Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 627 | 628 | (Page 629) | 630 | 631 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Na Mwandishi Wetu,
   KageraTAASISI ya kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mambo ya mikopo, jana imewakabidhi hundi ya Sh Milioni tatu watoto watatu wilayani Biharamulo, mkoani Kagera, kwa ajili ya kunufaika na huduma ya Bima ya Elimu iliyoachwa na mzee wao Karume Ochieng aliyefariki Dunia, huku akiwa amejiunga na huduma ya bima kwa ajili ya watoto wake hao.
  Mratibu Mauzo wa Bima ya Elimu wa Taasisi ya Kifedha inayotoa Mikopo(Bayport Financial Services, Ruth Bura akikabidhi mfano wa hundi kwa familia ya marehemu Karume ambaye alikuwa amejiunga na bima hiyo katika shule ya msingi Nyamuhuna iliyopo wilayani Biharamulo mkoani Kagera, kushoto ni Meneja Mauzo wa Bayport Kanda ya Ziwa, Lugano Kasambala. Taasisi hiyo imeanzisha bima ya elimu ili kusaidia kiasi cha ada kwa watu wa karibu walioainishwa na mteja wao endapo atakumbwa na umauti.

  Watoto hao ambao wamepewa hundi hiyo itakayowawezesha kila mwaka katika vipindi vya miaka mitatu mfululizo kupewa Sh Milioni moja kwa ajili ya kuwalipia ada katika shule wanazosoma ni pamoja na Athieno Karume, Chacha Karume na Aaptalius Karume.
  Makabidhiano ya hundi kwa familia ya marehemu Karume yakiendelea wilayani Biharamulo, mkoani Kagera.

  Akizungumza katika makabidhiano ya hundi hiyo kwa watoto hao, Mratibu wa Bima ya Elimu ya Bayport Financial Services, Ruth Bura, alisema kwamba kukabidhi hundi hiyo kutawafanya watoto hao wasome kwa raha, baada ya kuwekewa bima hiyo na marehemu baba yao kutokana na mapenzi mema na vijana hao wanaoendelea na masomo.


  Meneja Mauzo Kanda ya Ziwa kutoka Bayaport Financial Services, Lugano Kasambala, akitayarisha mfano wa hundi ya Sh Milioni Tatu kwa ajili ya kukabidhi familia ya marehemu Karume. Mwenye miwani ni Mratibu wa Bima ya Elimu wa Bayport, Ruth Bura.

  Alisema Bayport imekuwa ikilipa watu waliotajwa katika huduma ya bima kwenye taasisi yao, wakiamini kuwa huduma hiyo itakuwa na manufaa makubwa na Watanzania wote wenye ndoto za kuona watoto wao wanasoma kwa bidii.


  Gari linalomilikiwa na Bayport Financial Services, likiingia katika shule ya Msingi Nyamuhuna, iliyopo wilayani Biharamulo, mkoani Kagera kwa ajili ya kukabidhi hundi ya Sh Milioni Tatu.

  "Bayport ni taasisi ya Watanzania wote, hivyo tunaamini kukabidhi hundi hii kwa wanafunzi hawa ni jambo jema litakalowapatia mwangaza zaidi, ukizingatia kwamba kila mwaka tutawapa sh Milioni Milioni moja kwa kipindi cha miaka mitastu mfululizo
  .
  "Tunaomba watoto hawa watumie fursa hii vizuri na iwe njia moja wapo ya kuwafanya Watanzania wote waendelee kuiunga mkono taasisi hii yenye kutoa huduma bora za mikopo ya fedha, viwanja na, bima ya magari na huduma nyingine muhimu zinazokuza uchumi na kuwakwamua Watanzania wote,” alisema Ruth. Naye Chacha Karume, aliishukuru Bayport kwakuwapatia fedha hizo huku akisitiza kwamba zimekuja wakati muafaka kwa ajili ya kuwakwamua katika kipindi hiki cha kuelekea mwisho wa mwaka.

  “Tunashukuru kuona tumepewa fedha hizi bila usumbufu wowote na tunaamini tutasoma vizuri, maana changamoto za ada na huduma nyingine za kijamii zitakuwa zimekombolewa katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo tutakapopewa fedha hizo,” Alisema.
   
  Bayport ni taasisi ya kifedha inayotoa huduma bora za kifedha, ambapo imekuwa ikizindua huduma mbalimbali kama vile mikopo ya bidhaa, viwanja vya mradi wa Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, mikopo ya fedha na nyinginezo zinazowakwamua kiuchumia wateja wao ambao ni watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni zilizoidhinishwa na Bayport, huku huduma hizo zikitolewa pia kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz.  0 0

   Na Mwandishi Wetu,
  SERIKALI ya Tanzania imeelezea utayari wake wa kupiga jeki na kuwajumuisha wafanyakazi wa afya ya jamii katika nguvukazi ya sekta ya afya (national health workforce) ya taifa ili kuboresha afya ya jamii hususani katika maeneo ya vijijini.

  Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya wadau wa mradi wa mafunzo ya wafanyakazi wa afya ya jamii (Community Health Worker Learning Agenda Project - CHW-LAW) jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji (idara ya uzazi na afya ya mtoto) katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Bi Georgina Msemo alisema ni muhimu kuwajengea uwezo wafanyakazi wa afya ya jamii ili kukidhi mahitaji ya kijamii. 

  Akimwakilisha Mkurugenzi wa Huduma za Kinga katika Wizara ya Afya, Dkt Neema Rusibamayila, Msemo aliwaasa wadau kufanya tafiti ya kisayansi ili kukabiliana na hali ya upungufu wa wafanyakazi wa afya ya jamii, ambao umekuwa ni kikwazo kikubwa katika utoaji wa huduma za kiafya nchini. 

  Msemo alipongeza hatua ya wadau hao kwa kuzungumzia masuala ya wafanyakazi wa afya ya jamii pamoja na kuja na mradi utakaowezesha wafanyakazi hao kupata mafunzo ya kila mara ili kuboresha utendaji wao katika utoaji wa huduma ya afya ya jamii. 

  Alisema wafanyakazi wa afya ya jamii wanamchango mkubwa katika maendeleo ya jamii ikiwa pia katika uboreshaji wa sekta ya afya haswa katika magonjwa ya malaria, kifua kikuu, VVU/Ukimwi, afya ya Uzazi na mtoto. 

  Naye, Profesa Japhet Killewo, ambaye ni Mchunguzi Mkuu mradi wa mafunzo ya wafanyakazi wa afya ya jamii, alisema lengo la semina hiyo ya siku nzima iliyofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam lilikuwa ni kuwakutanisha pamoja wadau katika afya ya jamii pamoja na wahisani kujadili utekelezaji wa utafiti uliofanywa na njia bora za kuiboresha na kuikuza sekta ya afya nchini. 

