Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 648 | 649 | (Page 650) | 651 | 652 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Kuonyesha kwamba yuko fiti ana anastahili kupewa ridhaa ya kuiongoza Tanzania katika awamu ya kipindi cha tano,Dkt John Pombe Magufuli aliwashangaza wananchi wa mji huo kwa kupiga push up zaidi ya tano jukwaani,mbele ya wakazi wa mji huo ambao walishangilia na kupiga mayowe kila kona ya Uwanja.

   Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika viwanja vya Kayanga,Karagwe mjini asubuhi hii kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
     Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika viwanja vya Mashujaa mjini Misenyi asubuhi hi kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni
   wakazi wa mji wa Misenyi  katika viwanja vya mashujaa wakishangilia mara huku wakiendelea kumsikiliza mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli.

   PICHA NA MICHUZI JR-KARAGWE

  0 0


  Ndg Abel Mudo, mgombea wa udiwani kata ya Kisarawe kupitia CCM akichangia katika mdahalo wa ajenda ya watoto ambapo ulihusisha pia wakazi wa kata ya kisarawe
  Baadhi ya wakazi ya kata wa kisarawe wakifuatilia kwa makini mdahalo wa ajenda ya watoto ambapo wa  ajenda ya watoto ullohusisha wagombea wa udiwani kupiitia vyama vya ccm na chadema 

  Mmoja wa wananchi wa kata ya kisarawe akichangia katika mdahalo wa ajenda ya  watoto kuelekea uchaguzi mkuu  ambapo ulihusisha wanafunzi na wagombea  wa udiwani wa kata hiyo            Mwanafunzi Amina Joka akichangia katika mdahalo wa ajenda ya watoto ambapo wanafunzi wa shule za Msingi  chanzige A ,chanzige B na kisarawe  na wagombea wa udiwani kupitia vyama vya ccm na chadema walishiriki


  Ndg Abel Mudo ambaye ni mgombea wa Udiwani kupitia CCM akichangia katika mdahalo wa ajenda ya watoto kuelekea uchaguzi mkuu ambapo wanafunzi wa CHANZIGE ,na kisarawe 

  Mmoja wa wanafunzi wa shule msingi CHANZIGE A akifuatilia kwa makini mdahalo wa ajenda ya watoto uliowahusisha wagombea wa udiwani wa vyama vya chadema na CCM 

  Ndg .Baraka Musa, mgombea wa udiwani kata ya Kisarawe kupitia CHADEMA akichangia katika mdahalo huu uliowaohusisha wakazi wa kisarawe na wanafunzi  Picha za Wanafunzi ni za wanafunzi wa shule za msingi Chanzige A, Chanzige B na Kibasila zilizopo Kisarawe wakifuatilia kwa makini mdahalo huo.


  Ndg .Baraka Musa, mgombea wa udiwani kata ya Kisarawe kupitia CHADEMA akichangia katika mdahalo huu uliowaohusisha wakazi wa kisarawe na wanafunzi
  Ajenda ya watoto ilianzishwa na mashirika ya watoto Tanzania yakiongozwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa nia ya kuhakikisha maswala ya watoto na haki zao yanawakilishwa vyema katika serikali ya Tanzania.


  Katika kuhakikisha kwamba Ajenda za watoto zinazungumzwa katika jamii Kipindi cha redio cha Walinde Watoto leo kimeandaa mdahalo uliowahusisha wagombea wa udiwani kata ya Kisarawe ambao ni Abel Mudo (CCM) na Baraka Musa (CHADEMA) na wakazi wa Kata ya Kisarawe ili kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili watoto na mipango ya vyama vyao katika kutatua changamoto hizo.

  Mdahalo huo uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe ulihudhuriwa na wenyekiti wa vijiji, na vitongoji, walimu, maafisa ustawi wa jamii pamoja na wananchi wakazi wa Kata ya Kisarawe.

  Akiinadi Ilani ya chama cha Demokrasia na Maendeleo, Baraka Musa anayegombea udiwani kata ya Kisarawe, alisema chama chake kinaamini kuwa lishe bora ni muhimu kwa ustawi wa watoto kiafya na kielimu na akasema endapo kitaingia madarakani kitahakikisha kinawekeza kwenye kupata Katiba inayotambua na kutaja moja kwa moja haki za watoto.

  Naye mgombea wa udiwani kata ya Kisarawe kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Abel Mudo alisema endapo chama chake kitapata ridhaa ya kuendelea kuongoza nchi kitawekeza zaidi katika shule na kuhakikisha zina walimu wa kutosha na kwamba serikali yake imetengeneza mazingira rafiki na kutoa zana kwa watoto wenye ulemavu.

  Mgombea huyo aliahidi kwamba watafanya kazi pamoja na wadau mbalimbali ili kuhakikisha wanapunguza ukatili kwa watoto na kukabiliana na matatizo  ya mimba za utotoni sambamba na kutoa elimu bure kwa wanafunzi wa hadi kidato cha nne.

  Mwanafunzi Amina Joka aliwataka wagombea udiwani hao pindi mmoja wapo atakapochaguliwa, wahakikishe wanajenga hosteli za wanafunzi kufikia kwani kwa sasa wanalazimika kusafiri umbali mrefu sana kwenda shule hali ambayo ni hatarishi kwani wanakutana na vishawishi vingi njiani. 

  Katika hatua nyingine, wagombea hao walipata fursa ya kusikiliza kero za wanafunzi kutoka shule za msingi Chanzige A, Chanzige B na Kibasila wilayani kisarawe ambao walitaja kero za upungufu wa walimu, ukosefu wa huduma za afya, adhabu za mashuleni na ukosefu wa maji kama kero zao za mda mrefu. “Mgombea bora ni Yule atakayetuletea maji kwani tunaenda kutafuta maji umbali mrefu badala ya kujisomea” Alisema mwanafunzi mmoja.


  Unaweza kusikiliza kipindi cha Walinde Watoto mahali popote kupitia redio shiriki 19 ikiwemo TBC inayorusha matangazo hayo siku ya Jumamosi kuanzia saa nane mchana na pia kupitia tovuti ya www.walindewatoto.org

  0 0

  (Meneja msaidizi wa kituo cha walemavu cha Usa River Rehabilitation Centre,Sophia Moshi akibadilishana mawazo na meneja mkuu wa kituo hicho,Claus Heim).
   
  Mahmoud Ahmad, Arusha
  SERIKALI imeombwa kuchukua hatua kali kwa baadhi ya wazazi nchini wenye tabia ya kuwaficha watoto wao wenye ulemavu hali ambayo imekuwa ikiwafanya wakose mahitaji ya msingi kama elimu na afya.

  Ombi hilo limetolewa hivi karibuni na uongozi wa chuo cha walemavu cha Usa River Rehabilitation Centre  huku wakiiomba serikali iviangalie vituo vya kulea watoto walemavu kwa kuvipatia ruzuku .

  Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili chuoni hapo,meneja wa chuo hicho,Claus Heim alisema kwamba serikali inapaswa kuhakikisha inawachukulia hatua kali za kisheria baadhi ya wazazi wenye tabia ya kuwaficha watoto wao wenye ulemevu majumbani.

  Alisema kwamba serikali inapaswa kuweka sheria kali na kuhakikisha zinatekelezwa ili kuwapa fursa watoto wenye ulemavu nchini kupata huduma za msingi kama elimu,afya,chakula  pamoja malazi.

  “Hawa wazazi wanaowaficha watoto wenye ulemavu nchini je wanachukuliwa hatua gani?kila mtoto ana haki ya elimu na afya lakini nani anawajibika”alihoji Heim ambaye ni raia wa nchini ujerumani

  Hatahivyo,meneja msaidizi wa kituo hicho,Sophia Moshi kwa upande wake alisema kwamba ni wajibu wa serikali kuhakikisha inavipatia ruzuku vyuo vya ulemavu nchini ili viweze kujiendesha kwa kuwa vinakabiliwa na changamoto lukuki.

  Alisema kwamba mtoto mwenye ulemavu ana uwezo kama mtoto mwingine na hivyo kuitaka jamii kuwathamini watoto wenye mahitaji maalumu badala ya kuwanyanyapaa.

  Mbali na kauli hiyo Moshi alisema kwamba chuo chao kimejipanga kujenga shule ya sekondari kwa lengo la kuongeza mapato ya kuendesha chuo hicho badala ya kutegemea wafadhili ,kusajili kituo cha afya kwa ajili ya matibabu ya mguu kifundo(club foot) sanjari na kusajili chuo cha ufundi chuoni hapo.

  Chuo hicho kilianzishwa mnamo mwaka 1988 na kinasimamiwa na kanisa la Kiinjili la Kilutheri(KKKT) Dayosisi ya Meru  ,kwa sasa kina jumla ya wanafunzi 74 walemavu ambao ni wasichana na wavulana ambapo nchi ya ujerumani ndiye mfadhili mkuu kwa sasa.

