Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 625 | 626 | (Page 627) | 628 | 629 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Maafisa Waandamizi kutoka Mabunge ya Nchi za Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya Pamoja wakati wa Semina ya siku nne iliyowakutanisha kwa lengo la kubadilishana Uzoefu, Mjini Kampala - Uganda.
   Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Kimataifa kutoka Bunge la Tanzania Ndg. Jossey Mwakasyuka akifuatilia moja ya mada zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa warsha ya kubadilishana uwezo iliyowakutanisha Maafisa waandamizi kutoka Mabunge ya Nchi za Afrika Mashariki Mjini Kampala Uganda, jana.
   Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Kimataifa kutoka Bunge la Tanzania Ndg. Jossey Mwakasyuka akifuatilia moja ya mada zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa warsha ya kubadilishana uwezo iliyowakutanisha Maafisa waandamizi kutoka Mabunge ya Nchi za Afrika Mashariki Mjini Kampala Uganda, jana.


   Afisa Habari wa Bunge Owen Mwandumbya na Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya Elimu kwa Umma Bi. Neema Kiula nao wakifuatilia moja ya mada zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa warsha ya kubadilishana uwezo iliyowakutanisha Maafisa waandamizi kutoka Mabunge ya Nchi za Afrika Mashariki Mjini Kampala Uganda, jana
   Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Kimataifa kutoka Bunge la Tanzania Ndg. Jossey Mwakasyuka akiongoza mojawapo ya mijadala  wakati wa warsha ya kubadilishana uwezo iliyowakutanisha Maafisa waandamizi kutoka Mabunge ya Nchi za Afrika Mashariki Mjini Kampala Uganda, jana. Kushoto kwake ni mwakilishi kutoka Bunge la Rwanda

  0 0

   Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikhe Saleh Omar Kabii wakwanza kushoto akitoa maelezo juu ya haki za binaadamu  kwa mujibu wa Uislam wakati alipokuwa akifunguwa Mafunzo ya Haki za Binaadamu na kuwatambulisha wasaidizi wa Sheria kwa Viongozi wa Dini, katikati ni Mkurugenzi Mtendaji Harusi Miraji na mwisho Jina Mwinyi Waziri Afisa Mipango wa Kituo cha Huduma na Sheria.(Picha na Miza Othman- Maelezo Zanzibar).
   Baadhi ya washiriki wakisikiliza kwa makini maelezo kwa Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekhe Saleh Omar Kabii hayupo pichani katika Mafunzo ya Haki za Binaadamu na kuwatambulisha wasaidizi wa Sheria kwa Viongozi wa Dini Mazsons Hotel Zanzibar.
  SheikheThabit Nooman Jongo Afisi ya Mufti Zanzibar akiwafahamisha jambo washiriki wa mafunzo ya Haki za Binaadamu katika Ukumbi wa Mazsons Hotel Zanzibar.
  Picha na Miza Othman-Maelezo Zanzibar).

  Na Miza Othman –Maelezo Zanzibar         01/09/2015.
  MASHEKHE  na Walimu wa Madrasa wametakiwa kuwashajihisha wananchi kutojiingiza katika makundi yanayoweza kuvunja amani kutokana na kufuatiwa  kipindi kigumu cha uchaguzi Mkuu ujao.

  Hayo yameelezwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar  Sheikhe Saleh Omar Kabii ambae ni Mgeni rasmini alipokuwa akifunguwa mafunzo ya Haki za Binaadamu yaliyofanyika katika ukumbi wa Mazsons Hotel ya Shangani Mjini Zanzibar.

  Amesema Masheikhe na Walimu hao ndio wasimamizi wakuu katika maeneo mbalimbali ikiwemo Miskitini, Madrasani na hata ndani ya Nyumba zao kwani kufanya hivyo ni kutokiuka sheria iliyopangwa katika Nchi yao.

  “ Tofauti za dini, jinsia, cheo na Kabila sio njia  za ukiukwaji wa Sheria ndani ya Nchi yetu bali ni kutii sheria kwani nijukumu la kila raia,alisema Shekh Saleh Omar Kabii”.


  Nae Shekh Thabit Nooman Jongo kutoka Afisi ya Mufti Zanzibar amewataka Walimu na Mashekhe wenzake kuwamstari wa mbele katika kusimamia juu ya ukumbusho huo kwani kufanya hivyo ni kutekelaza majukumu yao.

  Aidha amewataka Masheikhe na Walimu  hao kuchukuwa juhudi za hali ya juu na kutumia maneno ya hekima, busara na unyenyekevu ili waweze kufanikiwa malengo waliyokusudia.

  Hata hivyo amesema kuwa wakati wanapotoa hutuba zao ndani ya Misikiti na Madrasa ziwe ni zenye kujenga amani kwani kufanya hivyo ni kuzitii sheria zilizowekwa katika nchi yao.

  Washiriki wa mafunzo hayo wamesema watayafanyia kazi bila ya kinyongo na kuyafikisha katika maeneo yao kama walivyoagizwa na Viongozi wenzao.

  0 0

    Mkazi wa Baracuda, Tabata Gaston Arbogasti akizungumza na mshereheshaji wa kampeni ya Fanyakweli Kiwanjani Gadner Habash (kulia) kabla ya kukabidhiwa zawadi yake ya fulana na bia za bure katika hafla ya kuipongeza baa ya Baracuda iliyopo Tabata jijini Dar es salaam ambayo iliibuka mshindi wa wiki kwenye kampeni ya Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na bia ya Tusker. Kampeni hii inaendelea mikoani pia ambapo itawafikia wakazi wa; - Arusha, Mbeya, Mwanza, Moshi na Morogoro.
  Msimamizi wa Mauzo wa Kampuni ya bia ya Serengeti kanda ya Chanika Tesha Stanslaus (kulia) akikabidhi zawadi ya fulana kwa mkazi wa Chanika Abdul Wasaili (katikati) katika hafla ya kuipongeza baa ya Check point iliyopo Chanika jijini Dar es salaam mara baada ya baa hiyo kuibuka mshindi wa wiki kwenye kampeni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na bia ya Tusker. (Kushoto) ni mshereheshaji wa kampeni hiyo Gadner Habash.
   Mkazi wa Tabata Proper Maro (wa kwanza kulia) akipokea zawadi yake ya mfuko wenye fulana toka kwa balozi wa bia hiyo Veronica Mbilinyi (kushoto) wakati wa wa hafla ya kuipongeza baa ya Baracuda iliyopo Tabata jijini Dar es salaam ambapo promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani ilifunga kambi eneo hilo mwisho wa wiki iliyopita kuipongeza baa hiyo iliyoibuka mshindi wa wa shindano la Fanyakweli kiwanjani. (Katikati) ni Mshereheshaji wa promosheni hiyo na mtangazaji wa redio E-fm Gadner Habbash.


