Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 669 | 670 | (Page 671) | 672 | 673 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mbunge wa jimbo la Moshi mjini aliyemaliza muda wake ,Philemoni Ndesamburo,akimnadi mgombea Ubunge katika jimbo hilo Jafary Michael (Chadema) katika mkutano wa kampeni uliofanyika jana katika kata ya Ngangamfumuni.
  Baadhi ya wananchi wakiwa kando ya barabara wakifuatilia mkutano huo.
  Mgombea Ubunge jimbo la Moshi mjini kupitia Chadema,Jafary Michael akiomba kura wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika kata ya Ngangamfumuni mjini Moshi.
  Mwenyekiti wa Chadema na mbunge anayemaliza muda wake katika jimbo la Moshi mjini,Philemoni Ndesamburo (katikati) akiwa na mgombea udiwani kata ya Ngangamfumuni,Anthony (kulia ) na mgombea udiwani kata ya Longuo Raymond Mboya. (kushoto).
  Mgo,bea Ubunge jimbo la Moshi mjini,Jafary Michael akiomba kura .
  Baadhi ya wafuasi na wananchi waliofika katika mkutano huo.
  Mgombea Ubunge katika jimbo la Moshi mjini,Jafary Michael akimumbea kura mgombea wa nafasi ya udiwani katika kata ya Ngangamfumuni,Anthony.
  Mgombea Ubunge katika jimbo la Moshi mjini,Jafary Michael akimuombea kura mgombea wa nafasi ya udiwani katika kata ya Rau,Peter Kimaro wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika kata ya Ngangamfumuni.

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,kandaya Kaskazini.

  0 0

  Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali vya Habari katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa Jijini Mwanza katika Semina ya siku tatu iliyoanza jana Octoba 19 na inatarajia kufika tamati kesho octoba 22 ikiangazia juu ya VYOMBO VYA HABARI NA UCHAGUZI iliyoandaliwa na Chama cha cha Wanahabari Wanawake nchini Tanzania (TAMWA-Tanzania Media Women Association).


  Katika Semina hiyo, imebainika kuwa katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu, Vyombo vya Habari na Waandishi wa Habari hawajaweka kipaumbele katika kuandika na kuripoti habari za Wagombea Wanawake katika nyadhfa mbalimbali nchini huku pia idadi ya Wanawake waliojitokeza kugombea katika uchaguzi huo ikionekana kuwa finyu ikilinganishwa na idadi ya Waume.

  Ni kutokana na hali hiyo, Wanahabari wamehimizwa kuandika na kuripoti habari/ Matukio ya Uchaguzi mkuu kiundani zaidi kwa kuzingatia usawa kwa wagombea wote bila kujali jinsi zao hususani kuwaweka kando Wanawake huku wanawake wenyewe wakihimizwa kuwa mstari wa mbele zaidi katika kushiriki masuala mbalimbali ikiwemo ya kiuongozi katika jamii.
  Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali vya Habari katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa Jijini Mwanza katika Semina ya siku tatu iliyoanza jana Octoba 19 na inatarajia kufika tamati kesho octoba 22 ikiangazia juu ya VYOMBO VYA HABARI NA UCHAGUZI iliyoandaliwa na Chama cha cha Wanahabari Wanawake nchini Tanzania (TAMWA-Tanzania Media Women Association).
  Semina ikiendelea kwa wanahabari kushiriki Utambuzi wa Mambo/Vitu kwa Vitendo.

  Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali vya Habari katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa Jijini Mwanza katika Semina ya siku tatu iliyoanza jana Octoba 19 na inatarajia kufika tamati kesho octoba 22 ikiangazia juu ya VYOMBO VYA HABARI NA UCHAGUZI iliyoandaliwa na Chama cha cha Wanahabari Wanawake nchini Tanzania (TAMWA-Tanzania Media Women Association).
  Mmoja wa Wanahabari akichangia Mada
  Wawezeshaji
  Godfrida Jola ambae ni Afisa Miradi TAMWA akitoa Mada
  Mshiriki wa Semina
  Mwezeshaji akiwasilisha Mada
  Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali vya Habari katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa Jijini Mwanza katika Semina ya siku tatu iliyoanza jana Octoba 19 na inatarajia kufika tamati kesho octoba 22 ikiangazia juu ya VYOMBO VYA HABARI NA UCHAGUZI iliyoandaliwa na Chama cha cha Wanahabari Wanawake nchini Tanzania (TAMWA-Tanzania Media Women Association).
  Wanahabari wakifuatilia habari za wagombea wanawake zilizoandikwa na Magazeti ya hii leo ambapo imebainika kuwa habari hizo hazikupewa kipaumbele
  Wanahabari wakifuatilia habari za wagombea wanawake zilizoandikwa na Magazeti ya hii leo ambapo imebainika kuwa habari hizo hazikupewa kipaumbele
  Wanahabari wakifuatilia habari za wagombea wanawake zilizoandikwa na Magazeti ya hii leo ambapo imebainika kuwa habari hizo hazikupewa kipaumbele
  Mmoja wa Watoa Mada, Mama Maimuna Amina Kanyamala ambae ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la MikonoYetu la Jijini Mwanza.
  Wanahabari wakifuatilia habari za wagombea wanawake zilizoandikwa na Magazeti ya hii leo ambapo imebainika kuwa habari hizo hazikupewa kipaumbele
  Selfie. Ni katika 
  Ni muda wa Tea Break
  Tea Break Time
  Tea Break Time
  BINAGI MEDIA GROUP, KWA PAMOJA TUIJUZE JAMII

  0 0

  Baadhi ya wahitimu wa kidato cha nne wa  Shule ya Sekondari ya Wavulana ya  Sullivan Provost , wakihudhuria mahafali yao ya kwanza yaliyofanyika shuleni hapo, Kibaha kwa Mathias, Mkoani Pwani hivi karibuni.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Shule ya Wavulana ya Sullivan Provost,  Rachel Mwalukasa (kushoto), akizungumza katika sherehe za mahafali ya kwanza ya kidato cha ya shule hiyo shuleni hapo, Kibaha kwa Mathias, Pwani hivi karibuni. Wengine kutoka kulia ni Mkuu wa Shule, Jacob Mkumbo, Mwenyekiti wa Bodi ya shule, Godfrey Zimba na mgeni rasmi Prof. Ibrahim Shao.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Shule ya Wavulana ya Sullivan Provost,  Rachel Mwalukasa (wa pili kushoto), akimpongeza Emmanuel Sebyo,  mmoja wa wanafunzi waliofanya vizuri kimasomo wakati sherehe za mahafali ya kwanza ya kidato cha ya shule hiyo shuleni hapo, Kibaha kwa Mathias, Pwani hivi karibuni. Kushoto ni mmoja wa wajumbe wa bodi ya shule hiyo, Prisca Mwalukasa.

