Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 691 | 692 | (Page 693) | 694 | 695 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ukiwa katika kikao na Ujumbe wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) uliotembelea Wizara hiyo.  Wa pili kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo. 
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, John Mngodo akizungumza na ujumbe wa Shrika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) (haupo pichani) uliotembelea Wizara hiyo ambapo masuala mbalimbali kuhusiana na wakimbizi yalijadiliwa.  Tanzania ni mojawapo ya nchi zinazohifadhi wakimbizi, hasa kutoka Ukanda wa Maziwa Makuu.
   Naibu Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Bi. Kelly Clements akizungumza katika kikao na Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (haupo pichani) wakati yeye na ujumbe wake walipotembelea Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Katikati ni Mkurugenzi wa UNHCR, Kanda ya Afrika na kushoto ni Mtendaji Msaidizi wa Naibu Kamishna Mkuu wa UNHCR, Bi. Geraldine Salducci.
  Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Harrison Mseke akizungumza katika kikao cha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na ujumbe wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) wakati ujumbe huo ulipotembelea Wizara. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.(Picha zote na Abubakari Akida,Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
  Imeandaliwa na Kitengo Cha  Mawasiliano ya Serikali-Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

  0 0

   Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Ufundi Stadi Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Thomas Katebalilwe akihutubia kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome, aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 10 ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Dar es Salaam leo asubuhi.
   Mkuu wa chuo hicho, Profesa Shadrack Mwakalila akielezea mafanikio ya chuo.
   Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Ufundi Stadi Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Thomas Katebalilwe (wa pili kushoto), akimkabidhi cheti kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome, mwanafunzi, Benard Nyoni, aliyefanya vizuri katika masomo yake wakati wa sherehe za mahafali ya 10 ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA), Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa chuo hicho, Profesa Shadrack Mwakalila na  Kaimu Mwenyekiti ya Bodi ya chuo, Evelyne Makalla.
   Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Ufundi Stadi Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Thomas Katebalilwe (wa pili kushoto), akimkabidhi cheti kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome, mwanafunzi, Godfrey Nchimbi aliyefanya vizuri katika masomo yake wakati wa sherehe za mahafali ya 10 ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA), Dar es Salaam leo asubuhi. Kutoka kushoto ni Mkuu wa chuo hicho, Profesa Shadrack Mwakalila, Kaimu Mwenyekiti ya Bodi ya chuo, Evelyne Makalla na Rais wa Serikali ya Wanafunzi (MASO), Elias Kumanya. 
   Wahitimu wa ngazi ya cheti, stashahada na shahada ya kwanza waliofanya vizuri katika masomo yao wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa vyeti na Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Ufundi Stadi Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Thomas Katebalilwe kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome, wakati wa sherehe za mahafali ya 10 ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)
   Meza kuu ilivyokuwa ikionekana kwenye mahafali hayo.
   Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Ufundi Stadi Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Thomas Katebalilwe (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na  Mkuu wa chuo hicho, Profesa Shadrack Mwakalila (kushoto),  na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya chuo, Evelyne Makalla katika mahafali hayo.
     Brass Bendi ya Magereza ikiongoza maandamano wakati wa mahafali hayo.
   Mgeni rasmi na viongozi wengine wakiongoza maandamano kuelekea eneo la sherehe.
   Wahitimu wa ngazi ya cheti, stashahada na shahada ya kwanza wakiwa katika sherehe za mahafali ya 10 ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA), yaliyofanyika Dar es Salaam.
   Wanafunzi wenzao wakiwapongeza watangulizi wao kwa kuhitimu.
   Brass Bendi ya Magereza ikitoa burudani katika mahafali hayo.
   Wahadhiri wa chuo hicho wakiwa katika mahafali hayo.
   Wageni waalikwa wakijumuika katika sherehe hiyo.
   Hapa ni kazi tu
   Wadau mbalimbali wakiwa kwenye mahafali hayo.
   Wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo.
   Wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo.
   Wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo.
   Wahitimu waliofanya vizuri masomo yao wakiwa katika icha ya pamoja na meza kuu.
   Wahitimu wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi.
  Hiyo ni furaha tupu ya kuhitimu.
  (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com.

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
  TAARIFA ZAIDI KUHUSU MAHUJAJI KUTOKA TANZANIA WALIOFARIKI AU KUJERUHIWA HUKO SAUDI ARABIA

  Mahujaji wengine wane (4) kutoka Tanzania ambao walikuwa miongoni mwa wale waliokuwa hawaonekani tangu ajali ya kukanyagana kwa mahujaji ilipotokea Makkah nchini Saudi Arabia tarehe 24 Septemba 2015 wametambuliwa kuwa, ni miongoni mwa mahujaji waliofariki  dunia. Kutambuliwa kwa mahujaji hao kunafanya idadi ya mahujaji wa Tanzania waliopoteza maisha katika ajali hiyo kufikia thelathini na mbili (32). 

  Majina ya Mahujaji hao kutoka kikundi cha Khidmat Islamiya ni:-
  1.Abdul Idd Hussein
  2.Adam Abdul Adam
  3.Rashida Adam Abdul
  4.Khadija Abdukhalik Said 

  Aidha, hadi sasa mahujaji saba (7) kutoka Tanzania bado hawajulikani walipo na jitihada za kuwatafuta bado zinaendelea. Majina ya Mahujaji hao ni:
  1.Burhani Nziru Matata
  2.Farida Khatun Abdulghani
  3.Juma Jecha Jaku
  4.Laila Manunga
  5.Nassor Mohammed Hemed
  6.Saleh Mussa Said
  7.Shabinabanu Ismail Dinmohamed

  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, 
  Dar es Salaam
  20 Novemba, 2015

  0 0

  Kalenda ya dirisha la usajili kwa vilabu vya Ligi Kuu (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL) lilofunguliwa Novemba 15, litafungwa Disemba 15 mwaka huu.
  Vilabu vinavyoshiriki ligi hizo zilizopo chini ya Shirikisho Mpira wa Miguu (TFF) vinaombwa kufanya usajili katika muda uliopangwa ili kuepukana na kuchelewa, na kufungwa kwa dirisha hilo.
  Usajili wa dirisha dogo ni kwa vilabu ambavyo havijajaza idadi ya wachezaji 30 katika usajili uliofanyika wakati wa dirisha kubwa la usajili (Juni – Agosti 2015), usajili huo wa wachezaji unafanyika katika tovuti ya TFF, www.tff.or.tz kisha kwenye link ya Club Registration.