  Mpenzi wa bia ya Tusker Njau Dismas (Katikati) akizungumza na mshereheshaji wa kampeni ya Fanyakweli kiwanjani Gadner Habash (kulia) mara baada ya meza yake kufikiwa na zawadi ya bia za bure na fulana katika hafla ya kuipongeza baa ya Baracuda iliyopo Tabata jijini Dar es salaam ambayo iliibuka mshindi wa wiki kwenye kampeni ya Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na bia ya Tusker. (Kushoto) ni balozi wa bia hiyo Veronica Mbilinyi. Nia ya kampeni hiyo ni kuhamasisha baa mbalimbali za mitaa inayotuzunguka kufanya kweli wanapotoa huduma kwa wateja wao.  

  0 0

    Ofisa Mkuu wa Idara ya Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Keith Tukei (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo katika maduka ya Shoppers plaza Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.Wengine katika picha kushoto ni mteja wa kwanza kufika kupata huduma katika duka hilo Bw.Argylle Tsvakai na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Rosalynn Mworia.
   Mteja wa kwanza kufika katika duka jipya la Vodacom Tanzania Bw.Argylle Tsvakai (kulia) akiangalia moja ya simu zinazouzwa kwa bei nafuu katika duka hilo lililopo katika maduka ya Shoppers Plaza Mbezi Beach jijini Dar es Salaam baada ya kuzinduliwa rasmi na Afisa Mkuu wa Idara ya Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Keith Tukei (kushoto). Katikati ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Rosalynn Mworia.
  Ofisa Mkuu wa Idara ya Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Keith Tukei (kushoto) akimmiminia mvinyo kwenye glasi Bw.Argylle Tsvakai ambaye alikuwa ni mteja wa kwanza kufika kupata huduma katika duka jipya la kampuni hiyo  lililopo katika maduka ya Shoppers Plaza Mbezi Beach jijini Dar es Salaam baada ya kuzinduliwa rasmi leo. Anayeshuhudia katikati ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Rosalynn Mworia. 
   Baadhi ya waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wakimfanyia mahojiano Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia baada ya kuzinduliwa kwa duka jipya la kampuni hiyo lililopo katika maduka ya Shoppers Plaza Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
  Picha ya pamoja ya baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na wadau wao walioshiriki katika uzinduzi wa duka jipya la kampuni hiyo leo lililopo katika maduka ya Shoppers Plaza Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.  KATIKA  kuhakikisha wakazi wa vitongoji vya Mbezi Beach na maeneo jirani ya Tegeta, Kawe na Boko wanapata huduma kwa karibu,Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom leo imefungua duka jipya  la kisasa katika  eneo la Mbezi Beach kwenye maduka ya Shoppers Plaza.

  Mbezi Beach ni moja ya kitongoji maarufu katika jiji la Dar es Salaam ambacho kinakua kwa kasi kwa maendeleo na kuwa kivutio cha wawekezaji wengi kutokana na kuwa na idadi kubwa ya watu na shughuli mbalimbali za kibiashara ikiwemo maofisi,mahoteli pia ni njia kuu ya kuelekea katika mji wa kihistoria wa Bagamoyo.

  Duka hili jipya lenye mazingira rafiki kwa wateja litakuwa linatoa huduma mbalimbali kwa wateja wa Vodacom ikiwemo huduma  kwa mawakala wa M-pesa na uuzaji wa bidhaa  mbalimbali za Vodacom na litawawezesha wateja wa  Mbezi Beach na vitongoji vyake   wakiwemo wasafiri wanaoelekea na kutokea Bagamoyo  na wateja kutoka maeneo ya Kawe,Tegeta,  Goba na Mbezi juu.

  Mtandao wa Vodacom unaongoza  kwa kupatikana vizuri na umeenea sehemu zote katika wilaya ya Kinondoni.

  Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasliano wa Vodacom Tanzania, Rosalyn Mworia, alisema ufunguzi wa duka hili la kisasa  ni mwendelezo wa malengo ya Vodacom kuendeleza  kuboresha maisha murua kwa kila mtanzania kwa kupata huduma za kampuni hiyo zenye ubora na kuwafikia wateja kwa urahisi zaidi popote pale walipo ikiwemo huduma mpya  za kilimo klabu  na M-Pawa zinazolenga kuwawezesha kuwawezesha wananchi na kuwarahishia maisha.

  “Uzoefu na utafiti umetuonyesha kuwa wananchi wanataka ubora,kama mtandao unaoongoza nchini tumejizatiti kuhakikisha tunafanya ubunifu wa hali ya juu wa kiteknolojia ili kutumia mtandao wa simu kuboresha maisha ya wananchi ikiwemo kutoa huduma bora na ndio maana tunazidi kufungua maduka kama haya kwa ajili ya kuwasogezea karibu wananchi huduma bora,na ninawahakikishia kuwa popote wateja wetu walipo tutawafikia na tunawashukuru sana wateja wetu kwa kutuunga mkono na tunawakaribisha ambao hawajajiunga na familia ya Vodacom kujiunga na kupata huduma bora kwa gharama nafuu.”Alisema Mworia.
  Naye Mkazi wa Mbezi beach na Mteja wa kwanza kupata huduma katika duka hilo baada ya kuzinduliwa duka hilo aliipongeza hatua ya kusogezewa huduma karibu “Tunapongeza jitihada za kampuni hii inazozifanya katika kuwasogezea wateja wao huduma za mawasiliano karibu na makazi yetu kwani itatuwia rahisi kupata huduma kwa karibu badala ya kwenda mbali na huu ni uthibitisho kuwa hivi sasa jiji la Dar es Salaam linazidi kupanuka na huduma kuwafuata wananchi kwa karibu”.Alisema Bw.Argylle Tsvakai  mkazi wa Mbezi Beach.