  0 0

  TAKWIMU zinaonyesha kwamba wananchi hawaelewi nafasi rasmi ya Ukawa
  22 Septemba, Dar es Salaam: Asilimia 62 ya wananchi wanasema kwamba wanajisikia wapo karibu zaidi na chama cha CCM kuliko vyama vingine. 
   
  Aidha, walipoulizwa watawachagua wagombea wa chama gani – bila kutajiwa majina ya wagombea – wananchi 6 kati ya 10 walisema kwamba watawachagua wagombea wa CCM kwa Urais (66%), Ubunge (60%) na Udiwani (60%). Takwimu hizi zinatoa picha kwamba CCM inaungwa mkono, kama ilivyokuwa mwaka 2012.

  Chadema ni chama cha pili kinachopendwa kushinda vyama vingine vya upinzani. Lakini wananchi wanaosema kwamba watawachagua wagombea wa Chadema kwa Urais, Ubunge na Udiwani wamepungua kidogo. Ikumbukwe kuwa, inawezekana wananchi wanaopenda zaidi mseto wa Ukawa waliunga mkono vyama vya CUF, NCCR-Mageuzi au NLD.

  Mbali ya CCM na vyama vinavyounda Ukawa, chama cha ACT-Wazalendo kilitajwa na zaidi ya asilimia moja ya wananchi.

  Walipoombwa kutaja moja kwa moja jina la mgombea Urais ambaye wangemchagua, asilimia 65 ya wananchi walimtaja mgombea wa CCM, John Magufuli. Asilimia 25 walimtaja mgombea wa Chadema (na Ukawa), Edward Lowassa. Asilimia 10 iliyosalia iligawanyika kati ya wale waliomtaja mmoja miongoni mwa wagombea urais wengine, waliokataa kujibu na waliokuwa bado hawana mgombea waliyempendelea. Hata hivyo, takwimu zilikusanywa kabla vyama vingine, kikiwemo ACT-Wazalendo, kuteua wagombea wao wa Urais. Takwimu hizi (zilizokusanywa kati ya Agosti na Septemba) sio utabiri wa matokeo ya uchaguzi. Zinaonyesha tu kwamba mwanzoni mwa kipindi cha kampeni, mgombea Urais wa CCM, John Magufuli, alikuwa anaongoza katika kura za maoni.

  Aidha, vigezo muhimu vinavyohusu makundi mbalimbali ya watu (demografia) vilitumika kuchambua ni nani au makundi gani yanayowaunga mkono John Magufuli na Edward Lowassa. Wahojiwa ambao walikuwa vijana zaidi, wasomi zaidi, wanaume na wakazi wa mijini, walimuunga mkono Edward Lowassa. Makundi ya wahojiwa wazee zaidi, waliokuwa na elimu ya msingi tu, wanawake na wakazi wa vijijini walielekea kumuunga mkono zaidi John Magufuli kuliko vijana zaidi, wasomi zaidi, wanaume au wanaoishi mijini.

  Hata hivyo, katika makundi yote haya, John Magufuli wa CCM anaonekana kuongoza. Kwa mfano, asilimia 33 ya wananchi wenye umri wa 18 – 29 na asilimia 30 ya wenye umri wa 30 – 39 wanamuunga mkono Lowassa, tofauti na asilimia 15 ya watu wenye umri zaidi ya miaka 50. Pamoja na hayo, asilimia 57 ya watu wenye umri wa 18 – 29 na asilimia 76 ya watu wenye umri wa 30 – 39 wanamuunga mkono Magufuli. Upande wa makazi, asilimia 28 ya wakazi wa mijini walimuunga mkono Edward Lowassa tofauti na asilimia 24 ya wakazi wa vijijini. Asilimia 66 ya wakazi wa vijijini na asilimia 61 ya wakazi wa mijini wanamuunga mkono John Magufuli.

  Asilimia 26 ya wanaomuunga mkono John Magufuli walidai kwamba ni kwasababu yeye ni mchapakazi, na asilimia 12 ya wanaomuunga mkono Edward Lowassa walisisitiza kwamba anaweza kuleta mabadiliko yanayohitajika nchini. Izingatiwe kwamba kauli hizi zinafanana karibu neno kwa neno na kauli mbiu za kampeni za wagombea hawa wawili.

  Hata hivyo, wananchi hawana taarifa sahihi juu ya nafasi rasmi ya Ukawa kama mseto. Asilimia 49 ya wananchi wanafikiri kwamba Ukawa ni chama cha siasa kilichosajiliwa, kinyume na hali halisi. Asilimia 57 wanafikiri kwamba neno ‘Ukawa’ litakuwepo kwenye karatasi zao za kupigia kura. Hii pia, sio kweli. Bila kampeni na juhudi za kuwaelimisha wapiga kura ili wawe na taarifa sahihi kuhusu jambo hili, hali hii inaweza kuleta wasiwasi siku ya uchaguzi. 

  Matokeo haya yalitolewa na Twaweza katika muhutasari wa utafiti mwenye jina la Sema mwananchi, sema | Maoni ya wananchi kuhusu uongozi wa kisiasa. Muhtasari huu umetumia takwimu kutoka Sauti za Wananchi, utafiti wa kwanza barani Afrika unaotumia simu za mkononi na wenye uwakilishi wa taifa zima. Matokeo yanatokana na Awamu ya 1 ya kuwapigia simu wahojiwa wapya 1,848 iliyoendeshwa kati ya Agosti na Septemba 2015. 
   
  Wahojiwa waliteuliwa kwa kutumia njia kama zinavyotumika na asasi za utafiti duniani kote. Unasibu (sampling) huu ulifanyika katika mikoa yote ya Tanzania Bara. Takwimu hizi zimelinganishwa na zile za awamu za utafiti katika miaka ya nyuma, zikiwemo:
  • Utafiti wa awali wa kwanza wa Sauti za Wananchi 2012
  • Sauti za Wananchi Awamu ya 10 ya Octoba 2013
  • Sauti za Wananchi Awamu ya 24 ya Septemba 2014
  • Awamu za utafiti za Sauti za Wananchi Aprili-Julai 2015
  • Utafiti mpya wa awali ulioendeshwa kati ya Julai na Agosti 2015

  Twaweza ilibaini kuwa zoezi jipya la kuwaandikisha wapiga kura lilifanikiwa kwa kiasi kikubwa. Asilimia 98 ya wahojiwa waliripoti kwamba wameshajiandikisha chini ya mfumo mpya wa Biometric Voter Registration (BVR). Hata hivyo, wananchi wengi walikumbwa na changamoto nyingi katika mchakato huo. Asilimia 68 ya wananchi walitaja urefu wa foleni za kujiandikisha kama tatizo kuu.
   
   Asilimia 51 walisema walisubiri au walishuhudia wananchi wengine wakisubiri muda wa zaidi ya masaa sita kabla ya kujiandikisha. Aidha asilimia 37 waliona au wao wenyewe walipa matatizo ya kusukumana kwenye foleni. Mashine za BVR kushindwa kufanya kazi ipasavyo kuliripotiwa na asilimia 26 ya wananchi. Upendeleo kwenye vituo vya kujiandikisha uliripotiwa na asilimia 19. Ukosefu wa uzoefu wa BVR ulilalamikiwa na asilimia 16 ya wananchi.

  Pamoja na kujiandikisha kupiga kura, asilimia 99 ya wananchi walisema kwamba wanadhamiria kupiga kura katika uchaguzi wa mwaka huu. Hata hivyo, izingatiwe kwamba asilimia 79 ya wahojiwa hawa walidai pia kwamba walipiga kura wakati wa uchaguzi wa 2010 wakati hali halisi inaonesha kuwa waliopiga kura walikuwa asilimia 43 tu. Aidha, ni asilimia 57 tu ya wananchi ndio walioweza kutaja tarehe sahihi ya uchaguzi, yani Oktoba 25. Takwimu hizi zinaonyesha kwamba mara nyingi kuna tofauti kati ya majibu ya watu wakati wa kura za maoni au tafiti mbalimbali, na vitendo vyao halisi.

  Asilimia 64 ya wananchi walisema kwamba wanakumbuka vyema ahadi zilizotolewa na Wabunge wao katika uchaguzi uliopita, na asilimia 86 kati ya hao walisema kwamba mbunge wao hakutekeleza ahadi hizo au alizitekeleza chache.

  Aidha, wananchi waliorodhesha changamoto kuu walizoona hapa nchini. Kama ilivyokuwa katika miaka ya nyuma, huduma za afya ni changamoto kwa asilimia 59 ya Wananchi, ukosefu wa maji ikitajwa na asilimia 46, elimu duni na asilimia 44, na umaskini, asilimia 39. Hata hivyo, kumekuwa na mabadiliko kadhaa. Watu wachache zaidi walitaja umaskini (wamepungua kutoka asilimia 63 mwaka 2014) na watu wengi zaidi walitaja maji (wameongezeka kutoka asilimia 27 mwaka 2014).

