Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 655 | 656 | (Page 657) | 658 | 659 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Dk. Magufuli asema iwapo atapata ridhaa yakuiongoza nchi atahakikisha anatoa mikopo kwa wasomi wanao maliza elimu ya juu nchini. https://youtu.be/bjV9jNZsh9Q

  Tanzania yapata mkopo wa zaidi ya shilingi bilioni 240 kutoka serikali ya Poland kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha matrekta. https://youtu.be/W70x_FxENZo

  Kampuni ya bima ya insuarance TANRI yasema huduma za bima ni muhimu kwa mtanzania sababu zinatoa kinga dhidi ya majanga mbalimbali. https://youtu.be/NAm0yAbsdJE

  Timu ya Azam Fc yasema swala la kuzalilishwa kwa mshambuliaji wa John Bocco na mlinzi wa Mbeya city Juma Nyoso wanaliacha mikononi mwa TFF. https://youtu.be/JsHwxJOMS3M

  Taasisi ya taifa ya utafiti wa magonjwa ya binadamu yatoa tahadhari kuhusu uwezekano mkubwa wa kutokea mlipuko wa homa ya bonde la ufa. https://youtu.be/3JxqAVSOb5o

  Mwili wa marehemu mama Celine Kombani waagwa leo huku makamu wa rais akiongoza maombolezo hayo katika viwanja vya karimjee. https://youtu.be/zHGeLbZA6Jo

  Mkutano wa mgombea urais Edward Lowassa wavunjika mkoani Tanga baada ya umati mkubwa wa watu kujitokeza na kuzimia kwa wingi. https://youtu.be/7tdAhq_BxY0

  Dk John Pombe Magufuli ahaidi mfumo wa utoaji huduma za afya kwa watanzania ikiwemo kuboresha upatikanaji wa dawa. https://youtu.be/IhsjD9GeFHE

  Bodi ya utalii Tanzania yatangaza kua maonesho ya kimataifa ya sekta ya utalii yatafanyika kuanzia oktoba 1-3 mlimani city. https://youtu.be/r0i-XZgYY5w

  Jumla ya wachezaji 24 wanaounda kikosi cha timu ya taifa stars kitakachocheza dhidi ya Malawi chatangazwa rasmi.https://youtu.be/ryM00jNJhZA

  Kundi la mashabiki wanaosadikiwa kua klabu ya Nice ya ligi kuu Ufaransa walishambulia gari la rais wa PSG kwa mawe.https://youtu.be/D3I_lBsseaA

  Mgombea uraisi wa CCM Dr.Magufuli amtaka mwekezaji wa mashine za kusagia mahindi Iringa kuhakikisha zinafanya kazi la sivyo atazirudisha. https://youtu.be/33w2SRw5_NA

  Ugonjwa wa Kipindu pindu waendelea kutishia maisha katika maeneo mbali mbali hapa nchini baada wakazi 11 kulazwa mkoani Singida. https://youtu.be/EEla58ZIofQ

  Uhalifu dhidi ya makanisa mkoani Kagera waendelea kushika kasi baada ya makanisa matatu kuvunjwa na thamani zake kuchomwa moto. https://youtu.be/9sKnCWfDYJs

  Umoja wa katiba ya wananchi mkoani Tabora walitaka jeshi la polisi nchini kutofungamana na chama chochote ili kutunza amani kuelekea uchaguzi mkuu. https://youtu.be/i2MyvoicC_w

  Mlipuko wa Kipindu pindu wazua tharuki na kutishia maisha ya wakazi wa musoma baada ya mtu mmoja kufariki huku wengine 60 wakilazwa. https://youtu.be/wktGWSoJ1Tk

  0 0


  0 0

  President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete meets the United Nations Secretary General’s Special Advocate for Inclusive Finance for Development (or as it's more simply known, UNSGSA) Netherlands Queen Maxima at the UN Headquarters in New York this afternoon  (photo by Freddy Maro)

  0 0


  THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS


  Telephone: 255-22-2114512, 2116898

  Website : www.ikulu.go.tz              

  Fax: 255-22-2113425  PRESIDENT’S OFFICE,

        STATE HOUSE,

                1 BARACK OBAMA ROAD,  

  11400 DAR ES SALAAM.

  Tanzania.

   
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Tanzania yatangaza hatua tano za kuendeleza haki za wanawake na usawa wa kijinsia

  ·        Yaahidi kufanya mabadiliko makubwa ya kisera na kisheria

  ·        Miongoni mwa Sheria zitakazohusika ni Sheria ya Ndoa na Sheria ya Urithi

  ·        Ni katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu  - SDG’s

  Tanzania imeahidi kuchukua hatua tano muhimu za kutetetea na kuendelea haki za wanawake kati ya sasa na mwaka 2030, ikiwa ni pamoja na kufanya mabadiliko makubwa ya kufuta sheria zinazokandamiza wanawake na kutunga sheria za kuleta usawa wa kijinsia, yote katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG) mapya kwa manufaa ya wanawake wa Tanzania.


  Miongoni mwa hatua hizo itakuwa ni pamoja na kufuta ama kufanya mabadiliko ambayo yanaendeleza vitendo vya kiutamaduni ambavyo kwavyo vinaendeleza ubaguzi wa wanawake kama vile Sheria ya Ndoa, Sheria ya Urithi na kutunga Sheria ya Kukomesha Ukatili dhidi ya wanawake.


  Msimamo huo wa Tanzania umeelezwa Jumapili, Septemba 27, 2015 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alipozungumza katika Mkutano wa Usawa wa Jinsia na Uwezeshaji wa Akinamama: Dhamira ya Kuchukua Hatua uliohudhuriwa na wakuu wa nchi mbali mbali duniani kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) mjini New York, Marekani.


