Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 667 | 668 | (Page 669) | 670 | 671 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Baadhi ya Wakimbizi kutoka Burundi wakipokelewa katika Kambi ya Wakimbizi ya Nduta, wilayani Kobondo, mkoani Kigoma. Idadi ya wakimbizi kutoka nchini humo inazidi kuongezeka siku hadi siku.
  Watoto wa Wakimbizi kutoka Burundi wakiwa katika Kambi ya Wakimbizi ya Nduta wilayani Kibondo, mkoani Kigoma ambapo wanahifadhiwa. 
  Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.   

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
  Idadi ya raia wa Burundi wanaoingia nchini kutafuta hifadhi ya ukimbizi inazidi kuongezeka siku hadi siku ambapo hadi kufikia tarehe `17 Oktoba, 2015 idadi hiyo ilikuwa imefikia 107,112.


  Raia hawa wa Burundi wanaendelea kuingia nchini kupitia vijiji vya mpakani na wengi wao ni wanawake na watoto kutoka Mkoa wa Makamba nchini Burundi.


  Vijiji wanapoingilia raia hawa kutoka Burundi ni pamoja na Bukililo na Katanga wilayani Kankonko, na Kitanga, Kigadye, Manyovu, Kilelema, Biharu, Migongo na Herushingo wilayani Kasulu.  Kijiji kingine ni Mabamba kilichopo wilayani Kibondo, ambapo wengine hupitia wilayani Ngara mkoani Kagera.

  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) na wadau wengine, imekuwa ikiwahifadhi wakimbizi hawa katika makambi ya wakimbizi ambapo hupatiwa huduma zote muhimu.  Huduma hizo ni pamoja za malazi, chakula, afya, elimu na ulinzi.


  Wakati huo huo, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imeanza zoezi la kuwahamisha wakimbizi wa Burundi waliokuwa wakihifadhiwa kwa muda katika kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu na kuwapeleka katika kambi ya Nduta iliyoko wilayani Kibondo.


  Zoezi hili ambalo limeanza tarehe 04 Oktoba, 2015 linalenga kupunguza msongamano uliokuwapo katika kambi ya Nyarugusu ambayo hadi wakati huo ilikuwa na jumla ya wakimbizi 102,773 kutoka nchini Burundi.


  Tangu zoezi hili lianze, kiasi cha wakimbizi 3,808 kutoka nchini Burundi wameshahamishiwa katika kambi ya Nduta kutoka kambi ya Nyarugusu ambayo  inahifadhi wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).  Kambi ya Nyarugusu ina kiasi cha wakimbizi 60,000 kutoka DRC.


  Zoezi la kuwahamisha wakimbizi hawa kutoka nchini Burundi litaendelea hadi wakimbizi wote kutoka nchi hiyo walioko katika kambi ya Nyarugusu watakapoisha.


  Pamoja na kambi ya Nduta, maeneo mengine yanayoendelea kuandaliwa ili kuwahifadhi wakimbizi hawa kutoka Burundi ni Mtendeli na Karago yaliyoko wilayani Kakonko mkoani Kigoma.

  Aidha, wakimbizi wote wanaoendelea kuingia nchini kutoka Burundi kwa sasa hupelekwa moja kwa moja katika kambi ya Nduta badala ya kambi ya Nyarugusu.


  Imetolewa na Isaac J. Nantanga

  MSEMAJI – WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

  0754 484286

  18 Oktoba, 2015  0 0

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
  *Asihi viongozi, watumishi wa umma wasiache kumuomba Mungu

  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema anamshukuru Mungu kwa kumuwezesha kumaliza salama utumishi wake Serikalini kwenye ngazi za juu ambao umedumu kwa takriban miaka 15.

  Akizungumza na waumini wa Kanisa Katoliki wakati wa Ibada ya Jumapili katika Parokia ya Mt. Anna iliyoko Hananasifu, Kinondoni leo mchana (Jumapili, Oktoba 18, 2015), Waziri Mkuu Pinda amesema anamshukuru Mungu kwa nafasi aliyopewa ya kulitumikia Taifa akiwa Waziri Mkuu kwa miaka minane na miezi tisa; pia katika ngazi ya uwaziri miaka miwili na nusu na miaka mitano akiwa Naibu Waziri.

  “Ninamshukuru Mungu kwa kuniwezesha kumaliza uongozi wangu Serikalini. Ninamaliza uongozi wangu kwa amani na furaha. Katika ibada hii ya shukrani nimemuomba Mungu anisamehe kwa matamshi niliyoyatoa nikiwa kiongozi… yanaweza kuwa yaliwaudhi watu bila mimi kujua,” alisema.

  “Uwaziri Mkuu ni kazi ngumu yenye changamoto nyingi. Nitakuwa mtu wa ajabu nisipomshukuru Mungu kwa uongozi wake katika kipindi chote hicho tangu nikiwa Naibu Waziri hadi kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu,” alisema.

  “Wito wangu kwa Watanzania wote ni kwamba msiache kumtaguliza Mungu maishani kwa sababu yeye ndiye mtoaji wa yote. Wote tuendelee kumtii Mungu na viongozi wetu wa kiroho kwa sababu wako hapa kumwakilisha yeye,” alisema.

  Alisema wako baadhi ya watu ambao wakipata madaraka wanaona kwenda kanisani ni kero au ni kupoteza muda. “Tatizo lao ni kutojijua, hawatambui kwamba bila Mungu hizo nafasi wasingezipata. Ninawaomba tujue kwamba kuna maisha hata nje ya utumishi wa umma na utumishi wa kisiasa,” alisema.

  Alisema katika utumishi wake wa umma amejifunza mambo mengi lakini kikubwa alichobaini ni kujua jinsi ya kuishi na watu. “Elimu kubwa ni kujua jinsi ya kuishi, hii ni elimu zaidi ya kitabuni,” alisema. Alitumia fursa hiyo kumshukru mke wake, Mama Tunu Pinda kwa kuwa nguzo ya familia na kuwalea watoto wote walionao wakati yeye akihangaika na masuala ya kitaifa.

  Katika hatua nyingine, Abate Thadei Mhagama kutoka Abasi ya Hanga iliyoko Songea ambaye aliongoza ibada hiyo, aliwataka waumini wote nchini wazidishe sala kwa kufunga na kuomba katika siku saba zilizobakia kabla ya uchaguzi mkuu kwa sababu hali ni tete.

  “Ninawaomba waumini wote tuzidishe sala ili kwanza pawe na amani na upendo na pia Mungu atuwezeshe kupata viongozi aliowandaa kwa maana ya Rais, Wabunge na Madiwani.”

  “Sote ni mashahidi, tumeona kwenye mikutano kila mgombea akija sote tunajaa huko… hii ni kwa sababu hatujuia yupi ni yupi, ndiyo maana nasisistiza kuwa tumuombe Mungu atuletee yule ambaye amemuandaa,” aliongeza.

  Alisema kila mwananchi amesikia kwamba uchaguzi ukishafanyika awe tayari kupokea matokeo. “Tumeambiwa mara kadhaa tuwe tayari kukubali matokeo… kwa vile tunamuomba Mungu kwa bidii, itakuwa rahisi kukubali hayo matokeo kuliko kwa wale ambao wanaenda bila kuongozwa na Mungu,” alisema.

  “Litakuwa jambo jepesi kwetu kukubali matokeo kwani tutasema Mungu amemleta yule aliyemuandaa, yule ambaye tumekuwa tukimuomba atuletee,” alisisitiza.

  Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Baraza la Walei la Parokia hiyo, Bw. Arbogasti Warioba alisema kama kanisa wao wanamshukuru Mungu kwa ulinzi aliompatia Mhe. Pinda kwa kipindi chake chote cha Uwaziri Mkuu.

  “Sote tunatambua kuwa kazi ilikuwa ngumu, misafara ilikuwa ni mingi na wakati mwingine ya mwendo mkali lakini Mungu alikutetea na kukulinda hadi leo uko salama. Tunakushukuru pia kwa ushirikiano ulioendelea kutuonyesha wakati ukiwa madarakani na tunakuombea uendelee kuwa na uchaji wa Mungu katika maisha yako ya uraiani,” alisema Bw. Warioba.

  (mwisho)

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S.  L. P. 3021,
  11410 DAR ES SALAAM
  JUMAPILI, OKTOBA 18, 2015.

  0 0

  Na Dotto Kahindi

  Kampeni ya uhamasishaji juu ya mabadiliko ya tabianchi kupitia uendeshaji wa baiskeli katika nchi mbalimbali Barani Afrika imeingia Tanzania Octoba 17 kwa waendesha baiskeli 21 kutoka Tanzania kuwapokea wenzao kutoka Malawi.

  Kampeni hiyo ambayo imeanzia Msumbiji, Afrika Kusini, Botswana, Zimbabwe, Zambia, Malawi na hatimaye Tanzania na itatia nanga Kenya mapema mwezi novemba mwaka huu.

  Msafara huo wa waendesha baiskeli kwa Tanzania umeanzia kwenye mpaka wa Tanzania na Malawi wa Kasumulu ambapo unataratia kwenda mpaka Namanga watakapoukabidhi kwa waendesha baiskeli wa Kenya.

  Kwa mujibu wa Meneja Miradi wa shirika la Norwegian Church Aid, Augustina Mosha lengo la msafara huo ni kujenga uelewa kwa jamii juu ya mabadiliko ya tabianchi kwa kutumia vijana kutoka kwenye taasisi za kidini nchini.

  Anasema msafara huo utahusisha pia uchukuaji wa saini za wananchi ili kuweka imani zao kwa viongozi wa kiserikali ambao watakwenda kwenye mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP21 utakaofanyika Desemba mwaka huu huko Paris, Ufaransa.

