Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 652 | 653 | (Page 654) | 655 | 656 | .... | 1898 | newer

  0 0

    Kaimu Mkuu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mzumbe ya mkoani Morogoro, Bi. Jemma Kimolo akipokea msaada wa tani 30 za saruji kutoka kwa Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni ya Saruji Tanga (Simba Cement), Diana Malambugi (wa pili kushoto) zilizolewa na kampuni hiyo kusaidia ukarabati wa majengo ya vyoo, mabweni na ofisi za walimu za shule hiyo. Hafla ya makabidhiano ilifanyika Saruji, Pongwe, Tanga jana. Wengine pichani ni maofisa wa kampuni na baadhi ya wanafunzi waliosoma Mzumbe.
    Kaimu Mkuu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mzumbe ya mkoani Morogoro, Bi. Jemma Kimolo akipokea msaada wa tani 30 za saruji kutoka kwa Ofisa Fedha Mkuu wa Kampuni ya Saruji Tanga (Simba Cement), Unguu Sulay (wa pili kushoto) zilizolewa na kampuni hiyo kusaidia ukarabati wa majengo ya vyoo, mabweni na ofisi za walimu za shule hiyo. Hafla ya makabidhiano ilifanyika Saruji, Pongwe, Tanga jana. Wengine pichani ni maofisa wa kampuni na baadhi ya wanafunzi waliosoma Mzumbe. 
    Mwenyekiti wa umoja wa wanafunzi waliosoma Shule ya Sekondari Mzumbe, ya mkoani Morogoro, Edwin Talawa akipokea msaada wa tani 30 za saruji kutoka kwa Meneja Huduma za Jamii na Mawasiliano ya Nje wa Kampuni ya Saruji Tanga (Simba Cement), Bi. Mtanga Noor (wa pili kushoto) zilizolewa na kampuni hiyo kusaidia ukarabati wa majengo ya vyoo, mabweni na ofisi za walimu za shule hiyo. Hafla ya makabidhiano ilifanyika Saruji, Pongwe, Tanga jana. Wengine pichani ni maofisa wa kampuni na baadhi ya wanafunzi waliosoma Mzumbe. 
   Kaimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mzumbe, Bi. Jemma Kimolo akipokea msaada wa tani 30 za saruji kutoka kwa Meneja Usalamaa na Mazingira wa Tanga Cement, Leon Breedt zilizolewa na kampuni hiyo kusaidia ukarabati wa majengo ya vyoo, mabweni na ofisi za walimu za shule hiyo. Hafla ya makabidhiano ilifanyika Saruji, Pongwe, Tanga jana. Wengine pichani ni maofisa wa kampuni na baadhi ya wanafunzi waliosoma Mzumbe. 
   Kaimu Mkuu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mzumbe ya mkoani Morogoro, Bi. Jemma Kimolo akipokea msaada wa tani 30 za saruji kutoka kwa Meneja Mauzo wa Kampuni ya Saruji Tanga (Simba Cement), Samuel Shoo, zilizolewa na kampuni hiyo kusaidia ukarabati wa majengo ya vyoo, mabweni na ofisi za walimu za shule hiyo. Hafla ya makabidhiano ilifanyika Saruji, Pongwe, Tanga jana. Wengine pichani ni maofisa wa kampuni na baadhi ya wanafunzi waliosoma Mzumbe. 

  0 0

   Meneja wa Program wa Restless Development,Oscar Kimaro akizungumza na vijana (Hawapo Pichani )kutoka asasi mbalimbali kuelelekea malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDGs) iliyofanyika katika Makao Makuu Asasi hiyo jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi wa Asasi ya Hope Foundation for Social Interprenuership na Mratibu wa Kampeni ua Beyond 2015 Tanzania,Tumaniel Mangi  akizungumza na vijana  (hawapo pichani) juu ya kuwa mabalozi wa malengo 17 ya SDGs katika mkutano  uliyofanyika Makao Makuu ya Asasi hiyo jijini Dar es Salaam.
  Vijana wakiwasha mishumaa kuashirishia kuonyesha njia ya utekelezaji wa Malengo 17 ya SDGs, katika mkutano  uliyofanyika Makao Makuu ya Asasi hiyo jijini Dar es Salaam.     
       Picha na Emmanuel Massaka.


  Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii
  LEO Septemba 25 hadi 27, wakuu wa nchi 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa wanakutana jijini New York, Marekani  kwa ajenda ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yanayoanzia 2016 -2030.

  Katika mkutano huo, nchi wanachama watapitisha ajenda za (SDGs) zenye Malengo 17 ya ambayo ni kukomesha umaskini, kuhamasisha usawa na kupinga uonevu, na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi,Afya Bora,Upatikanaji wa Maji Safi na Salama,Ujengaji wa Uchumi na Ajira zenye staha,Uboroshaji wa Majiji na Mitaa,Mahusiano ya Kimataifa ,Utawala wa Sheria na Haki na mengine mengi kufikia mwaka 2030.

  Malengo hayo ni dira ya Ulimwengu na kufika mwisho kwa malengo Nane ya Millenia katika kupambana na umaskini ambayo ulimwengu uliazimia kutafikia kwa mwaka 2015.

  Meneja wa Program wa Taasisi ya Restless Develoment,Oscar Kimaro amesema malengo ya  SDGs  ni vijana na wanawajibu kuwa mabalozi  kuhakikisha malengo hayo yanatekelezwa  kutokana na kuwepo kwa changamoto zinazoikabili kama nchi.

  Kimaro akizungumza katika mkutano wa vijana katika kuelekea malengo ya SDGs amesema vijana wanakabiliwa na changamoto kubwa likiwemo suala upatikanaji wa elimu.

  Katika Mkutano wa vijana waliwasha mishumaa kuonyesha njia kwa malengo hayo na viongozi  kuweza kuridhia kama nchi haiwezi kujitenga katika dira hizo ambayo dunia inaatamia.

  Mkurugenzi wa Asasi ya Hope Foundation for Social Interprenuership na Mratibu wa Kampeni ua Beyond 2015 Tanzania,Tumaniel Mangi amesema  malengo ya SDGs yana ushirikishwaji hivyo inahitaji utashi wa kisiasa kusukuma malengo hayo.

  Mangi amesema vijana ni sehemu ya kuleta msukumo chanya kwa kuyasemea masuala ya SDGs kuanzia ngazi ya chini  kutokana na ushirikishwaji uliopo wa malengo hayo.

  0 0

   Mgombea wa jimbo la kibaha mjini kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Sylivesta Koka akisalimiana na wananchi wa kata ya msangani kabla ya kuanza kwa mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi.
   Wananchi wakiwa wanashangilia jambo katika mkutano huo wa hadhara.(Picha zote na Victor Masangu)
   Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibaha Maulid Bundala akiwaonyesha wananchi waliohudhulia katika mkutano huo moja ya  kadi ya chadema iliyorudishwa na mwanachama wa chadema, kulia kwake ni mgombea ubunge jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka.

  NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
  MGOMBEA ubunge wa jimbo la Kibaha mjini Silvestery Koka amesema kwamba endapo akichaguliwa na wananchi  atahakikisha analivalia njuga suala la changamoto inayowakabili wakinamama  wajawato kwa kujenga wodi za kujifunguliwa pamoja na kuongeza vifaa tiba sambamba na kupatiwa matibabu bure  ili kupunguza ongezeko la vifo.
  Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa kampeni kwa wananachi wa kata ya Msangani mgombea huyo amesema kwamba wakinamama wajawazito wamekuwa wakipata usumbufu mkubwa wakati wa kujifungua na wakati mwingine wanapoteza maisha  hivyo ataweka mikakati madhubuti ya kuboresha huduma ya afya lengo ikiwa ni kuokoa maisha yao.
  Koka amebainisha kwamba mpango huo upo katika ilani ya chama cha mapinduzi na utekelezaji wake tayari umeshaanza kufanyika sambamba na kuongeza kasi ya ujenzi wa zahanati ili kuweza kuwasogezea huduma kwa urahisi wananchi wasipate shida ya kupatiwa matibabu.
  Aidha alisema kwamba katika kuboresha sekta ya afya ataweka utaratibu mzuri wa kuhakikisha wazee wote wanapatiwa matibabu bure bila ya kupaata usumbufu wowote na kuwa atakuwa anafanya ziara za mara kwa mara kutembelea zahanati vituo vya afya pamoja na hospititali ili kuweza kubaini changamoto.
  Akizungumzia kuhusiana na changamoto ya  maji katika kata ya Msangani mgombea pamoja na mikakati yake aliyojiwekea kuondokana na kero hiyo mgombea huyo alisema kwa sasa kuna miradi ya maji ipatayo  14   ambayo  imeshatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita na lengo la kuweza kutatua changamoto ya maji.
   Kwa upande wao wananchi wa kata hiyo ya Msangani akiwemo Said Mohamed na  Rashid Abed  awakusita kuzungumzia  changamoto zinazowakabili hususan suala la maji ambalo kwa upande wao limekuwa ni kero kubwa kutokana na kutembea umbali wa kilometa nane kwa ajili ya kwenda kufuata  maji.
  Walisema kwamba kwa sasa wana imani endapo mradi huo wa maji ukikamilika utaweza kuwanufaisha kwa kisi kikubwa na kutatua kero ya maji ambayo imekuwa ni kilio cha siku nyingi kwa wakazi wa kata ya msangani.
  “Kwa upande wetu kwa sasa tunaona juhudi ambazo zinafanywa na mbunge ambaye alimaliza muda wake tumeshuhudia baadhi ya maeneo wameshaaza kupata maji safi na salma hivyo kitu kikubwa kwa mgombea ambaye tutamchagua alitilie mkazo suala la maji ili tusiweze kusumbuka kutembea umbali mrefu,”alisema wananchi hao.
  Wananchi wa kata ya Msangani kwa sasa bado  wanakabiliwa na  changamoto mbali mbali katika sekta ya afya hususan wakinamama wajawazito pamoja na huduma ya maji hivyo kunahitajika kufanyike  juhudi za makusudi kwa viongozi watakaochaguliwa kuhakikisha    wanatafuta njia mbadala kuzitatua kero hizo.