  “Kuna mambo kadhaa ya kuzingatia hapa,” alisema Aidan Eyakuze, Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza. “Wananchi wanabadilisha mawazo kuhusu vipaumbele vyao. Waliweka kipaumbele kwa afya badala ya umasikini katika kipindi kifupi cha miezi 12.”

  “Watu wana hamu kubwa sana ya kupiga kura” aliongeza, “lakini hali hii si kigezo cha kuaminika katika kutabiri wangapi kweli watapiga kura siku ya uchaguzi. Wakijitokeza kwa wingi, itaipa uhalali mkubwa serikali ya awamu ijayo. Wakijitokeza wachache, inaweza kuashiria ama hali ya wananchi kukata tamaa, au hali ya kujiamini kwamba tayari wameshinda, au hali zote mbili kwa pamoja.”

  “Kwa pamoja, mambo haya mawili yanatoa picha kwamba huenda wapiga kura wakawa hawana uhakika wamchague nani. Yanaimarisha ujumbe kwamba mashindano haya ndio kwanza yameanza kupamba moto. Wagombea hawana budi kuimarisha mahusiano yao na wapiga kura wakiwa na malengo mawili makuu; Lengo la kwanza ni kunadi ubora wa ilani na sera zao. Lengo la pili ni kuhakikisha kwamba watajitokeza kwa wingi kuwapigia kura siku ya uchaguzi, Oktoba 25.”

  0 0
 • 09/22/15--02:42: ROTARY DAR MARATHON 2015
 • ROTARY Dar Marathon 2015 in partnership with Bank M will be held on 14th Oct (Public Holiday) -  Join us with your families and friends for Cycling /Run / Walk  at the Green, Kenyatta/Toure Drive.

   The Half Marathon run will start at 6.30am while the Cycling race, 9KM and 5KM walk will start at 7am sharp. Registration counters will be open from 4.30am and look out for other registration points closer to the time. Theme for this year is “Healing Lives. Transforming communities” and Proceeds from the Marathon will go towards building a multi-disciplinary hospital in Dar es salaam. 

  Register to run OR walk OR cycle NOW on www.RotaryDarMarathon.com, facebook at “Rotary Dar Marathon” or call on 0784 900 041#RotaryDarMarathon.


  0 0


  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
   WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

  JESHI LA POLISI TANZANIA.

   
         TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
     “PRESS RELEASE” TAREHE 22.09.2015. 

  ·         WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA BAADA YA BAJAJI WALIYOKUWA WAKISAFIRIA KUGONGA GARI.

  ·         MTU MMOJA AFARIKI DUNIA NA WENGINE KUJERUHIWA BAADA YA BAJAJI WALIYOKUWA WAKISAFIRIA KUACHA NJIA NA KUPINDUKA.


  ·         MTU MMOJA AFARIKI DUNIA NA WENGINE KUJERUHIWA BAADA YA BASI MALI YA KAMPUNI YA SAI BABA KUGONGA LORI LILILOKUWA LIMEEGESHWA.

  KATIKA TUKIO LA KWANZA:
  WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. ABILAH PHILIMON (17) MKAZI WA ILEMI, DEREVA WA BAJAJI NA 2. BARAKA SELEMANI (23) MKAZI WA SIMIKE WALIFARIKI DUNIA BAADA YA BAJAJI YENYE NAMBA ZA USAJILI MC 276 APL ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA MAREHEMU KUGONGA GARI  T.588 AMR AINA YA MITSUBISHI FUSO ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA DEREVA EMANUEL FRANSIS (35).
  AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 21.09.2015 MAJIRA YA SAA 17:00 JIONI HUKO KIJIJI CHA HATWELO, KATA YA HATWELO, TARAFA YA TEMBELA, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI, MKOA WA MBEYA.
  AIDHA KATIKA AJALI HIYO, WATU SITA KATI YAO WANAUME WATANO NA MWANAMKE MMOJA WALIJERUHIWA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA BAJAJI. MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA, MAJERUHI WAMELAZWA HOSPITALINI HAPO.

  KATIKA TUKIO LA PILI:
  MTU MMOJA MKAZI WA TEWELE – NAKONDE –ZAMBIA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FRAID AINKALA (67) AFARIKI DUNIA BAADA YA BAJAJI YENYE NAMBA ZA USAJILI MC 630 AFC IKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA KUACHA NJIA NA KUPINDUKA.
  AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 21.09.2015 MAJIRA YA SAA 15:00 ALASIRI HUKO KIJIJI CHA NKANGAMO, TARAFA YA NDALAMBO, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA, BARABARA KUU YA TUNDUMA/SUMBAWANGA.

  AIDHA KATIKA AJALI HIYO, WATU WAWILI WALIJERUHIWA AMBAO NI 1. MAGRETH MTAMBO (52) NA 2. ANASTAZIA NYAMUNGALA (55) WOTE WAKAZI WA KAKOZI –NAKONDE – ZAMBIA.  CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KITUO CHA AFYA TUNDUMA NA MAJERUHI WAMELAZWA KITUONI HAPO.

  KATIKA TUKIO LA TATU:
  MTU MMOJA AMBAYE BADO KUFAHAMIKA JINA LAKE, TINGO WA BASI MALI YA KAMPUNI YA SAI BABA AFARIKI DUNIA BAADA YA BASI HILO LENYE NAMBA ZA USAJILI T.668 BLD AINA YA SCANIA LILILOKUWA LIKITOKEA DAR ES SALAAM KUELEKEA SUMBAWANGA KUGONGA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.771 ATV/T.771 AUU SCANIA LORI ILIYOKUWA IMEEGESHWA BAADA YA KUHARIBIKA ENEO LA MLIMA NYOKA.
  AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 21.09.2015 MAJIRA YA SAA 22:00 USIKU HUKO ENEO LA MLIMA NYOKA, KATA YA NSALAGA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA MBEYA/NJOMBE.
  AIDHA KATIKA AJALI HIYO, ABIRIA WAWILI AMBAO PIA MAJINA YAO BADO KUFAHAMIKA WALIJERUHIWA NA WOTE WAMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA BASI HILO. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO, JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.

  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA/MICHORO NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO DEREVA WA BASI LA SAIBABA AZITOE ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.

  Imesainiwa na:
  [AHMED Z. MSANGI – SACP]
  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

  0 0

   Wananchi mbalimbali wakiwa katika banda la Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), katika maonyesho ya siku ya bahari duniani yanayoadhimishwa kitaifa Mkoani Mtwara Leo, Asubuhi.
    Wananchi mbalimbali wakipewa machapishi na mtaalam wa Mamlaka ya  Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA), wakati walipotembelea banda la Mamlaka hiyo leo asubuhi, wakati wa maadhimisho ya siku ya bahari duniani yanayoadhimishwa kitaifa mkoani Mtwara.
    Wananchi mbalimbali wakiwa katika banda la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), kwenye maonyesho ya Siku ya Bahari yanayoadhimishwa kitaifa mkoani Mtwara, kama walivyokutwa leo asubuhi.
   Kepteni Emmanuel Marijani kutoka Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini(SUMATRA), akiwapa wananchi maelezo ya namna boti zinavyotakiwa kujengwa kwa kiwango maalum kimataifa wakati walipotembelea banda la Mamlaka hiyo leo asubuhi katika maadhimisho ya siku ya bahari duniani yanyoadhimishwa kitaifa Mkoani Mtwara.
   Mtaalam kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya jamiiMifuko ya Jamii, akiwapa maelezo namna taasisi hiyo inavyofanya kazi katika maonyesho ya Siku ya BAhari Duniani yanayofanyika kitaifa Mkoani Mtwara.
  Wananchi wa Mkoani Mtwara, wakimsikiliza Afisa Mteule Daraja la Pili WOII kutoka Kikosi cha Wanamaji, Makao Makuu, Kigamboni, Dar es Salaam, Jackson Kavula, wakati wananchi hao walipotembelea banda la NAVY katika maonyesho ya Siku ya BAhari Duniani, yanayoadhimishwa Kitaifa Mkoani Mtwara.
  (Habari Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikali-Uchukuzi)

  0 0

  Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mheshimiwa Wilson Masilingi akimkabidhi Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Tuzo ya Utawala Bora ya Baraza la Biashara la Wana-Afrika Mashariki Waishio Marekani na nchi nyingine (East African Diaspora Business Council Award)  Jumatatu, Septemba 21, 2015 mjini Washington, D.C. Balozi Masilingi ndiye alimwakilisha Dkt. Kikwete katika sherehe ya kukabidhi tuzo hiyo usiku wa Jumapili, Septemba 20 kwenye Hoteli ya Hyatt Regency, Dallas, Jimbo la Texas. Picha na Freddy Maro.


