Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 700 | 701 | (Page 702) | 703 | 704 | .... | 1898 | newer

  0 0


    Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Ombeni Sefue akiwaonyesha waandishi wa Habari (hawapo pichani) beji yenye jina lake ambayo amewaagiza watumishi wa Umma kuivaa wanapokuwa katika maeneo yao ya kazi. Balozi Sefue alifanya mkutano na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es Salaam jana na kutoa taarifa ya Serikali kuhusu kesi ya Serious Fraud Office (SFO) dhidi ya Standard Bank.

  0 0

  EAST AFRICAN LEGISLATIVE ASSEMBLY 


  PRESS RELEASE
  EALA MARK EAC DAY VISITING STAKEHOLDERS 
  East African Legislative Assembly, Kigali, Rwanda, December 2, 2015:  EALA marked EAC Day (November 30th, 2015) by visiting and holding talks with different Private Sector stakeholders in Kigali.

  The first activity saw the legislators visit Positivo BGH, an electronics manufacturing company which uses Information Communications Technology (ICTs) to transform education.  The Latin-American company which has set up base in Kigali, Rwanda, envisages regional expansion in the near future.

  According to the Managing Director, Positivo BGH wants to make technology accessible to transform people’s lives from education, knowledge, development and communication up to comfort at home.  The Kigali based plant which is situate in the Special Economic Zone was set up in June 2014 but commenced manufacturing a year later with a roll-out of 150,000 units.

  The firm is set to broaden its base through diversified product portfolio and contract manufacturing.  It intends to serve the local Rwandan market and in due course expand to other African countries.

  The Assembly later visited the Strawtech Building Solutions that produces robust strawboard panels from wheat straw, as primary building materials from for mass housing and commercial construction projects.

  The company has created a local value chain from raw material supply to turnkey housing units leading to a number of economic benefits including income generation and a positive impact of trade, a move EALA Speaker, Rt Hon Daniel Kidega and the Members lauded.  

  Job creation has also been enhanced with over 5000 farmers supplying straw and other workers providing transport in addition to the specialized architects, engineers and specialized construction jobs.

  Chief Operating Officer, Til Loeper said the company had identified Rwanda as the ideal entry point into the African market due to sound leadership and effective economic reforms that have resulted in positive investment environment.

  “Rwanda is keen on implementing the Green growth and Climate Resilience Strategy as well as Government’s commitment to meeting future housing and construction demands,” Loeper said.

  The company has constructed 2000 pre-fabricated, modular housing units per annum. 

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo nchini, Mhe. Juma - Alfani Mpango   ambaye alikwenda ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 2, 2015.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi ya kinyago Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo  nchini, Mhe. Juma-Alfani Mpango ambaye alikwenda ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 2, 2015 kuaga.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mhe.  Juma- Alfani  Mpango  ambaye alikwenda ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 2, 2015 kuaga.
   (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambaye anamaliza muda wake, Bw. Juma-Alfani Mpango.

  Akizungumza na balozi Mpango leo (Jumatano, Desemba 2, 2015), ofisini kwake, Magogoni jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu alimshukuru balozi huyo kwa pongezi zake na kumuomba aendelee kuwa balozi mzuri wa kuitangaza Tanzania hata baada ya kurejea nyumbani.

  Pia alitumia fursa hiyo kuwaombea heri wananchi wa DRC pamoja na Rais Joseph Kabila katika maandalizi ya uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyika nchini humo mwakani.

  Kwa upande wake, Balozi Mpango ambaye alisema amekaa hapa nchini kwa miaka 12, alimweleza Waziri Mkuu kwamba amejifunza mengi sana kutoka kwa viongozi wa Tanzania kubwa vikiwa ni uchapakazi na unyenyekevu. “Nimeona utawala wa Rais Benjamin Mkapa, Rais Jakaya Kikwete na sasa Dkt. John Pombe Magufuli. Ninavutiwa na hatua mnazochukua hivi sasa katika kupambana na rushwa na ufisadi,” alisema.

  “Mambo niliyojifunza tangu nimekaa hapa ni uchapakazi na unyenyekevu. Unaona kabisa kwamba mtu anaamini kuwa madaraka siyo kitu cha kujivunia kwa mtumishi wa umma. Anachotakiwa kuwa nacho ni utayari wa kuwatumikia wananchi,” alisema kwa Kiswahili sanifu.

  Balozi Mpango aliomba mahusiano ya nchi hizi mbili yaendelezwe kwani DRC imekuwa ikinufaika na matumizi ya bandari ya Dar es Salaam katika kusafirishia bidhaa zake kwenda nchi za nje.

  “Bandari ya Dar es Salaam ni muhimu sana kwetu. Mwaka 2004 tulisafirisha tani za mizigo 200,000, mwaka 2014 ziliongezeka na kufikia tani milioni 1.3; na mwakani tunataraji zitaongezeka na kufikia tani milioni tatu,” alisema.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S.  L. P. 3021,
  11410 DAR ES SALAAM
  JUMATANO, DESEMBA 2, 2015.

  0 0

            Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao akizungumza leo wakati wa uzinduzi wa huduma mpya inayojulikana kama Vodacom Red jijini Dar es Salaam leo.

   Ni  huduma ya Vodacom Red
   Inayotoa ofa nafuu na maalumu kwa wateja.

  KAMPUNI ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania leo imezindua huduma mpya inayojulikana kama Vodacom Red ambayo imewalenga wateja wake wote wanaonunua muda wa maongezi kabla ya kupata huduma za mawasiliano ambayo ni bora zaidi,ina unafuu wa gharama na yenye kuwarahishia maisha.

  Akiongea wakati wa uzinduzi jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao amesema“Vodacom tumebuni huduma tukiwa tumewalenga wateja wetu wote hasa wale wenye shughuli nyingi ambao wanakosa  muda wa kununua vifurushi vya muda wa maongezi vya siku,wiki na vya mwezi.

  Huduma ya Vodacom Red itawapatia unafuu wa kupiga simu kwa mitandao yote kwa gharama ya shilingi 1.5 kwa sekunde na kwa gharama hiyo hiyo ya shilingi 1.5 kwa sekunde watawezeshwa kupiga simu katika nchi tano kubwa zenye mtandao mkubwa wa masuala ya biashara ambazo ni (China,Afrika ya Kusini,India,Canada na Marekani),Kuhusiana na  matumizi ya data alisema wateja watakaotumia huduma hii watapatiwa kifurushi chenye unafuu kitakachowawezesha kupata huduma za intaneti yenye  kukidhi mahitaji yao”.

