Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 692 | 693 | (Page 694) | 695 | 696 | .... | 1897 | newer

  0 0

    Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akiongea na baadhi uongozi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) na viongozi wa ulinzi na usalama wilaya ya Kinondoni kabla ya kuanza ziara yake ya kujionea hatua zilizofikiwa kwenye mradi wa upanuzi wa mtambo wa Ruvu Juu, ulazaji wa bomba kuu la maji kutoka Mlandizi hadi Kimara, ujenzi wa tanki jipya la Kibamba na kukarabati matenki ya maji Kimara mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
   Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda (wa kwanza kushoto) akiwa na baadhi viongozi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) na viongozi wa ulinzi na usalama wilaya ya Kinondoni walipotembelea na kujionea maeneo yaliyojengwa kuzunguka matenki ya maji Kimara mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam. Wa kwanza kulia ni Meneja wa Miundombinu Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi John Kirecha.
   Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda (wa pili kulia) akiwa na Meneja Uhusiano wa Jamii wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASA) Bi.Neli Msuya (wa pili kushoto) pamoja na baadhi viongozi wa Mamlaka hiyo na viongozi wa ulinzi na usalama wilaya ya Kinondoni walipotembelea na kujionea nyumba na makazi ya watu yaliyojengwa kuzunguka matenki ya maji Kimara mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam. Wa kwanza kulia ni Meneja wa Miundombinu Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi John Kirecha na Meneja DAWASA tawi la Kimara Bw. Robert Mugabe (wa kwanza kushoto).
    Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akiingia ndani ya eneo linapojengwa tanki jipya la maji eneo la Kibamba ambalo litakuwa uwezo wa ujazo wa lita milioni 10 kwa siku na kujionea shughuli za ujenzi huo unavyoendelea wakati wa ziara yake mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
   Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda na msafara wake wakiwa eneo linapojengwa tanki jipya la maji eneo la Kibamba ambalo litakuwa uwezo wa ujazo wa lita milioni 10 kwa siku na kujionea shughuli za ujenzi huo unavyoendelea wakati wa ziara yake mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.

   Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda (katikati) akiongea na viongozi wa kampuni ya MEGHA kutoka nchini India ambao ndiyo wanajenga mradi wa bomba la maji kutoka Ruvu Juu pamoja na tanki la maji linalojengwa Kibamba. Wa pili kulia ni Meneja wa kampuni ya MEGHA Mohan Dendkri.
   Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda na msafara wake wakiwa eneo la Kibamba Luguruni kujionea mabomba yanayotumika katika ujenzi wa mradi wa maji wa Ruvu Juu yalipozuiliwa na kuzungushiwa uzio kitu ambacho kinakwamisha kukamilika kwa ujenzi wa mradi huo kwa wakati.
    Baadhi ya mabomba yakiwa ndani ya uzio.
  (Picha na Eleuteri Mangi –MAELEZO)
   
   
   
   Na Eleuteri Mangi - MAELEZO
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda ameuagiza uongozi wa  Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) kuandaa orodha ya wananchi waliojenga juu ya miundo mbinu ya maji na kuipeleka orodha hiyo ofisini kwake kwa hatua zaidi.

  Akiongea na uongozi wa DAWASA mwishoni mwa wiki baada ya kuhitimisha ziara yake ya kujionea hatua zilizofikiwa kwenye mradi wa upanuzi wa mtambo wa Ruvu Juu, ulazaji wa bomba kuu la maji kutoka Mlandizi hadi Kimara, ujenzi wa tanki jipya la Kibamba na kukarabati matenki ya maji Kimara, Makonda alisema kuwa nia ya Serikali kuwapa huduma ya maji wananchi kwa wakati.

  “Nataka kazi hii ya ujenzi wa mradi wa bomba la maji ukamilike kwa muda ulivyopangwa uweze kuwaondolea wananchi kero ya maji inayowasumbua, huduma ya maji ni ya muhimu sana kwa wakazi wa Dar es salaam, upatikanaji wake utasaidia kupunguza magonjwa mengi hasa ya milipuko ambayo ni hatari kwa afya wananchi wetu” alisema Makonda.

  Agizo la Mkuu huyo wa Wilaya linafuatia kuwepo kwa vikwazo mbalimbali vinavyochelewesha mradi wa ujenzi wa bomba hilo kukamilika kwa wakati katika maeneo ya Kimara yalipo matangi ya maji ambapo makazi ya watu yamejengewa kuzunguka matangi hayo na kuhatarisha usalama wa maisha ya wakazi hao na usalama wa miundombinu ya maji.

  Eneo lingine ambalo limekuwa kikwazo cha kukamilisha mradi huo ni Kibamba Luguruni ambapo mabomba ya mradi yamezuiliwa kwa kufungiwa na kuzungushiwa kwenye uzio na mkazi wa eneo hilo Bw. Enock E. Mwakassala.

  Kwa mujibu wa DAWASA, mkazi huyo hana uhalali wa kumiliki eneo hilo maana amevamia eneo la Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kwa sababu zake binafsi na hivyo kuchelewesha ujenzi wa mradi.

  Aidha, Makonda ameuagiza uongozi wa DAWASA kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuwaainisha watu wote waliojenga ndani ya hifadhi ya eneo la miundombinu ya shirika hilo ambalo limetoa sehemu ya hifdhi yake kwa lengo la kujenga na kulaza bomba jipya la kusambaza maji kutoka Mlandizi hadi Kimara yalipo matangi ya kusambazia maji ambayo yatawanufaisha wakazi wa maeneo mbalimbali ya jiji hilo.

  Kwa upande wake Mhandisi Msimamizi wa Mradi huo kutoka DAWASA Christian Christopher amesema kuwa mradi huo wa ujenzi wa bomba la maji kutoka Ruvu Juu una jumla ya km 69 ambapo hadi sasa km 46 ujenzi wake tayari umekamilika na zimebakia km 23 ambazo zinatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Januari 2016.

  Mhandisi Christian alisema kuwa mradi wa ujenzi wa bomba la maji kutoka Ruvu Juu unatekelewa na kampuni ya MEGHA kutoka nchini India inayoongozwa na Meneja wake Mohan Dendkri  chini ya makubaliano ya kandarasi Na. AE/033/2012-13/WC/25.

