Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

SIKU YA CHANJO DUNIANI YAZINDULIWA ZANZIBAR

$
0
0
  Mratibu wa kitengo cha Chanjo ya Kinamama na Watoto Wizara ya Afya Zanzibar Yussuf Haji Makame, akizungumza na wandishi mbalimbali katika ukumbi wa Wizara hiyo kuhusu Wiki ya Chanjo Afrika 
 Wandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza Mratibu wa Chanjo ya Kinamama na Watoto Wizara ya Afya Zanzibar Yussuf Haji Makame (hayupo pichani) wakati alipokuwa akizungumza kuhusu Wiki ya Chanjo Afrika.

MOSTAFA BRAGGED TO DETHRONG NDOKOSHO BUT, THE CHAMPION WARNED HIM TO BE PREPARED

$
0
0

Egyptian hard puncher and most feared boxer Ibrahim "Butcher" Mostafa has vowed to take the "IBF Africa, Middle East & Persian Gulf (IBF AMEPG) Title" away from the current champion, the flamboyant and stylish boxer Gottlieb Ndokosho of Namibia.

Boxer Mostafa, trained and managed by Richard Nwoba of Luoaa Boxing Promotions, a company incorporated in Cairo, Egypt goes to the forthcoming tournament with a record of 13 wins (KO 6) + lost 4 (KO 2) + drawn 2 = 19 record against 12 wins (KO 3) + lost 3 (KO 1) + drawn 0 = 16 for champion Ndokosho. This is one tournament which is been waited with keen interests by both Namibian and Egyptian boxing stakeholders.

Raised at Giza in the ouskirt of of Cairo the capital city of Egypt, Ibrahim Mostafa's name is a boxing power house in Egyptian boxing fraternity. It is only natural that many Egyptians in their thousands are expected to chart planes from Cairo and Alexandria to watch thetournament slated for June 15, 2013 in Windhoek, Namibia.

The tournament will be promoted by Kinda Boxing Promotions a company with lots of experience and synonymous with professional boxing in Namibia managed by Mr. Kinda Nangolo of Namibia who doubles as the manage/promoter of the current "IBF World Youth Jr. Lightweight Champion" Albinus Felesianu.

This will be the first defense for Ndokosho since winning the title last year by beating Tanzania slugger, Rajabu Maoja in less than one minute in their first round duel. Many boxing fans in Namibia are waiting for this D-Day in June 15, 2013 and fill the venue at SPW Country Club in Windhoek, ready to cheer  their beloved boxer Nokosho to victory.

Watch out this space for more news.

Issues by:
INTRERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA)
DAR ES SALAAM, TANZANIA

evans bukuku's comedy club @ nyumbani lounge

wananchi watakiwa kuwapeleka watoto wao kupata chanjo.

$
0
0

Mratibu wa Chanjo ya Kinamama na Watoto Yussuf  Haji Makame alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichan) kuhusu maadhimisho ya Wiki ya Chanjo kwa upende wa Bara la Afrika yanayoendelea nchini kote..Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
=== =======  =========  ===== 
 Wananchi wametakiwa kuwapeleka Watoto wao kupata Chanjo za kujikinga na magonjwa mbalimbali ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Chanjo Barani Afrika.

Wito huo umetolewa na Mratibu wa Chanjo ya Kinamama na Watoto Yussuf  Haji Makame alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Wiki ya Chanjo kwa upende wa Bara la Afrika yanayoendelea nchini kote.

Amesema Chanjo zinasaidia kuokoa maisha ya Wanadamu na kuwataka wazazi waitumie Wiki hii kuwapeleka Watoto wao ambao hawajapata chanjo na wale waliokuwa hawajamaliza ili kukamilisha Chanjo hiyo.

Amefahamisha kuwa zaidi ya Vifo vya Watu Milioni tatu Duniani kote hukingwa kupitia Chanjo za Magonjwa mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa na Waratibu wa Chanjo hizo Mahospitalini.

Ameongeza kuwa Zanzibar imepiga hatua nzuri katika utoaji wa Chanjo ambapo zoezi la chanjo dhidi ya magonjwa mbali mbali limefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 90.

Aidha amewataka Wazazi kutobweteka na Takwimu hiyo nanakuomba waendelee kutoa ushirikiano kila inapostahiki ili kuwaweka Watoto katika mazingira mazuri ya kuepukana na hatari ya magonjwa.

Ameongeza kuwa katika Wiki hii ya Chanjo Vituo 156 vya kutolea huduma hiyo Unguja na Pemba vitakuwa wazi kwa muda wote wakazi kuanzi saa Moja na nusu hadi Tisa na nusu za jioni.

Aidha amebainisha kuwa kutokana na Wananchi kujua umuhimu wa Chanjo kumepelekea kwa kiasi kikubwa Magonjwa ya Kifaduro, Polio na Donda koo kupungua kwa kiasi kikubwa katika Visiwa vya Unguja na Pemba.

Katika maadhimisho hayo ujumbe wa mwaka huu utakuwa ni Okoa Maisha, Kinga Ulemavu na toa Chanjo.

IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR. NA MAELEZO ZANZIBAR

Gari Linauzwa(Carina Ti)

$
0
0


Aina:Toyota Carina Ti
Rangi: Silver
CC: 1490
Mileage: 80,000kms
Gear Option: Automatic
Price: 9.5Millions Tshs
Contact number: 0758 277 580

Gari imeingia kutoka Japan tarehe 18 April imesajiliwa kwa namba za usajili T220CJS.
Mdau,William.

Taswira mbalimbali kutoka Ifakara wilayani kilombero,Morogoro.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA BALOZI WA FALME ZA KIARABU IKULU DAR LEO

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Balozi wa Falme za Kiarabu, Abdulla Ibrahim Al-Suwidi, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, kwa amazungumzo leo. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Falme za Kiarabu, Abdulla Ibrahim Al-Suwidi, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, kwa amazungumzo leo. Picha na OMR

ABITAT OFFICIALLY LAUNCHED BY THE PRESIDENT OF THE REPUBLIC OF TANZANIA

$
0
0
 The President of the United Republic of Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete in a group photography with ABITAT board members during the official Launch of Alliance of Businessmen and Industrialists of Tanzania and Turkey(ABITAT),  at Hyatt Regency, The Kilimanjaro, Dar Es Salaam.
 The President of the United Republic of Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete officially unveiling ABITAT (Alliance of Businessmen and Industrialists of   Tanzania and Turkey) with the TUSKON President Mr. Rizar Nur Meral(R) -Hyatt Regency, The Kilimanjaro, Dar Es Salaam.

 Some of the guests invited in official launch of ABITAT at Hyatt Regency, The Kilimanjaro, Dar Es Salaam.
=========   =======  =======  =======
ABITAT – ALLIANCE OF BUSINESSMEN AND INDUSTRIALISTS IS NOW OFFICIALLY LAUNCHED
Officiated by His Excellency Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, the President of the United Republic of Tanzania-Hyatt Regency, The Kilimanjaro, Dar Es Salaam.

Dar es Salaam 23rd April 2013:  Through a colorful gala dinner, ABITAT was officially launched on the 19th of April 2013.  The event which was officiated by his Excellency, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete and was also attended by the President of TUSKON, Mr. Rizar Nur Meral.  TUSKON is the umbrella organization of ABITAT thus the latter presenting TUSKON in Tanzania, among other dignitaries.


Speaking at the event, the guest of honor, His Excellency, the president of the united Republic of Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete commended the good work that TUSKON and ABITAT has established in Tanzania.  “Turkey has the expertise and more so technology and Tanzania is well endowed with resources thus making the two countries able to implement the trade co-operation agreement of 2010 with ease”  He added, I wish to also note that Tanzanians  through  ABITAT’s initiative will be getting  the best there is in terms of quality from Turkey.” He also thanked the Turkish Ambassador to Tanzania Mr. Ali Davutoglu for his great work and support to the business communities in the two countries.


The president of TUSKON (confederation and Industrialists of Turkiye) Mr. Rizar Nur Meral thanked the guest of honor and noted that it was through the president visitation to Turkey that opened eyes of many Turkish businessmen and women to invest in Tanzania. 


“Tanzania has lots of potential and especially raw materials for our industries back in Turkey.  The peace that is prevailing in this country too makes its suitable for investors “. He added.


The exciting gala dinner event was attended by high ranking business men and industrialists in Tanzania who are both Tanzania and Turkish nationals.  Others were government officials including the minister of Industry and trade Dr. Abdallah Kigoda and Mr. Said Meck Sadiq the Dar es Salaam regional commissioner.   


ROBO FAINALI PAN-AFRICAN GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE

$
0
0


*NANI KUVISHWA UBINGWA WA PAN-AFRICAN GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ *


       Mashindano makubwa na mazuri ya GUINNESS® FOOTBALL™ CHALLENGE yamekuwa yakiwasisimua na kuwafurahisha watazamaji wake kwa wiki tano zilizopita.Sasa mashindano ya Pan-African yataanza kuoneshwa katika televisheni za ITV  na Clouds TV kuanzia kesho tarehe 24 April, 2013 saa 3:15 ITV na 2:15 Clouds TV. Sasa timu kutoka Cameroon, Ghana, Uganda, Kenya na Tanzania zitakutana uso kwa uso kushindana ili kujua ninani ana maarifa zaidi na ujuzi wa kusakata kabumbu,  hata kuvishwa ubingwa wa Pan-African.

Washiriki kutoka Afrika yote waliowashinda wapinzani zao ili kuwakilisha nchi zao sasa watakutana na timu bora za Pan-African ambazo zina maarifa na ujuzi zaidi. Katika hatua hii ya robo fainali washiriki wanawania kushinda hadi dola za Kimarekeni 250,000.