  Rais Kikwete ameuambia mkutano huo ulioitishwa  kwa pamoja na Jamhuri ya Watu wa China, Denmark, Mexico na Kenya kuwa hatua ya pili ambayo Tanzania inakusudia kuchukua ni kuridhia makubaliano yote ya kimataifa kuhusu haki za akinamama hasa Makubaliano ya Kimataifa Juu ya Kukomesha Aina Zote za Ubaguzi Dhidi ya Wanawake – Convention on the Elimination of All Forms of Discrimination Against Women (CEDAW).

  Hatua nyingine ambazo Rais Kikwete amesema kuwa Tanzania itachukua katika miaka 15 ijayo ili kuhakikisha usawa wa kijinsia nchini ni zifuatazo:

  ·        Kuendeleza na kuunga mkono upatikanaji wa raslimali fedha zinazolenga kuongeza usawa wa kijinsia kwa mujibu wa Ajenda ya Kugharimia Maendeleo ya Addis Ababa, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha zinatolewa pesa za kutekeleza mipango ya kitaifa na ya Serikali za mitaa za kukomesha ukatili dhidi ya wanawake.


  ·        Kuhakikisha utekelezaji wa uwakilishi wa uongozi wa asilimia 50-50 kati ya wanawake na wanaume katika nafasi zote za maamuzi kwenye ngazi zote.

  ·        Kupatikana na kutumiwa kwa data na habari za ukweli katika utunzi wa sera na utoaji maamuzi ya kukomesha ubaguzi wa kijinsia.

  ·        Kutunga na utekelezaji mfumo wa uwajibikaji na ufuatiliaji wa haki za kijinsia na haki za akinamama zilizokubaliwa kitaifa na kwenye ngazi ya Serikali za mitaa.


  Rais Kikwete pia amewaambia wajumbe wa mkutano huo kuhusu hatua za kisera na kisheria ambazo zimechukuliwa na Tanzania katika miaka ya karibuni kujenga usawa wa kijinsia, ikiwa ni pamoja na Sheria ya Ardhi ya mwaka 1999 na marekebisho yake ya mwaka 2004 ambayo yanawapa akinamama nafasi na haki ya kupata, kushikilia, kutumia na kumiliki ardhi.


  Hatua nyingine ni kuwapa wanawake nafasi za maamuzi na uongozi katika nyanja za kisiasa na maisha ya umma. Katika kutekeleza hilo, idadi ya wabunge wanawake imeongezeka kutoka asilimia 21.5 ya wabunge wote mwaka 2005 hadi kufikia asilimia 34.5 mwaka huu, mawaziri wanawake wameongezeka kutoka sita mwaka 2005 hadi kufikia 26 mwaka huu na idadi ya majaji wanawake imeongezeka kutoka wanane mwaka 2005 hadi kufikia 41 mwaka huu.


  Rais Kikwete amesema kuwa hatua nyingine zilizochukuliwa na Serikali ni kupunguza vifo vya wanawake wakati uzazi, kutunga Sheria dhidi ya ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya wanawake na watoto; kuanzishwa kwa uandaaji wa Bajeti inayotilia maanani mahitaji ya wanawake na kuongeza uwezekaji wa kiuchumi wa akinamama kupitia kuanzishwa kwa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB) yenye kulenga kutoa mikopo ya masharti nafuu kwa akinamama wafanyao biashara ndogo ndogo na za kati.

  Imetolewa na:

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

  Ikulu,

  DAR ES SALAAM.
  28 Septemba, 2015


  0 0

   Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwasalimia watoto Othman na Zainab waliokaa kwenye kisiwa kinachosadikiwa kuwa na mafuta katika eneo la Tundauwa.
   Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akipandisha bendera katika tawi la CUF Tandani shehiya ya Kilindi lililokuwa chini ya Chama cha ADC, kuashiria ufunguzi rasmi wa tawi hilo.
  Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na wanachama wa wanachama wa Jumuiya ya maendeleo ya wanawake Tundauwa. (Hawapo pichani). 
  Picha na Salmin Said, OMKR.


  Na: Hassan Hamad, OMKR
  Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, ametembelea kisima kinachosadikiwa kuwa na mafuta katika eneo la Tundauwa, na kusema kuwa mafuta ya Zanzibar yatachimbwa  katika kipindi kifupi kijacho.

  Amesema  kwa miaka mingi Zanzibar imeshindwa kuchimba mafuta yake kutokana na kutokuwepo mikakati imara, na kuahidi kuwa iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar atahakikisha kuwa suala hilo linawekewa mikakati imara ya uchimbaji, ili wananchi waweze kunufaika na rasilimali hiyo muhimu kwa maendeleo ya taifa.

  Kwa mujibu wa kumbukumbu zilizopatikana katika eneo hilo, kisima hicho chenye urefu wa zaidi ya futi 12 elfu na mia saba, kilijengwa miaka 53 iliyopita na kuonesha dalili za kuwepo mafuta.

  Wakati huo huo Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, ametembelea Jumuiya ya maendeleo ya wanawake Tundauwa, na kutoa wito kwa wananchi wa kijiji hicho kujiunga na jumuiya hiyo ili kupata mafanikio zaidi.

  Amesema jumuiya hiyo inayojihusisha na masuala mbali mbali yakiwemo uhifadhi wa mazingira na kilimo, imekuwa mfano mzuri wa kuigwa kutokana na mafanikio inayoyapata tokea kuanzishwa kwake.

  “Jumuiya hii inafanya kazi nzuri ya kupigiwa mfano, hivyo natoa wito kwa wananchi wa vijiji hivi kujiunga kwa wingi ili kuleta mafanikio zaidi” amesema Maalim Seif.

  Mapema akisoma risala ya Jumuiya hiyo, bibi Raya Abdallah Rashid amesema lengo la kuanzishwa kwa jumuiya hiyo ni kupambana na umaskini, maradhi pamoja na uhifadhi wa mazingira.

  Amesema Jumuiya hiyo pia imekuwa ikiielimisha jamii juu ya athari za mabadiliko ya tabia nchi na dawa za kulevya.