  Vodacom ina mtandao wa maduka 87 na wakala mbalimbali wa kuuza bidhaa zake nchini na  duka lililofunguliwa leo ni la  88 kufunguliwa katika wilaya ya Kinondoni.

  0 0

   Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe ya Siku ya Wahandisi  Tanzania mwaka 2015 Prof. Bakari Mwinyiwiwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Wahandisi nchini itakayofanyika Septemba 3 mpaka 4 jijini Dar es salaam.Kulia ni Msajili wa Wahandisi nchini Tanzania Muhandisi Steven Mlote na kushoto ni Msajili msaidizi wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania (ERB) Muhandisi Benedict Mukama
  Msajili wa Wahandisi nchini Tanzania Muhandisi Steven Mlote (kulia) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Wahandisi  nchini yatakayofanyika Septemba 3 mpaka 4 mwaka huu.
  Picha na Aron Msigwa-MAELEZO.

  Na.Aron Msigwa - MAELEZO,1/9/2015.Dar es salaam.
  KATIBU Kiongozi Balozi Ombeni Sefue anatarajiwa kuwa mgeni rasmi  wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Wahandisi nchini Tanzania itakayofanyika  Septemba 3 hadi 4 jijini Dar es salaam.

  Akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya sherehe hiyo Prof.Bakari Mwinyiwiwa amesema Kuwa Jumuiya ya Wahandisi nchini Tanzania inafanya maadhimisho hayo kwa mara ya 13 toka kuzinduliwa kwake mwaka 2003 kuenzi mchango wa wahandisi  katika kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini Tanzania.

  Amesema maadhimisho ya mwaka huu yanalenga kuwawezesha waajiri na wahandisi wazalendo na watumiaji wa huduma za kihandisi kutambua uwezo wa wahandisi wazalendo na kampuni zao pia kuwahamasisha wanafunzi wa kitanzania wanaosomea fani hiyo ili waweze  kufanya vizuri katika masomo yao.

  Ameongeza kuwa maadhimisho ya mwaka huu yatajikita katika kuangalia masuala mbalimbali ya maendeleo hasa ujenzi wa miundombinu,Maendeleo ya viwanda, ukuzaji wa uwezo, na maendeleo ya shughuli za kilimo nchini Tanzani.

  Kwa upande wake Msajili wa Bodi ya Wahandisi nchini Muhandisi Steven Mlote ameeleza kuwa wakati wa maadhimisho hayo shughuli mbalimbali za kitaaluma zitafanyika ikiwemo majadiliano ya kina kuhusu shughuli za kihandisi nchini na miaka 15 ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025.

  Amesema wakati wa maadhimisho hayo kutakuwa na utambuzi na utoaji wa Tuzo na zawadi mbalimbali  kwa wahandisi na wahitimu wa Taasisi waliofanya vizuri zaidi katika mitihani yao mwaka 2014/2015 pamoja na wahandisi kurejea kiapo cha utii kwa taaluma yao.

  Ameongeza kuwa wakati wa maadhimisho hayo kutakuwa na maonesho ya kiufundi ya jumuiya za wahandisi wa Tanzania kutoka taasisi mbalimbali zikiwemo Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Taasisi ya Teknolojia ya Dar es salaam (DIT), Chuo Kikuu cha Uhandisi na Teknolojia St.Joseph na Chuo cha Ardhi (ARU).

  Jumuiya nyingine ni ile ya Makandarasi ,Kampuni za Ushauri wa kihandisi,Mashirika na makampuni ya kibiashara na taasisi za utafiti.

  0 0

  Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya ulinzi  na Usalama Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride rasmi liliandaliwa na vikosi mbalimbali wakati wa sherehe ya kuagewa rasmi na vyombo vya ulinzi na usalama iliyofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo.

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege Zanzibar Bw. Said Ndubugani, akimueleza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, juu ya hatua zinazochukuliwa na mamlaka hiyo katika kuimarisha viwanja vya ndege, alipofanya ziara ya kutembelea eneo hilo.
   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akitembelea maeneo mbali mbali ya uwanja wa ndege wa Zanzibar katika ziara yake ya kutembelea eneo hilo.
   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiangalia maendeleo ya ujenzi wa jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Zanzibar alipotembelea eneo hilo.


   Mratibu wa ujenzi wa jengo jipya la abiria (terminal 2) katika uwanja wa ndege wa Zanzibar Bw. Yasser De Costa akimueleza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, juu ya maendeleo ya ujenzi huo.
   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiangalia maendeleo ya ujenzi wa jengo jipya la abiria katika uwanja wa ndege wa Zanzibar alipotembelea eneo hilo.
   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiangalia baadhi ya bidhaa zinazopatikana ndani ya duka la uwanja wa ndege wa Zanzibar, na kutoa wito wa kuzitangaza bidhaa zinazozalishwa hapa nchini zikiwemo karafuu na vitu vya sanaa. na vitu vya sanaa.
   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiangalia baadhi ya bidhaa zinazopatikana ndani ya duka la uwanja wa ndege wa Zanzibar, na kutoa wito wa kuzitangaza bidhaa zinazozalishwa hapa nchini zikiwemo karafuu.
   Raia wa Syria Bw. Mark Bachayani (kushoto) akijinasibu kupiga picha na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa katika ziara ya kutembelea uwanja wa ndege wa Zanzibar.
   Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar Bw. Abdallah Juma, akimueleza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, juu ya hatua zinazochukuliwa na shirika hilo katika kuimarisha huduma wakati wa ziara yake ya kutembelea eneo hilo.
   Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar Bw. Abdallah Juma, akimueleza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, juu ya hatua zinazochukuliwa na shirika hilo katika kuimarisha huduma wakati wa ziara yake ya kutembelea eneo hilo.Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na watendaji wa Shirika la Bandari Zanzibar, wakati akihitimisha ziara yake ya kutembelea eneo hilo. (Picha na Salmin Said, OMKR)

  0 0

  FAMILIA ya marehemu mzee Japhet Mbaga, wa Dar es Salaam kwa masikitiko makubwa inatangaza vifo vya kaka zao wapendwa, MICHAEL NA JOHN JAPHET MBAGA, vilivyotokea hapa DSM siku ya jumapili na jumatatu.

  Mazishi yanatarajiwa kufanyika makaburi ya Kinondoni, siku ya alhamisi tarehe 3 Septemba, 2015 saa 10.00 jioni. 

