Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46194 articles
Browse latest View live

WAHITIMU WAASWA KUACHANA NA FIKRIA POTOFU KUWA ELIMU WANAYOIPATA ITAWAPATIA AJIRA SERIKALINI AU KWENYE SEKTA BINAFSI

0
0

Muonekano wa nje wa Jengo la Maabara ya Masomo ya Sayansi katika Shule ya Sekondari ya Bwawani baada ya Mgeni rasmi kuweka jiwe la msingi.
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kwenye Mahafali ya Kidato cha Nne Shule ya Sekondari Bwawani.
Baadhi ya Walimu na Wafanyakazi wa Shule ya Sekondari Bwawani wakifuatilia kwa makini maelezo ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza kwenye Mahafali hayo ya Kidato cha Nne.
Wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari Bwawani wakigani shairi lao mbele ya Mgeni rasmi.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil akimkabidhi cheti Mwanafunzi Mhitimu kwenye Mahafali ya Kumi na mbili ya Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Bwawani Oktoba 16, 2015(kulia kwa Mgeni rasmi) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja.

Baadhi ya Wahitimu Kidato cha Nne Shule ya Sekondari Bwawani inayomilikiwa na Jeshi la Magereza wakipiga makofi wakati wa hotuba ya Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil(hayupo pichani).

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil(katikati) akiwa na Viongozi mbalimbali Meza Kuu wakiimba wimbo wa Shule ya Sekondari Bwawani kwenye hafla ya Mahafali ya Kidato cha Nne ya shule hiyo(wa pili kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(wa pili kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule, Kamishna wa Magereza wa Utawala na Fedha, Gaston Sanga
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil(kulia) akisoma jiwe la msingi la Jengo la Maabara ya masomo ya Sayansi kama anavyoonekana katika picha.


Na Lucas Mboje, Pwani.
WAHITIMU wa kidato cha nne nchini wameaswa kuachana na fikria potofu kuwa elimu wanayoipata itawapatia ajira Serikalini au kwenye Sekta binafsi badala yake watumie elimu hiyo kama nyenzo muhimu ya kuwawezesha kujiajiri wao wenyewe.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil alipokuwa mgeni rasmi wakati wa mahafali ya kumi na mbili ya kidato cha nne katika shule ya Bwawani Sekondari iliyopo Mkoani Pwani.

"Katika hali ya sasa ya utandawazi yapo mambo kadhaa ambayo mtu binafsi anaweza kuyafanya na kujipatia kipato cha kujiendeleza maisha yake". Alisema Bw. Abdulwakil.

Bw. Abdulwakil amesisitiza kuwa wanachotakiwa kufanya wahitimu hao ni kuyasoma mazingira ya maisha popote watakapokuwa na kuamua namna ya kujiajiri ili mradi isiwe shughuli zinazopingana na sheria na maadili ya kijamii, kama vile kuuza madawa ya kulevya, ukahaba, unyang'anyi na mambo mengine yanayofanana na hayo.

Awali akimkaribisha Mgeni rasmi Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja alisema kuwa uongozi wa Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na Bodi ya shule utaendelea kuzitafutia ufumbuzi changamoto mbalimbali zinazozikabili shule hiyo kadri uwezo wa kifedha unavyopatikana.

 Jeneral Minja alizitaja baadhi ya changamoto mbalimbali ambazo tayari zimefanyiwa kazi ikiwemo miradi ya miundo mbinu ya msingi kama vile Madarasa, Maabara, Maktaba na mradi wa maji ambapo kwa kiasi kikubwa miradi hiyo imechangia kuboresha maendeleo ya kitaaluma shuleni hapo.

Kwa upande wake Mkuu wa shule ya Sekondari Bwawani, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Emmanuel Lwinga alipokuwa akitoa taarifa fupi kwa mgeni rasmi katika mahafali hayo amesema kuwa shule yake ni miongoni mwa shule nchini ambazo zinafanya vizuri kitaaluma na masuala mengineyo yasiyoyakitaaluma.

Aliongeza kuwa mwaka 2014 kati ya wanafunzi 95 waliofanya mitihani ya kidato cha nne  katika shule hiyo wanafunzi 87 sawa na asilimia 91.6% walifaulu, aidha wanafunzi 52 walichaguliwa kujiunga na masomo ya Kidato cha Tano katika shule mbalimbali za serikali.


Shule ya Sekondari Bwawani inamilikiwa na Jeshi la Magereza, ilianzishwa Mwaka 1978 kwa lengo la kutoa elimu ya Sekondari kwa Watumishi wa Magereza ambapo hivi sasa shule hiyo inatoa elimu kwa vijana wa kike na kiume kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita.

