Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 5 | 6 | (Page 7) | 8 | 9 | .... | 1898 | newer

  0 0


  Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar            

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohammed Shein ametowa wito wa Taasisi za Serikali na Taasisi Binafsi kukitumia Chuo cha Utawala wa Umma ili kuwajengea uwezo wafanyakazi wao kwa manufaa ya Taifa. 

  Amesema kuwa Chuo hicho kitaweza kuwajengea uwezo ujuzi ubunifu uwandilifu na kuweza kuwa watumishi bora wa taifa na jamii kwa ujumla .

  Hayo aliyasema leo huko  Tunguu Mkoa wa kusini Unguja  wakati alipokuwa akifungua Jengo Jipya la Chuo cha Utawala wa Umma  ikiwa ni miongoni mwa  shamra shamra  za sherehe ya miaka 49 ya  Mapinduzi ya Zanzibar .

  Amesema kuwa madhumuni makubwa  yakujenga vyuo  hivyo ni kuleta mabadiliko yenye lengo la kupata ustawi bora wa maisha kwa Wazanzibar  na kuwa na wafanyakazi wenye taaluma inayostahiki .

  Pia  amesema kuwa chuo hicho kitaweza kutowa wanafunzi waliobora wenye misingi imara ya utawala bora na kuweza kujua haki na majukumu ya kazi zao. 
    
  Aidha Dkt Shein ameuomba uwongozi kujitahidi kuwa na wakufunzi ambao wataofundisha katika chuo hicho kuwa na sifa zinazokubalika ili chuo hicho kiweze kutoa wanafunzi bora .

  Halikadhalika aliutaka uwongozi  kuwajengea mazingira mazuri wakufunzi wa chuo hicho ili wasiweze kuvunjika nguvu katika utendaji wa kazi zao .

  Jumla ya shilling bilioni 1milioni mia moja na saba tayari zimeshatumika  mpaka sasa  kwa ajili ya Ujenzi huo na hivi sasa zinahitajika shilingi milioni elfu 3 kuweza kuinua Jengo hilo kuwa la ghorofa moja.

  Jengo la chuo hicho linatarajiwa kuwa na sehemu nyengine mbali mbali  zikiwemo za kuegesha magari,mkahawa,  mabweni  na uwanja wa michezo .

  0 0


  TIMU ya Kijitonyama Veterans, kesho (Jumapili) itacheza mchezo maalum dhidi ya timu inayoundwa na wanamuziki wa bendi ya African Stars ‘ Twanga Pepeta’ kwenye uwanja wa Leaders Club.
  Nahodha wa Twanga FC, Kalala Junior alisema kuwa mchezo huo ni maalum kwa wachezaji wake na mashabiki wa bendi hiyo  baada ya kukaribisha mwaka 2013 kwa  kishindo. Kalala alisema kuwa awali mchezo huo ulipangwa kuanza saa 4.00 asubuhi, waliamua kubadili muda kutokana na majukumu yao ya kazi na sasa utaanza saa 6.00 mchana.
  Alisema kuwa wamechagua kucheza na timu ya Kijitonyama Veterans kutokana na umakini na heshima ya timu hiyo ambao pia inaundwa na wachezaji ambao ni wadau wakubwa wa bendi yao.
  “Tumejiandaa vizuri na tunatarajia kuwa na mchezo mzuri, wachezaji na morali ya hali ya juu na lengo lao ni kufungua mwaka kwa kishindo,” alisema Kalala. Mratibu wa timu ya Kijitonyama Veterans, Majuto Omary alisema kuwa wanatarajia mchezo mzuri ambao ndiyo utawakutanisha kwa mara ya kwanza na timu hiyo ya Twanga FC.
  Majuto alisema kuwa wachezaji wake wamefurahi kupata fursa hiyo na wameahidi kuibuka na ushindi mnono. “Tunajua kuwa Twanga FC inaundwa na wachezaji wazuri, tumejiandaa vizuri pia, hivyo mashabiki watarajie mchezo mzuri na wenye upinzani mkubwa, ustaharabu utakuwa wa hali ya juu kwani baada ya hapo, Twanga FC watakuwa na jukumu la kutuburudisha jukwaani,” alisema Majuto.
  Mkurugenzi wa bendi ya Twanga Pepeta, Asha Baraka amewataka wachezaji wake na mashabiki kufika kwa wingi kuona vipaji vya soka vya wanamuziki wake na hasa baada ya kuanza mwaka kwa vishindo kwa upande wa burudani. Asha alisema kuwa baada ya mechi hiyo, bendi yake itafanya shoo kali ili kuwapa zawadi ya mwaka mpya kwa mashabiki wa Leaders Club.

  0 0


  Na Habari Maelezo Zanzibar .
  5/1/2013
   
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Mwinyihaji Makame Mwadini ameishukuru Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo JICA kwa kusaidia Maji safi na salama katika Visiwa vya Unguja na Pemba..
   
  Amesema Serikali imefarajika kuona Vijiji mbali  mbali vya Unguja  na Pemba vinafaidika na Miradi hiyo chini ya ufadhili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kushirikiana na Japan.
   
   Akizinduwa Mradi wa Maji Safi na Salama huko Fumba Dkt Mwinyihaji amewataka Wananchi hao kuendelea kushirikiana katika utekelezaj iwa Miradi ya Maendeleo ili kutekeleza kwa vitendo malengo ya Mapinduzi ya Zanzibar. ya mwaka 1964.
   
  Amesema ushirikiano waliouonesha katika  utekelezaji wa Mradi huo ni wakupigiwa mfano,hivyo hakuna sababu yakubaguwana katika Miradi ianayo waletea tija  ikiwemo ya Afya,Elimu na ya kiuchumi.
   
  Mradi wa Maji Safi na Salama wa Fumba umeanza utekelezaji wake mwaka 2009 na umegharimu kiasi cha shillini millioni Mia Moja  na 29 zilizotolewa na Serikali ya Mapinduzi  Zanzibar na Serikali ya Japan
   

  0 0

  BENDI YA MAPACHA WATATU.(WAKALI WA TOWN) 
  WANASHUKA NA ONESHO KABAMBEE LA FUNGUA MWAKA, NDANI YA  NEW MSASANI CLUB. IJUMAA HII YA TAREHE 11 MWEZI HUU JANUARI ,WAKISINDIKIZWA NA NYOTA WAZIRI NAKUNDI ZIMA LA MASHAUZI CLASSIC WATAKAOONGOZWA NA  ISHA MASHAUZI.