Kila timu sasa itacheza kuwakilisha nchi yake na kuonesha uwezo wao katika kusakata kabumbu. Washiriki watahitaji kucheza vizuri kwa kiwango cha juu katika mchezo ili kujipa nafasi ya kushinda mashindano haya na kufanya nchi zao kujivunia. Timu nne zitakazo shiriki katika robo fainali ya kipindi cha kwanza ni:       

·         Gregory Doamekpor na Kyei Edmond Nana, wenye umri wa miaka 21 kutoka Accra,Ghana. Hawa walikuwa washindi katika sehemu ya kwanza ya GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE Ghana. Gregory ni mwanafunzi wa Saikolojia na ndiye kichwa cha timu wakati Kyei ni mwanafunzi wa Mahusiano ya jamii, atakuwa anachezea mpira.


·         Timu kutoka Uganda itakuwepo pia, Ibra Kawooya(30) na Alex Muyobo(31),wote mashabiki wa Man.United, Ibra atakuwa kichwa cha timu wakati Alex atacheza uwanjani. ·         Kutoka Cameroon watakuwa Emerand Tchouta(24) na Abdul Salam(25). Emerand atakuwa kichwa cha timu na Abdul ataonesha uwezo wa kusakata kabumbu. Japo walifanikiwa kuondoka na dola 1,500 tu lakini walionesha kiwango kizuri hivyo wana nafasi kubwa ya kushinda. ·         

Timu nyingine kutoka Kenya Francis Ngigi(23) kutoka Nairobi na Kepha Kimani(25) kutoka Thika.Timu hii ilishinda dola 3,000 katika mashindano ya GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE. Francis atakuwa kichwa cha timu wakati Kepha ataonesha kipaji chake cha kucheza soka.

Meneja wa kinywaji cha Guinness, Davis Kambi alisema: “Tumeona timu mbalimbali kutoka mataifa mbalimbali zilishindana kufikia hatua ya robo fainali ya Pan-African- GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE na sasa tunafurahia kuona timu zetu bora katika hatua za mwisho. Kila timu imeiwakilisha vizuri nchi yake na wamefanya vizuri katika mashindano haya kwa kujiamini. Sasa timu zote zina nafasi ya kuthibitisha uwezo wao wa kucheza na si kuangalia tu pale watakapo shindana ili kufikia nusu fainali.Tunasubiri kwa hamu na kuzitakia timu zote kila la heri!”


Robo fainali ya kwanza ya Pan-African itaoneshwa katika televisheni za ITV na Clouds TV  kwa hiyo hakikisha unaangalia na kuishangilia timu ya taifa lako. Wapenzi wa kipindi hiki cha Guiness football challenge barani Afrika wanakumbushwa kwamba nao wanaweza kushiriki kwa kufuatilia kwa karibu.   Wanaweza kufanya hivyo kwa kujisajili  bure kabisa katika tovuti ya m.guinnessvip.com kwa kupitia simu ya mkononi.  

Hakikisha kuufwatilia ukurasa wa facebook wa GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE kwa habari mbalimbali.

-www.facebook.com/guinnesstanzania 

RAIS KIKWETE AKUTANA NA VIONGOZI WA MADHEHEBU MBALIMBALI YA KIKRISTO LEO IKULU

$
0
0
 Juu na chini anaonekana Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini ya Kikristo Ikulu jijini Dar es salaam leo ambapo amekuwa na mazungumzo nao ikiwa ni mojawapo ya jitihada za Rais Kikwete kutafuta muafaka na kutafuta utatuzi wa hali ya sintofahamu ambayo inanyemelea nchi yetu katika kipindi hiki.


 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini ya Kikristo Ikulu jijini Dar es salaam leo
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini ya Kikristo Ikulu jijini Dar es salaam leo. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano) Mhe Steven Wassira.
========   ======  ======

Viongozi wa dini wamewataka waumini kote nchini kulinda amani na  umoja uliopo  ili nchi isije ikaingia kwenye mgawanyiko wa kidini na kuleta machafuko hapa Tanzania.


Wito huo umetolewa na viongozi wa dini leo Ikulu ya Dar-Es-Salaam mara baada ya kikao cha pamoja baina ya viongozi wa dini na Rais Jakaya Kikwete.


Viongozi hao wa dini wamefika leo wakiongozwa na Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa, ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).


Viongozi wengine wametokea Baraza la Kikristo Tanzania (CCT) Seventh Day Advertist (SDA) na Baraza la Pentekoste Tanzania (PCT).


Mkutano huo umeanza kwa Askofu Ngalalekumtwa kusoma tamko lao la pamoja kwa Rais Kikwete ambalo ndilo limetoa muongozo wa mazungumzo hayo ya leo ambayo yamehusu Amani na Usalama wa Taifa na migogoro ya kidini ndani ya jamii.


Mkutano wa viongozi wa dini ya Kikristo Tanzania ni mojawapo ya jitihada za Rais Kikwete kutafuta muafaka na kutafuta utatuzi wa hali ya sintofahamu ambayo inanyemelea nchi yetu katika kipindi hiki.


