Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 665 | 666 | (Page 667) | 668 | 669 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati) akizungumza jambo na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick, wakati walipokuwa kwenye Hafla ya uzinduzi wa Mtandao mpya wa simu za Halotel Tanzania, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, jana usiku Okt 15, 2015.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri wa Mawasiliano wa Vietnam,Nguyen Bac Son, wakati walipokutana kwa mazungumzo kwenye hafla ya uzinduzi wa Mtandao mpya wa simu za Halotel Tanzania, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, jana usiku Okt 15, 2015.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri wa Mawasiliano wa Vietnam,Nguyen Bac Son, wakati walipokutana kwenye hafla ya uzinduzi wa Mtandao mpya wa simu za Halotel Tanzania, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, jana usiku Okt 15, 2015.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, Waziri wa Mawasiliano wa Vietnam,Nguyen Bac Son, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mtandao mpya wa simu za Halotel Tanzania, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, jana usiku Okt 15, 2015.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (wa tatu kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick (wa pili kushoto) Waziri wa Sayansi na Teknolojia) Makame Mbarawa (kushoto) Waziri wa Mawasiliano wa Vietnam, Nguyen Bac Son (wa tatu kulia) na wasaidizi wake (kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mtandao mpya wa simu za Halotel Tanzania, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, jana usiku Okt 15, 2015.

   Waziri wa Sayansi na Tknolojia, Makame Mbarawa, akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Makamu wa Rais,Dkt Bilal, kuzindua rasmi Halotel Tanzania katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jana usiku Okt 15, 2015.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa mtandao mpya wa simu za Halotel Tanzania, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jana usiku Okt 15, 2015.
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (katikati) akiwaongoza viongozi wenzake kupiga ngoma kama ishara ya uzinduzi rasmi wa Mtandao mpya wa mawasiliano wa Halotel Tanzania, wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, jana usiku Okt 15, 2015. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (katikati) akigonganisha glasi na baadhi ya viongozi wa Vietnam kama ishara ya furaha baada ya uzinduzi rasmi wa Mtandao mpya wa mawasiliano wa Halotel Tanzania, wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, jana usiku Okt 15, 2015.
    Picha ya pamoja baada ya uzinduzi huo.


  0 0

  HABARI ZILIZOTUFIKIA HIVI PUNDE:
  Aliye kuwa Mbunge wa jimbo la Ludewa na Mgombea wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM, Deo Filikunjombe (Pichani) amefariki dunia wakati akielekea kwenye jimbo lake akitokea jijini Dar es Salaam akiwa kwenye Chopa iliyoanguka jana katika hifadhi ya wanyama ya Selous iliyopo mkoa wa Morogoro. 

  Jeshi la Polisi limedhibitisha kutokea kwa ajali hiyo kuwa hakuna mtu aliyepona katika ajali hiyo.

  0 0    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini Kitabu cha Maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Marehemu, Pascal Mabiti, wakati wa shughuli ya Msiba iliyofanyika nyumbani kwa marehemu, Upanga jijini Dar es Salaam, leo Okt. 15, 2015.

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wanafamilia wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Marehemu Pascal Mabiti, wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu iliyofanyika nyumbani kwa marehemu Upanga jijini Dar es Salaam, leo Okt. 15, 2015.

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu marehemu, Pascal Mabiti, wakati wa shughuli za kuaga zilizofanyika nyumbani kwa marehemu, Upanga jijini Dar es Salaam, leo Okt. 15, 2015.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu marehemu, Pascal Mabiti, wakati wa shughuli za kuaga zilizofanyika nyumbani kwa marehemu, Upanga jijini Dar es Salaam, leo Okt. 15, 2015. Picha na OMR

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Mbeya mjini kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaombea kura wagombea wa nafasi za Urais , Ubunge na Udiwani.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Mbeya mjini ambapo aliwaambia Magufuli ni mchapakazi na yupo tayari kuleta mabadiliko ya kimaendeleo Tanzania.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Mbeya mjini ambapo aliwataka vijana kutohadaika na kudanganywa juu ya mabadiliko yanayodaiwa na upinzani na kusema kuwa hakuna njia ya mkato katika maisha ila ni kufanya kazi kwa bidii,aliwataka kuchagua viongozi kwa sifa za utendaji na si kwa misingi ya dini, ukabila ama rangi.
  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
  MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Mstaafu, Francis Mutungi alisema kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 25 kuweka kipaumbele cha amani ambayo isiweze kuharibiwa kwa kutokana na uchaguzi.

  Mtungi aliyasema hayo alipokutana na wahariri wa vyombo vya habari katika kusisitiza amani katika uchaguzi mkuu na kutaka waandishi kutumia kalamu vizuri kwani amani ikiharibika hakuna anayebaki salama.

  Amesema matatizo ambayo yameanza kutokea katika kamapeni yanayotokana na mtu mmoja yasiwekwe katika sura ya taifa na kuonekana vyombo vya serikali vinashindwa kusimamia.

  Jaji Mutungi amesema amani ikiangaliwa kwa jicho la karibu kwa kutambua kuna maisha baada  uchaguzi ambapo bila kufanya hivyo maisha hayatakuwepo.

  “Waandishi kwa kutumia kalamu zenu mtafanya nchi ibaki kuwa na amani kwani wananchi wanaamini vyombo vya habari kwa kila hatua inayotokea katika uchaguzi mkuu”amesema Mutungi.

