Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46367 articles
Browse latest View live

RAIS KIKWETE ATOA POLE WA FALME ZA SAUDI ARABIA

$
0
0
King of Saudi Arabia,  H.H. Salmanbin Abdulaziz Al Saud  
PRESS RELEASE 
H.E. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a sympathy and condolences massageto H.R. H. Salman bin Abdulaziz Al Saud, King of the Kingdom Saudi Arabia on great sadness the death of 107 pilgrims and more than 200 others injured due to collapse of construction crane at the Holy Mosque in Makka, Saudi Arabia on 11th September 2015.
The massage reads as follows:
“His Royal Highness Salman bin Abdulaziz Al Saud,
King of Saudi Arabia and Custodian of the Two Holy Mosques,
RIYADH,
SAUDI ARABIA
Your Royal Highness,
We have learned with great sadness the death of 107 pilgrims and more than 200 others injured due to collapse of construction crane at the Holy Mosque in Makka, Saudi Arabia on 11th September 2015.
On behalf of the Government and the people of the United Republic of Tanzania, I wish to convey to you and through you to the people of the Royal Kingdom of Saudi Arabia and all the bereaved pilgrims’ families, our heartfelt condolences and sympathies.
During this time of grief, our hearts and prayers are with the family of the pilgrims and all other people who have been inflicted by this tragic incident.
May Almighty Allah grant quick recovery to all wounded people.
Please accept, Your Royal Highness and dear colleague, the assurance of my highest consideration.
Issued by: The Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation, Dar es Salaam
13th September, 2015

MGOMBEA UBUNGE WA CCM JIMBO LA MAFINGA AAHIDI KUTATUA KERO YA MAJI

$
0
0
wananchi wa Mafinga mjini wakimpokea mwenyekiti wa chama cha CCM mkoa wa Iringa jana mjini mafinga
           MATUKIO KATIKA PICHA (picha: Baraka Nyagenda)
wananchi  wa jimbo la Mafinga  wakifurahia mkutano
mjumbe wa  NEC Marcelina Mkini akimnadi mgombea  ubunge Bw Chumi
Waliokuwa wanacham wa CHADEMA wakikabidhiwa kadi za chama cha mapinduzi CCM na mwenyekiti wa chama hicho mkoa baada ya kujiunga na cha cha CCM jana mjini Mafinga.

 
MGOMBEA ubunge jimbo la Mafinga Mjini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Cosato Chumi juzi amezindua kampeni zake za kuwania kiti hicho akiwataka watanzania kumpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kumtosa aliyekuwa rafiki yake wa jirani, Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa.
Baada ya kutoswa na CCM, Lowassa alikimbilia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na akateuliwa kuwa mgombea wake urais ambaye pia anawakilisha vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) katika kinyang’anyiro hicho.
Akimpigia debe mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli, Katibu wa CCM wa wilaya ya Mufindi, Jimson Mhagama amemfananisha mgombea huyo wa Ukawa na nyuki wa mashineni ambao kwa kawaida huwa hawana uwezo wa kung’ata.
Chumi aliyesindikizwa na wagombea wa Jimbo la Mufindi Kaskazini, Mahamudu Mgimwa na Mufindi Kusini, Mendrad Kigola katika uzinduzi huo, alisema kama Rais Kikwete angekuwa hamfahamu vizuri Lowassa huenda angemuunga mkono katika mchakato wa kumpata mgombea urais ndani ya CCM.
“Rais Kikwete aliamua kumtosa Lowassa kwasababu hakutaka kutuachia mtu mwenye matatizo na mpiga “deal”, kwahiyo kufahamiana naye kumekuwa na faida kubwa kwa watanzania,” Chumi alisema.
Akiomba kura kwa mamia ya wananchi waliofurika katika uzinduzi huo uliofanyika katika uwanja wa Mashuja mjini Mafinga, Chumi aliyeshika tochi kubwa muda wake wote aliokuwa akiongea, alisema anataka kuwa mbunge wa jimbo hilo ili akawamulike na kuwafichua wazembe wanaochelewesha au kuhujumu kwa makusudi huduma katika sekta mbalimbali jimboni humo.
Akitaja vipaumbele vyake endapo wananchi wa jimbo hilo watampa ridhaa ya kuwa mbunge wao, alisema atahakikisha katika kipindi cha miaka mitano ijayo jimbo hilo linakuwa na huduma bora ya maji, afya, miundombinu na elimu.
Alizitaja sekta zingine atakazozitupia jicho kuwa ni pamoja na ya biashara na ulinzi na usalama kwa kuhamasisha ujenzi wa vituo vidogo vya Polisi katika maeneo yenye mikusanyiko mikubwa ya watu.
Kwa upande wake, Mgimwa ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii alisema; “Majimbo yote wilaya ya Mufindi yamepiga hatua kubwa ya maendeleo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.”
“Tulikuwa hatuna lami mjini, leo tuna barabara zenye lami na tumeanza ujenzi wa barabara ya Mgololo kwa kiwango cha lami. Tumejenga kilomita tatu na tumepata fedha kwa ajili ya kujenga kilometa nane mwaka huu wa fedha,” alisema.
Katika sekta ya afya na fedha, alisema wodi ya kisasa ya wazazi imejengwa katika hospitali ya wilaya ya Mufindi ili kuboresha huduma kwa wajawazito huku huduma za benki zkiongezeka kutoka benki moja hadi tatu, ambazo ni Mucoba, NMB na Crdb.
Wengine waliohudhuria kampeni hizo ni pamoja na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu aliyezungumzia Ilani ya Uchaguzi ya CCM na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Mahamudu Madenge aliyeponda kipaumbele cha Lowassa, cha elimu, kwamba kinamsuta jimboni kwake Monduli.


MAANDALIZI YA TAMASHA LA KULIOMBEA TAIFA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU YA KAMILIKA LITAFANYIKA UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM, OKTOBA 4, 2015

$
0
0

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Msama Promotion ambayo inaandaa matamasha mbalimbali kama lile la Pasaka  na Chrismas , ambaye ni Mwenyekiti wa Tamasha hilo, Alex Msama, akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya Tamasha la kuliombea Taifa Amani kuelekea uchaguzi mkuu ambalo litafanyika Oktoba 4, 2015 Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na baadaye mikoa mingine 12.
 Hapa mkutano na wanahabari ukiendelea.
Wanahabari wakisubiri kuchukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

Mwimbaji wa kimataifa wa nyimbo za injili kutoka nchini Afrika Kusini, Solly Mahlangu, amethibitisha 
kutumbuiza katika tamasha la kuombe amani  linalotarajiwa kufanyika Oktoba 4 katika uwanja wa Taifa 
jiji Dar es Salaam.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Msama Promotion ambayo inayoandaa matamasha mbalimbali kama lile la Pasaka  na Chrismas , ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tamasha hilo kutoka kampuni hiyo, Alex Msama wakati akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu kukamilika kwa  maandalizi ya tamasha hilo sambamba na kutaja majina ya waimbaji wa nyimbo za injili wa ndani na nje ya nchi, wanaotarajiwa kutumbuiza katika tamasha hilo linalolenga kuombea nchi amani  hususani uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba 25 mwaka huu.



