Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 689 | 690 | (Page 691) | 692 | 693 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Kumekuwa na sheria na kanuni mbalimbali zinazoundwa, ingawa wakati mwingine hushindwa kutekelezeka kwa wakati. Ukifika katika hoteli ya Golden Tulip utakuta jinsi eneo hilo linavyozidi kujengwa na kuendelezwa kama lilivyokutwa na mpiga picha wetu. 

  Kujengwa kwa eneo hili lililokuwa pembezoni mwa Bahari ya Hindi ni kinyume cha sheria ya Hifadhi ya Bahari. Tumeshuhudia maeneo mengi yakivunjwa kwa nyumba zao baada ya kubainika yamejengwa katika hifadhi ya bahari. Haijafahamikaa mara moja kama eneo hili limeruhusiwa kuendelezwa, ikiwa ni tofauti na jengo la Hoteli ya Golden Tulip
  Sheria za Hifadhi ya bahari inasema ni marufuku kujenga nyumba mita 60 ilipokuwa bahari. Hali hii imeonekana kuwa tofauti baada ya kukuta hifadhi hii ikionekana kuanza kujengwa na kuanza kuzua maswali mengi kwa wadau wa maendeleo na Waanzania kwa ujumla wanaofuatilia mambo ya maliasili na utalii. Kibao hiki kinaonyesha jinsi eneo hilo lilivyotengwa kwa ajili ya kujenga jambo ambalo ni kinyume cha sheria za mita 60 za bahari.
  Gari likipita katika barabara inayoelekea katika barabara ya Golden Tulip Hoteli, ambayo pia inaonekana eneo hilo lililowekwa mabati kwa ajili ya kuanza kulijenga kama lilivyokutwa na mpiga picha wetu. na chini mkazi wa jiji la Dar es Salaam akipita katika eneo hilo, huku ikionekana ramani mbalimbali za ujenzi huo.

  0 0

  Daraja lililokuwa linawasumbua mno wakazi na wananchi wa Mbweni JKT, sasa linaelekea mwishoni, hali iliyoanza kuwafurahisha wananchi hao waliokuwa wakisumbuka kuvuka eneo hilo lililokuwa linajaa maji mara kwa mara yanayotoka baharini.

  Katika pita pita ya mitandaoni, tuliona picha hizi ambazo tayari zimeshapokewa kwa shangwe kutokana na wananchi hao kuanza kulitumia. Ikumbukwe kwamba kutokuwapo kwa daraja hili kulileta usumbufu mkubwa kwa wananchi. 

  Kabla ya uwapo wa daraja hili, magari yalilazimika kupita kwenye maji na pengine yanapokuwa mengi kushindwa kuvuka. Ni kutokana na daraja hili, shukrani za dhati ziende kwa JKT wanaojenga daraja hili, serikali Kuu kwa kupitia Mkuu wa Wilaya Kinondoni, DC Paulo Makonda na watendaji wote waliohakikisha kwamba utengenezaji wa daraja hili unakamilika ili kuondoa adha kwa wakazi na wananchi wa Mbweni JKT.

  Mkazi mmoja wa Mbweni aliyeshindwa kutaja jina lake alitumia muda mwingi kuwasifu wahusika kwa kulisimamia vyema daraja hilo litakalokuwa mkombozi kwa wananchi wa eneo hilo na wote wanaoishi jijini Dar es Salaam.
  Picha ya daraja hili la Mbweni JKT ilipigwa kwenye gari.

  0 0

    Wafanyakazi wa kampuni ya Mobisol wakikabidhi vifaa vya kuzalisha umeme wa jua kwa uongozi wa zahanati ya kijiji cha Ngasamo wilayani Simiyu katika  hafla iliyofanyika kijijini hapo kuadhimisha kufikisha wateja 30,000  wanaonufaika na umeme wa kampuni hiy

  -Mobisol yasherehekea mafanikio hayo kwa kutoa msaada wa nishati katika zahanati ya kijiji cha Ngasamo wilayani Simiyu.

  Kampuni ya Mobisol  yenye makao yake makuu mjini Berlini nchini ujerumani ambayo inajihusisha na uzalishaji wa umeme wa  jua tayari imewaunganisha wateja wapatao 30,000 nchini Tanzania katika kipindi cha miaka 2 tangia ianze kutoa huduma hizi barani Afrika.

  Kasi hii ya ongezeko la wateja wanaotumia umeme nishati ya jua kutoka kampuni hii inadhihirisha kuwa uwekezaji wake unaendana sambamba na kuunga mkono jitihada za serikali ya Tanzania za kupunguza tatizo la upatikanaji nishati ya umeme nchini.

  Katika kuadhimisha mafanikio ya kufikisha idadi ya wateja 30,000 Mobisol imetoa msaada wa kuinganisha na umeme wa nishati ya jua zahanati ya serikali ya kijiji cha Ngasamo kilichopo Simiyu ambapo anatokea mteja aliyejiunganisha na umeme wa kampuni hiyo akiwa anakamilisha idadi ya wateja 30,000  katika nchi hizi mbili  za Tanzania na Rwanda ambako  inatoa huduma zake.


  Akiongea wakati wahafla ya kutoa msaada huo iliyofanyika katika zahanati  hiyo,Meneja Masoko wa Mobisol, bwana Nkora Nkoranigwa amesema kuwa kampuni hiyo imejizatiti kuondoa tatizo la giza nchini na kuaikisha iawapatia wananchi umeme wa nishati ya jua wa uhakika kwa kutumia teknolojia ya kisasa na gharama nafuu.