BONDIA VICENT MBILINYI AMPIGIA MIKWALA DEO NJIKU KUPAMBANA DESEMBA 25

0
0
BONDIA VICENT MBILINYI


Na Mwandishi Wetu

BONDIA Vicent Mbilinyi amesaini mkataba wa kuzipiga na Deo Njiku wa Morogoro siku ya Desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri morogo wakisindikiza mpambano wa Fransic Cheka na Thomasi Mashali mpambano uho wa raundi sita

utakuwa wa kwanza kwa bondia Mbilinyi kucheza mkoa wa morogoro akizungumzia mpambano huo bondia huyo amesema kuwa anamjua mpinzani wake vizuri kutokana na ukongwe wake kwa kuwa alianza zamani kupigana ata hivyo mimi nina jiamini na nitamkalisha katika raundi za awali

bondia huyo alieweka kambi yake mkoa wa pwani maeneo ya Kibaha ambapo ameweka kambi yake kwa ajili ya mpambano huo
bondia huyo anaefundishwa na Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi ncini Rajabu Mhamila 'Super D' amejizatiti kumtwanga vizuri tu Deo njiku ili ajisafishie njia ya kuwa bingwa wa mchezo wa masumbwinchini

nae Kocha wake Rajabu Mhamila 'Super D;' aliongeza kwa kusema kuwa ana matumaini na bondia wake kwa kuwa na rekodi nzuri ya mchezo ambapo mpaka sasa amecheza michezo 7 kashinda 5 droo 1 na kupoteza 1 kwa rekodi hiyo bondia huyo ana uchu wa kubaki kileleni na kuendeleza kichapo kwa kila bondia anaekutana nae

MAMIA WAMUAGA MBUNGE WA LUDEWA DEO FILIKUNJOMBE NA NDUGU ZAKE NYUMBANI KWAKE KIJICHI JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
 Aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe enzi za Uhai wake.
 Msaidizi wa Mbunge huyo, Casablanga Haule enzi za Uhai wake.
 Padri Plasdus Ngabuma enzi za Uhai wake.
 Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deogratias Filikunjombe wakati wa ibada ya kuuaga iliyofanyika nyumbani kwake Kijichi Dar es Salaam leo mchana.
 Majeneza yenye miili ya aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deogratias Filikunjombe na ndugu zake, Plasdus Ngabuma na Casablanga Haule yakiwa yamewekwa mbele wakati wa ibada ya kuiombea iliyofanyika nyumbani kwa mbunge huyo Kijichi Dar es Salaam leo, kabla ya kusafirishwa kwenda Ludewa kwa mazishi.
 Mjane wa Deo Filikunjombe, Sarah (katikati) akisaidiwa na jamaa zake wakati wa ibada hiyo.
 Waombolezaji wakiwa kwenye ibada hiyo.
 Padri Maxmillian Wambura kutoka Parokia ya Mtakatifu Wote Kiluvya akiyamwagia mafuta ya baraka majeneza hayo.
 Waombolezaji wakiwa katika ibada hiyo.
 Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza la Plasdus Haule.

 Jamilia ya Filikunjombe ikiwa katika ibada hiyo.
 Waombolezaji wakiwa kwenye ibada hiyo.
Nyumba ya Filikunjombe ambayo inadaiwa amekaa wiki mbili tangu ahamie baada ya kukamilika ujenzi wake 'Hakika tumuache mungu aitwe mungu"
(Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com

PINDA AAGWA NA WATUMISHI WA OFISI YA WAZIRI MKUU

0
0
  Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda kizungumza katika hafla fupi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kumuaga Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda iliyofanyika kwenye makazi ya Waziri Mkuu jijjni Dar es salaam Oktoba 16, 2015.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu wakigonganisha glass na Watendaji wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu katika Hafla fupi ya kumuaga aliyoandaliwana  watumishi wa Ofisi yake kwenye makazi yake jijini Dar es salaam Oktoba 16, 2015.   Wapili kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florens Turuka, kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Regina Kikuli  na wapili kulia ni Msajili wa Vyama vya siasa, Jaji Francis Mutungi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MABONDIA YONAS SEGU NA IDI PIALALI WAPIMA KUZITO KUZIPIGA KESHO JUMAPILI

0
0


Mratibu wa mpambano wa masumbwi Antony Rutta Katikati akiwainuwa mikono juu mabondia Yonas Segu kushoto na Idi Pialali kwa ajili ya mpambano wao wa jumapili hii katika ukumbi wa frends corner manzese Dar es salaam Picha na SUPERD BOXING NEWS

Bondia Yonas Segu kushoto akitunishiana misuli na Idi Pialali mara baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa kesho jumapili utakaofanyika katika ukumbi wa Frends corner Manzese Dar es salaam Picha na SUPERD BOXING NEWS

Bondia Ismail Ndende kushoto akitambiana na Mwinyi Mzengela baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao kesho jumapili Picha na SUPERD BOXING NEWS

RAIS KIKWETE AAGANA NA WATUMISHI WA WIZARA YA MAMBO YA NJE

0
0

Balozi wa Tanzania Afrika ya Kusini Radhia Msuya na Balozi wa Tanzania nchini India Alan Kijazi wakimkabidhi zawadi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kwa niaba ya mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nchi za nje wakati wa hafla ya kutunuku tuzo kwa Mhe.Rais  iliyofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre(JNICC) jijini Dar es Salaam leo.  
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mabalozi pamoja na wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa wakati wa hafla ya kumuaga iliyofanyika katika ukumbi wa ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre(JNICC) jijini Dar es Salaam leo.
(picha na Freddy Maro) 

