Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel

Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels

Showcase

Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 654 | 655 | (Page 656) | 657 | 658 | .... | 1897 | newer

  0 0

  ·          Tanzania imetimiza masharti yote ya kupatiwa raundi ya pili ya fedha za maendeleo kutoka Shirika la Maendeleo ya Milenia la Millennium Challenge Corporation (MCC) la Marekani na itaanza kupata na kunufaika na mabilioni hayo ya fedha baada ya wajumbe wa Bodi ya MCC kupiga kura ya kuidhinisha kutolewa kwa fedha hizo chini ya Mpango wa MCC-2.

  Habari hizo njema zimetangazwa Jumamosi, Septemba 26, 2015, kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, na Mtendaji Mkuu wa MCC, Bi. Dana J. Hyde katika mkutano uliofanyika katika Hoteli ya JW Marriot Essex House, New York, na kuhudhuriwa na watumishi waandamizi wa MCC akiwamo Bwana Kamran Khan, Makamu wa Rais wa Operesheni za MCC. Rais Kikwete yuko New York kuhudhuria shughuli za mwaka huu za Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

  “Hongera Mheshimiwa Rais kwa sababu nchi yako, Tanzania imetimiza masharti yote ya kupata fedha nyingine chini ya mpango wa MCC - 2, ikiwa ni pamoja na uongozi wa MCC kuridhika kuwa Tanzania inachukua hatua za dhati kupambana na rushwa,” Bi. Hyde amemwambia Rais Kikwete na viongozi wengine wa Tanzania akiwamo Waziri wa Nchi za Fedha wa Zanzibar, Mheshimiwa Yusuf Omar Mzee.

  Bi. Hyde amemwambia Rais Kikwete kuwa Bodi ya MCC, katika mkutano wake wa Septemba 17, mwaka huu na chini ya Mwenyekiti wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Bwana John Kerry, imeafiki kuhusu kipengele pekee kilichokuwa kimebakia katika masharti ya kupata fedha za MMC kuwa ni kweli Tanzania inakabiliana ipasavyo na rushwa na kuchukua hatua stahiki kukabiliana na janga hilo la rushwa.

  MCC imetoa taarifa ya kuthibitisha kuwa Tanzania imetimiza masharti ya kuiwezesha kufaulu kupata raundi ya pili ya fedha za maendeleo na pia imetoa taarifa ya kuthibitisha kuwa ni kweli Bodi ya MCC imeridhishwa na hatua zinazochukuliwa kukabiliana na rushwa.
  Tofauti na fedha nyingi zinazotolewa na wafadhili wengi duniani, fedha za MCC hazitakiwi kurudishwa na nchi inayopewa fedha hizo na pia nchi husika hupewa uhuru wa kuchagua aina ya miradi ya maendeleo ambayo inaitaka igharimiwe na fedha hizo.

  Miongoni mwa wajumbe wengine wa Bodi ya MCC ni pamoja na Waziri wa Fedha wa Marekani ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi, Mwakilishi wa Biashara wa Marekani duniani, Mwendeshaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), nafasi ambayo kwa sasa anaikaimu Bwana Alfonsi Lenhardt, Mtendaji Mkuu wa MCC Bi. Hyde na Rais wa Taasisi ya International Republican Institute (IRI) Balozi Mark Green.
  Mabalozi Lenhardt na Green walikuwa mabalozi wa Marekani katika Tanzania wakati wa majadiliano, upitishaji na utekelezaji wa MCC–1.

  Bi Hyde amesema sasa linalobakia ni kwa wajumbe wa Bodi kupelekewa muhtasari wa kuidhinisha mabilioni hayo kwa Tanzania ambayo chini ya mpango wa uwekezaji wa MCC–2 yatakwenda katika kuboresha huduma za umeme katika Tanzania ikiwa ni pamoja na kusambaza umeme katika vijiji vingi zaidi nchini. Kiasi cha asilimia 46 ya Watanzania kwa sasa wanapata umeme kutoka asilimia 10 ya mwaka 2005 na sehemu kubwa ya asilimia hiyo imetokana na msaada wa MCC-1.

  Chini ya Mpango huo wa pili wa MCC, Tanzania itapatiwa kiasi cha dola za Marekani milioni 472.8 (sawa na sh. bilioni 992.80). Kwa kutilia maanani kiasi cha dola milioni 698 (sawa na sh. trilioni 1.46) ambazo zilitolewa chini ya MCC-1 basi Tanzania itakuwa imepata jumla ya dola za Marekani trilioni 2.45 za maendeleo kutoka Marekani katika kipindi cha miaka 10 tu iliyopita. Fedha za MCC-2 zitaanza kutolewa mwakani, 2016.

  Kiasi kilichotolewa kwa Tanzania wakati wa MCC-1 ndicho kilikuwa kiasi kikubwa zaidi ambacho kimepata kutolewa na Marekani chini ya Mpango huo wa Millennium Challenge Corporation na kwa kupita MCC-2 Tanzania itakuwa ni nchi ambayo itakuwa imepata kiasi kubwa cha fedha za maendeleo chini ya MCC duniani.

  Fedha zilizotolewa chini ya MCC -1 zilitumika kujenga Barabara za Tunduma-Sumbawanga, Tanga-Horohoro na Namtumbo-Songea-Mbinga.Aidha, fedha hizo zilitumika kujenga upya mfumo wa huduma za maji kwa ajili ya miji ya Dar es Salaam na Morogoro na zilitumika kusambaza umeme katika vijiji vya mikoa 10 ya Tanzania Bara.

  Fedha hizo vile vile zilitumika kutandaza njia ya pili ya kusafirisha umeme chini ya Bahari ya Hindi kati ya Bara na Tanzania Visiwani na pia zilitumika kujenga barabara zote kuu za Kisiwa cha Pemba na baadhi ya barabara za Unguja kwa kiwango cha lami.

  Imetolewa na:
  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu,
  DAR ES SALAAM.
  27 Septemba, 2015

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na  Mtendaji Mkuu wa MCC, Bi. Dana J. Hyde katika mkutano wao uliofanyika katika Hoteli ya JW Marriot Essex House, New York
  Rais  Jakaya Mrisho Kikwete katika mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa MCC, Bi. Dana J. Hyde katika mkutano uliofanyika katika Hoteli ya JW Marriot Essex House, New York, na kuhudhuriwa na watumishi waandamizi wa MCC akiwamo Bwana Kamran Khan, Makamu wa Rais wa Operesheni za MCC.
  Rais  Jakaya Mrisho Kikwete katika mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa MCC, Bi. Dana J. Hyde katika mkutano uliofanyika katika Hoteli ya JW Marriot Essex House, New York. Picha na Freddy Maro

  0 0

  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandali ya Tamasha la kuombea Amani na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, Alex Msama akifafanua jambo Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki, wakati akimtangaza Rais Jakaya Kikwete kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo, litakalofanyika Oktoba  4  kwenye uwanja wa Taifa. Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Hamisi Pembe. (Picha na Loveness Bernard)
  RAIS wa Jamnuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha  maalumu la kuombea amani Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 25.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati inayoratibu tamasha hilo, Alex Msama alisema ni faraja kubwa kwao kuona Rais anakubali mwaliko wao wa kuwa mgeni rasmi.

  “Tumefurahi sana kuona Rais wa nchi anakubali kuwa mgeni rasmi katika tukio hilo la kuombea amani Uchaguzi Mkuu kwa manufaa ya taifa letu, sisi tukiwa waratibu wa tukio hili tumefarijika mno,” alisema Msama.

  Alisema tukio hilo litakalowaleta pamoja viongozi wa kada zote wakiwamo wale wa madhehebu na dini mbalimbali bila ubaguzi, litasindikizwa na burudabi ya nyimbo za injili kutoka kwa waimbaji wa ndani na nje ya nchi.

  Msama alisema Kamati ya maandalizi iliamua kumuomba Rais Kikwete sio tu kwa kutambua nafasi yake katika taifa, pia moyo wake wa kuhimiza amani wakati wote wa utawala wake ikiwemo kushiriki matamsha ya injili.

  Alisema, mbali ya kuwaongoza Watanzania kuombea taifa lao lipite salama katika uchaguzi mkuu, pia wadau wa muziki wa injili watalitumia tukio hilo kumuga na kumshukuru kwa mchango wake katika kukuza muziki wa injili.

  Akifafanua nafasi ya Rais Kikwete kukuza muziki huo, Msama alisema katika harakati zake za kuratibu matukio ya muziki wa injili, kiongozi huyo amewahi kuwa mgeni rasmi katika tamasha la Pasaka mwaka 2011.

  Msama alisema kitendo cha Kikwete kutokuwa mbaguzi wa dini, ndio maana Kamati ya kuratibu Tamasha la kuombea Amani Uchaguzi Mkuu imempa heshima kutokana na kuwa kielelezo cha amani na mshikamano.

  Alisema ujumbe mahususi katika Tamasha hilo ni kwamba, suala la amani na utulivu, ni jukumu la kila mmoja kwa nafasi yake kwani thamani ya tunu ya amani haiwezi kuonekana kwa wepesi hadi pale inapotoweka.

  Msama alisema Kamati yake imejitwisha jukumu hilo la kuhimiza amani katika uchaguzi mkuu kutokana na kuwepo kwa viashiria vya uvunjivu wa hiyo amani kutokana ushindani mkali uliopo katika uchaguzi wa safari hii.

  Ushindani mkali katika uchaguzi huo umetuama kati ya mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa anayeungwa mkono na vyama vinne ninavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na Dk. John Magufuli wa CCM.

