mwashilindi aliyepata kura 34 akimshinda mgombea wa nafasi hiyo kutoka
  CCM,Kefas Mwasote Changani aliyeambulia kura 14.

  Kwa upande wa nafasi ya Naibu Mbeya mshindi wa kura nyingi
  aliyetangazwa ni Mch Ngogo(Chadema) aliyeipata kura 34 dhidi ya mgombea wa CCM
  katika kinyang’anyiro hicho,Modest Pantaleo Shiyo aliyeambulia kura 14 na hivyo
  kukifanya chama cha Chadema kuongoza halmashauri ya jiji hilo.

  Mara baada ya kutangaza matokeo hayo yaliyowashirikisha madiwani
  wa Chadema 34 dhidi ya wale wa CCM 14,msimamizi wa uchaguzi huo,Mbeyela alisema
  kuwa vyama vyote vilivyoshiriki kwenye mchakato huo sasa umekwisha na
  wanachotakiwa kukifanya madiwani wote ni kuchapa kazi kwa nguvu ili kusukuma
  kwa kasi maendeleo ya jiji hilo.

  Akizugumza mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa nafasi ya
  Naibu Meya,Ngogo alisema kuwa atahakikisha kuwa anaheshimu haki na uhuru wa
  kila diwani katika kushauri na kutoa maoni bila kujali itikadi ya vyama vyao
  kwa kuwa kazi kubwa iliyo mbele yao ni kuwatumikia wananchi wote.

  Mstahiki Meya wa jiji hilo kutoka Chadema,Mwashilindi akiwashukuru
  madiwani wote kwa kura nyingi alizopigiwa,alisema kuwa atahakikisha kuwa
  anashirikiana na madiwani wote na kuhakikisha kuwa kata zote za jiji hilo
  zinapiga hatua kubwa na huo ndio mtazamo wake.

  Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji hilo,Dk Samwel
  Lazaro alisema kuwa atahakikisha watendaji wa halmashauri hiyo wanatoa
  ushirikiano wa kutosha kwa madiwani wote pale wanapohitaji ufafanuzi wa
  kitaalamu ili kila jambo wanalotaka kulifahamu wapate kwa wakati.

  (Jamiimojablog-Mbeya

  0 0


  0 0

  download (3)
  Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO), limetangaza tatizo la upatikanaji  wa huduma ya Maji katika maeneo yote yanayohudumiwa na mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu chini pamoja na baadhi ya maeneo ya Mji wa Bagamoyo mkoani Pwani kutokana na mtambo huo kuzimwa kwa wastani saa 24 siku ya Jumapili tarehe 13/12/2015.
  Sababu ya kuzimwa kwa mtambo huo ni  kuruhusu kufanya matengenezo na maboresho ya njia kubwa ya Maji inayohudumia eneo la Salasala na viunga vyake vyote.
   
  Akiongea na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam Kaimu Meneja uhusiano wa Dawasco, Bi. Everlasting Lyaro, ametoa wito kwa wateja na wananchi  wote kuhifadhi Maji ya kutosha na kuyatumia kwa matumiz ya muhimu ili kuweza kukidhi mahitaji husika kwa kipindi hicho.
   
  Tupo katika maboresho ya huduma ya Maji, mtambo wetu wa Ruvu chini utazimwa kwa takribani saa 24, tunawaomba wateja wetu muhifadhi Maji ya kutosha na kuyatumia vizuri mpaka maketengezo yatakapokamilika, nasi tutajitahidi kadri tuwezavyo kuhakikisha tunarejesha huduma ya Maji kwa wakati uliopangwa” alisema Bi. Lyaro
   
  Amebainisha kuwa matengenezo hayo  yatasababisha maeneo mengi  ya Jiji la Dar es Salaam kukosa huduma ya Maji ikiwemo Mji wote wa  Bagamoyo, Bunju, Boko, Tegeta, Kunduchi, Salasala, Jangwani, Mbezi beach na Kawe, Mlalakuwa, Mwenge, Mikocheni, Msasani, Sinza, Manzese, Mabibo, Kijitonyama, Kinondoni, Oysterbay, Magomeni, Upanga, Kariakoo, City Centre, Ilala, Ubungo Maziwa, Kigogo, Mburahati, Hospitali ya Muhimbili pamoja na eneo la Buguruni.