  HAKIKA SI YAKUKOSA NI KWA KIINGILIO CHA ALFU 5,000 TU MLANGONI NA 15,000 KWA WATAOPENDA KAA VIP NA KUTRITIWA KVIP
  KUBOOK MEZA YAKO PIGA NAMBA 
  0713 701051, 0767 701051, 0786 701051 
  ....ULETEWE TIKETI
  meza chacheee
  2013 NI MWENDO WA BENDI....TUUENZI MUZIKI WETU... NJOO TUANZE NA
   MAPACHA WATATU.....WAKALI WA TOWN!!

  0 0

    Jengo jipya la kituo cha kukusanyia matangazo ya Vituo vya matangazo ya Dijitali  ambalo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein anatarajia kulifungua rasmi Januari 8 ikiwa ni shamra shamra ya sherehe za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar

  Jengo la Studio ya kurikodia Sana na Muziki lililopo Rahaleo mjini Zanz.ibar ambalo Januari 8 asubuhi litafunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barzaza la Mpinduzi Dkt Ali Mohamed Shein ikiwa ni shamra shamra ya sherehe za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.Picha Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

  0 0


  0 0


   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein wa katikati waliokaa katika picha ya pamoja na Maofisa mbali mbali katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa E-Government ikiwa ni shamra shamra za miaka 49 ya Mapinduzi.Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar
   Afisa Usalama wa Mradi wa E-Governmet Ali Mohamed Khitu akimfahamisha Rais Shein mchoro unaoonesha jinsi Waya wa Mradi huo ulivyosambazwa katika Visiwa vya Unguja na Pemba na kuwawezesha kugundua uharibifu popote pale utakapotokea. 
   Balozi  wa Watu wa China nchini Tanzania Lu Youqing akimkabidhi zawadi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa E-Government ikiwa ni shamra shamra za miaka 49 ya Mapinduzi. 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akitoa hotuba yake ya uzinduzi wa mradi wa E-Government Mazizini nje kidogo ya mji wa Zanzibar ikiwa ni shamra shamra za miaka 49 ya Mapinduzi
  =======  =======  ======  =====

  Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
                            
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed amesema Uzinduzi wa Mradi wa Serikali Mtandao E-Government umefungua ukurasa mpya katika uendeshaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na utekelezwaji wake utaakisi lengo kuu la Mapinduzi ya Zanzibar la kuwakomboa Wananchi kimawazo na kiuchumi.

  Rais Shein ameyasema hayo katika hotuba yake ya uzinduzi wa Mradi huo iliyofanyika Mazizini nje kidogo ya mji wa Zanzibar ikiwa ni shamra shamra za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar

  Amesema lengo la Mradi wa E-Government ni kuiwezesha Serikali kuendesha shughuli zake kwa njia za kitaalamu zaidi na kuhakikisha kuwa kila mwananchi popote alipo anapata huduma au taarifa muhimu zinazotolewa na Serikali kupitia mitandao mbalimbali itakayokuwa karibu naye.

  Ameongeza kuwa Mradi huo utaisaidia sana Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kufanya kazi zake kwa ufanisi mkubwa na kwa haraka katika kukabiliana na kasi ya mabadiliko ya kilimwengu kama yanavyoshamiri siku hadi siku duniani.

  “Ni jambo la fahari sana kuwa leo hii Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inajiunga rasmi na nchi zingine duniani katika mfumo mpya wa uendeshaji wa shughuli za kiserikali ujulikanao kama E-Government” alisema Shein.

  Ameongeza kuwa Mradi huo pia utakuwa ni kichocheo muhimu katika kuendeleza dhamira ya Serikali ya kukuza matumizi ya Teknologia ya habari na Mawasilino nchini.


  Amezitaja baadhi ya faida za Serikali Mtandao kuwa ni pamoja na kukuza Elimu katika Skuli za Msingi na Sekondari kwa kupitia Mradi wa T21, ili kukabiliana na mabadiliko yanayoikumba sekta ya habari na mawasiliano.

  Aidha Dkt. Shein amefahamisha kuwa Mradi huo pia unaweza kuipunguzia gharama Serikali ya kusafirisha wagonjwa nje ya nchi kwa matibabu ambapo Madaktari wa ndani wanaweza kuunganishwa na madaktaari waliopo nje ya nchi na kuweza kusaidiana kuwafanyia Operesheni wagonjwa waliopo Zanzibar.

  Dkt Shein pia amefahamisha kuwa Mradi huo utatoa fursa nzuri kwa wafanyabiashara na wawekezaji nchini katika kundesha biashara zao ikiwa ni pamoja na kujtangaza,kutafuta masoko na kutoa huduma bora kwa wateja wao.

  Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais utumishi wa Umma na Utawala Bora Haji Omar Kheri amesema Taasisi za Kiserikali zitaunganishwa katika utendaji na uendeshaji wa shughuli zao kwa njia za uhakika,salama na kwa uharaka.

  Aidha amewataka wananchi kuiheshimu miundombinu ya mradi huo ili uweze kuwa endelevu kwa manaufaa ya wananchi wote. Akitoa salam zake Balozi wa Watu wa China nchini Tanzania Lu Youqing ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mashirikiano ambayo imekuwa ikitoa kwa nchi ya China katika kuendeleza mahusiano ya nchi husika.

  Aidha ameahidi kuzidisha mashirikiano na Zanzibar katika kusaidia wananchi wake kukabiliana na changamoto za maisha hasa katika sekta ya uchumi,elimu na Afya.

  Mradi wa Serikali mtandao E-Government ambao umezinduliwa ikiwa ni shamra shamra za Sherehe za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar umeigharimu Dola Milion 19 za kimarekani ambazo ni Mkopo nafuu kutoka nchi ya China.

  IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR

  0 0


  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitumia laptop yake kuwaonyesha viongozi mbali mbali wa Mkoa wa Singida wakati alipokuwa akiwaelezea masuala muhimu ya maendeleo nchini.Rais Kikwete amewasili Mjini Singida Januari 5 kwa Ziara ya kikazi ya Siku Mbili.Picha na IKULU.