  Mama Mosha anasema kuwa wameamua kutumia uendeshaji wa baiskeli kama njia ya kuhamasisha jamii juu ya mabadiliko ya tabianchi kwa sababu chombo hicho ni rafiki wa mazingira na hakichangii uzalishaji wa hewa ukaa.
  Picha zote na tabianchi blog
  Waendesha baiskeli kutoka Malawi wakiwasili kwenye mpaka wa Tanzania na nchi hiyo tayari kwa kukabidhi kijiti cha kampeni hiyo kwa wenzao wa Tanzania.
  Mmoja wa waendesha baiskeli Tanzania ambaye pia ni Ofisa Miradi wa Norwegian Church Aid, Tanzania, Gilbert Mworia.
  Meneja Miradi wa shirika la Norwegian Church Aid, Augustina Mosha akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji juu ya mabadiliko ya tabianchi kupitia uendeshaji wa baiskeli.
  Waendesha baiskeli wa Tanzania wakiwa katika mji wa Kyela Mbeya
  Mama Mosha akiwa na baadhi ya waendesha baiskeli wa Tanzania.
  Balozi wa kampeni ya We Have Faith nchini Malawi, Father George Buleya (kushoto) akiwa na Mratibu wa Vijana kutoka YouthCAN Tanzania, Francisca Damian wakati wa hafla ya kukabidhiana kampeni hiyo iliyofanyika kwenye mji wa Kasumulu, Mbeya.

  0 0

    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Mohammed Gharib Bilal, akimkpongeza Askofu Dkt. Abednego Keshmshahara wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Magharibi, Mkoani Kagera (kushoto) wakati wa sherehe za kuwekwa Wakfu zilizofanyika kwenye Kanisa la KKKT mjini Bukoba, mkoani Kagera leo Okt 18, 2015. Katikati ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Alex Malasusa.
    Baadhi ya Viongozi na waumini wa dini ya Kikristu wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dkt.Bilal, wakati akihutubia kwenye Sherehe za kuwekwa Wakfu, Askofu Dkt. Abednego Keshmshahara wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Magharibi, Mkoani Kagera, zilizofanyika kwenye Kanisa la KKKT mjini Bukoba, mkoani Kagera leo Okt 18, 2015.
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Askofu Dkt. Abednego Keshmshahara wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Magharibi, Mkoani Kagera (kulia) wakati alipowasili kwenye sherehe za kuwekwa Wakfu Askofu huyo, zilizofanyika kwenye Kanisa la KKKT mjini Bukoba, mkoani Kagera leo Okt 18, 2015. Katikati ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Alex Malasusa. 
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na baadhi ya viongozi na waumini wa dini ya Kikristu katika Ibada ya Kuweka Wakfu Askofu Dkt. Abednego Keshmshahara wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Magharibi, Mkoani Kagera, zilizofanyika kwenye Kanisa la KKKT mjini Bukoba, mkoani Kagera leo Okt 18, 2015.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akielekezwa jambo na mmoja wa viongozi wa Kanisa hilo wakati wa ibada hiyo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi na Waumini wa dini ya Kikristu, wakati wa sherehe za kuwekwa Wakfu, Askofu Dkt. Abednego Keshmshahara wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Magharibi, Mkoani Kagera, zilizofanyika kwenye Kanisa la KKKT mjini Bukoba, mkoani Kagera leo Okt 18, 2015.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Askofu mpya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Magharibi, Mkoani Kagera,  Dkt. Abednego Keshmshahara (wa pili kushoto) Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Alex Malasusa (kulia) baada ya kukwekwa Wakfu.

   Askofu mpya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Magharibi, Mkoani Kagera,  Dkt. Abednego Keshmshahara, akihutubia baada ya kuwekwa Wakfu. Picha na OMR

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akimkabidhi kombe la Mchezo wa fainali ya Zanzibar Cup 2015 Mpira wa Miguu Nahodha wa Timu ya Wilaya ya Mjini Abubakar  Ameir Omar uliochezwa katika uwanja wa Amaan Studiuam Mjini Unguja jana,Mchezo huo ulimalizika kwa Wilaya ya Mjini kuwafunga W/Magharibi kwa matuta 3-1.
  [Picha na Ikulu.]

  0 0

  Dar es Salaam. Wiki moja kabla ya Uchaguzi Mkuu imebainika kwamba, ili mgombea yeyote wa nafasi ya urais ashinde kiti hicho ni lazima awe na ushawishi mkubwa kwa vijana, hasa wa kike.

  Taarifa iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ikiainisha idadi ya watu waliojiandikisha kiumri, inaonyesha kuwa asilimia 57 ya wapigakura wote waliojiandikisha na kuthibitishwa kupigakura Oktoba 25, wana umri chini ya miaka 35.

  Taarifa hiyo ambayo imewagawa wapigakura wote 22.75 milioni kwenye makundi matatu; miaka 18 mpaka 35; 36 mpaka 50 na 51 na kuendelea, inaonyesha mshindi wa urais ni lazima alishike kundi hilo ili aibuke kidedea wakati kinyang’anyiro hicho kitakapokuwa kinahitimishwa.

  Taarifa hiyo ambayo imewagawa wapigakura wote 22.75 milioni kwenye makundi matatu; miaka 18 mpaka 35; 36 mpaka 50 na 51 na kuendelea, inaonyesha mshindi wa urais ni lazima alishike kundi hilo ili aibuke kidedea wakati kinyang’anyiro hicho kitakapokuwa kinahitimishwa.

  Kati ya wapigakura wote waliopo, vijana wenye umri kati ya 18 na 35 ni 12,894,576. Kati yao wanaume ni 6,155,613 (asilimia 27) na wanawake ni 6,738,964 ( asilimia 30) ya wapigakura wote waliojiandikisha mwaka huu.

  Hii ina maana kwamba, endapo kundi hili lote litamuunga mkono mgombea mmoja na kumchagua, basi atashinda kwa asilimia 57 na ambazo haziwezi kupatikana kwa rika nyingine zilizobaki.

  Takwimu hizi zinadhihirisha mikakati ya ziada, ambayo vyama husika inatakiwa kuwa nayo ili kuongeza wafuasi na kujihakikishia ushindi.
  Mchanganuo huo unaonyesha zaidi kuwa watu wa rika ya kati, kati ya miaka 36 mpaka 50 hawafiki hata nusu ya vijana hawa, kwani wapo 5,690,668. Hiyo ni asilimia 25 ya wote waliojiandikisha. Wao wanajumuisha wanaume 2,744,422 (asilimia 12) na wanawake 2,946,247 (asilimia 13) ya wapigakura wote.

  Makundi haya mawili pekee yanatengeneza asilimia 82 ya wapigakura wote huku asilimia 18 zinazosalia yaani wapigakura 4,165,544 zikiwa ni za wazee.
  Kwa wazee hawa, wamo wanaume 1,900,555 au asilimia nane ya wanawake 2,264,990 ambao ni asilimia 10.

  Akizungumzia takwimu hizo, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udsm), Dk Benson Bana alisema kuna haja kwa washauri na wagombea kuzitumia vizuri taarifa hizi katika kunadi sera zao, kwani kila kundi lina mahitaji yake maalumu na ndani yake pia yapo madaraja.

  Alifafanua kwamba haitoshi kusema vijana au wanawake wanajitokeza kwa wingi bila kueleza ni kwa namna gani kero zao zitataliwa, endapo chama au mgombea husika atapewa ridhaa na kundi hilo.

  “Ni vigumu kutabiri misimamo ya kiitikadi ya kundi hili. Inaweza kuwa rahisi kujua wanafunzi wa vyuo wanahitaji nini kwa sababu mawazo na mitizamo yao ni kama huwa inafanana, lakini haiwezekani kwa wale wanaofuga, kulima au waliojiajiri.

  Ni muhimu sera zikabainisha zitafanya nini na wajane, wasio na ajira, wajasiriamali na makundi mengineyo ndani ya lile la vijana,” alisema Dk Bana.

  Profesa Gaudence Mpangala wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ruaha (Ruco), alisema kuna umuhimu wa kila kundi kushiriki kwa mapana kwenye mchakato wa uchaguzi ili kuwa na nafasi nzuri ya kufanya uamuzi unaostahili. Alisema ingawa ipo dhana, inayohitaji kufanyiwa utafiti, kwamba wanawake wanaipenda CCM na vijana upinzani bado haitoshi kujiaminisha juu ya ushindi.

