Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 690 | 691 | (Page 692) | 693 | 694 | .... | 1898 | newer

  0 0


  Ndugu Wasamaria wema,

  Napenda kutumia fursa hii kukushirikisha habari ya kusikitisha kuhusu dada Joyce Mwambepo (pichani akiwa na mwanaye wa miaka 4, na miguu yake iliyopooza) mkaazi wa Sinde jijini Mbeya. Dada huyu mwenye umri wa miaka 27 anaishi na bibi yake mwenye umri wa miaka 80 pamoja na huyo mwanaye.
  Kwa bahati mbaya mwezi April mwaka jana wa 2014 dada huyu alipata ajali ya kugongwa na gari ambayo haikusimama kumsaidia. Ila kwa msaada wa wasamaria wema alipelekwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa  Mbeya ambako inasemekana alikaa kwa miezi mitatu bila kupata matibabu, kwa kukosekana nyenzo za kumfanyia uchunguzi.
  Katika uchunguzi wa awali ilibainika kuwa Joyce amevunjika miguu yote miwili,  hivyo akahamishiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili ambako pia baada ya kukaa kwa miezi kadhaa alirejeshwa tena Mbeya baada ya kukosa shilingi 550,000/- za vipimo na matibabu.
  Hadi nakutana naye dada huyu alikuwa amelala nyumbani kwa bibi yake (pichani kushoto) ambaye ni mlezi wake tangu akiwa na miaka minne baada ya wazazi wake wote wawili kufariki dunia. 

  Hawezi kukaa wala kusimama na anajisaidia hapo hapo kitandani kwa msaada wa mwanaye huyp na bibi yake.  Inasikitisha.
  Hivyo nimejitahidi kufuatialia ili kujua mahitaji halisi lakini ili kumsaidia Joyce inatakiwa aanze mchakato (process)  upya za matibabu kuanzia hapa Mbeya referral Hospital  hadi Muhimbili jijini Dar es salaam.

  Gharama za matibabu ni kama ifuatavyo:
  1. shilingi 300,000/- za kupima CT-SCAN
  2. Shilingi 250,000/- za MRI
  3. Usafiri wa kutoka Mbeya-Dar kwa gari maalum la kukodi 700,000/-
  4. Gharama za msaidizi ambaye ni rafiki yake 300,000/-
  5. Chakula 450,000/- (Endapo watakaa hospitali mwezi mzima)
  6. Gharama za matibabu (CT-SCAN&MRI ni vipimo tu) 500,000/-
  7. Na mahitaji mengineyo wakiendelea kupata tiba 500,000/-

  Hivyo kwa kuanzia kiasi cha shilingi 3,000,000/- (milioni tatu) kinahitajika kumpunguzia mateso dada yetu huyu. Asante sana kwa moyo wako wa kujitoa na Mungu atakubariki.

  Deo Kakuru Msimu
  Msamaria mwema
  +255769 512 420

  Wakati huo huo kwa niaba ya Michuzi Media Group, Ankal amejitolea kusaidia uratibu wa kufanikisha matibabu ya dada Joyce. Hivyo unaweza kuwasiliana naye kwa email issamichuzi@gmail.com ama whatsapp namba +255 754 271266 kwa jina la Ankal.
  --------------------------------------
  UPDATES:
  Wasamaria wema kadhaa wamejitokeza kumsaidia dada Joyce. Hatuna uhakika kwamba wote wanapenda majina yao yawekwe hadharani, Ila tunapenda hadi sasa kukiri upokeaji wa Tshs:
  1. 505,000/-
  2. 50,000/-
  3.100,270/-
  4. 10,000/-
  5. 100,000/-
  6. 500,000/- (ahadi ya uhakika)
  7. 500,000/- (Michuzi Media Group)
  7. 800,000/-  (Kulipia gharama za vipimo vya CT Scan Regency Hospital mgonjwa atapofikishwa Dar es salaam).

  Hivyo ndiyo kusema jumla ya Tshs. 2,565,270/-  tayari zimekusanywa kumsaidia dada yetu huyu anayeteseka. Kwa niaba ya mgonjwa tunashukuru sana kwa msaada huo, hana cha kuwalipa zaidi ya kuwaombea kwa Mola mzidishiwe pale mlipopungukiwa.

  Pamoja na yote hayo, kiasi cha Tshs. 3,000,000/- za ziada zinahitajika kwa ajili ya kuhitimisha zoezi lote hili. Hiyo ikiwa ni gharama za usafiri, malazi ya mgongwa na wasaidizi wawili kwa mwezi mmoja (atapopelekwa Dar es salaam kwa vipimo na matibabu) ili kumsaidia. Hivyo michango zaidi inahitajika kumuokoa dada Joyce. KUTOA NI MOYO.

  Aidha, kwa kiasi kilichopatikan, mipango imeshafanywa kumpeleka dada Joyce katika hospitali ya rufaa ya Mbeya kwa uchunguzi mpya wa awali. Baada ya hapo tutawafahamisha nini kinachotakiwa kuendelea.


  Deo Kakuru Msimu
  Msamaria mwema
  +255769 512 420

  Wakati huo huo kwa niaba ya Michuzi Media Group, Ankal amejitolea sio tu kuchangia bali pia kusaidia uratibu wa kufanikisha matibabu ya dada Joyce. Hivyo unaweza kuwasiliana naye kwa email issamichuzi@gmail.com ama whatsapp namba +255 754 271266 kwa jina la Ankal.


  0 0

   Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Bw. Lanfang Liao (katikati) akimkabidhi jezi mmoja wa wawakilishi wa timu zinazoshiriki ligi daraja la kwanza ya StarTimes (SFDL) wakati wa hafla ya kukabidhi jezi hizo iliyofanyika jijini Dar es Salaam Jumatano. Kushoto akipiga makofi ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bw. Jamal Malinzi. (Picha na mpiga picha wetu).
   Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Bw. Lanfang Liao (Kushoto) akimkabidhi jezi mmoja wa wawakilishi wa timu zinazoshiriki ligi daraja la kwanza ya StarTimes (SFDL) wakati wa hafla ya kukabidhi jezi hizo iliyofanyika jijini Dar es Salaam Jumatano. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Ligi Kuu nchini, Bw. Boniface Wambura. (Picha na mpiga picha wetu)
  Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Bw. Lanfang Liao (Kulia) akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi jezi kwa timu za Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes (SFDL) iliyofanyika jijini Dar es Salaam Jumatano. Katikati ni ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bw. Jamal Malinzi na wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa TFF, Bw. Selestine Mwesigwa.
   (Picha na mpiga picha wetu).

  Na Mwandishi Wetu.
  KAMPUNI ya Urushaji wa Matangazo Kidijitali ya StarTimes ya Tanzania imekabidhi jezi kwa timu zinazocheza Ligi Daraja la Kwanza nchini Tanzania, ikiwa ni moja kati ya udhamini wa ligi hiyo ijulikanayo kama Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes (SFDL).


  Akizungumza na waandishi wakati wa kukabidhi jezi hizo jijini Dar es Salaam Jumatano, Kaimu Afisa Mkuu Mtendaji wa StarTimes Tanzania, Bw. Lanfang Liao alisema kuwa angependa kuona jezi hizo zinakuwa kama chachu ya kufanya vizuri kwa timu zote zinazoshiriki ligi hiyo msimu huu.
  “Kwanza napenda Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa ushirikiano huu wanaouonyesha kwetu kama StarTimes, lakini leo hii tunatoa jezi kwa timu za ligi hii ya daraja la kwanza ya StarTimes ikiwa ni sehemu ya udhamini wetu mbali na udhamini wa fedha za uendeshaji.”

