Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live

MSHAURI WA CHAMA CHA DUNIA CHA MCHEZO WA MPIRA WA KIKAPU AKUTANA NA UONGOZI WA SEKTA YA MICHEZO NCHINI

0
0
 Mkurugenzi Idara ya Michezo Bw. Leonard Thadeo (kulia) akizungumza na  Mshauri wa Chama cha Dunia cha Mchezo wa Mpira wa Kikapu (FIBA) Bw. Lubomir Kotleba (kushoto) alipofika nchini Tanzania kufuatilia maendeleo ya mchezo huo jana Jijini Dar es Salaam.
 Mshauri wa Chama cha Dunia cha Mchezo wa Mpira wa Kikapu (FIBA) Bw. Lubomir Kotleba (kulia) akizungumza na maafisa Michezo kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (hawapo pichani) alipofika nchini Tanzania kufuatilia maendeleo ya mchezo huo nchini. Kushoto ni rais wa Mpira wa Kikapu Tanzania Mhandisi John Bandiye.
 Katibu Mtendaji Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Henry Lihaya akizungumza wakati Uongozi wa Idara ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ulipokutana na Mshauri wa Chama cha Dunia cha Mchezo wa Mpira wa Kikapu (FIBA) kujadili masuala mbalimbali ya mchezo huo Jijini Dar es Salaam.

 Maafisa Michezo kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakifuatilia kwa makini majadiliano yaliyokua yakiendelea kati ya uongozi wa Idara ya Michezo pamoja na Mshauri wa Chama cha Dunia cha Mchezo wa Mpira wa Kikapu (FIBA) jana Jijini Dar es Salaam.
Picha na: Genofeva Matemu - Maelezo

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AMNADI MBUNGE WA MUFINDI KASKAZINI MOHAMED MGIMWA

0
0




 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. MOhammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Jimbo la Mufindi Kaskazini, mkoani Iringa wakati wa mkutano wa Kampeni za mgombea Ubunge wa jimbo hilo, Mohamed Mgimwa, uliofanyika juzi Okt 17.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Viongozi wa Jimbo la Mufindi Kaskazini, Mkoani Iringa wakati alipowasili Jimboni hapo juzi Okt 17, 2015 kwaajili ya kumnadi mgombea Ubunge wa Jimbo hilo, Mohamed Mgimwa.


 Baadhi ya Vijana wa CCM wa Jimbo la Mufindi Kaskazini, wakiruka na kucheza staili ya mgombea Urais kupitia CCM, John Magufuli, wakati wa mkutano wa kampeni za mgombea Ubunge wa jimbo hilo, Mohamed Mgimwa, zilizofanyika mwishoni mwa wiki, jimboni hapo
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini, Mohamed Mgimwa, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika mwishoni mwa wiki jimboni humo
  Sehemu ya WanaCCM, waliojitokeza katika mkutano huo, wakimshangilia mgombea wao MOhamed Mgimwa wakati akitambulishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya MUungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mufundi Kaskazini, baada ya kumalizika kwa mkutano wa kampeni wa mgombea Ubunge wa Jimbo hilo, Mohamed Mgimwa. Picha na OMR

KITABU KILICHOTUNGWA NA MTOTO WA KITANZANIA CHANG"ARA KIMATAIFA

0
0
MTOTO wa Kitanzania mwenye miaka 14 ametunga kitabu ambacho kimetambulika kimataifa. Kitabu hicho ni cha hadithi kinachoitwa ''LUCIANA AND THE SEVEN MAGICAL RINGS'' ambacho kimepigwa chapa na kampuni ya Kimarekani inayoitwa KIDPUB PRESS ya mjini Boston. Kinasambazwa pia na kampuni za Marekani za Amazon na Bookstore.

Mtunzi wa kitabu hiki ni Redempta Rugeiyamu ambaye kwa sasa anaishi nchini Afrika Kusini ambaye alizaliwa nchini Botswana walikokuwa wakiishi wazazi wake akiwa na ugonjwa unaoitwa Cerebral Palsy. 

Amekuwa akiishi na ugonjwa huo tangu alipozaliwa miaka 14 iliyopita. Japokuwa ugonjwa huo umeathiri viungo vyake na kumpa taabu ya kutembea na kuongea lakini haukumzuia ndoto yake ya kuandika vitabu, kuimba na kucheza muziki.

