Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

MKAZI WA DAR ES SALAAM AKAMATWA NA JESHI LA POLISI MBEYA AKIWA NA MENO YA TEMBO KILO 8.5

0
0

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi
Na Emanuel Madafa,Mbeya

Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia Lukas Wambura (38) Mkazi wa Banana – Dar es salaam mwenye shahada ya dharura ya kusafiria ab-10044029 akiwa na vipande vinne vya meno yadhaniwayo kuwa ya tembo vyenye uzito wa kilo 8.4 yenye thamani ya dola za kimarekani 30,000, sawa na tshs 64,140,000/=.Tukio hilo limetokea Novemba 30 -2015 majira ya saa12 jioni katika eneo la custom – mpakani tunduma, , wilaya ya momba Mbeya .

Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi amesema mtuhumiwa huyo alikuwa anavuka mpaka akitokea nchi jirani ya Zambia kuingia nchini na mzigo huo alikuwa ameuficha ndani ya begi lake la nguo.Wakati huo jeshi hilo la polisi linawashikilia watu wanne kwa kukutwa na silaha mbili pamoja na nyara za serikali.

Kamanda Msangi amewataja watuhumiwa hao kuwani M ohamed Ndilava [55], Mkazi wa Mkwajuni , Nassora Omary [65] Mkazi wa Tabora na Mwanza Mtokambali [39] Mkazi wa Njelenje pamoja na Frank Jonas [32], Mkazi wa Bitimanyanga. Msangi amesema watuhumiwa hao sita walikamatwa Novemba 30 mwaka huu majira ya saa 3 usiku katika kijiji cha Kapalala Wilayani Chunya Mkoani Mbeya .

Amesema watuhumiwa walikutwa na silaha moja aina ya riffle 416 yenye nambari c.6539833 na gobole moja lisilokuwa na namba, pia walikutwa na nyara za serikali kichwa kimoja cha paa, nyama ya paa na nyama ya sungura vyote vikiwa na thamani ya tshs 1,176,000/=.

Kufuatia matukio hayo Kamanda Msangi anatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa juu ya wahalifu wakiwemo majangili kuzitoa katika mamlaka husika ili hatua za kisheria dhidi yao zichukuliwe mara moja.

(JAMIIMOJABLOGMBEYA ) .


MKUU WA WILAYA AFANYA ZIARA YA KUKAGUA VYOO MANISPAA YA SHINYANGA.

0
0


Hiki choo cha ajabu kiko Shinyanga maelezo yapo chini.Leo Jumatatu Novemba 30,2015 ambapo mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ameanza kufanya ziara kutembelea kata za manispaa hiyo ili kuangalia hali ya usafi wa mazingira kubwa zaidi ni kukagua vyoo vya wananchi ilimkukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu.

Mkuu huyo wa wilaya ya Shinyanga alikuwa ameambatana na mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna,mwanasheria wa manispaa hiyo Simon Jilanga,afisa afya wa manispaa hiyo Heri Nakuzelwa,waandishi wa habari na askari wa jeshi la polisi.

Mkuu huyo wa wilaya ametembelea kata ya Chibe na Kambarage na kubaini kuwa kaya nyingi hazina vyoo na kuagiza wajenge vyoo haraka huku akifunga maduka matano kutokana na kukosa vyoo.Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo kwenye msafara huo ametusogezea picha 37 kilichojiri.


Ziara ilianzia katika ofisi ya afisa mtendaji wa kata ya Chibe katika manispaa ya Shinyanga.Pichani ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro(mwenye kofia) akijiandaa kutembea mtaa kwa mtaa kukagua vyoo.Ziara ya mkuu huyo wa wilaya imekuja siku chache tu baada ya kufanya mkutano mkubwa na akina mama wa manispaa ya Shinyanga kujadili namna ya kupambana na ugonjwa wa kipindupindu ambapo mpaka sasa umeua watu watatu kati ya wagonjwa 98 waliripotiwa kukumbwa na ugonjwa huo unaotokana na mtu kula au kunywa kinyesi cha mtu mwingine baada ya kuingia kwenye maji au chakula.

Msafara wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ukielekea katika mtaa wa Chibe ambapo katika kata ya Chibe ina jumla ya kaya 1500 lakini kaya 398 hazina vyoo,lakini kati ya hizo kaya 1500 nyingi hazina vyoo bora.


Mzee Jilili Njinya(kushoto) akijitetea kwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwanini hana choo katika familia yake na kuahidi kujenga ndani ya siku 7.



Hii ni familia katika mtaa wa Chibe katika manispaa ya Shinyanga kulia ni choo cha familia hiyo



Familia ya Shija Kabakuli katika mtaa wa Chibe iliyopewa wiki moja ijenge choo kwani hawana choo na matokeo yake hujisaidia vichakani hali inayochangia kuwepo kwa ugonjwa wa kipindu pindu




Mwananchi akijitetea na kuahidi kujenga choo




Choo katika moja ya familia katika mtaa wa Chibe



Kushoto ni mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna,katikati ni afisa mtendaji wa kata ya Chibe Daniel Mtasibwa na mwandishi wa gazeti la Nipashe wakiwa katika mtaa wa Chibe kuangalia vyoo vya wananchi




Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisikiliza maelezo kutoka kwa mtoto baada ya kuulizwa wazazi wake mbona hawaonekani nyumbani.....kumbe walikimbia baada ya kusikia kuna ukaguzi wa vyoo kutokana na familia hiyo kukosa choo na kulazimika kutumia choo cha jirani yao


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akitoa agizo kwa diwani wa kata ya Chibe John Kisandu juu ya familia ambazo hazina vyoo ambapo alitoa muda wa siku 7 wajenge vyoo na baada ya hapo atarudi kukagua





Waandishi wa habari wakishangaa choo cha aina yake...mchana hakitumiki kwa sababu hakina ukuta wala paa...yaani peupee....giza likiingia mtu anafanya yake



Choo katika familia mtaa wa Chibe kata ya Chibe manispaa ya Shinyanga




Diwani wa kata ya Chibe John Kisandu akizungumza wakati wa ziara ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akikagua vyoo katika kata hiyo ambapo aliahidi kuhamasisha wananchi kujenga vyoo ili kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu




Diwani wa kata ya Chibe John Kisandu akionesha shimo la choo lililopo mbele ya familia...Shimo hilo liko wazi japokuwa limefunikwa kwa miiba,nzi wapo wa kutosha hali inayoweza kuchangia mlipuko wa ugonjwa kipindupindu




Diwani wa kata ya Chibe John Kisandu akimwagiza mama wa familia hiyo kufunika shimo la choo lililopo mbele ya familia hiyo ili kuepuka ugonjwa wa kipindupindu




Bibi hana wasiwasi....Choo changu kile paleeeeee!!




Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro(kulia) akimweleza mwenyekiti wa mtaa wa Busambile bwana Charles Mayunga(mwenye kanzu) jinsi choo bora kinavyopaswa kuwa




Afisa afya wa manispaa ya Shinyanga(aliyevaa miwani) akiangalia shimo la choo kinachojengwa katika mtaa wa Busambile..ambapo alimtaka mama mwenye nyumba hiyo Severine Kulwa(katikati)kukamilisha ujenzi wa choo hicho haraka




Kushoto ni mwanasheria wa manispaa ya Shinyanga Simon Jilanga akimhoji kijana Sindi Fungwe kwanini hajajenga choo katika familia yake




Hapa ni Kata ya Kambarage-Pichani ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga akipokea maelezo kuhusu moja ya nyumba yenye wapangaji wengi ikiwa ni pamoja na ofisi ya serikali ya mtaa...Nyumba hiyo ni bora lakini hakuna choo




Muonekano wa nyumba hiyo isiyokuwa na choo bali bafu pekee kama linavyoonekana kulia likiwa na pazia la mifuko.Baada ya kusikia ugeni wa mkuu wa wilaya,mmiliki wa nyumba hiyo alitoweka



Muonekano wa mbele wa nyumba hiyo,ambapo mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro aliagiza maduka yaliyopo katika nyumba hiyo yafungwe mpaka pale watakapojenga choo




Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akitafakari jambo katika mtaa wa Mwasele "A" wakati akikagua vyoo na kubaini kuwa katika mtaa huo ambao una kaya 22 zisizokuwa na vyoo na zenye vyoo vingi siyo bora



Muonekano wa choo katika familia moja mtaa wa Mwasele A kata ya Kambarage



Kijana akipika wakati wa ziara ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga katika mtaa wa Mwasele A ..pembeni kuna choo hakijafunikwa..angalia hapa chini




Choo kikiwa wazi hali ambayo ni hatari kwa afya za watu wanaozunguka eneo hilo




Muonekano wa choo hicho kwa mbele




Hiki ni choo kingine katika mtaa wa Mwasele kata ya Kambarage katika manispaa ya Shinyanga


Hiki choo kipo katika senta ya Maduka Matatu mtaa wa Mwasele A kata ya Kambarage katika manispaa ya Shinyanga.Ni choo cha ajabu kweli kweli..hakuna tundu isipokuwa kuna bomba na matofali mawili..ukitaka kujisaidia kwanza lazima uwe na shabaha kulenga kwenye bomba lililolazwa chini..ukikosea tu lazima uzoe hakuna ujanja...kinatumiwa na wamiliki wa maduka katika senta hiyo..angalia hapa chini



Afisa afya wa manispaa ya Shinyanga Heri Nakuzelwa akiwapa muongozo wafanyabiashara katika senta ya Maduka Matatu baada ya mkuu wa wilaya kuagiza kufunga maduka hayo mpaka wajenge choo bora kuliko kile cha kulenga..angalia hapo juu




Mfanyabiashara wa duka la dawa za binadamu senta ya Maduka Matatu akifunga duka lake




Hatuna choo..Tunafunga duka....




Wananchi wakisikiliza maelekezo kutoka afisa afya wa manispaa ya Shinyanga Heri Nakuzelwa aliyewataka wajenge vyoo ili kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu




Afisa afya wa manispaa ya Shinyanga Heri Nakuzelwa akitoa elimu kwa wakazi wa Mwasele wakati wa ziara ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro




Baada ya agizo la mkuu wa wilaya...maduka yakafungwa..




Baada ya Ziara..Hapa ni katika ofisi ya mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna akizungumza na waandishi wa habari.Kalinjuna alisema tangu ugonjwa kipindu pindu ulipuke katika manispaa hiyo wagonjwa ni 98 na waliofariki dunia ni watatu hivyo kuitaka jamii kujenga tabia ya kufanya usafi,wajenge vyoo,wafanyabiashara wa matunda kuondoka katika maeneo yasiyo rasmi na vitendo vyote vinavyosababisha kuenea kwa ugonjwa huo.


Mkurugenzi huyo wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna alisema wananchi wengi hawana vyoo na wenye vyoo vingi siyo vyoo bora hivyo kuwataka kujenga vyoo bora na kuongeza kuwa tayari wamefunga maduka matano yasiyo na vyoo,kuagiza wananchi na viongozi kusimamia ujenzi wa vyoo na kwamba zoezi la kukagua,kukamata na kufunga maduka ni endelevu...Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKABIDHIWA RASMI OFISI

0
0
 Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majliwa  akipokea taarifa ya makabidhiano ya Ofisi ya Waziri Mkuu kutoka kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuujijini Dar es salaam Novemba 30, 2015. 
 Waziri  Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kupokea taarifa ya makabidhiano ya Ofisi kutoka kwa Waziri Mkuu Mtaafu, Mizengo Pinda kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 30, 2015. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Maka  Kikula. 
 Waziri  Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kupokea taarifa ya makabidhiano ya Ofisi kutoka kwa Waziri Mkuu Mtaafu, Mizengo Pinda kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 30, 215. Watatu Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Maka  Kikula.
 Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa  akifurahia  katika mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo  Pinda  na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florence Turuka baada ya Waziri Mkuu Mstaafu kukabidhi rasmi Ofisi ya Waziri  kwa  Waziri  Mkuu Majliwa , kwenye ukumbi wa Ofisiya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 30, 2015.
 Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akimkaribisha  Waziri Mkuu, Mstaafu, Mizengo Pinda  ambaye Novemba 30,2015 alikwenda ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam kukabidhi Ofisi.
  Waziri Mkuu, Majliwa Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo  Pinda ambaye alikwenda Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 30, 2015 kukabidhi Ofisi. 
 Waziri Mkuu, Majliwa Kassim Majaliwa na Waziri Mkuu, Mstaafu, Mizengo Pinda wakimsikiliza  Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt Florence Turuka aliposoma taarifa kabla ya Waziri Mkuu Mstaafu kukabidhi Ofisi, kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 30, 2015.
  Waziri Mkuu, Mstaafu Mizengo Pinda  akizungumza  kabla ya kukabidhi Ofisi kwa  Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa,  kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Novemba 30, 2015.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


WAZIRI MKUU MSTAAFU AKABIDHI OFISI KWA MAJALIWA

WAZIRI MKUU mstaafu Mizengo Pinda amekabidhi ofisi kwa Waziri Mkuu Kasim Majaliwa na kumtaka aimarishe ufuatiliaji wa maelekezo anayoyatoa kwenda ngazi za chini.

Akizungumza wakati wa makabidhiano yaliyofanyika jana jioni (Jumatatu, Novemba 30, 2015), kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam, Bw. Pinda alisema katika kipindi cha uongozi wake kulikuwa na ucheleweshaji wa kupata majibu kutoka ngazi ya chini katika maelekezo aliyokuwa akitoa.

“Ofisi ya Waziri Mkuu ni kubwa na ina mambo mengi ya kufuatilia. Kama kuna changamoto nilikumbana nayo ni ucheleweshaji wa majibu kutokana na maagizo niliyokuwa nikitoa. Itabidi uwe makini sana katika kufuatilia hili,” alisema Waziri Mkuu mstaafu.

Alimtaka ahakikishe kila idara inakuwa na mpango kazi na kunakuwa na ufuatiliaji wa kila kilichopangwa. “Pia ninashauri uandaliwe kikao na watu wa Hazina ili wakueleze jinsi bajeti ya Serikali inavyoandaliwa ili iwe rahisi kwako kufuatilia vipengele kadhaa vya bajeti ya Serikali pindi maswali yanapoulizwa bungeni,” alisema.

Pia alimkabidhi taarifa yenye kurasa 104 ambayo inaelezea majukumu mbalimbali ya taasisi na idara zilizo chini ya Ofisi wa Waziri Mkuu. Ofisi ya Waziri Mkuu ina taasisi nane, idara nane na vitengo saba. Taasisi hizo ni Msajili wa Vyama vya Siasa, Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Tume ya Kuratibu na Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS), Tume ya Uchaguzi (NEC) na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA). Nyingine ni Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Baraza la Biashara la Taifa (TNBC) na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

Idara zilizopo kwenye ofisi hiyo ni Utawala na Rasimali watu, Sera na Mipango, Uratibu wa Maadhimisho ya Kitaifa na Sekta binafsi na Uwezeshaji. Nyingine ni Bunge na Siasa, uatibu wa shughuli za Serikali, Mpigachapa Mkuu wa Serikali na Ofisi Binafsi ya Waziri Mkuu.