  0 0

   
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Hanne-Marie Kaarstad, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Dec 11, 2015 kwa mazungumzo.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Mhe. Hawa Ndilowe, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, jana Dec 10, 2015 kwa mazungumzo.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan, akiagana na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Hanne-Marie Kaarstad, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Mhe Makamu, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Dec 11, 2015.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Mhe. Hawa Ndilowe baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam,jana Dec 10, 2015. Picha na OMR
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Hanne-Marie Kaarstad (kulia kwake) na Mkurugenzi  wa Idara ya Ulaya na Marekani, Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine (kulia) na Msaidizi wa Balozi (kushoto) mara baada ya mazungumzo ao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo Desemba 11, 2015.
  MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA MABALOZI WA NORWAY NA MALAWI
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jana amekutana na Balozi wa Malawi nchini Tanzania na kufanya naye mazungumzo yaliyolenga kukuza uhusiano wa nchi hizi mbili, sambamba na kuongeza tija ya maendeleo huku wakifahamishana nia ya kuwa na miradi ya pamoja itakayolenga kuongeza uhusiano wa pamoja na kupunguza changamoto zinazozikabili nchi hizi.
  Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Makamu wa Rais leo Desemba 11, 2015 amekutana na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mheshimiwa Hanne-Marie Kaarstad ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo walizungumzia kuhusu uongezaji wa mahusiani na ushirikiano hasa katika suala la mazingira. Balozi Kaarstad ni mpya nchini Tanzania na ujio wake ameelezea kuwa unalenga katika kuongeza tija kwa nchi hizi mbili na kwamba Norway itabakia kuwa rafiki wa karibu wa Tanzania.
  Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
  Ikulu, Dar es Salaam

  0 0

  Katika kupambana na wimbi la kupunguza umaskini hapa nchini, kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania kupitia mpango wake wa “Airtel FURSA Tunakuwezesha” unaendelea kutoa mafunzo ya biashara ya ujasiriamali kwa vijana wenye lengo la kuwawezesha na kuwainua vijana hapa nchini .

  Mafunzo hayo ya biashara ambayo yamekuwa yakiendeshwa hapa nchini katika mikoa mbali mbali , wiki ijayo yatafanyika Dar Live  Mbagala Kuu karibu na Big Bon  siku ya Jumanne tarehe 15 ili kuwawezesha vijana kuweza kukabiliana na wimbi hili gumu la kuendesha biashara na kuweza kukidhi mahitaji yao ya kila siku na kuweza kuinua uchumi wa nchi hii.

  Akizungumzia kuhusu mafunzo hayo ambayo yamekuwa yakiendelea hapa nchini, Meneja huduma kwa jamii  wa Airtel , bi Hwa Bayumi, alisema “mafunzo haya yanalengo la kuwasaidia vijana wenye umri kati ya miaka 18- 24 ambao wanakiu ya kujikwamua na umasikini. Vile vile “Airtel FURSA Tunakuwezesha” Airtel inawawezesha vijana kwa kuwapatia elimu ya biashara na nyenzo za kuimarisha biashara zao.

  Hivyo basi tunapenda kuwakaribisha vijana wote waishio jijini Dar Es Salaam kuweza kuhudhuria mafunzo haya ambayo yatatolewa bure kabisa bila gharama yoyote. Ili kijana aweze kushiriki  anatakiwa kufika pale Dar Live siku ya jumanne tarehe 15 kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi jioni.

  Vile vile ili kijana kushiriki au kufaidika na mpango wa Airtel Fursa atatakiwa kutuma ujumbe mfupi kwenda kwa namba 15626 na kuweka maelezo yafuatayo:- Jina, Umri, aina ya biashara na eneo. 

  Pia wanaweza kutuma maombi yao kwa kupitia barua pepe airtelfursa@tz.airtel.com ambapo watatakiwa kutuma jina kamili, umri, na aina ya biashara. Maelezo kuhusu program ya Airtel FURSA pia yanapatikana kwenye tovuti ya Airtel www.airteltanzania.com> aliongeza, Bayumi.

  0 0

  Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Leah Kihimbi akitoa hotuba katika Warsha ya siku mbili kuhusu wasanii wanawake kupinga ukatili wa kijinsia, mafunzo hayo yamefanyika ili kuhitimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia na kusheherekea siku ya msanii Tanzania iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
  Rais wa Shirikisho la Sanaa za Maonyesho Tanzania Agnes Lukanga akitoa mada katika warsha ya siku mbili kuhusu wasanii wanawake kupinga ukatili wa kijinsia, mafunzo hayo yamefanyika ili kuhitimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia na kusheherekea siku ya msanii Tanzania iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.

