Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 664 | 665 | (Page 666) | 667 | 668 | .... | 1898 | newer

  0 0


    Ofisa Uhusiano wa MSD, Benjamin Massangya akimuonesha Mwananchi aliyetembelea banda la MSD  nembo ya MSD iliyowekwa katika makasha na vifungashiyo vya dawa.
   Mtaalamu wa Maabara kutoka Bohari ya Dawa (MSD), Twahiri Magoolo  (kushoto), akimuelekeza jambo mwananchi  aliyetembelea banda la MSD katika kongamano la 29 la wanasayansi wa utafiti wa magonjwa ya binadamu Dar es Salaam jana. Kongamano hilo liliandaliwa na Taasisi ya Utafiti  Magonjwa ya Binadamu (NIMR).
  Dawa na vifaa mbalimbali vikiwa katika banda la MSD katika kongamano hilo.

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI

   WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

  JESHI LA POLISI TANZANIA         TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

     “PRESS RELEASE” TAREHE 16.10.2015.


  ·         MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA NA MTOTO WAKE KUTOKANA NA MGOGORO WA KIFAMILIA.  ·         MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA JANGURUTU AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI WILAYANI MBARALI. 


  KATIKA TUKIO LA KWANZA:

  MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA MWASHIWAWALA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA DICKSON KAWAWA (50) ALIUAWA KWA KUPIGWA KWA VIPANDE VYA MATOFALI NA MTOTO WAKE AITWAE   SIKU DICKSON (20) MWENDESHA PIKIPIKI @ BODABODA, MKAZI WA MWASHIWAWALA. 


  TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 15.10.2015 MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI HUKO KATIKA KIJIJI CHA MWASHIWAWALA, KATA YA IWINDI, TARAFA YA USONGWE, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI, MKOA WA MBEYA.


  CHANZO CHA KIFO HICHO NI KIPIGO NA KUTOKWA DAMU NYINGI BAADA YA MAREHEMU KUKATAZWA NA MTOTO WAKE KUNYWA POMBE KWA MUDA MREFU NA KUKAIDI. MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA UPELELEZI WA TUKIO HILI UNAENDELEA.


  KATIKA TUKIO LA PILI:

  MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA JANGURUTU WILAYA YA MBARALI AITWAYE JAILOS GOYAGE (56) AFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T. 888 BRD AINA YA TOYOTA LAND CRUISER IKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE OMARY NURU (36) MKAZI WA MPAKANI UBARUKU.


  TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 15.10.2015 MAJIRA YA SAA 20:00 USIKU HUKO KIJIJI CHA JANGURUTU, KATA NA TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. DEREVA AMEKAMATWA.


  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WANAFAMILIA KUTATUA MIGOGORO YAO KWA KUKAA MEZA YA MAZUNGUMZO. PIA ANATOA WITO KWA WANANCHI KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA. AIDHA ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA/MICHORO NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
   Imesainiwa na:
  [AHMED Z. MSANGI – SACP]


  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

  0 0

    Mwakilishi wa  Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, akizungumza  siku ya Alhamis Usiku, muda mfupi  kabla ya  kuonyeshwa kwa filamu ya "the Boy from Geita" ambayo inaelezea uovu wanaotendewa watu wenye ulemavu hususani watoto Nchi Tanzania. Katibu Mkuu  Msaidizi wa ofisi ya Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa,  Bw.  Ivan Simonvic wapili kutoka kushoto alitambua mchango wa serikali katika kuukabili uovu dhidi ya  watu wenye ualibino  na akahidi  Taasisi hiyo na  nyingine za Umoja wa Mataifa  ushurikiano na  Serikali. wa Kwanza ni  Bw. Peter Ash mwanzilishi na Mkurugenzi wa  Asasi ya  Unter the Same Sun na  karibu na Balozi  ni  mwakilishi kutoka Uwakilishi wa Kudumu wa Canada katika  Umoja wa Mataifa
  Sehemu wa wageni  waalikwa  waliofika kuangalia filamu ya "the Boy from Geita" iliyonyeshwa Alhamisi usiku hapa  Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. 
    Mwandaaji wa mwongozaji wa filamu ya "the Boy from Geita Bw Vic Sarin akizungumza machache kuhusu kwanini  aliamua kutengeneza filamu   hiyo.
   Sehemu nyingine  ya waalikwa ambao pia walipata nafasi ya kuuliza maswali baada ya  filamu hiyo.
  Balozi akiteta jambo na Kijana huyu  ( jina halikupatikana) raia wa  Marekani mwenye  ulemavu wa  ngozi.
  (ualibino)

  Na  Mwandishi Maalum, New York
  SIKU moja  baada ya  Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kuelezea kwa waandishi wa habari juhudi zinazofanywa na serikali dhidi  uovu wanaofanyiwa  watu wenye  ulemavu wa ngozi.

  Kamisheni  ya   Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa (UNHR ) imesema itashirikiana na  Serikali ya Tanzania katika  juhudi hizo   za kuukabili  ouovu  unaofanywa dhidi ya  jamii  hiyo ya watanzania.


  Kauli hiyo  imetolewa Alhamisi  usiku   na   Katibu Mkuu Msaidizi wa Ofisi ya Kamisheni ya Haki za  Binadamu, Bw.  Ivan Simonovic   muda mfupi kabla ya kuonyeshwa kwa filamu ya “ the Boy from Geita”.


  Bw. Ivan Simonovic  amesema,  ushirikiano huo ni katika kutambua juhudi zinazofanywa na  serikali katika siyo  tu  kwa kuhakikisha tatizo hilo linatoweka lakini pia kwa kuwachukulia hatua za kisheria wale wote wanaohusika  na ukatili huo.


  “Tofauti na  nchi nyingine,  Serikali ya Tanzania imeonyesha ujasiri na uthubutu  wa kukabiliana na uovu unaofanywa dhidi ya watu wenye ualibino. Ni  kwa kutambua juhudi hizo  tutashirikiana  na serikali katika kukomesha  uovu huu” akasema Bw. Simonovic.


