Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 653 | 654 | (Page 655) | 656 | 657 | .... | 1897 | newer

  0 0
 • 09/25/15--21:33: Article 3


 • 0 0

  TAARIFA
  Assalamu Alaykum: Kwanza kabisa, napenda kumshukuru Allah Subhanahu Wa Taala kwa kutujaalia kuwa wazima na kuadhimisha Siku Kuu ya Idd Al-Adh-ha ya mwaka 1436H (2015). 
  Idd Al-Adh'ha ni Siku Kuu kubwa kati ya Siku Kuu mbili katika Uislamu, ni siku ya furaha, kwa familia na jamii kwa ujumla. Kwa niaba ya Uongozi wenu wa ZADIA, naungana na WanaZadia wote, Wazanzibari, na Waislamu kwa ujumla katika kuadhimisha siku hii adhimu.
  Kwa vile hii ni Siku Kuu Kubwa, furaha yangu ingekuwa kubwa zaidi katika kusherehekea. Hata hivyo, furaha hiyo imeingia doa kutokana na maafa yaliyowakumba ndugu zetu Waislamu waliofunga safari kwenda kuhiji, kuitikia wito wa Mola Wao Mlezi wa kuizuru Nyumba Yake
  Tukufu.
  Kutokana na hilo, napenda kuchukua fursa hii kutoa salamu zangu za rambirambi kwa Waislamu wote ulimwenguni ambao wamepoteza ndugu, jamaa na marafiki katika maafa hayo.
  Tunamuomba Allah awaingize wenzetu waliotangulia peponi kwa Rehma zake. Kama ambavyo, natoa pole kwa Mahujaji wote waliopata ajali na kujeruhiwa, na kumwomba Allah SWT awape afya na uzima na kuwarejea katika familia zao wakiwa katika afya na uzima.
  Ndugu Wanazadia na Wazalendo kwa ujumla,
  Huku tukiwa tunaendelea kusherehekea Siku Kuu ya Idd Al-Adh'ha, napenda kuwakumbusha kuhusu majukumu ya kila mmoja wetu ya kuendeleza umoja, mshikamano na amani katika Jumuiya yetu na nchi yetu Zanzibar kwa ujumla. Na hakuna njia nyepesi ya kufikia malengo hayo ispokuwa kushikamana na Kamba ya Mwenyezi Mungu.
  Tujifunze kutokana na somo la Hijja ambalo Waislamu kutoka sehemu zote duniani hukutan sehemu moja wakiwa katika vazi la aina moja kwa ajili ya kuabudu Mola mmoja, bila kujali kabila, nchi wanazotoka, umri, jinsia, vyeo au tofauti nyenginezo. Wote wako sawa wakiwa na lengo moja.
  Siku Kuu hii kwa mwaka huu inakuja ikiwa imebakia si zaidi ya mwezi mmoja kabla Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kuingia katika Uchaguzi Mkuu. Mara tu baada ya kumalizika kwa shamra-shamra za Siku Kuu, akili, macho na masikio yetu yote yataelekea kwenye kampeni za uchaguzi na vioja vyake.
  Kwa hivyo, nasaha kwetu sote, wadau wote, kulitumia funzo tulilolipata katika Hijja na Siku Kuu yake kuhakikisha kuwa tunashiriki kwa njia moja au nyengine kuufanya uchaguzi ujao upite kwa salama na amani kama ulivyopita ule uliotangulia wa mwaka 2010.

   Tukumbuke kuwa Umoja ni nguvu na Utengano ni Udhaifu. Kwa hivyo, kampeni na ushabiki wetu wa kisiasa vyote vilenge kwenye kuendeleza Serikali ya Umoja Wa Kitaifa Zanzibar na kuipa nguvu Zanzibar kuleta maendeleo.
  Ikumbukwe kuwa, Malengo Makuu ya ZADIA ni kuleta umoja wa Wazanzibari na Maendeleo yao nje na ndani ya nchi yetu tuipendayo. Hata hivyo, malengo hayo hayawezi kufikiwa bila kuwa na amani, usalama na utulivu ndani ya nchi yetu ya Zanzibar na hata Jamhuri yote ya Muungano wa Tanzania.
  Kila mmoja wetu ajaribu kuyalinda malengo hayo kwa kuzingatia kauli ya Bwana Mtume SAW aliposema: "Kila mmoja wenu ni mchunga, na kila mmoja wenu ataulizwa juu ya kile anachokichunga".
  Nawatakia Idi Njema, nawapa pole wafiwa na nawaombea majeruhi shifaa.
  Omar H. Ali,
  Mwenyekiti,
  ZADIA.

  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

  WANAFUNZI waliosoma  Shule ya Forodhani na Sasa St.Joseph Cathedral  wameanzisha  umoja wa shule hiyo kwa ajili ya kusaidia elimu pamoja na masuala ya kijamii.


  Wakizungumza nyakati tofauti wanafunzi waliosoma hapo wamewataka wanafunzi kufuata nyayo zao kutokana na shule hiyo kuwa na historia nzuri ambayo hadi sasa haijaweza kufutika.


  Wamesema kuwa umoja huo utakuwa imara katika kusaidia shule hiyo katika masuala mbalimbali ikiwemo na kusaidia jamii kutokana na malezi walioyapata katika shule hiyo tangu Ukoloni.


  Akizungumza katika uzinduzi huo mwanafunzi aliosoma shule hiyo,Miriamme Ziaror, amesema umoja wa wanafunzi waliosoma shule ya St Joseph convent school  iliodumu kuanzia mwaka 1932 hadi 1969, na Forodhani Sekondari  ilokuwapo 1970 hadi 2008 ( ilitaifishwa na serikali) na baada ya hapo St Joseph Cathedral High school 2009 (baada ya kurushwa kwa kanisa la katoliki)  hadi leo inatambulika   St. Joseph & Forodhani  ALUMNI .

  Miriamme amesema katika shule hiyo  kuna wanafunzi waliosoma shule hiyo, wanaoishi nje ya nchi, wanaotoka  Canada, Australia, New Zealand Uingereza na Seychelles wameungana kuhudhuria mkutano huu wa kishitoria wa kuanzisha umoja wa ALUMNI.


  Amesema baadhi ya wanaWengine hawajafika Tanzania kwa miaka zaidi ya 30.  Wanarudi kuona shule iliowalea.


  Aidha amesema katika watu maarufu wanaotoka nchi za nje atakuwapo Jaji Mkuu wa mahakama ya Rufaa Seychelles  ambaye alisoma hapo na kumaliza kidato cha nne mwaka 1968, na baada ya hapo, kuhamia Seychelles na wazazi wake alipo  kuendelea na masomo ya juu.


  Kwa upende wa Mbunge wa Viti Maalumu ,mwanafunzi wa shule hiyo zamani Ashymaa Kwegyry ametaka wanafunzi kuwa wadhubutu na kuweza kufanikisha ndoto zao.