  0 0

  Eliza Juma (30), mkazi wa Mtaa wa Mbwanga Manispaa ya Dodoma anaomba msaada wa hali na mali kutoka kwa yeyote ataeguswa ili aweze kufanyiwa upasuaji wa uvimbe tumboni ambao umekuwa ukiongezeka kila siku.

  Akizunguma na waandishi wa habari mjini hapa Dodoma, alisema kuwa uvimbe huo ambao umekuwa ukiongezeka kila siku umekuwa kikwazo kwake katika kutekeleza majukumu yake ya kujipatia kipato.

  Alisema kuwa uvumbe huo unaotokana na yeye kufanyiwa upasuaji wa utumbo aliofanyiwa miaka miwili iliyopita kutokana na utumbo wake kujikunja.

  “Nilifanyiwa upasuaji wa utumbo miaka miwili iliyopita katika hospitali ya mkoa wa Dodoma ambapo utumbo wangu ulikuwa umejikunja lakini mara baada ya kufanyiwa upasujai huo kidonda kilianza kuwasha na mimi nikawa napakuna ndipo pakaanza kuvimba hadi kufikia ukubwa huu unaouona sasa” alisema Eliza.

  Aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo alikwenda hopitali ya mkoa ili kuweza kuonana na daktali ambaye alimweleza kuwa tatizo hilo linatokana na ngozi ya ndani kulika hivyo anatakiwa kufanyiwa upasuaji kwa mara nyingine.

  Aidha alisema kuwa kutokanana hali yake ya kiuchumi na kiasi alicho ambiwa kulipia ili awze kufanyiwa upasuaji huo yeye hawezi kumudu kwakuwa hana msaada wowote anaoutegemea zaidi ya wasamailia wema.

  “Kiasi kinacho hitajika ili niweze kufanyiwa upasuaji ni zaidi ya shilingi laki tatu na mie kama mnavyo  hapa nilipo natunzwa na wasamilia wema sina mama wala baba hivyo nawaomba wasamalia wema kunisadia ili niweze kupata kiasi hicho kwaajili ya matibabu kabla tatizo halijawa kubwa zaidi”alisema Eliza.

  Alisema kuwa kwa yeyote atakaye guswa anaweza kumchangia anaweza kuwasiliana naye kupitia namba ya simu ya mkononi 0678164633ili aweze kupata kiasi hicho cha pesa na kupatiwa matibabu.

  0 0

  zi1

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akisalimiana na Uongozi wa Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji pamoja na Maofisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakati alipowasili Chuoni hapo kufunga mafunzo ya Sajini na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kozi ya Awali  yaliyofanyika hayo Chuoni hapo.
  zi2
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil, akikagua Gwaride la Heshima lililoandaliwa na Wahitimu wa Mafunzo ya Awali ya Sajini na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yaliyofanyika katika Chuo cha yaliyofanyika katika Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji, jijini Dar es Salaam.
  zi3
  Gwaride la Wahitimu wa Mafunzo yaKozi ya Awali ya Sajini na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji likipita mbele ya mgeni Rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (hayupo pichani) wakati wa kufunga mafunzo hayo katika Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji jijini Dar es Salaam.
  zi4
  Muhitimu wa Mafunzo ya Kozi ya Awali ya Sajini na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Semeni Daudi Chiunda, akipokea zawadi kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil, kutokana na kuwa Mhitimu Bora katika kipingere cha Ukakamavu wakati wote wa Mafunzo yaliyofanyika katika Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Abubakari Akida, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

  0 0

   Msemaji wa Wizara Mambo ya Ndani ya Nchi, Isaac Nantanga akizungumza na waandishi wa habari leo juu ya ufutaji wa vyama vya kijamii vilivyoshindwa kuendesha pamoja na kushindwa kulipa ada, kushoto ni Mwanasheria wa wizara hiyo, Berious Nyasembwa.
  Waandishi wa habari wakifatilia taarifa ya Msemaji wa Wizara Mambo ya Ndani ya Nchi, Isaac Nantanga leo jijini Dar es Salaam.
  Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

  Na Zainabu Hamisi, Globu ya Jamii.
  WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi imefuta vyama vya Kijamii 1,268 kutokana na kushindwa kutekeleza majukumu yao na sheria zilizowekwa katika uendeshaji wa vyama pamoja na mashirika yasiyo ya Kiserikali (NG’0s).