  Kauli ya  Bw. Ivan Simonovic ya kutambua juhudi hizo za serikali,  kumetokana na  shuttle diplomacy iliyofanywa na  Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania, Balozi Tuvako  Manongi ya kuonana na  wakuu wa Idara ambazo zimefadhili  kuonyeshwa kwa filamu hiyo hapa Umoja wa Mataifa,   pasipo kuushirikisha  wala  kuujulisha  Uwakilishi  wa Tanzania.  Aidha  maelezo ya awali kuhusu  filamu hiyo  yanaupotoshaji wa baadhi ya mambo  hali iliyomfanya Mwakilishi huyo wa Tanzania katika  Umoj wa Mataifa kuchukua  fursa ya  kuyatolea ufafanuzi.


  “Usiku huu   ninapenda kutambua juhudi zinazofanywa na  Moja ya nchi Mwanachama  wa Umoja wa Mataifa, Tanzania, ambayo Mwakilishi wake  Wakudumu Balozi Tuvako  Manongi  yupo  pamoja  nasi.  Siyo tu kwamba  Tanzania imeonyesha  ujasiri na uthubutu wa kutambua ukubwa wa  tatizo linalowakumba watu wenye  ualibino   lakini  pia  imefanya juhudi za kuwaelimisha wananchi wake huku ikuchukua hatua muhimu” akasema Bw. Ivan Simonovic.


  Akaeleza zaidi kwamba  kama watakavyoona kwenye   filamu hiyo. Waziri Mkuu  wa Tanzania  Mhe. Mizengo  Pinda amekuwa msemaji  na  mtetezi wa haki za watu wenye ualibino  kwa kufanya  ziara za kutembelea maeneo mbalimbali ya nchi kuhimiza   na  kuelimisha wananchi kuachana na  ukatili huo.


  “Kujituma kwake  na namna anavyolichukulia tatizo hili kwa uzito wa aina yake,  ni ushahidi wa namna  gani Tanzania  inavyokabiliana na changatomo hii.  juhudi hizi zimeleta matokeo chanya ambapo    hakuta taarifa za matukio ya kuvamiwa watu wenye ualibino  katika miezi ya hivi karibuni.


   “ Ofisi ya Haki za Binadamu inakaribisha na kutambua juhudi hizo za serikali ya Tanzania katika kukabiliana na Ubaguzi. Mfumo mzima wa Umoja wa  mataifa upo tayari kuwaunga mkono” akasema  katibu Mkuu  Msaidizi.


  Alipopewa  nafasi ya kuzumgumza mbele ya  hadhara hiyo. Balozi Tuvako Manongi   kwanza,  alimshukuru Katibu Mkuu  Msaidizi kwa kutambua mchango wa serikali,  na pia kumpatia fursa ya kuja kuzungumza na kutoa fafanuzi kwa niaba ya serikali yake.


  Balozi Manongi, alirejea kauli  aliyoitoa mbele ya  waandishi siku ya jumatano, kwamba, Tanzania  haikatai na wala haipingi kwamba kuna tatizo kwa  watu wenye ualibino.


  Akasema  pamoja na kukiri kuwapo  kwa matukio  ya uovu dhidi ya watanzania hao, lakini  angependa pia kuweka rekodi sawa  na hasa kufuatia  maelezo  ya upotoshaji ambayo yametolewa kwenye vipeperushi vinavyoitangaza filamu hiyo.


  Baadhi ya mambo ambayo Balozi  ameyatolea ufafanuzi  ni lile linaloelezwa  na waandaji wa filamu  hiyo  kuwa  eti  ualibino  ualianzia Tanzania  miaka 2000 iliyopita  jambo analosema    halijathibitishwa kisayansi.


   Akafafanua pia kwamba,  Watanzania ni waumini wa dini ya kiislamu au wakristo , kwa hiyo kusema   kuwa sehemu kubwa ya watanzania wanaamini katika uchawi halina mashiko. 


  Akasema kwamba si  sahihi pia kueleza kwamba wazazi ni washirika katika kutenda  maovu dhidi ya watoto wao wenye ualibino.  Amefafanua pia kuwa neno zeruzeru ni tafsri ya  Kiswahili ya neno alibino na kwamba tafsri inayotolewa na waandaji hao ni  upotoshaji.

  Balozi Manongi  pia amekanusha  taarifa zilizoelezwa na waandaji hao kwamba Asasi ya Under the Same Sun, ilipokuja Tanzania mwaka 2007  haikukuta  chama chochote cha kuwasema watu wenye ualibino si  kweli. Kwani  chama cha Tanzania Albinism Society ( TAS) kimekuwapo tangu mwaka 1978 na kimekuwa kikiendesha shuguli zake kwa kushirikiana na serikali.


  “ Mashambulizi dhidi ya watu wenye ualibino nchini Tanzania,  ni  makosa ya jinai, yanayofanywa na watu  binafsi ambao wamejawa na mawazo  uovu ambayo yanaweza tu kuthibitishwa na vyombo yha sheria” akasisitiza Balozi.


  Na kuongea kwamba  Tanzania inaheshimu haki za binadamu na utawala wa sheria na kwa kuheshimu  huko  haiwezi kutoa hukumu kiholela  bila ya kufuata mkondo wa sheria.


  Akifafanua Zaidi kwa takwimu Balozi Manongi amesema  watu bilioni moja au Zaidi wenye aina mbalimbali za ulemavu, asilimia 80 wanatoka  nchi zinazoendelea. Na kwamba kwa mujibu wa sensa ya watu iliyofanyika  nchini, watu  2.6  milioni sawa na asilimia 5.8 ya idadi yote ya watu wana aina moja ama nyingine ya ulemavu. Kati yao 16,477 au 0.04 asilimia wana ualibino.


