Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 673 | 674 | (Page 675) | 676 | 677 | .... | 1896 | newer

  0 0

  Na Mwandishi Wetu
  RAIS Jakaya Kikwete ambaye siku chache zijazo atamaliza muhula wake wa pili na wa mwisho wa kuiongoza Tanzania, amewaaga watumishi wa umma nchini kwa kutoa rai kuwa ili kuendeleza mageuzi katika kuwatumikia wananchi ni vyema wakautumia vyema mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).

  Rais Kikwete aliyasema hayo katika sherehe maalum iliyoandaliwa na watumishi wa umma kumuaga na kufanyika Dar es Salaam Alhamisi usiku. Watumishi wa umma walitumia fursa hiyo kumpa Rais tuzo na zawadi mbalimbali na kumshukuru kwa mageuzi makubwa aliyoyaasisi katika kuboresha maslahi ya watumishi na mfumo mzima wa mageuzi.

  Akitaja moja ya mambo ambayo Rais Kikwete atakumbukwa nayo, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alisema kuasisiwa kwa mfumo wa usimamizi na utekelezaji wa miradi wa BRN katika awamu ya pili ya Rais Kikwete kumesaidia kuongeza nidhamu ya utendaji unaopimika na ambao umesaidia kuleta mageuzi makubwa.

  “BRN imeleta nidhamu ya kuweka vipaumbele, kuvifuatilia kwa karibu na kuwawekea watumishi mfumo wa kupimwa kutokana na yale waliyotakiwa kuyatekeleza. Tunakushukuru kwa kuasisi mfumo huu,” alisema.

  Akionekana kufafanua hilo, Rais Kikwete alieleza historia na chimbuko la BRN kuwa ni matokeo ya mafanikio ya ziara zake za nje ya nchi ambapo akiwa Malaysia alijifunza jinsi nchi hiyo ilivyopata maendeleo makubwa na ya haraka kupitia mfumo kama wa BRN.

  “Si vibaya kuiga jambo jema. Niliposikia kuhusu ufanisi wa mfumo huu kule Malaysia niliomba fursa ya kuelezwa zaidi na ndipo nasi tukakubaliana kuuanzisha hapa nchini. Na katika kipindi kifupi zile sekta za mwanzo zilizoingizwa katika BRN utofauti umeanza kuonekana,” alisema Rais Kikwete.

  Akifafanua kuhusu mfumo huo unavyofanyakazi Rais aliongeza kuwa moya ya nidhamu za BRN ni kufanya uchambuzi wa kina wa kimaabara ambapo wataalum wa sekta husika; kutoka sekta za umma na binafsi hukaa pamoja ili kuchambua, kubaini changamoto na namna ya kuzifanyia utatuzi.

  Aliongeza kuwa baada ya kubaini mambo yanayohitaji kufanyiwakazi, mfumo wa BRN unasisitiza katika kuchagua vipaumbele vichache ambavyo hutekelezwa kwa mfumo wenye usimamizi madhubuti, ukomo wa utekelezaji huku pia wahusika wakisaini mikataba ya kuhakikisha malengo waliyowekwa yanatokea.

  “Huu ni mfumo wa utendajikazi ambao kila mmoja wetu anapaswa kuuchukua na kuutumia kuendesha shughuli zake,” alisema Rais huku akitoa mfano wa Mahakama ya Tanzania ambao waliichukua nidhamu BRN katika kupunguza mrundikano wa kesi hata kabla sekta hayo haijaingizwa rasmi katika BRN.

  “Siku moja Jaji Mkuu akaniambia kuwa wameanzisha BRN yao ambapo kila Jaji alipewa lengo na idadi ya kesi za kufanyiakazi kwa mwaka  na kweli baada ya muda mfupi ule mrundikano wa kesi ukapungua sana,” alisema Rais na kusisitiza.

  Sekta za awali zilizoingizwa katika BRN tangu Julai 2013 ni elimu, kilimo, nishati, maji, uchukuzi na ukusanyaji wa mapato. Kutokana na mafanikio yaliyoanza kuonekana katika sekta hizo Julai mwaka huu sekta za afya na uboreshaji wa mazingira ya biashara nazo zimeanza kusimamiwa kupitia mfumo wa BRN.


  0 0

  Afisa vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Godfrey Massawe (aliyesimama) akifuatilia majadiliano ya wawezeshaji kitaifa wakati wa kazi za kikundi kwenye Mafunzo ya Uwezeshaji wa Stadi za Maisha yaliyofanyika Kanda ya Ziwa.


  Na: Genofeva Matemu - Maelezo

  ILIGUNDULIKA kuwa ulimwenguni kote na hususan nchini Tanzania, Vijana walio nje ya shule ni miongoni mwa makundi yaliyo katika hatari ya magonjwa yanayoenea kwa njia ya ngono, VVU na UKIMWI kwa kutokuwa na taarifa na stadi za kuwaongoza hivyo kupoteza kundi kubwa la vijana ambalo ni taifa la kesho.


  Ufumbuzi wa tatizo hili umeweza kufanyika kwa kuwapa vijana stadi za maisha zenye upeo mpana wa maarifa na stadi zinazoweza kuwasaidia vijana kuendana na mazingira shindani yanayobadilika.


  Stadi za maisha ni moja kati ya mikakati iliyobainika kuleta mabadiliko ya tabia za mtu. Stadi hizi uhusisha stadi na uwezo wa kujenga tabia njema ili kuepukana na matatizo yaliyopo katika maisha ya kila siku.


  Mkabala wa stadi za maisha unalenga katika kuendeleza na kukuza stadi zinazoitajika katika mahitaji ya maisha ya kila siku kama vile mawasiliano, kufanya maamuzi, fikra, kuhimili mihemko, uthubutu, ujenzi wa kujiamini, kuzuia shinikizo rika pamoja na mahusiano.


  Mkabala huu pia unashughulikia ukuaji wa mtu ili awe na stadi za kumwezesha kutumia aina zote za taarifa kuhusiana na masuala kama vile magonjwa ya ngono, VVU na UKIMWI.

  Mahitaji ya stadi za maisha miongoni mwa vijana ni mengi na yanatofautiana baina ya vijana wadogo na wakubwa, vijana walio nje ya shule na walio shuleni, pamoja na walio na wasio katika ndoa hivyo kupelekea kuwa na viwango vya mafunzo ya stadi za maisha vilivyopendekezwa na kubuniwa kuwanufaisha vijana wasio mashuleni.


  Wizara inayosimamia masuala ya vijana imekua ikitoa mafunzo ya stadi za maisha kwa vijana walio nje ya shule ili kuwapa vijana stadi za kukabiliana na changamoto za kila siku katika maisha yanayowazunguka.


  Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa kushirikiana na shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA) wameweza kufikisha elimu ya stadi za maisha kwa wawezeshaji wa kitaifa kutoka kanda ya Ziwa hivi karibuni ili kuweza kusambaza elimu hiyo kwa vijana walio nje ya shule maeneo yote ya kanda ya ziwa hivyo kuwawezesha vijana kukabiliana na dunia hii ya sasa ya sayansi na teknolojia.


  Akifungua mafunzo ya wawezeshaji kitaifa kutoka kanda ya Ziwa yaliyofanyika Mkoa wa Mwanza hivi karibuni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga aliwataka wawezeshaji kitaifa wa stadi za maisha kuwasaidia vijana kujitoa katika mitazamo hasi na kuleta mabadiliko chanya katika jamii kwani vijana ndio nguvu kazi ya Taifa hili.  “Vijana wakijiimarisha katika shughuli za kijamii na kiuchumi wataepuka kuzungukwa na vihatarishi vya maisha kama vile VVU na Ukimwi, mimba zisizotarajiwa pamoja na dawa za kulevya hivyo kujenga nchi kwa kutumia nguvu kazi ya vijana” alisema Bibi. Nkinga.


  Mafunzo ya stadi za maisha yamekua yakiongeza hali ya kujiamini kwa vijana na kutoa mbinu za kukabiliana na matatizo ya maisha kwa kuwapa vijana uwezo wa kutumia muda wao kikamilifu kuzungumza na watu wasiowajua kuliko ilivyokua hapo awali.


  Aidha Bibi. Nkinga alisema kuwa matarajio ya serikali ni kuona vijana wa kitanzania  wanajitambua kua wao ni nani, wanaenda wapi, na watafikaje kwa kujua uwezo na udhaifu binafsi walionao ili  waweze kupanga malengo waliyonayo na kuyatekeleza kulingana na fursa zilizopo.


  Vijana wanaopata fursa ya kuwezeshwa katika stadi za maisha wameongeza viwango vyao vya stadi za kujitambua na uwezo wa kuwasiliana na watu wa rika zote hivyo kubadili tabia za vijana wa rika mbalimbali.


  Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. James Kajugusi amesema kuwa kila kijana ana sifa za kujiunga na mafunzo ya stadi za maisha zitakazowawezesha kukataa visingizio kama vile umasikini, maradhi na masuala yanayoshauriwa na marafiki ambayo yanaweza kuwaingiza katika vishawishi.


  Bw. Kajugusi amesema  kuwa Mafunzo ya stadi za maisha yamelenga kupata waelimishaji wa kitaifa wa stadi za maisha watatu kutoka kila mkoa katika mikoa yote ya Tanzania bara ambao watawafikia waelimishaji rika wa kila mkoa ili kuweza kufikisha elimu waliyoipata kwa vijana wa rika mbalimbali katika Mikoa, Wilaya, kata, vijiji, vitongoji, mitaa, vijiwe na sehemu rasmi za shughuli za vijana.


  Stadi za maisha zinaweza kuwekwa katika makundi matatu ambayo ni stadi za maisha kwa ajili ya kujitambua, kwa ajili ya fikra na kwa ajili ya mahusiano baina ya watu hivyo kwa pamoja aina hizi huweza kutoa majibu kwa vijana kuwa wao ni nani, wanataka kwenda wapi na watafikaje hapo wanapotaka kwenda.


  Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bibi. Susan Ndunguru amesema kuwa vijana waliopata mafunzo ya uwezeshaji wa stadi za maisha ni mabalozi ambao kama watatumia vizuri uwezo walioupata katika mafunzo hayo watabadili fikra za vijana wengi nchini hivyo kuweza kujenga taifa lenye afya nzuri, weledi pamoja na ujuzi.

  Stadi za maisha humjenga kijana kufanya maamuzi sahihi hivyo kuondokana na majuto na kumfanya kuwa huru katika kutoa maamuzi binafsi.


  Kwa kawaida stadi za maisha humpa kijana mwitikio wa uthubutu unaompa fursa ya kusimamia anachotaka au anachoamini bila kumdharau au kuumiza kihisia mtu mwingine.

  Mtaalamu wa masuala ya Stadi za Maisha Bw. Benny Lugoe amesema kuwa  wawezeshaji wa kitaifa waliopata Mafunzo ya Stadi za Maisha wana ari na motisha ya kujifunza na kama wataendelea kuwa na ari hiyo watakua wabunifu na wawezeshaji wazuri kwa vijana ndani ya jamii wanazoishi.


  Aidha Mwezeshaji wa Kitaifa wa Stadi za Maisha kutoka Mkoa wa Shinyanga Bw. Ezra Manjerenga amesema kuwa vijana wa Mkoa wa Shinyanga wamekua wakikabiliwa na ukosefu wa elimu ya afya ya uzazi hivyo ugeni wa mafunzo ya stadi za maisha katika Mkoa huo utawavutia vijana wengi jambo ambalo litapelekea kutimiza lengo la serikali kufikisha mafunzo hayo kwa vijana wa rika mbalimbali.


  Stadi za maisha zinatoa fursa kwa vijana kupata taarifa za afya ya uzazi na upatikanaji wa huduma ya afya ya uzazi, pia humpa kijana haki ya kutambuliwa, kusikilizwa na kuheshimiwa utu wake bila kujali kiwango cha elimu, hadhi yake au sifa nyingine itakayombagua na kumuweka katika mazingira hatarishi.


  Vijana waliopata mafunzo ya stadi za maisha wamepewa dhamana na serikali kwenda kuwatumikia vijana na kuhakikisha kuwa uhamasishaji wa mabadiliko chanya miongoni mwao ili kuweza kuachana na tabia zote hatarishi na kushiriki vyema kwenye shughuli za uzalishaji mali.


  Serikali inatambua kuwa vijana ni rasilimali muhimu kwa ajili ya ukuaji wa uchumi na kwa ajili ya maendeleo ya nchi kwa ujumla hivyo kusimamia kwa ukaribu zaidi elimu ya stadi za maisha kwa vijana wote nchini.   0 0

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akifanya ziara ya kukagua maandalizi ya kazi za usafishaji wa karo zinazohudumia uhifadhi ya Uchafu katika Nyumba za Maendeleo zilizopo Mtaa wa Mtemani Mjini Wete Kisiwani Pemba. Kushoto ya Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mh. Mar Khamis Othman. 
   Mkurugenzi wa Baraza la Mji wa Wete Kisiwani Pemba Ndugu Mgeni Othman Juma akitoa maelezo mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif juu ya hatua zilizochukuliwa katika kufanya usafi wa karo za Nyumba za Maendeleo Mtemani  Mjini Wete.
   Balozi Seif akiushauri Uongozi  wa Wizara ya Ardhi na Makaazi kuandaa utaratibu za kuzifanyia ukaguzi Nyumba za Maendeleo ili kukabiliana na changamoto zinazozikabili Nyumba hizo ikiwemo matengenezo ya kila mara.
  Picha na – OMPR – ZNZ.

  UONGOZI wa Wizara na Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Kisiwani Pemba kwa kushirikiana na Baraza la Mji wa Wete umeanza matayarisho ya kujiandaa na kazi ya usafishaji wa karo zilizotengwa kuhifadhi uchafu unaotoka katika  Nyumba za Maendeleo zilizopo Mtaa wa Mtemani Mjini Wete Kisiwani Pemba.

  Kazi hiyo imeanza kwa hatua ya awali ya uchimbaji  wa mashimo yatakayotumika kufukia mabaki ya uchafu utakaosafishwa kutoka kwenye Karo  Saba  zinazohudumia Nyumba hizo zilizojengwa katika miaka ya sabini.

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa Kisiwani Pemba alipata fursa ya kukagua hatua iliyofikiwa ya  kazi hiyo itakayosaidia kuimarisha hali ya usafi pamoja na utunzaji wa  mazingira katika Mtaa huo.


  Mkurugenzi wa Baraza la Mji wa Wete Pemba Ndugu Mgeni Othman Juma alimueleza Balozi Seif kwamba Wananchi wa Nyumba za Maendeleo Mtemani Wete wamewahi kujaribu kufanya usafi katika  eneo hilo bila ya kupata mafanikio yoyote.

  Ndugu Mgeni alisema changamoto zilizowakumba wakaazi hao na kushindwa kukamilisha  kazi waliyoamua kuitekeleza zilitokana na ukosefu wa vifaa vya kufanyia kazi ambavyo vinahitaji gharama kubwa.

  Naye Afisa Ujenzi Mkoa wa Kaskazini Pemba Ndugu Badru Hamad Hassan alisema kwamba kazi hiyo ingekuwa imeshamalizika kama uwezo wa kifedha ungeruhusu kuwalipa Vijana walio tayari kutekeleza jukumu hilo.

  Nd. Badru alisema kazi yote inayohitaji usafishaji wa kina kwenye mashimo ya karo hizo Saba inahitaji jumla ya shilingi Laki saba ambazo kwa hivi sasa tayari Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Pemba imeshatoa ahadi ya  kuzitafuta ili kazi hiyo ianze na kumalizika mapema kabla ya kuanza  kwa mvua za Vuli.

  Akitoa nasaha zake Makamu wa Pili  wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba  Nyumba za Maendeleo zilizojengwa katika maeneo mbali mbali ya Visiwa vya Unguja na Pemba  zililenga kuwapatia makaazi Bora wananchi wa Visiwa hivi.

  Balozi Seif alisema wazo la Taasisi hizo mbili za Umma la kufanya usafi ni zuri kwa vile mbali ya kulinda Afya za Wananchi hasa Watoto  wadogo lakini pia  litasaidia kuimarisha mazingira mazuri katika eneo hilo la Mji.

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwashauri watendaji wanaosimamia nyumba hizo kujitahidi kuweka utaratibu maalum utakaowapa muda maalum wa kufanya ukaguzi wa nyumba hizo ili kujua athari na baadaye kuitafutia ufumbuzi katika kipindi muwafaka.

  Ujenzi wa Nyumba za Maendeleo  katika Wilaya zote za Visiwa vya Unguja na Pemba uliosimamiwa na Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume ulifanywa ili kuwajengea mazingira bora ya Makaazi Wakwezi na Wakulima mara tu baada ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964.

  0 0

  Na Father Kidevu Blog
  WANANCHI wilayayani Newala wamehakikishiwa usalama wa kutosha siku ya kupiga kura na kutakiwa kujitokeza kupiga kura na kuwachagua viongozi wao bila wasiwasi wowote.

  Akizungumza na Habarileo kwa njia ya simu, Mkuu wa Wilaya ya Newala, Christopher Magala amesema wakazi wa Newala husususani katika majimbo ya uchaguzi ya Newala Mjini na Newala vijini wasiwe na hofu juu ya amani siku ya kupiga kura.

  “Nitumie nafasi hii kuwatoa hofu wananchi na kuwahakikishia usalama wenu na mali zenu, kwamba siku ya kupiga kura hakutakuwa na vurugu zozote, Hivyo wale wote waliojiandikisha kupiga kura wajitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura siku hiyo bila wasiwasi wowote,”alisema Magala.

  Magala amesema wananchi waendelea kuilinda na kuitunza amani katika kipindi hiki cha kumalizia kampeni na kipindi chote cha siku ya Uchaguzi na baada ya Uchaguzi pasipo kuvuruga amani na utulivu uliopo Wilayani humo.

  “Katika kipindi hiki cha kumalizia kampeni na kipindi chote cha siku ya Uchaguzi na baada ya Uchaguzi, tuendelee kuitunza amani iliyopo katika Wilaya yetu; upendo na mshikikamano tuliona siku zote tuuimarishe zaidi kipindi hiki ili tuvuke salama na kubaki salama baada ya zoezi la uchaguzi kukamilika,”alisema Magala.

  Aidha amesema Serikali imejipanga vizuri kuimarisha doria katika kipindi cha  siku za mwisho za kampeni, wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi.

  Magala amesema ni haki ya kila mwananchi aliyejiandikisha kupiga kura kutimiza haki yake ya kumchagua kiongozi anayemtaka katika nafasi ya Urais, Ubunge na Udiwani katika mazingira tulivu yasiyo nafujo na hivyo kuwataka wananchi kufanya hivyo na wakishapiga kura warudi majumbani na kusubiri kutangazwa matokeo.

  “Niwatahadharishe, kama wapo, Wananchi wanaokusudia kuvuruga Uchaguzi kwa namna yoyote ile kwamba Serikali haitawavumilia. Hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yao. Vyombo vya Ulinzi vyote vipo ‘standby’ kuhakikisha utulivu unakuwepo wakati wa kwenda kupiga kura na baada ya Uchaguzi kukamilika,”alisema Magala.

  Magala pia amewaomba wananchi kutoa taarifa kwa viongozi watakaokuwa jirani nao au vyombo vyausalama vitakavyokuwa karibu, pale watakapoona dalili zinazoashiria kuvunjika kwa amani na kuwataka wachague viongozi bora, waadilifu, wachapaka kazi, watakao waletea maendeleo katika maeneo yenu ya Kata na Wilaya yetu ya Newala kwa ujumla.

