Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 656 | 657 | (Page 658) | 659 | 660 | .... | 1896 | newer

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya Uchangishaji fedha kwa Uhifadhi wa vyanzo vya maji katika Mabwawa ya kuzalisha Umeme ya Mtera, Kihansi, Kidatu, Nyumba ya Mungu na Pangani. Hafla hiyo ilifanyika jana usiku Sept 28, 2015 kwenye Hoteli ya Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Mwenyekiti wa Mabibo Beer, Wines & Spirits na Mkurugenzi wa VIP Engineering Marketing Ltd, Benedicta Rugemalira, wakati wa hafla ya Uchangishaji fedha kwa Uhifadhi wa vyanzo vya maji katika Mabwawa ya kuzalisha Umeme ya Mtera, Kihansi, Kidatu, Nyumba ya Mungu na Pangani, iliyofanyika jana usiku Sept 28, 2015 kwenye Hoteli ya Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya IPTL, Parthiban Chandrasakaran,  wakati wa hafla ya Uchangishaji fedha kwa Uhifadhi wa vyanzo vya maji katika Mabwawa ya kuzalisha Umeme ya Mtera, Kihansi, Kidatu, Nyumba ya Mungu na Pangani, iliyofanyika jana usiku Sept 28, 2015 kwenye Hoteli ya Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Mkuu wa Idara ya Fedha na Utwala wa REA, George Nchwale,  wakati wa hafla ya Uchangishaji fedha kwa Uhifadhi wa vyanzo vya maji katika Mabwawa ya kuzalisha Umeme ya Mtera, Kihansi, Kidatu, Nyumba ya Mungu na Pangani, iliyofanyika jana usiku Sept 28, 2015 kwenye Hoteli ya Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam.

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Mkurugenzi wa Sheria wa TCRA, Elizabeth Nzagi,  wakati wa hafla ya Uchangishaji fedha kwa Uhifadhi wa vyanzo vya maji katika Mabwawa ya kuzalisha Umeme ya Mtera, Kihansi, Kidatu, Nyumba ya Mungu na Pangani, iliyofanyika jana usiku Sept 28, 2015 kwenye Hoteli ya Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam.
    Picha na OMR

  0 0

   Aliyekuwa  mbunge wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa akishuka katika gari la  polisi  baada ya  kufikishwa mahakamani  wakati wa vurugu za machingaji  eneo la mashine tatu  mjini Iringa mwaka  jana(picha na maktaba ya matukiodaima)

  Na MatukiodaimaBlog
  JESHI  la polisi kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) mkoani  Iringa watumia mabomu ya machozi kuwakamata wafuasi  zaidi ya 60  wa  chama  cha  Demokrasia  na maendeleo (chadema ) akiwemo mgombea  ubunge wao  jimbo la  Iringa mjini  mchungaji Peter Msigwa matatani  kwa kumpiga mawe mkuu wa kikosi cha  kutuliza ghasia (FFU) Iringa na   wananchi  waliokuwa  wakitoka katika mkutano  wa mgombea  Urais wa chama cha mapinduzi (CCM) Dr John Magufuli.

  Baada ya  polisi kufatua mabamo mawili ya machozi kwa ajili ya  kusambaratisha  wafuasi hao baadhi yao  walikimbia huku  mgombea  ubunge  huyo Mchungaji Msigwa akienda kujisalimisha mwenyewe  polisi baada ya  kutakiwa  kufanya   hivyo kabla ya  kukamatwa na  polisi.

  Imeelezwa  kuwa   wafuasi hao ambao  wengi  wao ni vijana walikuwa  wamekutana katika  eneo la kambi ya  kampeni ya Chadema  iliyopo  eneo la Hoteli  ya  Sambala jirani na kambi ya kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) kwa  ajili ya kikao cha ndani toka majira ya mchana na jioni  ndipo  walipofanya  vurugu   hizo  wakati wananchi  wakitoka katika  mkutano wa kampeni za mgombea  huyo wa Urais wa CCM.
   
  Kamanda  wa  polisi  wa  mkoa  wa Iringa Rmadhan Mungi aliwaeleza  jana  waandishi wa habari  kuwa tukio  hilo  lilitokea   jana  majira ya saa 12;30   jioni baada  ya  wafuasi hao  kufunga barabara  kuu ya  Iringa –Dodoma  na  kufanya  vurugu  hizo kwa kuwarushia mawe  wananchi  waliokuwa  wakitoka katika  mkutano wa kampeni za Dr Magufuli uwanja  wa  Samora.
   
  Alisema  kuwa  wakati  jeshi la polisi  likiwa katika mkutano wa mgombea  huyo wa Urais wa CCM walipokea taarifa kuwa  kuna  vijana wa  boda  boda  zaidi ya 150 walikuwa  wakijikusanya  kuelekea  katika eneo hilo la Sambala Lodge  na baada ya kufuatilia ndipo  walibaini  kuwa  wanakwenda katika  kikao chao cha  ndani  na kwa kawaida  jeshi la  polisi halikatazi  watu  kufanya  vikao  vyao vya  ndani .

  “Jeshi  la  polisi  halizuii  wanachama wa  chama  chochote cha siasa  kufanya vikao vya ndani kwani  ni haki yao ya  kisheria na kikatiba …..lakini  baada ya  kikao chao kumalizika  vijana hao  walitoka  nje ya ukumbi  huo uliopo kando kando ya  barabara na  kuanza  kufunga  barabara  na kucheza muziki katikakati ya barabara na kuzuia watumiaji wengine wa barabara  kushindwa  kupita  ……baada ya   vurugu hizo nilimuagiza mkuu wa FFU  kwenda  kuwatoa watu  hao  barabara ila  walipuuza na kuishia kumpiga mawe  na  baadae  kukimbilia kujifungia katika Lodge hiyo ya Sambala  eneo  ambalo  wamefanya kama makao makuu ya Kampeni za Chadema  “ alisema kamanda Mungi.

  Alisema  wakati wa vurugu  hizo baadhi ya  vijana  waliumia kwa  kuruka ukuta  na wengine kwa  kuanguka wakati wa  kujaribu  kukwepa  kukamatwa na  kuwa wale  wote waliokamatwa  watafikishwa mahakamani wakati  wowote  kuanzia  sasa na  kuwa miongoni mwao  yumo mgombea  ubunge  jimbo  hilo Mchungaji Msigwa .

  Mbali ya  mchangaji  Msigwa   wengine  waliokamatwa kwa tuhuma  za  vurugu  hizo  ni pamoja na mgombea  udiwani  kata ya  Gangilonga  ambae  pia ni mkuu wa kambi hiyo Dady Igogo
   
  Kamanda  Mungi  alisema  watuhumiwa  wote  watafikishwa mahakamani  wakati wowote  kuanzia sasa mara baada ya upelelezi  kumamilika  alisema  kuwa mchungaji Msigwa hakuwepo katika  eneo la  tukio wakati  vurugu hizo  zikitokea  ila ameingizwa katika  orodha  ya  watuhumiwa kwa  wakosaji wakuu  wapo  makundi manne likiwemo moja la  yule  anaendenda kosa kwa  mikono  yake ,kundi  la  pili  muwezeshaji au  mshauri  na  kundi la nne kutoa hamasa kwa  wakosaji hivyo  alisema mgombea  huyo anashikiliwa kwa kutuma za  kutoa hamasa kwa watuhumiwa hao  kufanya  vurugu.
   
  Wakati  huo  huo jeshi  hilo la  polisi  limepiga marufuku  vyama  vyote  vya  siasa kuwahamasisha wafuasi ama  wanachama  wake  kufanya  vurugu  za wakati  huu  wa kampeni na  kuwa kamwe jeshi  hilo halitamvumilia kiongozi ama mtu  yeyote atakayejihusisha na uvunjifu wa amani.

  “Amani ni  kitu cha kwanza na yeyote anayetishia  kuvuruga amani ya Iringa anatishia kazi  za  polisi Iringa kamwe  hatavumiliwa  zaidi ya  kuchukuliwa hatua kali na kuwataka  vijana  kuepuka  kutumiwa na wanasiasa  kufanya vurugu  “

  Kuhusu  mwenendo  wa  kampeni toka  zianze alisema  kuwa  hadi  sasa  tupo  nusu ya kampeni  hizo  toka  zianze na  kuwa  toka  tarehe 22 hadi 30  mwezi wa nane hakukuwa na  kosa  lolote   lililoripotiwa kutokea  kuhusiana na kampeni  ila  tarehe 1 hadi 5 mwezi wa tisa  kulikuwa na makosa 9  yaliyoripotiwa kituoni na  tarehe 5- 19 kulikuwa na makosa 17 yaliyoripotiwa na makosa 15  yalitokea  jimbo la Iringa mjini na makosa mawili  wilaya ya  Mufindi huku katika wilaya ya Kilolo hakuna  kosa hata  moja
  Hivyo amewataka  wagombea na  wafuasi wao  kufuata maelekezo  yaliyomo katika kitabu  cha maadili ya uchaguzi kilichotolewa na tume ya Taifa ya  uchaguzi .
   

  Kwa  upande  wake  mgombea  ubunge  wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Msigwa katika ukurasa  wake wa fecaboook alithibitisha kukukamatwa kwa  vijana  hao na kiongozi wa kambi  hiyo Bw Igogo wakiwa katika ngome    hiyo ya kampeni.

  0 0

  Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Stephen Wasira
  Na Eleuteri Mangi MAELEZO
  29/09/2015
  Serikali ya Tanzania na Poland zimeingia makubaliano ya ushirikiano yatakayosaidia kukuza sekta ya kilimo kwa kuwawezesha wakulima kupata zana bora za kilimo kupitia  Kampuni ya kutengeneza Matrekta ya Ursus kutoka nchini Poland itakayoanza kufanya kazi zake nchini Tanzania mwanzoni mwa mwaka 2016.

  Akizungumza mara baada ya kufanyika kwa mkutano wa makubaliano hayo kati ya Serikali ya Tanzania na  ujumbe wa wataalam wa kilimo kutoka nchini Poland ulioongozwa na Waziri wa Kilimo na Maendeleo Vjijini wa Poland Bi. Zofia Szalczyk jana jijini Dar es salaam, Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Stephen Wasira alisema kuwa makubaliano hayo yanalenga kuinua sekta ya kilimo na kurahisisha upatikanaji wa matrekta hapa nchini.