  0 0

   Kipa wa timu ya Kijitonyama Veterans, Abdallah Omary (kulia) akiokoa moja ya hatari iliyoelekezwa langoni kwake, wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa leo kwenye uwanja wa Leaders Club Kinondoni, ikiwa ni badala ya mchezo kati ya Twanga Pepeta Fc na Kijitonyama, baada ya Twanga Pepeta kuingia mitini bila kutokea uwanjani hapo, leo.
   Kipute hicho kikiendelea...
   Mapacha Frki, Hamza na Kondo wakipozi kwa picha.
  Kiungo mchezeshaji wa Kijitonyama Veterans, Isihaka Mussa, akiambaa na mpira wakati mchezo huo.

  ******************

  Na www.sufianimafoto.blogspot.com

  TIMU inayoundwa na wanamuziki wa bendi ya African Stars' Wana Twanga Pepeta' imeingia mitini kucheza mchezo  
  maalum wa kirafiki dhidi ya timu ya Kijitonyama Veterans uliopangwa kufanyika Jumapili asubuhi kwenye uwanja wa 

  Leaders Club. 

  Timu ya Kijitonyama Veterans ilifika uwanjani tayari kwa mchezo huo, hata hivyo wanamuziki wa Twanga Pepeta  

  hawakuonekana uwanjani mpaka saa 7.15 mchana huku mashabiki kibao pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, 
  Mheshimiwa, Idd Azzan wakikosa burudani ambayo iliwatoa majumbani mwao ikikosekana.


  Nahodha wa timu ya Twanga FC, Kalala Junior hakupokea simu yake pamoja na juhudi za kumtafuta  huku meneja wa  

  timu hiyo, Hassan 'Njoo Kesho' akisema kuwa hata yeye ameshindwa kumpata Kalala ili kujua hatma ya mchezo huo.


  "Mimi nimefika hapa kwa ajili ya kuona mechi hiyo, jana (Jumamosi) wanamuziki walitangaziana, hata hivyo sijui kwa  

  nini, labda baada ya shoo ya jana (Jumamosi) iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mango Garden na kuwafanya wachoke  
  zaidi," alisema Hassan.


  kutokana na hamu mashabiki kupata burudani ya mechi hiyo, mratibu wa timu ya Kijitonyama Veterans, Majuto  

  Omary aliwaomba wachezaji wanaocheza mechinza bonanza la kila siku ya Jumapili kuunda kombaini ili kucheza na  
  Kijitonyama Veterans.


  Ombi hilo lilikubaliwa na wachezaji hao ili kufanikisha kiu ya wachezaji Kijitonyama Veterans na mashabiki wa soka 

  ambao na mechi hiyo kufanyika. 

  Katika mchezo huo, Kijitonyama Veterans iliifunga Kombaini ya Leaders kwa mabao 2-0. Mabao ya Kijitonyama  

  Veterans yalifungwa na Salim Sariko baada ya pasi safi ya Kiki De Kiki huku la pili likifungwa na Dastan Lwoga 

  kufuatia pasi safi ya Brian Makundi.

  Wakati huo huo; katika mechi za bonanza za Leaders Club, timu ya Mango Garden iliiichapa timu ya Namaga kwa  

  mabao 3-1 huku Leaders ikiichapa Brake Point kwa mabao 3-1 vile vile. michezo hiyo ilianza saa 4.00 asubuhi na 

  mwingine ukianza saa 5.00 asubuhi.


  0 0  Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Sazi Salula akizungumza na Mkurugenzi wa Baraza la hifadhi na Usimamizi wa Mazingira {NEMC] Eng Benventure Baya na Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makmu wa Rais Dk Julias Ningu na Ofisa Mwandamizi Bw Timotheo Mande mara baada ya kutembelea Uchimbaji wa Madini ya Bauxite yanayochimbwa kwenye kijiji cha Marieni Wilaya ya Same Mkoa wa Kilimanjaro[Picha Ali Meja].
   Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Sazi Salula akionyeshwa-ex rey Mashine kwa ajili ya kupimia Bauxite na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kuchimba Madini ya bauxite ya kutengeneza Saruji Eng.Alumbwage Mhagama Katibu mkuu wakati alipofanya Ziara ya kikazi nakuona hali ya Mazingira kwenye Kijiji cha Marieni wilaya ya Same Mkoa wa Kilimanjaro,
    Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Sazi Salula akizungumza na wanakijiji cha Marieni Wilaya ya Same Mkoa wa Kilimanjaro alipokwenda kukagua Shughuli za Uchafudhi wa  Mazingira katika kjijihicho jana. 
   Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Sazi Salula akiangalia Maadini Bauxite yanayochimbwa na kampuni ya Willy Enterprises alipokwenda kuangalia hali ya Uchafuzi wa Mazingira katika Kijiji cha Marieni Wilayani Same Mkoa waKilimanjaro


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akifungua rasmini Bohari ya dawa iliopo maruhubi mjini Unguja ikiwa ni shamra shamra ya sherehe za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.Picha zote na Makame Mshenga - Maelezo Zanzibar.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr.Ali Mohamed Shein akimuuliza swali msambazaji dawa na vifaa tiba Bi Husna Maulid huko katika Bohari kuu ya madawa maruhubi mjini Unguja ikiwa ni shamra shamra ya sherehe za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
   Hii ni moja ya sehemu ya ndani ya Bohari la dawa lililopo  maruhubi mjini Unguja lililozinduliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein.
   Hili Ndio Bohari la madawa lililopo maruhubi mjini Unguja lililozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein . 
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake ya uzinduzi wa Bohari la Madawa lililopo maruhubi mjini Zanzibar.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mfamasia mkuu wa kwaza baada mapinduzi huko katika Bohari la madawa lililopo maruhubi mjini Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akifungua rasmini Bohari ya dawa iliopo maruhubi mjini Unguja ikiwa ni shamra shamra ya sherehe za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.Picha zote na Makame Mshenga - Maelezo Zanzibar.

  ==========    ========  =======

  Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzíbar     06/01/2013

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema uzinduzi wa Bohari kuu ya Dawa utaiwezesha Serikali ya Mapinduzi Zanzíbar kupanga bajeti yake vyema ya dawa na kusaidia utoaji wa huduma za afya kwa ubora wa hali ya juu.

  Rais shein ameyasema hayo katika hafla ya uzinduzi wa Bohari Kuu ya Dawa iliyopo Maruhubi mjini Zanzibar ikiwa ni mwendelezo wa shamra shamra za kutimiza miaka 49 ya Mapinduzi Zanzibar.

  Amesema Bohari hiyo ya kisasa ni matunda ya kujivunia ya Mapinduzi ya Zanzibar ambayo kwa hakika italeta tija katika upatikanaji wa dawa na uimarisha wa afya za wananchi.