  Vile vile Mhandisi Christian aliongeza kuwa kutoka eneo la Mlandizi ambalo ndiyo chanzo cha maji yanapotoka yatasafirishwa kwa bomba lenye kipenyo cha ukubwa mm 1200 hadi Kibamba ambapo linajengwa tangi la maji lenye uwezo wa ujazo wa lita milioni 10 kwa siku na baadaye maji hayo kusafirishwa hadi Kimara, kipenyo cha bomba la kutoka Kibamba hahi Kimara ni mm 1000 na kutoka Tanita hadi Kibamba bomba hilo lina kipenyo cha mm 900.

  Wakazi wa jiji la Dar es salaa asilimia 25 wanategemea maji kutoka chanzo cha Ruvu Juu na asilimia 75 wanapata maji kutoka chanzo cha maji kutoka Ruvu Chini. Mtambo  wa  Ruvu  Juu  unahudumia  wakazi  wa  Mlandizi,  mji  wa  Kibaha na  maeneo  ya Kiluvya,  Mbezi,  Kimara,  Ubungo,  Tabata  na  Segerea.  Mtambo  wa  Ruvu Chini unahudumia maeneo ya Mji wa Bagamoyo, Bunju. Boko, Mbezi Beach, Kawe, Kinondoni, katikati  ya  Jiji,  Sinza,  Magomeni,  Buguruni,  Ilala  na  Keko.  Mtambo  wa  Mtoni  unahudumia maeneo  ya  Temeke,  Tandika,  Kurasini,  baadhi  ya  maeneo  ya  Keko  na  Mbagala. 

  0 0

  Hawa watoto Zahra na Zarina wamezaliwa pacha walioungana tarehe 16/11/15  mama yao Bi Tausi Hageze akiwa njiani kwenye boda boda akitokea kijiji cha Nyarurema Tarafa ya Rulenge Wilaya ya Ngara akielekea hopitali ya misheni Rulenge. Alipopata uchungu wa kuzidi alimuomba bodaboda asimame akaweza kujifungua kwa shida mbele ya mumewe anaeitwa Hamdani hapo njiani.

  Baada ya hapo wakapelekwa hospitali ya misheni Rulenge. Mama na watoto wako salama, kama unavyo ona katika picha wameungana kiunoni. Msamaria  amekutana na changamoto hii hapo hospitali na kuamua kuwasaidia kuchangisha iliwapelekwe Mwanza Bugando Hospital walipo hivi sasa. 

  Inaelezwa na ma daktari hapo wameshauri watoto wapelekwe India kwa upasuji na matibabu zaidi.

  Msamaria anaewasaidia Bi Sabra Said Salum wa namba ya simu +255767220099 anaomba yoyote atakae guswa na kadhia hii afikishe mchango kwake ili aweze kuwafanyia safari hii muhimu kuokoa maisha ya mapacha hawa.

  Baba Hamdani Sibhoro na mama Tausi Hageze wote ni wakulima wa jembe la mkono hawana uwezo hata wa kufika Dar.  Bi Sabra kachangisha na kuweza kuwafikisha Bugando, kuwalipia mahitaji ya hapo.

  Mungu awabariki

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ambaye ni mlezi wa Chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADWU), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi nje ya chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Taifa ya kuhusu kifo cha utata cha aliyekuwa Katibu wa chama hicho Tanzania, Rashid Saleh kilichotokea hivi karibuni pamoja na ratiba ya mazishi yake yatakayofanyika jijini Mwanza.
   Marehemu, Rashid Saleh
   Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ambaye ni mlezi wa Chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADU), akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Pubrishers LTD, Eric Shigongo (katikati), na wadau wengine kuhusu taratibu za mazishi za katibu huyo.
   Mjumbe wa Chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADWU), Stanley Kilave (kulia), akizungumza na Mwenyekiti mstaafu wa chama hicho, Clement Masanja (kushoto), pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Pubrishers LTD, Eric Shigongo (katikati), wakati wa taratibu za mazishi zikifanyika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dar es Salaam leo.

   Msemaji wa familia ya marehemu, Jonas Marinyizu (katikati), akitoa shukurani kwa DC Makonda na wadau wengine kwa kuwezesha msiba huo pamoja na utaratibu wa mazishi utakavyo kuwa.  Mwenyekiti wa Chama hicho, Shaban Mdem akizungumza katika mkutano na wanahabari

   Ndugu na jamaa wa marehu wakiwa katika chumba za kuhifadhi maiti Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakisubiri kufanyika taratibu cha uchunguzi wa mwili huo kabla ya kusafirishwa kwenda jijini Mwanza kwa mazishi.
  Ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu wakiwa katika chumba za kuhifadhi maiti Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakisubiri kufanyika taratibu cha uchunguzi wa mwili huo kabla ya kusafirishwa kwenda jijini Mwanza kwa mazishi.


  Na Dotto Mwaibale

  MWILI wa Katibu Mkuu na Msemaji wa Chama Cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADWU), Rashid Saleh umesafirishwa jana kwenda kijijini kwao Kayenze wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza kwa maziko.

  Saleh alifariki jana Novemba 20 Majira ya saa 8 mchana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), wakati akipata matibabu ya maradhi ya figo ili kuokoa maisha yake baada ya kile kinachodaiwa kushindwa kufanya kazi ipasavyo.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ambaye pia ni mlezi wa chama hicho, Paul Makonda alisema kuwa wamepata pigo kutokana na umuhimu na umahiri ambao alikuwa nao marehemu hasa katika kutetea haki za madereva wenzake sanjari na kuibua mambo mbalimbali ambayo yatabaki kuwa historia na kumbukumbu kwao.

  "Saleh alifariki jana (Novemba 20) baada ya kusikia anaumwa ambapo hali yake haikuwa nzuri na madaktari walishauri nimlete Muhimbili kwa matibabu zaidi ambapo nilimfikisha lakini baada ya muda mfupi wakati madaktari wanahangaika kumtibu na kuokoa maisha yake alifariki,"alisema.

  Alisema marehemu amekiacha chama sehemu ya mafanikio makubwa zaidi ya mabadiliko na mikataba ya haki za madereva nchi nzima huku akibainisha mazingira ya kifo na kutaka uchunguzi zaidi ili kujiridhisha na kifo chake uliofanywa chini ya uangalizi wa polisi.


  "Hatukuona kama kuna haja ya kumuhifadhi mwili wa ndugu yetu hadi hapo tutakapojua nini chanzo cha kifo chake kwani majibu ndiyo yatatupa picha ya ugonjwa kwani tumehangaika tangu alipokuwa hospitali ya Kairuki ambapo tulipofika hapa ikabainika kuwa figo zake zote mbili hazifanyi kazi,"alisema.