  “Jezi hizi sasa ni kama chachu ya timu zote za ligi daraja la kwanza kuongeza bidii na kufanya vizuri katika ligi hii msimu huu ili kuvutia wadhamini wengi zaidi. StarTimes kupitia udhamini huu tunaamini tumefungua njia kwa wengine nao kujitokeza na pia kuinua ari ya timu hizi,” alisema Bw. Liao.
  Bw. Liao alisema kuwa kutokana na jitihada hizo angependa kuona wachezaji wanaocheza katika ligi hiyo wanacheza katika Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ na timu nyingine kubwa kimataifa.

  Kwa upande wake mwakilishi wa Timu zinazoshiriki ligi hiyo, Bw Masao Bwire, aliipongeza kampuni ya StarTimes kwa kujitokeza kuipiga jeki ligi hiyo ambayo imekuwa ikiendeshwa bila udhamini wowote kwa kipindi kirefu.

  Pamoja na hayo pia alilipongeza Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kwa jitihada zake za utafutaji wa wadhamini kwa lengo la kuinyanyua ligi daraja la kwanza nchini ambayo imekuwa ikizalisha wachezaji wanaocheza ligi kuu.

  “Naipongeza kampuni ya StarTimes kwa kujitokeza kudhamini ligi daraja la kwanza. Hii ni hatua kubwa kwa ligi hii, kwa kuwa imekuwa ikienda bila udhamini kwa muda mrefu. Kukosekana kwa udhamini kulikuwa kukisababisha timu kutojiendesha vizuri hasa katika masuala ya vifaa, kulipa wachezaji na viongozi posho, kusafiri mbali kwa ajili ya mechi na usajili. Tunashukuru sana hayo sasa yatabakia historia na tunawaomba wadau wengine wajitokeze kwani bado hitaji ni kubwa. Lakini pia naipongeza TFF kwa jitihada zake kubwa za kutafuta wadhamini ili kusaidia maendeleo ya ligi hii nchini,” alisema Bw. Bwire.

  Naye Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Bw. Jamal Malinzi aliishukuru kampuni ya StarTimes kwa ushirikiano inaoutoa ili kuhakikisha ligi hiyo inasonga mbele na kuziasa timu zinazoshirki ligi hiyo kuongeza jitihada na kufanya vizuri baada ya kupata msukumo huo toka StarTimes.

  “Napenda kuishukuru kampuni ya StarTimes kwa ushirikiano inaotuonyesha ili kuipeleka mbele ligi hii lakini pia naziasa timu zote zinazoshiriki ligi hii ya StarTimes ya Daraja la Kwanza kuongeza jitihada na kufanya vizuri katika msimu huu wa ligi. Pia ningependa kuwataka na nyinyi mfanye juhudi kutafuta wadhamini wengine kwani mnaweza kufanya hivyo ili kufanya ligi iwe na ushindani zaidi.” alihitimisha Bw. Malinzi.

  0 0

  Meneja Uhusiano wa kampuni ya TTCL, Nicodemus Thomas (wa pili kulia) akimkabidhi sehemu ya vifaa tiba Ofisa Muuguzi Mkuu wa Kituo cha Afya cha Buguruni, Alvera Mtembelea (wa tatu kushoto) vilivyotolewa na kampuni ya TTCL leo kwa Kituo cha Afya Buguruni cha jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Ofisa Uhusiano wa TTCL, Amanda Luhanga akishuhudia zoezi hilo.
  Meneja Uhusiano wa kampuni ya TTCL, Nicodemus Thomas (kulia) akimkabidhi moja ya mashine ikiwa ni sehemu ya vifaa tiba Ofisa Muuguzi Mkuu wa Kituo cha Afya cha Buguruni, Alvera Mtembelea (wa pili kulia) vilivyotolewa na kampuni ya TTCL leo kwa Kituo cha Afya Buguruni cha jijini Dar es Salaam. TTCL leo imetoa msaada wa mashuka 100, vyandarua 100, maboksi ya dawa mbalimbali pamoja na vifaa tiba ili kukabiliana na changamoto anuai za afya zinazokikabili kituo hicho.
  Meneja Uhusiano wa kampuni ya TTCL, Nicodemus Thomas ( wa pili kulia) akimkabidhi moja ya mashuka Ofisa Muuguzi Mkuu wa Kituo cha Afya cha Buguruni, Alvera Mtembelea (wa tatu kulia)  ikiwa ni sehemu ya msaada uliotolewa na kampuni ya TTCL leo kwa Kituo cha Afya Buguruni cha jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Ofisa Uhusiano wa TTCL, Amanda Luhanga akishuhudia zoezi hilo. TTCL leo imekabidhi msaada wa mashuka 100, vyandarua 100, maboksi ya dawa mbalimbali pamoja na vifaa tiba vingine li kukabiliana na changamoto anuai za afya zinazokikabili kituo hicho.
  Meneja Uhusiano wa kampuni ya TTCL, Nicodemus Thomas ( wa pili kulia) akimkabidhi moja ya mashuka Ofisa Muuguzi Mkuu wa Kituo cha Afya cha Buguruni, Alvera Mtembelea (wa tatu kulia)  ikiwa ni sehemu ya msaada uliotolewa na kampuni ya TTCL leo kwa Kituo cha Afya Buguruni cha jijini Dar es Salaam. TTCL leo imekabidhi msaada wa mashuka 100, vyandarua 100, maboksi ya dawa mbalimbali pamoja na vifaa tiba vingine li kukabiliana na changamoto anuai za afya zinazokikabili kituo hicho.
  Meneja Uhusiano wa kampuni ya TTCL, Nicodemus Thomas ( wa tatu kushoto)  akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kukabidhi sehemu ya msaada katika kituo cha afya cha Buguruni leo jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Ofisa Muuguzi Mkuu wa Kituo cha Afya cha Buguruni, Alvera Mtembelea na kushoto kwake ni Ofisa Uhusiano wa TTCL, Amanda Luhanga akishuhudia zoezi hilo.
  KAMPUNI  ya Simu nchini Tanzania (TTCL) leo imekitembelea kituo cha Afya cha Buguruni cha jijini Dar es Salaam na kutoa misaada mbalimbali ya vifaa pamoja na dawa kwa ajili ya kukiwezesha kutimiza majukumu yake ya kuwahudumiwa wagonjwa mbalimbali wanaokitegemea kituo hicho.


  Katika zoezi hilo, TTCL imekabidhi mashuka 100, Vyandarua 100, Maboksi ya dawa mbalimbali pamoja na vifaa tiba ili kukabiliana na changamoto anuai zinazokikabili kituo hicho kwa ajili ya kuwahudumiwa wakazi wa maeneo hayo kiafya.  Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo, Meneja Uhusiano wa kampuni ya TTCL, Nicodemas Mushi alisema zoezi hilo ni mwendelezo wa kampuni hiyo katika kurejesha faida kwa wananchi ambao ni wateja wa kampuni hiyo. Alisema wanaamini msaada huo unaenda kuwahudumia wananchi ambao ndiyo wateja wa kuu wa huduma za TTCL.  "...Vifaa hivi vinakwenda kuwatibu wananchi ambao tunaamini ni wateja wetu, hivyo wakiwa na afya njema ndiyo furaha kwetu na kuendelea kushirikiana nao kihuduma. Huu ni utaratibu wetu wa kawaida kila tunapopata kidogo tunakirudisha kwa wananchi...leo tumetoa mashine, mashuka 100, vyandarua 100 na dawa ambazo zitasaidia kuboresha huduma kwa wateja wetu," alisema Meneja huyo wa TTCL.

  Meneja Uhusiano wa kampuni ya TTCL, Nicodemus Thomas (kulia) akimkabidhi moja ya mashine ikiwa ni sehemu ya vifaa tiba Ofisa Muuguzi Mkuu wa Kituo cha Afya cha Buguruni, Alvera Mtembelea (wa pili kulia) vilivyotolewa na kampuni ya TTCL leo kwa Kituo cha Afya Buguruni cha jijini Dar es Salaam.