  Amesema Jumuiya hiyo iliyoanzishwa mwaka 2007 imepata mafanikio makubwa yakiwemo kutambuliwa kama jumuiya rasmi, kupanda mikoko ekari mbili kwa ajili ya uhifadhi wa mazingira, ufugaji wa nyuki na kilimo cha mboga mboga.

  Hata hivyo bi Raya amesema bado wanakabiliwa na changamoto ikiwa ni pamoja na ukosefu wa jengo la ofisi, na kulazimika kuanzisha ujenzi ambapo zaidi ya shilingi milioni saba na nusu tayari zimetumika kwa ajili ya ujenzi huo, na kuomba kupatiwa misaada zaidi ili wamewe ukamilisha ujenzi wao.

  Katika hatua nyengine Maalim Seif ambaye ni Katibu Mkuu wa CUF, amefungua tawi jipya la CUF Tandani shehiya ya Kilindi lililokuwa chini ya Chama cha ADC.

  Amesema Tawi hilo limebadilishwa kutoka ADC na kuwa tawi la CUF baada ya wanachama  25 wa ADC kuamua kujiunga na CUF na kuongeza idadi ya wanachama wa tawi hilo kufikia 103.

  Tawi jengine la ADC la eneo la meli tisa Wingwi, pia lilibadilishwa kuwa tawi la CUF baada ya wanachama wake kukihama chama hicho.

  0 0

  SIKU YA MOYO, WANANCHI KUPIMWA SHINIKIZO LA DAMU BURE. 

   KATIKA kuazimisha  siku ya afya ya Moyo Duniani Hospitali ya Taifa Muhimbili-MNH- leo itatoa huduma ya upimaji wa shinikizo la damu bure pamoja na kuwashauri wale watakaopatikana na tatizo hilo.

  Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu siku ya afya ya moyo Duniani ambayo huazimishwa Septemba 29 kila mwaka , Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo  Tulizo Shemu kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kitwete amesema magonjwa ya moyo yanachangia asilimia 31 ya vifo vyote vinavyosababisha takribani watu MIlioni 17. 3 kufa kila mwaka .


            Inasadikika itakapofika mwaka 2030 zaidi ya watu Milioni 25 watakuwa wanapoteza maisha kutokana na maradhi hayo hasa katika nchi zilizo na uchumi wa  chini na kati.


            Siku ya afya ya moyo Duniani hutoa fursa kwa watu wote Duniani kuazimisha kwa vitendo katika kujilinda na janga la magonjwa ya moyo na mishipa ya damu ambayo yanachangia vifo vingi .


            Dokta  Shem  ametaja baadhi ya visababishi vinavyochangia magonjwa ya moyo kuwa ni matumizi ya tumbaku, chumvi , pombe, vyakula vyenye mafuta, kutofanya mazoezi , unene uliokithiri , kutotibu ugonjwa wa kisukari na kuwa na mafuta mengi kwenye damu.  Kauli mbiu ya mwaka huu ni kuweka mazingira mazuri ya afya bora ya moyo katika sehemu zetu tunazofanyia kazi kwa kuhakikisha kila mtu anatoa mchango katika kujenga afya bora ya moyo ili kupunguza visababishi vinavyochochea magonjwa hayo.
   Daktari Bingwa wa magonwa ya moyo, Dk Tulizo Shemu (kulia) wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akizungumza na waandishi wa habari katika taasisi hiyo kuhusu siku ya afya ya moyo duniani ambayo inafanyika Septemba 29, kila mwaka.
   Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo nchini, Dk Tatizo Wane (kulia) wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akizungumza na waandishi wa habari katika taasisi hiyo kuhusu siku ya afya ya moyo duniani ambayo inafanyika Septemba 29, kila mwaka.  Kesho watu watapimwa bure shinikizo la damu na watakaopatikana na tatizo hilo watapewa ushauri wa bure. Pia siku ya kesho (Septemba 29, 2015) Taasisi hiyo itagawa vepeperushi, majarida na CD zinazozungumzia magonjwa ya moyo.
  Baadhi ya waandishi wa habari.


  0 0

                   KUSOMA  ZAIDI  links  goes  to  sheriayakub.blogspot.com
  Na  Bashir  Yakub.

  Tulipoandika namna  bora  na  taratibu  maalum  za  kufuata unapotaka  kununua  ardhi  tulisema  pia   kuwa   taratibu  za  ununuzi  wa  ardhi  huwa  zinatofautiana  kutegemea  na   mazingira  ya  kila  ardhi. 

  Tukasema  unaponunua  ardhi  kwa  msimamizi  wa  mirathi  ni  tofauti  na  unaponunua  kwa  mmiliki  mwenyewe. Unaponunua  ardhi  ya  familia  ni  tofauti  na  unaponunua  isiyo  ya  familia. 

  Vilevile  unaponunua  ardhi  ya  kijiji  ni  tofauti  na  unaponunua ardhi  isiyo  ya  kijiji.  Taratibu  hutofautiana  na  hasa  tofauti  ipo  katika  nyaraka  ambazo  zinatakiwa  kuambatanishwa  ikiwa  kama  ithibati  ya  ununuzi. Hata  uandishi  wa   mkataba  wa  manunuzi  pia  nao huwa na tofauti  katika  hili.


  1.ARDHI  YA  KIJIJI  KWA  UWEKEZAJI.

  Wako  watu  wamekuwa   wakinunua  ardhi  hasa  huko  vijijini  lakini  baadae  wamekuwa  wakijikuta  katika  migogoro  mikubwa  na  wenyeji. Mwamko  wa  kununua  maeneo  kama  bagamoyo, kisarawe, huko  chanika  dondwe na  maeneo  mengine  umekuwa  mkubwa  sana.

   Hata  hivyo  mwamko  unavyoongezeka  ndivyo  na  migogoro  inavyoongezeka. Kubwa  katika  migogoro  hii  ni  hatua  ya  wanunuzi  kutokufuata  utaratibu  wa  ununuzi aidha  kwa  kujua, kutokujua  au  kupotoshwa.