  Killewo alisema kuwa wafanyakazi wa afya ya jamii wamekuwa kwa miaka mingi wakikosa kutambuliwa kwa kuwa wengi wao walikuwa darasa la saba na wahitimu wa kidato cha nne, wengi wao mbali ya kuwa na uzoefu, wamekuwa wakifanya kazi za kuijtolea bila mshahara. 

  Alisema kuwa hilo limechangia kukosekana kwa jitihada madhubuti ya kazi miongoni mwao. 

  Alisema kuwa na ndiyo sababu CHW-LAW, wakishirikiana na serikali na wahisani ambao ni pamoja na USAID, Muhas na Johns Hopkins wameamua kuandaa semina hiyo kwa wafanyakazi wa afya ya jamii. 

  Alisema kuwa semina hiyo, ambayo pia itafanyika mwezi oktoba, itafanyika katika mikoa mitano ambayo ni Mwanza, Kigoma, Simiyu, Shinyanga na Tarime, ambayo ipo katika mpango wa serikali wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Result Now). Ambapo wapatao wafanyakazi 300 wa afya ya jamii wanatarajia kuudhuria. 

  Alisema semina kama hizo zikipewa msukumo na serikali na wahisani mbali mbali pia zitafanyika katika mikoa mingine nchini. 
  Mkurugenzi Mtendaji (idara ya uzazi na afya ya mtoto) katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Bi Georgina Msemo akizungumza na wadau wa sekta ya Afya ya Jamii (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa semina ya Wadau wa  Juu Agenda ya Mradi wa Mafunzo kwa Wafanyakazi wa Afya ya Jamii jijini Dar es Salaam Jumanne.
  Mchunguzi Mkuu mradi wa mafunzo ya wafanyakazi wa afya ya jamii, Profesa Japhet Killewo akizungumza na wadau wa sekta ya Afya ya Jamii (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa semina ya Wadau wa  Juu Agenda ya Mradi wa Mafunzo kwa Wafanyakazi wa Afya ya Jamii jijini Dar es Salaam Jumanne. 
  Mkurugenzi Mtendaji (idara ya uzazi na afya ya mtoto) katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Bi Georgina Msemo akizungumza na wadau wa sekta ya Afya ya Jamii (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa semina ya Wadau wa  Juu Agenda ya Mradi wa Mafunzo kwa Wafanyakazi wa Afya ya Jamii jijini Dar es Salaam Jumanne.
  Mkurugenzi Msaidizi, Ukuzaji Afya Bi Hellen Semu, kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii akizungumza na wadau wa sekta ya Afya ya Jamii (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa semina ya Wadau wa  Juu Agenda ya Mradi wa Mafunzo kwa Wafanyakazi wa Afya ya Jamii jijini Dar es Salaam Jumanne.


  Mwakilishi kutoka United States Agency for International Development (USAID), Bi Anna Bodipo akizungumza na wadau wa sekta ya Afya ya Jamii (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa semina ya Wadau wa  Juu Agenda ya Mradi wa Mafunzo kwa Wafanyakazi wa Afya ya Jamii jijini Dar es Salaam Jumanne. 
  Wadau wa sekta ya Afya ya Jamii katika picha ya pamoja wakati wa ufunguzi wa semina ya Wadau wa  Juu Agenda ya Mradi wa Mafunzo kwa Wafanyakazi wa Afya ya Jamii jijini Dar es Salaam Jumanne. Picha na mpiga picha wetu.

  0 0

  Washiriki wa Kongamano la Wasaidizi wa Kisheria Magerezani kutoka Magereza Mkoani tanga wakiendelea na majadiliano katika Kongamano hilo linalofanyika Mkoani Morogoro kwa siku tatu.


  Na, Lucas Mboje, Morogoro
  Jeshi la Magereza nchini limeahidi kuendelea kushirikiana na Asasi ya Envirocare katika kuimarisha Madawati ya Msaada wa Kisheria Magerezani ili kuleta tija katika utatuzi wa changamoto ya Msongamano wa Mahabusu inayolikabili Jeshi hilo.

  Kauli hiyo imetolewa jana Mkoani Morogoro na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja alipokuwa Mgeni rasmi wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Wasaidizi wa Kisheria Magerezani na Mahabusi za Watoto.

  Jenerali Minja amesema kuwa Serikali imeendelea kuchukulia kwa uzito stahiki suala la Msongamano wa Mahabusu Magerezani ikiwemo kushirikiana na Wadau wa Haki Jinai katika kupunguza changamoto ya Msongamano wa Mahabusu Magerezani.

  "Napenda kutoa rai kwa Asasi zingine zenye malengo yanayofanana na Asasi hii nazikaribisha kuja kufanya kazi na Jeshi la Magereza kwani mwelekeo wa Jeshi kwa sasa ni Urekebishaji wa Wafungwa(From Prisons to Corrections) ambapo Jeshi la Magereza watafanya kazi kwa karibu na Asasi za Kiraia na Jamii kwa ujumla". Alisema Jenerali Minja.


  Awali akimkaribisha Mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Envirocare, Bi. Loyce Lema amesema kuwa imekuwa ni faraja kwao kupata ushirikiano kama huo kutoka Jeshi la Magereza kwani umewezesha kutekelezwa kwa mradi huo wa kutoa Msaada wa Kisheria kwa Mahabusu waliopo Magerezani kwa matokeo chanya kwa muda mufupi.

  Bi. Lema alisema kuwa mradi huo umetekelezwa kwa miaka mitatu(2012 - 2015) na umetekelezwa kwenye Magereza 20 na Mahabusu 04 za Watoto katika Mikoa 05 ambayo ni Mkoa wa Kilimanjaro, Arusha, Tanga, Morogoro na Dar es Salaam.

  Asasi ya Envirocare kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza ilifanya utafiti wa awali wa kuangalia hali halisi ya Msongamano katika Magereza yaliyopo katika Mikoa mitano ya mradi. Matokeo ya jumla ya utafiti huo yalionesha kuwa kuna tatizo kubwa la Msongamano ambao unasababishwa na idadi kubwa ya Mahabusu katika Magereza ya Mikoa hiyo.

  0 0

   Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Juliana Yassoda akiikabidhi Timu ya Taifa ya Paralympic vifaa vya michezo kwa ajili ya kwenda nchini Congo Brazaville kwenye mashindano ya Afrika  (All African Games).Kushoto anayepokea vifaa hivyo ni Kocha wa Timu hiyo Bw. Zaharan Mwenemti. 

   Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Juliana Yassoda akiongea na kikosi cha Timu ya Taifa ya Paralympic wakati akiwakabidhi vifaa vya michezo kwa ajili ya kwenda nchini Congo Brazaville kwenye mashindano ya Afrika (All African Games).Kushoto aliyesimama ni Kocha wa Timu hiyo Bw. Zaharan Mwenemti.
   Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Juliana Yassoda akiongea na mmoja wa wachezaji wa Timu ya Taifa ya Paralympic Bw. Ignas Madumla wakati wa makabidhiano ya Vifaa vya michezo kwa ajili ya kwenda nchini Congo Brazaville kwenye mashindano ya Afrika (All African Games).
  Picha na Benjamin Sawe-WHVUM.