Alisema pia ameridhishwa na kasi ya utendaji kazi ambayo Rais Dk. John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu wameanza nayo na kwamba ana imani kwa uchapakazi wao na uadilifu wao,  anaamini wataweza kuivusha Tanzania na kuifikisha kwenye uchumi wa kati ambako Serikali imejielekeza kufika.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alimshukuru Waziri Mkuu mstaafu na kumuahidi kutekeleza yote yaliyomo kwenye taarifa aliyomkabidhi. Pia aliahidi kusimamia kwa karibu suala la ufuatiliaji wa maelekezo anayotoa pamoja na yale yanayotoka ngazi za juu.

Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Katibu Mkuu, Dk. Florens Turuka, Naibu Katibu Mkuu (OWM), Bibi Regina Kikuli, wakuu wa taasisi zote nane, wakuu wa idara na vitengo vya Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Wasaidizi wa Waziri Mkuu walioko ofisi yake binafsi.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMANNE, DESEMBA MOSI, 2015.

HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

0
0
SIMU.TV:  Rais Magufuli ametoa agizo kwa wenyeviti na wakurugenzi kusimamia mashirika ya umma na hukakikisha yanazalisha ili kuingizia taifa faida
SIMU.TV: Mwili wa aliyekuwa mfanyakazi wa Azam Media Ismail Hamza unatarajiwa kusafirishwa kesho na kuzikwa mkoani Morogoro.
 SIMU.TV: Jumla ya walemavu 65 nchini wamepatiwa msaada wa miguu mbadala na kampuni ya Kamal Steels kwa lengo la kuwasaidia kutembea.  https://youtu.be/aYgsa2IAGLU 
SIMU.TV: Mkuu wa Mkoa wa Mwanza amewataka wakazi wa Mkoa huo kujiunga na kituo cha kuwezesha wananchi kujikwamua kiuchumi POSO ili kupata mitaji ya kujiendeleza kiuchumi;https://youtu.be/9eiTOAdDYf8 
SIMU.TV: Wananwake Mkoani Mbeya walalamikia waume zao juu ya matumizi nabovu ya  fedha za TASAF wanazopokea kutoka serikalini; https://youtu.be/wzoJsMdzQSA 
SIMU.TV:  Rais Magufuli ametoa agizo kwa wenyeviti na wakurugenzi kusimamia mashirika ya umma na hukakikisha yanazalisha ili kuingizia taifa faida;https://youtu.be/_elnHPUbHyI 
SIMU.TV: Hali ya taharuki imeibuka katika mtaa wa Nyasaka B Mkoani Mwanza baada ya mkazi mmoja kumfungia mtoto wa miaka 2 ndani ya nyumba;https://youtu.be/OVGF2FVs-Jc 
SIMU.TV: Serikali yawataka wananchi wote kushiriki katika zoezi la usafi siku ya Uhuru kama kutii agizo la Rais Magufulihttps://youtu.be/mf611qpGt40 
SIMU.TV: Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ametoa siku 3 kwa viongozi wa manispaa za mji huo kuhakikisha wanaondoa taka katika maeneo yao ili kuepukana na mlipuko wa kipindupindu https://youtu.be/BgJzjfICyI4
SIMU.TV: Timu ya soka ya Tanzania chini ya miaka 15 inatarajia kuanza ziara yake ya mafunzo kwa nchi za Afrika Mashariki kwajili ya kujiandaa na michuano ya kimataifa; https://youtu.be/rwZQUGdICoo
TBC: Tanzania imeendelea kupata changamoto uanzishwaji wa ligi ya mpira wa miguu kwa wanawake jambo linalopelekea changamoto kwa wadau wa soka nchini; https://youtu.be/29UzpEUNTWQ

Kipindi cha JUKWAA LANGU Nov 30 2015 (Full Show)

0
0

Kipindi hiki hukujia kila jumatatu kuanzia saa 11 jioni kwa saa za Marekani ya Mashariki kuijadili Tanzania ya sasa na ile tuitakayo
Katika kipindi hiki tumejadili (mbali na mambo mengine) muelekeo wa serikali ya tano ya Tanzania,Yanayofanyika yanaleta taswira gani kwa Tanzania? Na Je!
Yataendelea ama?

TAMASHA LA MADIVA KUFANYIKA DISEMBA 4 MWAKA HUU MKOANI MBEYA

0
0
 Msanii wa kizazi kipya Vanessa Mdee (Wa pili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na madansa wake wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Trust “Divas Only” lililofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma. Tamasha hilo ni mahususi kwa utoaji elimu ya uzazi wa mpango kwa kina dada ambalo liliratibiwa na Shirika la DKT international.
 Msanii Vanessa Mdee (kushoto) akibadilishana mawazo na wafanyakazi mbalimbali wa Shirika la DKT International kabla ya kufungua rasmi Tamasha la Divas Only ambalo lilifanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki. (Katikati) ni Meneja Masoko DKT International Sialouise Shayo.
 Kaimu meneja wa DKT International tawi la Dodoma Bi.Zena Mgoi akitoa elimu ya uzazi wa mpango kwa kina dada waliohudhuria uzinduzi wa Tamasha la “Divas Only” ambalo lililofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma.

 Mwishoni mwa wiki TRUST wazindua mfululizo wa matamasha ya kusisimua ya Divas Only ambayo yalimshirikisha mwanadada na msanii wa muziki wa kizazi kipya Vanessa Mdee. 

Trust ni chapa ya njia za kisasa za uzazi wa mpango zenye kuaminika pamoja na bidhaa na huduma za maisha na urembo zinazotengenezwa na wanawake kwa ajili ya wanawake. 

Trust ipo ili kuhamasisha madiva wajipange kwa ajili ya baadaye,Madiva wa Trust wanataka kufanya maamuzi na kupanga kwa ajili ya mafanikio, Trust iko hapa kukusaidia wakati wa safari hii. 

Tulifurahia muda tuliopata kukaa na Vanesaa na Madiva wa Trust wa Dodoma, Kama wewe ni Diva wa Trust ama unataka kujua Trust inahusu nini, njoo ukutane na Madiva wa Trust wengine pamoja na Vanessa Mdee katika matamasha yetu mengine Mbeya Desemba 04 pale Sunset Hall, Soweto na Mwanza Desemba 13, Malaika Beach Resort. Huwezi kufika? Tafuta eneo lilipo Dodoma, Mbeya na Mwanza katika tovuti yetu (trustlife.co.tz) na ututembelee leo!

MAJALIWA AKUTANA NA MABALOZI WA CHINA, KOREA NA SUDAN

0
0
 Waziri Mkuu, Majliwa Kassim Majaliwa akisalimiana na balozi wa China Nchini Dkt. Lu Youqing kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es slaam  Disemba 1, 2015. 
 Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Sudan nchini, Dkt.Yassir  Mohamed Ali Ofisini kwake jijini Dar es salaam Disemba 1, 2015.
 Waziri Mkuu,Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza na balozi wa Korea nchini Mhe. Chung Il ambaye alikwenda Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Disemba 1, 2015 kuaga.


 Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa   akisalimiana na balozi wa Sudan nchini,Dkt. Yassir Mohamed Ali kabla ya mazungumzo yao Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Disemba 1, 2015.
 Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi ya kinyago balozi wa Korea nchini, Mhe. Chung Il ambaye alikwenda Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 1, 2015 kuaga.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

JAJI MAKURU AFUNGUA MAFUNZO MAALUM YA HUDUMA KWA WATEJA KWA WATUMISHI WA MAHAKAMA YA TANZANIA.