  0 0


  Wananchi wa Kijiji cha Igamba ambao ni wakulima wa Kahawa wakipiga picha ya pamoja baada ya kupata elimu na kujiunga na NSSF kama wanachama wa Hiari chini ya Mpango wa Wakulima Scheme ambao utawasaidia Kupata Matibabu bure na Kujipatia Mikopo ya pembejeo.
  Maafisa wa NSSF mkoa wa Mbeya wakiwaandikisha watu kutoka Sekta binafsi waliokusanyika kwenye kituo cha mabasi cha mbalizi kwenye kampeni maalum ya NSSF ya kutoa elimu na kuandikisha wanachama Mkoani mbeya ili kuongeza wigo wa wanachama.
   Meneja wa NSSF Mkoa wa mbeya, Robert Kadege akimsaidia mmoja wa Madereva wa Bodaboda kujaza fomu ya NSSF kwa ajili ya Kumuandikisha kujiunga na NSSF.
   Meneja Kiongozi Masoko na uhusiano wa NSSF Eunice Chiume na Meneja wa Mkoa wa Mbeya Robert Kadege wakitoa elimu kwa dereva wa daladala mkoani Mbeya kwenye kampeni maalumu ijulikanayo kama NSSF Kwanza iliyolenga kuwafikia watu walio kwenye sekta binafsi ili wajiunge na NSSF.
  Wananchi: Wananchi wa Mkoa wa Mbeya wakiwa wamekusanyika kwenye banda la NSSF ili kupata elimu na kujiandikisha na Mfuko huo eneo la stendi ya Magari ya Mbalizi Mkoani Mbeya.

  0 0

  1
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na wabunge muda mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015
  2
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Spika Mstaafu Mhe Pius Msekwa huku Spika Mstaafu mwingine Mhe Anne Makinda akisubiri zamu yake muda mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015
  4
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na mmoja wa wabunge muda mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 201
  6
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Marais wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Mhe. Benjamin William Mkapa  muda mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015
  7
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na viongozi wakuu na wabunge muda  mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015
  8
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisikiliza kwa unyenyekevu mawaidha toka kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi muda mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015
  9
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa na Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein,  Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe  Pandu Ameir Kificho  muda mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015
  10
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa wakijichanganya na wabunge kwenye mchapalo muda  mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015
  11
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo Mhe Zitto Kabwe muda mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015
  12
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Mhe Anthony Diallo muda mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015
  14
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea na  wabunge na wageni waalikwa kwenye mchapalo  muda mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015. Ni hapo alipoamuru kwamba zaidi ya shilingi milioni 200 zilizochangwa na wafadhili kwa ajili ya mchapalo huo zitumike kwa kununulia vitanda vya wagonja katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
  17
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimshukuru Spika Job Ndugai  wakati anaondoka baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015. 
  18
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimshukuru na kumkabidhi cheti Mkurugenzi Mkuu wa PSPF  Bw.Adam Mayingu kwa mchango wao  kwenye mchapalo  muda mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015. 
  19
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimshukuru na kumkabidhi cheti mwakilishi wa Benki kwa mchango wao  kwenye mchapalo  muda mfupi baada ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015. 
  21
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipozi na badhi ya mabalozi wa nchi za Kiafrika waliokaribishwa kwenye hafla ya kuhutubia na kuzindua rasmi Bunge la 11 mjini Dodoma Jumamosi Novemba 20, 2015. 
  Picha na Muhidin Issa Michuzi wa Ikulu

  0 0

  01
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Sophia Simba kwenye Viwanja vya Bunge mjini Dodoma, wakati wa hafla fupi ya Coktail (Mchapalo) iliyofayika baada ya Rais Magufuli kulihutubia Bunge jana jioni Nov 20, 2015.
  02
  Waziri Mkuu wa awamu ya Tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa, akizungumza jambo na Rais staafu wa awamu ya sita wa Zanzibar, Aman Abeid Karume, wakati wa hafla fupi ya Coktail (Mchapalo) iliyofayika baada ya Rais Magufuli kulihutubia Bunge jana jioni Nov 20, 2015 kwenye Viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
  03
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na baadhi ya Viongozi wakati wa hafla fupi ya Coktail (Mchapalo) iliyofayika baada ya Rais Magufuli kulihutubia Bunge jana jioni Nov 20, 2015 kwenye Viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
  04
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Waziri Mkuu mstaafu, Joseph Warioba wakati wa hafla fupi ya Coktail (Mchapalo) iliyofayika baada ya Rais Magufuli kulihutubia Bunge jana jioni Nov 20, 2015 kwenye Viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
  05
  Rais Magufuli (katikati) akizungumza jambo na Rais wa Zanzibar, Mohamed Ali Shein (kushoto) na Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, wakati wa hafla fupi ya Coktail (Mchapalo) iliyofayika baada ya Rais Magufuli kulihutubia Bunge jana jioni Nov 20, 2015 kwenye Viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
  06
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Mbunge wa Shinyanga mjini, Stephen Masele, wakati wa hafla fupi ya Coktail (Mchapalo) iliyofayika baada ya Rais Magufuli kulihutubia Bunge jana jioni Nov 20, 2015 kwenye Viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
  07
  Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza jambo na baadhi ya viongozi wakati wa hafla fupi ya Coktail (Mchapalo) iliyofayika baada ya Rais Magufuli kulihutubia Bunge jana jioni Nov 20, 2015 kwenye Viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
  08
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na mmoja kati ya wageni waalikwa wa Kimataifa, wakati wa hafla fupi ya Coktail (Mchapalo) iliyofayika baada ya Rais Magufuli kulihutubia Bunge jana jioni Nov 20, 2015 kwenye Viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
  09
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Vijana wa UVCCM, wakati wa hafla fupi ya Coktail (Mchapalo) iliyofayika baada ya Rais Magufuli kulihutubia Bunge jana jioni Nov 20, 2015 kwenye Viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
  010
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Gallawa, Spika wa Bunge, Job Ndugai na Katibu wake, baada ya hafla fupi ya Coktail (Mchapalo) iliyofayika baada ya Rais Magufuli kulihutubia Bunge jana jioni Nov 20, 2015 kwenye Viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
  Picha na OMR