  Kampeni hii inawarahisishia maisha watumiaji wake  kwa kutoa ofa  kwa watumiaji ambapo watafanya mawasiliano  kwa  kupiga simu  za ndani kwa malipo nafuu ya shilingi 1.5 kwa sekunde kwa mitandao yote pia kwa gharama hiyo hiyo ya shilingi 1.5 wanaweza kupiga simu kwenda nje ya nchi zipatazo 5 pia wanaunganishwa na huduma ya intaneti ya Mpango Mzima ambayo ina kasi kubwa na inawawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi  kwa muda wote.Katika kusherehekea uzinduzi wa huduma hii wateja watakaotumia shilingi 4,000/-na zaidi kwa kupiga simu za ndani watanufaika na mrejesho wa  asilimia 10% ya fedha hizo kupitia akaunti zao za M-Pesa kwenye simu zao.

  Akiongelea mkakati wa Vodacom kuwaunganisha watanzania wote katika mtandao wa mawasiliano,Ferrao alisema “Lengo letu ni kuendelea kubuni huduma za kurahisisha mawasiliano kwa wateja wetu tukiwa na dhamira ya kuwapeleka katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia.Vodacom Red ni mfano wa huduma ambayo imebuniwa  ikiwa ina ufanisi kubwa katika masuala ya biashara na yenye kuleta unafuu wakati huohuo kuwarahisishia maisha  wateja wetu”.

  Wateja wa Vodacom wanaotumia huduma ya kuongeza salio kwenye simu zao kabla ya maongezi  wanaweza kuchangamkia huduma mpya na yenye unafuu mkubwa wa gharama.Ili mteja aweze kunifaika na huduma hii anachotakiwa kufanya ni kupiga *149*73# hapo mteja utapata frusa ya kuchagua anachokitaka kupitia huduma ya Vodacom Red.

  Kwa maelezo zaidi wasiliana na
  Rosalynn Mworia
  Head: Corporate Communications and PR
  Mobile: +255754710661
  Email: rmworia@vodacom.co.tz.

  0 0
 • 12/02/15--02:51: BEI YA MADAFU LEO


 • 0 0


  Co- founder wa Pop Up Bongo Natasha Stambuli akionesha bidhaa za duka lake la Secret Habit ambalo nalo lilionesha bidhaa zake siku hiyo.


  Kutokea banda la Beauty Heaven kulikuwa na bidhaa mbalimbali pia

  Andrew Mahiga na rafiki ake walikuwapo.
  Mmoja kati ya wanawake wajasiriamali mahiri mjini, Aika Lawere mmiliki wa Mbezi Garden alikuwapo pia


  Mbunifu wa mavazi nchini wa lebo ya Branoz Collection, Bahati Kombe (katikati) akipanga bidhaa zake wakati wa Tamasha la Pop Up Bongo lililofanyika juzi Triniti Oyster bay chini ya udhamini wa kinywaji cha Smirnoff.


  Meneja chapa (pombe kali) wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Shomari Shija, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
  Wauzaji wa bidhaa mbalimbali kutoka duka la Beauty Haven wakiwa kwenye banda lao wakati wa Tamasha la Po Up Bongo lililofanyika juzi Triniti Oyster bay chini ya udhamini wa kinywaji cha Smirnoff
  Tanya akiwa na wadau mbalimbali waliojitokeza kwenye Pop Up shop  Atu Mynah akimtaja mshindi wa bahati nasibu siku hiyo


  Kutokea banda la Beauty Heaven kulikuwa na bidhaa mbalimbali pia


  Natasha akizungumza na mmoja kati ya washiriki waliojitokeza kuonesha bidhaa siku hiyo.

  ONESHO la mauzo ya bidhaa mbalimbali zitengenezwazo na wabunifu wa hapa nchini, Pop Up Bongo lilifanyika hivi karibuni na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.

  Mratibu wa onesho hilo lililofanyikia Triniti Oyster bay,Natasha Stambuli alisema kuwa zaidi ya wajasiriamali 15 walijiotokeza kuonesha na kuuza bidhaa zao.

  Alisema kuwa bidhaa mbalimbali kama vile nguo, vito, viatu na vinginevyo viliuzwa na wajasiriamali hao walipata wasaha wa kuongeza wigo wao kibiashara kwa kukutana na wanunuzi.

  "Pop Up Bongo inalenga kuwaweka karibu zaidi wajasiriamali na wanunuzi hao kwa kuwakutanisha mahala hapa na kisha hata wakishafanya mauzo wanakuwa na wasaha wa kuonana hata baada ya Tamasha hili na kuendeleza uhusiano wa kibiashara" alisema Natasha.

  Pia ametoa wito kwa wanajamii kujenga utamaduni wa kuhudhuria maonesho mbalimbali ya biashara ili kupanua wigo zaidi wa ufahamu wa aina mbalimbali za bidhaa ziuzwazo nchini.

  Natasha alisema kuwa kwa kutembelea maonesho hayo watapata wasaha wa kufahamu aina mbalimbali za bidhaa ziuzwazo na wafanyabiashara mbalimbali na kujua ni wapo pa kwenda kujipatia mahitaji.

  Alisema kuwa Pop Up Bongo ikiwa chini ya udhamini wa kinywaji cha Smirnoff inalenga kuwakutanisha pamoja wafanyabiashara wa bidhaa mbalimbali zitengenezwazo hapa nchini na wanunuzi kwa lengo la kuwasaidia wajasiriamali wa hapa nchini kuongeza pia wigo wa biashara zao.

  Kwa upande wake Meneja chapa (pombe kali) wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Shomari Shija, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) alisema kuwa kwa kampuni hiyo inatambua nafasi ya wajasiriamali katika kuendeleza uchumi wa nchi na ndio maana imeamua kuunga mkono Pop Up Bongo.

  "SBL kwa kupitia kinywaji chetu cha Smirnoff tumeamua kudhamini Pop Up Bongo kwa kuwa ni mahala pazuri kwa wapenzi wa kinywaji hiki kukutana huku wakijipatia mahitaji yao kadhaa kutoka kwa wauzaji wanaouza bidhaa zao katika Pop Up Bongo" alisema Shomari.

  0 0

   Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini DIGP Abdulrahman Kaniki, akikata utepe kuashiria ufunguzi wa jengo la kisasa litakalo tumika kwa ajili ya shughuli za michezo ya Taekwondo, lililofadhiliwa na serikali ya Korea kupitia kwa balozi wake hapa nchini Mh. II Chung, jana katika Chuo cha Taaluma ya Polisi DPA jijini Dar es salaam.
  Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini DIGP Abdulrahman Kaniki, akimkabidhi cheti Bw. Shinyoung Pyeon, wakati wa sherehe za kukabidhi jengo la kisasa la michezo ya Taekwondo lililofadhiliwa na serikali ya Korea kupitia kwa balozi wake hapa nchini Mh. II Chung, jana katika Chuo cha Taaluma ya Polisi DPA jijini Dar es salaam.

   Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini DIGP Abdulrahman Kaniki, akiwa katika picha ya pamoja na timu ya taekwondo, mara baada ya ufunguzi wa jengo la michezo lililofadhiliwa na serikali ya Korea, kupitia kwa balozi wake hapa nchini Mh. II Chung. jana katika Chuo cha Taaluma ya Polisi DPA jijini Dar es salaam.

  0 0

  SERIKALI kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imetenga kiasi cha Tsh. Bilioni 5 katika mwaka 2015/16 kwa ajili ya kuhudumia kambi za Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za matibabu ya magonjwa hayo kwa Watanzania.

  Lengo la mkakati huo ni kuhakikisha Wagonjwa wengi wanahudumiwa katika kipindi kifupi pamoja na kupunguza gharama za kusafirisha wagonjwa nje ya nchi, ambao wengi wao husafiri kwa ajili ya matibabu ya magonjwa ya moyo, figo na saratani.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Donald Mmbando (Pichani)wakati wa ziara yake ya kutembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

  Dkt. Mbando alisema katika wiki ya kwanza iliyoanza wiki hii Madaktari hao wanatarajia kutoa huduma kwa wagonjwa 20 na kuifanya Serikali kuokoa kiasi cha Tsh. Milioni 500 ambazo zingetumika kuwasafirisha wagonjwa hao nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

  “Tumeokoa kiasi cha Tsh. Bilioni 1 zilizopaswa kutumika kuwapeleka nje ya nchi wagonjwa hawa, tutahakikisha kuwa Wataalamu hawa wanafanya kazi kwa pamoja na Madaktari wetu ili waweze kuwajengea uwezo katika kutibu magonjwa haya”  alisema Dkt. Mmando.

  Alisema Serikali pia ipo katika mchakato wa kuzijengea uwezo hospitali mbalimbali nchini ikiwemo Taasisi ya Kansa ya Ocean Road na Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) kwa kuziwezesha hospitali hizo kuwa na Wataalamu na majengo ya kisasa kwa ajili ya kutoa huduma za matibabu kwa Watanzania.

  Aidha alisema Serikali imepanga kufanya mazungumzo na taasisi za kiraia na nyingine ikiwemo taasisi ya Rotary Club zilizokuwa zikisafarisha watoto wenye matatizo ya ugonjwa wa moyo, kuwekeza nguvu nchini kwani Tanzania kwa sasa ina wataalamu wa kutosha kwa ajili ya kuwatibu wagonja hao.

  Kwa mujibu wa Mmbando alisema magonjwa ya moyo ni miongoni mwa magonjwa yasiyoambukiza, hivyo aliwataka Watanzania kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi mara kwa mara na kuacha kunywa pombe na uvutaji wa sigara na kutazama desturi za ulaji.

  Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Prof. Mohammed Janabi alisema katika kipindi cha wiki mbili ambazo madaktari hao watakuwepo hapa nchini wanaweza kuhudumia jumla ya wagonjwa 55, na hivyo kuifanya Serikali kuokoa kiasi cha Tsh. Bilioni 1.2

  0 0
  Mkurugenzi wa kituo cha mafunzo cha Furahini kilichopo Kisangara wilayani Mwanga,Isack Msuya akimuongoza Meneja uendeshaji wa Modewji Foundation iliyoanzishwa na mfanyabiashara Mohamed Dewji,Francesca Tettamanzi kutembelea eneo kilipojengwa kituo hicho.

  Meneja uendeshaji wa Modewji Foundation ,Francesca Tettamanzi akiwa ameambata na wafanyakazo wa kampuni ya METL walipotembelea kituo cha mafunzo cha Furahini cha wilayani Mwanga.  Meneja uendeshaji wa Modewji Foundation ,Francesca Tettamanzi akitembelea majengo hayo yaliyojengwa kwa msaada wa Modewji Foundation.
  Majengo ya Madarasa katika kituo cha elimu cha Furahini cha wilayani Mwanga yaliyojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Mohamed Enterprises .  Afisa Udhibiti wa Ubora wa elimu ya msingi wilaya ya Mwanga ,Richard Joachim akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa kituo cha mafunzo cha vijana cha Furahini klichopo Kisangara wilayani Mwanga.
  Baadhi ya wanafunzi wanaosoma katika kituo hicho.
  Mwanafunzi Maureen Festo akisoma risala mbele ya mgeni rasmi ,Meneja uendeshaji wa Modewji Foundation ,Francesca Tettamanzi (hayupo pichani).
  Meneja uendeshaji wa Modewji Foundation ,Francesca Tettamanzi akifuatilia risala iliyokuwa ikisomwa na wanafunzi wakati wa uzinduzi wa kituo hicho.


  Meneja uendeshaji wa Modewji Foundation ,Francesca Tettamanzi akipena mikono na wanafunzi mara baada ya kumaliza kusoma risala.
  Mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzo cha Furahini kilichopo Kisangara wilayani Mwanga,Isack Msuya akizungumza wakati wa usinduzi wa kituo hicho.
  Meneja uendeshaji wa Modewji Foundation ,Francesca Tettamanzi aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kituo cha Furahini Youth Learning Center akizungumza katika uzinduzi huo.
  Meneja uendeshaji wa Modewji Foundation ,Francesca Tettamanzi akifungua mfano wa hundi kwa ajili ya kukabidhi kwa mkurugenzi wa kituo hicho.
  Meneja uendeshaji wa Modewji Foundation ,Francesca Tettamanzi akizungumza jambo mara baada ya kukabidhi kibao kinachoonesha msaada uliotolewa kwa kituo hicho cha ujenzi wa madarasa ya kituo .
  Meneja uendeshaji wa Modewji Foundation ,Francesca Tettamanzi akimkabidhi mkurugenzi wa kituo cha Mafunzo cha Furahini ,Isack Msuya mfano wa hundi ya kiasi cha sh Mil 7.7.
  Mchungaji Kajuna akitoa neno wakati wa uzinduzi wa kituo hicho.
  Wawakilishi wa METL wakiwa katika picha ya pamoja na walimu wa kito hicho pamoja na wanafunzi .