  Amesema amesoma shule kutokana na kuwa na ulemavu lakini walimu walimfundisha na kuamini kuwa na anaweza kufanya kitu kama binadam wengine.
  Mwanafunzi wa Zamani wa Forodhan,Miriamme Zailor akizungumza wakati wa uzinduzi wa umoja wa wanafunzi waliosoma shule ambayo kwa sasa ni St.Joseph Cathedral leo jijini Dar es Saalaam.
  Mwananfunzi wa zamani wa shule ya Sekondari ya St.Joseph hivi sasa, Ashymaa Kwegyry akizungumza katika uzinduzi wa umoja wa wanafunzi waliosoma katika shule hiyo leo jijini Dar es Salaam.
  Wanafuzi walohitimu mwaka 2014 wakisoma lisala ya shule hiyo, Damian Mapalala na Nancy Kimario.

  Baadhi ya wanafunzi wanaosoma shule ya Sekondari ya  St.Joseph walioshiriki katika uzinduzi wa umoja wa wanafuzi waliosoma shule hiyo jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wanafunzi waliosoma shule ya Sekondari ya  St.Joseph zamani wakiwa wameshuriki katika uzinduzi wa wanafunzi waliosoma shule hiyo jijini Dar es Salaam leo.
  Wanafunzi wakitumbuiza katika uzinduzi huo leo jijini Dar es Salaam. 
  Wapigangoma wakipiga ngoma leo jijini Dar es Salaam leo katika nuzinduzi huo.


  Baadhi ya wanafunzi wanaosoma shule hiyo wakiwa wamevalia mavazi ya kimasai mara baada ya kucheza ngoma inayowakilisha kabila la wamasai katika uzinduzi huo jijini Dar es Salaam leo. 
    Baadhi ya wanafunzi waliosoma shule hiyo zamani.

  Picha ya pamoja ya baadhi ya wanafunzi waliosoma shule ya St.Joseph 
   Picha ya pamoja ya wanakamati ya maandalizi ya uzinduzi wa Umoja wa wanafunzi waliosoma shule ya St.Joseph mara baada ya kumalizika uzinduzi huo jijini Dar es Salaam leo.
  Baadhi ya wanafunzi waliosoma shule hiyo.

  0 0

  Telephone: 2863748/2860485,

  Fax: 0255 - (022) - 286 0486

  Website: basata.or.tz

  CONTACTS

  P.O. Box. 4779,

  BASATA Arts Centre, Ilala Sharif Shamba,.

  Dar es Salaam, Tanzania

  National Arts CouncilBASATA  26/09/2015   

  PRESS RELEASE

  BASATA KURUDISHA HADHI YA MUZIKI WA REGGAE

  Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kushirikiana na Kampuni ya Reggae Production House iliyo chini ya Msanii Mkongwe wa reggae Innocent Nganyagwa limeandaa programu maalum kwa ajili ya kurudisha hadhi ya muziki wa reggae nchini.


  Programu hiyo ambayo itafanyika makao makuu ya BASATA yaliyoko Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam Jumatatu ya Tarehe 28/09/2015 kuanzia saa 4:00 hadi saa 6:30 Mchana kupitia Programu ya Jukwaa la Sanaa, itakuwa mahsusi kwa ajili ya kuurudisha muziki wa reggae jukwaani, kujadili mwelekeo wa muziki huu na kuja na mikakati bora ya kuurudishia hadhi yake.


  Ieleweke kwamba katika siku za karibuni muziki huu wa reggae umekuwa umeganda na kutokupiga hatua kubwa hali ambayo imewafanya wadau wa muziki kukosa burudani ambayo wamekuwa wakiipata huko nyuma kupitia kwa wasanii wakongwe kama Innocent Nganyagwa, Innocent Garinoma, Justine Kalikawe na wengineo.


  Changamoto kubwa si tu ni muziki huu kutochezwa kwenye vyombo vya habari bali pia kuna changamoto ya wasanii wenyewe kutokubadilika na kutengeneza muziki unaokwenda sambamba na soko pia hitaji la mashabiki.


  Ni nia ya BASATA kuona wasanii na wadau wote wa muziki nchini wanahudhuria programu hii mahsusi kwa lengo la kujadiliana kwa pamoja hatma ya muziki wa reggae, kupata historia ya jinsi ulivyokuwa huko nyuma, kutazama na kuburudika Jukwaani na muziki wa mmoja wa wasanii wakongwe wa muziki huu.


  BASATA linaamini kwamba baada ya programu hii wasanii wa reggae na wadau kwa ujumla watakuwa na mwanzo mpya katika kurudisha hadhi ya muziki wa reggae nchini na kuhakikisha unaendelea kudumu.

  Sanaa ni Kazi, tuikuze, tuitunze na kuithamini


  IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI BASATA


  0 0

  Mwenyekiti Kamati ya maandalizi ya Amani kuelekea uchaguzi mkuu, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu ujio wa waimbaji solly Mahlangu wa afrika kusini na Ifeanyi Kelechi wa uingereza. Kwaajili ya kutumbuiza matika tamasha hilo.
  Aidha Msama amesema kuwa katika Tamasha hilo Mgeni rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Jakaya Mrisho Kikwete.
  Kulia ni Mratibu wa maandalizi ya Tamasha la  kuombea amani kuelekea Uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu, Khamis Pembe na kushoto ni  Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhulia katika mkutano huo.


  RAIS Jakaya Mrisho Kikwete mgeni rasmi katika tamasha la kuombea amani ameyasema hayo mbele ya Waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha la kuombea amani kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 25 mwaka huu ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama amesema kuwa maandalizi yamekamilika pia waimbaji wa nyimo za Injili wa nje ya nchi wataanza kuingia hapa nchini.

  Msama aamesema kuwa viingilio ni kama kawaida hakuna mabadiliko yoyote kwa watoto watachangia shilingi 1000 na watu wazima na viti vya kawaidi shilingi elfu 3000  na VIP ni shilingi elfu 5000 pia ametoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi katika kufanikisha maombi ya amani katika nchi yetu.

  Aliongeza kuwa  katika tamasha hilo waimbaji mbalimbali watasindikiza maombi hayo sambamba na viongozi wa dini watakaochagiza maombi hayo kabla ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25.

  Aidha Msama alisema kauli mbiu ya tamasha hilo ni Tanzania ni ya kwetu, tuilinde na kuitunza amani yetu, hivyo ni nafasi ya Watanzania kuzingatia kauli hiyo ambayo inazuia machukizo kwa Mungu.