  0 0


  Je umekwama kifedha?,Hujui wapi pa kwenda? Je unahitaji kutimiza ndoto na malengo yako? usihangaike
  Kampuni ya mikopo ya wezesha mzawa microfinance ltd inatoa mikopo kwa wajasiriamali wa kati na wafanyakazi wa sekta zote ikiwemo biashara,viwanda na ufugaji.

  Kiwango cha mkopo kinaanzia 500,000/= hadi 50,000,000/=
  Mkopo unatolewa ndani ya masaa 24.  Sifa za mkopaji.
  .uwe ni mtanzania mwenye umri usiopungua miaka 18
  .uwe n uzoefu wa biashara usiopungua
  .uwe na namba ya utambulisho wa kodi (TIN)
  .Uwe na mkataba wa kazi (kwa mfanyakazi)
  .Uwe umeajiriwa na kampuni inayotambulika na kusajiriwa na serikali(kwa mfanyakazi)
  Ofisi zetu zipo Bamaga ,jengo la Global publishers.Tupigie kwa simu namba
  0715 620824  Nyote mnakaribishwa.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Viongozi wa Kamati ya Kudumu ya  Umoja wa Afrika( AU) wakati alipokuwa akiwasili kwenye Hoteli ya Mount Meru Jijini Arusha kwa ajili ya kufungua Mkutano wa Mashauriano kati ya Wawakilishi wa  Kamati ya Kudumu ya  Umoja wa Afrika( AU) na Wataalamu wa Masuala ya Haki na Sheria, uliofanyika kwenye Hoteli hiyo uliokuwa ukijadili kuhusu  kuimarisha demokrasi,  utawala wa sheria na masuala ya uchaguzi. Wa tatu (kulia) ni Jaji Mkuu Mstaafu  Agustino Ramadhan. Picha na OMR
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua Mkutano wa Mashauriano kati ya Wawakilishi wa  Kamati ya Kudumu ya  Umoja wa Afrika( AU) na Wataalamu wa Masuala ya Haki na Sheria, uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha jana Sept 2, 2015 ambao ulikuwa ukijadili kuhusu  kuimarisha demokrasi,  utawala wa sheria na masuala ya uchaguzi.   Baadhi ya washiriki wa Mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akihutubia. 
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kulia) akiteta jambo na Rais wa Mahakama ya Afrika, Jaji Mkuu Mstaafu, Agustino Ramadhan, wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo wa Mashauriano kati ya Wawakilishi wa  Kamati ya Kudumu ya  Umoja wa Afrika( AU) na Wataalamu wa Masuala ya Haki na Sheria, uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha jana Sept 2, 2015 ambao ulikuwa ukijadili kuhusu  kuimarisha demokrasi,  utawala wa sheria na masuala ya uchaguzi.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kulia) akikabidhiwa zawadi na Rais wa Mahakama Afrika Jaji Mkuu Mstaafu, Agustino Ramadhan, wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo wa Mashauriano kati ya Wawakilishi wa  Kamati ya Kudumu ya  Umoja wa Afrika( AU) na Wataalamu wa Masuala ya Haki na Sheria, uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha jana Sept 2, 2015 ambao ulikuwa ukijadili kuhusu  kuimarisha demokrasi,  utawala wa sheria na masuala ya uchaguzi. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Rais wa Mahakama ya Afrika, Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Agustino Ramadhan, wakisalimiana na baadhi ya washiriki wa mkutano huo baada ya kufunguliwa rasmi jana jijini Arusha. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Mahakama Afrika, Jaji Mkuu Mstaafu, Agustino Ramadhan, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano huo kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika baada ya ufunguzi jana jijini Arusha. Picha na OMR

  0 0

   Clerk of the National Assembly of Tanzania Dr. Thomas Kashilillah shares experience with the delegation of the leaders of the Southern Africa Development Community –Parliamentary Forum (SADC-PF) when it paid him a courtesy in his Office today. The delegation of five members led by the SADC-PF Secretary General Dr. Esau Chiviya arrived in the country on 22nd of August 2015 to carry out the pre-election observation towards the forth coming general election in Tanzania which is due next month.

              The pre-election observers are expecting to leave the country on 04th of  September 2015 after observing the preparedness level and the readiness of the     voters as they are eagerly waiting to elect their next government. While in the country, the delegation managed to meet with the National Electoral Commission team, (NEC),  Zanzibar Electoral Commission team, (ZEC), Political Parties forum, Media Council of Tanzania (MCT), MISA Tan,  and Association of     NGO,s (TANGO). The SADC-PF is widely renowned for setting benchmarks for free and fair elections.
    Southern Africa Development Community –Parliamentary Forum (SADC-PF)  Secretary General Dr. Esau Chiviya (left) and the Programme Manager for  Democracy and Good governance Mr. Sheuneni Kurasha also from SADC-PF keenly listening  to the Clerk of the National Assembly of Tanzania and the Regional Secretary of the Commonwealth Parliamentary Association-Africa Region  Dr. Thomas Kashillilah.

   

  Photos by Prosper Minja - Bunge

  0 0

  D3A_2835 MC's during the official opening of MultiChoice Africa Content Showcase Extravaganza, IK (right) and Eku at the Outrigger Beach Resort in Mauritius.(Photos by MultiChoice and Zainul Mzige of Modewjiblog).

  It was a magical night filled with #OnlyTheBest of African entertainment when MultiChoice Africa kicked off its second #OnlyTheBest Content Showcase Extravaganza in spectacular style at the Outrigger Resort. 

  The star-studded guestlist read like the who's who of Africa's entertainment and media.
  The guests walked down the African media Walk of Fame onto a red-carpet that opened up to a sensational night of dazzling entertainment. 

  The event, dubbed 'Night of a Thousand Stars' saw all the glitz and glamour of Hollywood, Bollywood and Nollywood come to life on the island paradise, as guests that include Genevieve Nnaji, Rita Dominic, Desmond Elliot and Ramsey Nuoah were given the full movie-star treatment. Flavour, Stonebwoy and The Mavins kept the guests on their feet with their popular hits while the night's MCs IK and Eku kept the glamorous proceedings running smoothly.

  Guest also experienced host IK who also brought his popular show, 'High Lites with IK', to the stage in Mauritius with a delightful interview with Nigerian crooner Banky W alongside music by DJ Sousa.
  D3B_6272 Red carpet treatment for the guest #OnlyTheBest.
  MultiChoice Africa's CEO Tim Jacobs also took to the stage to welcome guests with a promise that the video entertainment service provider will do all it can to make only the best content available to its subscribers on any platform, on any device and at any time.