  Wakiwa katika picha ya pamoja.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  0 0

  Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi Umma Bw.Peter Mushi (wa pili kushoto) akizungumza alipokuwa akiendesha mkutano kwa njia ya video na Sekretarieti ya Mkoa wa Mara jana jijini Dar es Salaam (watatu kulia) ni Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi Umma Bw. Leonard Mchau .
  Baadhi ya watendaji kutoka wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakiendelea na Mkutano kwa njia ya Video na Sektertarieti za Mikoa ya Lindi,Mara,Geita,Singida na Shinyanga jana jijini Dar es Salaam.

  Mwandishi wa Habari kutoka kituo cha Televisheni cha ITV Bw. Hendry Mabumo akimuuliza swali Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao Bw.Charles Senkondo ambaye hayupo katika picha jana jijini Dar es .

  Na Anna Nkinda – Maelezo
  WATANZANIA wametakiwa kutumia technolojia ya mawasiliano ikiwemo kufanya mikutano kwa njia ya video ambayo itawaondolea gharama ya kusafiri na hivyo kuokoa fedha  na muda.

  Rai hiyo imetolea   hivi karibuni na Mkurugenzi Mtendaji wa TaGLA Charles Senkondo wakati akiongea na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa kazi wa video conference kati ya Ofisi ya Rais  Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Taasisi zake, Sekretarieti za mikoa na Mamlaka za Serikali za mitaa.

  Senkondo alisema kufanya mikutano kwa njia ya video kunamfanya mtu asisafiri na hivyo kuepukana na ajali, kutopoteza muda awapo safarini na na kupata wasaa wa  kukaa na familia yake.

  “Kuanzishwa kwa TaGLA kumeongeza uwezo wa kufanya kazi kwa ubunifu zaidi, kwa njia ya kisasa, kwa maamuzi zaidi ya kiuendeshaji kwa kuangalia kila mara mahitaji ya wadau na kutumia mbinu za soko katika utoaji wa huduma bora”.

  “Kabla ya kukuwa kwa teknolojia watu walikuwa wanasafiri umbali mrefu kwenda kushiriki mikutano hivi sasa wamepunguza safari zisizo na umuhimu.  Mtu atasafiri katika mikutano ya umuhimu tu zamani ilikuwa lazima mtu aje sasa hivi anafuatwa popote alipo na kuletwa katika video conference”, alisema Senkoro.

  Akiongelea kuhusu kituo hicho Mkurugenzi huyo alisema zaidi ya washiriki elfu 20 wameshiriki midaharo na mafunzo 783 ya  kubadilishana maarifa kupitia Wakala wa Mafunzo kwa njia ya Mtandao (TaGLA) .

  Senkondo alisema wakala hiyo imeweza kutoa mafunzo kwa viongozi wakiwemo mawaziri, wakuu wa taasisi mbalimbali za umma na binafsi na kuleta urahisi wa vikundi na watu waliotengwa kijiografia kuonana, kusikilizana na kukubaliana kwa wakati mmoja.

  “Wakala kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa kutumia mitandao ya teknolojia imeweza kufundisha watendaji wakuu wa Taasisi za Serikali, wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya zote na wakurugenzi wa rasilimali watu wapatao 1,200 mfumo wa malipo ya mishahara kwa watumishi wa Serikali (HCMIS) Lawson version 7”, alisema Senkoro.

  Mkurugenzi  huyo mtendaji alizitaja changamoto wanazokabiliana nazo kuwa ni fikra potofu juu ya matumizi ya TEHAMA na kukubalika kwa kasi kwa teknolojia  na kuwaomba waandishi wa habari pamoja na wadau wengine kuelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa matumizi ya Tehama.
  Senkoro alisisitiza, “Tunawaalika wadau mbalimbali wakiwemo taasisi za Serikali na zisizo za kiserikali, waandishi wa habari, watu binafsi na asasi za jamii watumie huduma zetu ambazo tunazitoa kwa gharama naafuu kuweza kuwafikia wadau wengi kwa muda mfupi bila kujali umbali au changamoto za kijiografia.   Wakala wa Mafunzo kwa njia ya Mtandao umewezesha kufanyika kwa mahakama kwa kutumia mikutano ya video katika kesi mbalimbali kwa kutoa ushahidi wake kwa njia ya video na kusaidia kupunguza gharama  na kuhamasisha maamuzi na hivyo utoaji wa haki katika kesi husika.

  Mkutano huo wa kazi wa video conference kati ya Ofisi ya Rais  Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Taasisi zake, Sekretarieti za mikoa na Mamlaka za Serikali za mitaa ulijumuisha viongozi wa Serikali kutoka mikoa ya Dodoma, Lindi, Geita, Singida, Pwani, Mara, Iringa, Mtwara, Shinyanga na Njombe.

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Mkuu wa Shirika la Bandari Mbarouk Hamadi Mbarouk (wa pili kushoto) wakati alipotembelea Eneo la Ujenzi wa Bandari Mpya ya kisasa Mpigaduri Maruhubi Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi itakayojengwa Kampuni ya CHINA HARBOUR ENGINEERING COMPANY LTD (CHEC) kutoka Nchini China,(kushoto) Naibu Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Issa Haji Ussi.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akifuatana na Naibu Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Issa Haji Ussi (kushoto) Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Dkt.Juma Malik Akili (wa pili kulia)akifuatia Mhandisi Mkuu wa Shirika la Bandari Mbarouk Hamadi Mbarouk (katikati) wakati alipotembelea Eneo la Ujenzi wa Bandari Mpya ya kisasa Mpigaduri Maruhubi Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi itakayojengwa Kampuni ya CHINA HARBOUR ENGINEERING COMPANY LTD (CHEC) kutoka Nchini China.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akiuliza jambo alipokuwa akipewa maelezo na Mhandisi Mkuu wa Shirika la Bandari Mbarouk Hamadi Mbarouk (kushoto) wakati alipotembelea Eneo la Ujenzi wa Bandari Mpya ya kisasa Mpigaduri Maruhubi Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi itakayojengwa Kampuni ya CHINA HARBOUR ENGINEERING COMPANY LTD (CHEC) kutoka Nchini China.
  [Picha na Ikulu.]