“Nataka tuzungumze ni namna gani tunaweza kutoka kwenye hali hii na tunakwendaje mbele zaidi na kuhakikisha nchi yetu bado inakua ya  amani na umoja kama ilivyozoeleka” Rais amesema na kutoa nafasi kwa viongozi wa dini kutoa maoni yao.


Viongozi hao wa dini wamemueleza Rais Kikwete kuwa wanaunga mkono jitihada zake za kutafuta amani na kwa pamoja wamekubaliana uandaliwe mkutano wa pamoja baina ya viongozi wa dini zote ambapo masuala ya amani na umoja wa nchi utajadiliwa kwa kirefu.


Katika kikao cha leo pande zote zimekubaliana kuwa kuna changamoto zilizoko sasa zinahitaji kutatuliwa haraka iwezekanavyo ili kuepusha nchi kutumbukia katika mgogoro mkubwa zaidi, na pia kukubaliana kuwa pande zote, kwa maana ya serikali na taasisi za dini, zinawajibu mkubwa wa kuhakikisha amani inadumu.


Kabla ya kikao cha leo , Rais amewahi kukutana na viongozi wa dini ya kiislamu na kikristo mmoja mmoja ambapo alikua akitafuta maoni na ushauri wa pande zote kabla ya pande zote hazijakaa pamoja na kuwa na msimamo wa pamoja.


Kikao cha leo kimehitimisha jitihada hizo na kinachofuata ni mkutano mmoja ambapo Rais Kikwete atakutana na viongozi wa dini zote kwa pamoja hivi karibuni.


Imetolewa na:
Premi Kibanga,

Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,

Ikulu-DSM

23 Aprili, 2013

GRANDMALT EXCELLENT TREE PLANT IRINGA

$
0
0
Msanii wa Mziki wa kizazi kipya nchini Joh Makini akiwapagawisha wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya mkoa wa Iringa kwenye Uzinduzi wa Tamasha la kampeni ya kinywaji cha grandmalt ya kuwashindanisha wanafundi ili kuweza kujinyakulia zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja fedha taslimu ijulikanayo kama Exel with grandmalt, tamasha hilo lilifanyikia katika viwanja vya chuo kikuu Tumaini Mjini Iringa jana.
Wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Tumaini na Ruaha vya Mkoani Iringa wakichuana vikali katika Mpira wa Basketball kwenye Uzinduzi wa Tamasha la kampeni ya kinywaji cha Grandmalt ya kuwashindanisha wanafundi ili kuweza kujinyakulia zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja fedha taslimu ijulikanayo kama Exel with grandmalt, tamasha hilo lilifanyikia katika viwanja vya chuo kikuu Tumaini Mjini Iringa jana. 

Katibu Tawala wa wilaya ya Iringa Elvin Mwakajinga (katikati) akisaidiana kupanda Miti katika Viwanja vya Chuo Kikuu cha Tumaini Iringa, na Meneja wa Kinywaji cha Grandmalt, Consolatha Adam (kushoto) na Meneja Mauzo wa Grandmalt mikoa ya Iringa, Njombe na Songea, Raymond Degela. Upandaji mitio huo ni sehemu kampeni ya kinywaji cha Grandmalt ya kuwashindanisha wanafunzi ili kuweza kujinyakulia zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja fedha taslimu ijulikanayo kama Exel with grandmalt, tamasha hilo lilifanyikia katika viwanja vya chuo kikuu Tumaini Mjini Iringa jana. 

dkt shein kuwawezesha wananchi wake kuwapatia mikopo ili kujikwamua na umasikini.

$
0
0

MAKAMO Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dr Ali Mohamed Shein amesema katika ilani na sera ya Chama cha Mapinduzi imeziagiza  kuwajengea mazingira bora wananchi wake kwa kuwawezesha kuwapatia mikopo hatua kwa hatua ili kuweza kujikwamua na umasikini.

  Amesema kuwawezesha vijana kwa kuwajengea uwezo kutasaidia kuondokana na ukali wa maisha na upungufu wa ajira jambo ambalo ni changamoto kubwa inainayoikabili Taifa hivi sasa.

 Dr. Shein ameyaeleza hayo huo Amani mjini Unguja  wakati akizungumza na wana ccm baada ya kumaliza ziara yake kichama katika Wilaya ya Mjini.

Amesema katika kupambana na hali hiyo  serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia wizara yake ya Kazi Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika imekuwa ikitoa mikopo nafuu kwa vijana ili waweze kujiajiri na kujiongezea kipato.

Katika mkutano huo Makamo  Mwenyekiti  amewataka vijana kuijua na kuisoma historia ya nchi yao sambamba na kuwataka wazee wa CCM kukumbuka taratibu, maadili na mwelekeo wa chama kwani mafunzo ya itikadi ni muhimu  kwa kuongeza maarifa.

Hata hivyo alieleza kuwa mafunzo hayo yanawasaidia vijana kuweza kujua katiba, kanuni na maadili ya chama ambayo yatasaidia kuimarisha na kukiendeleza Chama cha Mapinduzi.