  “We believe television is an extremely powerful tool that can educate, entertain and inform. The evolution of this medium has become fast and furious and as a business we are constantly evolving to stay ahead,” said Jacobs at a glittering ‘Night of a Thousand Stars’ event.

   “MultiChoice’s business is built around three key pillars: people; content - in the form of great entertainment, news and sport - and the latest cutting-edge technology. 

  Our mission is to ensure that our subscribers do not miss out on any of the stories, events or moments that are shaping our future.”

  Jacobs lauded the success of MultiChoice’s GOtv DTT (Digital Terrestrial Television) offering, which currently operates in 8 countries, bringing low-cost digital television to homes and supporting governments in freeing up vital broadcast spectrum by switching from analogue to digital signal.

  He also acknowledged the challenges which the business faces. “Our growth over the last 20 years has been a result of massive investments we have made in people, content and technology – but as with any business, not all of these investments or changes have hit the spot…. so we have from time to time re-evaluated our position and made changes to our strategies. At the end of the day however it is really our subscribers we have to thank for staying with us, trusting us to deliver the best television experience and customer service to make their experience world class,” said Jacobs.
  D3B_6293 M-Net Regional Director West Africa, Wangi Mba-Uzoukwu (right) and Eku the MC flanked by another guest.

  M-Net Regional Director West Africa, Wangi Mba-Uzoukwu, reminded guests that M-Net has a near 30-year history on the continent, where it started with a daily 12-hour broadcast on a single channel. Now, having changed the way television is viewed across the continent, the broadcaster leads the way in producing, acquiring and showcasing the best entertainment content in Africa. 

  “Our first broadcast in 1986 led to other firsts like the launch of SuperSport and the Mzansi Magic, Zambezi Magic, Jango Magic and Africa Magic channels; and with the creation of exciting, genre-defining and iconic content like Carte Blanche and Tinsel, M-Net continues to shape cultures, build bridges and empower talent across Africa even as we remain synonymous with all things entertainment on the continent,” said Mba-Uzoukwu.

  She echoed Jacobs’ sentiments about the need for constant evolution, to stay ahead of the video entertainment service provision field. “We are launching and redefining channels and we continue to expand our content offerings to viewers across the continent. Our ongoing and significant investments in local productions have positioned Africa on the entertainment global arena and with new technology we continue to reach even more people, ensuring that no one ever misses the M-Net Magic.

   Our investment drive remains geared not only towards the industries in which we play, but also in the people who power them,” said Mba-Uzoukwu.
  The MultiChoice Africa Content Showcase is a dynamic 5-day content extravaganza, which sees a host of DStv’s biggest channels, including Sony, SuperSport, Zee TV, A+E, Disney, MTV Base, BET, Comedy Central, BBC and M-Net previewing their latest and greatest content, soon to be seen across the video entertainment services provider’s platforms. To keep track of happenings at the MultiChoice Africa Content Showcase, follow@multichoice_africa on Instagram, @mcashowcase on Twitter, or via #OnlyTheBest.
  D3B_6334 Celebrities upon the arrival at Marquee where the event took place.
  D8A_0828
  The guests walked down the African media Walk of Fame.
  IMG_6403 Flags from different countries include Tanzania which participate at the MultiChoice Content Showcase Extravaganza in Mauritius.
  D3A_1719
  MultiChoice Africa's CEO, Tim Jacobs giving a welcoming note.


  IMG_6500 M-Net Regional Director West Africa, Wangi Mba-Uzoukwu speaking to the guests.
  D3A_2492
  IK welcoming Banky W on the stage.
  IMG_6470 Entertainment to the guests.
  IMG_6524D3B_7252IMG_6579IMG_6621IMG_6503 
  Nights of thousand stars #OnlyTheBest.
  D3B_7081
  Nigerian Artist, Mr. Flavour rocking the stage.
  IMG_6780Good times,OnlyTheBest: Nigerian actress and singer who won the Africa Movie Academy Award for Best Actress in a Leading Role in 2005, Genevieve Nnaji feeling Mr' Flavours tune along side Nigerian actor Ramsey Nouah who also won the Africa Movie Academy Award for Best Actor in a Leading Role in 2010.
  IMG_6783 Nigerian Celebrities having good times at the MultiChoice Showcase Content Extravaganza in Mauritius.
  IMG_6785 Sing along with Mr. Flavour (not in picture) during his performance.
  IMG_6738 Banky W, Rita Dominic, Desmond Elliot, Ramsey Nouah, and Genevieve Nnaji.
  IMG_6739 Feeling the music....!
  IMG_6786 It's unforgettable night. #OnlyTheBest
  IMG_6875 Donjazzy, Prince Mavin, Tiwa Savage Korede Bello, Aphro DIJA, Reekado Banks and Dr. SID performing DOR rmx.
  D3B_7367
  IMG_6933 Genevieve Nnaji in a jovial mood.
  IMG_6934 Ramsey Nouah and Genevieve Nnaji chatting.
  IMG_6891 MC's IK and Eku introduce the dancers.
  IMG_6953 
  M-Net Regional Director West Africa, Wangi Mba-Uzoukwu (third right) poses for a photo with Nigerian Celebrities.
  IMG_6972
  Terry Mapurisana from ZBC News (left) with Nigerian Artist, Banky W.
  IMG_6334 
  Paul Owere from The Citizen News Paper and IK taking a selfie.
  IMG_6364 Lorraine Lusinje from Times Group in Malawi taking a selfie with IK.
  IMG_6966 
  Public Relations Officer, MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi poses for a photo with Nigerian Actress, Genevieve Nnaji.
  IMG_6343 Catching up on a few issues; Public Relations Officer, MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi (left), General Manager Corporate Affairs, MultiChoice Africa, Caroline Creasy (right) and centre is Masembe Tambwe from Daily News Paper from Tanzania.
  IMG_6340 From left: Public Relations Officer, MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi, General Manager Corporate Affairs, MultiChoice Africa, Caroline Creasy and Paul Owere from The Citizen News Paper poses for a photo during the official opening of MultiChoice Africa Content Showcase Extravaganza in Mauritius.
  IMG_6971 

  Public Relations Officer-MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi chatting with the Nigerian Artist, Banky W after the official opening of MCA Content Showcase in Mauritius.

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI

   WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

  JESHI LA POLISI TANZANIA.

   
          “PRESS RELEASE” TAREHE 03.09.2015.

  ·         MTU MMOJA AFARIKI BAADA YA KUGONGWA NA GARI WILAYA YA MBARALI.


  ·         MPANDA BAISKELI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI WILAYA YA MBOZI.


  ·         WATU SITA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA BAADA YA KUFANYIKA OPERESHENI.

  KATIKA TUKIO LA KWANZA:

  MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BOKA KASULA (50) MKAZI WA SONYANGA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI YENYE NAMBA ZA USAJILI ALP 3965 AINA YA SCANIA BASI MALI YA KAMPUNI YA WADACHOVU ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA DEREVA ERNEST CLEMENCE (42) MKAZI WA ILOMBA IKITOKEA DSM KUELEKEA MALAWI.


  AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 02.09.2015 MAJIRA YA SAA 23:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA SONYANGA, KATA YA MAHONGOLE, TARAFA YA ILONGO, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/NJOMBE.

  MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KITUO CHA AFYA IGURUSI. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI, DEREVA AMEKAMATWA. UPELELEZI UNAENDELEA.


  KATIKA TUKIO LA PILI:

   MPANDA BAISKELI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA THADEO MWASHILANGA (21) MKAZI WA ICHENJEZYA WILAYA YA MBOZI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI ISIYOFAHAMIKA.


  AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 02.09.2015 MAJIRA YA SAA 06:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI CHA ILOLO, KATA YA MLOWO, TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/TUNDUMA.


  MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA WILAYA YA MBOZI. CHANZO NI MWENDO KASI NA DEREVA ALIKIMBIA NA GARI BAADA YA TUKIO. UPELELEZI UNAENDELEA.


  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.


  TAARIFA ZA MISAKO:

  MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA AIDAN JOHN (32) MKAZI WA UYOLE-MBEYA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI UZITO WA GRAM 25.


  MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA OPERESHENI ILIYOFANYIKA MNAMO TAREHE 02.09.2015 MAJIRA YA SAA 15:30 JIONI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA KAMFICHENI, KIJIJI NA KATA YA MKWAJUNI, MKWAJUNI, TARAFA YA KWIMBA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.


  KATIKA OPERESHENI ILIYOFANYIKA MNAMO TAREHE 02.09.2015 MAJIRA YA SAA 12:00 MCHANA HUKO ENEO LA MATENKI, KATA YA NJISI, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA, MTU MMOJA AITWAYE MWINUKA NGONYA (30) MKAZI WA MATENKI  AKIWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI AINA YA RIDDER BOKSI 08 NA CHARGER BOKSI 2.


  AIDHA KATIKA OPERESHENI ILIYOFANYIKA WILAYANI CHUNYA MNAMO TAREHE 02.09.2015 MAJIRA YA SAA 15:30 JIONI HUKO KATIKA KIJIJI CHA MATUNDASI [B], KATA YA MATUNDASI, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA, WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA GEORGE SAWELA (44) MKAZI WA MATUNDASI NA GILBERT SILWANI (43) MKAZI WA MATUNDASI WAKIWA NA MILIPUKO BARUTI 136 PINI ZA MILIPUKO 35, COTEX MITA 70 NA DOTNETOR 2 BILA KIBALI.


  TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHUMIWA MARA BAADA YA UPELELEZI KUKAMILIKA ZINAENDELEA.


  Imetolewa na:

  [AHMED Z. MSANGI – SACP]

  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

  0 0

  Maandalizi ya mchezo kati ya Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya Nigeria (Super Eagles) yamekamilika, ambapo leo Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo huo wa jumamosi kati huku kiingilio cha chini kabisa kikiwa shilingi elfu saba tu.
  Viingilio vya mchezo huo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON Qaulifier 2017) kundi G itakua ni VIP A Tsh 40,000, VIP B Tsh 30,000, VIP C Tsh15,000, Rangi ya Machungwa (Orange) Tsh 10,000, na viti vya rangi ya Bluu na Kijani Tsh 7,000.
  Tiketi za mchezo huo zinatarajiwa kuanza kuuzwa kesho siku ya ijumaa saa 4 kamili asubuhi katika vituo kumi vifuatavyo:
  (i) Ofisi za TFF - Karume
  (ii) Buguruni – Oilcom
  (iii) Mbagala – Dar live
  (iv) Ubungo – Oilcom
  (v) Makumbusho – Stendi
  (vi) Uwanja wa Taifa
  (vii) Mwenge – Stendi
  (viii) Kivukoni-  Feri
  (ix) Posta – Luther House
  (x) Big Bon – Msimbazi Kariakooo
  TFF inawaomba watanzania, wapenzi na wadau wa mpira wa miguu kununua tiketi za mchezo huo katika magari yaliyopo kwenye vituo vilivyotajwa ili kuondokana na tatizo la kuuziwa tiketi zisizokuwa halali.
  Jeshi la Polisi nchini kwa kushirikiana na idara nyingine za kiusalama wameandaa usalama wa kutosha katika kuelekea kwenye mchezo na kuhakikisha kila mpenzi wa mpira wa miguu anaingia kushuhudia mchezo huo salama na kuondoka salama.
  Mchezo huo utaanza saa 10:30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki utachezeshwa na waamuzi kutoka nchini Rwanda ambao wanatarajiwa kuwasili leo jioni pamoja na kamisaa wa mchezo huo.
  Waamuzi wa mchezo huo ni Louis Hakizimana (mwamuzi wa kati) Honore Simba (mwamuzi msaidizi), Jean Bosco Niyitegeka (mwamuzi msaidizi), Abdoul Karim Twagiramukiza (mwamuzi wa akiba) wote kutoka Rwanda na kamisaaa ni Charles Kasembe kutoka nchini Uganda.

  0 0

  Wachezaji watatu wa kimataifa wa Tanzania wanacheza soka la kulipwa nje ya nchi, Mrisho Ngasa (Free State – Afrika Kusini) Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta (TP Mazembe – Congo DRC) wamejiunga na kambi ya Taifa Stars iliyopo katika hoteli ya Urban Rose – Kisutu jana jijini Dar es salaam.
  Kocha Mkuu wa Taifa Stars Charels Mkwasa amewapokea wachezaji hao na jana kufanya mazoezi pamoja na wachezaji waliokuwa kambini nchini Uturuki saa 10 jioni katika uwanja Taifa jijini Dar salaam.
  Kwa mujibu wa ratiba ya kocha Mkwasa Stars leo alhamis itaendelea na mazoezi jioni saa 10 katika uwanja wa Taifa kabla ya kufanya mazoezi mepesi ya mwisho kesho ijumaa asubuhi.
  Wachezaji waliopo kambini ni magolikipa Ally Mustafa, Said Mohamed, walinzi Juma Abdul, Shomari Kapombe, Haji Mwinyi, Mohamed Hussein, Kelvin Yondani, Hassan Isihaka na nahodha Nadri Haroub “Cannavaro”.
  Viungo ni Himid Mao, Frank Domayo, Mudathir Yahya, Said Ndemla, Salum Telela, Deus Kaseke, Saimon Msuva na Farid Musa, huku safu ya ushambuliaji ikiwa na John Bocco, Rashid Mandawa, Ibrahim Ajib, Thomas Ulimwengu, Mrisho Ngasa na Mbwana Samatta.

