Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 63 | 64 | (Page 65) | 66 | 67 | .... | 1896 | newer

  0 0

   Mtaalamu wa Kusaidia Utoaji Damu Mpango wa Taifa wa Damu Salama Kanda ya Mashariki, Peter Chame, akitoa Maelezo Kuhusiana na Mpango huo wa Kuchangia wakati wa Semina katika Chuo Cha Dar es Salaam City College Kilichopo Kibamba Jijini Dar es Salaam Leo(Picha Kwa Hisani ya Miss Demokrasia Tanzania)
  Afisa Uhamasishaji Mpango wa Taifa wa Damu Salama Kanda ya Mashariki, Desteria Nanyanga, akifanya Upimaji wa Damu kwa Mwanafunzi wa Chuo Cha Dar es Salaam City Colege, Devotha Butondo, wakati wa Semina katika Chuo Cha Dar es Salaam City College Kilichopo Kibamba Jijini Dar es Salaam Leo

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Bi. Margareth Thatcher, aliyefariki wiki iliyopita kwa ugonjwa wa Kiharusi. Makamu amesaini kitabu hicho kwenye Ofisi za Ubalozi wa Uingereza nchini zilizopo jijini Dar es Salaam.Picha na OMR
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Bi. Margareth Thatcher, aliyefariki wiki iliyopita kwa ugonjwa wa Kiharusi. Makamu amesaini kitabu hicho kwenye Ofisi za Ubalozi wa Uingereza nchini zilizopo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Balozi wa Uingereza nchini, Dianne Melrose.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi wa Uingereza nchini, Dianne Melrose, wakati alipowasili kwenye Ofisi za Ubalozi huo, zilizopo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusaini katika kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa Waziri wa zamani wa Uingereza, Margareth Thatcher, aliyefariki wiki iliyopita kwa ugonjwa wa Kiharusi.

  0 0


  0 0


   Picha ya pamoja ya wanachama  wa Jumuiya ya Uvuvi na Mazingira Endelevu Zanzibar baada ya kumalizika kwa uchaguzi uliowachagua viongozi mbalimbali wa Jumuiya hiyo.(PICHA NA MAKAME MSHENGA-MAELEZO ZANZIBAR.)
   Mmoja ya wanacha wa Jumuiya ya Uvuvi na Mazingira Endelevu Zanzibar Haji Khamis Hasan, akipiga kura kuwachaguwa viongozi mbalimbali watakayo iyongoza Jumuiya hiyo. 
    Katibu wa Jumuiya ya Uvuvi na Mazingira Endelevu Zanzibar Husen Muhammed Makame, akionyosha Cheti cha usajili pamoja na Katiba ya Jumuiya hiyo huko katika Skuli ya Sekondari ya JKU Mtoni. 
   Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uvuvi na Mazingira Endelevu Zanzibar Sheha Chum Mngana, akizungumza na wanachama mara tu baada ya kumaliza kwa uchaguzi huko katika Skuli ya Sekondari ya JKU Mtoni.
  =============  =========  ==========
   Miza Othman   Maelezo     Zanzibar         
                                 Imelezwa kuwa iwapo patakua na mashirikiano katika Jumuiya ya  Uvuvi na  Mazingira Endelevu Zanzibar (ZFSE) iliyopo  Mtoni  Kidatu hakuna sababu ya umoja huo kutoyafikia malengo waliyojipangia.
   Hayo yamelezwa na Mwenyekiti wa ZFSE  Sheha Chumu Mngana wakati alipokuwa akizungumza  na wanjumuiya hiyo baada ya kuchaguliwa  rasmi kuongoza Jumuiya hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu katika uchaguzi uliofanyika skuli ya  sekondari  ya JKU Mtoni nje kidogo ya Mji wa  Zanzibar.
  Amesema ni vyema  kwa Jumuiya  hiyo kutekeleza majumu yao   waliojipangia pamoja na kubuni miradi mbali mbali ili kuleta maendeleo katika Jumuiya yao.
  ‘’Bila mashirikiano, hatutofikia popote, kuwa makini au kujielewa na kutekeleza majukumu na kila mwanachama anawajibu wa kupatiwa haki’’ Alisema Sheha Chumu Mngana.
  Katika uchaguzi huo  wamechaguliwa wajumbe wanne wa Kamati Kuu  ikiwa ni njia mojawapo ya kuipa nguvu jumuiya hiyo  ambao ni  Zena Husein Suwedi, Haji Khamis Hassan,  Mansab Ramadhan Mansab na Mashavu Mzee Moh’d.
  Aidha Mwenyekiti  Sheha Chumu  amesema   Jumuiya yao  yenye wanachama 20 wakiwemo wanaume 10 na wanawake 10  inakabiliwa na changamoto mbali mbali katika  ikiwemo ofisi ya kudumu  pamoja na vitendea kazi  jambo ambalo linapelekea kukwamisha  ufanisi wa Jumuiya yao.
  Jumuiya ya Uvuvi na Mazingira Endelevu Zanzibar ilianzishwa mwaka jana na  imepatiwa  usajili rasmi tarehe 12 /4/ 2013  na Mrajisi  Mkuu  wa Serikali  Nd. Abdallah Wazir. 