  0 0

  Ofisa Masoko na Uhusiano Mwandamizi wa UTT AMIS, Martha Mashiku akitoa elimu ya uwekezaji wa pamoja kwa wafanyakazi wa hospitali ya rufaa ya Mbeya.
  Mkurugenzi wa Masoko Mwandamizi wa UTT AMIS, Daud Mbaga akitoa darasa la uwekezaji wa pamoja kwa wajasiriamali Mbeya mjini.
  Mkurugenzi wa Masoko Mwandamizi wa UTT AMIS, Daud Mbaga akitoa darasa la uwekezaji wa pamoja kwa wajasiriamali Mbeya mjini.
   Mkurugenzi wa Masoko Mwandamizi wa UTT AMIS, Daud Mbaga akitoa darasa la uwekezaji wa pamoja kwa wajasiriamali Mbeya mjini.


  0 0

   Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba (katikati), akimnadi Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba, katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu, uliofanyika katika Kata ya Makongo Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Jumapili Sept. 20.15. Kushoto ni Mgombea Udiwani wa Kata hiyo, Charles William Iteba.  PICHA ZOTE/JOHN BADI WA DAILY MITIKASI BLOG.

  Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba (katikati), akizungumza wakati akiwanadi Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba (kulia) na Mgombea Udiwani wa Kata ya Makongo, Charles William Iteba  katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu, uliofanyika Makongo Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

  Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba, akipongezwa na wanaCCM baada ya kumaliza kuhutubia  mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu, uliofanyika katika Kata ya Makongo Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. 
  Mgombea Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba, akiagana na wanaCCM baada ya kumaliza kuhutubia  mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu, uliofanyika katika Kata ya Makongo Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

  Kippi Warioba akihutubia umati wa wanaCCM na wananchi waliohudhuria mkutano huo.
  Kippi Warioba akibadilishana mawazo na Mmoja wa makada wa CCM waliohudhuria mkutano huo. Kulia ni Mkewe Nkaleni Warioba.
  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Zarina Madabida akiongozana na Kippi baada ya mkutano kumalizika.
  Mtoto akiwa bango lenye picha ya Kippi Warioba.

  XXXXXXXXXXXX


  Na Mwandishi Wetu

  MGOMBEA ubunge wa jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba, amesema anafahamu changamoto zinazowakabili wamachinga, mamalishe, baba lishe na wajaririamali wadogo; na kuomba wamchague ili azishughulikie.


  Aidha, baba mzazi wa mgombea huyo, Jaji Joseph Warioba, amewataka wakazi wa Kawe wamchague kijana wake kwa kuwa ni msikivu, anayejituma na siyo mtu wa kusukumwa.


  Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni kwenye uwanja wa Songas ulipo Kata ya Makongo Juu juzi, Kippi alisema amewahi kufanyakazi na sekta binafsi ambayo ilimkutanisha na wajasiriamali, vikundi vya ujenzi, Saccos na Vicoba, hivyo alifanikiwa kujua changamoto zinazowakabili.


  “Changamoto za makundi haya nazifahamu, nafahamu mnahitaji mafunzo na rasilimali mbalimbali kuendesha biashara zenu nithibitisheni Oktoba 25 nikazifanyie kazi,” alisema.


  Kuhusu Makongo Juu, Kippi alisema Ilani ya CCM ya mwaka 2015-2020, imeainisha kwamba barabara ya Makongo kuanzia Chuo cha Ardhi hadi Goba itajengwa kwa kiwango cha lami na tatizo la maji litakwisha kwa kuwa serikali itakamilisha mradi wa kutoa maji Kimbiji hadi Dar es Salaam.


  “Matatizo ya michango mingi shuleni ambayo wazazi wanailalamikia, uhaba wa madawati, matundu ya vyoo, vitabu na madawati ni mambo ambayo tutashirikiana kwa pamoja kuyatatua wala hayahitaji mipango mikubwa ya serikali,” alisema.


  Alisema wakazi wa Kawe wanapaswa kumchagua Dk. John Magufuli, yeye (Kippi) pamoja na madiwani wa CCM ili wakamsaidie kazi ya kutekeleza ilani.


  Naye Jaji Warioba alisema wakazi wa Kawe hawapaswi kufanya makosa ya kuchagua wagombea wa upinzani kwa kuwa serikali ya CCM chini ya uongozi wa Magufuli, itafanyakazi nzuri.


  Alisema Dk. Magufuli ni mtendaji mzuri asiyependa rushwa hivyo ni wajibu wa wananchi kumchagulia wasaidizi kutoka CCM ili wakafanyekazi ya kuwatumikia.


  Alisema hulka za Dk. Magufuli zinafanana na za mtoto wake (Kippi), kwa kuwa naye ni mchapakazi, msikivu na mtu mwenye ushirikiano mkubwa.  Naye mgombea Udiwani wa Kata ya Makongo Juu, William Iteba, alisema kero za wakazi wa kata hiyo zinajulikana ikiwamo ukosefu wa kituo cha polisi, soko na ajira; hivyo akichaguliwa atatatua kero hizo.


  0 0  KAIMU Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mushi (Kulia) akikadhi cheti cha Tuzo kwa mdau, Abbas Ally wa Kampuni ya Isere Sports inayouza vifaa vya michezo aliyeshiriki kufanikisha mkoa wa Dar es Salaam kutwaa ubingwa wa jumla katika mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) ysaliyofanyika mkoa wa Mwanza mapema mwaka huu na DAr es Salaam kutwa ushindi wa jumla kwa kujikusayia medali 26.
   WADAU wa Michezo mkoa wa Dar es Salaam wametakiwa kujitokeza kuisaidia Serikali kukuza michezo na kufufua vipaji vya wachezaji katika fani mbalimbali katika shule za msingi na Sekondari.

  Akizungumza katika sherehe ya kuwapongeza wachezaji na wadau mbalimbali walioshiriki michezo ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) Dar es Salaam juzi,Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mushi aliwataka wadau wa michezo kujitokeza kusaidia Serikali kufufua vipaji vya wachezaji kutoka ngazi ya shule ya msingi na sekondari.
  Mushi alimpongeza Rais Jakaya Kikwete anayemaliza muda wake kurudisha michezo hiyo mashuleni baada ya kuondolewa katika uongozi wa RAis Mpaka hivyo kuathiri vipaji vya vijana wengi kushindwa kung'ara katika medani ya michezo nchini.

  Katika sherehe hizo ambazo mkoa wa mkoa wa Dar es Salaam waliokuwa ukipongezwa kwa kutwaa ubingwa wa jumla za mashindano hayo yaliyofanyika mkoa wa Mwanza mapema mwaka huu,Meneja wa timu ya UMITASHUMTA ya Mkoa wa Dar es Salaam, Adolf Ally alisema haikuwa rahisi kupata ushindi huo kwa sababu mikoa mingi ilidhamiria kupata ushindi huo lakini wao walijiandaa zaidi kwa kushirikiana na wadau.

  Mkurugenzi wa MAsoko wa Kampuni ya Isere Sports, Abbas Ally ambao ni wauzaji wa vifaa michezo nchini aliyepata tuzo ya wadau waliofanikisha kupatikana kwa ushindi huo aliahidi kuongeza vifaa vyenye ubora kwa bei nafuu ili mwakani mkoa huo uendelee kuwa mabingwa.

  Aliwaomba wadau wengine kujitokeza kusaidia michezo ili kurejesha hadhi ya michezo katika shule za msingi na Sekondari ili kujenga timu imara za Ligi Kuu na timu ya Taifa ya Tanmzania (Taifa Stars).

  Mkoa wa Dar es Salaam uliochukua ushindi wa jumla kwa kutwaa medali  26 katika michezo mbalimbali lakini ikiwemo soka ya wanawake lakini ilijikuta inafungwa katika mchezo wa soka ya wamaume baada ya kupachikwa bao 1-0 na wenyeji Mwanza.

  0 0

  Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwasili kwenye Uwanja wa Boma, Mjini Masasi Mkoani Mtwara, kulikifanyika Mkutano wake wa Kampeni za kuomba ridhaa ya wananchi kugombea nafasi, uliofanyika leo Septemba 22, 2015.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI, MASASI.
  Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwapungia mkono wananchi wa Mji wa Masasi, Mkoani Mtwara, muda mfupi baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Boma, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni, leo Septemba 22, 2015.
  Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Masasi, Mkoani Mtwara, waliofikia kusikiliza sera zake katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Boma, leo Septemba 22, 2015. Ambapo amewashukuru wananchi wa Mji wa Masasi kwa mapokezi makubwa waliyompatia.
  .
  Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye akizungumza machache na wananchi wa Jimbo la Masasi Mjini, Mkoani Mtwara waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Boma, leo Septemba 22, 2015.
  .
  Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akipokea karatasi ya Shairi kutoka kwa Msoma Mashairi, Mohamed Ally (kushoto) mara baada ya kughani Shairi lake.
  Uwanja wa Boma mjini Masasi, palikuwa hapatishi pale Mgombea Urais alipowasili uwanjani hapo.

  Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akizungumza jambo na Mke wa Mwenyekiti wa Chama cha NLD, Dkt. Emmanuel Makaidi (kulia), Mama Modesta Makaidi, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Boma, leo Septemba 22, 2015.


  Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Masasi, Mkoani Mtwara, waliofikia kusikiliza sera zake katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Boma, leo Septemba 22, 2015. Ambapo amewashukuru wananchi wa Mji wa Masasi kwa mapokezi makubwa waliyompatia.
  Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye akizungumza machache na wananchi wa Jimbo la Masasi Mjini, Mkoani Mtwara waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Boma, leo Septemba 22, 2015.
  Chademaaaaaa.........
  Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akipokea karatasi ya Shairi kutoka kwa Msoma Mashairi, Mohamed Ally (kushoto) mara baada ya kughani Shairi lake.
  Mgombea wa Ubunge anaekubalika na wananchi wa Masasi kupitia Mwamvuli wa Chama cha Wananchi CUF, Ismail Makombe (Maarufu kwa Jina la Kundambada), akizungumza machache na wananchi hao waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Boma, leo Septemba 22, 2015.
  Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa kupitia Chama cha NLD, Dkt. Emmanuel Makaidi akiwa ameambatana na Mkewe, wakiwasalimia wananchi wa Mji wa Masasi, Mkoani Mtwara leo Septemba 22, 2015.

  Magambo yenye jumbe mbali mbali.
  Sehemu ya Wananchi wa Mji wa Masasi, Mkoani Mtwara wakiwa katika Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Boma, leo Septemba 22, 2015.
  Mmoja wa Wazee wa Mji wa Masasi, akiendeleo kuchukua taswira kupitia simu yake, katika Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Boma, leo Septemba 22, 2015.
  Umati wa Wananchi wa Mji wa Masasi, Mkoani Mtwara wakiwa katika Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Boma, leo Septemba 22, 2015.

  0 0

   Wananchi wa mji wa Ngara na vitongoji vyake wakiwa wamefurika kwenye viwanja vya posta mjini humo,huku wakishangilia wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi mbele yao na kuwaomba ridhaa ya kuwa Rais na kuiongoza nchi ya Tanzania katika awamu ya tano.Dkt Magufuli amekamilisha mikutano yake ya kampeni zake katika mkoa wa Kagera wenye jumla ya majimbo 9 ya Uchaguzi.   1
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. John Pombe Magufuli akitoa mpya jukwaani kwa kupiga Push Up kama kumi hivi ili kuwadhihirishia wananchi wa Mjini Karagwe mkoani Kagera  kuwa yuko fiti kiafya ili kuwatumikia watanzania mara watakapompa ridhaa ya kuwaongoza Watanzania ifikapo Oktoba 25 mwaka huu katika uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani .

  Huku umati wa Wakazi wa Karagwe ukishangilia kwa mayowe,Dkt Magufulia alieleza kuwa  kazi ya kuwatumikia Watanzania siyo rahisi ni muhimu kuwa na afya njema ili kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa na yuko tayari kuwatumikia Watanzania kwa kufanya kazi usiku na mchana.
  2
   Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika viwanja vya Posta,wilayani Ngara jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.Dkt Maguful kwa siku mbili mfululizo ameweza kukamilisha mikutano yake kwenye Wilaya  zote za Mkoa wa Kagera,ambapo kesho anaelekea mkoani Geita kwa ajili ya kujinadi kwa wananchi wa mkoa huo ili waweze kumpigia ya kuwa Rais wa awamu ya tano,katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.
    Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwafafanulia kwa umakini mkubwa alipokuwa akiwahutubia wananchi katika uwanja wa shule ya sekondari Rumanyika,wilayani Kyerwa mapema leo mchana mkoani Kagera kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
   Sehemu ya umati wa watu ulikuwa umefika kwenye mkutano wa kampeni wa Dkt Magufuli uliofanyika mapema leo mchana kwenye uwanja wa shule ya sekondari Rumanyika,wilayani Kyera mkoani Kagera.
   Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika uwanja wa shule ya sekondari Rumanyika,wilayani Kyerwa mapema leo mchana mkoani Kagera kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
   Wakazi wa Ngara na vitongoji vyale waliokusanyika kwenye viwanja vya Posta mjini Ngara jioni ya leo wakishangilia jambo,wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi mbele yao kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
     Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika viwanja vya Posta,wilayani Ngara jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
   Wananchi wa Ngara wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo wa kampeni
    Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akisisitiza jambo alipokuwa akiwahutubia wananchi katika viwanja vya Posta,wilayani Ngara jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
   Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika viwanja vya Kayanga,Karagwe mjini asubuhi hii kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
     Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi katika viwanja vya Mashujaa mjini Misenyi asubuhi hi kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni
   wakazi wa mji wa Misenyi  katika viwanja vya mashujaa wakishangilia huku wakiendelea kumsikiliza mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli,alipokuwa akijinadi kwa kumwaga sera zake na kuomba watanzania wamchague kwa ridhaa yao ili awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa awamu ya Tano

  0 0

   Mratibu wa Veta kanda ya Dar es Salaam Bi. Frorence Kapinga akiwakaribisha wakuu wa vyuo vya ufundi vyenye usajili wa awali wa VETA kanda ya Dar es Salaam kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Msimbazi jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar es Salaam. Bw.Habibu Bukko akizungumza jambo wakati wa mkutano la wakuu wa vyuo vya ufundi pamoja na kumkaribisha mgeni rasmi kwa ajili ya ufunguzi wa kutano huo. 
   Mgeni rasmi Mwalimu Charles Philemon akizungumza na wakuu wa vyuo na wawakirishi wao(hawapo pichani) wakati alipokuwa anafungua mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Msimbazi jijini Dar
  Bw. Asanterabi Kanza ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa VETA kanda ya Mashariki akiwasilisha mada kwa wakuu wa vyuo pamoja na wawakilishi wao(hawapo pichani) waliofika kwenye mkutano huo ili kukumbushana mmbo ya msingi kwenye uendeshaji wa vyuo hivyo vya ufundi.

  Mkutano ukiendelea
   
  Wakuu wa vyuo wakifuatilia kwa umakini kinachoendelea kwenye mkutano huo
   
   Picha ya Pamoja

  Na Mwandishi wetu

  KONGAMANO la wakuu wa vyuo pamoja na wamiliki wa vyuo vya ufundi stadi kanda ya Dar es Salaam lafanyika jijini Dar es Salaam kwa ajiri ya  kupeana maelekezo kwa vyuo vilivyo pata usajiri wa awali  ili waweze kupata usajiri wa kudumu vilevile kupewa hisibati na namna gani waweze kufuata taratibu ili kupata usajiri huo wa kudumu.

  Mwenyekiti wa bodi ya VETA kanda ya Dar es Salaam Mwalimu Charles Philemon  akiongea na wamiliki na wakuu wa vyuo vya ufundistadi kuhusiana na wamiliki hao kupata usajili wa kudumu kwani wao kama VETA familia wanauhitaji wa kutambua na haki ya kupata hisibati inayoonyesha aina ya kozi zinazotolewa na chuo husika kilichopo katika mfumo wa VETA, pia alisema wana mambo muhimu ambayo yanayopaswa kukumbushana ni pamoja na wanayotekeleza, kwani wao nia yao ni kutoa mafunzo kwa wanafunzi kwa uhakika ili  wao waweze kuwa mabalozi wazuri katika kazi zao wawapo nje , tuendelee kujenga mambo ya stadi za kazi katika vyuo vyetu ili kuwahakikishia wananchi kuwa tunaendelea kutoa wakufunzi wenye sifa zinazostahili lakini yote haya yanatokana na kuwa na chuo chenye usajili wa uhakika na wakufuata taratibu za mamlaka ya VETA.

