Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

CCM YANYAKUA UENYEKITI WA HALMASHAURI LINDI VIJIJINI

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Lindi Ndugu Yahaya Nawanda akihutubia wakati wa ufunguzi wa kikao cha kwanza cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Lindi Vijijini ambapo aliwataka madiwani wao kuhakikisha suala la usafi linatiliwa mkazo kwenye maeneo yao.
 Baadhi ya madiwani wakisikiliza kwa makini.


 Mbunge wa Jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye akipiga kura kumchagua Mwenyekiti wa Halmashauri ya Lindi Vijijini.

 Mbunge wa jimbo la Mtama ndugu Nape Nnauye (CCM) akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Mchinga ndugu Hamidu Bobali (CUF) walipokutana kwenye kika cha kwanza cha Halmashauri ya Lindi Vijijini ambapo pia ulifanyika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri na kuchagua kamati mbali mbali.
 
 Mwenyekiti aliyechaguliwa kuongoza Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Vijijini Ndugu Matei B. Makwinya ambaye ni diwani wa kata ya Nyangao (CCM) akitoa salaam za shukrani kwa wajumbe wote waliompigia kura nyingi ambapo alipata kura 26 dhidi ya mpinzani wake aliyepata kura 17.
 Mbunge wa Mtama Ndugu Nape Nnauye (CCM) akimsikiliza diwani wa kata ya Sudi Bw. Ali Athumani Njale (CUF) ,mwingine kushoto ni Mzee Masoud Chitende mara baada ya zoezi la kupiga kura kumchagua Mwenyekiti wa Halmashauri kukamilika.
Madiwani wakiwa kwenye vazi rasmi wakati wa kikao
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA MAGEREZA NCHINI AONGOZA KIKAO MAALUM CHA KUPITIA RASIMU YA MPANGO WA WA JESHI LA MAGEREZA KUJITOSHELEZA CHAKULA, JIJINI DAR

$
0
0
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akifungua Kikao Maalum cha Wadau kutoka nje ya Magereza(hawapo pichani) cha kujadili rasimu ya Mpango wa Jeshi la Magereza wa kujitosheleza kwa chakula cha Wafungwa waliopo Magerezani. Kikao hicho kimefanyika leo Desemba 8, 2015 katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam.
 Mshauri Mwelekezi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Beatus Kundy(aliyesimama) akiwasilisha rasimu ya Mpango wa Jeshi la Magereza wa kujitosheleza kwa chakula cha Wafungwa waliopo Magerezani. Jeshi la Magereza limeandaa rasimu hiyo ili kuipunguzia Serikali gharama za kuwalisha wafungwa waliopo magerezani.
 Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa makini uwasilishaji wa Andiko hilo(wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Eng. Deonice Chamulesile(wa pili kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa pili kushoto) ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga.

  Mwakilishi kutoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Bw. Hashim Kimmwe akitoa mchango wake wakati wa kujadili rasimu ya Mpango wa Jeshi la Magereza wa kujitosheleza kwa chakula cha Wafungwa waliopo Magerezani.
 Wataalam wa Jeshi la Magereza walioshiriki kikamilifu katika maandalizi ya Andiko la Mpango wa Jeshi la Magereza kujitosheleza kwa chakula kwa kushirikiana na Mshauri Mwelekezi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakifuatilia majadiliano ya rasimu hiyo.
(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

SALAMU ZA RAIS MAGUFULI KWA WANANCHI KATIKA KUMBUKUMBU YA MIAKA 54 YA UHURU

$
0
0

SALAAM ZA MHE. JOHN POMBE MAGUFULI, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KWA WANANCHI KATIKA KUMBUKUMBU YA MIAKA 54 YA UHURU,

TAREHE 09 DESEMBA, 2015.



Namshukuru Mwenyezi Mungu aliyeiwezesha nchi yetu kutimiza miaka 54 ya uhuru kwa salama na amani. Namshukuru Mungu pia kwa kuniwezesha kuiona siku hii nikiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Napenda kuchukua fursa hii, kuwapongeza Watanzania wenzangu kwa Taifa letu kutimiza 54 ya Uhuru tarehe 09 Desemba, 2015. Napenda kuwahakikishia kwamba, kama ilivyokuwa kwa Serikali za awamu zilizopita, Serikali ya Awamu ya Tano itafanya kila lililo ndani ya uwezo wake kuhakikisha kwamba Uhuru, Amani na Umoja na wa Taifa letu hauchezewi na mtu, kikundi au Taifa lolote.  Tutaendelea kudumisha Uhuru wetu na Mapinduzi ya Zanzibar, tunu ambazo ni msingi wa Muungano wetu na Utanzania wetu.



Tofauti na ilivyozoeleka tumeamua mwaka huu kusherekea kumbukumbu hizi kwa kufanya kazi,. Wakati tunapata Uhuru Taifa letu lilikuwa likiongozwa na kauli mbiu ya UHURU NA KAZI. Kauli hii ilikuwa na lengo la kuamusha moyo na uzalendo wa kufanya kazi miongoni mwa Watanzania kwa kutambua kuwa uhuru wetu hautakuwa na maana kama hatutafanya kazi kwa juhudi na maarifa ili kujenga Taifa linalojitegemea. 