  0 0

  Meza kuu kutoka kushoto ni Bi. Jennifer Jones ambaye ni ni mkuu wa Kamisheni ya wanawake kaunti ya Prince George, Afisa Suleiman Saleh ambaye alimwakilisha Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi. Kulia ni Dr. El Senzengakulu Zulu ambaye ndio mwanzilishi na mmiliki wa shule ya Ujamaa inayofundisha tamaduni za bara la Afrika. PICHA NA KWANZA PRODUCTION/VIJIMAMBO BLOG.
  Kutoka kushoto ni Dr. John Rutayuga ambaye ni mwanzilish wa Ukwimwi Orphans akiwa meza kuu na Mr and Mrs William.
  Mshereheshaji Tuma akifungua pazia ya kuashiria SHINA Gala imefunguliwa rasmi siku ya Jumamosi Octoba 17, 2015 ndani ya Hotel ya Hilton iliyopo Greenbelt, Maryland na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali Watanzania na marafiki zao wakiwemo wawakilishi wa makampuni yanayoshirikiana na SHINA kwa ajili ya kusaidia misaada mbalimbali ikiwemo ujenzi wa shule nchini Tanzania. 
   Kikundi cha sanaa cha Taratibu Youth Association kikifungua pazia la burudani hku wakishangilia muda wote kwa umahiri wao wa kucheza ngoma za asili kutoka Tanzania. Kundi hili hupata mialiko mabara mbalimbali kujifunza na kufanya maonesho ya ngoma za asili ambazo hua kivutia kwa watazamaji.
   Wapiga ngoma wa Taratibu Youth Association.
  Mwanzilishi na mmiliki wa SHINA kwa heshima na taadhima akiwashukuru watu waliofika kwenye SHINA Gala Dinner na kusaidia kuchangisha pesa za kusaidia misaada mbalimbali ikiwemo ujenzi wa shule nchini Tanzania.
   Afisa Suleiman Saleh akimwakilisha Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi ambaye ndiye aliyekua awe mgeni rasmi kwenye SHINA Gala iliyofanyika siku ya Jumamosi Octoba 17, 2015 katika hoteli ya Hilton, Greenbelt, Maryland nchini Marekani.
  Afisa wa Ubalozi Bwn. Suleiman Saleh akimzawadia Bi. Jessica Mushala zawadi kutoka Zanzibar ambayo baadae ilifanyiwa mnada ili fadha zisaidie kumalizia ujenzi wa shule nchini Tanzania.
  Bi. Jennifer Jones Kamisheni ya wanawake kaunti ya Prince George's ambaye ndiye aliyekua msemaji mkuu huku akishangiliwa muda wote kwa ujumbe mzito aliokua akiutoa mara kwa mara kwenye hotuba yake.
  Bi. Jessica Mushala akimzawadia Bi. Jennifer Jones zawadi maalum.
  Bwn. Amos Mushala akimzawadia Dr. John Rutayuga zawadi maalum kutambua mchango wake katika kuendelea kupambana ikiwemo kuwasaidia waathirika wa Ukimwi nchini Tanzania.
  Dr. John Rutayuga akitoa shukurani zake kwa SHINA.
  Mwimbaji wa nyimbo za injili DMV Bi. Rose Kachuchuru akiimba moja ya nyimbo zake.

  Mwambata wa Jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Canada Colonel Adroph Mutta katika picha na mkewe walipohudhuria SHINA Gala Dinner hiyo. 
  Kwa picha zaidi bofya HAPA

  0 0

  Mwanafunzi Fuad Thabit kutoka Feza Boys Secondary aliyeibuka mshindi wa kwanza shule za sekondari katika Shindano la Genius-Cup akipokea cheti na zawadi yake ya shilingi 300,000 toka kwa mgeni rasmi wa hafla hiyo, Ofisa Mkuu  wa Utafiti taasisi ya COSTECH, Athman Mgumia.
  Wanafunzi Sita Washindi wa Shindano la Genius-Cup (mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na vyeti vyao mara baada ya kuibuka washindi. Nyuma yao ni meza kuu katika hafla ya kuwazawadia ikipata picha ya ukumbusho na mabingwa hao. 
  Mkurugenzi wa Shule za Fedha Tanzania akizungumza katika hafla ya kuwazawadia washindi wa shindano la Genius-Cup.
  Baadhi ya wanafunzi walioingia fainali katika shindano la kuwatafuta washindi wa shindano la Genius-Cup wakifuatilia hafla hiyo jana.
  Ofisa Mkuu wa Idara ya Elimu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Fredrick Shuma akizungumza katika hafla ya shindano la Genius-Cup jana.
  Baadhi ya walimu na wazazi waliowaleta washiriki na kufanikisha ushindi wao wakiwa katika hafla hiyo jana.
  Mgeni rasmi katika hafla ya kuwazawadia washindi wa Shindano la Genius-Cup mgeni rasmi wa hafla hiyo, Ofisa Mkuu  wa Utafiti taasisi ya COSTECH, Athman Mgumia (wa pili kulia)  akiwa na viongozi wengine wa meaza kuu. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Feza, Ibrahim Yunus.
  Burudani toka kwa wanafunzi ikiendelea...!
  Mmoja wa wanafunzi washindi wa shindano la Genius-Cup (kushoto) akipongezwa mara baada ya kupokea cheti na zawadi yake.
  Mwanafunzi Shammah Kiunsi (kushoto) wa shule za msingi Mkoa wa Mbeya aliyeibuka msindi wa pili na kujishindia kitita cha shilingi 200,000 akipokea cheti na zawadi yake toka kwa mgeni rasmi katika hafla ya shindano la Genius-Cup jana.
  Mmoja wa washindi katika shindano la Genius-Cup, Fuad Thabit (katikati) ambaye ni mshindi wa kwanza kutoka Feza Boys Secondary akipiga picha na viongozi wa meza kuu katika hafla hiyo jana.
  WANAFUNZI Sita walioibuka mabingwa wa Shindano la Genius-Cup la masomo ya sayansi na hisabati wamezawadiwa zawadi zao jana katika fainali za mashindano hayo zilizofanyika katika Shule ya Wavulana ya Feza Sekondari iliyopo Tegeta Jijini Dar es Salaam.

  Shindano hilo lililoshindanisha shule mbalimbali za msingi na sekondari nchini Tanzania na kuratibiwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kushirikiana na uongozi wa Shule za Feza nchini limejumuisha zaidi ya wanafunzi 1,486 limelenga kukuza vipaji vya wanafunzi hasa masomo ya sayansi na hisabati.

  Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mara baada ya kumalizika kwa shindano hili, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Feza, Ibrahim Yunus alisema wanafunzi sita walioibuka washindi na kupatia vitita vya fedha ni pamoja na Fuad Thabit mshindi wa kwanza kutoka Feza Boys Secondary aliyejipatia shilingi 300,000 na Zulfa Khamis msindi wa pili toka shule za sekondari Mkoani Tanga aliyejishindia shilingi 200,000.

  Bw. Yunus alimtaja mshindi mwingine wa kwanza shule za msingi ni Mvano Michael Cabangoh kutoka shule ya Green Acres aliyejishindia shilingi 300,000 na Shammah Kiunsi mwanafunzi wa shule ya msingi kutoka Mkoa wa Mbeya aliyejishindia kitita cha shilingi 200,000 pamoja na Dorice Ernest Msafiri mshindi wa tatu (msingi) kutoka Mkoa wa Dodoma Ignatius School aliyejinyakulia shilingi 150,000/-.

  Akifafanua zaidi Mwalimu Mkuu wa Sekondari ya Wavulana ya Feza, Bw. Yunus alisema wanafunzi walioingia fainali na kukutanishwa kwa pamoja ni 70 kati ya wanafunzi 1,486 walioshiriki katika kinyang'anyiro hicho. Aliongeza kuwa hii ni mara ya pili shindano la GENIUS CUP linafanyika kwani kwa mara ya kwanza lilifanyika mwaka jana huku likilenga kukuza mapenzi ya masomo ya sayansi na hisabati kwa wanafunzi wa Tanzania.

  Kwa upande wake Ofisa Mkuu wa Idara ya Elimu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Fredrick Shuma akizungumza kabla ya kukabidhi vyeti kwa wanafunzi washindi aliupongeza uongozi wa shule za fedha nchini kwa kuliendeldeza shindano hilo kwani linachangia kuleta chachu ya mapenzi kwa masomo ya sayansi na hisabati kwa wanafunzi nchini Tanzania ambao wamekuwa wakiyaogopa masomo ya sayansi.


  0 0

  Queen wa ngoma ya 'Hakunaga' maarufu kwa jina la Lady Queen ambaye ni mwanadada mwenye umri wa miaka 23, 'Makelele na wewe' pia ni Track yake ambayo aliwahikufanya na Dullayo. 

  Hapa ni wakati alipo fanikiwa kukutana na mwandishi wetu face to face ambapo mwandishi wetu alimtaka Lady Queen kuzungumzia Tasnia ya muziki wa hapa bongo kufuatia yeye ni mdau ambaye anategemea hapo baadaye aje kuishi maisha mazuri kupitia sanaa ya muziki. Baada ya msanii huyo ambaye anachipkia kwa kasi nzuri kupata fursa ya kufafanua muziki hiki hapa chini ndicho alicho zungumza.

  LADY QUEEN: "Muziki wa Bongo fleva kiukweli umekuwa na ushindani mkubwa maana kila mmoja anatamani kufika mbali na kuwa juu ya mwenzie kwa kufanya vitu vizuri, so sasa hivi tunaangalia wakubwa zetu walifanya nini yaani ambao tayari muziki wao wameufikisha mbali mfano kama Vanessa, so nasisi tunaiga njia walizo tumia ili tuweze kufikisha na sisi muziki wetu panapotakiwa, kwa hatua hiyo naona tunaelekea pazuri kimuziki."

  LADY QUEEN: " Naangalia kitu ambacho nikiimba kila mmoja atatamani kusikiliza watoto kwa wakubwa haijalishi ni wimbo wa mapenzi au laa! pia now nipokwenye mchakato wa kuboresha kucheza coz nafanya mazoezi ya kudance maana hata nikiwaga kwenye stage huwa natamani nicheze vizuri ili mashabiki wangu wa -Enjoy".

  LADY QUEEN: "Kwenye muziki kiukweli ugumua ambao nauona ni kwenye kupata connection, maana hadi wadau wa muziki wakufahamu inahitajika juhudi ya kutosha, katika muziki wangu kitu ambacho naona kinamiss ni ushirikiano, maana baadhi ya mastaa wanatutenga sisi upcoming Artist unakuta mastaa kwa mastaa ndio wanakuwa na ushirikiano, so inakuwa ni ngumu kwetu kuyafikia malengo, mimi huwa najitahidi kuonesha ushirikiano kwa wasanii wote hasa kwa kuposta kazi zao ili basi hata namimi ninapo toa kazi zangu waweze kunisuport hata kwa kushare kazi ambayo nakuwa nimeitoa hiyo ni moja ya jitihada zangu."