  Dkt. Shein ameelezea matumaini yake kwa sekta ya afya kupitia Bohari hiyo na kwamba anaamini baada ya miaka mitatu Zanzibar itakuwa haipeleki tena Wagonjwa nje ya nchi kwa matibabu.

  Aidha Dkt. Shein amewataka watumishi wa Serikali kubadilika kiutendaji kulingana na kasi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wa Bohari hiyo kuitunza vyema ili iendelee kutoa huduma kama inavyotakiwa.

  Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya Sira Ubwa amesema Bohari hiyo itaboresha utoaji wa huduma kwa uhakika kutokana na ubora wa vifaa na mitambo ya kisasa ambapo wataalamu wataweza kubaini mahitaji ya Dawa zinazohitajika katika kila Hospitali za Unguja na Pemba.

  Kwa upende wao Mabalozi wa Marekani na Denmark wameelezea kufurahishwa kwao na juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha afya ya Wananchi hasa katika mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Malaria na Ukimwi.

  Aidha wameahidi kuendelea kutoa mashirikiano kwa Serikali hasa katika huduma za Afya kwa Mama na Watoto, Elimu,Mapambano dhidi ya magonjwa ya maambukizi pamoja na uzazi wa mpango.

  Bohari hiyo iliyojengwa na Serikali ya Mapinduzi kwa msaada wa Shirika la USAID na NIDA inaelezewa kuwa ya tatu duniani katika viwango vya ubora ambapo jumla ya Dolla za Kimarekani Milion 1.2 zimetumika kukamilisha ujenzi wake.

  IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR  06/01/2013

  0 0

   Beki wa Mwananchi Fc, Muhidin Sufiani 'Sufianimafoto'(kulia) akimtoka mchezaji wa Micovilla, wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Bora Kijitonyama Dar es Salaam leo asubuhi. Katika mchezo huo timu hizo zimetoka sare kwa kufungana mabao 2-2.
   Beki wa Mwananchi Masua Mgumu (nyuma) akimdhibiti mchezaji wa Micovilla, wakati wa mchezo huo.
   Abdallah Masoud wa Mwananchi (mbele) akimhadaa beki wa Micovilla, wakati wa mchezo huo.
  Nahodha wa Mwananchi, Majuto Omary akichuana na beki wa Micovilla kuwania mpira wakati wa mcheo huo.

  0 0


   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Maaskofu wa Kanisa la KKKT baada ya  sherehe ya  Kusimikwa Wakfu Askofu Mkumbo katika kanisa la KKKT la Singida leo Januari 6, 2013


   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Askofu mpya wa KKKT Dayosisi ya kati Dkt Alex Seif Mkumbo (mwenye fimbo) pamoja na viongozi wa kanisa hilo wakiongozwa na Askofu Mkuu Dkt Alex Gehaz Malasusa (kulia kwa Rais), Msaidizi mpya wa Dayosisi hiyo Mchungaji Syprian Yohana Hilinti (wa tatu kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Kone na viongozi wengine katika sherehe ya Kusimikwa Wakfu Askofu Mkumbo katika kanisa la KKKT la Singida leo Januari 6, 2013


  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na  kiongozi wa kanisa la KKKT nchini  Dkt Alex Gehaz Malasusa baada ya kupokea kamba kama ishara ya kupokea zawadi ya ngombe toka kwa Dayosisi  hiyo huku  Askofu  mpya wa KKKT Dayosisi ya kati Dkt Alex Seif Mkumbo akishuhudia  katika sherehe ya  Kusimikwa Wakfu Askofu Mkumbo katika kanisa la KKKT la Singida leo Januari 6, 2013.

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipkea ripoti ya mkoa wa Tabora toka kwa Mkuu wa Mkoa Mhe Fatma Mwassa huo aliyosomewa mara baada ya kuwasili kuanza ziara ya kikazi ya siku nne

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na kiongozi wa kanisa la KKKT nchini  Dkt Alex Gehaz Malasusa na  Askofu  mpya wa KKKT Dayosisi ya kati Dkt Alex Seif Mkumbo baada ya  sherehe ya  Kusimikwa Wakfu Askofu Mkumbo katika kanisa la KKKT la Singida leo Januari 6, 2013

  0 0
 • 01/06/13--13:08: kumekucha uhuru marathon


 • 0 0


  Ndugu waandishi wa habari, baadhi yenu mnafahamu kuwa Baraza la Vijana la Chadema Taifa (BAVICHA), limefanya kikao cha kawaida cha Kamati Tendaji, juzi 5 Januari 2013, katika Hotel ya Benzi Garden jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine, kilijadili masuala matatu mazito.

  Kwanza, Kamati Tendaji ilijadili kwa kina suala la kuporomoka kwa elimu nchini, ambapo serikali imepunguza alama za viwango vya kufaulu, jambo ambalo limesababisha mamia ya wanafunzi waliochaguliwa kutokuwa na sifa.

  Pili, Kamati Tendaji ilijadili jinsi Bavicha itakavyoshiriki katika maandilizi ya utekelezaji wa maazimio ya Kamati Kuu ya Chadema yalioeleza kuwa mwaka 2013 ni mwaka wa nguvu ya umma.

  Tatu, Kamati Tendaji ilijadili kwa kina “Tuhuma za usaliti na njama za kuvuruga chama, kutukana viongozi wakuu wa chama na kuvuruga wanachama wa Chadema na Baraza kwa ujumla.”

  Ndugu waandishi wa habari, yapo baadhi ya vyombo vya habari jana na leo vimeripoti kwa upotoshaji mkubwa wa baadhi ya masuala yaliyojadiliwa na kikao hicho. 

  Kwa mfano, gazeti moja la kila siku limemtaja mwanachama wetu mmoja kuwa ndiye aliyekuwa mtoa taarifa wetu muhimu na kusema mbunge mmoja wa CHADEMA alijadiliwa katika kikao hicho kuwa ni miongoni mwa kundi hili la MASALIA na kufika mbali zaidi kwa kusema, “…sasa amekalia kuti kavu.”

  Lakini ukweli wa kilichojadiliwa kikaoni ni huu ambao tunaueleza sasa:

  Kwanza, kuhusu ajenda ya kuporomoka kwa elimu: Kamati Tendaji imeagiza kuwa utafiti uliofanywa na BAVICHA katika ngazi ya sekondari, ambao umegundua madudu mbalimbali, uongezwe hadi shule za Msingi na taarifa yake ililetwe kwenye kikao kijacho cha Kamati Tendaji.