   Wakati  mwingine  ni  uelewa mdogo  miongoni  mwa  wenyeji  lakini  zaidi  ni  hili  la  kutofuata utaratibu. Mara  zote  huwa  tunasema  ni  bora  zaidi  mgogoro  unapotokea  halafu  ukukute  ulifuata  taratibu  wakati  wa  manunuzi. Bila  shaka hautakuwa  na  athari  kubwa  kwako  lakini  ni  mbaya   zaidi  ukitokea  halafu  ukukute kuna  taratibu  hukufuata kwa  bahati  mbaya  au  bila  kujua. Unakuwa  katika  hatari  ya  kupoteza. Unapokwenda  kununua  ardhi  ya  kijiji  kwasababu  yoyote  ile  hasa uwekezaji  upo  utaratibu maalum wa kufuata  nitakaoeleza.


  2.  ARDHI  YA  KIJIJI  NI  NINI.

  Ardhi  ya  kijiji  ni  ile  ardhi  iliyopo  katika  mipaka  ya  kijiji  fulani  ilyoainishwa  na  mamlaka  za  wilaya  husika  huku  ikiwa  na  hati ya  usajili  wa  kijiji. Ardhi  hii  hulindwa  kwa  taratibu  za  kimila  za  eneo  husika  ikiwa  ni  pamoja  na sheria  namba  4 ya  1999.


  3.    UTARATIBU  WA  KUNUNUA  ARDHI  YA  KIJIJI  KISHERIA.

  ( 1 ) Maombi  maalum huandaliwa  na  kuwasilishwa  kwa  mtendaji  wa  kijiji  ambaye  hupatikana  katika  kila  kijiji.

  ( 2 ) Maombi  huandaliwa  katika  fomu  maalum  ambazo  hupatikana  katika  kila  ofisi  za  kijiji. Si  maombi  ambayo  huandaliwa  kama  barua  za  kawaida za maombi.

  ( 3 ) Ikiwa  mwombaji  ni  mtu  mmoja   basi   atasaini  sehemu  maalum  na ikiwa  ni  maombi  kwa  niaba  ya  famliia  basi  watu  wawili  kutoka  ile  familia  watasaini  na  ikiwa  ni  ardhi  kwa  ajili  ya  kikundi  pia  wawakilishi  wasiopungua wawili  kutoka  kile  kikundi  watasaini  kwa  niaba  ya  wengine.

  ( 4 ) Kama  mwombaji  ni  chama  cha  ushirika  au  kampuni  basi  inatakiwa  kuwepo  wadhamini  wawili   kwa  ajili  ya  shirika  au  kampuni  hiyo. Wanaweza  kuwa  zaidi  ya  wawili  lakini  wasipungue.

  ( 5 ) Kama  anayeomba  ardhi  si  mwenyeji  wa  eneo  husika  basi  atatakiwa  kuwa  na  wadhamini  wasiopungua  watano  ambao  ni  wenyeji  wa  eneo  hilo. Sharti  ni  kuwa  kati ya  hao  wadhamini  wasiwepo  ndugu  wa  mwombaji.

  ( 6 ) Mwombaji  atatakiwa  kuambatanisha katika  maombi  yake  tamko  linaloonesha  ardhi  nyingine  anayoimiliki  Tanzania  nje  na  hiyo  anayoomba.

  ( 7 )  Ikiwa  ardhi  inaombwa  kwa  ajili  ya  makazi  basi  mwombaji  atatakiwa  kuambatanisha  tamko  linaloonesha  kuwa  ataanza  ujenzi wa  makazi hayo ndani  ya  miezi  mitatu  tangu  siku  ya  kuidhinishiwa  ardhi.

  ( 8 ) Ikiwa  mauzo  ni heka 50 au  kuendelea  ni lazima  yaidhinishwe  na  mkutano  mkuu  wa  kijiji.

  ( 9 ) Baada  ya  kukamilisha  taratibu  hizo  halmashauri  ya  kijiji  itakaa  vikao  na  ndani  ya  siku  tisini itatakiwa  kutoa  majibu.

  Kamwe  usikubali  kuuziwa  ardhi  ya  kijiji  na  viongozi   wa  kijiji  bila  kufuata  utaratibu  huu. Hii  hasa  ni kwa  wawekezaji  wanaochukua  maeneo  makubwa  kwa  shughuli  za  kiuchumi.

  MWANDISHI   WA   MAKALA  HAYA   NI   MWANASHERIA  NA  MSHAURI   WA  SHERIA  KUPITIA  GAZETI  LA  SERIKALI   LA   HABARI   LEO  KILA  JUMANNE  , GAZETI  JAMHURI   KILA  JUMANNE  NA  GAZETI  NIPASHE  KILA  JUMATANO.    0784482959,        0714047241              bashiryakub@ymail.com
  0 0

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Taarifa zaidi kuhusu Mahujaji kutoka Tanzania waliofariki na kujeruhiwa huko Saudi Arabia.  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kupitia Ubalozi wake mjini Riyadh, Saudi Arabia imepokea taarifa kuwa hadi kufikia tarehe 27 Septemba, 2015 watu waliopoteza maisha kufuatia tukio la mkanyagano (stampede) wa Mahujaji waliokuwa wakielekea Jamarat kutupa vijiwe huko Mina nje kidogo ya mji wa Makkah, lililotokea siku ya Alhamisi tarehe 24 Septemba, 2015 wameongezeka na kufikia 769 na majeruhi 934.


  Aidha, Wizara kupitia Ubalozi huo inaendelea kufuatilia hatma ya Mahujaji wa Tanzania waliopotea katika tukio hilo la ajali ambapo hadi sasa Mahujaji wa Tanzania wapatao 50 bado hawajaonekana. Vikundi wanavyotoka Mahujaji hao na idadi yao ni kama ifuatavyo:-

  1.  Ahlu Daawa-Mahujaji  30;

  2.  Khidma Islamiya-Mahujaji 16; na

  3.  TCDO-Mahujaji 4

  Vile vile juhudi za Ubalozi kwa kushirikiana na Tanzania Hajj Mission na viongozi wa vikundi vilivyopoteza Mahujaji wao zimefanikiwa kuutambua mwili wa hujaji mmoja aliyefariki dunia anayejulikana kwa jina la Shafi Khamis Ali kutoka kikundi cha Ahlu Daawa. Kutambuliwa kwa mwili wa hujaji huyo kunafanya idadi ya Mahujaji wa Tanzania waliofariki dunia katika ajali hiyo kufikia watano (5).