''Maandalizi ya tamasha hilo yamekamilika na baadhi ya waimbaji wa nyimbo za injili tayari wamethibitisha kushiriki ambao ni  Solly Mahlangu, Kundi la Kelechi kutoka  nchini Uingereza nalo  pia limethibitisha kuja kutumbuiza katika tamasha hilo.''. alisema Msama. 

Msama amewataja Waimbaji wengine kutoka nje ya nchi ambao  wamekwisha kuthibitisha kuja kutoa burudani katika tamasha hilo  ni Sarah Kei na Solomoni Mukubwa kutoka nchini Kenya.

''Waimbaji wa ndani waliokwisha kuthibitisha kutumbuiza katika tamasha hilo la kuombea amani ni pamoja na Boniface Mwaitege,Rose Mhando,Upendo Nkone,Upendo Kilahiro, John Lissu,Christopher Mwangila,kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama na kwaya moja kutoka mkoani Iringa'', alisema  Msama.

Kwa mujibu wa Msama, tamasha hilo linalotarajiwa kuzunguka katika mikoa kumi na mbili ya Tanzania 
Bara, limelenga kuhubiri na kuiombea nchi amani,Upendo na mshikamano wakati na baada ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika kote nchini Oktoba 25 mwaka huu na kuiiniza madarakani serikali ya awamu ya tano. 


(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

MGOMBEA MWENZA WA UKAWA JUMA DUNI HAJI AHUTUBIA MKUTANO WA KAMPENI MKOANI RUVUMA

$
0
0
 Mgombea Mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Duni Haji akisalimiana na mgombea udiwani wa Ukawa kata ya Tingi wilaya ya Nyasa, Bosco Mapunda alipowasili katika kijiji cha Tingi mkoani Ruvuma kwa ajili ya mkutano wa kampeni kijijini hapo. (Picha na Francis Dande)
 Mgombea Mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Duni Haji akisalimiana na baadhi ya madiwani wa Ukawa wa Kata ya Tingi alipowasili katika kijiji cha Tingi mkoani Ruvuma kwa ajili ya mkutano wa kampeni uliofanyika jimbo la Nyasa.
 Mgombea Mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Duni Haji akisalimiana na mgombea ubunge kupitia viti maalum, Anna Diwu.
 Wananchi wa kijijicha Tingi mkoani Ruvuma wakifuatilia mkutano wa kampeni.
 Mgombea Mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Duni Haji akiwa amembeba motto Tedy wa kijiji cha  Tingi mkoani Ruvuma wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kijiji hapo.
  Mgombea Mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Duni Haji akisalimia na wananchi wa kijiji cha Tingi katika jimbo la Nyasa wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika mkoani Ruvuma. 
  Mgombea Mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Duni Haji akisalimia na wananchi wa kijiji cha Tingi katika jimbo la Nyasa wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika mkoani Ruvuma. 
  Mgombea Mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Duni Haji akisalimia na wananchi wa kijiji cha Tingi katika jimbo la Nyasa wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika mkoani Ruvuma. 
 Mgombea Mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Duni Haji akiwatambulisha madiwani wa Ukawa wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika kijiji cha Tingi jimbo la Nyasa mkoani Ruvuma.
  Mgombea Mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Duni Haji akisalimia na wananchi wa kijiji cha Tingi katika jimbo la Nyasa wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika mkoani Ruvuma. 
Mgombea Mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Duni Haji akiwa amembeba motto Tedy wa kijiji cha  Tingi mkoani Ruvuma wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kijiji hapo.

SERIKALI YA AWAMU YA TANO ITAKUWA NI YA VIWANDA-MAGUFULI

$
0
0
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM,Dkt Magufuli akiwasalimia maelfu ya Wananchi waliofika katika uwanja wa Barafu mjini Igunga,Dkt Magufuli aliwahutubia wananchi hao.
 Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Magufuli akisisitiza mbele ya maelfu ya Wakazi wa mji wa Igunga jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara kuwa Serikali ya awamu ya tano itajenga viwanda mbalimbali vikiwamo viwanda vya nguo ikiwa ni mkakati wa kuinua zao la pamba ambalo linalimwa kwa wingi mikoa ya kanda ziwa,amesema kuwa Serikali yake imedhamiria kuleta mabadiliko bora na si bora mabadiliko na kuongeza kazi kubwa atakayofanya ni kusimamia vema rasilimali za nchi kwa maslahi ya Watanzania wote.
 Dkt Magufuli kwa nyakati tofauti kwenye mikutano ya hadhara akiwa katika wilaya ya Maswa na kisha jimbo la Kishapu na Igunga, Dk.Magufuli amesema kuwa anatambua umuhimu wa kuwa na viwanda nchini na hivyo serikali yake itasimamia ujenzi wa viwanda kwa lengo la kuimarisha uchumi na wakati huo huo kusaidia wakulima na wafugaji kunufaika na shughuli wanaofanya nchini.  
  Dk Magufuli akizungumza na wananchi wakati akijinadi  mjini Malampaka, Maswa, ambapo alisema akishinda urais ataanzisha viwanda vingi ili kuongeza thamani ya mazao nchini.
 Dk Magufuli akihutubia wananchi katika Mji wa Maganzo mkoani Shinyanga, ambapo aliomba kumpigia kura ali ashinde awasaidie kuboresha sekta ya uchimbaji madini kwa serikali kuwakopesha wachimbaji wadogo wadogo  kwa kuwapatia mitaji  na vifaa.
 Wakazi wa Maganzo wakiwa wamefunga barabara wakitaka kumsikiliza Mgombea Urais wa CCM,Dkt John pombe Magufuli alipokuwa akipita kuelekea Igunga mkoani Tabora kwenye mkutano wa hadhara
 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli (katikati) akishangiliwa na wananchi wenye ujumbe wa kumuunga mkono  huku akiwa na mfano wa msumeno wa kuwakatia wezi na mafisadi  akishinda urais wakati wa mkutano wa kampeni  mjini Igunga , Tabora jioni ya leo.
 Wananchi wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali wakati wa mkutano wa kampeni za CCM mjini Maswa.



 Wakazi wa Kishapu wakishangilia jambo mara baada ya Mgombea Urais wa CCM kuwahutubia wananchi hao mapema leo mchaa.
  Wananchi wa Kishapu wakimsikiliza kwa makini wakati Dk Magufuli alipokuwa akijinadi na kuelezea jinsi serikali ya CCM itakavyoboresha sekta mbalimbali nchini
 Sehemu ya umati wa wananchi katika mkutano wa kampeni za CCM wilayani Igunga leo
Msafara wa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli ukiwasili kwenye uwanja wa Barafu mjini Igunga jioni ya leo,kuhutubia kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni mkoani Tabora. 
 Mgombea wa Urais wa CCM Dkt Magufuli akiondoka kwenye uwanja wa Barafu mjini Igunga jioni ya leo mara baada ya kuwahutubia wananchi hao. 