  Alisema Kampuni ya kutengeneza Matrekta ya Ursus kutoka  Poland imepewa jukumu la kuleta vipuri vya matrekta na kuviunganisha hapa hapa nchini ikishirikiana na Shirika la Uchumi na Maendeleo la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT).

  “Tumeingia mkataba na Seikali ya Poland ili kuinua na kuimarisha sekta ya kilimo nchini kupitia  uundwaji wa matrekta haya hapa nchini, kazi hii itasaidia kupunguza  kilimo cha jembe la mkono ambacho kinafikia asilimia 62  na  asilimia 38 iliyobaki inajumuisha kilimo cha jembe la kukokotwa na wanyamakazi “plau” pamoja na matrekta” Alisema.

  Aliongeza kuwa Serikali itawajengea uwezo SUMA JKT ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo na  kuondoa hali iliyopo ya uagizaji wa matrekta yaliyounganishwa  ambayo hutumia gharama kubwa na kusababisha  wakulima wengi hushindwa kumudu gharama ya kuyanunua.

  “Wakulima wataunganishwa na Benki ya kilimo nchini kwa kupewa mikopo mbalimbali ya kununua vifaa vya kutendea kazi mbegu pamoja na mbolea ili kukifanya kilimo kiwe cha kisasa zaidi” alisema Wasira.

  Wasira alisema kuwa Maghala yaliyopo nchini yanauwezo wa kuhifadhi chakula tani 240,000 baada ya kukamilika ujenzi wa maghala hayo kutakuwa na uwezo wa kuhifadhi tani 446,000 za chakula ambapo zitatumika Dola za Kimarekani milioni 110 katika ujenzi wa maghala hayo.

  Aidha, Wasira aliongeza kuwa ili kuwa na mafanikio katika sekta ya kilimo nchini, Serikali itapeleka wataalamu wa matrekta kila mkoa.

  Kwa upande wake Waziri wa Kilimo na Maendeleo Vjijini wa Poland Bi Zofia Szalczyk alisema kuwa hatua iliyofikiwa na Serikali ya Tanzania ni ya muhimu katika katika kuongeza tija katika uzalishaji kupitia sekta ya kilimo.

  Alisema Poland imefanikiwa katika sekta ya kilimo kwa sababu inashirikiana na taasisi za kifedha za kimataifa ambapo ameisifu Tanzania kuchukua uamuzi huo ambao utaiwezesha kuwa na kilimo chenye tija.


  Adha, ameishukuru Serikali ya Tanzania kupitia Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika pamoja na Waziri wa Fedha nchini na kuahidi kuendelea kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili katika masuala mbalimbali ya kijamii, kiuchumi na kisiasa. 

  0 0

  Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi katika moja ya mikutano yake ya kampeni inayoendelea nchini akiinadi ilani ya CCM. Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi katika moja ya mikutano yake ya kampeni inayoendelea nchini akiinadi ilani ya CCM.

   MCHUANO wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajia kufanyika Oktoba 25, 2015 unaendelea maeneo mbalimbali ya nchini, huku vyama anuai vilivyofanikiwa kuingia katika ushindani huo wa kisiasa vikinadi ilani na sera zao kwa Watanzania ili kuwashawishi wachaguliwe.

   Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa mara ya kwanza kimemsimamisha mwanamke katika ngazi ya juu ya uongozi. Kimemteuwa mwanamama, Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea mwenza wa mgombea wa nafasi ya urais kupitia chama hicho, John Pombe Magufuli. 

  Kwa mantiki hiyo endapo kitafanikiwa kushinda urais Tanzania kwa mara ya kwanza mwanamke atashika nafasi ya juu ya madaraka ndani ya Serikali. Bi. Suluhu ambaye amewahi kufanya kazi kama kiongozi katika Serikali zote mbili yaani Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Zanzibar (Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar-SMZ) anauzoevu wa kutosha na elimu nzuri inayomuongeze sifa ya kuimudu nafasi aliyopewa kwa sasa.

   Ki historia, Bi. Suluhu alizaliwa Januari 27, mwaka 1960 nchini na kupata elimu yake ya msingi na sekondari Zanzibar, kabla ya kuendelea na elimu ya juu kwa kozi mbalimbali katika vyuo vikuu vya Mzumbe nchini Tanzania, Chuo Kikuu cha Manchester nchini Uingereza kwa ushirikiano na Chuo Kikuu Huri cha Tanzania (OUT). [caption id="attachment_62370" align="aligncenter" width="741"]Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan (kulia) akimjulia hali mmoja wa akinamama katika moja ya wodi za wazazi nchini. Kiongozi huyo anaahidi endapo atashinda uchaguzi kupitia chama chake ataziangalia zaidi huduma za afya ya uzazi ili kuboresha zaidi.Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan (kulia) akimjulia hali mmoja wa akinamama katika moja ya wodi za wazazi nchini. Kiongozi huyo anaahidi endapo atashinda uchaguzi kupitia chama chake ataziangalia zaidi huduma za afya ya uzazi ili kuboresha zaidi.

   Mwanamama huyu pia amefanikiwa kuchukua kozi ndogo ndogo anuai katika vyuo vya ndani na nje ya Tanzania, vikiwemo vya; 'Institute of Management for Leaders, Hyderabad, India', Zanzibar Institute of Financial Administration, ZIFA, pamoja na National Institute of Public Administration, Lahore Pakistan. Mgombea huyo mwanamama amekuwa waziri na mbunge kwa zaidi ya miaka mitano mfululizo na pia kufanikiwa kushika nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, nafasi ambazo kwa kiasi kikubwa zinamuongezea sifa ya kuweza kuimudu nafasi aliyopewa kwa sasa anasema hii ni nafasi pekee kwa akinamama wote bila kujali itikadi zao kumuunga mkono ili aweze kushinda na kuweka historia nchini ya mwanamke kushika nafasi ya juu kuliko zote nchini. 

  Kwa sasa kiongozi huyu anazunguka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani kuinadi ilani ya CCM. Bi. Suluhu anasema ilani ya CCM imepanga kufanya mengi mazuri kwa Watanzania, lakini pamoja na hayo amejitolea kuhakikisha anawapigania akinamama endapo atafanikiwa kushinda nafasi hiyo ili kuweza kukabiliana na changamoto anuai ambazo zimekuwa kero na kikwazo kwao.

   Anazitaja changamoto hizo ni pamoja na huduma za afya ya uzazi ambapo akinamama wengi na watoto wachanga wamekuwa wakipoteza maisha katika eneo hilo.

   Anasema licha ya ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM kufafanua zaidi itakavyo boresha huduma za afya kiujumla, lakini atalisimamia na kuongeza nguvu za ziada kuhakikisha akinamama wanapata huduma za kuridhisha maeneo wanapopata huduma za afya ya uzazi. 


   Akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika Jimbo la Mbulu Mjini anasema endapo CCM itashinda uchaguzi huu imepanga kuajiri watumishi 15,000 wa sekta ya afya wakiwemo madaktari 2020 ndani ya kipindi kifupi ili kuhakikisha inaboresha zaidi huduma za afya maeneo mbalimbali nchini hasa huduma za akinamama na watoto. 

  Bi. Suluhu anasema hatua hiyo ni mpango maalumu wa kuboresha huduma za afya kiujumla na hasa huduma za akinamama wajawazito na watoto ambapo wamekuwa na changamoto katika huduma hizo.
  Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan akiinadi ilani mpya ya Uchaguzi Mkuu ya CCM kwa wananchi (hawapo pichani) katika moja ya mikutano yake.Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan akiinadi ilani mpya ya Uchaguzi Mkuu ya CCM kwa wananchi (hawapo pichani) katika moja ya mikutano yake.[/caption] Aidha anaongeza kuwa mpango mwingine ni kuwawezesha akinamama na vijana kiuchumi kupitia vikundi vyao.

   Anabainisha kuwa eneo hili Serikali ya CCM kupitia ilani yake imetenga shilimi milioni 50 kwa kila kijiji fedha ambazo zitakuwa zikikopeshwa makundi hayo kwa masharti nafuu ili waweze kujikwamua kiuchumi. Anasema eneo hilo pia halmashauri zitasimamiwa kutoa asilimia tano ya mapato kuwaunga mkono akinamama na vijana ili kuchochea maendeleo yao. 

  Ili kukuza biashara zao Bi. Suluhu anasema Serikali itasimamia kuhakikisha asilimia 30 ya tenda ndogondogo za halmashauri mbalimbali zipewe vikundi vya akinamama na vijana.

   Anaeleza kuwa ili kuongeza thamani kwa mazao yatakaokuwa yakizalishwa na vikundi hivyo kupitia miradi ya kilimo imepanga kujenga viwanda vingi maeneo mbalimbali ya nchi ambavyo vitayaongezea thamani mazao na pia kuzalisha ajira kwa asilimia 40, jambo ambalo pia litakuza uchumia wa akinamama na vijana.

   Mwanamama huyo shupavu anabainisha kuwa kutokana na suala la kero ya maji pia kuwaumiza zaidi akinamama ilani ya chama chake imedhamiria kumalizia miradi ya maji na kuanzisha mingine anuai ili kukabiliana na changamoto ya kero ya maji safi na salama iliyopo maeneo mbalimbali ya nchini vijijini ama mjini.

   Bi. Suluhu anasema Serikali watakayoiunda itaendelea kushughulikia kero ya maji katika vijiji vyenye ukame na kuhakikisha kila kijiji kinapata maji safi na salama kwa matumizi. Lakini ili kumaliza kabisa kero hiyo anasema Serikali itaunda mfuko wa maji ambao utashughulikia kero za huduma za maji safi na salama. 

   Anasema migogoro yoyote inayosababisha mapigano idadi kuwa inayoathirika ni wanawake na watoto, hivyo Serikali itakayoundwa na CCM itahakikisha inapima ardhi yote ya vijiji pamoja na Wilaya na kuainisha mipaka ili kukomesha migogoro ya ardhi inayochangia mapigano ya wakulima na wafugaji baadhi ya maeneo ya Tanzania mara kwa mara.Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan (mwenye miwani) akisalimiana na baadhi ya akinamama na wananchi katika moja ya mikutano yake ya kampeni.Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan (mwenye miwani) akisalimiana na baadhi ya akinamama na wananchi katika moja ya mikutano yake ya kampeni.Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) akihutubia wananchi katika moja ya mikutano yake ya kampeni inayoendelea nchini akiinadi ilani ya CCM.Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) akihutubia wananchi katika moja ya mikutano yake ya kampeni inayoendelea nchini akiinadi ilani ya CCM.