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Isaac Nantanga amesema kuwa kufutwa kwa vyama hivyo ni kutokana na kukiuka masharti ya uwendeshaji wa taasisi ikiwemo kutolipa ada kwa mujibu wa sheria.

  Katika ufutwaji wa vyama hivyo chama kimojawapo kilichofutwa ni chama cha wapiga picha nchini ambacho kimeshindwa kukidhi vigezo vya uendeshaji na kushindwa hata kuendesha vikao vyake.

  Nantanga amesema kuwa vyama vingine 1,406 vimepewa kusudio la kufutwa na baada siku 21 kuanzia leo, kama havitatoa kusudio la kujitetea basi navyo vitafutwa.

  Amesema kufuatana na kanuni ya vyama inayoundwa na kifungu cha 38 cha sheria ya vyama vyote vya kijamii vinapaswa kulipa ada ya kila mwaka.

  Aidha, amesema kanuni ya 6 za vyama za kijamii inayosomwa pamoja na kifungu cha 22 cha sheria ya vyama inavitaka vyama vya kijamii kuwasilisha taarifa za kila mwaka za hesabu zilizokaguliwa za mapato na matumizi ya vyama kwa msajili wa vyama.

  Aliongeza kuwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inatoa angalizo kwa vyama vyote vya kijamii kuendesha shughuli zake kwa kufuatana na sheria zilizoanzisha vyama hivyo.

  0 0  son5

  Mmoja wa waongoza ndege katika Uwanja wa Ndege wa Songwe, Bw. Emmanuel Mgaza akitoa maelezo ya jinsi ndege inavyoongozwa mpaka kutua kwa timu ya ukaguzi iliyotembelea uwanjani  hapo
  son1
  Jengo la kuingilia na kutokea wageni na kwenye uwanja wa ndege wa Songwe mkoani Mbeya linavyoonekana.
  son2
  Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo  kutoka Tume ya Mipango ikitembelea uwanja wa ndege wa Songwe kujionea maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo.
  son3
  Jengo la kuoongozea ndege ambalo limekamilika kwa asilimia 100.
  son4 
  Mmoja wa waongoza ndege katika Uwanja wa Ndege wa Songwe, Bw. Emmanuel Mgaza akitoa maelezo ya jinsi ndege inavyoongozwa mpaka kutua kwa timu ya ukaguzi iliyotembelea uwanjani  hapo

  0 0

  nai1 
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (kushoto) akizungumza na washiriki wa Warsha ya Majadiliano kuhusu Mpango Mkakati wa Utangamanisho wa Raia Wapya wa Tanzania. Warsha hiyo iliyowashirikisha Makatibu Wakuu wa wizara mbalimbali, Wakuu wa Vyombo vya Usalama, Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) pamoja na wadau mbalimbali  ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Protea Courtyard, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  nai3
  Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrison Mseke akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo, kufungua Warsha ya Majadiliano kuhusu Mpango Mkakati wa Utangamanisho wa Raia Wapya wa Tanzania. Warsha hiyo iliyowashirikisha Makatibu Wakuu wa wizara mbalimbali, Wakuu wa Vyombo vya Usalama, Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) pamoja na wadau mbalimbali ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Protea Courtyard, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  nai4Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Suzan Chekani akizungumza na washiriki (hawapo pichani) wa Warsha ya Majadiliano kuhusu Mpango Mkakati wa Utangamanisho wa Raia Wapya wa Tanzania. Warsha hiyo iliyowashirikisha Makatibu Wakuu wa wizara mbalimbali, Wakuu wa Vyombo vya Usalama, Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) pamoja na wadau mbalimbali ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Protea Courtyard, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  nai5 
  Mshauri Mwelekezi wa Mradi wa Utangamanisho, Profesa Bonaventure Rutinwa akitoa elimu ya utangamanisho wa mradi huo kwa Washiriki wa Warsha ya Majadiliano kuhusu Mpango Mkakati wa Utangamanisho wa Raia Wapya. Warsha hiyo iliyowashirikisha Makatibu Wakuu wa wizara mbalimbali, Wakuu wa Vyombo vya Usalama, Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) pamoja na wadau mbalimbali  ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Protea Courtyard, jijini Dar es Salaam leo. Wapili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo na Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi katika wizara hiyo, Harrison Mseke. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  nai6 
  Sehemu ya Washiriki wa Warsha ya Majadiliano kuhusu Mpango Mkakati wa Utangamanisho wa Raia Wapya wa Tanzania, wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba ya ufunguzi wa Warsha hiyo iliyowashirikisha Makatibu Wakuu wa wizara mbalimbali, Wakuu wa Vyombo vya Usalama, Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) pamoja na wadau mbalimbali  ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Protea Courtyard, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  nai7 
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo (watatu kushoto waliokaa), Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Suzan Chekani (wapili kushoto waliokaa), Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke (wapili kulia waliokaa), Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole (watatu kulia waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Warsha ya Majadiliano kuhusu Mpango Mkakati wa Utangamanisho wa Raia Wapya wa Tanzania. Warsha hiyo iliyowashirikisha Makatibu Wakuu wa wizara mbalimbali, Wakuu wa Vyombo vya Usalama pamoja na wadau mbalimbali  ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Protea Courtyard, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

