Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live

STOP PRESS: RUFAA ZA MRAMBA NA YONA ZAGONGA MWAMBA, KUTUMIKIA MIAKA 2 BADALA YA MITATU, FAINI YA MILIONI 5 YAFUTWA

0
0

Na Mwene Saidi wa Globu ya Jamii

Rufaa iliyokatwa na mawaziri wa zamani  Basil Mramba (kushoto) na Daniel Yonah imegonga mwamba katika Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam leo, baada ya kuwapunguzia mwaka mmoja na kuwaondolea faini ya milioni 5 na kutakiwa kuendelea kutumikia kifungo cha miaka miwili  baada ya mahakama hiyo kuona hakuna ushahidi wa kuthibitisha shitaka la kusababisha hasara ya Sh. bilioni 11.7.

Kadhalika, mahakama hiyo imesema Mahakama ya Kisutu, ilikuwa sahihi kumwachia huru aliyekuwa Katibu Mkuu wa Hazina, Gray Mgonja kwa kuwa hakuna ushahidi uliothibitisha kuhusika na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na kusababisha hasara hiyo.

Hukumu hiyo iliyosomwa kwa saa mbili saa 3:28 hadi 5:00 na Jaji Projest Rugazia aliyesikiliza rufaa mbili zilizokatwa na pande zote mbili dhidi ya kesi hiyo.

Awali upande wa Jamhuri ulikata rufaa kupinga hukumu ya kumwachia huru Mgonja na utetezi ulikata rufaa kupinga hukumu ya kuwatia hatiani Mramba na Mgonja.Jaji Rugazia alisema hakuna ushahidi ulitolewa mahakamani kueleza namna gani washtakiwa walihusika kusababisha hasara na kwamba adhabu ya kosa hilo ilitolewa kimakosa dhidi ya washtakiwa.
Alisema kulingana na ushahidi uliotolewa hakuna lawama kwa Mahakama ya Kisutu, kumwachia huru Mgonja dhidi ya mashitaka yaliyokuwa yanamkabili kwenye kesi hiyo.Pia, alisema haoni kama kuna sababu ya kumhusisha rais (wakati huo Benjamini Mkapa) kwa kuwa alitoa maelekezo kulingana na maelezo aliyopewa na mshtakiwa wa Yona.


"Sioni sababu ya kumtumia rais kwa makosa yaliyotokea kwa kuwa alitoa maekezo kutokana na mapendekezo yaliyotolewa na mshtakiwa wa pili, Yona... pia hakuna ushahidi uliowaweza kuelezea mahakama namna gani washtakiwa walifanya kosa la 11 la kuisababishia serikali hasara ya Sh. bilioni 11.7, mahakama hii inatengua adhabu ya kosa hilo na washtakiwa watatumikia kifungo cha miaka miwili kila mmoja" alisema Jaji Rugazia.
Mapema Julai 6, mwaka huu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, iliwatia hatiani washtakiwa hao na kumwachia huru Mgonja.
Wafungwa hao kwa pamoja  wamekutwa na hatia ya makosa 10 ya kutoa msamaha wa kodi kwa Kampuni ya Alex Stewart ( ASSAYERS) Government Business Corporation kwa ajili  ya kufanya ukaguzi wa madini ya dhahabu nchini.

MAGUFULI AENDELEA NA KAMPENI ZAKE MKOANI SINGIDA,KESHO KUUNGURUMA SINGIDA MJINI LIVE

0
0
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiombewa Dua na mmoja wa kiongozi wa dini mara baada ya kusimamishwa na Wananchi wa kijiji cha Puma (hawapo pichani),alipokuwa akielekea mkoani Singida mara baada ya kumaliza mkutano wake wa hadhara wa kampeni.
PICHA NA MICHUZI JR-SINGIDA.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akimshukuru kiongozi huyo wa dini kwa kujitolea kumuombea Dua ya heri na afya njema katika nafasi yake ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi  kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mnadani Ikungi mkoani Singida jioni ya leo ,wakati akiwaomba  wananchi hao kumpigia kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu katika uchaguzi wa Rais , Wabunge na Madiwani. 

Dkt. Magufuli amesema serikali yake itahakikisha inazisaidia taasisi mbalimbali  hasa za mashirika ya  dini ambazo zinaendesha hospitali  katika kupata vifaa, Ruzuku, na ajira kwa wafanyakazi ili   kuimarisha huduma  za kiafya  kwa jamii.


Sehemu ya umati wa Wakazi wa mji wa Ikungi wakifuatilia mkutano wa hadhara wa kampeni,wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi kwenye mkutano wake wa mwisho kwa jioni ya leo,ambapo kesho anatarajia kuendelea na kampeni mkoani Singida na baadae kuhitimisha kampeni zake kwenye mkutano mkubwa ambao unatarajiwa kurushwa live na kituo cha Star TV.

 Kiongozi wa Msafara wa Kampeni za Mgombea Urais wa CCM Dkt John Magufuli,Ndugu Abdallah Bulembo akimkaribisha Mgombea Urais wa CCM Dkt.Magufuli kuwahutubia wananchi wa Ikungi jioni ya leo na kuwaomba kumpigia kura ya ndio ifikapo Oktoba 25 mwaka huu kwenye uchahuzi mkuu wa Urais,Wabunge na Madiwani.
Wananchi  wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mnadani Ikungi mkoani Singida,ambapo Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli aliwahutubia na pia kuwaomba  wananchi hao kumpigia kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu katika uchaguzi wa Rais , Wabunge na Madiwani.
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Singida Diana Chilolo akimpigia debe Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye  mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mnadani Ikungi,mkoani Singida.
 Msafara wa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli ukiwasili mjini Itigi mkoani Singida mapema leo mchana,tayari kwa ajili ya kufanya mkutano wa kampeni mjini humo.
 

 Baadhi ya Wazee wakifuatilia mkutano wa Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi mbele ya wananchi wa mji wa Itigi mkoani Singida mapema leo mchana kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
Baadhi ya Wakazi wa mji wa Manyoni wakishangilia jambo kwenye mkutano wa kampeni wa hadhara wa Dkt Magufuli alipokuwa akijinadi mbele yao na kuwaomba kura ili awe Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,ambapo ameaomba ifikapo Oktoba 25 mwaka huu wajitokeze kwa wingi kumpigia Kura za Urais,Ubunge na Udiwani..
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Manyoni Mashariki Ndugu Damiel Mtuka mara baada ya kukabidhiwa Kitabu cha Ilani ya chama hicho kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika mapema leo mchana mjini Manyoni mkoani Singida
 Baadhi ya Wakazi wa mji wa Manyoni wakifuatilia mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la Itigi Ndugu Yahaya Omar Masele mbele ya Wakazi wa mji huo (hawapo pichani),waliofika kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika mapema leo mchana.
  Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la Itigi Ndugu Yahaya Omar Masele mbele ya Wakazi wa mji huo (hawapo pichani),waliofika kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika mapema leo mchana.
 Baadhi ya wananchi wa mji wa Ikungi wakifuatilia mkutano wa hadhara wa kampeni,wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi.

TAHADHARI KWA WATUMIAJI WA BARABARA YA LUPA ENEO LA NJIA PANDA ISANGA JIJINI MBEYA

0
0
Kipande cha barabara ya njia Panda Isanga karibu na Hotel ya Lifti Valey jijini Mbeya (LUPA WAY )ambacho kimejengwa upya kwa kuongezewa njia kimeleta sura mpya jijini hapa  lakini kimeleta pia changamoto kwa madereva hasa kwa nyakati za usiku  kwani hakuna taa hivyo nivema watumiaji wa barabara hii wakachukua tahadhari kwa kuto endesha kwa mwendo kasi ili kuepuka ajali zisizo za lazima ...JAMIIMOJABLOG.