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu Meja Generali Makame Rashid, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya TMJ, jijini Dar es Salaam. Shughuli za kuagwa mwili wa marehemu Makame, zimefanyika leo Aprili 15, 2013 kwenye viwanja vya Makao Makuu ya JKT jijini.
  Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin William Mkapa akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu Meja Generali Makame Rashid, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya TMJ, jijini Dar es Salaam. Shughuli za kuagwa mwili wa marehemu Makame, zimefanyika leo Aprili 15, 2013 kwenye viwanja vya Makao Makuu ya JKT jijini.
  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,Jenerali Davies Mwamunyange akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu Meja Generali Makame Rashid, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya TMJ, jijini Dar es Salaam. Shughuli za kuagwa mwili wa marehemu Makame, zimefanyika leo Aprili 15, 2013 kwenye viwanja vya Makao Makuu ya JKT jijini.
  Makamanda wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa  marehemu Meja Generali Makame Rashid, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya TMJ, jijini Dar es Salaam. Shughuli za kuagwa mwili wa marehemu Makame, zimefanyika leo Aprili 15, 2013 kwenye viwanja vya Makao Makuu ya JKT jijini.
  Jeneza likiwekwa sehemu maalum kwa ajili ya heshima za mwisho.
  Makamu wa Rais Dkt. Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na Mkuu wa Majeshi Davis Mwamunyange.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya marehemu Meja Generali Makame Rashid, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya TMJ, jijini Dar es Salaam. Shughuli za kuagwa mwili wa marehemu Makame, zimefanyika leo Aprili 15, 2013 kwenye viwanja vya Makao Makuu ya JKT jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue akitoa mkono wa pole kwa ndugu wa Marehemu Meja Generali Makame Rashid, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya TMJ, jijini Dar es Salaam. Shughuli za kuagwa mwili wa marehemu Makame, zimefanyika leo Aprili 15, 2013 kwenye viwanja vya Makao Makuu ya JKT jijini.
  Toka kushoto ni Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi (JWTZ),Luteni Jenerali,Samuel Ndomba,Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,IGP Said Mwema na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini,Kamishna Jenerali John Minja wakiwa kwenye msiba wa Marehemu Meja Generali Makame Rashid, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya TMJ, jijini Dar es Salaam. Shughuli za kuagwa mwili wa marehemu Makame, zimefanyika leo Aprili 15, 2013 kwenye viwanja vya Makao Makuu ya JKT jijini.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akitoa mkono wa pole kwa ndugu wa Marehemu Meja Generali Makame Rashid, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya TMJ, jijini Dar es Salaam. Shughuli za kuagwa mwili wa marehemu Makame, zimefanyika leo Aprili 15, 2013 kwenye viwanja vya Makao Makuu ya JKT jijini.
  Ndugu wa Marehemu wakiwa ni wenye majonzi na huzuni kubwa ya kuondokewa na Mpendwa wao.Picha na OMR.

  0 0


  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kucheza ngoma ilkiyokuwa ikipigwa na kina mama, kwenye tawi la CCM Nawenge Ulanga, alipowasili kwenye tawi hilo kukagua uhai wa Chama, Aprili 15, 2013.
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika Kijiji cha Mwaya, Ulanga, Morogoro, Aprili 15, 2013.
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipokea kadi ya Chadema kutoka kwa aliyekuwa mwanachama wa chama hicho, Abeid  Mloka aliyetangaza kuhamia CCM, wakati Kinana alipohutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika kijiji cha Mwaya, Ulanga mkoani Morogoro, Aprili 15, 2013. Mloka alikuwa miongoni mwa vijana watano walioamua kuahamia CCM papo hapo.
   Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Muhammed Seif Khatib, akionyesha kadi za Chadema ambazo vijana waliokuwa wanachama wa chama hicho waliamua kumkabidhi papo hapo, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwenye mkutano  mkubwa wa hadhara  uliofanyika Aprili 15, 2013, kwenye  Kijiji cha Mwaya, Ulanga mkoani Morogoro.
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpokea Pancras Mogela aliyekuwa mwanachama wa Chadema akipoamua kujiunbga na CCM, Kinana alipotembelea tawi la CCM Viwanjani, Ulanga mkoani Morogoro, kukagua uhai wa Chama kwenye tawi hilo, Aprili 15, 2013. Kushoto ni Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Muhammed Seif Khatib.
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikabidhi Mbuzi kwa Nahodha wa timu ya Libenenga, Steven Maundu, baada ya timu hiyo kuibuka mshindi kwa kuibugiza timu ya Nkongo mabao 2-0, katika mechi ya fainali ya Kinana CUP, kwenye Uwanja wa Mwaya, Ulanga mkoani Morogoro, Aprili 15, 2013. Pamoja na zawadi hiyo, ameipatia timu hiyo zawadi ya sh. 100,000 kiasi kinacholingana na alichoipa timu iliyofungwa. Kulia ni  Nahodha wa timu ya Nkongo, Abdallah Mazengo.
  Mwenyekiti wa  CCM shina la Mawasiliano, Ulanga, mkoani Morogoro, Petro Kabisi akiwatambulisha viongozi wa shina hilo kwa  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana aliyetembelea tawi hilo kukagua uhai wa Chama, Aprili 15, 2013.
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitia saini kitabu wageni alipokagua uhai wa Chama kwenye tawi la CCM la Ulanga mjini,mkoani Morogoro, Aprili 15, 2013. Kushoto ni Katibu wa NEC, Oganaizesheni Mohammed Seif Khatib.
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikabidhi kadi kwa Magdalena Mashinga, alimkabidhi kadi za CCM kwa wanachama wapya kwenye tawi la CCM la Mawasiliano, wilayani Ulanga,Aprili 15, 2013, akiwa katika ziara ya kuimarisha uhai wa chama mkoani Morogoro. Kushoto ni Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Muhammed Seif Khatib na Mwenyekiti wa CCM mkoa hu, Innocent Edward.
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsikiliza kwa makini Katibu wa tawi la CCM  Kiwanjani, Ulanga,mkoani Morogoro,  Francis Kanyali aliyekuwa akisoma taarifa, Kinana alipotemebea tawi hilo kukagua uhai wa Chama, Aprili 15, 2013.
  Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Muhammed Seif Khatib akikagua daftari la wanachama wa CCM kwenye tawi la Mawasiliano, Ulanga mkoani Morogoro, alipofika hapo na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Aprili 15, 2013.
  Wananchi wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika Aprilki 15, 2013 kwenye Uwanja wa Mwaya, Ulanga mkoani Morogoro.
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana  akiwa katika picha ya pamoja na  viongozi wa CCM tawi la Ulanga Mjini mkoani Morogoro, baada ya kukagua uhai wa Chama kwenye tawi hilo, Aprili 15, 2013.Picha na Bashir Nkoromo