  “Sote tunaelewa kuwa nishati ya umeme inahitajika katika kuleta maendeleo ya haraka na kuwaongezea vipato hususani wakazi wa vijijini.Tutahakikikisa tunaunga mkono jitihada za serikali za kuzalisha na kusambaza umeme kwa kwa wananchi hususani wanaoisi maeneo ya vijijini kwa gharama nafuu ii uwasaidia katika itihada zao za kujiendelea kimaisha”.Alisema

  Bwana Nkoranigwa Alisema umeme  ikipatikana utasaidia wananchi kuachana na matumizi ya vibatari na kufurahia matumizi ya vifaa vya kisasa kama jokofu,feni ,kuchaji simu na viginevyo na kuwezesha watoto kujisomea katika mazingira mazuri wawapo majumbani na mashuleni  hali ambayo itasaidia kuongeza kiwango cha ufaulu katika masomo yao.

  Mganga Mkuu wa wilaya hiyo Bwana Patrick Onyango alishukuru kwa msaada huo na kusema kuwa utawaondolea kero ya kukosa nishati ya umeme waliokuwa nayo kwa muda mrefu na itarahisisha utoaji wa huduma za matibabu kwa wagonjwa na aliahidi kuwa watahakikisha wanatunza vizuri vifaa vya nishati hiyo walivyozawadiwa “Kuna msemo kuwa akufaaye kwa dhiki ndio rafiki wa kweli”.

  Tunaishukuru kampuni ya Mobisol kwa msaada huu wa kusaidia wananchi wengi”Alisema.Naye Afisa Utawala wa Wilaya hiyo Bwana Rabani Mageja kwa niaba ya serikali alishukuru  kwa zahanati hiyo kupatiwa msaada wa nishati na aliongeza kuwa serikali wilayani humo itazidi kuunga mkono wawekezaji wanaokuja na miradi ya kusaidia kuleta maendeleo katika  jamii kama ulivyo mradi wa nishati wa Mobisol.

  Kwa upande wake  mteja wa  30,000 wa kampuni ya Mobisol ambaye alisababisha hafla hiyo kufanyika kijijini hapo na zahanati kupatiwa msaada Bwana Kichoro alisema kuwa amefurahi kuona kampuni imemuenzi kwa kuleta msaada wa nishati kwenye zahanati wa kuwanufaisha wananchi wote.

  Akiwa ni mteja wa umeme unaozalishwa na kampuni hiyo alisema ni wa uhakika na gharama nafuu na  unafanya maisha kuwa rahisi na kisasa na kuwataka wanakijiji wajiunge kwa aili ya kuishi maisha ya kisasa na kuweza kuanzisha miradi midogo midogo ya uzalishaji kwa utumia nishati hiyo.


  0 0  0 0


  MKUU  wa kitengo cha mipango katika Ofisi ya Ukaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali, Malima Nkilijiwando ambae pia ni mdau wa elimu ametimiza ahadi yake ya kuinunulia Shule ya Sekondari ya Misitu iliyopo kata ya Kivule- Ukonga jijini Dar es Salaam Kompyuta na mashine ya kutolea kopi pamoja na kuchapisha.

  Ahadi hiyo ameitimiza leo katika shule hiyo ikiwa aliahidi kipindi walipofanya mahafali ya kidato cha nne katika shule hiyo.

  Mkuu wa shule ya Sekondari ya Misitu, Pantaleo Maghari amemshukuru  Mkuu wa kitengo cha mipango katika Ofisi ya Ukaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali, Malima Nkilijiwando kwa kuwa na moyo wa kusaidia elimu katika shule hiyo kwani shule hiyo ilikuwa inakabiliwa na tatizo la kompyuta pamoja na mashine ya  kuchapishia mitihani na kutolea kopi mitihani.

  Shule hii inakabiliwa na tatizo la uchache wa meza na viti vya kukalia wanafunzi, mpaka  sasa shule hii ya Sekondari ina wanafunzi 931 ikiwa ina viti na meza 567 tuu. Alisema Maghari

  Licha ya hivyo Maghari alisema kuwa pia wanaupungufu wa walimu wa masomo ya Sayansi, vyumba vya madarasa pamoja na matundu ya vyoo  ikiwa mpaka sasa wanavymba vya madara 12 tuu na matundu ya vyoo matundu 12 sita sita kwa wasichana na wavulana ambavyo wanafunzi wanatumia kuanzia kidato cha Kwanza mpaka cha nne ambavyo havikidhi mahitaji ya wanafunzi.