  Msama alisema, baada ya uzinduzi kufanyika Uwanja wa Taifa siku hiyo ambapo kiingilio kitakuwa sh 5000; 3000 kwa wakubwa na sh 1,000 kwa watoto, tamasha hilo litaelekea katika mikoa 10 kuhamasisha amani.

  Miongoni mwa waimbaji wa kigeni waliothibitisha kushiriki na nchi zao kwenye mabano ni Solly Mahlangu na Sipho Makhabane (Afrika Kusini), Ephraem Sekereti (Zambia), Anastazia Mukabwa na Solomon Mukubwa Kenya.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Mohammed Gharib Bilal,  akisaini kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo kufuatia kifo cha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Celina Kombani kilichotoke Nchini India juzi, wakati Makamu wa Rais alipokwenda nyumbani kwa marehemu Mikocheni      Dar es salaam leo Sept 27,2015.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Mohammed Gharib Bilal,  akizungumza na Mume wa Marehemu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Celina Kombani, alipokwenda nyumbani kwa marehemu Mikocheni Dar es salaam leo Sept 27,2015 kwa ajili ya kusaini kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo na kuifariji familia ya marehemu.(Picha na OMR).
   
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Mohammed Gharib Bilal,  akifariji watoto wa Familia ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Marehemu Celina Kombani wakati alipofika nyumbani marehemu Mikocheni     Dar es salaam leo Sept 27,2015.

  0 0

  Katibu wa TUICO  Mkoa wa Mbeya Ndugu Merboth Kapinga akizungumza na wajumbe wa Tuico siku ya uchaguzi uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Otu jijini Mbeya.(JAMIIMOJABLOG)
  Wajumbe wa mkutano wakiimba wimbo wa pamoja.

  Na Emanuel Madafa,Mbeya
  CHAMA cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri Mkoa wa Mbeya, kimefanikiwa kupata viongozi wapya watakao kiongoza chama hicho katika kipindi cha miaka mitano 2015  hadi 2020.

  Uchaguzi umefanyika katika chuo cha wafanyakazi (Otu) jijini Mbeya na kuhudhuriwa na wajumbe mbalimbali kutoka Taasisi za serikali na binafsi ambao wanawakilisha chama hicho cha (Tuico) mkoa wa Mbeya.

  Akizungumzia uchaguzi huo, Katibu wa TUICO  Ndugu Merboth Kapinga, amesema uchaguzi huo umefanyika kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za chama hicho ambacho zinaeleza kuwa kila baada ya miaka mitano ni lazima chama kichague viongozi wapya.

  Amesema, wafanyakazi wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali kwenye vituo vyao vya kazi lakini matatizo hayo yanashindikana kutatuliwa kutokana na mambo madogomadogo ambayo yanahitaji kupatiwa ufumbuzi kwa pande zote mbili.

  Hata hivyo amewataka viongozi hao kujenga uwezo wa kupambana na migogoro ya kifedha kwani ndio changamoto kubwa inayowakabili wafanyaazi na waajiri.

  Aidha amesisitiza kuwa , wafanyakzi ni lazima wawajibike kwanza halafu ndio tudai haki nzetu kama vile nyongeza ya mshahara na motisha mbalimbali.

  Viongozi hao waliopatikana ni Mwenyekiti wa chama hicho, Willium Mhando pamojana na wajumbe wa kamati tendaji, Boniface Mwanyamba kutoka kampuni ya vinywaji baridi ya Pepsi , Joyce Mwakifuna kutoka kampuni ya Coca Cola kwanza.

  Wengine ni Mwanaidi Thadei na Michael Msovakumwao wajumbe kitengo cha biashara,  sekta ya fedha, Winifrida Kinyakisu na Mohamed Tangulia.

  0 0

   Mwenyekiti Mpya wa Mashindano ya Miss Tanzania Juma Pinto akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.Kushoto ni msemaji wa kamati hiyo na Miss Tanzania namba 2 mwaka 2006 Jokate Mwegelo.

  Allen Mhina Na Ally Daud – Maelezo
  KAMATI inayosimamia mashindano ya Miss Tanzania Lino International Agency imepata Mwenyekiti na wajumbe wapya watakaoandaa ,kuratibu na kusimamia mashindano ya urembo ya Miss Tanzania.

  Akiwatambulisha wajumbe hao mbele ya waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam, aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati ya Miss Tanzania iliyomaliza muda wake  Hashim Lundenga amesema  kuwa kamati  mpya ndiyo itakayowajibika na shughuli zote zilizokuwa zikifanywa na kamati ya awali.

  Amesema kamati hiyo itafanya kazi zake kwa kuzingatia sheria na vigezo vyote vya kimaadili ili kuepuka  ukiukwaji wa taratibu za mashindano hayo.

   “Hatutamvumilia mwanakamati yeyote atakayevunja miiko ya mashindano haya, sisi tutakuwa nyuma tukiangalia kwa umakini”, amesema Bw. Lundenga.

  Kwa upande wake Mwenyekiti mpya wa kamati hiyo  Juma Pinto ametoa pongezi za dhati kwa kamati iliyomaliza muda wake na kuhaidi kukubaliana na mfumo unatumika kuratibu  mashindano hayo .

  “Namshukuru  Lundenga kwa  kunikabidhi nafasi hii ya mwenyekiti wa kamati ya miss Tanzania,  naahidi kuratibu mashindano haya kwa kuzingatia vigezo na masharti yaliyowekwa ili kamati yangu iweze kukidhi haja ya mashindano haya”. Amesema.

  Naye Msemaji Mkuu wa kamati hiyo na aliyekuwa Miss Tanzania namba mbili  mwaka 2006 Jokate Mwegelo, ametoa rai kwa wasichana wa kitanzania wajitokeze kushiriki mashindano hayo kwa kuonesha vipaji walivyonavyo na kupata ajira.

  Mwishoni mwa mwaka  jana Mashindano  ya Miss Tanzania  yalikumbwa na mtafaruku wa ukiukwaji wa maadili na vigezo vya mashindano na kulazimika kusimamishwa kwa muda na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA).

  0 0

   Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Mgombea Ubunge wa jimbo la Makambako Ndugu Deo Sanga wakiwaiambisha wananchi wa Mafinga katika uwanja wa Polisi Mwembetogwa mkoani Iringa leo Septemba 27 kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Mafinga katika uwanja wa Mafinga mkoani Iringa leo Septemba 27 kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni. 
   Mmoj wa Waangalizi wa Uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu,akifuatilia mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli mjini Makambako jioni ya leo Septemba 27 mkoani Iringa
  ????????????????????????????????????
  Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mufindi Kusini Ndugu Mahmoud Mgimwa akipiga push up mbele ya wakazi wa Mafinga waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni wa kumnadi mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli  ambaye anashuhudia tukio hilo katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vyaWambi  mjini Mafinga mkoani Iringa na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi.

  Dk. John Pombe Magufuli amewaambia wakazi hao wasihadaike na maneno ya kisiasa yanayotolewa na vyama vingine kuwa nchi ya Tanzania haijapiga hatua ikiwa chini ya utawala wa CCM wakati maendeleo yanaonekana wazi na nchi inazidi kusonga mbele kwa mambo mengi ikiwemo amani na utulivu wa nchi.
   Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa  Chimala,Mbarali mkoani Mbeya alipokuwa akielekea mkoani Iringa kuendelea na kampeni zake.
   Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli akionesha hisia zake mara baada ya kuonana uso kwa uso na Waziri Mkuu Mstaafu na Kada Mkongwe wa chama cha CCM. Samwel Malecela mjini Mbarali kabla ya kuwahutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni
   Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri Mkuu Mstaafu na Kada Mkongwe wa chama cha CCM. Samwel Malecela mjini Mbarali kabla ya kuwahutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni,huku Mjumbe wa kamati kuu ya CCM Ndugu  Bulembo akifuatilia kwa makini
   Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Rujewa mjini katika viwanja vya Barafu mjini Rujewa,wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya leo Septemba 27 kwenye mkutano hadhara wa kampeni.
    Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Rujewa mjini wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya leo Septemba 27 kwenye mkutano hadhara wa kampeni.
  Mgombea Ubunge wa jimbo la Makambako Ndugu Deo Sanga a.k.a Jah People akimuombea kura  Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika mjini Ilembula leo Septemba 27 mkoni Mbeya
   Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge wa jimbo la Wanging'ombe Injinia Gerson Rwenge,katika mji wa Ilembula
   Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasili kwenye mjini Makambako kwenye uwanja wa Polisi Mwembetogwa mkoani Iringa leo Septemba 27 kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
   wakazi wa Makambako wakishangilia wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akipanda jukwaani kwa kuruka ruka kuonesha yuko fiti kuwatumikia wananchi kwa namna yoyote ile.

   Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi na Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa Ndugu Abdalah Bulembo akiwahutubia wakazi wa Makambako kwenye mkutano wa kumnadi mgombea urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli leo Septemba 27 mkoani Iringa
   Dkt Magufuli akiwasalimia wananchi wa Makambako kabla ya kuanza kuwahutubia na kuwaomba kura
   Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Makambako gombea Ubunge wa jimbo la Makambako Ndugu Deo Sanga wakiwaimbisha wananchi wa Mafinga katika uwanja wa Polisi Mwembetogwa mkoani Iringa leo Septemba 27 kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
  Wananchi wa mji wa Makambako wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akimwaga sera zake na kuwaomba wajitokeze kwa wingi siku ya kupiga kura Oktoba 25 kwa kumpiga kura ya ndio na hatimae aibuke mshindi kwa nafasi ya Urais.