  Kwenye ajenda ya pili: Kamati ya Utendaji BAVICHA, ilipokea na kujadili agizo la Kamati Kuu ya Chama iliyoeleza kuwa mwaka 2013 ni mwaka wa nguvu ya umma. 

  Katika ajenda ya tatu juu ya tuhuma za usaliti na njama za kuvuruga chama, kutukana viongozi wakuu wa chama na kuvuruga wanachama wa CHADEMA, na Baraza, Kamati ya Utendaji ilipokea taarifa ya Kamati Ndogo ya Kamati Tendaji iliyoundwa Septemba mwaka jana kwenye kikao chake kilichofanyika mjini Morogoro. Kamati ilipewa muda wa mwezi mmoja kukamilisha kazi hii.

  Katika hili, watuhumiwa wakuu walikuwa ni kama ifuatavyo:


  1. Juliana Shonza, Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa
  2. Habib Mchange, mwanachama wa BAVICHA na CHADEMA
  3. Mtela Mwampamba, mwanachama wa BAVICHA na CHADEMA
  4. Gwakisa Burton Mwakasendo, mwanachama wa BAVICHA na CHADEMA
  5. Joseph Kasambala, mwanachama wa BAVICHA na CHADEMA


  Aidha, baada ya Kamati iliyoundwa kuwahoji baadhi ya watuhumiwa na wanachama wengine mbalimbali, ilibaini kwamba wapo baadhi ya wanachama wa BAVICHA ambao wameshiriki kwa namna moja au nyingine katika tuhuma hizi. Hao ni pamoja na Ben Saanane – maarufu kama Eight Oclock.

  Katika orodha hiyo, wakatajwa pia Exaud Mamuya lakini kamati ikashindwa kumpata Mamuya kwa kuwa hakukuwa na mawasiliano ya kutosha.

  Ndugu waandishi wa habari, hizi sasa ni tuhuma za kila mmoja:

  Ndugu Juliana Shonza:

  Alituhumiwa akiwa katika nafasi yake ya Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA, amekuwa akishirikiana na baadhi ya watu kupanga njama na kufanya usaliti dhidi ya Baraza, Chama na vijana wenzake wapenda mabadiliko nchini.

  Amekuwa akifanya mikutano na vikao vya siri, kwa manufaa ya CCM, akiwakusanya vijana wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali waliosimamishwa masomo au kufukuzwa vyuoni kwa kutimiza wajibu wao wa kudai haki zao za msingi na uwajibikaji wa serikali na ambao ni wanachama wa CHASO. 

  Juliana alifanya kazi yake hiyo kwa ushawishi wa hongo, ili wakubali kuitisha mkutano na waandishi wa habari, watoe matamko machafu dhidi ya CHADEMA na viongozi wake wakuu, akiwamo Dk. Willibrod Slaa na Freeman Mbowe.

  Mfano dhahiri hapa ni kikao alichofanya Baa ya Highland iliyoko maeneo ya Makumbusho, majira ya saa 9 hadi saa 11, ambapo aliwaita viongozi wa CHASO, akawashawishi kuwa watakuwa na maisha mazuri, watarudishwa vyuoni na kutunzwa vizuri hapa mjini kama anavyoishi yeye, endapo tu watakubali kufanya press conferences na kuisema CHADEMA kuwa inawavuruga vijana walioko vyuoni.

  Tarehe 6, Desemba, 2012 Hotel MIC, kuanzia saa 10 hadi saa 12, aliwaita baadhi ya vijana ambapo yeye na wenzake walipanga njama za kukichafua chama na kutukana viongozi, kwa manufaa ya CCM.
  Ifuatayo hapa chini ni moja ya sms ambazo Juliana Shonza alikuwa akiwaandikia vijana katika ushawishi wake wa usaliti kwa mapambano haya ambayo chama chetu kinafanya, kuwapigania Watanzania maskini na wanyonge katika nchi yao;

  “jembe chukua bodaboda basi jamaa washatia timu hela yako yakulinda mfuko wako utaikuta tumempa eddo mnaetoa naye tamko tutalindana tu jembe usijali.”

  Huu ni moja tu kati ya ushahidi mwingi, wa meseji, simu, sauti, video, picha na vikao kadhaa katika maeneo mbalimbali, unaomwingiza Shonza na wenzake wengine katika sifa mbaya ya usaliti wa chama, baraza na viongozi wake na wanachama wenzao na umma wa Watanzania kwa ujumla. 

  Hapo alikuwa akimwandikia mmoja wa viongozi wetu ili ashiriki katika press conference ambayo yeye Makamu Mwenyekiti kwa kushirikiana na wenzake wengine, walikuwa wameiandaa kwa nia ya kuchafua chama, kulichafua baraza, kutukana viongozi waandamizi pamoja na kuvuruga na kuchonganisha wanachama wa CHADEMA.

  Matokeo ya kikao hicho cha MIC Hotel, yalionekana siku moja baada ya kikao hicho, ambapo mtu mmoja anayejulikana kwa jina la Edo Mwamalala, aliyeshiriki kikao hicho cha MIC Hotel, aliitisha mkutano na waandishi wa habari, akijitambulisha kuwa ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CHADEMA, cheo ambacho hakuwa nacho. 

  Aidha, Shonza amekuwa akikutana na kufanya vikao vya siri na wenzake, wakipanga njama za kufanya kazi na majukumu ya CCM kuhujumu BAVICHA pamoja na CHADEMA. Mikakati ya kuvuruga baraza, kuchonganisha wanachama na kutukana chama na viongozi wakuu, kwa siri na hadharani, imekuwa ikipangwa katika vikao hivi. 

  Amebainika kukiuka kipengele cha 10.1(x) cha Maadili ya Viongozi, cha Katiba toleo la mwaka 2006, kinachomtaka kiongozi yeyote asitoe tuhuma zozote juu ya viongozi wenzake pasipo kupitia vikao halali, kwa kuzingatia taratibu na kanuni za chama.

  Ameonesha ubaguzi wa kikabila na kikanda kupitia maandiko yake kwenye mtandao kwa kutumia jina lake, anapungukiwa na sifa muhimu na mahsusi za kuwa kiongozi, kwa mujibu wa kipengele cha 10.1(iv) kinachomtaka kiongozi yeyote asijihusishe na vikundi vyenye misingi ya ukabila, udini au ukanda vinavyolenga kuleta ubaguzi ndani ya chama.