  0 0

  XX1
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa  Kaimu Mkurugenzi wa mamlaka ya Mji Mkongwe wa Zanzibar Nd,Mussa Awesu Bakari wakati alipokuwa akiangalia ramani ya Mradi wa ujenzi wa Ukuta wa Forodhani Mjini Unguja leo akiwa katika ziara maalum ya kutembelea maendeleo ya Miradi mbali mbali Mjini.
  XX2
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akimuuliza suala Kaimu Mkurugenzi wa mamlaka ya Mji Mkongwe wa Zanzibar Nd,Mussa Awesu Bakari wakati alipokuwa akiangalia   Mradi wa ujenzi wa Ukuta wa Forodhani Mjini Unguja leo akiwa katika ziara maalum ya kutembelea maendeleo ya Miradi mbali mbali Mjini,
  XX3
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akipata maelezo ya ramani ya ujenzi wa Mtaro wa maji ya Mvua katika viwanja wa mnazi mmoja kutoka kwa Mhandisi wa Manispaa ya Zanzibar Mzee Khamis Juma wakati alipotembelea mradi huo wa ujenzi unaojengwa na kampuni ya CRJ kutokaChina,
  XX4XX5

  0 0

   Mc katika kongaman0 la Mabadiliko ya Tabianchi kutoka Oxfam Tanzania Suhaila Thawer akiendelea kutoa utaratibu
   Eva Mageni  ambaye ni Rais wa wakulima wanawake vijijini na alikuwa mshiriki wa shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015, akifungua kongamano la Mabadiliko ya Tabianchi ambapo alizungumzia kwa kifupi kuhusu mkutano wa COP21 ambao utafanyika Paris Ufaransa hivi karibuni.
   Edward Tunyone kutoka Forum CC akieleza maana zaidi ya Mabadiliko ya Tabianchi ambapo alielekeza mazungumzo yake katika majanga asilia, mito kupotea kutokana na shughuli za wanadamu kama kulima jirani na maeneo hayo, mwisho alisisitiza swala la mabadiliko ya Tabianchi ni jukumu la kila mtu na taasisi zinazohusika na mamswala hayo tu.
   Bi Mwindiwe makame aliyekuwa mshiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula kutoka Zanzibar, akiendelea kueleza maana ya Mabadiliko ya Tabianchi alisisitiza kutunza mazingira.
   Denis Allan kutoka Norwegian Church Aid Actalliance akielezea umuhimu wa kutunza miti.
   Kikundi cha Ngonjela wakiendelea Kuburudisha
   Kushoto ni Mtaalam wa Mitandao ya kijamii toka Forum CC akitoa maelekezo ya shindano la Instagram
   Kikundi cha Ngoma kikitumbuiza
   Aliyewahi kuwa Mshindi wa Mama Shujaa wa Chakula 2012 St.Matha akielezea jambo kuhusiana na mabadiliko ya Tabianchi
   Bw. Gambaedya P.M kutoka Tume ya Ardhi akitoa somo juu ya kilimo hifadhi
   Bi.Tatu Kayumbu kutoka Wizara ya Kilimo akieleza ushirikiano wa kilimo na utunzaji wa Mazingira
   Kundi la Youth can wakiendelea kutumbuiza
   Meneja wa Kampeni Haki ya Uchumi kutoka Oxfam Eluka Kibona akitoa mwongozo wa kikao
   Mkutano wa Forum CC ukiendelea
   Baadhi ya washiriki wakijadili Michoro ambayo walipewa kazi ya kuipitia na kuijadili.
   Baadhi ya washiriki wakielezea michoro waliyopewa kuielezea
  Kushoto ni Mkurugenzi mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akijumuika na wananchi wengine katika Kongamano la Mabadiliko ya Tabianchi
   Baadhi ya waliokuwa washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula kwa nyakati tofauti wakionesha bidhaa zao
  Kushoto ni mmoja wa washiriki waliohudhulia kongamano la mabadiliko ya Tabianchi akipokea zawadi ya tsh 100,000 aliyoshinda Steven Albert.
  Baadhi ya washiriki katika Kongamano la Mabadiliko ya Tabianchi

  *******
  ASASI za Kiraia nchini zikiwemo Oxfam Tanzania, Forum CC na Norwegian Church Aid Actalliance  zafanya kongamano  la Kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa Chakula nchini.

  Akizungumza  Afisa Miradi Msaidizi wa Shirika la Forum CC,Jonathan Sawaya alisema asasi hizo zimeona ni vema kuwakilisha sauti za wakulima  kwa serikali katika kuhakikisha hatua stahiki zinachukuliwa katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi.

  Alisema  asilimia kubwa ya wakulima wengi hasa wanawake ambao karibia asilimia 70 wamekuwa wakiathirika na Mabadiliko hayo wakati wanapolima.

  Sawaya alisema  wananchi wanapaswa kuhifadhi mazingira na kutunza vyanzo mbalimbali vya maji  ili kupunguza athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.

  "Kwa kushirikiana  na shirika la Oxfam pamoja na Norwegian Church Aid  tumeamua kufanya kongamano hili ili kupaza sauti za wakulima na wafugaji katika suala zima la kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na serikali kutilia mkazo katika kusimamia suala hili kwa kuongeza bajeti,"alisema Sawaya.
  Aidha alisema asilimia kubwa ya wanawake wameonyesha juhudi mbalimbali za kukabiliana na athari hizo kutokana na wao kujihusisha katika uzalishaji wa chakula.

  "Tuwaunge mkono wazalishaji wa chakula wadogo,wafugaji pamoja na wavuvi  katika suala hili kwa kuwaunganisha na masoko na kuwapa mikopo,"alisema

  Aidha Kongamano  hili limehusisha wadau mbalimbali wakiwemo watendaji wa serikalini,wakulima pamoja na wafugaji katika kuhakikisha mabadiliko ya tabia nchi yanatokomezwa.