MAMA SAMIA AMALIZA KAMPENI SIMIYU LEO

0
0
 Kinamama wa mkoa wa Simiyu, wakimtawaza kuwa Mama Kiongozi wa Wasukuma, kwa kumvalisha mavazi rasmi Mgombea Mwenza wa Urais kwa timeti ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Maswa Mashariki mkoani humo leo. Jimbo hilo lilikuwa chini ya Mbunge wa Chadema, Kasulumbai
 Kinamama wa mkoa wa Simiyu, wakimtawaza kuwa Mama Kiongozi wa Wasukuma, kwa kumvalisha mavazi rasmi Mgombea Mwenza wa Urais kwa timeti ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Maswa Mashariki mkoani humo leo. Jimbo hilo lilikuwa chini ya Mbunge wa Chadema, Kasulumbai
 Kinamama wa mkoa wa Simiyu, wakimtawaza kuwa Mama Kiongozi wa Wasukuma, kwa kumvalisha mavazi rasmi Mgombea Mwenza wa Urais kwa timeti ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Maswa Mashariki mkoani humo leo. Jimbo hilo lilikuwa chini ya Mbunge wa Chadema, Kasulumbai
 Kinamama wa mkoa wa Simiyu, wakimtawaza kuwa Mama Kiongozi wa Wasukuma, kwa kumvalisha mavazi rasmi Mgombea Mwenza wa Urais kwa timeti ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Maswa Mashariki mkoani humo leo. Jimbo hilo lilikuwa chini ya Mbunge wa Chadema, Kasulumbai
  Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, baada ya kutazwa kuwa Mwanamke Kiongozi wa Wasukuma, kwa kuvalishwa mavazi rasmi wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Maswa Mashariki mkoani humo leo. Jimbo hilo lilikuwa chini ya Mbunge wa Chadema, Kasulumbai
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, baada ya kutazwa kuwa Mwanamke Kiongozi wa Wasukuma, kwa kuvalishwa mavazi rasmi wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Maswa Mashariki mkoani humo leo. Jimbo hilo lilikuwa chini ya Mbunge wa Chadema, Kasulumbai
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, baada ya kutazwa kuwa Mwanamke Kiongozi wa Wasukuma, kwa kuvalishwa mavazi rasmi wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Maswa Mashariki mkoani humo leo. Jimbo hilo lilikuwa chini ya Mbunge wa Chadema, Kasulumbai.

Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, akihutubia umati wa wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Maswa Mashariki mkoani humo leo. Jimbo hilo lilikuwa chini ya Mbunge wa Chadema, Kasulumbai
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, akiwasili kuhutubia mkutano wa kampeni leo katika jimbo la Maswa Mashariki mkoani Simiyu leo
Aliyekuwa mgombea Ubunge jimbo la Nkenge na kushindwa katika kura za maoni za CCM, Mama Asupta Mshama, akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo la Maswa Mashariki mkoani Simiyu leo
Wananchi wakimshangilia mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan alipohutubia mkutano wa kampeni leo katika jimbo la Maswa Mashariki leo
Mwananchi akiwa amembeba mtoto wake ili kumuona Mama Samia Katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo jimbo la Maswa Mashariki mkoani Simiyu leo
Mgombea Ubunge jimbo la Meatu, Salum Hamis Salum, akiomba kura wakati wa mkutano wa kampeni wa Mama Samia uliofanyika leo katika jimbo hilo mkoani Simiyu
Kijana akimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Meatu
Baadhi ya wananchi wakiwa juu ya mti ili kumuona vizuri mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Meatu mkoani Simiyu
Wananchi wakimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Meatu mkoani Simiyu
Wananchi wakifikisha ujumbe kwa Mama Samia kwa njia ya mabango, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Meatu mkoani Simiyu
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la Meatu  Salum Hamis Salum katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo hilo
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimsikilza kwa makini Fatuma Maselle, baada ya kuhutubia mkutano wa kampeni leo katika jimbo la Meatu mkoani Simiyu leo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

RAIS KIKWETE AAGWA RASMI NA TANZANIA PRIVATE SECTOR FOUNDATION

0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam kwa hafla maalum iliyoandaliwa kumuaga rasmi na Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) usiku huu.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na Dkt. Reginald Mengi katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam kwa hafla maalum iliyoandaliwa kumuaga rasmi na Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) usiku huu.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na wadau alipowasili katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam kwa hafla maalum iliyoandaliwa kumuaga rasmi na Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) usiku huu.

























































































MAFUNZO YA WASIMAMIZI NA MAAFISA UCHAGUZI MKOA WA DAR ES SALAAM YAFANYIKA LEO

0
0

2
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Mecki Sadiki Akifungua mafunzo ya siku mbili ya waratibu wa Uchaguzi,Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi na Maafisa uchaguzi leo Octoba 3, 2015 jijini Dar es salaam.Picha na Aron Msigwa- MAELEZO.
34
Waratibu  wa Uchaguzi,Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi na Maafisa uchaguzi waliohudhuria mafunzo leo jijini Dar es salaam kujiandaa usimamizi wa uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani Oktoba 25 mwaka huu.
……………………………………………………………………………………….
Na.Aron Msigwa- MAELEZO.Dar es Salaam.
Mkuu wa mkoa wa Dar es slaam Said Mecki Sadiki amewataka Waratibu wa Uchaguzi, Wasimamizi wa Uchaguzi na viongozi wa vyama vya Siasa katika mkoa huo kuhakikisha kuwa wanafanya kazi zao kwa ushirikiano ili kuwawezesha wananchi kupiga kura kwa amani na utulivu na kuepusha manung’uniko yanayoweza kujitokeza.
Akifungua mafunzo ya siku mbili ya waratibu wa Uchaguzi,Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi na Maafisa uchaguzi leo jijini Dar es salaam Mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa Dar es salaam ni miongoni mwa maeneo yenye wapiga kura wengi hivyo  mkoa kwa kushirikiana na Tume ya uchaguzi umejipanga kuhakikisha kuwa wananchi wote waliojiandikisha wanapiga kura kwa amani na utulivu Siku ya uchaguzi Oktoba 25 mwaka huu.
Amesema Wakurugenzi wa Halmashauri wa mkoa huo ambao ndiyo wasimamizi wa uchaguzi katika wilaya wanalo jukumu la kuwaita na kuwaelimisha viongozi wa vyama vya siasa juu ya taratibu na kanuni za kufuata wakati wa uchaguzi mkuu ili wajenge mazingira rafiki ya kufanya kazi kwa ushirikiano.
Aidha, amewasisitiza wasimamizi hao kutojihusisha kwa namna yoyote ile na kampeni za siasa wakati wa kutekeleza majukumu yao kwani kufanya hivyo watakuwa wanahujumu ufanisi wa uchaguzi mkuu katika mkoa wa Dar es salaam.Ili kudumisha amani na utulivu vituoni amewataka kufanya kazi zao kwa umakini mkubwa kwa kuwa suala la amani vituoni litakuwa mikononi mwao wakati wa kipindi chote cha upigaji wa kura Oktoba 25 mwaka huu. 
“Simamieni kanuni, sheria na taratibu, msionyeshe upendeleo wowote wala kufanya kampeni za aina yoyote ile ndani ya vituo vya kupigia kura, jambo hilo halikubaliki hata kidogo,mfanyeni kazi mliyotumwa ili msiwe sehemu ya tatizo katika nchi hii” Amesisitiza Sadiki.
Ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutunza kadi zao za kupigia kura ili waweze kuzitumia siku ya uchaguzi na kuvionya vikundi, watu au vyama vinavyojaribu kuwarubuni wananchi kwa kununua kadi zao za kupigia kura kuacha tabia hiyo.
” Watu wanaofanya hivi wanafanya unyang’anyi, nawataka waache tabia hii kwani haina tija kwa mamaendeleo ya taifa letu,ukichukua au kuiba kadi ya mtu unamnyima haki ya kupiga kura muhusika na huo sio uungwana” Amesisitiza.
Ametoa wito wananchi wa mkoa wa Dar es salaam kudumisha amani wakati wa upigaji wa kura na kuwataka wananchi wote waliopanga kufanya vurugu wakati wa uchaguzi kuacha“Sisi kama Serikali hatuvumilia aina yoyote ya uvunjifu wa amani, tutaimarisha ulinzi yapo maeneo korofi ambayo yamekuwa na vitendo vya uvunjifu wa amani tunayajua, tunawahakikishia wananchi watapiga kura kwa amani na kurudi makwao wakiwa salama”.
Kuhusu waangalizi wa Kimataifa waliowasili nchini ambao baadhi yao watafanya kazi jijini Dar es salam amesema watafanya kazi zao kwa mujibu wa taratibu na kanuni walizopewa na Tume na kuongeza kuwa kazi yao itakua ni kuangalia kama tumnazingatia na kufuata sheria tulizojiwekea na si kuingilia shughuli za wasimamizi wa zoezi la upigaji wa kura.
“Suala la kusimamia zoezi la upigaji wa kura ni letu wenyewe, msiwaruhusu waanze kuwapa taratibu za upigaji wa kura wa nchi walizotoka wala kutoa maamuzi yoyote, kazi yao itakua ni kuangalia mwenendo wa uchaguzi wetu na si vinginevyo” amesisitiza.Aidha, amevitaka vyama vya siasa kuhakikisha kuwa vinawapeleka mawakala wao mapema katika vituo vya kupigia kura kabla ya kuanza kwa zoezi la upigaji wa kura ili kuondoa manung’uniko yanayoweza kujitokeza.
Kwa upande wake Bi. Clesensia Mayala ambaye ni Kaimu Mkuu wa Sehemu, Kanda ya Kusini Tume ya Taifa ya Uchaguzi amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwakumbusha wasimamizi na Maafisa uchaguzi kuzingatia na kufuata taratibu zilizotolewa na Tume ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Amesema katika mafunzo hayo washiriki hao watajadili masuala mbalimbali ikiwemo wajibu na majukumu ya waratibu na wasimamizi wa uchaguzi,majukumu ya makarani waongozaji wa vituo vya kupigia kura ,kuangalia fomu zitakazotumika wakati wa upigaji kura,taratibu za upigaji kura, Fomu zitakazotumika wakati wa kuhesabukura, kujumlisha na kutangaza matokeo ya Urais,Wabunge na Madiwani.
Amefafanua kuwa wasimamizi wote wa uchaguzi watakua na jukumu la kuhakikisha kuwa vituo vyote ya uchaguzi vinafunguliwa kwa wakati na kufungwa kwa kuzingatia muda uliopangwa ili kuhakikisha kuwa wananchi wote wanatimiza wajibu wao wa kikatiba.
Kwa upande wake Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Temeke Bw. Photidas Kagimbo amesema uchaguzi mkuu katika eneo analolisimamia utafanyika kwa uhuru na usalama na kuongeza kuwa wamejipanga vyema kuwahudumia wananchi wote waliojiandikisha ambao watajitokeza kupiga kura siku hiyo.
Amesema Tume ya Taifa ya Uchaguzi inaendelea kupeleka vifaa mbalimbali katika maeneo mbalimbali ili kuwawezesha wananchi kupiga kura Oktoba 25 na kufafanua kuwa  kazi  inayoendelea sasa ni utoaji wa elimu ya mpiga kura kwa wananchi.
Kuhusu uhakiki wa taarifa za wananchi katika daftari la kudumu la Wapiga kura kwa wananchi walioshindwa kuhakiki kutokana na sababu mbalimbali amesema liko mikononi mwa Tume ya Taifa ya uchaguzi na kwamba wao wanasubiri maelekezo ya Tume hiyo na daftari kamili litakalokuwa na orodha ya wapiga kura wote litakalopelekwa kwenye vituo vya kupigia kura kabla ya tarehe ya  uchaguzi ili kutoa fursa kwa vyama vya siasa na wananchi kupitia majina yote.