  Meya Mteule wa jiji la Mbeya Diwani wa Kata ya Nzovwe(CHADEMA) Ndugu David Mwasilindi ambaye aliibuka kidedea kwa kupata kura 34 dhidi ya Mpinzani wake wa CCM aliyepata kura 14 katika uchaguzi uliofanyika Desemba 10 katika ukumbi wa Mkapa jijini humo.
  Katibu Tawala Wilaya ya Mbeya Ndugu Quip Mbeyela ambaye ndiye aliyekuwa Mwenyekiti katika Kikao cha Baraza la Madiwani ambacho kiliketi kufanya uchaguzi wa kumpata Meya wa jiji hilo pamoja na Naibu Meya katika Halmashauri ya jiji la Mbeya .
  Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya jiji la Mbeya Dkt Samuel Lazaro akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani ambalo liliketi kwa ajili ya kumchagua Meya pamoja na Naibu Meya katika Ukumbi wa Mkapa jijini humo.
  Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Jiji la Mbeya Dkt Samuel Lazaro akiteta jambo na Meya Mteule wa jiji la Mbeya Mh.David Mwasilindi katika kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya jiji hilo. 
  Wajumbe wa baraza la Madiwani Halmashauri ya jiji la Mbeya wakifuatilia kwa umakini majadiliano katika mkutano huo.

  Baadhi ya watumishi wa jiji la Mbeya wakiteta jambo katika mkutano huo wa baraza la Madiwani la Halmashauri ya jiji la Mbeya ambalo liliketi na kumchagua Meya na Naibu wa jiji hilo ambaye ni David Mwasilindi (CDM) baada ya kupata kura 34 dhidi ya mpinzani wake wa CCM aliyepata kura 14.
  Diwani akizungumza katika baraza hilo.
  Madiwani wakiimba wimbo wa taifa baada ya kukamiliza zoezi la uchaguzi katika baraza hilo la Madiwani halmashauri ya jiji la Mbeya .


  Baadhi ya wananchi na wafuasi wa vyama mbalimbali jijini mbeya wakifuatilia kwa umakini uchaguzi wa kumpata Meya wa jiji la Mbeya na Naibu Meya wakiwa nje ya ukumbi wa Mkapa jijini humo.
  Tukifuatilia Mkutano.
  Na EmanuelMadafa, Mbeya
  HATIMAYE Halmashauri ya jiji la Mbeya limepata Meya wake mara baada ya kufanyika kwa uchaguzi wa kugombea nafasi ya Meya na Naibu Meya watakaoongoza halmashauri ya jiji la Mbeya katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

  Meya huyo mpya wa jiji la mbeya ametokana na Chama cha Chadema Mch David Ponela Mwashilindi kutoka kata ya Nzovwe pamoja na Naibu wake Mch David Nelson Ngogo kutoka kata ya Nsalaga ambao wote wametokana na chama hicho.

  Katika uchaguzi huo uliofanyika Desemba 10 kwenye ukumbi wa Mkapa na kusimamiwa na Katibu tawala wa wilaya ya Mbeya Quip Mbeyela,alimtangaza mshindi wa Umeya kuwa ni Mwashilindi aliyepata kura 34 akimshinda mgombea wa nafasi hiyo kutoka CCM,Kefas Mwasote Changani aliyeambulia kura 14.