  Kwa kushiriki vikao vya kuanzisha chama kipya kinachoitwa CHAUMMA, kushiriki katika makundi yaitwayo MASALIA na PM7 ambayo yote yalikuwa na lengo la kuvuruga chama na wanachama, kukosanisha na kutukana viongozi wa chama, ndugu Shonza amevunja kipengele cha 10.1(i),(viii)(ix) na ibara ya 10.2(iv).

  Kwa kushiriki vikundi hivyo hapo juu, wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya BAVICHA wamejiridhisha pasi na shaka kuwa Shonza haendani na katiba, falsafa, sera na maadili ya chama makini na tumaini la watu, CHADEMA. Hivyo kwa mujibu wa ibara ya 5.1.4 na 5.1.5 anakosa sifa za kuwa mwanachama wa Baraza la Chama.

  Kwa kutoa tuhuma za uongo dhidi ya wanachama na viongozi wenzake, ameendelea kuvunja kanuni za uendeshaji kazi za chama ibara ya 10.1(viii). 

  Amehusika katika kuanzisha, kujihusisha na kuratibu moja kwa moja kundi la vijana waliokuwa wakizunguka mikoani na kushawishi viongozi wa vijana kutoa matamko kwa kutumia jina la CHADEMA kufanya kazi na majukumu ya CCM ya kukichafua chama, kugombanisha wanachama na kumtukana Katibu Mkuu kwa kutumia propaganda za CCM.

  Kamati Ndogo ilimuita Ndugu Shonza ili kumhoji. Lakini aligoma kwa madai kuwa haitambui kamati hiyo na wala hajui kuwa kuna mgogoro, jambo ambalo limetushangaza wengi kwa kuwa Ndugu Shonza alikuwapo katika kikao cha Morogoro kilichounda Kamati hii.

  Ndugu Shonza pia hakuhudhuria kikao cha Kamati Tendaji cha juzi kwa madai kuwa amebanwa na shughuli za familia. Baada ya kupitia maelezo yote hayo, Kamati Tendaji iliamua yafuatayo:

  Ndugu Juliana Shonza, amepoteza sifa na uhalali wa kuwa mwanachama wa Chadema kwa kukiuka ibara ya 5.3.4 na ibara ya 10.1(ix) ya katiba ya CHADEMA na hivyo imeamua kumuondoa katika nafasi yake ya makamu mwenyekiti na kumfuta uwanachama wake. 

  Hivyo basi, kwa maamuzi hayo ya Kikao cha Kamati ya Utendaji ya BAVICHA, kuanzia juzi tarehe 5 Januari 2013, Ndugu Juliana Shonza, si mwanachama wa BAVICHA na hivyo moja kwa moja amepoteza sifa za kuwa kiongozi wa baraza na kwa nafasi yake aliyokuwa nayo ya Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara. 

  Habib Mchange:

  Huyu alituhumiwa kutoa tuhuma za uongo, zikiwemo za mauaji, kinyume na maadili ya Wanachama (kipengele cha 10.3(3); kuunda vikundi vinavyojulikana kwa majina ya MASALIA na PM7 – Pindua Mbowe.

  Pia Ndugu Mchange alituhumiwa kuwavuruga wanachama, kuwachonganisha na kuwatukana viongozi, kisha kushiriki vikao vya kuanzisha chama kingine cha siasa cha CHAUMMA.

  Alituhumiwa pia kupotosha maamuzi halali ya vikao vya chama na Baraza hivyo kuendelea kukipaka chama matope.

  Kamati ilimuita Mchange, na kumhoji juu ya tuhuma zinazomkabili. Hakufika. Badala yake, aliandika barua kueleza kuwa hana imani na kamati:

  Aidha, pamoja na Mchange kugoma kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Kamati Tendaji, Sekretarieti ya Kamati Tendaji Taifa, ilimuita Ndugu Mchange kuhudhudhuria mkutano wa Kamati Tendaji ili kujibu tuhuma zinazomkabili. 

  Mwaliko huu ulifanywa kwa njia ya barua na simu. Njia hizo ndio zilizotumika kualika wahusika wote wakiwamo wajumbe wa Kamati Tendaji, 

  Ndugu waandishi wa habari, baadhi yenu mnafahamu kwamba Ndugu Mchange alikuwa miongoni mwa wanachama wa BAVICHA waliotaka kuwania nafasi ya uenyekiti wa taifa wa baraza hili. Jina lake liliondolewa na Kamati Kuu ya CHADEMA, kutokana na kukosa maadili ya uongozi.

  Kamati Tendaji baada ya kusikiliza hoja yake hii, ikajiridhisha kuwa mtuhumiwa ameamua kuibuka hoja hiyo ili kutaka Kamati Tendaji isimjadili ili aendeleze mradi wake wa kukichafua chama akiwa ndani ya chama.

  Hivyo Kamati Tendaji imefanya yafuatayo: Imempata na hatia ya kuvunja ibara ya 10.3(iii) na kwenda kinyume na kanuni za uendeshaji wa chama ibara ya 10.3(4), kinyume na Maadili ya Wanachama (kipengele cha 10.3(3); uendeshaji wa chama ibara ya 10.3(4) na kwamba mambo yote haya yanadhihirisha kuwa Ndugu Mchange hayuko tayari kushirikiana na viongozi wake kama mwanachama, hivyo kukiuka katiba ya chama ibara ya 5.3.4 na kuafikiwa uamuzi wa kumfukuza uwanachama wa Bavicha na Chadema.

  Mtela Mwampamba:

  Huyu ametuhumiwa kutoa tuhuma nzito za uongo hadharani, zikiwemo za mauaji, kinyume kabisa na Maadili ya Wanachama (kipengele 10.3(3).

  Kuvunja katiba ya chama ibara ya 5.3.4 na Kanuni za Uendeshaji kazi za chama Ibara ya 10.3(4) kwa kupotosha maamuzi halali ya vikao vya chama na baraza na kukipaka matope chama pamoja na kudhihirisha kuwa hayuko tayari kushirikiana na viongozi wake kama mwanachama.

  3.Amevunja Katiba ya CHADEMA ibara ya 5.3.3 na 5.3.4 kwa kutoa kauli za kichochezi dhidi ya chama, kuwachonganisha wanachama na kuwatukana viongozi.

  4.Kwa kujiunga na vikundi vinavyoitwa MASALIA NA PM7 na baadae kushiriki vikao vya kuanzisha chama cha CHAUMMA, Ndugu Mwampamba amevunja ibara ya 10.3(iii).