LAFARGE TANZANIA YAKABIDHI MRADI WA MAJI KWA KIJIJI CHA SONGWE VIWANDANI, MBEYA

$
0
0
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Lafarge Tanzania (Mbeya Cement), Catherine Langreney na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Nyirembe Sabi wakikata utepe kuzindua mradi wa maji uliojengwa na kampuni hiyo kwa ajili ya kuwaondelea tatizo la uhaba wa maji safi na salama wananchi wa kijiji cha Songwe Viwandani mkoani Mbeya katika hafla iliyofanyika kijijini hapo mwishoni mwa wiki.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Lafarge Tanzania (Mbeya Cement), Catherine Langreney na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Nyirembe Sabi wakimbebesha ndoo ya maji mmoja ya wananchi aliyekuwepo katika uzinduzi wa mradi wa maji uliojengwa na kampuni hiyo kwa ajili ya kuwaondelea tatizo la uhaba wa maji safi na salama wananchi wa kijiji cha Songwe Viwandani mkoani Mbeya katika hafla iliyofanyika kijijini hapo mwishoni mwa wiki.
Mmoja ya wananchi akitoa shukrani mara baada ya kuzinduliwa mradi wa maji uliojengwa na Lafarge Tanzania (Mbeya Cement) kwa ajili ya kuwaondelea tatizo la uhaba wa maji safi na salama wananchi wa kijiji cha Songwe Viwandani mkoani Mbeya katika hafla iliyofanyika kijijini hapo mwishoni mwa wiki.
---Lafarge Tanzania leo imekabidhi mradi wa maji uliogharimu zaidi ya shilingi milioni 10 kwa kijiji cha Songwe Viwandani mkoani Mbeya. Mradi huu unatarajiwa kuwanufaisha familia zaidi ya 200 na unahusisha tanki la kuhifadhi maji pamoja na vifaa mbalimbali vya kusaidia upatikanaji maji safi ya kunywa kwa kijiji hiki. 

Akiongea katika hafla fupi wakati wa kukabidhi mradi huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Lafarge Tanzania, Catherine Langreney amesema kwamba Lafarge Tanzania imedhamiria kusaidia jamii ipate maji safi kwa kuwapatia suluhisho la kudumu la tatizo la maji ikiwa ni sehemu ya mpango wake kusaidia jamii. 

 “Lafarge Tanzania inatambua kwamba maji ni kati ya mahitaji muhimu na kiungo muhimu kwa maendeleo ya nchi kijamii na kiuchumi. Kuwapatia wananchi suluhisho la kudumu la matatizo yao kunadhiirisha azma yetu kuisaidia jamii ambayo imezunguka eneo letu la biashara,” alisema Langreney na kuongeza kwamba upatikanaji wa maji safi ni muhimu kwa afya ya jamii na ni muhimu kwa mazingira pamoja na maendeleo kiuchumi. 

Langreney alisisitiza kwamba upatikanaji maji kwenye kijiji hicho utaboresha hali ya usafi na afya na kuwaletea maisha bora wananchi wa kijiji cha Songwe Viwandani. “Kabla ya mradi huu watu walikuwa wanavuka barabara kuu iendayo Tunduma kuja kuchota maji katika nyumba za kiwanda cha Lafarge Tanzania jambo ambalo limekuwa likihatarisha maisha ya jamii hii.” 

Akizindua mradi huo kama mgeni rasmi, Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Bw. Nyirembe Sabi aliwashukuru Lafarge Tanzania kwa jitihada zao kuboresha maisha ya wananchi na kuongeza kwamba hii inadhiirisha dhamira thabiti ya kiwanda hicho kusaidia jamii na mfano wa kuigwa na makampuni mengine. 

“Jamii pamoja na mazingira yaliyoizunguka vinahitaji maji ili kuweza kustawi, nafurahi kwamba mradi huu utaipatia jamii rasilimali hii muhimu na niwashukuru Lafarge Tanzania kwa jitihada zao,” 

alisema Nyirembe. Mkuu huyo wa wilaya pia aliainisha azma ya serikali kuendeleza ushirikiano na sekta binafsi kwa kusaidia mipango kama ambayo inaboresha maisha ya jamii. 

Mbali na msaada huo, Lafarge Tanzania pia imeanza kutekeleza mradi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu ili kuwapatia wananchi wa Songwe makazi bora na ya gharama nafuu.

DAR INSPIRED TO RECYCLE TRASH INTO HIGH END PRODUCTS

$
0
0
Participants of the Msasani Beach Clean up and Anza up-cycling event looking at some of the products made from waste materials during the event at the Msasani Bonde la Mpunga beach over the weekend.
 Participants of the Msasani Beach Clean up and Anza up-cycling event looking at some of the products made by Wonder Welders workshop from waste materials during the event at the Msasani Bonde la Mpunga beach over the weekend.
 Participants of the Msasani Beach Clean up and Anza up-cycling event collecting waste from the Msasani Bonde la Mpunga beach in Dar es salaam over the weekend.

 By Our Staff Writer Dar es Salaam residents have been challenged to creatively recycle trash materials and convert them into new materials or products of higher value and quality - which would lead to economic empowerment while giving waste materials a new purpose and most importantly avoiding adding them to landfill.

 Sarah Scott, the CEO of Archipelago Productions, organizers of the Msasani Beach Clean Up and Anza Up-cycle Fiesta which took place at Msasani Beach in Dar es Salaam over the weekend said during the event that waste products can be turned into treasure and people can make money from it while keeping the environment clean at the same time. Scott, who has been instrumental in the cleanup of the Msasani beachfront, says there is a lot of trash on this beach that can’t be reused but there are a lot of objects in the streets that can be reused.


 The Archipelago, the Anza magazine in collaboration with the Msasani Bonde la Mpunga community “This is a continuation on our monthly beach clean ups on Msasani beach. Archipelago and Anza magazine have collaborated to bring the community together for a day of cleaning, fun, music and up-cycling. 

We hope to inspire the community to keep their environment clean” said Scott. According to Scott, the event was designed to promote the up-cycling initiatives in Tanzania and it is also a platform for upcyclers to showcase, promote and sell their work and to open people’s eyes to all the possibilities that up-cycling brings. 

 The common denominator is that we make things from consumer recycled material, or what we lovingly call trash. If we want to succeed in closing the loops and creating a truly circular economy, we need to change the common perception that goods made from recycled materials are always a downgrade on what was recycled to make them, and suitable only for low-value applications. 

We need to think of how waste materials can be recycled, showing that you can take trash and create items that are higher value, higher performance and desirable for consumers. 

Msasani Beach Clean Up and Anza Up-cycle Fiesta was organized by Archipelago and sponsored by Coca Cola, Anza Magazine, Regent Tanzania, Knight Support, The Recycle, Impact Promotions, Hugo Domingo and Techno Brain.

MFANYABIASHARA MASHUHURI DEOGRATIUS KILAWE AMEFUNGA PINGU ZA MAISHA NA ANABAHATI MLAY.

$
0
0
 Mfanyabiashara  na mmliki wa makampuni ya excel Management, Mikono Speakers na Focus Outdoor Deogratius Kilawe Jumamosi 12th Sept amefunga  pingu za maisha (ndoa )katika kanisa la st.Peter na kisha kufanya mapokezi serena Hotel.Deogratius Kilawe amefunga Pingu za maisha na Anabahati Mlay.