  0 0

  0 0

     Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Michael Mhando akiangalia kadi za matibabu ambazo alizikabidhi kwa wasanii ambao wametimiza taratibu za kujiunga na Mfuko huo.
   Msanii Aisha Salvador akipokea kadi ya matibabu kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Michael Mhando.
     Msanii John Kitime akipokea kadi ya matibabu itakayomwezesha kupata huduma kote nchini.
    Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Rehani Athumani akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawako pichani) kuhusiana na utaratibu wa kujiunga na Mfuko huo
      Baadhi ya wasanii waliohudhuria hafla hiyo pamoja na waandishi wa habari.
  1 Bw. John Kitime akielezea jambo kwa waandishi wa habari muda mfupi baada ya kupokea kadi yake ya matibabu.

  0 0

   Mungu huyo wa mdogo wa kiume mwenye daraja kubwa anayejulikana kwa zaidi ya majina 125 (Ganpati Bappa Morya)  mwenye sura ya tembo akiwa amewekwa juu ya gari maalumu wakipita mitaa kadhaa ya jiji la Dar es Salaam leo mchana akipelekwa Baharini ili kuungana na mungu wa kike waliopo kwenye mito mitatu mikubwa mitakatifu iliyopo nchini India.
   Mungu huyo akiwa amewekwa juu ya paa la gari akiwa katika uangalizi wa heshima.
   Wanawake wa madhehebu hayo ya kihindu wakicheza wakati wa kuadhimisho siku hiyo.
   Hapa ni furaha tupu ya maadhimisho hayo.
   Hapa wazazi na watoto wakiwa kwenye maandamano hayo kuelekea baharini kumuweka ili kuungana na mungu wengine wa kike waliopo katika mito mitatu mitakatifu iliyopo nchini India.
   Maandamano yakiendelea.
  Hapa ni furaha tupu kwa wanawake, wanaume, wazee na watoto.
   Watoto wakifurahia maadhimisho hayo.
   Hapa wakiwa juu ya magari kuelekea kumsindikiza mungu wao huyo.
   Hapa wakiwa kwenye magari kuelekea baharini.
   Ni furaha tupu ndani ya gari.
  Safari ya kwenda baharini ikiendelea.

  Na Dotto Mwaibale

  WATANZANIA wenye asili ya India wa dhehebu la Hindu (Baniani), leo wameadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Mungu wa mdogo wa kiume mwenye daraja kubwa (Ganpati Bappa Morya) na mwenye sura ya tembo.

  Mungu huyo hufanyiwa sherehe baada ya kufanyika kwa ibada ya siku tisa ambapo siku yake ya kuzaliwa alipelekwa baharini kwaajili ya kuungana na Mungu wa kike walio kwenye mito mitatu mitakatifu iliyopo nchini India ambayo ni Sarasgad, Amba na Raigad.

  Sherehe hizo zilianza kwa ibada ambapo pia walitumia fursa hiyo kuiombea amani ya nchi hii katika maadhimisho ya kusheherekea siku yake ya kuzaliwa iliambatana na utoaji wa sadaka za vyakula mbalimbali na maombi hupelekwa baharini kwa ajili ya kuungana na Mungu kike.

  Katika sherehe hizo jijini hapa zilianzia katika nyumba zao za ibada ambapo kulikuwa na msafara mkubwa ambao ulihusisha na magari yaliyobeba Mungu huyo huku wanawake wakijipamba kwa mavazi mazuri huku wakitembea na kucheza kwa furaha kumsindikiza wakipita barabara kadhaa za katikati ya jiji la Dar es Salaam zikiwemo za Azikiwe na Kivukoni hadi Baharini.

  Baada ya kufanyika kwa sherehe hizo pia baada ya miezi miwili kutakuwa na maadhimisho ya mwaka mpya ambao ni Diwali ambapo mwaka ujao wataadhimisha tena sherehe hizo.

  Mungu huyo ambaye pia hujulikana kwa majina zaidi ya 125 na ndiye Mungu mdogo na mwenye daraja kubwa zaidi.Baadhi ya majina hayo ni Ganesh Chaturthi, Vinayaka Chaturthi

  Inaaminika kuwa unapoomba kitu chochote kutoka kwake unafanikiwa. Ambapo mungu huyo ambaye ni mwanaume aliyetengenezwa kwa aina ya udongo maalumu huyeyuka anapowekwa baharini ikiwa na maana ya kwenda kuungana na Mungu wa kike waliokatika mito hiyo.

  0 0

  D3A_5097
  Mkurugenzi M-Net Kanda ya Afrika Magharibi, Wangi Mba-Uzoukwu akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kutoka nchi za Afrika waliokusanyika kwenye jukwaa kubwa la kuonesha vitu mbalimbali vinavyoburudisha katika chaneli za DStv na GoTv kupitia MultiChoice hivi karibuni nchini Mauritius.
  D3A_5116
  Mkurugenzi wa M-Net kwa nchi za Afrika Mashariki na SADC, Theo Erasmus akifurahi jambo kwenye mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) kutoka nchi mbalimbali za Afrika.

  Na Modewjiblog, Mauritius
  Moja ya makampuni yanayoongoza katika utoaji wa vipindi vya burudani barani Afrika M-Net imesema kwamba itazindua chaneli maalumu kwa ajiri ya wakazi wa Tanzania itakayojulikana kama maisha Magic Bongo.
  MAISHA MAGIC BONGO itaruka hewani kupitia chaneli 160 ya DStv kuanzia Alhamisi ya Oktoba Mosi mwaka huu na itapatikana katika vifurushi vyote vya Access, Family, Compact, Compact Plus na Premium.

  Imeelezwa kuwa ingawa mambo yametengenezwa mahsusi kwa ajili ya Watanzania mataifa jirani yaAfrika Mashariki ikiwamo Kenya, Uganda, Ethiopia na DRC wanaweza kuona.

  Uamuzi huo wa M-Net umefanyika wakati mchakato unaendelea wa kuboresha zaidi ulaji kwa wateja wake.

  Hata hivyo wamesema kwamba MAISHA MAGIC EAST ambayo kwa sasa inaruka kupitia chaneli 158 itajiimarisha zaidi katika soko la Kenya huku ikiendelea na mara moja kwa wiki kwa ajili ya soko la Uganda ndani ya Luganda.

  D8A_1979
  Pichani ni waandishi wa habari kutoka nchi mbalimbali za Afrika waliokusanyika kwenye jukwaa hilo lililoandaliwa na MultiChoice Africa hivi karibuni.

  MAISHA MAGIC BONGO imelenga kuhudumia soko la Tanzania likionesha vipindi vya Kiswahili kwa ajili ya kutimiza pia lengo la taasisi la kuhudumia soko kwa kuangalia makundi.

  Mkurugenzi wa M-Net kwa nchi za Afrika Mashariki na SADC, Theo Erasmus amesema ingawa kwa miaka mingi wamekuwa wakitoa vipindi vyenye lugha mchanganyiko kwa sasa wamepania kutoa vipindi kwa lugha ya eneo kutokana na soko kuruhusu.

  “Tumefanya mabadiliko kwa nchi za Afrika Mashariki kwa siku za karibuni. Kasi ya mabadiliko hayo yanaonesha kujali kwetu. Na tutaangalia mafanikio katika MAISHA MAGIC BONGO, kuona uwezekano wa kuendelea kutengeneza chaneli zinazokidhi mahitaji Fulani.” Amesema Erasmus.

  Chaneli mpya itakuwa na matangazo ya saa sita ambayo yatarejewa mara tatu kwa siku na inatarajiwa saa za vipindi kuongezeka zaidi.

  Katika chaneli hiyo kutakuwa na kipindi cha saa moja cha muziki Mzooka, ambayo itakuwa mwishoni mwa wiki majira ya jioni na itakuwa kipindi cha miziki ya karibuni kutoka Tanzania. Kitakuwa ni kipindi cha wapenzi wa hip hop na Bongo.
  D3B_8767
  Mkurugenzi M-Net Kanda ya Afrika Magharibi, Wangi Mba-Uzoukwu (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Movie Stars wa nchini Nigeria, Rita Dominic na Desmond Elliot mara baada ya mkutano na waandishi wa habari.
  Pia kutakuwa na michezo ya kuigiza ambayo ni tamthilia Talaaka itakayokuwa ikizungumzia masuala ya ndoa na talaka na kupeleka ujumbe kwanini kunakuwa na talaka. Pia kutakuwa na kipindi cha mapishi cha Jikoni na Marion. Kwenye kipindi hiki tutawaona masupastaa wa Tanzania wakipika chakula huku wakizungumzia mambo yao.
  MAISHA MAGIC BONGO kutakuwa na sinema za Kiswahili kama Nusra iliyochezwa na Ashura Iddy, Ammar Ruweth, Riyama Ally na Zuberi Mohammed. Pia kutakuwa na sinema ya Hard Price iliyochezwa na akina Sabrina Tamim na Jacqueline Wolper .
  Ikiwa imebaki mwezi mzima kabla ya MAISHA MAGIC BONGO kuingia katika runinga za watanzania kwa sasa angalia kipindi gani kipo hewani ukipendacho kupitia www.dstv.com.
  D3A_5080
  Mkuu wa chaneli ya Maisha Magic, Margaret Mathore akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).

  0 0

  1.     Viko Mbweni  usalama  wa  taifa, vina  hati miliki, viko  karibu na  barabara  ya  lami na viko  karibu  na  beach,  vipo  Sqm  600 – 1500, bei  ni  kuanzia  milioni 35 mpaka  45.

  2.     Nyumba 3 zinauzwa, zipo Mwananyamala “A”, moja vyumba 12, nyingine vyumba  6 na  nyingine vyumba 4. Zote  zina  leseni  ya  makazi, gari  mpaka mlangoni, umeme  upo. Kila  moja  bei  milioni 65.