WATANZANIA WATAKIWA KULINDA SHAHADA ZAO ZA KUPIGIA KURA.

0
0
 Harakati za kusaka nafasi ya juu  ya uongozi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo zimepiga kambi mkoani Singida kwa mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi CCM, Dkt John Pombe Magufuli pichani kuwahutubia maelfu ya wananchi waliokusanyika katika uwanja wa Peoples mjini humo kwenye mkutano wa kampeni.

Dkt Magufuli ameishauri tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC kutimiza wajibu wake wa kutenda haki kwa wagombea wote wa ngazi za Uraisi,pia amewataka Wananchi wakatae kulaghaiwa na baadhi ya watu wanaotaka madaraka kwa nguvu,kwa kuzinunua shahada zao za kupigia kura,badala yake amewaomba wazitunze shahada hizo ili ifikapo Oktoba 25 mwaka huu wapige kura.
 Maelfu ya Wananchi wa Singida wakimshangilia Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akiwahutubia na kujinadi kwa kuwaomba ridhaa ya kuwaongoza iwapo watamchagua kuwa Rais ifikapo Oktoba 25 mwaka huu,kwenye uchaguzi mkuu,Dkt Magufuli amewaomba wananchi hao alipokuwa akiwahutubia kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Peoples ,mjini Singida.
 Wakazi wa mji wa Singiga na vitongoji vyake wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi na kuwaomba wampigie kura za ndio ifikapo Oktoba 25 Mwaka huu kwenye uchaguzi mkuu wa Urais,Wabunge na Madiwani.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi,Dkt Joh Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge jimbo la Singida mjini Mussa Sima mbele ya maelfu ya Wananchi (hawapo pichani) kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Peoples  mjini Singida jioni ya leo.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akimnadi mgombea Ubunge jimbo la Iramba Magharibi kwa wakazi wa Iramba mapema leo mchana kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni,mara baada ya kumkabidhi Ilani ya chama hicho. 
Msafara wa Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli ukikatiza katika bonde la Sibiti kupitia barabara ya Nduguti kuelekea wilayani Mkalama,kwenye mkutano wa kampeni mapema leo mchana.
 Ujenzi wa Daraja la Sibiti wilayani Mkalama likiwa katika hatua za mwisho kukamilika,Daraja hilo limeleta matumaini mapya kwa wakazi hao wa Mkalama,kwani wakati wa mvua ilikuwa ni kikwazo kikubwa kwao wakati wa kusafiri na hata kusafirisha mazao yao ya biashara.

 Wananchi wa Singida na vitongoji vyake wakiwa wamekusanyika kwenye uwanja wa People's,mjini Singida katika mkutano wa kampeni wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli kabla ya kuanza kuwahutubia jioni ya leo.
   Mjumbe wa Kamati ya Kampeni CCM,Ndugu Mwigulu Nchemba akiwaomba wakazi wa mji wa Singida na vitogoji vyake waliofurika kwenye mkutano wa kampeni,kuwa ifikapo Oktoba 25 mwaka huu wajitokeza kwa wingi kumpigia kura za ndio za kutosha Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli pamoja na Mbunge na Madiwani ili wapate ushindi wa kishindo. 

  Mjumbe wa Kamati ya Kampeni CCM,Ndugu January Makamba akimuombea kura za kutosha mmgomea Urais wa CCM Dkt Maguli pamoja na Mbunge na Madiwani wa Singida mjini kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Peoples  mjini humo.
Baadhi ya Kadi za Wanachama wa Chadema zilizokabidhiwa kwa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa shule ya msingi Kiomboi,Wilayani Iramba mapema leo mchana.
 Maelfu ya wakazi wa Singida wakiwa kwenye mkutano wa kampeni za Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli,uliofanyika katika uwanja wa Peoples mjini humo.
Aliyekuwa Mbunge wa Singida Mjini (Mbunge Mstaafu),Mohamed Dewji akimwombea kura Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli kwa wananchi wa Singida na vitongoji vyake katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Peoples ,mjini Singida,Dewji pia ametangaza kumuunga mkono aliyemrithi kiti chake cha Ubunge,Ndugu Mussa Sima.