  0 0

  Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Nchini (NHIF) Mkoani Manyara, Isaya Shekifu akizungumza jana katika kongamano la uhamasishaji wa mpango wa bima ya afya wa kikoa kwa wajasiriamali na vikundi vilivyosajiliwa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro (kulia) ni Mkuu wa wilaya hiyo Mahamoud Kambona na kushoto ni mratibu wa NHIF na mfuko wa afya ya jamii (CHF) mkoani humo Reginald Kileo.
  Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambonaakizungumza wakati akifungua kongamano la uhamasishaji wa mpango wa bima yaafya wa kikoa kwa wajasiriamali na vikundi vilivyosajiliwa Mji mdogo wa Mirerani, (kushoto) ni Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Nchini (NHIF) wa mkoahuo, Isaya Shekifu na kulia ni Ofisa Tarafa ya Moipo Joseph Mtataiko .
  Vikundi mbalimbali vya wajasiriamali wa Vicoba, Saccos na wasindikaji
  ngozi waMji mdogo wa Mirerani Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara,
  wakiwa kwenye kongamanola uhamasishaji wa mpango wa bima ya afya kwa wajasiriamali na vikundivilivyosajiliwa (Kikoa).

   Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Nchini (NHIF) wa Mkoawa
  Manyara, Isaya Shekifu akiandika maswali yaliyokuwa yanaulizwa katika
  kongamano la uhamasishaji wampango wa bima ya afya wa kikoa kwa
  wajasiriamali na vikundi vilivyosajiliwa Mjimdogo wa Mirerani Wilayani
  Simanjiro. 

  Na Woinde Shizza 
  MKUU wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambona amewaasa viongozi wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya nchini (NHIF) kuishinikiza bohari ya dawa nchini (MSD) kutoa dawa zinazohitajika.  Kambona aliyasema hayo jana mji mdogo wa Mirerani kwenye uzinduzi wa
  kongamano la uhamasishaji wa mpango wa bima ya afya kwa wajasiriamali na 
  vikundi vilivyosajiliwa (Kikoa).

  Kambona alisema amepata malalamiko kwenye vituo vya afya Mirernai na
  Orkesumet kuwa wamekuwa wanaomba dawa MSD na kuzilipia lakini wanapatiwa 
  dawa ambazo hawana mahitaji nayo hivyo kupata hasara.

  “Haina maana watu waagize dawa za malaria wao wawape dawa za kuvimba miguu 
  zisozohitajika, ila NHIF mpo karibu na watu wa MSD, zungumzeni nao ili 
  watoe dawa zinazoombwa na siyo kwa matakwa yao,” alisema Kambona. 

  Pia, alivitaka vikundi vya ushirika wa Saccos, Vicoba, Amcos, Vibindo,
  wachimba madini, waendesha bodaboda, mama na baba lishe na wasindika ngozi, 
  wajiunge na bima ya afya ya Kikoa ili wapatiwe matibabu kwa unafuu. 


  *Meneja wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya nchini (NHIF) mkoani Manyara
  Isaya Shekifu alisema mpango huo wa kikoa utamwezesha mwanachama wa
  kikundi kupata matibabu yote kama watumishi wa serikali wanavyopata kwenye 
  zaidi ya vituo 6,000 nchini nzima kwa mchango mtu mmoja sh76,800 kwa mwaka.

  *Shekifu alisema gharama za matibabu nchini zinapanda kila uchao na huwa
  vigumu kwa mwananchi wa kawaida kuweza kuzimudu pindi anapougua, bali 
  kupitia kikoa wajasiriamali nchini watanufaika kupitia matibabu
  watakayoyapatiwa.

  *“Ugonjwa haupigi hodi bali humpata mtu wakati wowote na gharama za
  matibabu zipo juu, ila kupitia kikoa wajasiriamali watapata matibabu bila
  tatizo lolote, hivyo wanapaswa kujiunga kwa wingi kwenye bima hii,”
  alisema.

  *Mratibu wa NHIF na mfuko wa afya ya jamii (CHF) mkoani Manyara, Reginald 
  Kileo alitaja mafao hayo yatahusisha* *gharama za kujiandikisha kumuona 
  daktari, dawa zote zilizoidhinishwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, 
  vipimo vidogo na vikubwa kama MRI na CT Scan, kulazwa na miwani ya kusomea.

  “Mafao mengine ni upasuaji mdogo na mkubwa na upasuaji wa kujifungua kwa 
  wanawake, matibabu ya kinywa na meno, matibabu ya macho, mazoezi ya 
  kimatibabu ya viungo (physiotherapy) na vifaa saidizi kama magongo na
  vishikizi vya shingo,” alisema Kileo. 

  0 0

   Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Miundombinu waliofika Bandari Kuu ya Zanzibar kushuhudia kuwasili kwa Meli mpya ya MV. MAPINDUZI II ikitokea Korea kusini.
  Meli mpya ya  MV. MAPINDUZI II ikiwa nje kidogo ya Bandari ya Zanzibar kabla ya kufunga gati Bandarini hapo. 

    Waziri wa Fedha Omar Yussuf Mzee akitoa maelezo kwa waandishi wa Habari juu ya matumizi ya gharama zilizotumika mara baada  ya kuwasili kwa Meli ya MV. MAPINDUZI II Mjini Zanzibar.

  Meli ya MV MAPINDUZI II yatia nanga Bandari kuu ya Zanzibar ikitokea Korea Kusini.
  Picha na Miza Othman-Maelezo Zanzibar. 

  Na Naryam Kidiko MAELEZO Zanzibar.
  MELI mpya ya MV.Mapinduzi ( ii) imewasili bandarini zanzibar kwa ajili ya kuanza safari zake baada ya kukamilika ujenzi wake huko  korea ya kusini.                                   
  Hafla ya kuwasili kwa meli hiyo imeongozwa na waziri wa fedha Omar Yussuf Mzee ambapo amesema ujenzi  wa meli hiyo ni agizo la Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dk. Ali Moh’d shein.

  Amesema meli hiyo bado iko katika mikono ya wajenzi hadi sasa na inatarajiwa kuzinduliwa rasmi wiki ijayo na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Moh’d Shein ambaye ni mgeni rasmi katika uzinduzi huo.

  Waziri mzee amesema meli hiyo inavifaa vya kutosha kama vile life jacket, pamoja na boti ndogo ili kuweka usalama kwa abiria wataosafiri katika meli hiyo.

  Hata hivyo amesema meli hiyo itasafiri pemba pamoja na Dare-salam hivyo amewataka wananchi kuitunza meli hiyo kwani ni matunda yao.

  Nae Katibu Mkuu Wizara ya Miundo mbinu na Mawasiliano Zanizar Dk. Juma Malik amesema lengo kulifanya shirika la meli lifanye kazi kibiashara ili kuongeza pato la Taifa.

  Amewaomba wananchi kuitunza na kuitumia vizuri meli hiyo kwani wamefanya kazi kubwa na kutumia gharama hadi kufikia kukamilika kwa meli hiyo.