   Anasema mara baada ya kupima ardhi na kuweka mipaka kati ya maeneo ya wakulima na wafugaji watahakikisha mipaka hiyo inatambulika na kuheshimiwa na jamii zote mbili ili kuzuia migogoro na mapigano ambayo yamekuwa na uhasama mkubwa na kupoteza uhai na mali za raia wasio kuwa na hatia katika maeneo yenye mgogoro. 

   Hata hivyo katika kampeni zake mara zote amemalizia kwa kuwaomba wananchi kutunza amani iliyoasisiwa na viongozi wetu wa taifa kwa kutokubali kuyumbishwa na kushawishia kuvuruga amani ya nchi. "...Tusikubali kuchokozwa na kuchokoseka na kuvuruga amani...bila amani hakuna maendeleo," alisema Bi. Suluhu. 

   Anawataka viongozi wa siasa kuacha kutoa vitisho kwa wapiga kura kwani hali hiyo ni kuibaka demokrasia hivyo CCM na vijana wake hawatakuwa tayari kuona demokrasia inabakwa nchini na wapuuzi wachahe. "...Vijana wa CCM naomba mkikamata kibaka wa demokrasia shughulikeni naye kidogo kabla ya kumpeleka polisi...CCM itashinda kwa kishindo," alisema Nape Nnauye. Miongoni mwa vyama vinavyoshiriki uchaguzi huo kulingana na taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ni pamoja na CCM, CUF, CHADEMA, UMD, NCCR- Mageuzi, NLD, UPDP, NRA, TADEA, TLP, UDP, DEMOKRASIA MAKINI, CHAUSTA, DP, APPT-Maendeleo, Jahazi Asilia, SAU, AFP, CCK, ADC, CHAUMMA na ACT-Wazalendo.
   *Imeandaliwa na www.thehabari.com

  0 0

  3
   Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva akiteta jambo na Kamishna wa Tume hiyo, Jaji mstaafu Vincent Msena wakati wa mkutano baina ya NEC na wawakilishi wa vyama vya watu wenye ulemavu nchini uliofanyika leo Jumanne Septemba 29, 2015 Jijini Dar es Salaam.PICHA NA ISMAIL NGAYONGA
  5Mwenyekiti wa Shirikisho la Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Mkoa wa Mwanza, Alfred Kapole akichangia mada wakati wa mkutano mkutano baina ya taasisi za watu wenye ulemavu nchini na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) uliofanyika leo Jumanne Septemba 29, 2015 Jijini Dar es Salaam.
  1Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva akisalimiana na Mwakilishi wa Chama cha Kitaifa cha Watu Wasioona Zanzibar (ZANAB), Adili Mohamed wakati wa mkutano baina ya taasisi za watu wenye ulemavu nchini na NEC iliyofanyika leo Jumanne Septemba 29, 2015 Jijini Dar es Salaam.
  2  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva akisalimiana na Mwakilishi wa Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Mkoa wa Dar es Salamm Mohamed Chazi wakati wa mkutano baina ya taasisi za watu wenye ulemavu nchini na NEC iliyofanyika leo Jumanne Septemba 29, 2015 Jijini Dar es Salaam.
  4  Mwakilishi wa Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Mkoa wa Pwani Hussein Kibindu akisoma taarifa ya mada ya tathimini ya uchaguzi mkuu wa oktoba 25 mwaka huu wakati wa mkutano baina ya taasisi za watu wenye ulemavu nchini na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) uliofanyika leo Jumanne Septemba 29, 2015 Jijini Dar es Salaam.
  6Mkalimani wa lugha ya alama, Kudra Munishi akitoa ufafanuzi wa mada na hoja kwa watu wenye ulemavu wa kusikia wakati wa mkutano baina ya taasisi za watu wenye ulemavu nchini na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) uliofanyika leo Jumanne Septemba 29, 2015 Jijini Dar es Salaam.

  ………………………………………………………………………………..
  Na Ismail Ngayonga -MAELEZO Dar es Salaam
  TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imevitoa wasiwasi vyama vya siasa kuwa hakutakuwepo na wizi na udanganyifu wa kura katika matokeo ya uchagauzi wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajia kufanyika nchini tarehe 25 Oktoba, mwaka huu.
   AIdha NEC imesema ipo tayari kushirikiana na wataalamu wa vyama hivyo katika kubaini vyanzo vya wizi wa kura iwapo tatizo hilo litajitokeza na hivyo kuhakikisha haki inatendeka kwa vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi huo.
   Hayo yamebainishwa leo Jumanne (Septemba 29, 2015) Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Damian Lubuva wakati wa mkutano wake na wawakilishi wa vyama vya watu wenye ulemavu aliokutana nao kwa ajili ya kupata ushauri na maoni ya taasisi hizo kuelekea uchaguzi mkuu mwezi oktoba mwaka huu.
   Jaji Lubuva alisema hadi kufikia sasa, vyama vyote vyote vinavyoshiriki uchaguzi huo vimefanyika kampeni za kistaarabu ingawa katika siku za hivi karibuni baadhi ya vyama vimekuwa vikitoa kauli na matamshi yaliyovuka mipaka, ambapo NEC imevionya vyama kuacha mara moja tabia hiyo.
   “Vipo baadhi ya vyama vya siasa na wagombea wao wamekuwa wakitumia muda mwingi kutoa lugha zisizofaa baada ya kunadi sera ya vyama vyao, vyama hivyo tumekutana nao na kuwataka kuacha mara moja kampeni za aina hiyo” alisema Jaji Lubuva.
   Jaji Lubuva alisema tarehe 27 Julai mwaka huu, vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi mkuu vilisaini maktaba wa maadili ya uchaguzi huo, hivyo ni wajibu wa vyama hivyo kuzingatia viapo walivyotoa katika maktaba huo.
   Akifafanua zaidi Jaji Lubuva alisema iwapo chama chochote hakina hoja ya kuzungumza na wananchi ni vyema kikawa kimya hadi siku ya uchaguzi tarehe 25 Oktoba mwaka huu.
   Aidha Jaji Lubuva alivitaka vyama vya siasa kuacha tabia ya kuingilia masuala ya utawala ya tume hiyo, kwani kwa kufanya hivyo vyama hivyo vitakuwa vikifanya kazi za tume hiyo na hivyo kuingilia masuala ya ndani ya kiutendaji ya taasisi hiyo.
   Akizungumzia maandalizi ya uchaguzi huo, Jaji Lubuva alisema mahitaji yote ya msingi ya uchaguzi huo tayari yamepokelewa na NEC ikiwa karatasi, wino, na masanduku ya kura ambapo baadhi yake yameanza kusafirishwa katika maeneo mbalimbali nchini.
   Kuhusu Daftari la kudumu la wapiga kura, Jaji Lubuva alisema katika kipindi cha siku 10 zijazo kuanzia sasa Tume hiyo inatarajia kusambaza daftari la kudumu katika mikoa yote nchini na wananchi watatakiwa kuhakiki majina yao katika kipindi cha siku 8.

  0 0

  imagesNa Jovina Bujulu –MAELEZO Dar es Salaam………………………………….
  KATIBU MKUU wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Servacius Likwalile anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Chama cha Wanawake Wanataaluma Wahasibu Nchini (TAWCA) utakaofanyika tarehe 6 Oktoba mwaka huu.
   Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo Jumanne (Septemba 29, 2015) Jijini Dar es Salaam, Mratibu wa TAWCA Rose Majuva alisema uzinduzi unatarajia kufanyika katika hotel ya Hyatt Regency Kilimanjaro Jijini Dar es Salaam. 
   Majuva alisema chama hicho chenye jumla ya wanachama 500 kinajumuisha wanawake wahasibu wenye shahada ya juu ya uhasibu walioandikishwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA).
   Alisema Lengo la taasisi yao ni kuwahamasisha wanawake wote wenye taalamu ya uhasibu ambao hawajasajiliwa katika Bodi hiyo kujiunga na Bodi hiyo pamoja na kuwahimisha wasichana waliopo katika taasisi mbalimbali za elimu ya juu kutoogopa somo la hisabati, ambalo ndio kiungo muhimu katika taalauma ya uhasibu.
   Aidha Majuva alisema Chama hicho kipo kisheria na kinaongozwa na katiba ambapo malengo ya taasisi hiyo ni kujenga mtandao, kupanua wigo wa elimu ya uhasibu, uongozi na shughuli mbalimbali za kiuchumi nchini.

  0 0

  MGOMBEA jimbo la Monduli kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Namelok Sokoine, akihutubia mkutano wa hadhara wakati wa uzinduzi wa kampeni zake zilizofanyika katika viwanja vya Nanja Mnadani Monduli mkoani Arusha Septemba 28,2015 ambapo pamoja na mambo mengine ameahidi kuendeleza yote aliyoasisi, kusimamia na kutekeleza aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Edward Lowassa.
  Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro akihutubia mkutano wa  uzinduzi wa Kampeni za Mgombea Ubunge wa Jimbo la Monduli Mkoani Arusha kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Namelok Sokoine.
  Mgombea Ubunge wa Jimbo la Monduli kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Namelok Sokoine akihutubia wananchi katika mkutano huo wa hadhara wa uzinduzi wa kampeni zake.
   Namelok Moringe Sokoine akiwasili katika uwanja huo wa Nanja tayari kwa uzinduzi wa kampeni.
   
  Wazee wa Kimila wa Jamii ya Kimaasai wa Monduli wakiongoza dua maalim ya kumuombea Binti yao Namelok.
   Mwalimu Lorinyu Nkoosi, mmoja wa waliochuana na Namelok Sokoine katika mchakato wa uteuzi ndani ya CCM akiongea.
   Wananchi wa Monduli wakiwa katika mkutano huo.
  Wajane wa Waziri Mkuu wa Zamani wa Tanzania, Edward Moringe Sokoine ambao ni mama za Namelok Sokine wakitambulishwa mkutanoni hapo na Mwenyekiti wa kamati ya kampeni za CCM jimbo la Monduli, Paul Kiteleki.
   Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro (kulia) akimkabidhi ilani ya Chama cha Mapinduzi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Monduli Mkoani Arusha kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Namelok Sokoine wakati wa uzinduzi wa jkampebni zake uliofanyika Monduli jana.
   Dk Asha-Rose Migiro akisalimiana na wamama wa kimaasai alipowasili mkutanoni hapo.