ACACIA YADHAMINI PAMBANO LA SOKA LA VIONGOZI WA DINI NA MABALOZI KUHAMASISHA AMANI

0
0
 Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye ni nahodha wa timu ya viongozi wa dini, Alhadi Mussa Salum, akinyanyua juu kikombe cha ushindi wa pili baada ya kumalizika kwa pambano la soka kati ya viongozi hao na mabalozi kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam leo Oktoba 17, 2015. Mabalozi walishinda kwa mikwaju ya penati 3-2 na kutwaa kombe. Katikati ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, na wakwanza ushoto ni Meneja Mkuu wa kampuni ya Acacia, anayeshughulikia ustawi wa kampuni, Assa Mwaipopo

NA K-VIS MEDIA
KAMPUNI ya Acacia imedhamini pambano la soka kati ya viongozi wa dini na mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa Tanzania, pambano lililopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana Oktoba 17, 2015
Katika pambano hilo, mabalozi waliibuka washindi kwa njia ya mikwaju ya penalty 3-2 na kutwaa kombe.
Akitoa nasaha zake kabla ya kuanza pambano hilo la kuenzi amani taifa linapoelekea kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwezi huu, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, aliwaambia washiriki kuwa, serikali inaunga mkono jitihada za viongozi wa dini na mabalozi katika kuwaleta pamoja wananchi hususan katika kipindi hiki ambacho taifa linaelekea kwenye uchaguzi.
Pambano hilo la soka lililodumu kwa muda wa dakika 40, lilikuwa la utangulizi kabla ya pambano la ligi kuu soka Tanzania bara kati ya Yanga na Azam FC.
Akizungumza mwishoni mwa mchezo huo, Meneja Mkuu wa Acacia anayeshugulikia  a ustawi wa kampuni,  Assa Mwaipopo, alisema, kampuni yake imedhamini pambano hilo kwa kutambua umuhimu wa amani hapa nchini, ambapo Acacia kama wawekezaji wanao wajibu wa kuunga mkono jitihada zozote za kijamii katika kuhakikisha amani inakuwepo hapa nchini inakuwepo.
“Sote tunatambua kuwa hivi karibuni taifa litaingiankwenye uchaguzi mkuu wa kuchagua viongozi wetu, hivyo pambano hili la soka la viongozi wa dini na mabalozi ambalo nia yake kubwa ni kuhamasisha amani miongoni mwa Watanzania katika kipindi hiki cha uchaguzi limekuja wakati muafaka nasi kama Acacia tumeona tuchangie katika jambo hili muhimui.” Alisema Assa.
Katika pambano hilo lililofana, wachezaji wa timu zote mbili walionyesha ukakamavu wa hali ya juu kwa kumudu kucheza kwa nguvu na umahiri mkubwa na kuwapa burudani safi wapenzi wa soka.
  Balozi wa Jumuiya ya Ulaya hapa nchini, Filiberto Sebregondi, ambaye alikuwa nahodha wa timu ya soka ya mabalozi, akinyanyua juu kombe baada ya timu yake kuishinda timu ya mabalozi kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015. Wanaoshuhudia kushoto ni Meneja Mkuu wa kampuni ya Acacia, anayeshughulikia ustawi wa kampuni, Assa Mwaipopo, na Mkuu wa Mahusiano ya Serikali, Alex Lugendo (wapili kushoto).



 Waziri Chikawe, (kushoto), akisalimiana na Assa Mwaipopo
 Chikawe, akisalimiana na Alex Lugendo
 "Ball Boys" wakiwa wamebeba bendera ya Acacia, wakati timu zikiingia uwanjani
 Sheikh Alhadi akiwa kwenye mazoezi ya viungo na viongozi wenzake wa dini kabla ya mpambano huo

 Sheikh Alhadi akifumua shuti


 Mwamuzi wa pambano hilo Kamishna wa Polisi na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, akipuliza kipyenga
 Sheikh Alhadi akijaribu kufunga penalty ambayo hata hivyo hakufanuikiwa kufunga

 Timu ya viongozi wa dini iliyomenyana na mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini
 Timu ya soka ya mabalozi na wakuu wa mashirika ya kimataifa wanaowakilisha mashiorika na nchi zao hapa nchini
 Waziri Chikawe, viongozi wa Acacia, na wale wa TFF wakisalimiana na wachezaji wa timu zote mbili
 Viongozi wa dini wakiongozwa na kocha wao wakati "wakipasha" kabla ya pambano hilo
 Meneja Mkuu wa kampuni ya Acacia, anayeshughulikia ustawi wa kampuni, Assa Mwaipopo, akiwaeleza waandishi wa habari sababu za kampuni hiyo mudhamini pambano hilo la soka.“Sote tunatambua kuwa hivi karibuni taifa litaingiankwenye uchaguzi mkuu wa kuchagua viongozi wetu, hivyo pambano hili la soka la viongozi wa dini na mabalozi ambalo nia yake kubwa ni kuhamasisha amani miongoni mwa Watanzania katika kipindi hiki cha uchaguzi limekuja wakati muafaka nasi kama Acacia tumeona tuchangie katika jambo hili muhimui.” Alisema Assa.
 "Benchi la ufundi" la viongozi wa dini, kutoka kushoto, Sheikh Basaleh, Mkuu wa wilaya ya Temeke, Sophia Mjema, na Sheikh Othman, wakifuatilia kwa karibu pambano hilo
 Nasaha za mgeni rasmi kwa timu zote mbili
 Waziri Chikawe, (kulia), akiongozana na Assa Mwaipopo, (kushoto) na Mkuu wa Mahusiano ya Serikali wa kampuni ya Acacia, Alex Lugendo, mara baada ya ukaguzi wa timu

 Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, (kushoto), ambaye alikuwa kamisaa wa mchezo aisalimiana na Assa Mwaipopo
Mazoezi ya viungo yakiendelea

HIVI NDIVYO MAGUFULI ALIVYOPOKELEWA JIJINI MWANZA

0
0


DKT MAGUFULI ASHIRIKI KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MAREHEMU DEO FILIKUNJOMBE NA WENZAKE WAWILI WALIOFARIKA KATIKA AJALI YA HELIKOPTA..

0
0
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli  akitoa heshima za mwisho mbele ya majeneza ya aliyekuwa Mbunge wa Ludewa(CCM) Marehemu Deo Filikunjombe na wenzake wawili waliofariki katika ajali ya helikopta juzi katika pori la akiba la mbuga ya Selous. Marehemu aliagwa katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akimfariji Mke wa Marehemu Bi Sarah Filikunjombe wakati wa kuaga mwili wa marehemu katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015.
 Mke wa Marehemu Bi Sarah Filikunjombe akilia kwa uchungu kufuatia kifo cha Mumwe Deo Filikunjombe,wakati wa kuaga katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015.
 Dkt Magufuli akifarijiana na Mh.Zitto Kabwe  wakati wa kuaga mwili wa marehemu katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015.
 Dkt Magufuli alishindwa kujizuia kutoa machozi ya huzuni  wakati wa kuaga mwili wa marehemu katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015.
 Majeneza yenye miili ya aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deogratias Filikunjombe na ndugu zake, Plasdus Ngabuma na Casablanga Haule yakiwa yamewekwa mbele ya waombolezaji  wakati wa kuaga katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2015. kabla ya kusafirishwa kwenda Ludewa kwa mazishi mkoani Njombe.

MAGUFULI ALIVYOUNGURUMA VIWANJA VYA FURAHISHA JIJINI MWANZA

0
0

TAMASHA LA KANDANDA DAY LAFANYIKA LEO JJINI DAR ES SALAAM

0
0
 Mgeni rasmi  Angetile Osiah akizugumza katika  Tamasha la Kandanda Day 2015, hufanyika kila mwaka mwezi oktoba kwa kuzikutanisha Team Ismail  (Blue Jersey)na Dizo Moja (White Jersey) lilofanyika katika viwanja vya TCC Sigara, leo jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi Patrick Dumulinyi  akisisitiza jambo katika tamasha hilo.
 Mkurugenzi wa Bin Slum Tyres, Nassor Binslum, akionesha makeke yake uwanjani wakati wa Tamasha hilo leo jijini Dar es Salaam.
 Wachezaji wa timu  Ismail wakionyesha furaha ya ushindi Tamasha hilo leo jijini Dar es Salaam.

 Mgeni rasmi  Angetile Osiah akiwa na wanakamati wa timu katika picha ya pamoja katika  Tamasha la Kandanda Day 2015, Lilofanyika katika viwanja vya TCC Sigara, leo jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi  Angetile Osiah akimkabidh kombe captain Ismail Mohamed  katika  Tamasha la Kandanda Day 2015, Lilofanyika katika viwanja vya TCC Sigara, leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Bin Slum Tyres, Nassor Binslum, akipima afya wakati wa Tamasha hilo.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya Jamii)


TAMASHA la Kandanda Day 2015, Lilofanyika katika viwanja vya TCC Sigara,ambalo hufanyika kila mwaka mwezi Oktoba kwa kutanisha Team Ismail  (Blue Jersey) na Dizo Moja (White Jersey).

Mwaka jana Team Ismail ilipoteza kwa bao 4-1, na mwaka huu Team Ismail imeibuka kwa ushindi wa bao 2-0.

Mbali na mchezo huo Wakandanda walipata nafasi ya kupima Afya zao kupitia Chama cha Madaktari  Wa Michezo Tanzania, (TASMA), pia kulikuwa na mauzo ya Tshirts ambazo zinachangia mfuko wa MpiraMmoja, KitabuKimoja kwa shule na vituo vya watoto. Hivyo katika kila mwanakandanda aliekuwa amevaa T-Shirt ya Kandanda Day alikuwa mechangia mfuko huu.

Kwa wale ambao walikuja na magari yao, waliwekewa Tiketi  yenye Muhuri na Namba ya Gari, watatkiwa kwenda na karatasi hizo katika Duka la Mac Auto Accessories  watapata discount ya asilimia 10% kwa huduma zao

Awadh Massawe ateuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu TPA

0
0
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Rais Dkt. Jakaya Kikwete amemteua Bw. Awadh Massawe kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).