  0 0

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwasili katika viwanja vya Chuo cha Amali Mkokotoni akipokelewa na Waziri wa Sheria na Katiba Zanzibar Mhe. Abubakary Khamis Bakar, kwa ajili ya kuhudhuria Baraza la Eid El Hajj, kitaifa zimefanyika Mkoa wa Kaskazini Unguja.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad, akiwasili na katika viwanja vya Chuo cha Amali Mkokotoni akisalimiana na Waziri wa Sheria na Katiba Zanzibar Mhe. Abubakary Khamis Bakar, kwa ajili ya kuhudhuria Baraza la Eid El Hajj, kitaifa zimefanyika Mkoa wa Kaskazini Unguja.
  Rais Mstaaf wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume,akiwasili katika viwanja vya Chuo cha Amali Mkokotoni akipokelewa na Waziri wa Sheria na Katiba Zanzibar Mhe. Abubakary Khamis Bakar, kwa ajili ya kuhudhuria Baraza la Eid El Hajj, kitaifa zimefanyika Mkoa wa Kaskazini Unguja.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwasili kwa msafara wa mapikipiki ya Polisi wa Usalama Barabara kuhudhuria Baraza la Eid El Hajj zilizofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja,  
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwasili kwa msafara wa mapikipiki ya Polisi wa Usalama Barabara kuhudhuria Baraza la Eid El Hajj zilizofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja, 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe Juma Kassim Tindwa , tayari kwa huhudhuria hafla ya Baraza la Eid El Hajj zilizofanyika Kitaifa katika Mkoa wa Kaskazini Unguja katika Ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni Unguja. 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akiwasili viwanja vya Chuo cha Amali Mkokotoni akiongozana na Kamishna wa Polisi Zanzibar Kamishna Hamdani tayari kwa kupokea salamu za Bwaride lililoandaliwa kwa ajili yake na Jeshi la Polisi Kikosi cha FFU, katika viwanja hivyo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akipokea saluti maalum ilioandaliwa na Jeshi la Polisi Kikosi cha FFU kwa ajili ya Baraza la Eid El Hajj.lililofanyika katika viwanja vya Chuo cha Amali Mkokotoni Unguja.
  Kikosi cha FFU kikitowa heshima ya Bwaride Maalum lililoandaliwa kwa Ajili ya Baraza la Eid El Hajj kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya Chuo cha Amali Mkokotoni Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akielekea Ukumbi wa Baraza la Eid El Hajj baada ya kupokea Saluti ya Bwaride Rasmin la Jeshi la Polisi Kikosi cha FFU.
  Viongozi wa meza Kuu wakiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, na Viongozi wengine wakimsikiliza msoma Quran wakati wa ufunguzi wa Baraza la Eid El Hajj lililofanyika kitaifa katika Mkoa wa Kaskazini Unguja, kutoka kushoto Naibu Musti wa Zanzibar Shekh. Mussa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad na kulia Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Abubakar Khamis Bakar Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Rais Mastaaf wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume na Mama Fatma Karume. 
  Msoma Quran Ust Juma Said akisoma Quran wakati wa ufunguzi wa Baraza la Eid El Hajj lililofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni Zanzibar. 
  Ust. Machano Faki akisoma Tafsiri ya Quran wakati wa hafla ya Baraza la Edi El Hajj lililofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Amali Zanzibar Mkoa wa Kaskazini Unguja.
  Waziri wa Sheria Katiba Zanzibar Mhe. Abubakar Khamis Bakar akitowa maelezo na kukaribisha Mgeni Rasmin, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kuhutubia Wananchi katika Hafla ya Baraza la Eid lililofanyika Kitaifa Mkoa wa Kaskazini Unguja.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akihutubia Wananchi katika Baraza la Eid El Hajj katika ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja. 
  Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar wakati wa hafla ya Baraza la Eid El Hajj.
  Viongozi wa Serikali na Wananchi wakihudhuria Baraza la Eid El Hajj wakifuatilia Hutuba ya Baraza la Eid iliyokuwa ikisomwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,
  Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja wakifuatilia hutuba ya Baraza la Eid ikisomwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, Baraza la Eid El Hajj Kitaifa limefanyika katika Mkoa wa Kaskazini Unguja.
  Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja wakifuatilia hutuba ya Baraza la Eid ikisomwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, Baraza la Eid El Hajj Kitaifa limefanyika katika Mkoa wa Kaskazini Unguja.
  Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja wakifuatilia hutuba ya Baraza la Eid ikisomwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, Baraza la Eid El Hajj Kitaifa limefanyika katika Mkoa wa Kaskazini Unguja.
  Wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) wakiwa kazini kurusha matangazo wakati wa hafla ya Baraza la Eid El Hajj lililofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni Zanzibar.
  Naibu Mufti wa Zanzibar Shekh. Mussa, akisoma dua baada ya kumalizika kwa hutuba ya Mgeni rasmin Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein.
  Viongozi wa Serikali wakiitikia dua.
  Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja wakiitikia Dua.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza na Balozi Ali Karume nje ya Ukumbi wa Baraza baada ya kumalizika kwa hafla hiyo wakipata viburudisho vilivyoandaliwa kwa ajili ya Baraza la Eid El Hajj.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza na Viongozi wa Serikali kutoka kushoto Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalif Seif Shariff Hamad, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Rais Mstaff wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume.
  Viongozi na Wananchi wakipata dhifa ilioandaliwa kwa ajili ya Baraza la Eid El Hajj kwa Wananchi katika viwanja vya Chuo cha Amali Mkokotoni Zanzibar.
  Wananchi wakipata vitafunio baada ya kumalizika kwa Baraza la Eid El Hajj kumalizika kwa hutba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein,  
  Wananchi wakipata vitafunio baada ya kumalizika kwa Baraza la Eid El Hajj kumalizika kwa hutba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein,  

  Wananchi wakipata vitafunio baada ya kumalizika kwa Baraza la Eid El Hajj kumalizika kwa hutba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein,  
  Wananchi wakipata vitafunio baada ya kumalizika kwa Baraza la Eid El Hajj kumalizika kwa hutba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein.  
  iMETAYARISHWA NA OTHMANMAPARA.BLOGSPOT. ZANZINEWS.COM

  0 0

  Pumzika kwa Amani mpendwa wetu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Celina O. Kombani (pichani enzi za uhai wake).
  Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu na watumishi wote wa Ofisi ya Rais-Utumishi wataendelea kukukumbuka daima kwa busara zako na uongozi wako mzuri. Mola ailaze Roho yako 
  pahala pema peponi - AMIN
  -------------------------------------------------------------------

  Wakati huo huo mwili wa Marehemu Celina O. Kombani umewasili muda huu katika uwanja wa ndege wa kimatifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam. Utaratibu wa msiba unasimamiwa na serikali na ofisi za Bunge. Tutaendelea kuwafahamisha ratiba kila tutapopata taarifa. 
  Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani umewasili muda huu Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam
   Familia ya marehemu, viongozi mbalimbali na wananchi wakisubili mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani  ulipowasili jioni hii Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam. Aliyeshikwa bega wa tatu kushoto ni Mume wa Marehemu Mzee Kombani.
   Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani  ukitelemshwa baada ya kuwasili jioni hii Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
    Msafara wa mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani  ukipelekwa kwenye ambulance  baada ya kuwasili jioni hii Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
  Msafara wa mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani  ukipakiwa  kwenye ambulance  baada ya kuwasili jioni hii Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
  Spika wa Bunge Mhe Anne Abdallah na viongozi wengine wakiwa Uwanja wa ndege kupokea mwili wa marehemu Kombani. 
  Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii.