Watanzania katika miaka ile waliitikia wito huo kwa kufanya kazi za kuwaongezea kipato na za kujitolea katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kuwaletea maendeleo. Katika miaka ya hivi karibuni moyo na uzalendo wa kufanya kazi miongoni mwetu umepungua sana. Kwa sababu hiyo, niliamua kutumia siku ya kumbukumbu za uhuru wetu mwaka huu kukumbushana na kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya UHURU NA KAZI kwa kufanya kazi hususan ya usafi wa mazingira. Madhimisho ya Uhuru mwakani yatasherehekewa kama kawaida.



Nawapongeza viongozi wa Mikoa na Wilaya na wa Taasisi za umma na binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali yaliyojitokeza katika kuhakikisha kuwa zoezi la usafi wa mazingira linafanikiwa.



Napenda kutoa wito kwa Halmashauri zote nchini kuhakikisha zinaweka mifumo na taratibu thabiti zitakazowezesha usafi wa miji yetu kuwa endelevu. Viongozi wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri waache visingizio, uwezo na mamlaka ya kuhakikisha kwamba usafi katika miji yao unadumishwa wanao. Uwezo wa utendaji wao utapimwa pia kutokana na hali ya usafi wa miji yao.



Naomba wananchi tushirikiane katika kuhakikisha kuwa nyumba na mazingira ya nyumba zetu yanakuwa safi na maji ya kunywa katika maeneo ambayo hayawekwi dawa yanachemshwa. Aidha, wananchi wajizuie kutupa taka ovyo na viongozi wa Serikali za mitaa, vijiji na vitongoji wahakikishe kwamba kila nyumba inakuwa na choo. Tutashinda vita dhidi ya maradhi kama kipindupindu ikiwa sote tutazingatia kanuni za afya. Kila mtu atimize wajibu wake.



Mwalimu alisema Uhuru na Kazi na mimi nasema Hapa Kazi Tu.

Jeshi la wananchi watanzania JWTZ lawashikilia wafanyakazi 4 wa shirika la huduma za viwanja vya ndege la SWISS PORT kwa tuhuma za kupiga picha vifaa vya jeshi..

TASWIRA MBALIMBALI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Uhaba wa usafiri wahatarisha usalama wa Abiria, kama walivyonaswa na kamera ya mtaa kwa mtaa leo   jijini Dar es Salaam. 
 Mwendesha Baiskeli ya Magurudumu Matatu Maarufu kama Guta Akiwa amepakiza Wachuuzi wa Matunda katika Barabara ya Uhuru Kariakoo jijini Dar es salaam.
 Mwendesha Baiskeli ya Magurudumu Matatu Maarufu kama Guta akiwa amempakiza Mchuuzi wa Matunda aina ya Nanasi akiwa amening'inia nyuma ya Guta hilo ambapo ni Hatari kwa  Maisha yake, leo kama alivyonaswa jijini Dar es Salaam.
 Mwendesha Baiskeli ya matairi matatu maarufu kama Guta akiwa amempakia mchuuzi ambapo ni sehemu yake ya kujitafutia kipato chake cha kila siku leo   jijini Dar es Salaam.

 Kila mtu anaukaaji wake katika  Baiskeli ya Magurudumu Matatu Maarufu kama Guta.
 Mjasilia mali akiwakatika harakati za kujipatia kipato chake cha kila siku kama alivyo naswa na Kamera ya Mtaa kwa Mtaa  leo   jijini Dar es Salaam.
 Sehemu  ambayo sio rasmi kuvukia watembea kwa miguu ambayo inaonekana nihatari kwa  usalama wao, Kamera ya Mtaa kwa Mtaa  ya nasa  leo jijini Dar es Salaam.
 Kamera ya Mtaa kwa Mtaa yamnasa mwendesha Pikipiki maarufu kama Boda boda akivunja sheria za Barabarani kwa kupita upande ambao si rasmi, na kutokujali kuvaa kofia ngumu maarufu kama Helment ambapo ni hatari kwa usalama wake leo   jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanue Massaka wa Globu ya jamii).