  Ratiba ya kutoa heshima za mwisho itafanyika siku hiyo hiyo, saa 7.00 mchana nyumbani kwa Mary Rusimbi (Mkurugenzi Mkuu, WOMEN FUND TANZANIA) eneo la Tabata - shule, nyumba za TAZARA.

   Baadaye saa 9.00 Ibada ya kuwaaga wapendwa wetu itafanyika Kanisa la KKKT Kijitonyama.


  Marehemu MICHAEL NA JOHN JAPHET MBAGA ni kaka wa MARY RUSIMBI, HILLARY MBAGA, ROSE MSHANA (ROZELLA) NA STELLA MBAGA.  "Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake na lihimidiwe."

  0 0

  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.

  Na Anitha Jonas – MAELEZO.
  TUME ya Taifa ya Uchaguzi  nchini  imefuta rufaa 38 za wagombea nafasi za ubunge kati ya 54 zilizowasilishwa kupinga baadhi ya wagombea hao kwa kuwatuhumu kutotimiza vigezo mbalimbali na kusema wagombea hao wanaweza kuendelea na Kampeni majimboni mwao.

  Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Uchaguzi  Bw.Kailima Ramadhan kwenye mkutano na waandishi wa habari.
  Alisema kuwa baada ya Wakurugenzi wanaoshughulikia uchaguzi kuzipitia ,waligundua kuwa rufaa hizo waliziona hazina mantiki na kukosa ushahidi wa kutosha.

  “Wagombea waliokuwa wamewekewa pingamizi na kuenguliwa katika uchaguzi ni 16 na Tume imewarudisha wagombea 13 kati ya hao na waliobaki watatu ,Tume imeridhia maamuzi ya wasimamizi wa Uchaguzi”,alisema Bw.Ramadhani.

  Aliongeza kuwa Tume hiyo inaendelea kupitia rufaa za wabunge zilizobaki  kwa kushirikiana na wasimamizi wa uchaguzi  ili kupata vielelezo  vinavyohusika na pindi itakapokamilisha zoezi hilo itatoa  taarifa yake ikiwa ni pamoja na rufaa 198 za madiwani kutoka halimashauri mbalimbali nchini.

  Aidha  alisema kuwa Tume hiyo  itaendelea kusimamia haki na kufanya maamuzi ya kuzingatia sheria kwa wagombea wa vyama vyote vilivyoshiriki katika uchaguzi wa mwaka huu na kuwataka kuwa na imani na kazi inayofanywa na Tume katika rufaa hizo.

  Mbali na hayo Mkurugenzi  wa uchaguzi alisema kuwa  Tume inatarajia kuanza zoezi la uhakiki wa daftari la mpiga kura visiwani Zanzibar kuanzia tarehe keshokuwa (03/09/2015) ambapo zoezi hilo litadumu kwa muda wa siku saba.

  Akiongelea juu ya uhakiki wa taarifa za mpiga kura  aliyejiandikisha alisema unaweza kuhakiki taarifa zako kwa kupitia mtandao wa tume www.nec.go.tz au kwa  kupiga *152*00// katika simu na kupata taarifa zote.

  0 0

   Mshiriki wa mafunzo elekezi juu ya uingizaji wa takwimu za mashauri kwa njia ya kielectroniki (Judicial Stastical Dashboard System JSDS) kwa Makarani wa Mahakama Mkoa wa Dar Es Salaam, Bi. Tumaini Mwalioga akisisitiza neno wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo katika chuo cha LearnIt leo Jijini Dar Es Salaam.
   Mgeni rasmi Mhe. Solanus Nyimbi (aliyesimama mbele) akitoa nasaha kwa niaba ya Mtendaji Mkuu Mahakama kwa washiriki wa mafunzo maalum ya uingizaji wa takwimu za mashauri kwa njia ya kielectroniki kwa Makarani wa Mahakama Mkoa wa Dar Es Saalaam yanayofanyika katika chuo cha LearnIt Jijini Dar Es Salaam. Lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha Makarani waweze kufungua mashauri na kuyaingiza kwa njia ya kiielectroniki. Mpaka sasa mafunzo hayo tayari yameshatolewa kwa jumla ya Makarani 860. Kwa upande wa Dar es Salaam mafunzo haya yatatolewa kwa jumla ya Makarani 90.
  Kiongozi wa darasa akisoma risala fupi mbele ya mgeni rasmi kabla ya ufunguzi wa mafunzo hayo.
   Mgeni rasmi katika mafunzo maalum ya mfumo wa kuingiza taarifa ya mashauri (Judicial Stastical Dashboard System (JSDS)  Mhe.Solanus Nyimbi (walioketi katikati)  Mhe. Mustapha Sihani, Naibu Msajili Mwandamizi Kanda Kuu Dar es Salaam, Patricia Ngunguru, Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Mafunzo,  Mhe. Said Mkasiwa, Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Ilala, (kushoto) ni kwenye picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo

  0 0

  Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano Kampuni ya Tumbaku Tanzania na Kiwanda cha Kusindika Tumbaku (TTPL), Bw.Richard Sinamtwa (Kulia) akifafanua jambo kwa wadau wa tumbaku kutoka Zimbabwe walipotembelea kiwanda hicho kwa ziara ya mafunzo Mjini  Morogoro.
  Meneja Uhusiano wa Kiwanda cha Kusindika Tumbaku (TTPL), Bw. Mazehiew Folleto (Kulia) akifafanua jambo kwa wadau wa tumbaku kutoka Zimbabwe walipotembelea kiwanda hicho kwa ziara ya mafunzo Mjini  Morogoro.
  Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano Kampuni ya Tumbaku Tanzania (TLTC) na Kiwanda cha Kusindika Tumbaku (TTPL), Bw.Richard Sinamtwa (Kulia) akiwaongoza wageni kutoka Bodi ya Tumbaku na Masoko ya Zimbabwe walipotembelea kiwanda hicho kwa ziara ya mafunzo Mjini  Morogoro.
  Meneja Mapokezi wa Tumbaku kwenye Kiwanda cha Kusindika Tumbaku (TTPL), Bw.Nico Zambetakis akifafanua jambo kwa wadau wa tumbaku kutoka Zimbabwe walipotembelea kiwanda hicho kwa ziara ya mafunzo Mjini  Morogoro.