  Pia, Wizara kupitia Ubalozi wake imepokea taarifa ya kupatikana kwa hujaji mwingine anayeitwa Nasra Abdullah akiwa hai naye kutoka kikundi hicho cha Ahlu Daawa.


  Kuhusu majeruhi, taarifa kutoka Ubalozini zinaeleza kuwa, hujaji mmoja aliyejulikana kwa jina la Mahjabin Taslim Khan alipata majeraha yaliyopelekea kukatwa mguu na kwa sasa anaendelea kupata matibabu huku hali yake ikiendelea vizuri.


  Ubalozi unaendelea na juhudi za kuwatafuta Mahujaji wengine wa Tanzania ambao bado hawajaonekana kwa ajili ya kubaini wale waliofariki au majeruhi wanaoendelea kupatiwa matibabu.


  Mahujaji wengine wa Tanzania wapo salama ambapo tarehe 26 Septemba, 2015 walimaliza ibada ya hija na tarehe 28 Septemba, 2015 wameanza safari ya kurejea nyumbani.


  Wizara inaendelea kuwaomba Wananchi kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu wakati Serikali ikiendelea kufuatilia.

  Imetolewa na:

  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,

  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,

  Dar es Salaam


  28 Septemba, 2015

  0 0

   Mratibu wa Kampeni upande wa Vijana CCM kwa Mkoa wa Dar es Salaam na Vyuo Vikuu Bw. Daniel Zenda akizungumza na Zaidi ya Vijana 500 kutoka Jimbo la Mbagala wakati wa uzinduzi wa MAGUFULI Club jijini Dar es Salaam jana. MAGUFULI Club imeanzishwa kama jukwaa la kuwakutanisha vijana nchini kote wanaomuunga mkono mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dkt. John Pombe Magufuli.
   Mratibu wa MAGUFULI Club wilaya ya Temeke Bw. Peter Dafi akizungumza na vijana kutoka Jimbo la Mbagala wakati wa uzinduzi wa MAGUFULI Club jijini Dar es Salaam jana. MAGUFULI Club imeanzishwa kama jukwaa la kuwakutanisha vijana nchini kote wanaomuunga mkono mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dkt. John Pombe Magufuli.
   Baadhi wa vijana wakifuatilia uzinduzi wa MAGUFULI Club katika Jimbo la Mbagala jana jijinI Dar es Salaam.
   Wanachama wa MAGUFULI Club wakifurahia wakati uzinduzi wa Club hiyo katika Jimbo la Mbagala jana jijini Dar es Salaam.  Picha na:  Frank Shija


  0 0
 • 09/28/15--21:09: MUZIKI MNENE KIBAHA

 • 93.7 EFM yajinyakulia ushindi baada ya kuwafunga kibaha veterans mabao mawili kwa moja, katika mchezo  uliochezwa mwishoni mwa wiki  katika uwanja wa Tamco kibaha, Mechi hiyo ni baadhi ya mechi zinazoendelea baina ya EFM na timu mbalimbali za wasikilizaji wake, Kupitia kampeni ya Muziki mnene bar kwa bar .


  Burudani haikuishia hapo,  baada ya mechi hiyo shangwe ziliendelea ndani ya kibaha kontena. Ilikuwa ni bandika bandua ya ngoma kali kutoka kwa Rdj’s wa 93.7 EFM na  shamra shamra kutoka  kwa timu nzima ya EFM na wakazi wa kibaha.

  0 0

  NA JAMIIMOJABLOG)
  WATU wengi wanasumbuliwa na tatizo hili ambalo huwafanya kuwa na uoga na aibu wa kuelezea na kushindwa hata kwenda hospital kupata tiba
  JE, UNAJUA BAWASIRI/HEMORRHOIDS NI NINI????!!
  ~Ni ugonjwa unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu ya ndani na Inje ya sehemu ya haja kubwa na wakati mwingine mishipa hiyo huweza kupasuka/kuteleza na kuvuja damu kwenye njia ya haja kubwa na kasababisha kutoka kinyama au uvimbe.