WATANZANIA WAASWA KUWAPELEKA WATOTO WAO KATIKA SHULE YA SEKONDARI IMPERIAL ILIYOPO CHALIZE MSOLWA. MKOANI PWANI

0
0
Wanafunzi wa kidato cha kwanza wa Shule ya Sekondari ya Imperial wakielekea kupandisha bendera ya Taifa wakati wakisherekea mwaka mmoja wa shule hiyo iliyopo Chalinze Msolwa mkoani Pwani.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Imperial wakiwa  ndani ya darasa la Komputa
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Imperial wakijibu maswali ya kuhusiana na komputa katika darasa hilo.
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Imperial, Ivonne Mnyitafu akitoa ufafanuzi kwa wazazi pamoja na walimu wa shule hiyo.
Mwalimu wa Taluma  wa Shule ya Sekondari ya Imperial, Peter Mwanda akizungumza katika siku ya Imperial iliyofanyika leo katika shule hiyo iliyopo Chalinze Msolwa mkoani Pwani.
Wazazi wakiwasikiliza wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Imperial wakati wa kusherekea siku ya Impirial iliyofanyika Shuleni hapo leo.
Wazazi waliowatembelea wanafunzai wa shule ya Sekondari Imperial wakielekea katika chumba cha masomo ya Sayansi (Laboratory) wakati waliposherekea siku ya Imperial iliyofanyika leo katika shule hiyo iliyopo Chalinze-Msolwa mkoani Pwani.
wanafunzai wa shule ya Sekondari Imperial wakifanya majaribio ya masomo ya Sayansi ambayo ni Fizikia pamoja na Kemia katika chumba hicho cha majaribio ya masomo hayo shuleni hapo leo.
Mkuu wa Shule na Mkurugenzi Mtendaji wa shule ya Sekondari Imperial, Arup Mukhopadhyay akitolea ufafanuzi moja ya kifaa kinachotumika kuchuja maji ambayo yamechanganywa na mchanga mbele ya wazazi na walezi waliofika shuleni hapo kwaajili  ya siku ya Imperial iliyofanyika leo shuleni hapo.
Mwenyekiti wa bodi ya shule ya Sekondari Imperial,Buhela Lunogelo akiwapongeza kuwapongeza wanafunzi wa shule hiyo mara baada ya kufanya majaribio ya masomo ya Kemia na Fizikia shuleni hapo leo.Kulia ni Mkuu wa Shule na Mkurugenzi Mtendaji wa shule ya Sekondari Imperial, Arup Mukhopadhyay.
Baadhi ya wazazi wakichukua kumbukumbu zao (Taswira mbalimbali) wakati wanafunzi wa shule hiyo wakifanya majaribio ya masomo ya Fizikia na Kemia katika chumba hicho katika shule ya Sekondari Imperial leo.
Baadhi ya wanafunzi  shule ya Sekondari Imperial wakifafanua somo la hesabu la pembe zinazoundwa na pembe tatu mbele ya wageni waalikwa na wazazi au walezi wao (hawapo pichani) waliohudhulia katika siku ya Imperial iliyofanyika Chalinze Msolwa mkoani Pwani leo.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Imperial wakifanya mdahalo katika siku  Imperial iliyofanyika leo katika shule hiyo.
Mwenyekiti wa bodi ya shule ya Sekondari Imperial, Buhela Lunogelo akizungumza na waandishi wa habari leo katika shule hiyo kuhusiana na maendeleo pamoja na uzuri wa taaluma inayotolewa katika shule hiyo kuwa ni ya kimataifa, aidha amewaomba wazazi wenye watoto wanataka kusoma kidato cha kwanza mpaka cha nne wawapeleke watoto wao katika shule hiyo iliyonzishwa Machi 3 Mwaka huu.
 Mwenyekiti wa bodi ya shule ya Sekondari Imperial, Buhela Lunogelo akiwapa zawadi wanafunzi wa shule hiyo leo Chalize Msolwa Mkoani Pwani, kushoto ni Mkuu wa Shule na Mkurugenzi Mtendaji wa shule ya Sekondari Imperial, Arup Mukhopadhyay.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Imperial wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa na vikombe na vyeti vyao walivyozawadiwa leo
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Imperialwakitoa burudani katika siku ya Imperial iliyofanyika leo mkoani Pwani.

MAHAFALI YA SITA YA BODI YA WATAALAM WA UNUNUZI NA UGAVI

0
0
Mwenyekiti wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi Dr Sr Hellen Bandiho akifungua rasmi kusanyiko la mahafali.
 Dk Hamis Mwinimvua katikati aliyemuwakilisha Mgeni Rasmi, Mwenyekiti wa Bodi, Dk Sr Hellen Bandiho  na Mtendaji Mkuu Clemence Tesha wakimshuhudia Mgeni Rasmi akizidua mtaala mpya.
 Dk Hamis Mwinimvua akitoa hutuba kwa niaba ya mgeni rasmi.
 Mgeni Rasmi, wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi na baadhi ya wahitimu katika picha ya pamoja
 Sehemu ya wahitimu wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi.
WATAALAM wa Ununuzi na Ugavi nchini wameaswa kutekeleza majukumu yao kwa weledi na kuzingatia miiko na maadili inayoongoza taaluma yao ili kuleta tija kwenye matumizi ya fedha za watanzania. Aidha Bodi imeagizwa kusimamia kwa ukaribu zaidi mienendo ya wanataaluma waliosajiliwa. 

Hayo yalisemwa na Dk. Hamis Mwinimvua Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha akimwakilisha Mgeni Rasmi Waziri wa Fedha  Mheshimiwa Saada Mkuya Salum kwenye sherehe za mahafali ya sita ya wataalam wa ununuzi na ugavi (PSPTB).

Aidha Bodi imepongezwa kwa kuzindua mtaala mpya wa masomo utakaonza kufundishwa kuanzia Januari 2016 na kutahiniwa mwezi Novemba 2016. “ni matumaini yangu pia kuwa mtaala huo utawajengea uwezo wataalam wote wa ununuzi na ugavi ili wazidi kuwa mahiri na wenye weledi mkubwa katika kufanya kazi zao” alisisitiza.

 Waziri wa Fedha aliipongeza Bodi kwa kuongeza  masomo ya maadili, ujasiliamali, utafutaji wa masoko na usimamizi wa mikataba kwani eneo hili ni  mahsusi katika kuleta maendeleo na tija katika matumizi ya rasilimali fedha. “ni matumaini yangu kwamba masomo haya yatakuza ajira kwani yatafungua wigo kwa wahitimu kuanza kujiajiri” alisema Mheshimiwa Waziri. Pia aliongeza kusema, serikali kwa upande wake imeboresha na itaendelea kuboresha zaidi mazingira ya ajira binafsi kwa minajili ya kuwawezesha wananchi kujipatia kipato halali cha kuendesha maisha yao.

Aidha aliwaagiza waajiri wote kuhakikisha kwamba wanazingatia mahitaji ya sheria juzuu Na 179, inayowataka kuhakikisha kwamba wanaajiri watumishi waliosajiliwa na Bodi.

Alihitimisha kwa kuwapongeza wahitimu 494 walitunukukiwa vyeti katika ngazi za cheti cha awali, msingi na taaluma.

MAMA SAMIA SULUHU ASIMIKWA UMALKIA WILAYANI MASWA, WAMWITA NGOLE

0
0
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa nafasi ya urais, Mama Samia Suluhu Hassan (kulia) akisimikwa kuwa Malkia wa Wasukuma Wilaya ya Maswa na akinamama wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania ya CCM (UWT) alipowasili Jimbo la Maswa Mashariki kufanya mkutano wa hadhara wa kampeni kunadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa wanaMaswa.
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa nafasi ya urais, Mama Samia Suluhu Hassan (kulia) akisimikwa kuwa Malkia wa Wasukuma Wilaya ya Maswa na akinamama wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania ya CCM (UWT) alipowasili Jimbo la Maswa Mashariki kufanya mkutano wa hadhara wa kampeni kunadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa wanaMaswa.
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa nafasi ya urais, Mama Samia Suluhu Hassan (kulia) akisimikwa kuwa Malkia wa Wasukuma Wilaya ya Maswa na akinamama wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania ya CCM (UWT) alipowasili Jimbo la Maswa Mashariki kufanya mkutano wa hadhara wa kampeni kunadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa wanaMaswa.
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa nafasi ya urais, Mama Samia Suluhu Hassan (kulia) akivishwa vazi maalum kuwa Malkia wa Wasukuma Wilaya ya Maswa na akinamama wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania ya CCM (UWT) alipowasili Maswa kufanya mkutano wa hadhara wa kampeni kunadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa wanaMaswa.
Pichani juu ni umati wa wanaCCM na wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM leo, Mama Samia Suluhu Hassan Uwanja wa Nguzo Nane Maswa Mashar.
Aliyekuwa mbunge wa CCM Jimbo la Nkenge, Asumpta Mshama akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara Uwanja wa Nguzo Nane Maswa leo.
MGOMBEA mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa nafasi ya urais, Mama Samia Suluhu Hassan leo amepewa heshima ya kusimikwa kuwa malkia wa Wasukuma Wilaya ya Maswa na kupewa jina jipya la Ng'walu Majura.