  0 0

  Picha juu na chini Mgeni rasmi Mh. Mstahiki meya wa Halmashauri ya manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akikabidhi jezi na mipira kwa baadhi ya timu 17 zilizoshiriki katika bonanza hilo.
  Diwani wa Kata ya Kipawa Mheshimiwa Bonna Kaluwa akigawa jezi na mipira kwa timu zilizoshiriki Bonanza la Stakishari Veterans kutimiza miaka 5.
  Mgeni rasmi Mh. Mstahiki meya wa Halmashauri ya manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akijiandaa kupiga penati kuashiria ufunguzi wa Bonanza hilo lililofanyika katika viwanja vya Stakishari kata ya Gongo la Mboto jijini Dar.
  Mstahiki Meya Jerry Silaa akionyesha ufundi na kufunga goli wakati akipiga penati ya kuzindua rasmi bonanza la Stakishari Veterans FC kutimiza miaka 5.


  Mstahiki Meya Jerry Silaa akipongezwa na Golikipa aliyemfunga goli kwa penati wakati akizundua Bonanza hilo.
  Mgeni rasmi Mstahiki Meya Katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa timu ya Stakishari Veterans FC iliyofanya Bonanza la kutimiza miaka 5 Kipawa jijini Dar.
  Bonanza likirindima katika viwanja vyaStakishari Kipawa kata ya Gongo la Mboto baada ya kupewa baraka na Mstahiki Meya Jerry Silaa.

  Picha juu na chini ni Mgeni rasmi Mh. Mstahiki meya wa Halmashauri ya manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akizungumza wananchi pamoja na washiriki wakati wa bonanza la timu ya Stakishari Veterans FC kutimiza miaka 5 ambapo amesema mpira wa soka unawakutanisha watu na kuwasidia kujenga mahusiano pamoja na kujenga afya za miili yao.  Timu zilizoalikwa kushiriki Bonanza la Sitakishari VSC
  New Ukonga Veteran - Ukonga
  Pugu Kajiungeni Veteran - Pugu
  Pugu Kigogo Fresh Veteran -Pugu
  Segerea Veteran - Tabata
  Kivule Veteran - Kivule
  Kipunguni B Veteran - Kipunguni
  Kinyerezi Veteran - kinyerezi
  Tabata Veteran - Tabata
  Bandari Veteran - Kurasini
  Mbagala Veteran - Mbagala
  Makangarawe Veteran - Mbagala
  Airport Veteran - Airport
  Kisukulu Veteran – Kisukulu Tabata
  Kigamboni Veteran - Kigamboni
  Vingunguti veteran - Vingunguti
  Wenyeji Sitakishari veteran

  0 0


  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kuzalisha mbegu bora za mazao ya mboga ya Rijk Zwaan  Bwana Kees Reinink akimuonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete baadhi ya miche inayotokana na mbegu bora wakati Rais alipotembelea makao makuu ya Kampuni hiyo katika kitongoji cha De Lier nje kidogo ya jiji la The Hague,nchini Uholanzi jana. Wapili kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa SAGCOT Bwana Geoffrey Kirenga.Kampuni ya RIJK ZWAAN tayari imewekeza nchini Tanzania huko Arusha ambapo inazalisha mbegu bora za mazo ya mbogamboga zilizofanyiwa utafiti kudhibiti magonjwa.

   Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholanzi Frans Timmermans akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika makazi rasmi ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo jijijini The Hague na kufanya naye mazungumzo rasmi.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo Rasmi na ujumbe wa Serikali ya Uholanzi ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya nchi za nje wan chi hiyo Bwana Frans Timmermans jijini The Hague Uholanzi.


   -Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na uongozi wa Kampuni ya Utafiti na Uzalishaji mbegu bora za mazao ya mboga ya RIJK ZWAAN jana katika kitongoji cha De Lier nje kidogo ya jiji la The Hague.

   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa pamoja na Malkia Beatrix wa Uholanzi wakati walipomtembelea Malkia huyo katika makazi yake Rasmi jijini The Hague jana.Rais Kikwete yupo nchi Uholanzi kwa Ziara rasmi.Picha na Fred Maro-Ikulu.

  0 0

  Timu nne zitakazochuana katika kipindi cha tano cha Guinness Football Challenge wiki hii. Kutoka kushoto ni timu kutoka Kenya(wamevaa nyekundu), Tanzania – bluu, Uganda- kijani na nyeusi.

  ==========  ========  

  *TIMU NNE MPYA KUINGIA KIPINDI CHA MWISHO CHA GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ AFRIKA MASHARIKI*


  April 10, 2013, Dar es Salaam; Jumatano iliyopita katika sehemu ya nne kupitia televisheni za ITV na Clouds TV, mashindano ya GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ yalikuwa na ushindani mkubwa  lakini washiriki kutoka Kenya Enphatus Nyambura na Samuel Papa waliweza kumudu vishindo na kufanikiwa kuwa timu ya tatu kutoka Kenya kuingia katika hatua ya Pan- Africa, baada ya kuwapiga chini timu za Tanzania na Uganda.

   Katika kipindi hiki cha nne washiriki walijitahidi kufanya vizuri katika kuonesha uwezo wao wa kuchezea mpira na kujipatia alama nyingi japo walishindwa kujibu maswali kwa ufasaha.Washiriki kutoka Kenya walifanikiwa kufika katika hatua ya mwisho ya kulenga  ukuta  wa pesa wa Guinness ambapo walijishindia dola kimarekani  1,500.