Rais alitangaza uamuzi huo Ijumaa iliyopita wakati wa tukio la kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa bandari mpya ya Bagamoyo inayosemekana kuwa kubwa katika ukanda huu wa Afrika mara itakapomalizika.

Akihutubia wakati wa tukio hilo, Dkt. Kikwete alisema yeye alishamaliza uteuzi huo na kumwambia Bw. Massawe afuatilie tu barua yake rasmi ya uteuzi.

“Mimi nilishalimaliza hilo, fuatilia tu barua yako ya ajira,” alisema Rais huku akishangiliwa na umati.

Kabla ya uteuzi huo, Bw. Massawe amekuwa akifanya kazi kama Kaimu katika nafasi hiyo tangu mwezi wa Pili mwaka huu na kufanikiwa hadi sasa kufanya mageuzi makubwa katika kuleta ufanisi katika bandari hapa nchini. 

Pia kabla ya kukaimu nafasi hiyo, alikuwa Meneja Bandari ya Dar es Salaa.

Baada ya kuwa Kaimu Mkurugenzi, alianzisha mikutano ya wadau yenye lengo la kurudisha mahusiano yaliyokuwa yameyumba kati ya pande hizo mbili.

Mikutano hiyo inayofanyika kila Alhamis ya mwisho ya kila mwezi inalenga kuhusisha wadau mbalimbali katika majadiliano ya jinsi ya  kuboresha ufanisi katika bandari ya Dar es Salaam.

Pia mwisho wa mwezi wa Sita mwaka huu, TPA ilifungua ofisi ndogo katika mji wa Lusaka, Zambia.
Mafanikio mengine ya hivi karibuni ni kuanza kwa mfumo mpya wa malipo kwa njia ya mtandao katika bandari ya Dar es Salaam.
Inatarajiwa kuwa baada ya kukamilika kwa ujenzi huo wa bandari ya Bagamoyo unaotarajiwa kugharimu dola bilioni 10, kutaongeza uwezo wa bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara zinazohudumia tani milioni 12 za mizigo kwa mwaka, makasha 6,000 na kuajiri watu 3,200 na vibarua 1,500.
Bandari hiyo mpya inatarajiwa kuhudumia tani 600,000 za mizigo na makasha 1,000 kwa mwaka na kuajiri watu 1,000.
Awamu ya kwanza ya mradi huo itahusisha gati nne ambapo mbili kati ya hizo zitatumika kwa huduma ya makasha pekee, moja kwa ajili ya mizigo mingine.
Tayari TPA iko katika hatua za mwisho kabisa kulipa fidia kwa wanavijiji zaidi ya 2,000 walioachia ardhi yao kupisha mradi huo.
Mradi huo utatekelezwa kwa makubaliano ya pande tatu za serikali ya Tanzania, China Merchants Holdings International (CMHI) ya China na State Government Reserve Fund (SGRF) ya Oman.

UDA yaahidi msaada zaidi kwa jeshi la Polisi

0
0
 Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam (UDA), Bw. Tumaini Magila (kushoto) akimkabidhi gari namba PT 0828 Toyota Land Cruiser, ASP Charles Hamza (katikati) aliyepokea gari hilo kwa niaba ya Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Pwani, ACP Japhari Mohamed baada ya kazi ya ukarabati wa gari hilo kukamilika.  Tukio hilo lilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.  Kulia ni dreva, G. 6633 PC Pendael.

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
KAMPUNI ya Usafiri Dar es Salaam (UDA) imesema itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kusaidia shughuli za kijamii na taasisi mbalimbali likiwemo Jeshi la Polisi ili kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali za kujenga taifa bora.

Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa kampuni hiyo, Bw. Tumaini Magila amesema hayo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam wakati wakikabidhi gari la Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani ambalo lilifanyiwa matengenezo kwa msaada wa kampuni yao baada ya gari hilo kuwa bovu kwa muda mrefu.

“Tumekuwa tukishiriki kusaidia masuala ya kijamii yakiwemo ya watoto yatima, na taasisi mbalimbali hapa nchini,” alisema wakati wa makabidhiano ya gari hilo lenye namba PT. 0828 aina ya Toyota Land cruiser.

Naye ASP Charles Hamza akipokea gari hilo kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani ACP Japhari Mohamed aliishukuru kampuni hiyo kwa msaada huo.

“Baada ya matengenezo haya, doria zetu zitaimarika,” alisema.

Alitoa wito kwa jamii na kampuni mbalimbali kuiga mfano wa kampuni hiyo katika kusaidia jeshi la polisi katika changamoto zake mbalimbali ili liweze kuendelea na majukumu yake vizuri.

Alisema ulinzi wa watu na mali zao ni jambo la msingi ambapo kila mmoja anatakiwa kuunga mkono juhudi hizo ili kutoa fursa kwa jamii, taasisi na kampuni mbalimbali kufanya shughuli za uzalishaji kwa usalama.

KALAMU EDUCATION FOUNDATION YASHEHEREKEA MWAKA MPYA WA KIISLAM-1437H KIJIJINI RUFIJI NA KUKABIDHA MISAADA MBALI MBALI.