  Prof. Ibrahim Shao (wa pili kulia) aliyekuwa mgeni rasmi akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu wa kidato cha nne wa Shule ya Sondari ya wavulana ya Sullivan Provost, Christopher Mfulu (kulia), wakati wa mahafali ya kwanza ya shule hiyo, shuleni hapo  Kibaha kwa Mathias, Pwani hivi karibuni. Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa shule hiyo, Rachel Mwalukasa na Mwenyekiti wa Bodi, Godfrey Zimba.
   Prof. Ibrahim Shao (wa pili kulia) Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, aliyekuwa mgeni rasmi akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu wa kidato cha nne wa Shule ya Sondari ya wavulana ya Sullivan Provost, Abdul Waziri (kulia), wakati wa mahafali ya kwanza ya shule hiyo, shuleni hapo  Kibaha kwa Mathias, Pwani hivi karibuni. Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa shule hiyo, Rachel Mwalukasa,  Mwenyekiti wa Bodi, Godfrey Zimba na Mkuu wa shule hiyo, Jcob Mkumbo.
  0 0

   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akiwafariji baadhi ya majeruhi wa ajali mbali mbali zilizotokea katika ziara za mikutano ya Kampezi mbali mbali za vyama vya Siasa hapa Nchini.
   Balozi Seif akiwapa pole vijana waliojeruhiwa katika ajali ya gari iliyokuwa ikielekea kwenye Mkutano wa Kampeni wa CUF Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja Hapo Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja.
   Mkuu wa Kitengo cha kupokea Wagonjwa wa dharura katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Dr. Juma  Salum Mbwana kati kati akimueleza Balozi Seif hatua zilizochukuliwa na Madaktari katika kuwahudumia majeruhi wa ajali mbali mbali za mikutano ya Kampeni.
   Balozi Seif na Mkuu wa Kitengo cha kupokea Wagonjwa wa dharura katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Dr. Juma  Salum Mbwana wakibadilishana mawazo kwenye Wodi ya akina Mama ambao baadhi yao walipata ajali ya gari katika Mikutano ya Kampen za Uchaguzi.

  MAJERUHI 10  wanaendelea kupatiwa huduma za matibabu katika Hospitali kuu ya Mnazi Mmoja kufuatia ajali tofauti walizopata  wakati wakielekea kwenye mikutano ya Kampeni  za uchaguzi inayoendelea katika sehemu mbali mbali hapa Nchini.

  Ajali hizo takriban zote zimehusisha zaidi vijana  waliokuwa wamepanda vyombo ambavyo vyengine vikiendeshwa kwa mwendo wa kasi  na baadhi  vilijaa idadi ya abiria  kupindukia mpaka.

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipata wasaa wa kufika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja kuwakagua majeruhi hao waliopata athari mbali mbali zikiwemo za kuvunjika viungo na michubuko.


  Akiwafariji majeruhi hao  kutoka Vyama vya Siasa vya  CCM katika  Mkutano wao wa  Makunduchi na CUF katika  Mkutano wao wa Nungwi Balozi Seif  aliwatakia Vijana hao kupoa haraka na kurejea katika familia zao waendelee na harakati zao za Kimaisha.

  Balozi Seif katika nasaha zake aliwaasa Vijana hao kuwa na tahadhari wakati wanapoendesha vyombo vya usafiri wa Bara barani kama gari na vespa kwani ni vyema wakaelewa kuwa mwendo wa kasi mbali ya kusababisha vifo lakini pia unachangia kuacha vilema vya maisha.

  Naye Mkuu wa Kitengo cha kupokea wagonjwa wa dharura katika Hospitali Kuu ya Mnamo Mmoja Dr. Juma Salum Mbwana { Mambi } alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba hali za wagonjwa hao zinaendelea vyema.

  Dr  Mambi alisema majeruhi waliotokana na ajali hizo wwengi kati yao tayari wamesharuhusiwa kurejea nyumbani baada ya kupatiwa huduma za Matibabu katika Hospitali hiyo.

  Kampeni za uchaguzi zilizokuwa zikiendelea katika maeneo mbali mbali Nchini Tanzania zinatarajiwa kufikia kilele chake ifikapo Tarehe 24 Mwezi huu na uchaguzi Mkuu utafanyika Tarehe 25 zikiwa zimebakia siku tano.
  Othman  Khamis Ame
  Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
  20/10/2015.

  0 0

    Bi. Bahati Muriga alifika Ubalozi wa Tanzania, Washington DC kuhudhuria tafrija iliyoandaliwa na Oxfam America. Bi. Muriga aliongelea maisha yake katika Mkoa wa Mwanza alipokuwa anafanya kazi kama Mkuu wa shule ya msingi, pamoja na hayo pia aliweza kuingia katika shughuli za kilimo akitafuta kipato ya kusomesha watoto wake wawili ili kuwapatia maisha bora.


  Ubalozi wa Tanzania Washington DC ulipata ugeni wa wasau kutoka mashirika mbalimbali waliokuja kuungana na Oxfam America inayoandaa Siku ya Chakula Duniani “World Food Day 2015” tarehe 16 Octoba. Bi. Muriga atasafiri kwenda katika mji wa Des Moines, Iowa kushiriki katika ziara na Oxfam inayoandaa matamasha mbalimbali kama ya “World Food Prize”.


   Bi Bahati Muriga akielezea ni jinsi gani alivyo na furaha kufika ubalozini na kuweza kukutana na watu mbalimbali kutoka mashirika tofauti hususan OXFAM.
   Bi Bahati Muruga akiwa pamoja na mwenyeji wake wa jioni hiyo Afisa ubalozi Suleiman Saleh.
   Wageni mbalimbali waliweza kuhudhuria na kuchanganyika pamoja na wenyeji wao ambao ni wafanyakazi wa ubalozi Pichani ni Mayor Mlima pamoja na Alice .

  0 0

  Huu ni uchambuzi wa Habari toka vituo mbalimbali vya Televisheni  October 20, 2015.

  Kamati ya Saidia Taifa Stars ishinde yatoa dira kuhakikisha timu hiyo inashinda   katika michezo yake ya kimataifa ;https://youtu.be/x5PxjRc9zpY

  Shirikisho la soka Ulaya UEFA yatangaza ratiba ya mechi za mchujo za timu zitakazowania   kufuzu kucheza finali  za Ulaya mwakani nchini Ufaransa ; https://youtu.be/aq31NLL6HHg

  NEC imewatahadharisha wananchi kuwa hakuna kifungu cha sheria kinachoruhusu mtu kubakia katika kituo cha kura baada ya kuoiga kura;  https://youtu.be/AGlLlvVXmdM

  Tambua sababu zinapolekea ugonjwa wa figo ambao umeonekana kuathiri kundi kubwa la watu hapa Nchini,kama anavyotueleza Dk.John; https://youtu.be/b9gESJoPPwg

  Fuatilia ujue Vipaumbele vya vyama mbalimbali kuelekea uchaguzi Mkuu Oktoba 25 mwaka huu vinazingatiwa?:https://youtu.be/X_0dHoFR_jU

  Fuatilia namna ambavyo watanzania walivyojipanga kuhakikisha Nchi inakuwa na amani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu: https://youtu.be/hq0__StJoM4
  Tambua Mchango wa vyombo vya habari katika kutuliza vurugu katika wakati huu wa kuelekea uchaguzi Mkuu zikiwa zimesalia siku 4 tu:  https://youtu.be/c0UldkD7TcE

  Fuatilia muamko wa wananchi baada ya kusambazwa kwa elimu ya kupiga kura zikiwa zmesalia siku chache kuelekea uchaguzi mkuu: https://youtu.be/nGtbDZVIBxc

  Mgombea Uraisi CCM Zanzibar Dkt. Ali Shein awaahidi wananchi kuendeleza mradi mkubwa wa viwanda Wa FUMBA kusaidia ajira kwa Vijana. https://youtu.be/VAF-4N0L09Q
  Mgombea Uraisi CCM Dkt. John Magufuli aahidi kupambana na wavuvi haramu katika Ziwa Viktoria endapo atapata ridhaa ya wananchi. https://youtu.be/QPgoO8cztgw
  Mjumbe wa Halmashauri Kuu Ya CCM Taifa Balozi Ali Abeid Karume asema wananchi wa Zanzibar wana mamlaka kamili ya kuchagua kiongozi wanayemtaka. https://youtu.be/PaTFO8jhyo8
  Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Raisi Jakaya Kikwete amezindua awamu ya pili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa vita ndani ya kamandi ya anga Ngelengele. https://youtu.be/ll36RCNB_qo

  Jeshi la polisi nchini limewahakikishia wananchi kuwa limejipanga vema kuhakikisha ulinzi na usalama katika vituo vya kupigia kura. https://youtu.be/e2HOVGUBcLw

  Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA yavitaka vyombo vya habari kutoa habari zenye kuelimisha na kudumisha amani. https://youtu.be/nyZxEAcu9wc 

  0 0

   SenSei Rumadha Fundi, amesimama mbele ya bendera ya Tanzania.
   Wakicheza Kata ya kundi kwa pamoja "Shisochin Kata"
  Wakuu matawi nchi shiriki.
  Kundi la wawakilishi sita wa nchi za Ulaya.