UNFPA Yakutanisha Wadau wa Kupinga Ukatili na 'Amani Nyumbani Forum'

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sihaba Nkinga ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na wasichana akizungumza kabla ya kuzinduwa rasmi kongamano. Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sihaba Nkinga ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na wasichana akizungumza kabla ya kuzinduwa rasmi kongamano.Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa idadi ya watu (UNFPA), Dk. Natalia Kanem akizungumza kwenye kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na wasichana wakiimba wimbo wa taifa kabla ya kuzinduliwa kwa kongamano hilo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa idadi ya watu (UNFPA), Dk. Natalia Kanem akizungumza kwenye kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na wasichana wakiimba wimbo wa taifa kabla ya kuzinduliwa kwa kongamano hilo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.Sehemu ya washiriki wa kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na wasichana wakiimba wimbo wa taifa kabla ya kuzinduliwa kwa kongamano hilo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Sehemu ya washiriki wa kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na wasichana wakiimba wimbo wa taifa kabla ya kuzinduliwa kwa kongamano hilo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Meza Kuu katika kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na wasichana, Kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa idadi ya watu (UNFPA), Dk. Natalia Kanem, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sihaba Nkinga na Ofisa Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Zambia, Elizabeth Phiri wakiwa katika kongamano hilo. Meza Kuu katika kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na wasichana, Kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa idadi ya watu (UNFPA), Dk. Natalia Kanem, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sihaba Nkinga na Ofisa Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Zambia, Elizabeth Phiri wakiwa katika kongamano hilo.Baadhi ya washiriki wa kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na wasichana lililofanyika leo jijini Dar es Salaam wakifuatilia mada na majadiliano anuai katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere. Baadhi ya washiriki wa kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na wasichana lililofanyika leo jijini Dar es Salaam wakifuatilia mada na majadiliano anuai katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere.Baadhi ya washiriki wa kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na wasichana lililofanyika leo jijini Dar es Salaam wakifuatilia mada na majadiliano anuai katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere. Baadhi ya washiriki wa kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na wasichana lililofanyika leo jijini Dar es Salaam wakifuatilia mada na majadiliano anuai katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere.
Mwakilishi wa Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi akizungumza na washiriki wa kongamano hilo. Mwakilishi wa Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi akizungumza na washiriki wa kongamano hilo.
Baadhi ya vikundi vya maigizo vikiigiza katika kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na wasichana lililofanyika leo jijini Dar es Salaam wakifuatilia mada na majadiliano anuai katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere. Baadhi ya vikundi vya maigizo vikiigiza katika kongamano la kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na wasichana lililofanyika leo jijini Dar es Salaam wakifuatilia mada na majadiliano anuai katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere.

MASHINDANO BAISKELI KILOMITA 115 YAKUZA VIPAJI VYA VIJANA

$
0
0
Washindi wa kwanza wa mashindano.ya baiskeli, ya  Rift Valley Odyssey  ya liyofanyika  jijini arusha  DEC 6 Mwaka huu Sophia Husseni wa kwanza (kulia) na Sophia Adson wa (pili) kutoka kulia wakiwa na Mkurugenzi wa 6degrees Simone Paine wa pili kutoka kulia yaliyo fanyika Arusha ambapo wachezaji toka ndani nan je ya nchi wameshirikai kwa takriban siku mbili kuendesha kwa umbali wa kilomita 115. Masindano ambayo yanawapa ushindi timu ya Warriors ambao wametumia masaa matano na dakika 28
 Mshindi wakwanza wa mashindano ya kuendesha baiskeli  ya   Rift Valley Odyssey  Sophia Husseni ya liyofanyika  jijini arusha  DEC  Jijini Arusha.
Washiriki wa mashindano ya baiskeliya  Rift Valley Odyssey  yaliyofanyika  jijini arusha ambapo wachezaji toka ndani nan je ya nchi wameshirikai kwa takriban siku mbili kuendesha kwa umbali wa kilomita 115
 Mkurugenzi wa 6degrees Simone Paine akizungumza na washiriki wa shindano hilo.
Mshindi wakwanza wa mashindano ya kuendesha baiskeli  ya   Rift Valley Odyssey  Sophia Husseni

UCHAMBUZI WA HABARI ZA MAGAZETINI

$
0
0
Magufuli kila kona duniani. Wengi waguswa na utendaji kazi wake, wataka viongozi wa Afrika kumuiga.
SIMU.TV:  Siku 35 za Magufuli. Vigogo 78 wafyekwa, kasi yake yawatia wengi tumbo joto. CCM yampa baraka kutumbua majipu; https://youtu.be/mZba3DzjuvU
SIMU.TV:  Geti namba 5 kichaka ufisadi bandari. Mgombea CUF Mbagala ashinda pingamizi.  Daktari wa Tanzania apeta kimataifa; https://youtu.be/lSTzVW2uL08  
SIMU.TV:  Yanga kama Magufuli. Azam yaipiga mkwara Simba. SECAFA inahitaji mipango mipya. Stars under 15 yarejea Dar; https://youtu.be/-te0uv3RjP4  
SIMU.TV:  Pata habari motomoto zilizotawala katika magazeti ya leo Disemba 9.2015 hapa Simu.tv;https://youtu.be/EpSCvEEWeDM

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AFANYA USAFI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 HAPA KAZI TU ya  Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt. John Pombe  Joseph Magufuli  ikiendelea kufanyiwa kazi kama Rais  huyo akionekana katika picha akiwa akifanya usafi leo jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiokota taka taka katika eneo la ufukwe wa ferry jijini Dar es Salaam.