  LADY QUEEN: "Natamani sana kufikia level ya Vanessa Mdee na hata katika ndoto zangu ni kujakufanyanaye kazi, so kwa sasa najitahidi kutengeneza mazingira mazuri kwa kutoa kazi nzuri ili hata siku nikisema nimfuate kusiwe na ugumu wa yeye kukubali kufanya kazi na mimi I wish. Sitegemei kutoka kwa kukutumia skendo za kutengeneza maana nikitu ambacho nakishangaa sana coz unakuta msanii ni maarufu halafu anatengeneza skendo huko nikujishusha, nafuu sikendo ya kweli kuliko ya kufoji huo ni ushauri wangu kwa wasanii wanaopenda skendo."

  LADY QUEEN: "Mwisho napenda kuwaambia mashabiki wangu kuwa nashukuru 'Hakunaga' wameipokea vizuri kinacho fuata ni zaidi ya 'Hakunaga' baada ya uchaguzi nitaachia Audio & Video ya wimbo wangu mpya ambao unaitwa 'Chunga Mzigo wako'. Stay tuned nawapenda sana."


  0 0

   Bando la kumkaribisha Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia Suluhu Hassan,likiwa limeshikwa na wananchi katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine mjini Sumbawanga mkoani Rukwa  leo
   Chopa iliyomsafirisha Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan ikiwasili katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Sumbawanga mkoani Rukwa leo, ambako mgombea huyo alihutubia mkutano mkubwa wa kampeni.
   Chopa iliyomsafirisha Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan ikiwasili katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Sumbawanga mkoani Rukwa leo, ambako mgombea huyo alihutubia mkutano mkubwa wa kampeni.
   Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akipanda jukwaani baada ya kuwasili kwa Chopa, katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Sumbawanga mkoani Rukwa, kuhutubia mkutano wa mkutano  wa kampeni.

   Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia suluhu Hassan akisalimia wananchi baada ya kuwasili kwa Chopa kuhutubia mkutano wa kampeni leo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Sumbawanga
   Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akijadili jambo na Mgombea Ubunge jimbo la Sumbawanga mjini Aeshi Hilary, wakati wa mkutano wa kampeni aliofanya leo katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jatika jimbo hilo mkoani Rukwa
   Wananchi wakiwa wamefurika katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Sumbawanga mkoani Rukwa leo katika mkutano wa kampeni wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan
   Mjumbe wa Kamati ya kampeni za CCM, Mwigulu Nchemba akisisitiza jambo alipohutubia mkutano wa kampeni wa Mama Samia uliofanyika leo katika Uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine mjini Sumbawanga mkoani Rukwa
   Mjumbe wa Kamati ya Kamapeni ya CCM Kitaifa Mwigulu Nchemba, akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la Sumbawanga Mjini Aeshi Hilalry katika mkutano wa kamepni wa Mama Samia (kushoto), uliofanyika leo katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.
   Wananchi wakishangilia katika mkutano wa kampeni uliofanywa na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Sumbawanga mkoani Rukwa
   Mgombea Ubunge jimbo la Sumbawanga mjini Aeshi Hilary akiomba kura wakati wa mkutano wa kampeni wa Mama Samia uliofanyika leo katika jimbo hilo mkoani Rukwa
   Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia mkutano wa kampeni aliofanya leo katika Uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jimbo la Sumbawanga mjini mkoani Rukwa
   Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Sulhu Hassan akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la Sumbawanga mjini Aeshi Hilary katika mkutano wa kampeni aliofanya kwenye Uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine katika jimbo hilo mkoani Rukwa
  Vijana wa kazi wakiwa pamoja wakati wa mkutano wa kampeni wa Mama Samia uliofanyika leo katika Uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jimbo la Sumbawanga mjini mkoani Rukwa. 
  PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

  0 0

  Hakika ilikuwa ni Furasa isiyo na Kifani kwa Wanafunzi wa Awali kutoka Shule ya Msingi Green View English Medium ya Jijini Mwanza baada ya kufika katika mandhari iliyopo ndani ya Mamiz Grand Resort Mkolani Jijini Mwanza kwa ajili ya ziara yao ya Kimasomo (Study Tour) siku ya juzi Octoba 16,2015.
  Wanafunzi hao walifurahia michezo ya aina mbalimbali inayopatikana Mamiz Grand Resort kama ambavyo Kamera ya BMG (Binagi Media Group) ilivyonasa matukio ya hapa na pale. Hakika Watoto sasa wamepata pahala pa kufurahia utoto wao ndani ya Jiji la Mwanza.
  Mmoja wa Wanafunzi wa Green View English medium akifurahia Michezo ya Chopa ndani ya ndani ya Mamiz Grand Resort iliyopo Mkolani Jijini Mwanza 
  Mmoja wa Wanafunzi wa Green View English Medium akifurahia Michezo ya Chopa ndani ya ndani ya Mamiz Grand Resort iliyopo Mkolani Jijini Mwanza 
  Mmoja wa Wanafunzi wa Green View English Medium akifurahia Michezo ya Chopa ndani ya ndani ya Mamiz Grand Resort iliyopo Mkolani Jijini Mwanza 
  Wanafunzi wa Wanafunzi wa Green View English Medium wakifurahia Michezo mbalimbali ndani ya ndani ya Mamiz Grand Resort iliyopo Mkolani Jijini Mwanza.
  Wanafunzi wa Wanafunzi wa Green View English Medium wakifurahia Michezo mbalimbali ndani ya ndani ya Mamiz Grand Resort iliyopo Mkolani Jijini Mwanza
  Wanafunzi wa Wanafunzi wa Green View English Medium wakifurahia Michezo mbalimbali ndani ya ndani ya Mamiz Grand Resort iliyopo Mkolani Jijini Mwanza
  Wanafunzi wa Wanafunzi wa Green View English Medium wakifurahia Michezo mbalimbali ndani ya ndani ya Mamiz Grand Resort iliyopo Mkolani Jijini Mwanza
  Wanafunzi wa Wanafunzi wa Green View English Medium wakifurahia Michezo mbalimbali ndani ya ndani ya Mamiz Grand Resort iliyopo Mkolani Jijini Mwanza
  Wanafunzi wa Wanafunzi wa Green View English Medium wakifurahia Mchezo wa bembea ndani ya ndani ya Mamiz Grand Resort iliyopo Mkolani Jijini Mwanza
  Wanafunzi wa Wanafunzi wa Green View English Medium wakifurahia Mchezo wa bembea ndani ya ndani ya Mamiz Grand Resort iliyopo Mkolani Jijini Mwanza
  Wanafunzi wa Wanafunzi wa Green View English Medium wakifurahia Mchezo mbalimbali ndani ya ndani ya Mamiz Grand Resort iliyopo Mkolani Jijini Mwanza
  Wanafunzi wa Wanafunzi wa Green View English Medium wakifurahia Mchezo mbalimbali ndani ya ndani ya Mamiz Grand Resort iliyopo Mkolani Jijini Mwanza
  Mamiz Grand Resort inawajali watoto
  Kwa walio na Umri kuanzia miaka 18 na kuendelea wanaruhusiwa kupoza koo maeneo haya.
  Vitu vya Mamiz Grand Resort iliyopo Mkolani Jijini Mwanza.
  Bonyeza HAPA Kuona zaidi.


  0 0

   Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Nghwira (kulia), na Mgombea nafasi hiyo kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Chifu Litayosa Yemba wakijibu maswali mbalimbali katika mdahalo wa wagombea urais ulioandaliwa na Taasisi ya Twaweza Dar es Salaam leo. Hata hivyo wagembea nafasi hiyo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk.John Magufuli na Edward Lowassa kupitia Chadema hawakuweza kuhudhuria kwa sababu mbalimbali.
   Waongozaji wa mdahalo huo wakiwa kazini. 
   Wadau wakiwa kwenye mdahalo huo.
   Raia wa kigeni na wadau wengine wakifuatilia mdahalo huo.
   Mdahalo ukiendelea.
  Vijana wakiwa kwenye mdahalo huo.


  Na Dotto Mwaibale.

  MGOMBEA wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John  Magufuli pamoja na Mgombea wa nafasi hiyo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), pamoja na vyama vinaunda Ukawa, Edward Lowassa leo wameshindwa kuhudhuria mdahalo maalumu wa wagombea urais ulioandaliwa na mkimkiki kutokana na sababu mbalimbali.

  Mdahalo huo ulikuwa unajadili mambo mbalimbali kama vile uchumi,katiba ya uchaguzi,malengo endelevu ya umoja wa mataifa, katiba inayopendekezwa, viashiria vya uvunjifu wa amani nchini,uchumi na huduma za kijamii kwenye sekta ya afya.


  Wakizungumza kwenye mdaharo huo Dar es Salaam wagombea nafasi za urais kupitia vyama vya ACT-wazalendo, ADC na TLP walikuwa na mengi ya kuelezea kuhusu mstakari wa taifa la Tanzania. 


  Mgombea urais wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Chief Lutasola Yemba akijibu swali lilioulizwa kwamba wagombea hao watawezaje kuondoa rushwa kwa wanafunzi pindi wanapotafuta ajira endepo akipata ridhaa ya kuingia madarakani alisema. 


  SWALI  

  Mtawezaje kuondoa tatizo la rushwa kwa wanafunzi waliokoswa nafasi za kazi kwa maadai ya kukoswa uzoefu huku wakiombwa chochote kabla ya kupewa ajira rasmi.