  Enphatus na Samwel wana nafasi ya kuiwakilisha nchi yao katika mashindano yajayo ya Pan-African ambapo wanaweza kubahatika kujinyakulia  kitita cha fedha  za kimarekani hadi kufikia dola  250,000. Washiriki bora watakwenda kukutana uso kwa uso na mashabiki wa soka kutoka nchi za Cameroon,Ghana,Tanzania, Kenya, na Uganda  ili atakayeonesha ufahamu na ujuzi zaidi wa soka atavishwa taji la ubingwa wa` Pan-African’.


  GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha runinga kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya  Endemol.  Kipindi hiki kinarushwa kila Jumatano katika televisheni za ITV na clouds TV.  Kipindi kitaruhswa na kituo cha ITV kuanzia saa tatu na dakika kumi na tano(3:15) usiku  ambapo  Clouds TV itarusha kipindi hicho  saa mbili na dakika kumi na tano(2:15) usiku .


  Katika kipindi cha tano cha mashindano haya yatakayooneshwa na vituo vya televisheni vya ITV na Clouds TV, timu nne ndizo zitakua uwanjani kuchuana vikali, ni timu ipi itakayowapiga chini wengine na kuingia katika hatua ya Pan Africa? Majibu yote yatapatikana Jumatano hii.

                 

  Timu ya blu-Tanzania:

  ·         Khenry Sadallah(26) na Abubakari Mohamed(19)  kutoka Dar-es-Salaam watashiriki katika sehemu ijayo. Harry atakuwa kichwa cha timu ambaye ni mshabiki wa AC Milan wakati Abubakari  ambaye ni mwanafunzi na mshabiki wa Manchester United ataonesha  uwezo wake wa kucheza mpira


  Timu nyekundu-Kenya:

  ·         Ken Muturi (26) na Chris Mwamgi (19) wote kutoka Nairobi wanamatumaini makubwa yakuwa timu ya mwisho kuingia kwenye mashindano ya Pan African.  Ken ni mfanyabiashara kwa njia ya mtandao, ni mpenzi wa mpira wa miguu ambapo atakuwa kichwa cha timu wakati Chris ambaye ni mchezaji wa Springland FC ataonesha kipaji chake cha mpira wa miguu.

    
  Timu ya kijani-Uganda

  ·         Mfanyabiashara Ian Ford(24) na mwanafunzi wa uchumi Herbet Odipio(23) kutoka Kampala ni mashabiki wa Manchester United watashiriki katika kipindi kijacho cha mashindano Guinness Football Challenge. Ian atakuwa kichwa cha timu wakati Herbet ataonesha uwezo wake wa kusakata kabumbu.


  Timu nyeusi-Uganda:
  Edward Lyukamuzi(23) na Timothy Nimungu(22) kutoka Kampala ni timu ya pili kutoka Uganda watashiriki kipindi cha 5 cha mashindano haya. Edward ni mtaalamu wa Teknolojia ya mawasiliano ndiye kichwa cha timu wakati Timothy ambaye ni mtaalamu wa masoko atonesha uwezo wake wa kucheza soka.


  Wapenzi wa kipindi hiki cha Guinness Football Challenge barani Afrika wanakumbushwa kwamba, wanaweza kushiriki kwa kufuatilia kwa njia ya mtandao. Wanaweza kufanya hivyo kwa kujisajili  bure kabisa katika tovuti ya m.guinnessvip.com.  


  Pia GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE ina kurasa ya Facebook ambayo ni www.facebook.com/guinnesskenya, Ili kufuatilia kwa karibu yanayojiri, unatakiwa kufuatilia  ukurasa huu ‘like’ na utakuwa unapata habari zote zinazohusu mchezo huu.


  GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha mchezo wa soka kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya Endemol.  Usikose kuangalia na kufuatialia kipindi hiki katika runinga yako kupitia televisheni za ITV na Clouds TV kila siku ya Jumatano usiku.


  Usisahau kuwa na chupa ya bia uipendayo ya  Guiness wakati unaangalia kipindi hiki. 


  *Haiuzwi kwa walio na Umri chini ya miaka kumi na nane.  Tafadhali Kunywa kistarabu.


  0 0


  The President of Comoros, Dr. Ikililou Dhoinine, cuts a ribbon to inaugurate Exim Bank’s third branch in the Union of Comoros at the weekend. Looking on at the left is the Exim Bank Tanzania Board Chairman Yogesh Manek. 

  The President of Comoros, Dr. Ikililou Dhoinine (left) signs a visitors book during a function to inaugurate Exim Bank’s third branch in the in the Union of Comoros at the weekend.Looking on is the Exim Bank Tanzania Managing Director Anthony Grant (second right) and the Exim Bank Tanzania Board Chairman Yogesh Manek (second left). 
    
  ========  ========  ========
  Exim Bank opens third branch in Comoros


  By Correspondent, Moheli, Comoros
  EXIM Bank Comoros, an affiliate of Exim Bank Tanzania has continued to strengthen its position as the fastest growing bank in the Union of Comoros with the opening of the bank’s third branch on the Island of
  Moheli in a ceremony presided over by the President of Comoros,  Dr. Ikililou Dhoinine, and by the Chairman of the Exim Bank  Tanzania Board Chairman , Mr. Yogesh Manek.
  The new Exim Bank branch apart from offering tailor-made banking services will facilitate remittances and payments through MoneyGram, and will enable acceptance of Visa and MasterCard on the island through the Exim Bank ATM services. Speaking during the inauguration of the new branch at the weekend, Chairman Manek said the branch will contribute to the development of an effective, efficient and sustainable financial sector in the Union of Comoros, in line with the bank’s mission of taking affordable banking services closer to the people.


  “About five years ago, I officiated at the opening of Exim Bank’s first branch in Comoros [on Moroni Island]. I am happy take part in the inauguration of our third branch in Comoros today [on Moheli Island].” Chairman Manek said that Exim Bank had become Tanzania’s fifth largest bank with a branch network stretching across Tanzania. 