  5.Kinyume na ibara ya 5.3.3 na 5.3.4 ya Katiba ya CHADEMA na Ibara ya 4.3(g) na (i) ya kanuni za BAVICHA, zinazopinga ubaguzi wa aina yoyote ile, Ndugu Mwampamba ameonesha hisia za ubaguzi wa kikabila na kikanda.

  Gwakisa Burton Mwakasendo:

  Huyu amekuja kwenye kikao na kukiri kutenda makosa yake ambayo takriban yote ni sawa yanayowahusu watuhumiwa waliotangulia hapo juu. Mbele ya kikao cha Kamati ya Utendaji alikiri kushiriki vikao, akisema kuwa ‘lakini’ alilazimika ‘kuikimbia’ dhambi kwa kuondoka katika baadhi ya mikutano na watu hao, wakati mwingine hata nyumbani kwake hakuweza kulala akihisi ‘dhambi’ hiyo anayoikimbia itamfuata nyumbani.

  Kamati Tendaji, iliamua kumpa adhabu ya kuwekwa chini ya uangalizi kwa mwaka mzima, katika wakati wote huo amezuiwa kugombea nafasi yoyote ndani ya BAVICHA na onyo kali la barua.

  Ben Saanane:

  Huyu pamoja na kwamba hakuwa miongoni mwa watuhumiwa alipewa adhabu ya onyo kali na uangalizi wa miezi 12, kutokana na makosa yafuatayo. Kutoa tuhuma nzito, zinazomhusu pia Kiongozi wa juu mwandamizi wa chama, Ben amekiuka Maadili ya Wanachama (kipengele 10.3(3).

  Kukiri kuwa mmoja wa waanzilishi wa vikundi vinavyoitwa MASALIA na PM7 na kisha kushiriki vikao vya kuanzisha chama kingine cha CHAUMMA, amevunja ibara ya 10.3(iii), kwa nia ya kuvuruga chama na kutukana viongozi wake:

  Mbele ya Kamati Tendaji, Ben alikiri makosa na akaomba radhi.

  Aidha, Ben alitoa ushirikiano mkubwa kwa Kamati Ndogo jinsi ya kupatikana kwa taarifa na ushahidi wa namna wanachama wa BAVICHA walivyokuwa wanafanya kazi za kundi hili la MASALIA na PM 7 na hasa juu ya majina wanayotumia katika mitandao mbalimbali ya kijamii, wakifanya juhudi za kuivuruga CHADEMA, kuvuruga BAVICHA, kutukana viongozi na kuwavuruga wanachama, lakini kikubwa wakionesha kila dalili ya tabia ya usaliti.

  Exaud Mamuya:

  Huyu hajapata nafasi ya kusikilizwa kwenye vikao. Hivyo suala lake litaendelea kufanyiwa kazi na uongozi wa BAVICHA.

  Aidha, kikao cha Kamati ya Utendaji pia kilipitisha kwa kauli moja, moja ya maazimio ya BAVICHA Mkoa wa Mwanza, waliopendekeza kufukuzwa uanachama kwa aliyekuwa Katibu wa Mkoa wa Mwanza, Salvatory Magafu, kwa tuhuma za kukiuka Kanuni ya 10.1(xii) kwa kutoa tamko kwenye vyombo vya habari kwa nia ya kumfarakanisha Katibu Mkuu na wanachama wa CHADEMA na umma wa Watanzania, ikiwa ni sehemu ya uratibu wa kundi lililokuwa likiendeshwa na watuhumiwa wengine hapo juu.

  Kamati ya Utendaji pia ilimkuta na makosa ya kiuongozi katika tuhuma zilizowasilishwa vikaoni na kufanyiwa kazi na Kamati Ndogo, Mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Mbeya, Joseph Kasambala na hivyo amepewa adhabu ya onyo kali. 

  Hitimisho
  Tunaomba kuwahakikishia vijana wenzetu wa CHADEMA na wengine wote wapenda mabadiliko nchini, hakuna kijana mwanachama wa BAVICHA, atafanya kazi za kuhujumu baraza na chama kwa ujumla na kusaliti matumaini pekee ya Watanzania, akifanya kazi za mahasimu wetu, kisha akaachwa. 

  Ni lazima na muhimu tuoneshe kuwa tuna uthubutu kwa kuchukua hatua kadri inavyotakiwa, pale panapotakiwa. Tuliopewa dhamana za uongozi, tutatimiza wajibu kuhakikisha hakuna mtu ataonewa wala kupunjwa haki yake katika kusimamia utendaji na utoaji utumishi bora wa baraza kwa wanachama wake na chama kwa ujumla. 

  Daima tutasimamia katiba ya chama, maadili, kanuni, taratibu, itifaki na miongozo ya mabaraza. Baraza hili halitakuwa tayari kuwa sehemu ya kuruga matumaini makubwa ya Watanzania waliyonayo juu ya CHADEMA. 

  Baraza liko imara. Wanachama wetu wasifadhaishwe na upotoshaji unaofanywa na wasaliti kuwa tumevurugika au ‘kumechafuka’. Hatuwezi kuchafuka wala kuvurugika kwa kuchukua maamuzi dhidi ya watu wabinafsi wanaotaka kukwamisha mapambano ya awamu ya pili, kupigania mabadiliko ya kweli ya kimfumo na kiutawala, kwa ajili ya Watanzania.

  Historia inatuonesha kuwa mara zote ambapo mapambano yamefikia hatua ya juu ya kutimiza malengo, ndipo ambapo wasaliti hujitokeza. Hivyo vikwazo hivi vya baadhi yetu kuanza kugeuka nyuma ni dalili za mwisho mwisho kuwa ushindi unakaribia. Ni lazima kama vijana tuendelee kujenga imani na matumaini ya Watanzania waliyonayo juu ya CHADEMA kutukabidhi dola mwaka 2015.