Mama Samia Suluhu amepewa heshima hiyo leo na Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania ya CCM (UWT) alipowasili Jimbo la Maswa Magharibi kufanya mkutano wa hadhara wa kampeni kunadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa wanaMaswa.


Mama Suluhu ambaye amepewa jina jipya la heshima hiyo la Ng'walu Majura alivishwa mavazi maalum ya kimila ya heshima 'Ngole' yaani malkia na kukabidhiwa mkuki maalum, ungo na usinge pamoja na kupewa zawadi anuai za vyakula vya kimila kwa kabila la Wasukuma eneo hilo.

Wakimpa heshima hiyo akinamama wa UWT walisema Mama Samia Suluhu amepewa heshima hiyo kwa kuwa ni mwanamke aliyekuja kuibua mambo mazuri kwa ushindi wa CCM na Tanzania kwa wanawake. Akinamama hao waliahidi kumuunga mkono ili kuhakikisha anashinda na kuwatoa kimasomaso Wanawakea wa Tanzania.

Kwa upande wake Mama Samia Suluhu amewashukuru akinamama hao kwa heshima na zawadi mbalimbali walizompa na kuwaahidi kupigania maslahi yao zaidi endapo chama chake kitafanikiwa kuunda Serikali katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25, 2015. Alisema licha ya kupigania maendeleo ya taifa zima yeye kama mwanamama ana ajenda maalum za kuwapigania akinamama kuanzia huduma za kijamii hadi uwezeshwaji kwao ili kuleta usawa na maendeleo kwa jamii hiyo.

Alisema amepokea kilio cha maji Maswa na kwa kuwa wanawake ndio waathirika wakubwa wa ukosefu wa maji atahakikisha Maji yanapatikana kupitia miradi anuai inayotekelezwa eneo hilo na kwa kuanzia watachimba visima 10 maeneo mbalimbali ya Maswa ili kuwapatia maji wakazi wa maeneo hayo.

Mapema majira ya asubuhi Mama Samia Suluhu alifanya mkutano wa kampeni katika Jimbo la Meatu akiinadi ilani ya CCM kwa wananchi, ambapo aliwaomba kuichagua CCM kwani imepanga kufanya mengi kwa wanaMeatu ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya barabara, ujenzi wa malambo na majosho kwa ajili ya kuhudumia mifugo yao.

Alisema ili kuondoa migogoro kwa wafugaji na wakulima safari hii Serikali itakayoundwa na CCM imepanga kupima ardhi yote ya vijiji na Wilaya na kisha kuainisha mipaka ya wakulima na wafugaji na kuwamilikisha jamii hizo kumaliza migogoro.

Msanii Snura Majanga (wa nne kutoka kushoto) akiwaburudisha wananchi walio hudhuria mkutano wa hadhara ulofanyika Mwabuzo Jimbo la Meatu leo asubuhi.
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM Taifa akinadi Sera za CCM mkutano wa hadhara Meatu leo.
Wananchi wa Mwabuzo Jimbo la Meatu wakiwasilisha kilio chao kwa mgombea mwenza CCM alipofanya mkutano eneo hilo.
Umati katika mkutano wa mgombea mwenza leo.
CCM Oyeeeeeeee....katika mkutano wa hadhara Jimbo la Maswa Mashariki.
Akinamama wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania ya CCM (UWT) alipowasili Jimbo la Maswa Magharibi wakikabidhi zawadi zao kwa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa nafasi ya urais, Mama Samia Suluhu Hassan baada ya kumsimika 'Ng'walu Majura'
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa nafasi ya urais, Mama Samia Suluhu Hassan akiwahutubia wananchi Maswa Magharibi.
Mgombea ubunge wa Jimbo la Maswa Magharibi, Mashimba Ndaki akiwahutubia wananchi kwenye mkutano huo wa hadhara.
Mgombea ubunge wa Jimbo la Maswa Magharibi, Mashimba Ndaki akiwahutubia wananchi kwenye mkutano huo wa hadhara.
Ulinzi...! Askari wa Jeshi la Polisi kikosi maalum cha ulizi kwa viongozi wakilisindikiza gari la mgombea mwenza Mama Samia Suluhu mara baada ya kumaliza kuwahutubia wananchi Maswa. 
*Imeandaliwa na www.thehabari.com

RAIS ALIPOKUTANA NA MADEREVA UBUNGO PLAZA JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na madereva wa mabasi pamoja na kuwaanga madereva hao katika hoteli ya Blue Peal jijini Dar es Salaam leo.

TAHADHARI KWA WATUMIAJI WA BARABARA YA LUPA ENEO LA NJIA PANDA ISANGA JIJINI MBEYA

0
0
Kipande cha barabara ya njia Panda Isanga karibu na Hotel ya Lifti Valey jijini Mbeya (LUPA WAY )ambacho kimejengwa upya kwa kuongezewa njia kimeleta sura mpya jijini hapa  lakini kimeleta pia changamoto kwa madereva hasa kwa nyakati za usiku  kwani hakuna taa hivyo nivema watumiaji wa barabara hii wakachukua tahadhari kwa kuto endesha kwa mwendo kasi ili kuepuka ajali zisizo za lazima ...JAMIIMOJABLOG







WASIMAMIZI NA WARATIBU WA UCHAGUZI MIKOA YA IRINGA MBEYA WATAKIWA KUJIEPUSHA NA UPENDELEO KWA WAGOMBEA

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro (PICHA MAKTABA)

Na Kahema Emanuel,Mbeya
Wito umetolewa kwa Waratibu  wa uchaguzi wa mikoa ,wasimamizi  wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi pamoja na maafisa uchaguzi wa halmashauri mikoa ya kanda za juu kusini  kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa waledi na kwa uadilifu bila kuwa na upendeleo wa chama chochote cha siasa ua mgombea .
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro wakati akifungua mafunzo ya wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi pamoja na maafisa uchaguzi halmashauri ambao ni wakurugenzi wa halmashauri na maafisa uchaguzi katika mikoa  ya Iringa na Mbeya.
Amesema ili zoezi hilo la uchaguzi liende vizuri na lisighubikwe na vurugu nivema wasimamizi hao wakatumia waledi wao na udilifu bila kuwa na upendeleo wa chama chochote cha siasa au mgombea yoyote ili kuepuka hali hiyo. 
Amesema mara baada ya kupatiwa mafunzo hayo nivema wakaendelea kutumia muda wao wa ziada kusoma na kupitia  vitabu vya maelekezo waliyopatiwa kwa kutumia kanuni na maadili ya uchaguzi ili kuimarisha uelewa zaidi kuhusu wajibu na majukumu yao katika zoezi hili la uchaguzi mkuu mwezi Oktoba.
Amesema pamoja na majukumu mengine waliyonayo pia wametakiwa kutoa kipaumbele katika kutekeleza zoezi hili la kitaifa kwa ufanisi zaidi na kwa muda uliopangwa kwani uchaguzi huu utafanyika kwa siku moja tu kwa kila baada ya miaka mitano.
Aidha amesema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetekeleza jukumu lake katika hatua ya mafunzo na maandalizi ya vifaa na rasilimali nyingine hivyo wao kama wasimamizi wanatakiwa kutekeleza wajibu wao katika ngazi zote kwa mujibu wa taratibu zilizopangwa na Tume.
Katika semina hiyo wasimamizi hao watajifunza wajibu wa wasimamizi wa vituo vya kupigia kura  ,uwendeshaji wa zoezi la upigaji kura vituoni  sanjali na uendeshaji wa zoezi la kuhesabu kura,kujumlisha kura na kutanganza matokeo ya uchaguzi.
Mwisho.