 






RAIS KIKWETE AFUNGUA CHUO CHA UKAMANDA NA UNADHIMU ARUSHA

$
0
0
 Mkuu wa Chuo Cha Ukamanda na Unadhimu Meja Jenerali Ezekiel Kyunga kulia akimuonyesha Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete maeneo mbalimbali ya Chuo hicho muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuzindua Chuo hicho eneo la Duluti nje kidogo ya mji wa Arusha leo.Kushoto ni Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua vitabu katika maktaba ya Chuo cha Unadhimu na Ukamanda alichokizindua leo.
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia mitaala inayofundishwa katika chuo cha Ukamanda na Unadhimu katika moja ya kompyuta chuoni hapo muda mfupi baada ya kuzindua chuo hicho eneo la Duluthi nje kidogo ya mji wa Arsuha leo.Kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho Meja Jenerali Ezekiel Kyunga.

 
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete akitoa ushauri wakati akikagua majengo ya Chuo Cha Ukamanda na Unadhimu kilichopo eneo la Duluti nje kidogo ya mji wa Arusha leo. Wapili kushoto ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda,kushoto ni Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange, Wapili kushoto ni Mkuu wa chuo hicho Meja Jenerali Ezekiel Kyunga na kulia ni mwakilishi kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu Balozi Ibrahim Al Suweidy.umoja wa Falme za Kiarabu ulishirikiana na Serikali kufadhili ujenzi wa Chuo hicho.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Chuo cha Ukamanda na unadhimu Dukuti nje kidogo ya mji wa Arusha.
 Muonekano wa baadhi ya majengo ya Chuo cha Unadhimu na ukamanda.
(picha na Freddy Maro),.

UFAHAMU VYEMA MOYO WAKO "CARDIAC ARRHYTHMIA"

$
0
0
‘Cardiac Arrhythmia’ ni pale mtu anapokuwa na mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida au yanayodunda sana. 

Mwili una mfumo asili wa umeme unaosaidia moyo kufanya kazi. Mfumo huu husababisha moyo kutanuka na kusinyaa ambapo husababisha damu kuingia na kutoka kwenye moyo; umeme kwa kawaida hufuata mkondo na mapigo ya moyo kwa kasi ya kawaida. 

Ingawa, kama mkondo wa kawaida wa umeme huu ukivurugwa moyo hushindwa kufanya kazi na kusababisha mapigo ya moyo ama kwenda taratibu sana, haraka sana au yasiyoimara.
Kuna aina kadhaa za ‘Arrhythmia’; Baadhi ni pamoja na zijulikanazo kitaalamu kama Supra-Ventricular Tachycardia, Ventricular Tachycardia, Ventricular Fibrillation, Atrial flutter and Atrial Fibrillation.
Mapigo ya moyo yasiyo imara hasa husababishwa na ugonjwa wa moyo na moyo kushindwa kufanya kazi. ‘Arrhythmia’ ndogo pia huweza kusababishwa na mtindo wa maisha usiozingatia afya bora ikiwa ni pamoja na uvutaji sigara uliopitiliza, Ulevi na kuzidisha matumizi ya kafeini au msongo wa mawazo.
Ingawa imegundulika hasa katika uchunguzi wa mara kwa mara wa matibabu dalili za ‘arrhythmia’ ni chache zinazoweza kuonekana ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa mapigo ya moyo, kupungua kwa mapigo ya moyo, maumivu ya kifua, kizunguzungu, kuchoka sana na kukosa pumzi.
‘Arrhythmia’ mara nyingi hutokea kwa nyakati tofauti tofauti. Hali ya kutotabiri kwa ‘arrhythmia’ na kutokea kwake kwa nyakati tofauti tofauti hufanya uchunguzi kuwa mgumu. Moja ya vifaa vitumikavyo zaidi kwa uchunguzi wake kitaalamu ni ‘electrophysiology (EP)’ na kinachukuliwa kuwa bora zaidi katika taaluma hii.
Utafiti wa EP hufanya kazi kwa kupima na kurekodi shughuli za umeme wa moyo na kuonesha njia za umeme. Inaonesha sababu na mahala penye tatizo la mapigo ya moyo. Matatizo yanayotokea katika utafiti wa EP ni machache sana kwa kuwa umekuwa ukifanyika salama kwa miaka mingi sasa. 
Taarifa inaweza kuundwa katika namna mbili, ama kupitia ramani ya shughuli za umeme wa moyo kupitia kifaa maalumu kitaalamu ‘electrocardiogram (ECG)’ inayoonesha wapi ishara zisiyo za kawaida zinaanza kutokea ndani ya moyo.

Mfumo wa wa kitaalamu wa ‘Carto3’ ujulikanao kama ‘3D mapping’ ni teknolojia mpya inayotoa muonekano wa moyo kwa ukubwa mara tatu zaidi. Hii hupelekea kuboreshwa kwa usahihi wa vipimo na matibabu ya mgonjwa.
Kwa kesi ya kushuka kwa mapigo ya moyo, utafiti wa EP unatoa nafasi kutathmini haja ya vifaa kama vile ‘peacemaker’ au ‘defibrillator’ ambavyo husaidia kuzuia vifo vya ghafla vya magonjwa ya moyo.
Baada ya uchunguzi kupitia utafiti wa EP, mirija maalum ya ‘Radiofrequency (RF) catheter ablation’ huingizwa katika mishipa ya damu ambapo viwango vya juu na vya chini vya mzunguko wa nguvu ya umeme vinapokelewa katika tishu za moyo na kuharibu tishu zile zinazohusika na mapigo ya moyo ‘arrhythmia’. Baada ya matibabu kwa kawaida wagonjwa sasa huweza kikamilifu kupunguza matumizi ya dawa ambapo mgonjwa ataweza kupumua vizuri na mapigo ya moyo kwenda vizuri.  
kwa mujibu wa Dkt A M Karthigesan wa hospitali za Apollo baadhi ya ‘arrthythmia’ zilitibiwa kupitia kipimo maalumu kijulikanacho kitaalamu kama ‘RF Ablation’ ni ‘Supraventrical Tachycardia (SVT’; hii inatokea kwenye vyumba vya juu vya moyo na kwa ujumla inaelezewa kama moyo kupiga kwa kasi. 