  Aidha amesema amevitaka vyama vya siasa kutambua wajibu na sio kuangalia uchaguzi huru na haki kwani wajibu ndio utafanya vitu view salama na kuweza kuvuka suala hili la uchaguzi mkuu.
   Msajili wa Vyama vya Siasa nchini,Jaji Mstaafu,Francis Mutungi akizungumza  mkutano wa wahariri na waandishi (hawapo pichani) juu ya amani kuelekea uchaguzi mkuu 25 ,uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.
   Wahariri na waandishi wa habari wakimsikilia Msajili wa Vyama vya Siasa nchini,Jaji Mstaafu,Francis Murungi hayupo pichani katika mkutano wake uliofanyika jijini Dar es Salaam.
  Wahariri na waandishi wa habari wakiwa katika picha ya pamoja na Msajili wa Vyama Siasa nchini,Jaji Mstaafu Francis Mutungi,jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
  RAIS  DK.Jakaya Kikwete ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kufanya tathimini upya kwa wakazi wa vijiji vitatu wanaopisha bandari ya Bagamoyo.

  Dk.Kikwete ameyasema hayo leo  Bagamoyo wakati wa kuweka jiwe la msingi la uzinduzi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ,amesema kuwa wananchi wasiondoke katika maeneo yao wakiwa na manunguniko.

  Amesema kuwa mradi wa ujenzi ni mkubwa hivyo wananchi wanatakiwa kupewa haki yake kutokana na eneo ikiwa pamoja na kujengewa nyumba katika kuanza upya kwa makazi ya Kidagoni.

  Rais Kikwete amesema mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo umekuja wakati mwafaka kwa kuongeza fursa nyingi baada ya kukamilika kwa mradi huo na kuongeza uchumi wa nchi.

  Aidha ameiagiza Mthamini wa Halmashauri  kutafutiwa sehemu nyingine kutokana na kufanya tathimini isiyoendana na malipo hali ya wakazi hao ambao wameachia eneo hilo kwa ajili ya uchumi.

  “Nchi haiwezi kuwa safi kuwepo mradi mkubwa wa bandari kubwa Afrika lakini wananchi waliocha eneo hilo wakiwa wananungunika kwa kupuchwa mali zao kwa ajili ya mtu mmoja tu”amesema  Rais Jakaya. 
   Rais Dk.Jakaya Kikwete akizungumza leo  wananchi wa Bagamoyo katika  hafla ya  kuweka jiwe la msingi la uzinduzi wa Bandari ya Bagamoyo.
   Rais Dk.Jakaya Kikwete akifungua pazia kwa kuweka jiwe la msingi la uzinduzi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo leo.
   Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akizungumza leo  wananchi wa Bagamoyo katika  hafla ya  kuweka jiwe la msingi la uzinduzi wa Bandari ya Bagamoyo.

  Waziri wa Uchukuzi,Samwel Sitta akizungumza  leo wananchi wa Bagamoyo juu ya ujenzi wa bandari ya Bangamoyo. 
  Makamu wa Rais Mtendaji wa  Umoja wa Wafanyabiashara wa China, Dk.Hu Jianhua akizungumza katika uzinduzi wa Bandari ya Bagamoyo leo. 
   Sehemu ya viongozi wa waliohudhuria uwekaji wa jiwe la la msingi na uzinduzi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo  leo.
   Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha na viongozi mbalimbali baada ya kuweka jiwe la msingi na ujenzi wa  bandari ya bagamoyo leo.
  Baadhi ya wananchi wa Bagamoyo waliohudhuria uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bandari ya Bagamoyo.
  ( Picha na Emmanue Massaka wa Globu ya Jamii)

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa jengo jipya la makao makuu ya NMB na tawi jipya la NMB Private Banking kwenye jengo la makao makuu ya NMB jana jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia tukio hilo ni Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa NMB – Prof. Joseph Semboja(kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa NMB – Ineke Bussemaker (wapili kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam – Saidi Meck Sadiki (kulia) pamoja na wafanyakazi wa NMB.


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Jakaya Kikwete akifurahia zawadi aliyokabidhiwa na Mkurugenzi wa NMB – Ineke Bussemaker (kushoto) jana katika hafla ya ufunguzi wa jengo jipya la makao makuu ya NMB na tawi jipya la wateja maalumu (NMB Private Banking) iliyopo ndani ya jengo jipya la NMB. 
   Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania – Dr. Jakaya Kikwete katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa NMB – Idara ya huduma kwa wateja. Raisi Kikwete alikuwa anakagua Jengo jipya la NMB ambao ndimo makao makuu mapya ya benki hiyo kubwa kuliko zote nchini.

  Raisi Jakaya Mrisho Kikwete amezindua rasmi jengo jipya na la kisasa kabisa ambalo ni makao makuu mapya ya NMB lenye ghorofa saba huku likiwa na uwezo wa kubeba wafanyakazi zaidi ya 800. Mbali na uzinduzi wa jengo hilo, Raisi Kikwete pia alizindua tawi jipya la benki lililo ndani ya jengo jipya la NMB.

  Uzinduzi wa jengo la makao makuu ya NMB ni mwendelezo wa maadhimisho ya Miaka 10 ya NMB ambayo yameadhimishwa kwa mafanikio makubwa. Baadhi ya mafanikio ya benki hiyo ni pamoja na kukuza mtaji wake mpaka kuwa benki kubwa na bora kuliko zote nchini huku ikiwekeza vya kutosha katika tekinolijia ya mawasiliano inayowezesha benki kumudu kutoa huduma bora na karibu zaidi ya wateja wake.

  NMB wakati inabinafsishwa mwaka 2005, ilikuwa na matawi chini ya 100, huku ikiwa haina ATM hata moja na wateja si zaidi ya 600,000, hii leo inapoadhimisha miaka 10 tangu kubinafsishwa, imefikisha matawi 173 na ATM zaidi ya 600 huku ikifikisha wateja hai zaidi ya milioni mbili na huduma zake zikienea mpaka vijijini.


  Raisi kikwete aliipongeza NMB na kusema kuwa serikali inajivunia benki hiyo huku akiahidi kuwa serikali inaitunza benki kama mboni ya jicho na haina mpango wa kuuza hisa zake. Serikali ina hisa asilimia 32.