  Wakati wa kipindi cha majibu na maswali baadhi ya  watizamaji walihoji sababu ya waandaji wa filamu hiyo kuionyesha  Marekani ili hali kwamba katika  Marekani yenyewe  pia  kuna vitendo  vya  ubaguzi   wa hali ya juu yakiwamo matukio ya watu  kuuwa.


  Wengine walitaka kujua ni watu gani wanaonunua viungo vya watu wenye ualibino  swali lililojibiwa na waandaji wa filamu hiyo kuwa ni   ni matajiri  wakiwamo wanasiasa  kiuhalifu. Wakasema pia kwamba  ni watanzania wachache ambao bado wanaimani potofu dhidi ya watu wenye ualibino, huku wakibainisha  uhuru wa vyombo vya habari nchi Tanzania imechangia kwa kiasi kikubwa  kufahamika kwa madhila wanayofanyiwa watu wenye  ualubino.

  0 0
 • 10/16/15--01:04: MKOA WA MJINI MAGHARIBI
 • Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwahutubia wafuasi wa Chama hicho katika viwanja vya Fumba Kids, jimbo la Dimani. 
   Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akimtambulisha mgombea Uwakilishi wa jimbo la Dimani kupitia chama hicho Bw. Mohamed Hashim Ismail, katika mkutano uliofanyika viwanja vya Fumba Kids.
   Wafuasi wa CUF wakifuatilia hotuba na mgombea urais wa Chama hicho katika viwanja vya Fumba Kids, jimbo la Dimani.
   Afisa uchaguzi wa CUF Bw. Muhene Said Rashid, akitoa elimu ya wapiga kura kwa wafuasi wa chama hicho kwenye mkutano uliofanyika viwanja vya Fumba Kids, jimbo la Dimani.
  Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiungana na wafuasi wa CUF kuimba nyimbo za kuhamasisha alipowasili katika barza ya “Radio One” kuonana na wanabarza hiyo. (Picha na Salmin Said, OMKR)
   
  MKOA WA MJINI MAGHARIBI          
  Na: Hassan Hamad, OMKR
  Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amesema iwapo atachaguliwa kura Rais atazipitia upya fidia walizolipwa wananchi wa maeneo ya Fumba, Bwefumu na Bweleo ili kuwalipa fidia zinazostahiki kulingana na maeneo yao yaliyochukuliwa kwa ajili na uendelezaji wa maeneo huru ya kiuchumi.

  Amesema serikali atakayoiongoza iwapo atachaguliwa kuwa Rais inakusudia kuondosha kabisa vitendo vya dhulma dhidi ya wananchi, hivyo wananchi hao watapatiwa fidia zinazostahiki baada ya kufanyiwa tathmini.

  Akizungumza katika mkutano wa kampeni za chama hicho uliofanyika viwanja vya Fumba jimbo la Dimani, Maalim Seif amesema Serikali inapaswa kulipa fidia zinazoendana na thamani ya maeneo ya wananchi inapoamua kuyachukua kwa maslahi ya umma, na kwamba serikali yake haitosita kufanya hivyo katika maeneo ya ukanda wa Fumba.

  Aidha Maalim Seif amewahakikishia wananchi wa maeneo hayo upatikanaji wa maji safi na salama, ili kuondosha kabisa tatizo hilo linalowakabili kwa muda mrefu sasa.

  Akizungumzia kuhusu mchakato wa uchaguzi Maalim Seif amesema licha na vitendo vinavyofanywa kuashiria kuingilia kati mchakato huo, uchaguzi mkuu utafanyika tarehe 25 Oktoba kama ulivyopangwa.

  Kabla ya mkutano huo Maalim Seif alifanya ziara ya kutembelea baadhi ya matawi na barza za majimbo ya Kijitoupele, Dimani Mwanakwerekwe na Welezo ikiwemo barza ya “Radio One” na kuelezea kuridhishwa na jinsi wananchi walivyohamasika kushiriki  uchaguzi ujao.
   
  Nae Mgombea Uwakilishi wa jimbo la Dimani kupitia chama hicho Bw. Mohamed Hashim Ismail amewataka wananchi wanaoitakia mema Zanzibar kuwachagua wagombea waliosimamisha na Chama Cha Wananchi CUF katika uchaguzi ujao ambao amesema ni muhimu kwa ukombozi wa Zanzibar.

  Amesema akiwa mgombea wa jimbo hilo atahakikisha kuwa anapita nyumba kwa nyumba ili kuona kuwa kila aliyejiandikisha kupiga kura wakiwemo wagonjwa wanatekeleza jukumu hilo.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Timu ya ushindi CUF Mhe. Ismail Jussa Ladhu  amelishauri jeshi la polisi kuendeleza mahumiano mema kati yake na wananchi kama lilivyofanya wakati wa kuanza kwa kampeni.

  Amesema  ni vyema kwa jeshi hilo kufanya juhudi za kudhibiti vitendo vinavyoashiria shari ikiwa ni pamoja na baadhi ya hujuma vinazofanywa dhidi ya majengo na wanachama wa chama hicho.


  0 0

  Huu ni uchambuzi wa Habari za Magazeti toka vituo mblimbali vya Televisheni October 16, 2015

  TBC
  Magufuli Ataja Tiba ya Ajira na Foleni Dar, Msajili wa Vyama Aonya wanaotaka kubaki vituoni. Ungana nasi upate dondoo za magazeti ya leo. https://youtu.be/E83liI7wTOM

  Star TV
  Mwenyekiti mwenza wa UKAWA Afariki Dunia, Ujenzi Barabara ya Juu Dar kuanza mwezi ujao, kwa hayo na mengine mengi habarika hapa. https://youtu.be/cXwsSqS_iAc

  CH 10
  Lowassa ainyooshea kidole NEC, Magufuli kuwasainisha mikataba mawazili wake, Magufuli ataja Mafisadi CCM. Pata dondoo hizi zaidi hapa. https://youtu.be/gwXZTku5k6w