Aidha amewataka viongozi wa chama hicho kuepuka kutumia vyeo kwa maslahi yao binafsi na kuamini kwamba cheo ni dhamana  na  ni jukumu la kuwatumikia wananchi.

“Chama chetu kina maadili na kinafuata katiba ya nchi hivyo tukifuate kwa kuzingatia katiba inavyoeleza”, alieleza Dr Shein.

Akizungumzia Muungano Dr. Shein amesema kuwa sera za msingi katika chama cha  Mapinduzi ni mfumo wa serikali mbili hivyo wanachama wana wajibu wa kuitetea  na kuinga mkono.

Aidha ameeleza kuwa serkali ya Umoja ya kitaifa imeundwa kutokana na kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi na kufuata katiba  kwa azma ya kuleta maendeleo katika nchi hivyo ni lazima kuendeleza na kuyafahamu maendeleo hayo.

 Katika ziara yake makamo mwenyeti alitembelea CCM wilaya na kuweka jiwe la msingi katika skuli ya maandali ya Amani wazazi na baadae kukabidhi kadi kwa wanachama wapya na vitendea kazi kwa wajasiri amali pamoja na kukabidhi vitabu na kufungua madarasa ya itikadi katika tawi la CCM Meya.

 Na Miza Kona –Maelezo  Zanzibar  

ZIFF announces workshops for this year

Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa akutana na Waziri wa Ushirika wa Kimataifa wa Canada Mhe. Julian Fantino kujadili vipaumbele vya maendeleo ambavyo ni Elimu, Nishati, Rasilimali Fedha, Kilimo, Maji na Usafirishaj

$
0
0
 Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa akisalimiana na Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa nchini Canada Bw. Julian kabla ya kikao kuanza Fantino
 Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa akisisitiza jambo kwa Waziri wa ushirikiano wa Kimataifa Bw. Julian Fantino mara baada ya kikao kumalizika.
 Kamishna wa Fedha za Nje Zanzibar Bi. Bihindi Nassor akisalimiana na Waziri wa ushirikiano wa Kimataifa nchini Canada Mhe. Julian Fantino.
 Waziri wa ushirikiano wa Kimataifa nchini Canada Mhe. Julian Fantino aliyesimama, akisoma hotuba yake mbele ya ujumbe wa Tanzania. Aliyekaa kushoto kwake ni Bi Margaret Biggs ambaye ni Rais wa shirika la maendeleo la kimataifa (CIDA).
 Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa akimtambulisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Zanzibar, Bw. Khamis Mussa.
 Waziri wa ushirikiano wa Kimataifa nchini Canada Mhe. Julian Fantino akisikiliza kwa makini ujumbe wa Tanzania kuhusu masuala ya Nishati, Elimu, Maji, Usafirishaji, Rasilimali Fedha na Kilimo.
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt Wiliam Mgimwa pamoja na ujumbe wa Tanzania katika majadiliano ya pamoja na  Mhe. Julian Fantino ambaye ni Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa wa katikati mbele.  Aliyekaa kushoto kwake ni Bi. Margaret Biggs ambaye ni Rais wa Taasisi ya maendeleo ya  kimaifa(CIDA).

MAGIGE FOUNDATION YATOA MSAADA DODOMA

$
0
0

Mama Tunu Pinda akihutubia
 Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akihutubia katika hafla hiyo.

Asasi ya Kijamii ya Catherine Foundation jana imetembelea kituo  cha kulelea wa watoto cha Matumaini Village kilichopo mkoani Dodoma ambapo walikwenda kutoa misaada mbalimbali wakiongozwa na Mkurugenzi wa Asasi hiyo, Catherine Magige. 
 Katika Hafla hiyo Mgeni Rasmi alikuwa Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda ambapo asasi hiyo ilitoa vitu mbalimbali vikiwemo, Madaftari, Mafuta, Sabuni, Juice, miswaki na dawa zake, mchele, sukari, nguo za watoto, kanga za wakinadada wanaowalea watoto hao na vingine vingi
 Mkurugenzi wa Catherine Foundation, Mhe Catherine Magige akihutubia katika hafla hiyo
 Mkurugenzi wa Catherine Foundation, Catherine Magige akizungumza na watoto wanaolelewa kwenye Kito cha Matumaini Village kilichopo Dodoma alipokwenda kutoa msaada 
Mhe Catherine Magige akicheza na mmoja wa watoto wa kituo hicho
 Mkurugenzi wa Catherine Foundation, Mhe Catherine Magige akiwa na mtoto mchanga anaye lelewa katika Kituo cha Matumaini Village mjini Dodoma jana.
 Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda na Mkurugenzi wa Catherine Foundation, Mhe Catherine Magige wakizungumza na watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho.
Mama Tunu Pinda na Mhe Catherine Magige wakiwa na watoto hao
 Mama Tunu Pinda akikabidhi zawadi mbalimbali zilizotolewa na asasi hiyo 
Misaada mbalimbali ikitolewa
Mkurugenzi wa Catherine Foundation, Catherine Magige akizungumza na watoto wanaolelewa kwenye Kito cha Matumaini Village kilichopo Dodoma alipokwenda kutoa msaada 

UNIC Dar yawahamasisha wanafunzi kujijengea utamaduni wa kusoma vitabu.