  0 0

  Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Mohamed Shein akimnadi Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli mbele ya maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja,kisiwani Unguja jioni ya leo.

  Dkt Shein emebainisha wazi kwenye mkutano huo wa kampeni kuwa Dkt Magufuli ni mtu sahihi na anatosha kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,amesema kuwa iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano atashirikiana nae kwa kila jambo kuhakikisha Tanzania inapiga hatua zaidi kimaendeleo.
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja,kisiwani Unguja jioni ya leo.
  Sehemu ya umati wa wakazi wa Kisiwani Unguja na vitongoji vyake wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja mjini humo,ambapo Mgombea Urasi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufui aliwahutubia.
  Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Mohamed Shein akimsikiliza kwa makini Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli kabla ya kupanda jukwaani na kuwahutubia maelfu ya wakazi wa kisiwani Unguja kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja,kisiwani humo.
  Wananchi wa kiswani Unguja wakishangilia jambo kwenye mkutano huo wa kampeni.
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja,kisiwani Unguja jioni ya leo.
  Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Mh Al Hassan Mwinyi  akiwahutubia Wananchi (hawapo pichani) ,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja,kisiwani Unguja jioni ya leo.
  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini,Ndugu Boraafya Silima akizungumza machache kwenye mkutano wa kampeni kabla ya kumkaribisha Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli kuwahutubia wananchi wa kisiwani Unguja.

  Nyomi la wakazi wa Kisiwani Unguja ndani ya mkutano wa kampeni.
  Sehemu ya umati wa wakazi wa kisiwani Unguja na vitongoji vyake wakiwa  wamekusanyika kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja,kisiwani Unguja jioni ya leo.
  Baadhi ya Wafuasi wa chama hicho wakishangilia jambo kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli
  Wadau wakifuatilia mkutano wa kampeni ndani ya uwanja wa Mnaji Mmoja kisiwani Unguja.
  Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Mh Al Hassan Mwinyi  akiwahutubia Wananchi (hawapo pichani) ,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja,kisiwani Unguja jioni ya leo.

  wakifuatilia mkutano wa kampeni.
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano Dkt Jonh Pombe Magufuli akiwapungia wananchi wa Kisiwani Unguja (hawapo pichani),alipokuwa akiwasili kwenye mkutano wa kampeni katika viwanja vya Mnazi Mmoja mjini humo.
  Balozi Seif Ali Iddi akiwahutubia wananchi wa Kisiwani Unguja kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja.

  Baadhi ya Wafuasi wa chama hicho wakifurahia jambo kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli
  Sehemu ya umati wa wakazi wa kisiwani Unguja na vitongoji vyake wakiwa  wamekusanyika kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja,kisiwani Unguja jioni ya leo.
  Wananchi wa Kisiwani Unguja wakifuatilia mkutano wa kampeni ndani ya viwanja vya Mnazi Mmoja.

  0 0

  Pichani Kulia ni Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akimnadi aliyekuwa Mgombea Ubunge wa jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe (enzi za uhai wake),wakati Dkt Mgufuli alipopita kwenye jimbo hilo wakati wa kampeni
   
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amepokea kwa mshtuko na huzuni nyingi taarifa za vifo vya Mbunge wa Jimbo la Ludewa, mkoani Njombe Ndugu Deo Filikunjombe Haule, Kepteni William Silaa pamoja na abiria wengine wawili ambao wameaga dunia jana, Alhamisi, Oktoba 15, 2015 kwa ajali ya helkopta iliyotokea katika eneo la Hifadhi ya Selous mkoani Morogoro.

  Katika salamu za rambirambi ambazo amewatumia Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Ndugu Deo Sanga, na Meya wa Manispaa ya Ilala Mstahiki Jerry Silaa, Dkt. Magufuli amesema: “Kwa hakika, nimeshtushwa na kuhuzunishwa mno na taarifa za vifo vya Ndugu Filikunjombe na Ndugu Silaa ambavyo nimetaarifiwa kuwa vimetokea kwa ajali ya helkopta aliyokuwa akiitumia Ndugu Filikunjombe kwa Kampeni zake za Ubunge katika jimbo hilo la Ludewa.

  Katika salamu zake hizo za rambirambi Dkt. Magufuli ameongeza kuwa: “Kama unavyojua, namfahamu vizuri Ndugu Filikunjombe. Alikuwa Mbunge mwenzangu katika Bunge lililomaliza muda wake mwaka huu. Nimefanya kazi naye  kwa karibu na kwa miaka mitano ndani ya bunge letu. 

  Alikuwa mtumishi hodari, mtumishi mwaminifu na mwadilifu kwa wananchi wa Tanzania, na hasa wananchi wa Jimbo la Ludewa, ambao aliwawakilisha kwa miaka mitano iliyopita akiwa Mbunge wao. Hata nilipofanya ziara ya kampeni katika jimbo lake la Ludewa mwezi uliopita nililala nyumbani kwake, hiyo inaonesha nilivyokuwa karibu naye. Tutakosa utumishi wake mahiri sana.”

  Salamu zake za rambirambi  kwa Mstahiki Meya Jerry Silaa, Dkt. Magufuli amesema: “Nimesikitishwa sana na taarifa ya kifo cha Baba yako Kepteni William Silaa, kwani ni tukio lisilozoeleka. Ni jana tu nimeshiriki nawe katika kampeni kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa 2015 katika jimbo unalogombea Ubunge, jimbo la Ukonga, naungana nawe katika kipindi hiki kigumu cha msiba mkubwa. Nakupa pole wewe binafsi, familia yenu, ndugu, jamaa na marafiki wote”.