  Kwa upande wa nafasi ya Naibu Mbeya mshindi wa kura nyingi aliyetangazwa ni Mch Ngogo(Chadema) aliyeipata kura 34 dhidi ya mgombea wa CCM katika kinyang’anyiro hicho,Modest Pantaleo Shiyo aliyeambulia kura 14 na hivyo kukifanya chama cha Chadema kuongoza halmashauri ya jiji hilo.

  Mara baada ya kutangaza matokeo hayo yaliyowashirikisha madiwani wa Chadema 34 dhidi ya wale wa CCM 14,msimamizi wa uchaguzi huo,Mbeyela alisema kuwa vyama vyote vilivyoshiriki kwenye mchakato huo sasa umekwisha na wanachotakiwa kukifanya madiwani wote ni kuchapa kazi kwa nguvu ili kusukuma kwa kasi maendeleo ya jiji hilo.

  Akizugumza mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa nafasi ya Naibu Meya,Ngogo alisema kuwa atahakikisha kuwa anaheshimu haki na uhuru wa kila diwani katika kushauri na kutoa maoni bila kujali itikadi ya vyama vyao kwa kuwa kazi kubwa iliyo mbele yao ni kuwatumikia wananchi wote.

  Mstahiki Meya wa jiji hilo kutoka Chadema,Mwashilindi akiwashukuru madiwani wote kwa kura nyingi alizopigiwa,alisema kuwa atahakikisha kuwa anashirikiana na madiwani wote na kuhakikisha kuwa kata zote za jiji hilo zinapiga hatua kubwa na huo ndio mtazamo wake.


  Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji hilo,Dk Samwel Lazaro alisema kuwa atahakikisha watendaji wa halmashauri hiyo wanatoa ushirikiano wa kutosha kwa madiwani wote pale wanapohitaji ufafanuzi wa kitaalamu ili kila jambo wanalotaka kulifahamu wapate kwa wakati.

  0 0

  JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linawashikilia watuhumiwa 40 ambao wanahojiwa kwa tuhuma za kula njama na kuikosesha serikali mapato. Uchunguzi unafanywa kwa pamoja na maafisa wa Jeshi la Polisi na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kwa lengo la kubaini jinsi ambavyo makontena 329 na mengine 2489 yalivyotolewa bandarini kinyume cha taratibu.

  Kati ya hao, watuhumiwa 26 ni watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)na watumishi 03 kutoka Bandari kavu (ICD) YA AZAM wanatuhumiwa kuhusika na upotevu wa makontena 329. Aidha, watuhumiwa 11 ambao ni watumishi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA)  kwa kuhusika na upotevu wa makontena 2489.

  Uchunguzi unaoendelea pia unahusisha kupitia kumbukumbu mbalimbali na kadhia za forodha ili kubaini mtindo uliotumika na kuwabaini wote waliohusika katika mchakato huo. Makontena 329 yaligundulika kukosekana kwenye ICD ya AZAM kuanzia mwezi Julai hadi Novemba 2015, wakati  makontena  2489 yaligundulika kutolewa Bandarini kuanzia Mwezi Machi mpaka Septemba, Mwaka 2014   kinyume cha taratibu kwa lengo la kukwepa kodi na ushuru. 

  Uchunguzi bado unaendelea ili kuwabaini wote wanaohusika na hatimaye majalada ya kesi yatapelekwa kwa mwanasheria wa serikali ili watuhumiwa watakaobainika kuhusika na makosa mbalimbali wafikishwe mahakamani.
  Kamanda wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na watuhumiwa 40 washikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum kwa tuhuma za ukwepaji kulipa kodi pamoja na mtu mmoja ambaye anatafutwa na Jeshi la Polisi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya REGIONAL CARGO SERVICES LTD,ABDULKADIR S/O KASSIM ABDI, Miaka 38, Mkazi wa Temeke Mikoroshini.
  Kamanda wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova akionyesha picha ya Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya REGIONAL CARGO SERVICES LTD,ABDULKADIR S/O KASSIM ABDI, Miaka 38, Mkazi wa Temeke Mikoroshini ambaye anatuhumiwa kwa kutoa makontena 329 kwenye bandari kavu ya AZAM (AZAM ICD) bila kulipia kodi anayetafutwa na jeshi hilo pia ni mmoja wa wakurugenzi wa kampuni za “JAS EXPRESS FREIGHT LTD” na “XL CLEARING AND FOWARDING Co. LTD” ambazo zote zilitumika kutoa makontena hayo. Ameonyesha picha ya mtuhumiwa huyo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
  Meneja wa Huduma na elimu kwa mlipa kodi kutoka wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Diana Masalla akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Kukusanya jumla ya shilingi 10,075,979,462.08 kutoka kwa makampuni 22 ambayo yalihusika na uondoshwaji wa makontena bandarini kinyume cha sheria na taratibu za forodha hadi kufikia tarehe 10 Desemba 2015. 