Kitabu hicho kilizinduliwa mjini Gaborone na Mwenyekiti wa Chama Cha Watanzania waishio Botswana, Bw. Nieman Kissasi, siku ya jumamosi usiku. Mgeni rasmi kwenye shuhuli hiyo alikuwa ni Balozi wa Tanzania nchini Arika Kusini ambaye aliwakilishwa na Afisa wa Ubalozi, Bw. Elibahati Lowassa.
 Mwenyekiti wa Watanzania Waishio Botswana, Bwana Nieman Kissasi, akizindua rasmi kitabu hicho mjini Gaborone siku ya jumamosi usiku kwenye mkutano mkuu wa Chama hicho. Wengine pichani ni wazazi wa Redempta, Bw. Theo Rugeiyamu na Celina Rugeiyamu.

WITO WATOLEWA NA MISS TANZANIA 2013/2014 KWA WAKINA MAMA KUJITOKEZA KUFANYA UCHUNGUZI WA SARATANI YA KIZAZI

0
0
 Miss Tanzania 2013/2014 ,Happiness Watimanywa ambaye ni Balozi wa Saratani ya mlango wa kizazi kupia hospitali ya Marie Stopes( kushoto) na  Meneja wa Masoko wa hospitali hiyo Lilian Charles wakiingia kwenye uwanja wa taifa kutoa elimu kuhusiana na ugonjwa wa kansa ya kizazi wakati wa mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kati ya Yanga na Azam, ikiwa nisehemu ya kampeni ya kuhamasisha akinamama kwenda kufanya uchunguzi wa saratani ya Kizazi kwanye vituo mbalimbali vya afya ikiwemo Marie Stopes.Ambapo timu hizo zilitoka sare ya 1-1.
 Balozi wa Saratani ya mlango wa kizazi kupitia hospitali ya Marie Stopes,Miss Tanzania 2013 /2014,Happiness Watimanywa(kushoto)akifafanua jambo kwa  Ofisa wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude(katikati) na Menaja masoko wa hospitali hiyo Lilian Charles(kulia)Kuhusiana na kampeni ya kuwahamasisha wakina mama kufanya uchunguzi wa saratani ya shingo na kizazi katika vituo mbalimbali vya afya. Uhamasishaji huo ulifanyika kwenye uwanja wa Taifa  jijini Dar es Salaa wakati wa mechi ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kati ya Yanga na Azam ambapo timu hizo zilitoka sare ya 1-1.
 Miss Tanzania 2013/2014 ,Happiness Watimanywa,Ambaye ni Balozi wa Saratani ya kizazi kupitia hospitali ya Marie Stopes(watano toka kushoto)akiwa na maofisa wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF pamoja na Ofisa Udhamini na Matukio wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude(wa kwanza kulia) wakihamasisha kwa wakina mama kujitokeza kwenda kupima saratani ya kizazi katika vituo mbalimbali vya afya wakati wa mechi kati ya Azam FC na Yanga iliyochezwa mwishoni mwa wiki kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo timu hizo zilitoka sare ya 1-1.
Wachezaji wa timu ya Azam FC na Yanga sports Club wakichuna vikali wakati wa mechi yao ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara iliyopigwa mwishoni mwa wiki ambapo timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.Kabla ya kuanza kwa mchezo huo Balozi wa Saratani ya mlango wa kizazi kupitia hospitali ya Marie Stopes,Miss Tanzania 2013 /2014,Happiness Watimanywa(hayupo pichani)alitumia frusa hiyo ya kuwahamasisha wakina mama kufanya uchunguzi wa saratani ya shingo na kizazi katika vituo mbalimbali vya afya.

BALOZI WA SWETZERLAND AMTEMBELEA RAIS WA ZANZIBAR

0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi wa Switzerland katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi.Florence Tinguely Mattli  wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza  na Balozi wa Switzerland katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi.Florence Tinguely Mattli wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
[Picha na ikulu.]

UNDP YASISITIZA VITA YA UMASKINI KWA KUTUMIA MAZINGIRA

0
0
IMG_6436
Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) Tanzania, (Ushauri na Miradi), Amon Manyama akitoa maelezo kuhusu mradi wa PEI na salamu kutoka UNDP kwa washiriki wa mafunzo hayo hivi karibuni jijini Mwanza.

Na Mwandishi Wetu, Mwanza
MKURUGENZI Msaidizi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Amon Manyama, alisema vita dhidi ya umaskini inakuwa na maana kubwa kama inalinganishwa na mazingira.

Alisema kwamba umaskini wa kipato ambao umekuwa ukipiganwa sana kwa sasa unastahili kupiganwa kwa kuangalia umaskini kutokana na ukweli kuwa kuboreshwa kwa mazingira ndio hatua kubwa ya kupigana na umaskini katika sura zote zilizobaki.