  Aidha Maghari alitoa wito kwa wadau mbalimbali wa Elimu kuiangalia shule hiyo ya kata ya Kivyule kwa jicho jingine ili wanafunzi waweze kupata elimu vile inavyotakiwa.
   Mkuu wa kitengo cha mipango katika Ofisi ya Ukaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali, Malima Nkilijiwando akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika shule ya Sekondari ya Misitu iliyopo katika kata ya Kivule-Ukonga jijini Dar es Salaam kulia  ni Mkuu wa shule ya Sekondari ya Misitu, Pantaleo Maghari.
  Mkuu wa kitengo cha Mipango katika Ofisi ya Ukaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali, Malima Nkilijiwando akikabidhi baadhi ya msaada wa Kompyuta na (nukushi) Printa katika shule ya Sekondari ya Misitu iliyopo katika kata ya Kivule-Ukonga jijini Dar es Salaam ikiwa ni ahadi aliyoitoka katika mahafari ya shule hiyo. Kulia ni Mkuu wa shule ya Sekondari ya Misitu, Pantaleo Maghari akipokea msaada huo leo shuleni hapo jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa kitengo cha Mipango katika Ofisi ya Ukaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali, Malima Nkilijiwando akimkabidhi kifaa cha kupunguza umeme Mkuu wa shule ya Sekondari ya Misitu leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni kutimiza ahadi yake aliyoiaidi siku ya mahafali ya kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Misitu.
  Mkuu wa shule ya Sekondari ya Misitu akipokea baadhi ya vifaa vya Kompyuta kutoka kwa Mkuu wa kitengo cha Mipango katika Ofisi ya Ukaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali, Malima Nkilijiwando leo jijini Dar es Salaam . Nyuma ni wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Misitu wakishuhudia mkuu wao wa shule akipokea msaada huo ili kupunguza changamoto mbalimbali zinazowakumba walimu kwa kuwa walikuwa nanatumia pesa nyingi kwenda kutoa kopi nyingi za mitihani sehemu nyingine, hivyo basi hawatafanya hivyo kutokana na kutatuliwa changamoto hiyo.

  0 0

   Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, SSRA, Omar Kahlfan, (katikati), Mkurugenzi wa Uendeshaji wa PSPF, Neema Muro, (wapili kushoto), Meneja wa Mpango wa Uchagiaji wa Hiari wa PSPF,Mwanjaa Sembe, (wakwanza kushoto) na maafisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF, (kulia waliosimama), wakishuhudia Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayinhu, (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Michael Mhando, wakitia saini makubaliano ambayo yatawezesha taasisi hizo mbili kushirikiana ambapo Wanachama wa PSPF wa Uchangiaji wa Hiari, watadhaminiwa na Mfuko huo ili waweze kuingizwa kwenye utaratibu wa kupatia bima za afya kutoka NHIF. Makubaliano hayo yaliyofikiwa leo Jumatano Novemba 18, 2015 makao makuu ya PSPF jijini Dar es Salaam. 


  Na K-Vis Media/Khalfan Said

  MFUKO wa Pensheni wa PSPF, na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF, wameingia makubaliano yatakayowezesha wanachama wa PSPF, kupitia mpango wa Uchangiaji wa Hiari yaani PSS, kuanza kupata matibabu kwenye hospitali zote zenye mkataba na NHIF.


  Makubaliano hayo yametiwa saini leo Jumatano Novemba 18, 2015, kati ya Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw.Michael C.t.M Mhando na kufuatiwa na uzinduzi rasmi ambapo wanachama wa kwanza zaidi ya 10 wamepatiwa kadi za Bima ya Afya.


  Hafla hiyo ilifanyika makuu ya PSPF, jingo la Jubilee Towers jijini Dar es Salaam leo.

  Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Mayingu alisema, uamuzi huo wa PSPF kushirikiana na NHIF, ni utekelezaji wa malengo na ahadi za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais, Dtk. John Pombe Magufuli, ambaye aliwaahidi Watanzania wote wanapata huduma za afya zilizo bora. “  Katika kuhakikisha ahadi hiyo ya Mheshimiwa Rais inatimizwa PSPF kwakushirikiana na wenzetu wa Mfuko waTaifa wa Bima ya Afya tutatoa huduma za afya kwa wanachama wa Mpango wa Uchangaji wa Hiari wa PSPF.” Alsiema Bw. Mayingu katika hotuba yake. 

  Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw. Michael Mhando alisema, wakati PSPF wamebobea katika suala la pesheni, NHIF wao wamebobea katika kutoa huduma za afya, hivyo ushirikiano wa Taasisi hizi mbili zenye uzoefu wa kuhudumia maisha ya Watanzania, utakuwa umewapa unafuu mkubwa wa maisha, wajasiriamali wadogo ambao kwa kuwekeza katika afya kutawawezesha ushiriki kikamilifu katika shughuli za ujenzi wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Michael Mhando, (wapili kulia), wakizindua mpango huo huku Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Omar Khalfan akishuhudia
   Bw. Mayingu, (kushoto) na Bw. Mhando wakibadilishana hati baada ya kuzisaini.
   Bw. Mayingu akitoa hotuba yake.
    Bw. Mhando hotuba yake.
   Maafisa kutoka NHIF.

   Mwanachama wa PSPF, akisoma vipeperushi, vyenye maelezo na huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko huo.
   Mmoja wa waandishi wa habari akijaza fomu za kujiunga na Mpango wa Uchangiaji wa Hiari PSS.
   Kaimu Murugenzi Mtendajiw a NHIF, Bw. Michael Mhando (kushoto), akifurahia jambo na Meneja Uendeshaji wa PSPF, Bi. Neema Muro
   Mwanachama wa mpango wa Uchagiaji wa Hiari PSS, akipokea kadi ya bima ya Afya, kutoka kwa mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Omar Khalfan (kulia)
   Mwanachama wa PSPF, Constantine Edward (kushoto) akipokea kadi yake
   Meneja Msoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Costantina Martin,akitoa maelezowakati wa hafla hiyo.
   Meneja wa Mpango wa Uchangiajiwa Hiari, PSS, wa Mfuko wa Penshni wa PSPF, Bi.Mwanjaa Sembe, (wakwanza kulia), na afisa wa PSPF, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafaidika wakwanza wa mpango wa Mfuko huo kuwapatia matibabu wanachma wake wa mpango wa PSS

  Mzee Mohammed Madenge, watatu kushoto), ambaye ni Mwanachama wa PSPF, wakwanza kufaidika na mpango wa bima ya afya, akitoa neon la shkrani kwa niaba ya wenzake.