  Sambamba na hayo amesema meli hiyo ina uwezo wa kupakia abiria  wasiopungua 1,200 pamoja na tani za mizigo 200.

  Meli hiyo mpya ya MV.Mapinduzi ( ii) imetengenezwa Korea kusini na kugharimu jumla ya dola mil.30.4 za Marekani ambapo ujenzi wake hadi kukamilika umechukua jumla ya miezi 18. 
  Imetolewa na maelezo zanzibar.

  0 0

  muh1 
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Donan Mmbando (wa pili kutoka kushoto) akikata utepe kuashiria kufungualiwa kwa  duka la dawa leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) ambalo linalomilikiwa na Bohari Kuu ya Dawa (MSD). Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi  wa MNH, Profesa Lawrence Mseru.Picha zote kwa hisani ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
  muh2 
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Donan Mmbando akipewa taarifa ya utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli kuhusu kufungua duka la dawa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.
  muh3muh4 
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Donan Mmbando akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua duka la dawa linalomilikiwa na Bohari Kuu ya Dawa (MSD).  Duka hilo limefunguliwa leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

  muh5 
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Lawrence Mseru akizungumza na waandishi wa habari baada ya uzinduzi wa duka la dawa la MSD.
  muh6 
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Donan Mmbando (wa pili kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Laurean Rugambwa (kulia) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Mseru (wa tatu kutoka kulia) wakiwa katika picha ya pamoja leo katika hospitali hiyo baada ya kufunguliwa kwa duka la dawa la Bohari Kuu ya Dawa (MSD) leo jijini Dar es Salaam.
  ……………………………………………………………………………………………
  Serikali imewahakikishia Watanzania kwamba mashine ya Magnetic Resonance Imaging (MRI) pamoja na Computerized  Tomography Scan (CT-SCAN) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)  hazitakwama kufanya kazi kwa kuwa imeweka utaratibu mzuri wa kuzitengeneza.
   
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Donan Mmbando amesema serikali imezungumza na Philips na wamekubaliana kwamba mashine hizo hazitakwama na endapo litatokea tatizo la kiufundi watashughulikia mara moja.
   
  “Mwaka ujao ni mwaka wa bajeti  serikali itatenga fedha kwa ajili ya kutengeneza mashine za CT-SCAN na MRI,  lakini mtambue kwamba si tu mashine hizo zinapaswa kutengenezwa bali na mashine nyingine.”amesema Dk Mmbando.
   
  Pia, Dk Mmbando  amefungua duka la dawa  la Bohari Kuu ya Dawa (MSD) ndani ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kueleza kwamba kufunguliwa kwa duka hilo kutasaidia wananchi kupata huduma haraka na kununua dawa kwa gharama nafuu  na huduma hiyo itatolewa kwa saa 24.
   
  Akifafanua  kuhusu mashine za MRI na CT-Scan, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Lawrence Mseru amesema Novemba 25, 2015  alifika fundi kutoka Afrika Kusini ambaye pia ni fundi wa MRI na kuitengeneza na kuanza kufanya kazi tangu Novemba 26 mpaka Disemba 2, mwaka huu. Wagonjwa 152   wamepimwa na kwamba wengi wagonjwa wa dharura.
   
  Amesema hivi sasa mafundi wanafunga mashine ya Digital X-Ray iliyotolewa na serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambapo  usimikaji unatarajiwa  kukamilika mwishoni mwa juma hili.
   
  Akielezea utekelezaji wa agizo la wagonjwa wanaolala chini kupatiwa vitanda, Profesa Mseru amesema ili kuondoa wagonjwa wote waliolala chini, serikali kupitia MSD ilileta vitanda 300 pamoja na magodoro yake, vitanda hivyo vyote vilipelekwa kwenye Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) na tayari MOI imeanza kuhamisha wagonjwa waliokuwa wamelala chini kutoka wodi za MNH walizokuwa wanazitumia, mpaka sasa wagonjwa 120 wamehamishwa.
   
  Novemba 9, mwaka  huu Rais John Magufuli alifanya ziara MNH na kutoa maagizo kwamba ndani ya wiki mbili mashine ya MRI na CT-SCAN ambazo zilikuwa zimeharibika ziwe zinafanya kazi, wagonjwa waliolala chini wawe wamepata vitanda  na Bohari Kuu ya Dawa (MSD) ifungue duka la dawa ndani ya hospitali ili kuondoa ukosekanaji wa dawa.

  0 0

  ga2Mkurugenzii Mkazi wa Taasisi ya kimataifa inayojishughulisha na masuala ya kidemokrasia na utawala bora (The international Republican Institute) Bi. Robina Namusisi akimweleza Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai mipango ya taasisi yake inayokusudia kushirikiliana na Bunge katika kutoa mafunzo ya kidemokrasia kwa Wabunge vijana na wanawake. Bi. Namusisi alimtembea Mhe. Ndugai Ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.
  ga3 
  Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akifafanua jambo wakati wa mazungumzo na Mkurugenzii Mkazi wa Taasisi ya kimataifa inayojishughulisha na masuala ya kidemokrasia na utawala bora (The international Republican Institute) Bi. Robina Namusisi alipomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.  Taasisi hiyo inayokusudia kushirikiliana na Bunge katika kutoa mafunzo ya kidemokrasia kwa Wabunge vijana na wanawake.
  ga4 
  Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya kimataifa inayojishughulisha na masuala ya kidemokrasia na utawala bora (The international Republican Institute) Bi. Robina Namusisi (kulia kwake)alipomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.  Taasisi hiyo inayokusudia kushirikiliana na Bunge katika kutoa mafunzo ya kidemokrasia kwa Wabunge vijana na wanawake.  Wengine katika picha ni maafisa kutoka taasisi hiyo.Picha na Hassan Silayo, Idara ya Habari Maelezo.
  ga1Mkurugenzii Mkazi wa Taasisi ya kimataifa inayojishughulisha na masuala ya kidemokrasia na utawala bora (The international Republican Institute) Bi. Robina Namusisi akisalimiana na Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai alipomtembea Ofisini kwake Dar es Salaam leo kuelezea mipango ya taasisi yake inayokusudia kushirikiliana na Bunge katika kutoa mafunzo ya kidemokrasia kwa Wabunge vijana na wanawake.


  0 0

  fl1 
  Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo akielezea namna sekta ya Filamu ilivyo piga hatua hapa nchini wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Genofeva Matemu na kushoto ni Afisa Habari wa Idara ya Habari MAELEZO Bi. Fatma Salum.
  fl2 
  : Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutana wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo uliokuwa unahusu ukuaji wa sekta ya Filamu Tanzania leo jijini Dar es Salaam.Picha na Frank Shija, WHVUM……………………………………………………………………………………………
  Na Jovina Bujulu-MAELEZO
  Sekta ya filamu imekuwa na mchango mkubwa kwa kutoa jumla ya ajira 732,681ikiwa ni mchango wake katika kutatua tatizo la ajira nchini kwa mwaka wa fedha 2014/2015.
   
  Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Joyce Fissoo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
   
  Fissoo alifafanua kuwa idadi hiyo ya ajira zilizotolewa inajumuisha wataalamu wa filamu 944 na wadau wengine wasio wataalamu 731,737 ikilinganishwa na takwimu zilizotolewa na Shirika la Milki Bunifu Ulimwengini liliripoti kuwa mwaka 2007 tasnia ya filamu iliajiri watu 36.
  ‘Katika kipindi cha miaka ya 2000 utengenezaji wa filamu umebadilika kutoka ule wa awali wa kuburudisha na kuelimisha na kuwa biashara inayoingiza kipato na kutoa ajira katika jamii hivyo kuongeza kipato cha Taifa letu”. Alisema Fissoo.
   
  Aidha, kuanzia miaka ya 2000 sekta binafsi ilianza kutengeneza filamu hivyo filamu zilianza kufadhiliwa, kutengenezwa, kumilikiwa na kusambazwa kwa kiasi kikubwa na wadau na makampuni binafsi hivyo kupelekea ongezeko kubwa la makampuni ya uzalishaji na usambazaji kutoka kampuni 1 miaka ya 2000 hadi kufikia makampuni 250 mwaka 2015.
   
  Tasnia hiyo imechangia kukuza uchumi wa nchi na ule wa mtu binafsi ambapo kwa mujibu wa Shirika la Milki Bunifu Ulimwenguni (WIPO) kwa mwaka wa 2007 ilichangia shilingi 2,134,860 na kufikia mwaka 2010 ilichangia shilingi 11,398,440, ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 433.9.
   
  Akizungumzia ukuaji huo wa tasnia ya filamu, Fissoo alisema kuwa ukuaji wa teknolojia umepelekea utumiaji wa vifaa vyenye teknolojia ya hali ya juu vilivyowekezwa na baadhi ya wadau vinavyopatikana kirahisi kama vile kamera za kisasa, na mashine za kufungashia kazi za filamu hivyo kupunguza gharama za uzalishaji wa filamu nchini.
   
  Aidha, kumekua na uuzaji wa filamu kwa njia ya mtandao suala linalopanua wigo wa masoko na kuitangaza nchi kwa wepesi zaidi hivyo kupelekea umahususi wa mandhari ya Tanzania kutumika na watengenezaji wa ndani na makampuni ya nje yapatayo 169 kutengeneza filamu mbalimbali.
   
  Tasnia ya filamu nchini imeendelea kukua na kushamiri kwa kushirikiana na Washirika wa Maendeleo na wadau wa ndani ya nchi ikiwemo kuandaa, kuratibu  na kuendesha matamasha na Tuzo za Filamu za Tanzania (TAFA),Tamasha la Filamu la Bara la Ulaya, Tamasha la Filamu la Misri, Tamasha la Filamu la India, Tamasha la Filamu la Bara la Asia, Tamasha la Filamu la Brazil na Arusha African Film Festival.

  0 0

  MOR1
  MOR2 
  Afisa Habari Mkuu kutoka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Aisha Malima akipata maelekezo kutoka kwa mfanyakazi wa Kampuni ya Ujenzi ya Estim bw. Joseph Shauri kuhusu ujenzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco.
  MOR3 
  Vifusi vikiwa vimekusanywa katika maeneo ya Mwenge ikiwa ni hatua za awali za ujenzi wa Barabara ya kutoka Mwenge hadi Morocco kazi iliyoanza Desemba Mosi, mwaka huu na inatarajiwa kuisha baada ya miezi sita chini ya Kampuni ya Ujenzi ya Estim jijini Dar es Salaam.
  MOR7 
  Mafundi wakiendelea na harakati za ujenzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco ikiwa ni moja ya hatua ya upanuzi wa barabara hiyo kutoka njia mbili hadi kuwa barabara ya njia tano lengo ni kupunguza msongamano wa foleni.
  MOR9 
  Barabara ya Mwenge hadi Morroco inavyoonekana katika picha kwa sasa ambayo inatarajiwa kuwa barabara ya nia tano badala mbili kama ilivyo sasa lengo ikiwa ni kupunguza msongamano wa foleni kwa watumiaji wa barabara hiyo. (Picha na Lorietha Laurence –Maelezo).


  MOR4 
  Afisa Habari Mkuu kutoka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Aisha Malima akionesha alama zilizowekwa katika maeneo ya Bamaga ikiashiria kuwa tayari ujenzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco imeshaanza kufanya kazi tangu Desemba Mosi, mwaka huu na inatarajiwa kuisha baada ya miezi sita.
  MOR5 
  Afisa Habari Mkuu kutoka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Aisha Malima akiongea na mmoja wa wachuuzi wa vyungu vya maua maeneo ya Bamaga Bw.Emmanuel Kilua ambaye tayari ameshapewa maelekezo ya kupisha eneo hilo ili kupisha ujenzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco inayojengwa na Kampuni ya Ujenzi ya Estim na inatarajiwa kuisha baada ya miezi sita.
  MOR6 
   Vifusi vikiwa vimekusanywa katika maeneo ya Mwenge ikiwa ni hatua za awali za ujenzi wa Barabara ya kutoka Mwenge hadi Morocco kazi iliyoanza Desemba Mosi, mwaka huu na inatarajiwa kuisha baada ya miezi sita chini ya Kampuni ya Ujenzi ya Estim jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Mwongozaji mahiri wa filamu ya Homecoming inayotarajiwa kuingia sokoni hivi karibuni, Seko Shamte. Filamu hiyo iliyotengenezwa na kampuni ya Alkemist Media ina ujumbe wa kuhusiana na vishawishi vya rushwa pamoja na athari zake kwa wafanyakazi na jamii kwa ujumla.
  Crew nzima pamoja na baadhi ya waigizaji
  Moja kati ya kamera kali zilizotumika.
  Kazi ikiendelea location.


  Na Mwandishi Wetu
  WASANII mahiri wameshiriki kwenye filamu ya Homecoming inayotarajiwa kuingia sokoni hivi karibuni akiwamo Daniel Kijo, Mzee Chilo pamoja na mastaa wengine.