  3.     Nyumba yenye geti  la  gari, vyumba 4, kimoja master, umeme, sebule, dining, jiko, stoo, na  hati miliki inauzwa. Ipo Mbagala  Kuu, bei  milioni  65.

  4.     Pia  nyumba  za  milioni 65 – 70  zipo  Mbweni  na  boko.
  Mawasiliano  0784482959.

  0 0

  IMG_2370
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza wakati akizindua Malengo Endelevu 17 ya Maendeleonchini (SDG’s) Tanzania katika shule ya Uhuru mchanganyiko, katika hafla ambayo pia benki ya Standard Chartered Tanzania ilishiriki na kugawa vitu mbalimbali kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo. (Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, amesema uondoaji umaskini nchini unawezekana kwa ushirikiano kati ya wadau mbalimbali wa maendeleo.Kauli hiyo ameitoa mwishoni mwa wiki wakati akizindua Malengo Endelevu 17 ya Maendeleo nchini (SDG’s) Tanzania katika shule ya Uhuru mchanganyiko, katika hafla ambayo pia benki ya Standard Chartered ilishiriki na kugawa vitu mbalimbali kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo.

  Katika hafla hiyo ambayo ilitengenezwa mahususi kuanzisha utekelezaji wa Malengo Endelevu (SDG’s) yakiwemo ya elimu, afya na mazingira Standard walipeleka miti 150 ya kupanda, kompyuta na pia kutumia muda kuangalia afya za wanafunzi.

  Alisema katika kukabiliana na umaskini kwa kuangalia Maendeleo Endelevu hakuna kitu kigumu ukilinganisha na ugumu wa mwanafunzi asiyeona kujifunza kwa kupitia vitabu vya nukta nundu na asiyesikia kuwasiliana na mtu mwingine lakini pamoja na ugumu huo watoto hao wanaweza.

  Alisema kwa ushirikiano wa wadau kama walivyofanya wao na benki ya Standard Chartered Tanzania anaamini kwamba maendeleo yatafikiwa na Tanzania itafanikiwa kuzika umaskini ifikapo mwaka 2030.Alisema kutiwa saini kwa Malengo Endelevu na viongozi wa nchi 190 kumeonesha wazi nia ya seriakli mbalimbali duniani kushughulikia umaskini na kuuzika kwa kutekeleza malengo hayo endelevu.

  IMG_2313
  Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole akitoa salamu za Mkurugenzi wake ambapo benki hiyo imeahidi kushiriki kikamilifu katika kuhakikisha utekelezaji wa malengo mapya ya Maendeleo Endelevu (SDG's) yanafanikiwa nchini Tanzania. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu (kulia) pamoja na Mkuu wa Mahusiano wa benki ya Standard Chartered Tanzania, Juanita Mramba (wa pili kulia).
  Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole, alisema kwamba ni lengo la benki hiyo ni kurejesha faida kwa jamii kupitia miradi yake mbalimbali na kwamba kusaidia shule hiyo ya Uhuru mchanganyiko iliyoanzishwa 01-01-1921 awali ikiitwa Government African secondary school kabla ya kuhamishiwa Mzumbe Morogoro 01-01-1953 na kubadilishwa jina kuwa Kichwele African boys middle school ikiwa na madarasa ya V-VII, ni sehemu ya kurejesha faida kwa jamii.
  Alisema ni lengo la benki hiyo kwa mwaka huu kuwezesha kupatikana kwa dola za Marekani milioni 5 kusaidia mambo mbalimbali ya watoto kwa mwaka huu kwa nchi za Afrika mashariki huku Tanzania pekee watoto milioni 10 wakifikiwa.
  Benki hiyo yenye matawi Dar es salaam, Mwanza na Arusha katika miradi yake ya afya, vijana na elimu wamekusudia kushirikiana na Umoja wa Mataifa kutekeleza malengo mbalimbali endelevu ikiamini kwamba jamii ikiboreshwa itakuwa katika mfumo mzuri wa maendeleo na kupiga vita umaskini.
  Malengo ya SDG’s yamepangwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka 15.
  IMG_2324
  Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Uhuru mchangayiko, Anna Mshana akitoa risala fupi ya shule yake sambamba na changamoto zinazoikabili shule yake kwa ugeni huo kutoka Umoja wa Mataifa na Benki ya Standard Chartered Tanzania.
  Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Anna Mshana alisema shule hiyo ambayo ilianzisha kitengo cha wanafunzi wasioona 1962 na kubadilishwa kuwa Shule ya msingi Uhuru mchanganyiko mwaka 1964, inakabiliwa na changamoto mbalimbali.
  Miongoni mwa matatizo ni miundombinu ya shule hiyo isiyokidhi mahitaji halisi, ukosefu wa ukuta, mashine za kufundishia watoto wasioona, upungufu wa mabweni, magodoro, vitanda na gari la kuwakimbiza hospitalini inapotokea dharura.
  Alisema ingawa kuna taasisi hutoa msaada wa gari na matibabu kwa watoto mchana, lakini nyakati za usiku kukitokea dhararu inabidi shule igharamie ingawaje wakati mwingine hatuna fedha inakuwa ni changamoto kwetu.
  Alisema Shule ya msingi Uhuru mchanganyiko yenye kutoa elimu jumuishi ina vitengo vya ufundi seremala (1975) wanafunzi wenye mahitaji maalumu ulemavu wa akili (1984) na viziwi na wasioona (Deafblidn) kilichoanzishwa mwaka 1994.
  IMG_2346
  Wanafunzi ambao ni viziwi nao walipata fursa ya kuja kila kinachoendelea kutoka kwa mkalimani wao.
  IMG_2470
  Mkuu wa Mahusiano wa benki ya Standard Chartered Tanzania, Juanita Mramba akitangaza wanafunzi 17 ambao walishiriki shindano la kuhifadhi malengo mapya ya Maendeleo Endelevu (SDG's) wakati wa kukabidhi zawadi kwa wanafunzi hao wa shule ya Uhuru mchanganyiko.
  IMG_2480
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akikabidhi zawadi zilizotolewa na Benki ya Standard Chartered Tanzania kwa wanafunzi hao, sambamba na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole.
  IMG_2428
  Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko, Anna Mshana (wa pili kushoto) moja kati ya kompyuta tano zilizolotolewa na Benki hiyo ikiwa ni kama ishara ya utekelezaji wa lengo namba nne “Quality Education” wakati wa uzinduzi wa Malengo mapya ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) uliofanywa na Benki ya Standard Chartered Tanzania kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa katika shule ya msingi Uhuru mchanganyiko jijini Dar mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya Shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko, Bw. Abubakar Mwambungu wakishuhudia tukio hilo.
  IMG_2407
  Kompyuta tano zilizotolewa na Benki ya Standard Chartered Tanzania kwa shule ya Uhuru mchanganyiko.
  IMG_2448
  Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole (wa tatu kushoto), Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati), Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Uhuru Mchangayiko, Anna Mshana (wa pili kushoto), Mjumbe wa bodi ya kamati ya Shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko, Abubakari Mwambungu (kushoto) pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania katika picha ya pamoja huku wakiwa wameshikilia miche ya miti mbalimbali ikiwemo ya matunda ambapo zaidi ya miche 150 ya miti ilipandwa kuzunguka mazingira ya shule hiyo kulinda mazingira ikiwa ni ishara kwa vitendo ya utekelezaji wa lengo namba 13 "Climate Action" kati ya Malengo 17 mapya ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) nchini Tanzania.
  IMG_2338
  Pichani juu na chini baadhi ya wanafunzi na walimu wa shule ya msingi Uhuru mchanganyiko waliohudhuria uzinduzi huo.
  IMG_2393
  IMG_2541
  Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole sambamba na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakishiriki zoezi la upandaji miti kuzunguka maeneo ya shule ya Uhuru mchanganyiko jijini Dar mwishoni mwa wiki.
  IMG_2563
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akishiriki zoezi la upandaji miti sambamba na baadhi ya wanafunzi wa shule Uhuru mchanganyiko.
  IMG_1924
  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchangayiko, Anna Mshana akitoa maelezo kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (aliyeinama) na Mkuu wa Mahusiano wa benki ya Standard Chartered Tanzania, Juanita Mramba (kulia) walipotembelea darasa la awali la watoto wenye ulemavu wa macho (upofu) katika shule hiyo. Nyuma ya Mwalimu Mkuu ni Mjumbe wa Kamati ya Shule ya Msingi Uhuru Mchangayiko, Abubakar Mwambungu.
  IMG_1942
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akicheza na mtoto Fatuma Haji wa darasa la awali katika shule hiyo ambaye ni mlemavu wa macho alipotembelea darasa hilo kabla ya kuzindua wa Malengo mapya ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) hafla iliyoandaliwa na Benki ya Standard Chartered Tanzania kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa katika shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko jijini Dar mwishoni mwa wiki.
  IMG_2032
  Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, Mkuu wa Mahusiano wa benki ya Standard Chartered Tanzania, Juanita Mramba pamoja na ujumbe wao katika nyuso za masikitiko walipotembelea darasa la watoto wenye ulamavu wa macho (vipofu) na matatizo ya kutosikia (viziwi) katika shule ya msingi Uhuru mchanganyiko.
  IMG_2075
  Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, Mkuu wa Mahusiano wa benki ya Standard Chartered Tanzania, Juanita Mramba na ujumbe wao katika picha ya pamoja na wanafunzi ambao ni walemavu wa macho ambao pia ni viziwi katika shule ya msingi Uhuru mchanganyiko.
  IMG_1995
  Walimu wa darasa la watoto wenye ulemavu wa macho ambao ni viziwi wakicheza ngoma na wanafunzi wao.
  IMG_2082
  Maana ya ulemavu wa macho na kuwa kiziwi.
  IMG_1844
  Mkutubi wa maktaba ya shule ya Uhuru mchanganyiko, Masanja akitoa maelezo ya namna mashine za kukuzia maandishi kwa wale wanafunzi wenye uono hafifu katika shule hiyo kwa Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole (kushoto) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez walipotembelea maktaba hiyo.
  IMG_1833
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akipitia Katiba maalum kwa watu wenye ulemavu wa macho iliyopo kwenye maktaba ya shule hiyo. Kushoto kwake ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole.
  IMG_2119
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Ujumbe wa Benki ya Standard Chartered Tanzania ulioongozwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole wakitembelea mambweni ya wanafunzi katika shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko.
  IMG_2696
  Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko.
  IMG_2723
  Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole (kulia) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Uhuru mchanganyiko Issa Abasi Wenge w darasa la pili (wa pili kushoto) mlemavu wa ngozi na Fatuma Haji (wa pili kulia) wa shule ya awali mwenye ulemavu wa macho.
  IMG_2742
  Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole (kulia) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Mwanafunzi Mariana Alex (Mariana the voice of the SDGs in TZ) wa darasa la tano katika shule ya msingi Uhuru mchanganyiko jijini Dar. about the
  IMG_2672
  Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu akiserebuka na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Uhuru mchangayiko.
  IMG_2264
  Bango lililoorodhesha Malengo 17 mapya ya Maendeleo Endelevu (SDG’s).
  IMG_2874
  Siku ilimazika kwa mechi ya kirafiki baina ya Shule ya msingi Uhuru mchanganyiko na wafanyakazi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania katika viwanja vya shule ya sekondari Benjamin Mkapa ambayo ilizinduliwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole (kulia) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.