  In Comoros and in Tanzania, Mr. Manek noted, “Exim Bank will always work towards striking a balance between bank profitability and the provision of unmatched banking service to all sectors of the community. ”  In Comoros, the bank had already acquired over 25,000 customers and operated Exim Bank on Wheels allowing those living in remote areas to have access to real time banking operations.
  During the occasion, the President of Comoros Dr. Ikililou Dhoinine thanked the bank, and expressed his determination to support the country's continuous development process.


  “I believe Exim Bank will be one of the players in supporting this development process. East Africa has a lot of unexploited investment potentials. That is why all eyes of the world are turning to Eastern Africa,” he added. For his part, the Governor, Central Bank of Comoros Mohamed Ali said the opening of Exim Bank’s new branch is a major boost to the country’s banking system. Exim Bank Tanzania Managing Director Anthony Grant said “the bank has a positive outlook on the economic developments in all countries where
  the bank operates,”

  0 0


  Katibu wa NEC-CCM Itikadi, Siasa na Uenezi, Nape Nnauye akiweka shada la maua kwa miaba ya chama hicho, wakati yeye na viongozi wengine walishiriki kwenye mazishi ya msiba wa marehemu Galus Matanji yaliyofanyika katika makaburi ya Kanisa la Katoliki Kalengakelo la Mtakatifu Petro, Kata ya Mtimbila, wilayani Ulanga, Morogoro jana. Nape ambaye alikuwa kwenye ziara ya kikazi ya kuimarisha uhai wa chama hicho, aliamua kusitisha baadhi ya shughuli na kuamua kushiriki misiba miwili iliyotokea eneo hilo ukiwemo wa Mwanaiba Seif. (PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG).

   Nape akimkabidhi ubani baba mzazi wa marehemu Mwanaiba Seif, Abdul Seif
  Katibu wa NEC-CCM Itikadi, Siasa na Uenezi, Nape Nnauye, akishiriki katika maziko ya Mwanaiba Seif yaliyofanyika eneo la Kalengakelo, Mtibila wilayani Ulanga, Nape ambaye alikuwa kwenye ziara ya kikazi ya kuimarisha uhai wa chama hicho, aliamua kusitisha baadhi ya shughuli na kuamua kushiriki misiba miwili iliyotokea eneo hilo ukiwemo wa marehemu Galus Matanji.
   Mbunge wa Ulanga Magharibi, Dk. Hadji Mponda (katikati)akitoa salamu za rambirambi katika maziko ya marehemu Matanji.


   Pape akishiriki katika maziko ya marehemu Matanje

                                      Nape akimkabidhi ubani mmoja wa wanafamilia ya marehemu Matanji.
   Marehemu Mwanaiba akizikwa
   Katibu wa NEC-CCM Itikadi, Siasa na Uenezi, Nape Nnauye, na Mbunge wa Jimbo la Ulanga Magharibi, Dk. Hadji Mponda (CCM), wakiwa katika ibada ya kuuombea mwili wa marehemu Matanji katika Knisa la Mtakatifu Petro.
  Nape katikati akiwaongoza baadhi ya viongozi kwenda kushiriki ibada ya kuuombe mwili wa marehemu Matanji katika Kanisa la Katoliki  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Bunengi ya Afrika Kusini Bi. Savannah Maziya akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya NDC (National Development Coorporation) ambaye pia Mbunge Mstaafu wa Jimbo la KwelaNdugu Chrissant Mzindakaya walipoonana na uongozi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa katika kujadili namna Kampuni hiyo kwa kushirikiana na NDC katika uratibu watakavyosaidia katika kuwekeza kwenye miundombinu ya bandari, reli na barabara kuunganisha Mkoa wa Rukwa Mikoa pamoja na Nchi jirani kuwezesha rasilimali zilizopo Mkoani Rukwa zinapata masoko yakiwemo mazao, madini na utalii. Utalii huo ni pamoja na Kalambo Falls maporomoko ya maji makubwa barani Afika na Bismark Fort iliyokuwa ngome ya wajerumani iliyopo hapa Mkoani Rukwa. 
   Muwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Ndugu Moshi Chang'a akiongoza kikao hicho kilichohudhuriwa na muwekezaji huyo, wawakilishi wa NDC, Wakuu wa Idara katika Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa na Halmashauri za Wilaya ya Kalmbo na Sumbawanga. 
   Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Ndugu Iddi Hassan Kimanta akiwa anazungumza katika kikao hicho. 
   Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Ndugu Samson Mashalla akiwa anatoa mchango wake juu ya fursa za uwekezaji zinazopatikana Mkoani Rukwa kwa muwekezaji huyo. 
  Afisa katika dawati la Uwekezaji Ndugu Misasi Marco akimwaga sera kutoka katika dawati lake uwekezaji. (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa - @rukwareview.blogspot.com)

  0 0

   
  Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) leo imeanza mkutano wake wa 27 wa mwaka kwa watafiti Wanasayansi jijini Arusha ambapo Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohamed Shein anataraji kuufungua rasmi jioni ya leo.

  Pamopoja na Mkutano huo wa NIMR, pia mkutano wa pili wa Wanasansi kuhusiana na Masuala ya Afya barani Afrika unafanyika sambamba na mkutano huo ambapo watafiti mbalimbali duniani wanatoa mada juu ya tafiti mbalimbali za magonjwa ya binadamu.

  Mkutano huo ambao umebeba kauli Mbiu ya Mabadiliko ya Mazingira katika Utafiti wa Afya 'Changing landscape in Health Research' utafanyika kwa siku nne katika Hotel ya Snow Crest jijini Arusha.

  Pichani ni Dk. Jeff Waage kutoka Uingereza akiwasilisha mada juu ya Kilimo na Afya katika Mabadiliko ya Mazigira katika Utafiti wa Afya.