  0 0

  Kuimarika kwa uhifadhi wa misitu katika misitu ya tao la Mashariki iliyoko kwenye milima ya Usambara kumesaidia kuboresha shughuli za kijamii kwa wananchi wanaoishi kwenye vijiji kuzunguka misitu hiyo katika wilaya ya Muheza na Korogwe mkoani Tanga, mashamba haya ya mpunga ni katika kijiji cha Mkwakwani kata ya Mnyuzi wilaya ya Korogwe yamestawi vizuri kutokana na juhudi hizo za uhifadhi wa misitu, zinazofanywa na wadau mbalimbali wa uhifadhi ikiwemo wakala wa huduma za misitu nchini TFS na Mfuko wa kuhifadhi misitu ya tao la Mashariki EAMCEF juhudi ambazo zimesaidia kuimarisha mtiririko wa maji yanayotumika kwa shughuli za kijamii, ikiwemo kilimo cha umwagiliaji. Kilimo katika maeneo haya hakitumii mbolea wala kemikali za viwandani.
   Picha na Vedasto Msungu.

  0 0  0 0


  0 0

  SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF)  limeanza  kampeni  ijulikanayo kama NSSF Kwanza ambayo itafanyika katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, Kampeni hiyo imeanza kwa kuwafikia wakulima kwenye vijiji vyao na Mashamba yao  Mkoani Mbeya ili kuweza kuwapa elimu juu ya hifadhi ya jamii na faida zake.

  Kampeni hiyo imeanzia kwenye Kijiji cha Iyumpi wilayani Mbozi ambako wakulima wa Kahawa zaidi ya 44 wamejiunga na NSSF. Pia Kampeni hiyo inatarajia kwenda Wilayani Ileje, Vijiji vya Mloo na Igamba.

  NSSF inaendelea kuwasihi Wakazi wa Mbeya na Vitongoji vyake waendelee kujiunga na NSSF ili waweze kujipatia Mafao bora yakiwemo Bima ya Matibabu bure kwa Mwanachama na familia yake.
  Wakazi wa Kijiji cha Itumpi wilaya ya Mbozi wakiwa wamekusanyika ili kusikiliza elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa Wakulima kupitia Mpango maalumu wa Wakulima Scheme kwenye kampeni inayoendeshwa na NSSF ijulikanayo kama NSSF Kwanza.
   Afisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF,  Salim Kimaro akitoa elimu kwa wakazi wa kijiji cha Itumpi Wilaya ya Mbozi juu ya mpango wa Wakulima Scheme .
   Wakulima wa Kijiji cha Iyumpi wakisikiliza kwa makini maelezo yanayotolewa na wafanyakazi wa NSSF juu ya huduma zitolewazo na NSSF .
  Maafisa Matekelezo  Mkoa wa Mbeya wakitoa elimu jinsi ya kujaza fomu ya kujiunga na NSSF kwa mmoja wa wakulima wa Kijiji cha Iyumpi.
  Gari maalumu la matangazo la NSSF likiwa limefungwa mitambo ya matangazo ambalo hutumika kuzunguka mitaani na kutoa matangazo kwa wakazi wa vijiji mbalimbali vya mkoa wa Mbeya.

  0 0

  Anaitwa Yusuph Kisiba a.k.a Yuskiss Kisiba ambae ni Blogger @Lake Zone Media & Kisibasharesky Media, Graphics Desiner & Video Editor @Shafineys Film Production Jijini Mwanza.

  Na:George Binagi-GB Pazzo wa Binagi Media Group
  Tarehe kama ya leo (Nevemba 19) miaka kadhaa iliyopita alizaliwa hivyo hii leo anafurahia siku yake ya kuzaliwa na ndugu, jamaa na Marafiki. Nasi tunamtakia maisha mema katika kuzaliwa kwake.

  "Novemba 19 ni tarehe ambayo Mwenyezi Mungu aliweza kuniruhusu kutoka katika tumbo la mama yangu kipenzi na kuuona ulimwengu huu. 

  Na hapo ndipo safari yangu ilipoanzia na ikawa ndiyo chanzo cha kufahamiana na wewe hivi sasa. Novemba 19 ni siku ambayo huwa ya kipekee sana kwangu katika huzuni na furaha kutokana na kuishi mazingira haya ya ulimwengu uliojaa kila aina ya uzuri na ubaya wake.

  Ukiwa kama ndugu/rafiki yangu sina budi kukukumbusha kuungana nami kufanya ibada ikiwa na lengo moja la kumuomba  Mungu atusamehe makosa yetu. Kwa yeyote niliewahi kumkosea sina budi kukuomba radhi katika siku hii". Anasema Kisiba.