   Gasshuku au semina ya Karate mtindo wa Okinawa Goju Ryu
  Jundokan So Honbu, imefungwa Jumapili usiku na kufuatiwa kwa
   tafrija kubwa ya kuwaaga washiriki "Sayonara Party" wa kike
   na kiume, umri kuanzia miaka 13 had 70 toka nchi mbalimbali
   za Ulaya na Japan ikiwemo na Tanzania iliyowakilishwa na
   sensei Rumadha. Viongozi wa Karate wa nchi zilizoshiriki ni:
   sensei Rene Ramanitrandrasana 9 Dan  wa Ufaransa,
   Sensei Antoine, Ufaransa 5 Dan, Sensei Bob Honiball 8 Dan
   Uingereza, Sensei Tony  Green 8 Dan , Uingereza, Sensei
   Jenni 5 Dan, Uingereza,  Sensei Ilpo, Sweden, 7 Dan,
   Sensei Caideiro 5 Dan, Ureno, Sensei Dr. Freidrich Gsodam 9
   Dan, Austria.

   Hii ilikuwa ni semina kubwa ya kipekee kufanyika 
   Uingereza na wakuu wake wa tano kushiriki toka visiwa vya
   Okinawa; walio ongozwa na mwenyekiti wa sasa wa mtindo huo
   Sensei Yoshihiro Miyazato, Kancho.

   Mbinu na matumizi yake ya kujihami kutumia sanaa ya Karate
   pamoja na ubora wa kata zilifanyiwa mazoezi sana katika
   semina hiyo. Kuzingatia nidhamu na utamaduni wa jadi wa
   Karate na kuheshimu desturi zake halisi, viongelewa
   katika  mfumo huo wa Goju Ryu Karate. Kwa ujuml, semina
   hiyo iliwakutanisha  washiriki  wapatao  120,

   wakiwemo na watoto wa umri wa kuanzia miaka 13 had 17.

  0 0

    Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw. Idd Ramadhan Mapuri akiwasalimia wazee na watetezi wa haki za binadamu (hawapo pichani) wakati wa semina juu ya haki za wazee mapema hii leo jijini Dar es Saam.
   Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi. Mary Massay akitoa neno la ufunguzi kwa wazee na watetezi wa haki za binadamu (hawapo pichani) wakati wa semina juu ya haki za wazee mapema hii leo jijini Dar es Saam.
   Mkurugenzi wa shirika lisilo la Kiserikali la Help Age Bw. Smart Daniel akiwasilisha mada kwa wazee na watetezi wa haki za binadamu (hawapo pichani) wakati wa semina juu ya haki za wazee mapema hii leo jijini Dar es Saam.
   Baadhi ya wazee na watetezi wa haki za binadamu walioshiriki semina elekezi juu ya haki za wazee iliyoratibiwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala kwa kushirikiana na shirika lisilo la Kiserikali la Help Age mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

   Baadhi ya wazee na watetezi wa haki za binadamu walioshiriki semina elekezi juu ya haki za wazee iliyoratibiwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala kwa kushirikiana na shirika lisilo la Kiserikali la Help Age mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
   Baadhi ya wazee na watetezi wa haki za binadamu walioshiriki semina elekezi juu ya haki za wazee wakimsikiliza kwa makini Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi. Mary Massay wakati akitoa neno la ufunguzi mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
  Picha zote na Eliphace Marwa- Maelezo.

  Na Eliphace Marwa - Maelezo
  TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Tanzania kwa kushirikiana Shirika lisilo la kiserikali la Help Age Tanzania zinaujulisha umma kwamba tarehe 21 Oktoba 2015 kutakuwa na maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu Afrika.

  Maadhimisho hayo yatakayofanyika katika Hoteli ya New Afrika jijini Dar es Salaam ambapo viongozi mbalimbali wa Serikali na Mabalozi wa Afrika watahudhuria maadhimisho hayo yenye lengo la kulinda na kutetea haki za wazee Tanzania.

  Akizungumza na Wazee na watetezi wa haki za binadamu, Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi. Mary Massay amesema kuwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inawajibika Kitaifa kufuatilia hatua za utekelezaji wa haki za binadamu hususani wazee ili waweze kuishi kwa furaha, amani na usalama kinyume na sasa Ambapo wazee wamekuwa wakiuawa kwa imani za kishirikina.

  Maadhimisho haya ya haki za Binadamu Afrika ni sehemu ya Mpango-Kazi wa Kitaifa wa Haki za Binadamu ambao ni mkakati wa Serikali wa miaka mitano (2013 – 2017) wenye lengo la kutoa dira kwa Serikali yenyewe kwa maana ya Wizara, Idara, Taasisi za Serikali na Asasi za Kiraia na wananchi kwa ujumla jinsi ya kukuza, kulinda na kuhifadhi haki za binadamu ili kuimarisha utawala bora nchini. 

  Naye Mkurugenzi toka Shirika lisilo la Kiserikali la Help Age Bwana Smart Daniel amesema kuwa kati ya nchi 96 Duniani Tanzania iko katika nafasi ya 92 kwa kulinda haki za wazee kwa kuzingatia vigezo vya upatikanaji wa huduma bora za afy, mazingira wezeshi kwa wazee, uhakika wa kipato kwa wazee pamoja na uwezeshwaji wa wazee katika fursa mbalimbali ili kujipatia kipato.

  "Katika suala la kipato Tanzania iko nafasi ya 94 kwa kujali wazee kwa kuwalipa pensheni, katika suala la Afya kwa wazee Tanzania iko nafasi ya 66 na katika suala la mazingira wezeshi kwa wazee Tanzania iko nafasi ya 88 na hii inatokana na kutokuwepo kwa sheria ya wazee", alisema Bwana Smart. 