0
0

Mmoja wa wenyeji wa msafara wa Taasisi ya Kalamu Education Foundation, Ustaadh Thabit pamoja na watoto wakipokea vifaa mbali mbali vya malazi na maji kutoka kwa baadhi ya wajumbe wa taasisi hiyo.
 Mmoja wa wajumbe wa Taasisi ya Kalamu Education Foundation Ndugu Hussein akimkabidhi magodoro Ustaadh Thabit wa kitoa cha elimu cha Irada – Bungu kwa ajiri ya vijana wanaolala hapo kwa masomo ya dini.

 Baadhi ya wajumbe wa wakitembea na kukagua maeneo mbali mbali ya kijamii na kujifunza changamoto za wananchi waishia maeneo ya eneo la Msafari Rufiji – Pwani
Wana Kalamu Education Foundation wakijumuika na mabinti wa Kituo Cha Madrassa Cha Irada wakati wa usomaji wa risala fupi ya kituo hicho na kufahamu changamoto za jamii ya kijiji hicho ambapo Taasisi ya Kalamu Education Foundation ilitembelea kama sehemu ya sherehe za mwaka Mpya wa Kiislam 1437H ulioanza siku 3 zilizopita.

MGOMBEA URAIS ZANZIBAR (CUF )MAALIM SEIF AOMBA KURA KWA WAKAZI WA BUBUBU

0
0
MGOMBEA Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, ameahidi kuweka mazingira bora kwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu ujao.

Akiwahutubia wafuasi wa Chama hicho katika mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Kwageji Bububu, Maalim Seif amesema atarekebisha mfumo wa ushuru katika bandari ili kuepusha wafanyabiashara kulipa ushuru mara mbili wanaposafirisha mizigo yao kuelekea bandari ya Dar es Salaam.

Amesema hali hiyo imekuwa ikiwadhoofisha wafanyabiashara wa Zanzibar, jambo amesema ataliwekea utaratibu mzuri, ili wafanyabiashara waweze kuendesha shughuli zao bila ya usumbufu.

Akizungumzia wafanyabiashara wadogo wadogo wakiwemo wale wa Jua kali, Maalim Seif amesema atawaekea mazingira mazuri kuweza kufanya shuguli zao.

Amesema chini ya uongozi wake iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar atahakikisha kuwa wafanyabiashara hao hawanyanyaswi, na watawekewa maeneo maalum ya kufanya biashara zao, na kwamba hakutokuwa na ulipaji wa kodi zisizotambulika katika maeneo yao.

Aidha ameahidi kuanzisha benki ya uwekezaji, ili kukuza mitaji ya wafanyabiashara wadogo wadogo.

Nae afisa uchaguzi wa CUF Bw. Muhene Said Rashid, amewataka wanachama hao kuweka utaratibu mzuri wa kuwasaidia wasioweza kupiga kura wakiwemo wagonjwa, wazee na wenye ulemavu,  ili kila aliyejiandikisha aweze kupiga kura kwa mgombea anayemtaka.

Aidha amewataka kuelimishana juu ya namna ya upigaji kura, ili kuepuka uharibifu wa kura na kupiga kura kwa usahihi.

 Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwahutubia wafuasi wa Chama hicho katika viwanja vya Kwageji Bububu.

  Wafuasi wa CUF wakisikiliza na kushangilia hotuba ya mgombea Urais wa Chama hicho katika viwanja vya Kwageji Bububu.

 Imail Jussa Ladhu, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Timu ya Ushindi CUF, akihutubia kwenye mkutano huo. (Picha na Salmin Said, OMKR)

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA MRADI WA VITUO VYA MAPUMZIKO NA VYOO VYA WASAFIRI KATIKA BARABARA KUU NCHINI, KATIKA KIJIJI CHA IDETERO, MUFINDI-IRINGA.

0
0
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mgimwa, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais Dkt. Bilal, kuhutubia wananchi wa Kijiji cha Idetero Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa, wakati wa hafla ya uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Mradi wa Vituo vya Mapumziko na Vyoo vya Wasafiri katika Barabara Kuu nchini, leo Okt 17, 2015.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wananchi wa Kijiji cha Idetero Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa, wakati wa hafla ya uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Mradi wa Vituo vya Mapumziko na Vyoo vya Wasafiri katika Barabara Kuu nchini, leo Okt 17, 2015. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua kitambaa kuweka Jiwe la Msingi la wa Mradi wa Vituo vya Mapumziko na Vyoo vya Wasafiri katika Barabara Kuu nchini, wakati wa hafla ya kuweka jiwe la Msingi iliyofanyika katika Kijiji cha Idetero Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa leo, Okt. 17, 2015.