  0 0

    Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam(CBE) Prof.Emanuel Mjema(kushoto) akizungumza na viongozi  na baadhi ya watumishi wa Hospitali ya wilaya ya Kisarawe leo  kabla ya kukabidhi msaada wa  shuka 176 kusaidia wodi ya Wazazi ya hospitali hiyo.
   Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe Dkt.Martin Msokela akiongea na watumishi wa hospitali ya wilaya ya Kisarawe kabla ya kupokea msaada wa mashuka ya wagonjwa wilayani humo leo. Mashuka hayo yametolewa na chuo cha Elimu ya Biashara Dar es Salaam (CBE). 
   Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam(CBE) Prof.Emanuel Mjema(kushoto) akikabidhi msaada wa shuka 176 kwa Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe Dkt.Martin Msokela (kulia) leo. Mashuka hayo yametolewa na chuo hicho kusaidia wodi ya Wazazi ya Hospitali hiyo iliyokuwa ikikabiliwa na uhaba wa mashuka.
   Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam(CBE) Prof.Emanuel Mjema(katikati), Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya  wilaya ya Kisarawe  Dkt.Martin Msokelo(kulia) na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Mohamed Mzige kwa pamoja wakitandika sehemu ya msaada wa mashuka 176 yaliyotolewa na CBE kwenye  wodi ya Wazazi ya hospitali hiyo.
   Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam(CBE) Prof.Emanuel Mjema(wa pili kushoto), Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya  wilaya ya Kisarawe  Dkt.Martin Msokelo(kushoto ) na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Mohamed Mzige (kulia) na baadhi ya watumishi wa hospitali ya Kisarawe wakielekea lilipo jengo la wodi ya wazazi.
  Wauguzi wa Hospitali ya wilaya ya Kisarawe wakifurahia msaada wa mashuka yaliyotolewa kwa wagonjwa na Chuo cha Elimu ya Biashara, CBE leo.
  Picha/Aron Msigwa - MAELEZO.


  Aron Msigwa -MAELEZO.
  WITO umetolewa kwa Taasisi, mashirika na makampuni kote nchini kujenga utamaduni  wa kutumia sehemu ya faida wanayoipata katika kuisaidia jamii kupitia sekta ya afya ambayo inakabiliwa na changamoto mbalimbali.

  Wito huo umetolewa leo mjini Kisarawe na Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam Prof.Emanueli Mjema wakati akikabidhi msaada wa shuka 176 zilizotolewa na chuo hicho kusaidia wodi ya Wazazi ya Hospitali ya wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani.

  Amesema CBE mwaka huu imetimiza miaka 50 toka kuanzishwa kwake mwaka 1965, hivyo ukongwe na umri wake nchini Tanzania umekua ukiendana na mabadiliko ya kiuchumi  yanayotokea ndani na nje ya nchi ili kukidhi mahitaji na matarajio ya watanzania.

  "CBE tukiwa chuo kikongwe nchini tumefanya mengi yenye manufaa kwa uchumi wa nchi yetu na jamii ya watanzania,kwa kuwathamini wananchi tunaowahudumia tuna utaratibu wa kurudisha sehemu ya faida tunayoipata kwa jamii na mwaka huu tulitenga kiasi cha shilingi milioni 9 kusaidia wodi za wazazi katika hospitali zetu" Amesisitiza.

  Ameeleza kuwa ndani ya miaka 50, CBE  imewanufaisha wananchi na kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa kupitia Fani za Biashara, Ugavi na manunuzi, Vipimo, TEHAMA , Utawala katika biashara pamoja na kutoa huduma mbalimbali kwa jamii.

  Amesisitiza  kuelekea miaka 50 ijayo chuo chake kimeelekeza nguvu katika kuwekeza kwenye ubora na ujuzi wa kumuwezesha muhitimu kuitumia elimu aliyoipata kuleta manufaa na mabadiliko katika jamii inayomzunguka.

  “Sisi kama chuo cha Elimu ya Biashara tumeona uhitaji uliopo nchini wa kukosa wataalam wenye ujuzi wa Biashara ndio maana tumeanza kufuandisha wanafunzi wa Shahada ya Elimu katika Biashara ili tupate wahitimu bora watakaokidhi mahitaji ya soko” Amesisitiza.

  Kwa upande,Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Martin Msokela akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo kwa niaba ya Mkurugenzi wa wilaya hiyo, ameushukuru uongozi wa CBE kwa kuwakumbuka wagonjwa wa Hospitali ya wilaya ya Kisarawe.

  Amesema msaada uliotolewa na chuo hicho umepunguza uhitaji wa mashuka waliokuwa nao kwani Hospitali hiyo inakabiliwa na tatizo la uhaba wa mashuka kwenye vitanda vya wagonjwa.

  Dkt.Msokela amewaomba wadau wengine kujitokeza kwa wingi kuisaidia hositali hiyo kama  walivyofanya CBE ili kuboresha afya za wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kutibiwa.

  " Nawaomba wadau wengine wajitokeze kusaidia kama walivyofanya CBE, licha ya hili la mashuka ukiangalia Jiografia ya Kisarawe,Hospitali yetu imekua na tatizo la upatikanaji wa maji  na uchakavu wa mitambo" Amebainisha. 

  Aidha katika hatua nyingine Dkt.Msekela ameeleza kuwa hali ya ugonjwa wa Kipindupindu wilayani humo inaendelea kudhibitiwa  kupitia timu ya wataalam iliyoundwa kukabiliana na tatizo hilo na kuongeza kuwa hospitali hiyo    imepokea mgonjwa mmoja  mwenye tatizo hilo.

  0 0

  Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif Ali Iddi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ustawi wa Jamii Zanzibar Bi Asha Abdalla wakiongozana na mlezi wa Wazee Welezo wakiwasili katika viwanja vya Makaazi ya Wazee Welezo Unguja kumuwakilisha Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, kutowa Mkono wa Eid kwa Wazee hao kusherehekea Sikukuu hiyo ya Eid El Hajj.
  Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha akizungumza na Wazee wa Welezo wakati alipofika katika makaazi yao kuwajulia hali na kutoa mono wa Eid El Hajj kwa Wazee hao kwa Niaba na Mama Mwanamwema Shein.
  Wazee wa Makaazi ya Wazee Welezo Zanzibar wakimsikiliza Mama Asha wakati alipofika katika makaazi ya Wazee Welezo kuwatembelea na kutoa Mkono wa Eid El Hajj kwa Wazee hao.  
  Wazee wa Makaazi ya Wazee Welezo Zanzibar wakimsikiliza Mama Asha wakati alipofika katika makaazi ya Wazee Welezo kuwatembelea na kutoa Mkono wa Eid El Hajj kwa Wazee hao
  Kwa Niaba ya Wazee wanaoishi Makaazi ya Wazee Welezo Mzee Shein Kombo akitowa shukrani kwa niaba ya wazee wezake kwa Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, kwa kuwajali na kuwatembelea mara kwa mara anapopata nafasi kuja kuwajuliana hali na kujua shida zao,  
  Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif, akitowa mkono wa Eid El Hajj kwa Wazee wa Welezo kwa Niaba ya Mama Mwanamwema Shein, 
  Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif, akimjulia hali na kumpa mkono wa Eid El Hajj Mzee Chui anayeishi katika makaazi ya Wazee Welezo Zanzibar 
  Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif, akimjulia hali Bi Riziki anayeishi katika Nyumba za Makaazi ya Wazee Welezo wakati alipowatembelea na kutoa mkono wa Eid kwa wazee hao kwa niaba na Mama Mwanamwema Shein.
  Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif akizungumza na Wazee wa Makaazi ya Wazee Sebleni Zanzibar, alipofika kuwatembelea na kutoa mkono wa Eid El Hajj kwa niaba ya Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein.  
  Wazee wa Makaazi ya Wazee Sebleni Zanzibar wakimsikiliza Mama Asha Balozi wakati alipowatembelea na kutoa mkono wa Eid El Hajj. 
  Wazee wa Makaazi ya Wazee Sebleni Zanzibar wakimsikiliza Mama Asha Balozi wakati alipowatembelea na kutoa mkono wa Eid El Hajj. 
  Wazee wa Makaazi ya Wazee Sebleni Zanzibar wakimsikiliza Mama Asha Balozi wakati alipowatembelea na kutoa mkono wa Eid El Hajj. 
  Mzee Omar akisoma Dua wakati wa hafla hiyo 
  Wazee wakiitikia dua. 
  Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi akitowa mkono wa Eid El Hajj kwa Wazee wa Nyumba Sebleni Zanzibar.
  Katibu Mkuu Wizara ya Ustawi wa Jamii Ndg Asha Abdalla akitowa mkono wa Eid kwa Wazee wa Makaazi ya Wazee Sebleni Zanzibar kwa niaba ya Mama Mwanamwema Shein.
  Imetayarishwa na Othmanmapara.Blogspot. zanzinews.com.