  Aidha, Maadhimisho haya yanalenga kuongeza uelewa kwa umma juu ya wajibu alionao kila mwananchi wa kutetea, kulinda, kuhifadhi na kuhamasisha haki za binadamu nchini ili kudumisha amani, utulivu na maendeleo endelevu.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo kufuatia kifo cha marehemu Rubani William Slaa aliyefariki Dunia wiki iliyopita kwa ajali ya Helkopta wakati Makamu wa Rais alipofika nyumbani kwa Marehemu Slaa Gongolamboto jijini Dar es salaam leo Octoba 20, 2015.  
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na kumfariji Bibi Tabita Slaa aliyekuwa Mke wa Marehemu Rubani William Slaa aliyefariki wiki iliyopita kwa ajali ya Hekopta wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Gongolamboto jijini Dar es salaam leo Octoba 20,2015 kwa ajili ya kutowa mkono wa pole.
  (Picha na OMR)

  0 0
 • 10/20/15--04:44: ZIARA YA WANAJESHI SONGWE
 •  handisi Mshauri wa Mradi wa ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Songwe, Khalil Jadallah akibadilishana mawazo na Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Songwe, Mbeya, Khamisi Amiri wakati wa ziara ya Maofisa  Wanadhimu wa Jeshi la ulinzi la Wananchi wa chuo cha Arusha (College of Senior Commandants- CSC) katiika kiwanja hicho Oktoba 15 kwa ajili ya kujifunza masuala ya usafiri wa anga.
   Naibu Mkuu wa Chuo cha Maofisa Wanadhimu wa Jeshi la ulinzi la Wananchi wa chuo cha Arusha (College of Senior Commandants- CSC), Meja Jenerali Alfred Kapinga (kushoto) akisaini kitabu cha wageni alipowasili kwenye ofisi ya Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Songwe, Mbeya jana Oktoba 15 na ujumbe wake wa maofisa 30 wa chuo hicho kwa ajili ya kujifunza masuala ya usafiri wa anga.
    Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Songwe, Mbeya, Khamisi Amiri akiwaongoza Maofisa Wanadhimu wa Jeshi la ulinzi la Wananchi wa chuo cha CSC Arusha (College of Senior Commandants- CSC) kutembelea kiwanja hicho Oktoba 15 kwa ajili ya kujifunza masuala ya usafiri wa anga.
   Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Songwe, Mbeya, Khamisi Amiri akiwaongoza Maofisa Wanadhimu wa Jeshi la ulinzi la Wananchi wa chuo cha CSC Arusha (College of Senior Commandants- CSC) kutembelea kiwanja hicho Oktoba 15 kwa ajili ya kujifunza masuala ya usafiri wa anga.

    Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Songwe, Mbeya, Khamisi Amiri (katikati mbele) akiwaongoza  Maofisa Wanadhimu wa Jeshi la ulinzi la Wananchi wa chuo cha CSC Arusha (College of Senior Commandants- CSC) kutembelea kiwanja hicho Oktoba 15 kwa ajili ya kujifunza masuala ya usafiri wa anga.  Kushoto kwake ni Mhandisi Mshauri wa Mradi wa ujenzi wa jengo jipya la abiria la kiwanja hicho, Mhandisi  Khalil Jadallah. 
   Mhandisi Mshauri wa Mradi wa ujenzi wa jengo jipya la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Songwe, Mbeya, Mhandisi Khalil Jadallah akiwaelezea Maofisa Wanadhimu wa Jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania wa chuo cha CSC Arusha (College of Senior Commandants- CSC) kuhusu jengo la abiria walipotembelea kiwanja hicho Oktoba 15 kwa ajili ya kujifunza masuala ya usafiri wa anga. 
   Mhandisi Mshauri wa Mradi wa ujenzi wa jengo jipya la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Songwe, Mbeya, Mhandisi Khalil Jadallah akiwaelezea Maofisa Wanadhimu wa Jeshi la ulinzi la Wanananchi wa Tanzania wa chuo cha CSC Arusha (College of Senior Commandants- CSC) kuhusu barabara ya kutua na kuruka walipokitembelea Oktoba 15 kwa ajili ya kujifunza masuala ya usafiri wa anga. 
    Muongoza Ndege wa Kiwanja cha Ndege cha Songwe, Mbeya, Berti Ngowi akiwaelezea Maofisa Wanadhimu wa Jeshi la ulinzi la Wanananchi wa Tanzania wa chuo cha CSC Arusha (College of Senior Commandants- CSC) kuhusu utendaji kazi wa kituo hicho walipotembelea kiwanja hicho jana Oktoba 15 kwa ajili ya kujifunza masuala ya usafiri wa anga.
  Maofisa Wanadhimu wa Jeshi la ulinzi la Wanananchi wa Tanzania wa chuo cha CSC Arusha (College of Senior Commandants- CSC) wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Kiwanja cha Ndege cha Songwe, Mbeya baada ya kumaliza ziara yao ya kutembelea hicho Oktoba 15 kwa ajili ya kujifunza masuala  ya usafiri wa anga. 
   Inspekta Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto katika Kiwanja cha Ndege cha Songwe, Mbeya, Inspekta Msaidizi James Waziri akiwaelezea Maofisa Wanadhimu wa Jeshi la ulinzi la Wanananchi wa Tanzania wa chuo cha CSC Arusha (College of Senior Commandants- CSC) kuhusu utendaji kazi wa magari ya zimamoto wakati walipotembelea kiwanja hicho Oktoba 15 kwa ajili ya kujifunza masuala ya usafiri wa anga.
   Naibu Mkuu wa Chuo cha Maofisa Wanadhimu wa Jeshi la ulinzi la Wananchi wa chuo cha Arusha (College of Senior Commandants- CSC), Meja Jenerali Alfred Kapinga akimkabidhi zawadi Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Songwe, Mbeya,  Khamisi Amiri ikiwa ni kumshukuru kwa mapokezi mazuri wakati maofisa hao walipotembelea kiwanja hicho kwa ajili ya kujifunza masuala ya usafiri wa anga jana Oktoba 15. Kushoto ni Ofisa Uendeshaji wa Kiwanja hicho, Jordan Chami.
   Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Songwe, Mbeya, Khamisi Amiri akiwashukuru  Maofisa Wanadhimu wa Jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania wa chuo cha Maofisa Wanadhimu Arusha (College of Senior Commandants- CSC), kwa kutembelea kiwanja hicho jana Oktoba 15 kwa ajili ya kujifunza masuala ya usafiri wa anga. Kushoto ni Naibu Mkuu wa Chuo cha Maofisa Wanadhimu wa Jeshi la ulinzi la Wananchi wa chuo cha Arusha (College of Senior Commandants- CSC), Meja Jenerali Alfred Kapinga.
   Naibu Mkuu wa Chuo cha Maofisa Wanadhimu wa Jeshi la ulinzi la Wananchi wa chuo cha Arusha (College of Senior Commandants- CSC), Meja Jenerali Alfred Kapinga akimshukuru Ofisa Uendeshaji wa Kiwanja cha Ndege cha Songwe, Mbeya, Jordan Chami baada ya kutembelea kiwanja hicho kwa ajili ya kujifunza masuala ya usafiri wa anga jana Oktoba 15. Katikati ni Ofisa Uhusiano wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Godfrey Lutego.
  Abiria wakiteremka kutoka kwenye ndege ya Fast Jet baada ya kutua katika Kiwanja cha Ndege cha Songwe, Mbeya jana asubuhi Oktoba 15. 
  (PICHA ZOTE NA MPIGA PICHA WETU).

  0 0

  Mshambuliaji wa timu ya Simba, Hamisi Kiiza ndiye mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi Septemba.
  Kwa kuibuka mchezaji bora, Kiiza atazawadiwa sh. milioni moja kutoka kwa mdhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom.
  Kiiza ambaye ameisadia Simba kufanya vizuri kwenye mwezi huo, ikiwemo kufunga mabao matatu (hat trick) kwenye mechi dhidi ya Kagera Sugar aliwashinda washambuliaji wa timu za Stand United (Elias Maguli) na Yanga (Amisi Tambwe).
  Ndani ya mwezi Septemba ambapo zilichezwa raundi tano, Kiiza amefunga jumla ya mabao matano.


  0 0

   Mwezeseshaji wa mafunzo ya waandishi wa habari katika uchaguzi jumuishi,kwa watu wenye ulemavu,Blandina Sembu akizungumza na waandishi wa (habari hawapo pichani) juu ya waandishi kuhamasisha watu wenye ulemavu kupiga kura katika mazingira rafiki katika semina iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

  Sehemu ya waandishi wakifatilia maada katika semina iliyoandaliwa  na SHIVYAWATA BA panoja na Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Dar es Salaam(DCPC) iliyofanyika jijini Dar es Salaam

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 
  WAANDISHI wa habari wametakiwa kuandika habari kwa usahihi wakiwataja watu wenye ulemavu kwa kutumia majina sahihi kuepuka unyanyapa dhdi yao .