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro (PICHA MAKTABA)
  Na Kahema Emanuel,Mbeya.
  Wito umetolewa kwa Waratibu  wa uchaguzi wa mikoa ,wasimamizi  wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi pamoja na maafisa uchaguzi wa halmashauri mikoa ya kanda za juu kusini  kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa waledi na kwa uadilifu bila kuwa na upendeleo wa chama chochote cha siasa ua mgombea .
  Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro wakati akifungua mafunzo ya wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi pamoja na maafisa uchaguzi halmashauri ambao ni wakurugenzi wa halmashauri na maafisa uchaguzi katika mikoa  ya Iringa na Mbeya.
  Amesema ili zoezi hilo la uchaguzi liende vizuri na lisighubikwe na vurugu nivema wasimamizi hao wakatumia waledi wao na udilifu bila kuwa na upendeleo wa chama chochote cha siasa au mgombea yoyote ili kuepuka hali hiyo. 
  Amesema mara baada ya kupatiwa mafunzo hayo nivema wakaendelea kutumia muda wao wa ziada kusoma na kupitia  vitabu vya maelekezo waliyopatiwa kwa kutumia kanuni na maadili ya uchaguzi ili kuimarisha uelewa zaidi kuhusu wajibu na majukumu yao katika zoezi hili la uchaguzi mkuu mwezi octobar.
  Amesema pamoja na majukumu mengine waliyonayo pia wametakiwa kutoa kipaumbele katika kutekeleza zoezi hili la kitaifa kwa ufanisi zaidi na kwa muda uliopangwa kwani uchaguzi huu utafanyika kwa siku moja tu kwa kila baada ya miaka mitano.
  Aidha amesema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetekeleza jukumu lake katika hatua ya mafunzo na maandalizi ya vifaa na rasilimali nyingine hivyo wao kama wasimamizi wanatakiwa kutekeleza wajibu wao katika ngazi zote kwa mujibu wa taratibu zilizopangwa na Tume.
  Katika semina hiyo wasimamizi hao watajifunza wajibu wa wasimamizi wa vituo vya kupigia kura  ,uwendeshaji wa zoezi la upigaji kura vituoni  sanjali na uendeshaji wa zoezi la kuhesabu kura,kujumlisha kura na kutanganza matokeo ya uchaguzi.

  Baadhi ya wakurugenzi na Maafisa uchaguzi kutoka mikoa ya Mbeya na Iringa wakiwa katika mafunzo ya waratibu wa uchaguzi mikoa ,wasimamizi wa uchaguzi ,wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi na maafisa uchaguzi wa halmashauri yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Septemba 29 ,2015.  Afisa TEHAMA kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Ndugu Sanif Khalifan akitoa maelezo kwa washiriki wa semina ya mafunzo ya waratibu wa uchaguzi wa mikoa ,Wasimamizi wa uchaguzi ,Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi na Maafisa wa uchaguzi Halmashari katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Septemba 29 ,2015.Picha JAMIIMOJABLOG


  Daniel Kalinga Afisa Uchaguzi akitoa ufafanuzi kwa washiriki wa semina hiyo ambayo itafanyika kwa siku mbili ikihusisha waratibu wa uchaguzi,Maafisa Uchaguzi ,Maafisa wasaidizi wa uchaguzi na maafisa uchaguzi Halmashauri kutoka mikoa ya Mbeya na Iringa .
  Afisa Uchaguzi Kanda ya Nyanda za juu kusini -Tume Ndugu Jane Tungu akizungumza katika semina hiyo.  0 0  0 0

   Pichani kati ni Mgombea Urais wa CCM Dkt John Magufuli akiwa sambamba na Mgombea Ubunge wa jimbo la Mtera Ndugu Livingstone Lusinde kwa pamoja wakiwapungia wananchi wa jimbo la Mtera (hawapo pichani),ndani ya mji wa Mvumi wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
   Wakazi wa jimbo la Mtera,mjini Mvumi,Wilayani Chamwino wakishangilia jambo wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akimwaga sera zake za kuomba kura za Urais jioni ya leo,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Mvumi wilaya ya Chamwino mkoani Dododma.
   Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia  Wakazi wa jimbo la Mtera huku akiwamwagia sera zake za kuomba kura za kuwania nafasi ya Urais katika awamu ya kipindi cha tano,mapema jioni ya leo,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Mvumi wilaya ya Chamwino mkoani Dododma.
   Mgombea Ubunge wa jimbo la Kibakwe,Wilayani Mpwapwa,Ndugu Dkt.Simba Chawene akimuombea kura Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli kwa wananchi wa kijiji cha  Chipogolo (hawapo pichani),wakati akitokea Iringa vijijini akielekea mkoani Dodoma kuanza kampeni zake mkoani humo,kulia kwake ni Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akiwatazama wananchi waliokuwa wakimuuunga mkono kuwa watampa kura za ndio 
   Dkt Magufuli akiwapungia Wananchi wa kijiji cha Chipogolo Wilayani Mpwapwa,mara baada ya kuwahutubia mapema leo mchana kwenye mkutano wa kampeni,shoto kwake ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma,Alhaji Adam Kimbisa.
   Waziri Mkuu Mstaafu na Kada mkongwe wa chama cha Mapinduzi (CCM),Mh.John Samuel Malecela akimuombea kura Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli kwa wakazi wa jimbo la Mtera,mjini Mvumi,Wilayani Chamwino jioni ya leo,kwenye mkutano wa kampeni.
  Wakazi wa jimbo la Mtera,mjini Mvumi,Wilayani Chamwino wakishangilia jambo wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akimwaga sera zake za kuomba kura za Urais jioni ya leo,kwenye mkutano wa kampeni  uliofanyika mjini Mvumi wilaya ya Chamwino mkoani Dododma.
   Mgombea Ubunge wa Jimbo la Isimani Ndugu William Lukuvi akiwahutubia wakazi wa Kijiji cha Idodi na Pawaga kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika mjini humo mapema leo asubuhi mkoani Iringa wakati wa kumnadi Mgombea wa nafasi ya Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli
    wakazi wa Kijiji cha Idodi na Pawaga wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia mapema leo asubuhi kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni
    Mgombea Ubunge wa Jimbo la Isimani Ndugu William Lukuvi akiwahutubia wakazi wa Kijiji cha Idodi na Pawaga kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika mjini humo mapema leo asubuhi mkoani Iringa wakati wa kumnadi Mgombea wa nafasi ya Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli 
   Wanannchi wakifuatilia mkutano wa Dkt Magufuli katika kijiji cha Pawaga na Idodi mapema leo asubuhi.
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia  wakazi wa Kijiji cha Idodi na Pawaga mapema leo asubuhi kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni akimalizia kiporo cha baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Iringa aliyoanza kampeni zake hapo juzi mkoani humo,ambapo leo amewasili mkoani Dodoma na kuanza kampeni zake wilayani Mpwapwa katika jimbo la Kibakwe na baadae jimbo la Mtera. 


  0 0

   Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  (NEC), Jaji Damian Lubuva akisalimiana na Mwakilishi wa Chama cha Kitaifa cha Watu Wasioona Zanzibar (ZANAB), Adili Mohamed wakati wa mkutano baina ya taasisi za watu wenye ulemavu nchini na NEC iliyofanyika leo Jumanne Septemba 29, 2015 Jijini Dar es Salaam.
    Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  (NEC), Jaji Damian Lubuva akisalimiana na Mwakilishi wa Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Mkoa wa Dar es Salamm Mohamed Chazi  wakati wa mkutano baina ya taasisi za watu wenye ulemavu nchini na NEC iliyofanyika leo Jumanne Septemba 29, 2015 Jijini Dar es Salaam.
    Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva akiteta jambo na Kamishna wa Tume hiyo, Jaji mstaafu Vincent Msena wakati wa mkutano baina ya NEC na wawakilishi wa vyama vya watu wenye ulemavu nchini uliofanyika leo Jumanne Septemba 29, 2015 Jijini Dar es Salaam.
    Mwakilishi wa Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Mkoa wa Pwani Hussein Kibindu akisoma taarifa ya mada ya tathimini ya uchaguzi mkuu wa oktoba 25 mwaka huu wakati wa mkutano baina ya taasisi za watu wenye ulemavu nchini na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) uliofanyika leo Jumanne Septemba 29, 2015 Jijini Dar es Salaam.
   Mwenyekiti wa Shirikisho la Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Mkoa wa Mwanza, Alfred Kapole akichangia mada wakati wa mkutano mkutano baina ya taasisi za watu wenye ulemavu nchini na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) uliofanyika leo Jumanne Septemba 29, 2015 Jijini Dar es Salaam.

    Mkalimani wa lugha ya alama, Kudra Munishi akitoa ufafanuzi wa mada na hoja kwa watu wenye ulemavu wa kusikia wakati wa mkutano baina ya taasisi za watu wenye ulemavu nchini na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) uliofanyika leo Jumanne Septemba 29, 2015 Jijini Dar es Salaam.

  (PICHA NA ISMAIL NGAYONGA).


  Na Ismail Ngayonga MAELEZO

  TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)  imevitoa wasiwasi  vyama vya siasa  kuwa hakutakuwepo na wizi na udanganyifu wa kura katika matokeo ya uchagauzi wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajia kufanyika nchini tarehe 25 Oktoba, mwaka huu.

  AIdha NEC imesema ipo tayari kushirikiana na wataalamu wa vyama hivyo katika kubaini vyanzo vya wizi wa kura iwapo tatizo hilo litajitokeza na hivyo kuhakikisha haki inatendeka kwa vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi huo.


  Hayo yamebainishwa leo Jumanne (Septemba 29, 2015) Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Damian Lubuva wakati wa mkutano wake na wawakilishi wa vyama vya watu wenye ulemavu aliokutana nao kwa ajili ya kupata ushauri na maoni ya taasisi hizo kuelekea uchaguzi mkuu mwezi oktoba mwaka huu.


  Jaji Lubuva alisema hadi kufikia sasa, vyama vyote vyote vinavyoshiriki uchaguzi huo vimefanyika kampeni za kistaarabu ingawa katika siku za hivi karibuni baadhi ya vyama vimekuwa vikitoa kauli na matamshi yaliyovuka mipaka, ambapo NEC imevionya vyama kuacha mara moja tabia hiyo.