  Azam TV
  Chopa iliyobeba makada CCM Yaanguka Selous, Mtuhumiwa kesi ya Bilionea Msuya aeleza alivyoteswa. Habarika kwa yaliyojiri hapa. https://youtu.be/D5SDMREvh9Q


  0 0

   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (kulia) akizungumza na uongozi na watendaji wa Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma alipofanya ziara wilayani humo kwa ajili ya kukagua Kambi ya Nduta wilayani humo pamoja na Kambi za Mtendeli na Karago wilayani Kakonko ambazo zipo katika maandalizi ya kuwapokea wakimbizi wa Burundi wanaohifadhiwa kwa muda katika Kambi ya Nyarugusu mkaoni humo. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Ruth Msafiri.
   Mhandisi wa Maji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Msafiri Mtyaule akitoa maelezo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (wa pili kulia) kuhusu kisima ambacho kitasambaza maji kwa ajili ya wakimbizi kutoka Burundi ambao watahifadhiwa katika Kambi ya Mtendeli wakitokea Kambi ya Nyarugusu ambapo wanahifadhiwa kwa muda. 
   Mkuu wa Kambi ya Wakimbizi ya Nduta, Fred Nisajile akimuonyesha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (wa pili kulia) moja wapo ya madarasa yatakayotumiwa na wakimbizi watakaohamishiwa katika Kambi ya Karago kutoka Kambi ya Nyarugusu wanapohifadhiwa kwa muda. Ubaoni ni picha na maandishi yaliyoachwa na wakimbizi walioishi katika kambi hiyo kabla ya kufungwa mwaka 2007.
   Baadhi ya Wakimbizi kutoka Burundi wakipokelewa katika Kambi ya Wakimbizi ya Nduta. Idadi ya wakimbizi kutoka nchini humo inazidi kuongezeka siku hadi siku.

   Askari Polisi wanaosimamia usalama katika Kambi ya Wakimbizi ya Nduta wakikagua mizigo ya wakimbizi kutoka Burundi wanaopokelewa katika kambi hiyo ili kuhakikisha usalama wa mizigo yao.
    Watoto wa Wakimbizi kutoka Burundi wakiwa katika Kambi ya Wakimbizi ya Nduta ambapo wanahifadhiwa.
  Baadhi ya mahema yanayojengwa katika Kambi ya Wakimbizi ya Nduta wilayani Kibondo mkoani Kigoma ambayo yatatumika kuwahifadhi wakimbizi kutoka Burundi wanaoendelea kuwahamishiwa kambini hapo kutoka Kambi ya Nyarugusu ambapo walikuwa wamehifadhiwa kwa muda.

  Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

  SIMUtv: Utambue mpango wa kujitolea kuwasaidia watanzania kiafya ikiwemo magojwa ya saratani ya matiti na magojwa mengine yasioambukizwa:Huu ni uchambuzi wa Habari toka vituo mbalimbali vya Televisheni October 17, 2015.

  SIMUtv: Fuatilia namna ambavyo vuguvugu la kampeni za uchaguzi Mkuu linavyoweza kusababisha vurugugu siku ya uchaguzi https://youtu.be/EUyKaqh2fgQ

  SIMUtv: Tambua ni kwa kiasi gani sera za wagombea kutoka vyama mbalimbali zimegusia saula la kupunguza ajari za barabarani: https://youtu.be/hnHRM2cXuY4

  SIMUtv: Fuatilia namna serikali ilivyojipanga kulinda amani ya Nchi zikiwa zimesalia sikiu chache kuelekea uchaguzi Mkuu: https://youtu.be/otIRUog8MTY

  SIMUtv: TFF yaunda kamati maalumu itakayoshugulikia mwenendo na maandalizi ya timu ya soka Taifa Stars kukabiliana na michuano ya kimataifa https://youtu.be/H5oCwIy6gcc

  SIMUtv:  Mgombea uraisi CCM Dkt. Magufuli aahidi kudumisha muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulioanzishwa na Baba Wa Taifa https://youtu.be/_ReVGfr6qHI

  SIMUtv: Waangalizi 86 wa Uchaguzi toka Nchi wanachama wa SADC kutawanywa katika mikoa 25 kuangalia mwenendo wa Uchaguzi Mkuu https://youtu.be/vRovhW4YHSU

  SIMUtv: Mgombea Uraisi CHADEMA adai tume ya Taifa NEC kuwa chanzo cha kusababisha vurugu endapo itashindwa kubainisha idadi ya wapiga kura. https://youtu.be/JU-OUxS5rvI
  SIMUtv: Serikali kupitia mfuko wa bima ya afya wafungua kituo cha afya mkoani Dodoma itakayosaidia kuongeza wigo wa huduma za figo nchini https://youtu.be/jSYcr4neIGM
  SIMUtv: Kutotambulika  kisheria kwa wasaidiza wa sheria nchini kumechangia kwa kiasi kikubwa wananchi kushindwa kupata haki zao kwenye vyombo vya sheria; https://youtu.be/tv-fKzYyGvA

  Serikali yasaini mkataba na serikali ya China kwajili ya mradi wa ujenzi wa barabara za juu  katika eneo la TAZARA;https://youtu.be/oHaYxYCvtsc

  SIMUtv:  Serikali kupitia mfuko wa bima ya afya wafungua kituo cha afya mkoani Dodoma itakayosaidia kuongeza wigo wa huduma za figo nchini https://youtu.be/jSYcr4neIGM
  SIMUtv: Kutotambulika  kisheria kwa wasaidiza wa sheria nchini kumechangia kwa kiasi kikubwa wananchi kushindwa kupata haki zao kwenye vyombo vya sheria; https://youtu.be/tv-fKzYyGvA

  SIMUtv: Serikali yasaini mkataba na serikali ya China kwajili ya mradi wa ujenzi wa barabara za juu  katika eneo la TAZARA; https://youtu.be/oHaYxYCvtsc

  0 0

  Uwezo annual learning assessments are citizen-led assessments, aimed at collecting household data on children’s mastery levels of reading and arithmetic. On 14th October, 2015, Twaweza inaugurated this assessment for Handeni District. 