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akicheza bao la kete na mzee Abdalla Salim Kitambo wa Wilaya ya Mjini wakati alipofika kuyafunga mashindano ya fainali ya mchezo huo na mchezo wa Karata katika viwaja vya Eacrotanal leo
   Baadhi ya Timu mbali mbali za Michezo ya Bao la Kete na karata wakiwa katika fainali ya michezo hiyo iliyofanyika leo katika viwanja vya Eacrotanal Mjini Unguja,wakati mgeni rasmi akiwa  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
   Timu za mchezo wa karata kutoka kibanda mawazo Miembeni Chake chake Pemba na kwamtipura Unguja zikichuana katika fainali iliyofanyika leo katika viwanja vya Eacrotanal Mjini Unguja,mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na vikundi mbali mbali vya michezo ya bao na karata wakati wa fainali ya michezo hiyo iliyochezwa leo katika viwanja vya Eacrotanal Mjini Unguja
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  akimkabidhi kombe bingwa wa mchezo wa Bao la Kete Kidodi Salum Kidodi wa klabu ya Mwembeladu baada ya kumfunga mpinzani wake katika fainali Mzee Nassor Othman wa klabu ya Bora imani ya Jangombe wilaya ya Mjini  iliyochezwa leo katika viwanja vya Eacrotanal Mjini Unguja
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  akimkabidhi kombe bingwa wa mchezo wa Bao la Kete Kidodi Salum Kidodi wa klabu ya Mwembeladu baada ya kumfunga mpinzani wake katika fainali Mzee Nassor Othman wa klabu ya Bora imani ya Jangombe wilaya ya Mjini  iliyochezwa leo katika viwanja vya Eacrotanal Mjini Unguja
   [Picha na Ikulu.]

  0 0

  Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnadi kwa wananchi, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Freeman Mbowe, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mpira wa Machame, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro Septemba 26, 2015.
  Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Freeman Mbowe, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Bomang'ombe, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye uwanja wa Half London, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro Septemba 26, 2015.
  Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi, Mh. James Mbatia akiwahutubia wananchi wa Mji wa Bomang'ombe, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye uwanja wa Half London, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro leo Septemba 26, 2015.
  Waziri Mkuu wa zamani, Mh. Fredrick Sumaye akiwahutubia wananchi wa Mji wa Bomang'ombe, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye uwanja wa Half London, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro leo Septemba 26, 2015.
  Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Bomang'ombe, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye uwanja wa Half London, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro  Septemba 26, 2015. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Shinyanga mjini waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Kambarage ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa wakati umefika wa kujenga Tanzania mpya yenye viwanda vya kutosha kutoa ajira kwa vijana wengi.
  Alisema pia kuwa Serikali yake itakuwa rafiki wa sekta binafsi na kuwajengea uwezo wafanya biashara ndogo ndogo ili waweze kujiendeleza.
   Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Shinyanga kwenye mkutano wake wa Kampeni ambapo aliwaambai wananchi hao kuwa serikali yake itakuwa ya kufanya kazi zaidi kwa maendeleo ya nchi.
   Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisisiti za jambo wakati wa mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika Shinyanga mjini.


   Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Shinyanga mjini Ndugu Stephen Massele kwenye mkutano wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi uliofanyika kwenye viwanja vya Kambarage.
   Mgombea Ubunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Ndugu Stephen Massele akihutubia wakazi wa Shinyanga mjini kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaambia wananchi hao Mgombea urais anazo changamoto za Shinyanga mjini na anaamini atazitatua hivyo amewataka watu wake kumpa kura nyingi za Dk. John Pombe Magufuli ifikapo tarehe 25 Octoba.

   Katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga Alhaji Saad Kusilawe akihutubia wakazi wa Shinyanga mjini na kuwaambia CCM ipo imara kipindi hiki kuliko kipindi kingine chochote hasa baada ya mizigo kuhama.
   Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM Mzee Samuel Sitta akihutubia wakazi wa mkoa wa Shinyanga kwenye mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli.
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi na Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa Ndugu Abdalah Bulembo akihutubia wakazi wa Shinyanga mjini kwenye mkutano wa kumnadi mgombea urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli.

  Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwaaga wakazi wa mji wa Shinyanga mara baada ya kumaliza mkutano wa kampeni kwenye uwanja wa Kambarage.
   Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiteta jambo na mgombea ubunge wa jimbo la Solwa Ndugu Ahmed Ally Salum (kushoto)kabla ya kuwahutubia wakazi wa Solwa waliojitokeza kwa wingi kwenye viwanja vya Solwa Joshoni.
   Wananchi wa Jimbo la Solwa wakimsikiliza Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli
  Mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akitemkabidhi ilani ya uchaguzi ya CCM mgombea ubunge wa jimbo la Solwa Ndugu Ahmed Ally Salum (kushoto) kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Solwa Joshoni.


   Mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini akihutubia wakazi wa mji huo kwenye mkutano wa kampeni za CCM zilizofanyika kwenye uwanja wa Kambarage.
   Kikundi cha Ngoma za Asili kutoka Mwanza maarufu kwa jina la Mchele Mchele kikitumbuiza kwenye mkutano wa kumnadi mgombea wa Urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli.
   Msanii wa muziki wa kizazi kipya Abdul Kiba akionyesha uwezo wake kwenye mkutano wa kampeni za CCM mjini Shinyanga.
   Vijana kutoka Temeke jijini Dar es Salaam ,Chegge na Temba wakishambulia jukwaa pamoja na mgombea ubunge wa jimbo la Shinyanga mjini Ndugu Stephen Massele.
   Mwasiti akiimba wakati wa mkutano wa kampeni za CCM mkoani Shinyanga.
   Wasanii wakipiga push up jukwaani kabla ya mgombea wa urais kupitia CCM hajahutubia.
   Msanii wa muziki wa kufoka foka Mwana FA akishambulia jukwaa wakati wa kampeni za CCM zilizofanyika kwenye uwanja wa Kambarage,Shinyanga mjini.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

   KUMEKUWAPO UVUMI WENYE KUUPOTOSHA UMMA KUWA MKUU WA MAJESHI YA ULINZI NCHINI AMENUSURIKA KIFO BAADA YA KUWEKEWA SUMU KATIKA CHAKULA NA HIVI SASA AMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA AGA KHAN ILIYOPO NAIROBI, NCHINI KENYA, HUKU WENGINE WAKIDAI KUWA YUKO NCHINI INDIA KWA MATIBABU. 
  TAARIFA HIZO NI UONGO WENYE KILA DALILI YA KUTENGENEZWA KWA LENGO LA KUWATIA HOFU WATANZANIA JUU YA USALAMA WA KIONGOZI HUYU WA JUU WA MAJESHI YETU.