  Rai hiyo ilitolewa juzi jijini Dar es Salaam na Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Lucas Kija, wakati wa mafunzo ya siku mbili ya waandishi wa habari juu ya uandishi wa habari za uchaguzi kwa watu wenye ulemavu.

  Mafunzo hayo ambayo yaliwashirikisha waandishi wa habari kutoka Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Lindi, Mtwara, Kilimanjaro na Tanga  yaliandaliwa na Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) kwa kushirikiana na Klabu ya Waandishi wa Habari wa Jiji la Dar es Salaam (DCPC),  kupitia Mradi wa Uchaguzi Jumuishi.
  "Kuna majina sahihi na yasiyo sahihi kwa watu wenye ulemavu, hivyo waandishi wa habari lazima mtaje mhusika kwa kutumia jina sahihi," alisema Kija alipokuwa akitoa mada katika mafunzo hayo.

  Kwa mujibu wa mwezeshaji huyo, miongoni mwa majina yasiyo sahihi ni kipofu, wasiosikia, vichaa, chizi, zeruzeru na watu wenye mtindio wa ubongo ambayo hayapaswi kutumiwa.

  Mwezeshaji huyo aliyataja baadhi ya majina sahihi yanayopaswa kuwaita watu wenye ulemavu kuwa wasioona, viziwi na walemavu wa akili.

  Katika mafunzo hayo, washiriki walipata fursa ya kupata elimu kuhusu vikwazo vikuu vinavyokwamisha ushiriki wa watu wenye ulemavu katika uchaguzi. Elimu hiyo ilitolewa na Wawezeshaji Kija na Blandina Sembu.

  Wawezeshaji hao walisema vikwazo hivyo vimegawanyika katika mitazamo ya kijamii, mazingira na kitaasisi.

  Amesema kuna  vikwazo vya vimekuwepo katika mchakakato wa uchaguzi kunazia kampeni,usalama kutokana na mazingira ya jamii hiyo,kukosekana kwa takwimu sahihi za watu wenye ulemavu, miundombinu isiyo rafiki na sheria kandamizi mfano gharama za uchaguzi.

  Kaimu Mkurugenzi wa SHIVYAWATA, Francis Gugu ambaye pia ni mlemavu wa usikivu hafifu, alisema shirikisho hilo linajumuisha vyama 10 vya watu wenye ulemavu kitaifa na limekuwa likifanya ushawishi na utetezi kwa watu wote.
  Akizungumzia mradi huo, Gugu alisema Mei 20, mwaka huu, SHIVYAWATA ilitia saini mradi huo wa mwaka mmoja na Shirika la Wanawake la Umoja wa Mataifa (UN-Women) kwa lengo la kuchoche ushiriki wa watu wenye ulemavu katika uchaguzi mkuu.

  0 0

  Ligi kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) inatarajiwa kuendelea kesho Jumatano kwa michezo minne kuchezwa katika viwanja tofauti nchini, huku timu 8 zikisaka kupata pointi tatu muhimu.
  Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Young Africans watawakaribisha Toto Africans, mchezo utakaonza majira ya saa 10:30 jioni, mjini Shinyanga Stand United watakua wenyeji wa Majimaji katika uwanja wa Kambarage mjini humo.
  Tanzania Prisons watawakaribisha Simba SC katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, huku Wagosi wa Kaya, Coastal Union wakiwakaribisha Kagera Sugar katika uwanja wa Mkwakani jijini Tanga.
  Alhamis ligi hiyo itanendelea kwa michezo minne pia kucheza katika viwanja mbalimbali, JKT Ruvu wataikaribisha Mtibwa Sugar uwanaj wa Karume jijini Dar es salaam, Mwadui FC watacheza dhidi ya Mgambo Shooting katika uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga.
  Jijini Mbeya, Mbeya City watawakaribisha African Sports katika uwanja wa Sokoine, huku Ndanda FC wakiwa wenyeji wa waoka mikate wa bakhresa Azam FC katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

  0 0

  IMG_20151016_175545
  Pichani juu na chini ni muonekano wa Jengo la kituo cha afya Kivunge Wilaya ya Kaskazini "A" visiwani Unguja kilichojengwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa.

  Na Mwandishi wetu
  BAADHI ya Wananchi wa Kijiji cha Kivunge Wilaya ya Kaskazini “A” wameelezea kuridhishwa kwao na huduma za afya zinazotolewa katika kituo kipya cha afya cha Kivunge.

  Kituo hicho kimejengwa chini ya mradi wa Umoja wa Mataifa(UN) wa kuviwezesha vituo vya afya mbali mbali nchi ambapo kituo hicho kinatoa huduma mbali mbali za akina mama na watoto pamoja na masuala ya kutibu vidonda na majeraha mbali mbali.

  Akizungumza na waandishi wa habari Mkazi wa kijiji hicho, Kassim Haji Simai alisema kituo hicho kimekuwa mkombozi wa wananchi kwani pindi panapotokea mgonjwa wa ghafla ufika katika kituo hicho na kupewa matibabu ya haraka.

  Alizitaja changamoto kubwa iliyopo kituoni hapo kuwa ni pamoja na upungufu wa madakta na wauguzi jambo ambalo baadhi ya wananchi ukaa muda mrefu wakisubiri huduma kwani wagonjwa wanakuwa wengi kuliko watoa huduma.
  IMG_9525
  “Tunawashukru sana wafadhili waliojenga kituo hiki na serikali kwa ujumla kwani wametusaidia sana huduma hizi tulikuwa tunazifuata mbali sana”, alisema Haji.

  Kwa upande wake Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez alifika katika kituo hicho na kutembelea maeneo mbali mbali ya kituo hicho na kuona ni jinsi gani kinatoa huduma kwa wananchi.

  Alisema kuwa ufanisi wa mradi huo unaongeza ushawishi kwa Umoja wa Mataifa kuongeza zaidi msaada hasa vifaa vya kisasa vya huduma za afya pamoja na wataalamu wa afya ili kuhakikisha wananchi wanaendelea kupata huduma za afya kwa ufanisi zaidi.

  “ Kituo hiki kinatoa huduma kwa wananchi wengi hivyo nitapeleka salamu makao makuu ili tujadiliane na kuona ni jinsi gani tunaendelea kusaidia kituo hiki hasa katika suala la vifaa vya kisasa na madaktari.”, alifafanua Bw.Rodriguez.
  IMG_9533
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akitazama jengo la kituo cha afya Kivunge alipofanya ziara fupi ya kukagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa visiwani Unguja ikiwa ni sehemu ya sherehe za miaka 70 ya Umoja wa Mataifa tangu kuaznishwa. Kulia ni Daktari wa kujitolea wa kituo cha afya Kivunge, Alexander Vogt.

  Naye Mratibu wa Mradi wa Health Improvement Project (HIP), Jabir James alisema kituo hicho kinatoa huduma bora na zenye kukidhi mahitaji kwa wananchi ambapo kwa siku wanapokea zaidi ya wagonjwa 100 hadi 200 hali ambayo kitathimini ni kubwa kutokana na uwezo wa kituo hicho kimatibabu.