  The Handeni District Commissioner, Honorable Husna Rajab Msangi, emphasizes a point during the inauguration of a two-days training of community volunteers who are prepared to undertake the Uwezo Annual Assessment on literacy and numeracy in Handeni Town Council. The workshop was held on 14th October, 2015 at Bwawani Hotel, in Handeni.
   Mr. Musa Gunda, the facilitator of the Uwezo Annual Assessment for 2015 volunteers’ workshopcoordinated by Twaweza, clarifies a point during the session. The workshop was held on 14th October, 2015at Bwawani Hotel, Handeni District.
  Participants of the Uwezo Annual Assessment for 2015 volunteers’ workshop prepare to present their group work. The workshop was held on 14th October, 2015at Bwawani Hotel, Handeni District. 
  (Photos by Masozi Nyirenda)

  0 0

   Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, TPB, Sabasaba Moshingi(wapili kulia), akihudumia wateja kwenye tawi la benki hiyo Kijitonyama jijini Dar es Salaam, leo Ijumaa Oktoba 16, 2015, kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja ya benki hiyo. (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)

  NA K-VIS MEDIA

  KATIKA kuhakikisha inatoa huduma bora kwa wateja wake hapa nchini, Benki ya Posta Tanzania, imeweka mashine maalum ambayo wateja wa benki hiyo wanaofika kupatiwa huduma watatoa maoni yao juu ya huduma wazipatazo kwa kubonyeza vitufe vinavyoelekeza nini maoni yake juu ya huduma aliyoipata.

  Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja ya benki hiyo, kwenye tawi lake la Kijitonyama jijini Dar es Salaam, Oktoba 16, 2015, Aisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Sabasaba Moshingi alisema, benki yake imelenga kutoa huduma zilizo bora na za kisasa ili kurahisisha utendaji wake wa kazi.
  Moshingi ambaye aliongoza maafisa wa benki hyo kutoka makao makuu kwa kutoa huduma kwa wateja, kuwasikiliza na kuwasaidia namna ya kujaza fomu na kutoa pesa, alisema,hatua ya yeye kuongoza maafisa wake kutoa huduma, ni kuwaonyesha wateja kuwa benki yao inawajali.

  “Ili kufanikisha lengo hili benki imeanzisha matumizi ya mashine za kisasa zitakazomuwezesha mteja kutoa maoni ya jinsi gani anafurahia au kutofurahia huduma zetu bila kuhitaji kuandika kwenye karatas, mteja atabofya kitufe ili kupata maoni yake, nasi tutayafanyia kazi maoni yake haraka iwezekanavyo.”i.” Alisema Moshingi.

  Alisema matumizi ya mashine hizo yataboresha utoaji huduma za kibenki, na hivi sasa mipango ya kuziweka kwenye kila tawi inaendelea.
   Moshingi akimuelekeza mteja namna ya kujaza fomu za kuweka pesa
   Afisa wa operesheni wa TPB tawi la Kijitonyama, Agatha Ngoile, (kushoto), akimuhudumia mteja

   Mteja akibonyeza kitufe kutoa maoni yake baada ya kupata huduma
   Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi, akibadilishana mawazo na Meneja wa shirika anayeshughulikia mawasiliano, Norvis Moses
   Moshingi, (wapili kushoto), akizungumza na Norvis, huku Meneja wa tawi la TPB, Kijitonyama, Emmanuel Kimola akiteta jambo na Afisa Habari Theo Mwakifulefule
   Meneja Masoko wa TPB, Deo Kwiyukwa, (kushoto), Meneja Biashara, Frank Mushi, (katikati), na Afisa Masoko, Grace Majige, wakibadilishana mawazo

   Agatha akiwa kazini

  Moshingi akiwa anahudumia mteja kwenye teller

  0 0

  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi (Anayehojiwa na waandishi wa habari pichani)ametuma salamu za rambirambi kwa Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa kiongozi wa klabu hiyo Emmaneul Makaidi aliyefariki Dunia jana mkoani Lindi.
  Katika salam zake, Malinzi amewapa pole wafiwa, ndugu, jamaa, marafiki, wapenzi wa klabu ya Simba pamoja na wadau wa mpira wa miguu nchini, kufuatia kifo hicho cha kiongozi huyo.
  Marehemu Emmanuel Makaidi alipata kuwa kiongozi wa klabu ya Simba 1960-1970 katika nafasi mbalimbali zikiwemo nafasi za Katibu mwenezi, Katibu Mkuu na kukaimu Uenyekiti wa klabu ya Simba kabla ya kujiunga na masuala ya kisiasa.
  Kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini na watanzania, TFF inawapa pole wafiwa na kuwatakia faraja katika kipindi hichi cha maombelezo.

  0 0

  Bukoba Veteran kucheza mchezo wa Kirafiki kesho jumamosi 17.10.2015 kwenye Uwanja wa shule ya seminari ya Ntungamo Bukoba na Timu ya Buswelu Veteran kutoka Jijini Mwanza. Mtandao wa Bukobasports.com ukiongea na Nahodha wa Timu hiyo Kepteni Mwinyi Rajab umeelezwa kwamba mpambano huo wa kirafiki utapigwa kesho jioni na amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi katika Viwanja hivyo. Pia ameweza kuongeza kuwa kutapigwa mtanange mwingine wa kirafiki utaochezwa kesho yake jumapili 18.10.2015 kwenye Uwanja huo kuanzia 10:00 jioni. Bukoba Veteran Sports Club ni umoja wa wanamichezo waliowahi kucheza klabu mbalimbali zikiwemo za Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara maskani yake yakiwa mjini Bukoba, Kagera.
  Baadhi ya Wachezaji wa Timu ya Bukoba Veteran yenye maskani yake mjini Bukoba.
  Maandalizi hayo ni pamoja na kujiandaa na Mtanange mkubwa wa Kirafiki kati ya Bukoba Veteran na Masaka Veteran utakaofanyika mwezi ujao tarehe 28.11.2015 huko Kampala Uganda.Wapenzi wa Soka Mjini Bukoba mnaombwa kujiokeza kwa wingi katika safari hiyo ya Masaka mwezi ujao na kwa kujua zaidi ya safari hiyo mnaombwa kuwasiliana na Uongozi wa Bukoba Veteran kupitia kwa Nahodha wa Timu hiyo au Viongozi wake.
  Salum Bonge, Kepteni Mwinyi Rajab na Mohamed Kassimu(Moha")