  0 0

  Eng.Philbert Rweyemamu akifafanua jambo katika moja ya mabanda ya maonyesho kwa baadhi ya maafisa wa uhamiaji walipokuwa wakitembelea mabanda ya maonyesho.
  Eng.Philbert Rweyemamu akifafanua jambo katika moja ya mabanda ya maonyesho.
  Wageni wakijionea namna mradi wa matofali ya gharama nafuu ulivyowanufaisha wenyeji wanaozunguka mgodi wa Buzwagi.
  Wageni wakipata maelezo kutoka kwa wataalamu wa kampuni ya KALTIRE ambayo imekuwa ikihudumia mgodi wa Buzwagi kwa kuwauzia matairi kwa ajili ya mitambo ya uchimbaji mgodini hapo.
  Wageni pamoja na baadhi ya maafisa wa mgodi wa Buzwagi na wale wa serikalini wakijionea matairi makubwa yanayotumika katika mgodi huo.
  Wageni wakipata maelezo wakati walipotembelea banda la PANAF
  Sehemu ya familia za wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi wakiwa wameketi baada ya kutembelea mabanda mbalimbali
  Kama vile hawaamini!!!! Ni kweli anacheza na nyoka hivyo?
  Kuhakikisha kumbukumbu hii haipotei kamera za simu zikafanya kazi yake
  Kikundi hiki cha Ngoma kutoka Shinyanga kilitia fola kwa burudani safi ya Ngoma waliyoitoa.
  Baadhi ya maafisa wakuu wa kampuni ya Acacia wakifuatilia burudani ya ngoma
  Michel Ash-Afisa Mkuu wa Masuala ya uendeshaji wa kampuni ya Acacia akizungumza na familia pamoja na wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi
  Baadhi ya maafisa wa idara ya ufanisi wa Mgodi wa Buzwagi wakiwa katika picha ya pamoja katika banda lao wakati wa maonyesho
  Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi mwenye shati la bluu akiongozwa na mkuu wa kitengo cha ulinzi Jamal Rwambol kutembelea mabanda ya maonyesho
  Azael Kitange-Mkufunzi wa idara ya ufanisi wa kampuni akitoa maelezo kwa wageni walipotembelea banda la idara ya Ufanisi katika kitengo cha Mafunzo.
  Ufugali wa nyuki wa kisasa ni moja kati ya shughuli zinazofanywa na mgodi wa Buzwagi kupitia idara ya Mahusiano ya Jamii kwa kuwawezesha wenyeji wanaozunguka maeneo ya mgodi kujipatia shughuli zinazowaongezea kipato.
  Wataalamu wa idara ya afya wakionyesha baadhi ya vifaa mbalimbali vinavyotumika kupima afya za wafanyakazi wakati wote ili kuhakikisha afya za wafanyakazi wa mgodi huo muda wote zinakuwa salama.
  Wataalamu wa miamba wakionyesha aina mbalimbali za miamba yenye dhahabu na namna wanavyotumia vifaa vya kisasa kuitafuta dhahabu.
  Kikundi cha Ngoma cha kabila la wasukuma kikitoa burudani ya ngoma wakati wa maadhimisho ya siku ya familia kwa wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi
  Baadhi ya wanafamilia wa wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi.
  Baadhi ya maafisa kutoka Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu wakifurahia moja ya burudani wakati wa sherehe hizo.
  Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Eng. Philbert Rweyemamu (katikati) na Meneja wa Biashara wa Mgodi huo wakifuatilia kwa makini burudani zilizokuwa zikiendelea wakati wa sherehe hizo, kushoto kwao ni mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Kahama.

  Meneja Ufanisi wa Mgodi wa Buzwagi Bwana Saimon Sanga akizungumza na wafanyakazi wa Mgodi huo wakati alipokuwa akimkaribisha meneja Mkuu wa mgodi wa Buzwagi.
  Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Eng.Philbert Rweyemamu akizungumza na wafanyakazi wa Mgodi huo pamoja na familia zao wakati wa sherehe za siku ya familia.
  Watoto wakishiriki michezo mbalimbali iliyokuwepo maalum kwa ajili yao
  Watoto wakishiriki michezo wakati wa sherehe hizo.

  Graham Crew-Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu (kushoto) akiteta jambo na Michelle Ash-Afisa Mkuu wa masuala ya uendeshaji wa kampuni ya Acacia wakati wa sherehe hiyo
  Mtaalamu wa masuala ya uchimbaji wa Mgodi wa Buzwagi akitoa maelezo kwa wageni waliotembelea banda la idara yake.
  Mmoja wa wafanyakazi wa wa Idara ya masuala ya usalama wa Mgodi wa Buzwagi akitoa maelezo kwa baadhi ya familia za watumishi wa mgodi huo wakati walipo tembelea banda maalum la maonyesho la idara ya usalama mgodini.
  Mmoja wa wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi Bwana Moses Msofe akiwa na familia yake kusherekea siku ya familia
  Wazazi wakiwasimamia watoto wao walipokuwa wakishiriki michezo mbalimbali ya watoto.
  Watoto wa baadhi ya wafanyakazi wa Mgodi huo wakifurahia michezo mbalimbali wakati walipokuwa wakiadhimisha siku ya familia mgodini hapo
  Baadhi ya ndugu wa wafanyakazi wa Mgodi wa Buzwagi wakiangalia aina mbalimbali za mashine zinazotumika katika shughuli za uchimbaji katika mgodi huo.
  Moja kati ya magari makubwa kabisa yanayotumika katika mgodi huo likiwa katika eneo la maonyesho.
  Kutoka kushoto ni meneja wa uendelezaji wa Mgodi wa Buzwagi George Mkanda, katikati ni Graham Crew-Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu na  Michelle Ash-Afisa Mkuu wa masuala ya uendeshaji wa kampuni ya Acacia wakati wa sherehe za siku ya familia ya Mgodi wa Buzwagi.
  Baadhi ya familia za watumishi wa Mgodi wa Buzwagi zikitambulishwa wakati wa hafla hiyo.
  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii aliyekuwa Kahama.
  BUZWAGI imeanzisha mkakati wa kukuza na kuboresha hali ya utendaji kazi kwa wafanyakazi wake kwa kuanzisha utaratibu wa kuwakutanisha wafanyakazi wa mgodi huo na familia zao mara moja kwa mwaka katika siku maalumu ya familia ambayo hutoa fursa kwa familia za wafanyakazi wa mgodi huo kuweza kujionea namna ambavyo shughuli za uchimbaji wa madini hufanyika na hivyo kuwa mabalozi wazuri wa kampuni kwa ujumla.
  Mwaka huu wafanyakazi wa kampuni hiyo wamepata fursa ya kukutana na kujionea shughuli mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanyika mgodi hapo. Pamoja na mambo mengine wafanyakazi hao pia walipata fursa ya kutembelea eneo ambapo shughuli za uchimbaji zinafanyika.
  Sherehe hizo zilihudhuliwa na Afisa mkuu wa masuala ya uendeshaji  Michelle Ash, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulur-Graham Crew na meneja mkuu wa masuala ya ufanisi wa kampuni Janet Ruben pamoja na meneja mahusiano na mawasiliano wa Acacia Nector Foya, pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali..