  Alisema kuwa bado wanaendelea kutafuta ufumbuzi wa kuongeza vifaa na madaktari ili kuhakikisha wanaongeza ufanisi katika utoaji wa huduma bora ili kufikia dhana ya umoja wa mataifa katika masuala ya afya ya kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na uhakika wa kupata huduma bora za afya na endelevu.
  IMG_9557
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akikagua maeneo mbalimbali ya kituo hicho huku akiwa ameambatana na Mkuu wa ofisi ndogo ya Umoja wa Mataifa Zanzibar, Anna Senga (nyuma ya Alvaro) pamoja na Mtaalamu wa Mawasiliano na Mahusiano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu. 
  Kulia ni Daktari wa kujitolea anayehudumia wangonjwa katika kituo hicho Alexander Vogt.

  IMG_9564
  Daktari wa kujitolea wa kituo cha afya Kivunge, Alexander Vogt akimwonyesha Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez baadhi ya ripoti za magonjwa yanayowasumbua watoto chini ya umri wa miaka 5 wanaopatiwa matibabu katika kituo hicho.
  IMG_9574
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) akizungumza na Dr. Mohamed Abdallah (kulia) aliyekuwa akitoa huduma kwa mtoto Salma Shamis mwenye siku 10 ambaye anasumbuliwa na masikio wakati Bw. Rodriguez alipofanya ziara fupi ya kukagua kituo cha afya Kivunge Wilaya ya Kaskazini “A” visiwani Unguja kilichojengwa na Umoja wa Mataifa ikiwa ni sehemu ya sherehe za miaka 70 ya Umoja huo tangu kuanzishwa.
  IMG_9591
  Pichani juu na chini ni baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Kivunge Wilaya ya Kaskazini “A” wakiwa kwenye foleni ya kuingia kwenye vyumba vya madaktari kama walivyokutwa na kamera yetu.
  IMG_20151016_175753IMG_9612
  Mratibu wa Mradi wa Health Improvement Project (HIP), Jabir James akizungumza na waandishi wa habari waliombatana kwenye ziara hiyo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (hayupo pichani).
  IMG_9621
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiwa amembeba mtoto Shekha Khamis (3) mkazi wa Kijiji cha Kivunge Wilaya ya Kaskazini “A” aliyefika kituoni hapo kupatiwa matibabu.

  0 0

  Kipindi hiki hukujia kila JUMATATU, kujadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015
  Ni kipindi cha mwisho kabla ya uchaguzi, na washiriki wengi walishiriki kutoa mchango wao kuhusu mchakato ulivyokuwa, na neno ama wosia wao kwa waTanzania wote
  KARIBU

  0 0

   Mwandishi Wetu, Geita
  MGODI wa dhahabu wa geita (GGM), umezalisha ajira zaidi ya 200 kwa jamii baada kuwekeza zaidi ya Sh1.7 Bilioni kupitia programu ya Uchumi na Maendeleo (GEDP) ambayo imelenga kusaidia wakulima na wajasiriamali wadogo na wa kati, wanaoishi jirani na mgodi.


  Akizungumza wakati Mkuu wa Mkoa wa Geita, Fatma Mwassa alipotembelea mgodini hapo juzi, Makamu wa Rais wa Anglo Gold Ashanti/GGM, Simon Shayo alisema mpango umelenga kubadili hali za maisha ya wakazi kuwa tofauti na ilivyokuwa kabla mgodi haujaanza kufanyakazi.


  Alisema mradi umewasaidia wakazi hao na familia zao kuwa na fani ambazo wanazitumia kwa uzalishaji na mbinu za kujipatia masoko katika mji wa Geita na maeneo mengine nje ya mgodi huo.


  "Hiyo inatokana na ubora wa mafunzo ambayo tunawapa sanjari na mbinu za biashara" alisema meneja huyo na kuongeza kuwa zaidi ya ekari 800 zimetengwa kwa ajili ya kilimo cha Alizeti, Mpunga na mazao mengine na utafiti wa udongo umekamilika.


  Pia utengenezaji wa miundombinu kwa ajili ya umwagiliaji unafanyika na upande mwingine, ununuzi wa mashine za umwagiliaji, uchomeaji, mashine za kuzalisha umeme, vyerehani na mashine za kudarizi kwa ajili ya wananchi hao wa Geita vinafanyika.


  Meneja huyo alibainisha kuwa lengo ni kuhakikisha kunakuwa na mnyororo endelevu wa thamani ya mazao ya kilimo kwa kuongeza viwango vyao vya ufahamu katika mfumo wa masoko na kuongeza ubora wa mazao na wigo wa biashara kwa wajasiriamali hao wadogo na kati.


  "Tunatumia programu hiyo kwa ajili ya kuwawezesha wakazi iuchumi na pia kupunguza kiwango cha umaskini" anasema na kuongeza kuwa mpango huo utapunguza idadi ya vijana wasio na ajira Geita na wengine ambao wamekuwa wakijitumbukiza katka uhalifu mgodini.


  Mkuu wa Mkoa wa Geita, Fatma Mwassa alisema kuna matumaini makubwa kuwa jitihada hizo za GGM zitazidi kukua na kubadili maisha ya walio wengi kwa kuwawezesha kiuchumi wananchi wa Geita.


  "Naamini sasa watauza mazao na bidhaa zilizokamilika na sio ghafi kama awali na sio kwa Geita pekee bali pia nchi jirani" alisema Mwassa. Kulingana na takwimu za hivi karibuni, kilimo kimetoa ajira kwa asilimia 88 ya watanzania nchini.

  0 0

  Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kupitia mwamvuli wa Ukawa, Mhe Edward Lowassa akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mwenza wa umoja huo, Dk. Emmanuel Makaidi wakati wa ibada ya kuuaga iliyofanyika viwanja vya Karimjee Dar es Salaam leo mchana. Katika ibada hiyo viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa na serikali walihudhuria.
  Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye ibada hiyo.
  Wananchi wakiwa wamejipanga foleni wakati wakienda kutoa heshima za mwisho kwa marehemu.
  Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Ndg. Philip Mangula (kulia), akipeana mkono wa pole na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mhe. Freeman Mbowe wakati alipofika kuhudhuria ibada hiyo.

  Mjane wa marehemu, Dk. Emmanuel Makaidi, Modesta Ponela akiwa ameinua mikono wakati akimuaga mumewe katika ibada hiyo
  Msajili wa Vyama Vya Siasa, Jaji Francis Mtungi, akizungumza kwa niaba ya serikali wakati wa misa hiyo ya kumuaga Dk. Makaidi.


  Na Dotto Mwaibale
  MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Profesa Mwesiga Baregu amesema kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha National League for Democratic (NLD), na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) Dk. Emmanuel Makaidi ni kiashiria tosha cha ushindi wa umoja huo.
  Mwenyekiti huyo mwenza wa Ukawa, amezikwa leo jioni  katika makaburi ya Sinza jijini hapa, huku yakihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa
  Profesa Baregu aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati akitoa salamu za rambirambi na kwa wanafamilia, wanandugu, wanachama na wanasiasa mbalimbali nchini walioguswa na kifo hicho wakati ibada fupi kutoa heshima za mwisho Dk.Emanuel Makaidi yaliyofanyika katika viwanja vya Karimjee.