  Aidha aliongeza “Nakutumia wewe Ndugu Sanga, Mwenyekiti wetu wa CCM mkoa wa Njombe salamu za rambirambi za dhati ya moyo wangu kuomboleza kifo cha Ndugu Filikunjombe na abiria hao wengine. Aidha, kupitia kwako namtumia rambirambi nyingi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Anna Semamba Makinda na Wabunge wote kwa kuondokewa na mwenzao.”

  Dkt. Magufuli ameongeza “Nakuomba pia unifikishe salamu zangu za rambirambi kwa wananchi wa Jimbo na Wilaya ya Ludewa ambao wamepoteza Mbunge wao aliyewatumikia kwa ustadi mkubwa kwa kipindi chote. Aliwawakilisha vizuri na kujali sana maslahi yao. “Ametuma pia salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa Ndugu Filikunjombe kwa kuondokewa na mhimili wa familia na rafiki yao mpenzi.

  Amewaombea kwa Mwenyezi Mungu awape subira na nguvu ya uvumilivu katika kipindi hiki kigumu na cha majonzi. Pia naungana nao kumwomba Mwenyezi Mungu aziweke pema peponi roho ya Deo Filikunjombe Haule”. Amen.

  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano
  CCM Ofisi Ndogo, Lumumba
  DAR ES SALAAM.
  16 Oktoba, 2015

  0 0


  Asakari polisi na wataalamu wakikagua mabaki ya chopa namba  5Y-DKK iliyoanguka jana jioni ikitokea Dar kuelekea Ludewa sehemu ya hifadhi ya wanyama ya Selous ambapo Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe, rubani Capt. William Slaa na abiria wengine wawili - Casablanca Haule na Ngondombwitu Nkwera - walipoteza maisha.
   Timu ya waokoaji wakibeba mabaki ya miili ya marehemu
   Askari wakiwa eneo la ajali 


  Mbunge wa Ludewa Mhe Deogratias Haule Filikunjombe (chini) amefariki dunia katia ajali ya Chopa katika hifadhi ya wanyama ya Selous, pamoja na rubani Kepteni William Silaa (juu kulia), mfanyakazi wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa na ndugu yake Marehemu Filikunjombe ambao majina  hayajapatikana mara moja.

  Mhe. Deo Filikunjombe, rubani na  na abiria wengine walipata matatizo ya engine ya chopa namba  5Y-DKK jana jioni wakitokea Dar kuelekea Ludewa.

  Kwa mujibu wa Meya wa Ilala aliyemaliza muda wake Mhe Jerry Silaa, ambaye ni mtoto wa rubani, hakuna mtu aliyenusurika katika ajali hiyo ya Chopa. 

  "Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa rasmi kutoka kwa timu ya uokoaji kuwa imefanikiwa kufika eneo la ajali na kukuta abiria wote na rubani wamepoteza maisha.
  "Ni mepoteza Baba na rubani mzuri wa nchi yetu Capt. William Silaa.
   Nimepoteza rafiki na kiongozi wangu Mhe. Deo Filikunjombe. Nawapa pole wote waliopoteza ndugu zao. Nawaombea marehemu mapumziko ya Amani. Nawashukuru wote walioshirikiana na familia kusaidia uokozi", amesema Mhe Jerry Silaa katika kurasa zake za mitandaoni.

  tangia jana habari za kuanguka kwa nchopa hiyo zilitapakaa kila kona na katika mitandao, na kuendelea hadi leo tangia asubuhi hadi baada ya ujumbe wa Jerry Silaa kupatikana mchana huu.


  0 0


  0 0

  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura akizungumza katika hafla fupi iliyowakutanisha baadhi ya wateja wa kampuni hiyo na maofisa wa TTCL kubadilishana uzoefu na kupata maoni ya wateja wao jana jijini Dar es Salaam Double Tree by Hilton Hotel. Tukio hili ni mwendelezo wa Wiki ya Huduma kwa wateja wa Kampuni ya simu ya TTCL iliyozinduliwa hivi karibuni.
  Baadhi ya wateja, wafanyakazi wa TTCL wakibadilishana mawazo kwenye  hafla fupi iliyowakutanisha baadhi ya wateja wa kampuni hiyo na maofisa wa TTCL kupata maoni juu ya huduma wanazopatiwa na kampuni hiyo.
  Ofisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota akizungumza kwenye hafla hiyo iliyokutanisha baadhi ya wateja wa kampuni hiyo na maofisa wa TTCL kubadilishana uzoefu jana jijini Dar es Salaam Double Tree by Hilton Hotel.
  Baadhi ya wateja, wafanyakazi wa TTCL wakibadilishana mawazo kwenye  hafla fupi iliyowakutanisha baadhi ya wateja wa kampuni hiyo na maofisa wa TTCL kupata maoni juu ya huduma wanazopatiwa na kampuni hiyo.
  Baadhi ya wateja, wafanyakazi wa TTCL wakibadilishana mawazo kwenye  hafla fupi iliyowakutanisha baadhi ya wateja wa kampuni hiyo na maofisa wa TTCL kupata maoni juu ya huduma wanazopatiwa na kampuni hiyo.
  Meneja wa Kitengo cha Habari na Mausiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Thomas Mushi akizungumza kwenye hafla hiyo iliyokutanisha baadhi ya wateja na maofisa wa TTCL kubadilishana uzoefu jana jijini Dar es Salaam Double Tree by Hilton Hotel.
  Mmoja wa wateja wa TTCL akitoa maoni yake juu ya huduma zinazotolewa na kampuni hiyo kwa wateja wake.
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kulia) akigonganisha glasi ya mvinyo na baadhi ya wageni waalikwa kwenye hafla fupi ya baadhi ya wateja wa kampuni hiyo na maofisa wa TTCL kubadilishana uzoefu na kupata maoni ya wateja wao jana jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya maofisa wa TTCL, wateja na wageni waalikwa wakibadilishana mawazo kwenye  hafla fupi iliyowakutanisha baadhi ya wateja wa kampuni hiyo na maofisa wa TTCL kupata maoni juu ya huduma wanazopatiwa na kampuni hiyo.
  Ofisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota (kushoto) akizungumza jambo na mmoja wa wanahabari kwenye hafla hiyo iliyokutanisha baadhi ya wateja na maofisa wa TTCL kubadilishana uzoefu jana jijini Dar es Salaam Double Tree by Hilton Hotel.
  Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja TTCL, Laibu Leonard akizungumza kwenye hafla hiyo ya baadhi ya wateja wa kampuni hiyo na maofisa wa TTCL kubadilishana uzoefu jana jijini Dar es Salaam Double Tree by Hilton Hotel.