 Baadhi ya Vijana wa Jeshi la KIjenga Taifa wakiendelea na ujenzi wa Mradi huo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo ya ujenzi huo kutoka kwa msimamizi wa Ujenzi, Stanley Ndosite Nzowa, wakati wa hafla ya uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Mradi wa Vituo vya Mapumziko na Vyoo vya Wasafiri katika Barabara Kuu nchini, leo Okt 17, 2015. Picha na OMR

WATOTO BADO WANAENDELEA KUDHULUMIWA UTOTO WAO- UMOJA WA MATAIFA

0
0
 Picha hii kutoka maktaba inamwonyesha mtoto ambaye anatumika kama askari na hivyo kumnyima haki yake ya msingi ya kuishi utoto wake,  pamoja na kupata huduma zake za msingi kama vile afya, elimu, malenzi na ukuaji  wenye hadhi. Pamoja na  Umoja wa Mataifa kuendelea na kampeni yake ya kupinga watoto  kutumika kama askari, bado  taarifa za hivi karibu za Umoja wa Mataifa, zinaeleza kuwa watoto bado wanaendelea kutumika katika baadhi ya maeneo kama askari,  huku wengine wakiingizwa katika  biashara haramu  zikiwamo za ngono.
 Vickness Mayao kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii,  Jinsia na  Watoto,  akichangia majadiliano kuhusu haki za mtoto wakati wa Mkutano wa   Kamati ya Tatu ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Kamati iliyokuwa ikijadili kuhusu   haki za mtoto ambapo  akizungumza kwa  Niaba ya Serikali   Bi. Mayao amesema Serikali  inaendelea na uboreshwaji wa Sheria mbalimbali zinazolinda haki ya Mtoto  huku  ikisisitiza kwamba wajibu wa kwanza wa kumlinda mtoto  dhidi ya  madhara yoyote  ni ya Wazazi wenyewe.  aliyekaa nyuma ni Afisa mwingine kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii,  Jinsia na Watoto Bi. Grace Mbwilo
 .Pamoja na  kufanyika kwa  mikutano ya Kamati ya Tatu ya Baraza  Kuu la  Umoja wa Mataifa,  Mikutano  ya Kamati nyingine zikiwamo ya Pili inayohusika na masuala ya  Uchumi na Maendeleo pia imekuwa ikiendelea na vikao vyake. Pichani (katikati)ni Bw. Ahmed Makame Haji Kamishna wa  Tume ya  Mipango kutoka Serikali ya  Mapinduzi Zanzibar akiwa katika  moja wa Mikutano ya Kamati ya   Uchumi na Maendeleo  wapo  pia Bi. Halima Wagao kutoka Wizara ya Fedha ( ZNZ na Bi. Mtumwa Idrissa kutoka  Tume ya Mipango ( ZNZ)
 Bw. Suleiman Said Ali. Afisa  Mambo ya Nje , Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ( ZNZ) akifuatilia Majadiliano ya Kamati ya Nne ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, iliyokuwa ikijadili kuhusu masuala ya  misaada  ya  ulipuaji wa mabomu ya  Ardhini,  Bw.  Ali pia alishiriki katika Majadiliano ya Umalizwaji wa Ukoloni kwa  Makoloni 17 ambayo bado  hayajapata fursa ya kujitawala na kujiamulia  mambo yake yenyenyewe likiwamo  Koloni la Western Sahara, koloni pekee barani Afrika.

WATUMISHI WA WIZARA YA MAMBO YA NJE WAMUAGA RAIS KIKWETE

0
0
Picha zote za juu zikimuonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Viongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje wakati alipowasili kwenye Kituo cha Kimataifa cha cha Mikutano cha Julius Nyerere ambapo Wizara ya Mambo ya Nje ilifanya hafla ya kumuaga Mhe. Rais.
Rais Kikwete akifunua kitambaa ambapo nyuma yake kuna picha ya Jengo la Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje linalokusudiwa kuanza kujengwa hivi karibuni. Rais Kikwete alifunua kitambaa hicho kuashiria kuanza ujenzi wa jengo hilo.
Rais Kikwete akipiga makofi kuonesha furaha yake kuwa Wizara ya Mambo ya Nje itapata ofisi za kisasa hivi karibuni
Rais Kikwete akiongozwa kuelekea ukumbi ulioandaliwa kwa ajili ya kufanya hafla ya kumuaga. Wanaomuongoza ni Waziri wa Mambo ya Nje na Uhirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe wa kulia kwa Rais Kikwete na Katibu Mkuu, Balozi Liberata Mulamula.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga akitoa neno la kuwakaribisha wageni waalikwa akiwemo Rais Kikwete katika hafla ya kumuaga.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula akitoa utambulisho wa wageni waalikwa wakiwemoWaheshimiwa Mabalozi waliostaafu.
Balozi Mstaafu akisalimia wajumbe baada ya kutambulishwa
Watumishi wa Wizara wakiwemo Wakuu wa Idara/Vitengo, Waheshimiwa Mabalozi wanaowakilisha Tanzania nje ya nchi wakiwa wameketi kwa ajili ya kushuhudia matukio ya hafla ya kumuaga Rais Kikwete.
Sehemu ya watumishi wa Wizara waliohudhuria hafla ya kumuaga Rais Kikwete
Watumishi wa Wizara katika hafla ya kumuaga Rais Kikwete
Mtumishi wa Wizara akisoma utenzi wa kumsifu na kumpongeza Rais Kikwete namna alivyoongoza Taifa la Tanzania kwa umahiri mkubwa katika kipindi chake cha miaka 10 ambacho kinakamilika Oktoba 2015.
Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Bernard K.Membe akisoma hotuba yake katika hafla hiyo. Hotuba ya Waziri Membe iligusia mafaniki ambayo Serikali ya awamu ya nne imeyapata katika kipindi cha miaka 10 ikiwa ni pamoja na kuvutia wawekezaji wakubwa, kuongeza uwakilishi nje ya nchi,kujenga ofisi za kibalozi na utatuzi wa migogoro.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri Membe wakionesha Tuzo aliyotunukiwa Rais Kikwte na Wizara ya Mambo ya Nje.
Picha za juu zinaonesha zawadi mbalimbali ambazo Rais Kikwete amekabidhiwa wakati wa hafla hiyo
Rais Kikwete akiongea na watumishi wa Wizara na wageni waalikwa. Katika mazungumzo yake Rais Kikwete alisisitiza umuhimu wa watumishi wa Wizara kudumuisha na kuimarisha mahusiano mazuri na nchi zote duniani. Alisema katika kipindi cha uongozi wake mafanikio makubwa ya kidiplomasia yamepatikana hivyo ni vyema watumishi wa Wizara wakayaendeleza kwa kiwango cha juu zaidi.
Picha ya pamoja kati ya Mhe. Rais Kikwete, Mhe. Waziri Membe, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje,Wakuu wa Idara/Vitengo na Waheshimiwa Mabalozi wa Tanzania nje ya nchi
Mhasibu Mkuu wa Wizara, Bw. Paul Kabale akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya  watumishi wa Kitengo cha Fedha na Uhasibu