  0 0

   Mshiriki wa shindano la mwisho la kumtafuta Serengeti Masta kwa wilaya ya Temeke Emmanuel Nyaulingo (kulia) akipokea zawadi ya fulana kabla ya shindano hilo kuanza rasmi ambalo lililofanyika mwishoni mwa wiki katika baa ya Kisuma iliyopo Temeke jijini Dar es salaam. (kushoto) ni balozi wa bia ya Serengeti Premium Lager Caroline Vincent na anayeshudia (katikati) ni mshereheshaji wa shindano hilo Richard Godwin. Kampeni hiyo inafikia tamati jijini Dar es salaam baada ya kumalizika mikoani pia ambapo imefanikiwa kuzifikia baa zaidi ya 200 kwa kipindi cha miezi mitatu ya Kampeni.
   Mshiriki wa shindano la Serengeti Masta Sebastian Kaluma akionja ladha tofauti za chapa za bia mbalimbali kutoka Kampuni ya bia ya Serengeti ili kuweza kuitambua ladha halisi ya bia ya Serengeti Premium Lager katika shindano la kumtafuta Serengeti Masta wa wa wilaya ya Temeke ambalo lilifanyika katika baa ya Kisuma ya Temeke jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki hii. Shindano hilo la miezi mitatu linalodhaminiwa na bia ya Serengeti Premium Lager limewakutanisha wapenzi mbalimbali wa bia hiyo huku likitoa elimu juu ya bia yake na zawadi mbalimbali kama fedha taslim na fulana za bure katika kipindi chote cha kampeni.
   Msimamizi wa mauzo ya Kampuni ya bia ya Serengeti kanda ya Temeke Amani Kimaro (Katikati) akionyesha kiasi cha Tsh. 100,000/= ambayo alimkabidhi mshindi wa shindano la Serengeti Masta Elisha Mwenga (kulia) ambaye aliyewabwaga wenzake wane (4) katika kuitambua ladha halisi ya bia Serengeti Premium Lager wakati wa shindano hilo ambalo lilifanyika katika Baa ya Kisuma iliyopo Temeke jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki hii. (Kushoto) ni mshereheshaji wa shindano hilo Richard Godwin.
   Msimamizi wa mauzo ya Kampuni ya bia ya Serengeti kanda ya Temeke Amani Kimaro (Kushoto) akikabidhi kiasi cha Tsh. 100,000/= kwa mshindi wa shindano la Serengeti Masta Elisha Mwenga ambaye aliibuka mshindi wa jumla wa wilaya ya Temeke katika kuitambua ladha halisi ya bia Serengeti Premium Lager wakati wa shindano hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki katika Baa ya Kisuma iliyopo Temeke jijini Dar es salaam. Shindano hilo la “Serengeti Masta” linalodhaminiwa na bia ya Serengeti linafikia tamati jijini Dar es salaam baada ya kuwafikia wapenzi mbalimbali wa bia hiyo huku wengi wakijinyakulia Tsh.50, 000/= mwanzoni mwa kampeni na kupewa cheo cha Serengeti Masta.

  Mshindi wa jumla wa shindano la Serengeti Masta kwa wilaya ya Temeke Elisha Mwenga akionyesha juu fedha taslim Tsh. 100,000/= alizopokea wakati wa shindano la la kumtafuta mshindi wa jumla wa wilaya hiyo lililofanyika mwishoni mwa wiki hii katika baa Kisuma iliyopo Temeke jijini Dar es salaam. Ushindi wa jumla wa Bw. Elias umekuja baada ya kuwabwaga washiriki wenzake wanne katika mtanange wa mwisho wa kuitambua ladha halisi ya bia ya Serengeti Premium Lager kati ya chapa nyingine nne za Kampuni ya bia ya Serengeti.  Shindano hilo la “Serengeti Masta” limefanikiwa kuwafikia wahudumu wa baa mbalimbali jijini Dar es salaam na mikoani katika kipindi chote cha Kampeni na kuwaelimisha  juu ya utoaji huduma kwa wateja wa bia hiyo jambo ambalo liliongeza mauzo ya bia hiyo katika baa zao.


  Na Mwandishi wetu.
  KAMPENI ya “Serengeti Masta” iliyokua ikiendeshwa na Kampuni ya bia ya Serengeti chini ya udhamini wa bia yake namba moja ya Serengeti Premium Lager, imefikia kilele jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki baada ya kampeni hiyo kuzunguka kwa muda wa miezi mitatu katika miji ya Arusha, Mbeya, Mwanza na Morogoro.

  Katika kufunga Kampeni hiyo kwa kishindo, kwa kushirikiana mameneja wa bia ya Serengeti Premium Lager, walijipanga kuwafikia mashabiki wengi zaidi wa bia hiyo ambapo iliwalazimu kufanya shindano la “Serengeti Masta” katika baa tatu zilizopo jijini Dar es salaam kwa siku tofauti.

  Sherehe hizo ambazo zilionekana kuwafurahisha mashabiki wengi wa bia ya Serengeti Premium Lager, ziliambatana na burudani ya mziki, zawadi za fedha taslim, fulana na bia za bure.

  Baadhi ya baa za jijini Dar es Salaam, ambazo zilizochaguliwa kuimalizia promosheni hiyo ni pamoja na Kisuma iliyopo Temeke, Zambezi Ubungo na Havana Park ya Segerea.

  Akiizungumzia promosheni hiyo mmoja wa wateja maarufu wa bia ya Serengeti Premium Lager aliyehudhuria shindano la “Serengeti Masta” katika baa ya  Kisuma iliyopo Temeke jijini Dar es Salaam, Bw. Salehe Kitwana, aliipongeza Kampuni ya bia ya Serengeti na mameneja wa bia hiyo, kwa kuibua kampeni ambayo imeweza kuwahamasisha wahudumu wa baa mbalimbali jijini Dar es Salaam na mikoani katika utoaji huduma bora kwa wateja wa bia hiyo, sambamba na kuwazawadia fedha taslim washiriki mbalimbali walioweza kuitambua ladha halisi ya bia ya Serengeti baada ya bia hiyo kushindanishwa na bia nyingine tano zinazotengenezwa na Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL).

  “Promosheni kama hii inawaunganisha mashabiki na kuwafanya waipende bia yao zaidi na zaidi pia nadhani huu ni mfano wa kuigwa na bia nyingine zinaweza kujifunza mengi kutokana na promosheni kama hii”.alisema Bw. Salehe.

  Naye Meneja Masoko wa bia ya Serengeti Premium Lager Bi. Anitha Msangi alisema,”Kampeni hii imekuwa ikiendeshwa kwa muda wa miezi mitatu sasa na kuanza kupamba moto baada ya mashabiki kuipokea kwa mikono miwili na kuifanya kuwa maarufu.

  Alisisitiza kuwa, shindano la “Serengeti Masta” ni moja kati ya kampeni kubwa ambazo zimeweza kufanikiwa kiutekelezaji kwa mwaka huu, ikiwa ni moja ya kazi kubwa zilizofanywa na Kampuni ya bia ya Serengeti.

  Bi. Msangi pia alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wateja wote wa bia ya Serengeti Premium Lager mameneja wa baa mbalimbali walioshiriki kwenye kampeni hii na wafanyakazi wote wa SBL nchi nzima kwa kuwaunga mkono na kushiriki kikamilifu katika kufanikisha zoezi zima la kampeni hiyo.

  Aliongeza kuwa pamoja na ushiriki wa wateja kuwa mzuri lakini pia wamefanikiwa kuongeza mauzo ya bia ya Serengeti kufikia kiwango kikubwa kuliko hapo awali kwa mwaka huu.

  Tafiti mbalimbali zilizofanywa na SBL katika kipindi cha miezi mitatu ya kampeni hii imedhihirisha kuwa kampeni hiyo haikufaidisha tu kampuni ya bia ya Serengeti bali pia baa zaidi ya 4000 zilizotembelewa na shindano hilo nchi nzima katika kipindi chote cha miezi mitatu.

  Vilevile kampeni hiyo imeibua washindi mbalimbali waliopewa cheo cha Serengeti Masta ambao walijizolea fedha taslim na bia za bure, fulana na zawadi mbalimbali.

  “Namshukuru Mungu na sisi pia tumebahatika kuweza kuwa sehemu ya kampeni hii kabla ya kufikia tamati na ninajiona kama mwenye bahati sana” alisema Meneja wa baa ya Kisuma Thomas Kimaro ambaye alihojiwa na waandishi wa habari wakati wa shindano la mwisho la Serengeti Masta lililofanyika kwenye baa yake.

  Kimaro aliipongeza Kampuni ya bia ya Serengeti kwa kuwa mashuhuri wa kubuni mambo mapya kila kukicha na kuwasihi kuendelea kuleta promosheni kama hizi kwa kuwa zinaongeza mauzo ya bia hizo kwenye baa zao.                                                                                                              
  Kampeni ya Serengeti Masta ilianzishwa mahususi kwa ajili ya kurudisha shukrani kwa wateja wa bia ya Serengeti Premium Lager mara baada ya bia hiyo kushinda kinyang’anyiro cha bia ya kimataifa yenye viwango bora katika tuzo za “monde selection” za mwaka huu.

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  OFISI YA WAZIRI MKUU

   TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA  Mkoa wa Dodoma

  Anwani ya Simu REGCOM

  Simu Nambari: 2324343/2324384

  E-Mail No. ras@dodoma.go.tz

  Fax No. +255 026 2320046


      Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,

                              S.L.P.  914,

                                DODOMA.

  Ndugu wananchi wa Mkoa wa Dodoma, tarehe 25 Oktoba, 2015 ni siku ya Uchaguzi Mkuu hapa nchini; ambapo, Watanzania wale wenye sifa za kupiga kura na waliojiandikisha, watapata fursa na kutumia haki yao ya kikatiba kuchagua viongozi mbalimbali wa nchi yetu, kuanzia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge na Madiwani.


  Maandalizi ya kufanikisha zoezi la Uchaguzi Mkuu kwa Mkoa wa Dodoma yamekamilika. Hadi kufikia siku ya leo tayari wasimamizi wa uchaguzi wa wilaya zote saba za Mkoa wa Dodoma wameshapokea vifaa vyote vitakavyo tumika kwenye zoezi la uchaguzi. Hadi tunavyozungumza sasa, vifaa hivyo vinapelekwa kwenye vituo vya kupigia kura.