  0 0

  chopa
  Aliyekuwa Mbunge wa Ludewa kwa tiketi ya CCM, Deogratias Filikunjombe, enzi za uhai wake akipanda chopa yake.
  Nakupenda Deo
  Nimesikitishwa sana na kifo chako. Kweli kifo kipo na kila mmoja wetu atakipitia lakini cha aina hii, cha kijana aliyekuwa akipigania watu wake kiasi hiki? Kinaumiza sana, hata hivyo, hatuna budi zaidi ya kukubali kuwa Deo Filikunjombe, jembe la mkono limeondoka.
  chopa 2
  Chopa iliyosababsha kifo cha Filikunjombe, Capt. William Silaa na watu wengine wawili.
  Nasema kutoka ndani ya moyo wangu, taifa limepoteza mtu muhimu sana, hakusita kupigania alichokiamini bila uoga wala hofu! Wakati mwingine alitofautiana na msimamo wa chama chake kwa maslahi ya Watanzania maskini, kwako ukweli ulikuwa nguzo. Nenda Deo, nenda kapumzike muda si mrefu tutaungana nawe, kila mwanadamu atafariki dunia maana ndivyo ilivyoandikwa.
  Lakini cha muhimu ni mtu atakuwa anafanya nini wakati anakufa! Je, atakuwa akiiba au akifanya uzinzi? Deo umekufa ukitumikia watu wako, umekufa kifo chema na Wanaludewa watakuombea. Nenda Deo, pumzika Deo, mema yako yamekutangulia.
  Hayo ndyo yatakutetea mbele ya Maulana! Mwisho nasema kwa uchungu na ninakuahidi, pale ulipoishia, sisi tutaendelea bila kujali tupata nini mpaka siku moja wananchi wa taifa hili wafaidi mema ya nchi yao.

  Nenda Deo, kapumzike kwa amani, umekufa katika mapambano. Natoa pole kwa familia yako, mkeo, watoto, wazazi na wananchi wote wa Jimbo la Ludewa, msiumie sana, Mungu anajua ni kwa nini ameamua jambo hili litokee. Naamini Deo yuko mahali sahihi, kutokana na kile alichokuwa akikifanya wakati anakutwa na mauti, kwetu sisi, kibinadamu ni maumivu lakini kiimani, Deo yuko mahali salama. Nenda kaka Deo. Pumzika kwa amani kaka!
  Eric James Shigongo,


  Mkurugenzi, Global Publishers Ltd.
  Nenda kamanda wangu Deo

  JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS!

  0 0

  Jana Ijumaa ya Octoba 16,2015 Baraza Kuu la Waislamu Mkoa wa Mwanza liliungana na Waislamu wengine kuadhimisha mwaka mpya wa Kiislamu ambao ni 1437. 
  Kwa kalenda ya Kiislamu sherehe hizo zilifanyika jana tarehe mbili, mwezi Muharamu mwaka wa 1437 (02.01.1437) ikiwa maadhimisho yanayoambatana na kumbukumbu ya Kuhama kwa Mtume Muhammad kutoka Mji wa Macca kwenda Madina.

  Katika kuadhimisha sherehe hizo, Baraza hilo kupitia kwa Katibu wake Mkoani Mwanza Sheikh Mohamed Balla (Kulia Pichani) alitoa tamko kwa niaba ya Waislamu wote Mkoani Mwanza kutokana na kauli inayoelezwa kutolewa na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima kwamba ana ndoto ya Misikiti yote nchini kugezwa kuwa Sunday School na Masheikh watakwenda kuangukia katika misalaba. 

  Alisema kauli za namna hiyo si njema kwa mstakabali wa Taifa ambapo alisema kuwa Waislamu wote Mkoani Mwanza wanalaani na kukemea kauli hiyo na nyingine zote za aina hiyo na wale wanaozitoa.

  Aliwataka Watanzania kuungana kwa pamoja hususani katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu na kwamba Wamchague kiongozi muadilifu, Mchapakazi na anaechukia rushwa ambae ataendelea kuwaunganisha watanania wote. 
  Imam wa Msikiti Khadija Jijini Mwanza Mohammed Awadhi akisoma Ibada ya Quran katika Sherehe za Mwaka mpya wa Kiislamu ulioadhimishwa jana katika Uwanja wa Mbugani Jijini Mwanza na kuambatana na ibada mbalimbali ikiwemo kuliombea taifa amani.