$
0
0

Katika maadhimisho ya siku ya siku ya uandishi wa Vitabu na Hati Miliki Duniani Afisa Habari wa Kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa (katika ngazi ya Kimataifa) UNIC Bi. Stella Vuzo akizungumza na wanafunzi wa shule mbalimbali waliohudhuria semina fupi iliyoandaliwa na UNIC na kuwafafanulia umuhimu wa kusoma vitabu mbalimbali ambapo wanaweza kujifunza mambo tofauti ikiwemo kujua takwimu za ugonjwa hatari wa Malaria hapa nchini ambao umekuwa ukiongoza kwa kusababisha vifo vya watoto wenye umri chiniya miaka 5, hivyo kwa usomaji vitabu wanaweza kujua namna ya kujikinga na wanapogundua dalili kuweza kuwahi kupata matibabu.
Wanafunzi wa darasa la Saba shule ya msingi Oysterbay wakimsikiliza kwa makini Afisa Habari wa UNIC (katika ngazi ya Kimataifa) Bi. Stella Vuzo (hayupo pichani) wakati akielezea kazi zinazofanywa na Shirika la Afya Duniani WHO lililochini ya Umoja wa Mataifa katika kuhakikisha Ugonjwa wa Malaria unatokomezwa duniani katika nchini za kusini mwa Jangwa la Sahara. Ikiwa zimebaki siku mbili kuadhimisha siku ya Malaria duniani inayodhimishwa kila mwaka Aprili 25 wakati wa siku ya kuadhimisha siku ya uandishi wa vitabu na hati miliki duniani.
Msaidizi wa Maktaba ya UNIC Harriet Macha akiendesha chemsha bongo kwa wanafunzi walioshiriki semina hiyo kupima uelewa wao kuhusiana na Ugonjwa wa Malaria.
Picha juu na chini ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Usomaji na Maendeleo Bi. Demere Kitunga ambaye ni mmiliki wa Book Cafe iliyopo maeneo ya Mikocheni jijini Dar akiwaelezea wanafunzi umuhimu wa kuwa na nia na dhamira ya kujenga utamaduni wa kujisomea vitabu vya nyanja mbali mbali ikiwemo vya Kiada, Ziada na vya maarifa ambapo amewapa changamoto kujianzisha Maktaba binafsi na vikundi ambapo wanaweza kuchangishana fedha kidogo kwa uwezo wao ili kuweza kujinunulia kitabu ambacho wanaweza kushirikiana kusoma ambavyo vitawapa uwezo wa kujitambua, kuwa na maamuzi, kupata uelewa wa vitu tofauti vinavyoweza kuwajengea kujiamini na kuwawezesha kubadilisha mfumo wa maisha katika makuzi yao.
Katibu Mkuu wa Mtandao wa Vilabu vya Umoja wa mataifa Tanzania (UNCTN) Bernadetha Mshana akionyesha moja ya kitabu kilichomsaidia kuweza kupata uelewa wa kuongea Kingereza kwa urahisi zaidi ikiwa ni ushuhuda wake kwa vijana wenzake kuwa usomaji vitabu hupanua uelewa wa mtu na kujua mambo mengi.
Msaidizi wa Maktaba ya UNIC Harriet Macha (wa pili kulia) akiwa na baadhi ya walimu waliombatana na wanafunzi kutoka shule za msingi Kumbukumbu, Oysterbay na Hananasif.
Katibu Mkuu wa Mtandao wa Vilabu vya Umoja wa mataifa Tanzania Bernadetha Mshana akishirikiana uzoefu na wanafunzi wa shule za msingi za jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya siku ya usomaji vitabu duniani na Hati miliki ambapo amesema ambapo amewataka wanafunzi hao kujiunga na vilabu vya usomaji vitabu ambavyo vitawapatia uzoefu kama ambavyo yeye vimemwezesha kujiamini kuwa na uelewa na kufikia hapo alipo sasa.
Afisa habari wa UNIC katika ngazi ya Taifa Usia Nkhoma akitoa neno la shukrani kwa wanafunzi walioshiriki semina fupi iliyoandaliwa na kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIC katika maadhimisho ya siku ya uandishi wa Vitabu na Hati Miliki Duniani. Siku hii imetengwa rasmi ili kuhamasisha usomaji, auandishi na uchapishaji wa vitabu kupitia hati miliki.
Katibu Mkuu wa Mtandao wa Vilabu vya Umoja wa mataifa Tanzania Bernadetha Mshana (kushoto) akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa Book Cafe iliyopo Mikocheni jijini Dar.
Baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi wakisoma vitabu mbalimbali vinavyopatikana katika Maktaba ya Book Cafe yenye mandhari nzuri ya kujisomea ambapo pia panapatikana viytabu vya watu wazima vinavyohusiana na nyanja mbalimbali.

picha mbalimbali za matukio bungeni.