  0 0

   Mfanyaakzi wa Airtel, (kulia), akijaza fomu ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari (Wote Scheme), wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakati wa ufunguzi wa wiki ya Wafanyakazi wa Airtel, makao makuu ya kampuni hiyo ya simu za mikononi, jijini Dar es Salaam, Septemba 26, 2015.

   Wafanyakazi wa Airtel, wakipatiwa maelezo juu ya huduma mbalimbali zitolewazo na PPF, wkati wa wiki ya wafanyakazi wa kampuni hiyo ya simu makao makuu ya Airtel, Morocco jijini Dar es Salaam, Septemba 26, 2015.

   Meneja Masoko wa PPF, Elihuruma Ngowi, (kulia), akizungumza jambo na Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mbando, wakatyi wa ufunguzi wa wiki ya Wafanyakazi wa Airtel


  NA K-VIS MEDIA

  MFUKO wa Pensheni wa PPF, umevuna wanachama wapya kadhaa kwenye Wiki ya Wafanyakazi wa kampuni ya simu za mikononi, Airtel, iliyoanza leo Septemba 26, 2015 pale makao makuu ya Airtel, Morocco jijini Dar es Salaam.

  Akizungnumza na waandishi wa habari wakati wa utoaji huduma kwa wafanyakazi hao, Meneja Masoko wa PPF, Elihuruma Ngowi, amesema, Airtel ni moja ya “Akaunti’ kubwa za PPF, kwa maana ya Mfuko kuwa na idadi kubwa ya wanachama kutoka kampuni hiyo, hivyo wameitumia fursa hiyo kutoa elimu ya huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko.

  “Pamoja na kusajili wanachama wapya chini ya Mpangop wa Wote Scheme, yaani ucnangiaji wa hiari, pia tumewaeleza wanachama wetu kuhusu mafao mapya yatolewayo na Mfuko kama fao la Uzazi.” Alifafanyua Ngowi.

  Meneja Msoko huo wa PPF pia alisema, Wanachama wa PPF kupitia mpango huo wa wote scheme, wanaweza kujiunga na bima ya afya ya NHIF, ambapo PPF inakuwa mdhamini wa wanachama wake kupitia mpango huo wa uchangiaji wa hiari (Wote Scheme).

   Afisa Uwekezaji Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Anna Shayo, (kulia), akimsikiliza Mwanachama wa Mfuko huo, wakati wa utoaji huduma kwenye wiki ya wafanyakazi wa kampuni ya simu za mikononi ya Airtel, makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam

   Afisa wa Operesheni wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Kanda ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Saluna Aziz Ally, (kushoto), akimeuelekeza Mwanachama wa Mfuko huo jinsi ya kupata taarifa za michango yake kupitia simu ya mkunoni, huduma ijulikanayo kama “PPF Taarifa), wakati wa ufunghuzi wa wiki ya wafanyakazi wa Airtel, iliyoanza leo Sptemba 26, 2015 pale makao makuu ya kampuni hiyo ya simu za mikononi, Morocco jijini Dar es Salaam

   Mwanachama mpya wa PPF Sitti Mweneyuni, akijaza fomu za kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari (Wote Scheme), wakati wa ufunguzi wa wiki ya wafanyakazi wa kampuni ya simu za mikononi, Airetel, jijini Dar es Salaam

   Mwanachama mpya wa PPF akijaza fomu za kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari (Wote Scheme), wakati wa ufunguzi wa wiki ya wafanyakazi wa kampuni ya simu za mikononi, Airetel, jijini Dar es Salaam

   Afisa Operesheni wa Kanda wa Mfuko wa Pensehni wa PPF, Upendo Singinika, (kulia), akimpatia zawadi mwanachama wa Mfuko huo baadab ya kupatiwa maelezo ya huduma mbaklimbali zitolewazo na Mfuko huo, kwenye ufunguzi wa wiki ya wafanyakazi wa Airtel makao makuu ya kampuni hiyo ya simu za mikononi jijini Dar es Salaam

   Afisa Masoko wa PPF, Francis Kihinga, akimpatia maelezo ya kina mwanachama wa PPF

   Abib Kibiki, (kushoto), Afisa Masoko wa PPF, akimpatia maelezo Mfanyakazi huyu wa Airtel, wakati wa wiki ya wafanyakazi wa Airtel

   Afisa operesheni wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Upendo Singinika, (kulia), akishauriana jambo na Mtaalamu wa mifumo ya Computer wa Mfuko huo, Gideon Mwashihongo, wakati wa wiki ya wafanyakazi wa Aiortel,ambapo PPF ilitumia fursa hiyo kusajili wanachama wapya chini ya mpango wa Wote Scheme

  Mfanyaakzi wa Airtel, (kulia), akitumia simu yake ya mkononi, kupata taarifa za michango yake ya uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, kupitia huduma ya PPF Taarifa

  0 0


  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA

  Simu: 255-22-2114615, 211906-12

  Barua pepe: nje@nje.go.tz

  Barua pepe: gcu@nje.go.tz

  Nukushi: 255-22-2116600

                

   


                  20 KIVUKONI FRONT,

                             P.O. BOX 9000,

                    11466 DAR ES SALAAM, 

                                      Tanzania.


   

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
    
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kufariki kwa Mahujaji zaidi ya 700 na wengine zaidi ya 800 kujeruhiwa wakati wakishiriki ibada ya Hijja iliyofanyika Makkah, Saudi Arabia tarehe 24 Septemba, 2015.


  Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ubalozi wa Tanzania, Saudi Arabia

  Mahujaji hao walifariki na kujeruhiwa kutokana na msongamano mkubwa wa watu uliotokea kwenye eneo la Mina.


  Aidha, taarifa hizo zinaeleza kuwa hadi sasa Mahujaji wapatao watano (5) kutoka Tanzania wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa. Majina ya Watanzania waliofariki na kutambuliwa ni Bi. Mwanaisha Hassan Juma, Mkungwe Suleiman Hemedi na Sefu Saidi Kitimla. Mtu mwingine aliyefariki ni Raia wa Kenya anayeishi nchini ambaye ametambulika kwa jina la Bi. Fatuma Mohammed Jama.


  Ubalozi unaendelea na jitihada za kupata jina la Mtanzania mwingine aliyefariki kwenye tukio hilo. Aidha, Serikali ya Saudia imetangaza kuwa itatoa taarifa kamili ikiwemo idadi ya watu waliofariki na majeruhi na nchi wanazotoka mara itakapokamilika.


  Pia Ubalozi wetu kwa kushirikiana na Taasisi zinazoshughulikia masuala ya Hijja za Tanzania ikiwemo BAKWATA pamoja na Mamlaka za Serikali ya Saudi Arabia unaendelea kufuatilia kwa karibu ili kujua endapo kuna vifo na majeruhi wengine kutoka Tanzania.


  Hivyo basi, Wananchi wanaombwa kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu wakati Serikali ikiendelea kufuatilia.
  Imetolewa na:

  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,

  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,

  Dar es Salaam

  25 Septemba, 2015

  0 0

  Na Muwandishi wetu Swahilivilla Washington DC 

  Waislamu kote ulimwenguni jana waliadhimisha Siku Kuu ya Idd Al-Adh'ha kwa Ibada na sherehe mbalimbali.Wanadiaspora wa Tanzania noa walijumuika na Waislamu wenzao ulimwenguni kuadhimisha siku hiyo muhimu katika Dini ya Kiislamu.
  Baadhi ya waumini wa Tanzanian Muslim Community Washington DC wakipata picha ya pamoja baada ya kumaliza sala ya Eid Al-Adhw-haa iliosaliwa Siku ya Alhamis Sept 24, 2015 katika msikiti wa Islamic Center New Hampshire Maryland US.( Picha zote na swahilivilla.blogspot.com)
  Katika kuadhimisha siku hiyo, Jumuiya ya Waislamu wa Tanzania waishio katika jiji la Washington na vitongoji vyake (TAMCO), iliandaa sherehe iliyoendelea hadi usiku katika viwanja vya wazi.
  Akizungumza na Swahilivilla, mmoja wa wanachama wa jumuiya hiyo Bwana Abubakar Qullatein, aliiambia Swahilivilla kuwa amefurahi kuadhimisha siku hii adhimu katika dini ya Kiislamu. Hata hivyo furaha yake hiyo imeingiwa na dosari kutokana na maafa ya ajali zilizotokea huko Makka, Saudi Arabia zilizosababishwa na moto na mkanyagano wa watu.
  Bwana Abubakar Qullatein, akipata picha ya 
  pamoja na Abou Shatry baada ya swala ya Eid.
  "Iddi hii imekumbwa na misukosuko kidogo kutokana na ajali za hapa na pale zilizotokea, sehemu mbalimbali duniani, na hata huko Makka", alielezea masikitiko Bwana Qullatein, na kendelea kusema kuwa, Iddi hii inakuja baada ya kukamilika kwa Ibada ya Hijja, kwa hivyo kwenye Hijja yenyewe kukitokea ajali kama hizi, inaleta huzuni.
  Aliwatolea wito Waislamu kuondoa shari na fitna miongoni mwao na kuitetea Dini yao kwa kuonesha tabia na mtendo mema, jambo ambalo litasaidia kuondosha chuki kutoka kwa wasiokuwa Waislamu.
  "Waislamu tushikamane, tupendane, tuondoe fitna na shari, tuwe kitu kimoja, tuoneshe tabia nzuri na mahusiano mema na watu wa dini nyengine, hii itasaidia kuondoa chuki zao" alihubiri Sheikh Qullatein, na kuelezea matumaini yake kuwa kuadhimisha Siku Kuu ya Idd Al-adh'ha siku moja kote ulimwenguni, kutakuwa ni mwanzo wa kuelekea kufunga na kufungua Ramadhani kwa pamoja.
  Kwa upande wake, Mratibu wa sherehe za Siku Kuu wa TAMCO Bibi Asha Harris, aliiambia Swahillivilla kuwa, siku hii kama ilivyo adhimu kwa Waislamu kote ulimwenguni, pia ina umuhimu mkubwa kwa Jumuiya yake.
  Bi Asha Hariz, kulia, akipata picha na  waumuni wa Tanzanian Muslim Community Washington DC, kwa chai ya asubuhi."Siku hii ina umuhimu mkubwa kwa jumuiya yetu, kwa vile tunapata fursa ya kujumuika pamoja, na kuhuisha upendo na ushirikiano miongoni mwetu", alielezea Bi Hariss, na kuendelea kuwa ''Maadhimisho haya tunayagawa katika sehemu mbili; asubuhi na jioni"
  Katika sehemu ya subuhi, Bi Harris ameelezea kuwa, mara tu baada ya Swala ya Iddi Wanajumuiya hukutana katika ukumbi maalum na kujipatia chai na vitafunio vyepesi. "Lakini kabla ya chai, kwanza huanza kwa Dua maalum ili kuwaombea wazee wetu na wenzetu wengine waliotangulia mbele ya Haki", alifafanua Bi Hariss.
  Baada ya sehemu hiyo kumalizika, Wanajumuiya huondoka na baadaye kukutana tena jioni ili kuanza sehemu ya pili ya sherehe za Iddi Al-Adh'ha.
  "Baadaye tunakutana tena jioni kwenye viwanja vya wazi kwa ajili ya nyama-choma na shamra-shamra nyengine" aliendelea kufafanua Bi Harris, na kusema kuwa sehemu hii ya pili ina umuhimu mkubwa zaidi, kwa vile huwajumuisha Watanzania wote hata wasiokuwa Waislamu.
  Miongoni mwa vibwagizo vya sherehe hizo ni pamoja na michezo na mashindano ya watoto. Watoto hupata nafasi ya kupokea zawadi za aina mbalimbali, na kwa wale wanaoshinda kwenye mashindano yaliyoandaliwa hupata zawadi za nyongeza.
  Mashindano ya watoto hujikita zaidi kwenye umuhimu wa Siku Kuu ya Idd Al-Adh'ha. "Tunafanya chemsha bongo kwa jili ya watoto, na maswali yote hujikita kwenye kuwahamasisha watoto juu ya umuhimu wa siku hii", alisema Bi Hariss.
  Aliidokeza kuwa hapo awali, TAMCO ilikuwa inafanya sherehe za Idd wakati wa jioni tu, lakini katika miaka ya karibuni ikaonekana umuhimu wa kuwepo kwa sehemu ya asubuhi ambayo mbali na chai hujikita zaidi kwenye dua na maombi kama ilivyo ada nyumbani Tanzania.Katika Jimbo la Washington, Watanzania nao hawakuwa nyuma katika kuadhimisha Siku Kuu ya Idd A-Adh'ha.
  Bwana Adullah Kidume, alisema kuwa, Waislamu wa Tanzania waishio katika jiji la Seattle na vitongoji vyake walikodi ukumbi maalum kwa jili ya Swala ya Iddi.Akizungumza na Swahilivilla kutoka Tacoma, Bwana Kidume alisema kuwa ni ada ya Waislamu katika maeneo hayo kukodi ukumbi kwa jili ya Ibada, na baadaye kuendelea na sherehe za kawaida.
  Licha ya kutokuwa na Jumuiya rasmi, Waislamu wa Tanzania katika eneo hilo wameweza kudumisha ada ya kujumuika pamoja katika Siku Kuu mbalimbali za kidini. "Ni sisi wenyewe tu Waislamu tunaojuana...., siyo Kamati rasmi" alisema Bwana Kidume.Hapo awali Waislamu hao walikuwa hukutana kwa ajili ya Swala tu, lakini, juhudi za akina mama ndizo zilizozaa wazo la kuendeleza sherehe hizo ambazo hudumu mpaka usiku wa manane.
  Miongoni mwa vikorobwezo vya sherehe hizo ni pamoja na vyakula vya aina mbalimbali vinavyoonyesha ustadi wa mapishi ya Kitanzania, mavazi, michezo na mengineyo.
  Licha ya Ibada ya Hija mwaka huu kukumbwa na maafa ya moto na watu kufariki dunia kutokana na mkanyagano huko Makka, hata hivyo, Hija hiyo imekuwa na umuhimu wa aina yake kwa baadhi ya Wazanzibari kwa vile ni mara ya mwanzo bendera ya Zanzibar imepepea katika Maeneo hayo Matakatifu.
  Akiongea na mwandishi wetu kutoka Dar es Salaam, Bwana Omar Abdullah ameelezea furaha yake kuona bendera ya Zanzibar ikipepea katika Hija ya mwaka huu. 
  "Tulipopata taarifa za maafa kule Makka, Moyo wangu uliingiwa na huzuni.., japokuwa hakuna ndugu yangu, lakini Waislamu wote ni ndugu", alisema Bwana Abdullah, na kuongeza kuwa "lakini kitu kilicholeta furaha katika Siku Kuu hii kwangu, ni kuiona bendera ya Zanzibar ikipepea kule, japo kuwa kwa juu kulikuwa na kibendera kidogo cha Tanzania".
  Alielezea matumaini yake kuwa katika Hija ya mwakani, Mahujaji kutoka Zanzibar watabeba bendera yao kamili bila kuwa na kibendera chengine ndani yake. Angalia Taswira mbali mbali za Eid Al- Adhw-haa Washington DC hapa

  0 0

  Taarifa mpya kutoka kwa familia ya Jullu inasema kuwa mtoto wao Loveness Coletha aliyepotea na yaya wake amepatikana na mzazi wake amesafiri kwenda jijini Mwanza kumchukua.

  Tunashukuru wote waliojumuika kuifariji familia kwa maneno ya kutia moyo, walioguswa na kuombea matumaini kwa sala, wote waliosambaza ujumbe kwa njia mbalimbali na zaidi sana, kwa watendaji wote wa mamlaka husika waliofanya kazi yao katika kufanikisha hili.

  Asanteni!

  0 0

  Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Mererani, katika Mkutano wa Kampeni zake, uliofanyika kwenye uwanja wa Machinjioni, Simanjiro Mkoani Manyara leo Septemba 25, 2015.

  Sehemu ya Wananchi wa Mji wa Mererani, Jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara wakionyesha furaha yao mbele ya Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, wakati akiwahutubia katika Mkutano wa Kampeni zake, uliofanyika kwenye uwanja wa Machinjioni, Mererani, leo Septemba 25, 2015.
  Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye, akivishwa vazi maalum la jamii ya watu wa Kimasai, wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye uwanja wa Machinjioni, Mji wa Mererani, Simanjiro Mkoani Manyara leo Septemba 25, 2015.
  Meneja wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, John Mrema akizungumza na Wananchi wa Mji wa Mererani, Jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara. 
  Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye, akipokea kadi za wanachama wa CCM walioamua kurudisha kadi na kujiunga na UKAWA, wakati wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye uwanja wa Machinjioni, Mji wa Mererani, Simanjiro Mkoani Manyara leo Septemba 25, 2015.
  Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye, akizikusanya kadi hizo baada ya kuzipokea.
  Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye, akiwahutubia Wananchi wa Mji wa Mererani, Jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara. 
  Aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Ole Zanzibar, Mh. Rajab Mbarouk akiwahutubia Wananchi wa Mji wa Mererani, Jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara. 

  0 0

  Maelfu ya Wakazi wa Mji wa Kahama na Vitongoji vyake wakimsikiliza  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akimwaga sera zake na kujinadi kwa kuwaomba wampigie kura ya ndio asubuhi na mapema Oktoba 25 mwaka huu kwenye uchaguzi mkuu,ili aibuke mshindi na kupata ridhaa ya kuwaongoza Watanzania katika awamu ya tano.
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia maelfu ya Waananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni,uliofanyika katika viwanja vya CCM mjini Kahama jioni ya leo.

  Dkt.Magufuli leo amefanya mikutano yake ya kampeni  katika wilaya za Mbogwe, Bukombe mkoani Geita  na baadae halmashauri mpya ya Ushetu baadaye mkutano mkubwa wa kampeni  uliofanyika mjini Kahama mkoani Shinyanga na kuhudhuriwa na umati wa watu uliorushwa moja kwa moja na kituo cha Televisheni cha Star TV .