  "Kongamano hili ni sehemu ya maandalizi ya  Mkuu wa  21 wa Mkutano wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi unaotarajia kufanyika Novemba 30 nchini Ufaransa,"alisema Sewaya

  0 0

  Wachezaji wa timu ya soka ya Panone fc wakipasha misuli moto kabla ya kuanza kwa mchezo wa ligi ya shirikisho inayodhaminiwana Azam.
  Wachezaji wa timu ya Polisi Dar wakipasha misuli moto kabla ya kuanza kwamchezo wa ligi ya shirikisho hidi ya Panone fc mchezo uliopigwa katika uwanja wa Chuo cha Ushirika.
  Kocha wa timu ya soka ya Panone fc,Atuga Manyundo akizungumza na Azam TV iliyokuwa ikirusha mchezo huo moja kwa moja.
  Wapiga picha wa Azam Tv wakiweka sawa mitambo yao kwa ajili ya kurusha live mchezo huo.
  Vikosi vya timu za Polisi Dar na Panone fc vikiwa tayari kuingia uwanjani.
  Vikosi vikiingia uwanjani.
  Panone fc
  Polisi Dar.
  Wachezaji wa timu hizo wakisalimiana.
  Benchi la Polisi Dar.
  Benchi la Panone fc.
  Kikosi cha Panone fc.
  Waamuzi wa mchezo uo.
  Camera maalum aina ya Drone akipiga picha za juu katika uwanja wa Ushirika wakati wa mchezo wa ligi ya Shirikisho kati ya Panone fc na Polisi Dar.
  Azam Tv walikuwa live kurusha mchezo huo.
  heka heka katika mchezo huo.
  Panone fc wakishangilia baada ya kupata bao la kwanza.
  Heka heka.
  Heka heka langoni mwa timu ya Polisi Dar.
  Wachezaji wa Polisi Dar wakishangilia mara baada ya kusawazisha bao.
  Panone fc wakifanya mabadiliko ,mchezaji Pompy akinngia.
  Baadhi ya Mashabiki waliojitokeza katika mchezo huo.
  Figisu figisu ilipotokea uwanjanihapa kidogo wachezaji wa timu zote mbili akioneshana msuli.
  Mmoja wa wachezaji wa timu ya Panone fc akiwa chini akisikilizia maumivu baada ya kuchezewa vibaya na mchezaji wa Polisi Dar.
  Mchezaji wa Panone fc akipewa msaada wa huduma ya kwanza mara baada ya kuchezewa vibaya.
  Mlinzi wa timu ya Panone fc Pompy akijaribu kumiliki mpira.
  Aliyekuwa Kocha wa timu ya soka ya JKT Ruvu ,Felix Minziro akiwa katika uwanja wa Ushirika akifuatilia mchezo kati ya timu ya Panone fc na Polisi Dar ,
  Moja ya heka heka langoni mwa timu ya Panone fc.
  Pompy akijaribu kumzuia msgambuliaji wa timu ya Polisi  Dar,
  Mwamuzi wamchezo huo ,Nathan akiashiria kumalizika kwa dakika 90 za mchezo huo.
  Mwisho wa mchezo Panone fc 2 Polisi Dar 1.
  Waamuzi wakitoka uwanjani.
  Wazee wa kubeti nao hao hawako nyuma sasa hivi wanatembea na mashine zao hadi katika viwanja vya michezo.
  Wapiga picha wa Azam Tv wakichukua matukio mbalimbali.

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  0 0

  m1
  Mke wa Waziri  Mkuu, Mama Mary Majaliwa  (kushoto) akikaribishwa na mke wa Waziri Mkuu, Mstaafu Mama Tunu Pinda wakati alipowasili nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda katika kijiji cha  Zuzu nje kidogo ya mji wa Dodoma kwa mazungumzo Novemba 21, 2015  .
  m2
  Mke wa Waziri  Mkuu, Mama Mary Majaliwa  (kushoto) akikaribishwa na mke wa Waziri Mkuu, Mstaafu Mama Tunu Pinda wakati alipowasili nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda katika kijiji cha  Zuzu nje kidogo ya mji wa Dodoma kwa mazungumzo Novemba 21, 2015  .
  m3
   Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majliwa  akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda wakati alipomtembelea nyumbani kwake katika kijiji cha Zuzu, nje kidogo ya mji wa Dodoma Novemba 21, 2015.
  m4
   Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majliwa  akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda wakati alipomtembelea nyumbani kwake katika kijiji cha Zuzu, nje kidogo ya mji wa Dodoma Novemba 21, 2015.
  m5
   Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa na mkewe Mary (wapili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mkuu,Mstaafu Mizengo Pinda na mkewe Tunu (kulia) Wakati Waziri Mkuu alipomtembelea Waziri Mkuu Mstaafu, nyumbani kwake katika kijiji cha Zuzu nje kidogo ya mji wa Dodoma Novemba 22, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  o1
  Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori akizungumza wakati akifungua kongamano la waajiri wa Taasisi mbalimbali ikiwemo za Kiserikali na zisizokuwa za kiserikali zilizokuwa na makao makuu yake mkoani Dar es Salaam lililofanyika jana mkoani Tanga kwenye hotel ya Tanga Beach,Picha na Mwandishi Wetu.
  o3
  Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori akizungumza wakati akifungua kongamano la waajiri wa Taasisi mbalimbali ikiwemo za Kiserikali na zisizokuwa za kiserikali zilizokuwa na makao makuu yake mkoani Dar es Salaam lililofanyika jana mkoani Tanga kwenye hotel ya Tanga Beach,Picha na Mwandishi Wetu.
  o4
  Meneja Matekelezo na Kumbukumbu wa NSSF Makao Makuu,Maryam Muhaji akizungumza kwenye kongamano la waajiri wa Taasisi mbalimbali ikiwemo za Kiserikali na zisizokuwa za kiserikali zilizokuwa na makao makuu yake mkoani Dar es Salaam lililofanyika mkoani Tanga kwenye hotel ya Tanga Beach,Picha na Mwandishi Wetu.
  o5
  Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa kongamano la waajiri wa Taasisi mbalimbali ikiwemo za Kiserikali na zisizokuwa za kiserikali zilizokuwa na makao makuu yake mkoani Dar es Salaam lililofanyika mkoani Tanga kwenye hotel ya Tanga Beach,Picha na Mwandishi Wetu.
  o6
  Baadhi ya Washiriki wakiwa kwenye kongamano la waajiri wa Taasisi mbalimbali ikiwemo za Kiserikali na zisizokuwa za kiserikali zilizokuwa na makao makuu yake mkoani Dar es Salaam lililofanyika mkoani Tanga kwenye hotel ya Tanga Beach wakimsikiliza Mgeni Rasmi Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori,Picha na Mwandishi Wetu.