  “Vipo baadhi ya vyama vya siasa na wagombea wao  wamekuwa wakitumia muda mwingi kutoa lugha zisizofaa baada ya kunadi sera ya vyama vyao, vyama hivyo tumekutana nao na kuwataka kuacha mara moja kampeni za aina hiyo” alisema Jaji Lubuva.


  Jaji Lubuva alisema tarehe 27 Julai mwaka huu, vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi mkuu vilisaini maktaba wa maadili ya uchaguzi huo, hivyo ni wajibu wa vyama hivyo kuzingatia viapo walivyotoa katika maktaba huo.


  Akifafanua zaidi Jaji Lubuva alisema iwapo chama chochote hakina hoja ya kuzungumza na  wananchi ni vyema kikawa kimya hadi siku ya uchaguzi tarehe 25 Oktoba mwaka huu.

  Aidha Jaji Lubuva alivitaka vyama vya siasa kuacha tabia ya kuingilia masuala ya utawala ya tume hiyo, kwani kwa kufanya hivyo vyama hivyo vitakuwa vikifanya kazi za tume hiyo na hivyo kuingilia masuala ya ndani ya kiutendaji ya taasisi hiyo.


  Akizungumzia maandalizi ya uchaguzi huo, Jaji Lubuva alisema mahitaji yote ya msingi ya uchaguzi huo tayari yamepokelewa na NEC ikiwa karatasi, wino, na masanduku ya kura ambapo baadhi yake yameanza kusafirishwa katika maeneo mbalimbali nchini.


  Kuhusu Daftari la kudumu la wapiga kura, Jaji Lubuva alisema katika kipindi cha siku 10 zijazo kuanzia sasa Tume hiyo inatarajia kusambaza daftari la kudumu katika mikoa yote nchini na wananchi watatakiwa kuhakiki majina yao katika kipindi cha siku 8.

  0 0


  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA


  Simu: 255-22-2114615, 211906-12

  Barua pepe: nje@nje.go.tz

  Barua pepe: gcu@nje.go.tz

  Nukushi: 255-22-2116600

                

   


                  20 KIVUKONI FRONT,

                             P.O. BOX 9000,

                    11466 DAR ES SALAAM, 

                                      Tanzania.


   


  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


  Taarifa za kupatikana kwa majina 18 ya Mahujaji kutoka Tanzania waliopotea huko Saudi Arabia


  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imepokea majina 18 ya Mahujaji kutoka Tanzania ambao hadi sasa hawaonekani kufuatia tukio la mkanyagano wa Mahujaji lililotokea eneo la Mina, Makkah tarehe 24 Septemba, 2015 na kusababisha vifo vya watu 769 na wengine 934 kujeruhiwa.


  Itakumbukwa kuwa tarehe 28 Septemba, 2015 Wizara ilitoa taarifa kuwa Mahujaji wa Tanzania wapatao 50 bado hawajaonekana huku wengine watano wakiwa wamefariki dunia.


  Majina ya baadhi ya Mahujaji wa Tanzania ambao mpaka sasa bado hawajaonekana ni kama ifuatavyo:-


  1. Abdul Iddi Hussein

  2. Awadh Saleh Magram

  3. Burhani Nzori Matata

  4. Yussuf Ismail Yusuf

  5. Saleh Mussa Said

  6. Adam Abdul Adam

  7. Archelaus Antory Rutayulungwa

  8. Farida Khatun Abdulghani

  9. Rashida Adam Abdul

  10. Hamida Ilyas Ibrahim

  11. Rehema Ausi Rubaga

  12. Faiza Ahmed Omar

  13. Khadija Abdulkhalik Said

  14. Shabinabanu Ismail Dinmohamed

  15. Salama Rajabu Mwamba

  16. Johari Mkesafiri Mwijage

  17. Alwiya Sharrif Salehe Abdallah

  18. Hafsa Sharrif Saleh Abdallah


  Mbali na taarifa za kupatikana kwa majina hayo, Wizara imepokea taarifa ya kutambuliwa kwa mwili wa hujaji mmoja wa Tanzania anayeitwa Hadija Shekali Mohammed wa kikundi cha Ahlu Daawa.


  Aidha, Serikali ya Saudi Arabia imetoa picha za maiti za Mahujaji waliokufa Makkah ambao wamehifadhiwa katika vyumba vya kuhifadhia maiti kwa ajili ya utambuzi. Hivyo, Ubalozi wa Tanzania nchini humo kwa kushirikiana na Tanzania Hajj Mission pamoja na vikundi vya Mahujaji unaendelea na zoezi la kuzihakiki picha hizo ili kubaini kama zinalingana na sura za Mahujaji wetu waliopotea.


  Vilevile, Mamlaka ya Serikali ya Saudi Arabia imesema kuwa imechukua alama za vidole za Mahujaji waliokufa ili wazilinganishe na zile walizozichukua Uwanja wa Ndege wakati Mahujaji hao wakiingia nchini humo. Wizara inaamini kuwa taarifa za alama za vidole zitakapotolewa zitasaidia sana kuwatambua Mahujaji wetu.


  Pamoja na jitihada zote hizo, Ubalozi pia unaendelea na juhudi za kuwatambua Mahujaji wengine wa Tanzania ambao hawajaonekana kwa kutembelea katika hospitali zilizohifadhi maiti na kulaza majeruhi wa ajali hiyo.  Imetolewa na:

  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,

  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,

  Dar es Salaam


  29 Septemba, 2015

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro (PICHA MAKTABA)
  Na Kahema Emanuel,Mbeya

  WITO umetolewa kwa Waratibu  wa uchaguzi wa mikoa ,wasimamizi  wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi pamoja na maafisa uchaguzi wa halmashauri mikoa ya kanda za juu kusini  kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa waledi na kwa uadilifu bila kuwa na upendeleo wa chama chochote cha siasa ua mgombea.


  Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro wakati akifungua mafunzo ya wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi pamoja na maafisa uchaguzi halmashauri ambao ni wakurugenzi wa halmashauri na maafisa uchaguzi katika mikoa  ya Iringa na Mbeya.


  Amesema ili zoezi hilo la uchaguzi liende vizuri na lisighubikwe na vurugu nivema wasimamizi hao wakatumia waledi wao na udilifu bila kuwa na upendeleo wa chama chochote cha siasa au mgombea yoyote ili kuepuka hali hiyo. 


  Amesema mara baada ya kupatiwa mafunzo hayo nivema wakaendelea kutumia muda wao wa ziada kusoma na kupitia  vitabu vya maelekezo waliyopatiwa kwa kutumia kanuni na maadili ya uchaguzi ili kuimarisha uelewa zaidi kuhusu wajibu na majukumu yao katika zoezi hili la uchaguzi mkuu mwezi Oktoba.


  Amesema pamoja na majukumu mengine waliyonayo pia wametakiwa kutoa kipaumbele katika kutekeleza zoezi hili la kitaifa kwa ufanisi zaidi na kwa muda uliopangwa kwani uchaguzi huu utafanyika kwa siku moja tu kwa kila baada ya miaka mitano.


  Aidha amesema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetekeleza jukumu lake katika hatua ya mafunzo na maandalizi ya vifaa na rasilimali nyingine hivyo wao kama wasimamizi wanatakiwa kutekeleza wajibu wao katika ngazi zote kwa mujibu wa taratibu zilizopangwa na Tume.


  Katika semina hiyo wasimamizi hao watajifunza wajibu wa wasimamizi wa vituo vya kupigia kura  ,uwendeshaji wa zoezi la upigaji kura vituoni  sanjali na uendeshaji wa zoezi la kuhesabu kura,kujumlisha kura na kutanganza matokeo ya uchaguzi.
  Baadhi ya wakurugenzi na Maafisa uchaguzi kutoka mikoa ya Mbeya na Iringa wakiwa katika mafunzo ya waratibu wa uchaguzi mikoa ,wasimamizi wa uchaguzi ,wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi na maafisa uchaguzi wa halmashauri yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Septemba 29 ,2015.

  Afisa TEHAMA kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Ndugu Sanif Khalifan akitoa maelezo kwa washiriki wa semina ya mafunzo ya waratibu wa uchaguzi wa mikoa ,Wasimamizi wa uchaguzi ,Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi na Maafisa wa uchaguzi Halmashari katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Septemba 29 ,2015.Picha JAMIIMOJABLOG


  Daniel Kalinga Afisa Uchaguzi akitoa ufafanuzi kwa washiriki wa semina hiyo ambayo itafanyika kwa siku mbili ikihusisha waratibu wa uchaguzi,Maafisa Uchaguzi ,Maafisa wasaidizi wa uchaguzi na maafisa uchaguzi Halmashauri kutoka mikoa ya Mbeya na Iringa .  Afisa Uchaguzi Kanda ya Nyanda za juu kusini -Tume Ndugu Jane Tungu akizungumza katika semina hiyo.