  0 0  SIMU.TV:  Rais Magufuli awekewa kigingi bungeni, serikali kurudisha viwanda vilivyouzwa, ahadi za rais zaanza kutekelezwa;

  SIMU.TV:  Mtihani wa kwanza kwa Rais Magufuli leo, kesi za rufaa Zanzibar kuunguruma Novemba 27, zimo za Mv.Spice Islander na Sheikh Farid; https://youtu.be/XT3SaS0mWoo

  SIMU.TV:  CCM, CUF Zanzibar sasa washindania mafusho, viti maalum vyazua balaa CHADEMA Zanzibar. Zitto kufufua makaburi bungeni; https://youtu.be/tTqc5K52ydY 

  SIMU.TV:  Makocha wachambua kipigo cha Taifa Stars, TFF yatoa pole kwa mashabiki. Simba yawatema rasmi Ndaw, Sserunkuma,  mikoa 10 yajitosa kikapu Taifa; https://youtu.be/jkvg46M1XZM  

  SIMU.TV:  Waziri mkuu kaa la moto, serikali yatoa agizo kupitia upya mikataba ya ubinafsishaji. Bomoa bomoa Dar Es Salaam yashika kasi; https://youtu.be/REOvUAUSdKs

  0 0

   Mkulima wa karafuu wilaya ya Wete akionyesha matawi ya mkarafuu yaliyokatwa na wezi shambani kwake kwa lengo la kuiba karafuu.


  Na Ali Mohamed
  SERIKALI imepiga marufuku uuzaji na ununuzi wa karafuu usio rasmi (vikombe) kuepusha wizi wa karafuu mashambani na ukataji wa mikarafuu unaofanywa na baadhi ya watu kutokana na kuzoeleka kwa biashara hiyo. 

  Wakizungumza katika nyakati tofauti Wakuu wa Wilaya za Unguja na Pemba wamesema hakuna ruhusa kwa mtu yoyote kuuza au kununua karafuu mbichi au kavu na atakaebainika kujihusisha na biashara hiyo atashughulikiwa ipasavyo.

  Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Hemed Suleiman Abdalla alisema tatizo la ununuzi wa karafuu kwa vikombe, wizi na ukataji wa mikarafuu kwa lengo la kuiba karafuu lipo.

  Alibainisha kuwa Serikali haiwezi kuvumilia makosa hayo kwa sababu wanaofanya uhalifu huo hawana imani na Serikali haina imani nao. Alifahamisha kuwa watakaokamatwa watachukuliwa hatua kwa misingi ya kisheria. 

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini ‘B’ Haji Makungu Mgongo alisema  Serikali ya Wilaya yake kupitia kamati za Ulinzi na Usalama ya Wilaya kwa kushirikiana na Masheha wataendesha zoezi maalumu la kuwakamata watu wanaojihusisha na masuala hayo na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.


  Alisema karafuu ni zao la uchumi wa Taifa hivyo Serikali ya Wilaya yake haitokuwa tayari kuona baadhi ya watu wakihujumu kwa wizi hasa kukata mkarafuu kwa tamaa ya kupata maslahi ya muda mfupi.

  Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Mohamed Omar Hamad alisema wizi wa karafuu ambao pia hupelekea kukatwa matawi na mikarafuu midogo unawakatisha tamaa wakulima.

  Nae Mkuu wa wilaya ya Wete ambae pia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Hassan Khatib Hassan alisema ukataji wa mikarafuu ni uhalifu mkubwa ambapo tatizo hilo limewahi kuripotiwa ofisini kwake.

  Alishauri kurejeshwa kwa utamaduni wa uchumaji karafuu kwa kambi ambapo Wakulima na Wafanyabiashara ni vyema wakajenga kambi katika maeneo wanayochuma karafuu, kufanya hivyo kutapunguza uhalifu unatokea katika mashamba yao.

  Wakuu hao wa Wilaya na baadhi ya Masheha walilishauri Shirika la ZSTC kuanzishwa dawati maalumu la kufatilia kesi za uhalifu dhidi ya karafuu na mikarafuu zinazoripotiwa katika vituo vya Polisi.

  Mapema akiwasilisha malalamiko hayo ya wakulima kuibiwa na kukatiwa mikarafuu yao kwa Wakuu hao wa Wilaya Mkurugenzi wa Mfuko wa Maedeleo ya Karafuu Ali Suleiman Mussa alisema matatizo hayo yanawaumiza sana Wakulima.

  Alisema wizi wa karafuu na ukataji wa mikarafuu unachangiwa na baadhi ya watu wanaonunua karafuu  mbichi ambapo kisheria ni kosa kwa vile Shirika la   ZSTC ndio Taasisi pekee  iliyopewa  mamlaka ya kununua na kuuza karafuu. 

  Alisema Shirika kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Karafuu umejipanga kufanya usajili wa wakulima wenye mashamba na wanaokodi karafuu ambapo watapewa vitambulisho maalumu vya kuwatambua. Alifahamisha kuwa utaratibu huo utazuia wizi wa karafuu kwa vile wezi hawatokuwa na nafasi ya kuuza karafuu ZSTC.

  Akizungumzia suala la ubora wa karafuu, Mkurugenzi huyo amewaomba Wakuu hao wa Wilaya kwa kushirikiana na Masheha kupiga vita uwanikaji usiozingatia ubora, (uwanikaji kwenye barabara, sakafu na juu ya bati) na kuwataka Wakulima kuendelea kutumia majamvi kwa shughuli za uanikaji.

  Katibu ambae pia ni Mwanasheria wa Shirika la ZSTC Ali Hilal Vuai aliwakumbusha Wakuu hao wa Wilaya na Masheha kuwa kukata mikarafuu kwa ajili ya kuiba karafuu ama kwa matumizi mengine  yoyote ni makosa kwa mujibu wa sheria namba 2 ya Maendeleo ya Karafuu ya mwaka 2014.