Mkurugenzi msaidizi huyo alisema hayo hivi karibuni mjini Mwanza wakati akielezea mradi wa mtaji na elimu wa UNDP ambao umefanyiwa kazi kwa pamoja kati ya shirika hilo, Tume ya Mipango, Hazina na Ofisi ya Makamu wa Rais, katika mafunzo ya siku moja ya Uimarishaji wa Ushirika wa Akiba na Mikopo, yaliyofanyika Mwanza.

Mradi huo umelenga kuwezesha ushirika wa akiba na mikopo katika wilaya sita nchini kuwezesha wananchi kushiriki katika kukabili umaskini unaosababishwa na mazingira.

Akifafanua alisema kwamba inawezekana muda wa kusubiri kuvuna samaki ziwani umekwisha kwa hiyo kinachotakiwa kufanyika ni kupanda samaki ndani au nje ya ziwa na watu waweze kutumia nafasi hiyo kuboresha maisha yao.
IMG_6389
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi Kida akitoa maelezo ya utangulizi juu ya madhumuni ya mafunzo hayo kwa washiriki kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua rasmi.

Alisema hali hiyo pia ipo katika misitu. Wakati watu wanakata misitu unawapa elimu na mtaji wa kupanda misitu mingine na hivyo mazingira yakaendelea kubaki na kuwa mtaji wa kukabili umaskini.

Mradi huo ambao upo katika wilaya sita kwa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2021 na ifikapo muda huo utakuwaupo wilaya 21 na kutumika kama kichochea cha utekelezaji wa malengo 17 ya maendeleo endelevu yenye nia ya kupiga vita umaskini, kuondoa ubaguzi na njaa.

Alisema mafunzo yaliyotolewa katika kongamano la viongozi mbalimbali wa vyama vya ushirika vya aina mbalimbali mjini Mwanza kwa msaada wa UNDP na kutekelezwa na Taasisi ya utafiti wa masuala ya kiuchumi na kijamii (ESRF) yamelenga kuwezesha SACCOS kutambua fursa hizo za mazingira kukabili umaskini.


Alisema katika mazingira ya sasa wanawake ndio wanaathirika zaidi katika umaskini kutokana na wao kuwa wazazlishaji na wahudumiaji wa kaya na kwamba kama kutakuwepo na mabadiliko na mazingira yakatengeneza fursa ya kupiga vita umasikini wanawake wataendelea kustawi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya utafiti wa masuala ya kiuchumi na kijamii (ESRF) ESRF Dk. Tausi Kida alisema lengo la mafunzo hayo ni kuimarisha ushirika wa akiba na mikopo mkoani Mwanza.

Akizungumzia historia ya mradi alisema wao kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) pamoja Tume ya mipango, walianza kutekeleza mradi wa kukuza uchumi, kuleta maendeleo endelevu kupitia utunzaji mazingira, usawa wa kijinsia na kupunguza na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi yaani (PEI) toka mwaka 2014.
IMG_6182
Pichani juu na chini ni baadhi ya Viongozi wa Vyama vya Ushirika (SACCOS na VICOBA) na Maafisa Ushirika wa kutoka Wilaya za Bunda, Bukoba na Sengerema wakifuatilia kwa umakini mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa.

Alisema tafiti mbili chini ya mradi wa PEI zilizofanyika katika wilaya za Bunda, Ileje, Sengerema, Bukoba vijijini, Ikungi na Nyasa kubaini changamoto na fursa zinazopatikana katika wilaya hizo.

Alisema matokeo ya tafiti yalionyesha umuhimu wa kuzipa uwezo taasisi za kifedha kama SACCOSS, VICOBA na vikundi mbalimbali vya kifedha kwa kuzijengea uwezo wa kitaaluma na kifedha.

Alisema hata hivyo pamoja na matokeo hayo Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) ilitenga na kutoa fungu la fedha na kuipatia benki ya Twiga ili kukopesha kwa riba nafuu kwenye taasisi kama SACCOSS na VICOBA kwa lengo kuu kuweza kuwafikia wananchi wengi zaidi ili waweze kupata fursa ya kukuza mitaji yao na kuwafanya muweze kutekeleza fursa hizi katika maeneo yao.