Pingili za ‘Atirioventrikali (AVNRT)’, ‘atirioventrikali reentry (AVRT)’ na ‘focal atrial tachycardia’ ni baadhi ya aina nyingi za SVT.
Zaidi ‘Atrial Flutter (AFL)’ inaweza pia kutibiwa kwa upasuaji wa RF. AFL ni wakati atria inapopiga haraka sana kwa kiwango cha karibu mapigo 300 kwa dakika yanayotokea katika chumba cha juu cha moyo.
Arrhythmia nyingine maarufu inayotibiwa kwa RF ni ‘Atrial Fibrillation (AF)’. Hii ni wakati uwezo wa moyo kufanya kazi zake unapunguzwa kwa mapigo yasiyo na mpangilio ya chumba cha juu cha moyo. Ingawa ‘atrial fibrillation’ haitishii maisha, kuongezeka kwa mapigo ya moyo huweza kupelekea matatizo kama vile damu kuganda ambapo hatimaye inaweza kusababisha kiharusi.
Mwisho ‘Ventricular Tachycardia (VT)’ ambayo kama ikiachwa bila kutibiwa inaweza kuwa aina ya ‘Arrhythmia’ ya kuhatarisha maisha, hii hutokea wakati chumba cha chini cha moyo kikimpiga kwa kasi sana
Dkt. A M Karthigesan wa hospitali za Apollo anasema kuwa baadhi ya manufaa ya kufanyiwa tiba ya upasuaji kwa mirija ni kuwa mtu atarajie mabadiliko ya haraka katika ubora wa maisha sababu ya kuongezeka kwa uwezo wake wa kufanya kazi; Huduma ya matibabu iliyoboreshwa kwa jinsi mgonjwa anavyohitaji imeondoa upotevu wa muda; Kupungua kwa gharama za tiba na kuokoa maisha ambapo mgonjwa anapewa nafasi nyingine ya kuishi.
Imechangiwa na:
Dkt A M Karthigesan
Mshauri wa tiba ya umeme wa moyo
Hospitali za Apollo, Chennai

KITUO CHA RADIO 5 ARUSHA - CHASAKA WASANII WENYE VIPAJI MTAANI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
????????????????????????????????????
Wasanii wenye vipaji vya kuimba wakihakiki majina yao kwa DJ Haazu, wa Radio 5 wakati wa mchakato wa RADIO 5 KAMATA KIPAJI uliofanyika katika viwanja vya TP SINZA Jijini Dar es salaam Septemba 12, 2015.wenye lengo la kusaka vijana wenye vipaji na kuwainua kutokana na vipaji vyao.
PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON-FULLSHANGWEBLOG
Katika kuonyesha kuwa wapo karibu na vijana wa kitanzania katika kuwasaidia kuwainua kiuchumi na kiuwezo,kituo cha Radio maarufu kutoka kaskazini mwa Tanzania ARUSHA Radio 5 kimenzisha mchato maalum wa kusaka vipaji kwa vijana wa kitanzania mchakato ambao umeanzia Jijini Dar es salaam ukiwa na lengo la kuhakikisha kuwa wanamuwezesha kijana mwenye kipaji kufikia malengo na ndoto zake
3
DJ Haazu akiwajibika.
Radio 5 imekuwa na michakato mbalimbali ili kusaidia vijana katika secta tofauti tofauti zinazohusu maisha yao ya kiuchumi huku ikiwa inawaunga mkono vijana wenye shughuli mbalimbali ambao hufika radioni hapo kuomba saport ikiwa ni pamoja na vijana wa sarakasi,ujasiriamali na fani nyingine. Mchakato ambao sasa unatajwa kuwa utakuwa msaada mkubwa kwa vijana ambao umezinduliwa Jijini Dar es salaam na kupewa jina la RADIO 5 KAMATA KIPAJI katika viwanja vya TP sinza darajani ilishughudiwa vijana wengi wakijitokeza kuonyesha vipaji vyao ili waweze kuibuka na zawadi mbalimbali ambazo zinatolewa na waandaji hao.
2
WAfanyakazi wa RADIO 5 wakishangilia wakati Wasanii mbalimbali ambao ni vijana wenye vipaji wakati wakionesha vipaji vyao jukwaaji (kulia), Mtangazaji wa Redio 5 Mwangaza Jumanne (katikati), Meneja masoko na mawasiliano Sarah Keiya na kushoto ni Meneja Vipindi, Mathew Philip.
Katika zoezi hilo vijana walitakiwa kutuma nyimbo zao radioni ikiwa ni pamoja na kujiandikisha majina yao ili siku waandaaji hao watakapofika katika mtaa waliopo basi waweze kupata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao,na kupatikana washindi ambapo mchakato huo utapita katika maeneo yote ya jiji la Dar es salaam na mwisho kuwapata washindi wanne ambao ndio watakaoibuka na zawadi kabambe. Lengo kuu la mchakato huo ni kuwasaka vijana ambao wanavipaji na wapo mtaani kutokana na sababu mbalimbali ambazo wameshindwa kuonyesha vipaji hivyo ambapo RADIO 5 wameamua kupita katika mitaa hiyo kuhakikisha kuwa vijana hao wanapata nafasi ya kuonyesha vipaji walivyo navyo kwa watanzania.
16
Umati wa mashabiki waliojitokeza kushuhudia wasanii wenye vipaji jukaani.
Wakati zoezi hilo likiendelea mtandao huu ulipata nafasi ya kuzngumza na mkurugenzi wa RADIO 5 Bw ROBERT FRANCIS ambaye amesema kuwa ni jambo jema kuona kazi hilo imeanza kwa amani na furaha hivyo watanzania waendelee kuwaunga mkono huku akiwataka vijana mbalimbali wenye vipaji mkoani Dar es salaam kuendelea kujitokeza maeneo mbalimbali ambapo ziezi hilo litakuwa linafanyika pamoja na kuendelea kusikiliza Radio hiyo.
 
Naye meneja vipindi wa RADIO 5 Ndugu MATHEW PHILIP Akizungumza na mtaandao huu wakati zoezi hilo likiendelea amesema kuwa kupitia vipindi vya Radio hiyo hasa vipindi vya kutafuta vipaji nyumba kwa nyumba Dar es salaam vijana wataweza kuinua vipato vyao huku akisisitiza kuwa watanzania waendelee kusikiliza RADIO 5 kwani kuna mambo mengi na mazuri yanaendelea kuwajia.
4
Msanii akilimiki jukwaa.
Meneja biashara wa kituo hicho cha Radio Bi ANGELA MAINA alisema kuwa maana halisi ya kufanya zoezi hilo ni kuwapa vijana nafasi ili kukuza vipaji vyao hasa katika tasnia ya music ili miaka ijayo watanzania waone matunda ya kazi hiyo haswa kwa washiriki wa zoezi hilo.
Aidha meneja masoko na mahusiano wa RADIO 5 Bi SARAH LAZARO alisema kuwa pamoja na lengo kuu la mchakato huo ni kuvumbua na kunyanyua vipaji lakini pia ni nafasi kwa wadau wa biashara na mashirika binafsi haswa yanayojihusisha na maswala ya kijamii kuanza sasa kushirikiana na radio 5 ili kukuza biashara zao na kushiriki katika kuendeleza jamii.
5
Mtangazaji wa kituo hicho Julius Kamafa.
Katika mchakato huo endelevu utakao fanyika katika jiji la Dar es salaam unataraji kuwapata washindi wanne wa mkoa huu ambapo washindi hao watajinyakulia zawadi mbalimbali kama ifuatavyo
Mshindi wa kwanza anataraji zawadi ya kurekord albam nzima bure kwenye studio za kisasa na kupata promotion kubwa ya kazi yake,mshindi wa pili anataraji kurekord nyimbo mbili bure pamoja na pamoja na promotion ya miezi sita(6),mshindi wa tatu atapata kurekord nyimbo moja pamoja na promotion ya miezi mitatu,huku mshindi wan ne ataweza kurecord nyimbo moja pamoja na promotion ya mwezi mmoja.
6
Msanii Hance Mpozi kutoka Tegeta Dar es Salaam akionesha kipaji chake.
7
Mashabiki.
9
Wanii wa kundi moja wakimiki jukwaa.
10
Ni Msaga Sumu akitoa burudani.
DSC_0166
Mtalamu wa kiduku.
11
14
12
DSC_0180
Kulia ni DJ Haazu, pamoja na wasanii.
15
????????????????????????????????????
20
Wafanyakazi wa Redio 5 wakiwa katika picha ya pamoja.