  0 0

  Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo, baada ya kukaa kimya kingi sana tangu mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia  Chama cha Demokrasia na Maendeleo  chini ya mwamvuli wa UKAWA, Edward Lowassa kuhamia chama hicho. Leo ameibuka na kusema  ya moyoni kuwa amejivua uanachama  rasmi wa chama cha Chadema pamoja na Ukatibu Mkuuu wa Chama cha hicho na kuaachana  kabisa na siasa  kutokana na mambo yaliyokuwayakifanyika ndani ya chama chake hayakumlidhisha na hakukubaliana nayo.

  Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa pia amesema kuwa mambo yaliyotokea katika chama chake ndio maana ameamua kuachana na siasa  rasmi hii leo.
   Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika harakati za kupata taswira nzuri za Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo.

  Baadhi ya wananchi pamoja na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari wakimsikiliza aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Dk.  Wilbroard Slaa leo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) inatarajiwa kuondoka nchini kesho usiku kuelekea nchini Congo-Brazzavile kwenye michuano ya Michezo ya Afrika (All Africa Games) inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 3, mwaka huu.
  Kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa TFF, Twiga Stars haikuondoka leo kuelekea nchini Congo – Brazzavile, Shirikisho bado linasubiri mwongozo wa Wizara ya Habari,Viajana, Utamaduni na Michezo.
  Imani ya TFF ni kuwa timu itasafiri na kuwahi mechi ili kuepuka hatari ya kuadhibiwa na CAF ikiwa ni pamoja nan a kulipishwa fainai au kuondolewa kwenye michuano hiyo.
  Mchezo wa kwanza wa Twiga Stars katika michuano hiyo  utakua dhidi ya Ivory Coast tarehe 6, Septemba, mchezo wa pili dhidi ya Nigeria Septemba 9 na mchezo wa mwisho katika kundi hilo utakua dhidi ya      Congo-Brazzavile Septemba 12, 2015.
  Timu mbili kutoka kundi A zitaungana na timu mbili nyingine kutoka kundi B kucheza hatua ya nusu fainali.

  0 0

   Katibu Mkuu wa  Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akizungumza siku ya Jumanne, wakati  Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipopitisha Azimio linalowasilisha kwa Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali  Malengo na Ajenda mpya za Maendeleo Endelevu ( Ajenda 2030)   Anaonekana pia Rais wa Baraza Kuu la 69, Bw. Sam Kutessa .
  Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  akiwa na Afisa Mkuu Siongelael Shilla wakati wa upitishaji wa Azimio  namba A/69/L.85   kuhusu Ajenda 2030  ambapo baada ya kupitishwa  kwa kauli moja azimio hilo wazungumzaji  wanaowakilisha  makundi ya kikanda walipata fursa ya kuelezea misimamo yao juu ya  baadhi ya   mambo ambayo walikuwa wakitofautiana kimtizamo na kimsimamo.

  Na Mwandishi Maalum,   New York

  AFRIKA,  imesisitiza  na kubainisha kwamba  itatekeleza malengo mapya ya maendeleo endelevu kwa  kuzingatia  maslahi, vipaumbele, sera,   mila na tamaduni ambazo nchi za Afrika  zimejiwekea.


  Aidha  Afrika inasema kuwa,  utekelezaji wa  malengo hayo    pia utazingatia  sheria za kimataifa  na ambazo nchi  za Afrika  zimeridhia na si vinginevyo.


   Hayo yameelezwa na  Balozi Fode Seek,  Mwakilishi wa Kudumu  wa Senegal katika Umoja wa Mataifa ambaye ni  Mwenyekiti wa    nchi za Afrika   kwa mwezi Septemba.


    Alikuwa  akizungumza  kwa  niaba ya  nchi   za Afrika wakati Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipokutana  siku ya jumanne, kupitisha Azimio namba A/69/L.85  ambalo linawasilisha  ajenda ya  Maendeleo Endelevu (ajenda 2030) itakayotekelezwa kwa miaka   15 ijayo.

  Ajenda 2030 inachukua nafasi ya   Malengo ya Maendeleo ya Millenia ( MDGs) yanayofikia ukingoni  mwishoni mwa  mwaka huu.


  Kupitishwa kwa  azimio hilo  la ajenda 2030, inayojumuisgha  malengo 17 na ambalo sasa litawasilishwa  baadaye mwezi huu wa Septemba   kwa Viongozi Wakuu wa  Nchi na Serikali tayari kwa kuridhiwa na  kuanza utekelezaji wake mwakani, kunakamilisha mchakato  uliodumu kwa  zaidi ya miaka miwili ya majadiliano yaliyozaa malengo mapya na ajenda mpya.

  “Afrika  itashirikiana na  wadau wa maendeleo katika utekelezaji wa malengo haya  yanayolenga  katika kuondoa umaskini, kuboresha huduma za jamii,  upatikanaji wa fursa za maendeleo na ajira  na bila ya  kumwacha yoyote nyuma. Lakini  tutatekeleza kwa kuzingatia  mipango yetu, vipaumbele vyetu, sera  zetu na kwa  maslahi ambayo  ambayo kila  nchi itaona inafaa  kutoka na mazingira na uwezo wa nchi  yenyewe” akasema Balozi. Seek


  Baadhi ya mambo ambayo Afrika inasema  kimsingi haikubaliani katika ujumla wake na ambayo kwayo utekelezaji wake utazingatia utashi wa kila nchi,   kuzingatia Imani za kidini,  mila na tamaduni na  sheria  za nchi husika ni pamoja na  tafsri sahihi ya neno familia ambalo  Afrika na baadhi ya  nchi nyingine  inasema  familia ni  Baba, Mama na  watoto na si  tafsili ile inayopigiwa chapuo na baadhi ya nchi za  magharibi.


  Jambo  jingine ambalo   Afrika na   Nchi nyingine   imetoa msimamo ,   linahusu tafsiri ya  jinsia ambayo kwa Afrika inaamini kwamba jinsia ni ya kike na kiume.


    Utolewaji   na upatikanaji wa   huduma za afya, elimu na mafunzo yanayoambatana na eneo hilo  na  hususani uzazi wa mpango, ni eneo jingine ambalo Afrika na mataifa mengine yanayoendelea  yanasisitizia kuwa utekelezaji wake usiwe wa shurutisho na ufanyike kwa kuzingatia mila na desturi za nchi husika.