MAGUFULI AKIENDELEA NA MIKUTANO YAKE YA KAMPENI MCHANA HUU SENGEREMA NA GEITA VIJIJINI

0
0

  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasikiliza wananchi wa jimbo la Buchosa mapema walipokuwa wakishamgilia mara baada ya kupanda jukwaani na kuwasalimia,mkutano huo wa kampeni umefanyika mapema leo asubuhi katika kijiji cha Nyehunge wilayani Sengerema mkoani Mwanza.Pamoja na mvua kunyesha hapa hapa na pale katika maeneo hayo,Dkt Magufuli anatarajia kuhutubia mkutano mkubwa wa kampeni katika jimbo la Geita Vijjini katika kijiji cha Nkome.
  Wakazi wa jimbo la Buchosa wakishangilia jambo wakati Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi mbele yao kuomba kura za kutosha ifikapo Oktoba 25 kwenye uchaguzi mkuu
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa jimbo la Buchosa mapema leo asubuhi katika kijiji cha Nyehunge wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
 Wakazi wa jimbo la Buchosa wakishangilia jambo wakati Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi mbele yao kuomba kura za kutosha ifikapo Oktoba 25 kwenye uchaguzi mkuu
Wakazi wa jimbo la Buchosa wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli uliofanyika mapema leo asubuhi kijiji cha Nyehunge wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli akimnadi Mgmbea Ubunge jimbo la Buchosa,Dkt Charles Tizeba mapema leo asubuhi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Nyehunge wilayani Sengerema mkoani Mwanza
 Magufuli akiwasili kwenye mkutano wa kampeni,Nyehunge jimbo la Buchosa mapema leo mchana huku akishangiliwa .
 Dkt Magufuli akiwasalimia wananchi wa Nyehunge jimbo la Buchoasa kwenye kutano wa kampeni wilayani Sengerema.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Kamanga mapema leo asubuhi aliposhuka akitokea mkoani Mwanza kuelekea wilayani Sengerema kuendelea na Mikutano yake ya kampeni
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa kijiji cha Lwezera mara baada ya kupokelewa na viongozi mbalimali wa chama cha CCM mkoa wa Geita,akielekea jimbo la Geita Vijijini kuhutubia wananchi kwenye kutano wa kampeni
 Wanamsikiliza Mgombea Urais wa CCM alipokuwa akimwaga sera zake kwa wakazi wa kijiji cha Lwezera,Geita vijijini

20 WACHAGULIWA KUSHIRIKI KATIKA SHINDANO LA BONGO STYLE COMPETITION.

0
0
 
Kipande cha Video ya mahojiano.
 Majaji kwa Upande wa wabunifu wa Mitindo-Mavazi na Upigaji wa Picha wakiwa wanaendelea na kazi za uhakiki wa Majina ya kuwapata washiriki 20 ambao wataingia katika Shindano hilo.
Mbunifu na Mwanamitindo wa Mavazi ambaye pia ni Balozi wa Fasdo Martin kadinda akiongea kwa niaba ya Majaji upande Majaji wa Mitindo akielezea jinsi mchakato ulivyo kwenda.
 Majaji upande Ubunifu wa Mavazi wakiwa wanaendelea na kazi 
 Jaji katika upande wa kupiga Picha Sameer Kermalli akizungumzia mchakato mzima walioufanya kuwapata washiriki ambao wataingia katika shindano kwa upande wa upigaji picha.

Majaji upande wa kupiga picha wakiendelea na Mchakato wa kuwapata washiriki 10 ambao wataingia katika ushiriki wa kumpata mshindi wa upande wa kupiga picha.
Mratibu wa FASDO Tanzania Joyce Msigwa akizungumzia mchakato mzima wa shindano la Bongo style Competition 
Kulia ni Philipo Florian kutoka kitengo ya Mitandao ya Kijamii Fasdo akiendelea na Kazi.

Kuelekea Shindano la Bongo Style  Competition , Ambalo linatarajiwa kufanyika Mwishoni mwa mwezi wa Kumi na moja mwaka huu, Majaji wamefanikiwa kuwapata washiriki ambao wataingia katika Kinyang'anyiro hicho

Akizungumzia Shindano hilo Mratibu wa FASDO Tanzania Joyce Msigwa alisema shindano hilo linalengo la kuibua vipaji vya vijana wenye kati ya umri wa miaka 18-25 katika nyanja za ubunifu mitindo na upigaji picha ili kuwahamasisha kutumia vipaji vyao kujiajili wenyewe. Aliongeza kuwa idadi ya Fomu zilizotumwa kwa njia ya mtandao zilikuwa 310 kati ya hizo zilizo pitiwa na Majaji pande zote ili kupata washiriki 20 zilikuwa fomu 285.