  "Tutaendelea kumkumbuka hususani pale ilipokundwa Ukawa kwani alikuwa miongoni mwa wabunge waliodiriki kususia bunge la katiba lililokuwa likiendelea," alisema.
  Alisema kuwa kwa sasa nguvu ya Ukawa inaonekana kukuwa waziwazi na kifo chake kina ashiria kwamba katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika 25 mwezi huu umoja huo utashinda.
  Msajili wa vyama vya siasa.
  Kwa upande wake Msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi alisema kifo hicho kimeacha pengo kubwa kwani alikuwa mkereketwa wa mabadiliko katika siasa.
  Makamu Mwenyekiti NLD.
  Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti NLD, Mfaume Hamisi, alisema kuwa chama hicho kitaendelea kiukumbuka na kuyasimamia misimamo na mambo aliyoyaamini Dk.Makaidi wakati wa uhai wake.
  Mhe. James Mbatia.
  Akizungumza kwa niaba ya Ukawa, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi na Mwenyekiti Mwenza wa umoja huo, James Mbatia alisema umoja huo utaendelea kumuenzi Dk.Makaidi na kubainisha kuwa alikuwa akiamini mageuzi na mabadiliko nchini lakini hadi leo hawako nae tena.
  Msemaji wa Familia.
  Kwa upande wake Oscar Makaidi ambaye ni msemaji wa familia ya marehemu aliutaka umoja huo kuendelea na kazi katika siku hizi chache zilizobaki kuelekea katika uchaguzi mkuu na kuongeza ushirikiano katika chama hicho kwani aliyekufa ni Makaidi na si chama.
  Philip Mangula.
  Akitoa salamu za pole na rambi rambi, Makamu Mwenyekiti Chama cha Mapinduzi (CCM), Philip Mangula alitoa pole kwa wanafamilia wanasiasa kwa kuondokewa mwenzao.

  0 0


  Mgombea Urais kupitia chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia maelfu ya wananchi wa Sengerema jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika mjini humo.Katika mkutano huo wa kampeni Dkt Magufuli amezishauri halmashauri nchini kuacha tabia ya kukopa pesa kutoka katika taasisis za kifedha na kulipia fidia za wananchi ambao serikali inataka kutumia maeneo yao kwa ajili ya huduma za kijamii. 

  Akiomba kura katika wilaya mpya ya Nyang'wale mkoani Geita,Dkt Magufuli ametumia jukwaa hilo kukataza mpango wa kukopa pesa kutoka kwa taasisi za kifedha,ambapo wamekua wakitaka riba kubwa  ili kuweza kulipa fidia kwa wakazi ambao wameamishwa kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za halmashauri  hiyo mpya ya Nyang'wale kwa kutaka kutafutwa kwa njia nyingine za upatikanaji wa fedha hizo kupitia mapato yao.
   Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akisalimiana na mkazi wa Sengerema aliposimama kuwasalimia wananchi alipokuwa akielekea kwenye mkutano wa kampeni. 
   Mkuu wa msafara wa Kampeni za Mgombea Urais wa CCM,Ndugu Abdallah Bulembo akitoe maeleoz mafupi kwa wakazi wa Nyang'wale namna ya kuwapigia kura wagonbea wa CCM. 

  Mgombe Urais wa CCM Dkt John Magufuli akiwanadi madiwani wa wilaya ya Sengerema mbele ya maelfu ya wananchi alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo kwenye mkutano wa Kampeni,ambapo aliwaomba wampigie kura za kutosha ili aibuke mshindi na kuwa rais wa awamu ya tano
   Wakazi wa mji wa Sengerema wakimsikiliza Mgombe Urais wa CCM Dkt John Magufuli alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo kwenye mkutano wa Kampeni,ambapo aliwaomba wampigie kura za kutosha ili aibuke mshindi na kuwa rais wa awamu ya tano.
    Wananchi wakiwa wamefunga njia wakitaka Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli awasalimie na pia wamweleze shida zao,ili iwapo akichaguliwa katika nafasi ya Urais baasi aweze kuwakumbuka na kuwasaidia.
  Msafara wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli ukiingia kwenye kivuko cha Mv Misungwi katika feri ya Busisi akitokea wilayani Sengengerema kuelekea jijini Mwanza baada ya kumaliza mikutano yake ya kampeni aliofanya katika wilaya ya Geita vijijini,wilaya ya Nyang'wale pamoja na Sengerema mkoani Mwanza.
   Wakazi wa mji wa Sengerema wakishangilia ujio wa Dkt Magufuli alipokuwa akipita mjini Sengerema kuelekea jijini Mwanza.
   Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akiwahutubia wananchi wa Wilaya  Sengerema kwenye mkutano wa kampeni 
   Wananchi wa Sengerema wakimsikiliza Mweyekiti wa chama cha CCM mkoa wa Mwanza,Ndugu Anthony Dialo,alipokuwa akimkaribisha kiongozi wa msafara wa Kampeni za Mgombea Urais wa CCM Ndugu Abdallah Bulembo ili amkaribishe mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli awahutubie Wananchi.
   Maelfu ya wananchi wa Sengerema wakifuatilia mkutano wa kampeni.
   Wananchi wakiwa wamefunga njia wakitaka Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli awasalimie na pia wamweleze shida zao,ili iwapo akichaguliwa katika nafasi ya Urais baasi aweze kuwakumbuka na kuwasaidia.

   Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akiwahutubia wananchi wa Wilaya mpya ya Nyang'wale,katika uwanja wa shule ya msingi ya Jitundu,kwenye mkutano wa kampeni.
   Vijana na Mabango yao
   Wanachi wa Sengerema wakishangilia msafara wa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akipita kuendelea na mikutano yake ya kampeni.

  0 0

  Suneeta Reddy, mkurugenzi wa hospitali za Apollo

  Na Mwandishi Wetu,
  SARATANI inasemwa kuwa chanzo kikubwa cha pili kinachosababisha vifo ulimwenguni. Saratani ya matiti peke yake inaripotiwa kuwa ya pili kama sababu kubwa ya vifo vinavyohusisha saratani kwa wanawake nchini Tanzania.

   Kuchelewa kupata ugunduzi wa haraka na tiba kwa wagonjwa wengi wa saratani ya matiti kunachangia kuleta ugumu kwenye matibabu pale ugonjwa unapoingia ngazi ya juu zaidi, Gonjwa hili limeendelea kuwa janga hasa kwa nchi zinazoendelea.

  Ulimwenguni,mwezi Oktoba ni mwezi maalumu wa kutoa maarifa na elimu juu ya saratani ya matiti. Kwa kawaida tarehe 19 Oktobanikilele cha saratani ya matiti nalengo kuu likiwa ni kutoa maarifa ya msingi na yenye faida kuhusiana na ugonjwa huo. Silaha bora ya kupigana na saratani ya matiti ni kuigundua mapema.

  Ongezeko kubwa la namba ya vifo kutokana na saratani linatikisa Tanzania, jinsii navyoathiri namba kubwa ya wanawake kwa sasa. Kutokana na takwimu za hivi karibuni kutoka hospitali ya Ocean Road kitengo cha saratani (ORCI), tafiti zinaonyesha ongezeko kubwa la namba kutoka mwaka 2013-2014 (nusu ya kwanza ya mwaka) zaidi ya kesi mpya  400 zimeripotiwa.

  Maoni kwenye hizo takwimu, Dk. Crispin Kahesa mkurugenzi wa Ocean National Health Insurance Fund alisema kutokana na wingi wa vifo vitokanavyo na saratani, lazima kuwe najitihada shirikishi zakupigana na saratani ya matiti.

  Kuhamasisha njia bora za afya kwenye matukio kama haya imekuwa ni wajibu mkuu kwa hospitali za Apollo ambazo zimetunukiwa tuzo za kimataifa.

  Katika kuhamasisha na kutoa elimu kuhusu maada hii, mkurugenzi wa hospitali za Apollo, Suneeta Reddy, amesema kwa miaka sasa,saratani ya matiti imedhihirika kuwa moja ya janga kubwa kwa wanawake wote ulimwenguni. Ni muhimu kwa wanawake wote kujali afya zao maana wanamajukumu makubwa sio tu kwenye familia ila pia kwenye jamii kwa ujumla. Wajibu wa mwanamke mara zote haupo tumuhimu kwenye maisha ya familia ila pia kwenye nyanja za jamii na uchumi hasa kwa nchi zinazoendelea.