  Akizungumza katika mkutano huo wakati akiwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi Oktoba 25 mwaka huu kumpigia kura za ndiyo,Dkt Magufuli amesema kuwa Serikali yake itashughulikia migogoro ya madereva na kuhakikisha wanapata mikataba kutoka kwa waajiri wao ili kuboresha maslahi yao.

  Amesema Madereva ni watu muhimu katika sekta ya usafirishaji na wanafanya kazi ngumu,lakini maslahi yao hayatiliwi maanani,hivyo amesema kuwa atahakikisha yanaboreshwa ili na waone faida ya kazi yao,na iwe yenye kuthaminika ,hivyo serikali ya awamu ya tano itakayoongozwa na Dk. John Pombe Magufuli italifanyia kazi ipaswavyo.
  Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Wilaya ya Bukombe mapema leo mchana,alipokuwa akielekea mkoani Shinyanga kuendelea na kampeni zake za kuomba ridhaa kwa wananchi ya kuiongoza Tanzania katika kipindi cha awamu ya tano.
   Mjumbe wa kamati ya ushindi ya kampeni za Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli,Mh.Samweli Sitta akiwahutubia wananchi wa mji wa Kahama jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni za Urais,uliofanyika kwenye viwanja vya CCM mjini humo na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu,Mh.Sitta a.k.a Mzee wa viwango na kasi pia alimnadi Dkt Magufuli na kumwombea kura kwa wananchi hao za ushindi na hatimaye akaibuke mshindi kwa nafasi ya Rais na kupata ridhaa ya kuwaongoza Watanzania katika kipindi cha awamu ya tano.
   Maelfu ya wananchi wa mji wa Kahama wakiwa wamekusanyika mkutano wa hadhara wa kampeni,uliofanyika katika viwanja vya CCM mjini Kahama jioni ya leo.
  Mgombea Urais wa CCM Dkt Jonh Pombe Magufuli akiwanadi Mgombea Ubunge wa Kahama Ndugu Jumanne Kishimba pamoja na Mgombea Ubunge wa jimbo la Msalala Ndugu Ezekiel Maige mbele ya maelfu ya wakazi wa mji huo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
  Wachimbaji wadogo wadogo waishio eneo la Nyarugusu,Wilayani Geita wakimshangilia mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli mapema leo jioni alipokuwa akielekea mkoani Shinyanga kuendelea na kampeni zake.

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano wa 70 wa Umoja wa Maiataifa akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na ushurikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe, Waziri wa Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto Mhe Sophia Simba, Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Yussuf Mzee na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi  Liberata Mulamula 
   Rais Kikwete akiwa na Waziri Mkuu wa Denmark Mhe. Lars Loekke Rasmussen 
   Rais Kikwete akiwa na Rais mstaafu wa Finland Mama Tarja Halonen
   Rais Kikwete na ujumbe wa Tanzania Waziri wa Mambo ya Nje na ushurikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe, Waziri wa Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto Mhe Sophia Simba, Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Yussuf Mzee,  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi  Liberata Mulamula na .Balozi Tuvako Manongi, Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa.
   Rais Kikwete na Waziri Mkuu wa Bahamas Mhe Perry Christie. Hapo Mhe Rais alimfahamisha Waziri Mkuu huyo kwamba yey anamaliza muda wake na Waziri Mkuu akaeleza matumaini yake kwamba atakayemrithi ataendelea kuimarisha uhusisno wa Tanzania na Bahamas na nchi za Caribbean.  
  Rais Kikwete akiwa na Rais Filipe Jacinto Nyusi wa Mzumbiji na mawaziri wao wa nchi za nje
  Rais Kikwete na Ujumbe wake wakimlaki Baba Mtakatifu Francis alipowasili kuhutubia Umoja wa Mataifa kwa mara ya kwanza. Picha kwa hisani ya Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa.

  0 0

   Taarifa zinazosambaa kumhusu Mkuu wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) Jenerali  Davis Mwamunyange zilizosambaa kwenye mitandao ya jamii kwamba amekula chakula chenye sumu na amekimbizwa jijini Nairobi nchini Kenya kwa matibabu hazina ukweli wowote.Ni uzushi.

  Kwa mujibu wa taarifa za familia ya Jenerali Mwamunyange pamoja na makao makuu ya jeshi ambazo Globu ya Jamii imezisaka na kuzipata, kiongozi huyu wa JWTZ hivi sasa yupo nchini Italia kwa ziara ya kikazi ya siku tisa kama anavyoonekana pichani na hajambo kabisa na yu bukheri wa afya.
  Hii ni changamoto kwa wakala wa mawasiliano nchini (TCRA) ambayo imekuwa ikilaumiwa kwa ukimya wake wa kutochukua hatua thabiti kuthibiti uongo kama huu kwa kuwatafiti, kuwabaini na kuwachukulia hatua watu kama hawa wenye nia ya kuleta taharuki na machafuko nchini.
  Wananchi wengie waliohojiwa na Globu ya Jamii wanahoji endapo kama kweli TCRA ipo na kama ipo ina vifaa vya kisasa iliyodai wanavyo kuwabaini watu kama hawa, na kwa nini hawajafanya kweli toka sheria ya mitandao (Cyber Law) iliyoanza kutumika.
  "Endapo kama TCRA watashindwa kumnasa mhusika wa uongo huu wa kuogofya, inabidi mamlaka husika iangalie upya ajira ya watendaji wake maana kama taasisi nyeti kama JWTZ inaguswa na wao wakae kimya tu basi ujue kuna tatizo ambalo inapaswa Serikali ilifanyie kazi", amesema msomaji mmoja wa Globu ya Jamii katika maoni yake.


  0 0  0 0

  Na Mwandishi Wetu, 
  IBRAHIM (jina limebadilishwa) alizaliwa nchini Tanzania na alipokuwa na umri wa miezi 9 tu alionekana anang’aa na hakuwa na uwezo wa kula na kukua vizuri kama watoto wengine wa umri wake.

   Alikuwa na maambukizi ya mara kwa mara na vipimo vya damu vilionyesha upungufu mkubwa wa damu na kiwango cha ukosefu wa damu kwa gm 3.5! Ibrahim alikuwa akiishi na chini ya robo ya kiwango cha oksijeni kinachohitajika kwenye damu na alihitaji haraka kuongezewa damu ili kuokoa maisha yake. 

  Vipimo vya damu yake na ya wazazi wake vilithibitisha kuwa alikuwa na thalasemia kuu.

  Thalassaemia kuu ni hali ya kurithi ambapo huwa na ukosefu wa chembe nyekundu za damu. Katika mwili seli shina Uboho huzalisha aina tatu za seli za damu katika mwili- nyekundu, nyeupe na chembe chembe za damu. Thalasemia ni hali ya kurithi inayoathiri seli nyekundu za damu. Hutokea wakati mtu anashindwa kuzalisha kiasi cha damu kinachotakiwa. Mwili wako hautafanya kazi vizuri kama chembechembe nyekundu za damu hazizalishi damu ya kutosha yenye afya.

  Dkt. Revathi Raj wa  Hospitali za Apollo Chennai anaeleza zaidi kwamba thalasemia ni ya kurithi. Ni kutoka kwa wazazi kwenda kwa watoto kwa njia ya jeni. Watu ambao hurithi jeni za damu mbaya kutoka kwa mzazi mmoja lakini jeni za kawaida kwa mzazi mwingine wanaitwa kitaalamu ‘career’. ‘Carriers’ mara nyingi hawana dalili za ugonjwa mwingine zaidi ya kuoneshwa upungufu mkubwa wa damu. 

  Hata hivyo, wanaweza kurithisha jeni mbaya kwa watoto wao. Watu ambao wana wastani wa kati wa thalasemia wamerithi jeni mbaya kutoka kwa wazazi wote wawili. Kama ‘carriers’ wawili wakizaa mtoto, kuna 25% ya nafasi ya kuwa na mtoto aliyethirika.
  Kwa mujibu wa Dkt Revathi Raj madhara ya kuacha thalassaemia bila kutibiwa ni pamoja na kushindwa kwa wengu, ini na moyo. Pia, inaweza kusababisha mifupa myembamba na migumu na mikunjo usoni. Ni kawaida kwamba watoto wasiotibiwa hudumaa ukuaji wa mwili na akili. Watoto wenye Thalasemia huwa wanakufa kutokana na moyo kushindwa kufanya kazi na maambukizi ikiwa hali hiyo haitatibiwa.
  Matibabu pamoja na kuongezewa damu mara kwa mara na dawa za kuzuia maambukizi huweza kupunguza kasi ya ugonjwa. Watoto wenye thalasemia wanaweza kutibiwa kwa kuongezewa damu mara kwa mara. Zoezi hili linatakiwa kufanyika kila baada ya wiki 3 au 4 na husaidia kuweka kiwango cha damu kawaida. Wakati viwango vya damu vikiwa kawaida mtu anaweza kujaribu kuzuia baadhi ya matatizo ya ugonjwa kwa hiyo kuzuia moyo kushindwa kufanya kazi na ulemavu wa mfupa na hivyo kupelekea ukuaji mzuri na afya kwa ujumla.
  Hali ya Ibrahim ina maana kwamba wazazi wake walihitaji kusafiri pamoja naye kwa zaidi ya km 1,000 kila mwezi kwa ajili ya kuongezewa damu kutokana na ukosefu wa vifaa vya kutosha Tanzania. Huku kuongezwa damu kulihitajika ili kuendelea kwa maisha yote ya Ibrahim hii ikiwa ni hali ya kudumu.