  0 0

  Maelezo ya Picha zikimuonesha Mgombea Urais Kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Dkt. John Pombe Magufuli akiendesha Mtambo maalum unao changanya Saruji, Kokoto na Udongo(Pulverizer or Rotary Mixer) katika ujenzi wa Barabara ya Kutoka Tunduru kwenda Mangaka katika eneo la Kilimasera-Matemanga km 68.2. 

  0 0

  Kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tamasha la Amani, Alex Msama.

  Na Mwandishi Wetu
  KAMATI ya Maandalizi ya Tamasha la Amani, imesema inapata wakati mgumu kuhusiana na idadi ya waimbaji ambao wanaomba kushiriki tamasha hilo litakalofanyika Oktoba 4, mwaka huu.
   
  Mwenyekiti wa kamati hiyo, Alex Msama amesema wiki hii kuwa idadi ya wanaoomba washiriki tamasha hilo imekuwa kubwa kuliko kawaida, ambapo hadi juzi walikuwa waombaji wamefikia 74.
   
  “Tunapata maombi mengi, tunajitahidi kadri ya uwezo wetu kujipanga ili kuweza kila mmoja ashiriki, lakini tuna vigezo ambavyo tunaviangalia kwanza,” alisema.
   
  Msama amesema tamasha hilo pia litashirikisha waimbaji wa nyimbo za Injili kutoka nchi kadhaa za Afrika ikiwa ni pamoja na Kenya, Uganda, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Afrika Kusini na Zambia.


  "Waimbaji wengi maarufu wa muziki wa injili watakuwepo, tumejipanga vizuri kuhakiksha tamasha hili linakuwa gumzo kila mahali.

  "Wapendwa wajiandae kushiriki kwa wingi kwani watashiba kiroho kwa vile kutakuwa na waimbaji wengi wenye hamasa ya kiroho," alisema Msama.

  Msama amesema lengo la kuwajumuisha wasanii hao ni kutaka kulifanya tamasha hilo lenye lengo la kuombea amani liwe bora na lenye tija kwa Taifa.

  0 0

   Ofisa Habari wa Kituo cha Redio cha EFM, Samira Sadiq (kushoto), akizungumza na wanahabari (hawapo pichani), kabla ya kumkaribisha Meneja wa Mawasiliano wa redio hiyo kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu tamasha la muziki mnene bar kwa bar litakaloanza kesho kutwa Jumamosi, Agosti 5, 2015 Mkuranga mkoani Pwani. Kulia ni Meneja Usambazaji na Mauzo wa Kampuni ya Simu ya Smart, Haidari Chamshama na katikati ni Meneja wa Mawasiliano wa EFM Redio, Denis Ssebo. Kampuni ya simu ya Smart wamedhamini tamasha hilo.
   Meneja wa Mawasiliano wa EFM Redio, Denis Ssebo (kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Meneja Usambazaji na Mauzo wa Kampuni ya Simu ya Smart, Haidari Chamshama.
   Meneja Usambazaji na Mauzo wa Kampuni ya Simu ya Smart, Haidari Chamshama (kulia), akizungumza kwenye mkutano huo.
   Mkutano na wanahabari ukiendelea.


   Meneja wa Mawasiliano wa EFM Redio, Denis Ssebo (kushoto), na Meneja Usambazaji na Mauzo wa Kampuni ya Simu ya Smart, Haidari Chamshama, wakiwaonesha moja ya jezi zilizotolewa na kampuni hiyo kwa ajili ya tamasha hilo.
  Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo kuchukua taarifa hiyo.


   Dotto Mwaibale

  TAMASHA la Muziki Mnene Baa kwa Baa linatarajia kuanza kufanyika jumamosi ya Septemba 5, mwaka huu, wilayani Mkuranga mkoani Pwani.

  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, Meneja wa Mawasiliano wa Kituo cha Redio cha EFM, Denis Ssebo alisema kuanza kwa tamasha hilo kesho ni baada ya kumalizika kwa Tamasha la musiku mnene Mtaa kwa Mtaa awamu ya kwanza, (Muziki mnene bango) ambapo mashabiki na wasikilizaji wengi wa EFM wameweza kujishindia zawadi kabambe, Sasa ni zamu ya wapenzi wa burudani na mambo ya party.


  Ssebo amesema Muziki mnene bar kwa bar ni tukio ambalo lina wakutanisha wasikilizaji na mashabiki wa EFM na wakali wa EFM kutoka wilaya za kinondoni, Ilala na Temeke katika mkoa wa Dar er Salaam, na sasa wameamua kuupekea katika mkoa wa Pwani.

  Ametaja maeneo ambayo wanatakiwa kukaa tayari  kwa Muziki mnene bar kwa bar utakaoporomoshwa  na Rdjs wakali wa Efm, ni pamoja na Kibaha, Mlandizi, Mkuranga, Bagamoyo, Kisarawe,  

  Kigamboni na maeneo mengine mengi kwa ajili ya kuhakikisha tunakonga nyoyo za mashabiki wetu.

  Ameongeza kuwa Muziki Mnene bar kwa bar mwaka huu utaanza rasmi kesho jumamosi Mkuranga ambako mbali na kutoa Burudani, wataanza na mchezo wa mpira ili kuwapa nafasi wale wasio na uwezo wa kujumuika nasi tuonane nao mchana. 


  Ssebo amesema  mwishoni watafanya Tamasha kubwa la hitimisho ambalo litafanyika jijini Dar es salaam ambalo safari hii limeboreshwa na kuongezwa vionjo vingi sana.


  “Ninawaomba wasikilizaji wetu wakae mkao wa kula maana 

  tutawafikia na kuwamiminia burudani ambayo pia itarushwa live 
  kutoka eneo husika kupitia kituo chao cha 93.7 EFM. Njoo 
  tuonane, tufahamiane na tuijenge Radio yetu efm ambayo kwetu 
  Muziki unaongea”. 

  Muziki mnene awamu hii  umedhaminiwa na kampuni ya simu mpya kabisa hapa Tanzania ya Smart, kampuni ambayo  huduma zake ni za gharama ndogo zaidi, kwa hiyo mwaka huu Smart watakuwa na sisi katika kuupeleka  Muziki Mnene bar kwa bar kwa mashabiki wa EFM. 
  (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

  SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Dunia itakuwa mwenyeji wa Mkutano wa Takwimu Huria Kanda ya Afrika.


  Mkutano huo utakaofunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete utafanyika tarehe 4 – 5 Septemba, 2015 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.  Kauli Mbiu ni “Tumia Takwimu Huria  Kuendeleza Afrika” (Developing Africa Through Open Data).


  Washiriki takribani 400 kutoka Serikalini, Asasi za Kiraia, Sekta Binafsi, Taasisi za Elimu ya Juu na Washirika wa Maendeleo kutoka ndani na nje ya Nchi wanatarajiwa kushiriki.  

  Miongoni mwa washiriki kutoka Serikalini ni pamoja na Wakurugenzi kutoka Idara za Sera na Mipango, Wakuu wa Vitengo vya TEHAMA na Maofisa Takwimu Waandamizi wa Wizara zote.