  Aliongeza kuwa marehemu alipelekwa hospitalini hapo kwa kitengo maalum huku akibainisha endapo figo zinashindwa kufanya kazi mzunguko mzima wa damu mwilini nao husimama ambapo madaktari walishirikiana lakini hawakuweza kuokoa maisha yake.


  Mwenyekiti wa Chama hicho, Shaban Mdem alisema kuwa msiba huo umewasikitisha sana kutokana na mazingira ya kifo chake huku akiitaka mamlaka husika kulisimamia suala hilo la kupatika kwa majibu sahihi juu ya kifo chake.

  "Tunataka uchunguzi ufanyike na majibu yatoke yakiwa sahihi na yanayoridhisha juu ya kifo chake kwani amekufa na madai ambayo yapo ndani yao, hivyo serikali itambue kifo cha Saleh ni katika harakati za kudai haki ambayo tuliyawasilisha mbele ya aliyekuwa waziri mkuu Mizengo Pinda,"alisema. 

  Alisema Saleh ni kiongozi wa taifa zima hivyo alimtaka rais Magufuli kuingilia kati suala hilo kwani kutokana na hali hiyo watamaliza wafanyakazi wote kwa kuwauwa katika mazingira kama hayo sambamba na kutenga siku rasmi kwa ajili ya maombezo ya msemaji huyo.

  Mazingira ya Kifo

  Akizungumzia mazingira ya kifo Msemaji wa Familia ya Marehemu Jonas Ernest alisema kuwa Novemba 9 mwaka huu marehemu alipokea simu kutoka kwa rafiki yake ma kumtaka waende kwenye kikao, ambapo baada ya hapo mwenzake alidai kuwa na njaa.

  Alidai baada ya hapo walikwenda kuagiza chakula ambapo mwenzake hakula na kumuacha marehemu akiwa anakula huku mwenzake akiwa amemuaga kwenda msalani."Baada ya kurudi msalani alimkuta marehemu akilalamika tumbo linamuuma na hivyo kuondoka eneo hilo pasi na huyo rafiki kula chochote,"alisema.

  Alidai kuwa baada ya kuhisi maumivu makali ya tumbo alianza kuharisha na kutapika na alikimbizwa hospitali lakini uchunguzi ulibaini hakuwa na tatizo na kurudishwa nyumbani ambapo siku inayofuata alirudi hospitali na kuambiwa kuwa ana malaria 4.

  "Alianza kutumia dawa za malaria na baadaye kujiskia vibaya na kumrudisha tena hospitali ya Kairuki laikini madaktari walidai kuwa anatatizo ndani ya mwili ambalo ni figo kushindwa kufanya kazi vizuri,"alidai na kuongeza kuwa hadi marehemu anafariki alikaririwa akidai kuwa"Nyama inanitenganisha na mwanangu lakini"na kumtaja mmoja wa wafanyakazi wenzake huku akidai kumuona mtoto wake.  

  Harakati za kudai haki ya madereva

  Saleh alizaliwa mwaka 1966 Mwanza, ambapo hadi anafariki alikuwa katika harakati za kudai na kutetea haki za madereva ambapo Oktoba 2, mwaka huu alikaririwa akisema wamechoshwa na uozo unaoendelea kufanywa na Mamlaka ya Usafirishaji Majini na Nchi Kavu (Sumatra) na Wizara ya Kazi na Ajira kuhusu kufumbia macho kero zinazoitatiza sekta ya usafirishaji hasa kwa madereva wa mabasi ya abiria na magari ya mizigo.


  0 0


  SE8
  Rais wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitega Uchumi Zanzibar Nd,Salum Khamis Nassor wakati alipokuwa akiangalia ramani ya Ujenzi wa Nyuma za Kisasa zitakazojengwa na Kampuni ya Azam Group kwa kushirikiana Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika maeneo ya fukwe za Kijiji cha Fumba Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja alipofanya ziara maalum.
  SE2
  Rais wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akipata maelezo kwa ufupi kutoka kwa  Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Bw.Said Salim Bakhresa alipowasili Fumba Mkoa wa Mjini Magharibi jana katika ziara ya kutembelea maeneo ya ujenzi wa Mji mpya wa Nyumba za kisasa zinazojengwa na Kampuni ya Azam Group kwa kushirikiana Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,(kushoto) Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitega Uchumi Zanzibar Nd,Salum Khamis Nassor.
  SE3
  Rais wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akipata maelezo kwa ufupi kutoka kwa  Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Bw.Said Salim Bakhresa alipowasili Fumba Mkoa wa Mjini Magharibi jana katika ziara ya kutembelea maeneo ya ujenzi wa Mji mpya wa Nyumba za kisasa zinazojengwa na Kampuni ya Azam Group kwa kushirikiana Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,(kushoto) Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitega Uchumi Zanzibar Nd,Salum Khamis Nassor .
  SE4
  Rais wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kwa ufupi kutoka kwa  Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Bw.Said Salim Bakhresa alipowasili katika eneo linalotarajiwa kujwga kiwanda cha utengezaji wa Lami katika Kijiji cha Fumba Mkoa wa Mjini Magharibi jana katika ziara ya kutembelea maeneo ya ujenzi wa Mji mpya wa Nyumba za kisasa zinazojengwa na Kampuni ya Azam Group  kwa kushirikiana Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
  SE5
  Rais wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Bw.Hudhaifa Yussuf Ali Mchoraji wakati alipokuwa akiangalia zamani za ujenzo wa Nyumba za kisasa zitakazojengwa katika fukwe za Kijiji cha Fumba Mkoa wa Magharibi Unguja alipokuwa katika ziara maalum ya kutembea maeneo hayo jana,ujenzi huo utafanyika kwa ushirikiano wa Kampuni ya Azam Group na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,[Picha na Ikulu.]
  SE6
  Rais wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akifuatana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Bw.Said Salim Bakhresa (katikati) Mkuu wa Wilaya ya Magharibi A. Bw.Ayoub Mohammed Mahmoud (kushoto)   na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitega Uchumi Zanzibar Nd,Salum Khamis Nassor wakati alipofanya ziara maalum  ya kutembelea maeneo ya ujenzi wa Mji mpya wa Nyumba za kisasa zitakazojengwa na Kampuni ya Azam Group kwa kushirikiana Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

  SE9
  Rais wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group Bw.Said Salim Bakhresa alipowasili Fumba Mkoa wa Mjini Magharibi jana katika ziara ya kutembelea maeneo ya ujenzi wa Mji mpya wa Nyumba za kisasa zinazojengwa na Kampuni ya Azam Group kwa kushirikiana Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
  SE10
  Rais wa Zanzinbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na viongozi mbali mbali wakati alipowasili Fumba Mkoa wa Mjini Magharibi jana katika ziara ya kutembelea maeneo ya ujenzi wa Mji mpya wa Nyumba za kisasa zinazojengwa na Kampuni ya Azam Group kwa kushirikiana na Serikali nya Mapinduzi ya Zanzibar [Picha na Ikulu.]