  ~ugonjwa huu wa bawasiri kwa lugha ya kitaalamu tunauita HEMORRHOIDS ilhali kwa lugha ya kingereza unafahamika kama piles
  ~tatizo hili huwaathiri watu wote ila zaidi huwaathiri watu wazima kuliko watoto na inakadiriwa kuwa karibu 50%ya watu wote wako katika hatari ya kupata tatizo hili katika umri wa miaka 30_50
  AINA ZA BAWASIRI
  ~Kuna Aina mbili za bawasiri
  (A) BAWASIRI YA NDANI
  ~Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa huwa haiambatani na maumivu na wengi huwa hawajitambui kuwa Wana tatizo hili
  ~Aina hii hutokana na kuvimba na kuharibika kwa mshipa wa artery za ndani ya mfereji wa haja kubwa
  ~Aina hii imegawanyika katika madaraja manne
  (1)DARAJA LA KWANZA ~Hii ni bawasiri ambayo haitoki mahali pale panapohusika
  (2)DARAJA LA PILI ~hii hutokea wakati wa haja na kurudi yenyewe ndani baada ya kujisaidia.
  (3)DARAJA LA TATU :hii hutokea wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kurudisha ndani yeye mwenywe.
  (4)DARAJA LA NNE :hii ni bawasiri inayotoka na huwa ngumu kurudi
  (B)BAWASIRI YA NNJE
  ~Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa na huambatana na maumivu makali na kuwashwa kwa ngozi katika eneo la tundu Hilo pia husababisha mishipa ya damu (vena) kupasuka na damu kuganda na kasababisha Aina ya bawasiri iitwayo THROMBOSED HEMORRHOIDS
  CHANZO CHA TATIZO
  ~chanzo halisi cha ugonjwa huu hakijapatikana ila Kuna vitu ambavyo huwa chanzo cha kupata ugonjwa wa bawasiri ambayo ni ÷
  👉KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE
  👉KUHARISHA KWA MUDA MREFU
  👉TATIZO LA KUTOPATA CHOO
  👉MATATIZO YA UMRI
  👉KUKAA KITAKO KWA MUDA MREFU
  👉UZITO KUPITA KIASI
  👉MATUMIZI YA VYOO VYA KUKAA KWA MUDA MREFU
  DALILI ZA BAWASIRI
  👉Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
  👉kupata maumivu makali wakati wa kujisaidia
  👉kutokea uvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
  👉kujitokeza kwa kinyama katika eneo la tundu Hilo
  👉kinyesi kuwa na damu na kunuka harufu mbaya sana
  MATIBABU NA JINSI YA KUEPUKA TATIZO LA BAWASIRI
  ~matibabu ya bawasiri hutegemea na Aina ya bawasiri pia tiba iliyozoeleka ni kukatwa kinyama na kuendelea na lishe ya chakula hata hvyo tiba hii si nzuri kwasababu huwa haitibu chanzo cha tatizo hivyo huwa rahisi kujirudia hivyo tiba nzuri ni kutumia dawa na anion chip kubandika mahali penye tatizo na kuondoa tatizo Hilo
  ~Pamoja na hayo bawasiri ni ugonjwa unaoweza kuepukika kwa kuzingatia
  👉KULA MBOGAMBOGA ZA MAJANI, MATUNDA, NA NAFAKA ZISIZOKOBOLEWA
  👉KUNYWA MAJI MENGI ANGALAU GRASS 6/12 Kwa siku
  👉EPUKA KUKAA CHOONI KWA MUDA MREFU
  MADHARA YA TATIZO LA BAWASIRI
  👉kupata upungufu wa damu (anemia)
  👉Kupata tatizo la kutokuweza kuhimil choo
  👉hupunguza nguvu za kiume na kuondoa hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake
  👉kuathirika kisaikolojia
  👉kukosa moral ya kufanya Kazi kutokana na maumivu makali
  WASILIANA KWA 0717035770 AU 0753692612.

  0 0

   Bi Harusi mtarajiwa Ester Diana Nana (kushoto) akigonisha glasi na msimamizi wake, Hellen, wakati wa sherehe ya kuagwa (Send off) iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
   Ester akikata keki huku akisaidiana namsaidizi wake
   Bi Harusi mtarajiwa Ester Diana Nana (kushoto) akimlisha keki msimamizi wake, Hellen, wakati wa sherehe ya kuagwa (Send off) iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
   Bi Harusi mtarajiwa Ester Diana Nana akimkabidhi keki, Naibu Katibu Mkuu wa Ofoso ya Makamu wa Rais, Bi. Angelina Madete, wakati wa sherehe ya kuagwa (Send off) iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
   Mwendesha Shughuli Mc Bazil, akifanya yake katika sherehe hiyo.
   Mama Mzazi wa Bi harusi mtarajiwa, akimkabidhi zawadi ya Biblia mwanae Ester
   Wakwe wakiandaa zawadi ya Bi harusi mtarajiwa kabla ya kumkabidhi
   Mc Bazil. akimkabidhi zawadi ya Cd Bi Harusi mtarajiwa ukumbini hapo
   Wakati wa zawadi.....
  Bi harusi mtarajiwa akiwa na mumewe mtarajiwa wakielekea kupata chakula cha usiku ukumbini hapo. Watarajiwa hao wanatarajia kufunga ndoa jumamosi ya wiki hii.
  Wakati wa mlo wa usiku

  0 0
 • 09/29/15--01:07: MECHI ZA UEFA USIKU HUU
 • Hii ni ratiba ya mechi za Jumanne ya September 29Mechi hizi zote zitachezwa saa 21:45 kwa saa za Afrika Mashariki
  Hii ni ratiba ya mechi za Jumatano ya September 30

  0 0

  THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

  TANZANIA ni nchi ya kwanza duniani kutoa huduma za pesa, kutoa mikopo na kutoa riba kwa kutumia mawasiliano ya simu, Benki ya Dunia imesema na kuongeza kuwa Tanzania ni moja ya masoko makubwa zaidi duniani ya kutoa huduma ya fedha kwa njia ya simu.


  Benki hiyo ya Dunia pia imesema kuwa Serikali ya Tanzania imewekeza kwa kiwango cha juu katika mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) ikilinganishwa na nchi nyingine duniani na kulingana na uwezo wake.


  Benki hiyo pia imesema kuwa nchi jirani ya Kenya inaongoza kwa kutuma pesa kupitia mfumo wa M-Pesa katika eneo ambalo miaka michache iliyopita lilikuwa eneo la kujidai la nchi tajiri tu duniani.


  “Huu ni mfano kutoka Afrika ambao unaweza kuigwa na nchi zote duniani,” amesema Profesa Kaushik Basu, Mchumi Mkuu wa Benki ya Dunia (WB) wakati akiwasilisha kwa ufupi tu yaliyomo katika Ripoti ya Benki hiyo ya World Development Report ambayo itatolewa hivi karibuni.


  Profesa Basu alikuwa anazungumza jana, Jumatatu, Septemba 28, 2015 kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi uliozungumzia Hali ya Enzi za Digitali (Digital Age) uliofanyika kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN), ikiwa ni sehemu ya majadiliano kuhusu Malengo ya Maendeleo Mapya (SDG’s) ambayo yanachukua nafasi ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDG’s) ambayo muda wake wa utekekezaji wa miaka 15 umefikia mwisho mwaka huu.