  0 0

   Mkurugenzi mkuu wa Airtel Tanzania Sunil Colaso akiangalia bidhaa aliyopokea kutoka kwa Marius Mutashobelwa  mkazi wa Mbeya, ambaye ni miongoni mwa vijana waliowezeshwa na Airtel FURSA walipotembelea ofisi za Airtel jijini Dar es Salaam na kupata mafunzo ya kuendeleza biashara zao mwishoni mwa wiki hii.
   Mkurugenzi mkuu wa Airtel Tanzania Sunil Colaso akisalimiana na vijana waliowezeshwa na Airtel Kupitia mradi wake wa Airtel Fursa walipotembelea ofisi za Airtel jijini Dar es Salaam na kupata mafunzo ya kuendeleza biashara zao mwishoni mwa wiki hii.
   Mhandisi wa Airtel Gabriel Mshiu akiongea na vijana 13 waliowezeshwa na Airtel kupitia mradi wake wa Airtel FURSA walipotembelea ofisi za Airtel jijini Dar es Salaam na kupata mafunzo ya kuendeleza biashara zao mwishoni mwa wiki hii.
    Mkurugenzi mkuu wa Airtel Tanzania Sunil Colaso akiongea na vijana 13 waliowezeshwa na Airtel kupitia mradi wake wa Airtel FURSA walipotembelea ofisi za Airtel jijini Dar es Salaam na kupata mafunzo ya kuendeleza biashara zao mwishoni mwa wiki hii.Akishuhudia ni Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Beatrice Singano (katikati) and  (kushoto) Meneja huduma kwa jamii Hawa Bayumi.

  KAMPUNI  ya simu za mikononi ya Airtel kwa kupitia mradi wake wa  Airtel FURSA imewakaribisha vijana wajasiriamali 13 katika Makao makuu yake yaliyopo Morocco na kujifunza uendeshwaji wa shughuli zake na kupatiwa mafunzo zaidi ya kibiashara kwa muda wa siku tatu mwishoni mwa wiki iliyopita.

  Meneja uhusiana na huduma kwa jamii  wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi akizungumzia hilo alisema, “Airtel kwa kupitia mradi wake wa Airtel FURSA imeendelea kuwa mstari wa mbele kushirikiana na vijana katika kutatua changamoto wanazozipata katika kujikwamua kiuchumi.

  Alisema, “Tunayofuraha kuwakaribisha vijana wetu 13 tuliowawezesha katika biashara zao nakujikwamuakiuchumi kwa kuwapa nyenzo za kisasa zinazosaidia kukuza biashara zao na kujiongezea mapato.

   Pia ndani ya siku tatu wameweza kupatiwa mafunzo zaidi yatakayo wafanya waweze kuendesha biashara zao kwa njia ya kisasa na kuona ni jinsi gani wanaweza kuboresha biashara zao”
  Pia walifanikiwa kukutana na Meneja wa Airtel Tanzania Bwana. Sunil Colaso na kumuelezea mafanikio waliyopata katokana na kuwezeshwa na Airtel FURSA.

  Bwana Sunil Colaso aliwaasa kutumia nafasi waliopata kujiendeleza katika biashara zao na Airtel iko pamoja na vijana ili kuhakikisha malengo yao yanatimia.

  Iddi Chilumba mwakilishi wa vijana hao alisema, “Airtel FURSA ilinikuta nikiwa na nauwezo wa kubanjua korosho chache kutokana na vifaa duni, ila toka nimewezeshwa kwa mashine za kisasa na usafiri, sasa nabanjua korosho nyingi na kusafirisha kwenye masoko mbalimbali kwa haraka Zaidi. 

  Nawashukuru sana Airtel kwa fursa walionipa na nawahasa vijana wenzangu wajishughulishe kuliko kukaa kijiweni na kujishughulisha na vitendo viovu”.

  “Tunafurahishwa sana na juhudi zinazofanywa na vijana za kujitafutia maendeleo kwa njia zilizo halali na tuko tayari kushirikiana nanyi katika kutatua changamoto mnazozipata kwa kupitia mradi wa Airtel FURSA” alisema bwana Sunil Colaso. 

  0 0

   Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya  (NHIF) Bwana Michael Mhando akizungumza na wafanyabiashara   wa wasamaki katika Soko la  feri  hawapo pichani juu ya vikundi  vya    wajasiliamali wadogo na wakubwa  kujiunga na  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
   Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya  (NHIF) Bwana Michael Mhando  akimkabidhi kadi ya uanachama ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya  (NHIF)  Mvuvi wa Samaki wa Soko Kuu la Feri Bwana Mohamed Ally Masoud mwishoni mwa wiki Jijini Dara es Salaam.
   Afisa Elimu kwa Umma wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya  (NHIF) Grace Michael akotowa eli kwa wavuvi  jinsi ya na kujiunga na mfuko huo
  04.Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii  Eugen Mikongoti akimffanulia jambo Mvuvi wa samko katika soko Kuu la samaki Fer leo jijini Dar es Salaam.

  Maofisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakiendelea kueli misha leo jijini Dar es Salaam.
  Picha na Emmanuel Massaka  ) 

  MFUKO  wa Taifa wa Bima ya Afya  NHIF leo umekabidhi bima ya Afya kwa Wavi wadogowadogo (UWAWADA) wa mkoa wa Dar es Salaam,na Kaimu Mkurugenzi  wa mfuko huo,Michael Mhando .

  Mhando amekabidhi Bima hizo leo kwenye soko kuu la kuuzia samaki Jijini Dar es Salaam maarufu ‘soko la feri’ ambapo awali ua kukabidhi bima hizo alisema kuwa anawapongeza wanachama wote wa uwawada waliojikusanya kwa vikundi vya watu kumi na kuhitaji siku ya leo kukabidhiwa Bima zao za NHIF kwa wanachama 10 waliojiunga na mfuko huo.

  Alisema wanachama hao baada ya kukaa na kusikiliza huduma zinazotolewa na shirika hilo, namna ambavyo wamefanikiwa kufikia hatua hiyo ya kukabidhiwa bima zao kupitia mpango wa KIKOA ambao unawalenga hasa wajasiliamali wadogowadogo.

  Aidha alisema kuwa vikundi husika kujiunga na mfuko huo ,hunufaika  na mafao ya matibabu sawa  na wanachama  wanaochangia kupitia mishahara yao ya kila mwezi.

  Mhando alisisitiza kuwa lengo kubwa la mpango wa Mfuko wa Taifa wa Biama ya Afya ni kuyafikia makundi yote ya wajasiliamali wadogo na wakubwa ili kuwajumuisha katika mpango huo.

  ”Lengo letu kubwa la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ni kuyafikia makundi yote ya wajasiliamali wadogo na wakubwa ili kuweza kuwajumuisha katika mpango huu”alisema Mhando.

  0 0

  Afisa utafiti na maelezo wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Sengiyumva Gasirigwa(wa kwanza kushoto) akitoa ufafanuzi alipokuwa anafungua mkutano huo kwa waandishi wa habari na wageni waalikwa kutoka kwenye taasisi mbalimbali za Serikali kwenye siku ya kimataifa ya haki ya kupata taarifa ambayo uadhimishwa Septemba 28 kwa kila mwaka.
  Mwenyekiti msaidi wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Andrew Marawiti (kulia) akizungumza jambo mbele ya waandishi wa habari(hawapo pichani) kwenye siku ya kimataifa ya haki za kupata taarifa inayoadhimishwa Septemba 28 kwa kila mwaka na kushoto ni   Mwenyekiti  wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege.
    Mwenyekiti  wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege akizungumza na wageni waalikwa pamoja na waandishi wa habari waliofika kwenye mkutano wao uliofanyika leo kwenye ofisi za MISA Tanzania  zilizopo eneo la Kinondoni Mkwajuni jijini Dar es Salaam  kushoto ni Ofisa Habari Umoja wa Mataifa (UN), Bi. Usia Nkhoma Ledama.
  Mwenyekiti  wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege (katikati) akikata utepe wakati wa uzinduzi rasmi wa chapicho la ripoti ya matumizi bora ya utoaji wa habari katika sekta za umma hapa nchini akisaidiwa na Ofisa Habari Umoja wa Mataifa (UN), Bi. Usia Nkhoma Ledama (kushoto) pamoja na Mwenyekiti msaidi wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Andrew Marawiti (kulia) 
  Waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa(hawapo pichani) wakioneshwa kitabu cha ripoti ya haki ya kupata taarifa halali katika sekta za umma kwa mwaka 2015 kilichozinduliwa leo siku ya kupata habari iliyofanyika kwenye ofisi za MISA Tanzania.
   Mwenyekiti wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege akionesha tuzo ya cheti cha kufuri la Dhahabu kwa kubana sana taarifa kwa mwaka 2015 kwa umma iliyokwenda kwenye Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
  Mwenyekiti wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege(kulia) akimkabidhi Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Anthony Ishengoma tuzo ya cheti cha kufuri la Dhahabu kwa wizara hiyo kwa kubana sana taarifa kwa umma mwaka 2015.
     Mwenyekiti wa Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika) Bwana Simon Berege(kulia) akimkabidhi tuzo ya cheti cha funguo la Dhahabu walioibuka washindi wa mwaka 2015 Kaimu Mkuu wa Mawasiliano wa Huduma kwa Jamii wa NHC Bw. Muungano Saguya kwa kutoa taarifa kwa uwazi kwa umma.
  Mkuu wa Habari na Mawasiliano kutoka Idara ya Mahakama, Nurdin Ndimbe akitolea ufafanuzi wa hatua walizozichukua baada ya mwaka jana kuchukua Kofuri la Dhahabu kwa kutotoa taarifa kwa umma
  Mkurugenzi wa Shughuli za Takiwimu ofisi ya Taifa ya Takimu Bi. Aldegunda Komba akizungumza jambo baada ya ofisi yao kuibuka washindi wa kwanza kwa mwaka jana

  Waandishi wa Habari pamoja na wageni waalikwa wakifuatilia mkutano huo

  Mkutano ukiendelea  0 0

  IMG_2370
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza wakati akizindua Malengo Endelevu 17 ya Maendeleo nchini (SDG’s) Tanzania katika  shule ya Uhuru mchanganyiko, katika hafla ambayo pia benki ya Standard Chartered Tanzania ilishiriki na kugawa vitu mbalimbali kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo. (Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

  Na Mwandishi wetu
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, amesema uondoaji umaskini nchini unawezekana kwa ushirikiano kati ya wadau mbalimbali wa maendeleo.