Aliwataja waliopita kushiriki katika upande wa picha ni pamoja na hao kwa upande wa  ni pamoja na Daniel Msirikale, Anneth Mgowano, Travis Gaudence, Victor Mpalile,Ebenezer Mmasi, Hassan Mohammed Ally, Rasheed Hamis, Erick Mwan'gonda, Nicetas Mtey na Nicetas Mtey

kwa upande wa Ubunifu wa mavazi na mitindo aliwataja washiriki hao ni pamoja na Anna Ben Paul,Eva Mary Sospeter,  Jocktan mwakeke
Lilian Ndanshau, Cecilia lyakulwa,Milly's Fenary Collection,Mamaland,Shahbaaz Sayed Yusuf,Salome Sebastian, na  Andrew Kalema

Nae Jaji wa Eneo la Mitindo Ambaye pia ni Balozi wa FASDO Martin Kadinda alizungumzia shindano hilo kuwa ni zuri na lipo kwa ajili ya kuibua vipaji vipya vya wanamitindo na kuongeza pia wale wote walioshiriki katika Shindano hili hasa walioleta fomu zao walikuwa wanauwezo lakini kwa kuwa ni shindano wachache ndio walikuwa wanatakiwa kulingana na vigezo na Masharti walivyoweka.

Akiongezea Jaji upande wa Picha Sameer Kermalli kwa niaba ya majaji wengine  amesema kuwa wamepokea na kupitia picha za washiriki wengi walioleta picha wamepitia na kugundua baadhi yao wamepiga picha nzuri ambazo zipo kitaalam na wengine wamepiga picha ka kuzi 'edit' sana jambo ambalo limesababisha kupunguza alama zao na pia wengine wametumia picha ambazo sio zao, pia aliongeza kwa kusema baadhi yao ambao wamechukuliwa pia wamefanya vizuri kutokana na ubunifu wao. 

Philipo Florian ambao wapo katika mitandao ya kijamii na waliokuwa wakipokea fomu hizo alisema kuwa fomu fomu nyingi zilikuja kwa kurudiwa rudiwa kitu ambacho kilichanganya kidogo mchanganuo, pia watu wengi  walipaa shida wakati wa kuweka Picha lakini hata hivyo wengi walifanikiwa na kushiriki kikamilifu. Pia Anna Semiono aliongeza kuwa zoezi lilienda kikamilifu na idadi ya wanawake na wanaume ambao walileta fomu zilikuwa sahihi ingawa baadhi yao walikosea kwa namna moja au nyengine kutokana na kuto elewa vizuri ni namna gani wangeweza wasilisha kazi zao, hata hivyo alisema changamoto hiyo haitakuwepo katika shindano lijalo kwa kuwa kutakuwa kuna elimu mbadala kupitia VIDEO CLIP itakayo onesha namna ya kutuma kazi zao.

BEI YA MADAFU HII LEO

0
0

PAPA WEMBA KUTUMBUIZA TAMASHA LA KARIBU MUSIC FESTIVAL NOVEMBA 6-8 MWAKA HUU

0
0
 Ofisa Mauzo wa Karibu Cultural Promotions Organization (KCPO), Ernest Biseko katikati  ambao ni waratibu wa Tamasha la Karibu Music Festival akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. kushoto ni  ni msanii, Jhikolabwino Manyika - Jhikoman na Meneja Uvumbuzi wa kinywaji cha Jebel cha Kampuni ya SBL, Attu Mynah
 Msanii Jhikolabwino Manyika - Jhikoman   wasanii wa Tamasha la Karibu Music Festival walivyojiandaa na  akionesha umahiri wake wa kupiga gitaa mbele ya waandishi wa habari  leo jijini dar es saalam
 Baadhi ya waandishi wa  habari
Jhikolabwino Manyika - Jhikoman (kulia) akionesha ufundi wake wa kuimba na gitaa kwa wanahabari leo baada ya mkutano.
Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.

MWANAMUZIKI nguli wa dansi kutoka nchini Congo DR, Papa Wemba ni miongoni mwa wasanii wanaotarajia kutumbuiza katika tamasha kubwa la Kimataifa la Muziki la 'Karibu Music Festival' linaloratibiwa na Karibu Cultural Promotions Organization (KCPO) na Legendary Music Entertainment and Promotions Co. Ltd. 

 Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Ofisa Mauzo wa KCPO, Ernest Biseko alisema wanamuziki wengine na bendi zinazotarajia kutumbuiza katika tamasha hilo ni pamoja na Sarabi Band, H-Art The Band, Yuzzo & Frontline Band. 

Alisema wasanii kutoka Tanzania watakaotumbuiza ni pamoja na Jhiko Manyika (Jhikoman) na band yake ya Afrikabisa, Tomgwa Ensembe, Misoji Nkwambi mshindi wa BSS 2008, Ze Spirit. 

Isha Mashauzi, Damian Soul na babd yake, Juma Nature, Msafiri Zawose na band yake. Akifafanua zaidi Biseko alisema tamasha hilo la mwaka huu lenye kauli mbiu ‘Fahari ya Tanzania’ litafanyika kwa siku tatu mfululizo kuanzia Novemba 6 hadi 8 mwaka huu katika viwanja vya Mwanakalenge karibu na Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA). ".