  Vilevile, wasimamizi wa uchaguzi kwenye wilaya zote saba za Mkoa wa Dodoma wameshapokea fedha za kuendeshea uchaguzi Mkuu.  Aidha, Mafunzo kwa watendaji wote watakaoshiriki katika zoezi la uchaguzi yanahitimishwa kwenye wilaya za Dodoma.


  Mkoa wa Dodoma tumefanikiwa kuandikisha jumla ya wananchi 1,053,136 kuwa wapiga kura sawa na asilimia 102.74 ya lengo, ambapo lengo ilikuwa kuandikisha watu/wapiga kura 1,025,084, Hivyo, natumia fursa hii kuwataka wale wote waliojiandikisha kupiga kura katika Mkoa wa Dodoma, kujitokeza kwa wingi kupiga kura siku ya Jumapili Oktoba 25.


  Vituo vya kupigia kura vitafunguliwa kuanzia saa 1:00 asubuhi na zoezi la kuhesabu kura litaanza saa 10:00 jioni. Natumia fursa hii kusisitiza mambo machache ya muhimu kwenye zoezi la uchaguzi Mkuu mwaka 2015 kwa wananchi wa Mkoa wa Dodoma na wadau mbalimbali wanaoshiriki Uchaguzi Mkuu kama ifuatavyo:

  ·        Wananchi wale wenye sifa za kupiga kura, wanahimizwa kwenda kupiga kura kwa amani na utulivu kwa kuzingatia muda na kisha kurejea makwao/majumbani baada ya kumaliza kupiga kura.


  ·        Viongozi wa vyama vya siasa na wagombea wa nafasi mbalimbali wawaandae wanachama na wafuasi wao kwenda kupiga kura, bila kuvunja sheria za uchaguzi, taratibu na kanuni zilizowekwa; wakidumisha hali ya Amani na utulivu.


  ·        Hairuhusiwi kwa mtu yeyote siku ya uchaguzi kufanya kampeni ya aina yoyote wala kuvaa mavazi ya chama chochote cha siasa.

  ·        Hairuhusiwi kwa mtu yoyote kutoa Rushwa kwa lengo la kumshawishi mtu kupiga kura au kumshawishi asipige kura.  ·        Kila mtu aliyejiandikisha kupiga kura atunze shahada yake ya kupigia kura na asiitoe kwa mtu mwingine wala yeye kutumia shahada ya mtu mwingine kwani ni kosa la jinai kutumia shahada ya mtu mwingine kupigia kura. vilevile ni kosa kutumia shahada bandia.


  ·        Ni vizuri kila mmoja akahakikishe jina lake kwenye kituo alichojiandikishia ili kupata uhakika wa kuwepo kwenye orodha na kupiga kura kabla ya siku ya kupiga kura Oktoba 25.


  ·        Wananchi wote wakae katika hali ya utulivu wasiwe na hofu wala woga, Jeshi la polisi litafanya doria mbalimbali zenye lengo la kuhakikisha kunakuwa na hali ya Utulivu na hali ya Amani ili kila mtu apate fursa ya kushiriki zoezi la Uchaguzi.


  Kabla sijahitimisha salamu zangu, narudia kuwasisitiza Wananchi wote wa Dodoma wale wenye sifa za kupiga kura wajitokeze kwa wingi kupiga kura siku ya Jumapili, Serikali imejiandaa vya kutosha na kuwahakikishia wananchi uchaguzi Mkuu kufanyika kwa amani, utulivu na kuwa uchaguzi wa Huru na Haki.


  Nawaomba wananchi wote wajiepushe na vitendo vyovyote vinavyosababisha vurugu na Uvunjifu wa Amani; tuendeleze sifa yetu ya Mkoa wa Dodoma kufanya Uchaguzi tukiwa katika hali ya usalama.


  Mwisho kabisa, nawatahadharisha wale wote wenye nia mbaya au wanaojipanga kutaka kujaribu kuvuruga zoezi la uchaguzi au kuleta vurugu ya aina yoyote hapa Mkoani Dodoma kuwa,  vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga imara na vitamshughulikia mara moja mtu huyo. Wananchi mnaombwa kutoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama au kwa kiongozi yoyote wa eneo husika.

    
  Ahsanteni sana kwa kunisikiliza.


  Imetolewa na:

  OFISI YA MKUU WA MKOA WA DODOMA


  Oktoba 23, 2015.

  0 0


  TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

  Kitalu Na. 8, Mtaa wa Luthuli

  S.L.P 2643, DAR ES SALAAM

  Simu: +255 22 2135747/8; 2137125; 2135222

  Faksi: +255 22 2111281

  Barua Pepe: chragg@chragg.go.tz

  Tovuti: www.chragg.go.tz


  Oktoba 23, 2015


  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI              
  Tamko la Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kuhusu umuhimu wa kuzingatia sheria kwa ajili ya Uchaguzi Huru, wa Haki na Amani


  TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB)  imekuwa ikifuatilia kwa karibu matamshi mbalimbali ya wanasiasa, viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa Serikali, Tume ya Uchaguzi, na Jeshi la Polisi kuhusu nini kifanyike baada ya kupiga kura siku ya uchaguzi mkuu, Oktoba 25, 2015. Matamshi haya yamesababisha mkanganyiko na malumbano miongoni mwa viongozi na wananchi pia.


  THBUB inapenda kusema kwamba, licha ya changamoto kadhaa zilizojitokeza katika baadhi ya maeneo, wakati wa kampeni za uchaguzi, kwa ujumla kampeni za uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani zimefanyika nchi nzima kwa amani na utulivu. Ni wajibu wetu sote kudumisha amani katika nchi yetu muda wote, wakati wa uchaguzi na baada ya kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu.


  Tume (THBUB) inawashukuru na kuwapongeza wananchi kwa jinsi walivyoonyesha utulivu wakati wa mikutano mikubwa ya kampeni, ambayo imekuwa ikivuta maelfu ya wananchi.


  Tume (THBUB) inatoa pongezi kwa Jeshi la Polisi kwa ulinzi ambao umekuwepo katika mikutano hiyo. Aidha, inavipongeza vyombo vya habari kwa kazi nzuri ya kuwapasha wananchi habari mbalimbali za uchaguzi.


  Tume (THBUB) inatambua na kupongeza jitihada zinazofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, na Tume ya Uchaguzi Zanzibar kwa maandalizi ya uchaguzi.


  Tume (THBUB) inapenda kutahadharisha kwamba malumbano haya ambayo yanaendelea hayaonyeshi dalili nzuri, pamoja na jitihada za wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini kuhubiri umuhimu wa uchaguzi wa amani. Malumbano haya yasipotafutiwa ufumbuzi wa haraka, kwa kutumia busara na kuzingatia sheria, haki za binadamu, na misingi ya utawala bora, kuna dalili kubwa ya kuwepo vurugu, uvunjifu wa sheria na amani, kwani pande zote hizi zimeendeleza malumbano na kushikilia misimamo yao.  Tume (THBUB) inaonya kwamba vurugu zinaweza kutokea, ama kwa makusudi, au kwa bahati mbaya, iwapo wananchi na wafuasi wa vyama vya siasa watashikilia misimamo yao, ama watagoma na kukaidi amri ya Polisi. Lolote katika hayo likitokea, kuna uwezekano mkubwa wa kuvurugika kwa uchaguzi, na haki za binadamu zitaathirika.


  Vile vile, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imesikitishwa na matamshi yanayoashiria kutoiamini Tume ya Uchaguzi, na hata tuhuma za uwezekano wa wizi wa kura. Pia kumekuwa na matamshi ya kuwataka wananchi walinde kura, jambo ambalo halina msingi wowote wa sheria.


  Ni vyema ifahamike kuwa, wajibu wa ulinzi wa kura upo kisheria, na ni wajibu ambao wamepewa mawakala wa vyama vya siasa na wagombea, ama wagombea wenyewe, wanaoruhusiwa kuwa ndani ya vituo, wakisaidiana na wasimamizi wa Tume ya Uchaguzi na Jeshi la Polisi kuhakikisha kwamba taratibu zote zinazosimamia upigaji kura zimefuatwa.


  Kwa mujibu wa Vifungu vya 48(2) na 49 vya Kanuni za Uchaguzi (Urais na Ubunge) za mwaka 2010, Tanzania Bara, vyama vya siasa vinavyoshiriki katika uchaguzi vinatakiwa kuteua mawakala wao wa uchaguzi kwa kila kituo, jambo ambalo Tume (THBUB) inaamini limefanyika. Mawakala wanatakiwa kula kiapo cha uaminifu.


  Vifungu vya 59 na 60 vya Kanuni za Uchaguzi vinaeleza jinsi wakala wa chama au mgombea, atakavyoshiriki katika taratibu za kuhesabu kura, na jinsi malalamiko yatakavyo shughulikiwa na Msimamizi wa Uchaguzi.


  Vifungu vya 61 hadi 66 vya kanuni hizo vinaeleza utaratibu wa kujumlisha kura za wagombea, na kutangazwa matokeo. Kanuni zinazungumzia pia uhusika wa mawakala katika hatua zote. Mawakala watapewa nakala za fomu mbalimbali husika, zikiwemo zenye malalamiko yaliyowasilishwa, na matokeo. Utaratibu huu wa sheria ndiyo unaotoa ulinzi mahususi wa kura.


  Tume (THBUB) inawataka mawakala wafanye kazi zao kwa uadilifu na weledi. Mawakala wasiende kwenye vituo wakiwa na nia potofu (bad faith/malafide) ya kuharibu zoezi la kupiga kura. Tume (THBUB) inalisema hili kwa kuwa imebaini kuwepo matamshi yanayoonyesha hisia za kutoiamini Tume ya Uchaguzi. Tume (THBUB) inasisitiza umuhimu wa kuiamini na kuipa ushirikiano Tume ya Uchaguzi ili itekeleze majukumu yake bila ya kuingiliwa ama kubezwa.


  Kwa hiyo Tume (THBUB) inapenda kutamka kwamba mlinzi mkuu wa kura ni wakala wa chama cha siasa, mgombea, na siyo mpiga kura au mwananchi wa kawaida ambaye hajapewa majukumu hayo kwa mujibu wa sheria.