  Kauli hiyo ameitoa mwishoni mwa wiki wakati akizindua Malengo Endelevu 17 ya Maendeleo nchini (SDG’s) Tanzania katika shule ya Uhuru mchanganyiko, katika hafla ambayo pia benki ya Standard Chartered ilishiriki na kugawa vitu mbalimbali kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo.

  Katika hafla hiyo ambayo ilitengenezwa mahususi kuanzisha utekelezaji wa Malengo Endelevu (SDG’s) yakiwemo ya elimu, afya na mazingira Standard walipeleka miti 150 ya kupanda, kompyuta na pia kutumia muda kuangalia afya za wanafunzi.

  Alisema katika kukabiliana na umaskini kwa kuangalia Maendeleo Endelevu hakuna kitu kigumu ukilinganisha na ugumu wa mwanafunzi asiyeona kujifunza kwa kupitia vitabu vya nukta nundu na asiyesikia kuwasiliana na mtu mwingine lakini pamoja na ugumu huo watoto hao wanaweza.

  Alisema kwa ushirikiano wa wadau kama walivyofanya wao na benki ya Standard Chartered Tanzania anaamini kwamba maendeleo yatafikiwa na Tanzania itafanikiwa kuzika umaskini ifikapo mwaka 2030.
  Alisema kutiwa saini kwa Malengo Endelevu na viongozi wa nchi 190 kumeonesha wazi nia ya seriakli mbalimbali duniani kushughulikia umaskini na kuuzika kwa kutekeleza malengo hayo endelevu.
  IMG_2313
  Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole akitoa salamu za Mkurugenzi wake ambapo benki hiyo imeahidi kushiriki kikamilifu katika kuhakikisha utekelezaji wa malengo mapya ya Maendeleo Endelevu (SDG's) yanafanikiwa nchini Tanzania. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu (kulia) pamoja na Mkuu wa Mahusiano wa benki ya Standard Chartered Tanzania, Juanita Mramba (wa pili kulia).

  Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole, alisema kwamba ni lengo la benki hiyo ni kurejesha faida kwa jamii kupitia miradi yake mbalimbali na kwamba kusaidia shule hiyo ya Uhuru mchanganyiko iliyoanzishwa 01-01-1921 awali ikiitwa Government African secondary school kabla ya kuhamishiwa Mzumbe Morogoro 01-01-1953 na kubadilishwa jina kuwa Kichwele African boys middle school ikiwa na madarasa ya V-VII, ni sehemu ya kurejesha faida kwa jamii.
  Alisema ni lengo la benki hiyo kwa mwaka huu kuwezesha kupatikana kwa dola za Marekani milioni 5 kusaidia mambo mbalimbali ya watoto kwa mwaka huu kwa nchi za Afrika mashariki huku Tanzania pekee watoto milioni 10 wakifikiwa.

  Benki hiyo yenye matawi Dar es salaam, Mwanza na Arusha katika miradi yake ya afya, vijana na elimu wamekusudia kushirikiana na Umoja wa Mataifa kutekeleza malengo mbalimbali endelevu ikiamini kwamba jamii ikiboreshwa itakuwa katika mfumo mzuri wa maendeleo na kupiga vita umaskini.

  Malengo ya SDG’s yamepangwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka 15.
  IMG_2324
  Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Uhuru mchangayiko, Anna Mshana akitoa risala fupi ya shule yake sambamba na changamoto zinazoikabili shule yake kwa ugeni huo kutoka Umoja wa Mataifa na Benki ya Standard Chartered Tanzania.

  Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Anna Mshana alisema shule hiyo ambayo ilianzisha kitengo cha wanafunzi wasioona 1962 na kubadilishwa kuwa Shule ya msingi Uhuru mchanganyiko mwaka 1964, inakabiliwa na changamoto mbalimbali.

  Miongoni mwa matatizo ni miundombinu ya shule hiyo isiyokidhi mahitaji halisi, ukosefu wa ukuta, mashine za kufundishia watoto wasioona, upungufu wa mabweni, magodoro, vitanda na gari la kuwakimbiza hospitalini inapotokea dharura.

  Alisema ingawa kuna taasisi hutoa msaada wa gari na matibabu kwa watoto mchana, lakini nyakati za usiku kukitokea dhararu inabidi shule igharamie ingawaje wakati mwingine hatuna fedha inakuwa ni changamoto kwetu.

  Alisema Shule ya msingi Uhuru mchanganyiko yenye kutoa elimu jumuishi ina vitengo vya ufundi seremala (1975) wanafunzi wenye mahitaji maalumu ulemavu wa akili (1984) na viziwi na wasioona (Deafblidn) kilichoanzishwa mwaka 1994.
  IMG_2346
  Wanafunzi ambao ni viziwi nao walipata fursa ya kuja kila kinachoendelea kutoka kwa mkalimani wao.
  IMG_2470
  Mkuu wa Mahusiano wa benki ya Standard Chartered Tanzania, Juanita Mramba akitangaza wanafunzi 17 ambao walishiriki shindano la kuhifadhi malengo mapya ya Maendeleo Endelevu (SDG's) wakati wa kukabidhi zawadi kwa wanafunzi hao wa shule ya Uhuru mchanganyiko.
  IMG_2480
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akikabidhi zawadi zilizotolewa na Benki ya Standard Chartered Tanzania kwa wanafunzi hao, sambamba na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole.

  IMG_2428
  Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko, Anna Mshana (wa pili kushoto) moja kati ya kompyuta tano zilizolotolewa na Benki hiyo ikiwa ni kama ishara ya utekelezaji wa lengo namba nne “Quality Education” wakati wa uzinduzi wa Malengo mapya ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) uliofanywa na Benki ya Standard Chartered Tanzania kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa katika shule ya msingi Uhuru mchanganyiko jijini Dar mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya Shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko, Bw. Abubakar Mwambungu wakishuhudia tukio hilo.
  IMG_2407
  Kompyuta tano zilizotolewa na Benki ya Standard Chartered Tanzania kwa shule ya Uhuru mchanganyiko.
  IMG_2448
  Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole (wa tatu kushoto), Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati), Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Uhuru Mchangayiko, Anna Mshana (wa pili kushoto), Mjumbe wa bodi ya kamati ya Shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko, Abubakari Mwambungu (kushoto) pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania katika picha ya pamoja huku wakiwa wameshikilia miche ya miti mbalimbali ikiwemo ya matunda ambapo zaidi ya miche 150 ya miti ilipandwa kuzunguka mazingira ya shule hiyo kulinda mazingira ikiwa ni ishara kwa vitendo ya utekelezaji wa lengo namba 13 "Climate Action" kati ya Malengo 17 mapya ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) nchini Tanzania.
  IMG_2338
  Pichani juu na chini baadhi ya wanafunzi na walimu wa shule ya msingi Uhuru mchanganyiko waliohudhuria uzinduzi huo.
  IMG_2393
  IMG_2541
  Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole sambamba na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakishiriki zoezi la upandaji miti kuzunguka maeneo ya shule ya Uhuru mchanganyiko jijini Dar mwishoni mwa wiki.
  IMG_2563
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akishiriki zoezi la upandaji miti sambamba na baadhi ya wanafunzi wa shule Uhuru mchanganyiko.
  IMG_1924
  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchangayiko, Anna Mshana akitoa maelezo kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (aliyeinama) na Mkuu wa Mahusiano wa benki ya Standard Chartered Tanzania, Juanita Mramba (kulia) walipotembelea darasa la awali la watoto wenye ulemavu wa macho (upofu) katika shule hiyo. Nyuma ya Mwalimu Mkuu ni Mjumbe wa Kamati ya Shule ya Msingi Uhuru Mchangayiko, Abubakar Mwambungu.
  IMG_1942
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akicheza na mtoto Fatuma Haji wa darasa la awali katika shule hiyo ambaye ni mlemavu wa macho alipotembelea darasa hilo kabla ya kuzindua wa Malengo mapya ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) hafla iliyoandaliwa na Benki ya Standard Chartered Tanzania kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa katika shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko jijini Dar mwishoni mwa wiki.
  IMG_2032
  Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, Mkuu wa Mahusiano wa benki ya Standard Chartered Tanzania, Juanita Mramba pamoja na ujumbe wao katika nyuso za masikitiko walipotembelea darasa la watoto wenye ulamavu wa macho (vipofu) na matatizo ya kutosikia (viziwi) katika shule ya msingi Uhuru mchanganyiko.
  IMG_2075
  Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, Mkuu wa Mahusiano wa benki ya Standard Chartered Tanzania, Juanita Mramba na ujumbe wao katika picha ya pamoja na wanafunzi ambao ni walemavu wa macho ambao pia ni viziwi katika shule ya msingi Uhuru mchanganyiko.
  IMG_1995
  Walimu wa darasa la watoto wenye ulemavu wa macho ambao ni viziwi wakicheza ngoma na wanafunzi wao.
  IMG_2082
  Maana ya ulemavu wa macho na kuwa kiziwi.
  IMG_1844
  Mkutubi wa maktaba ya shule ya Uhuru mchanganyiko, Masanja akitoa maelezo ya namna mashine za kukuzia maandishi kwa wale wanafunzi wenye uono hafifu katika shule hiyo kwa Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole (kushoto) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez walipotembelea maktaba hiyo.
  IMG_1833
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akipitia Katiba maalum kwa watu wenye ulemavu wa macho iliyopo kwenye maktaba ya shule hiyo. Kushoto kwake ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole.
  IMG_2119
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Ujumbe wa Benki ya Standard Chartered Tanzania ulioongozwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole wakitembelea mambweni ya wanafunzi katika shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko.
  IMG_2696
  Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko.
  IMG_2723
  Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole (kulia) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Uhuru mchanganyiko Issa Abasi Wenge w darasa la pili (wa pili kushoto) mlemavu wa ngozi na Fatuma Haji (wa pili kulia) wa shule ya awali mwenye ulemavu wa macho.
  IMG_2742
  Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole (kulia) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Mwanafunzi Mariana Alex (Mariana the voice of the SDGs in TZ) wa darasa la tano katika shule ya msingi Uhuru mchanganyiko jijini Dar.  about the 
  IMG_2672
  Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu akiserebuka na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Uhuru mchangayiko.
  IMG_2264
  Bango lililoorodhesha Malengo 17 mapya ya Maendeleo Endelevu (SDG’s).
  IMG_2874
  Siku ilimazika kwa mechi ya kirafiki baina ya Shule ya msingi Uhuru mchanganyiko na wafanyakazi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania katika viwanja vya shule ya sekondari Benjamin Mkapa ambayo ilizinduliwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Charles Katongole (kulia) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.