  Chief Yemba alisema Serikali ya ADC itahakikisha wanafunzi wanatakiwa kupata kazi punde baada ya kuhitimu masomo yao bila kusubiri kupata uzoefu huku akiwa anafanya kazi katika taaluma yake hata kama ni kwalipo kidogo na kwa baadae atakuwa na uzoefu mkubwa.


  Kwa upande wake mgombea urais kupitia Chama cha  ACT- wazalendo ,Anna mghira akijibu swari hilo alisema rushwa ni utamaduni lakini chama cha ACT- wazalendo kiatatoa elimu ya rushwa tangu wakiwa wadogo,ambapo itakuwa ni utamaduni wa mwanafunzi tangu akiwa mdogo.


  ''Pia tumeweka mikakati ya utekelezaji ambapo ni namna tutakavyoshughulika na mikakati mbalimbali huku tukiwajumlisha wananchi kutoa maoni yao na kurudi kwetu kiutekelezaji ili kuziba mianya ya rushwa ,''alisema


  Swali

  Nini tofauti kati ya ugonzi na mfumo wa uendeshaji wa Serikali yaani utawala?

  Mghira alisema Chama hicho kitahakikisha kinashirikiana na watanzania katika suala zima l;a uongozina  kuongoza kwa uhuru huku akisema utawala ni kuendesha watu kwa kutoa amri na masharti bila kujali.


  Kwa upande wake Chief Yemba akijubu swari hilo alisema kupitia chama cha ACT wazalendo tutahakikisha tunawashirikisha wananchi kila jamabo ili kuwa viongozi ambao wanashirikiana na wananchi wake na kufikia maendeleo kwasababu sisi hatutaki kutawala wananchi bali  kuwaongoza watanzania,''alisema.


  Sifa za kuwa Rais


  Mghira Naielewa nchini yangu vema,mimi nimwanasheria kitaluuma ni elimu inayoweza kumleta mtu kumudu kuishi pamoja na kushughulikia migogoro ya jamii


  ''Nikichanganya na hii ya elimu ya haki za binadamu naamini kabisa naweza kuwa Rais wa nchi na upole wangu sio udhaifu,upole ni nguvu na naweza kuwatumikia watanzania na kuwa kiongozi wao mzuri,''alisema.


  Alisema Taifa lilipofikia kwa sasahivi linahitaji mtu anae weza kutatua migogoro kwa njia ya busara na si kupiga kelele na upole wangu ni nguvu kwa taifa hasa katika wakati huu abao taifa linaonekana kuwa katika mgongano.


  Chief Yemba alisema Urais hauna uzoefu wala mtu asiseme mimi siwezi kwasababau uraisa ni tasisi na hakuna mtu anaeweza kuwa Rais peke yake bila kushirikiana na wezake mimi ni rais bora wa Tanzania.


  ''Nimekuwa Rais wa klabu za soka katika kipindi chote cha maisha yangi tangu mwaka 1886 na sasa nimeteuleiwa na chama changu kuongoza ilani ya chama ili kufikia mafanikio ya kuondoa umasikini maradhi na ujinga,''alisema.


  Alisema amekuwa mfanyakazi bora katika kipindi chote alipokuwa nikifanya kazi katika klabu za mpira na amekuwa akiibua vipaji vya wachezaji pia hajawahi  kufanya kazi bila mafanikio kwa wananchi.


  Kukomesha rushwa


  Mghira Rushwa ni tatizo kubwa katika taifa letu,mimi nitashughulikia kuondoa mazingira magunu kazini,kuboresha mazingira ya kazi ili kuwafaya wafanyakazi kuwa huri.


  Alisema Atajitahidi kuweka sera katika utumishi wa umma kuweza sheria na taratibu ambazo zikifuatwa zinaweza kuondoa tatizo la rushwa nchini.


  ''Taifa linahitaji kuwa na ukusanyaji wa mapato wa kutosha kutoka asilimia 11 ya sasa na kufikia asilimia 25 kama chama changu kilivyojipangia pamoja na kuzibiti kodi katika ukusanyaji na kuziba mianya ya ukusanyi kodi na hapo tutapa mapato yanayopotea,''alisema.


  Tume ya uchaguzi.


  Mghira alisema kitendo cha watu kuambiwa wakishapiga kura warudi nyumbani hii ni hali inayoonesha tume haipo huru kwaababu kama ingekuwa huru isingefanya hivyo, lakini labda nikwasababu bado tunatumia utaratibu wa tume ya zamani.


  ''Naaiamnini na ningeomba watende haki katika kipindi hiki ili kutoa haki kwa wagombea wa nafasi mbalimbali katika mchakato huu,''alisema.


  Chief Yemba tume naaimani lakini haipo huru kwasababu ya mfumo wa kiutawala unaingiliana na chama tawala kwa asilimia kubwa haifanyi mambo yake kama tume,pengine utasikia kamuli mbalimbali laini tume haitoa onyo.


  Uzalendo


  Chif Yemba alisema uzalendo ni hari ya kujitoa katika kulitumikia taifa na kuhakikisha kwamba wanalililetaea taifa faida na si hasara, na kwamba kama atapata ridhaa ya kuwa Rais wa nchi atashirikiana na chama chake kuweka misingi ya  umoja ustahimilivu,uwajibikaji,ushirikishwaji na maadili ya uongozi ambayo yatasaidia kuondoa ufisadi.


  Mghira alisema yeye akiingia madarakani kama atapa ridhaa anataka kuweka uzalendo kwanza kwenye usambazaji wa habariili kutoa fursa pana na uhuru wa habari nchini.


  ''Mimi naamini katika kutoa habari na kuzisambanza kwa wanachina hili likpokatika ilani ya chama changu ambapo tuatahakikisha wanahabari wanakuwa huru kutafta habari na kurejesha kwa wananchi,''alisema.  Chief Yemba alisema yeye anaamini katika ushirikishwaji wa wananchi katika mambo mbalimbali yanayofanyiwa tafti kwajili ya maendeleo ya Taifa na pia ,chama chake kinaamini katika tafti za kisayansi.


  ''Suala la sheria ya makosa ya mtandao ni zuri lakini inabidi kuangaliwa ili kutowabana wanahabari kutoa habari kwa wananchi kwasababu taifa bila habari ni taifa lilokufa,''alisema.   Msimamo wao katika katiba pendekezwa.


  Yemba mimi sisemi kama kuna katiba mpya bado tunatumia katina ya zamani maana hata ile anayosemwa imefanyiwa marekebisho lakini bado haijafika kwa wananchi.


  Alisema kama atapata ridhaa ya wananchi kuchaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano atahalkikisha mchakato wa katiba unarudiwa upya na pia kwenda kwenye tafti kuangalia katiba ya jaji waryoba kama inakidhi vigezo kama la wataongeza vipengere vya msingi.


  Mghira alisema akam atapata ridhaa ya kuwa Rais wa Tanzania kwa wamu ya tano atahakikisha chakato wa katiba unarejeshwa kwasababau mchakato huo haukukubalika na wananchi mwanzoni.


  Swali

  Viashiria vibaya vya mgawanyiko ambayo vinajitokeza,hali hii mnaionaje na mkiingia madarakani mtaikomeshaje.

  Chief Yemba tatizo kubwa linaletwa na watu wanaofikiri tumbo badala ua watu,ili kuondoa viashiria hivi inabidi kupata mtu ambaye anaangalia watu na si utu wala tumbo lake.


  ''Tutahakikisha tunaondoa misngi ya viashiria kwa misngi ya haki katika dini zote na kutokuwepo kwa ukanda,nawashauri watanzania kuchangua ADC kuondoa tofauti,''alisema.


  Mgwilla akijubu swali hilo alisema anafuriki ubaguzi upo kwa viongozi zaidi kuliko wananchi,japo yeye hakukutana na ubaguzi wa aina yeyote katika kupita huko na kule kwenye kampeni zake.


  ''Mwanzoni nilikuwa na fikra za kukutana na ubaguzi kwasababau katika Taifa letu kuna kawaida ya kumkubali mwanamume kwa kila kitu anachokifanya lakini si mwanamke,namshukuru Mungu sikukutana na ubaguzi wa aina yeyote walifrahi kuniona na wamenikubali,''alisema.


  Muungano


  Mghira akizumngumza kuhusiana na muungano alisema   muungano wa tanganyika bado hauna ukubali wa wananchi na kwamba hiyo ni changamoto kubwa kwani wananchi wahana ridhaa ya muungano kikatiba hali inayofanya wananchi wa pande zote mbili kugomgana.


  Chief Yemba alisema Muungano hauna haki sawa na ili kuwepo na makubaliano ya muungano nilazima haki sawa ipatikane kwa watu wote wa tanzania na Zanzibar,kutoa fursa sawa kwa wote kiuchumi na hata katika sekta ya afya na sekta zingine.


  ''Tunatakiwa kufikiria kuwa na fursa sawa ili kuondoa malalamiko pamoja na kuwa na mfumo wa Serikali unaopendekezwa na pande zote mbili,''alisema  Chief Yemba.


  Mabadiliko ya kweli nchini


  Yemba alisema mafanikio ya ADC ni kujikita katika kuondoa ujinga umasiki na maradhi paoja na kuondoa mfumo ambao unafanya kazi katika Serikali ya CCM.


  Mghira alisema mabadiliko ya kweli nchini katika Serikali ya  wazalendo ni mtumizi mazuri ya rasilimali za nchi kama vile mafuta gesi na vyanzo vya mapato.


  Alisema dhana ya kuiondoa CCM madarakani ni dhana ya   kisiasa lakini CCM yenyewe ingefanya utaratibu wa kuondoka madarakani ili vyama vingine tujaribu kuleta maendeleo katika Taifa hili.