  0 0

  D4
  Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na Madaktari wa kujitolea kutoka Hispatinia mara baada ya Chakula cha usiku alichowaandalia kwa lengo la kuwashukuru kutokana na mchango wao mkubwa wanaoutoa katika sekta ya Afya Zanzibar, hafla hiyo ilifanyika Hoteli ya Ocean View.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar
  D1
  Profesa Jose Pinquet kulia akitambulisha Timu ya Madaktari wanaotoa huduma za Matibabu ya Uti wa Mgongo na Ubongo katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi mmoja kwa Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo.
  D2
  Baadhi ya Madaktari wanaotoa huduma za Matibabu ya Uti wa Mgongo na Ubongo katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi mmoja wakipata Cahakula cha Usiku kilichoandaliwa ni Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo.
  D3
  Profesa Jose Pinquet akizungumza mara baada ya Chakula cha usiku kilichoandaliwa kwa ajili yao ambapo pia alishukuru mashirikiano wanayopewa na Madaktari Wazawa katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Ocean View.


  0 0

  c1
  Mkuu wa Chuo cha Habari Zanzibar Dkt. Aboubakar Rajab akitoa hutuba ya ufunguzi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Ally Mwinyikai katika Mkutano Mkuu wa Wadau wa Jumuiya ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) uliofanyika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean mjini Zanzibar ambapo alisitiza wanahabari kuzingatia maadili ya kazi zao. Kulia ni Katibu wa Tume ya Utangazaji Zanzibar Chande Omar na kushoto ni Mwenyekiti wa ZPC Abdallah Mfaume.
  c2
  Katibu wa Tume ya Utangazaji Zanzibar Chande akitoa Mada ya umuhimu wa kuzingatia Maadili kwa Wanahabari katika fani yao.
  c3
  Makamu wa Rais wa Chama cha Siasa ADA-TADEA akichangia katika Mkutano wa Wadau wa Mkutano wa Wadau wa ZPC uliofanyika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean mjini Zanzibar.
  c4
  Mkulima kutoka kikundi cha Ushirika cha Bambi Mwaka Saburi akichangia katika Mkutano wa Wadau wa ZPC uliofanyika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean mjini Zanzibar ambapo alishauri Wanahabari kuandika zaidi habari za Vijijini bada ya mijini pekee.
  c5
  Katibu wa Jumuiya ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) Faki Mjaka akisoma maazimio ya Mkutano wa Wadau wa ZPC uliofanyika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean mjini Zanzibar.
  c6
  Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa Wadau wa Zanzibar Press Club ZPC wakiwa katika Picha ya pamoja na Mgeni rasmi wa Mkutano huo Dkt. Aboubakar Rajab wakatikati waliokaa huko Hoteli ya Zanzibar Ocean mjini Zanzibar.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar 

  …………………………………………………………………………………………
  Na Maelezo Zanzibar
  Wanahabari wametakiwa kuendelea kutii Sheria zilizopo zinazoongoza mwenendo wa utoaji wa habari nchini, huku Taasisi za kihabari zikiendelea kufuatilia upatikanaji wa sheria Bora za habari zinazoendana na wakati uliopo.

  Hayo yameelezwa na Katibu wa Tume ya Utangazaji Zanzibar Chande Omar alipokuwa akiwasilisha Mada katika Mkutano Mkuu wa Wadau wa Jumuiya ya Waandishi wa Habari Zanzibar ZPC uliofanyika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean mjini Zanzibar.

  Amesema licha ya kuwepo kwa baadhi ya Sheria za habari zilizopitwa na wakati, ni vyema Wanahabari kuziheshimu na kuzitii huku juhudi mbalimbali zikifanywa na Wadau kuondoa Sheria hizo.

  Chande amefahamisha kuwa Taasisi kama Vile Baraza la Habari Tanzania, Tume ya Utangazaji na Jumuiya ya Waandishi wa Habari Zanzibar ZPC ni miongoni mwa Taasisi ambazo zinafanya kazi za kuwepo kwa Sheria zinaendana na wakati kwa maslahi mapana ya Taifa.

  Aidha katika Mkutano huo uliojumuisha Washiriki kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali na Binafsi maazimio mbalimbali yalipitishwa ikiwemo Wamiliki wa Vyombo vya Habari na Waaandishi kwa ujumla kuzingatia Weledi katika utekelezaji wa majukumu yao.

  Azimio jingine ni kuhakikisha kuwa Taasisi kama Vile Baraza la Habari Tanzania, Tume ya Utangazaji na Jumuiya ya Waandishi wa Habari Zanzibar ZPC zinashiriki kikamilifu katika kuhamasisha upatikanaji wa Maslahi bora kwa Wanahabari ili kuwaepusha kupokea Zawadi kutoka Vyanzo vya habari ambazo hupelekea kukiuka maadili yao.
  Aidha wameazimia kujiepusha na Ushabiki wa Kisiasa ili kuepuka upendeleo wa habari wanazojitoa kwa jamii.

  Mmoja wa Wachangiaji kutoka Jumuiya ya Wakulima Mpwapwa amewaomba Waandishi wa habari kuandika pia habari za watu wa shamba badala ya kuandika habari zinazohusu watu wa mijini pekee.
  Ametoa mfano kwamba katika uchaguzi Mkuu uliopita habari zilizoandikwa zilihusu Watu wa Mijini ambapo kwa  upande wa Vijijini Waandishi walishindwa kuonekana kwenda kuchukua habari.