  0 0
 • 09/29/15--20:20: NYOSO AFUNGIWA MIAKA MIWILI
 • Kamati ya masaa 72 ya uendeshaji wa Ligi Kuu iliyokutana leo kupitia ripoti mbalimbali za michezo iliyochezwa ya Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza nchini imemfungia mchezji Juma Nyoso wa timu ya Mbeya City kucheza mpira wa miguu kwa kipindi cha miaka miwili na faini ya shilingi milioni mbili (2,000,000) kufutia kitendo cha udhalilishaji alichomfanyia mchezaji wa Azam FC John Bocco.
  Nyoso alifanya kitendo hicho katika mchezo no namba 32 wa VPL kati ya Azam FC na Mbeya City uliofanyika kwenye uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam, kutokana na kuwa tabia ya kufanya vitendo hivyo vya utovu wa nidhamu mara kwa mara kwenye michezo ya Ligi Kuu.
  Klabu ya Young Africans imepigwa faini ya shiligi laki tano (500,000) kufutia wachezaji wake watano kuonyeshwa kadi za njano katika mchezo dhidi ya Simba SC. Kwa mujibu wa kanunu namba 42 (11) timu ambayo wachezaji wake watapata kadi zaidi ya tabo katika mchezo mmoja itapigwa faini ya shilingi laki tano.
  Wachezaji waliopata kadi za njano wa Young Africans katika mchezo huo ni ni Salum Telela, Mbuyu Twite, Malimi Busungu, Ali Mustafa na Mbuyu Twite.
  Aidha klabu ya Yanga imepigwa faini nyingine ya shilingi laki tano (500,000) kufutia wachezaji wake kwenda kushangilia upande wa Simba SC mara baada ya mchezo kumalizika.
  Mchezo utatazamwa tena ili kuangalia malalamiko ya Simba SC dhidi ya mwamuzi.
  Simba pia inapigwa faini baada ya wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kuwashambulia waamuzi baada ya mchezo ambapo waliwarushia chupa za maji ambazo nyingine ziliwakosa waamuzi na kumpata kocha wa Yanga Hans Van Pluijm.
  Mchezo namba 26 wa VPL kati ya Coastal Union na Mwadui uliofanyika kwenye uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Chumba cha Coastal Union kilikuwa na harufu kali sana. Baadhi ya mashabiki wa Coastal Union waliokuwa nyuma ya goli la upande wa kaskazini walitoa  lugha ya matusi kwa waamuzi na kutishia kuwapiga na pia walimrushia mawe mwamuzi msaidizi wa pili Shafii Mohamed na jiwe moja lilimpiga mgongoni na kumjeruhi kidogo mwamuzi na aliomba msaada wa jeshi la polisi kutuliza ghasia, mchezo ulisimama kwa dakika 3.
  Kwa mujibu wa kanuni namba 42 (1) ya udhibiti wa wachezaji Coastal Union itatozwa faini ya Tsh 500,000/=
  Mchezo namba 22 wa VPL kati ya Mtibwa Sugar na Ndanda uliofanyika kwenye uwanja wa Manungu, Turiani. Ndanda hawakuleta watu wa kutosha kwenye pre match meeting hivyo wanapigwa faini ya shilingi laki mbili (200,000/=)
  Mchezo namba 23 wa VPL kati ya Simba SC na Kagera Sugar uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa, Dar es salaam. Simba walikuwa na wajumbe watatu na Kagera Sugar walikuwa na mtu mmoja tu tena hakuja na vifaa. Timu zote zimepigwa faini ya shilingi laki mbili (200,000).
  Mchezo namba 17 wa VPL kati ya Stand united na African Sports kocha wa Stand United alitolewa nje ya eneo la ufundi kwa kutoheshimu taratibu za eneo hilo na pia alikataa kuongea na vyombo vya habari kwa hiyo kwa mujibu wa kanuni namba 40 (11) anafungiwa kukaa kwenye benchi la ufundi kwa mechi mbili na faini ya sh 500,000/= kwa kila kosa jumla 1,000,000/=.
  Friends Rangers na KMC Mechi Na 8 Kundi A iliyofanyika uwanja wa Karume 27.9.2015. Timu ya KMC ya kinondoni ilifanya mabadiliko kwa kuingiza wachezaji 4 ambao ni kinyume cha kanuni. Kwa mujibu wa taarifa ya mwamuzi wachezaji waliofanyiwa mabadiliko ni
  i. Frank Mashoto badala ya Kudra Omari
  ii. Kamongo Morris badala ya Mrisho Simon
  iii. Mfanyeje Musa badala ya Kabange Mgunda na
  iv. Sultani Kasiras badala ya Adam Said
  Kwa mujibu wa kanuni namba 14 (25) KMC imepoteza mechi na kupigwa faini ya Tsh 200,000/=. Mwamuzi wa akiba anafutwa kuchezesha ligi msimu huu na mwamuzi wa kati anapewa onyo.


  0 0

  IMG_3349
  Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez (kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UN Women nchini Tanzania, Anna Collins-Falk (katikati) wakipata picha ya kumbukumbu sambamba na mmoja wa wadau wa maendeleo. (Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
  Na Mwandishi wetu
  UMOJA wa Mataifa kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania wamezindua rasmi malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
  Malengo hayo ambayo pia yanajulikana kama malengo ya dunia yamezinduliwa jana Septemba 29 katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
  Uzinduzi huo ulifanywa na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez, Kamishina wa mipango (POPC) Bw. Paul Kessy, na Kamishina wa Mipango wa Zanzibar, Bw. Ahmed Makame kwa niaba ya serikali, Bi. Fionnuala Gilsenan, Balozi wa Ireland na Bi. Liz Lloyd, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania kwa niaba ya wadau wa mradi wa Project Everyone Partners.
  SDGs ni wito wa dunia wa kuchukuliwa kwa hatua za kuufuta umaskini, kuihami dunia dhidi ya uharibifu wa mazingira na kuhakikisha kwamba kila mwanadamu anaishi maisha stahiki katika amani na ustawi.
  Katika malengo hayo 17 yapo makusudio 169 yanayotoa ramani ya utengenezaji wa sera za maendeleo na namna ya kutekeleza kwa miaka 15 ijayo.
  Malengo hayo yakijengwa juu ya mafanikio ya malengo ya milenia (MDGs), yameingiza vitu vipya kama mapambano dhidi ya tofauti za kiuchumi, ubunifu, mabadiliko ya tabia nchi, lishe, amani na haki. SDGs ni mpango wa dunia unaojikita kwa ustawi wa wanancni na dunia.
  IMG_3303
  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Awa Dabo (kushoto) na Kiongozi wa mabalozi wa nchi za nje hapa nchini Mheshimiwa Juma Mpango, ambaye ni balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakiwa wameshikilia lengo namba 16 na 17 kati ya malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya Dunia ambayo yamezinduliwa rasmi nchini Tanzania jana 29, Septemba 2015.
  Akizungumza umuhimu wa malengo hayo, Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez amesema: “Kwa mara ya kwanza katika historia ya dunia , serikali zimekutana na kukubaliana kupeana malengo kwa ajili ya kila mtu. Malengo haya yatasaidia mataifa yote kushirikiana katika kuwezesha ustawi, kupunguza matumizi na kuilinda dunia dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.Katika hilo watashughulikia elementi zinazohusu maendeleo endelevu: ukuaji wa uchumi, ustawi wa jamii na kulinda mazingira.”
  Akizungumzia malengo hayo Bw. Paul Kessy amesema kwamba serikali ya Tanzania ipo tayari kwa malengo hayo.
  Alisema kwamba Rais Jakaya Kikwete alikuwa New York, Marekani kwa ajili ya kutia saini malengo hayo na hilo linaonesha ni kiasi gani serikali ya Tanzania iko tayari kushirikiana na wadau wengine kuufuta umaskini.
  Pia alisema:“Wakati huu, masuala ya uimarishaji wa muundo wa utekelezaji na kuamsha upya ushirikiano wa kidunia katika maendeleo ni msingi mzuri”
  Naye Kamishina wa mipango wa Zanzibar, Bw Ahmed Makame : “Nikiangalia malengo haya 17 ya SDGs, ninafuraha kuona kwamba Zanzibar imekuwa sehemu ya mchakato huu...”.
  IMG_3392
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Bi. Liz Lloyd akipozi kwa picha na lengo na tisa kabla ya uzinduzi rasmi wa Malengo ya Dunia kwa Maendeleo Endelevu.
  Aidha alisema kwamba Tanzania imeanza vyema katika utekelezaji wa malengo hayo.

  Alisema kwa kuangalia uzoefu uliopatikana katika malengo ya milenia, inaonekana namna bora ya kuuoanisha malengo ya kitaifa na ya dunia.
  Ninafurahi kusema kwamba Zanzibar tuko katika mchakato wa kutengeneza mkakati wa maendeleo wa kitaifa na tumepanga kufikia malengo ya SDGs.
  Akisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika kufanikisha maendeleo, Bi.Fionnuala Gilsenan, amesema taifa lake Ireland lipo tayari kusaidia kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu.
  “Malengo ya dunia yaliyojengwa katika Malengo ya Milenia yamelenga kukabiliana na matatizo ya zamani kwa mbinu mpya. Zimelenga kukabiliana na tatizo la umaskini na ukosefu wa usawa katika masuala ya uchumi. SDGs haiwezi kufanikiwa bila kuyaangalia masuala ya mabadiliko ya tabia nchi, usawa wa jinsia, haki za biandamu na kukabiliana na mfumo inayobagua.”
  Akizungumza kwa niaba ya wadau wa Project Everyone, Bi. Liz Lloyd alielezea umuhimu wa sekta binafsi kushirikiana na Umoja wa Mataifa na serikali ya Tanzania katika kusambaza ujumbe wa malengo ya dunia.
  IMG_3397
  Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), nchini Tanzania, Dk.Rufaro Chatora akipozi la lengo namba 3.
  “Kama benki huwa tunazungumza na umuhimu wa kuendelea kuwapo. Huu si tu msemo bali ahadi tunayoishi nayo kila siku. Malengo ya Dunia yanatoa nafasi adhimu ya ushirikiano na taasisi kubwa duniani, kutekeleza malengo 17 kwa nia ya kufufua ushirikiano wa dunia kwa maendeleo endelevu.
  Standard Chartered inajisikia furaha ya kuwa nchini Tanzania kwa miaka mingi na inatumaini kwamba kwa ushirikiano huu kila mtu anayeishi nchini hapa atafaidika na maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii.”
  Malengo ya Maendeleo Endelevu yalizinduliwa Septemba 25 wakati viongozi wa dunia walipokutana pamoja mjini New York. Malengo haya yataanza kutumika Januari 1,2016.
  IMG_3226
  Mkuu wa ushauri wa ufundi wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Peter Malika akipozi na lengo na 17.
  IMG_3280
  Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni waalikwa kabla ya uzinduzi rasmi wa malengo hayo nchini Tanzania.
  IMG_3390
  Mtaalam wa mawasiliano kutoka UNFPA, Sawiche Wamunza (kushoto) sambamba na Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama katika picha ya ukumbusho.
  IMG_3789
  Meza kuu katika halfa ya uzinduzi wa malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs) nchini Tanzania, kutoka kushoto ni Mtaalamu wa masuala ya uchumi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Dar es salaam, Rogers Dhliwayo, Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Mh. Fionnuala Gilsenan, Kamishina wa mipango (POPC) Bw. Paul Kessy, Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez, Kamishina wa Mipango wa Zanzibar, Bw. Ahmed Makame pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Bi. Liz Lloyd.
  IMG_3781
  Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez, akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
  IMG_3554
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Bi. Liz Lloyd akielezea ushiriki wa benki yake katika utekelezaji wa malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
  IMG_3580
  Kamishina wa mipango (POPC) Bw. Paul Kessy akizungumza kwa niaba ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye hafla ya uzinduzi wa malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
  IMG_3640
  Kamishina wa Mipango wa Zanzibar, Bw. Ahmed Makame akiwakilisha serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
  IMG_3772
  Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Mh. Fionnuala Gilsenan akizungumza kwenye hafla hiyo ambapo alisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika kufanikisha maendeleo.
  IMG_3754
  Baadhi ya wadau wa maendeleo kutoka mashirika na balozi mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs) iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
  IMG_3796
  Baadhi ya wageni waalikwa na wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania wakifuatilia maoni na maswali yaliyokuwa yakiwasilishwa kwenye hafla hiyo.
  IMG_3829
  Mmoja wa wawakilishi wa vijana akiuliza swali meza kuu.
  IMG_3868
  Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Joyce Mends-Cole akijibu moja ya swali lililoulizwa na kijana (hayupo pichani).
  IMG_3857
  Sehemu ya wadau wa Maendeleo, taasisi mbalimbali, asasi za kiraia, waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo.
  IMG_3851
  Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA), Dkt. Natalia Kanem akifafanua jambo katika kipindi cha maswali na majibu.
  IMG_3900
  Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez (kulia), Kamishina wa Mipango wa Zanzibar, Bw. Ahmed Makame ( wa pili kulia), Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Mh. Fionnuala Gilsenan (kushoto) Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahaya (wa pili kushoto) kwa pamoja wakifunua pazia maaluma kuashiria uzinduzi rasmi wa malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
  IMG_3912
  Sasa yamezinduliwa rasmi.
  IMG_3921
  Shamra shamra za uzinduzi zikiendelea.
  IMG_3950
  Fataki zikisherehesha uzinduzi wa malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
  IMG_3975
  Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Uhuru mchangayiko na wadau mbalimbali wa maendeleo, waandishi wa habari wakiwa kwenye picha ya pamoja na vibao vya malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
  IMG_3997
  Meza kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Uhuru mchangayiko walioshiriki kutengeneza tangazo maalum la kuelimisha jamii kuhusiana na malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
  IMG_4021
  Meza kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
  IMG_4029
  Meza kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya waandishi wa habari akiwemo Mwanahabari mkongwe Mama Eda Sanga walioshiriki kwenye uzinduzi huo.
  IMG_4097
  Bendera ya Umoja wa Mataifa, SDG's na bendera za nchi mbalimbali zikipepea kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
  IMG_4078