  Mwisho

  Imetolewa leo Januari 7, 2013, Dar es Salaam na;

  John Heche
  Mwenyekiti wa Taifa, 
  Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA)

  0 0

  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa amevipatia vukundi saba vya Vikoba vilivyopo Wilayani Monduli,kiasi cha shilingi milioni nane kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao.Lowassa amesema yeye ni mkereketwa mkubwa wa Vikoba huku akisisitiza kuwa ni chachu ya maendeleo na kumkwamua mtanzania kutoka katika umasikini. kila kikundi kimepata shilingi millioni moja ambapo kikundi kilichofanya vizuri kimeongezewa shilingi millioni moja zaidi.Pichani ni Mh. Lowassa akikabidhiwa zawadi na mwenyekiti wa Vikoba Kijiji cha Monduli Juu,Dawson Kaaya wakati viongozi wa vikundi hivyo walipomtembelea nyumbani kwake Monduli.
  Mmoja wa viongozi wa vikundi vya vikoba Kijiji cha Monduli Mjini akisoma risala mbele ya Mh Lowassa.
  Baadhi ya wanavikoba wa Monduli Mjini wakimsikiliza Mh. Lowassa.
  Mhe Edward Lowassa akipewa zawadi na Bi Arafa Ismaild kutoka katika vikundi vya Vikoba Monduli mjini ambao walikwenda kumtembelea nyumbani kwake. Kushoto kwa Mhe ni Bw. Dawson Kaaya ambaye ni Mwenyekiti wa Vikoba Monduli Mjini.

  0 0  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mawaziri, wabunge na maofisa waandamizi wa wizara na wakala wa ujenzi (TANRODS) pamoja na viongozi wa bodi ya wakandarasi akikata utepe kuzindua rasmi ujenzi wa daraja hilo.Picha na Ikulu.
  ======  =====    =====
  0 0


  NI ZAIDI YA MIAKA MITATU SASA UBALOZI WA TANZANIA-US TUNAUTAARIFU UBADILI HII HABARI NA NYINGINE KATIKA WEBSITE YAKE HAWATAKI. KAMA UNA NDUGU HUKO HEBU MWAMBIE WAONDOE AIBU HII......Music: The Tanzanian national anthem is titled “ Mungu Ibariki Afrika” (God Bless Africa), composed by a South African composer - Enock Sontonga. The song is also the national anthem of South Africa and Zimbabwe.

  The music industry in Tanzania has evolved over the years. Due to the mixture of various cultures in Tanzania, native music is morphing into new music that is a combination of the old, new and imported sounds and rythms. Tanzanian musicians are among the the best in Eastern Africa. You have legendary artists such as RemyOngala, Dionys Mbilinyi, Sabinus Komba, Siti binti Saad, Bi Kidude, Saida Karoli, Hukwe Zawose Nasibu Mwanukuzi aka Ras Nas, Jah Kimbuteh and many others. 

  You also have new vibrant artists such as Imani Sanga, Judith Daines Wambura Mbibo aka Lady Jaydee, Rose Mhando, Joseph Haule aka Professor Jay, Ray C, Saleh Jaber aka Saleh J, Joseph Mbilinyi aka Sugu/ Mr. II/ 2-proud and many more. They mix native music with imported sounds and the result is a range of interesting flavors of music.

  Traditional Tanzanian music includes; Zouk, Ngoma, Taarab and Ndombolo. Some of these tradional music types have been incoporated into exported music to create unique sounds that are refered to as Mtindo, Sikinde, Modern Taarab, Bongo flavor, African hip hop, Bolingo and Reggae......UKITAKA UKASIRIKE ZAIDI INGIA HAPA http://www.tanzaniaembassy-us.org/tzepeo.html

  0 0


  MSANII nyota wa miondoko ya Mnanda a.k.a Mchiriku, Omari Omar amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua kwa muda mrefu. Habari za kuaminika mapema asubuhi hii zinaeleza kuwa, Omar Omar aliyetamba na nyimbo mbalimbali ukiwemo ule maarufu wa 'Kupata ni Majaliwa' alifariki nyumbani kwao Temeke, saa chache baada ya kurejeshwa toka hospitali ya temeke alipokuwa amelazwa kwa siku kadhaa. 

  Taarifa hizo zinasema kuwa mara baada ya kurejea nyumbani, msanii huyo alizidiwa na hatimaye kufariki na kwamba msiba wake upo nyumbani kwao Temeke Mikoroshini kwa ajili ya mipango ya mazishi. Msiba wa msanii huyo umekuja siku chache baada ya tasnia ya sanaa na burudani kumpoteza Juma Kilowoko 'Sajuki' msanii nyota wa filamu aliyefariki pia kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya muda mrefu. dj sek blog inamuombea kila la heri Omar Omar na wengine waliotangulia mbele ya haki mapumziko mema katika safari yao ya Ahera. Innallillah Waina Illah Rajiun. 

  Taarifa zaidi tutakuwa tunawaletea kujua mkali huyo wa mduara aliyewafanya wasanii wengine kufuata mkondo wake akiwemo Dogo Mfaume, Ferouz, Easy Man na wengine SIKILIZA WIMBO WAKE  HAPO JUU-ANAITWA OMARY OMARY - MAJALIWA .HABARI HII KWA HISANI YA dj sek blog.

  0 0
 • 01/08/13--11:47: CLOSER by Vanessa Mdee

 • Dar Es Salaam, Tanzania : January 11, 2013 brings great Tanzanian music to your ears. The velvet voice that is Vanessa (Vee) Mdee, launches her first single of her musical career, "Closer" that is sure to make you dance and sing along to the catchy tune created by popular Tanzanian producers Hermy B and Pancho Latino. Having super musicians like AY, Chidi Benz and Nakaaya on their list of credits, Hermy B and Pancho Latino now bring you a flavor that is sure to give you multiple eargasms.
  This trio of excellence finally decided to unleash the track, which has been on the shelf for two years, to bring you the best in what Vee describes as "a fusion of afro pop, soul, RnB and Hip Pop (not Hop)." The debut is set to take place at the trendy Java Lounge in Masaki, Dar Es Salaam at 9pm. "Closer" is set to take Tanzania by storm as it was proved in a private listening session at the teams Kawe studio attended by close friends and relatives just a few nights ago, allowing them to get an insight into what the reaction would be from the outside world. Needless to say, it was a complete and immense success.

  They now invite you to join them for an exclusive listening party this Friday January 11, 2012 for the debut of the song of the year. "Closer" will be going viral on all social media networks at the same time including but not limited to Twitter, Facebook, You Tube and more.

  Song : Closer

  Artist : Vanessa (Vee) Mdee

  Producers : Hermy B and Poncho  Latino

  Event : Listening Party and Closer Launch

  Date : January 11, 2013 at 9PM

  Venue : Java Lounge – Dar Es Salaam, Tanzania

older | 1 | .... | 5 | 6 | (Page 7) | 8 | 9 | .... | 1898 | newer