  Hata hivyo Washiriki wa Mkutano huo pia Waliafiki wazo hilo na kuazimia kufanya kazi kizalendo na kushirikisha makundi yote ya kijamii ikiwemo kuandika habari za Vijijini ili kuibua Fursa na changamoto zinazowakabili.
  Akitoa hutuba ya Ufunguzi Mkuu wa Chuo cha Habari Zanzibar Dkt. Aboubakar Rajab kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Ally Mwinyikai alisisitiza wanahabari kuzingatia maadili ya kazi zao ili waheshimike katika jamii.
  Amesema kukosekana kwa Maadili ya Habari hupelekea Migogoro mingi ikiwemo kuzalisha chuki na fitna miongoni mwa jamii husika.

  Jumuiya ya Waandishi wa Habari Zanzibar hufanya Mkutano Mkuu wa Wadau wake kila mwaka na kujadili mada kulingana na wakati husika ambapo katika Mkutano huo Walijadili umuhimu wa Waandishi kuzingatia Maadili katika kupatikana uchaguzi huru na Wahaki.

  0 0

   Wadau waandamizi wa Globu ya Jamii Archbold Josaphat Kiwia na Agnes Samwel Likongo wamemeremeta leo katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam. Wadau hawa, ambao ni wafanyabishara maarufu wa mbao, hivi sasa wanaelekea hoteli ya Serena kwa mnuso wa nguvu waliouandaa. Globu ya Jamii inawatakia Archbold na Agness maisha mazuri na ya furaha!
   Bwana harusi amvisha pete mkewe
   Bi Harusi amvisha pete mumewe 
   Archbold akimwaga wino
  Agness naye anamwaga wino

  0 0


  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Agizo alilolitoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli la kutaka fedha zilizochangwa na wadau mbalimbali kwa ajili ya kugharamia hafla ya wabunge zipelekwe Katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kununulia vitanda na magodoro ya wagonjwa wanaolala chini limetekelezwa.

  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema fedha hizo zimefanikisha kupatikana vitanda 300 vya wagonjwa pamoja na magodoro yake, shuka 600, Baiskeli za kubebea wagonjwa na vifaa vingine na kwamba hivyo vyote tayari vimepelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

  Balozi Sefue ameuagiza uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha vitanda vyote vinafungwa kesho jumapili na kwamba atakwenda kuvikagua siku ya jumatatu vikiwa tayari vinatumiwa na wagonjwa waliokua wanakosa vitanda vya kulalia na kulazimika kulala chini.

  Wadau mbalimbali walichanga fedha kiasi cha shilingi milioni 225 kwa ajili ya kugharamia hafla ya wabunge baada ya uzinduzi rasmi wa bunge la 11 lakini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli aliagiza fedha hizo zitumiwe kwa kiasi kidogo kisichozidi shilingi milioni 15 na nyingine zipelekwe hospitali ya Muhimbili kutatua tatizo la uhaba wa vitanda.

  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano IKULU,

  Novemba 21, 2015.

  0 0

   Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, (hawapo pichani), ambapo aliwaeleza kuwa amefungua kesi ya kupinga matokeo ya ubunge wa Jimbo la Temeke,ili haki ipatikane. Kushoto ni Katibu wa Jimbo la Temeke,  Kassim Kiame.

  Walioshitakiwa ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, ambaye pia ni Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Temeke, Protidas Kagimbo Mbunge aliyeshinda, Abdallah Mtolela na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, (PICHA NA KHAMIS MUSSA)


  0 0

  Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake na Katiba na Uchaguzi, Profesa Ruth Meena (kushoto) akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania. Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake na Katiba na Uchaguzi, Profesa Ruth Meena (kushoto) akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania.Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Wanawake Tanzania, Mary Rusimbi (kushoto) ambaye ni mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba na Uchaguzi akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake na Katiba na Uchaguzi, Profesa Ruth Meena. Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Wanawake Tanzania, Mary Rusimbi (kushoto) ambaye ni mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba na Uchaguzi akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake na Katiba na Uchaguzi, Profesa Ruth Meena.
  huku ikiwa nautekelezaji wa vitendo na kwa uhakika," alisisitiza Bi. Rusimbi.Mjumbe wa Mtandao huo, Dk. Ave-Maria Semakafu (kulia) akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo jijini Dar es Salaam. Mjumbe wa Mtandao huo, Dk. Ave-Maria Semakafu (kulia) akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania akisisitiza jambo kwenye mkutano na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Wanawake Tanzania, Mary Rusimbi na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake na Katiba na Uchaguzi, Profesa Ruth Meena. Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania akisisitiza jambo kwenye mkutano na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Wanawake Tanzania, Mary Rusimbi na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake na Katiba na Uchaguzi, Profesa Ruth Meena.
  Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia mkutano wao na viongozi wa Mtandao wa Wanawake na Katiba na Uchaguzi leo jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia mkutano wao na viongozi wa Mtandao wa Wanawake na Katiba na Uchaguzi leo jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia mkutano wao na viongozi wa Mtandao wa Wanawake na Katiba na Uchaguzi leo jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia mkutano wao na viongozi wa Mtandao wa Wanawake na Katiba na Uchaguzi leo jijini Dar es Salaam 


  MTANDAO wa Wanawake na Katiba na Uchaguzi umeitaka Serikali ya Awamu ya Tano iliyopo chini ya Rais Dk. John Pombe Magufuli ijenge misingi imara itakayoondoa mazingira kandamizi kwa jamii ya chini hasa kwa akinamama. Aidha umeitaka serikali kuhakikisha inasimamia ipasavyo suala zima la uwajibikaji na kupambana na vitendo vya kifisadi ambavyo ndivyo vinavyowakandamiza wananchi.

   Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na jopo la viongozi wanaounda mtandao huo likiongozwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Mtandao, Profesa Ruth Meena walipokuwa wakitoa tathmini juu ya mtazamo wa mtandao huo baada ya Uchaguzi Mkuu na suala zima la usawa wa jinsia kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari. 

   Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Wanawake Tanzania, Mary Rusimbi ambaye ni mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba na Uchaguzi alisema serikali ya awamu ya tano ina kila sababu ya kumjali mwanamke na kutambua kuwa anamchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi. Alisema Serikali hainabudi kujenga misingi imara ya uwajibikaji wa kweli na kutambua makundi mbalimbali ya jamii kwa jinsia zote. "...Tunataka haki yetu iwe haki kweli kweli na itambulike 

  Alisema kuwa wangependa kushuhudia idadi ya kutosha ya wanawake inaingia katika ngazi mbalimbali za uongozi na vyombo vya maamuzi ili waweze kuingiza changamoto zao na kuzisemea ipasavyo kwa lengo la kupatiwa ufumbuzi. Kwa upande wake Prof. Meena akizungumzia mtazamo wa mtandao baada ya Uchaguzi Mkuu juu ya ushirikishwaji wa wanawake katika kugombea nafasi anuai za uongozi alisema bado kuna changamoto kubwa kwa kundi hilo kwani kulingana na matokeo ya sasa Tanzania itafikia usawa wa 50/50 mwaka 2055. 

   Alisema licha ya ongezeko la fursa ya vitimaalum kupandishwa hadi kufikia asilimia 40 bado fursa hizo zinachangamoto kubwa kwani viti hivyo ndani ya vyama hutolewa kwa wanawake kama aina fulani ya zawadi jambo ambalo huwazuia wanawake hao kusimamia ajenda zao za msingi kwa kuhofia kuonekana wasaliti. "...Viti hivi maalum hutolewa na vyama na vyama ndio vyenye ushawishi na misimamo hivyo wanawake hawawezi kusimamia hoja zao ipasavyo...," alisema Prof. Meena. 

  Aidha Profesa Meena alivitaka vyombo vya habari kusaidia kubeba ajenda za wanawake na kukemea mfumo dume ili kuibadili jamii ambayo bado inamtazamo hasi juu ya wanawake na uwezo wao. Alisema wanawake walijitokeza kwa wingi katika uchaguzi huu licha ya kwamba ndani ya vyama vyao bado kuna aina fulani ya ugumu katika kuwapa nafasi kundi hilo. 

   Naye Mjumbe wa Mtandao huo, Dk Ave-Maria Semakafu aliitaka serikali kuendelea kuondoa vikwanzo na changamoto mbalimbali katika jamii ambazo bado zinamtesa mwanamke. Alisema huduma za elimu bado mtoto wa kike anachangamoto jambo ambalo linamnyima kufikia malengo yake huku huduma nyingine za maji na utafutaji wa nishati ya kuni ikiwa ni mzigo kwa mwanamke. .Imeandaliwa na www.thehabari.com

  0 0

  Parliament_chamber01Bunge la Jamhuri ya Muungano.

  Nawasalimu nyote katika jina la nchi yetu Tanzania, Mimi ndugu yenu sijambo, naendelea kusukuma mbele gurudumu la maendeleo kujenga nchi yetu. Nawapongezeni sana kwa ushindi mkubwa mlioupata ambao leo umewawezesha kutuwakilisha Watanzania wote katika Bunge la Jamhuri ya Muungano, muhimili namba mbili katika nchi yetu. Najua mmepita katika safari ndefu, wengi wenu mna majeraha, hayo yote yamepita, sasa ni kazi moja tu; kuwawakilisha vyema wananchi waliowatuma ili muweze kulisogeza taifa letu mbele kwa kuisimamia vyema serikali na zoezi zima la utungaji wa sheria. 

  Nawapongezeni sana kwa uchaguzi wa Spika Mheshimiwa Job Ndugai, Naibu Spika Mheshimiwa Dk. Tulia Mwansasu na pia Mheshimiwa Waziri Mkuu wa 10 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Majaliwa Kassim Majaliwa. Hongereni sana. Najua mtawakumbuka sana wabunge wenzenu ambao hawakupata nafasi ya kurejea bungeni, kama David Kafulila, kijana aliyejitolea kwa nguvu zake zote na hata kuhatarisha maisha yake mwenyewe katika Sakata la Escrow, lakini wananchi wa jimbo lake wakamuona alikuwa mbunge wa taifa si mbunge wao, wakamkata. 

  Pia mtawakumbuka sana wabunge walioaga dunia kama Deo Filikunjombe, Dk. Abdallah Kigoda, Celina Kombani, Kapteni John Komba, Mariam Mfaki, Clara Diana Mwatuka, Mungu azilaze roho zao mahali pema peponi, ni vyema mkasimama hata kwa dakika moja kuwakumbuka na ninamwomba Mungu wa Mbinguni, atuinulie watu wengine kama wao katika Bunge hili, watakaokuwa tayari kusimama kidete kutetea maslahi ya wanyonge. 

  Baada ya kusema hayo nielezee dhumuni la kuwaandikia barua yangu, kwani imekuwa ni desturi yangu sasa kuandika barua moja kila wiki, naandika barua hii kuwakumbusheni juu ya jukumu lililowapeleka Dodoma na matarajio ya wananchi waliowatumeni kazi, najua mnafahamu lakini si jambo baya kukumbushana ili asiwepo mtu atakayedhani amekwenda Dodoma kufaidi maisha, akabweteka kwa sababu ya heshima anayoipata hivi sasa kama mbunge, miaka mitano si karne, 2020, mtakutana na wananchi kwenye boksi la kura, yasije yakawapata yaliyowapata ambao hawakurejea. 

  Ndugu zangu waheshimiwa wabunge wa Jamhuri ya Tanzania, Mmepata bahati ya kuwa wabunge wa kwanza wa Bunge la 11 la awamu ya tano chini ya Rais Dk. John Pombe Magufuli, mmeupata ubunge katika kipindi ambacho uchumi wa nchi yetu katika robo ya pili ya mwaka 2015 unakuwa kwa kasi ya asilimia 7.9, hii ni kasi nzuri kwani kuanzia mwaka 2002 -2014 uchumi wa taifa hili hili ambao ninyi ni wabunge wake ulikuwa ukikua kwa wastani wa asilimia 6.72. Waheshimiwa wabunge, Wakati uchumi wa nchi yetu ukikua kwa asilimia 7.9, nchi nyingi za Afrika zinasuasua sana nyuma yetu, kasi ya ukuaji wa uchumi wetu kwa mujibu wa taarifa za benki ya dunia umezidi mataifa makubwa duniani kama China ambayo uchumi wake umekuwa kwa asilimia 6.9 tu!