$
0
0
 
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda,(kulia)akidilishana mawazo na Mkurugenzi wa Kampuni za Msama,Alex Msama aliesimama kushoto,walipokutana nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dododma,katikati ni John Shibuda Mbunge wa Maswa Mashariki (CHADEMA). 
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda,akipewa pole kwa kazi na Mkurugenzi wa Kampuni za Msama,Alex Msama, walipokutana kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma, mara baadaya kuahirishwa kikao cha kujadili bajeti ya Wizara ya kilimo na Ushirika . 

 Mbunge wa Simanjilo (CCM)Ole Sendeka,mwenye suti(kulia)akipeana mkono wa salamu na Naibu Meya wa Jiji la Mbeya,Fungo Mwambe,nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma,katikati ni Dk,Mary Mwanjelwa,Mbunge wa Viti maalum,(CCM) wegine ni Madiwani wa Jiji la Mbeya,waliotembelea Dodoma ili kujionea vikao vya bunge la bajeti vinavyoendelea Bungeni mjini Dodoma.
 Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM)Nimrod Mkono,(kushoto)akitafakari hoja mbali mbali za kikao cha bajeti ya wizara ya Kilimo na Ushirika,sambamba na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion,Alex Msama walipokutana kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma,mara baadaya kuahirishwa kwa kikao cha kujadili bajeti ya kilimo kwa mwaka wa 2013..2014.

 Wabunge wa Viti maalum (CCM)rI Ritha Kabati,(kushoto)na Dk,Mary Mwanjelwa(kulia)wakifurahia pamoja na Madiwani wa Jiji la Mbeya nje ya ukumbi wa bunge, waliowatembelea Bungeni mjini Dodoma kujionea vikao vya bunge la bajeti vinavyoendelea mjini Dodoma.
.Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa,Shamsi Vuai Nahodha,(kushoto)akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Alex Msama,walipokutana nje ya ukumbi wa bunge mjini Dodoma,mara baadya kuahirishwa kwa kikao cha kujadili hotuba ya bajeti ya wizara ya kilimo na ushrika,katikati ni Mbunge wa Igalula,(CCM)Dk,Athumani  Mfutakamba..

Huawei showcases convergent communication solutions in Dar es Salaam

$
0
0


Huawei’s Technologies Tanzania Product Manager Zeng Tao (left) briefs the Ministry of Communication Science and Technology, Assistant Director Manyiri Isack (right) on one of Huawei’s new products during the road show event held at Kilimanjaro Hotel in Dar es Salaam yesterday. (Photo by our correspondent)  
========  =======  ========
Huawei showcases convergent communication solutions in Dar es Salaam


By Our Correspondent

HUAWEI, a leading global information and communications technology (ICT) solution provider yesterday held a one day road show in Dar es Salaam geared towards showcasing the company’s various products.

The company during the event exhibited its unique omnipresent connectivity technology, including Smart Fixed-Mobile Convergence (FMC) bearer network and the SIngleFAN solutions, eSpace IVS (intelligent video surveillance ) and Video conference Solution, Huawei Storage and Server Portfolio, Huawei Distribute Cloud Data Center Solution, Huawei Container and Modular Data Center(IDS) Solution and Huawei Virtual Desktop Infrastructure(VDI) Solution among others.

Speaking during the event graced by the Assistant Director, Manyiri Isack from the Ministry of Communication, Science and Technology, the Huawei’s Technologies Tanzania Channel Director Mr. Moses Hella said the rapid development of mobile technologies has accelerated mobile broadband from megabit to gigabit levels via the generation of various service applications.

“Mobile broadband has redefined the way we communicate and live. With new and innovative business models emerging, mobile broadband presents the telecom industry with significant challenges and opportunities,” he said.

Mr Hella said Huawei has developed the value growth solution that will see local operators benefiting significantly from Mobile Broadband (MBB) and its offerings.

He reiterated that Huawei will continue with the road shows the whole week. Road shows will also be conducted at the Airtel Tanzania, Tigo and Vodacom offices.  

He underscored his company’s commitment in supporting growth of Tanzania’s ICT sector urging that ICT is an enabler of technology innovation, driving social and economic development, and creating value for individuals and society as a whole.

“We have seen companies in the telecom industry striving to bridge the digital divide - so everyone can afford to enjoy the benefits of communications. Some have moved farther to shift their focus from ‘a phone for everyone’ to ‘broadband for everyone’, to enable users to tap the infinite possibilities that a connected world presents,” he said.

On his part, the Assistant Director from the Ministry of Communication, Science and Technology, Mr Manyiri Isack said the development of ICT sector in the country will enable easy and effective communication among people.

“We thank Huawei for supporting our government especially in the ICT sector in making sure our people have better and effective ways of communication. We believe that the introduction of these new technologies will help people have easy access to information and have more open communication,” said Isack.

The road show apart from attracting Dar es Salaam residents, targeted telecom service providers that included Tigo, Airtel Tanzania, and Vodacom Tanzania.