  Tume (THBUB) inatahadharisha kuwa ni vyema kila mdau wa uchaguzi atimize majukumu yake kwa mujibu wa sheria na kanuni za uchaguzi. Jeshi la Polisi liendelee kutumia weledi katika kutoa ulinzi siku ya uchaguzi, kama lilivyofanya wakati wa kampeni za uchaguzi ambapo tulishuhudia mikutano mikubwa ikimalizika kwa usalama.


  Kwa maana hiyo wananchi wanawajibu mkubwa wa kuwa watulivu  wakati wa zoezi zima la uchaguzi kuanzia kupiga kura na kusubiri matokeo kwa amani.


  Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inaamini kuwa utawala wa sheria lazima uheshimiwe na kila mtu, vikiwemo vyombo vya dola na mamlaka za Serikali.


  Hivyo basi Tume (THBUB) inatamka:

  1.    Viongozi wa vyama vya siasa na wagombea waepuke lugha zinazoweza kusababisha hofu, vurugu na uvunjifu wa amani.


  2.    Inazishauri  Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Tume ya Uchaguzi Zanzibar, na Jeshi la Polisi kuzingatia sheria na kudumisha misingi ya utawala bora, mambo ambayo ndiyo msingi wa kulinda haki za binadamu.


  3.    Aidha, THBUB inawataka wananchi kupiga kura kwa amani na kuheshimu sheria zinazoongoza zoezi zima la uchaguzi.


  4.    Vyama vya siasa vihakikishe kuwa Mawakala wao wanafanya kazi zao kwa uadilifu na wahakikishe kuwa wanatambua wajibu wao na wanazingatia taratibu za uchaguzi.


  5.    Jeshi la Polisi litoe ulinzi mahsusi, bila vitisho, ili kuhakikisha kwamba zoezi la kupiga kura linafanyika kwa amani na kwa kuzingatia haki za binadamu na misingi ya utawala bora.


  6.    Viongozi wa vyama vya siasa na wafuasi wao wawe wavumilivu na wajiepushe na matamshi au matendo yanayo weza kusababisha uvunjifu wa sheria, haki za binadamu, misingi ya utawala bora na kusababisha vurugu na kutoweka kwa amani.


  7.    Tume ya Uchaguzi na Wasimamizi wa uchaguzi, na mawakala wa vyama wahakikishe kuwa zoezi zima la kupiga kura, kuhesabu kura, kubandika na kutangaza matokeo linafanyika kama sheria inavyotamka.


  Tume ya Haki za Binadamu itaendelea kufanya ufuatiliaji wa mchakato wa uchaguzi nchini kote ili kuimarisha ulinzi wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora.


  Tume inawataka wananchi watakaobaini uvunjifu wowote wa haki za binadamu, au uvunjifu wa sheria ya uchaguzi, kuzijulisha mamlaka husika zinazosimamia zoezi la uchaguzi.

  Aidha, wanaweza kutoa taarifa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kupitia ujumbe mfupi wa simu ya kiganjani (SMS) kwenda Na. 0754 460 259.


  Ujumbe lazima uanze na neno 'TAARIFA' au ' RIPOTI' kisha andika taarifa yenyewe. Namba hii inapokea ujumbe mfupi tu. Kwa taarifa zaidi piga Na. +255 22 2135747-8.

    

  Kauli mbiu ya THBUB katika kuelekea Uchaguzi Mkuu ni “Watanzania wote tufanye Uchaguzi Mkuu kwa utulivu ili uwe Huru, wa Haki, na Amani.”


  Imetolewa na:


  (SIGNED) 
  Bahame Tom Nyanduga

                                                     Mwenyekiti


  TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA 

  Oktoba 23, 2015

  0 0

   Wakazi wa Ubungo wakimshangilia kwa shangwe mgombea wa Urais kwa Tiketi ya CCM, Dk. Magufuli.
   Wananchi wakiwamtandikia apite.

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI

   WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

  JESHI LA POLISI TANZANIA
           “PRESS CONFERENCE” TAREHE 23.10.2015. 

  NDUGU WAANDISHI WA HABARI,

  TUNAJUA KUWA TAREHE 25 OKTOBA, 2015 NI SIKU AMBAYO TUTASHIRIKI KUPIGA KURA KUWACHAGUA MADIWANI, WABUNGE NA RAIS KWA KIPINDI CHA MIAKA MITANO IJAYO.

   KATIKA KUELEKEA SIKU HIYO, YAPO MAMBO KADHA WA KADHA AMBAYO KILA MMOJA WETU KWA NAFASI ALIYONAYO ANAPASWA KUYAFUATA NA KUYAZINGATIA KWA LENGO LA KUHAKIKISHA UCHAGUZI MKUU UNAKUWA HURU NA HAKI.


  TUTAMBUE KUWA KILA MMOJA WETU ALIYEFIKISHA UMRI WA MIAKA 18 NA KUENDELEA NA ALIYEJIANDIKISHA ANA HAKI YA KUPIGA KURA. NI MUHIMU KUFIKA KATIKA KITUO CHA KUPIGIA KURA UKIWA NA KADI YA MPIGA KURA [SHAHADA YA KUPIGIA KURA] KWA MUJIBU WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI VITUO VYA KUPIGIA KURA VITUFUNGULIWA KUANZIA SAA 07:00 ASUBUHI HADI 16:00 JIONI.


  KILA MMOJA AKUMBUKE KUJIEPUSHA KUFIKA KATIKA KITUO CHA KUPIGIA KURA AKIWA AMEVAA NGUO ZENYE PICHA ZA WAGOMBEA, MANENO AU NEMBO AMA RANGI ZA CHAMA CHA SIASA, KUEPUKA KUTUMIA UVUMI, MANENO YA UONGO, HISIA AU VISINGIZIO VYENYE LENGO LA KUWAZUIA WENGINE KWENDA KUPIGA KURA, KUEPUKA KUFANYA KAMPENI KATIKA KITUO CHA KUPIGIA KURA IWE KWA MANENO YA USHAWISHI AU KWA KUONYESHA ISHARA YA CHAMA FULANI CHA SIASA.


  AIDHA NI VYEMA KILA MWANANCHI KUPIGA KURA KWA KUTUMIA JINA NA KITAMBULISHO CHAKE NA SIO CHA MTU MWINGINE, ALIYEKUFA AU MGONJWA, KUEPUKA KUFANYA FUJO AMA VURUGU KATIKA KITUO CHA KUPIGIA KURA. NI MUHIMU KILA MPIGA KURA MARA BAADA YA KUPIGA KURA KUONDOKA KWENYE KITUO CHA KUPIGIA KURA NA KUENDELEA NA SHUGHULI NYINGINE KWANI NI KOSA KUPIGA KURA NA KUENDELEA KUBAKI KATIKA ENEO LA KITUO CHA KUPIGIA KURA.


  AIDHA NI WAJIBU WA JESHI LA POLISI KUWALINDA MAOFISA WANAOSIMAMIA UCHAGUZI, KUHAKIKISHA KWAMBA ZOEZI LA UPIGAJI KURA LINAENDA SAWA, BILA VIKWAZO AU BUGHUDHA NA KUHAKIKISHA VIFAA VYA KUPIGIA KURA VIKO SALAMA.

  KWA MKOA WA MBEYA TUNA JUMLA YA MAJIMBO 13 YA UCHAGUZI, VITUO 3,899 VYA KUPIGIA KURA, KILA KITUO KITALINDWA NA ASKARI ILI KUHAKIKISHA SUALA LA ULINZI NA USALAMA LINAIMARISHWA KWA KIPINDI CHOTE CHA ZOEZI LA KUPIGA KURA, KUHESABU KURA NA KUTANGAZA MATOKEO YA UCHAGUZI.

  JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LIMEJIPANGA KUIMARISHA ULINZI KATIKA MAENEO YOTE IKIWA NI PAMOJA NA VITUO VYA KUPIGIA KURA. PIA KUTAKUWA NA DORIA ZA MAGARI, PIKIPIKI, MBWA NA ASKARI AMBAO WATAKUWA WAKITEMBEA HUKU NA KULE KWA LENGO LA KUDHIBITI VITENDO VYOVYOTE VYA UVUNJIFU WA AMANI. IELEWEKE KUWA, VITENDO VYOVYOTE VYA UVUNJWAJI WA SHERIA KABLA, WAKATI NA BAADA YA UCHAGUZI NI UHALIFU HIVYO KILA MMOJA AWE MAKINI NA AFUATE SHERIA/TARATIBU NA ATIMIZE WAJIBU WAKE WAKATI WOTE.

  JESHI LA POLISI LINAWATAKA WANANCHI WAHESHIMU MAELEKEZO YA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI. KWAMBA WALE WOTE WATAKAOPIGA KURA NA MARA BAADA YA KUPIGA KURA WAONDOKE MAENEO YA VITUO VYA KUPIGIA KURA WAENDE KUENDELEA NA SHUGHULI ZAO, “WASIKUSANYIKE” WASIWEKE MKUSANYIKO KWANI KWA KUFANYA HIVYO WATAKUWA WANAFANYA MKUSANYIKO USIO HALALI “UNLAWFUL ASSEMBLY” MKUSANYIKO WOWOTE USIOFUATA UTARATIBU HALALI.

  NARUDIA, JESHI LA POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VYA DOLA LIMEJIPANGA VIZURI KUIMARISHA ULINZI NA USALAMA KATIKA MAENEO MBALIMBALI ILI KUHAKIKISHA ZOEZI ZIMA LINAKWENDA VIZURI, KWA USALAMA NA AMANI NA UTULIVU. KWA HIVYO WANANCHI WOTE WENYE SIFA WAENDE KUPIGA KURA, WASIOGOPE.

  NAOMBA TUELIMISHANE ILI KUEPUKA MAKOSA AMA UHALIFU, KILA MMOJA ANA WAJIBU WA KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA ILI KUUFANYA UCHAGUZI UWE WENYE AMANI NA UTULIVU, HURU NA HAKI. NI IMANI YANGU KUWA KUNA MAISHA BAADA YA UCHAGUZI HIVYO TULINDE NA KUTETEA AMANI YA NCHI YETU. 
  AHSANTENI KWA KUNISIKILIZA!