  Mbali ya  msemaji huyo kwa niaba ya nchi za Afrika kuanisha baadhi ya maeneo ambayo  Afrika itayatekeleza  pasipo kushurutishwa.  Wazungumzaji   zaidi ya 30 wakiwakilisha  makundi ya  kikanda  na baadhi wakizungumza kwa niaba  ya nchi zao walichangia maoni yao   kuhusu ajenda 2030.


  Mwakilishi wa  Kudumu wa Afrika ya Kusini  Balozi Kingsley Mamabolo ambaye ni   Mwenyekiti wa  Kundi la G77& China. Akizungumza kwa niaba ya kundi hilo anasema.  

    Haikuwa kazi nyepesi   kufikia makubaliano    yaliyopelekea kupitishwa kwa kauli moja  Malengo   na Ajenda  2030

  “   Ajenda hii  ambayo tumeipitisha kwa kauli moja,  hatuwezi kusema kwamba haina mapungufu.  lakini tumefika hapa tulipo baada ya  majadilliano marefu na magumu na kukubaliana kuto kukubaliana”.


    Na   akaongeza  Ajenda 2030 ina mambo mengi yakiwamo malengo    17  na viashiria  169. Lakini jambo   moja la msingi na muhimu  ni kwamba, utekelezaji wake  utategemea  kila nchi inavyopanga vipaumbele vyake na sera zake” akasema Balozi Mamabolo.


  Awali akizungumza mara baada ya kupitishwa kwa Azimio hilo, Katibu  Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban   Ki   Moon,   amesema. Agenda 2030   ni makubaliano ambayo kila   nchi inapashwa kujivunia na kwamba utekelezaji wake utahitaji ushirikiano wa karibu baina ya wadau mbalimbali.

  Akasema   Agenda   2030 itapitishwa na Viongozi Wakuu wa   Nchi na Serikali kutoka  Mataifa mbalimbali duniani akiwamo Baba Mtakatifu Francis.  0 0

  Aliyekuwa Katibu wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa Frank Leonard (Kulia) akifungua mkutano mkuu wa IPC jana katika ukumbi wa Maktaba ya Iringa katikati ni Daud Mwangosi ambaye alikuwa ni mwenyekiti wa IPC akifikiri jambo.

  Aliyekuwa mwenyekiti wa IPC Daud Mwangosi (kushoto) akihojiwa na mzee wa matukio daima Bw Francis Godwin  ambaye alikuwa ni katibu msaidizi wa IPC juu ya wanahabari kudumisha umoja na mshikamano wakati wa uhai wake.

  Mwandishi wa habari wa Chanel Ten mkoa wa Iringa na Mwenyekiti wa cha chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Daud Mwangosi tarehe Kama ya leo miaka mitatu iliyopita aliuwawa  katika vurugu za Polisi  na wafuasi wa Chadema katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa .
  Mwanahabari huyo Daud Mwangosi aliuwawa majira ya saa 10 jioni katika ofisi za Chadema Nyololo huku askari mmoja akijeruhiwa vibaya kwa risasi .
  Kabla ya kuuwawa kwa mwanahabari huyo mabomu yaliweza kupigwa eneo hilo kuwatawanya wafuasi hao wa Chadema ambao walikuwa wakigoma kutawanyika eneo hilo na kuamua kukaa chini kuwa haapo tayari kuondoka katika ofisi yao.
  Chanzo cha mwanahabari Mwangosi kuuwawa kilitokana na kukamatwa kwa mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe mkoa wa Iringa Godfrey Mushi na hivyo mwanahabari huyo kkutaka kuhoji polisi sababu ya kukamatwa kwa mwanahabari huyo ndipo askari hao walipoanza kumshambulia kwa kichapo na baadae mlio kama wa bomu ulisikika eneo hilo na mwandishi huyo na askari mmoja waliaguka chini .
  Ndani ya dakika tano ilisikika sauti kutoka kwa askari huyo kuwa afande nimekufa ndipo walipomchukua na kumpeleka Hospitali ya wilaya ya Mufindi huku mwili wa mwanahabari huyo ukipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti .
  Katika vurugu hizo zilizodumu kwa takribani dakika 30 kwa askari na wafuasi wa Chadema kurushiana mawe kwa mabomu zaidi ya magari matano ya Chadema na ya wananchi yameharibiwa huku watu kadhaa wamejeruhiwa na mwanahabari mmoja Godfrey Mushi akijeruhiwa vibaya.
  Hii ni taarifa ya Jeshi la polisi kabla ya tukio kwa vyombo vya habari
  JESHI la polisi mkoa wa Iringa limesema limezuia mikutano ya vyama vya siasa kwa vyama vyote na sio kwa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) pekee hivyo laonya vyama vyote kutii sheria bila shuruti.
  Hata hivyo jeshi hilo la Polisi limesema kuwa halifanyi kazi kwa matakwa ya chama chochote cha siasa na kuwa si kweli kama wanavyodai viongozi wa Chadema kuwa jeshi la polisi linatumiwa na chama cha mapinduzi (CCM) kuzuia mikutano hiyo.
  Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Michael Kamuanda ametoa kauli hiyo leo ofisini kwake alipozungumza na waandisha wa habari kuhusu zuio la mkutano wa Chadema uliopangwa kuanza leo katika wilaya ya Mufindi.
  ” Nawatangazia wanasiasa na vyama vyote vya siasa pamoja na wananchi wa mkoa wa Iringa kuwa hakutakuwa na mikutano ya kisiasa kutokana na shughuli za sensa zinazoendelea ….hivyo basi nawaomba wananchi wote kutoshiriki mikutano yoyote ya kisiasa itakayoitishwa na wanasiasa “alisisitiza.