Wimbo Mpya: Isha Mashauzi - Jiamini

CHANGIA DAMU, OKOA MAISHA YA NDUGU

MKUU WA WILAYA YA MOSHI ,NOVATUS MAKUNGA AFANYA ZIARA HOSPITALI YA RUFAA YA KCMC.

$
0
0

Mkuu wa wilaya akizunumza jambo mara baada ya kutembelea chumba chenye mashine ya CT -Scan katika hosptali hiyo,kulia ni mkuu wa kitengo hicho Dkt Fatma.

Mwangalizi wa sehemu ya kuhifadhia maiti katika hosptali ya rufaa ya KCMC,Bwana Issa akitoa maelezo kwa Dc Makunga (hayupo pichani ) alipotemblea chumba hicho.

Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga alipofanya kikao na viongozi wa hosptali ya rufaa ya KCMC ya mkoani Kilimanjaro.








Mkurugenzi mkuu wa Hosptali ya Rufaa ya KCMC,Dkt Giliard Masenga (kulia) akitoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali yanayotajwa kuwa changamoto kwa Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga alipotembelea hosptalini hapo.
Baadhi ya wakuu wa idara waliongozana na mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga alipofanya ziara katika hospali hiyo.
Baadhi ya wakuu wa itengo katika hosptali ya KCMC.
Mganga mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Dkt Timoth Wonanji akichangia jambo wakati wa kikao cha mkuu wa wilaya ya Moshi ,Novatus Makunga (kulia) alipokutana na viongozi wa Hopstali ya Rufaa ya KCMC.


Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akiwa katika kitengo cha macho alipofanya ziara katika Hosptali ya Rufaa ya KCMC. Mkuu wa Wilaya Makunga akitoka kitengo cha Macho akiongozana na Mkurugenzi mkuu wa Hosptali ya Rufaa ya KCMC ,Dkt Giliard Masenga .
DC Makunga akipita katika wodi mbalimbali hosptalini hapo.




Dk Bingwa wa magonjwa ya figo,Dkt Kilonzo akitoa maelezo kwa mkuu wa wilaya ya Moshi ,Novatus Makunga alipotembelea hosptali hiyo.




Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.(0755659929)

MWANAMUZIKI ROBERTO AMARULA KUTOKA ZAMBIA KUTUMBUIZA DAR ES SALAAM, DODOMA KATIKA TAMASHA LA INSTAGRAM WIKIENDI HII

$
0
0

Mwanamuziki na mtangazaji wa redio, Roberto Chindaba Banda 'maarufu Roberto Amarula kutoka nchini Zambia (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana , kuhusu onyesho lake atakalolifanya leo katika fukwe za Escape One Mikocheni jijini Dar es Salaam na kesho ukumbi wa Ngalawa Pub mkoani Dodoma katika Tamasha la Instagram Party Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Freconic Ideaz, Fred Ngimba ambao wamemleta msanii huyo hapa nchini kwa kushirikiana na Kampuni ya C&G Solutions na kulia ni Mwanamuzi David Banda 'General Ozzy kutoka Zambia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Freconic Ideaz, Fred Ngimba (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
Meneja Mawasiliano wa Freconic Ideaz, Krantz Mwantepele (kushoto), akizungumza katika mkutano huo ambapo alisema kampuni yao itaendelea kuleta wanamuziki wengine kutoka pande mbalimbali za dunia kama walivyofanya kwa Robarto Amarula.
Mwanamuzi David Banda 'General Ozzy kutoka Zambia (kulia), akizungumza na wanahabari.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mwanamuziki na mtangazaji wa Redio, Roberto Chindaba Banda 'maarufu Roberto Amarula kutoka nchini Zambia, akifanya vitu vyake mbele ya wanahabari.


Mwanamuzi David Banda 'General Ozzy, akiimba mbele ya wanahabari. Mwanamuziki huyu atamsindikiza Roberto Amarula wakati wa shoo yao.
Mwanamuziki, Clinton Nyirongo kutoka Zambia naye atakuwepo kutoa burudani.



Na Dotto Mwaibale

MWANAMUZIKI wa Zambia anayetamba na wimbo maarufu wa Amarula, Robert Banda ‘Roberto Amarula’, kesho anatarajia kufanya shoo kubwa na ya aina yake katika Ufukwe wa Escape One uliopo Mikocheni, jijini Dar es Salaam kabla ya kufanya hivyo mjini Dodoma kesho kutwa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo asubuhi, Roberto Amarula, ameahidi kutoa burudanio ya aina yake kwa wakazi wa Dar es Salaam na Dodoma, akiwataka mashabiki wa muziki na burudani kujitokeza kwa wingi kwenye shoo zake hizo.

“Nimefurahia sana kuja Dar es Salaam na ninaahidi kutoa shoo ya aina yake kesho (leo) na Dodoma ili kuwaburudisha Watanzania, lakini pia nitatembelea vituo vya watoto yatima ili kuwafariji na kuwapa nguvu wajione nao ni sehemu ya jamii ya Watanzania na Afrika kwa ujumla,” alisema aliyeambatana na wasanii wenzake wa Zambia, David Banda ‘General Ozzy’ na Clinton Ntirongo ‘Mandela’.