  KATIKA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, MNAMO TAREHE 20.10.2015 MAJIRA YA SAA 14:00 MCHANA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LILIPOKEA TAARIFA KUWA, MTU MMOJA AITWAYE RAMADHANI JUMA MSUMA @ RAMA BAJAJI (25) MKAZI WA FOREST YA ZAMANI JIJINI MBEYA, ANATUHUMIWA KWA MAKOSA YA MATUMIZI MABAYA YA MTANDAO KWA KUTUMIA PICHA ZA KUZALILISHA WAGOMBEA WA VYAMA VYA SIASA NA KUTOA TAARIFA ZA UCHOCHEZI DHIDI YA VYOMBO VYA DOLA NA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI, KINYUME NA SHERIA.


  NJIA ALIYOKUWA AKITUMIA MTUHUMIWA NI KUTUMIA NAMBA ZA SIMU ZAKE ZA MKONONI ZILIZOSAJILIWA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII @ WHATSAPP, FACEBOOK, INSTRAGRAM NA TWITTER AMBAPO ALIKUWA AKITENGENEZA PICHA ZA UZALILISHAJI NA TAARIFA ZA UCHOCHEZI NA KISHA KUZITUMA KWA NJIA YA MTANDAO KATIKA MAKUNDI MBALIMBALI YA MITANDAO YA KIJAMII TAJWA HAPO JUU.


  AIDHA PICHA HIZO NA TAARIFA HIZO ZINATOA KASHFA KWA WAGOMBEA WA VYAMA VINGINE NA KUTOA VITISHO KWA KUELEKEA UCHAGUZI KWA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI. PIA TAARIFA HIZO NI VIASHIRIA VYA UCHOCHEZI WA VURUGU/FUJO NA UVUNJIFU WA AMANI NA USALAMA HUSUSANI KATIKA KIPINDI HIKI CHA UCHAGUZI MKUU.


  MTUHUMIWA ANAHOJIWA NA PINDI UPELELEZI UKIKAMILIKA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI MARA MOJA KUJIBU MASHITAKA YANAYOMKABILI CHINI YA SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO NA. 14 YA 2015.


  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUWA MAKINI NA MATUMIZI YA MTANDAO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA ZA MATUMIZI SALAMA YA MTANDAO ILI KUJIEPUSHA NA MADHARA YANAYOWEZA KUEPUKIKA HASA KATIKA KIPINDI HIKI CHA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU HAPO OKTOBA 25, 2015.

   Imesainiwa na:
  [AHMED Z. MSANGI – SACP]

  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
  0 0

  Huu ni uchambuzi wa Habari toka vituo mbalimbali vya Televisheni Mchana Huu October 23, 2015.
  Klabu ya soka ya Azam FC imeendelea kukabana koo na Mabingwa wa Ligi kuu soka Klabu Ya Yanga baada ya kufikisha Pointi 19 sawa na Yanga
  Timu Ya soka Ya Stand United ya shinyanga imrjinasibu na kusema wembe ni ule ule wa ushindi ili kushika usukani wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara. https://youtu.be/GDoHdphwLMA
    
  Timu ya Taifa Ya Tanzania Taifa Stars inatarajiwa kuweka kambi ya kujinoa kuikabili Aljeria kwa mtanange wa pili kuwania kushiriki kombe la Dunia.  https://youtu.be/lBtz8cMDX-o
     
  Raisi Kikwete amesema kuwa Mkongo wa Taifa Mawasiliano katika idara za Serikali kumechangia kupunguza mianya Ya Rushwa Nchini. https://youtu.be/7vBg4FRspsA
    
  Waandishi wa Habari Nchini wameombwa kuwa mstari wa Mbele katika kutetea na kulinda amani ya Taifa Uchaguzi Mkuu. https://youtu.be/68BiCiwH6Ac
    
  Wananchi Mkoani Simiyu Wameungongeza Mpango wa TASAF wa Kunusuru kaya masikini kwa kuwa umesaidia walengwa kununua chakula. https://youtu.be/O9-RVyGFkSc

  Wawakilishi wa serikali za mtaa wana wajibu gani katika kuhakikisha maendeleo ya sehemu wanazowakilisha?;https://youtu.be/PwMvBw3TgVs

  Je ni kwa namna gani sera za wagombea mbalimbali zimeweza kumgusa mkulima wa Tanzania na sekta ya kilimo kwa ujumla?; https://youtu.be/R7AGuhXyoIQ

  Hii ndiyo tathmini ya siku za wanasiasa walizojinadi katika majukwaa mbalimbali na mchambuzi huru wa maswala ya katika kampeni zao;  https://youtu.be/OUwRixFpXp0

  0 0

   Katibu Mkuu Kiongozi na Mkuu wa Utumishi wa Umma Balozi Ombeni Sefue akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete orodha ya zawadi mbalimbali kutoka katika taasisi za umma wakati wa sherehe ya watumishi wa umma kumuaga Rais iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam jana.
   Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Dkt.Edward Hosea kwa niaba ya watumishi wa Umma akimkabidhi Tuzo Maalum Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutambua mchango wake katika kuboresha Utumishi wa Umma nchini wakati wa  sherehe ya Watumishi wa Umma Kumuaga Rais iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam jana usiku.
   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania Bwana Awadh Masawe akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mfano wa ufunguo wa trekta alilokabidhiwa na watumishi wa taasisi za umma jana wakati wa sherehe za kumauaga Rais katika ukumbi wa Mlimani City jana.
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete,Katibu Mkuu Kiongozi na Mkuu wa Utumishi wa Umma Balozi Ombeni Sefue,Jaji Mkuu Othman Chande,Mwanasheria Mkuu Mh.George Masaju pamoja Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bwana Florence Turuka wakiwa katika picha ya pamoja na Makatibu wakuu wa Wizara Mbalimbali wakati wa Sherehe ya Watumishi wa Umma Kumuaga Rais iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam jana. 
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia viongozi na wawakilishi wa Watumishi wa Umma katika ukumbi wa Mlimani City wakati wa Sherehe ya Watumishi wa Umma Kumuaga Rais jana.
  (Picha na Freddy Maro).

  0 0

  Vijana Kisiwanin Pemba wakiingia katika viwanja vya Gombani kuhudhuria Mkutano wa Ufungaji wa Kampeni ya CCM ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein.
  Wanachama wa CCM wakiwa katika viwanja vya Gombani ya Kale Pemba wakihudhuria mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein.
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akiwasili katika viwanja vya mkutano wa ufungaji wa kampeni katika viwanja vya Gombani ya Kale akisalimiana na Viongozi wa CCM Pemba.
  Mgombea Mwenza wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokelewa na Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Mhe Salama Aboud Talib.akiwasili katika viwanja vya mkutano Gombani ya Kale. Pemba.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.


  Mgombea Mwenza wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ziwani Pemba Ndg Mohammed Othman Omar alipowasili katika viwanja vya mkutano.
  Mgombea Mwenza Mhe Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Viongozi wa CCM kisiwani Pemba alipowasili katika viwanja vya mkutano wa Kampeni Gombani ya Kale Pemba. 
  Mgombea Mwenza wa CCM Mhe Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Balosi Seif Ali Iddi, katika viwanja vya mkutano Gombani ya Kale. 
  Mgombea Mwenza wa CCM Mhe Samia Suluhu Hassan akizungumzac na Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif Iddi. wakiwa katika viwanja vya mkutano Gombani ya Kale Pemba.
  Wananchi wakiwa katika viwanja vya Gombani Pemba wakihughuria Mkutano wa Ufungaji wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein.
  Hapa Kazi Tu. 
  Ndivyo inavyoonesha Kijana huyu akisema akiwa na picha za Wagombea Urais kupiti CCM katika viwanja vya mkutano Gombani ya Kale Pemba.
  Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ziwani Pemba kwa tiketi ya CCM Ndg Mohammed Othman Omar, alipowasili katika viwanja vya Gombani ya Kale Pemba kuhudhuria Mkutano wa Ufungaji wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein.
  Mwenyekiti wa CCMTaifa Dk Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Viongozi wa CCM Kisiwani Pemba. 
  Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan jukwaa kuu.
  Wanachama wa CCM wakishangilia wakati wa mkutano wa Kampeni wa CCM uliofanyika viwanja vya Gombani ya Kale Pemba.
  Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Taifa wakati akiwasili katika jukwaa kuu la viongozi kwa ajili ya kuwahutubia wananchi wa Pemba katika mkutano wake wa kampeni ya Ufungaji iuliofanyika katika viwanja vya Gombani ya Kale.
  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kuskazini Pemba Mhe Mberwa Hamad Mberwa akizungumza na Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk. Jakaya Kikwete katika viwanja vya mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein. 
  Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk Jakaya Mrisho Kikwete na Mwakamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, wakibadilisha mawazo kabla ya kuaza kwa mkutano wa ufungaji wa kampeni kisiwani Pemba katika viwanja vya Gombani ya Kale.
  Msoma Quran akisoma quran kabla ya kuaza mkutano wa ufungaji wa kampeni ya mgombea Urais wa Zanzibar Dk Shein. viwanja vya Gombani ya Kale.
  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Ndg Mberwa Hamad Mbwera akitowa salamu za Wananchi kisiwani Pemba wakati wa mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein.
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akiwahutubia Wananchi wa kisiwani Pemba katika mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein.uliofanyika katika viwanja vya Gombani ya Kale.
  Umati wa Wananchi Kisiwani Pemba wakimsikiliza Mgombea Urais wa Zanzibar Kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein.katika viwanja vya Gombani ya Kale. 
  Hapa Kazi Tu 
  Wanachama wa CCM wakishangilia wakati wa Mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, uliofanyika kisiwani Pemba katika viwanja vya Gombani ya Kale.
  Mgombea Mwenza wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akiwahutubia Wananchi kisiwani Pemba katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Gombani ya Kale Pemba na kufungwa na Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein.
  Wanachama wa CCM Kisiwani Pemba wakishangilia Wakati Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, akiwahutubia katika mkutano wake wa ufungaji wa kampeni uliofanyika viwanja vya Gombani ya Kale Pemba.
  Viongozi wa jukwaa kuu la viongozi wakimsikiliza Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wananchi wa Pemba katika mkutano wake wa ufungaji wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya gombani ya kale Pemba.
  Wanachama wa CCM wakiwa katika viwanja vya mkutano Gombani wakifuatilia mkutano wa ufungaji wa Kampeni uliofanyika viwanja vya Gombani ya Kale.Pemba.
  Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungani wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia wananchi wa kisiwani Pemba wakati wa ufungaji wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Gombani ya Kale Pemba.
  Wananchi kisiwani Pemba Wakimsikiliza Mgombea Urais wa Znzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein, akiwahutubia wakati wa mkutano wake wa ufungaji wa Kampeni kisiwani Pemba uliofanyika katika viwanja vya Gombani ya Kale Pemba.
  Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia Wananchi kisiwani Pemba katika mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, uliofanyika katika viwanja vya Gombani ya Kale Pemba.
  Mgombea Urais wa Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wananchi katika viwanja vya Gombani ya Kale Pemba na kuwaomba kura ya Ndio kumchagua yeye kuiongoza Zanzibar kwa kipindi cha Pili kutekeleza Ilani ya CCM ya Uchaguzi ya miaka mitano ijayo ya Uongozi wake.
  WanaChama wa CCM Kisiwani Pemba wakimsikiliza Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya Gombani ya Kale Pemba.
  Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wananchi kisiwanin Pemba katika mkutano wake wa kampeni ya ufungaji uliofanyika katika viwanja vya mpira vya Gombani ya Kale Chakechake Pemba.
  Mwanachama wa CCM akifuatilia mkutano wa Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein uliofanyika katika viwanja vya Gombani ya Kale Pemba.akiwa na picha za Wagombea Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli na Mgombea Mwenza Mhe Samia Suluhu Hassan. 
  Viongozi wa Jukwaa kuu wakiitikia dua baada ya ufungaji wa Mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya gombani ya kale Pemba.
  Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mama Fatma Karume wakati wa mkutano wa kufunga kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, iliofanyika katika viwanja vya gombani ya kale Chakechake Pemba.
   Mwenyekiti wa CCM Dk Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Wananchi katika viwanja vya mkutano wa kampeni viwanja vya Gombani ya Kale.
  Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiagana na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete, baada ya kumaliza kuwahutubia Wananchi wa Pemba katika mkutano wake wa Ufungaji wa Kampeni kisiwani Pemba uliofanyika katika uwanja wa Gombani ya Kale Chakechake Pemba. 