  Alisema sheria hiyo inakataza  kuihujumu mikarafuu kwa aina yoyote ile na atakaebainika kufanya vitendo hivyo anapaswa kupelekwa katika vyombo vya sheria.

  Aliwaomba Wakuu wa Wilaya kupitia Kamati zao za  ulinzi na usalama za Wilaya, Masheha na Polisi Jamii  kupambana na vitendo hivyo vya uhalifu dhidi ya biashara ya zao la karafuu vinavyofanywa na baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu.

  0 0

   Dar es Salaam, 19 November 2015– Lack of access to toilets is endangering millions of the world’s poorest children, UNICEF said today, pointing to emerging evidence of links between inadequate sanitation and malnutrition.

  Some 2.4 billion people globally do not have toilets and 946 million – roughly 1 in 8 of the world’s population – defecate in the open. Meanwhile, an estimated 159 million children under 5 years old are stunted (short for their age) and another 50 million are wasted (low weight for age).
   
  In Tanzania, access to improved toilets is still very low and, as a result, the country did not achieve the Millennium Development Goal (MDG) for water and sanitation. It is estimated that only one in three families (34 per cent) in Tanzania has access to improved toilets, with wide disparities between regions, across urban and rural areas. Access to improved sanitation in schools and health care facilities is also a concern. In addition, one in three children under five (35 per cent) is stunted.

  A report issued today, Improving Nutrition Outcomes with Better Water, Sanitation and Hygiene, from UNICEF, USAID and the World Health Organization, for the first time brings together years of research and case studies which demonstrate the link between sanitation and malnutrition. More importantly, it provides guidance for action. 

  Lack of sanitation, and particularly open defecation, contributes to the incidence of diarrhoea, cholera and to the spread of intestinal parasites, which in turn cause malnutrition.

  “We need innovative solutions to an old problem that has huge, negative consequences for children. Without innovation, children will continue to suffer from preventable diseases including cholera”, said Dr. Jama Gulaid, UNICEF Tanzania’s Representative.

  Globally, diarrhoea accounts for 9 per cent of the deaths of children under 5 years old each year and is essentially a faecal-oral disease, where germs are ingested due to contact with infected faeces. Where rates of toilet use are low, rates of diarrhoea tend to be high.


  Children under 5 years old suffer 1.7 billion cases of diarrhoea per year. Those in low income countries are hit hardest, with an average of three episodes per year. The highest frequency is in children under 2 years old, who are weakest and most vulnerable. Multiple episodes of diarrhoea permanently alter their gut, and prevent the absorption of essential nutrients, putting them at risk of stunting and even death. 

  Some 300,000 children under 5 years old die per year – over 800 every day – from diarrhoeal diseases linked to inadequate water, sanitation and hygiene. The poorest children in sub-Saharan Africa and South Asia are particularly at risk.

  Intestinal parasites such as roundworm, whipworm and hookworm, are transmitted through contaminated soil in areas where open defecation is practiced. Hookworm is a major cause of anaemia in pregnant women, leading to malnourished, underweight babies.

  0 0

  Mkuu wa kitengo cha Bidhaa katika benki ya Barclays, Oscar Mwakyusa na Kaimu mkuu wa kitengo cha Masoko benki ya Barclays, Joe Bendera wakiwa wameshika picha ya kombe la mpira ambayo litatembezwa Disemba 3 na 4 mwaka huu jijini Dar es Salaam kwaajili ya wapenzi wa mpira wa miguu kupiga nalo picha ikiwa mwaka huu benki ya Barclays ni mwisho wa kudhamini ligi kuu uingereza.
  Kaimu Mkuu wa kitengo cha Masoko benki ya Barclays, Joe Bendera akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na benki hiyo kutembeza kombe la Barclays premier ligi ya Uingereza kulitemeza jijini Dar es Salaam kwaajili ya wapezi wa soka jijini hapa kupiga nalo picha ambazo itakuwa kumukumbu kwao.Kusoto ni Grace Josef na kulia ni Rhobina Justine wakiwa ni miongoni wa washiriki wa benki hiyo katika kutembeza kombe hilo jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa kitengo cha Bidhaa katika benki ya Barclays, Oscar Mwakyusa akizungumza na waandishi wa habari kuhuriana na ratiba ya kombe hilo litakavyokuwa likizungushwa ili wapenzi wa soka kupiga picha na kombe ikiwa benki ya Barclays ni mwaka wa mwisho kudhamini ligi ya Uingereza.

  BENKI  ya Barclays hapa nchini inatarajia kuwaletea wapenzi wa soka kombe la ligi kuu ya Uingereza kwa ajili ya kupiga nalo picha ikiwa mwaka huu ni mwisho wa benki hiyo kudhamini ligi kuu nchini Uingereaza, Pia wananchi wameombwa kujitokeze kufungua akaunti kwa ajili ya mshara katika benki hiyo ili kujishindia tiketi mbili za kwenda kuangalia ligi kuu ya Uingereza.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar,Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Masoko benki ya Barclays, Joe Bendera alifafanua kuwa  "Wapenzi wa soka wajitokeze kwa mujibu wa ratiba ya benki a Barclays kwaajili ya kugipatia picha wakiwa na kombe la benki hiyo ikiwa ni mwaka huu ni wa mwisho kudhamini ligi kuu ya Uingereza iliyokuwa ikijulikana kama Barclays Premier League." Bendera 

  Nae Mkuu wa kitengo cha Bidhaa katika benki ya Barclays, Oscar Mwakyusa  amesema kuwa  Disemba 3 mwaka huu kombe hilo litaanzia katika tawi kuu la benki benki hiyo Posta kuelekea Mwembe yanga kupitia barabara ya Pungu mpaka Temeke Hospitali, Uwanja wa Taifa, kituo cha magari cha Mombasa na kumalizia viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.