  Mmoja wa Maofisa Wauguzi wa Kituo cha Afya cha Buguruni (kushoto) akimshukuru Meneja Uhusiano wa kampuni ya TTCL, Nicodemus Thomas (kulia) mara baada ya kukabidhi sehemu ya msaada huo ambao ni pamoja na vifaa tiba.
  Alisema wanatambua mchango mkubwa unaotolewa na kituo hicho cha afya na hasa kuwahudumia wagonjwa wa kipindupindu ugonjwa ambao umekuwa changamoto kwa jiji la Dar es Salaam. 


  Kwa upande wake, Ofisa Muuguzi Mkuu wa Kituo cha Afya cha Buguruni, Alvera Mtembelea ameishukuru kampuni ya simu Tanzania kwa ukarimu wao na kuamua kukisaidia kituo hicho kwani wamesaidia kutatua changamoto anuai zinazokikabili kituo hicho katika kutoa huduma za afya. Aliomba makampuni mengine kufuata nyayo za TTCL kusaidia kutatua changamoto za huduma za afya katika vituo vya afya na hospitali anuai kulingana na mahitaji ya maeneo husika.


  Kituo cha afya cha Buguruni ambacho leo kimenufaika na msaada huo ndicho kilichoteuliwa katika eneo hilo kuwahudumia wagonjwa wa kipindupindu ugonjwa ambao ulilipuka hivi karibuni kwa baadhi ya maeneo jijini Dar es Salaam na ambapo madhara yake yaliziathiri baadhi ya jamii jijini hapa.

  0 0

  Katibu wa klabu ya Gofu ya Lugalo Kanali Mstaafu John Nyalusi akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam juu ya mashindano ya siku moja ya gofu ya kumuenzi Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara yatakayofanyika katika klabu ya Gofu ya Lugalo jumamosi hii. Kulia ni Meneja chapa (vileo vikali) wa Serengeti Breweries Limited, Shomari Shija ambao wanahusika na udhamini wa utoaji tuzo, vinywaji na burudani katika kipindi chote cha mashindano.
   Meneja chapa (vileo kali) wa Serengeti Breweries Limited, Shomari Shija, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam kuhusiana na mashindano ya siku moja ya gofu ya kumuenzi Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara yatakayofanyika katika klabu ya Gofu ya Lugalo jumamosi. Kushoto ni katibu wa klabu ya Gofu ya Lugalo Kanali Mstaafu John Nyalusi. Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake kikali cha Johnnie Walker kitadhamini mashindano na kutoa zawadi mbalimbali kwa washindi wa mchuano huo.
  Mabalozi wa pombe kali ya Scotch Whisky “Johnnie Walker” wakionyesha aina mbalimbali za chapa za pombe hiyo wakati wa mkutano na waandishi wa habari juu ya mashindano ya gofu ya waitara ambayo yanatarajiwa kuanza rasmi siku ya jumamosi katika viwanja vya Lugalo jijini Dar es salaam. Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia pombe hiyo kali ndio wadhamini wa mashindano hayo ambapo pia watahusika na utoaji tuzo, vinywaji na burudani katika kipindi chote cha mashindano.

  KAMPUNI ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia pombe yake kali ya Johnnie Walker imetangaza rasmi udhamini wa mashindano ya gofu ya Waitara ambayo yanatarajiwa kuanza siku ya jumamosi katika viwanja vya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja hivyo, Meneja Chapa wa pombe wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Bw. Shomari Shija alisema kuwa udhamini wa mchezo huu wa gofu ni kuhakikisha kuwa unaweza kuendelea na kusifika kama michezo mingine ikiwa pia kama moja ya sehemu ya kurudisha fadhila kwa jamii inayotuzunguka.

  “SBL inadhamini michuano hii kwa kipindi cha miaka mitano sasa na itajikita hasa katika udhamini wa utoaji wa tuzo, vinywaji na burudani katika kipindi chote cha mashindano”…alisema Bw. Shomari.

  Naye katibu wa michuano hiyo ya gofu Kanali mstaafu John Nyalusi aliishukuru SBL kwa kuendelea kusaidia maendeleo ya mchezo huo na kuyaomba makampuni mengine kujitokeza na kuunga mkono jitihada hizo za kuinua mchezo wa gofu nchini.

  “SBL imekuwa katika mstari wa mbele katika kuuendeleza mchezo wa gofu nchini. Ni moja kati ya wadhamini wetu wa kudumu kwa sasa…hivyo tunawashukuru sana… tunaomba makampuni mengine zaidi yajitokeze kuunga mkono jitihada hizi,” alisema Kanali Nyalusi.

  Aliongeza kuwa mashindano hayo yanatarajiwa kufunguliwa na jaji mstaafu Ndugu Mark Bomani siku ya jumamosi saa nne asubuhi na kuwa mpaka sasa mwitikio umekua mkubwa na tayari wachezaji 150 wameahidi kushiriki mashindano hayo kutoka vilabu mbalimbali ikiwa ni pamoja na wenyeji wa Lugalo Golf club, Dar es salaam Gymkhana club, Morogoro Gymkhana club, Arusha n.k.

  Mashindano ya gofu ya Mkuu wa Majeshi mstaafu Jenerali George Waitara huandaliwa na kufanyika kila mwaka kwa madhumuni ya kuenzi mchango wake wa kimichezo nchini kwa kuasisi uwanja wa gofu wa Lugalo golf club. Uwanja wa gofu wa Lugalo ulianzishwa mwaka 2006 kwa mchango mkubwa uliotolewa na Generali mstaafu George Waitara kipindi alichokuwapo madarakani, pia kuendelezwa na Mkuu wa Majeshi aliyefuata na aliyeko madarakani kwa sasa Generali Davis Mwamunyange. 

  0 0


  0 0

  Dkt. Tulia Ackson Mwansasu

  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limempitisha Dkt. Tulia Ackson Mwansasu kuwa Naibu Spika wa Bunge, kwa kura 250 sawa na 71.2% dhidi ya mpinzani wake, Mh. Magdalena Sakaya aliepata kura 101 sawa na 28.8%.

  0 0

  Dkt Hamisi Kigwangalla Mbunge Mteule Nzega Vijijini CCM.

  Mbunge mteule jimbo la Nzega vijijini  Dkt Hamisi Kigwangalla  (CCM) ametoa ushauri kwa wizara husika juu ya udhibiti wa kuvuja kwa madawa serikalini na kwenda kwenye maduka binafsi.

  Kupitia ukarasa wake facebook Kigwangalla amesema #‎SasaKaziTuChangamoto ya Udhibiti wa Kuvuja Madawa Kutoka Mfumo wa Serikali Kwenda Kwenye Maduka ya Watu Binafsi ni Katika Mambo ambayo mgombea Urais wa CCM, Ndg. John Pombe Magufuli alionesha kuwa yanamkera sana. Hivyo wananchi wanasubiri kuona nini kitafanyika kutatua changamoto hii...kuna 'expectation gap' ambayo ni lazima izibwe ndipo watu wasadiki kushuhudia #‎MabadilikoYaKweli

  Nimesikia kuna mkakati wa kutaka kuondoa maduka yote jirani na hospitali za serikali. Si wazo baya sana lakini ninaamini na ninajua kwa hakika kabisa kuwa kuna suluhisho bora zaidi ya hilo. 

  Inawashangaza watu wengi kuwa kwenye pharmacy za watu binafsi nje tu ya hospitali kuna dawa za kutosha za kila aina wakati kwenye pharmacy ya serikali ndani ya hospitali hakuna! Kuna watalamu wetu wanadhani suluhisho ni kuzuia uwepo wa pharmacy karibu zaidi na hospitali. 