0
0
 Elizabeth J. Kisamba, (aliyesimama), mshiriki toka Mahakama ya Wilaya Temeke Dar es Salaam, akichangia mada katika mafunzo ya Huduma kwa wateja, yaliyofanyika mkoani Dodoma.
 Praxeda S. Joseph, (aliyesimama), mshiriki toka Mahakama Kuu Tabora, akifafanua jambo juu ya mada iliyotolewa katika kuboresha huduma kwa wateja mahakamani.
 Watumishi wa Kada mbalimbali wa Mahakama ya Tanzania waliohudhuria mafunzo ya Huduma kwa wateja ili kuweza kuwajengea ujuzi na ufanisi katika kazi mahakamani.
 Simon Berege, Mwenyekiti wa MISA-TAN Afrika, akielezea umuhimu wa mafunzo ya huduma kwa wateja hasa kwa watumishi wa Mahakama ili kuweza kutoa taarifa sahihi ambazo zitarahisisha  kutoa haki na kwa wakati.

 Bw. Nurdin Ndimbe, Mkuu wa Kitengo cha Habari, Mahakama ya Tanzania, akitoa risala fupi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua mafunzo ya Huduma kwa Wateja kwa Watumishi wa Mahakama ya Tanzania. 
 Mhe. Jaji Crescencia Makuru, Jaji Mfawidhi Kanda ya Dodoma, akifungua rasmi mafunzo maalumu ya Huduma kwa Wateja kwa watumishi wa Mahakama ya Tanzania, leo mkoani Dodoma. 
Mhe. Jaji Crescencia Makuru, Jaji Mfawidhi Kanda ya Dodoma, (aliyeketi wa pili toka kushoto), Nurdin Ndimbe, Mkuu wa Kitengo cha Habari, Mahakama ya Tanzania, (wa pili kulia), Deus Kibamba, Mkurugenzi wa TCIB, (wa kwanza kulia), Simon Berege, Mwenyekiti wa MISA-Tanzania, (wa kwanza kushoto), katika picha ya pamoja na Watumishi wa Kada mbalimbali wa Mahakama ya Tanzania washiriki wa mafunzo ya Huduma kwa Wateja,                                                                 Mkoani Dodoma.                                                                                                                                                                     
MAFUNZO maalumu ya siku mbili yahusuyo huduma kwa wateja na haki ya kupata taarifa kwa watumishi wa Mahakama, yamemalizika leo katika hoteli ya St.Gaspar mjini Dodoma.

Akifungua rasmi mafunzo hayo  Jaji Mfawidhi Kanda ya Dodoma, Mhe. Crescencia Makuru, amesema moja ya malengo makuu ya mafunzo hayo, ni kuwajengea uwezo watumishi wa Mahakama kwa kuwapa mbinu na mikakati mbalimbali itakayowasaidia kuongeza ufanisi katika utendaji kazi.

“Mahakama ya Tanzania kwa sasa inaendelea na maboresho ya utendaji kazi wake kama sehemu ya kuhakikisha kuwa inatoa huduma iliyo bora na kwa wakati”, Jaji Makuru amebainisha.

Mwaka 2014 Mahakama ya Tanzania kama moja ya Taasisi ya Serikali ilifanyiwa tathmini kuhusu utoaji wa haduma zake hasa katika nyanja ya upatikani na utoaji wa taarifa kwa Umma iliyoendeshwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, (Media Institute of Southern Africa-MISA). 

Katika tathmini ile, Mahakama ilikuwa ya mwisho na ilizawadiwa kufuli la dhahabu kama alama ya kuonyesha kuwa taasisi hii ni moja kati ya zilizojifunga sana kutoa taarifa kwa wananchi. Moja ya maeneo yaliyoonekana na udhaifu ni namna masijala za Mahakama zinavyopokea na kutunza nyaraka na hata wanavyowahudumia wateja kwa ujumla.

Mafunzo hayo endelevu yamelenga kuwafundisha makarani na watumishi wa kada mbalimbali nini maana ya uhuru wa Habari na habari ni Nini?, Huduma kwa wateja na ujuzi wa mawasiliano kwa watumishi wa Umma , Njia mbalimbali za upatikanaji wa taarifa katika Taasisi za Umma na Sheria ya utoaji wa  habari katika Mahakama.

Mafunzo haya yameandaliwa na kufadhiliwa na Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) pamoja na Taasisi ya Friedrick Ebert Stiftung (FES) ofisi ya Tanzania.

MKUTANO WA KUKUZA SEKTA YA UKARIMU NA UTALII HUFANYIKA KWA MARA YA PILI JIJINI DAR DISEMBA 7 NA 8 MWAKA HUU

0
0
INTERNATIONAL hospitality consultancy HD Partnership (HDP) kwa  kushirikiana na shirika la wamiliki wa Hoteli Tanzania (HAT), wanafanya mkutano wa awamu ya pili wa mwaka Disemba 7 na 8 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

 Mkutano huu unahusu sekta ya ukarimu na utalii,Katika jukwaa hilo litategemea kuzungumzia ujumbe juu ya ukarimu kwa wadau wa sekta ya utalii wakiwemo wawekezaji, wamiliki wahoteli, kampuni za usimamizi, bidhaa, mashirika ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali, wasambazaji na watoaji huduma. Pamoja watajadili juu ya malengo yanayohusu ukarimu na utalii katika nchi zilizopo kusini mwa jangwa la sahara.

Mkutano huu ambao unahusisha wadau wa ndani ya nchi na nje ya nchi, una lengo la kuchochea ukuaji endelevu wa sekta hizi kwa kutoa wataalamu husika kuongea na kutoa ushauri  pia kutengeneza mazingira ya maonyesho ambayo yatatoa fursa za kubadilishana ujuzi baina ya kampuni tofauti kwenye sekta ya ukariimu na utalii. Kwa mujibu wa Meelis Kuuskler ambaye ni mshauri wa kimataifa kuhusu ukarimu na Mkurugenzi mkuu wa HDP anasema “ mkutano wa mwaka huu umejikita katika masuala maalumu ya kiutendaji yanayoathiri shughuli za kiutalii.

 Ikiwa ni pamoja na mjadala kuhusu jinsi gani ya kuiinua ubora wa rasilimali watu, jinsi ya kuchochea zaidi mazingira mazuri ya biashara kwa maendeleo mapya na yaliyopo ya ukarimu, na jinsi ya kuimarisha uhusiano wa sekta zinazoingiliana kwa maendeleo endelevu ya sekta”.

Tanzania inashika nafasi ya 7 kati ya nchi 141 kwa mwaka 2015 katika ushindani wa sekta ya utalii kutokana na rasilimali za asili nyingi zilizopo, hii ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na jukwaa la uchumi duniani. 

Hata hivyo, ripoti pia inaeleza umuhimu wa kuboresha miundo mbinu na mazingira ya kibiashara ili kuimarisha ushindani wa sekta hii kwa ujumla. Kwa mujibu wa Kuuskler anasema “Tanzania imejaliwa  kuwa na mbunga za wanyama, fukwe  na vivutio mbali mbali vinavutia uwekezaji mkubwa katika sekta ya ukarimu na utalii. 
Hata hivyo, faida za maliasili hizi haziwezi kujulikana kwa undani zaidi mpaka masuala kama usafiri wa anga na nchi kavu, soko la ajira and sera za mazingira endelevu zimepatiwa ufumbuzi. Kwa mujibu wa Lathifa Sykes Mkurugenzi mkuu wa HAT anasema   “Vikwazo hivi katika maendeleo ya sekta haviwezi kushughulikiwa ipasavyo na sekta binafsi lakini badala yake vinahitaji ukaribu na umakini zaidi wa kiutendaji wa sekta za umma”.