  Na Disemba 4 litaanzia kutembezwa kutokea katika benki ya Barclays tawi la Alpha kuelekea ofisi za IPP Media, Mlimani City, tawi la benki hiyo la Slip way Kinondoni Biafra, Mazese Darajani na kuishia katika viwanja vya Karume jijini Dar es Salaam.

  Aidha Mwakyusa aliyoa wito kwa wapenzi wa soka kujitokeza kwa wingi kwaajili ya kupiga picha na kombe la ligi kuu ya Uingereza ambapo mwaka huu ni mwisho wa benki ya Barclays kudhamini ligi kuu Uingereza.

  0 0


   Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Dianna Melrose (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF), Koshuma Mtengeti (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Wanawake wa Afya, Utafiti na Maendeleo (Forward), Naana Otoo-Oyortey MBE, wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Filamu ya Simulizi halisi ya Ghati na Rhobi ulifanyika nyumbani kwa balozi huyo, Oysterbay Dar es Salaam jana.
   Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Dianna Melrose (kulia), akizungumza kabla ya uzinduzi wa filamu hiyo.
   Mwakilishi kutoka taasisi ya DFID, Jane Miller OBE (kushoto), akizungumza katika uzinduzi huo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF), Koshuma Mtengeti na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Wanawake wa Afya, Utafiti na Maendeleo (Forward), Naana Otoo-Oyortey MBE.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Wanawake Tanzania, Mary Rusimbi (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo.
   Wadau mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo.
   Sehemu ya filamu hiyo inavyoonekana.
   Sehemu ya filamu hiyo inavyoonekana.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Wanawake wa Afya, Utafiti na Maendeleo (Forward), Naana Otoo-Oyortey MBE (katikati), akichangia jambo katika uzinduzi huo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF), Koshuma Mtengeti (kulia), akielezea kuhusu filamu hiyo na changamoto mbalimbali za ukeketaji nchini.


  Na Dotto Mwaibale

  LICHA ya MKOA wa Dar es Salaam kuwa na watu wenye uelewa mkubwa lakini unaongoza kwa asilimia 38 ya ukeketaji imeelezwa.

  Hayo yalibanishwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto Wizara ya Wanawake na Watoto, Margaret Mussai Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa Filamu ya Simulizi halisi ya Ghati na Rhobi uliofanyika nyumbani kwa Balozi wa Uingereza hapa nchini.

  "Hali ya ukeketaji hapa nchini bado ni changamoto kubwa kutokana na jamii kutokuwa na uelewa mkubwa ikiwa ni pamoja na mila za baadhi ya makabila" alisema Mussai.

  Alisema suala la ukeketaji limekuwa na changamoto kubwa kwa sababu ya wahusika wanaofanya ukeketaji wanatengeneza fedha na kwa msichana anayefanyiwa kitendo hicho anaonekana kuwa na thamani kuliko yule ambaye hajakeketwa.

  Alisema kwa mkoa wa Dar es Salaam kuna maeneo ambayo yanaongoza kwa ukeketaji na wasichana hupenda kufanyiwa hivyo ili waonekane wenye heshima.

  Alisema mkoa wa Dar es Salaam una asilimia 38 ya ukeketaji, Mara asilimia 58, Shinyanga asilimia 55 huku ikifuatia mikoa mingine.

  Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Dianna Melrose filamu hiyo inawahusu wasichana wawili ambao wanapinga ukeketaji katika jamii yao.

  Alisema wasichana hao waqnaonesha ujasiri wa kukataa kitendo hicho chenye maumivu makali na kwa msaada wanafanikiwa kubadisha jinsi jamii yao inavyomchukulia msichana katika kipindi chake cha mpito kutoka usichana hadi kwenda kufikia utu uzima.

  "Filamu hii inaonesha kwamba si jamii zote ndani ya Tanzania zinazojihusisha na ukeketaji na kwamba maeneo mengi wameamua kuachana na ukeketaji na kuamini kwamba ukeketaji unawezwa kutokomezwa" alisema Melrose.

  Alisema mtoto wa kike ana haki ya kusomeshwa na kuendelezwa badala ya kuachwa nyumbani na kufanyiwa vitendo hivyo vinavyodumaza jamii kimaendeleo.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF), Koshuma Mtengeti alisema changamoto kubwa ni sheria ya makosa ya ukeketaji kuto kuwa na meno kwani ni mtu mmoja tu aliyehukumiwa kati ya watu 43 waliobainika na makosa hayo.  


  Filamu hiyo imeandaliwa na ubalozi huo kwa kushirikiana na Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF) na Mfuko wa Wanawake wa Afya, Utafiti na Maendeleo (Forward).