  Pia kati ya hao makampuni 06 amesema kuwa yamelipa kodi yote iliyokadiriwa pamoja na adhabu, ambapo makampuni 16 yamelipa sehemu ya kodi iliyokadiriwa pamoja na adhabu. 

  Aidha, makampuni 26 hayajalipa kodi kiasi cha shilingi 4,789,924,609.69 pamoja na kwamba zoezi la ukadiriaji limefanyika. 

  hata hivyo amesema kuwa leo ni siku ya mwisho iliyotolewa na Mheshimiwa Rais kwa wafanyabiashara waliokwepakulipa kodi ya makontena,

  Amewasisitiza wananchi wote watoe taarifa kuhusu vitendo vya ukwepaji kodi kutumia namba 0784210209. Pia taarifa za mwenendo wa wafanyakazi wa TRA Wasio waadilifu zitolewe kupitia simu namba 0689 122515 na ujumbe mfupi 0689 122516.
  Baadhi ya Waandishi wa habari waliohudhulia katika mkutano na Kamanda wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova wakimsikiliza leo jijini Dar es Salaam.

  Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

  0 0


  0 0

  Diwani wa Kata ya Nyegezi Jijini Mwanza kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Edith Emily Mudogo akiapa jana ili kuwatumikia wananchi wa Kata hiyo katika kikao cha kwanza cha baraza la Madiwani wa halmshauri ya Jiji la Mwanza.

  Na:George Binagi-GB Pazzo @Binagi Media Group (BMG)
  Mudogo ni miongoni mwa Madiwani wachapa kazi ambao wanaendana na Kauli Mbiu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli ya "HAPA KAZI TU" hii ikiwa ni kutokana na utendaji wake wa kazi uliotukuka.Kulia ni Hakimu Mkazi Mwandamizi Mkoa wa Mwanza akisimamia zoezi la uapishaji Jijini Mwanza.
  Madiwani wa Jiji la Mwanza wakiapa kuwatumikia wananchi
  Baadhi ya Madiwani wa Jiji la Mwanza akiwemo diwani wa Kata ya Nyegezi (CCM) Edith Emily Mudogo.
  Diwani wa Kata ya Nyegezi (CCM) Edith Emily Mudogo baada ya kuapishwa jana. Yeye kwake ni Kazi Tu.
  Wananchi na wageni viongozi mbalimbali wakifuatilia kikao cha kwanza cha baraza la Madiwani wa halmashauri ya Jiji la Mwanza.
  Kwa Picha Zaidi BONYEZA HAPA

  0 0

  Waandaaji wa Mdajala kuhusu Hotuba ya Rais Dk. John Magufuli, aliyoitoa wakati wa kufungua Bunge mjini Dodoma, wakizungumza na waandishi wa habari leo, katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam.
  0 0

  Na Ezekiel Kamanga ,Mbeya.

  Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya imememhukumu kwenda jela miaka mitatu Martin Mhina Dereva wa basi la Majinja kwa kuendesha gari kwa uzembe.

  Waendesha Mashitaka wa Serikali Hannarose Kasambala na Catherine Gwatu wameiambia Mahakama kuwa Dereva huyo aliendesha Basi la Kampuni ya Majinja kwa uzembe mapema mwaka huu majira ya saa 12 asubuhi kwa kuigonga gari aina ya Toyota Hilux na kusababisha kifo cha mtu mmoja.

  Mawakili hao wameiambia Mahakama kuwa Kesi hiyo namba 46/2015 ambapo Dereva huyo alitenda kosa hilo kinyume cha Sheria ya usalama barabarani namba 40(1),63(2)(a),27(1)(a)III(c) kifungu cha 168 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.
  Akijitetea mbele ya Mahakama Martin ameiomba Mahakama kumsamehe kwa kuwa hilo ni kosa lake la kwanza na kwamba anayo familia inayo mtegemea hivyo imwonee huruma kutokana na kosa hilo.