   Na India ni asilimia 7, kwangu mimi hii ni dalili nzuri inayonyanyua matumaini yangu kwamba, hata kama hali ni mbaya hivi sasa, kama serikali itasimamiwa vizuri na Bunge ambalo ninyi ni wabunge wake, hakika tumekaribia kufika katika nchi ya ahadi. Kwa nini nimeamua kuwaandikia barua hii? Waheshimiwa wabunge, pamoja na takwimu zote zilizoko hapo juu ambazo zinaashiria mema huko tuendako, ni ukweli ulio wazi kwamba ukuaji wa uchumi wetu haujaonekana kwenye meza ya chakula na maisha ya Mtanzania wa kawaida. Katika nchi yetu yenye jumla ya watu wasiopungua milioni 48, milioni 12 kati yao bado wanaishi katika umaskini mkubwa, hizi ni takwimu za mwaka 2015!

   Huduma za afya bado ni mbaya, watu wengi wanakufa kwa magonjwa yanayoweza kutibika, elimu yetu bado ni duni, watumishi wetu wa umma bado hawalipwi vizuri na wamevunjika moyo, huduma za maji na umeme vijijini bado ni duni, vifo vya akina mama na watoto bado viko juu. Sarafu yetu inazidi kuporomoka, imeshuka kwa karibu asilimia ishirini ikilinganishwa na thamani ya dola ya Kimarekani!

   Jambo ambalo limesababisha kupanda katika bei ya vitu vinavyoagizwa nje ya nchi na kufanya mfumuko wa bei ambao mwaka 2011 ulikuwa asilimia 20 ukashuka mpaka asilimia 4 , Juni 2015, upande tena mpaka asilimia 6.4 jambo ambalo limechangiwa pia na kupanda kwa vyakula. Waheshimiwa wabunge mnaingia bungeni Tanzania ikiwa na tatizo kubwa sana la ajira, takwimu zikionyesha kwamba karibu nguvu kazi ya vijana 800,000 huingia sokoni kila mwaka, soko ambalo halina ajira kwa ajili yao! 

  Hili ni tatizo kubwa sana kwa taifa kama Tanzania ambalo vijana wake wengi wametegemezwa kuwa mara wamalizapo vyuo (ambazo hivi sasa ni vingi kila kona ya nchi) kutakuwa na ajira za kuwapa. Nawaandikieni barua hii kuwakumbusheni ndugu zangu juu ya jukumu kubwa mlilonalo kwa taifa na watu wenu, hakika haiko sababu ya ninyi kusherehekea kuwa wabunge, kwani ushindi wenu ndiyo mwanzo wa kazi kubwa mliyonayo mbele, ambayo kwa mtu mwenye uzalendo wa kweli kwa taifa lake ubunge ni mzigo. 

  Najua mmeingia Bungeni kwa kupitia vyama mbalimbali, wengine mmeteuliwa, najua mnazo tofauti mbalimbali, zikiwemo za dini, rangi, kabila na itikadi, nawaombeni sasa muweke tofauti zenu zote pembeni na kusimama pamoja kama wawakilishi wa watu ili kuisimamia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vyema iweze kutimiza majukumu yake.

   Kuendelea kusimama na U-CCM, U-Chadema, U-Cuf, U-NCCR MAGEUZI, hakika hakutaisaidia lolote Tanzania yetu na watu wake, hivi sasa ninyi ni wawakilishi wa Watanzania, simamieni maslahi ya watu wa taifa hili na maslahi ya taifa kwa ujumla wake. Mnapoingia bungeni katika kipindi hiki ambacho taifa letu linakabiliwa na hali ngumu ya uchumi, kukiwa hakuna fedha za kutosha kujiendesha, si jambo jema hata kidogo kuendelea kugawanyika, umoja peke yake ndiyo utaweza kubadilisha mambo.

   Najua ninyi nyote ni wazalendo kwa taifa lenu, basi uonyesheni uzalendo wenu kwa vitendo ili kuhakikisha uwepo wenu Bungeni kwenye Bunge la 11 unakuwa ni wa kihistoria, wengi wenu ni vijana, matarajio yangu ujana, elimu na vipaji mlivyonavyo mtavitumia vizuri katika kuhakikisha vipaumbele vya taifa hili vinaandaliwa vyema kwa faida ya waliopo na watakaofuata baada ya sisi. Nasi tulioko huku nje ya Bunge hatutawaachia mzigo huu peke yenu, tutatimiza wajibu wetu kama Watanzania wawajibikaji.

   Tutapiga kelele kila tutakapoona mambo hayaendi sawa, ufisadi unafanyika hadharani na rasilimali za taifa hili zinatumiwa na watu wachache kwa faida yao wao na familia zao, huu kwetu utakuwa ni uzalendo kwa taifa ambalo tumeapa kulitetea wakati wote na kuvitetea vyama vyetu pale tu vinapostahili. Tanzania inasonga mbele, ilipo leo ni bora kuliko ilikokuwa jana, kama uchumi wetu ukiendelea kukua jinsi unavyokua kwa kasi, nina uhakika tutawapita waliokuwa mbele yetu wakiwa wamekaa! Hili halitakuja kama zawadi bali matokeo ya matendo yetu mema tutakayoyafanya, ninyi Bungeni na sisi huku nje ya Bunge, sote tuna wajibu wa kujenga taifa letu. 

  Baada ya kusema haya niwatakieni bunge jema lenye mafanikio na nimtakie Mheshimiwa Spika Job Ndugai hekima na Busara za kuliendesha bunge hili vizuri, vivyo hivyo kwa msaidizi wake, pia waziri mkuu wetu mpya ambaye ni msimamizi wa shughuli zote za serikali Bungeni, namtakia kila la kheri. Mungu ibariki Tanzania, Mungu libariki Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wabariki wabunge wote na wape moyo wa kizalendo na hekima za kuwafikiria wananchi wa taifa hili katika maamuzi yao. Wasalaam, Eric Shigongo James ............................................... BARUA KALI

  0 0older | 1 | .... | 691 | 692 | (Page 693) | 694 | 695 | .... | 1897 | newer