  Ninafahamu kwa mfano, kuna tafiti zimefanyika pale Muhimbili kuhusiana na idadi ya dawa zilizopo ukilinganisha na pharmacy mojawapo pale nje; matokeo ya utafiti huo yakawa, Muhimbili kuna dawa tofauti tofauti 850 (lines), wakati kwenye hiyo pharmacy kuna dawa tofauti tofauti takriban 3200! 

  Unaweza kusema si busara kuziondoa pharmacy hizi wakati tunajua kabisa kwenye hospitali yetu pale hakuna dawa za kutosha, maana itakuwa ni usumbufu kwa wagonjwa wanaoagizwa kutafuta dawa fulani ambayo Muhimbili haipo. 

  Unaweza kusema kuwa aina mbalimbali zaidi ya 2300 za madawa zimeibiwa kutoka Muhimbili, na mimi hapo utanipa shida sana kukuelewa. Na nitakuuliza, zimepitia wapi pamoja na ulinzi uliopo? Na kama ziliwahi kuweza kutoka nje ya hospitali mpaka pharmacy, kwani pharmacy hiyo ikihamia Kariakoo ama Posta kutakuwa kuna ugumu gani wa 'wezi' hao wa madawa kuzifikisha huko pia kama wameweza kuzitoa?
  Nadhani njia hii ni too 'mechanical' na haitoondoa tatizo zaidi ya kuzalisha tatizo lingine 'la usumbufu kwa wagonjwa'.

  Nini kifanyike kudhibiti dawa zisikosekane kwenye mfumo wa afya?
  1. Tuhakikishe tuna dawa za kutosha kwenye Idara ya Bohari ya Dawa (MSD) kwa kuongeza 'capacity' yake kununua 'lines' nyingi zaidi za dawa kuliko ilivyo sasa, ambapo MSD inaweza ku-supply only 65% ya mahitaji.
  2. Bohari ijiendeshe kibiashara.

  3. Tuweke 'color code' kwenye dawa zote za serikali kwenye bohari; mfano labda dawa za serikali ziwe na rangi ya 'pink' pekee, na rangi hii iambatane na 'bar code', na kuwe na 'task force' maalum ya ukaguzi wa pharmacy za binafsi na ikitokea dawa ya serikali ikakutwa kwenye pharmacy yoyote ile kuwe na adhabu kali.

  4. Bohari ya Dawa (MSD), kwa makubaliano maalum na hospitali husika, iruhusiwe kufungua pharmacy zake kwenye hospitali zote nchini ili iuze moja kwa moja kwa wateja. Tunaweza kuanza na hospitali chache za mfano - kama Muhimbili, Amana, Mwananyamala, Temeke, Sekou Toure, Za Rufaa za Mikoa na baadhi ya Wilaya, Vituo Vya Afya na Zahanati; Ili kuliko wateja wa hospitali za serikali kwenda kununua dawa kwa bei ya kurusha kwenye pharmacy za watu binafsi kule nje wanunue kwa bei nafuu ya serikali ndani ya hospitali zetu. 

  5. Tuongeze kasi ya kusajili wananchi wote kwenye Mfumo wa Bima ya Afya kwa Wote ili kuongeza financing kwenye mfumo wa afya wa serikali zaidi ya kutegemea bajeti tu. 

  6. MSD wakiishakuwa na pharmacy yao ndani ya health facility watakaa na wataalamu na menejimenti ya hospitali husika na kuorodhesha madawa wanayohitaji na MSD kuhakikisha yapo kwenye pharmacy yao kwenye kituo husika.

  (JAMIIMOJABLOG)

  0 0

  KAMPUNI ya SBC Tanzania Limited, watengenezaji na wasambazaji wa vinywaji baridi imepunguza bei ya vinywaji vyake kutoka shillingi mia sita (600) hadi mia tano (500) kwa chupa yenye ujazo wa Mililita 350 na 300.

  Hayo yamesemwa na Meneja Mafunzo na Uwezeshaji Bw.Rashid Chenja (Pichani)alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam na kuongeza kuwa lengo la kupunguza bei ni kutokana na hali ngumu ya uchumi iliyopo.

  “Imekuwa vigumu kwa mnywaji kuweza kudumu bei ya kinywaji akipendacho cha pepsi , gharama za maisha zinapanda kila mwaka na soda imekuwa ghali kiasi cha wananchi wa kawaida kushindwa kumudu kununua soda hivyo kampuni imeamua kupunguza bei” alifafanua Meneja huyo.

  Pia amesema kuwa kampuni ya SBC Tanzania imefanya punguzo hilo  kuanzia tarehe 16/11/2015 kwa vinywaji vya Pepsi, Mirinda,7up, Mountain Dew na Evervess na maeneo yatakayo husika na punguzo hilo la bei ni Dar es salaam,Morogoro, Dodoma, Pwani, Tanga, Lindi, Mtwara na Zanzibar.

  “Ni matumaini yetu mtaendelea kutuunga mkono katika biashara yetu kwa kununua soda zetu kwa bei iliyopendekezwa ya shilingi Mia Tano kwa chupa, shilingi elfu tisa mia nne (9,400) kwa kreti moja na faida kwa wauzaji wa rejareja itakuwa ni shilingi 2500 kwa kila kreti” aliongeza Bw. Chenja.  

  Mbali na hayo Kampuni ya SBC Tanzania Limited inawashukuru wateja wake kwa kuwaunga mkono katika biashara yao kwa kipindi cha miaka 14 hapa nchini.

  0 0


  Dkt Hamisi Kigwangalla Mbunge Mteule Nzega Vijijini CCM.


  MBUNGE mteule jimbo la Nzega vijijini  Dkt Hamisi Kigwangalla  (CCM) ametoa ushauri kwa wizara husika juu ya udhibiti wa kuvuja kwa madawa serikalini na kwenda kwenye maduka binafsi.

  Kupitia ukarasa wake facebook Kigwangalla amesema #‎Sasa Kazi Tu Changamoto ya Udhibiti wa Kuvuja Madawa Kutoka Mfumo wa Serikali Kwenda Kwenye Maduka ya Watu Binafsi ni Katika Mambo ambayo mgombea Urais wa CCM, Ndg. John Pombe Magufuli alionesha kuwa yanamkera sana. Hivyo wananchi wanasubiri kuona nini kitafanyika kutatua changamoto hii...kuna 'expectation gap' ambayo ni lazima izibwe ndipo watu wasadiki kushuhudia #‎MabadilikoYaKweli.

  Nimesikia kuna mkakati wa kutaka kuondoa maduka yote jirani na hospitali za serikali. Si wazo baya sana lakini ninaamini na ninajua kwa hakika kabisa kuwa kuna suluhisho bora zaidi ya hilo.

  Inawashangaza watu wengi kuwa kwenye pharmacy za watu binafsi nje tu ya hospitali kuna dawa za kutosha za kila aina wakati kwenye pharmacy ya serikali ndani ya hospitali hakuna! Kuna watalamu wetu wanadhani suluhisho ni kuzuia uwepo wa pharmacy karibu zaidi na hospitali. 

  Ninafahamu kwa mfano, kuna tafiti zimefanyika pale Muhimbili kuhusiana na idadi ya dawa zilizopo ukilinganisha na pharmacy mojawapo pale nje; matokeo ya utafiti huo yakawa, Muhimbili kuna dawa tofauti tofauti 850 (lines), wakati kwenye hiyo pharmacy kuna dawa tofauti tofauti takriban 3200!.

  Unaweza kusema si busara kuziondoa pharmacy hizi wakati tunajua kabisa kwenye hospitali yetu pale hakuna dawa za kutosha, maana itakuwa ni usumbufu kwa wagonjwa wanaoagizwa kutafuta dawa fulani ambayo Muhimbili haipo. Unaweza kusema kuwa aina mbalimbali zaidi ya 2300 za madawa zimeibiwa kutoka Muhimbili, na mimi hapo utanipa shida sana kukuelewa. Na nitakuuliza, zimepitia wapi pamoja na ulinzi uliopo? Na kama ziliwahi kuweza kutoka nje ya hospitali mpaka pharmacy, kwani pharmacy hiyo ikihamia Kariakoo ama Posta kutakuwa kuna ugumu gani wa 'wezi' hao wa madawa kuzifikisha huko pia kama wameweza kuzitoa?
  Nadhani njia hii ni too 'mechanical' na haitoondoa tatizo zaidi ya kuzalisha tatizo lingine 'la usumbufu kwa wagonjwa'.