  Kepteni Mwinyi Rajab
  Moha"

  0 0

   Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Azania ya jijini Dar-es-Salaam akizima moto kwa kutumia kizimia moto cha aina ya dry powder baada ya kupewa mafunzo ya kukabiliana na majanga ya moto kutoka Jeshi la Zimamoto na Ukoaji mkoa wa Ilala.
   Wanafunzi wa shule ya Secondari Azania ya jijini Dar-es-Salaam wakizimamoto kwa kutumia blanketi ya kuzimia moto baada ya kupewa mafunzo ya kukabiliana na majanga ya moto kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Ilala.

  ‘’Tayari tumeuzima’’ walisikika wanafunzi wa shule ya Sekondari Azania jijini Dar-es-Salaam baada ya kufanikiwa kuuzima moto kwa kuufunika kwa kutumia blanketi maalumu, huku wakishangiliwa mafunzo hayo utolewa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini bila malipo yoyote. 
  (Picha na FC Godfrey Peter).

  0 0

  Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Unicef  Dkt Jama Gulaid akitoa hotuba katika sherehe ya makabidhiano ya magari ya kubebea  wagonjwa Mkoa wa Mbeya15 Octobar  2015
  Mratibu wa Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto Ndugu Prisca Butuyuyu akitoa taarifa ya huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto katika Mkoa wa Mbeya kwenye hafla fupi ya makabidhiano ya magari ya kubebea wagonjwa 15 Octobar 2015.
  Mwakilishi UNICEF Dkt Jama Gulaid kulia akimkabidhi Kaimu katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Ndugu Kastro Msigala taarifa muhimu za magari hayo yenye thamani ya shilingi mil 700.
  Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Mbeya pamoja na wageni waalikwa wakishiriki kikamilifu tukio la makabidhiano ya magari ya wagonjwa  Mkoa wa Mbeya 15 Octobar 2015 kutoka kwa shirika la kimataifa la UNICEF.
  Timu ya Uendeshaji wa huduma za za Afya Mkoa wa Mbeya

  Kastro Msigala Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo za makabidhiano ya magari kumi ya kubebea wagonjwa ambayo yametolewa na shirika la kimataifa la UNICEF Octobar 15 mwaka huu.
  Kaimu Katibu tawala Mkoa wa Mbeya Kastro Msigala akikata utepe kuashiria kupokea rasmi msaada wa magari hayo kutoka kwa shirika la kimataifa la UNICEF msaada ambao umegharimu kiasi cha shilingi Mil 700. 

  Meza kuu katika  picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa wa Mbeya na wawakilishi wa Shirika la UNICEF.
  Meza kuu katika picha ya pamoja na waganga wakuu wa Halmashauri za Mkoa wa mbeya .
  Meza Kuu katika picha ya Pamoja na timu ya Uendeshaji wa Huduma za Afya Mkoa wa Mbeya .
  Meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi shirika la UNICEF.


   
  SHIRIKA la Umoja wa Mataifa  linalo shughulikia watoto Duniani (UNICEF) limekabidhi msaada wa magari kumi  ya Kubebea wagonjwa yenye tahamni ya shilingi mil 700.7  kwa serikali ya Mkoa wa Mbeya .


  Aidha shirika hilo lina mpango wa kuboresha vituo 184 vya kutolea huduma za afya katika mkoa huo wa mbeya ambavyo ni vituo afya na hospital 30 pamoja na zahanati 154  sanjali na kuvipatia vifaa muhimu vya kutolea mafunzo kwa watumishi wake.


  Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Octobar 15 mwaka huu  Mwakilishi wa shirika la  UNICEF   nchini Tanzania Dkt Jama Gulaid  amesema shirika hilo limetenga kiasi cha shilingi bilioni 2 kwa ajili ya mradi huo.


  Amesema mchango wa UNICEF katika sekta afya na lishe hapa mkoani mbeya imepanua wigo kutoka halmashauri mbili za mkoa huo hadi kufikia halmashauri zote katika kipindi cha miaka miwili .


  Aidha Dtk, Jama amesema katika kukabiliana na magonjwa na vifo vya watoto na wanawake wajawazito ,UNICEF imechangia vifaa tiba muhimu ikiwa ni pamoja vile vya uchunguzi wa ujauzito ,upasuaji  sanjali na vifaa kuwasaidia watoto wachanga kupumua mara wanapo zaliwa na vifaa vingine vya utoaji wa huduma katika idara ya uangalizi maalumu  ICU.


  Aidha  amewataka viongozi hao wa mkoa wa Mbeya kuhakikisha wanaweka juhudi kubwa zaidi katika kupunguza vifo vya akina mama na watoto wachanga kwa kuhakikisha kwamaba kina mama wajawazito wote wanapata huduma za afya bure kwa wakati.


  Awali akisoma  taarifa ya huduma za afya ya uzazi na mtoto katika mkoa mbeya mratibu wa huduma za afya ya uzazi na mtoto Ndugu Prisca  Butuyuyu amesema toka shirika hilo la UNICEF  lianze kufanya mwaka 2012 huduma za afya zimeimalika kwa kiasi kikubwa hususani kwa kuweza kuzuia vifo vya uzazi na vya watoto wachanga.