  Wangewezaje kutoa damu kila mwezi? Kwa nini hakuna mtu aliyegundua kwamba walibeba jeni mbovu ambazo zinaweza kuleta madhara kwa mtoto wao? Haya ni baadhi tu ya maswali kadhaa ambayo wazazi wa mtoto huyu wanakabiliwa nayo.


  Changamoto nyingine iliyowakumba wazazi Ibrahim ililikuwa kwamba pamoja na kila kuongezewa damu kuna hatari ya madini chuma katika kila kiasi cha damu kinachoongezwa. 

  Kujijenga kwa madini chuma husababisha uharibifu wa moyo na ini na viungo vingine. Kuepuka, kuzuia au kuchelewesha madini chuma kujijenga mtu anahitaji tiba ya madawa kila siku. Kwa bahati mbaya hata hivyo, kwa Tanzania tiba hii si rahisi hivyo kupatikana.

   Maisha kwa Ibrahim yalionekana hatarini sana mpaka baada ya familia kusikia kuhusu BMT kusaidia kumtibu mtoto wao mdogo na kusafiri hadi Hospitali ya Apollo, Chennai nchini India ambako walikutana na Dkt Revathi Raj. Hospitali ya Apollo, India ni jina la kuaminiwa katika BMT kwa ajili ya wagonjwa wa kimataifa, kama hospitali ina si tu yenye timu ya BMT inayosifika, lakini pia masharti magumu sana kudhibiti maambukizi ambayo ni muhimu kwa ajili ya wagonjwa wa BMT.
  Kwa BMT ‘Haematopoietic’ seli shina inapatikana kutoka kwa ndugu ambaye hajaathirika anayeendana au mfadhili yeyote na kupandikizwa kwa mtu mwenye thalasemia. Kwa bahati mbaya, Ibrahim hakuwa akiendana na wafadhili wa familia. Hata hivyo, mfadhili waliyeendana kikamilifu katika shina kiini la uboho aliyejisajili nchini India aitwaye DATRI alitoa mwanga mpya wa matumaini.
  Mkakati wa kupandikiza uboho kwa watoto katika Hospitali ya Apollo nchini India ina timu ya wataalam wenye ujuzi wa juu na mratibu wa BMT anayefanya kazi kama sehemu ya timu ya wataalam mbalimbali kutoa huduma iliyoboreshwa kwa ajili ya watoto ambao wanapata tiba ya shina. Hospitali za Apollo nchini India zina uzoefu mkubwa nchini humo katika kuhudumia watoto wachanga na wadogo wanaoendelea na upandikizaji wa seli za shina.

  BMT ni tiba yenye hatari kubwa ambayo inawezekana kwa asilimia ndogo sana ya wagonjwa iwapo mfadhili uboho anayefaa yupo. Hata kama kiwango cha mafanikio ya BMT ni sawa na 95%, ni kazi ya hatari na huweza kusababisha kifo. Kiwango cha mafanikio hutegemea zaidi iwapo au hakuna uharibifu mkubwa uliofanyika kwa kiungo chochote kama vile madini chuma kwenda mahali pasipofaa.

  Dawa mpya katika soko na muendelezo wa ugunduzi katika taaluma ya utabibu imewezesha mchakato wa upandikizaji kuwa salama zaidi, hata kwa watoto wachanga na watoto wadogo. Hospitali Maalum ya Apollo, imelifanya upandikizaji wa seli shina kwa zaidi ya wagonjwa 800 ikiwa zaidi ya robo kati yao waliokuwa na thalasemia na zaidi ya kufanikiwa kwa Zaidi ya 90%.

  Ujumbe muhimu zaidi mtu anahitajika kuchukua katika hili ni umuhimu wa kupima wajawazito. Vipimo vya damu vinaweza kuonyesha kama mtu ana thalasemia au ni ‘carrier’ kwa kuwa kinga ni bora kuliko tiba. Dkt Revathi Raj katika Hospitali ya Apollo Chennai anashauri kuwa ni bora kumweleza daktari wako kumpima mtoto wako kiwango cha ‘ferritin’ cha mtoto wako kama ana upungufu wa damu kabla ya maagizo ya vitamini yoyote. 

  Ni jambo la kawaida kwa madaktari kutoa maelekezo ya vitamini kwa watoto ambazo huonyesha dalili za upungufu wa madini chuma. Hata hivyo, ni muhimu kuchunguza tahadhari, kwa maagizo ya kuongeza madini chuma kwa ajili ya upungufu wa madini hayo anemia inaweza kuwa sahihi, inaweza kusababisha kuzidi kwa madini chuma kwa watoto wenye aina yoyote ya thalasemia. Jaribio rahisi kuamua kiwango cha madini chuma, au kiwango cha ‘ferritin’, katika mwili wa mtu linaweza kufanywa.

   Kama mtu anaonekana kuwa na upungufu wa madini chuma, lakini kiwango cha ‘ferritin’ kipo kawaida, pengine wana aina ya kwanza ya ‘beta thalasemia’.

  Ndugu kuoana mara kwa mara pia husababisha mtu kuwa ‘carrier’ wa thalasemia. Ndoa kati ya ndugu ziepukwe kwa kuwa kuna ongezeko la ugonjwa wa kurithi na kama inaepukika uchunguzi wa damu kwa wanandoa kabla ya ndoa unashauriwa.

  Tunahitaji pia kuongeza uelewa miongoni mwetu Watanzania juu ya umuhimu wa kujitolea kwa kuchangia damu na seli za shina kama msaada kuokoa maisha haya. Kuna matumaini kwa watoto wote kupata nafasi ya tiba kwa kuwa kuna wengi waliojisajili – hasa watu wazima ili kusaidia wagonjwa wote wa thalasemia kuu.
  Imechangiwa na:

  Dkt. Revathi Raj
  Mtaalamu wa magonjwa ya watoto ‘Hematology’, Kupandikiza uboho (BMT)
  Apollo Hospitals Chennai

  0 0

  Msafara wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan ukiwasili mkoani Morogoro leo ukitokea mkoani Dodoma.
  Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, MamaSamia Suluhu Hassan akimsalimia Katibu wa CCM mkoa wa Morgoro Rojas Rumuli wakati wa mapokezi yake, alipowasili mkoani Morogoro kufanya mikutano ya kameni katika mkoa huo leo
  Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimsalimia mgombea Ubunge Jimbo la  Gairo, Ahmed Shabby wakati alipowasili mkoani Morogoro, kufanya mikutano ya kampeni mkoani humo.
  Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwapungua mkono wananchi waliofika kumlaki alipowasili mkoani Morogoro leo. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa na wapili ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro, Inocen Karogeresi
  Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Gairo A, kuhutubia mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Gairo mkoani Morogoro.
  Baadhi ya wananchi wakiwa na mabango kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika jimbo la Gairo leo.
  Katibu wa CCM, mkoa wa Morogoro, Rojas Romuli akihutubia wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika viwanja vya shule ya msingi Gairo A katika jimbo la Gairo mkoani Morogoro
  Mgombea Ubunge jimbo la Gairo Sadik Ahmed Shabiby akihutubia wananchi atika mkutano wa kampeni wa Mama Samia uliofanyika leo katika jimbo hio mkoani Morogoro
  Umati wa wananchi ukiwa umefurika kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Gairo A, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo la Gairo mkoani Morogoro
  Mwananchi akionyesha bango la kumfagilia Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Gairo mkoani Morogoro
  Mbunge wa Afrika Mashariki, Angela Kizigha akimvalisha kanga za CCM, Bibi Fatuma Farijala, baada ya kuona mavazi yake yamechakaa, akiwa mmoja wa wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika katika jimbo la Gairo mkoani Morogoro leo
  Wananchi wakimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassa alipohutubia mkuano wa kampeni leo katika jimbo la gairo mkoani Morogoro
  Wananchi wakimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassa alipohutubia mkuano wa kampeni leo katika jimbo la gairo mkoani Morogoro
  Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Gairo mkoani Morogoro
  Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimtambulisha aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema wilaya na Gairo, Yona Senyagwa, baada ya kutangaza kuhamia CCM wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Gairo mkoani Morogoro. Kulia ni aliyekuwa Katibu wa zamani wa Chadema kwa miaka kumi John Mwenda ambaye pia alitangaza kuhamia CCM wakati wa mkutano huo
  ---------------------------------------------------------------------------------------
  JIMO LA MIKUMI
   Msafara wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama samia Sulihu ukiwa umezuliwa njian na wananchi katika eneo la Rudewa, wakati akiwa njiani kwenda kuhutubia mkutano wa kampeni leo katika jimbo la Mikumi mkoani Morogoro
   Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hasan akizungumza na wananchi baada ya kuzuia mksafara wake katika eneo la LKilosa mkoani Morogoro leo
   Mkazi wa Kilosa mkoani Morogoro, akiwa amembeba mtoto wake mabegani huku akimsikiliza Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama samia Suluhu, baada ya wananchi kuzuia msafara wake katika eneo hilo  leo
   Wananchi wakiwa wamezuia msafara wa mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika eneo la Masanze mkoani Morogoro leo
   Mwananchi akiwa amemkinga jua mtoto aliyembeba mgomgoni wakati Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan alipozungumza na wananchi baada ya kuzia msafara wake katika eneo la  Masanze mkoani Morogoro leo
   Msafara wa Mama Samia ukishangiliwa wakati ukiondoka eneo la Masanze
   Mgombea Mwenza wa Uras kwa tiketi ya CCM Mama Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwanamuziki wa Kizazi Kipya Juma Kiroboto maarufu kwa jina la Juma Nature, alipowasili kwenye mkutano wa kampeni aliofanya katika jimbo la Kilosa mkoani Morogoro leo.
   Msani wa Bongo Movie, Vincent Kigosi maarufu kwa jina la Ray, akizungumza kwenye mkutano wa kampeni wa Mama Samia uliofanyika leo katka jimbo la Kilosa mkoani Morogoro leo. Ray ambaye awali alikuwa Ukawa, sasa yupo CCM katika kampeni inayoitwa "Nimestuka".
   Wananchi wakishangilia wakati wa mkutano wa kampeni wa Mama samia uliofanyika leo katika jimbo la Kilosa mkoa wa Pwani
   Msani wa Bongo Movie, Wema Sepetu akimuombea kura mgombea Uras kwa tiketi ya CCM, John Magufuli katika mkutano wa kampeni uliofanyika Jimbo la Kilosa mkoani Morogoro
   Mgombea ubunge jimbo la Kilosa, Jonas Nkya akiomba kura baada ya kunadiwa na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia Suluhu Hassan wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo hilo.
   Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia mktano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Kilosa mkoani Moroogoro.
  -------------------------------------
  JIMBO LA MVOMELO
   Wananchi wakiwa na mabango ya kumlaki Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan alipowasili kuhutubia mkutano wa kampeni leo katika jimbi la Mvomelo mkoa wa Morogoro
   Mgombea Ubunge jimbo la Mvomelo,  Suleiman Sadik, akiomba kura baada ya kutambulishwa na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kampeni uliofanyika Mlali katika jimbo hilo leo.
   Mkuu wa wilaya ya Mvomelo, Bety Mkwasa (katikati) akifuatilia kwa makaini hotuba ya Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katikaMlali jimbo la Mvomelo mkoani Morogoro.Kushoo ni Mgmbea Udiwani Jimbo la Mlalo, Frank Mwananziche
   Mgombea Mwenza wa Urais kwa kiketi ya CCM, Mama samia Suluhu Hassan akimnadi Mgombea Udiwani Kata ya Mlali Frank Mwanaziche katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Mvomelo mkoa wa Morogoro. Kulia ni Mgombea Ubunge jimbo la Mvomelo Sadik Murad
   Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiagana na Mkuu wa mkoa wa Mvomelo Bety Mkwasa baada ya mkutano wa kampeni uliofanyika leo jimbo la Mvomelo mkoani Morogoro.PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