  Mkutano wa Takwimu Huria kwa Kanda ya Afrika ni wa kwanza wa aina yake  Barani Afrika Tanzania ikiwa nchi ya kwanza kuwa mwenyeji.  

  Heshima hiyo imetokana na Tanzania kujiunga na Mpango wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa Uwazi (Open Government Partnership – OGP) unaolenga kuifanya Serikali kuwa wazi zaidi na hivyo kuleta uadilifu na uwajibikaji katika kuwahudumia Wananchi. 

  Katika utekelezaji wa Mpango wa OGP, Tanzania iliweka kipaumbele katika kuanzisha Tovuti ya Takwimu Huria itakayoweka wazi takwimu mbalimbali za Serikali na Taasisi zake.


  Madhumuni ya Mkutano ni kujadiliana kuhusu mfumo wa Takwimu Huria na jinsi utakavyoleta maendeleo hususan kwa nchi za Afrika. 


  Mkutano utawawezesha wadau kujadiliana na kubadilishana uzoefu kuhusu mfumo wa Takwimu Huria na kuona jinsi gani Sera za nchi zenye mfumo huo zinavyofanya kazi na kusimamia viwango vya upatikanaji wa Takwimu Huria.


  Aidha, Mkutano huo utaihusisha sekta binafsi na wadau wengine katika matumizi ya Takwimu Huria katika kuleta maendeleo ya kasi zaidi Barani Afrika.


  Washiriki watajadili jinsi ya kukuza na kuimarisha matumizi ya Mfumo wa Takwimu Huria katika kutoa huduma kwa wananchi hasa katika sekta ya Huduma za Jamii za elimu, afya, maji na kilimo.


  Tunaomba ushirikiano wenu ili Mkutano huu ufanyike na kukamilika kwa ufanisi.


  Imetolewa na Ofisi ya Rais, Ikulu

  0 0


  0 0
 • 09/03/15--05:37: MAALIM SEIF AREJESHA FOMU
 •  Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akikabidhi fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Bw. Jesha Salim Jecha huko hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar
  Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Bw. Jesha Salim Jecha akionesha fomu za kugombea Urais wa Zanzibar, baada ya kukabidhiwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, huko hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar. (Picha na Salmin Said, OMKR)

  Na: Hassan Hamad (OMKR)
  Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, leo amerejesha fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar katika Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC).

  Maalim Seif amerejesha fomu hizo majira ya saa nne asubuhi katika ofisi za tume hiyo zilizoko Hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar, baada ya kukamilisha masharti yaliyowekwa na Tume hiyo.

  Miongoni mwa masharti hayo ni pamoja na kula kiapo mahakamani pamoja kuambatanisha shilingi milioni mbili, mambo ambayo ametayatekeleza.
  Baada ya kukabidhi fomu hizo kwa Mwenyekiti wa Tume hiyo Bw. Jecha Salim Jecha, Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, ameitaka tume hizo kufanya kazi kwa uhuru na uadilifu.
  Amesema kufanya hivyo kutapelekea kufanyika kwa uchaguzi wa amani, huru na wa haki, jambo ambalo litailetea sifa kubwa Zanzibar katika jamii ya kimataifa.

  Katika hafla hiyo, Maalim Seif ameambatana na baadhi ya viongozi wa Chama hicho wakiwemo Mgombea uwakilishi wa Jimbo la Malindi Mhe. Ismail Jussa Ladhu, Mgombea uwakilishi wa Jimbo  la Chukwani Mhe. Mansoor Yussuf Himid na Mratibu wa uchaguzi wa CUF Bw. Muhene Rashid.

  0 0

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe. Mizengo Pinda akizungumza katika hafla ya maadhimisho ya Miaka 50 ya Mahusiano ya Kidiplomasia kati ya Tanzania na Vietnam. Katika hotuba yake Mhe. Pinda alilishukuru Taifa la Vietnam kupitia Ubalozi wake nchini kwa kuendelea kuimarisha ushirikiano  na Tanzania katika nyanja mbalimbali zikiwemo za kiuchumi, biashara na kidiplomasia. Hafla hiyo ilifanyika katika Hotel ya Serena Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Septemba 2015.
  Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Vothanh Nam naye akizungumza katika hafla hiyo.
  Afisa Mambo ya Nje Bw. Emmanuel Luangisa (katikati) akifuatilia hotuba kwenye kitabu iliyokuwa ikisomwa na Mhe. Waziri Mkuu (hayupo pichani) 
  Waziri Mkuu, Mhe. Pinda (kulia) na Balozi wa Vietnam nchini Mhe. Vothanh Nam (kushoto) wakitakiana afya njema  kwenye hafla hiyo. 
  Waziri Mkuu akitakiana afya njema na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Yahya Simba (wa pili kutoka kulia). Mwenye nguo nyekundu  ni Mke wa Balozi wa Vietnam nchini  na kulia ni Afisa kutoka  Ubalozi wa Vietnam nchini. 


  Mhe. Pinda akikata Keki pamoja na Balozi Nam ikiwa ni ishara ya kuadhimisha miaka 50 ya ushirikiano wa Kidiplomasia kati ya Tanzania na Vietnam. 
  Balozi wa Vietnam, Mhe. Nam (kulia) akimpokea Waziri Mkuu, Mhe. Pinda (kushoto) alipowasili kwenye maadhimisho hayo anayeshuhudia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje Balozi Yahya Simba
  Mhe. Pinda (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje, Bi. Mindi Kasiga.
  Waziri Mkuu, Mhe. Pinda akisalimiana na raia wa Vietnam waishio nchini waliojitokeza kumpokea alipowasili kwenye maadhimisho hayo.
  Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda (kulia) na Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Vothanh Nam (kushoto) wakiwa wamesimama kwa pamoja tayari kwa nyimbo za mataifa yao.
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Yahya Simba (wa pili kutoka kulia) kwa pamoja na Mke wa Balozi wa Vietnam nchini na Kiongozi wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini ambaye pia ni Balozi wa Demokrasia ya Kongo nchini Balozi Juma Mpango (kushoto) wakiwa wamesimama wakati nyimbo za taifa la Tanzania na Vietnam zikiimbwa. 
  Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini nao wakiwa wamesimama tayari kwa kuimba  nyimbo za Taifa
  Kikundi cha Polisi cha Brass Band kikipiga nyimbo za Mataifa hayo mawili wakati wa Maadhimisho hayo
  Sehemu ya wageni waalikwa kwenye maadhimisho hayo.
  Maafisa kutoka Wizara ya  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nao wakiwa na nyuso za furaha wakati wa maadhimisho hayo. 
  Picha na Reginald Philip

  0 0

  Mahmoud Ahmad Arusha
  WATANZANIA 500,000 wanatarajiwa kutembelea mbuga zote 16 za hifadhi za taifa mwaka huu ikiwa ni hatua ya kuimarisha na kukuza utalii wa ndani ambapo watajionea vivutio mbalimbali vilivyomo ndani ya hifadhi hizo.