  Baadhi ya washiriki mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa mkutano huo jijini Arusha hii leo. Baadhi ya Wabunge nao wamealikwa kushiriki katika mkutano huo.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua rasmi Mkutano wa kimataiafa wa siku mbili wa Udhibiti wa Huduma za Kiuchumi Bara la Afrika, ulioshirikisha mataifa mbalimbali kutoka Bara la Afrika, ulioanza leo Aprili 16, 2013 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC jijini Arusha.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizindua Kitabu cha Udhibiti wa Huduma za Kiuchumi Bara la Afrika, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa siku mbili wa Udhibiti wa Huduma za Kiuchumi Bara la Afrika, ulioshirikisha mataifa mbalimbali kutoka Bara la Afrika, ulioanza leo Aprili 16, 2013 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC jijini Arusha. Kitabu hicho kimetungwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) Prof. Mark Mwandosya. Kulia ni Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) ni Mkurugenzi wa Ewura, Haruna Masebu.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyesha Kitabu cha Udhibiti wa Huduma za Kiuchumi Bara la Afrika, baada ya kukizindua wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa siku mbili wa Udhibiti wa Huduma za Kiuchumi Bara la Afrika, ulioshirikisha mataifa mbalimbali kutoka Bara la Afrika, ulioanza leo Aprili 16, 2013 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC jijini Arusha. Kitabu hicho kimetungwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) Prof. Mark Mwandosya (kulia). Katikati ni Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyesha zawadi baada ya kufungua wa Kimataifa wa siku mbili wa Udhibiti wa Huduma za Kiuchumi Bara la Afrika, kutoka kwa Mkurugenzi wa Ewura, Haruna Masebu. Mkutano huo ulioshirikisha mataifa mbalimbali ya Bara la Afrika, umeanza leo Aprili 16, 2013 katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC jijini Arusha.
  Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakiwa ukumbini wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal wakati akiwahutubia.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano huo baada ya ufunguzi.Picha na OMR.

  0 0

  Meneja Biashara wa Nokia Nchini Tanzania Samson Majwala, Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde na menjeja masoko wa Airtel Edwin Byampanju kwa pamoja wakionyesha simu za rangi tofauti za Nokia Lumia 620 wakati wa wakati wa uzinduzi wa Nokia Lumia 620 kwa ushirikiano kati ya Airtel na Nokia utakaowawezesha wateja wa Airtel na watanzania kupata simu ya Nokia Lumia 620 yenye technologia ya kisasa na offa kabambe ya Muda wa Maongezi wa dakika 275, sms bila kikomo na internet ya 3GB kwa muda wa mienzi mitatu.
  Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde akiongea wakati wa uzinduzi wa simu Nokia Lumia 620 , ushirikiano kati ya Airtel na Nokia utakaowawezesha wateja wa Airtel na watanzania kupata simu ya Nokia Lumia 620 yenye technologia ya kisasa na offa kabambe ya Muda wa Maongezi wa dakika 275, sms bila kikomo na internet ya 3GB kwa muda wa mienzi mitatu.
  Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde akiongea wakati wa uzinduzi wa simu Nokia Lumia 620 , ushirikiano kati ya Airtel na Nokia utakaowawezesha wateja wa Airtel na watanzania kupata simu ya Nokia Lumia 620 yenye technologia ya kisasa na offa kabambe ya Muda wa Maongezi wa dakika 275, sms bila kikomo na internet ya 3GB kwa muda wa mienzi mitatu.
  Meneja Biashara wa Nokia Nchini Tanzania Samson Majwala, Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde na menjeja masoko wa Airtel Edwin Byampanju kwa pamoja wakionyesha kipeperushi cha Nokia Lumia 620 wakati wa wakati wa uzinduzi wa Nokia Lumia 620 kwa ushirikiano kati ya Airtel na Nokia utakaowawezesha wateja wa Airtel na watanzania kupata simu ya Nokia Lumia 620 yenye technologia ya kisasa na offa kabambe ya Muda wa Maongezi wa dakika 275, sms bila kikomo na internet ya 3GB kwa muda wa mienzi mitatu.
  Meneja Biashara wa Nokia Nchini Tanzania Samson Majwala( kushoto) akimkabidhi simu ya Nokia Lumia 620 Batuli Chombo mwandishi wa habari wa Sikuba kwenye bahati nasibu wakati wa uzinduzi wa Simu hiyo kwa ushirikiano kati ya Airtel na Nokia utakaowawezesha wateja wa Airtel na watanzania kupata simu ya Nokia Lumia 620 yenye technologia ya kisasa na offa kabambe ya Muda wa Maongezi wa dakika 275, sms bila kikomo na internet ya 3GB kwa muda wa mienzi mitatu. Wakishuhudia ni Afisa Uhusiano Jane Matinde akifatana na menjeja masoko wa Airtel Edwin Byampanju.

  0 0  Na Ripota wetu, Dar es Salaam

  BENDI ya Twanga Pepeta ya Jijini Dar es Salaam,inatarajia kutumbuiza katika ukumbi wa Wood Land Yombo Vituka .

  Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya J&kk Entertainment Jane Mkumbwa, alisema shoo hiyo itakua kamambe huku akiwataka wapenzi wa mziki huo kujitokeza kwa wingi ili kujionea shoo hiyo.

  Jane alisema kuwa shoo hiyo itapigwa siku ya April 19 na siku kuu ya Muungano Aprili 26 itakua katika viwanja vya Kibaha Picha ya Ndege katika ukumbi wa Tripple J na huku akiwataka wananchi wa kibaha kujitokeza kwa wingi sambamba na kusherekea sikukuu hiyo.

  Aliendelea kueleza kua siku ya Mei 10 mwaka huu atakuwa na bendi hiyo katika viwanja vya Bunge yaani katika jiji la Dodoma,ukumbi wa Loyal Village ambapo wabunge pamoja na wapenzi wengine wakiwemo wanavyuo wanatakiwa kujitokeza kwa wingi.