Ujumbe wa Tanzania katika chakula cha pamoja na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania – Washington DC katika ofisi za ubalozi

$
0
0



Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Fedha Bi. Ingiahedi Mduma, Mdau wa Ubalozini Bw. Baraka Daudi na Afisa Mawasiliano wa Wizara ya Fedha Bi. Eva Valerian wakitabasamu mara baada ya chakula cha pamoja katika ofisi za ubalozi wa Tanzania Washington DC.


Baadhi ya viongozi wa Tanzania waliohudhuria mikutano ya majira ya kipupwe katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa ubalozi wa Tanzania Washington DC. Waliokaa, kutoka kushoto ni Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Harry Kitilya, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu, Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa Kaimu Balozi wa Tanzania Washington DC Bibi. Lily Munanka na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Bi. Natu Mwamba.


Ujumbe wa Tanzania katika picha ya pamoja na Kaimu Balozi wa Tanzania Washington DC aliyevaa blauzi nyekundu Bibi. Lily Munanka baada ya chakula cha pamoja.   

Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Fedha Bi. Ingiahedi Mduma, Mchumi Mwandamizi wa Mkakati wa kupunguza umasikini Afrika Bw. Yutaka Yoshino pamoja na mchumi wa Wizara ya Fedha Bw. Patrick Pima wakibadilishana mawazo wakati wa chakula hicho.


Kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dr. Silvacius Likwelile, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Burundi na Uganda Bw. Philippe Dongier pamoja na Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa  pia Gavana wa Banki kuu alikuwepo mwisho kulia.


Kutoka kushoto ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Bi. Natu Mwamba, Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Harry Kitilya pamoja na Katibu wa Waziri wa Fedha Bw. Omary Khama wakati wa chakula cha pamoja.


Ujumbe wa Tanzania katika chakula cha pamoja. Kutoka kushoto ni Afisa Mawasiliano Ubalozi wa Tanzania-Washington DC Bi Mindi Kasiga, Afisa Itifaki Wizara ya Fedha Bw. Cyprian Kuyava, Naibu Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Prof. Longinus Rutasitara, watatu wanaofuata ni wachumi wa Wizara ya Fedha Bw. Erasto, Patric Pima, Veronica Maina na mchumi wa Benki Kuu ya Tanzania Dkt. Dickson Lema.

BALOZI WA UINGEREZA NCHINI AMTEMBELEA WAZIRI WA MUUNGANO OFISNI KWAKE LEO.

$
0
0
Wazii wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Samia Suluhu, akizungumza na Balozi wa Uingereza Nchni Tanzania, Diana Melrose, wakati alipofika Ofisini kwa Waziri Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam, leo Aprili 24, 2013 kwa mazungumzo. Picha na Ali Meja
========  ========= ========
Balozi wa Uingerereza nchini Bibi Diana Melrose amemtembelea ofisini kwake Waziri wa Nchi ofisi ya Mkamu wa Rais – Muungano Mheshimiwa Samia Suluhu. Dhumuni la ziara yake  ni kujadiliana na Waziri mambo mbalimbali yanayohusu muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Aidha, Balozi Melrose alipenda kufahamu zaidi kuhusu, maoni ya waziri juu ya Muungano wa iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar na pia changamoto zitokanazo na muungano huo. Mh. Suluhu alisema kwa upande wake anaona ni bora kuendelea na muungano kuliko kuuvunja.  Ila akashauri mabadiliko yafanyike ili kuuboresha, sababu zipo sehemu mbalimbali zinazohitaji mabadiliko. 

Pia alisema yapo makundi yenye  ushawishi mkubwa katika jamii hivyo hutumia nafasi waliyonayo  kuwashwishi  wananchi  kuwa muungano uvunjike sababu hauna  maana.  Alitoa mfano wa baadhi ya makundi hayo ni wanasiasa na viongozi wa dini sababu wao wanao ushawishi mkubwa katika jamii.

Akijibu swali la Balozi Melrose ambaye alitaka  kujua kwamba inasemekana watu wa Zanzibar hawana furaha sababu ya muungano hivyo ndo maana wanashauri uvunjwe, Waziri Suluhu alisema kuwa kweli wapo watu wanasema hivyo lakini yeye anafikiri ni ubinafsi  tu. Aliongeza kuwa,yeye anchoona cha msingi ni kuwafanya watu wa pande zote mbili kuelewana na kuishi maisha bora.

Mwisho Balozi Melrose alitaka kujua changamoto anazokutana nazo Waziri katika nafasi aliyonayo. Mheshimiwa Samia alizitaja baadhi ya changamoto ni kukosa rasilimali za kuwezesha kuwafikia watu hata sehemu za vijijini na kuwaelewesha juu ya dhana nzima ya muungano. Sababu wengi wao hawaelewi. Hivyo alimuomba Balozi kuongea na wafadhili wengine ili wawapatie rasilimali za kufanikisha lengo hilo. 

Monica Sapanjo- Afisa Habari Ofisi ya Mkamu wa Rais.
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images