  Nini kifanyike kudhibiti dawa zisikosekane kwenye mfumo wa afya?
  1. Tuhakikishe tuna dawa za kutosha kwenye Idara ya Bohari ya Dawa (MSD) kwa kuongeza 'capacity' yake kununua 'lines' nyingi zaidi za dawa kuliko ilivyo sasa, ambapo MSD inaweza ku-supply only 65% ya mahitaji.
  2. Bohari ijiendeshe kibiashara.

  3. Tuweke 'color code' kwenye dawa zote za serikali kwenye bohari; mfano labda dawa za serikali ziwe na rangi ya 'pink' pekee, na rangi hii iambatane na 'bar code', na kuwe na 'task force' maalum ya ukaguzi wa pharmacy za binafsi na ikitokea dawa ya serikali ikakutwa kwenye pharmacy yoyote ile kuwe na adhabu kali.

  4. Bohari ya Dawa (MSD), kwa makubaliano maalum na hospitali husika, iruhusiwe kufungua pharmacy zake kwenye hospitali zote nchini ili iuze moja kwa moja kwa wateja. Tunaweza kuanza na hospitali chache za mfano - kama Muhimbili, Amana, Mwananyamala, Temeke, Sekou Toure, Za Rufaa za Mikoa na baadhi ya Wilaya, Vituo Vya Afya na Zahanati; Ili kuliko wateja wa hospitali za serikali kwenda kununua dawa kwa bei ya kurusha kwenye pharmacy za watu binafsi kule nje wanunue kwa bei nafuu ya serikali ndani ya hospitali zetu.

  5. Tuongeze kasi ya kusajili wananchi wote kwenye Mfumo wa Bima ya Afya kwa Wote ili kuongeza financing kwenye mfumo wa afya wa serikali zaidi ya kutegemea bajeti tu.
  6. MSD wakiishakuwa na pharmacy yao ndani ya health facility watakaa na wataalamu na menejimenti ya hospitali husika na kuorodhesha madawa wanayohitaji na MSD kuhakikisha yapo kwenye pharmacy yao kwenye kituo husika.

  (JAMIIMOJABLOG)

  0 0

  ALVARO KUPANDA MTI-2
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akipanda mti kama ishara ya uhifadhi mazingira baada ya kuzindua mradi wa kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia nishati jadidifu ya jua (Mitigating Climate change in vulnerable communities of Dodoma region, Machali village, Chamwino District), katika Kijiji cha Machali A, wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma katika utekelezaji wa moja kati ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).
  ALVARO MWAGILIA MAJI-3
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akimwagilia maji kama ishara ya uhifadhi mazingira baada ya kuzindua mradi wa kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia nishati jadidifu ya jua (Mitigating Climate change in vulnerable communities of Dodoma region, Machali village, Chamwino District), katika Kijiji cha Machali A, wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma katika utekelezaji wa moja kati ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).
  ALVARO NA BURUDANI-2
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Awa Dabo (kulia) wakieleka kukagua mradi wa ufugaji wa shirika la Tanzania Environmental Friendly Association (TEFA) huku wakiburudishwa na ngoma ya wenyeji wa kabila wa Kigogo, katika Kijiji cha Machali A, wilaya ya Chamwino mkoa wa Dodoma katika utekelezaji wa moja kati ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).
  ALVARO NA MAJI-2
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa Kijiji cha Machali A wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma, Zena Mwalko baada ya kuzindua mradi wa kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia nishati jadidifu ya jua (Mitigating Climate change in vulnerable communities of Dodoma region, Machali village, Chamwino District), katika Kijiji cha Machali A, wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Awa Dabo.
  ALVARO NA WANANGOMA
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiwa kwenye picha ya pamoja na wanakikundi cha ngoma cha Kijiji cha Machali A, wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia nishati jadidifu ya jua (Mitigating Climate change in vulnerable communities of Dodoma region, Machali village, Chamwino District), katika Kijiji cha Machali A, wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Awa Dabo.

  ALVARO ZUNGUMZA
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Machali A, wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia nishati jadidifu ya jua (Mitigating Climate change in vulnerable communities of Dodoma region, Machali village, Chamwino District), kijijini humo. Kutoka kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Awa Dabo na Mwakilishi Msaidizi wa Shirika la UNFPA, Dk. Hashina Begum.
  AWA KUBEBA NDOO
  Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Awa Dabo akiwa amebeba ndoo ya maji baada ya uzinduzi wa mradi wa kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia nishati jadidifu ya jua (Mitigating Climate change in vulnerable communities of Dodoma region, Machali village, Chamwino District), katika kijiji cha Machali A wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma huku Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na wanakijiji wakishuhudia tukio hilo.
  AWA KUPANDA MTI-3
  Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Awa Dabo akipanda mti kama ishara ya uhifadhi mazingira baada ya kuzindua mradi wa kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia nishati jadidifu ya jua (Mitigating Climate change in vulnerable communities of Dodoma region, Machali village, Chamwino District), katika Kijiji cha Machali A, wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.
  DK HASHINA KUPANDA MTI-2
  Mwakilishi Msaidizi wa Shirika la UNFPA, Dk. Hashina Begum akimwagilia maji mti kama ishara ya kutunza mazingira baada ya uzinduzi wa wa kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia nishati jadidifu ya jua (Mitigating Climate change in vulnerable communities of Dodoma region, Machali village, Chamwino District), katika Kijiji cha Machali A, wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.
  YOHANA KUPANDA MTI-3
  Mratibu wa Mradi wa kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia nishati jadidifu ya jua (Mitigating Climate change in vulnerable communities of Dodoma region, Machali village, Chamwino District) kutoka Shirika la Tanzania Environmental Friendly Association (TEFA), Yohana Kadiva akimwagilia maji mti kama ishara ya kutunza mazingira baada ya uzinduzi wa mradi huo unaofadhiliwa na Umoja wa Mataifa kupitia Shirika lake la Mpango wa Maendeleo (UNDP).
  NGOMA
  Wanakikundi cha ngoma ya asili katika kijiji cha Machali A wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma wakiburudisha wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi huo.
  UZINDUZI MRADI
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akizindua mradi wa kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia nishati jadidifu ya jua (Mitigating Climate change in vulnerable communities of Dodoma region, Machali village, Chamwino District), kijijini humo.