  Filamu hiyo iliyotengenezwa na kampuni ya Alkemist Media ina ujumbe wa kuhusiana na vishawishi vya rushwa pamoja na athari zake kwa wafanyakazi na jamii kwa ujumla.

  Kijo ambae anafahamika zaidi katika tasnia ya habari aliwahi kutangaza kwenye kipindi cha Daladala kinachorushwa na Star Tv, katika filamu hii ameigiza kama mhusika mkuu akitumia jina la Abel Mshindi.

  Mzee Chilo ambae jina lake halisi ni Ahmed Olotu ameigiza kama mzazi wa Kijo ambae amekuwa akiishi kijijini miaka yote huku Mzee mwigizaji mwengine mahiri nchini Hashim Kambi ameigiza kama Mjomba wa Kijo.

  Filamu inaanza kwa kumuonesha Kijo akitokea Marekani ambapo alisomea masuala ya fedha na kisha kurejea nchini na kuajiliwa katika kazi ya benki, kwa muda wote akiwa nchini amekuwa akiishi na mjomba wake ambae ni Kambi huku baba yake (mzee chilo) akiwa anaishi kijijini.

  Kijo alijikuta akiingia katika janga la rushwa kutokana na kushawishiwa na shida za baba yake huyo aliekuwa akimtegemea kwa kila kitu huku pia kukiwa na mwanamke ambae nae alikuwa akitaka mahitaji.

  Kutokana na changamoto za kimaisha Kijo alijiingiza katika janga la rushjwa na kujikuta akikamatwa na kufungwa.

  Wengine katika filamu hiyo ni Susan Lewis maarufu kama Natasha, Uncle Mshindi, maarufu kama Hashim Kambi pamoja na Abby Plaatjes aliewahi kuwa mshiriki wa Big Brother Afrika.

  Pia wapo akina Alpha Mbwana, Magdalena Munisi, Godliver Gordian, Michael Kauffmann na itaanza kuoneshwa kwenye kumbi ya cinema kabla ya kuingia rasmi sokoni. zaidi tembelea www.homecomingtz.com

  0 0

  el1 
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel (watatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Shirika la Voluntary Serverce Overseas (VSO)Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Vijana Bibi. Esther Liwa,Mkurugenzi wa Kanda wa VSO Bibi. Niki Kandirikirika, Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika lisilo la Kiserikali la Volountary Service Overseas (VSO) Dkt.Philip Goodwin, Mkurugenzi wa Voluntary Service Overseas nchini Bw. Jean Van Wetter na Meneja Mradi wa ICS kutoka VSO Bibi. Imisa Masinjila.Picha na Frank Shija, WHVUM
  .el3 
  Afisa Mtendaji Mkuu wa shiriki lisilo la Kiserikali la Volountary Service Overseas (VSO) Dkt.Philip Goodwin akifafanua jambo wakati wa kikao baina ya wajumbe kutoka shirika hilo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel (kulia) jana jijini Dar es Salaam.
  el2 
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel (kulia) akizungumza na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika lisilo la Kiserikali la Volountary Service Overseas (VSO) Dkt.Philip Goodwin alipo mtembelea ofisini kwake jana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuishukuru Serikali kwa ushirikiano inaowapa katika kufanikisha majukumu yao.
  el4 
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel (katikati) akielezea jambo wakati wa kikao baina yake na ujumbe kutoka Shirika la Voluntary Serverce Overseas (VSO) jana jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika lisilo la Kiserikali la Volountary Service Overseas (VSO) Dkt.Philip Goodwin na kulia ni Mkurugenzi wa Voluntary Service Overseas nchini Bw. Jean Van Wette

  0 0

   

  Mwenyekiti wa kamati ya amani mkoa wa Arusha(APET) Petro Ahham akimkabidhi kikombe cha ushindi wa bonanza la amani na utalii mkoa wa Arusha,nahodha wa timu ya Kitambi Noma, James Lugangira.
  wanamichezo wa kitambinoma wakiwa wanashabikia ushindi mara baada ya kukabidhiwa kombe katika kiwanja cha General Tyre jijini Arusha.
  Na Woinde Shizza,Arusha

  Klabu ya Kitambi noma ya jijini Arusha, juzi ilitwaa ubingwa wa soka
  katika tamasha la kwanza la amani na utalii ambalo lilifanyika viwanja vya
  General Tyre jijini Arusha.

  Timu hiyo ilitwaa ubingwa baada ya kuzishinda timu za Wazee Klabu na chuo  cha Uandishi wa habari Arusha(AJTC) kwa kukusanya alama nyingi kutokana na   mashindano yaliyoendeshwa kwa mfumo wa Ligi.

  Katika tamasha hilo, liliandaliwa na taasisi ya Arusha media jumla ya timu
  sita zilishiriki katika michezo mbali mbali na sambamba na kutolewa
  burudani ya ngoma za asili kutoka kikundi cha Cultural Arts Center cha
  chuo kikuu cha Makumira.

  Hata hivyo kwa upande wa mpira wa pete, timu ya Wazee Qeen ilifanikiwa
  kutwaa ubingwa baada ya kuichapa katika mchezo wa fainali timu ya AJTC Qeen magoli 34-7.

  Katika mchezo wa kukimbiza kuku, timu ya Kitambi noma ilishinda dhidi ya
  Wazee Klabu na kwa upande wa wasichana AJTC ilishinda dhidi ya Wazee Qeen.

  Akikabidhi zawadi za washindi , Mwenyekiti wa kamati ya amani mkoa wa
  Arusha, Petro Ahham alipongeza timu zote zilizoshiriki kutokana kudumisha
  amani kwa vitendo.

  "tamasha hili limekuja wakati muafaka kwani Arusha ni jiji la kitalii
  ambalo linahitaji amani wakati wote hivyo kufanya michezo kuhimiza amani na utalii ni jambo jema sana"alisema

  Awali Katibu wa chama cha soka wilaya ya Arusha,Zakhayo Mjema alipongeza  taasisi ya Arusha Media kwa kuandaa tamasha hilo la amani na utalii katika  jiji la Arusha.

  "matamasha kama haya yalipaswa kufanywa na chama cha soka lakini tumekwama  hivyo, tunapongeza Arusha Media kwa kusaidia kuendeleza michezo katika jiji  la Arusha"alisema.

  Tamasha hilo, lilidhaminiwa na Shirika la hifadhi za taifa(TANAPA),kampuni  ya vinywaji ya Cocacola, kampuni ya Sunny Safaris, kampuni ya Big   Expedition na kampuni ya Marera Lodge &tours.


   


older | 1 | .... | 700 | 701 | (Page 702) | 703 | 704 | .... | 1898 | newer