  Kwani watu mbalimbali hupimwa kutokana na stadi zao mbalimbali wanazozipata  katika vyuo vyetu na kwenda nazo katika kuzitekeleza  maeneo tofauti , watu hao ambao wamepita  kupitia katika mafunzo ya ufundi stadi  VETA ndio watu wenye stadi za kazi kwani hutenda kazi kutokana na elimu na utashi  mkubwa wanaoupata katika mafunzo yao kupitia vyuo mbalimbali vyenye usajili wa VETA, anasema  “kutokana na semina zinazoendelea najua sisi ni familia moja hata kama katika familia kuna watoto warefu na wengine wafupi lakini wote ni watoto wa VETA tufanye kazi kwa umoja ili kutoa vitu vilivyobora zaidi kutofautisha na aina nyingize za utoaji mafunzo, kwani ninaamini walimu wenye ubora ndio wanaopatikana katika mamlaka ya VETA”

  Pia aliweza kusisitiza fursa ya kujengana kwa kutembeleana baina ya chuo kimoja na chuo kingine kwa ajiri ya kupata ufanisi zaidi  katika mafunzo mbalimbali pamoja na fani kwani familia inajengwa kwa kuwa na uhusiano mzuri na uzuri wa familia huonekana ndani ya VETA ni pale watu mnavyofaidika katika mambo mbalimbali iwe kwa kujengana na kusaidiana kwa kuinua kile kinacho patikana kwani muda mwingi  huwa tunakutana mara moja katika maonesho mbalimbali lakini familia hii ya VETA ni mamlaka inayo unganisha vyuo mbalimbali.

  Naye mkurugenzi wa VETA  kanda ya Dar es Salaam Bwana Habibu Bukko alisisitiza kuhusiana na kusajiliwa pamoja na kupata Hisibati itakayo saidia katika vyuo vyetu, hivyo aliweza kusema baada ya kupata usajili ndani ya miezi kumi na mbili (12) ni lazima kila chuo kiwe kimepata hisibati kwa wale wote waliokamilisha usajili huo wa mafunzo ya ufundi stadi, pia aliweza kuzungumzia nini maana ya ambapo alisema HISIBATI ni kutambua zile fani ambazo zinatolewa na chuo au umahili wachuo chako upo kwenye fani zipi.

  0 0

  Ofisa Mwandamizi Matekelezo wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bw. Frank Kilimba akifanunua jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bi. Halima Dendegu, wakati wa maonesho ya Siku ya Bahari yaliyofanyika mkoani Mtwara hivi karibuni.
  Baadhi ya wananchi waliotembelea banda la SSRA wakichukua vipeperushi mbalimbali vya SSRA katika monyesho hayo.
  Maofisa wa SSRA wakitoa maelezo kuhusu shughuli mbalimbali za mamlaka hiyo, kwa wanachi waliohudhuria maonesho ya Siku ya Bahari mkoani Mtwara.
  Maofisa wa SSRA wakitoa maelezo kuhusu shughuli mbalimbali za mamlaka hiyo, kwa wanachi waliohudhuria maonesho ya Siku ya Bahari mkoani Mtwara.
  Naibu Waziri wa Miundombinu na Uchukuzi wa Zanzibar, Issa Ussi Gavu akizungumza wakati alipotembelea banda la SSRA, wakati wa maonesho ya Siku ya Bandari yaliyofanyika mkoani Mtwara hivi karibuni. Katikati ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dkt. Juma Malik Akil.  
  Ofisa Mwandamizi Matekelezo wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bw. Frank Kilimba akimpatia maelezo Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, wakati alipotembelea banda la SSRA katika maonesho ya Siku ya Bandari yaliyofanyika mkoani Mtwara hivi karibuni.
  Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimsalimu Ofisa wa SSRA, Ally Masaninga, wakati alipotembelea banda la Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), katika maonesho ya Siku ya Bandari yaliyofanyika mkoani Mtwara hivi karibuni.
   (Picha zote na mpigapicha wetu)

  0 0

  Sehemu ya wanaCCM na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo mjini Korogwe, Mkoa wa Tanga.
  Mgombea mwenza nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na wasanii na wananchi wengine alipokuwa akiwasili katika viwanja vya Shule ya Msingi Mazoezi leo Mjini Korogwe ambapo alifanya mkutano wa kampeni.
  Mgombea mwenza nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu Hassan (kulia) akiwapokea baadhi ya wanachama wapya waliojiunga na CCM katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo Korogwe. Jumla ya wanachama 25 walijiunga na CCM katika mkutano huo.
  Sehemu ya wanaCCM na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo mjini Korogwe, Mkoa wa Tanga.
  Baadhi ya wasanii waigizaji, Wema Sepetu (kulia) na Bibi Mwenda wakizungumza na WanaCCM na wananchi katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza kuwashawishi waichague CCM kutokana na mazuri mengi iliyowafanyia wasanii.
  Mgombea mwenza nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu Hassan (kulia) akimtambulisha na kumuombea kura mgombea ubunge wa Jimbo la Bumbuli, January Makamba (katikati) katika mkutano wa hadhara wa kampeni wa mgombea mwenza uliofanyika Lushoto Jimbo la Mlalo. Kulia ni mgombea wa ubunge Jimbo la Lushoto, Shaban Shekilindi.
  Mgombea Ubunge Jimbo la Korogwe Mjini, Mary Pius Chatanda akizungumza na wanaCCM na wananchi wa jimbo hilo walipojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza leo viwanja vya Shule ya Msingi Mazoezi.

  Mgombea Ubunge Jimbo la Korogwe Mjini, Mary Pius Chatanda akizungumza na wanaCCM na wananchi wa jimbo hilo walipojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza leo viwanja vya Shule ya Msingi Mazoezi kunadi sera za CCM, huku mgongoni akiwa amebandika kipeperushi cha mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli.
  Mgombea Ubunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Profesa 'Maji Marefu' akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara wa kampeni za mgombea mwenza uliofanyika Korogwe Mjini leo.
  Sehemu ya wanaCCM na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo mjini Korogwe, Mkoa wa Tanga.

  Mwenyekiti wa CHADEMA Kata ya Kwagunda, Salehe Abdullah (kushoto) akizungumza mara baada ya kujiunga na CCM leo kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza na kukikimbia chama chake cha CHADEMA.
  Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wanaCCM na wananchi wa jimbo la Korongwe Mjini walipojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea huyo leo kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Mazoezi.
  Baadhi ya wananchi wakiwa wamemsimamisha njiani mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan eneo la Mombo ili asikilize kilio na changamoto zao kabla ya kuendelea na safari kwenda kuhutubia mkutano wa kampeni Wilaya ya Lushoto.
  Baadhi ya wananchi wakiwa wamemsimamisha njiani mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan eneo la Mombo ili asikilize kilio na changamoto zao kabla ya kuendelea na safari kwenda kuhutubia mkutano wa kampeni Wilaya ya Lushoto.
  Sehemu ya wananchi  na wanaCCM wakiwa wamemsimamisha njiani mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan eneo la Soko la Soni Lushoto ili asikilize kilio na changamoto zao hasa akinamama kabla ya kuendelea na safari kwenda kuhutubia mkutano wa kampeni Wilaya ya Lushoto.
  Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza huku wakiendelea na biashara zao sokoni hapo.
  Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza huku wakiendelea na biashara zao sokoni hapo.
  Sehemu ya wananchi  na wanaCCM wakiwa wamemsimamisha njiani mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan eneo la Soko la Soni Lushoto ili asikilize kilio na changamoto zao hasa akinamama kabla ya kuendelea na safari kwenda kuhutubia mkutano wa kampeni Wilaya ya Lushoto.
  Mgombea ubunge wa Jimbo la Bumbuli, January Makamba (kushoto) akibadilishana jambo na Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Lushoto, Balozi Abdul Mshangama leo katika Jimbo la Mlalo.
  Sehemu ya wanaCCM na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo katika Jimbo la Mlalo, Lushoto.
  Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mlalo, Shaban Omar Shekilindi akizungumza na wapiga kura wake jimboni Mlalo.
  Mgombea ubunge Jimbo la Bumbuli, January Makamba akizungumza na umati katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza, Makamba akizungumza aliwaomba wananchi wasikipe kura chama cha Chadema na ushilika wao wa UKAWA kwani wapo kwa ajili ya mabadiliko ya nafsi zao na si vinginevyo.
  Sehemu ya wanaCCM na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo katika Jimbo la Mlalo, Lushoto.
  Mgombea mwenza, Bi. Samia Suluhu (katikati) akimtambulisha mgombea ubunge wa Jimbo la Lushoto, Shaban Shekilindi.
  Mgombea mwenza, Bi. Samia Suluhu Hassan (kushoto) akimtambulisha Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mlalo, Shaban Omar Shekilindi alipokuwa akizungumza na wapiga kura wake jimboni Mlalo.
  *Imeandaliwa na www.thehabari.com

  0 0

  Ofisa Masoko na Uhusiano Mwandamizi wa UTT AMIS, Martha Mashiku akitoa elimu ya uwekezaji wa pamoja kwa wafanyakazi wa hospitali ya rufaa ya Mbeya.
  Mkurugenzi wa Masoko Mwandamizi wa UTT AMIS, Daud Mbaga akitoa darasa la uwekezaji wa pamoja kwa wajasiriamali Mbeya mjini.
  Mkurugenzi wa Masoko Mwandamizi wa UTT AMIS, Daud Mbaga akitoa darasa la uwekezaji wa pamoja kwa wajasiriamali Mbeya mjini.
   Mkurugenzi wa Masoko Mwandamizi wa UTT AMIS, Daud Mbaga akitoa darasa la uwekezaji wa pamoja kwa wajasiriamali Mbeya mjini.