  0 0

  index

  MRS BARKE M. UBAYA LEO UMETIMIZA MIAKA MIWILI TANGU UTUTOKE DUNIANI SISI TULIO HAI BADO TUNAKUKUMBUKA KWA UPOLE UCHESHI NA UKARIMU WAKO UNAKUMBUKWA NA MUMEO BW.MWINYI UBAYA WANAO SALAMA NA RAHMA MAMA YAKO FAMILIA YA MAGOHA NA UBAYA JIRANI NA MARAFIKI INSHA'ALLAH M MUNGU AKUSAMEHE MAKOSA YAKO AMIN INNA LILLAH WA INNA LILLAH RAJIUN

  0 0
 • 11/19/15--22:55: UCHAMBUZI WA MAGAZETI LEO
 • SIMU.TV:  Mh.Majaliwa asema hakutegemea, aahidi kutumikia wote bila ubaguzi. Dk.Tulia achaguliwa kuwa Naibu Spika Bunge la 11; 
  SIMU.TV:  Wazimia baada ya nyumba 25 kuvunjwa Dar,  watoto watatu wauwawa  kikatili. Wazanzibari waandamana London; https://youtu.be/2OWnUdzu-rI     
  SIMU.TV:  Vyama vya siasa vyatakiwa kuvunja vikundi vya ulinzi. Profesa Lipumba amsifu Rais Magufuli kwa uteuzi wa Waziri Mkuu; https://youtu.be/Me8XZ1KxDy0

  SIMU.TV:  Mkwasa abeba lawama zigo la 7-0. MCameroon atua rasmi Simba, safari ya Miss Tanzania , China yaiva. Pata habari motomoto zilizotawala katika magazeti ya leo; https://youtu.be/1wBDkbbtnak


  0 0

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulamula akiwa kwenye ukumbi wa Sanaa, Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulamula akipata maelezo ya Michoro ya Mapangoni kutokwa kwa Mtaalam wa Makubusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam Bi Agnes Gidna.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulamula akipata maelezo ya Chimbuko la mwanadamu kutokwa kwa Mtaalam wa Makubusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam Dkt Amandus Kweka. Fuvu lilipo kulia kwenye sanduku lililo nakshiwa na dhahabu ni la Zinjanthropus lililo gunduliwa zaidi ya miaka milioni 1.7 iliyo pita huko Ngorongoro Oldvuvai kwenye miaka ya 1959. 
  Balozi Mulamula akiagana na Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw Achiles Bufure baada ya kumaliza kuitembelea Makumbushi hiyo.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulamula akitembezwa kujionea miundombinu ya Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam kulia ni Mkurugenzi wa Makumbusho hiyo Bw Achiles Bufure.


  Na Sixmund J. Begashe.
  WIZARA ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imeridhishwa na huduma mbali mbali zinazo tolewa na Makumbusho ya Taifa kwa wageni mbali mbali wanao tembelea Makumbusho hizo ili kujionea na kujifunza mambo mbali mbali yanayo huyu Tanzania.

  Akiwa kwenye ziara ya kimafunzo katika Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mukamula amesema kuna umuhimu mkubwa wa kuitumia Makumbusho za Taifa ili kutoa elimu kwa wageni mbali mbali wanaotembelea Tanzania.

  Ameongeza kuwa Wizara yake hupokea wageni wengi wa kimataifa wanaokuja kwa shughui za kiserikali hivyo ofisi yake itafanya utaratibu wa kuhakikisha wageni hao wanatembelea makumbusho kwa maana ndio sehemu pekee wanapo weza kuifahamu Tanzania kwa muda mfupi bila kuizunguka nchi yote.

  “Nimekuja mwenye kujionea na kujifunza huduma mnazo toa hapa, ili nijiridhishe kwanza kabla ofisi yangu haijaanza kuwaleta wageni hapa, kiukweli nimeridhishwa sana na huduma yenu na licha ya kujifunza nimeona vipo vivutio vingi vinaweza kuwavutia wageni wa kiserikali na kujifunza kupitia vitu hivi, hongereni sana” Alisema Balozi Mulamula.

  Akimshukuru Balozi Mulamula kwa kutembelea Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni, Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw Achiles Bufure alisema kuwa amependezwa na Wizara ya Mambo ya Nje kwa kuona umuhimu wa kuitumia Makumbusho kama Mwalimu Mwelekelezi wa Mambo yanayo thaminiwa na watanzania

  “Viongozi wetu wa kubwa wakienda kikazi nchi za wenzetu, wakifika huko hutembezwa Makumbusho, ili kuwafanya wasiondoke bila kuzifahamu hizo nchi kihistoria na hata kimaendeleo ya kisayansi na teknolojia, vivyo hivyo wanapokuja hapa nchini wanapaswa kutembezwa Makumbusho ili wapate sura sahihi ya nchi yetu” Aliongeza Bw Bufure.

  Mkurugenzi huyo wa Makumbusho ametoa  wito kwa Wizara zote za Serikali, Taasisi za watu binafsi na Watanzania kwa ujumla wenye kutembelewa na wageni kutoka nje ya Tanzania kuwa na Utamaduni wa kuwatembeza wageni wao Makumbusho ili kujifunza mambo ya Tanzania.

  0 0

  Baba, God saw you struggling and no cure in this world was there to make you stay, he then decided to call you that day of 20th November 2013. They were days, weeks, months and now 2 years without you. It is true that you are gone.

  Our hearts were hurt but we had no choice, we had to let you go. We miss your smile, your words, and many more that we cannot express .We continue praying for you papa that your heart continue to rest in Eternal Peace. 

  There will be a holy mass at University od Dar es Salaam Chepel on 20th November 2015  and on Saturday 21st November 2015 at 1500hrs onward we will gather at your home Mapinga for lunch and remembrance of your great life teachings. 

  Our friends and family please join us when commemorating the life of a beloved HUSBAND,DAD,BABU,UNCLE and a BROTHER. 

  May your gorgeous soul continue to Rest In eternal Peace. Amen.

  0 0

   Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando akionyesha huduma mpya ya "Airtel TV" inavyofanya kazi wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo
  itakayowawezesha wateja wa Airtel kuangalia vipindi katika vituo
  mbalimbali vya television kupitia simu zao za mkononi, akishuhudia ni
  Meneja huduma za ziada wa Airtel,Prisca Tembo.
  Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando akiongea wakati wa
  uzinduzi wa huduma  mpya ya "Airtel TV" itakayowawezesha wateja wa
  Airtel kuangalia vipindi katika vituo mbalimbali vya television
  kupitia simu zao za mkononi.

    *   Kuunganishwa na chanel  8 za ndani na nje
    *   Kujiunga na vifurushi vya kuangalia TV bila kikomo vya siku, wiki na mwezi 
  Dar es Salaam, Tanzania 19 Novemba 2015, kampuni ya simu za mkononi ya 
  Airtel leo imezindua huduma ya ziada itakayowawezesha wateja wake nchi 
  nzima kuangalia vipindi vya televisheni katika vituo vya ndani na nje 
  ya nchi kupitia simu zao za mkononi.

  Huduma hii mpya ijulikanayo kama "Airtel TV" imeunganishwa na vituo 8
  za televisheni vya ndani na nje ya nchi na kuwawezesha wateja wa
  Airtel kuangalia vipindi vilivyopita katika tamsilia wanazozipenda,
  kuangalia sinema na video wanazohitaji  kupitia simu zao.

  Akiongea wakati wa uzinduzi wa "Airtel TV" Meneja Uhusiano wa Airtel ,
  Bw Jackson Mmbando alisema "kwa kawaida mara nyingi watanzania
  wanaangalia vipindi vya televisheni wakiwa nyumbani  wakati wa jioni
  baada ya kutoka katika kazi zao. Tunazindua huduma yenye gharama nafuu 
  itakayowawezesha wateja wetu kupata taarifa pindi wasipokuwapo
  majumbani mwao.

   "Airtel TV" itawapatia uzoefu wa kipekee na
  kuwahabarisha wateja wetu wakati wowote  wakiwa katika shughuli zao au 
  kwenye foleni,  bila kikomo kupitia simu zao za mkononi"
  " huduma hiii imelenga kukidhi mahitaji ya wateja kwa kuwapatia habari
  kiurahisi kwa kujiunga na kifurushi cha siku , wiki au mwezi.

  Tunaamini huduma hii itapunguza uwiano wa watu wasiokuwa na fursa ya
  kuangalia Televishoni na pia kuwawezesha kupata matukio kwa wakati
  kupitia simu zao mahali popote pale walipo" aliongeza Mmbando
  Akiongea kuhusu mahudhui na jinsi ya kujiunga na huduma hiyo, Meneja
  huduma za ziada ,Prisca Tembo alieleza zaidi  kuhusu dhamira yao ya
  kutoa huduma yenye kiwango cha juu na gharama nafuu. 