  Amesema kwa ujumla hali ya vifo hususani vilivyokuwa  vinatokea katika vituo vya huduma vimepungua kutoka 140  kwa mwaka 2012 na kufikia vifo 94 kwa kwa mwaka 2014 pamoja na kupunguza vifo vya watoto wachanga kutoka 602 kwa mwaka 2012 hadi kufikia 568  mwaka 2014 ambapo punguzo hilo ni sawa na asilimia 33.9 na 5.7 kwa watoto wachanga.


  Akipokea msaada huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Kaimu katibu Tawala Ndugu Kastro Msigala amelishukuru shirika hilo kwa msaada wa magari hayo sanjali na kutoa wito kwa viongozi  wa halmashauri ambao ni wakurugenzi na waganga wakuu kuhakikisha wanayatunza magari hayo ili yaweze kutoa huduma stahiki kwa wananchi.


  Msaada huo wa magari imegawanywa katika halmashauri zote mkoa huo wa mbeya ambazo ni Ileje,Mbozi,Mbeya vijijini,Rungwe,Busokelo,Mbarali pamoja na Kyela na Momba.

  0 0
 • 10/16/15--03:43: BEI YA MADAFU HII LEO


 • 0 0  IFC, a member of the World Bank Group, this week launched a $5 million program to increase access to energy in Tanzania by developing a market for mini-grids. The initiative aims to bring affordable, off-grid renewable energy to households and businesses in rural Tanzania. 

  IFC will work with project developers in Tanzania to promote commercially viable mini-grid business models, and will advise banks and financial institutions on how to extend long term finance to mini-grid developers.

  Tanzania has been selected as one of the first countries to test the concept of using small-scale renewable energy production sources under a new program, called the Scaling-up Renewable Energy in Low Income Countries Program. In Tanzania, it aims to help diversify energy production away from fossil fuel based sources.

  Mini-grids are technically and commercially viable for high-density populations that live outside the reach of the national electricity grid. The Tanzanian government estimates that about half of the country’s rural population could be served by off-grid options in a cost-effective manner. Mini-grids could provide access to electricity for 9.1 million people in Tanzania. 

  Lutengano Mwakahesya, Director General of Tanzania’s Rural Energy Agency said, “We have an urgent task ahead of us to increase energy access in Tanzania. Mini-grids are a key part of the solution, so this program with IFC is an essential step to improve the quality of life of households, demonstrating the role of the private sector.” 

  Tanzania’s Ministry of Energy and Minerals was closely involved in developing the mini grids program, and was represented at the event by the Assistant Commissioner, Mr. Edward Ishengoma. 

  Dan Kasirye, IFC’s Resident Representative for Tanzania, said “IFC aims to help develop a robust mini-grid market in Tanzania, which will create investment opportunities in the renewables sector and help fill the country’s energy gap. We plan to mobilize the financial resources and expertise of the private sector to expand energy services to low-income communities.”

  IFC, a leader in renewable energy finance, helps developing countries transition to a low carbon future. Over the past three years, IFC has financed close to $3.5 billion in renewable energy projects worldwide, including biomass, geothermal, hydro, solar, and wind.

  About IFC

  IFC, a member of the World Bank Group, is the largest global development institution focused on the private sector in emerging markets. Working with more than 2,000 businesses worldwide, we use our capital, expertise, and influence, to create opportunity where it’s needed most. In FY15, our long-term investments in developing countries rose to nearly $18 billion, helping the private sector play an essential role in the global effort to end extreme poverty and boost shared prosperity.

  0 0

  Mshiriki wa shindano la kumsaka Serengeti Masta wa jumla kwa jiji la Mbeya Ibrahimu Allam aliyetokea baa ya Liz Pub iliyopo Mafiat jijini Mbeya akinywa bia ya Serengeti Premium Lager kabla ya kuingia kwenye mchuano wa kumpata mshindi wa jumla wa kampeni ya Serengeti Masta kwa jiji la Mbeya uliofanyika kwenye baa maarufu ya Mbeya Pazuri iliyopo Sae jijini humo mwishoni mwa wiki. Kampeni hiyo imefikia tamati jijini Mbeya baada ya kudumu kwa takribani miezi miwili ikizunguka baa kwa baa kusaka washindi mbalimbali wanaotambua ladha halisi ya bia hiyo lakini pia imetoa elimu kwa wateja wake kuhusiana na chapa hiyo namba moja kutoka SBL.


  Mshindi wa jumla wa shindano Serengeti Masta kwa jiji la Mbeya Faraji Mbwambo kutoka baa ya Gambino jijini Mbeya akionesha kitita cha fedha sh. 100,000 alizotunukiwa baada kuibuka mshindi wa jumla wa kuitambua ladha ya bia ya Serengeti Premium Lager kati ya vinywaji vitano vinavyozalishwa na kampuni ya SBL. Kampeni hiyo ya Serengeti Masta imewakutanisha wateja na mameneja wa bia hiyo katika kujifunza kwa undani kuhusiana na bia hiyo ambapo mameneja hao walitoa zawadi mbalimbali kwa washindi walioweza kuitambua ladha halisi ya bia hiyo katika kipindi cha kampeni.
  Mshiriki wa shindano la Serengeti Masta na mkazi wa Arusha Sebastian Michael akionja ladha tofauti za bia zilizo mbele ya meza yake ili kuitambua ladha halisi ya bia ya Serengeti Premium Lager katika shindano la kumpata Serengeti Masta wa mkoa wa Arusha ambalo lilifanyika katika Baa ya Bondeni, Kijenge juu jijini Arusha mwishoni mwa wiki hii. Shindano hilo linalodhaminiwa na bia ya Serengeti Premium Lager limewakutanisha wapenzi mbalimbali wa bia hiyo huku likitoa elimu juu ya bia yake na zawadi mbalimbali kama fedha fulana na bia za bure katika kipindi chote cha miezi miwili jijini humo.
  Mshindi wa jumla wa shindano la Serengeti Masta kwa wakazi wa Arusha Laota Elias akionyesha fedha taslim Tsh. 100,000/= alizopokea wakati wa shindano la mwisho la kumtafuta “Serengeti Masta” wa jumla wa mkoa huo lililofanyika katika baa ya Bondeni iliyopo Kijenge juu jijini Arusha. Ushindi wa jumla wa Bw. Elias umekuja baada ya kuwabwaga washiriki wenzake watatu katika mtanange wa mwisho wa kuitambua ladha halisi ya bia hiyo na kuibuka “Serengeti Masta” wa mkoa wa Arusha. Shindano hilo la “Serengeti Masta” limezunguka katika baa mbalimbali za jiji la Arusha likiwaburudisha wateja wa bia hiyo na kuwafundisha wahudumu wa baa mbalimbali juu ya utoaji huduma kwa wateja.