Kwa upande wake, Mkugenzi wa Freconic Ideaz, Fred Ngimba, alisema kuwa shoo ya leo itawahusisha pia wasanii wa Tanzania kama Ben Pol, Roma Mkatoliki, Fred Swag, Msouth na wengine wengi na kwamba onyesho la Dodoma litafanyika kwenye ukumbi wa Ngalawa Pub, ikiwa ni sehemu ya tamasha la Instagram Party. 

Kwa upande wake, Meneja Mawasiliano wa Frecon Ideaz, Krantz Mwantepele, alisema: “Tunafahamu kiu ya Watanzania katika suala zima la burudani ndio maana tumewaletea msanii huyu ambaye kwa sasa ni maarufu mno Afrika na kwingineko tukiahidi kuwaleta wasanii zaidi wakubwa Afrika na hata Marekani ili kukata kiu ya mashabiki wa muziki hapa nchini.

Ziara ya Roberto Amarula ambaye ni mshindi wa tuzo za uandishi bora, mwanamuziki, mtayarishaji muziki na mtangazaji wa redio, iliyoratibiwa kwa pamoja na Freconic Ideaz na C&G Solutions, imedhaminiwa na Millard Ayo, Morena Hotel, Shabiby Bus Service na Clouds FM.

MTOTO HUYU ANATAFUTWA NA WAZAZI WAKE

$
0
0
MWANAFUNZI Evelina Edwin Kazaura (13), (pichani) wa shule ya msingi Dodoma mlimani, Manispaa ya Dodoma amepotea katika mazingira ya kutatanisha.

Kwa mujibu wa mzazi wa mwanafunzi huyo, Joyce Nchimbi, alisema mtoto huyo alitoweka nyumbani miezi mitatu iliyopita akiwa amevaa nguo hiyo.

Alisema mara ya mwisho alionekana mitaa ya Railways akiwa na wanafunzi wenzake lakini baada ya hapo hajaonekana tena.

Joyce alisema juhudi za kumtafuta mtoto huyo kwa ndugu na jamaa hazikufanikiwa na kutoa taarifa katika kituo cha polisi cha kati Dodoma na kufunguliwa jalada namba DOM/RB/5005/2015.

Joyce ameomba kwa yeyote atakayemuona mtoto huyo atoe taarifa kituo chochote cha  polisi au apige simu namba 0756- 365064 au 0654- 666755.

MATUKIO MBALIMBALI YA MAADHIMISHO YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

$
0
0
Kilimanjaro, Maandamano yakipita eneo la kituo kuu cha Mabasi cha mjini Moshi yakieekea katika viwanja vya kituo hicho ambako uzinduzi wa kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kanda ya kaskazini.
Dar es salaam, Madereva wa boda boda wakiongoza maandamano ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake jijini Dar es salaam. Maandamano hayo yalianzia uwanja wa Tipi ulioko Sinza hadi katika hotel ya Blue Pearl iliyopo Ubungo.
Dar es salaam, Ujumbe mbalimbali wa maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.
 
Kilimanjaro, Mkuu wa wilaya ya Moshi, Novatus Makunga akisikiliza malezo kutoka katika banda la shirika la NAFGEM linalopambana na vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake.

Mwanza, Shirika la kutetea haki za wanawake la KIVULINI la jijini Mwanza likikabidhi zawadi mbalimbali zikiwemo laptop kwa waandishi walioandika habari zinazotetea haki za wanawake.


Kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia inahitimishwa leo tarehe 10 Disemba ambayo ni siku ya kimataifa ya tamko la Haki za Binadamu ikiwa ni ishara ya kuhusisha ukatili dhidi ya wanawake na haki za binadamu na kutia msisitizo kwamba ukatili kama huu ni ukiukwaji wa haki za binadamu.

Maadhimisho haya yalianza rasmi tarehe 25 Novemba siku ambayo ilichaguliwa na Umoja wa Mataifa mwaka 1993 kuwa ni siku ya kimataifa ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake ambapo kila mwaka, Umoja wa Mataifa unashauri, mashirika ya Kimataifa na asasi zisizo za kiserikali kufanya shughuli zinazolenga kufahamisha jamii juu ya ukatili wa kijinsia, hususani ukatili dhidi ya wanawake.

Mwaka huu, kauli mbiu inasema FUNGUKA, CHUKUA HATUA, MLINDE MTOTO APATE ELIMU yenye lengo la kuhamasisha jamii kutambua changamoto mbalimbali zinazohatarisha usalama na kuchochea ukatili wa kijinsia mashuleni ikiwa ni pamoja na suala la viboko kuendelea kuwa tatizo kubwa, adhabu kali wanazopewa watoto ambao haiendani na umri wao pamoja na mila na desturi potofu zinazokandamiza watoto wa kike kama mimba za utotoni na ukeketaji.