  Imetayarishwa na OthmanMapara.blogspot.
  Email.othmanmaulid@gmail.com
  Phone 0777424152 or 0715424152.
  Zanzinews.com

  0 0

    Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na Viongozi wa Taasisi za Kiislamu katika ukumbi wa Baitul-Yamin, Malindi mjini Zanzibar.
   Baadhi ya Viongozi wa Taasisi za Kiislamu Zanzibar wakimsikiliza Maalim Seif.
   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiitikia dua baada ya mazungumzo yake na viongozi hao wa dini.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiagana na viongozi hao wa dini baada ya mazungumzo yao. 
  (Picha na Salmin Said, OMKR)

  Na: Hassan Hamad, OMKR.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, ameahidi kushirikiana na taasisi zote za dini nchini sambamba na kuziendeleza madrasa za Kur’an, ili ziendane na wakati uliopo.

  Maalim Seif ambaye pia ni Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Wananchi CUF ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na viongozi wa taasisi za Kiislamu katika ukumbi wa Baitul-Yamin Malindi mjini Zanzibar.

  Amesema Serikali atakayoiongoza iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar itashirikiana kwa karibu na taasisi hizo ili kuona kuwa michango yao inasaidia kuchangia juhudi za maendeleo na ustawi wa Zanzibar.

  Amewataka viongozi hao wa dini kudhibiti tofauti ndogo ndogo za kimadhehebu, ili zisiwe chanzo cha kuvuruga umoja wa waislamu nchini.

  Sambamba na hilo Maalim Seif amesema bado madrasa za Kur’an hazijapewa umuhimu unaostahiki, na kuahidi kulishughulikia suala hilo ili kuzijengea mazingira bora na kuangalia maslahi ya walimu wa madrasa hizo.

  Amesema iwapo atachaguliwa kuongoza nchini, Serikali yake itatoa mchango wake katika kuziendeleza madrasa ili ziwe za kisasa kwa kuzipatia mahitaji yote ya msingi yakiwemo vikalio pamoja vifaa vya kusomea.

  Amewakumbusha walimu wa madrasa kuweka mbele maendeleo ya watoto kwa kuwajenga kimaadili, ili waweze kuwa raia wema na viongozi bora wa baadae.

  Mapema akizungumza kwa niaba ya viongozi wa taasisi hizo za Kiislamu, Sheikh Khamis Yussuf amesema taasisi hizo ziko tayari kuzungumza na kushirikiana na kiongozi yeyote wa serikali kwa lengo kuweka mustakbali mwema wa Zanzibar.

  Amewaomba viongozi wa Serikali kutoa ushirikiano katika kuulinda na kuuendeleza utamaduni wa Zanzibar ili usiharibiwe na tamaduni nyengine, na kwamba utamaduni ni rasilimali muhimu kwa taifa.

  Wiki iliyopita Maalim Seif alikutana na viongozi wa dini ya kikristo waliopo Zanzibar katika kituo cha utengamano Welezo, kuzungumzia juu ya umuhimu kutunza na kuilinda amani ya Zanzibar. 

  0 0
 • 10/23/15--06:28: BEI YA MADAFU HII LEO


 • 0 0

   Meneja  wa Mawasiliano  Efm, Denis Ssebo akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya kumpata mshindi wa  shindano la kubuni maneno ya Kanga kupitia kipindi cha UHONDO ambacho huruka hewani kila siku za Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa sita mchana hadi saa tisa alasiri, kikiwa na Matangazaji mahiri Dina Marios, kikao hicho kimefanika leo jijini Dar es Salaam, katikati ni mshindi wa shindano hilo Sekela Richard na wakulia ni Matangazaji wa Efm  Radio Dina Marios.
   Matangazaji mahiri Dina Marios, akimkabidhi kitita cha shilingi Kitanzania milioni moja. mshindi wa shindano hilo, Sekela Richard kulia ni Meneja  wa Mawasiliano Efm, Denis Ssebo.
  Waandishi wa habari wakimsikiliza Meneja  wa Mawasiliano Efm, Denis Ssebo
  Picha na Emmanue Massaka.

  MENEJA  wa Mawasiliano  Efm, Denis Ssebo  shindano hilo halitaishia hapo, kwani baada ya kupata mshindi neno lake la Ushindi  zitatengenezwa  kanga zitakazoandikwa neno hilo ikiwa ni hatua ya pili sasa ya kumwezesha mwanamke kujikwamua kiuchumi.

  Zikishatengenezwa kanga hizo, Efm kupitia kipindi hicho cha Uhondo, itatatoa nafasi kwa  wanawake kutengeneza pesa na kujikwamua kwa kuuza Kanga hizo na  Mwanamke yoyote hasa kwa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani atachukua kanga hizo na kuziuza ambapo kwa kila doti moja ya kanga atapata asilimia 30% ya pesa.

  0 0

  TIMU ya taifa ya mpira wa magongo ya wanawake kesho inacheza mechi yake ya kwanza ya ufunguzi dhidi ya 
  zimbambwe itakayopigwa nchini Afrika kusini,katika mashindano kuwania kufuzu michuano ya Olympic ya mwaka 2016 ambayo itafanyika mjini Rio de Janeiro, nchini Brazil.

  Kocha wa timu ya taifa ya wanawake ya mpira wa Magongo  Varentina Quaranta amesema kwa upande wa wanaume mechi yao ya ufunguzi watacheza na misri siku ya jumapili. 

  Kocha Quaranta ambaye yuko na timu nchini afrika kusini amesema wachezaji wote wako tayari na morali ya kutosha kuelekea katika mashindano hayo,huku pia akitoa shukrani kwa benki ya NMB na baadhi ya wadau wa mchezo huo kwa kuwezesha safari hiyo

  0 0

  Na Mwene Said wa blogu ya jamii, Dar es Salaam.
  George Aloyce Kimaryo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka la kusambaza taarifa zauongo kupitia katika kundi la Adios la mtandao wa WhatsApp  kuwa Mwanafunzi  wa Chuo cha DIT,  Benedict Angello  Ngonyani amejitokeza  kwa mara ya pili mahakamani na kuishangaza kwa kumtaka Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange ajitokeze na kukanusha kuwa amelishwa sumu.

  Wakili wa Serikali  Jaquline Nyantori akishirikiana na Wakili Mwandamizi wa TCRA, Johannes Kalungula  walidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa Oktoba 13,2015 katika mtandao huo wa kijamii mshtakiwa huyo alisambaza taarifa hiyo kinyume na kifungu cha  16 cha sheria  ya Mtandao namba 14 ya 2015.

  Baada ya kusomewa shtaka hilo, Mshtakiwa huyo alikana na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi bado haujakamilika na Hakimu Simba aliiahirisha kesi hiyo hadi Novemba 3,2015 kwa ajili ya kutajwa na kufikiria juu ya maombi ya  dhamana.

  Mwanafunzi  huyo  wa Chuo cha DIT,  Benedict Angello  Ngonyani  yeye anakabiliwa na kesi  ya  kusambaza taarifa za uongo kupitia mtandao wa  WhatsApp na Facebook kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange amelishwa sumu.

  Tangu afikishwe mahakamani hapo kwa mara ya kwanza siku 14 zilizopita leo yaani jana ndiyo alipanda kwa mara ya pili  kizimbani mbele ya Hakimu Respicius Mwijage ambapo Wakili Nyantori alidai kuwa kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi wake bado haujakamilika.