RAIS DK.SHEIN AMUAPISHA MKUU MPYA WA WILAYA

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Nd,Mwinyiussi Hassan Abdalla kuwa Mkuu wa Wilaya Magharibi A Unguja katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi hati ya kiapo Nd,Mwinyiussi Hassan Abdallabaada ya kumuaapisha kuwa Mkuu wa Wilaya Magharibi A  katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
 [Picha na Ikulu.]

 Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Mkuu mpya wa Wilaya ya Magharibi A Unguja Nd,Mwinyiussi Hassan Abdalla,iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu,(kutoka kulia)Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara maalum Haji Omar Kheir,Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis,Meya wa Manispaa ya Mji wa ZanzibarMr.Khatib na Mshauri wa Rais wa Uwezeshaji wananchi Kiuchumi Bw.Abrahman Mwinyijumbe

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MATOKEO YA OPERESHENI GIBOIA II

$
0
0
 Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Hiiti Sillo akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini(TFDA) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi  imefanya operesheni katika maeneo 243 na kufanikiwa  kukamata bidhaa bandia na zile zilizomaliza muda wa kutumika ambapo zina thamani  zaidi ya shilingi milioni 135. katika mkutanono uliofanyika leo jijini Dar es Salaam kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Dawa wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Henry Irund.
 Naibu Kamishina wa Polisi (DCI) Makao Mkuu ya Upelelezi na Jinai, Hezron Gyimbi akuzungumza na wanahabari hawapo pichani juu ya Operesheni GIBOIA II iliyofanyika sanjari katika nchi nane zilizopo kusini mwa jangwa la Sahara ambazo ni Afrika Kusini, Zimbabwe, Malawi na Msumbiji. Operesheni GIBOIA II ameyasema hayo katika mkutano ulifanyika jijini Dar es Salaam kulia ni  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Hiiti Sillo.
 Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Hiiti Sillo na wakionesha waandishi wa habari bidhaa bandia  katika mkutano huo jijini Dar es Salaam.
Mkaguzi wa Dawa Mwandamizi, Sonia Mkumbwa akiwaonesha  Bidhaa bandia  katika mkutano jijini Dar es Salaam.
Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya  Jamii.

LOWASSA AENDELA NA ZIARA YA KAMPENI MKOANI SHINYANGA LEO

$
0
0
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiongozana na aliekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Ndg. Hamis Mngeja wakiwapungia wananchi wa Mji wa Kahama, wakati wakiwasili kwenye Uwanja wa Stendi mpya, Nyasubi, Kahama Mjini leo Septemba 14, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akipokelewa na Mwenyeji wake, Mgombea Ubunge wa Ukawa kupitia CHADEMA, Mh. James Lembeli, wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Stendi mpya, Nyasubi, Kahama Mjini leo Septemba 14, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akilakiwa na maelfu ya wakazi wa mji wa Kahama, leo Septemba 14, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwasalimia wananchi wa Mji wa Kahama.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiteta jambo na Mgombea Ubunge wa Ukawa kupitia CHADEMA, Mh. James Lembeli, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Stendi mpya, Nyasubi, Kahama Mjini leo Septemba 14, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akihutubia Mkutano wa Kampeni wa hadhara wa kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Stendi mpya, Nyasubi, Kahama Mjini leo Septemba 14, 2015.
Mwanasheria wa CHADEMA, Mh. Tundu Lissu akihutubia Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Stendi mpya, Nyasubi, Kahama Mjini leo Septemba 14, 2015.
Mgombea Ubunge wa Ukawa kupitia CHADEMA, Mh. James Lembeli, akihutubia Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Stendi mpya, Nyasubi, Kahama Mjini leo Septemba 14, 2015.
Sehemu ya Umati wa wananchi wa Mji wa Kahama, wakiwa wamefurika kwenye Uwanja wa Stendi mpya, Nyasubi, Kahama Mjini leo Septemba 14, 2015, wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnadi Mgombea Ubunge wa Ukawa kupitia CHADEMA, Mh. James Lembeli, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Stendi mpya, Nyasubi, Kahama Mjini leo Septemba 14, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwanadi Wagombea wa Udiwaki wa Kata mbalimbali za Kahama, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Stendi mpya, Nyasubi, Kahama Mjini leo Septemba 14, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akipokea mfano wa funguo yenye ujumbe wa "Mabadiliko", kutoka kwa Mgombea Ubunge wa Ukawa kupitia CHADEMA, Mh. James Lembeli, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Stendi mpya, Nyasubi, Kahama Mjini leo Septemba 14, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwa ameinua juu mfano wa funguo.
Mdau akijipoza kwa maji wakati akiwa kwenye Mkutao wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Stendi mpya, Nyasubi, Kahama Mjini leo Septemba 14, 2015.

TAZAMA GHARIKA YA MAGUFULI NDANI YA TABORA LEO.


TASWIRA ZA UWANJA WA KAITABA UNAVYOENDELEA MPAKA SASA MJINI BUKOBA. KUMALIZIKA KUJENGWA MWEZI DESEMBA 2015

$
0
0
Taswira ya Uwanja wa Kaitabaulivyo kwa sasa.



Nyasi bandia zikiwa zimewekwa pembeni ya Uwanja tayari kwa kutandikwa katika Uwanja huo
Mwakilishi kutoka shirikisho la soka Duniani (FIFA) baada ya kukagua maendeleo ya uwekaji nyasi bandi katika uwanja wa mpira wa Kaitaba Amewaomba mafundi kuongeza kasi ili ukamilike kwa muda uliopangwa. Mwakilishi huyo wa FIFA Mhandisi Kelvin Macklain, alitua Bukoba wiki iliyopita na kukagua hatua kwa hatua uwanja huo na alifika hapo kukagua hatua za mwisho kabla ya nyansi husika kuanza kutandazwa, ambazo tayari zipo katika uwanja huo. Picha zote na Faustine Ruta wa bukobasports.com

Hata hivyo Katibu wa chama cha Soka Wilaya ya Bukoba Malick Tibabimale, alisema kuwa sehemu ya kati ya uwanja itakamilika ndani ya mwezi mmoja, na timu ya Kagera sugar itaanza kuutumia uwanja huo baada ya mechi zake nne za mzunguko wa kwanza. Timu ya Kagera Sugar kwa sasa itaendelea kutumia Uwanja wa Musoma kama uwanja wake wa nyumbani katika Ligi kuu ya vodacom iliyoanza kutimua vumbi jumamosi septemba 12, 2015.
Mhandisi kutoka kampuni ya Artificial Grass africa, wanaojenga uwanja huo Pierre De Groote baada ya kuukagua Uwanja huo alisema watamaliza kazi yote mwezi Disemba mwaka huu 2015.Mhandisi Kelvin Macklain Mwakilishi kutoka FIFA akifanya vipimo katika Uwanja wa Kaitaba unaoendelea kujengwa mpaka sasa. Picha zote na Faustine Ruta wa bukobasports.com