  Hayo yameelezwa leo na Meneja uhusiano wa shirika la hifadhi za taifa, Tanapa, (Pichani)Pascol Shelutete, makao makuu ya TANAPA, jijini ,Arusha,  alipokuwa akizindua hatua ya mwisho ya  kampeni  maalumu ya miezi sita ya  kuhamasisha Watanzania kutembelea hifadhi  ili kujionea vivutio kwenye hifadhi wanazopakana nazo ili kuimarisha utalii wa ndani 

  Kampeni hiyo ni Makakati maalumu uliobuniwa na Tanapa,  unaotoa  hamasa kwa watanzania kutembelea mbuga za hifadhi zilizopo karibu na maeneo yao kwa gharama nafuu hasa siku za mwishoni mwa wiki na hivyo kuwapunguzia matumizi ya fedha wanazotumia kwenye starehe na badala yake wazitumie kutembelea hifadhi .

  Meneja uhusiano wa Tanapa,  Shelutete, amesema kuwa  kadiri miaka inavyozidi kusonga mbele mwamko wa watanzania kutembelea mbuga za hifadhi unaongezeka, ambapo mwaka 2013 watanzania 362,217, walitembelea hifadhi zote 16 nchini, na mwaka 2014 watanzania 427,258 wametembelea mbuga hizo .

  Amesema hatua ya mwisho ya uzinduzi wa kampeni hii inafanyika mkoani Arusha,ambao unapakana na mbuga za hifadhi za Arusha, Ziwa Manyara na Tarangire,na kampeni hiyo itadumu kwa muda wa miezi 6  na itahitimishwa Desemba mwaka huu.

  Kauli mbinu ya kampeni hiyo ni “Tembelea hifadhi uzwadike , akatoa wito kwa watanzania kubadili mitizamo kwa siku za mwishoni mwa wiki zitumike kwa ajili ya kutembelea hifadhi badala ya kuzitumia kwa ajili ya starehe ambazo zinatumia fedha nyingi.

  Uzinduzi huo umeshirikisha wakuu wa Idara za utalii wa hifadhi za Tarangire, Ziwa Manyara na hifadhi ya Arusha, pamoja na wadau ambao ni Chama cha waongoza utalii nchini TATO,ambao kwa pamoja wameelezea manufaa ya kutembelea hifadhi za taifa na sanjari kutatolewa zawadi mbalimbali kwa watanzania watakaotembelea hifadhi hizo.

  0 0

  Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu akipokea kadi kutoka kwa aliyekuwa mgombea wa udiwani wa Chadema Kata ya Mlowa Barabarani baada ya kujiunga na chama hicho. Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu akipokea kadi kutoka kwa aliyekuwa mgombea wa udiwani wa Chadema Kata ya Mlowa Barabarani baada ya kujiunga na chama hicho.Baadhi ya wanaCCM na wapenzi wa chama hicho wakiwa wamefurika katika mkutano wa hadhara ulofanyika Viwanja vya Chang'ombe mjini Dodoma. Baadhi ya wanaCCM na wapenzi wa chama hicho wakiwa wamefurika katika mkutano wa hadhara ulofanyika Viwanja vya Chang'ombe mjini Dodoma.Mgombea ubunge Jimbo la Mtera, Livingstone Lusinde akizungumza mkutano wa kampeni viwanja vya Chang'ombe Dodoma. Mgombea ubunge Jimbo la Mtera, Livingstone Lusinde akizungumza mkutano wa kampeni viwanja vya Chang'ombe Dodoma.
  Baadhi ya wanaCCM na wapenzi wa chama hicho wakiwa wamefurika katika mkutano wa hadhara ulofanyika Viwanja vya Chang'ombe mjini Dodoma.Baadhi ya wanaCCM na wapenzi wa chama hicho wakiwa wamefurika katika mkutano wa hadhara ulofanyika Viwanja vya Chang'ombe mjini Dodoma.Baadhi ya wanaCCM na wapenzi wa chama hicho wakiwa wamefurika katika mkutano wa hadhara ulofanyika Viwanja vya Chang'ombe mjini Dodoma.Baadhi ya wanaCCM na wapenzi wa chama hicho wakiwa wamefurika katika mkutano wa hadhara ulofanyika Viwanja vya Chang'ombe mjini DodomaBaadhi ya wanaCCM na wapenzi wa chama hicho wakiwa wamefurika katika mkutano wa hadhara ulofanyika Viwanja vya Chang'ombe mjini Dodoma.Baadhi ya wanaCCM na wapenzi wa chama hicho wakiwa wamefurika katika mkutano wa hadhara ulofanyika Viwanja vya Chang'ombe mjini Dodoma.Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu akiwasili na kuwapungia mkono wananchi katika viwanja vya jangani.Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu akiwasili na kuwapungia mkono wananchi katika viwanja vya jangani

  Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu viwanja vya chang'ombe. Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu viwanja vya chang'ombe.Bi. Samia Suluhu kulia akimtambulisha mgombea ubunge wa jimbo la Mtera, Livingstone Lusinde jimboni humo. Bi. Samia Suluhu kulia akimtambulisha mgombea ubunge wa jimbo la Mtera, Livingstone Lusinde jimboni humo.Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Jimbo la Kibakwe. Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Jimbo la Kibakwe.Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu (kulia) akiwatambulisha mgombea ubunge Jimbo la Kibakwe, George Simbachawene (katikati). Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu (kulia) akiwatambulisha mgombea ubunge Jimbo la Kibakwe, George Simbachawene (katikati).Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Jimbo la Kibakwe. Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Jimbo la KibakweAliyekuwa Katibu Mwenezi wa Chadema Wilaya ya Dodoma Mjini, Peter Chiuyo akizungumza mbele ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara ulofanyika Viwanja vya Chang'ombe mjini Dodoma. Aliyekuwa Katibu Mwenezi wa Chadema Wilaya ya Dodoma Mjini, Peter Chiuyo akizungumza mbele ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara ulofanyika Viwanja vya Chang'ombe mjini Dodoma.Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Jimbo la Kibakwe. Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia
  Suluhu Jimbo la Kibakwe.Baadhi ya wanaCCM na wapenzi wa chama hicho wakiwa wamefurika katika mkutano wa hadhara ulofanyika Viwanja vya Chang'ombe mjini Dodoma. Baadhi ya wanaCCM na wapenzi wa chama hicho wakiwa wamefurika katika mkutano wa hadhara ulofanyika Viwanja vya Chang'ombe mjini Dodoma.Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Jimbo la Mtera. Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Jimbo la Mtera.Meza kuu katika mkutano wa hadhra jimbo la Kibakwe.

older | 1 | .... | 627 | 628 | (Page 629) | 630 | 631 | .... | 1897 | newer