NJOO LEO ESCAPE ONE UCHEZE MZIKI MZURI KUTOKA KWENYE BENDI YA SKYLIGHT

0
0

 Sony Masamba ambaye ni mmoja wa waimbaji wa Skylight akiendelea kutoa burudani akisindikizwa na waimbaji wenzake jumapili iliyopita.Njoo leo kuona mambo mapya kutoka katika bendi ya Skylight katika kiota cha Escape One.
 Mwimbaji wa bendi ya skylght Natasha akiwa anawapa mashabiki vionjo vya nyimbo za taratibu (kistaarabu) huku akisindikizwa na Sam Mapenzi jumapili iliyopita ndani ya kiwanja cha Escape One Mikocheni. 
 Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower akiimba kwa hisia moja ya nyimbo zinazombamba Afrika ya Mashariki katika hatua yake ya kukusanya mashabiki ili tu waende sawa aisee huyu jamaa ni hatari jumapili hii atakuwepo pale Escape One Mikocheni bila kukosa sogea taratibu uje ushuhudie vitu kutoka skylight band.
Sam Mapenzi akicheza na mashabiki wa bendi hiyo.

 
 Hakika ukiwa ndani ya Skylight ni kusakata rhumba ,o jambo la kawaida katika kiota cha Escape One Mikocheni
Mpiga Bass, Tofe aka 2be(kushoto) pamoja na mpiga gitaa Alen Kisso wakiendelea kuwakonga nyoyo mashabiki wao waliofika katika kiota cha Escape One Mikocheni jumapili iliyopita.
Joniko Flower  akicheza na mmoja wa shabiki mkubwa wa bendi ya Skylight jumapili iliyopita katika kiota cha Escape One Mikocheni
DaudiTumba aka Kabakangedere(kushoto) pamoja Tofe aka 2be ambaye ni Mpiga Bass wakiendelea kuwakonga nyoyo mashabiki wao katika kiota cha Escape One Mikocheni jumapili iliyopita
Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower akiimba moja ya sebene la bendi hiyo uku waimbaji wa Skylight wakendelea kuserebuka ndani ya Kiota cha Escape One Mikocheni
Mashabiki wa Bendi ya Skylight wakiendelea kulisakata Rhumba la nguvu kutoka katika bendi hiyo
Hii ni moja wapo ya Style mpya ya Bendi ya Skylight kama unataka kuijua basi jisogeze wewe na rafiki yako katika kiota cha Escape One uone mambo mapya kutoka katika bendi hiyo
Mashabiki wakicheza kwa kuzungusha duala hapa ni kukata mauno mpaka kieleweke

Mwimbaji wa Bendi ya Skylight,  Sony Masamba akiimba na kucheza na mashabi wao waliofika kijione mziki mkubwa wa bendi ya Skylight ndani ya Kiota Cha Escape One
Mashabiki na wapendi wa bandi wakiendelea kuserebuka na mziki mkali kutoka katika bendi ya Skylight maana tunasema usisubili kupewa raha jipe raha mwenyewe

Washindi wa Shindano la 'Genius-Cup' Wazawadiwa

0
0
Mwanafunzi Fuad Thabit kutoka Feza Boys Secondary aliyeibuka mshindi wa kwanza shule za sekondari katika Shindano la Genius-Cup akipokea cheti na zawadi yake ya shilingi 300,000 toka kwa  mgeni rasmi wa hafla hiyo, Ofisa Mkuu  wa Utafiti taasisi ya COSTECH, Athman Mgumia.

Viewing all 46194 articles
Browse latest View live




Latest Images