  Akizungumza katika mkutano huo uliohudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Estonia Mheshimiwa Toomas Hendrik Ilves na Rais wa Benki ya Dunia (WB) Dkt. Jim Kim, Profesa Kaushik alisema:


  “Tuko katikati ya mapinduzi makubwa ya teknolojia, ambayo athari zake bado ni ngumu sana hata kubashiri. Na hizi ni shughuli ambazo miaka michache iliyopita zilikuwa hata hazina jina, lakini sasa inteneti na teknolojia ya digitali inabadilisha maisha ya kijamii na kisiasa ya binadamu,” alisema Profesa Basu.


  Aliongeza: “Chukulia takwimu hizi – kuna kiasi cha utafuta habari kwenye google kiasi cha bilioni 4.2 kwa siku moja, kila sekunde watu wanatuma tweet 6,000 na rekodi ilikuwa Agosti mwaka 2013 wakati zilipotumwa tweet 143,199 kwa sekunde wakati ilikuwa inaonyeshwa filamu moja ya sanaa.”

  Aliongeza: “Mfumo wa uwekaji na utumaji pesa wa M-Pesa katika Kenya sasa unashindana na mifumo ya siku nyingi ya nchi matajiri duniani. Kila watu wazima 1,000 kuna akaunti 700 katika Kenya ikiwa ni ongezeko 103 kutoka mwaka 2013.”


  “Jirani na Kenya kuna mfano mwingine wa mafanikio makubwa zaidi duniani katika nchi jirani ya Tanzania. Tanzania imewekeza sana katika ICT na katika mfumo wa kuhamisha na kusambaza fedha. Sasa Tanzania ni soko kubwa zaidi duniani la kutuma fedha kwa njia ya simu,” alisema Profesa Kaushik.


  Aliongeza: “Tanzania sasa ni nchi ya kwanza duniani kutoa huduma ya pesa, kutoa mikopo na kutoa riba kwa njia ya simu. Hii ni mifano ambayo nchi zote duniani zinaweza kuiga kutoka Afrika.”


  Wakati huo huo, Rais Kikwete leo, Jumanne, Septemba 28, 2015, amekutana na kufanya mazungumzo na Malkia wa Uholanzi, Malkia Maxima wa Uholanzi, Mke wa Mfalme Willem-Alexander kuhusu jinsi gani ya kuzidi kuisaidia Tanzania kuongeza kasi yake katika kuboresha huduma za pesa kupitia ICT.

  Imetolewa na:

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

  Ikulu,

  DAR ES SALAAM.

  29 Septemba, 2015

  0 0

   Afisa Masoko wa Airtel kanda ya ziwa akiongea na mawakali mara baada
  ya kuendesha seminar inayowapatia fulsa Mawakala wa Airtel Money
  nchini nzima kupata mikopo kupitia simu zao za mkononi

  Wakala wa Airtel Money katika maeneo ya Metro Mwanza, Bwn John Hainga
  akichangia mada wakati wa semina ya mawakala inayowapatia  fulsa ya
  kupata mikopo isiyo na dhamana ijulikanayo kama Timiza Mikopo kwa
  Mawakala

   KAMPUNI ya simu za mkononi nchini Tanzania Airtel imeendelea
  kuboresha huduma zake  kwa wateja hususani wajasiliamali
  wanaojihusisha na shughuli mbalimbali za kibiashara, ikiwa ni pamoja
  na utoaji wa huduma za Airtel Money , kwa kuwawawezesha mawakala
  kupata mikopo inayoitwa " Timiza mikopo kwa Mawakal " Kupitia simu zao
  za mikononi.

  Airtel imewakutanisha  mawakala wa Airtel Money kutoka sehemu
  mbalimbali za jiji la Mwanza ili kuwapatia mafunzo ya uboreshaji na
  ukuzaji vipato katika biashara zao.

  "Ukosefu wa  elimu ya uendeshaji biashara kwa wajasiliamali walio
  wengi hapa nchini umeendelea kuwa ni tatizo linaloshusha kiwango cha
  mapato kwa wajasiliamali kupitia shughuli zao hivyo kuzorotesha uchumi
  wa taifa .

   Kwa kutambua tatizo hili Airtel imeona ipo haja kuwapatia mafunzo ya
  uendeshaji biashara yatakayomwezesha mjasiliamali kutambua njia bora
  ya uendeshaji biashara, Ikiwa ni pamoja na utoaji mikopo isiyo na
  dhamana  kwa zaidi ya mawakala 20,000  kote nchini Ili kusaidia kukuza
  biashara za mawakala , kuongeza faida zaidi katika shughuli zao na pia
  upatilkanaji wa huduma ya za fedha katika jami". alisema meneja kanda
  ya ziwa wa Airtel, Bwana Raphael Daudi.

  Kwa upande wake mmoja ya wakala aliyehudhuria semina hiyo  bwana John
  Paschal alisema" tunayofuraha kuwezesha kupata mikopo kupitia huduma
  hii ya Timiza mikopo kwa mawakala. Na hii itaturahisishia kuboresha
  biashara zetu kwani sasa tuna uhakika wa mitaji.  Lakini pia mafunzo
  haya yatatusaidia sana katika kutunza mahesabu na kuendesha biashara
  zetu kwa ufanisi zaidi."

  Airtel katika kukabiliana na changamoto za kijamii na kiuchumi kwa
  wateja wake imefanikiwa kuzindua huduma hii ya timiza mikopo kwa
  mawakala, huduma itakayowawezesha mawakala  wa airtel money kote
  nchini kupata mikopo isiyo na dhamana ya kuanzia sh. 50,000/- hadi  500,000/-

  0 0
 • 09/29/15--02:00: BEI YA MADAFU HII LEO


 • 0 0

   Mrajisi Bodi ya Chakula, Dwa na Vipodozi  Zanzibar Dkt. Burhani Othman Simai  akizungumza na wadau wa madawa  Zanzibar katika mkutano wa uwiano wa udhibiti wa bidhaa hizo kwa Nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni.