Waandaaji wa HRT mwaka huu wamebaini umuhimu wa kuhakikisha kuwa wanawashirikisha watendaji wa sekta za umma ili kupata mitazamo, mawazo na taarifa za kutoka kwa watendaji hao ili zishirikishwe kwenye sekta binafsi. Na mialiko imefikishwa hadi kwenye wizara ya kazi na ajira, wizara ya maliasili na utalii, idara iliyo chini ya ofisi ya rais inayoshulika na matokeo makubwa sasa (PDB) pamoja na sekta ya uwekezaji Tanzania (TIC). Kwa mujibu wa Kuuskler anasema “Uwezo wa sekta binafsi katika kutekeleza mabadiliko utakuwa bora kama utalindwa na ushirikishwaji wa wazi wa sekta za umma”.  Kwahiyo pamoja na kutoa jukwaa la kuchochea ushirikiano mpya, mkutano unalenga kuendeleza na kukuza dira ya pamoja ya maendeleo na harakati za maendeleo kati ta ya wadau wa umma na binafsi.

KUHUSU MRATIBU.
HDP ambaye ni mshauri wa ukarimu wa kimataifa, anafanya kazi na wateja wetu, wamiliki, wawekezaji, shughuli za ukarimu , na mashirika ya usimamizi ili kuendesha matokeo yanayoonekana, katika kuboresha, kuendeleza, kutoa msaada wa kifedha na kuendesha shughuli kubwa na ndogo za ukaarimu pamoja na miradi kadhalika ya F&B. 

Ikiwa na ofisi zilizoko nchini Dubai, HDP walileta ofisi yake nchini Tanzania mwaka 2014 ili kusaidia ukuaji mahiri na endelevu wa utalii na ukarimu katika Afrika Mashariki. Kutumia utaalamu mkubwa wa washirika, HDP inaangalia kiundani zaidi juu ya ufumbuzi wa viwango ili kuendeleza mtazamo mpya na kufanya mashirika yawe ya ushindani zaidi. Kwa njia ya uchambuzi wa hali ya juu kwa kila mteja na kuendeleza ufumbuzi wa wateja ambao unakidhi mahitaji ya shirika husika. 

KIINGILIO NI BURE KWA WAJUMBE WOTE WA TANZANIA.
Kiingilio ni bure kwa wajumbe waliojisajili mtandaoni. Tunawahamasisha wamiliki hoteli, mameneja, mawakala wanunuzi, wawekezaji na wadau wote kuungana na sisi, ili muendeleze na mkuuze biashara zenu sasa.

Kujisajili tafadhali tembelea tovuti ifuatayo http://www.hospitalityroundtabletz.com/ 

TAARIFA KUHUSU UTATUZI WA MGOGORO WA WAKULIMA WA MIWA KILOMBERO

0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UTATUZI WA MGOGORO WA WAKULIMA WA MIWA KILOMBERO .
Bodi ya Sukari Tanzania imefuatilia na kubaini chanzo cha malalamiko ya wakulima wa miwa wanaozunguka Kiwanda cha Sukari cha Kilombelo (ILOVO).  

Akizungumza katika taarifa yake, Mkurugenzi Mkuu Bodi ya Sukari Tanzania Bwana Henry Semwanza alisema kuwa, chanzo cha malalamiko yanatokana na kiwanda kuharibika bila kutarajia na kusimamisha uzalishaji kuanzia tarehe 14 hadi 18 Novemba 2015.  

Hali hiyo ilisababisha miwa ya wakulima ambayo ilikuwa imekatwa kuharibika na hivyo kukosa sifa ya kuchukuliwa na kiwanda kwa ajili ya usindikaji. 

Bwana Semwanza aliongeza kuwa hali hiyo ilisababisha tani 250 za miwa kutoruhusiwa kuingia kiwandani kwa vile zilishapita zaidi ya siku tano tangu miwa ilipochomwa. 

 “Miwa hiyo ilichomwa tangu tarehe 14 Novemba 2015 siku ambayo kiwanda kiliharibika, na kilipotengamaa zilikuwa zimeshapita siku tisa, hivyo miwa hiyo kukosa sifa na ubora unaokubalika, na hivyo ikazuiliwa kuingia kiwandani”  

Akizungumzia utekelezaji wa mkataba wa ugavi wa miwa baina ya Kampuni na Vyama vya Wakulima, Bwana Semwanza alibainisha kuwa Kifungu cha 5.2.3.3 cha mkataba huo kinasisitiza kutokuikubali miwa ambayo kiwango cha ubora wake uko chini ya asilimia 80 au miwa iliyopitisha siku tano tangu ilipochomwa kwa mujibu wa kifungu cha 5.2.3.4. 

Ili kupunguza hasara inayoweza kutokea kwa wakulima, Bwana Semwanza aliwakumbusha wakulima  na wamiliki wa kiwanda kuzingatia taratibu za uvunaji wa miwa. 

 “ninatoa wito kwa wakulima kupitia vyama vyao kuzingatia taratibu za uvunaji kwakuwa imedhihirika pasipo shaka kuwa baadhi wamekuwa wanavuna miwa mingi zaidi ya mgao wao wa siku, mambo haya yasipozingatiwa yanaweza kuibua migogoro isiyo ya lazima ” Bwana Semwanza alibainisha katika taarifa yake. 

Aidha, alisisitiza kuwa kamati iliyoundwa chini ya mkataba wa ugavi wa miwa inayojumuisha wakulima na uongozi wa Kiwanda na ambayo hukutana kila siku iendelee kuwa msingi wa kuamua kiasi cha miwa inayotakiwa kuvunwa na kupelekwa kiwandani katika siku inayofuata. 
Semwanza aliongeza kuwa Bodi yake inaendelea kufuatilia utekelezaji wa makubaliano kati ya kiwanda na wakulima, na haitasita kuchukua hatua sitahiki kwa upande utakao kiuka ili kutatua migogoro inayoweza kuzuilika kwa haraka.

Semwanza alisisitza kuwa kwa sasa hali ni shwali ambapo uvunaji na upokeaji wa miwa kiwandani unaendelea kama kawaida na wakulima wameongezewa mgawo wa miwa inayotakiwa kuingizwa kiwandani kila siku. 

“hali ya uvunaji inaendelea kama kawaida na mgao wa wakulima kuingiza miwa yao kiwandani umeongezwa kwa zaidi ya asilimia 50; ili kuhakikisha miwa yote ya wakulima wanaozunguka kiwanda cha Kilombero inavuwa” 
Bodi ya Sukari Tanzania inashirikiana kwa karibu na uongozi wa mkoa na Wilaya ili kushughulikia migogoro isiyo ya lazima. Alihitimisha Bwana Semwanza. 

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika
Kilimo Complex, 
1 Mtaa wa Kilimo 15471
DAR ES SALAAM.