  " tunayo furaha kuwawezesha watanzania kuangalia vipindi vya televisheni kupitia simu
  zao kwani tunaenda sambamba na mpango wa serikali wa kidigitali wenye
  lengo la  kuwa na jamii kupata taarifa za yanayotokea ndani na nje ya
  nchi kwa wakati na kiwango cha juu.

  Tembo aliongeza kwa kusema ili kupata huduma ya  "Airtel TV" mteja
  anatakiwa kupakua  au kudownload application kwa kupitia linki  ya
  https://goo.gl/iSvaJC kwa simu za Android na   https://goo.gl/IMvzCt
  kwa simu za IOS.

  Baada ya kuzi download mteja ataweza kununua kifurushi cha internet
  maalum cha Televisheni  kwa kupiga *148*88#  tozo za kujiunga ni Tshs
  499 kwa siku, Tshs 2,999 kwa wiki naTshs 11,999 kwa mwezi. Vituo
  vinavyopatikana katika "Airtel TV" ni pamoja na Star TV, TBC, Fight
  Box, 360 tune box, Citizen, FilmBox, Channel Ten na Aljazeera.

  0 0

  SIMU.TV:  Viongozi Mbalimbali wawasili katika ukumbi wa Ikulu Ya Chamwino Dodoma kushuhudia kiapo cha Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa. 
  SIMU.TV:  Mhe. Kassim Majaliwa ni waziri wa 11 tangu Tanzania ipate uhuru wake toka kwa wakoloni.https://youtu.be/w8QL1Xqn-uE
   SIMU.TV:  Makamu wa Rais Mstaafu Mhe. Gharib Bilal awasili kushuhudia kiapo cha Mhe. Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania. https://youtu.be/UDtuYyt5jVI
  SIMU.TV:  Hatimaye Waziri mkuu mteule na Rais Magufuli wawasili ndani ya ukumbi wa Ikulu ya Chamwino na wimbo wa Taifa kuibwa. https://youtu.be/AYcNgFIxW00 
  SIMU.TV:  Hatimaye Mhe Kassim Majaliwa ala kiapo cha uaminifu na kuahidi kuhifadhi na kulinda katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. https://youtu.be/G_JWuGmfyrw
  SIMU.TV:  Viongozi mbalimbali wajongea kutoa Mkono wa pongezi  Waziri mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  SIMU.TV:  Hii ndiyo orodha ya waliowahi kushika wadhifa wa Waziri Mkuu katika Serikali ya Tanzania;https://youtu.be/K0YdS_RB7yQ

  0 0

   Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Waziri Mkuu- TAMISEMI Bi. Rebecca Kwandu akifurahia jambo na waandishi wa habari (hawapo pichani)leo jijini Dar es Salaam wakati akiwaeleza mafanikio ya mfumo wa ukusanyaji mapato kwa njia ya kielektroniki katika mamlaka za Serikali za Mitaa (LGRCIS). Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Mifumo ya TEHAMA wa ofisi hiyo Bw. Mtani Yangwe na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa.
   Mkurugenzi Msaidizi Mifumo ya TEHAMA kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu- TAMISEMI Bw. Mtani Yangwe akifafanua kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam namna mfumo wa wa ukusanyaji mapato kwa njia ya kielektroniki unavyorahisisha ulipaji wa kodi mbalimbali kwa kuhusisha mifumo ya kielektroniki ya malipo na mifumo ya kibenki. Kulia ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa ofisi hiyo Bi. Rebecca Kwandu.
   Afisa Msimamizi wa Fedha Ofisi ya Waziri Mkuu- TAMISEMI Bw. Elisa Rwamiago akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Dar es Salaam kuhusu mikakati mbalimbali ya kuongeza mapato ya mamlaka za Serikali za Mitaa ili kuondokana na utegemezi wa ruzuku kutoka Serikali Kuu. Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa ofisi hiyo Bi. Rebecca Kwandu.
   Mhasibu wa Mfumo wa Mapato Jiji la Arusha Bw. Prosper Mlacha akiwaeleza waandishi wa habari leo Dar es Salaam kuhusu ongezeko la mapato katika jiji la Arusha kutokana na matumizi ya mfumo wa ukusanyaji mapato kwa njia ya kielektroniki (LGRCIS) ambapo kwa mwaka 2014/2015 zimekusanywa bilioni 10.7.

   Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa maafisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu- TAMISEMI uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

  Picha zote na Fatma Salum (MAELEZO)

  Na Georgina Misama.
  SERIKALI imeboresha matumizi ya mfumo wa ukusanyaji wa mapato kwa njia ya kielekitroniki katika mamlaka za serikali za mitaa.

  Hayo yamesemwa na msemaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) Bi. Rebecca Kwandu leo jijini Dar es salaam.

  Bi Rebecca amesema kuwa TAMISEMI imekuwa ikiendelea kwa nyakati tofauti kufanya maboresho mbalimbali ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa jamii na kuzisaidia mamlaka hizo katika kuongeza mapato ya ndani na kuondokana na uteuzi wa ruzuku kutoka Serikali Kuu.

  “Ofisi ya Waziri Mkuu –TAMISEMI iliamua kuanzisha mfuko wa Local Governement Collection Information System (LGRCIS) baada ya kufanya tafiti mbalimbali kwa nyakati tofauti na zilionyesha kuwa hakukuwa na mfumo wowote wa kielektroniki kurahisisha ukusanyaji na usimamizi wa mapato ya Halmashauri” alifafanua Bi. Rebecca.

  Mbali na hayo Msemaji huyo alisema kuwa miongoni mwa malengo makuu ya kuanzishwa kwa mfumo wa LGRCIS ni pamoja na kupata taarifa za walipa kodi wa mamlaka za serikali za mitaa na kuhifadhiwa kwa usahihi katika kanzi data ya mfumo.

  “ Kupata takwimu sahihi ya vyanzo vya mapato na kufanya usuluhishi kati ya kilichokusanywa na kilichotarajiwa kukusanywa, kuongeza mapato kwa kasi zaidi kwa kuwa na uhakika wa makusanyo katika vyanzo vikuu, kuweka uwazi na uwajibikija katika makusanyo ya mapato,na kuhimarisha ulipaji miamala ya kodi na tozo itakayofanywa na walipakodi” aliongeza Bi Rebecca.

  Pia alisema kuwa matarajio ya TAMISEMI ni kuwa mfumo wa LGRCIS utaleta mabadiliko makubwa katika Halmashaurina kuachana na utegemezi wa ruzuku kutoka Serikali kuu.

  Hata hivyo teknolojia pekee ya matumizi ya TEHAMA haiwezi kuleta mabadiliko pasipo fikra za watumiaji wa mfumo wa walipakodi kubadili mazoea.

  0 0

  Manispaa ya wilaya ya Kinondoni kushirikiana na Wizara ya Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi wakiwa wameweka tangazo lao katika ukuta wa uzio wakimaanisha eneo hilo lisitumike kwa maana ya maeneo ya wazi.

    Nyumba nyingine eneo hilo nayo ikisubili kubomolewa na manispaa ya Kinondoni. 
   Ubomoaji ukiendelea.   
  Familia ya nyumba inayotakiwa kubomolewa na manispaa wakitoa dhamani za ndani ili kupisha ubomoaji.   Ubomoaji ukiendelea katika maeneo ya Mbezi Bichi jijini Dar es Salaam.
   Wazee wa kazi wakiwa katia geti la nyumba inayotakiwa kubomolewa  maeneo ya mtaa wa  Libermann Mbezi Bichi jijini Dar es Salaam leo.
   Ubomoaji wa uzio wa nyumba maeneo ya Libermann Mbezi Bichi jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kubisha hodi na kutokufunguliwa.
   Magari ya kitolewa nje ili kupisha ubomoaji wa nyumba maeneo ya  Libermann Mbezi Bichi jijini Dar es Salaam leo.
  Wenyeji wa nyumba ambayo imeanza kubomolewa uzio wakitoa vitu ndani ili kupisha ubomoaji wa nyumba hiyo.
   