Tamasha hili linalenga kukuza muziki wa Kiafrika na kuonesha tamaduni za Kiafrika kwa dunia nzima kupitia jukwaa la muziki litakalokutanisha wanamuziki kutoka sehemu mbalimbali duniani," alisema Biseko.

 Aidha alibainisha kuwa tamasha hilo ni sehemu ya kukutanisha wadau wote wa muziki kutoka dunia nzima, kubadilishana uzoefu wa kikazi na kufungua milango kwa wasanii kukuza mtandao wa marafiki na kujifunza vitu vipya toka wasanii wa je ya Nchi. Aliongeza kuwa wanamuziki wote watakaopanda jukwaani siku zote tatu za tamasha watatumbuzia na vyombo vyao 'live' na hakutakua na kutumia CD (playback). 

SERIKALI YATAKIWA KUKABILIANA NA VIASHIRIA VYA UVUNJIFU WA AMANI

0
0
Na Woinde Shizza,Arusha
Kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Octoba 25 mwaka huu Serikali imetakiwa kukabiliana na viashiria vya uvunjifu wa amani na kuvipatia ufumbuzi ili kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki utakaodumisha amani ya taifa.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Amani ya Apet Jijini Arusha Peter Aham  katika mjadala wa masuala ya amani hasa katika kipindi cha uchaguzi ulioudhuriwa na Wawakilishi kutoka tume ya uchaguzi,Jeshi la Polisi,Vyama vya Siasa pamoja na wadau wa amani.

Peter Ahham amesema kumekua na dalili za wazi za baadhi ya mamlaka kuonekana kuegemea upande mmoja ikiwemo Tume ya Uchaguzi,Jeshi la Polisi na baadhi ya Vyombo vya habari jambo ambalo linapingana na taaluma na weledi  na linaweza kuathiri amani.

Mkuu wa wilaya ya Arusha Fadhili Nkulu amesema kuwa kwa muda mrefu amani iliyodumu nchini imekua ikihatarishwa na masuala ya udini,ukabila na itikadi za kisiasa hivyo kila mtanzania anajukumu la kulinda amani katika kipindi hiki cha uchaguzi

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika lisilokua la Kiserikali la USIP ,Dr.James Jesse pamoja na Kamishna wa Polisi mkoa wa Arusha  Edward Balele amesema kuwa kila mtanzania,vyama vya siasa vinawajibu wa kulinda amani na kuhakikisha kuwa uchaguzi unakua huru na salama

Siku chache zimesalia kufikia Octoba 25 ambapo uchaguzi mkuu wa kitaifa unatarajia kufanyika ambapo Watanzania watapata viong ozi wapya kuanzia ngazi ya Urais ,Ubunge na Udiwani huku suala kubwa linalogonga vichwa vya watu wengi ni juu ya uwepo wa haki na amani katika uchaguzi huo.

teknolojia ya mikutano kwa njia ya video na picha za video conference yafanyika dar es salaam

0
0
unnamedBBBBMkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) Bw. Charles Y. Senkondo (kulia)  akifafanua jambo kwa  Waandishi wa Habari namna ofisi yake inavyoratibu uendeshaji wa mikutano kwa njia ya video (Video Conference). Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais – Utumishi Bw. Florence Temba.
unnamedBBBMkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) Bw. Charles Y. Senkondo (kulia),  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais – Utumishi Bw. Florence Temba (katikati) na Mratibu wa Mafunzo wa TaGLA Bw. Dickson Mwanyika (kushoto) wakishiriki mkutano kwa njia ya video (Video Conference) uliofanyika kwa kushirikiana na Kenya School of Government. Wengine ni Waandishi wa Habari kutoka katika Vyombo mbalimbali vya habari nchin.
……………………………………………………………………………..
Na Anitha Jonas – MAELEZO. Dar es Salaam.
Serikali imewasihi watanzania kutumia huduma ya mafunzo kwa njia ya mtandao kwani inapunguza gharama  na kurahisisha upatikanaji wa majibu ya haraka.
 
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji,Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao(TaGLaA) Bw.Charles Senkondo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Oktoba 19, 2015  jijini Dar es Salaam kuhusu mafanikio ya taasisi hiyo pamoja na kuanzishwa kwa maktaba ya kisasa za maendeleo ikishirikiana na wadau mbali mbali ndani na nje ya nchi.
 
“Wakala imefanikiwa kushirikiana na Ofisi ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa kutumia mitandao ya kiteknolojia na  imeweza kufundisha mfumo wa malipo ya mishahara kwa watumishi wa serikalini watendaji wakuu kutoka taasisi za serikali,  wakurugenzi wa halmashauri  za wilaya pamoja na wakurugenzi wa rasilimali watu wapatao 1,200,”alisema Bw.Senkondo.
 