  Sheikh Mahamood Khasan akisoma ibada ya kuliombea taifa amani katika Sherehe za Mwaka mpya wa Kiislamu ulioadhimishwa jana katika Uwanja wa Mbugani Jijini Mwanza na kuambatana na ibada mbalimbali ikiwemo kuliombea taifa amani.
  Imam wa Msikiti wa Ibadhi Jijini Mwanza Nouh Othman akisoma mada juu ya mwaka mpya wa kiislamu wa 1437 katika Sherehe zilizofanyika jana katika Uwanja wa Mbugani Jijini Mwanza na kuambatana na ibada mbalimbali ikiwemo kuliombea taifa amani.
  Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Mwanza na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuendeleza Quran na Sunna nchini JUQUSUTA Sheikh Hassan Kabeke akiwasilisha mada juu ya amani katika Sherehe za Mwaka mpya wa Kiislamu ulioadhimishwa jana katika Uwanja wa Mbugani Jijini Mwanza na kuambatana na ibada mbalimbali ikiwemo kuliombea taifa amani.
  Qaswida
  Qaswida
  Waumini wa dini ya kiislamu wakiwa katika Sherehe za Mwaka mpya wa Kiislamu ulioadhimishwa jana katika Uwanja wa Mbugani Jijini Mwanza na kuambatana na ibada mbalimbali ikiwemo kuliombea taifa amani.
  Waumini wa dini ya kiislamu wakiwa katika Sherehe za Mwaka mpya wa Kiislamu ulioadhimishwa jana katika Uwanja wa Mbugani Jijini Mwanza na kuambatana na ibada mbalimbali ikiwemo kuliombea taifa amani.
  Waumini wa dini ya kiislamu wakiwa katika Sherehe za Mwaka mpya wa Kiislamu ulioadhimishwa jana katika Uwanja wa Mbugani Jijini Mwanza na kuambatana na ibada mbalimbali ikiwemo kuliombea taifa amani.
  Waumini wa dini ya kiislamu Mkoani Mwanza wakiwa katika Sherehe za Mwaka mpya wa Kiislamu (1437) ulioadhimishwa jana katika Uwanja wa Mbugani Jijini Mwanza na kuambatana na ibada mbalimbali ikiwemo kuliombea taifa amani.
  Waumini wa dini ya kiislamu Mkoani Mwanza wakiwa katika Sherehe za Mwaka mpya wa Kiislamu (1437) ulioadhimishwa jana katika Uwanja wa Mbugani Jijini Mwanza na kuambatana na ibada mbalimbali ikiwemo kuliombea taifa amani.
  Waumini wa dini ya kiislamu Mkoani Mwanza wakiwa katika Sherehe za Mwaka mpya wa Kiislamu (1437) ulioadhimishwa jana katika Uwanja wa Mbugani Jijini Mwanza na kuambatana na ibada mbalimbali ikiwemo kuliombea taifa amani.
  Waumini wa dini ya kiislamu Mkoani Mwanza wakiwa katika ibada ya Sherehe ya Mwaka mpya wa Kiislamu (1437) ulioadhimishwa jana katika Uwanja wa Mbugani Jijini Mwanza na kuambatana na ibada mbalimbali ikiwemo kuliombea taifa amani.
  Waumini wa dini ya kiislamu Mkoani Mwanza wakiwa katika ibada ya Sherehe ya Mwaka mpya wa Kiislamu (1437) ulioadhimishwa jana katika Uwanja wa Mbugani Jijini Mwanza na kuambatana na ibada mbalimbali ikiwemo kuliombea taifa amani.
  Waumini wa dini ya kiislamu Mkoani Mwanza wakiwa katika ibada ya Sherehe ya Mwaka mpya wa Kiislamu (1437) ulioadhimishwa jana katika Uwanja wa Mbugani Jijini Mwanza na kuambatana na ibada mbalimbali ikiwemo kuliombea taifa amani.
  Waumini wa dini ya kiislamu Mkoani Mwanza wakiwa katika ibada ya Sherehe ya Mwaka mpya wa Kiislamu (1437) ulioadhimishwa jana katika Uwanja wa Mbugani Jijini Mwanza na kuambatana na ibada mbalimbali ikiwemo kuliombea taifa amani.
  Waumini wa dini ya kiislamu Mkoani Mwanza wakiwa katika ibada ya Sherehe ya Mwaka mpya wa Kiislamu (1437) ulioadhimishwa jana katika Uwanja wa Mbugani Jijini Mwanza na kuambatana na ibada mbalimbali ikiwemo kuliombea taifa amani.
  Waumini wa dini ya kiislamu Mkoani Mwanza wakiwa katika ibada ya Sherehe ya Mwaka mpya wa Kiislamu (1437) ulioadhimishwa jana katika Uwanja wa Mbugani Jijini Mwanza na kuambatana na ibada mbalimbali ikiwemo kuliombea taifa amani.
  Waumini wa dini ya kiislamu Mkoani Mwanza wakiwa katika ibada ya Sherehe ya Mwaka mpya wa Kiislamu (1437) ulioadhimishwa jana katika Uwanja wa Mbugani Jijini Mwanza na kuambatana na ibada mbalimbali ikiwemo kuliombea taifa amani.

  0 0


  0 0

  Mkuu wa Shule ya Sekondari Mkolani iliyopo Jijini Mwanza Mwl.Asensio Mathias (Mwenye Kinasa Sauti) akizungumza katika Mahafali ya 14 ya Kidato cha Nne katika shule hiyo yaliyofantika jana Octoba16,2015 katika Ukumbi wa Shule hiyo.
  Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 14 ya kidato cha Nne Mkolani Sekondari ya Jijini Mwanza Ndg.Bituro Kazeri (Wa tatu kila upande) ambae ni Afisa Habari wa Taasisi ya Sayansi ya Jamii TASAJA akijiandaa kuwakabidhi vyeti wahitimu wa shule hiyo katika Mahafali yaliyofanyika jana shuleni hapo
  Wahitimu wa Kidato cha Nne wakipokea Vyeti katika Mahafali ya 14 ya Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Mkolani iliyopo Jijini Mwanza yaliyofanyika jana shuleni hapo
  Wahitimu wa Kidato cha Nne wakipokea Vyeti katika Mahafali ya 14 ya Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Mkolani iliyopo Jijini Mwanza yaliyofanyika jana shuleni hapo