  Mmoja wa washiriki wa shindano la kumtafuta Serengeti Masta wa jiji la Mbeya akitokea Power bar ya Mbalizi Maxmilian Majaliwa Kamanga akijaribu ladha tofauti za vinywaji vya kampuni ya SBL katika baa ya Mbeya Pazuri ambapo shindano la mwisho la kumtafuta mshindi wa jumla kwa mkoa huo lilifanyika mwishoni mwa wiki. Shindano hilo limezunguka katika baa mbalimbali jijini humo ambapo kwa ujumla shindano hilo limewafikia wahudumu zaidi ya 4000 Tanzania nzima katika kipindi cha miezi miwili ya kampeni na kuwafunza juu ya utoaji huduma kwa wateja.

  0 0

   Mkurugenzi  wa Mipango na Maendeleo ya Biashara, Mhandisi Kato Kabaka (aliyesimama), kutoka Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania akitoa elimu kwa wananchi wa kata ya Kisaki wilaya ya Morogoro Vijijini namna ya kutafiti nishati ya Jotoardhi hadi hatua ya kuzalisha umeme na jinsi itakavyoweza kubadili maisha ya wananchi wa kata hiyo.
  Wananchi wa kata ya Kisaki, Morogoro Vijijini wakimsikiliza kwa makini Bi. Eva Nyantori, Afisa Sayansi ya Jamii kutoka Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania alipokuwa akiwaelimisha juu ya fursa ambazo watazipata kupitia mradi wa Jotoardhi.
   Afisa Mawasiliano na Mahusiano ya Umma, Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania Bi. Johary Kachwamba, aliyesimama akiongea na wananchi wa kijiji cha Kichangani Morogoro Vijijini juu ya mikakati na mipango ambayo kampuni imejiwekea kuhakikisha megawati 200 za umeme zinalishwa nchini Tanzania kutokana na nishati ya Jotoardhi ifikapo mwaka 2020. 

   Mhandisi wa Mazingira wa Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi Tanzania Bi. Esther Range (aliyesimama) akiwaelimisha wananchi wa kijiji cha Kichangani namna ambavyo nishati ya umeme wa Jotoardhi ilivyo rafiki wa mazingira tofauti na nishati nyingine za umeme.
  Mwananchi wa kijiji cha Kichangani Morogoro Vijijini Bwana Hamisi Kadobwa (aliyesimama) akiuliza swali kuhusu teknolojia ya kuvuna nishati ya Jotoardhi, aidha ilipongeza juhudi za Serikali kuwaletea wananchi maendeleo.

  (Picha Na: Lilian Lundo – Maelezo)

  0 0

  The former president Hon. Ally Hassan Mwinyi giving the medal to the winner of the Marathon on mens side, Emmanuel Ginmiki during  Rotary Dar Marathon which took place in Dar es salaam on the Nyerere Day. Rotary Dar Marathon is taking place every year being organised by the Rotary Clubs in partnership with Bank M.Looking on is the Bank M's Deputy CEO Ms. Jacqueline Woiso and The Rotary District Governor Mr. Robert Waggwa Nsibirwa.
   The former president Hon. Ally Hassan Mwinyi flagging off the Rotary Dar Marathon 2015 which took place in Dar es salaam during Nyerere Day, right is the Bank M’s Deputy CEO Ms. Jacqueline Woiso (With the flag). Rotary Dar Marathon is taking place every year being organised by the Rotary Clubs in partnership with Bank M.
  Winners of the Rotary Dar Marathon 2015 on men’s runners side, Emmanuel Ginmiki (Winner), Ismail Juma (2nd place) and Joseph Toefil (3rd Place) posing for a photo after receiving their prizes which were handed over by the former Tanzanian president Hon. Ally Hassan Mwinyi (standing in the middle).Others from right are Ms. Agnes Batengas, The Rotary Dar Marathon committee chair, Ms. Sharmila Bhatt, rotary Board chair, Mr. Robert Waggwa Nsibirwa, The Rotary District Governor, Ms. Jacqueline Woiso, Deputy CEO Bank M and Vikash Shah, The Rotary Dar Marathon 2015 committee member.

  0 0
 • 10/16/15--04:31: TANZIA
 • Ee Mwenyezi Mungu ziweke mahari pema peponi Roho za marehemu.AMINA

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi kutoka China (ZHEJING UNIVESITY  OF MEDIA&COMMUNICATIONS) Rrof.Dk.Peng Shaojian wakati alipofika Ikulu mjini Zanzibar akiwa na ujumbe aliofuatana nao leo.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Ujumbe kutoka nchini China katika Chuo cha (ZHEJING UNIVESITY  OF MEDIA&COMMUNICATIONS) chini ya kiongozi wake Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi  Rrof.Dk.Peng Shaojian (katikati) wakati alipofika Ikulu mjini Zanzibar akiwa na ujumbe aliofuatana nao leo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na mgeni wake Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi  Rrof.Dk.Peng Shaojian kutoka Chuo cha (ZHEJING UNIVESITY  OF MEDIA&COMMUNICATIONS) nchini China baada ya mazungumzo na Ujumbe  aliofuatana nao walipofika  Ikulu mjini Zanzibar leo,[Picha na Ikulu.]

older | 1 | .... | 664 | 665 | (Page 666) | 667 | 668 | .... | 1898 | newer