  "Nimeamua mei 10 kuwapelekea  wabunge burudani hivyo wanatakiwa kujitokeza kwa wingi sambamba na wanafunzi wa vyuo vikuu kwa kua itakua ni siku ya mapunziko ndio itakuwa sehemu sahihi ya kupumzisha vichwa vyao huo,"alisema Jane.
   
   Hata hivyo alisema kwa kushirikiana na bendi hiyo ataendelea kuwapa raha watanzania katika sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam, na hata mikoani.

  0 0

   Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba (Kulia) akiwa katika picha ya pamoja katika dua maalum ya kuwaombea wanachama wa Mtandao wa SHIWATA, iliyofanyika hivi karibuni kwenye ukumbi wa Starlight, Makamba alikuwa mgeni rasmi katika dua hiyo akiongozana na Mkurugenzi wa Utamaduni, Profesa Hermas Mwansoko na Ofisa Utamaduni Wilaya ya Ilala, Shani Kitogo.
  Mh Januari Makamba (Kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Mtandao wa Shiwata, Taalib Cassim kabla ya dua ya kuwaombea dua waliokuwa wanachama wa mtandao huo

  0 0
  WASHIRIKI wa Jukwaa la wazi la Semina za Jinsia na maendeleo (GDSS) linaloratibiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) wamejitokea na kulalamikia mchakato mzima wa upatikanaji wajumbe wa mabaraza ya Katiba uliofanyika maeneo mbalimbali hivi karibuni. Wawakilishi hao ambao baadhi yao walishiriki kugombea nafasi mbalimbali za uwakilishi, wametoa malalamiko hayo leo jijini Dar es Salaam walipokuwa wakizungumza na vyombo anuai vya habari.

  Akizungumza katika mkutano huo na wanahabari, Katibu wa jukwaa hilo, Badi Darusi kutoka TOWSF, alisema kulikuwa na dosari nyingi katika uchaguzi wa wajumbe wa mabaraza ya katiba ya wilaya uliofanyika hivi karibuni, hivyo kuitaka Tume ya Mabadiliko ya Katiba ifanye tathmini ya zoezi zima na kuangalia namna ya kuondoa kasoro hizo.

  Alisema kwa baadhi ya maeneo baadhi ya wasimamizi wa mchakato huo ngazi za mitaa waliingiza itikadi za vyama, dini na pia kuwepo kwa mazingira ya rushwa hivyo kushauri kuna kila sababu ya mchakato huo kwa mkoa wa Dar es Salaam urudiwe upya ili haki itendeke.

  Alisema vyama vya siasa vilikuwa vinatumia fursa ya kufanya kampeni chafu kinyume na utaratibu na muongozo uliowekwa na Tume ya Taifa ya mabadiliko ya Katiba, na kuongeza kuwa katika baadhi ya mitaa waliongeza sifa ya kuwa mwanachama wa chama fulani ili uchaguliwe kuwa mjumbe wa baraza la katiba jambo ambalo ni kinyume na maelekezo yaliyotolewa na tume.

  “Tumeshtushwa sana na namna mchakato huu ulivyogubikwa na kasoro mbalimbali ambazo zisipochukuliwa hatua madhubuti tunaweza tukawa na katiba ambayo haitokani na wananchi. Mchakato huu uligubikwa na vitendo vya udini, siasa, rushwa, vitisho na ubaguzi wa kijinsia. Hali hii ilipelekea baadhi ya watu waliokuwa na sifa za kuwa wajumbe wa mabaraza ya Katiba kuenguliwa kimakosa kutokana na utashi na maslahi binafsi ya watu wachache,” alisema Darusi.

  Aidha alitolea mfano katika mitaa ya Msakuzi, Kata ya Mbezi na Mtaa wa Mbagala Rangitatu kata ya Charambe wagombea wa ujumbe wa mabaraza ya katiba ambao hawajulikani misimamo yao katika siasa waliulizwa wazi wazi kuwa wao ni wafuasi wa chama gani na baadhi ya viongozi wa mitaa ambao ndio walikuwa wasimamizi wakuu wa mchakato huo.

  “Mfano hai ni kata ya Mabibo yenye wakazi 72,000 (sensa ya 2002) imeshindwa kupata wajumbe wa mabaraza ya katiba kwa sababu ya wajumbe 7 wa baraza la maendeleo la kata (WDC) kushindwa kuafikiana eti kila mmoja akitaka mtu wa chama chake ndio awe mjumbe wa baraza la katiba la wilaya ya kinondoni kinyume na maelekezo na muongozo wa kuwapata wajumbe hao uliotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Hali hii inawafanya wakazi wa kata ya mabibo kukosa uwakilishi katika baraza la katiba la wilaya,” alisema kiongozi huyo.


  Aliongeza kuwa mchakato huo pia uligubikwa na vitendo vya ubaguzi na unyanyasaji wa jinsia uliofanya na baadhi ya viongozi wa mitaa na vyama vya siasa, kwenye baadhi ya mitaa wasichana waliokuwa na umri wa miaka 18 hadi 35 walienguliwa katika kundi la vijana na kuwekwa katika kundi la Wanawake watu wazima kinyume na utashi wa mtu binafsi aliyegombea. Mfano ni mtaa wa Mbagala Rangi Tatu kata ya Charambe.

  Hata hivyo waliiomba Serikali na Tume ya Mabadiliko ya Katiba zichukue hatua madhubuti za kukabiliana na vitendo vya udini vinavyoshika hatamu kwa mgongo wa mchakato wa katiba mpya ili kuhakikisha katiba haiundwi kwa itikadi za mazingira hayo. Alisema endapo mchakato huo utarudiwa walipendekeza Kamati ya Maendeleo ya Kata isiwe na dhamana ya kuwachagulia wananchi wajumbe wa mabaraza ya katiba kwani wengi wanaongozwa na utashi wa kisiasa na wananchi pekee ndio wawe na dhamana ya kuwachagua wawakilishi wao.