  NA RAMADHANI ALI/MAELEZO ZANZIBAR     
  BODI ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDB) imeandaa miongozo ya utoaji huduma bora katika kufanikisha  Mpango wa uwiano wa Itifaki ya pamoja kwa Nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki.

  Mkurugenzi wa ZFDB  Dkt. Burhani Othman Simai ameeleza hayo katika Mkutano wa wadau wa Madawa Zanzibar ulioandaliwa na Mpango wa Udhibiti wa bidhaa za Chakula na Dawa wa Jumuia ya Afrika Mashariki katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

  Alisema kuanzia sasa bidhaa zote za chakula na madawa za  Zanzibar na zinazotoka nje  zitasajiliwa na Bodi yake na Viwanda vinavyotengeneza bidhaa hizo vitafanyiwa ukaguzi wa mara kwa mara ili kuhakikisha usalama wa  bidhaa hizo.

  Aliongeza kuwa katika kufanikisha mpango huo,  Zanzibar inategemea kupata ithibati ya Kimataifa (ISO Certification) mwezi Disemba na kuanzia Januari 2016 maombi na kazi zote za udhibiti wa bidhaa za chakula na madawa zitafanywa kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya ZFDB.

  Dkt. Burhani  aliwataka wadau wa bidhaa za chakula na madawa kutoa ushirikiano kwa  Bodi kwa kujisajili  katika Ofisi  yao  iliyopo Mombasa kwa Mchina na kuandaa utaratibu mzuri wa kurahisisha ukaguzi wa  bidhaa na viwanda vyao.

  Alisema taratibu hizo zinazochukuliwa na ZFDB zinalengo la kulinda afya za wananchi wa Zanzibar na Nchi wa wananchama wa Jumuia ya Afrika Mashariki.

  Mwakilishi kutoka Sekriteriati ya Jumuia ya Afrika Mashariki Mjini Arusha Mwesige John Patrick aliipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwa mstari wa mbele kufanikisha Mpango wa uwiano wa Nchi wanachama wa Jumuia hiyo.

  Alikumbusha  kuwa Mpango huo ulioanza mwaka 2012 kwa awamu ya kwanza ya miaka mitatu, ukizishirikisha Nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Ruwanda  umeanza kuleta mafanikio makubwa kwa nchi zote  wanachama na mwaka huu umeanza awamu ya pili ya miaka miwili.

  Akifungua Mkutano huo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bibi Halima Maulid ameitaka ZFDB kuendelea kusimamia mpango wa uwiano wa Udhibiti wa Bidhaa za chakula na dawa  na kuhakikisha zinakuwa salama kwa matumizi ya binadamu.

  Mkutano huo uliokuwa na lengo la kuwafahamisha wadau wa Zanzibar miongozo mipya iliyoandaliwa kwa pamoja na wataalamu wa Mamlaka za udhibiti wa Chakula na Dawa wa Wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki.
                           IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR.

  0 0

  Na Mwandishi Wetu
  VIONGOZI  wa kiroho 250 wa madhehebu mbalimbali ya dini ya kikristo wamealikwa kushiriki kwenye Tamasha la Amani Jumapili wiki hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

  Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ilieleza kuwa kati ya viongozi hao 200 ni Wachungaji na 50 ni Maaskofu.

  “Idadi inaweza kuwa kubwa zaidi, lakini hadi sasa niseme hao ndiyo ambao tuna uhakika nao watashiriki katika Tamasha la Amani Jumapili, ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais Jakaya Kikwete.

  “Maandalizi kuhusu tamasha yanaenda vizuri na nina imani Watanzania na wapenda amani wote waliopo hapa nchini hata kama sio raia wa hapa watajitokeza kwa wingi siku hiyo.

  “Ni tamasha ambalo dhamira yake ni kuomba kwa Mungu tuweze kupita kwa usalama kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu,” alisema Msama katika taarifa hiyo.

  Tamasha hilo lenye dhamira ya kuombea nchi amani kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani litahusisha wasanii mbalimbali wa nyimbo za Injili kutoka Tanzania na nje ya Tanzania.

  Baadhi ya wasanii wa nje waliothibitisha kushiriki ni Sipho Makhabane, Sohly Mahlangu wa Afrika Kusini, Sarah K wa Kenya, Ephraim Sekeleti wa Zambia na Solomon Mukubwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) anayeishi Kenya.

  Baadhi ya wasanii wa Tanzania watakaoshiriki ni Rose Muhando, Upendo Nkone, John Lissu, Upendo Kilahiro, Boniface Mwaitege , kwaya ya St. Andrew ya Dodoma na kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama.

  0 0

  Kipindi hiki hukujia kila JUMATATU, kujadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015
  Hiki ni kipindi kilichosikika Septemba 28, 2015
  Kutoka Tanzania tuliungana na Liberatus Mwang'ombe. Mgombea ubunge jimbo la Mbarali kwa tiketi ya CHADEMA
  Studioni alikuwepo Dj Luke Joe, na kwa njia ya simu tukaungana na wasikilizaji wengi ndani na nje ya Marekani
  KARIBU


  0 0

  Ajali ya roli imetokea Sinza Mori mida hii baada ya roli hilo kuchomoka tairi ya nyuma lakini hakuna mtu aliyepata madhara katika ajari hiyo pamoja na tairi kwenda mbali zaidi na eneo la tukio, hata hivyo dereva wa roli hilo amesema alikuwa anaenda kubadilisha ekseli iliyochomoka.
  Roli lenye namba za usajili T 245 DEZ  limechomoka taili ya nyuma maeneo la Sinza Mori leo barabara ya Shekilango jijini Dar es Salaam.. 
   Roli likiwa barabarani ya Shekilango barabara ya Shekilango jijini Dar es Salaam.
   Hapo ndipo taili lilipochomoka wakati gari likiendelea kutembea.

older | 1 | .... | 655 | 656 | (Page 657) | 658 | 659 | .... | 1897 | newer