  0 0

  index1
  Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu mpya Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa mara baada ya kumuapisha mwishoni mwa wiki katika Ikulu Ndogo ya Chamwino mjini Dodoma. Wengine kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zandibar Dkt Abdulhamid Yahya Mzee, Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Balozi Ombeni Sefue, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe Mohamed Chande Othman, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Pandu Ameir Kificho na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Mkungu.
  index2
  Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu mpya Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa mara baada ya kumuapisha mwishoni mwa wiki katika Ikulu Ndogo ya Chamwino mjini Dodoma.
  PICHA NA IKULU

  0 0


  fr1
  Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Balozi Nicholas Kuhanga (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wahitimu Bora wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) wakati wa Mahafali ya nane ya chuo hicho yaliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Profesa William Anangisye, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Lwekaza Mukandara na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) Bw. Peter Kuhanga. Picha na Frank Shija, MAELEZO
  fr5
  Baadhi ya wahitimu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) wakifuatilia hotuba mbalimbali wakati wa Mahafali ya nane ya Chuo hicho yaliyofanyika chuoni hapo jana.
  fr7
  Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ,Balozi Nicholas Kuhanga akiwatunuku Shahada wahitimu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) (hawapo pichani) alipokuwa mgeni wa Chuo katika Mahafali ya nane ya chuo hicho jana jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Bw. Peter Ngumbulu.
  fr11
  Muhitimu wa mwaka wa tatu ambaye ameongoza kwa ufauli kwa kupata GPA ya 4.8 Bi. Ummul Kheir Mustafa akipongezwa na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Bw. Peter Ngumbulu mara baada ya kupokea zawadi yake ikiwemo kukabidhiwa Cheti chake mbele ya hadhara wakati wa Mahafali ya nane ya chuo hicho jana jijini Dar es Salaam. Muhitimu huyo amekuwa mwanafunzi wa kwanza kunufaika na mpango wa chuo hicho wa kutoa fursa ya kuajiriwa chuoni hapo kwa wanafunzi wanaofanya vizuri katka masomo yao ikiwa ni njia ya kukabiliana na uhaba wa wanataaluma chuo hapo.
  fr12 
  Muhitimu wa mwaka wa tatu ambaye ameongoza kwa ufauli kwakupata GPA ya 4.8 Bi. Ummul Kheir Mustafa akionyesha Cheti chake cmbele ya hadhara mara baada ya kuwa muhitimu wa kwanza kukabidhiwa cheti wakati wa Mahafali ya nane ya chuo hicho jana jijini Dar es Salaam. Mbali na kukabidhiwa Cheti chake cha Shahada papo hapo muhitimu huyo amekuwa mwanafunzi wa kwanza kunufaika na mpango wa chuo hicho wa kutoa fursa ya kuajiriwa chuoni hapo kwa wanafunzi wanaofanya vizuri katka masomo yao ikiwa ni njia ya kukabiliana na uhaba wa wanataaluma chuo hapo. 
  fr2
  Mgeni rasmi  wa Mahafali ya nane ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaama (DUCE) Profesa Martha Qorro akizungumza wakati wa Mahafali hayo yaliyofanyika jana chuoni hapo. Katika mahafali hayo jumla ya wahitimu 1156 walitunukiwa Shahada na Stashahada za juu.
  ………………………………………………………………………………………………..

  Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
  Wanafunzi wenye mahitaji maalum wanaosoma vyuo vikuu nchini wameaswa kutumia elimu wanayoipata kuendesha maisha yao ili waweze kujiletea maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

  Hayo yamesemwa na Prof. Mshiriki wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Kituo cha Studi za Mawasiliano Martha Qorro ambaye alikuwa Mgeni Mashuhuri wakati wa Mahafali ya nane ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaama (DUCE) yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaaam.

  Prof. Qorro alisema kuwa mwamko wa wanafunzi wenye mahitaji maalum kujiunga na elimu ya juu nchini ni mzuri licha ya changamoto zinazowakumba wanafunzi hao wanapokuwa chuoni.

  “Hawa ni wanafunzi wenye uelewa mzuri wakipata mahitaji yao ya lazima yakiwemo fimbo nyeupe, vifaa vya kuandikia kwa kutumia nukta nundu, baiskeli za miguu mitatu, viti maalu na mahitaji mengine ya kijamii” alisema Prof.Qorro.

  Prof.Qorro aliongeza kuwa ni wajibu wa vyuo vikuu nchini kikiwepo Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam kuwasisitiza kwa kuwauliza wanafunzi wanapojaza fomu za kujiunga waoneshe kuwa wanamahitaji maalum ili waandaliwe mahitaji hayo ikiwemo usafiri wa bajaji ndani ya chuo ili kuwawezesha kuwahi vipindi vyao katika maeneo mbalimbali ndani ya chuo.

  Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Profesa William Anganisye alipokuwa akitoa taarifa fupi kuhusu mafanikio chuo wakati wa Mahafali hayo alisema kuwa chuo hicho kimetimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake ambapo hadi sasa wamehitimu wanafunzi zaidi ya 8000 na jumla ya wahitimu 1156 walitunukiwa Shahada na Stashahada za juu katika mahafali hiyo ya nane.

  Naye muhitim wa mwaka wa tatu katika ngazi ya shahada ya ualimu katika masomo ya sanaa Andrea Sanga ambaye pia ni mwanafunzi mwenye mahitaji maalum (mlemavu asiyeona) alisema kuwa mafanikio yake katika masomo yametokana na kuheshimu ratiba kuu ya masomo chuoni hapo pamoja na ratiba yake binafsi ya kujisomea.