  ”Tume ya Mabadiliko ya Katiba iangalie namna mpya ya kuyashirikisha makundi ya watu walio pembezoni kwenye mabaraza ya katiba ili kuwa na uwakilishi katika kujadili rasimu ya katiba. Mfano muongozo uliotolewa na tume hauja ainisha ni namna gani watu wenye ulemavu watashikiriki katika kuingia kwenye mabaraza ya katiba ya wilaya,”.

  Mchakato wa katiba mpya usiendeshwe kwa haraka kwani unawafanya wananchi walio wengi wasiwe na taarifa sahihi kuhusu kinachoendelea katika  mchakato huu wa uundaji wa katiba mpya. Tume ya katiba iangalie mfumo wa kuwafikishia wananchi taarifa kuhusu mwenendo wa mchakato wa katiba mpya nchini kwani taarifa nyingi hazifiki kwa wananchi walio wengi na kwa wakati.

  0 0


   Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Bw. Benno Ndulu akitoa maelekezo kwa wajumbe kutoka Tanzania waliohudhuria mkutano wa Kipupwe. Gavana alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho kwa niaba ya Waziri wa Fedha.
    Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Harry Kitilya akitoa ufafanuzi katika  kikao cha pamoja cha wajumbe kutoka Tanzania kilichofanyika katika ubalozi wa Tanzania mjini Washington DC.
    Kutoka kushoto Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Fedha Bi. Ingiahedi Mduma, Msaidizi wa Gavana Bw. Msafiri Nampesya pamoja na Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Bw. Suleiman Saleh wakisikiliza jambo kwa makini kutoka kwa Afisa Mwambata anayeratibu masuala ya Uchumi, Biashara, na Uwezeshaji ya Benki ya Dunia na IMF Bw. Paul Mwafongo.

   Baadhi ya Wajumbe kutoka Wizara ya Fedha wakifurahia jambo kabla ya kuanza kwa kikao.Kutoka kulia ni Kamishna wa Bajeti Bi. Monica Mwamunyange, Mhasibu Mkuu wa Serikali Bi. Mwanaidi Mtanda pamoja na Kamishna wa Sera Bw. Beda Shallanda.
  Wajumbe wakisikiliza kwa makini hoja zilizotolewa na Gavana wa Benki Kuu hayumo pichani, Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Utafiti na Sera za Uchumi wa BOT Dr. Joseph Masawe, Kamishna wa Fedha za Nje Wizara ya Fedha Zanzibar Bi. Bihindi Nassor  pamoja na Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Dr. Philip Mpango. 
   Kutoka kushoto Mkuu wa Kitengo cha Sheria Bi Susan Mkapa pamoja na Kamishna wa Fedha za Nje Bw. Said Magonya wa Wizara ya Fedha wakisikiliza kwa makini katika kikao hicho pembeni ni Mchumi mwandamizi wa Wizara ya Fedha Bw. Patric Pima. 


  Mikutano ya kipupwe imeanza rasmi mjini Washington DC kuanzia tarehe 15/4/2013 na kuhudhuriwa na nchi wanachama zaidi ya 188. Kila kunapokuwa na mikutano ya kipupwe maelfu ya wafanyakazi wa Serikali, waandishi wa habari, mashirika yasiyo ya kiserikali, washiriki waalikwa kutoka sekta za elimu na binafsi, wanakutana mjini Washington DC kwa mikutano hii ya kipupwe ya Benki ya Dunia na Shrika la Fedha la kimataifa pamoja na kamati za kifedha, ambazo zinajadili maendeleo ya kazi za Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa. Picha zote na Bi.Ingiahedi Mduma na Bi.Eva Valerian-Wasington DC.

  0 0


  She has seen the world. She has hosted shows across the globe. She has walked on red carpets all over the world while interviewing and interacting with some of the globally recognized and loved celebrities. Simply put it this way; she lives her dream.

  Her name is Vanessa Mdee, a 24 year old who is also known as Vee among her friends and fans. In 2007, when she was just 19 years old, Vee made history by becoming the first ever MTV VJ from Tanzania. Today, she is one of the most recognized VJs in Africa and even beyond the African borders.

  As if being a VJ is not enough, Vee is also a DJ/ Host of “The Hit List” show at Choice FM broadcasting from Mikocheni in Dar-es-salaam.  That’s not all; Vee is a HIV/AIDS Activist, Model, Motivational Speaker and MC. Recently, she added the title Singer/ Musician to her long and ever growing resume.
   
  Vanessa, a graduate of The Catholic University Of Eastern Africa where she studied Law, is passionate about everything she does. You can feel the energy in her veins through the discipline and ethics she places into all that she does.  She is a humanitarian who deeply believes in Africa as the future.

  I recently had a chance to interview her. Here are the excerpts;

  BC: Hi Vanessa, I can’t even put it well how happy I am to have this opportunity to interview you. Welcome to BC. How are you doing?
   VEE: I'm sound so well Thank YOU - how you feeling? Thanks so much for taking the time.

  BC: When I was researching for this interview, at certain point I think I got shocked. At this young age, it seems like you have achieved and have been involved in a lot. I, therefore, guess my first question should be how do you manage to do that you are doing and involved with? You must have excellent time and organizational management skills! Tell me about it…

  VEE: Thanks, it’s funny when it's all put down on paper it feels like a whole lot but I’m just getting started. I really do have my parents to thank for the discipline. Our household was one of rules and curfews, pleases and thank You’s. Until the age of 18 it was mandatory for my siblings and I to be in bed by 11pm - not one minute later. I hated it then but I get it now. Structure is vital.

  BC: You were  (and I suppose still is) Tanzania’s first ever MTV VJ. I believe that was a dream that came true since you always wanted to be on TV…can you remind our readers how did that come about? How was the process?
  TO READ MORE CLICK HERE.

older | 1 | .... | 63 | 64 | (Page 65) | 66 | 67 | .... | 1896 | newer