RAIS WA ZANZIBAR ATEMBELEA MRADI WA UIMARISHAJI MRADI WA MAJI SAFI MAKUNDUCHI

0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya maji safi (ZAWA) Dkt. Mustafa Ali Garu (kulia) wakati alipotembelea Uimarishaji wa mradi wa maji safi na salama wa uchimbaji wa Kisima kipya na ukarabati wa tangi la maji Makunduchi Wilaya ya Kusini Mkoa wa Unguja leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya maji safi (ZAWA) Dkt.Mustafa Ali Garu (kulia) wakati alipotembelea Uimarishaji wa mradi wa Maji safi na salama wa uchimbaji wa Kisima kipya na ukarabati wa tangi la maji Makunduchi Wilaya ya Kusini Mkoa wa Unguja leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza na baadhi ya wanachama cha Mapinduzi na Wananchi wa Makunduchi wakati  alipotembelea Mradi wa Uimarishaji wa  Maji safi na salama wa uchimbaji wa Kisima kipya na ukarabati wa tangi la maji Makunduchi Wilaya ya Kusini Mkoa wa Unguja.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban (wa pili kulia) wakati alipotembelea Mradi wa Uimarishaji wa  Maji safi na salama wa uchimbaji wa Kisima kipya na ukarabati wa tangi la maji Makunduchi Wilaya ya Kusini Mkoa wa Unguja leo (kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dkt.Idriss Muslim Hija na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma Haroun Ali Suleiman.[Picha na Ikulu.]

KIKOSI CHA TIMU YA KILIMANJARO STARS KUREJE KESHO

0
0

KIKOSI cha timu ya taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ kinatarajiwa kuwasili kesho mchana jijini Dar ess alaam kikitokea nchini Ethiopia kilipokuwa kinashiriki michuano ya Kombe la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati.


Kilimanjaro Stars imetolewa katika hatua ya robo fainali na wenyeji Ethiopia kwa mikwaju ya penati, baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika dakika 90 za mchezo huo, na wenyeji kushinda kwa penati 4-3.


Timu ya Kilimanjaro Stars inayonolewa na kocha Abdallah Kibadeni na msaidizi wake Juma Mgunda, iliongoza kundi lake katika hatua ya makundi kabla ya kukutana na wenyeji Ethiopia katika mchezo wa robo fainali.

Katika michezo wa makundi, Kilimanjaro iliibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Somalia, ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Rwanda, na sare ya bao 1-1 dhidi ya Ethiopia.


Baada ya kurejea nyumbani, TFF kwa kushirikiana na benchi la ufundi wataanza maandalizi ya michezo dhidi ya Chad itakayochezwa Machi 2016 kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Mataifa Afrika mwaka 2017.

UJENZI WA KISIWA CHA KITALII WAANZA KATIKA ENEO LA MTONI MARINE KASKAZINI MAGHARIBI ZANZIBAR

0
0
 Sehemu  inayoendelea kufukiwa hapo Mtoni Marine ambayo itatumika hapo baadae kwa ajili ya eneo maalum litakalotoa fursa kwa Wananchi  kupata mapumziko.{ Public Beach }. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar { ZIPA } Nd. Salum Khamis Nassor  akimueleza Balozi Seif  hatua zinazochukuliwa na Taasisi yake katika kuona taratibu za uwekezaji zinachukuliwa kwa wanaowekeza vitege uchumi vyao Nchini. 
Balozi Seif akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Baghresa Group Bwana Said Salim wakitembelea kuona  mradi wa Ujenzi wa Majengo Mapya ya Hoteli ya Mtoni Marine ambayo iko chini ya Kampuni hiyo kwa hivi sasa.

MRADI mkubwa wa Kimataifa wa ujenzi wa kisiwa cha Kitalii  ambacho kitatengenezwa kwa mfumo wa ufukiaji Bahari umeanza rasmi katika eneo la Hoteli ya Utalii iliyopo Mtoni Marine kaskazini Magharibi ya Mji wa Zanzibar.

Hata hivyo gharama kamili za Mradi huo bado hazijafahamika  wakati utakapokamilika  rasmi ujenzi wake hapo baadaye.

Mradi huo unaoendeshwa na Kampuni ya Kizalendo  ya Baghresa Group utahusisha ujenzi wa Hoteli ya Kimataifa ya Ghorofa  Tano ya Daraja la Tano { Five Star + }, utengenezaji wa eneo la wazi la mapumziko { Public Beach } pamoja na kutengeneza  Kisiwa cha Mji mpya.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alishuhudia harakati za ujazaji wa mchanga katika eneo linalofukiwa ambazo hufanywa kwa utaalamu wa hali ya juu.

Mhandisi wa Mradi huo Bwana Ahmed Shamsi alimueleza Balozi Seif  kwamba chombo maalum kinachotumika kwa kazi ya uchimbaji wa mchanga Baharini  kina uwezo wa kunyonya  na kusafirisha mchanga kutoka ndani ya Bahari sambamba na kukata Majabali.

Mhandisi Shamsi alisema kazi hiyo inafanyika kwa saa 12 kila siku ambapo takwimu zinaonyesha wazi kwamba uchimbaji huo wa mchanga unaokwenda  zaidi ya mita 15 chini ya Bahari unafikia  Tani 600 za mchanga kwa saa Moja.

Alifahamisha kwamba harakati za uchimbaji na kufukia mchanga katika eneo hilo zilizoanza Mwezi uliopita wa Novemba zinatarajiwa kukamilika mwezi Januari mwaka ujao.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Baghresa  Group  Bwana Said Salim Baghresa alisema kwamba ujenzi wa mradi huo muhimu kwa uchumi wa Nchi utasaidia mapato ya Taifa pamoja na kutoa ajira kubwa kwa vijana Wazalendo hapa Nchini.

Bwana Baghresa alisema mfumo wa ufukiaji Bahari kwa ajili ya kuanzisha miradi ya Kiuchumi ni mfumo unaotumiwa na Mataifa mbali mbali Duniani ambapo kwa Afrika  mradi kama tayari umeanza kutumiwa katika Kisiwa cha Seycheles.

Akitoa nasaha zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameupongeza Uongozi wa Baghresa Group kwa uamuzi uliochukuwa wa kuanzisha mradi huo mkubwa wa Kimataifa.

Balozi Seif alieleza kwamba kukamilika kwa mradi huo mkubwa  ambao umeshazoeleka katika Mataifa yaliyoendelea utasaidia kuitangaza Zanzibar na Tanzania kwa ujumla  Kiutalii Kimataifa.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliuhakikishia Uongozi huo wa Baghresa Group kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itatoa kila msaada unaohitajika katika  kuona mradi huo unafikia malengo uliojipangia.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamui wa Pili wa Rais wa Zanzibar
1/12/2015.

KATIBU MKUU WA WIZARA YA UCHUKUZI ATEMBELEA KARAKANA YA KUTENGENEZEA BREAKPAD ZA VICHWA VYA TRENI LEO JIJINI DAR

0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi atembelea karakana kutengenezea breakpad za vichwa vya treni kinachomilikiwa na kampuni miliki ya rasilimali za Reli(RAHCO) leo asubuhi jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Shaaban Mwinjaka (wa nne kutoka kushoto), akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Miliki ya Rasilimali za Reli (RAHCO), Mhandisi Benhadard Tito, wakati akimwelezea namna karakana ya  kutengenezea breakpad za vichwa vya treni kilivyokuwa kinafanya kazi, na sasa hakifanyi kazi, wakati Katibu Mkuu huyo alipotembelea kiwanda hicho leo asubuhi, Katibu Mkuu ameipa wiki mbili kampuni hiyo na Shirika la Reli Tanzani (TRL) kuuanda timu na kufanya tathmini ya mitambo iliyoharibika na kuhakiki kiwanda hicho kinaanza kufanya kazi.
 Jengo ambalo lilikuwa likitumika kama karakana ya kutengenezea breakpad za vichwa vya treni, linavyoonekana baada ya kusitisha uzalishaji wa breakpad hizo.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka akitoa maelekezo kwa uongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), mara baada ya kutembelea eneo la Reli sehemu ya Malindi leo asubuhi.
Reli  ambazo hutumika kubadilisha baada ya ziliyopo kuchakaa, zikiwa kwenye eneo la Malindi, kama zilivyokutwa leo asubuhi.
(Habari Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikali-Uchukuzi)