Baadhi ya wakurugenzi na Maafisa uchaguzi kutoka mikoa ya Mbeya na Iringa wakiwa katika mafunzo ya waratibu wa uchaguzi mikoa ,wasimamizi wa uchaguzi ,wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi na maafisa uchaguzi wa halmashauri yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Septemba 29 ,2015.




Afisa TEHAMA kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Ndugu Sanif Khalifan akitoa maelezo kwa washiriki wa semina ya mafunzo ya waratibu wa uchaguzi wa mikoa ,Wasimamizi wa uchaguzi ,Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi na Maafisa wa uchaguzi Halmashari katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Septemba 29 ,2015.Picha JAMIIMOJABLOG



Daniel Kalinga Afisa Uchaguzi akitoa ufafanuzi kwa washiriki wa semina hiyo ambayo itafanyika kwa siku mbili ikihusisha waratibu wa uchaguzi,Maafisa Uchaguzi ,Maafisa wasaidizi wa uchaguzi na maafisa uchaguzi Halmashauri kutoka mikoa ya Mbeya na Iringa .




Afisa Uchaguzi Kanda ya Nyanda za juu kusini -Tume Ndugu Jane Tungu akizungumza katika semina hiyo.


WANANCHI WA KIJIJI CHA KENYAMANYORI WILAYANI TARIME WANASTAHILI PONGEZI.

0
0
Kwa mbali kabisa, Kamera ya Binagi Media Group-BMG ikapata fursa ya kunasa picha za Shule ya Sekondari Kenyamanyori ambayo ilijengwa kwa nguvu za Wananchi miaka michache iliyopita na kuanza kupokea wanafunzi mwaka 2013 baada ya kukamilika ambapo wanafunzi waliokuwa kidato cha pili katika shule zilizokuwa mbali walihamia shuleni hapo na kuendelea na kidato cha pili huku wengine walichaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huo.
Na:George Binagi-GB Pazzo
Ni ukweli usiopingika kuwa uongozi wa kijiji hicho pamoja na wananchi wake ambao asilimia kubwa ni wakulima, wanastahili pongezi kwani wazo lao la kujenga shule ya sekondari ni wazo bora na limewasaidia watoto wa kijiji hicho na wale wanaotoka vijiji jirani kupata elimu karibu zaidi hivyo ni vyema wakaendelea kushirikiana na serikali pamoja na wahisani wengi katika kuhakikisha kwamba wanaiboresha zaidi shule hiyo ili iweze kuwa mkombozi kwa ajili ya watoto wao kielimu.
Kulia ni jengo la Utawala na Majengo mengine matatu kushoto ni majengo ya maabara tatu za Sayansi
Majengo mawili ya Maabara
Jengo moja la Maabara
Jengo la Utawala.

Madarasa
Vyoo 
Kuna majengo mawili ya nyumba za waalimu ambayo yamefikia hatua hii na moja limekamilika.
Shamba la Shule

WANAWAKE JITOKEZENI KWA WINGI KUPIGA KURA - MAMA SALMA KIKWETE

0
0
X1 
Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi,CCM, Mama Salma Kikwete akiwapungia mkono viongozi na wanachama wa UWT wa Mkoa wa Mara wakati akiwasili kwenye ukumbi wa Musoma Community Centre kwa ajili ya mkutano wa ndani na wanachama hao-Octoba 3, 2015.
X3 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na wanachama wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa Mkoa wa Mara wakati alipokutana nao kwenye ukumbi wa Musoma Community Centre.
X2 
Umati wa wajumbe wa Umoja wa Wanawake (UWT) wa Mkoa wa Mara wakimsikiliza kwa makini Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (hayupo pichani) wakati alipokuwa akiongea nao Mjini Musoma.PICHA NA JOHN LUKUWI.



Na Anna Nkinda – Tarime.
 Wanawake wilayani Tarime wametakiwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura siku ya uchaguzi mkuu utakaofanyika mwishoni mwa mwezi huu itakapofika na wachague viongozi watakaowaona wanafaa ambao watawaletea  maendeleo.

Rai hiyo imetolewa leo na  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea na wanawake wa wilaya hiyo iliyopo mkoani Mara katika ukumbi wa mikutano uliopo katika hoteli ya CMG.

Mama Kikwete ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM kupitia wilaya ya Lindi mjini alisema kupiga kura ni haki ya kila mtu hivyo basi haitakuwa busara kwa  wanawake hao kuharibu kura zao kwa kukaa majumbani siku ya uchaguzi ikifika bali waende kupiga kura katika vituo walivyojiandikisha .

“Kura ni siri ya mtu, wewe ndiye unayefahamu kiongozi gani wa kumchagua nawasihi chagueni viongozi wazuri na siyo bora viongozi, wahimizeni wanawake wote waliojiandikisha washiriki kupiga kura kwani kura zenu yako ndiyo itakayokupatia kiongozi unayemtaka”, alisema Mama Kikwete.

Alisema siasa siyo uadui wala ugomvi bali ni mchakato wa kidemokrasia na kuwataka wagombea wote kunadi sera zao kwa kufuata utaratibu na amani kwa kuzingatia kanuni na sheria zilizopangwa na tume ya Taifa ya Uchaguzi ili utulivu na Amani viendelee kutawala nchini.

Aliwasihi, “Msigombane kutokana na tofauti ya itikadi za vyama vya siasa, angalieni siasa zisiwafarakanishe ikafika hatua mkashindwa hata kusaidiana ikiwa ni pamoja na kushindwa kuzikana kumbukeni nyinyi ni ndugu wa wilaya moja ya Tarime”.

Aidha Mama Kikwete aliwataka  wanawake hao kujenga tabia ya  kujiwekea akiba Benki kutokana na fedha wanazozipata katika kazi wanazozifanya kwa kufanya hivyo wataweza kukopa fedha nyingi ambazo watafanyia shughuli za maendeleo na hivyo kujikomboa kiuchumi. 

“Unganeni  pamoja ili muweze kujikwamua kiuchumi, simameni katika majukwaa teteeni haki zenu, pingeni mila zilizopitwa na wakati ambazo zinamkandamiza mwanamke na hivyo kumrudisha nyuma kimaendeleo kwa kufanya hivyo mtaweza kujikomboa  kutoka katika hali ya unyanyasaji”,alisisitiza .

EALA SITTING TO BE HELD IN NAIROBI NEXT WEEK

0
0

EALA SITTING TO BE HELD IN NAIROBI NEXT WEEK

EAST African Legislative Assembly, Arusha, October 3, 2015: The East African Legislative Assembly (EALA) resumes its sitting in Nairobi, Kenya next week. The Plenary which takes place from Monday, October 5, 2015 to Thursday, October 15, 2015, is the Second Meeting of the Fourth Session of the Third Assembly.

The Assembly is to be presided over by the Speaker, Rt. Hon Daniel F. Kidega. Top on the agenda during the two week period is a Special Sitting that is expected to be addressed by President Uhuru Kenyatta. 

The Assembly is also expected to debate on and pass key pieces of legislation, adopt reports and pose questions to the Council of Ministers.Three key Bills on the cards at the EALA meeting are the EAC Forestry and Management Protection Bill, 2015, the EAC Electronic Transactions Bill, 2014 and the EAC Disaster Risk Reduction and Management Bill, 2015. 

The EAC Forestry and Management Protection Bill, 2015 hopes to promote the development, protection, conservation, sustainable management and use of the forests in the Community especially trans-boundary forests ecosystems, in the interest of present and future generations.  It further wants to espouse the scientific, cultural and socio-economic values of forests and harmonise national forest laws.