  Mapato wanataluuma na wanasiasa.


  Watalaam hawapewi mshahara stahiki kama inavyotakiwa,nilazima waboreshe mishahara ya wanataluma,Serikali inatakiwa kutofautisha kulipa mshara wafanyakazi wa kudumu ambao ni watalaamu mkubwa badala ya wabunge ambao ni wana muda mfupi Serilakini.


  Chife Yembe Urafiki katika utawala ni tataizo tunachohitaji ni kuwa na mchanganuo mzuri wa kufanya kazi kulingana na taaluma zetu pasipo kuangalia huyo ni rafiki au ndungu maana hii inachangia upendeleo wa mapato kazini katika taluma mbalimbali.
  Mghira wanasiasa wanakipato kikubwa kuliko watalaamu kwa sasa lakini sisi chini ya chama changu tutakuza sekta mhimu na kkisha kushughukia sekta za uzalishaji na wanawekeji kuiletea nchi mapato na ttafta posho za wanasiasa ili kuita uwiano wa wanataluma na wanasiasa


  ''Hakuna uhusiano wa huru unaoonekana kati ya Srikali na Zaki mara nyingi sekta binafsi inakinzana na sekta ya umma,Mimi na chama changu tukiwa tumepewa ridhaa tutaunda kikundi huru ambacho kitashughulikia tatizo hilo ili kuleta mahusiano mazuri kati ya hawa watatu,''alisema Anna.


  Uchumi


  Mghira alisema ACT tumezungumzia viwanda lakini bado suala hili linachangamoto kubwa kwasababu Tanzania bado hatuna umeme imara na maji ya kutosha katika semunu za vijijini hivyo tutahiji kuweka mikakati madhubuti ya kuweka mifumo rasmi ili kuanza kujenga na kufufua viwanda.


  ''Mikataba yote itakuwa ya wazi si ya siri ili kuwezesha wananchi kushiriki katika kuisoma na kutoa maamuzi na wale wasioona watapelekewa katika maeneo yao ili kukuza ushrikishaji wa wananchi,''alisema 


  Kwa upande wake Chief Yemba alisema ADC wamekubaliana Viwanda vinatakiwa kutokana na wananchi wenyewe huku akitolea mfano wa dhahabu kwamba inatoko chini ya ardhi na mwananchi aliyopo hapo anatakiwa kuwezesha kabla ya kuhamishwa ili kusaidia kuwaendeleza.


  TLP


  Lazima kuwe na bajeti za kuwesha upanuzi soko la ajira na lazima soko hilo liwashirikishe wazawa yaani wananchi wenyewe na hivyo dhahabu kama ni 2.2 lazima ieleweke kwa wananchi.  Huduma za kijamii kwenye sekta ya afya.

  Suala la kujiunga na mifuko ya jamii iwe lazima au hiari.

  Mghira Tukifanikiwa kuinua uchumi wa nchi yetui tutweza kuchukua jukumu ya kutoa huduma za afya kwa wananchi bure,na mifuko ya jamii tunaichukulia kama kichocheo cha mapato katika jamii.


  Yemba Serikali ya ADC itahakikisha inawaondolea wananchi wake maradhi na ujinga,Serikali itategeneza mfumo wa kumuwekea mwananchi fedha kutoka kwenye rasilimali alizonazo katika eneo lake,hakuna ulazima wa kumlazimisha mwananchi kuchangia huduma za fya.


  ''Tanzania imejaa rasilimali za asilimi hivyo hakuna sababu ya kumulazimisha mwananchi kulipipa gharama za afya,kinachotakiwa ni kutegeneza mfumo unaotoa fursa kwa wananchi.


  Kwanini Hospitali nyingi za umma hazina dawa?


  Mghira alisema watapambana na ufisadi kuweka miondombinu imara ili kuhahakisha kuna dawa za kutosha katika hospitali za umma pia dawa zinakosekana kwenye hospitali za umma kukoswa maadili ya kiutabibu.


  Chief yemba Kunatakiwa uwajibishaji watu wanaohusika kufanya hivyo wanatakiwa kuwajibishwa na pamoja na kuondoa tabaka la walio nacho na wasio nacho nchini pamoja na kuziba mianya ya rushwa ili kutoa fursa ya kupata matibabu kwa wote    Tanzania Labour Party(TLP), Macmillan Lyimo akinzungumzia suala la kuisha dawa kwenye hospitali za umma alisema

  Lazima mifumo ya ufuatiliaji wa dawa uboreshwe na kuondoa mianya ya rushwa ili kutoa haki kwa watu wanyonge ikiwa ni pamoja na kuwapatia wananchi haki ya kupata matibabu.

  Uchumi.


  Umejiandaaje kumaliza deni la taifa


  Chief Yemba alisema Suala linabakai palepale kuziba mianya ya rusha,lakini tatizo la viongozi wa Tanzania huajibika wakati wa kampeni pekee,ingekuwa vema kama viongozi waliochangia kuingizia nchi deni kubwa wangewajibishwa katika mchakato wa kurejesha fedha,ili kutoa nafasi kwananchi kufanya maendeleo katiik taifa na si kulipa deni kila mwaka.
  (Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com

  0 0

  ufafanuzi na jinsi ambavyo Kamati ya Maadili ya vyama vyenye wagombea Urais Taifa Ilivyo shughulikia malalamiko toka kwa Mgombea Mwenza wa CHADEMA Ndg J. Duni , kwamba Tume ya taifa ya Uchaguzi imeandaa Vituo vya wapiga kura HEWA zaidi ya 20,000.
  Viambatanisho 
  1. Maamuzi ya Kamati 
  2. Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Hamid Mahmoud Hamid

  0 0

  Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali vya Habari katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa Jijini Mwanza katika Semina ya siku tatu (Octoba 19 hadi 22) juu ya VYOMBO VYA HABARI NA UCHAGUZI iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA.

  Wanahabari watapata fursa ya Kujadili yale yanayoendelea katika kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Octoba 25 mwaka huu na nanma Vyombo vya Habari/ Waandishi wa Habari wanavyoripoti habari za Uchaguzi Mkuu kwa kuzingatia haki sawa kwa pande zote ikiwemo wagombea, wapiga kura huku suala la gender balance pia likizingatiwa.
  Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali vya Habari katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa Jijini Mwanza katika Semina ya siku tatu juu ya VYOMBO VYA HABARI NA UCHAGUZI iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA.
  Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali vya Habari katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa Jijini Mwanza katika Semina ya siku tatu juu ya VYOMBO VYA HABARI NA UCHAGUZI iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA.

  Majadiliano yakiendelea
  Majadiliano yakiendelea
  Beatrice Bandawe (Kushoto) ambae ni Mhariri wa Gazeti la Nipashe akiwa pamoja na Godfrida Jola (Kulia) ambae ni Afisa Programu TAMWA wakitoa ufafanuzi juu ya Semna kwa wanahabari inayofanyika Jijini Mwanza.
  Leonida Kanyuma ambae ni Afisa Habari TAMWA akizungumza katika Semina kwa Wanahabari juu Vyombo vya Habari na Uchaguzi inayofanyika Jijini Mwanza.

  0 0

   Mheshimiwa Naibu Balozi wa Tanzania, London, Mhe. Msafiri Marwa, akizungumza machache kumkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), Bwana Michael P. Mwanda, kuzungumza na baadhi ya Maafisa wa Ubalozi huo. Mwenyekiti huyo wa TPDC, alipata fursa ya kutembelea Ofisi za Ubalozi mara baada ya kumalizika kwa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Baraza la utetezi, ukuzaji na uendelezaji wa shughuli za kiuchumi (Global Local Content Council), kutokana na ugunduzi wa rasilimali za mafuta na gesi katika nchi husika, uliofanyika hapa London (13-15 October 2015), Mwenyekiti Michael Mwanda aliambatana na Mtaalam wa Mafuta na Gesi kutoka TPDC, Engineer Antelimi D nchini Uingereza.
   Naibu Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Msafiri Marwa (kushoto), kwenye picha ya Pamoja na  Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), Bwana Michael P. Mwanda (kati) na Engineer Engineer Antelimi. Ujumbe huo wa TPDC ulitembelea Ofisi hizo za Ubalozi na kupata nafasi ya kuzungumza na baadhi ya Maafisa wa Ubalozi.
  Naibu Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Msafiri Marwa ( wa nne, kushoto), kwenye pichani, pamoja na  Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), Bwana Michael P. Mwanda ( wa nne, kulia) na Engineer Engineer Antelimi (pili kulia). Pichani kutoka kulia ni Bwana Magnus Ulungi (kwanza kulia), dada Isabella Kafumba, Bwana Michael Mwanda, Balozi Msafiri Marwa, Bwana Yusuf Kashangwa, Bwana Allen Kuzilwa pamoja na Kanali Jackson Mwaseba.


  UJUMBE WA TPDC WATEMBELEA UBALOZI

  TANZANIA ilikuwa ni miongoni mwa nchi zilizowakilishwa kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka wa Baraza la utetezi, ukuzaji na uendelezaji wa shughuli za kiuchumi (Global Local Content Council), kutokana na ugunduzi wa rasilimali za mafuta na gesi katika nchi husika, uliofanyika hapa London (13-15 October 2015)


  Lengo kuu la Baraza hili ni kuzifanya nchi husika zinufaike na rasilimali inayopatikana katika nchi hizo na isiwe ni kwa wawekezaji wa kigeni tu (ambao ndio wenye mitaji na teknolojia ya kutosha inayowawezesha kutafiti na hatimaye kufikia kuivuna rasilimali hiyo).


  Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo uliongozwa na Ndugu Michael P. Mwanda, ambaye ndiye Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC). Wajembe wengine waliokuwa naye mkutanoni ni Engineer Antelimi D. Raphael kutoka TPDC na Yusuf Kashangwa kutoka Ubalozi wa Tanzania hapa London.  Baada ya Mkutano huo, ujumbe wa TPDC pia uliutembelea Ubalozi na kupata fursa ya kuongea na watumishi juu ya masuala ya msingi yanayoihusu sekta ya mafuta na gesi nchini Tanzania. Ndugu Mwanda alianza kwa kuieleza historia fupi ya utafiti wa mafuta nchini, kwamba ulianza (1954) kabla hata hatujapa uhuru. Hata baada ya Uhuru, utafutaji wa mafuta mafuta uliendelezwa tena kwa bidii zaidi hasa baada ya kuundwa kwa TPDC. Alisema pamoja na lengo kuwa la utafutaji wa mafuta, Tanzania haikuweza na haijaweza kuyapata, na badala yake imefanikiwa kugundua tu gesi.


  Kampuni ya Agip ndiyo iliyokuwa ya mwanzo kugundua gesi hapo Songo Songo baada ya kufanya utafiti kwa kipindi kirefu (1969-79). Lakini mwanzo walisema kiasi kilichopatikana ni kidogo hakitoshelezi mahitaji ya kibiashara. Agip walendelea kufanya utafiti na hatimaye waliweza kugundua tena gesi mara hii hapo Mnazi Bay mwaka 1982. Gesi hii haikupata kutumika kutokana na wagunduzi kudai haitoshelezi. 

  Kutokana na matatizo ya umeme unaotokana na nguvu ya maji kwa sababu ya ukame, ndipo wataalamu wa Shirika la Taifa la Petroli (TPDC) walipochukua hatua mnamo mwaka 1992 ya kufanya tena tathmini ya kiasi cha gesi iliyokwishagunduliwa na hatimaye waliweza kugundua kuwa kulikuwa na kiasi kikubwa cha gesi hapo Songo Songo mwaka 1999, hatua iliyopelekea Serikali kufanya uamuzi wa kuitumia gesi hiyo kuzalisha umeme hapo Songo Songo (2004) na Mnazi Bay (2006).


  Baada ya hapo shughuli za utafiti wa mafuta na gesi ukaelekezwa zaidi baharini na hatimaye kiliweza kugundulika kiasi kikubwa cha gesi baharini mwaka 2010. Kuanzia hapo macho na masikio ya walimwengu yakaelekezwa Tanzania na Makampuni mwengi ya kigeni yakaonyesha nia zaidi ya kuja kuwekeza katika sekta hii.


  Kwa hiyo mpaka sasa kiasi cha rasilimali hii ya gesi ni 47 TCF kilichopatikana baharini na 8TCF zilizopatikana pwani. Jumla ya kiasi cha gesi kilichikwisha thibitishwa kupatikana na 55 TCF.

  Baada ya historia hiyo fupi, ndugu Mwanda alieleza baadhi ya hatua zilizokwishachukuliwa na Serikali katika kufanya maandalizi ya kuhakikisha kuwa nchi au Watanzania wananufaika na ugunduzi wa rasilimali. Alizitaja hatua hizo kuwa ni pamoja na kuzipitia na kutunga Sera mpya za Utafiti wa Petroli na Gesi, Nishati, na kutungwa kwa Sheria za ushirikishaji wa wazalendo na ya Matumizi ya mapato yatokanayo na rasilimali hizi.


  Hatua nyingine ni kuanza kutumia gesi katika kuzalisha umeme palepale inapopatikana na kuwanufaisha wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara na kiasi kingine kusafirishwa kwa njia ya bomba hadi Dar es Salaam, kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa nishati ya umeme ili kupunguza makali ya mgao wa umeme uliokuwa ukiikabili nchi kutokana na kutegemea nguvu ya maji ambayo yameendelea kupungua mwaka hadi mwaka kutokana na ukame.


  Hatua nyingine ambayo imechukuliwa na Serikali ni kuwaelimisha wananchi wananchi juu ya masuala yanayoihusu Sekta hii ili wasiwe na matarajio yasiyoweza kutekelezeka kutokana ushawishi wa taarifa zisizokuwa sahihi zinatolewa na watu tu mitaani kutokana na ugunduzi wa rasilimali hii, ikawa ndiyo sababu ya kubweteka kiuchumi au ya uvunjifu wa amani iliyopo.  Kwa mfano, uvunaji wa gesi iliyopo baharini, unahitaji maandalizi makubwa ya ujenzi wa miundo mbinu na viwanda huku Pwani vitakavyotumia gesi hiyo. Sghuli hizo bila shaka haziwezi kukamilishwa hivi karibuni. Wataalam wanasema kuwa zinaweza kukamilishwa labda katika kipindi cha miaka kumi ijayo. 

  Hivyo ni vizuri pia wananchi wakaendeleza shuguli zao za kiuchumi katika sekta nyingine, kwani utegemezi katika sekta moja hauwezi kuwa ni ufumbuzi wa matatizo yote ya kiuchumi. Muda huu wakati hatua za maandalizi zinaendelea, ni vyema vijana wakaendelezwa kitaaluma ili baadae waweze kupata fursa za ajira katika sekta hii.

  0 0

  Maalim Seif awaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura siku ya oktoba 25 ili aweze kuwa rais wa Zanzibarhttps://youtu.be/R8WS3XvK1dM  

  Rais mstaafu wa awamu ya pili Mzee Mwinyi awaomba vijana mjini Zanzibar  kutokubali kutumika na wanasiasa kuharibu amani; https://youtu.be/BxVbGJH8ezk  

  Dkt Magufuri azidi kung’ara mjini Mwanza kwa watu wengi kujitokeza na huku akiahidi kuboresha bei ya pamba: https://youtu.be/mQ3jniGJGPc 

  Wanaharakati mjini Arusha waiomba tume ya taifa ya uchaaguzi kufanya uchaguzi kwa uwazi na ukweli ili uwe huru na wa haki: https://youtu.be/SlpOpS5Rmxw

  Mgombea urais Zanzibar Maalim Seif ameahidi kuboresha  mazingira ya wafanyabiashara wakubwa na wadogo iwapo atachaguliwa kuwa rais; https://youtu.be/f3duvz37pF8

  NEC yaeleza sheria za uchaguzi na wajibu wa mpiga kura tayoa tathmini ya muelekeo wa kampeni  na kutoa angalizo kwa wagombea; https://youtu.be/6kyRP10yDCk

   Katika kuelekea uchaguzi mkuu  je ni haki gani za binadamu zinapaswa kuzingatia katika uchaguzi mkuu? Fuatilia hapa;  https://youtu.be/ZGgTuZt1I-o
   Je sheria inasema nini juu ya kukaa mita 200 kutoka kituo cha kupigia kura siku ya uchaguzi mkuu Octoba 25,2015. https://youtu.be/gcb2OQCu9es

  Leo hii katika mjadala. Wataalam wanazungumzia mada ya Kura ya Mtanzania na Tanzania. Endelea kufuatilia hapa; https://youtu.be/zeSaLxZobR8

   Kutana na mgombea ubunge katika jimbo la Ilala kupitia TLP Bw.Salim Bendera katika mjadala; https://youtu.be/w-UBADbLUSM


  0 0

   Wakulima wakifurahia mbegu bora za mahindi, alizeti pamoja na mbolea mara baada ya kukabidhiwa na meneja miradi wa kampuni ya Agrics. Wakulima walionufaika na mbegu hizo ni pamoja na Maswa, Meatu na Shinyanga vijijini.
  Afisa Miradi wa kampuni ya Agrics Ltd, Bwana Semeni Kime (wa pili kulia) akifurahi na wakulima wa kijiji cha Mwakabeya baada ya kuwakabidhi wakulima hao mbegu za mahindi, alizeti pamoja na mbolea kwa ajili ya msimu mpya kilimo.
  Kampuni ya Agrics imetimiza ahadi ya kuwakabidhi mbegu bora za mahindi, alizeti na mbolea wakulima wa Maswa, Meatu na Shinyanga vijijini. Zoezi hili limefanyika kwa wakati kufuatia msimu mpya wa kilimo kutazamiwa kuanza hivi karibuni. Kampuni ya Agrics iliwapa fursa wakulima kuchagua aina ya mbegu wazitakazo ili kuhakikisha wanapata kile wakipendacho. Wakulima wanaendelea kuandaa mashamba yao huku wakiwa huru kabisa kwani tayari Agrics imewapatia mbegu zao kwa mkopo nafuu kabisa na wametanguliza asilimia 25%.  Zoezi la kukabidhi mbegu lilisindikizwa na viongozi mbalimbali wa vijiji ili kuhakikisha wakulima wanajipatia mbegu zao kwa manufaa ya kijiji na mkoa kwa ujumla.