  Meza Kuu
  Mahafali ya 14 ya kidato cha nne Mkolani Sekondari Jijini Mwanza
  Wazazi/Walezi
  Wazazi/Walezi
  Wazazi/Walezi
  Wazazi/Walezi
  Mwonekano ndani ya Ukumbi
  Wahitimu katika Ubora wao
  Mshereheshaji Mwl.Isaack Wakuganda
  Ukumbini
  Ukumbini
  Kumbukumbu
  Vijana katika ubora wao
  Binagi Media Group, Kwa Pamoja Tuijuze Jamii

  0 0

   Mkurugenzi wa Mipango na Maendeleo ya Biashara, Mhandisi Kato Kabaka (aliyesimama) kutoka Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania, akitoa elimu ya nishati ya Jotoardhi kwa wafanyakazi wa hifadhi ya wanyamapori Selous na jinsi gani nishati hiyo itaongeza idadi ya watalii.
   Wafanyakazi wa hifadhi ya wanyamapori Selous na kampuni ya uendelezaji wa Jotoardhi Tanzania wakimsikiliza kwa makini Mhandisi Kato Kabaka (hayuko pichani) alipokuwa akiwaelimisha namna nishati ya Jotoardhi itakavyoongeza idadi ya watalii kupitia mabwawa ya kuogelea ya maji moto yatakayojengwa ndani ya hifadhi hiyo.

  Bwana Eneck Majahasi (aliyesimama) akihitaji ufafanuzi ikiwa mitambo ya uzalishaji wa nishati ya Jotoardhi itakayojengwa ndani ya hifadhi ya Selous haitakuwa na madhara kwa wanyamapori walioko ndani ya hifadhi.


  Na. Lilian Lundo - Maelezo

  Kuendelezwa kwa nishati ya Jotoardhi Tanzania itaipelekea kupanda hadhi kwa hifadhi ya wanyamapori Selous.


  Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Mipango na Maendeleo ya Biashara, Mhandisi Kato Kabaka kutoka Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania wakati akizungumza na wafanyakazi wa hifadhi ya wanyamapori Selous, kambi ya Matambwe alipokuwa akitoa elimu ya nishati ya Jotoardhi yenye viashiria (majimoto) ndani ya hifadhi hiyo, leo.


  “Kama utafiti utaonyesha chanzo cha nishati ya Jotoardhi kipo ndani ya hifadhi, basi nishati hiyo itapelekea hifadhi ya Selous kuongeza idadi ya watalii kwa kujenga mabwawa ya kuogelea yatakayokuwa na maji ya moto na kujenga vibwawa vidogo ndani ya vibanda vya kupumzikia kwa ajili ya kuweka miguu wageni watakao kuwa wakitembelea hifadhi hiyo.” Alisema Mkurugenzi Kato.


  Mkurugenzi Kato aliongeza kwa kusema kuwa, mabwawa ya maji moto yatakuwa ni utalii mwingine ambao utakuwa umeongezeka ndani ya hifadhi ya Selous, kwani watalii watakapokuja kuangalia wanyama watapata fulsa ya kupumzika ndani ya mabwawa ya maji ya moto.


  Bwana Eneck Majahasi, mfanyakazi wa hifadhi ya Selous alihitaji ufanunuzi kama hakutakuwa na madhara kwa wanyamapori ikiwa mitambo ya uzalishaji wa nishati ya Jotoardhi itajengwa ndani ndani ya hifadhi.


  “Kwa sasa kampuni inafanya utafiiti, utakapokamilika wataalam kutoka Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania na hifadhi ya wanyamapori Selous wataenda kujifunza namna ambavyo nchi nyingine zimefanikiwa kuzalisha nishati ya Jotoardhi ndani ya hifadhi za wanyamapori,” Alijibu Mkurugenzi Kato.  Akiongeza kujibu swali hilo, Afisa Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma Bi. Johary Kachwamba alisema kuwa nchi ya Kenya imefanikiwa kuvuna zaidi ya megawati 550 za  umeme unaotokana na Jotoardhi na asilimia kubwa ya mitambo ya uzalishaji ipo ndani ya hifadhi za wanyamapori zilizopo maeneo ya Olkaria nchini Kenya. Hivyo Tanzania haina budi kujifunza kutoka Kenya na kufanya vizuri zaidi.


  Bwana Tipa Lazaro mfanyakazi wa hifadhi ya wanyamapori Selous aliipongeza timu nzima ya Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania kwa elimu nzuri waliyoitoa juu ya nishati ya Jotoardhi na kusema kuwa wafanyakazi wa hifadhi ya Selous hawana pingamizi lolote juu ya uendelezaji wa utafiti huo ndani ya hifadhi. Kwani kukamilika kwa mradi huo ni mafanikio makubwa kwa taifa la Tanzania.


  Serikali ya Tanzania kupitia TANESCO ilisajili kampuni ya kuendeleza nishati itokanayo na Jotoardhi nchini. Mpaka sasa kampuni hiyo imegundua zaidi maeneo 50 yenye viashiria vya Jotoardhi hapa nchini. Maeneo hayo yamegawanyika katika kanda nne, ambazo ni kanda ya kaskazini, kanda ya kusini, kanda ya magharibi na kanda ya mashariki inayohusisha Utete(Pwani), Luhoi(Pwani) na Kisaki(Morogoro) ilipo hifadhi ya Selous.
  0 0

  Baada ya kumalizika kwa mkutano wa Viongozi TEHAMA Nchini Kenya Vyombo kadhaa vya habari vimepata Kunihoji ikiwa ni pamoja na Radio One - Kupitia African Panorama.
  Ambapo nimetolea ufafanuzi wa key take a ways kwenye mkutano na hasa kubobea kwenye eneo langu la utaalam ambapo ndio mijadala niliyo jadili - Usalama mitandao.