  0 0

  KUSOMA  ZAIDI  links  goes  to  sheriayakub.blogspot.com
  Na  Bashir  Yakub.

  KISHERIA  haizuiwi  kuweka  rehani  nyumba  ya  makazi  kwa  ajili  ya  kupata  mkopo  kutoka  taasisi  yoyote  ya  fedha. Jambo la msingi  sana  ni  kuwa  watoa  mkopo   wajiridhishe   na  umiliki  wa  nyumba  hiyo  hasa  kwa  kuangalia ikiwa  ni  mali  ya  familia  au  hapana ili wachukue  hadhari  za  kisheria.


  Nyumba  ya  makazi  ni  ipi.  Nyumba  ya  makazi  ni  ile  nyumba  ambayo  inatumiwa  na  binadamu  kuishi  lakini  zaidi  wanaoishi  mle  ndani  iwe  ni  familia  ya  mchukua  mkopo.  Yawezekana  nyumba  ikawa  ni  ya makazi kwa  watu  wengine  lakini  ni  ya  biashara  kwa  mchukua  mkopo. Kwa  mfano  nyumba  za  kupanga  ambapo  mwenye  nayo  anaishi  kwingine   na nyumba  iko  kwingine ikiwa  na  watu  wengine.

   Nyumba  ya  namna  hii  haitaingia  kwenye  nyumba  ya  makazi  kwa  tafsiri  hii.  Hata  hivyo  haitarajiwi  mchukua  mkopo  kuhamia  kwenye  nyumba  ambayo  sio  ya  makazi  kwa  makusudi  na kuifanya  ya  makazi  akilenga   kuhadaa  ili  kupata  upendeleo  wa  mahakama.  Akifanya  hili  atakuwa  amedanganya  na  ni  kosa  kama  tutakavyoona.


  1.MAKOSA  YA  KISHERIA  KWA  MKOPAJI.

  ( a ) Sheria  ya  masuala  ya  rehani  ya  2008  inamtaka  mkopaji  kutofanya  udanganyifu  wa  aina  yoyote  kwa  taasisi inayotarajia  kumpa mkopo. Moja  ya  udanganyifu  ni  kama  ilivyoelezwa  hapo  juu  lakini  pia  upo  udanganyifu  mwingine  mwingi  ambao hufanywa  na  wakopaji. Kwa  mfano  kuweka  rehani  nyumba  moja  kwa  taasisi  tofauti,  kudanganya  nyumba  sio  ya  familia  wakati  ni  ya  familia  na  udanganyifu  mwingine  mwingi  ambao  hulenga  kumnufaisha  mkopaji.  


  2. ADHABU  YA  KUTENDA KOSA  LA  UDANGANYIFU  KATIKA  KUCHUKUA MKOPO.

  Kisheria  tendo  likishakuwa  kosa  ni  lazima  iwepo  adhabu  yake.  Vivyo  hivyo  mkopaji  kumdanganya  mkopeshaji  nalo  ni  tendo  ambalo  huadhibiwa. Sheria  inasema  kuwa  hatia  ya udanganyifu  wa mkopaji   inapotangazwa  basi  adhabu  yake  ni  kulipa  faini  ambayo  ina  thamani  ya  nusu ya  mkopo  aliokuwa  amechukua. Hii  ina  maana kuwa,  kama  alichukua  mkopo  wa  milioni  200  basi  faini  yake  ni  milioni 100  halikadhalika  kama  alichukua  milioni  kumi  basi  faini  yake  ni  milioni tano.

  Ikiwa  hana  hizo  hela  basi  itatakiwa  kwenda  jela  kutumikia  kifungo  kisichopungua  miezi  kumi  na  mbili. Kifungo  kisichopungua  miezi  kumi  na  mbili  maana  yake kinaweza  kuzidi miezi  kumi  na  mbili kutegemea  na  ukubwa  wa tatizo  lenyewe.  Hivyo  wakopaji  wajihadhari  na  kutoa  taarifa  za  uongo  hasa  kudanganya  kuwa  mali  si  ya  familia  au  kutumia  mali  moja  kuchukulia  mkopo  sehemu  zaidi  ya  moja n.k.


  3.  UPENDELEO  KWENYE  NYUMBA  YA  MAKAZI

  ( a ) Sheria  inasema  kuwa   iwapo  itabainika  kuwa  nyumba   iliyowekwa  rehani  ni ya  makazi  na  mkopaji  analeta  zuio la  kutouzwa   nyumba  hiyo  basi  mahakama  ikijiridhisha  na  hilo  inaweza  kukubali  ombi  hilo.


  Mahakama  itakubali  ombi  hilo  la  kuzuia  nyumba  kuuzwa  kwa  kuzingatia  kiwango  cha  hela  kilichosalia  yaani kile kiasi  ambacho   mkopaji  ameshindwa  kulipa. Mara  kadhaa  hutokea  kuwa  mkopaji  amelipa  kiasi  kikubwa  na  kusalia na  deni  la kiasi  kidogo  ambacho  kwa   akili  ya  kawaida  tu  na kutokana  na  mazingira  yaliyopo  akipewa  muda  mwingine  anao  uwezo  wa  kulipa  na  kumalizia  kabisa  deni. Ni  katika  mazingira  haya  zuio  la  kutouzwa  nyumba   ya  makazi  litakubaliwa.


  ( b ) Hili  litakwenda  sambamba  na  kuangalia  iwapo  wajibu  wa  mkopaji  uliowekwa  katika  mkataba  wa  mkopo unaweza  kuzungumzika. Ikiwa  mkopaji  alikuwa  mgonjwa  sana  na  ushahidi  upo  na  hivyo  alishindwa  kuendelea  na  biashara  na  hivyo  kutokurejesha, na sasa  ana  afya  njema  na  anaweza  kufanya  biashara  na  kurejesha, basi  wajibu  wake ikiwa  unaweza kurekebishika  kwa  namna  hiyo  au  namna  nyingine mahakama inaweza  kutoa  zuio  ili  kutoa  nafasi  nyingine  kwa  mkopaji.


  ( c ) Pia  ikiwa mahakama  itajiridhisha   kuwa  nyumba  husika  ina  thamani kubwa  kiasi  kwamba hata   mkopaji  akiongezewa  muda  mwingine  bado  akishindwa  kulipa  huko  mbeleni   nyumba  husika  ikiuzwa  mtoa  mkopo  hatakuwa  na  hasara  ataweza  kurejesha  hela  yake  yote pamoja  na  riba,  basi  zuio  la  kutouza  linaweza  kutolewa  kwa  kulizingatia  hilo.

  Izingatiwe  kuwa  zuio  katika mazingira  haya  niliyoeleza   linawezekana  ikiwa nyumba  ilyowekwa rehani  ni  ya  makazi.

  MWANDISHI   WA   MAKALA  HAYA   NI   MWANASHERIA  NA  MSHAURI   WA  SHERIA  KUPITIA  GAZETI  LA  SERIKALI   LA   HABARI   LEO  KILA  JUMANNE  , GAZETI  JAMHURI   KILA  JUMANNE  NA  GAZETI  NIPASHE  KILA  JUMATANO.    0784482959,        0714047241              bashiryakub@ymail.com

  0 0

  IMG_3000
  Kamishina wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Eusella Bhalalusesa akizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome kuzindua maonesho ya Tehama yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

  Na mwandishi wetu
  JUMLA ya wanafunzi 60,000 katika shule 150 nchini wamepitiwa na mafunzo ya programu ya Bridge IT yenye lengo la kuongeza ubora wa elimu kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya kidijiti (digital technology) katika ufundishaji na ujifunzaji wa Hisabati,Sayansi na Stadi za Maisha.
  Hayo yamsemwa na Kamishina wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Eusella Bhalalusesa akimkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome kuzindua maonesho ya Tehama.

  Alisema kutokana na mafanikio yaliyotokea sasa wanatanua wigo baada ya kuwezeshwa kifedha na Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya elimu (Global Partnership For Education) kwa ajili ya kuendeleza teknolojia hiyo katika kujifunza na kufundisha katika shule za msingi na hasa darasa la awali la kwanza hadi la nne.

  Aidha maonesho hayo yanayofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere yana lengo la kuonesha ubunifu ambao upo tayari kutumika kufanikisha mafunzo hayo.