Hata hivyo Bw.Senkondo alisema gharama za kutumia huduma hizi za mafunzo ya mtandao kupitia video ni shillingi 400,000/= kwa saa moja na mikutano hii inaweza kufanyika hata kwa kuwaunganisha watu wa mikoani moja kwa moja na nchi za kimataifa.
 
Mkurugenzi huyo aliendelea kusema wakala  imefanikiwa kuendesha kesi za mahakama kwa kutumia huduma ya mahojiano ya video kwa watu kuweza kutoa ushahidi kwa njia ya video na kusaidia kupunguza gharama pamoja na huhamasiha maamuzi.
 
Aidha Mkurugenzi Mtendaji huyo alieleza changamoto mbalimbali zinazoikumba taasisi hiyo ikiwemo ufinyu wa nafasi za  ofisi  na kufafanua kuwa kuna jitihada za kupata eneo la kujenga ofisi zitakazo kidhi mahitaji ya wakala.
 
Jumla ya washiriki 20,322 wamepata mafunzo kutokana na midahalo iliyofanyika pamoja na mafunzo 783 ya kubadilishana maarifa yaliyoendeshwa kupitia wakala katika kipindi cha mwaka 2005 mpaka 2015.

MAZISHI YA DK.EMMANUEL MAKAIDI KUFANYIKA MAKABURI YA SINZA, MWILI WAKE KUAGWA KESHO ASUBUHI VIWANJA VYA KARIMJEE JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
Mjane wa aliyekuwa Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Dk. Emmanuel Makaidi, Modesta Ponela Makaidi akiwa katika huzuni baada ya kuondokewa na mpendwa wake.
Mtoto wa kwanza wa Dk. Makaidi, Hilda Emmanuel Makaidi akizungumza na wanahabari (hawapo pichani)
Mtoto wa marehemu Mhandisi Emmanueli Makaidi (kulia), akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ratiba ya mazishi ya baba yake.
Ndugu, jamaa, marafiki na waombolezaji wakiwa msibani nyumbani kwa Dk.Makaidi Sinza.
Mjane wa aliyekuwa Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Dk. Emmanuel Makaidi, Modesta Ponela Makaidi (kulia), akiwa na waombolezaji wengine nyumbani kwake Sinza Vertican Dar es Salaam kesho asubuhi.

Na Dotto Mwaibale

MWILI wa Mwenyekiti Mwenza wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) Dk. Emmanueli Makaidi unatarajiwa kuagwa kesho katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, mtoto wa marehemu Mhandisi Emmanueli Makaidi alisema mwili huo baada ya kutoka Masasi ulipelekwa Hospitali ya Jeshi ya Lugalo na leo jioni utapelekwa nyumbani kwa marehemu maeneo ya Sinza Vertican ambapo itafanyika ibada fupi na kupata fursa ya ndugu na majirani kuuaga.

Alisema kesho mwili huo utaagwa katika viwanja vya Karimjee ambapo viongozi mbalimbali wa kisiasa, serikali watakuwepo na kisha kufanyika mazishi yake katika makaburi ya Sinza. 


"Unajua baba alikuwa ni mwanasiasa na amefariki akiwa bado ni mwanasiasa hivyo ni lazima uweze kuagwa na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa na serikali" alisema.

Akimzungumzia baba yake alisema marehemu alikuwa ni mtu ambaye anapenda utu ambapo alipenda kila binadamu ni sawa na hapaswi kubaguliwa.

Alisema wameamaua kumzika baba yao Dar es Salaam na si Mtwara kutokana na mke na mama yake kuzikwa Dar es Salaamna ndio utaratibu waliouweka wa kuzikwa.

"Baba alitaka kila mtu ambaye atafariki ni vyema akazikiwa hapo kwani hata wakati wa kulimia makaburi inakuwa rahisi,"alisema.

Kwa upande wake mtoto wa pili wa Marehemu Hilda Makaidi alisema baba yao alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo kwa muda mrefu.

"Nakumbuka nilimpigia baba simu akiniambia mwanangu Hilda Masasi kugumu, na mimi nikamwambia baba rudi nyumbani tukutibu lakini hakukubali haraka,"alisema.

Alisema baba ameacha mjane na watoto 10 huku ikiwa wakike wakiwa wanne na wakiume sita na wajukuu 10 na vitukuu sita.

Kwa upande wake Katibu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi George Kahangwa alisema mazishi hayo yatahuduliwa na mgombea urais wa umoja huo Edward Lowassa  pamoja na viongozi wa taifa wa serikali na vyama vya siasa na vyama vya michezo.