  UKWELI NI KUWA MKUU WA MAJESHI YA ULINZI, JENERALI DAVIS MWAMUNYANGE NI BUKHERI WA AFYA NA HAYUPO NCHINI KENYA WALA INDIA KAMA ILIVYOENEZWA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII NA VYOMBO VYA HABARI.
  Jenerali Mwamunyange mara baada ya kuwasili na kupokelewa na mwenyeji wake Rome, nchini Italia.
  TUNAPENDA KUWATOA HOFU WANANCHI KUWA TAARIFA HIZO NI UZUSHI MTUPU KWANI JENERALI MWAMUNYANGE ALIONDOKA NCHINI TAREHE 22 SEPTEMBA 2015, SAA 10.45 JIONI KWA NDEGE YA SHIRIKA LA NDEGE LA EMIRATES KUELEKEA ROME, ITALIA KWA ZIARA YA KIKAZI KUFUATIA MWALIKO WA MKUU WA MAJESHI WA JAMHURI YA ITALIA, JENERALI CLAUDIO GRAZIANO. TUNAPENDA KUWAHAKIKISHIA WANANCHI KUWA JENERALI MWAMUNYANGE PAMOJA NA UJUMBE WAKE WANAENDELEA NA ZIARA HIYO KAMA ILIVYOPANGWA NA AMESIKITISHWA NA UVUMI HUO.

  WIZARA YA ULINZI YA JESHI LA KUJENGA TAIFA IMESIKITISHWA NA TABIA HII YA UZUSHI INAYOPINGANA NA WELEDI NA KANUNI ZA UANDISHI KATIKA TASNIA YA HABARI. NI DHAHIRI TABIA HII INAIDHALILISHA TASNIA YA HABARI NA WANAHABARI WANAOZINGATIA WELEDI NCHINI. TUNAPENDA KUCHUKUA FURSA HII KUKEMEA TAARIFA ZA AINA HII ZISIZOKUWA NA TIJA KWA TAIFA LETU NA ZILIZOLENGA KUWASUMBUA NDUGU, JAMAA, MARAFIKI NA WATUMISHI WENYE MAPENZI YA DHATI NA JENERALI MWAMUNYANGE.

  TUNAWAASA WANAHABARI KUTOZITUMIA VIBAYA KALAMU ZAO NA UHURU WALIONAO KWA NAMNA YOYOTE ISIYOKUWA NA TIJA KWA TAIFA LETU. AIDHA, WIZARA NA TAASISI ZAKE WAKATI WOTE ZIMEKUWA TAYARI KUTHIBITISHA JAMBO LOLOTE AU KUTOA UFAFANUZI PALE ULIPOHITAJIKA. INASTAAJABISHA KUONA WALIOANZISHA UZUSHI HUO NA KUUENEZA HAWAKUWA TAYARI KUOMBA UTHIBITISHO WA NAMNA YOYOTE. JAMBO HILI LINATIA SHAKA JUU YA NIA YA MTU AU KIKUNDI KILICHOANZISHA UVUMI HUO.

  WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA NA TAASISI ZAKE ZITAENDELEA KUTOA USHIRIKIANO WA DHATI KWA WANAHABARI WENYE NIA YA DHATI YA KUJENGA NA KUILETEA SIFA TASNIA YA HABARI KWA KUZINGATIA WELEDI. UHURU WA VYOMBO VYA HABARI UWE NI UHURU WENYE KUZINGATIA WAJIBU ULIOBAINISHWA KATIKA MAADILI NA KANUNI ZA UANDISHI WA HABARI.

  MWISHO, TUNAWATAKA WALIOANZISHA UZUSHI HUO KUMUOMBA RADHI JENERALI MWAMUNYANGE KAMA ISHARA YA USTAARABU NA KUTAMBUA KUTELEZA KWAO. KUTOFANYA HIVYO ITATAFSIRIKA KUWA NI KUKIRI KUWA KUENEZA UZUSHI HUO HAIKUWA KUTELEZA, BALI ILIKUSUDIWA KWA DHAMIRA FULANI, NA HIVYO KUSHAWISHI HATUA ZAIDI KUCHUKULIWA.
  JESHI NA WIZARA ZITAENDELEA KUSHIRIKIANA NA MAMLAKA HUSIKA KUWABAINI WATU WALIOHUSIKA KUUTUMIA VIBAYA UHURU WA HABARI NA HIVYO KUUPOTOSHA UMMA NA KULETA USUMBUFU KWA FAMILIA YA JENERALI MWAMUNYANGE, JESHI NA TAIFA KWA UJUMLA.
  Imetolewa na Katibu Mkuu, Wizara ya Ulinzi na JKT
  September 26, 2015.

   Jenerali Mwamunyange akikagua gwaride lililoandaliwa kwa heshima yake na mwenyeji wake Rome, nchini Italia.
   Jenerali Mwamunyange akikagua gwaride lililoandaliwa kwa heshima yake na mwenyeji wake Rome, nchini Italia.
  Jenerali Mwamunyange akiteta jambo na mwenyeji wake Rome, nchini Italia.

  0 0

  Na Mwandishi wetu, Bagamoyo
  WATANZANIA wametakiwa kujenga tabia ya kukopa na kurejesha kwa wakati mikopo katika taasisi za fedha kwani huo ni msingi muhimu wa kujipatia maendeleo kwa mtu binafsi na katika ngazi ya taasisi pia.

  Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Afrika, Bw. Mussa Mwachaga amesema mwishoni mwa juma wakati akikabidhi msaada wa Tsh. milioni 10 kwa shule ya Sekondari ya Baobab kuwa uaminifu katika kurejesha mikopo huleta maendeleo ya haraka kwa watu binafsi na taasisi mbalimbali.

  “Hili ni wazi, wale wanaojenga uaminifu na taasisi za fedha hufanikiwa kwa kiwango kikubwa,” alisema.

  Alisema uongozi wa shule hiyo ya sekondari ni mfano hai wa taasisi zilizojijengea uaminifu mkubwa wa kurejesha mkopo na sasa imejijengea mahusiano mazuri ya kuendelea kukopa zaidi na kufikia malengo yake.

  Msaada huo ni sehemu ya ahadi ya Tshs milioni 40 zilizoahidiwa na benki kwa shule hiyo.

  Pesa hizo zitatumika katika ukarabati wa bweni la wasichana ambalo nalo lilijengwa mwaka 2006 kwa mikopo toka benki hiyo.

  Mkurugenzi na mmiliki wa shule hiyo, Bw. Halfan Swai aliipongeza benki hiyo kwa kuamua kumpatia msaada huo ambao utatolewa kwa awamu kwa jili ya ukarabati wa majengo ya shule.