  Baada ya kupitia ushahidi uliotolewa Mahakamani na Upande wa Mashitaka na utetezi wa Mshitakiwa Hakimu Zawadi Laizer alimtia hatiani kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela ili iwe fundisho kwa madereva wasifuata sheria za usalama barabarani.

  Mwisho.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbaraka Abdulwakili akikagua gwaride la askari wahitimu wa mafunzo ya awali ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. Jumla ya askari 482 wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wamehitimu mafunzo ya awali ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yaliyofanyika nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kwenye Chuo cha Uongozi cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kimbiji. 
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbaraka Abdulwakili akipokea heshima toka kwa askari wahitimu wa mafunzo ya awali ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (hawapo pichani).
  Meza Kuu ya viongozi kutoka vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama ikipokea heshima toka kwa wahitimu wa mafunzo ya awali ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
  Baadhi ya Askari wahitimu wa mafunzo ya awali ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakiwa katika gwaride la kuhitimisha mafunzo hayo yaliyofanyika nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kwenye Chuo cha Uongozi cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)  Kimbiji.
  Baadhi ya ndugu na jamaa wa Askari wahitimu wa mafunzo ya awali ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakiwa katika hafla ya kuhitimisha mafunzo hayo yaliyofanyika nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kwenye Chuo cha Uongozi cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)  Kimbiji.
  Baadhi ya Askari wahitimu wa mafunzo ya awali ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakiwa katika gwaride la kuhitimisha mafunzo hayo yaliyofanyika nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kwenye Chuo cha Uongozi cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)  Kimbiji.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbaraka Abdulwakili (katikati) akikabidhi cheti kwa baadhi ya askari waliofanya vizuri kwenye mafunzo hayo ya askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbaraka Abdulwakili (katikati) akikabidhi cheti kwa baadhi ya askari waliofanya vizuri kwenye mafunzo hayo ya askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.  Baadhi ya ndugu na jamaa wa Askari wahitimu wa mafunzo ya awali ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakiwa katika hafla ya kuhitimisha mafunzo hayo yaliyofanyika nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kwenye Chuo cha Uongozi cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)  Kimbiji.
  Askari wahitimu wa mafunzo ya awali ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakicheza sarakasi kuonesha wanavyomudu fani mbalimbali.
  Askari wahitimu wa mafunzo ya awali ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakicheza kareti kuonesha kumudu mafunzo ya kujilinda wawapo kazini.
  Baadhi ya askari wahitimu wa mafunzo ya awali ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakionesha namna wanavyoweza kuokoa watu katika ajali.
  Baadhi ya askari wahitimu wa mafunzo ya awali ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakionesha namna wanavyoweza kuokoa watu katika ajali.

  Baadhi ya askari wahitimu wa mafunzo ya awali ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakionesha namna wanavyoweza kuokoa watu katika ajali.
  Baadhi ya askari wahitimu wa mafunzo ya awali ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakionesha namna wanavyofanya kazi zao kwa vitendo.
  Baadhi ya askari wahitimu wa mafunzo ya awali ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakionesha namna wanavyoweza kuokoa watu katika ajali.
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Pius Nyambacha akizungumza katika hafla ya Askari wa Kikosi hicho kuhitimu mafunzo ya awali ya Jeshi hilo iliyofanyika nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kwenye Chuo cha Uongozi cha Jeshi la Kujenga Taifa Kimbiji.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbaraka Abdulwakili akizungumza katika hafla ya Askari wa Kikosi hicho kuhitimu mafunzo ya awali ya Jeshi hilo iliyofanyika nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kwenye Chuo cha Uongozi cha Jeshi la Kujenga Taifa Kimbiji.

  Picha ya pamoja ya mgeni rasmi na wahitimu pamoja na viongozi wa menza kuu katika hafla hiyo.
  Picha ya pamoja ya mgeni rasmi na wahitimu pamoja na viongozi wa menza kuu katika hafla hiyo.

  *Imeandaliwa na www.thehabari.com _____________________________________________________________________________

older | 1 | .... | 708 | 709 | (Page 710) | 711 | 712 | .... | 1898 | newer