Sehemu ya katikati ya Uwanja wa Kaitaba ambayo itakamilika mwezi huu wa tisa.
Picha zote na Faustine Ruta wa bukobasports.com

EFM YAANZISHA SHINDANO LA KANGA KWA WANAWAKE KUPITIA KIPINDI CHA UHONDO

$
0
0
 Ofisa Habari, Lydia Moyo (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo wakati akimkaribisha Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Redio EFM, Denis Ssebo  kuzungumza na wanahabari.
 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Redio EFM, Denis Ssebo (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu shindano lililoanzishwa na redio hiyo la Kanga kupitia kipindi cha Uhondo kwa ajili ya wanawake wote wasikilizaji wa redio hiyo ambalo limeanza rasmi jana. Kulia ni Mtangazaji wa kipindi hicho, Dina Marios na Ofisa Habari, Lydia Moyo.
 Mtangazaji wa kipindi cha Uhondo, Dina Marios (kulia), akizungumzia shindano hilo.
Wapiga picha kazini katika mkutano huo 'Kazi yote  hiyo wanatafuta shibe chezea njaa wewe' 
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com

BONAH KALUWA AFUNGUA KAMPENI DHIDI YA UKATILI WA JINSIA KATIKA SOKO LA TABATA MUSLIM DAR ES SALAAM LEO

$
0
0

 Mwanaharakati wa kutetea wanawake na mgombea Ubunge wa Jimbo la Segerea kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bonah Kaluwa (kulia), akizungumza na wanawake wakati akifungua kampeni ya kupinga ukatili wa jinsia dhidi ya wanawake katika Soko la Tabata Muslim lililopo mtaa wa Msimbazi,  Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Mjumbe wa mtaa huo, Tatu Lazaro na Mwenyekiti wa mtaa huo, Beatries Mkama.
Wanafunzi na wakazi wa Tabata Muslim wakiwa kwenye mkutano huo.
Meza kuu inavyoonekana katika ufunguzi wa kampeni hiyo.
Mgeni Rasmi Bonah Kaluwa akiwa meza Kuu.
Mgeni rasmi katika picha ya pamoja na wadau wapinga ukatili wa kijinsia masokoni.
Mgeni rasmi Bonah Kaluwa akiwa katika picha ya pamoja na wanawake wapinga ukatili wa kijinsia wa Tabata Muslim.
Mgeni rasm akiondoka eneo la mkutano.
Wasanii wa kundi la Machozi wakitpoa burudani katika uzinduzi huo.
Maofisa wa Shirika la Equality for Growth (EfG), wakiwahamasisha wananchi kujaza fomu za kuwa mabalozi wa kampeni ya kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake masokoni. 

MCHANGANYIKO WA ASALI NA MDALASINI KATIKA KUTIBU CHUNUSI SUGU

$
0
0
Asali ikiwa imechanganywa na mdalasini tayari kwa matumizi
Wadau wetu wale ambao wanasumbuliwa sana na CHUNUSI iwe USONI, KIFUANI,MGONGONI n.k wanaweza tumia mchanganyiko mzuri wa ASALI na MDALASINI WA UNGA
kwa kupaka angalau mara moja kwa siku.

ASALI na MDALASINI zinasaidia kuponyesha kwasababu zina tabia za
ANTI-BACTERIAL( zinaua na kuzuia mazalia ya bacteria)
Jinsi ya kufanya:-

1. Chukua vijiko vitatu(3) vya chai vya ASALI
2. Chukua nusu kijiko cha chai cha MDALASINI WA UNGA safi
3. Changanya pamoja kupata uji uji mzuri
4. Paka sehemu yenye chunusi na kisha kaa nayo kwa angalau dakika 10-30
kisha osha kwa maji ya uvuguvugu.
ANGALIZO: MDALASINI unaweza kuwasha kwenye ngozi hivyo unashauriwa ujaribu
kupaka kidogo kwenye kiganja cha mkono kwanza ili kupata uhakika kua
haitakusumbua.
(Imeandaliwa na Honey Spring na Jamiimojablog)
 0683370065 au 0769129351

Mgombea Mwenza CCM Aupukutisha Upinzani Lindi, 61 Wajiunga CCM, Wamo Viongozi

$
0
0
Umati wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho ukiwa umefurika katika uwanja wa Mnazi Mmoja nje kidogo ya mji wa Lindi Mjini kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu.
Umati wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho ukiwa umefurika katika uwanja wa Mnazi Mmoja nje kidogo ya mji wa Lindi Mjini kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu.
Umati wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho ukiwa umefurika katika uwanja wa Mnazi Mmoja nje kidogo ya mji wa Lindi Mjini kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu.
Mke wa Rais Kikwete, Mama Salma Kikwete akizungumza na umati wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho uliokuwa umefurika katika uwanja wa Mnazi Mmoja nje kidogo ya mji wa Lindi Mjini kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu.
Katibu, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akizungumza na wanaCCM na wananchi kwenye mkutano wa kampeni za mgombea mwenza wa CCM, Mama Samia Suluhu jana Mkoani Lindi.
Bi. Samia Suluhu (kulia) akimtambulisha mgombea mmoja wa wagombea udiwani katika Jimbo la Mchinga, kuzungumza na wapiga kura wa eneo hilo.
Samia Suluhu akimpokea mmoja wa wanachama mpya aliyejiunga na CCM katika Jimbo la Mchinga.

Bi. Samia Suluhu akimpokea mmoja wa wanachama mpya aliyejiunga na CCM katika Jimbo la Mchinga.
Mmoja wa wanachama wapya wa CCM aliyejiunga na CCM mara baada ya mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza katika Jimbo la Mchinga.
KAMPENI za mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu zinazoendelea mkoani Lindi zimekuwa tishio kwa vyama vya upinzani baada ya mkutano uliofanyika jana eneo la Mnazi Mmoja nje kidogo ya mji wa Lindi Mjini kuzoa wanachama 61 waliotoka upinzania na kujiunga na CCM.

Mkutano huo wa kampeni uliohudhuriwa pia na Mke wa Rais Mama Salima Kikwete umeacha maumivu kwa vyama vya upinzani vya CUF, Chadema na NCCR-Mageuzi baada ya kujikuta wanachama 61 wakivikimbia vyama vyao na kujikuta wakijiunga na Chama Cha Mapinduzi na kukabidhiwa kadi mpya za CCM kila mmoja.