  Zaidi ya hayo, Sanga alisema kuwa maktaba ya chuo, ushirikiano mzuri kati yake na wanafunzi wenzake na walimu wake, kuhudhuria semina na kufanya kazi kwa wakati na kupunguza msongamano wa kazi nyingine ndiyo vimekuwa dira yake kuu ya mafanikio.

  0 0

  indexWaziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakisalimiana na viongozi wa mkoa wa Morogoro wakati waliposimama kwa muda mjini  Morogoro wakiwa njiani kuelekea Dar es salaam wakitoka Dodoma Novemba 22, 2015. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Rajabu Rutengwe (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0


   Magari ya Bohari ya Dawa (MSD), yakishusha vifaa tiba Taasisi ya Moi kufuatia agizo la Rais Dk.John Magufuli kulitaka Bunge kutumia sh.milioni 15 kwa ajili ya kujipongeza na fedha zilizobaki kuzipeleka katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kukabiliana na uhaba wa vifaa tiba na magodoro. 
  Na Dotto Mwaibale
  …………………………………………………………………………
  BOHARI ya Dawa (MSD) imeanza kupeleka Vifaa Tiba kwenye Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI), Vifaa ambavyo vimenunuliwa na Ofisi ya Bunge kwa agizo alilotoa Rais Dk. John Magufuli.
  Vifaa hivyo vilianza kupelekwa juzi katika Taasisi hiyo ili kukabiliana na uhaba alioubaini Rais  Magufuli baada ya kufanya ziara ya kushitukiza katika mapema mwezi huu.
  Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu akizungumzia kuhusu vifaa hivyo jijini Dar es Salaam juzi wakati wa usambazaji alisema  hivyo vyenye gharama ya sh.milioni .251 ni pamoja na vitanda 300, magodoro 300, viti vya kusukuma (Wheel Chairs) 30, vitanda vya kubebea wagonjwa (Stretchers) 30, mashuka 1,695 na mablanketi 400.
  Alisema MSD ilianza kupeleka Vifaa hivyo MOI mwishoni mwa wiki na kuwa itaendelea kutoa vifaa hadi wiki hii inayoanza leo.
  Fedha hizo zilizotumika kununulia vifaa hivyo zilitokana na agizo la Rais Dk.John Magufuli alilolitoa wakati akilihutubia bunge mjini Dodoma mwishoni mwa wiki ambapo alilitaka bunge kutumia sh.milioni 15 tu kwa ajili ya kujipongeza na kiasi hicho kilichobaki kitumike kununulia vifaa hivyo.

  0 0

  KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Komredi Abdulrahman Kinana katikati ya wiki iliyopita aliongoza ujumbe wa Tanzania nchini Msumbiji kuhudhuria mkutano wa Vyama vya Siasa Kusini Mwa Afrika. 
  Mkutano huo uliohudhuriwa na baadhi ya Wenyeviti na Makatibu Wakuu wa vyama  hivyo, umemalizika mwishoni mwa wiki mjini Maputo kwa mafanikio makubwa.

  Mkutano huo ulijadili masuala yaliyolenga kutatua changamoto mbalimbali za mataifa hayo na mipango ya maendeleo kwa ujumla.

  Baadhi ya viongozi wa vyama hivyo vya siasa waliohudhuria ni pamoja na Mwenyekiti wa ANC ya Afrika Kusini Rais Jacob Zuma, Mwenyekiti wa FRELIMO ya Msumbiji Rais Filipe Nyusi, Mwenyekiti wa SWAPO ya Namibia Rais Hage Geingob pamoja na Komredi Kinana na ujumbe wake.

  Ujumbe kutoka Tanzania ulioongozwa na Komredi Kinana umewajumuisha Katibu wa NEC anayeshughulikia Siasa na Mambo ya Nje Dkt. Asha-Rose Migiro pamoja na Makatibu Wakuu wa Jumuiya za CCM.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman  Kinana (kulia)akiwa kwenye picha ya pamoja na Zuma Mwenyekiti wa ANC ya Afrika Kusini Rais Jacob  (kushoto) na Mwenyekiti wa FRELIMO ya Msumbiji Rais Philipe Nyusi  (katikati).
   Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Chama cha SWAPO cha Namibia Rais Hage Gengob,  katika mkutano wa viongozi wa vyama vya siasa
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kushoto) akizungumza kwenye mkutano wa viongozi wa vyama vya siasa vya Kusini mwa Afrika mjini Maputo, Msumbiji.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa na Makatibu Wakuu wa vyama vya ANC, FRELIMO, MPLA, SWAPO na ZANU PF mjini Maputo.

  0 0

  Tuzo iliyotolewa kwa Mradi wa EEVT baada ya kupata ushindi katika eneo la Mazingira na Huduma kwa Jamii.
   Afisa Mtendaji Mkuu wa BG Bw. Helge Lund akizungumza na washiriki wa hafla hiyo ya kutunuku tuzo kwa washindi iliyofanyika Kensington Palace nchini Uingereza hivi karibuni.
   Mkurugenzi wa VETA kanda ya Kusini Mashariki Joseph Kibehele (watatu kutoka kushoto) akiwa ameshikilia tuzo hiyo katika picha ya pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa BG Bw. Helge Lund (wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Meneja uwekezaji kwa jamii wa LNG Tanzania Bi. Kate Sullam, Mwakilishi kutoka LNG Tanzania Bi. Patricia Muhondo, Meneja Mradi wa Hali Bora ya Maisha (Livelihood) wa VSO Bi. Rose Tesha na mmoja wa majaji wa shindano hilo.
   Washiriki kutoka nchi mbalimbali walioshiriki katika hafla hiyo katika picha ya pamoja wakati wa chakula cha jioni.  MRADI wa Kuongeza Sifa za Kuajirika kupitia Mafunzo ya Ufundi Stadi (EEVT) unaoendeshwa kwa ushirikiano kati ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), shirika la VSO na Kampuni ya Gas LNG nchini Tanzania umepata ushindi kwa mwaka 2015 katika eneo la Mazingira na Huduma kwa Jamii.

  EEVT ilitangazwa mshindi miongoni mwa kundi la washiriki wanne bora walioingia fainali kwenye eneo la Mazingira na Huduma kwa Jamii wakati wa halfa ya kutunuku tuzo iliyofanyika Kensington Palace nchini Uingereza tarehe 12 Novemba, 2015 ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Afisa Mtendaji Mkuu wa BG Bw. Helge Lund.