The Objective of the Disaster Risk Reduction and Management Bill, 2015 is to provide a legal framework at regional and national level for timely intervention in disaster situations and to protect the people and the natural environment affected by disaster through comprehensive disaster risk reduction and management.

EALA is further set to revisit debate on the EAC Electronic Transactions Bill, 2014 which was deferred at the last Sitting in Kampala, Uganda to pave way for additional stakeholders to make their input.   The Bill seeks to meet the need of exploiting electronic transactions in the modern day business transactions.

The Bill further wants to promote technology neutrality in applying legislation to electronic communications and transactions and to develop a safe, secure and effective environment for the consumer, business and the Governments of the Partner States to conduct and use electronic transactions. 

While in Nairobi, the House is also expected to receive and to debate on a number of reports.  They include that of the Committee on Regional Affairs on the goodwill mission to Kigoma, Tanzania and Eastern Province of Rwanda to interact with refugees from Burundi.

The Committee on Communications, Trade and Investments on its part will table for debate its Report on the oversight of EAC One-Stop Border Posts (OSBP).

At its last Sitting in Uganda in August this year, the Assembly passed the EAC Culture and Creative Industries Bill, 2015, adopted three Resolutions as well as six Reports.
 
For more Information, contact: Bobi Odiko, Senior Public Relations Officer; 
East African Legislative Assembly; Tel: +255-27-2508240 Cell: +255 787 870945+254-733-718036; Email:  bodiko@eachq.org This e-mail address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it   Web: http://www.eala.org Arusha, Tanzania

TATHMINI YA SHERIA MTANDAO - RADIO ONE

0
0

SERIKALI imeshauriwa kuutumia vema mwezi Oktoba, mwaka huu kukuza uelewa  kwa wananchi juu ya masuala ya mitandao ili kupunguza kama si kuondoa kabisa uhalifu mitandaoni.

Rai hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mtaalamu wa Usalama wa Mitandao na Uchunguzi wa Makosa ya Kidijitali, Yusuph Kileo wakati akizungumza na Majira.

"Nichukue nafasi hii kutambua na kuhamasisha tukio la kipekee katika anga ya usalama katika mitandao jambo ambalo limekuwa likiadhimishwa kila mwaka katika mwezi wa Oktoba, ambapo mataifa yanaadhimisha siku ya uelewa wa masuala ya usalama wa mitandao duniani kote," alisema Kileo.

Alisema, wakati mataifa mbalimbali duniani yakitarajiwa kuadhimisha tukio hilo anaamini Tanzania itauchukulia mwezi huo kinamna ya kipekee ili kuweza kukuza uelewa kwa watu wake.  Hilo ni tukio ambalo nategemea kampuni mbalimbali na maeneo mengine yataandaa programu mbalimbali za kukuza uelewa wa masuala ya usalama mitandaoni ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa na wanausalama wote wa mitandao duniani kote," aliongeza mtaalamu huyo.

Aidha, alisema inaaminika kama ilivyo katika uhalifu mwingine wowote kuwa ni vigumu kumaliza kabisa tatizo ila kuna njia kadhaa ambazo kwa umoja wake zikifanyiwa kazi vizuri zinaweza kabisa kupunguza kwa kiasi kikubwa  tatizo la uhalifu kwenye mitandao. 

"Tatizo kubwa  ni kuwa njia hizi zimekuwa zikiishia katika maandishi baada ya kujadiliwa na wanausalama wa mitandao; mimi binafsi nilikuwa miongoni mwao," alifafanua Kileo.

Alisema, baadhi ya njia za kukabiliana  na tatizo hilo ni kupitia elimu ya uelewa wa uhalifu katika mtandao na namna ya kujilinda. 

"Elimu hii inatoa fursa kwa mwananchi wa kawaida kutambua aina mbalimbali za uhalifu kwenye mitandao, athari zake, njia ya kujilinda na namna ya kulinda wenzake," alisema Kileo.

KUPITIA KIPINDI CHA KUMEPAMBAZUKA CHA RADIO ONE NIMEPATA KUSHIRIKI KWA NJIA YA SIMU HOJA ILIYO HOJI ---- IKIWA NI TAKRIBANI MWEZI MMOJA BAADA YA KUANZA KUTUMIKA KWA SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO HAPA NCHINI,WIZARA YA MAWASILIANO,SAYANSI NA TEKNOLOJIA PAMOJA NA WADAU WENGINE WANATOA TATHIMINI GANI.

MSIWAKEKETE WATOTO WENU - MAMA SALMA KIKWETE

0
0
Na Anna Nkinda – Maelezo, aliyekuwa Tarime
WAKAZI wa wilaya ya Tarime wametakiwa kuachana na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia hasa mila za ukeketaji na ndoa za utotoni kwa watoto wa kike.

Mwito huo umetolewa hivi karibuni na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akizindua uboreshaji wa Hospitali ya wilaya ya Tarime iliyopo mkoani Mara.

Mama Kikwete alisema ukeketaji unaleta matatizo  makubwa ikiwa ni pamoja na kupata matatizo wakati wa kujifungua, mtoto wa kike kupata maumivu makali wakati wa ukeketaji na pia kitendo hicho husababisha kutoka damu nyingi na matokeo yake ni kifo.

“Wazazi na walezi acheni mila hizi ambazo hazina faida kwa wakati huu na ni ukiukwaji wa haki za binadamu bali wasomesheni watoto wenu wa kike ili waweze kuwa walezi bora wa familia zao na jamii kwa ujumla”, alisisitiza.

Aliendelea kusema kuwa katika jamii baadhi ya wanawake wanadhalilishwa, kunyanyasika kijinsia na kupata mateso ya aina mbalimbali kama vile kupigwa, kunyimwa haki ya kumiliki mali na kutokuwa na maamuzi ya matumizi ya mali ya familia hata kama wao ndiyo wazalishaji.

Alisema, “Tabia hizi hazikubaliki kabisa katika Dunia ya leo.Mwanamke anayo haki ya kumiliki mali kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu pia anayo haki ya kufanya maamuzi  ya pamoja kwa kile alichozalisha kwani mwanamke ni binadamu na siyo chombo cha kuzalisha mali. Binadamu wote ni sawa”.

Kwa upande wa  watumishi wa kada ya afya aliwahimiza kufanya kazi kwa bidii na weledi kwa kuzingatia kwamba miundombinu ya Hospitali hiyo imeboreshwa  lengo likiwa ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya hususani akina mama , watoto na wazee.

Mama Kikwete aliwaomba viongozi, kina baba na wadau mbalimbali  waliohudhuria uzinduzi huo  kushirikiana kwa pamoja ili kupunguza  na hatimaye kuokoa kabisa vifo vya akina mama wajawazito na watoto katika wilaya hiyo pia wahakikishe kina mama na watoto wanapata huduma bora za afya. 

“Akina mama wajawazito wahudhurie kliniki muda wote wa ujauzio pia hakikisheni wanajifungulia katika vituo vya afya na hospitali. Wapelekeni watoto kliniki hadi watakapotimiza umri wa miaka mitano ili wapate kinga wanazostahili”,  aliwasihi. 

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Tarime Dkt. Calvin Mwasha alisema wazo la uboreshaji wa Hospitali hiyo liliasisiwa na Mkuu wa wilaya hiyo Glorius Luoga alipofanya ziara Hospitalini hapo mwanzoni mwa mwaka huu na kubaini kuna matatizo ya uchakavu mkubwa wa majengo.

Uchakavu wa miundombinu ya maji safi na taka, ubovu wa mfumo wa umeme, uchakavu wa vitanda na matandiko,uchakavu na uhaba wa vifaa tiba na vitendea kazi, uhaba wa madawa, ukosefu wa jengo la utawala na upungufu wa watumishi mbalimbali.