  0 0

  Washiriki wa Semina ya wadau watakaoshiriki katika Utafiti wa Ujifunzaji wa Watoto (Wanafunzi) walio na Umri kati ya Miaka Saba hadi 16 katika Kusoma Kiswahili, Kiingereza na Kufanya Hesabu inayofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime kuanzia leo Septemba 22,2015 hadi kesho Septemba 23, 2015 wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Enock Waitara (Wa pili kushoto Waliokaa) ambae ni Afisa Elimu Wilaya ya Tarime Mkoani Mara.

  Na:Binagi Media Group
  Semina hiyo imeratibiwa na Shirika la Maendeleo Tarime SHIMATA chini ya Shirika la TWAWEZA kupitia mradi wake wa UWEZO ambao unafanya tathmini ya Kielimu katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda kwa wanafunzi walio na umri wa miaka Saba hadi 16 katika kujua kusoma Kiswahili, Kiingereza na Kufanya Hesabu.

  Baada ya Semina hiyo, Washiriki hao watatembelea shule za Msingi pamoja na Kaya mbalimbali kwa ajili ya utafiti huo na baadae kuwasilisha taarifa yao kwa SHIMATA na baadae TWAWEZA kwa ajili ya kupata tathimini ya hali ya elimu ilivyo Wilayani Tarime. Nchini Tanzania Mradi huo wa UWEZO unajumuisha Wilaya 159.

  Akifungua Semna hiyo, Afisa Elimu Wilaya ya Tarime Enock Waitara amewataka washiriki hao kuja na tathimi ya hali halisi ya kielimu Wilayani Tarime na namna ya kufanya ili kupandisha kiwango cha ufaulu kwa kuwa tafiti zilizopita zinaonyesha kuwa hali ya ufaulu kwa shule za msingi siyo nzuri huku akisikitishwa wanafunzi kumaliza darasa la saba na kuijiunga na kidato cha kwanza huku wakiwa hawajui kusoma na kuandika. 
  Washiriki wa Semina ya wadau watakaoshiriki katika Utafiti wa Ujifunzaji wa Watoto (Wanafunzi) walio na Umri kati ya Miaka Saba hadi 14 katika Kusoma Kiswahili, Kiingereza na Kufanya Hesabu inayofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime kuanzia leo Septemba 22,2015 hadi kesho Septemba 23, 2015 wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Enock Waitara (Wa pili kushoto Waliokaa) ambae ni Afisa Elimu Wilaya ya Tarime Mkoani Mara.
  Washiriki wa Semina ya wadau watakaoshiriki katika Utafiti wa Ujifunzaji wa Watoto (Wanafunzi) walio na Umri kati ya Miaka Saba hadi 14 katika Kusoma Kiswahili, Kiingereza na Kufanya Hesabu inayofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime kuanzia leo Septemba 22,2015 hadi kesho Septemba 23, 2015 wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Enock Waitara (Wa pili kushoto Waliokaa) ambae ni Afisa Elimu Wilaya ya Tarime Mkoani Mara.
  Washiriki wa Semina ya wadau watakaoshiriki katika Utafiti wa Ujifunzaji wa Watoto (Wanafunzi) walio na Umri kati ya Miaka Saba hadi 14 katika Kusoma Kiswahili, Kiingereza na Kufanya Hesabu inayofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime kuanzia leo Septemba 22,2015 hadi kesho Septemba 23, 2015 wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Enock Waitara (Wa pili kushoto Waliokaa) ambae ni Afisa Elimu Wilaya ya Tarime Mkoani Mara.
  Edward Mulemwa ambae ni Mratibu wa Mradi wa UWEZO Wilayani Tarime akizungumza wakati wa semina
  Edward Mulemwa ambae ni Mratibu wa Mradi wa UWEZO Wilayani Tarime akizungumza wakati wa semina

  Edward Mulemwa ambae ni Mratibu wa Mradi wa UWEZO Wilayani Tarime akizungumza wakati wa semina
  Edward Mulemwa ambae ni Mratibu wa Mradi wa UWEZO Wilayani Tarime akizungumza wakati wa semina
  Mwenyekiti wa Shirika la Maendeleo Tarime SHIMATA Joseph Magabe akizungumza wakati semina
  Mgeni Rasmi ambae ni Afisa Elimu Wilaya ya Tarime Enock Waitara
  Mgeni Rasmi ambae ni Afisa Elimu Wilaya ya Tarime Enock Waitara akifungua Semna
  Seemina ikiendelea
  Washirki wa Semina
  Wshiriki wa Semina
  Washiriki wa Semina
  Washiriki wa Semina
  Chai
  Chai
  Chai
  Muda wa Chai
  Mapumziko kwa ajili ya chai
  Washiriki wa Semina Wakitokelezea na kamera ya BMG
  Kushoto ni Mwanahabari kutoka Sahara Media Group akifanya Mahojiano na Edward Mulemwa ambae ni Mratibu wa Mradi wa UWEZO unaosimamiwa na Taasisi ya TWAWEZA Wilayani Tarime
  Kushoto ni Mwanahabari kutoka Sahara Media Group akifanya mahojiano na Mwenyekiti wa Shirika la Maendeleo Tarime SHIMATA Joseph Magabe (Kulia)
  Baita Matinyi ambae ni Mratibu kutoka Shirika la Maendeleo Tarime SHIMATA

  0 0

  Kulia ni Mzee Hezekia (Maina) Binagi wa Kenyamanyori Tarime Mkoani Mara akipokea Mahali ya binti wa Kaka yake kutoka kwa Mzee Samweli Chaha Kebasa (Kushoto) Mkazi wa Rebu Tarime.
  Na:George GB Pazzo
  Baadhi ya Watu wamekuwa wakiita ni Zawadi inayotolewa kwa Wazazi ama Walezi pindi binti anapokuwa katika mipango ya kuolewa. Lakini kwa umaarufu wake, watu wengi wamekuwa wakiita Mahali.


  Kwa siku za hivi karibuni kumekuwepo na majadiliano makali juu ya dhana halisi ya Mahali. Hoja mbalimbali zimekuwa zikitolewa zikieleza kuwa suala la Mahali kwa sasa si muhimu sana kama ilivyokuwa katika miaka ya zamani hususani kwa baadhi ya makabila nchini ikiwemo kabila la Wakurya wanaopatikana Mkoani Mara ambapo wazee wa kabila hilo walikuwa wakipokea mamia ya ng’ombe kama mahali pindi mabinti zao walipokuwa katika mipango ya kuolewa.


  "Kwa kabila la Wakurya bado suala la Mahali lina umuhimu mkubwa japo kumekuwepo na mabadiliko kidogo. Zamani binti wa kikurya alipokuwa akitaka kuolewa, Wazazi ama Walezi wake walikuwa wakipokea mamia ama makumi ya ng’ombe kama sehemu ya mahali". Anaeleza mmoja wa wazee Wilayani Tarime na kuongeza;


  "Lakini hivi sasa hali haiko hivyo tena kwani binti wa kikurya anaweza kuolewa kwa Mahali chini ya ng’ombe 10 ama pesa kati ya Shilingi Laki Nne hadi Milioni Moja na Laki Tano hii ikitegemea nafasi aliyo nayo binti. Mfano Mahali inaweza kupanda kama binti ni msomi, Mrembo ama mwenye nidhamu na maadili mema katika jamii".


  Miongoni mwa maoni yanayotolewa na baadhi ya wanaharakati wa kutetea haki za binadamu yanakinzana na uhalali wa Mahali kwa misingi kwamba suala la Mahali limekuwa halichukuliwi kama zawadi na watu wengi na badala yake limekuwa likisababisha muoaji (Mme) kumnyanyasa muolewaji (Mke) kwa minajili ya kwamba yeye ndie mwenye maamuzi ya mwisho juu ya mkewe kwa kuwa tayari anakuwa amemlipia mahali ambapo hatua hiyo huondoa dhana kuwa Mahali ni zawadi na kugeuka kuwa kumtolea binti Mahali ni sawa na kumnunua ijapokuwa dhana hii inapingwa sana na watu wengi.


  Hata hivyo baadhi ya Wazee kutoka Kabila la Wakurya Wilayani Tarime waliozungumza na Binagi Media Group wanaeleza kuwa bado suala la Mahali lina umuhimu mkubwa sana hususani katika Kabila la hilo la Wakurya na kwamba binti akitolewa mahali hueshimika katika jamii huku urafiki baina ya pande zote mbili za familia kwa maana ya Mme na Mke ukiimarika zaidi.