Video: Uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia: https://www.youtube.com/watch?v=TdGTQiAi4Fg

Mkurugenzi wa shirika la WiLDAF, Dr. Judith Odunga akizungumza wakati wa ufunguzi wa kampeni hizi alitaja changamoto nyingine kuwa ni miundombinu ambayo ni pamoja na kuwa na madarasa ya kutosha, madawati, vyoo na sehemu za kujisitiri kwa watoto wa kike, mabweni, uzio kuzunguka mashule pamoja na mazingira magumu ya usafiri wakati wa kwenda na kurudi nyumbani na kutokuwa na chombo cha wanafunzi cha kutumika kusemea matatizo yao pale ambapo wanakutana na changamoto mbalimbali.

Akiongezea, Dr. Odunga alisema kampeni hii kwa mwaka huu ilifanyika kikanda chini ya uratibu wa mashirika na wadau mbalimbali wa maendeleo. Kanda hizo ni kanda ya Ziwa (Mwanza, Mara na Shinyanga), Kanda ya Kaskazini (Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga), Kanda ya Kati (Dodoma, Morogoro na Singida), Kanda ya Kusini (Mtwara, Songea, Mbeya, Iringa na Lindi), Kanda ya Pwani (Dar es salaam na Pwani) na kuratibiwa na wadau mbalimbali wakiwemo mashirika ya KIVULINI, CWCA, NAFGEM, Morogoro Paralegal,  Mtwara paralegal, WiLDAF, TWCWC pamoja na Jeshi la Polisi.

Ujumbe wa maadhimisho haya na picha zinapatikana kupitia ukurasa wa Facebook wa WILDAF ambao ni www.facebook.com/WILDAFTZ

ASKOFU CHARLES GADI AONGOZA UMOJA WA MAKANISA YA DODOMA KUMUOMBEA RAIS DK.JOHN MAGUFULI NA SERIKALI YA AWAMU YA TANO

$
0
0

Viongozi wa Makanisa mbalimbali ya mkoani Dodoma wakiwa wameshika picha za Rais Dk.John Magufuli, Waziri Mkuu, Majaliwa Kasimu Majaliwa na Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu wakati wa kufanya maombi ya kuwaombea yaliyofanyika mjini Dodoma juzi. Maombi hayo yaliongozwa na Askofu wa Kanisa la Good News for All Ministry International la jijini Dar es Salaam.

Viongozi hao na waumini wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa maombi hayo.

Picha ya pamoja ndani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), wakati wa maombi hayo. Maombi hayo yalifanyika mjini humo baada ya viongozi hao na waumini mbalimbali kushiriki kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dk. John Pombe Magufuli la kuitumia siku ya Maadhimisho ya Siku ya Uhuru kufanya usafi nchi nzima.
 

Millicom kuanza utekelezaji wa mkakati wake wa uwekezaji kwa kampuni ya simu ya Zantel Tanzania

$
0
0
 Mwenyekiti wa Bodi ya Zantel Bi Rachel Samren, akizungumza na waandishi wa habari leo juu ya mikakati ya Millicom katika kuiboresha kampuni ya Zantel.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Millicom upande wa Africa, Cynthia Gordon, akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano huo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel, Benoit Janin akizungumza na waandishi juu ya mipango ya kampuni yake ikiwamo kuzindua mtandao wa 4G upande wa Zanzibar.
 Wafanyakazi wa Zantel katika mkutano huo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel akijibu maswali ya waandishi katika mkutano huo. Kushoto kwake ni Rachel Samren, Mwenyekiti wa Bodi ya Zantel na kulia ni Cynthia Gordon, Mkurugenzi Mtendaji wa Millicom Upande wa Afrika.


Mwenyekiti wa Bodi, Rachel Samren akizungumza na waandishi wa habari. Katikakati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel, Benoit Janin na kulia ni Cynthia Gordon, Mkurugenzi Mtendaji wa Millicom Upande wa Afrika.





Kampuni ya Millicom leo imetangaza kuanza utekelezaji wa mpango wake wa uwekezaji katika kampuni ya Zantel, ambao utajumuisha uboreshaji wa huduma na mtandao wa kampuni hiyo.

Akizungumza baada ya mkutano wa kwanza wa bodi ya Zantel tangu Millicom iliponunua asilimia 85% ya hisa za Zantel, Mkurugenzi Mtendaji wa Milicom upande wa Africa, Cynthia Gordon, alisema maboresho hayo yatajajikita katika kuimarisha  kwa huduma za simu, intaneti, pamoja ambayo yatapelekea Zantel kutoa huduma bora na ya uhakika.

'Millicom itajikita katika kuiwezesha Zantel kukuza na kuboresha ukuaji  na upanuzi wa shughuli zake hapa nchini ili kuifanya Zantel iendelee kuongoza soko la Zanzibar na kuendelea kutoa huduma zenye  ubunifu zaidi pamoja na kuongeza wigo wa kuwafikia wateja wengi zaidi’ alisema Gordon.