  0 0

  Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na mwenyekiti wa taasisi ya Global Change for Africa Award Mhe. Dr. Phillip Collins baada ya kutunukiwa nishani ya Balozi Bora wa Afrika Brussels wa mwaka 2015. Balozi Kamala katunukiwa nishani hiyo jijini Berlin Ujerumani kwa kuzingatia utendaji wake alipokuwa Waziri wa Afrika Mashariki, Mwenyekiti wa Mabalozi wa Afrika, Mwenyekiti wa Mabalozi wa Afrika, Karibiani na Pacific, na Balozi wa Tanzania Ubeligiji, Uholanzi, Luxembourg na Jumuiya ya Ulaya.

  0 0

   Meneja wa benki ya Exim Tanzania tawi la Shinyanga  Bw. Emmanuel Nkelebe akijiandaa kukata utepe ikiwa ni ishara ya kukabidhi msaada wa madawati 50 kwa shule ya msingi Mapinduzi ‘A’ iliyopo Manispaa ya Shinyanga, ikiwa ni muendelezo wa mpango wa benki hiyo katika kuboresha ubora wa elimu hapa nchini. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mwenyeki wa Bodi ya shule hiyo Bw. Sylvester senga (wa tatu kulia) na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo.
  Meneja wa benki ya Exim Tanzania tawi la Shinyanga  Bw. Emmanuel Nkelebe akizungumza na mmoja wa wanafunzi wa shule ya Msingi Mapinduzi ‘A’ iliyopo manispaa ya Shinyanga mara baada ya kukabidhi msaada wa madawati 50 kwa shule hiyo ikiwa ni muendelezo wa mpango wa benki hiyo katika kuboresha ubora wa elimu hapa nchini

  Na Mwandishi wetu,
  BENKI ya Exim Tanzania imetoa msaada wa madawati 50 kwa shule ya msingi Mapinduzi ‘A’ iliyopo Manispaa ya Shinyanga, ikiwa ni muendelezo wa mpango wa benki hiyo katika kuboresha ubora wa elimu hapa nchini.

  Akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi madawati hayo iliyofanyika kwenye viwanja vya shule hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita, Meneja wa benki hiyo tawi la Shinyanga  Bw. Emmanuel Nkelebe alisema msaada huo wenye thamani ya sh. Milioni nne ni sehemu tu jitihada ambazo benki hiyo imekuwa ikifanya kusaidia jamii inayoizunguka.

  Alisema kuwa benki hiyo imekuwa mstari wa mbele kushirikiana na serikali katika kufanikisha mipango mbalimbali hususani katika kuboresha sekta ya elimu hapa nchini hatua aliyoilezea kuwa ndio chachu ya maendeleo kwa sekta zote ikiwemo ya benki pia.

  “Mchango wetu huu wa kuchangia katika elimu unatokana na imani yetu kwamba bila kuwa na jamii iliyoelimika hata huduma za kibenki tunazozitoa lazima zitateteleka kutokana na ukweli kuwa biashara yetu hii inategemea sana mafanikio ya jamii inayotuzunguka…mafanikio ambayo tunaamini yataletwa na elimu,’’ alisema.

  Akizungumza kwenye hafla hiyo, mkuu wa shule Bi Savera Rwabuyongo pamoja na kuishukuru benki hiyo kwa msaada huo alisema msaada huo umepatikana kwa wakati muafaka kwa kuwa shule hiyo ipo kwenye mkakati wa kutafuta madawati zaidi kutokana na uhaba wa madawati unaoikabili shule hiyo.

  Alisema shule hiyo yenye wanafunzi 816 wakiwemo wanafunzi wa kiume 342 na  wa kike 474 kwa sasa bado inakabiliwa na uhaba wa madawati 93 zaidi na hivyo kutoa wito kwa taasisi na mashirika mengine kuiga mfano wa benki hiyo kwa kuisadia zaidi shule hiyo.

  Akitoa neno la shukrani kwa benki hiyo kwa niaba ya wanafunzi wenzie, mwanafunzi Musa Peter alisema msaada huo ni sawa na ukombozi kwao kwa kuwa awali walikuwa wanapata maumivu na uchovu mwingi kutokana na wao kukaa chini hali iliyokuwa ikichangia uzorotaji wa ufahulu wao darasani.

  “Tunashukuru sana benki ya Exim kwa msaada huu kwa kuwa sasa tunauhakika wa kusoma tukiwa tumekaa kwenye madawati na tunaahidi kuyatunza madawati haya.Zaidi tunaomba na wasamalia wema wengine waje watusaidie kwa sababu bado tunahitaji madawati zaidi,’’ alisema.

  0 0

  Baadhi ya Wasanii nyota wa Filamu hapa nchini wakiongozwa na Jacob Steven a.k.a JB wakiwa wamenyanyua juu mikono yao kwa pamoja ni Ushindi sambamba na Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli (wa tatu kushoto),kuonesha kuwa wasanii hao wanamuunga mkono Dkt Magufuli katika mbio zake za kuusaka Urais kwa kutembea nchi nzima kutumia Bajaji zao tano,ambapo Bajaj mojawapo itakuwa na kazi ya kukusanya kadi za wale wanaomua kurudi/kujiunga na chama cha CCM.
   Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wananchi wa Iringa na vitongoji vyake kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika jioni ya leo septemba 28 ndani ya uwanja wa Samora mkoani Iringa.

    Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akiwaeleza wananchi sababu zilizosababisha CCM kutomteua Lowasa kuwa mgombea urais kupitia CCM hasa kutokana na hasa kile kilichoelezwa kuwa na kadhia ya ufisadi ya rushwa,mbapo pia Nape amewaomba Wananchi kumuombea afya Mgombea huyo wa Urais kupitia Chadema, ili aje ashuhudie CCM ikishinda  nafasi ya Urais.
    Wananchi wa Iringa na vitongoji vyake wakishangilia wakati Dkt Magufuli alipokuwa akiwaomba wampigie kura ya ndio itakapofika Oktoba 25,mwaka huu (ambapo uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika )ili aweze kuibuka mshindi na kuchaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano
   Dkt Magufuli akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya CCM Mgombea ubunge Jimbo la Iringa mjini, Ndugu Frederick Mwakalebela wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja samora mjini Iringa.
   Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kazini kwenye mkutano wa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli,jioni ya leo kwenye uwanja wa Samora mkoani Iringa.
   Magufulika staili kama kawa,hata baadhi ya wasanii nyota wa Bongo Movie hapa nchini wakiongozwa na Nnape Nnauye (pili shoto) walikumbwa na zoezi hilo jioni ya leo mbele ya wakazi wa Iringa na vitongoji vyake waliokuwa wamefurika kwenye mkutano wa kampeni ndani ya uwanja wa Samora,zoezi hilo kwa sasa limeanza kujizolea umaarufu mkubwa hapa nchini,la kupiga push up kama ionekanavyo pichani.
   Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Kilolo Ndugu Venance Mwamoto,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Ilula,mkoani Iringa.
    Dk Magufuli akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Kalenga kupitia CCM, Ndugu Godfrey Mgimwa wakati wa mkutano wa kampeni katika Mji wa Ifunda
   Vimbwanga vya hapa na pale vilikuwepo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Ifunda mapema leo mchana
  wazee wa kimila wa kabila la Wahehe wakifuatilia mkutano wa kampeni wa Dkt Magufuli uliofanyika mapema leo mchana katika Mji wa Ilula Jimbo la Kilolo mkoani Iringa.
    Mjumbe wa Kamati ya Kampeni za CCM, William Lukuvi akitangaza wasifu wa mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni kwenye Uwanja Samora mjini Iringa.
   Wananchi wakiwa wamefurika ndani ya Uwanja wa Samora wakisikiliza sera za Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo.
   Wananchi wa Iringa na vitongoji vyake wakifuatilia mkutano wa kampeni,wakati Dkt Magufuli alipokuwa akiwaomba wampigie kura ya ndio itakapofika Oktoba 25,mwaka huu (ambapo uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika )ili aweze kuibuka mshindi na kuchaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano

older | 1 | .... | 654 | 655 | (Page 656) | 657 | 658 | .... | 1897 | newer