  Je wewe una mtazamo gani juu ya Mahali kwani licha ya kuchukuliwa kama zawadi, baadhi ya watu wamekuwa wakisema kuwa kumtolea binti Mahali ni sawa na kumnunua. Wasiliana nasi kupitia nambari +255 (0) 757 43 26 94 au barua pepe binagimediagroup@gmail.com  Tazama picha za Sherehe ya Mahali ya Milika Daniel Marwa Binagi Mzaliwa wa Kijiji cha Kenyamanyori kwa sasa akiishi Mtaa wa Rebu ambae anatarajia kufunga ndoa na John Samwel Chacha Kebasa mkazi wa Mtaa Rebu pia ikiwa ni Wilaya ya Tarime Mkoani Mara.


  Wa pili Kulia waliokaa ni Mzee Hezekia (Maina) Binagi wa Kenyamanyori Tarime Mkoani Mara akipokea Mahali ya fedha kwa ajili ya kumuoza binti wa Kaka yake aitwae Milika Daniel Marwa Binagi kutoka kwa Mzee Samweli Chacha Kebasa (Kushoto) Mkazi wa Rebu Tarime.
  Mahali Ikihesabiwa
  Kushoto ni Professor Lloyd Binagi (Manamba) na Kulia ni Mzee Chaha Binagi wakihesabu pesa kwa jili ya Mahali ya binti yao
  Baada ya Mahali kukamilika hatua iliyofuata ni familia ya mme na mke kusaini mkataba wa Makubaliano chini ya usimamizi wa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa
  Mkataba ukisainiwa
  Kulia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Buguti Rebu James Masoya akikabidhi Mkataba wa Mahali na Mzee Maina (Kushoto) ikiwa ni upande wa binti
  Kulia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Buguti Rebu James Masoya akikabidhi Mkataba wa Mahali na Mzee Samwel Chacha Kebasa (Kushoto) ikiwa ni upande wa mme
  Sasa ni Msosi ambapo wageni upande wa binti wamekaribishwa na wenyeji wao upande wa mme
  Sasa ni Msosi ambapo wageni upande wa binti wamekaribishwa na wenyeji wao upande wa mme
  Wa kwanza kushoto waliosimama ndie Mkwe na hapo anatambulishwa Wazee
  Picha ya Pamoja baina ya familia zote mbili kwa maana na mme na mke
  Wazee wakibadilishana mawazo
  Ndugu, jamaa na marafiki wakifurahia
  Ndugu, Jamaa na Marafiki walioalikwa
  Ndugu, Jamaa na Marafiki walioalikwa
  Ndugu, Jamaa na Marafiki walioalikwa
  Ndugu, Jamaa na Marafiki walioalikwa
  Wazee upande wa binti wakirejea nyumbani baada ya sherehe ya kuchukua Mahali kufikia tamati
  Ndugu upande wa Binti wakirejea nyumbani baada ya sherehe ya Mahali kukamilika
  Ndugu upande wa Binti wakirejea nyumbani baada ya sherehe ya Mahali kukamilika
  Hatimae wazee wakafika nyumbani na kufikisha habari njema kuwa Mahali imechukuliwa na hapa wakaweka kumbukumbu ambapo Kutoka Kushoto ni Mzee Maina Binagi, Milika Daniel Binagi na mwanae, Mzee Chacha Binagi, Leah Daniel Binagi pamoja na Professor Lloyd Binagi

  0 0

  Mkurugenzi wa Maendeleo wa Don Bosco toka Ubeligiji, Filip Lammens (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari katika Mkutano wa kujadili Uwezeshaji kwa vijana ulioandaliwa na Don Bosco Kanda ya Afrika Dar es Salaam leo asubuhi.
  Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi wa Don Bosco, Afrika Mashariki, Padri Eric Mairura (kushoto), akizungumza na wanahabari kuhusu mkutano huo.
  Mkurugenzi wa Ofisi ya Mipango na Maendeleo Afrika Magharibi wa Don Bosco, Tsedi Yao Ati akizungumza na wanahabari.
  Mkurugenzi wa Ofisi ya Mipango na Maendeleo na Msimamizi wa Fedha na Uchumi wa Nchi za Maziwa Makuu, Rwanda, Burundi na Uganda, Br. John Njuguna akizungumza na wanahabari kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Don Bosco.
  Mtunza Mitaala wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA), Rehema Binamungu (kushoto), akitoa mada katika Mkutano huo wa kujadili Uwezeshaji kwa vijana ulioandaliwa na Don Bosco Kanda ya Afrika Dar es Salaam leo asubuhi.
  Mwezeshaji akitoa mada.
  Washiriki kutoka nchi mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.
  Mkutano ukiendelea.
  Washiriki kutoka nchi mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.
  Mkutano ukiendelea.

  Wajumbe wakiwa kwenye mkutano huo.
  Wajumbe wakiwa kwenye mkutano huo.
  Taswira katika chumba cha mkutano.
  Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.

  Na Dotto Mwaibale

  CHUO cha Ufundi Stadi (VETA), kimesema kipo katika mchakato wa kuandika vitabu vya ufundi  ili kwenda sambamba na ukuaji wa teknolojia nchini.

  Hayo yalibainishwa na Mtunza Mitaala wa VETA, Rehema Binamungu katika Mkutano wa kujadili Uwezeshaji kwa vijana ulioandaliwa na Don Bosco Kanda ya Afrika Dar es Salaam leo.

  Alisema vitabu hivyo vitasaidia kutoa elimu ya ufundi katika vyuo vingine na shule mbalimbali nchini.

  Katika hatua nyingine Binamungu alisema Veta inahitaji kuwa na vifaa vya ufundi vya kisasa ili kukabiliana na kukua kwa teknolojia ya ufundi ambayo inahitaji kuwa na vifaa hivyo ili kwenda sambamba na soko la ajira.

  "Kutokana na kukua kwa teknolojia kwa sasa tunahitaji vifaa vya kisasa na maboresho ya vifaa ili twende sambamba na soko la ajira,"alisema Rehema.

  Aliongeza changamoto nyingine inatokana na chuo hicho kutoa elimu ya ufundi kwa watu wenye elimu tofauti hivyo jitihada zinahitajika ili kutoa elimu bora,"alisema Rehema.

  Pia alisema VETA ipo katika mchakato wa kuandika vitabu vya kiufundi ambavyo vitasaidia kuinua elimu ya ufundi nchini.

  Akizungumzia uwezeshaji kwa vijana wanaopata mafunzo kwenye vyuo mbalimbali alisema ushirikiano unahitajika kati ya serikali na wadau mbali ili kuhakikisha wanashirikiana kutoa elimu bora na yenye manufaa kwa jamii.

  Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi wa Don Bosco Afrika Mashariki, Padri Erick Mairura alisema mkutano huo utasaidia kuwaondoa vijana katika lindi la umaskini.

  Alisema hali ya kiuchumi kwa vijana bado ipo chini hivyo ni vyema serikali na wadau wa elimu ya ufundi wakashirikiana kuandaa maisha bora kwa vijana.

  Alisema  mkutano huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kuwaondoa vijana katika lindi la umaskini na utachangia kukuza ushirikiano kati ya sekta binafsi, wamiliki wa vyuo vya ufundi pamoja na serikali.

  “Masomo ya ufundi yakitolewa ipasavyo yatasaidia kuwakwamua vijana katika changamoto mbalimbali hivyo ni muhimu sote tuone namna ya kuboresha vyuo vyetu na kuwawezesha vijana,” alisema Mairura.

  Alisema anatoa wito kwa serikali kuviwezesha vyuo vya ufundi kwa kushirikiana navyo kwa karibu kama ambavyo nchi nyingine zinafanya.

  Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Ofsi ya Mipango na Maendeleo Afrika Magharibi- Don Bosco, Tsedi Yao Ati alisema kuwafundisha vijana ufundi kutasaidia kuboresha maisha yao kwani vijana wapo wengi na hawana shughuli maalum wanazozifanya kwa sababu mbalimbali.

  Meneja Mradi wa Don Bosco, Badru Juma alisema wamekuwa wakishirikiana na makampuni mbalimbali katika kuwawezesha vijana kupata elimu mbalimbali kwa ajili ya kujikwamua.

  Alisema barani Afrika kuna nchi 154 ambazo zina vituo vya Don Bosco na wamekuwa wakishirikiana katika kuondoa changamoto mbalimbali pamoja na kuwakwamua vijana ili waweze kujiajiri ama kuajiriwa.

  “ Tumekuwa tukiangalia mambo mbalimbali ambayo yatasaidia kuwawezesha vijana na hivi sasa tumeanzisha utaratibu mpya wa kuboresha mahusiano kati yetu , sekta  binafsi, VETA na serikali ili tuone jinsi ambavyo tunaweza kuwaondoa vijana katika lindi la umaskini,”alisema Juma.
  (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com

older | 1 | .... | 648 | 649 | (Page 650) | 651 | 652 | .... | 1898 | newer