  0 0
 • 09/25/15--21:01: EAMCEF FUNDRAISING GALA 2015

 • 0 0

   Fuso ikipita Njiani kwenye Maonyesho ya "NDIO Fuso ni Faida" jijini Dar, Maonyesho hayo yanatarijiwa kupita kwenye Mikoa kama Tanga – Moshi- Arusha- Mwanza –Shinyanga -Kahama- Dodoma – Iringa – Mbeya  na Songea ambapo shughuli mbali mbali za uchimbaji wa madini, kilimo, ujenzi na usafirishaji wa mizigo zinafanyika
   Wadau wa Usafirashaji wakiwa katika Maonyesho ya 'Fuso ni faida' jijini Dar
   Wadau wakipata maelekezo ya Huduma ya 'Ndiyo Fuso ni Faida'
  Na Mwandishi Wetu,


  Mtandao wa miundombinu ya barabara nchini Tanzania inayokadiriwa kuwa na kilometa za mraba 91,049 ambayo ni mara 30 zaidi ya mtandao wa reli ambayo inaambaa kwenye eneo lenye ukubwa wa takribani kilomita za mraba 3,682 ikidhihirisha kuwa barabara ndiyo njia kuu inayopendelewa kutumika katika usafirishaji wa mizigo. 
  Usafirishaji nchini Tanzania unajumuisha mitandao ya barabara, anga, reli na maji ambapo katika njia zote hizi, barabara na reli zinaongoza zikifuatiwa na maji na anga.  Hakika katika suala la umbali, mtandao wa barabara za Tanzania unashika nafasi ya 51 duniani, kutokana na taarifa zilizonukuliwa katika kitabu “ CIA world fact book”
  Wakati ajali za barabarani zikiendelea kugharimu maisha ya watu, ufanisi wa njia hii ya usafirishaji kwa ujumla wake unahitaji kudumisha ubora wa usafirishaji wa barabara nchini Tanzania kutokana na ufanisi wake, kuokoa mda na kuaminika pamoja na kuchukuliwa kuwa kiunganishi kikubwa cha barabara ndogo kwenye barabara kuu za nchi.

  Diamond Motors limited hivi karibuni wamekuwa katika safari ya kuzunguka mtandao huu wa barabara wakihamasisha pamoja na mambo mengine usalama barabarani katika kampeni yao ya “Ndio! Fuso ni Faida” Kampeni hiyo iliyozinduliwa mwezi julai mwaka huu jijini Dar es salaam ilifika katika mikoa ya Tanga-Moshi- Arusha – Mwanza – Shinyanga – Kahama – Dodoma – Iringa – Mbeya – na Songea ambapo shughuli mbali mbali za uchimbaji wa madini, kilimo, ujenzi na usafirishaji wa mizigo zinafanyika. Pamoja na mambo mengine, kampeni hiyo ilidhamiria kujenga uelewa kwa wateja wake juu ya jinsi ya kuboresha usafirishaji salama wa mizigo kwa kutumia magari ya kisasa zaidi.

  Akifafanua kwa undani juu ya malori mapya yaliyohusika katika kampeni hiyo ya “Ndio! Fuso ni Faida” msemaji rasmi wa kampuni ya Diamond Motors Limited ambao ni wadau na wataalamu katika sekta ya usafirishaji wa masafa marefu kwa kutumia malori yao ya Fuso alisema soko la Tanzania linahakikishiwa malori ya aina ya Fuso FZ na FJ yaliyoboreshwa kiteknolojia na kuwa na uwezo wa kuboresha usalama barabarani.

    “Malori haya yametengenezwa na kitako imara kilichotengenezwa kwaajili ya uzito mkubwa na mazingira magumu ya kufanya kazi” alisema Meneje Mkuu (Masoko) wa diamond Motors Ltd bwana Laurian Martin.  Aliongeza kusema kuwa “tuna nia ya kuborsha sekta ya usafirishaji iliyo bora na salama kwa kutumia malori yetu ya Fuso yaliyo boreshwa ki teknolojia” 
  Alisistiza na kusema kuwa “aina mbali mbali mpya za malori yatolewayo na Diamond Motors Ltd sio yanaaminiki katika utendaji tu, bali pia yana uwezo mkubwa wa ubebaji ambayo ni sifa pekee isiyopatikana katika malori mengine ambayo yanalazimika kutumia mafuta mengi ili kukidhi kigezo hicho. Kizuri zaidi, malori haya gharama zake za matengezo ni ndogo zaidi na hutembea umbali mrefu zaidi wa takribani kilomita 45,000 kabla ya kuhitaji matengenezo ya kawaida kama kubadilisha vilainishi”.

  Bwana Laurian Martin aliendelea kusema kuwa “Sifa hizi ndizo zinafanya malori ya Fuso FZ na FJ kuwa suluhisho kamili la usafirishaji na biashara nchini Tanzania”.

   Katika kampeni hiyo mikoa ya kaskazini ikiwemo Tanga, Kilimanjaro, na Arusha ilipata  fursa ya kuona faida zinazopatikana katika malori haya mbalimbali ya Fuso maboyo ni malori ya ubebaji mkubwa yanayopatikana katika kampuni ya Diamond Motors Ltd. 

   Miji ya mikoa hii imendelea kukua katika shughuli za kiuchumi kama vile usafirishaji wa mizigo, biashara, viwanda kama vile cementi, malighafi mbalimbali, maua, matunda, mazao mbalimbali yatokanayo na miti yanayohitaji kusafirishwa kwenda katika sehemu mbalimbali za nchi na nje ya nchi.  Wasafirishaji kutoka mikoa hii wameaswa kutumia teknolojia hii ya malori ya Fuso FZ na FJ ambayo inaweza kuwapatia Faida zaidi katika biashara zao.

  Kampeni hiyo pia  ilifika katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha ambayo imeunganishwa katika ukanda wa kaskazini na barabara za nchi za jirani kama Kenya na Uganda kupitia mipaka yake ya Namanga ikiwa na biashara nyingi baina ya nchi hizo zinazopitia njia ya barabara. 

   Wakazi na wafanyabiashara waliohudhulia kampeni hiyo walipata fursa ya kujionea sifa zipatikanazo katika malori hayo ya Fuso Fz kutoka Diamond Motors Limted ambayo yanauwezo wa kubeba mizigo mikubwa katika mazingira magumu katika ukanda huo. 

   “Ni kwa teknolojia ya kisasa ya magari haya mabapo wafanya biashara wanaweza kupata Faida ya biashaza zao kwa kutumia malori haya inayotumia mafuta vizuri, ambapo gari hii ina kifaa maalumu cha kuzuia mafuta yasitumike endapo gari hii inatembea katika mteremko ili kukupa umbali mrefu zaidi kwa mafuta kidogo. 
  Mikoa ya Mwanza na Shinyanga ambayo ni kitovu cha biashara, usafirishaji, ushirikano wa kikanda na maendeleo ya kiuchumi katika kanda ya ziwa ikiunganishwa na bandari kavu ya Isaka, ilifikiwa na maonyesho haya ya Fuso Fz.  Mikoa hii pia inaunganisha nchi jirani za Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi and Demokrasia ya Kongo ambazo ni nchi zenye biashara nyingi kubwa miongoni mwake na Tanzania.