  0 0

  Watoto wawili wa familia moja wakazi wa mkoani Singida wamefariki mara baada ya kuangukiwa na nyumba kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani humo. https://youtu.be/E4vbul_POEc
  Mkuu wa wilaya ya Tarime amewataka viongozi wa halimashauri ya walayani humo kuacha siasa maofisini badala yake wawajibike ipasavyo. https://youtu.be/WeGWoXpvFa8
   Bodi ya Korosho nchini imesema itaendelea kutoa asilimia 7 ya ushuru  wa mauzo ya Korosho nje ya nchi kwa lengo la kuimarisha shughuli za utafiti wa zao hilo; https://youtu.be/X4SDodiqSxQ

  Inaelezwa kuwa mauzo ya hisa katika soko la hisa la Dar es Salaam yaanza kuongezeka baada ya kushuka wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania; https://youtu.be/sketAaFAyPw
  Mfuko wa pensheni wa PSPF imeingia makubaliano na mfuko wa bima wa  taifa wa NHIF kwa lengo la kutoa bima ya afya kwa wananchama wa PSPF. https://youtu.be/CDoSmMTvtIY
  Raisi wa shirikisho la mpira wa miguu nchini,Bwana Jamal  Malinzi amewataka watanzania kuwa wavumilivu na timu yao ya tifa,Taifa Stars. https://youtu.be/zEOIV3pSjxg
  Wabunge wateule wa serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania wamemtaka waziri mkuu ajaye kusimamia serikali ipasavyo; https://youtu.be/pf3wnk-ZIfU

  Serikali ya manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam imepiga marufuku uuzaji wa viwanja kiholela kwa lengo la kuepusha migogoro ya ardhi. https://youtu.be/seBn8GURMpE
  Inaelezwa kuwa hukumu inayomkabili katibu wa jumuiya za kiislamu Tanzania Sheikh Issa Ponda imeharishwa adi tarehe 30 mwezi wa 11 mwaka huu. https://youtu.be/Y29MTgmOKV8
  Serikali kupitia wizara ya nishati na madini imeliagiza shirika la umeme TANESCO kuimarisha kitengo chake cha ukaguzi kuongeza mapato. https://youtu.be/VfxKyrTqTuI
  Raisi wa TFF amesema kipigo ilichokipata Taifa Stars haikihusu uongozi wake kwani TFF imewapa wachezaji kila kitu wanachokita; https://youtu.be/afJ-tr4QmbI

  Klabu ya Simba imetangaza kuwaacha wachezaji wawili katika dirisha hili dogo la usajili.https://youtu.be/JZEI5I_m4tY

  [12:09:52 AM] samwel kamugisha: Taratibu za kukabidhi jina la waziri mkuu bungeni zatolewa ufafanuzi na mkuu wa kitengo cha habari,elimu na mawasiliano cha Bunge. https://youtu.be/NlIfe1rLAN8

  Kitendawili cha wawania kiti cha naibu spika chafikia patamu baada ya wanawake wawili kuwekwa hadharani.https://youtu.be/MHLVC72sWzc
  Makamo wa Raisi wa Tanzania Bi.Samia Suluhu aapa kupambana na uzembe hasa katika suala la utendaji serikalini. https://youtu.be/uoyVms8ey0w

  Tanzania yaelezwa kushika nafasi ya kwanza duniani kwa kuzalisha korosho bora lakini cha kusikitisha ni kwamba Tanzania huuza korodho ghafi nje ya nchi. https://youtu.be/LAAjTzlT9Fc
  Shamra shamra zaendelea kutawala katika viwanja vya bunge huku baadhi ya wabunge wakipongezwa na wageni na familia zao. https://youtu.be/275wNDk17j4
  Mwanasheria mkuu wa serikali atoa ufafanuzi juu ya hoja na mambo mbalimbali yaliyoibuliwa na viongozi wa UKAWA kabla ya raisi Magufuli kuhutubia bunge. https://youtu.be/Fjh_jVY3uEg
  Saa chache zijazo jina la atakaye kuwa waziri mkuu wa 11 wa Tanzania litafahamika na kutangazwa bungeni huku baadhi ya watu wakihusishwa. https://youtu.be/QsP5eif6QHY

  0 0  0 0

  Waziri Mkuu mpya Mh. Kassim Majaliwa.

  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, muda mfupi uliopita limepitisha jina la Mbunge wa Jimbo la Rwangwa, Mh. Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Serikali ya awamu ya tano baada ya jina lake kupelekwa Bungeni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

  Mh. Majaliwa amepitishwa kwa kura 258 sawa na asilimia 73.5% ya kura zote za ndio.

  0 0

   Mhandisi wa Manispaa ya Kinondoni, Baraka Mkuya akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salam leo na kuwaomba wananchi wa eneo la Basihaya kata ya bunju kuwa watii wa sheria bila shuruti wakati wa ubomoaji wa majengo yaliyojengwa kwenye sehemu za wazi, pia amewahi wananchi kujua maeneo ya wazi yaliyo karibu nao, pia ameongezea kuwa wananchi wakiona maeneo ya wazi yanajengwa watoe taarifa manispaa ya Kinondoni au wizara ya Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi.
  Ubomoaji wa maeneo ya wazi katika Mtaa wa Basihaya Kata ya Bunju jijini Dar es Salaam Ukiendelea.
  Wananchi wakiondoa mbao katika eneo la wazi walipokuwa wameziweka ili kupisha ubomoaji uniendelea.

older | 1 | .... | 689 | 690 | (Page 691) | 692 | 693 | .... | 1897 | newer