  Nyantori alidai katika kesi hiyo, kuwa kesi hiyo inahusisha mtandao bado wanakusanya taarifa ambazo ni za muhimu kupitia mfumo huo.

  Hata hivyo wakili wa kujitegemea, Mnyela Abdallah alijitokeza mahakamani hapo na kujitambulisha kuwa yeye atakuwa wakili wa mshtakiwa huyo atakayemtetea kwenye kesi hiyo na akajulishwa kuwa mteja wake amewekewa zuio la dhamana na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

  Hakimu Mwijage aliuambia upande wa mashtaka kuwa uliweka zuio hilo la dhamana na kutoa sababu ndani ya siku hizo 14  na kuwaambia kuwa sasa kuna umuhimu wa kulijadili dhamana ya mshtakiwa huyo na kitu ambacho kinapelekea andelee kuzuiwa kwa dhamana yake maana lazima kuwepo na sababu hivyo aliwataka  Novemba 3,2015 kesi itakapotajwa kwa ajili ya kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la, waeleze sababu.

  Ngonyani amekuwa ni mshtakiwa  wa kwanza kufikishwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka kupitia sheria hiyo mpya ya mtandao ambayo inazuia mtu yoyote kusambaza ama kuchapisha data, taarifa za uongo, uzushi  na zile ambazo hazijathibitishwa ama hazina chanzo pamoja na  picha za matusi katika mitandao ya kijamii.

  Katika kesi hiyo,  Ngonyani anadaiwa kuwa Septemba 25,2015, jijini Dar es Salaam, alisambaza taarifa za uongo kupitia mitandao ya WhatsApp na Facebook kuwa Jenerali Mwamunyange  amelishwa sumu na kwamba amepelekwa Nairobi Kenya kwa matibabu wakati akijua taarifa hizo zilikuwa na lengo la kupotosha umma.

  Mbali na kesi hiyo, Mshtakiwa  Raia wa China, Royce Lee na raia wa Pakistani Iqbal Wasif na Mohamed Jamil wamepandishwa kizimbani mahakamani hapo wakikabiliwa na kesi tofauti za kuingiza mitambo  ya kielektroniki ya mawasiliano nchini bila ya kuwa na leseni kutoka TCRA, wakaisimika na kutoa huduma za simu za Kimataifa kinyume cha sheria na kuisababishia mamlaka  hiyo hasara ya zaidi ya Sh 500 milioni.

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman S. Suleiman (kulia) akipewa maelezo na mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Pugu, Godwin Ogweyo kuhusu utengenezaji wa kadi ambazo hazichafui mazingira alipotembelea maonesho ya shughuli zinazofanywa na wanafunzi hao alipokuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya 46 ya wanafuzi wa kidato cha nne shuleni hapo, Dar es Salaam juzi (Oktoba 22). Kulia kwake ni Mkuu wa Shule hiyo, Jovinus Mutabuzi.
   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman S. Suleiman (katikati) akiongozwa na  Mkuu wa Shule ya Sekondari Pugu, Jovinus Mutabuzi kukagua bweni la wanafunzi la Ujamaa alilokuwa akilala alipokuwa mwanafunzi hapo miaka ya 70 wakati alipohudhuria sherehe za Mahafali ya 46 ya wanafunzi wa kidato cha nne shuleni hapo, Dar es Salaam juzi (Oktoba 22). Kushoto ni Mkuu Mwandamizi wa Taaluma, Simon Chumila.
   Wahitimu wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Pugu, Dar es Salaam wakipiga makofi kumkaribisha mgeni rasmi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman S. Suleiman wakati akiwasili ukumbini kuhudhuria sherehe za mahafali ya 46 ya wanafunzi hao, shuleni hapo juzi (Oktoba 22).

   Sehemu ya wanafunzi wenye ulemavu wa Shule ya Sekondari Pugu wakifuatilia matukio ya sherehe za Mahafali ya 46 ya wanafunzi wa kidato cha nne yaliyohudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman S. Suleiman, shuleni hapo, Dar es Salaam juzi (Oktoba 22).
   Wazazi wa wahitimu wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Pugu, Dar es Salaam wakiwa wamesimama kumkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman S. Suleiman alipokuwa akiwasili kuhudhuria sherehe za mahafali ya 46 ya wanafunzi hao shuleni hapo, Dar es Salaam juzi (Oktoba 22).
   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, Mhandisi Suleiman S. Suleiman akivishwa skafu na mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Pugu kama heshima ya kuwa mgeni rasmi katika sherehe za mahafali ya 46 ya wanafunzi wa kidato cha nne shuleni hapo, Dar es Salaam juzi (Oktoba 22). Kushoto ni Mkuu wa Shule hiyo, Jovinus Mutabuzi.

  0 0

  Maelfu ya wananchi wakiwa wamefurika kwenye Viwanja vya Kibandamaiti, wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za CCM, uliofanyika leo kwenye Viwanja hivyo mjini Zanzibar.
   Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dk. Ali Mohammed Shein akisalimiana na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu hassan baada ya kuwasili kwenye mkutano wa kufunga kampeni za CCM uliofanyika leo kwenye Viwanja vya Kibandamaiti mjini Zanzibar.
   Mgombea wa Urais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein akimsalimia Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za CCM uliofanyika kwenye Viwanja vya Kibandamaiti mjini Zanzibar leo. Wengine ni Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi na Waziri Kiongozi Mstaafu, Shamsi Vuai Nahodha
   Mgombea Mwenza Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dk. Ali Mohamed Shein, katika mkutano wa kufunga kampeni za CCM uliofanyika leo katika viwanja vya Kibanda maiti mjini Zanzibar.

   Kijana wa Kimasai anayeishi Zanzibar, akishangilia kwa dhati wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za CCM uliofanyika leo kwenye Viwanja vya Kibandamaiti mjini Zanzibar.
   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Makamu wa Rais Dk.Mohammed Gharib Bilal akihutubia mkutano wa kufunga kampeni za CCM uliofanyika leo kwenye Viwanja vya Kibanda maiti mjini Zanzibar
   Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi akizungumza kwenye mktano wa kufunga kampeni za CCM uliofanyika leo kwenye Viwanja vya Kibandamaiti mjini Zanzibar
   Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Blal akimpongeza kwa hotuba nzuri Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi baada ya kuhutubia mktano wa kufunga kampeni za CCM uliofanyika leo kwenye Viwanja vya Kibandamaiti mjini Zanzibar
   Dogo Aslay akitumbuiza wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za CCM uliofanyika leo Kibandamaiti mjini Zanzibar
   Shabiki wa CCM akishangilia kiaina wakati wa mkutano wa kufunga kapnei za CCM uliofanyika leo kwenye viwanja vya Kibandamaiti mjini Zanzibar leo

   Mgomea Mwenza wa Urais kwa tikei ya CCM Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia mkutano wa kufunga kampeni za CCM uliofanyika leo kwenye Viwanja vya Kibanda maiti mjini Zanzibar. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO).

  0 0

  Mwenyeki wa chama cha Mapinduzi Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimnadi Mgombea Urais wa CCM Dt John Pombe Magufuli,mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Dar na vitongoji vyake kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Jangwani.

  Mgombea Urais wa CCM Dkt Jonh Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa jiji la Dar es salam na Vitongoji vyake,katika uwanja wa Jangwani

  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM Dkt Jonhn Pombe akihutubia maelfu ya wananchi waliojitokeza kwa wingi katika viwanja vya jangwani,alipokuwa akijinadi na kuwaomba wampigie kura za ndio na hatimae aibuke kinara katika nafasi ya Urais ifikapo Oktoba 25 mwaka huu kwenye uchaguzi Mkuu.
  Nyomi uwanja wa Jangwani likiwa tuliiiii.
  Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia wananchi wa jiji la Dar na viunga vyake wakati wa kufunga kampeni za lala salama za Mgombea Urais wa chama hicho.Dkt Magufuli,uliofanyika viwanja vya Jangwani,jijini Dar.
  Sehemu ya umati wa wananchi wakiwa wametulia wakisikiliz Sera za Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akijinadi mbele yao kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika ndani ya viwanja vya Jangwani.
  Sehemu ya umati wa watu
  Wananchi wa jiji la Dar na vitongoji vyake wakifutilia mkutano wa kampeni wa CCM .
  Sehemu ya maelfu ya wananchi wakiwa wamekusanyika katika viwanja vya Jangwani kwenye mkutano wa kampeni za lala salama,ambapo Mwenyekiti wa CCM,Dkt Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa ndiye mgeni rasmi,wakiwemo vingozi mbalimbali wa cma na Taifa kwa ujumla.
  Mwenyeiti wa CCM Dkt Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Katibu MKuu wa chama hicho cha CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana wakishangilia jambo wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Dar waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Jangwani jijini Dar.Pichani kulia ni  Mke wa Mwenyekiti wa CCM,Mama Salma Kikwete
  Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,na Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi,Mama Salma Kikwete akijadiliana jambo na Mke wa Mgombea Urais wa CCM,Mama Janeth Magufuli ,kwenye mkutano wa kampeni za lala salama uliofanyika viwanja vya Jangwani jijini Dar.
  Mzuka umempanda basi kwa raha zake viwanja vya jangwani.
  Mwenyeiti wa CCM Dkt Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Katibu MKuu wa chama hicho cha CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana wakishangilia jambo wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Dar waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Jangwani jijini Dar.Pichani kulia ni  Mke wa Mwenyekiti wa CCM,Mama Salma Kikwete
  Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,na Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi,Mama Salma Kikwete akijadiliana jambo na Mke wa Mgombea Urais wa CCM,Mama Janeth Magufuli ,kwenye mkutano wa kampeni za lala salama uliofanyika viwanja vya Jangwani jijini Dar.

  Mfuasi wa CCM katika umakini wa kufautilia yanayojiri kwenye mkutano wa kampeni viwanja vya Jangwani jijini Dar  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Kawe Ndugu Kipi Warioba.

  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Ukonga Ndugu Jerry Silaa.

older | 1 | .... | 673 | 674 | (Page 675) | 676 | 677 | .... | 1896 | newer