  Kwa usafirishaji wa masafa marefu katika nchi hizi, Fuso Fz ina muundo maridhawa kupasua upepo usiwe kizingiti ambayo haikupatii umbali mrefu tu, bali pia inampunguzia dereva uchuvu kwa kuwa na kibini iliyoninginizwa vizuri kupumguza sana mtikisiko wa barabarani hasa kwenye matuta au barabara mbovu na kupunguza kelele za kutoka kwenye injini. 

   Sifa hii ni muhimu sana kumpunguzia dereva uchovu na hivyo kuweza kutosababisha ajali zitokanazo na uchvu wa dereva na kusinzia wakati akiendesha.  
  Mikoa ya nyanda za juu kusini pia ilikuwa katika mpango wa kupata faida zitokanazo na matumizi ya malori mapya Fuso Fz yenye teknolojia mpya kutoka Diamond Motors ltd baada ya kufikiwa na kampeni hiyo ya “Ndio! Fuso ni Faida” Kampeni hiyo ilipokelewa vizuri na wakazi wa mikoa ya Dodoma, Iringa, Mbeya na Songea ambapo pia kuna shughuli za kiuchumi kama uchimbaji wa madini, kilimo cha chai, misitu na kilimo cha kibiashara. 

   Wafanyabiashara walionyeshwa haja ya wao kubadilisha njia za usafirishaji kwa kutumia Fuso Fz na Fuso FJ na hivyo kupunguza gharama za uendeshaji na kupata Faida zaidi katika biashara za kiuchumi nchini na ukanda wa Africa Mashariki na kati.

  0 0

  Mkuu wa Shule ya Sekondari Rebu iliyopo Tarime Mkoani Mara Mwl.Nelson Richard jana Septemba 25,2015 akisoma Risala ya shule katika Mahali ya Nane ya Kidato cha nne ya shule hiyo ambayo ni ya kutwa ikiwa na mchanganyiko wa Wavulana na Wasichana kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.
  Na:George Binagi-GB Pazzo
  Katika risala hiyo, Mwl.Richard alibainisha kuwa shule inakabiliwa na baadhi ya changamoto ikiwemo ukosefu wa wigo wa shule pamoja na uchakavu wa madarasa ikiwemo kukosa sakafu hali inayosababisha ugumu kwa wanafunzi katika kujifunza.

  Mahafali hayo yalikuwa ya kuvutia sana kwa kuwa wanafunzi wa shule hiyo walionyesha vipawa vya aina mbalimbali ikiwemo Igizo, Kuruka Sarakasi, Kuimba pamoja na Kucheza Muziki (Dance).
  Mkuu wa Shule ya Sekondari Rebu iliyopo Tarime Mkoani Mara Mwl.Nelson Richard jana Septemba 25,2015 akisoma Risala ya shule katika Mahali ya Nane ya Kidato cha nne ya shule hiyo ambayo ni ya kutwa ikiwa na mchanganyiko wa Wavulana na Wasichana kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.
  Mkuu wa Shule ya Sekondari Rebu iliyopo Tarime Mkoani Mara Mwl.Nelson Richard jana Septemba 25,2015 akisoma Risala ya shule katika Mahali ya Nane ya Kidato cha nne ya shule hiyo ambayo ni ya kutwa ikiwa na mchanganyiko wa Wavulana na Wasichana kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.
  Mgeni Rasmi katika Mahafali ya nane ya Kidato cha nne katika shule ya Sekondari Rebu iliyopo Wilayani Tarime George Obuto ambae ni Afisa Elimu Sekondari katika Wilaya hiyo akizungumza katika Mahafali hayo.

  Zaidi aliwasihi wazazi kushiriki katika kutatua baadhi ya changamoto zinazoikabiri shule hiyo ikiwemo suala la ukarabati na ujenzi wa madarasa pamoja na utatuzi wa changamoto ya ukosefu wa wigo shuleni hapo.
  Mgeni Rasmi akikabidhi cheti kwa mhitimu
  Mhitimu akipokea cheti
  Mgeni Rasmi akikabidhi cheti kwa mhitimu
  Mgeni Rasmi akikabidhi cheti kwa mhitimu
  Mhitimu akipokea cheti
  Mgeni Rasmi akikabidhi cheti kwa mhitimu
  Mwalimu alietimiza vyema wajibu wake akipongezwa
  Wahitimu wa Kidato cha Nne Rebu Sekondari 2015
  Wahitimu wa Kidato cha Nne Rebu Sekondari 2015
  Wahitimu wa Kidato cha Nne Rebu Sekondari 2015
  Wahitimu wa Kidato cha Nne Rebu Sekondari 2015
  Wazazi wa Wahitimu wa Kidato cha Nne Rebu Sekondari 2015
  Waalimu
  Mwalimu Wambura Mhoni alikuwa Mshereheshaji
  Washereheshaji walikuwa ni Mwalimu Mengi Mohamed (Kushoto) pamoja na Mwalimu Wambura Mhoni (Kulia)
  Mmoja wa wahitimu akikata keki
  Mmoja wa wahitimu akimlisha mzazi wake keki
  Mhitimu (Wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mwalimu wake (Kulia), mzazi wake (wa pili kushoto) na mmoja wa mwanafunzi wa Rebu Sekondari
  Mhitimu akimlisha keki mwalimu wake
  Ni wasaa wa keki
  Ni wasaa wa keki
  Keki time
  Mhitimu akiwa na wanafamilia
  Kushoto ni Mhitimu akiwa na mwanafamilia
  Msosi
  Mwalimu Manguye (kushoto) akiwa pamoja na Mwalimu Mussa (kulia) wote kutoka Shule ya Sekondari Rebu.
  BINAGI MEDIA GROUP, INAWATAKIA WAHITIMU WOTE KILA LA KHERI KATIKA MTIHANI WAO WA MWISHO.