  Ukosefu wa elimu na hamasa umesababisha wimbi kubwa la wanawake kukosa fursa ya kugundua mengi kuhusu saratani ya matiti. Njia pekee ya kufanya hayo ni kupata elimu sahihi na uelewa wa kina kuhusu nini ni saratani ya matiti. 

  Elimu yakutosha inatakiwa itolewe kwa jamii kusaidia kupunguza zigo la ugonjwa huu. Saratani ya matiti kama isipogundulika mapema itapelekea kifo moja moja. Alisema Suneeta Reddy, mkurugenzi wa hospitaliza Apollo.
  Hebu tuanze kufanya kitu sasa hivi. Chagua njia ya ugunduzi, jifanyie uchunguzi mwenyewe wa saratani ya matiti au kwa kutumia kifaa kijulikanacho kitaalamu kama mammogram hiki ni chombo madhubuti kitakacho saidia kugundua ugonjwa katika ngazi ya awali kabisa, alisema mkurugenzi Suneeta Reddy.

  Ugunduzi wa saratani ya matiti mapema kwa kutumia kifaa cha mammography kumepunguza vifo vingi kwa wanawake ambao walionekana hawana dalili zozote waliokuwa na uvimbe na waliokuwa hawana uvimbe kwaile ngazi ya kwanza.

  Mkg.SuneetaReddy anawataka watanzania wote tuheshimu na tutenge dakika tano tu za kujifanyia uchunguzi, alisema.

  Kwa kushirikiana na wito wa Mkg. Suneeta Reddy kuhusu ugunduzi wa saratani ya matiti katika ngazi ya awali, mkuu wa idara ya mionzi katika taasisiya Ocean Road, Dk. Yekebeth Vuhahula, aliongeza kuwa saratani ya matiti bado ni changamoto kubwa Tanzania kwasababu wanawake wengi wanashindwa kujitokeza mapema kwa matibabu. Kwa jinsi ambavyo saratani ya matiti inazidi kukomaa na kusambaa, ndivyo inasababisha nafasi ndogo ya matitabu kufanya kazi. Kama saratani ya matiti ikigundulika mapema inatibika kirahisi.

  Kwa ujuzi wake kuhusu wagonjwa wa saratani ya matiti Tanzania, wanawake wa Tanzania wanaoufahamu mdogo na wengine hawana ufahamu kabisa kuhusiana na vitu hatarishi, dalili, na matibabu ya saratani ya matiti. Imani potofu kutoka kwenye jamii na tamaduni ni sababu nyingine zinazopelekea saratani ya matiti kuwa sugu kwa wanawake hapa nchini.

  Kuhusu Hospitaliya Apollo
  Hospitaliza Apollo ni za kwanza katika eneo la Asia Pacific kutoa huduma za upasuaji kwa kutumia mfumo huu wa Robot, ambayo ni aina ya upasuaji isiyo kuwa na madhara. Taasisi ya upasuaji kutumia Robot iliyopo hospitalini hapo wamejitoa kipekee katika kutoa huduma bora kwa wagonjwa.

  Taasisi inawataalamu waliobobea kwenye mafunzo ya upasuaji, upendo katika utoaji wa huduma vifaa vya matibabu vya kisasa vinavyolenga kutoa uzoefu bora kwa mgonjwa. Vifaa hivyo ni pamoja na vifaa Robot ya Da Vinci inayotumika katika upasuaji.

  Mfumo huu wa upasuaji hutumika katika teknolojia ya upasuaji wa magonjwa yanayohusiana na mfumo wa mkojo (Urology), magonjwa ya wanawake (Gynaecology), moyo, utumbo, na magonjwa ya watoto na matatizo ya uti wa mgongo.

  0 0

  22332492835_c6540fb80e_z

  Zanzibar’s child rights law is the winner of the 2015 Future Policy Award on securing children’s rights, beating 29 other nominated policies to the prize. The Award will be presented at a ceremony in Geneva today by the World Future Council, the Inter-Parliamentary Union (IPU) and UNICEF during the 133rd IPU Assembly.

  The “Children’s Act” is an outstanding piece of legislation. It earned the 2015 Award for its balanced coverage of child abuse and violence against children and for its promotion of child rights – two important topics for children worldwide. Since the enactment of the law Zanzibar has seen favourable and significant shift of social attitudes towards children.

  The Act lays the foundation for the establishment of a comprehensive national child protection system to deal with cases of children in need of care and protection and already notable achievements have been recorded in its operationalization. These include the establishment of district child protection committees, the establishment of Children’s Courts, the designation of Police Gender and Children’s Desks in every Police Station in Zanzibar and the roll out of training to social welfare and frontline justice professionals. 

  An exciting feature of this legislation was the child consultation process which provides young people with an understanding of the law and their rights. It gave children a voice in the development of the legislation and resulted in the establishment of over 200 Children’s Councils in the Isles.
  21711616543_42e3d29f57_z
  On learning about the Gold prize, Asha Abdullah, Principal Secretary of the Zanzibar Ministry of Empowerment, Social, Welfare, Youth, Women and Children said: “This is a great honour. The Award will not only raise global awareness of our model of child rights legislation, but also enhance our commitment to its implementation in Zanzibar.”


  UNICEF in Tanzania played a key role in providing the Government of Zanzibar with technical and financial support in the development of the Act and continues to provide assistance, with support from the European Union, in working towards bringing the legislation from paper to practice. Dr. Jama Gulaid, UNICEF Tanzania Country Representative congratulated the Government of Zanzibar on receiving the Future Policy Award 2015 and noted: 

  ‘Hongera Sana, Zanzibar! UNICEF commends the Government and people of Zanzibar for the broad consultation on the Act which heightened public awareness of children’s rights. Child protection is drawing attention from decision makers, media and communities in Zanzibar’.
  Birgithe Lund-Henriksen, Chief of Child Protection for UNICEF in Tanzania, added: 

  ‘We are delighted to continue to support the roll out of the Children’s Act 2011 in order to make a meaningful impact on the lives of children in Zanzibar. We are particularly encouraged by the steps that already have already been taken towards implementation and the real ownership the frontline child protection professionals have demonstrated over the new legislation in working to protect children in Zanzibar’.
  22145738849_4866c4b32b_z
  Jakob von Uexkull, Founder and Chair of the World Future Council, said: “This prize celebrates policies that help us to do the right thing by creating the right rules. Children are among the most vulnerable group facing a host of the world’s emerging challenges. We need more laws that support a just world and protect the rights of future generations.” 

  IPU Secretary General Martin Chungong said: Parliaments can lead the response against child abuse and violence by ensuring international commitments on children’s rights are adhered to nationally through laws that are effectively implemented and monitored. The winning policies can only inspire parliaments and parliamentarians everywhere on concrete action to take. ”

  UNICEF Executive Director Anthony Lake commended the recognition bestowed by the awards: “Children’s rights are brought to life not through pronouncements, but through practical action. Parliamentarians are among UNICEF’s most important partners in driving that action and the results it can achieve in children’s lives. We applaud the World Future Council for spurring more parliamentarians to leverage their powers on behalf of the world’s most disadvantaged and vulnerable children.”

  The Future Policy Award is the only award which honours policies rather than people on an international level. The World Future Council will now work to globally raise awareness of the winning model policies and assist policy-makers to develop and implement similar initiatives.

older | 1 | .... | 669 | 670 | (Page 671) | 672 | 673 | .... | 1897 | newer