  Akiongea kwa niaba ya Agrics Meneja miradi Bwana Charles Laswai alisema, “Tunajivunia kuwatimizia wateja wetu mahitaji yao kwa wakati. Kwa sasa wakulima wanasubiri mvua wakiwa na amani kabisa kwani tayari wana mbegu zao na wapo tayari kuanza kilmo. Kupitia mkopo wetu wakulima wamejipatia mbegu zao kwa kulipia 25% tu ya mkopo na watalipa asilimia inayobakia baada ya kuwa wamevuna mazao yao. Hii ni fursa kubwa kwa mkulima kwani kwa sasa amepata nafasi nzuri ya kuzingatia kilimo bila kuwaza jinsi ya kupata pesa ya kulipa. Lengo la Agrics ni kuhakikisha kauli mbiu ya ‘Kilimo Kwanza’ inazingatiwa na inakuwa ni yenye tija kwa mkulima wa Shinyanga vijijini, Maswa pamoja na Meatu.  ”

  “Kwa upande wetu kukabidhi mbegu kwa mkulima ni mwanzo wa mengi makubwa tutakayomsaidia mkulima katika msimu huu wa kilimo. Mara zote tumekuwa tukiwajali wateja wetu kwa kushirikiana na viongozi wa serikali pamoja na wataalamu wa kilimo kuhakikisha tunawapa mafunzo juu ya kilimo bora na cha kisasa. Elimu hii haiishii tu wakati wa kulima bali hata wakati wa kuvuna na kuhifadhi ili uvunaji na uhifadhi pia uzingatie teknolojia mpya inayompa fursa mkulima kuvuna mazao yake na kuyahifadhi vizuri kwa matumizi ya baadae.  Tunahakikisha mazao yanahifadhiwa kitaalamu ili yasiathiriwe na wadudu kwa kuhakikisha mafunzo yanatolewa kwa wakulima wetu”. Aliongeza Bw. Jonathan Kifunda, Mkurugenzi wa Agrics Tanzania.

  Kampuni ya Agrics huwapatia wakulima wake mbegu za mahindi aina ya Seedco Tumbili, Seedco Pundamilia, Pannar na Faru pia huwapatia mbegu za alizeti aina ya Kenyafedha pamoja na mbolea ya kukuzia aina ya CAN (YARA). Mkulima hujipatia mbegu hizi kwa mkopo nafuu na hulipa kwa awamu tano ndani ya miezi 9. Mbegu hizi zimedhibitisha na zinastahimili ukame na wadudu hivyo zinaendana na hali ya hewa ya mikoa ya Simiyu na Shinyanga na kuwawezesha wakulima kupata mazao mengi zaidi.

   “Kampuni ya Agrics imekuwa mkombozi wetu kwa miaka mingi sasa! Tumekua tukikopeshwa mbegu kwa gharama nafuu kabisa na sasa wametukabidhi mbegu kwa ajili ya msimu huu kwa wakati, hivyo tuna amani na tunachosubiri ni mvua zianze kunyesha ili tupande mbegu zetu. Kupitia Agrics kijiji chetu kina mabadiliko makubwa sana kwani wakulima wengi wameweza kujenga nyumba za kisasa (kwa vigezo vya nyumba za vijijini) na tuna akiba ya chakula tofauti na zamani kwani mavuno yalikuwa ni kidogo sana. Binafsi nimeweza kuwasomesha watoto watatu sekondari na mmoja amejiunga na chuo kikuu. Na nimefanikiwa yote haya kupitia kilimo, suala ambalo lilikuwa ni ndoto kwetu maana tulitegemea mifugo tu ili tuweze kuwasomesha watoto wetu.” Alieleza bwana Emmanuel Titus mkazi wa kijiji cha Ipililo wilayani Maswa.

  Agrics Ltd ni kampuni ya kibiashara inayofanya kazi zake kwa kushirikiana na shirika la ICS. Agrics inawapa wakulima wadogo wa kanda ya ziwa nchini Tanzania na Kenya fursa ya kujipatia mbegu bora na za kisasa kwa mkopo nafuu unaolipwa kwa awamu zinazompa mkulima nafasi nzuri ya kujiendeleza. Pia Agrics inahakikisha akiba ya chakula kwa mkulima ni lazima kwa ajili ya kupunguza njaa kwa wakulima.
  Kwa mhariri,

  Kwa maelezo Zaidi wasiliana na Salima Salum, Afisa mawasiliano na masoko, Agrics Tanzania                                                                                                                                    kupitia  0716120482 or salima.salum@agrics.org    

  0 0

    Umati wa wananchi wa kimara michungwani  wakimsikiliza mgombea ubunge kwa tiketi ya chama cha mapinduzi(CCM) Dkt Fenella Mukangara(hayupo pichani) wakati alipokuwa akinadi sera za chama chake jimboni kibamba.
   Mgombea Udiwani kata ya Saranga kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi(CCM) Bw.Haroun Yusuph Mdoe(kushoto) akizungumza  na wakazi wa Kimara Michungwani wakati wa kampeni za chama cha mapinduzi(CCM) jimbo la  kibamba.Kulia kwake ni Mgombea ubunge wa jimbo la kibamba kupitia chama hicho Dkt Fenella Mukangara.
   Mgombea Ubunge kwa tiketi ya chama cha mapinduzi(CCM)  Dkt Fenella Mukangara akizungumza na wakazi wa kimara michungwani  wakati alipokuwa akinadi sera za chama chake.Dkt Fenella aliwaahidi wakazi hao kuwa wakimchagua atafanikisha kutatua suala la ajira kwa vijana ikiwemo kuwapa elimu ya ujasiriamali, kusimamia tatizo la maji,elimu na afya Bora.

  Mgombea Ubunge kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi(CCM)  Dkt Fenella Mukangara akipongezwa na baadhi ya wanachama wa chama hicho baada ya kumaliza mkutano wa kampeni  Kimara michungwani.

  0 0

  Mgeni Rasmi katika Mahafali ya kwanza ya Shule ya Sekondari Adili High School,Moshono Jijini Arusha,Profesa Raymond Mosha akiangalia kazi zilizoandaliwa na wanafunzi wa masomo ya Sayansi ikiwa ni sehemu ya mahafali ya kidato cha Nne.
  Wazazi wa wanafunzi wanaotarajia kuhitimu Kidato cha Nne wakifatilia kazi za ubunifu zilizoandaliwa kwaajili ya kuonesha uwezo wao katika masomo ya Sayansi kwenye  Mahafali ya kwanza ya Shule ya Sekondari Adili High School.
  Wahitimu wakiwa na nyuso za tafakari kwenye mahafali ya kwanza ya Shule Adili High School iliyopo Moshono,Jijini Arusha. 
  Wanafunzi hao wakionesha igizo linalopiga vita ukeketaji kutokana na madhara yake kwa wanawake jambo linaloweza kusababisha ulemavu wa kudumu na vifo.
  Profesa Raymond Mosha akizungumza kwenye mahafali hayo,amesisitiza maadili kama msingi mkuu wa mafanikio katika masomo na utendaji kazi,kushoto ni Mkuu wa Shule hiyo,Mwalimu Andrew Shayo na Mwenyekiti wa bodi ya shule,Wakili Modest Akida.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Shule ya Sekondari Adili High School .
  Mwanafunzi Nolam Mike akipokea cheti cha kuhitimu masomo yake kutoka kwa mgeni rasmi.
  Wafanyakazi wakiburudika mbele ya wazazi na mgeni rasmi wakifurahia wahitimu wa kwanza wa kidato cha Nne.

  0 0

  THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
  Miaka 10 inatosha kwa yeyote kutumikia Urais – Rais Kikwete

  ·        Awataka watumishi wa Ikulu kumsaidia Rais ajaye kwa ari na nguvu zaidi kuliko walivyomsaidia yeye.


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa miaka 10 ya uongozi inatosha kabisa kwa mkuu wa nchi kufanya mambo mengi na kuwa hahitaji muda zaidi kuweza kumaliza ajenda yake.


  Aidha, Rais Kikwete amewataka watumishi wa Ikulu kumsaidia Rais ajaye hata kwa ari na nguvu zaidi kuliko hata walimvyosaidia yeye katika miaka yake yote 10 ya uongozi wake.


  Rais Kikwete aliyasema hayo usiku wa  Ijumaa, Oktoba 16, 2015, wakati alipozungumza na watumishi wa Ikulu katika hafla ya chakula cha jioni ambako watumishi hao waliagana na Rais Kikwete ambaye wamemtumikia kwa vipindi tofauti, wengine wakiwa wamekaa naye kwa miaka yote 10 ya uongozi wake.


  Akizungumza na watumishi hao, Rais Kikwete amesema kuwa anaondoka madarakani kwa furaha sana hata kama anaona huzuni kuagana na watumishi hao wa Ikulu ambao amekaa nao kwa miaka mingi, baadhi miaka 10.


  “Kwa hakika, naondoka mwenye furaha sana. Ni kweli nasikitika kuwa tunaachana lakini mambo yote mazuri yana mwisho wake. Nimeifanya kazi ya urais kwa miaka 10, nyie mnajua aina ya kazi hii.

   Miaka 10 ni mingi. Ni miaka inayotosha kabisa kwa mkuu wa nchi kukamilisha ajenda yake. Sidhani kama mtu anahitaji zaidi ya miaka 10 kutekeleza ajenda yake ya msingi,” amesema na kuongeza:


  “Na hata ukitaka kukaa zaidi huwezi kuyamaliza yote. Mzee Nyerere alikaa miaka 23 hakumaliza yote na yaliyobakia alimwachia Mzee Mwinyi ambaye naye alimwachia yaliyobakia Mzee Mkapa. Rais Mkapa naye alifanya mengi lakini hakumaliza yote na akaniachia mimi. Na mimi nitamwachia yaliyobakia Rais ajaye.”


  Kuhusu Rais ajaye ambaye atakuwa mkazi mpya ndani ya Ikulu, Rais Kikwete amesema: “Napenda kuwaombeni msaidieni sana Rais wetu ajaye. Kwa hakika nawaombeni tumsaidie kwa ari na nguvu zaidi kuliko hata mlivyonisaidia mimi.”
  Imetolewa na:

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

  Ikulu,

  DAR ES SALAAM.

  19 Oktoba, 2015.

older | 1 | .... | 667 | 668 | (Page 669) | 670 | 671 | .... | 1898 | newer