  “Kwa vile jengo hili lilijengwa kwa mkopo wao, leo nimewapa fursa ya kulizindua rasmi,” alisema na kuongeza kuwa kwa heshima ya benki hiyo bweni litapewa jina la ‘Bweni la Benki ya Afrika.’

  Alisema benki hiyo imeisaidia shule yake na kuwa hadi ilipofikia imeshapata mkopo zaidi ya Tshs bilioni 2.

  Alifafanua kwamba siri ya kuendeleza mahusiano na benki ni kurejesha mikopo kwa wakati sababu bila hivyo haiwezekani kuendelea kukopa.

  Meneja wa shule hiyo, Bi. Sophia Mawenya alisema bweni linalokarabatiwa linachukua wanafunzi 408 ambapo kila chumba kina uwezo wa wanafunzi nane.

  “Tunahitaji benki hii iendelee na ushirikiano huu kwa vile malengo yetu ya kujenga shule ya msingi na chuo kikuu bado hayajafikiwa,” alisema.

  Alisema malengo hayo yatafikiwa tu kwa kukopa fedha katika taasisi za fedha kama Benki ya Afrika.

  Katika tukio hilo, wafanyakazi wa benki hiyo walishiriki katika kazi ya kupaka rangi bweni  hilo.

  0 0

   Mgeni rasmi katika Maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Septemba 26,1995, Jaji Mstaafu Osebia Munuo (katikati), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kitabu cha maadhimisho ya miaka 20 cha LHRC yaliyofanyika Makao Makuu ya LHRC Kijitonyama Dar es Salaam jana. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya LHRC, Geoffrey Mmari na Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk.Helen Kijo-Bisimba.
    Mgeni rasmi katika Maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Jaji Mstaafu Osebia Munuo (kushoto), akikata keki maalumu ya Maadhimisho ya miaka 20 cha LHRC yaliyofanyika Makao Makuu ya LHRC Kijitonyama Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya LHRC, Geoffrey Mmari na Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk.Helen Kijo-Bisimba.
   Wimbo wa taifa ukiimbwa kabla ya kuanza maadhimisho hayo.
   Waimbaji wa Kwaya ya LHRC ya Mwalusanya wakiimba wa wimbo wa Taifa.
   Wimbo wa Taifa ukiimbwa.

   Kwaya ya LHRC ya Mwalusanya ikifanya vitu vyake katika maadhimisho hayo.
   Hapa ni Kwaya ya Mwalusanya ikiserebuka kwa kwenda mbele. 'Jamaa wa mbele kushoto yupo vizuri kiuchezaji chezea maadhimisho ya miaka 20 ya LHRC wewe'
   Mwenyekiti wa Bodi ya LHRC, Geoffrey Mmari (katikati), akitoa hutuba fupi katika maadhimisho hayo. Kulia ni Mwakilishi kutoka Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Rehema Ntimizi na kushoto ni Mgeni rasmi wa hafla hiyo, Jaji Mstaafu, Osebia Munuo.
   Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk.Helen Kijo-Bisimba (katikati), akisoma hutuba yake ya maadhimisho hayo. Kushoto ni Mjumbe wa LHRC, Emeliana Mboye.
   Meza Kuu ikionesha Kitabu cha Maadhimisho ya Miaka 20 tangu kuanzishwa LHRC baada ya kuzinduliwa kwenye hafla hiyo. Kutoka kushoto ni Mdau wa LHRC, Profesa Chris Peter,  Mjumbe wa LHRC, Emeliana Mboye, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk.Helen Kijo-Bisimba, Mgeni rasmi wa hafla hiyo, Jaji mstaafu, Osebia Munuo, Mwenyekiti wa Bodi LHRC, Geoffrey Mmari na Mwakilishi kutoka Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Rehema Ntimizi.
   Mdau wa masuala ya haki za binadamu, Ally Said Mwashongo akichangia jambo kwenye hafla hiyo.
   Mgeni rasmi Jaji Osebia Munuo akisoma hutuba yake.
   Wadau wakisoma kitabu hicho baada ya kuzinduliwa.
  Wasanii wakicheza ngoma ya Mganda kwenye uzinduzi huo.


  Na Dotto Mwaibale

  MATUKIO ya ukiukwaji wa haki za binadamu yanayofanywa na vyombo vya dola hususan jeshi la polisi hapa nchini yameongeza kufikia asilimia 60 imefahamika.

  Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk.Helen Kijo -Bisimba Dar es Salaam jana katika sherehe za maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa  LHRC Septemba 26, 1995.

  "Matukio ya ukiukaji wa haki za binadamu kwa vyombo vya dola bado yapo juu ingawa uelewa kwa wananchi kuhusu haki za binadamu ni mkubwa ukilinganisha na miaka ya nyuma wakati tunaanzisha LHRC" alisema Dk. Bisimba.

  Alisema baadhi ya matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu yanayofanywa na jeshi la polisi ni pamoja na kuua raia na kesi zinapofikishwa mahakama zinashindwa kuendelea kwa madai ya kukosekana kwa ushahidi.

  Dk. Bisimba alisema matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu yanayofanywa na wananchi hasa familia ni asilimia 40 ambapo wamekuwa wakijichukulia sheria mkononi ya kuua watu wanaotuhumiwa kwa makosa mbalimbali pamoja na kuvamia vituo vya polisi na kupora silaha.


  Alisema katika kipindi cha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa LHRC jamii imekuwa na uelewa mkubwa wa matukio ya kifisadi yaliyowahi kutokea kama Sakata la Epa, Richmond, ununuzi wa ndege ya rais, mfuko wa kufufua uchumi na Escrow.

  Mgeni rasmi katika hafla hiyo Jaji Mstaafu Osebia Munuo alitoa pongezi kwa LHRC kutimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwake na kutetea haki za binadamu.

  Munuo alikiomba kituo hicho na mashirika mengine kuendelea kuhamasisha wananchi waliojiandikisha kujitokeza kwenda kupiga kura wakati utakapo wadia na kujiepusha na vitendo vyovyote vinavyoweza kuharibu amani ya nchi yetu.

  "Naamini sauti ya kituo cheni cha LHRC ni kubwa hivyo baso muitumie vizuri kuhakikisha makundi yote katika jamii yanashiriki vyema katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu bila ya kubaguliwa" alisema Jaji Munuo.

  0 0


    TAREHE 26-9-2015 jana jumamosi kulifanyika mechi ya ligi kuu ya vodacom Tanzania bara baina y a klabu yetu ya Simba na timu ya Yanga.
  Kwenye mchezo huo timu yetu imepoteza mchezo huo kwa kufungwa goli mbili kwa bila.


  Tumeanza kuandika hvyo hapo juu kwa maksudi kuonyesha sisi Simba tumeyakubali matokeo hayo ya dakika tisini za mchezo na tutumie nafasi hii kiungwana kabisa kuwapongeza watani wetu wa jadi kwa ushindi huo walioupata.

  Pili tumshukuru mungu kwa kutuwezesha kumaliza mchezo huo salama nahapa mungu ashukuriwe sana pamoja na wapenzi wetu pia.sababu washabiki wetu wameonyesha utulivu wa kiunamichezo kwa kutokufanya fujo yoyote licha ya mwamuzi wa mchezo huo Israel Nkongo kuharibu mchezo kwa makusudi.