   Wakazi wa nyumba nyeupe inayobomolewa wakitoka nje ya nyumba baada ya kuanza kubomolewa na manispaa ya Kinondoni.

  Wananchi waangalia jinsi manispaa inavyobomoa nyumba Mbezi bichi jijini Dar es Salaam leo
  Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

  0 0

   Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza (Kulia) akisisitiza jambo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wa vyama vya wasanii yaliyoandaliwa na Baraza hilo mapema wiki hii. Kulia kwake ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utamaduni anayeshughulikia Lugha kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Shani Kitoga
   Msanii mkongwe wa Sanaa za Maonesho Bw. Kassim Mbelemba maarufu kwa jina la Mzee Jangala akipokea cheti chake kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utamaduni anayeshughulikia Lugha kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Shani Kitoga baada ya kumaliza mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wa vyama vya wasanii yaliyoandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) mapema wiki hii.  
   Mwezeshaji wa mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wa vyama vya Wasanii katika eneo la Hakimiliki na Hakishiriki Bw. John Kitime akipokea zawadi kutoka kwa mmoja wa viongozi wa vyama vya wasanii baada ya kutoa mafunzo kwa viongozi hao. 
  Viongozi wa vyama vya Wasanii walioshiriki mafunzo ya Kujengewa Uwezo wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi Bi. Shani Kitoga
  IMETOLEWA NA KITENDO CHA HABARI NA MAWASILIANO, BASATA.

  BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limewapa mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo katika maeneo mbalimbali viongozi wa vyama na taasisi zinazojihusisha na wasanii ili kujenga ufanisi zaidi katika sekta ya Sanaa.

  Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa siku tatu kuanzia Jumanne hadi Alhamisi ya wiki hii yalijikita katika kuwajengea uwezo Wasanii kwenye maeneo ya uandaaji bajeti, uandaaji wa mipango mikakati na sheria ya hakimiliki na hakishiriki na mikataba kwenye kazi za Sanaa. 

  Akizungumza kwenye hafla ya kuyafunga mafunzo hayo, Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza alisema kwamba ana matumaini makubwa kwamba mafunzo haya kwa viongozi wa wasanii yataamsha ari katika utawala na utendaji wa sekta ya Sanaa na kufanikisha kupiga hatua kwa sekta hii muhimu.

  “Nina imani katika mafunzo haya tutawaona viongozi wa wasanii mnakuwa na mipango ya muda mrefu, wa kati na mfupi maana hakuna jinsi tunaweza kuwaongoza wasanii bila kuwa na mipango” alisisitiza Mngereza.

  Kuhusu suala la hakimiliki, hakishiriki na mikataba kwenye kazi za Sanaa  alisema kuwa ni tatizo linalowakumba wasanii wengi hivyo imani ya BASATA ni kuona viongozi hawa waliopatiwa mafunzo wanakuwa msaada kwa wasanii walio chini ya vyama vyao.


  “Suala la hakimiliki linamgusa kila msanii, naamini kwenye suala hili mmejifunza vya kutosha. Aidha, mmejifunza suala la mikataba katika kazi za Sanaa, nawaomba muwe mabalozi katika kuwaelimisha wasanii umuhimu wa mikataba katika kazi wanazozifanya” Aliongeza Mngereza.

  Awali akiongea kabla ya kukabidhi vyeti kwa washiriki, mgeni rasmi ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Shani Kitoga aliwataka viongozi hao kuzingatia mafunzo waliyoyapata na kuhakikisha wanakuwa mabalozi wa mabadiliko kwenye sekta ya Sanaa.

  “Sanaa tunasema ni kazi hivyo lazima mafunzo haya mliyoyapata myatafsiri katika vitendo kwa kuonesha utendaji kazi ulio bora na unaozingatia mipango” alisema Bi. Kitoga.

  Akiongea kwa niaba ya viongozi wa wasanii zaidi ya arobaini (40) waliohudhuria mafunzo hayo, Msanii mkongwe wa Sanaa za Maonesho Kassim Mbelemba maarufu kwa jina la Mzee Jangala alilipongeza BASATA kwa kuandaa mafunzo hayo na kuwaeleza wasanii kuwa sasa hakuna sababu ya kulalamika bali kuyafanyia kazi yale waliyojifunza.

  Mafunzo haya ambayo ni sehemu ya kutekeleza mpango mkakati wa BASATA yaliwezeshwa na wakufunzi Rashid Masimbi ambaye ni mtaalam wa kuandaa mipango mikakati, Mrisho Mtumwa ambaye ni mtaalam wa kuandaa bajeti na John Kitime ambaye ni Msanii na mtaalam wa masuala ya hakimiliki na hakishiriki. 

  0 0

  SHUKRANI
  Habari Ndugu zetu Watanzania mlio ndani na nje ya nchi nawasalimu.

  Natumaini wote mko salama.
  Kwa niaba ya Dada yetu Ndugu yetu Mtanzania Mwenzetu AMINA ALLY JUMA na Familia yake yote kwa ujumla, Leo tunarudi kwenu kwa SHUKRANI ZA DHATI kwa Moyo kwa kujitolea kwenu kwa hali na Mali na Sala zenu.

  Tangu Mwezi uliopita tulikuja kwenu kwa ajili ya kuomba msaada kwa ajili ya Dada yetu AMINA anayesumbuliwa na maradhi ya Saratani ya Damu (ACUTE AMELOID LEUKEMIA) Ambaye kwa sasa yuko nchini India akiendelea na Matibabu.

  Napenda Kuwashukuru sana Wadau wote walioweza kuusambaza ujumbe, hasa kwa njia ya mitandao (Social Media) kwani mchango wenu umekuwa mkubwa mno na uliozaa matunda mema. 

  Tumefanikiwa kupata kiasi ($7500.00) ambacho kilitakiwa kwaajili ya kutimiza malengo ya dada Yetu AMINA kwa matibabu yake, TUNAWASHUKURU WOTE WALIOJITOLEA KWA HALI MALI NA SALA ZENU MWENYEZI MUNGU AZIDI KUWABARIKI NA TUENDELEE NA USHIRIKIANO HUU.

  Pia tunatanguliza shukrani zetu za dhati kwa, MICHUZI BLOG, WANAWAKE LIVE, SMILEY KIDS EVENTS, ZAMARADI MKETEMA, JOKATE MWEGELO, 8020 FASHION BLOG, SARAH RAQEY, DINA MARIOS, ITV na wengine wote kwa njia moja tuliweza kujitoa kwa nia njema katika kuwajibika, TUNASEMA ASANTENI SANA SANA NA MUNGU AWABARIKI.

  KUANZIA LEO HII 20/11/2015 TUNASITISHA MICHANGO HII NA TUKIMSHUKURU SANA MUNGU KWA WEMA WAKE WOTE.

  Tunawashukuru sana kwa Michango yenu yote, kwa ushirikiano tumetimiza lengo, na sasa tumemkabidhi Mungu mwenyezi muumba wetu atende miujiza yake kwa Dada yetu AMINA na ndugu zetu wote walioadhirika na ugonjwa huu tuzidi Kuombeana Kupendana na Kushirikiana.

  PS: KUTAKUWA NA DUA YA SHUKRANI NYUMBANI KWA AMINA MIKOCHENI B’ WARIOBA, TAASISI STREET, SIKU YA IJUMAA 27/11/2015 KWA WALE WATAKAOWEZA KUFIKA KARIBUNI SANA.

  ASANTENI SANA KAZI NJEMA NA MUNGU AWABARIKI ……AMEN

older | 1 | .... | 690 | 691 | (Page 692) | 693 | 694 | .... | 1898 | newer