Miongoni mwa wanachama ambao walipokelewa leo ni pamoja na Katibu wa Chadema Wilaya ya Lindi Mjini, Abdullah Madebe, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Mtaa wa Nananji Lindi, Bakari Kalulu na wanachama wengine kutoka vyama vya CUF na Chadema. Akizungumza baada ya kumkabidhi kadi, Bi. Samia Suluhu Katibu wa Chadema Wilaya ya Lindi Mjini alisema awali alipokuwa upinzani alikuwa amepotea na amegunduwa kuwa alikuwa anapoteza muda hivyo kuomba wananchi wamsamehe na ameamua kurudi kundini na kuendelea kulkijenga taifa.

Akizungumza baada ya kuwapokea wanachama hao, mgombea mwenza Suluhu alisema Serikali ya awamu ya tano imeandaa mambo mengi mazuri kwa mikoa ya Lindi na Mtwara na jambo la kwanza kulifanya baada ya kuunda serikali ni kuubadili mji wa Mtwara na Lindi kuwa miji ya viwanda, hali ambalo itakuza uchumi kwa kiasi kikubwa hivyo kunufaisa wananchi.

Alisema kwa kuanzia Serikali inajenga viwanda vinane mkoani Mtwara na vingine vitajengwa mkoani Lindi viwanda ambavyo vitategemea gesi katika uzalishaji wake bidhaa ambayo tayari inapatikana kwa wingi katika maeneo hayo. Alisema ujenzi wa viwanda utaongeza kasi ya ukuaji wa uchumi na kuongeza nafasi za ajira jambo ambalo litawanufaisha wakazi wa eneo hilo na wawekezaji.

"...Tunataka kuitenga Lindi kuwa mji wa viwanda vitakavyoitumia gesi kwa uendeshaji, lengo ni kuwa na viwanda vitakavyozalisha nafasi za ajira takribani asailimia 40...," alisema Bi. Suluhu. Awali akihutubiwa katika mkutano wa kampeni ulofanyika Kata ya Mingumbi Kilwa Kusini, alisema Serikali inatambua hali ya kuyumba kwa soko la korosho na ufuta ili kukabiliana na hali hiyo imejipanga kujenga viwanda vya kubangua na kufunga korosho pamoja na kukamua mafuta kwa lengo la kumuongezea thamani mkulima katika zao analozalisha.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa Mnazi Mmoja Katibu, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye aliwatoa hofu akinamama na wapiga kura wengine juu ya vitisho vya kuwepo na vurugu kipindi cha uchaguzi kwa lengo la kuwatisha wapiga kura, hivyo kuwataka wananchi wasiogope kwani Serikali na CCM kupitia vijana wake imejipanga kupambana na wafanya fujo hao.

Alisema kitendo cha kutoa vitisho kwa wapiga kura ni kuibaka demokrasia hivyo CCM na vijana wake hawatakuwa tayari kuona demokrasia inabakwa nchini na wapuuzi wachahe. "...Vijana wa CCM naomba mkikamata kibaka wa demokrasia shughulikeni naye kidogo kabla ya kumpeleka polisi...CCM itashinda kwa kishindo," alisema Nape Nnauye.

Aidha msemaji huyo wa Chama Cha Mapinduzi alisema mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa pamoja na mpambe wake anayemuunga mkono Fredrick Sumaye hawawezi kuiponda Serikali ya CCM kwa kuwa wao wamekuwemo na kushika nafasi za juu za utendaji ndani ya serikali na kama walishindwa kuleta mabadiliko hawawezi kufanya hivyo leo.

Aliongeza kuwa kitendo cha kuendelea kuiponda ni sawa na kujidhalilisha wao wenyewe kwa wananchi hivyo kuwataka wasiwarubuni Watanzania kwamba wanamabadiliko ya msingi zaidi ya maslahi yao binafsi, ambayo ndiyo yanayowasukuma kukimbilia walipo.

Mgombea mwenza wa urais CCM, Bi. Suluhu bado anaendelea na ziara ya kuinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi Mkoani Lindi na baada ya kumaliza majimbo ya mkoa huo ataendelea katika Mkoa wa Mtwara, kuwashawishi wananchi kuichangua CCM ili iweze kupata ridhaa ya kuunda Serikali ya awamu ya tano.

Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Suluhu kwenye Jimbo la 

Kutoka kushoto ni mgombea mwenza wa CCM nafasi ya uraisa, Bi. Samia Suluhu na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mwantumu Maiza na mgombea wa Jimbo la Mchinga Said Mtanda wakiwa kwenye mkutano wa kampeni katika Jimbo la Mchinga jana.
Mgombea Jimbo la Mchinga Said Mtanda akizungumza na wannaCCM na wananchi jana jimboni kwake ambapo mgombea mwenza alihutubia wananchi.
Sehemu ya wanaCCM na wananchi jana jimboni kwake ambapo mgombea mwenza alihutubia wananchi.
Mbunge wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam, Anjela Kiziga akizungumza katika mkutano wa kampeni za CCM. 
Aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya Ushindi Chadema Taifa, Greison Nyakarungu ambaye kwa sasa amejiunga na CCM akizungumza katika moja ya mikutano ya kampeni ya CCM.
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Nkenge, Asumpta Mshama akipiga madongo kwa wapinzani kwenye moja ya mikutano ya kampeni ya CCM.  
Umati wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho ukiwa umefurika katika uwanja wa Mnazi Mmoja nje kidogo ya mji wa Lindi Mjini kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu.
Katibu, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye (kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bi. Mwantumu Mahiza.
Umati wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho ukiwa umefurika katika uwanja wa Mnazi Mmoja nje kidogo ya mji wa Lindi Mjini kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mwantumu Mahiza akizungumza na wanaCCM na wananchi kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM, Mama Samia Suluhu.
Mke wa Rais Kikwete, Mama Salma Kikwete, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi, Mzee Ally Mtopa pamoja na mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu wakijadiliana jambo kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM viwanja vya Mnazi Mmoja.
Sehemu ya umati wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho ukiwa umefurika katika uwanja wa Mnazi Mmoja nje kidogo ya mji wa Lindi Mjini kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu.
Katibu wa Chadema Wilaya ya Lindi Mjini, Abdullah Madebe akikabidhi kadi ya chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Aliyekuwa Katibu wa Chadema Wilaya ya Lindi Mjini, Abdullah Madebe (kulia) akipongezwa na Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu mara baada ya kujiunga na CCM, Katikati ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Mmoja wa wananchi waliojiunga na CCM katika mkutano huo akizungumza baada ya kujiunga na chama hicho tawala.
Mmoja wa wananchi waliojiunga na CCM katika mkutano huo akizungumza baada ya kujiunga na chama hicho tawala.
Mama Salma Kikwete pamoja na Bi. Samia Suluhu wakipokea kadi za wanachama waliojiunga na CCM jana Mkoani Lindi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi, Mzee Ally Mtopa kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM viwanja vya Mnazi Mmoja.

Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu akizungumza na wanaCCM pamoja na wananchi viwanja vya Mnazi Mmoja.
Kada wa CCM na mbunge wa zamani wa Mchinga, Mudhir Mudhir akizungumza na wanaCCM pamoja na wananchi wa Jimbo la Mchinga katika mkutano wa kampeni.
*Imeandaliwa/www.thehabari.com
Viewing all 46367 articles
Browse latest View live




Latest Images