  0 0

  Na Muwandishi wetu Swahilivilla Washington DC Waislamu kote ulimwenguni jana waliadhimisha Siku Kuu ya Idd Al-Adh'ha kwa Ibada na sherehe mbalimbali.Wanadiaspora wa Tanzania noa walijumuika na Waislamu wenzao ulimwenguni kuadhimisha siku hiyo muhimu katika Dini ya Kiislamu.
  Baadhi ya waumini wa Tanzanian Muslim Community Washington DC wakipata picha ya pamoja baada ya kumaliza sala ya Eid Al-Adhw-haa iliosaliwa Siku ya Alhamis Sept 24, 2015 katika msikiti wa Islamic Center New Hampshire Maryland US.( Picha zote na swahilivilla.blogspot.com)
  Katika kuadhimisha siku hiyo, Jumuiya ya Waislamu wa Tanzania waishio katika jiji la Washington na vitongoji vyake (TAMCO), iliandaa sherehe iliyoendelea hadi usiku katika viwanja vya wazi.
  Akizungumza na Swahilivilla, mmoja wa wanachama wa jumuiya hiyo Bwana Abubakar Qullatein, aliiambia Swahilivilla kuwa amefurahi kuadhimisha siku hii adhimu katika dini ya Kiislamu. Hata hivyo furaha yake hiyo imeingiwa na dosari kutokana na maafa ya ajali zilizotokea huko Makka, Saudi Arabia zilizosababishwa na moto na mkanyagano wa watu.
  Bwana Abubakar Qullatein, akipata picha ya 
  pamoja na Abou Shatry baada ya swala ya Eid.
  "Iddi hii imekumbwa na misukosuko kidogo kutokana na ajali za hapa na pale zilizotokea, sehemu mbalimbali duniani, na hata huko Makka", alielezea masikitiko Bwana Qullatein, na kendelea kusema kuwa, Iddi hii inakuja baada ya kukamilika kwa Ibada ya Hijja, kwa hivyo kwenye Hijja yenyewe kukitokea ajali kama hizi, inaleta huzuni.
  Aliwatolea wito Waislamu kuondoa shari na fitna miongoni mwao na kuitetea Dini yao kwa kuonesha tabia na mtendo mema, jambo ambalo litasaidia kuondosha chuki kutoka kwa wasiokuwa Waislamu.
  "Waislamu tushikamane, tupendane, tuondoe fitna na shari, tuwe kitu kimoja, tuoneshe tabia nzuri na mahusiano mema na watu wa dini nyengine, hii itasaidia kuondoa chuki zao" alihubiri Sheikh Qullatein, na kuelezea matumaini yake kuwa kuadhimisha Siku Kuu ya Idd Al-adh'ha siku moja kote ulimwenguni, kutakuwa ni mwanzo wa kuelekea kufunga na kufungua Ramadhani kwa pamoja.
  Kwa upande wake, Mratibu wa sherehe za Siku Kuu wa TAMCO Bibi Asha Harris, aliiambia Swahillivilla kuwa, siku hii kama ilivyo adhimu kwa Waislamu kote ulimwenguni, pia ina umuhimu mkubwa kwa Jumuiya yake.
  Bi Asha Hariz, kulia, akipata picha na  waumuni wa Tanzanian Muslim Community Washington DC, kwa chai ya asubuhi."Siku hii ina umuhimu mkubwa kwa jumuiya yetu, kwa vile tunapata fursa ya kujumuika pamoja, na kuhuisha upendo na ushirikiano miongoni mwetu", alielezea Bi Hariss, na kuendelea kuwa ''Maadhimisho haya tunayagawa katika sehemu mbili; asubuhi na jioni"
  Katika sehemu ya subuhi, Bi Harris ameelezea kuwa, mara tu baada ya Swala ya Iddi Wanajumuiya hukutana katika ukumbi maalum na kujipatia chai na vitafunio vyepesi. "Lakini kabla ya chai, kwanza huanza kwa Dua maalum ili kuwaombea wazee wetu na wenzetu wengine waliotangulia mbele ya Haki", alifafanua Bi Hariss.
  Baada ya sehemu hiyo kumalizika, Wanajumuiya huondoka na baadaye kukutana tena jioni ili kuanza sehemu ya pili ya sherehe za Iddi Al-Adh'ha.
  "Baadaye tunakutana tena jioni kwenye viwanja vya wazi kwa ajili ya nyama-choma na shamra-shamra nyengine" aliendelea kufafanua Bi Harris, na kusema kuwa sehemu hii ya pili ina umuhimu mkubwa zaidi, kwa vile huwajumuisha Watanzania wote hata wasiokuwa Waislamu.
  Miongoni mwa vibwagizo vya sherehe hizo ni pamoja na michezo na mashindano ya watoto. Watoto hupata nafasi ya kupokea zawadi za aina mbalimbali, na kwa wale wanaoshinda kwenye mashindano yaliyoandaliwa hupata zawadi za nyongeza.
  Mashindano ya watoto hujikita zaidi kwenye umuhimu wa Siku Kuu ya Idd Al-Adh'ha. "Tunafanya chemsha bongo kwa jili ya watoto, na maswali yote hujikita kwenye kuwahamasisha watoto juu ya umuhimu wa siku hii", alisema Bi Hariss.
  Aliidokeza kuwa hapo awali, TAMCO ilikuwa inafanya sherehe za Idd wakati wa jioni tu, lakini katika miaka ya karibuni ikaonekana umuhimu wa kuwepo kwa sehemu ya asubuhi ambayo mbali na chai hujikita zaidi kwenye dua na maombi kama ilivyo ada nyumbani Tanzania.
  Katika Jimbo la Washington, Watanzania nao hawakuwa nyuma katika kuadhimisha Siku Kuu ya Idd A-Adh'ha.
  Bwana Adullah Kidume, alisema kuwa, Waislamu wa Tanzania waishio katika jiji la Seattle na vitongoji vyake walikodi ukumbi maalum kwa jili ya Swala ya Iddi.
  Akizungumza na Swahilivilla kutoka Tacoma, Bwana Kidume alisema kuwa ni ada ya Waislamu katika maeneo hayo kukodi ukumbi kwa jili ya Ibada, na baadaye kuendelea na sherehe za kawaida.
  Licha ya kutokuwa na Jumuiya rasmi, Waislamu wa Tanzania katika eneo hilo wameweza kudumisha ada ya kujumuika pamoja katika Siku Kuu mbalimbali za kidini. "Ni sisi wenyewe tu Waislamu tunaojuana...., siyo Kamati rasmi" alisema Bwana Kidume.
  Hapo awali Waislamu hao walikuwa hukutana kwa ajili ya Swala tu, lakini, juhudi za akina mama ndizo zilizozaa wazo la kuendeleza sherehe hizo ambazo hudumu mpaka usiku wa manane.
  Miongoni mwa vikorobwezo vya sherehe hizo ni pamoja na vyakula vya aina mbalimbali vinavyoonyesha ustadi wa mapishi ya Kitanzania, mavazi, michezo na mengineyo.
  Licha ya Ibada ya Hija mwaka huu kukumbwa na maafa ya moto na watu kufariki dunia kutokana na mkanyagano huko Makka, hata hivyo, Hija hiyo imekuwa na umuhimu wa aina yake kwa baadhi ya Wazanzibari kwa vile ni mara ya mwanzo bendera ya Zanzibar imepepea katika Maeneo hayo Matakatifu.
  Akiongea na mwandishi wetu kutoka Dar es Salaam, Bwana Omar Abdullah ameelezea furaha yake kuona bendera ya Zanzibar ikipepea katika Hija ya mwaka huu. 
  "Tulipopata taarifa za maafa kule Makka, Moyo wangu uliingiwa na huzuni.., japokuwa hakuna ndugu yangu, lakini Waislamu wote ni ndugu", alisema Bwana Abdullah, na kuongeza kuwa "lakini kitu kilicholeta furaha katika Siku Kuu hii kwangu, ni kuiona bendera ya Zanzibar ikipepea kule, japo kuwa kwa juu kulikuwa na kibendera kidogo cha Tanzania".
  Alielezea matumaini yake kuwa katika Hija ya mwakani, Mahujaji kutoka Zanzibar watabeba bendera yao kamili bila kuwa na kibendera chengine ndani yake. Angalia Taswira mbali mbali za Eid Al- Adhw-haa Washington DC hapa

  0 0

  Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola ukiendelea pembezoni mwa Mkutano wa 70 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Jijini New York, Marekani.
  Sekretarieti ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola wamesifu kazi iliyofanywa na Tanzania kama Mwenyekiti wa Kikundi Kazi cha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa jumuiya hiyo ya kusimamia na kuimarisha misingi imara ya jumuiya katika kipindi cha miaka miwili iliyopita. 
  Hayo yamesemwa na Dkt. Josephine Ojiambo Makamu Katibu Mkuu wa Sekretarieti hiyo, kwenye taarifa fupi ya utekelezaji wa kazi za Jumuiya kwenye Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola uliofanyika Septemba 24, pembezoni mwa Mkutano wa 70 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.
  Taarifa hiyo ilieleza kuwa uongozi wa Mhe. Bernard Membe (Mb.), ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania umeibua mbinu za kisasa za kutatua matatizo ya nchi wanachama zilizokuwa na changamoto ya kuheshimu misingi na taratibu za Jumuiya ya Madola. 
  Waziri Membe ambaye anamaliza muda wake wa uongozi kwenye kikundi kazi hicho mwaka huu, amesema mafanikio hayo yametokana na ushirikiano mzuri aliokuwa anaupata kutoka kwa Sekretarieti inayoongozwa na Kamalesh Sharma, ambao ndio waratibu wa shuguli za Kikundi Kazi cha Mawaziri. Vilevile ushirikiano aliopewa na Makamu Mwenyekiti wa Kikundi hicho Mhe. Murray McCully, Waziri wa Mambo ya Nje wa New Zealand pamoja na wajumbe wengine wa Kikundi hicho maalum kimewezesha kazi za kuratibu kazi za Jumuiya hiyo kuwa na mafanikio makubwa. 
  Masuala mengine yaliyojadiliwa kwenye mkutano wa Mawaziri ni utekelezaji wa maamuzi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya hiyo kuhusu uimarishwaji wa mifumo ya tehama na  nyenzo mbalimbali za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwenye nchi wanachama uliofanyika mwaka 2013  Jijini Colombo, nchini Sri Lanka. 
  Kwenye mkutano huo pia Mhe. George William Vella, Waziri wa Mambo ya Nje wa Malta alitoa taarifa fupi kuhusu maandalizi ya Mkutano wa mwaka huu wa wakuu wa nchi na serikali wa Jumuiya hiyo utakaofanyika Novemba 2015, nchini Malta. 
  (Pichani juu na chini) Mhe. Bernard Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akifuatilia Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola

  0 0

   Taarifa zinazosambaa kumhusu Mkuu wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) Jenerali  Davis Mwamunyange zilizosambaa kwenye mitandao ya jamii kwamba amekula chakula chenye sumu na amekimbizwa jijini Nairobi nchini Kenya kwa matibabu hazina ukweli wowote.Ni uzushi.

  Kwa mujibu wa taarifa za familia ya Jenerali Mwamunyange pamoja na makao makuu ya jeshi ambazo Globu ya Jamii imezisaka na kuzipata, kiongozi huyu wa JWTZ hivi sasa yupo nchini Italia kwa ziara ya kikazi ya siku tisa kama anavyoonekana pichani na hajambo kabisa na yu bukheri wa afya.

  Hii ni changamoto kwa wakala wa mawasiliano nchini (TCRA) ambayo imekuwa ikilaumiwa kwa ukimya wake wa kutochukua hatua thabiti kuthibiti uongo kama huu kwa kuwatafiti, kuwabaini na kuwachukulia hatua watu kama hawa wenye nia ya kuleta taharuki na machafuko nchini.
  Wananchi wengie waliohojiwa na Globu ya Jamii wanahoji endapo kama kweli TCRA ipo na kama ipo ina vifaa vya kisasa iliyodai wanavyo kuwabaini watu kama hawa, na kwa nini hawajafanya kweli toka sheria ya mitandao (Cyber Law) iliyoanza kutumika.
  "Endapo kama TCRA watashindwa kumnasa mhusika wa uongo huu wa kuogofya, inabidi mamlaka husika iangalie upya ajira ya watendaji wake maana kama taasisi nyeti kama JWTZ inaguswa na wao wakae kimya tu basi ujue kuna tatizo ambalo inapaswa Serikali ilifanyie kazi", amesema msomaji mmoja wa Globu ya Jamii katika maoni yake.


older | 1 | .... | 652 | 653 | (Page 654) | 655 | 656 | .... | 1898 | newer