  Nkongo kwa dhamira ya kusudi jana aliamua kuwatoa wachezaji wetu mchezoni kwa kuanza kugawa kadi kwa wachezaji wetu pasi na sababu na kwa rafu zilezile kuacha wachezaji wa Yanga kucheza bila kuwaonya.
  Kilichoshangaza washabiki wote waliokuwa uwanjani na walioangalia kwenye televisheni ni kumuacha mchezaji wa Yanga Donald Ngoma kuendelea na mchezo ilhali alimpiga kichwa cha maksudi mchezaji wetu Hassan kessi!!

  Mbali ya vitendo hvyo wachezaji wetu wametulalamikia kutukanwa na mwamuzi wa mchezo huo Nkongo. 

  Tunaamini Tff watachunguza malalamiko yetu na kuchukua hatua stahiki kwa mwamuzi huyo ambaye kila mtu aliyeuona mchezo huo anakiri kuwa alishindwa kuumudu. 


  Mwisho na kwa umuhimu wa kipekee klabu ya Simba inaendelea kuwashkuru washabiki kwa utulivu wao licha ya vitendo vya mwamuzi huyo  ambavyo vingeweza kabisa kuharibu amani iliyokuwepo uwanjani jana.
  Tunawaomba waendelee kuwa watulivu katika kipindi hiki ambacho uongozi  wenu umewaandikia TFF na bodi ya ligi ambazo tunaamini zitatenda haki..

  Reclaming our glrory
  Simba nguvu moja
  Imetolewa na Haji S.Manara
  Mkuu wa habari wa Simba


  Simba sports club
  27-9-2015
  Nb.mchezo dhidi ya yanga ushapita na sasa tunajipanga kwa game ijayo.  Tunawaomba wapenzi wetu mjitokeze kwa wingi kwenye mechi yetu dhidi ya Stand united jtano ijayo ya tarehe 30-9-2015

  0 0
 • 09/27/15--04:55: Article 0

 • 0 0

  dickson busagaga & salome mhozya wedding (9)
  Dickson Busagaga (Blogger) na Salome Mhozya katika picha baada ya kufunga ndoa iliyowafanya kuungana na kuwa mwili mmoja tukio lililofanyika katika kanisa la Mt. Teresia wa Mtoto Yesu jimbo kuu la Tabora mnamo tarehe 23 Sep, 2015.
  dickson busagaga & salome mhozya wedding (8)
  Waharusi (Dickson na Salome) wakionesha pete zao mara baada ya kuungana na kuwa kitu kimoja.
  dickson busagaga & salome mhozya wedding (2)
  Hakika ilikuwa ni siku ya furaha sana kwao, hata walipoingia ukumbini katika sherehe ya usiku walidhihirisha kuto kubahatisha kuungana kwao.
  dickson busagaga & salome mhozya wedding (3)
  Furaha ilitawala sana miongoni mwao na waalikwa wote.
  dickson busagaga & salome mhozya wedding (4)dickson busagaga & salome mhozya wedding (5)dickson busagaga & salome mhozya wedding (6)
  MC Ndagula katika ubora wake wa kazi.
  dickson busagaga & salome mhozya wedding (7)
  ZIFUATAZO NI PICHA ZA SENDOFF ILIYOFANYIKA TAREHE 19/09/2015 ORION(TABORA HOTEL)

  salome_mhozya_sendoff (1)
  Picha ya pamoja ya maids, matron na aliyekuwa bibi harusi mtarajiwa
  salome_mhozya_sendoff (2)salome_mhozya_sendoff (3)
  Mrs Patrick na Salome (aliyekuwa bibi harusi mtarajiwa) wakiingia ukumbini
  salome_mhozya_sendoff (4)salome_mhozya_sendoff (5)salome_mhozya_sendoff (6)salome_mhozya_sendoff (7)salome_mhozya_sendoff (8)
  Wazazi wa Salome wakisalimia waalikwa katika sherehe za kumuaga mtoto wao Salome
  salome_mhozya_sendoff (9)salome_mhozya_sendoff (10)
  Wanakamati katika ubora wao wa kukabidhi zawadi za kamati
  salome_mhozya_sendoff (11)
  Dickson Busagaga, Mume halala wa Salome.
  salome_mhozya_sendoff (12)
  Bw. Patrick (Best man)
  salome_mhozya_sendoff (13)salome_mhozya_sendoff (14)salome_mhozya_sendoff (15)salome_mhozya_sendoff (16)salome_mhozya_sendoff (17)salome_mhozya_sendoff (18)salome_mhozya_sendoff (19)
  Picha na aloyson.com -TBN Tabora

  0 0

  Wanachama wa CCM wakiingia katika viwanja vya mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, wakiwa na picha za Wagombea 
  Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ndg Ramadhan Abdalla alipowasili katika viwanja vya Bungu kuendelea na Kampeni zake za kugombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM.
  Mgombea Urais wa Zanzibar pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwasili katika viwanja vya bungi kuaza kwa kampeni yake akiwa na Viongozi wa CCM kushoto Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg Vuai Ali Vuai na kushoto Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ndg Ramadhan Abdalla, wakielekea jukwaa kuu kwa ajili ya mkutano huo. 
  Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakimsikiliza Mgombea Urais wa Zanzibar  kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein. uliofanyika katika viwanja vya bungi.
  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM  Mhe Shamsi Vuai Nahodha akisalimiana naViongozi wa CCM wa Mkoa wa Kusini Unguja baada ya kuwasili katika viwanja vya mkutano wa hadhara wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, uliofanyika viwanja vya mpira bungi. 
  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Viongozi wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja alipowasili katika viwanja vya mpira bungu kuhudhuria Mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein.
   

  0 0

  Dog Domo Baya kachoka lawama  ! Katimuwa wageni wa kamanda Ras Makunja....Kamanda kanuna !


  Kuishi kwingi kuona mengi ! katika hali ya utata juzi kati wageni waliokwenda kumtakia heri ya siku ya kuzaliwa mwanamuziki mahili na kiongozi wa Ngoma Africa band kamanda Ras Makunja kule ujerumani wageni walijikuta wakitimuliwa mbio na mlinzi namba one Kopro Dog Domo Baya wa Kamanda Ras Makunja,mbwa huyo aliyechoka lawama za boss wake kuwa amekuwa mzembe kazini , siku ya jumamosi 19 Septemba 2015 majira ya saa 2.00 usiku aliamua kupiga doria ndani ya makao ya himaya Kamanda Ras Makunja, na kila mgeni aliyegusa au kukaribia geti alibwakiwa na kutemewa kibesi na mbwa huyo.
   
   Timbwili hilo lilichukua muda masaa mawili bila kibosile kamanda Ras Makunja kujua kinachoendelea nje ya nyumba,kwani alikuwa ndani na familia yake.ndipo mmoja wa watu wake wa karibu alipomtumia ujumbe wa simu asitegemee wageni mbwa kachomoka ndani ya banda na akupiga doria ! baadhi ya marafiki wanamlalamikia Dog Domo baya kuwa anachagua watu wa kuwatimua... mbwa huyo anawajua wanamuziki wa Ngoma Africa band aka FFU..lakini wa wageni wengine yeye ni kazi moja tuu

older | 1 | .... | 653 | 654 | (Page 655) | 656 | 657 | .... | 1897 | newer