“Wadau mbalimbali wa ndani na nje ya wilaya ya Tarime wakiwemo wafanyabiashara wakubwa na wakati, wachimbaji madini wakubwa (ACACIA North Mara Gold Mine) na wadogo, Taasisi za Umma na binafsi, watumishi wa Umma na wananchi walifanikiwa kuchanga shilingi milioni 345, mashuka 80 na vitanda tisa”, alisema Dkt. Mwasha.

Aliyataja maboresho yaliyofanyika kuwa ni majengo ya wagonjwa wa nje, akina mama na watoto, maabara, upasuaji ambapo mwanzo kulikuwa  na chumba kimoja cha upasuaji baada ya maboresho kuna vyumba vinne na jengo la upimaji virusi kwa hiari (VCT).

Wodi za wazazi, magonjwa ya akina mama na upasuaji, akina baba, TB wanaume na wanawake, majengo ya jiko ambalo kwa sasa litatumika kama jengo la kuhudumia wateja wa mifuko ya bima ya afya (CHF na NHIF) na jengo la ufuaji.Ujenzi ambao bado kuanza ni Jengo la utawala na sehemu ya kupumzikia  wagonjwa.

Dkt. Mwasha alisema kuna  vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 263 ambavyo vimeagizwa kutoka China kupitia kwa mwenyekiti wa maboresho Peter Zacharia. Kutokana na mahusiano yake mazuri na wafanyabiashara wa huko vifaa hivyo ambavyo bado  havijalipiwa vimeshafika wilayani Tarime.

Baadhi ya vifaa hivyo ni mashine ya standard stabilizer moja, oxygen concentrator moja, vitanda 130, baiskeli za kubebea wagonjwa 20, mashine ya kupimia full blood picture moja, BP Machine Digital 50 na nguo za kuvaa wagonjwa.

Hospitali ya wilaya ya Tarime ilijengwa mwaka 1956 tangu kipindi hicho inahudumia wananchi wa wilaya  hiyo, Serengeti na Rorwa.

Mpango mkubwa hati za umiliki ardhi kimila mbioni

0
0
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
SERIKALI  imesema inafanyia kazi mpango mkubwa wa kupima ardhi zinazomilikiwa kimila na kutoa hati kwa wahusika.

Mpango huu ambao uko mbioni kuanza kama majaribio ni moja ya maazimio ya mkutano wa 9 wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) uliomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Akitoa majumuisho ya mkutano huo kwa waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya TNBC, Balozi Ombeni Sefue alisema kuharakishwa kwa mpango wa kutoa hati za umiliki wa ardhi za kimila kutasaidia watanzania walio wengi zaidi kuweza kwenda katika vyombo vya fedha, kupata mikopo na kuboresha maisha.

Balozi Sefue ambaye pia ni Katibu Mkuu Kiongozi alisema tayari ofisi ya Mpango wa Kurasimisha Mali na Biashara Tanzania (MKURABITA) na Wizara ya Ardhi na Makazi zinaoanisha mifumo itakayowezesha mchakato huo kuwa wa haraka na gharama nafuu.

“Hatua hii itasaidia kupunguza gharama na watu wengi zaidi kufikiwa,” alisema, na kuongeza kuwa timu ya wataalamu kutoka serikalini itaundwa kushughulikia swala hilo.

Mpango huo utatumia vifaa na njia za kisasa na taarifa zote za ardhi zitaweza kupatikana kielektroniki.

Mapema, Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa TNBC alisema mpango huo utasaidia kuongeza thamani ya ardhi na kusaidia kuondoa migogoro ya ardhi hapa nchini.

Kwa mujibu wa Balozi Sefue utaratibu wa kuanzisha idara itakayosaidia ushiriki wa watanzania katika uwekezaji wa ndani na nje unaendelea.

Idara hiyo itakayokuwa katika Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) inalenga kujenga uwezo kwa watanzania na kuwafanya kuwa sehemu ya mchakato mzima ujenzi wa uchumi na sio kubaki kuwa watazamaji tu.

Mkutano huo pia uliongelea maswala mbalimbali yanayolenga kuimarisha mazingira ya biashara nchini na utalii.  Muda maalumu wa utekelezaji wa maswala hayo uliwekwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bw. Godfrey Simbeye alisema mkutano huo ulikuwa wa mafanikio.

“Hii inaonyesha kuwa sekta binafsi na umma zinaweza kufanya kazi pamoja kwa maendeleo ya nchi,” alisema.

Katibu Mtendaji wa TNBC, Bw. Raymond Mbilinyi alisema mkutano huo ulikuwa ni uthibitisho kuwa maendeleo yanaweza kupatikana kwa haraka kama sekta hizo zitafanya kazi kwa ushirikiano wa dhati.

Wakati wa mkutano huo, Rais Kikwete alizindua mfumo wa kielektroniki wa usajili wa majina ya biashara.

Mfumo huo ulioanza kutumika na wateja wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) mwezi wa Sita mwaka huu unamwezesha mwananchi kupata jina la biashara ndani ya dakika kumi tu kama kila kinachohitajika kipo.



Mkutano huo ulikuwa wa mwisho kuendeshwa na Rais Kikwete kama Mwenyekiti wa TNBC kabla ya kumalizika kwa muda wake wa uongozi mwaka huu.

FREIGHT IN TIME (TZ) LTD, UPS’ AUTHORISED SERVICE CONTRACTOR IN TANZANIA HOLDS CUSTOMER EVENT

0
0
Mr Shamit Shah,Group Executive Director FiT
Mr Shamit Shah, Group Executive Director FiT.
Mr Dave(Centre) Freight in Time Financia Controller and guests
Mr Dave (Centre) Freight in Time Financial Controller and guests.
Mr Fred Mlay Freight in Time Business Development Manager Tanzania with Guests
Mr. Fred Mlay, Freight in Time Business Development Manager Tanzania with Guests.
victor maina, air and sea freight commercial manager
Victor Maina, Air and Sea Freight Commercial Manager exchanging views with the invited guests.
CEO sign industries M.P Esmail
CEO sign industries M.P Esmail giving a comment.

IMG_9978
Invited guests mingle during the event.
IMG_9889
Freight In Time (TZ) LTD (‘FiT’), the Authorized Service Contractor of UPS (NYSE: UPS), a global leader in logistics,opened its doors tovalued customers at a special event today at The Southern Sun Hotel in Dar es Salaam. The event highlighted FiT’s appreciation to local customers and in turn provided customers with an opportunity to meet FiT’s management and ask questions first hand.

FiTopened in Tanzania in 1997 and provides customers with a broad range of services with flexible pick-up and delivery times. Since 2005, the company became the authorized service contractor in Tanzania ofUPS and has served its customers with the highest level of service backed by UPS’s world class network and technology, its focus on service quality, and a deep-rooted culture of precision and innovation..UPS is a recognized leader with expertise in international air freight forwarding, regional supply chain management and intra-Africa logistics. Customers can combine package and freight services for greater supply chain efficiency and cost-effectiveness.

Shamit Shah, Group Executive Directorof FiT commented, “FiT and UPS’partnership in Tanzania has gone from strength to strength over the last 10 years and we wanted to give something back to our loyal customers. The event is a testimony of our commitment to providing our customers with an efficient, reliable service. Providing a platform for discussion and interaction, the event also offered an opportunity to demonstrate our appreciation of their loyalty.”

“Our customers are at the heart of what we do, we will continue to support our clients to develop their businesses, through our global network and innovative services facilities”, he added.

FiTemploys 72 local citizens and operates at airports in Dar, Zanzibar, Kilimanjaro, Mbeya and Mwanza. UPS Border point offices include Namanga, Holili,HoroHoro, Tunduma, Kasumulu and Sirare, whilst also serving seaports in Dar Es Salaam and Mombasa.
UPS, a global leader in logistics with 435,000 employees worldwide, has been in the region since 1988, with its regional headquarters based in the UAE. The India Sub-Continent, Middle East and Africa region is the largest UPS region with more than 70 active countries. Through access to a worldwide network serving over 220 countries and territories, UPS is invested to the success of a daily delivery average of more than 18 million packages and documents.
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live




Latest Images