"Sote tushiriki kumpa heshima za mwisho na kumsindikiza mpendwa wetu katika safari ya mwisho,"alisema. 

CHADEMA YAWATAKA WAPIGA KURA WAKAE MITA MIA MBILI KUTOKA KITUO CHA KUPIGIA KURA

0
0
 Mwanasheria wa chama cha Demokrasia na Maendeleo [CHADEMA]   John Malya, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)  kuhusu  wananchi wakiisha piga kura wakae umbali wa mita mia mbili kutoka katika vituo vya kupigia kura, kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa millenium tower jijini Dar es saalam
 Afisa habari wa chama  cha Demokrasia na Maendeleo [CHADEMA] Tumaini Makene  akisisitiza jambo katika mkutano huo  kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam.
Waandi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mwanasheria wa chama cha Demokrasia na Maendeleo [CHADEMA]   John Malya leo jijini Dar es Salaam  . (Picha na Emmanuel Massaka

MAOMBI YA KULIOMBEA AMANI TAIFA LA TANZANIA KUFANYIKA OKTOBA 21 KWAKA HUU

0
0
 Mwenyekiti  wa  Good News Ministry International,  Charles Gadi akizungumza na waandishi wa habari  hawapo pichani  juu ya kuombea amani Taifa letu hususani  katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu ili ufanyike na kuisha amani ,maombi hayo yatafanyika katika Ukumbi wa Karimjee Oktoba 21 mwaka huu kuanzia mnamo majira taa tatu asubuhi,Mkutano huo umefanyika leo jijini Dar es  Salaam.kulia ni  mchungaji  wa kanisa la Pentecostal  James Manyama.
Wandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti  wa Good News Ministry Internation  Charles Gadi. Picha na Emmanuel Massaka

DK. SHEIN AOMBA KURA DIMANI MKOA MJINI MAGHARIBI, ZANZIBAR

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akiwahutubia wananchi na WanaCCM katika Mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM Mkoa wa Kusini Unguja Jimbo la Makunduchi katika uwanja wa mpira wa Jamhuri.
Baadhi ya wanaCCM waliohudhuria katika Mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM Jimbo la Dimani Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja wakimskiliza mgeni rasmi katika mkutano huo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza nao leo katika uwanja wa mpira wa Dimani.

SOMA MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KWA MPIGA KURA

0
0

UCHAMBUZI WA HABARI ZA MAGAZETI OKTOBA 20,2015

0
0
Kesi ya mita 200 ya uchaguzi mkuu kuanza leo. Pata habari motomoto zilizopamba kurasa za magazeti ya leo; https://youtu.be/NbbanyVNgHg

Dk.Magufuli asema mabadiliko sio kuzungusha mikono, vyama vinavyounda UKAWA wasitisha kampeni; https://youtu.be/47_EU73pBfQ

Tume yatoa muongozo wa upigaji kura. Mabilioni ya Mbowe yaivuruga CHADEMA. Pata habari katika dondoo za magazeti ya leo; https://youtu.be/eFvmJ9YAsyk 

Taifa Stars kuiendea Algeria ng’ambo, Bin Zubeity avutwa TFF. Ligi kuu yapisha uchaguzi mkuu.Ni katika magazeti ya leo;   https://youtu.be/dM0CCFihJ4s

Samia afuta nyayo za Lowasa Mbeya. Dk.Dau aweka historia NSSF, NSSF yajenga daraja la kihistoria Kigamboni;https://youtu.be/z-nhKJGpXeA

RAIS KIKWETE AFUNGUA KITUO CHA MICHEZO KIDONGO CHEKUNDU

0
0
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa Ufunguzi wa Kituo cha michezo cha Jakaya M.Kikwete Youth park huko Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amembeba mtoto wakati wa Sherehe za ufunguzi wa kituo cha michezo cha Jakaya M.Kikwete Youth park huko kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi kituo cha michezo  cha Jakaya M.Kikwete Youth park huko Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam.Kituo hicho kimejengwa kwa msaada wa klabu ya michezo ya Sunderland ya Uingereza kwa kushirikiana na kampuni ya kufua umeme ya Symbion.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe  katika ufunguzi wa Kituo cha michezo cha Jakaya Kikwete Youth park huko Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam.

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akicheza mpira na baadhi ya watoto wanaopata mafunzo ya michezo katika kituo hicho kinachofunza mpira wa miguu,kikapu na volleyball ya ufukweni.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto wanaopata mafunzo katika kituo kipya cha michezo.



Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Symbion Bwana Paul Hinks baada ya sherehe za ufunguzi wa kituo(picha zote na Freddy Maro)

BEI YA MADAFU HII LEO

0
0


Viewing all 46201 articles
Browse latest View live




Latest Images