KATIBU MKUU WA WIZARA YA UCHUKUZI AZINDUA SAFARI ZA NDEGE YA SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LA NCHINI ABU DHABI LEO

0
0
Balozi wa Nchi za Falme za Kiarabu (United Arab Emirate) nchini Tanzania, Balozi Abdullah Ibrahim Al Suwaidi (wa pili kutoka kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka (wa tatu kutoka kulia), pamoja na Viongozi Wengine wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Safari za ndege za shirika la Shirika la Ndege la Etihad la Nchini Abu Dhabi leo mchana, katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Mwl. Julius Nyerere (JNIA).
 Magari ya Zimamoto yakimwaga maji kuashiria uzinduzi na ukaribisho wa Safari za Ndege ya Shirika la Ndege la Etihad la Nchini Abu Dhabi, leo mchana katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Mwl. Julius Nyerere (JNIA).
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Shaaban Mwinjaka, akiteta jambo na Balozi wa Nchi za Falme za Kiarabu(United Arab Emirate) nchini Tanzania, Balozi Abdullah Ibrahim Al Suwaidi, kabla ya Uzinduzi wa Safari za Ndege ya Shirika la Ndege la Etihad la Nchini Abu Dhabi, leo mchana.
 
(HABARI PICHA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-UCHUKUZI).

FEDHA ZA 9 DISEMBA ZAANZA UJENZI WA KUPANUA BARABARA MWENGE-MOROCCO JIJINI DAR

0
0


Scaveter ikisafisha sehemu ya barabara kuanzia Mwenge hadi Morocco kwaajili ya upanuzi wa barabara mbili zinazojengwa kwa fedha ambazo zilitakiwa kutumika katika sherehe za uhuru ambazo hufanyika kila mwaka Disemba 9 ikiwa ni kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Joseph Magufuli kazi hiyo imeanza kutekelezwa leo jijini Dar es Salaam.
Vijana wakigombania bango ambalo limevunjwa katika upanuzi wa barabara kuanzia Mwenge hadi Morocco leo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanul Massaka wa Globu ya jamii).

MSIMU WA MATUNDA AINA YA EMBE SOKONI BUGURUNI LEO

0
0

  

NAPE: CCM ITAMPA USHIRIKIANO MKUBWA DK. MAGUFULI ATEKELEZE ILANI KIKAMILIFU

0
0
 Mazungumzo yakiendelea
 Naam hayo ndivyo yalivyo.....
 Mkurugenzi wa New Habari Corporation  Erasto Matasya akizungumza.

NA BASHIR NKOROMO.
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesema, kitampa ushirikiano mkubwa, Rais Dk. John Magufuli, ili aweze kwa ufanisi zaidi mapambano yake dhidi ya mafisadi na mikakati mingine ya kuinua uchumi wa Watanzania.

Kimesema, kitampa ushirikiano huo Rais Dk. Magufuli, kwa sababu, aliyoanza kuyafanya na atakayoyafanya baadaye katika uongozi wake wa Urais anatekeleza yale yaliyomo katika ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015-2020.

Hayo yalisemwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alipokuwa akijibu maswali kadhaa yaliyoulizwa na baadhi ya wahariri, aliokuwa akizungumza nao, katika ziara aliyofanya leo, katika Kampuni ya New Habari Corporation, Sinza jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wahariri, waliohoji ni kwa nini CCM haijitokezi kumpongeza Dk. Magufuli katika juhudi ambazo ameanza kuonyesha katika kupambana na ufisadi ikiwemo kubana fedha za walipa kodi ambazo zingepotea bure katika masuala yasiyo ya lazima na wakati huohuo kuanza kuwabana wafanyabiashara wanaodaiwa kukwepa kulipa ushuru.

"Yapo mengi tuliyoanisha katika ilani yetu ya Uchaguzi, na yote yahahusiana sana na haya mnayoyaona yanafanywa na Rais Dk. John Magufuli, tena Ilani hii tumeitunga hata kabla ya kumteua kugombea Urais, Sasa anachofaya ni kuitekeleza ilani hii, isipokuwa mbinu anazotumia ni ubunifu wake na hili hatuna tatizo nalo kama Chama maana kiongozi wa aina hii ndiye tuliyemtaka", alisema Nape.

"Najua wapo wanaojaribu kutengeneza mazingira ya kumtaka kumtenganisha Dk. Magufuli na CCM, nawambieni Dk. Magufuli ni zao la CCM na mwana CCM Kindakindaki, hivyo ni upotoshaji wa hali ya juu kujaribu kuuaminisha umma kwamba anayofanya Dk. Magufuli hayana uhusiano na maelekezo ya CCM", aliongeza Nape.


Alisema, baada ya kutengeneza ilani yake, CCM, ilidhamiria kwamba, awamu hii ya tano ni ya kutafsiri uchumi katika nyanja za huduma za Jamii, ikiwemo miundomboni, maji, afya na elimu.

"Ni kutokana na lengo hili, ndiyo sababu tukakaa kwa makini na kuhakikisha ilani hii ya sasa tunamkabidhi mwana CCM ambaye utekelezaji wake hautakuwa wa mashaka mashaka, Ndiyo huyo Dk. Magufuli, bila shaka sasa na ninyi ni mashahidi mmeanza kuuona utekelezaji wake wa ilani", alisema Nape.

Akizungumzia kuhusu Rais Dk. Magufuli kuchelewa kutangaza Baraza lake la Mawaziri, Nape alisema, Chama Cha Mapinduzi kimeshaunda serikali kwa kumpata Rais, kilichobaki sasa ni kwa Rais mwenyewe kuteua watendaji wake, lakini katika kufanya hivyo hakuna mda aliopangiwa kuanza kufanya hivyo na hashurutishwi na Chama wala sheria.

Nape alisema, Dk. Magufuli hachelewi kuteua Baraza la Mawaziri kwa sababu anakosa wakuwateua, isipokuwa, anayo namna na mda ambao mwenyewe Kama Rais amejipangia, na mda huo ukijiri wa kuamua kufanya hvyo atafanya.

"Tatizo hapa ni kwamba mnayo kiu kubwa ya kutaka kujua nani atawateua, sasa kiu yenu imepita kiasi, ndiyo maana mnaanza kuhoji, lakini mimi naamini Dk. Rais Magufuli ataikata kiu yetu, wala msipate taabu ya kuhoji kila kukicha", alisema Nape.

Nape alisema, mbali na Chama kutengeneza ilani ambayo italeta mageuzi makubwa ya kiuchumi hapa nchini, pia Watanzania watarajie kuona mageuzi makubwa ndani ya CCM, kwa sababu yapo njiani kuwadia.

"Kama ilivyo kawaida yetu, kila baada ya uchaguzi mkuu huwa tunafanya tathmini, baada ya tathmini hiyo, huwa lazima tufanye mageuzi kwa yale ambayo tumebaini kuwa ni kikwazo kwa uhai na maendeleo ya Chama katika nyanja mbalimbali, na mageuzi haya tunayafanya kuzingatia mahitaji ya sasa na wakati ujao", alisema Nape.

Kuhusu Mwenyekiti wa sasa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete kumwachia Ueneyekiti Rais Dk. Magufuli, Nape alisema, hayo si mambo mageni kwa CCM, imekuwa ikifanyika katika awamu zote za Urais, hivyo Kikwete anaweza akaamua kumwachia kabla ya uchaguzi mkuu wa CCM utakaofanyika mwaka 2017 au kabla ya hapo akiona inafaa.