  Tuzo za BG hutolewa kila mwaka kwa kubaini, kushirikishana na kusherehekea mwenendo ulio bora miongoni mwa washirika wa BG.

  Mchakato wa Tuzo za mwaka 2015 ulihusisha washiriki 147 kutoka nchi mbalimbali na wakiwa katika makundi matano ya Ushirikiano katika Kazi; Mazingira na Huduma kwa Jamii; Uthabiti na Ubora katika Utendaji Kazi; Utendaji kazi kwa Usalama na Uadilifu katika matumizi ya Rasilimali; na Ugunduzi. Washiriki wanne bora kutoka kila kundi walichaguliwa kuingia katika kinyang’anyiro cha mwisho.

  0 0

  Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili kanda ya Kaskazini na Meneja Miradi wa Shirika lisilo la kiserikali la NAFGEM,Honorata Nasuwa akizungumza na wanahabari(hawako pichani ) juu ya uzinduzi huo,kushoto kwake ni Afisa Ushawishi na utetezi (KWIECO) na mratibu wa maadhimisho hayo kanda,Hilary Tesha.
  Baadhi ya wajumbe wa kamati ya maandalizi ya uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili kanda ya Kaskazini.
  Baadhi ya waandishi wa habari mkoa wa Kilimanjaro wakifuatilia taarifa juu ya uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.


  0 0   Mwenyekiti  wa Kamati ya maandalizi ya tamasha la kumshukuru mungu kwa amani na utulivu wakati wa uchaguzi mkuu, Alex Msama akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo, kuhusu maandalizi ya tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika Desemba 25 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar na kuwahusisha waimbaji mbalimbali wa nyimbo za kiroho kutoka ndani ya nje ya nchi. Kushoto ni Mratibu wa tamasha hilo, Khamis Pembe.

   KANISA la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) mkoani Dodomalimewataka waandaaji wa Tamasha la Kushukuru, Kampuni ya Msama Promotions kuukumbuka mkoa wa Dodoma katika tamasha hilo linalotarajia kufanyika Desemba 25 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.


  Akizungumza  mwishoni wa wiki jijini Dar, Mwenyekiti  wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo,Alex Msama alisema amepokea taarifa hiyo kutoka kwa Mchungaji wa kanisa hilomkoani Dodoma, Elia Meshack.


  Msama alisema Mchungaji Meshack ameliomba tamasha hiloili kufikisha asanteyao kwa Mungu baada ya kufanikisha uchaguzi Mkuu wa Tanzaniauliofanyika Oktoba 25 nchini kote.


  Aidha Msama kwa kuwa waliandaa tamasha la kuombea amani uchaguzi Mkuu, hapana budi kurudisha shukrani kwa Mungu baada ya kuomba amani katika uchaguzi huo.


  “Nimezungumza na Mchungaji Meshack akinieleza kwamba itakuwa vema Tamasha la Shukrani nikilifikisha mkoani Dodoma, Kamati yangu inafanya mikakati ya kuweza kufikisha asante kwa Mungu,” alisema Msama.

  0 0


   Picha ya mpendwa wetu Nyamiti Ivan Lusinde ikiwa kanisani siku ya Jumapili Novemba 22, 2015 siku ilikofanyika misa takatifu ya kumbukumbu na kuhudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi akiwa ameongozana na mkewe pamoja na mwanae. Nyamiti alikua mfanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani alipatwa na mauti alipokua likizo Tanzania katika hospitali ya Kariuki alipokua amekwenda kwa matibabu baada ya kuugua ghafla alipokua huko na baadae kuaga Dunia Novemba 17, 2015. Picha na Vijimambo/Kwanza Production.

  Father Honest Munishi akiongoza misa takatifu ya kumbukumbu ya mpendwa wetu Nyamiti Ivan Lusinde siku ya Jumapili Novemba 22, 2015 na kuhudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi akiwa ameongozana na mkewe pamoja na mwanae. 

  Father Lehandry Kimario akisaidiana na Father Honest Munishi katika kuongoza misa takatifu ya mpendwa wetu Nyamiti Ivan Lusinde iliyofanyika siku ya Jumapili Novemba 22, 2015 Baltimore, Maryland nchini Marekani.
  Mhe. Balozi Wilson Masilingi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani akiwa na mkewe Marystella Masilingi wakifuatilia misa takatifu ya kumbukumbu ya mpendwa wetu Nyamiti Ivan Lusinde iliyofanyika siku ya Jumapili Novemba 22, 2015 Baltimore, Maryland nchini Marekani.
  Balozi Mhe. Wilson Masilingi akiongea machache jinsi alivyomjua Nyamiti na kutoa shukurani zake kwa watu mbalimbali ikiwemo kamati iliyowezesha kufanikisha misa hiyo na shukurani za pekee kwa Father Honest Munishi na Father Lehandry Kimario.

  Kulia ni Sima Kazaura akisoma soma la kwanza huku akiwa amesindikizwa na Dorothy.
  Kulia ni Farida Sarita akisoma soma la pili huku akiwa amesindikizwa na Dorothy.
   Mshereheshaji Tuma akiongea jinsi alivyomfahamu mpendwa wetu Nyamiti.
   Kulia ni Rosemary Commodores akisoma wasifu wa marehemu.
   Kulia ni Afisa Ubalozi Suleiman Saleh akitoa salamu za Ubalozi, kushoto ni mkewe.
   Dorothy akieleza jinsi alivyomfahamu mpendwa wetu Nyamiti.
   Sima Kazaura akieleza jinsi alivyomfahamu mpendwa wetu Nyamiti
   Patrick Kajale akieleza jinsi alivyomfahamu mpendwa wetu Nyamiti
  Eddah Gachuma akieleza jinsi alivyomfahamu mpendwa wetu Nyamiti
  Dj Luke akieleza jinsi alivyomfahamu mpendwa wetu Nyamiti
  Joyce akieleza jinsi alivyomfahamu mpendwa wetu Nyamiti
  Pius Mtalemwa kiongozi wa kanisa la ibada ya Kiswahili DMV akihitimisha kwa kutoa shukurani kwa wote.

  Nelson Masilingi, mtoto wa Mhe. Balozi akifuatilia misa takatifu ya kumbukumbu ya mpendwa wetu Nyamiti Ivan Lusinde.

  Mwambata wa Jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Canada Col. Adolph Mutta akiwa na mkewe wakifuatilia misa takatifu ya kumbukumbu ya mpendwa wetu Nyamiti Ivan Lusinde.