  0 0

  Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu (wa pili kutoka kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu namna Serikali  inavyoshughulikia madai ya watumishi walio katika Serikali za Mitaa wasio walimu. 

  Na Magreth   Kinabo-maelezo
  SERIKALI  imetenga  kiasi cha fedha cha  Sh. bilioni tano ( 5.93) ikiwa ni madeni ya mishahara ya  Watumishi wa Mamlaka za Serikali za  Mitaa(TALGWU) na  Sh. bilioni nne(4) kwa ajili ya kulipa madeni  ya yasiyohusu mishahara, fedha ambazo zitalipwa Oktoba mwaka huu.

  Kauli hiyo ya Serikali imetolewa leo na  Kaimu  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, HAB  Mkwizu  wakati akizungumza  na waandishi wa habari kuhusu  madai na madeni  ya watumishi hao  kwenye  ukumbi  wa  Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dares Salaam.

  Aidha Serikali imefafanua kwamba madai ya watumishi hao yanayohusu mishahara mpaka kufikia Oktoba Mosi,mwaka huu,ambao si walimu   malimbikizo yake yalikuwa takribani Sh. bilioni 6.147,  na idadi ya watumishi wanaodai ni 5,695  katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2015/2016.

  Hivyo hadi kufikia Oktoba , mwaka huu Serikali ilikuwa  imewalipa watumishi 1,551 wakiwemo wa Serikali za Mitaa jumla ya Sh. bilioni 1.6 na malipo hayo  hayajumuishi yale yaliyofanyika kwa walimu.
  “Aidha Watumishi  wa Serikali  za Mitaa wapatao  455 wenye madai  ya Sh. milioni 593.2 watalipwa mwezi  Oktoba, mwaka huu. Madai yaliyosalia yataendelea  kulipwa  kila mwezi kadri uhakiki unavyokamilika,” alisema Kaimu Katibu Mkuu huyo.  

  Alisema  kwa upande wa madai  yasiyohusu mishahara , ambayo yamekuwa yakilipwa  kupitia fungu la Matumizi  Mengineyo, madai ya kiasi  Sh. bilioni 18 yalikwishahakikiwa na yanasubiri kulipwa.  

  Mkwizu aliongeza kwamba  madeni hayo  ya watumishi hao ni yale  yaliyolimbikizwa hadi mwaka  2012/2013.
  “ Serikali imepanga kulipa deni hilo lote katika kipindi cha kuanzia Oktoba 2013 hadi Januari,2016,kwa kuanzia Oktoba 2015 Serikali imetenga kiasi cha Sh. bilioni 4 na kiasi cha sh. bilioni 14 kitakachosalia kitalipwa kwa awamu ndani ya kipindi kilichopangwa,” alisisitiza.

  Aidha Kaimu Katibu Mkuu huyo alisema wakati wa kutekeleza malipo hayo, waajiri wameaagizwa kuwaandikia barua watumishi ambao madai yao yamekataliwa au kupunguzwa ili kuwafahamisha sababu za kutakataliwa  kwake na hivyo kuwawezesha kuwa na taarifa sahihi kuhusu madai  yao na kuondoa uwezekano wa kudai mara nyingine.

   Akizungumzia kuhusu suala la uhakiki wa madeni alisema  kwa upande wa madai yasiyohusu mishahara yalikuwa ni sh.  bilioni 18,lakini baada ya kuhakikiwa yakafikia Sh. bilioni 14.

   Alizitaja sababu mbalimbali za kukataliwa  baadhi ya madeni hayo  kuwa ni  zipo tofauti na zinatokana na kutofuata  sheria, kanuni na taratibu.


  0 0


  EAST AFRICAN COMMUNITY  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


  KUNDI la waangalizi wa uchaguzi Mkuu nchini Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki, wanatarajia kuwasili Dar es Salaam Jumapili, tarehe 18 October  2015 tayari kwa uangalizi wa uchaguzi kwa upande wa Tanzania Bara na Visiwani.


  Kuwasili kwa kundi la Jumuiya ya Afrika Mashariki lenye takribani watu hamsini na tano, ni kuitikia mwaliko kutoka kwa Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pia kufuata Maazimio ya Baraza la Mawazili la Jumuiya ya Afrika Mashariki juu ya uangalizi wa uchaguzi kwa nchi Wanachama wa Jumuiya.


  Kazi ya wasimamizi wa uchaguzi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki itakuwa ni kuangalia kwa ujumla wake mazingira ya uchaguzi na kutathmini kwa kina mchakato wa uchaguzi nchini kote kabla, kipindi cha uchaguzi na baada ya siku ya uchaguzi.


  Kundi la waangalizi wa uchaguzi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki litaongozwa na aliyekuwa Makamu wa Rais wa Kenya, Mh. Awori Arthur Athansius Moody.


  Kundi waangalizi wa uchaguzi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki litatangaza uwepowake inchini Tanzania kwenye mkutano na Waandishi wa Habari utakaofanyika Jumatatu, tarehe 19, October 2015, saa mbili na dakika thelathini (8.30am) asubui, New Africa Hotel, Dar es Salaam.


  ·         NINI KITAFANYIKA- Kutoa taarifa ya kuwasili kwa waangalizi wa uchaguzi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki


  ·         WAPI- New Africa Hotel, Dar es Salaam


  ·         LINI- Tarehe 19th October 2015 from 8.30 am -10.30am

    
  Ndugu   Muandishi wa Habari, unaombwa kuthibitisha uwepo wako kwenye mkutano huu kupitia anuani zifutazo hapa chini;


  Owora Richard Othieno,

  Press and Protocol Coordinator

  EAC Election Observer Mission

  New Africa Hotel


  Dar es Salaam, Tanzania
  Tel: +255 784 835021; 

older | 1 | .... | 665 | 666 | (Page 667) | 668 | 669 | .... | 1897 | newer