Kampuni ya Millicom pia imeelezea nia yake ya dhati ya kuimarisha ushirikiano wake na Serikali ya Zanzibar, ambayo pia anamiliki asilimia 15% ya hisa za Zantel katika kuhakikisha kampuni inakuwa msitari wa mbele katika kuwajengea uwezo na kuboresha maisha ya watu wa Zanzibar.

'Kama kampuni inayoongoza Zanzibar, ushirikiano wetu na serikali ya Zanzibar una umuhimu wa kipekee, na katika hili, Millicom itahakikisha wananchi wa Zanzibar wanawezeshwa kupitia miradi mbalimbali ya kijamii’ alisema Rachel Samren, Makamu wa Rais, Mambo ya Nje wa Millicom.

Pia akizungumza katika mkutano huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Zantel, Benoit Janin alisema kampuni ya Zantel pia itazindua mtandao wa kwanza kabisa wa 4G kwa Zanzibar ambao una lengo la kuimarisha nafasi yao kama kampuni inayoongoza katika huduma za intaneti pamoja na kuimarisha upatikanaji wa huduma za mtandao kwa wakazi wa Zanzibar.

‘Zantel itafaidikia moja kwa moja na uzoefu pamoja na utamaduni wa ubora wa Millicom, hivyo kuhakikisha Zantel inaingia katika zama mpya za kuboresha bidhaa zake na kuongeza ubora wa huduma ikiwemo huduma za kifedha kwa njia ya simu ya mkononi na kupanua maeneo ya ushirikiano katika miradi ya kijamii’ alisema Benoit.

Benoit ambaye hivi karibuni alitembelea wafanyakazi upande wa Zanzibar, amesema amejionea namna walivyo na ari ya kushirikiana na uongozi mpya wa Zantel katika kuhakikisha kampuni yao inaendelea kuongoza Zanzibar.

Kuanzia mwanzoni mwa mwaka 2016, Zantel pia itafanya uzinduzi wa huduma za kusisimua ikiwa ni pamoja na kupanuliwa kwa huduma za 3G na 4G na pia  kuboresha  huduma za kifedha kwa njia ya simu ili kuifanya Zantel kufikia malengo yake katika utoaji wa huduma kwa jamii.

MBUNGE WA UVCCM KIGOMA AONGOZA VIJANA WENZAKE KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS MAGUFULI

$
0
0

Mbunge wa viti Maalum Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia UVCCM Mkoa wa Kigoma, Zainab Katimba (aliyevaa Gum Boots), akiwaongoza Vijana wenzake katika zoezi la kufanya usafi, ambapo wamefanya usafi katika eneo la Hospitali ya Maweni.

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Kigoma wakiongozwa na Mbunge wa Vijana Mh. Zainab Katimba wameunga mkono agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli kwa kufanya usafi katika hospitali ya Rufaa Mkoa wa Kigoma Maweni.

Usafi huo ambao umeenda sambamba na kugawa zawadi mbali mbali kwa wagonjwa hospitalini hapo, ambazo ni sabuni na vifaa mbali mbali vya usafi juisi na biskuti umelenga kuunga mkono zoezi la kufanya usafi katika siku ya maadhimisho ya siku ya Uhuru.

Akizungumza hospitalini hapo Bi. Katimba alisema kuwa, wao kama vijana wameamua kuwa mfano kwa kuanza kutekeleza agizo hilo kwa kufanya usafi hospitalini hapo, Soko la Mwanga lililopo mjini Kigoma pamoja na kutembelea kituo cha watoto yatima ambapo wamefanya usafi kituoni hapo na kugawa zawadi mbalimbali kwa watoto ikiwemo vyakula.

Alisema lengo la kufanya usafi ni kuhakikisha magonjwa mbali mbali kama kipindupindu yanatokomezwa kwa kuweka maeneo yote kuwa safi. "Leo tumeamua kuanza na hili zoezi rasmi, lakini zoezi hili ni endelevu" Katimba alisema.

Aidha Mhe. Katimba alitoa wito kwa vijana wote tanzania nzima wajikite kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano katika kuboresha maisha ya watanzania. Mhe. Katimba ametoa agizo kwa vijana wote Tanzania nzima kuwa mstari wa mbele katika kufanya usafi siku ya tarehe 9 Dec 2015.

MADIWANI KUTOKA KATIKA MAJIMBO YA ILALA,UKONGA NA SEGEREA WAAPISHWA-UCHAGUZI WAKUMPATA MEYA NA NAIBU WAHIRISHWA.