Zanzibar
Akizungumzia mgogoro wa Zanzibar uliotokana na kufutwa uchaguzi mkuu wa Rais wa Zanzibar, Nape alikiri kamba ni mbaya na unaitia doa Tanzania, akisema, lakini akasisitiza kwamba njia pekee ya kuumaliza ni kwa mazungumza baina ya viongozi wa ndani bila kushirikishwa mataifa ya nje.

Alisema, msingi wa mgogoro uliojitokeza Zanzibar, si wa kisheria, bali ni wa kisiasa zaidi, hivyo juhudi ziwekwe kwenye mazungumzo kuutatua, na baada ya kuutatua yaendelee kufanyika mazungumzo ambayo yataleta suluhisho la kudumu kwa kuwa imekuwa ni kawaida kwa Zanzibar kuzuka migogoro kila baada ya uchaguzi mkuu jambo linaloonyesha kuwa tatizo ni la asili zaidi kuliko inavyodhaniwa.

Katika mazungumzo yake na wahariri hao wa New Habari Corporation Ltd, Wachapishaji wa magazeti ya Rais, Mtanzania na Dimba, alivitaka vyombo vya habari nchini, sasa kushirikiana na Serikali kulijenga taifa.

"Tunajua wakati wa kampeni kulikuwa na mambo mbalimbali ambayo wakati mwingine vyombo vya habari vililazimika kukampenia vinaowaona kuwa wanafaa kutokana na sababu mbalimbali, lakini kama tulivyokuwa tukisema, kwamba baada ya uchaguzi maisha yataendelea, sasa umefika wakati wa kuendelea na maisha tuwe kitu kimoja", alisema Nape.

Alivitaka vyombo vya habari, kusaidia kuishari Serikali na CCM, katika kutekeleza yaliyo bora kwa taifa na hata pale vyombo hivyo vitakapoona kwamba Chama au serikali vinaenda kinyume, visihofii kukosoa.

Kwa upande wao, Mtariri Mtendaji wa Habari Corporation, Absalom Kibanda akimpongeza Nape kwa ushirikiano ambao amekuwa akivipa vyombo vya habari, na kumtaka aendelee kuwacha milango wazi kwa waandishi wa habari kama ambavyo amekuwa akifanya.

Ziara hiyo ya Nape aliyoianza jana, kwenye vyombo vya habari inatarajiwa kuendelea kesho kwa kutembelea vyombo vingine vya habari vyenye makao yake makuu jijini Dar es Salaam.

BREAKING NYUZZZZZ: BENKI YA STANBIC TANZANIA MATATANI TENA

0
0
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, akizungumza na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es salaam leo kuhusiana na tuhuma zilizoelekezwa kwa benki ya Stanbic Tanzania kuwa imetumika katika kufanya udanganyifu wa riba ya mkopo dola Milioni 600 iliyopewa serikali ya Tanzania na Uingereza kupitia Kampuni ya Egma ya Tanzania.

Amesema kuwa Benki kuu ilifanya ukaguzi wa benki hiyo na mambo mengine,walibaini malipo yasiyokuwa ya kawaida kuhusiana na kampuni ya kitanzania inayoitwa Egma,malipo hayo yalikuwa kinyume na taratibu za kibenki na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo walishindwa kuvumilia.

" kwa hiyo tetesi tukazipata, wakaguzi wa benki kuu walifuatilia malalamiko hayo na kujiridhisha kuwa uongozi wa benki ya Stanbic Tanzania ulifanya mambo ambayo yalikuwa ni kinyume na taratibu zinazokubalika kibenki, ambapo fedha kiasi cha dola milioni 6 ziliingizwa kwenye kampuni ya Egma na siku chache baadae zilitolewa zote kwa fedha taslimu wala benki haikukusanya kodi ya zuio ambayo kwa mujibu wa sheria ya kodi ilipaswa kutozwa"amesema Balozi Ombeni Sefue. 



  

PINDA ATOA WITO KUENZI UTAMADUNI

0
0
miz1 
Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda (katikati) akipata maelekezo toka kwa Mshauri wa Masuala ya Utamaduni toka Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China Bw. GAO Wei (kulia) wakati Waziri Mkuu akifungua kituo cha Utamaduni wa China nchini Tanzania mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel.Picha zote na Eliphace Marwa – Maelezo
miz2 
Mshauri wa Masuala ya Utamaduni toka Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China Bw. GAO Wei akitoa ufafanuzi wa picha za matukio mbalimbali kwa Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda (katikati) mara baada ya Waziri Mkuu Mstaafu kufungua kituo cha utamaduni wa China nchini Tanzania mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
miz3 
Kundi la Muziki la Zinijncheng kutoka chuo Kikuu cha Sanaa ya Muziki cha China kikitoa burudani kwa mgeni rasmi Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda (hayupo pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa kituo cha Utamaduni wa China nchini Tanzania.
miz4 
Baadhi ya wanafunzi wa Kitanzania wanaojifunza lugha ya Kichina katika kituo cha Utamaduni wa China nchini Tanzania wakiimba nyimbo kwa lugha ya Kichina mbele ya mgeni rasmi Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda (hayupo pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa kituo hicho.
miz5 
Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda (kushoto) akifungua kituo cha utamaduni wa China nchini Tanzania mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel na kulia ni Mkurugenzi wa Utamaduni toka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Hermas Mwansoko.

………………………………………………………………………………………
Na Nyakongo ManyamaMAELEZOWaziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda ametoa wito kwa Watanzania kutambua kuenzi na kuutunza utamaduni wetu ikiwemo lugha ya Kiswahili kwani ndiyo utambulisho mkubwa wa nchi yetu. 
 Mhe. Pinda ametoa wito huo leo jijini Dae es Salaam wakati akifungua kituo cha Utamaduni China nchini. Kituo hicho pekee cha utamaduni Afrika Mashariki kitatoa fursa kwa Watanzania na Wachina kubadilishana utamaduni.
 Kwa kutumia kituo hichi, Watanzania wanaweza kuongeza uhusiano kwa vijana wetu hasa wenye umri mdogo kujifunza utamaduni wa China. “Watanzania tunatakiwa kuutambua, na kuuenzi utamaduni wetu hasa lugha yetu ya Taifa ya Kiswahili badala ya kuona raha kuongea lugha za wageni. Tuongee na tutumie fursa hii ya kituo cha utamaduni kuendeleza utamaduni wetu ,” amesema.
 Kwa mujibu wa Mhe. Pinda, utamaduni kwa nchi yoyote ni kila kitu ambacho mtu anakua nacho katika maisha ya kila siku.“Ndio maana taifa lolote linalopuuzia utamaduni wake linajidhalilisha bila kujua,” amesema na kuongeza kuwa, “wenzetu wanaenzi utamaduni wao. Wana ngoma zao za asili na wamekataa kuiga tamaduni za nje hata katika ala za muziki wao zinatokana na asili yao.”
 “Ala zao zinatumia Bamboo (mianzi), hata hapa tunazo kule Iringa, sisi pia tunaweza kuitumia kwa mambo mazuri kama haya badala ya kunywea pombe.”Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante ole Gabriel amesema wizara yake itashirikiana na taasisi, au mtu yoyote mwenye lengo la kukuza uatmaduni wetu.
 “Wizara itatoa ushirikiano kwa kila mtu au taasisi yenye lengo la kukuza utamaduni wetu kwasababu suala la utamaduni ni jukumu letu sote, kuulinda kwa nguvu zetu zote,” amesema.Hafla hiyo pia imehudhuliwa na Balozi wa China nchini Dr. Lu Youqing.
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live


Latest Images