  Watu mbalimbali waliohudhuria misa.

  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Na Mwandishi wetu, Dar es salaam
   Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini umekanusha kuwepo kwa madai yaliyotolewa na Hospital ya Rufaa  Mkoani Mbeya kuwa  wanaudai Mfuko jumla ya shilingi bilioni 2 na kwamba wanaudai Mfuko kutoka mwezi Juni, 2015.

  Akizungumza jijini Dar es salaam Kaimu Mkurugenzi Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya  Ndugu Michael Mhando amesema madai yaliyotolewa na Hospitali hiyo ya Rufaa Mkoa wa Mbeya  hayana ukweli wowote nakwamba mfuko huo  unalipa madai baada ya mtoa huduma kuwasilisha kwenye Mfuko.

  Amesema madai   ya mwisho ya Hospitali hiyo kulipwa ni ya mwezi Agosti, 2015. Madai ya mwezi Septemba, 2015 yamewasilishwa kwenye Mfuko Novemba 4,2015 ambayo mpaka sasa yana siku 15 tu. Kwa hiyo Hospitali ya Rufaa ya Mbeya tumewalipa madai yao yote na kwa mwaka huu wa 2015 kuanzia Januari hadi Agosti 2015 tumewalipa kiasi cha shilingi bilioni 4.3.

  Madai mengi ambayo yamekuwa yakiwasilishwa kwao yamegubikwa na udanganyifu mkubwa hali inayowafanya kuchukua muda mrefu katika uhakiki wake ikiwemo kuwapigia simu wagonjwa waliopewa huduma za matibabu.

  Aidha Mhando amesema mfuko huo unatoa onyo kali kwa watoa huduma ambao wamekuwa bado wakijihusisha na udanganyifu wa aina yoyote kwa kuwa haitawaonea haya kuwafutia usajili na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

  Amesema Mfuko pia unazidi kutoa rai kwa watoa huduma kutumia fursa zinazotolewa na Mfuko katika kuhakikisha huduma za matibabu zinaboreshwa kwa wanachama na Watanzania kwa ujumla.

   Wakati huo Kaimu mkurugenzi huyo amesema Katika kipindi hiki, baadhi ya watoa huduma wamekuwa wakitoa sababu mbalimbali za kushindwa kutoa huduma nzuri ama za kuridhisha kwa wanachama wao  na wananchi kwa ujumla kwa kisingizio cha kukosa fedha hali inayosababisha kukosa dawa, kukosa vifaa tiba na vitendanishi pamoja na kushindwa kuboresha mazingira ya vituo.

  Watoa huduma hao wanadai hayo ama wanatoa visingizio vya kukwama huduma katika maeneo yao kutokana na NHIF kuchelewa kulipa fedha fedha za madai ambayo wametibia wanachama wake.

  Amesema taarifa  hizo zinajenga mazingira kuwa NHIF ni kikwazo katika ufanisi wa vituo hivyo jambo ambalo si la kweli na limebeba taswira ya kuleta chuki baina ya wanachama ama wananchi na chombo chao ambacho kina dhamana ya kuwatibia.

  Hata hivyo Mhando amekanusha kuwa wao  ndio kikwazo ama sababisho la huduma mbovu katika vituo hivyo nah ii inatokana na ukweli kwamba zipo jitihada mbalimbali ambazo NHIF imekuwa ikizifanya kuhakikisha inasaidiana na Serikali katika kuboresha huduma za vituo hivyo ili wananchi kwa pamoja wapate huduma zinazostahili.
  (Imeandaliwa na Mtandao wa www.Jamiimoja.blogspot.com)

  0 0

  Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Louis Montfort iliyoko jirani na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, akiwaongoza baadhi ya wahitimu wa kidato cha nne 2015, wa shuke hiyo kuburudisha kwenye mahafali ya nne iliyofanyika shuleni hapo Novemba 21, 2015.  
   Mkurugenzi wa Sheria wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, (TAA), ambaye pia anashughulikia Mahusiano, Ramadhan Maleta, (Kulia), akitoa hotuba wakati wa mahafali ya nne ya Shule ya Sekondari Louis Montfort, iliyoko Yombo jijini Dar es Salaam Novemba 21, 2015. Maleta ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, alisema TAA inafarijika sana kushirikiana na jamii iliyo jirani na viwanja vyake vya ndege kote nchini na kwamba itasaidia kutatua baadhi ya changamoto zinazoikabili shule hiyo ili kuendelea kushirikiana katika kutunza uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

    Mkurugenzi wa Sheria wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, (TAA), ambaye pia anashughulikia Mahusiano, Ramadhan Maleta, (Kushoto), akimkabidhi cheti, Mwanafunzi bora kielimu wa kidato cha nne Emmy Bosco Mduma, wakati wa Mahafali ya nne ya Shule ya Sekondari Louis Montfort iliyoko Yombo jijini Dar es Salaam, Novemba 21, 2015. Maleta ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, alisema TAA inafarijika sana kushirikiana na jamii iliyo jirani na viwanja vyake vya ndege kote nchini na kwamba itasaidia kutatua baadhi ya changamoto zinazoikabili shule hiyo ili kuendelea kushirikiana katika kutunza uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Katikati ni Mkuu wa Shule hiyo, Dkt.Jim Madavana.

  Mkurugenzi wa Sheria wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, (TAA), ambaye pia anashughulikia Mahusiano, Ramadhan Maleta, (wapili kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na mwanafunzi wa kidato cha nne ambaye amefanya vizuri kwenye masomo ya kuhitimu kidato cha nne, Emmy Bisco Duma, (watatu kushoto), wakati wa mahafali ya nne ya Shule ya Sekondari Louis Montfort iliyoko Yombo jijini Dar es Salaam Novemba 21, 2015. Wengine kutoka kushoto ni viongozi wa Shule hiyo, Jimmy George, Mkuu wa Shule, Jim Madavana, na Mkuu wa Taaluma, Chiku J. Sekilasi.
   Mkurugenzi wa Sheria wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, (TAA), ambaye pia anashughulikia Mahusiano, Ramadhan Maleta, (kulia), akipokea zawadi kutoka kwa kiongozi wa Shule ya Sekondari ya Louis Montfort iliyo jirani na uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, wakati wa mahafali ya nne ya kidato cha nne shuleni hapo Novemba 21, 2015. Maleta ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, alisema TAA inafarijika sana kushirikiana na jamii iliyo jirani na viwanja vyake vya ndege kote nchini na kwamba itasaidia kutatua baadhi ya changamoto zinazoikabili shule hiyo ili kuendelea kushirikiana katika kutunza uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
  (Picha Kwa Hisani ya TAA)

  0 0

  TANZANIA NATIONAL PARKS
  PRESS RELEASE

   
  TANAPA RECEIVE ANTI-POACHING AIRCRAFT FROM GERMANY


  Germany Foreign Minister Frank-Walter Steinmeier yesterday handed over symbolic key of two Husky aircrafts to Tanzania National Parks and Tanzania Wildlife Authority respectively. The aircrafts will be used for anti-poaching operations in the protected areas.