$
0
0
SH1
Baadhi ya Madiwani kutoka katika Majimbo ya Ilala,Ukonga na Segerea wakila kiapo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama Wilaya ya Ilala Mhe: Adelf Sachore (hayupo pichani) kwenye Ukumbi wa Arnautoglo,Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam (wakwanza kushoto), Diwani wa Viti Maalum Wilaya ya Ilala Jimbo la Ukonga, Mhe: Tickey Kitundu (kulia katikati), Diwani wa Kata ya Kariakoo, Mhe: Abdulkarim Masaki.
PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON-FULLSHANGWEBLOG
SH2
Madiwani wakijaza fomu ya kiapo wa pili kutoka kulia ni Diwani wa Viti Maalum Wilaya ya Ilala Jimbo la Ukonga, Mhe: Tickey Kitundu.
SH3
Madiwani wakijaza fomu ya kiapo.
SH4
Hakimu Mkazi wa Mahakama Wilaya ya Ilala Mhe: Adelf Sachore akiwaapisha Madiwani (hawapo pichani), kutoka katika Majimbo ya Ilala,Ukonga na Segerea kwenye Ukumbi wa Arnautoglo,Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
SH5
Wageni waalikwa walioudhuria wakishuhudia Madiwani wakila kiapo.
....................................................................................................
Manispaa ya Ilala Dar es Salaam nako wameshindwa kuchagua Meya na Naibu Meya baada ya baadhi ya madiwani kuamua kukiuka taratibu za uchaguzi kwa kuamua kupiga picha kwa kutumia simu ya mkononi karatasi ya kupigia kura. 

Uchaguzi huo ulitakiwa kufanyika jana saa nne lakini kutokana na kuibuka kwa dosari hizo ambazo zilisababisha uchaguzi huo kuahirishwa.Baada ya kuahirishwa kwa uchaguzi huo, Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala ambaye alikuwa mwenyekiti wa uchaguzi John Ngonyani alisema wameamua kusitisha uchaguzi huo hadi kesho(leo), saa nane mchana kwasababu ya baadhi ya taratibu kukikuwa.

 Pia Mwanasheria wa Manispaa ya Ilala Dar es Salaam Mashauri Mussimu alistoa ufafanuzi wa vipengele vya sheria ya uchaguzi huo ambapo alisema uchaguzi huo utakuwa wa siri kulingana na muongozo. 

Baada ya ufafanuzi huo, Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara (Chadema), alisimama na kuomba muongozo ambapo alitaka uchaguzi huo uwe wa wazi na si kufanyika kwa siri.Madiwani wa Chadema wakati wanapiga kura hizo waliamua kuoneshana nani ambaye amepigiwa kura na hapo ndipo ilipoanza kuibua maswali miongoni mwa wajumbe wa uchaguzi huo.Wakati kwa madiwani wa CCM wao waliunga mkono mongozo wa kikao hicho kuwa kura iwe ni siri ya mpiga kura.

Hata hivyo hakukua na maelewano na ndipo ilipoamriwa uchaguzi huo kuahirisha ambapo kabla ya uamuzi huo wasilitisha kikao kwa muda kwenda kupata muafaka lakini ikashindakana.Wapambe wa CUF na Chadema waliokuwa kwenye eneo hilo la ukumbi waliamua kuzomea madiwani wa CCM hasa kwa kuzingatia mbali ya kutakiwa kufanya uchaguzi wa meya na Naibu Meya kulifanyika tukio la kuapisha madiwani ambapo wengi wao walikuja na wafuasi wao.

MKUU WA WILAYA YA ARUSHA ASISITIZA MSHIKAMANO KUWALETEA WANANCHI MAENDELEO

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Fadhil Nkurlu akifungua rasmi Baraza la Madiwani wa Jiji la Arusha
Mwenyekiti wa muda wa Mkutano wa Baraza Ndg. Daniel Machunda ambaye pia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha akikabidhi madaraka hayo kwa Mstahiki Meya mara baada ya kuchaguliwa kwa kura 33 kati ya kura 34 zilizopigwa.
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg. Juma Iddi ambaye pia ni Katibu wa Mkutano wa Baraza akitoa muongozo wa namna Mkutano huu wa kwanza unavyoendeshwa kwa mujibu wa kanuni,kushoto ni Katibu Tawala mkoa wa Arusha,Addoh Mapunda.
Diwani wa Kata ya Sokon I, Mheshimiwa Calist Lazaro Bukhai(Chadema) akikishukuru baada ya kuchaguliwa kuwa Meya wa Jiji la Arusha.
Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha ,Mhe Calist Lazaro Bukhai akiwa na Naibu Meya wake Viola Lazaro Likindikoki kwenye Mkutano wa kwanza wa Baraza la Madiwani
Diwani wa Kata ya Kaloleni Mhe Lewis Kessy (Kushoto) na Diwani wa Kata ya Levolosi Mhe. Efatha Nanyaro wakiwa kwenye Kikao cha kwanza cha Baraza la madiwani wa Jiji la Arusha
Mhe. Abdulrasul Tojo (kulia) ambaye ni diwani pekee wa CCM kwenye Baraza la Halmashauri ya Jiji la Arusha alipokua akiomba kura katika nafasi ya Naibu Meya wa Jiji hilo.

Mstahiki Meya Mhe. Calist Bukhai (aliyevaa Taji) Naibu Meya Mhe. Viola Likindikoki (tatu kushoto) Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Fadhil Nkurlu (nne kulia), Mkurugenzi wa Jiji, Ndgugu Juma Iddi (tatu kulia) pamoja na Madiwani wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya Kikao cha Baraza la madiwani.


Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images