  Pia maonesho hayo yanatarajia kujadili na kuangalia mbinu za kielektroniki zitakazoweza kuendana na mazingira ya Tanzania katika ufundishaji na kujifunza kwa gharama nafuu.

  Pia wanatarajia kuangalia utayari wa walimu na namna ya kuwabadilisha mtazamo ili waweze kufundisha na kufundishika.
  “Lengo la serikali kupitia Wizara ya Elimu ni kupanua wigo wa elimu hasa elimu ya awali kwa kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano ambayo itabadilisha ufundishaji kutoka kutumia vitabu vilivyopo katika mfumo wa ‘hard copy’ na kuwa katika mfumo wa sauti na picha au ‘soft copy’,” alisema Profesa Bhalalusesa.
  IMG_3089
  Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome akifuatilia kwa makini risala Kamishina wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Eusella Bhalalusesa (hayupo pichani).

  Alisema hadi kufikia wakati huu serikali imeshapiga hatua kubwa katika matumizi ya Tehama ambayo katika majaribio yake yameonesha kufanikiwa na wadau mbalimbali wa elimu wameyapongeza na kuyaunga mkono.

  Profesa Bhalalusesa alisema kwa sasa wagunduzi mbalimbali wa mifumo ya Kompyuta inayoweza kutumika kufundishia ndio watakoonesha kazi zao na kutoa ufafanuzi wa kina kwa majaji wataochagua kazi chache na kuzifanyia majaribio kabla ya kuanza kutumika kufundishia.

  Kwa Upande wake Mratibu wa Mpango wa Kukuza stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu kutoka Wizara ya Elimu, Agripina Habichi alisema mpango huo wa matumizi ya Tehama utasaidia wanafunzi kufahamu kusoma na kuandika kabla ya kuendelea na masomo ya darasa la tatu.

  “Maonesho haya yanafanyika katika wakati muafaka ukizingatia tunataka kupiga hatua kubwa katika kuboresha elimu yetu. Washiriki wa maonesho haya wamekuja kutuonesha utawaalamu wao unaoweza kutumika kufundishia.

  Lengo letu ni kuwafikia wanafunzi wengi zaidi ambapo tumeazimia kuzifikia shule zaidi ya 2000 katika mwaka wa fedha wa 2016/2017 na hivyo tutakuwa katika kiwango bora zaidi cha utoaji wa elimu inayojitosheleza,” alisema Habichi.
  IMG_3142
  Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome akizungumza kabla ya kuzindua rasmi maonesho ya Tehama yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Katika maonesho hayo serikali imesema inatarajia kuanza kutumia rasmi Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) katika kufundishia wanafunzi kuanzia ngazi ya chini kabisa ya elimu ambayo ni chekechea.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome alisema matumizi ya Tehama katika ufundishaji wa wanafunzi wa chekechea yataimarisha kiwango cha elimu.

  “Dunia imebadilika sana hasa katika sekta ya elimu na mawasiliano, hatuna budi kuendana nayo kwa kasi ileile ya ukuaji wake kwa kuimarisha mifumo yetu ya ufundishaji,” alisema Profesa Mchome.
  Alisema wizara yake imeanzisha mpango maalum utakaosaidia wanafunzi kujifunza kwa njia ya kisasa ya kutumia mbinu za kielektroniki katika kujifunza na hivyo kuimarisha uelewa na kuongeza hamasa ya ufundishaji kwa wanafunzi.
  Profesa Mchome alisema maonesho hayo yana lengo la kupata wadau mbalimbali waliobuni programu zinazoweza kutumika katika kufundishia kwa kutumia mifumo ya kielektroniki na hivyo watachaguliwa wachache wenye sifa na watakowezesha mafunzo hayo katika shule za Msingi na baadae katika ngazi ya sekondari.
  IMG_3160
  Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome akijianda kuzindua rasmi maonesho ya Tehama yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
  IMG_3161
  Sasa yamezinduliwa rasmi.
  IMG_3214
  Ofisa Miradi ya Elimu kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Faith Shayo akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na shirika lake katika kuendeleza sekta ya elimu nchini kwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome (kushoto) mara baada ya kuzindua maonesho hayo ambapo pia UNESCO inashiriki. Katikati ni Kamishina wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Eusella Bhalalusesa.
  IMG_3217
  Ofisa anayeshughulikia masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmari (katikati) akimsikiliza mmoja wa wadau wa elimu aliyetembelea banda la UNESCO kwenye maonesho ya TEHAMA yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Miradi ya Elimu kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Faith Shayo.
  IMG_2982
  Ofisa anayeshughulikia masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmari (kulia) akiwa na wadau wengine wa elimu wakipitia makbrasha mbalimbali katika mkutano huo.
  IMG_3006
  Pichani juu na chini ni baadhi wadau wa elimu waliohudhuria uzinduzi wa maonyesho hayo.
  IMG_3004
  IMG_3028
  Baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali za msingi jijini Dar walioshiriki hafla hiyo.
  IMG_3105
  Mkurugenzi Mkuu wa Shule Direct, Faraja Nyalandu akipozi na wadau kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam yanakoendelea maonesho ya TEHAMA.

  0 0

  Msigwa na wengine 62 mbaroni Mkoani Iringa .Fahamu kilichojiri katika nyanja za siasa kama yasemavyo magazeti ya leo;  https://youtu.be/yt0b6QW10-c

   Simba yamshitaki Donald Ngoma. Viti  vyaizuia Yanga kufanya mazoezi katika uwanja wa Jamuhuri,   https://youtu.be/mDzS67eL7wE

   NEC yapiga marufuku kusafirisha masanduku ya kura.Rais mpya kujulikana ndani ya masaa 72 tu; https://youtu.be/updRyyX0WSg

  Magufuli asisitiza kufa na mafisadi.Siri ya Lowasa kuhairisha mkutano Tanga yawekwa wazi, Lowasa asimamishwa na wakazi wa Muheza akiwa safarini kuelekea Dar; https://youtu.be/D3v9n1X91iM  0 0

   Mgombea wa Ubunge wa jimbo la Kinondoni, Iddi Azzan akizungumza wakati akinadi sera za chama Cha Mapinduzi,CCM  mbele ya wanaCCM wa mtaa wa Kisiwani, Kata ya  Ndugumbi jana jijini Dar es Salaam na kuaidi kuwa endapo atachaguliwa kurudi katika kiti chake kuwa atatatua tatizo la maji linalowakabili wananchi wa kata hiyo.
    Mgombea wa Ubunge wa jimbo la Kinondoni, Iddi Azzan akiwa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Kinondoni, Marry Kalisinje wakati  wakati mbunge wa Kinondoni akinadi sera zake katika  mtaa wa Kisiwani, mtaa wa Ndugumbi jana jijini Dar es Salaam. 

   Kushoto ni Mgomea wa Udiwani wa kata ya Ndugumbi, jimbo kinondoni a ya  kwa tiketi ya chama cha CCM,Thadey Massawe akionyesha Ilani ya chama hicho mara baada kupewa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Kinondoni, Marry Kalisinje.

  Mgombea wa Ubunge wa jimbo la Kinondoni, Iddi Azzan akiwa na wajumbe wa CCM.
  Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Mgombea wa Ubunge wa jimbo la Kinondoni, Iddi Azzan.

  0 0


  Promota Kaike Silaju katikati akiwainuwa mikoni juu mabondia Thomas Mashali kushoto na Fransic Cheka baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri Morogoro Picha na SUPER D BOXING NEWS

  Mabondia Thomas Mashali kushoto na Fransic Cheka wakionesha mikataba yao baada ya kusaini kuzipiga desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri Morogoro Picha na SUPER D BOXING NEWS
  Bondia Fransic Cheka kushoto na Thomas Mashali wakisoma mkataba kabla ya kutia saini kwa ajili ya kuzipiga desemba 25 katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro Picha na SUPER D BOXING NEWS
  Wakili Paul Kalomo kutoka Mega Attorneys akiwafafanulia kifungu kwa kifungu mabondia Thomas Mashali wa pili kushoto na Fransic Cheka kulia kabla awajasaini
  Promota Kaike Silaju katikati akipitia mkataba kabla ajawasainisha mabondia Thomas Mashali kushoto na Fransic Cheka ambapo wamekubaliana kuzipiga desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri Morogoro Picha na SUPER D BOXING NEWS

  Wakili Paul Kalomo akiwaelekeza mabondia Thomas Mashali kushoto na Fransic Cheka jinsi ya kusaini mkataba wa pili kushoto ni promota Kaike Silaju  mabondia hawo watapigana desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri morogoro .

   Na Mwandishi Wetu
  Mabondia Thomasi Mashali na Fransic Chaka Jana wamesaini mkataba wa kuzipiga siku ya desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri Morogoro

  akisimamia utiaji saini huo 
  Wakili Paul Kalomo kutoka Kampuni ya  Mega Attorneys amesema mkataba huo ni rasmi kwa mabondia hawo watapambana siku hiyo kwenye mpambano wa raundi kumi kwa dakika tatu kila raundi na kupumzika kwa dakika moja mpambano utakuwa wa raundi kumi na mabondia watapimwa afya zao siku moja kabla ya mchezo ili kujiridhisha kuwa wako fiti

  nae promota wa mpambano uho ambaye amekuwa akiandaa mapambano makubwa makubwa na yenye msisimko nchini amesema kuwa mpambano uho unasubiliwa na mashabiki lukuki na nimeamua kuweka katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro ili kuwapa fursa nyingine kwa wakazi wa morogoro kumwona Cheka ambaye kwa mda mrefu ajacheza

  nae bondia Fransic Cheka amewaomba wapenzi na mashabiki wajitokezekwa wingi ili kuja kujionea kichapo atakachompa Mashali ambapo ndio kitamfanya ajutie kabisa kucheza mchezo wa ngumi

  kwa upande wa Mashali amesema amefurai kupata nafasi nyingine ya kucheza na cheka kwani anataka kuonesha kiwango chake kilivyo kikubwa kwa sasa na yeye ni nambari wani katika ngumi nchini
  katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na mapambano ya utangulizi ambapo bondia Vicent Mbilinyi atapambana na Deo Njiku wakati Mohamed Matumla atakabiliana na Cosmas Cheka

older | 1 | .... | 656 | 657 | (Page 658) | 659 | 660 | .... | 1896 | newer