  Director General of TANAPA Allan Kijazi said that the aircrafts would take the joint approach by the Germany Government through Frankfurt Zoological Society, TANAPA and TAWA to tackle poaching in the protected areas.


  The Husky A-1C is an ideal plane for monitoring and anti-poaching surveys as it operates at low heights and slow speeds-similar to that of a helicopter and has proven long-term success rate for its use in finding poacher camps and recording GPS positions for follow-up actions by teams on the grounds.


  The Huskies will be used to monitor two of Tanzania’s elephant hotspots, Selous Game Reserve and Serengeti National Park.


  Tanzania is home to some of the most elephant and rhino populations on the planet but of recent days it has experienced a severe threat from a massive upsurge in poaching.  Issued by Corporate Communications Department

  Tanzania National Parks

  23rd November, 2015

  T: 027 250 1933

  Germany Foreign Minister Hon. Frank –Walter Steinmeier (right) handing over a symbolic key of a light Husky aircraft for anti-poaching operations to Director General of TANAPA Allan Kijazi. Others in the picture from left are Director of Wildlife Herman Keraryo and Acting Director General of Tanzania Wildlife Authority Martin Loibooki.
  Director General of TANAPA Allan Kijazi making a brief presentation about TANAPA to Germany Foreign Minister Hon. Frank –Walter Steinmeier during the handing over event of two surveillance aircrafts from Germany to Tanzania yesterday.
  Director General of TANAPA Allan Kijazi presenting some of the souvenirs of TANAPA to Germany Foreign Minister Hon. Frank –Walter Steinmeier.
  Germany Foreign Minister Hon. Frank –Walter Steinmeier (second right) posed in a group picture with some of the Germany Members of Parliament who accompanied him during the handing over event of two surveillance aircrafts from Germany to Tanzania yesterday.

  Germany Ambassador to Tanzania Hon. Egon Kochanke (right) and the Permanent Secretary Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation Ambassador Liberata Mulamula during the event.
  Director General of TANAPA Allan Kijazi in a joyous mood when presenting some of the souvenirs of TANAPA to Germany Foreign Minister Hon. Frank –Walter Steinmeier.
  Director General of TANAPA Allan Kijazi speaking with media during the event.
  Some of the invitees during the handing over event. From left to right are Arusha Regional Administrative Secretary Mr. Mapunda, African Wildlife Foundation Country Director John Saleh and TANAPA’s Director of Tourism and Marketing Ibrahim Mussa.

  0 0

   Picha mbalimbali zikionesha mandhari halisi yenye kuendelea kukukumbatia Ugonjwa wa Kipindu pindu hapa jijini Dar na kwingineko,pichani ni wachuuzi wa matunda na maji wakiendelea na biashara zao bila kujali afya na usalama wa wateja wao kama waonekanavyo pichani.  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anamtumia salamu za rambirambi Mwenyekiti wa Chama Cha Madereva Tanzania (TADWU) kufuatia kifo cha aliyekua Katibu Mkuu wa Chama hicho Bw. Rashid Salehe kilichotokea Tarehe 20 Novemba, 2015 katika Hospitali ya Taifa Mhimbili.

  Katika salamu hizo Rais Magufuli amesema taifa limempoteza mtu shupavu, mkweli, makini na aliyependa kupigania haki pale alipoamini kuwa panastahili haki hiyo na alithibitisha kwa kupigania uanzishwaji wa Chama Cha Madereva na kusimama kidete kutetea haki zao.

  "Nawatakia moyo wa uvumilivu familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki,  madereva na wengine wote ambao wameguswa na kifo cha Rashid Salehe na wote tuungane kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ampumzishe mahali pema peponi".

   Marehemu Rashid Salehe enzi za uhai wake.

  Dr Magufuli anaungana na wote walioguswa na msiba huo katika kipindi hiki kigumu na kwamba taifa litauenzi mchango mkubwa alioutoa marehemu Rashid Salehe.

  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi Mawasiliano, IKULU
  23 Novemba, 2015.

  0 0

  index
  Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa  akizungumza na Spika Mstaafu, Anne Makinda  kwenye ikulu ya Chamwino mjini Dodoma hivi karibuni.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  index2

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Dkt. James Mataragio akuzungumza mbele ya waandishi wa habari kuhusu ujio wa ndege ya pili ya utafiti wa awali wa mafuta na gesi asilia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) mwishoni mwa wiki, ndege hiyo inatarajia kuanza utafiti wiki hii katika kitalu cha Eyasi Wembere na Mandawa.
   Mkurugenzi Mtendaji TPDC Dkt. James Mataragio akipatiwa maelekezo ya jinsi ndege hiyo inavyofanya kazi (ndani ya ndege) kutoka kwa Meneja wa Mradi Brett Robinson wa kampuni inayoendesha utafiti huo ya “CGG AVITION LTD”  katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), utafiti huo unagharamiwa na TPDC kutoka katika mfuko wa fedha za maendeleo.
   Ndege ya utafiti wa awali wa mafuta na gesi asilia inayotarajia kuanza utafiti katika kitalu cha Eyasi Wembere na Mandawa ikiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Mkoani Kilimanjaro mwishoni mwa wiki.
  Meneja wa Mradi Brett Robinson wa kampuni inayoendesha utafiti huo ya “CGG AVITION LTD” (kushoto) akitoa ufafanuzi mbele ya waandishi wa habari jinsi ndege hiyo itakavyofanya utafiti, Mkurugenzi Mtendaji TPDC Dkt. James Mataragio (kulia).

older | 1 | .... | 692 | 693 | (Page 694) | 695 | 696 | .... | 1897 | newer