  Kuwa mikutano hiyo imezuiliwa kwa kipindi hiki cha sensa kilichoongezwa hadi hapo tamko litakapotolewa tena na msajili wa vyama vya siasa John Tendwa kama alivyokwisha kutoa tamko la kuzuia shughuli hizo za vyama vya siasa kwa kipindi hiki cha sensa.
  “Wananchi wote wa mkoa wa Iringa mnaombwa kutii sheria bila shuruti hii ni amri ….nawaombeni sana wananchi kutodanganywa na wanasiasa kwa kuvunja sheria “aliongeza kamanda huyo wa polisi.
  Hata hivyo alisema kuwa kimsingi zoezi la sensa lilipaswa kuhitimishwa Septemba mosi mwaka huu ila kutokana na serikali kuongeza muda wa zoezi hilo bado jeshi hilo la polisi linazingatia maagizo ya Msajili wa vyama vya siasa kama alivyoyatoa kwa jeshi hilo.
  Kamanda Kamuanda alisema kuwa jeshi hilo la polisi wala msajili wa vyama vya siasa hajazuia vyama vya siasa kuendelea na vikao vyao vya ndani kwa kipindi hiki na kuwa hata Chadema wakiwa mkoani Iringa wameendelea kufanya vikao vyao vya ndani katika kata mbali mbali za mkoa wa Iringa na hakuna mtu aliyewazuia kuendelea kufanya hivyo.
  Majibu ya Dkt Slaa
  Wakati jeshi la polisi likipinga shughuli hizo za vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara katibu mkuu wa Chadema Taifa Dkt Willbroad Slaa ameibuka na kusema kuwa chama chake kitaendelea na mikutano kama kilivyojipangia na kuwa wapo tayari kwa lolote litakalojitokeza .
  Dkt Slaa alisema kuwa walivumilia mara ya kwanza walipozuiwa mikutano hiyo mkoani Iringa na kuvuta subira hadi jumamosi zoezi hilo lilipomalizika sasa anashangazwa kuona jeshi hilo likiendelea kuzuia mikutano hiyo tena.
  “Tumemsikiliza kamishina wa sensa Hajati Amina Mrisho Said kuwa hadi sasa watu asilimia 95 wameandikishwa huku akiwata wale ambao bado kuwapigia simu wenyeviti wa mitaaa na vijiji ili wakaandikishwe na makarani wa sensa ….sasa jeshi la polisi linataka kutuambia kuwa hao watu asilimia 5 waliobaki wapo Iringa peke yake hadi wakazuia mikutano yetu? tunasema hatutakubali tutaendelea na mikutano yetu kama kawaida hatupotayari kabisa kusubiri hadi tarehe nane” alisema Dkt Slaa.
  Pia alisema kuwa kama ni uzalendo sasa umefika kikomo na kuwa wataendelea na ratiba zao za mikutano kama ilivyopangwa na watapambana kwa lolote .

  CHANZO Maktaba ya www.matukiodaima.co.tz 

  0 0

   Marehemu Mzee Anyosisye Mwakyusa enzi za uhai wake.
   Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Anyosisye Mwakyusa, baba mzazi wa mwandishi mwandamizi wa gazeti la Jambo Leo, Peter Ambilikile, wakati wa ibada ya kumuombea iliyofanyika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Ubungo Kibangu Dar es Salaam jana, kabla ya kuusafirisha kwenda mkoani Mbeya kwa mazishi yatakayofanyika leo.
   Ndugu jamaa na marafiki wakiaga mwili wa marehemu.

   Waombolezaji wakiwa kwenye ibada ya kuuga mwili wa mzee wetu Anyosisye Mwakyusa.
   Familia ya marehemu ikiwa na huzuni wakati wa ibada hiyo.


   Waomblezaji wakiwa ibadani.
   Wafiwa wakipewa pole.
   Mwanahabari Peter Ambilikile aliyefiwa na baba yake 
  akiwa katika huzuni.
   Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Ubungo Kibangu, Kishe Mhando (katikati), akiomba kabla ya kuanza kwa safari ya kwenda mkoani Mbeya.
   Mwili ukiondolewa kanisani.
   Waombolezaji wakisubiri gari lililobeba mwili huo kuondoka kwendaa mkoani Mbeya kwa mazishi.
  Ni huzuni tupu.

  Na Dotto Mwaibale

  MZEE Anyosisye Mwakyusa ambaye ni baba wa Mwandishi Mwandamizi wa Gazeti la Jambo Leo, Peter Ambilikile mwili wake umeagwa jana kwenda mkoani Mbeya kwa maziko. 

  Anyosisye alifariki juzi jijini Dar es Salaam kutokana na ugonjwa wa saratani uliokuwa ukimsumbua kwa muda mrefu.

  Ibada ya kuaga mwili wa marehemu huyo ilifanyika  katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Ubungo Kibangu jijini  Dar es Salaam jana  ikiongozwa na Mchungaji Kishe Mhando wa ushirika huo.

  Mchungaji Mhando alimwelezea Mwakyusa  kama mtu jasiri ambaye siku zote alikuwa mtu wa ibada na alikuwa akihudhuria ibada zote. Aliwaambia waumini kuwa mshahara wa dhambi ni mauti na mshahara wa kuwa na ibada ni maisha ya milele na Bwana Mungu. 

  Alisema watu huwa wana ratiba yao na hakuna mtu hata mmoja anayejua ratiba ya Mungu. "Msiba hauchagui mtoto mchanga, mtu mzima, mwanamke au mwanaume. Mipango yote ni ya Mwenyezi Mungu, yeye ndiye anajua anayefuata ni nani," alisema.

  Mazishi ya Mzee Mwakyusa yanatarajiwa kutafanyika mkoani nyumbani kwa marehemu eneo la Makungulu jijini Mbeya leo. Mwakyusa alizaliwa Mei 10, 1942. Alifunga ndoa yake mwaka 1968. Alifanya kazi serikalini na alistaafu mwaka 1980. 

  Mwaka 1999  Mwakyusa alianza kulalamika kuwa na matatizo ya koo na kuanza kupatiwa matibabu katika hospitali mbalimbali, ikiwemo Hospitali ya Ocean Road hadi kifo chake. 


  (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com

  0 0

   Moja kati ya majengo ya shule ya Msingi Busindi, yaliyomaliziwa kujengwa na mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu ulioko wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga. Mgodi huo unaomilikiwa na kampuni ya Acacia, umekabidhi miradi minne ya elimu na maji yenye thamani ya shilingi bilioni 1 ikiwa ni sera ya kampuni kujenga mahusiano mema na jamii inayozunguka migodi.

  NA K-VIS MEDIA

  MGODI wa dhahabu wa Bulyanhulu, BGML, Jumatatu Agosti 31, 2015, umekabidhi miradi, yenye thamani ya shilingi Bilioni Moja kwa Mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga.

  Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi miradi hiyo, Meneja Mkuu wa Mgodi huo unaomilikiwa na Kampuni ya uchimbaji madini, Acacia, Michell Ash, alisema, “Sisi BGML tulitoa ufadhili wa kugharimia miradi ya kijamii kwa wenyeji wetu na leo tunakabidhi miradi hiyo minne baada ya kukamilika kwake ikiwa ni ishara ya muendelezo wa utekelezaji wa ahadi zetu za kampuni kuwajibika kusaidia jamii.

  ” Alisema

  “Ninayo furaha kuu kutangaza kuwa BGML ilifadhili miradi minne kwa thamani ya shilingi bilioni 1,100,546,766 na tunatarajia kutoa fedha zaidi mwaka huu kusaidia sekta za Afya na Elimu.”Alifafanua

  Akitoa mchanganuo wa miradi iliyogharimiwa na mgodi huo ulioko wilayani Msalala, Ash alisema, BGML ilikamilisha ujenzi wa nyumba sita za walimu wa shule ya msingi Bugarama kwa thamani ya shilingi milioni 403,437,000, kukamilisha ujenzi wa madarasa sita na na ujenzi wa tenki la maji kwenye shule ya msingi Busindi kwa thamani ya shilingi 129,333,860 na ukamilishaji wa ujenzi wa nyumba mbili za walimu na ofisi ya walimu shule ya msingi Busindi kwa gharama ya shilingi 137,229,200.  Miradi mingine ni Ujenzi wa visima sita vya maji huko Kakola(1) na Kakola (9), Buyange, Bushing’we, shule ya sekondari Bugarama, Mwasabuka yote ikiwa na gharama ya shilingi 174,392,000.  Hali kadhalika BGML ilikamilisha ujenzi wa maabara ya Biolojia, Kemia na Fizikia kwenye shule ya msingi Nyikoboko ikitumia kiasi cha shilingi 256,154,706.  Akitoa shukrani za wilaya baada ya kupokea miradi hiyo, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Msalala, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya alisema, ni faraja ilioje kuona wawekezaji wanaonyesha moyo wankuisaidia jamii inayozunguka mgodi huo.  “Nataka niseme, mafanikio haya tunayoyaona leo hii ni matokeo ya ushirikiano mzuri kati ya wananchi na wawekezaji, ambapo wameamua kusaidia pale wananchi wanapokwama.” Alisema na kutoa wito kwa uongozi wa shule na maeneo yaliyokabidhiwa miradi hiyo kuitunza.

  Kukabidhiwa kwa miradi hiyo ni utekelezaji wa Sera ya kampuni ya Acacia inayomiliki mgodi huo ya mahusiano mema na jamii inayozunguka migodi yake.


   Kaimu Mku wa Wilaya ya Msalala, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Benson Mpesya, Meneja Mkuu Mgodi wa Dhahabu Bulyanhulu, BGML, Michelle Ash, (katikati) na Mkurugenzi wa Maendeleo Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, wakipapu maji wakati wa uzinduzi rasmi wa kisima kirefu cha maji kilichojengwa kwa ufadhili wa kampuni hiyo huko Bugarama. BGML, inayomilikiwa na Kampuni ya Acacia, imekabidhi miradi mine ya elimu na maji kwa Halmashauri hiyo yote ikiwa na thamani ya shilingi Bilioni 1.


  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Msalala, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Benson Mpesya, (kushoto), akiongozana na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu ulioko wilaya ya Msalala Mkoani Shinyanga, Michelle Ash, (katikati), na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Busindi, Joseph Misungwi, baada ya kuzindua moja kati ya nyumba kadhaa za walimu, zilizojengwa kwa msaada wa mgodi huo. Mhgodi huo unaomilikiwa na kampuni ya uchimbaji na utafutaji madini, Acacia, umekabidhi halmashauri ya wilaya hiyo, miradi ya elimu na maji yenye thamani ya shilingi Bilioni 1, kwenye hafla hiyo iliyofanyika Agosti 31, 2015. 


  0 0

  kushoto Mwenyekiti wa kamati ya tamasha la kuombea Amani hapa nchini,Alex Msama .

  Na Mwandishi Wetu
  MAASKOFU wa madhehebu mbalimbali na Wachungaji wanatarajiwa kushiriki kwenye Tamasha la Amani linalotarajiwa kufanyika Oktoba 4, mwaka huu Dar es Salaam.

  Tamasha la Amani ambalo litahusisha waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili ni maalum kwa ajili ya kuombea amani katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu.

  Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ilieleza kuwa maandalizi muhimu yanaenda vizuri.

  “Niseme kwamba Maaskofu na Wachungaji mbalimbali wamekubali kujumuika nasi siku hiyo katika tukio muhimu, ambapo baada ya tamasha la Dar es Salaam tutaelekea pia mikoani,” alisema Msama.

  Alisema wasanii mbalimbali wanaendelea kuomba kushiriki katika tamasha hilo alilosema litakuwa la aina yake.

   “Tunaandelea na mazungumzo na wasanii mbalimbali, ambapo tayari Rose Muhando ameshakubali kutumbuiza na wengine tuliowatangaza,” alisema Msama.

  Baadhi ya wasanii maarufu ambao wamewahi kushiriki matamasha yanayoandaliwa na Msama ni Rose Muhando, Rebecca Malope, Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa, Atosha Kissava, Ephraim Sekeleti na kundi la Glorious Celebration.

  Pia kwaya mahiri ya Kinondoni Revival, Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Sohly Mahlangu.

  0 0

  [Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa akizungumza na akinamama wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi, UWT (hawapo pichani) Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa akizungumza na akinamama wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi, UWT (hawapo pichani)Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa akicheza wimbo wa hamasa wa kampeni za CCM kabla ya kuanza kumnadi Dk. Magufuli kwa wanaUWT, Mkoa wa Dodoma. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa akicheza wimbo wa hamasa wa kampeni za CCM kabla ya kuanza kumnadi Dk. Magufuli kwa wanaUWT, Mkoa wa Dodoma.Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa akizungumza na akinamama wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi, UWT (hawapo pichani)Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa akizungumza na akinamama wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi, UWT (hawapo pichani)'...Na wapigwe tu maana hamna namna nyingine..' Mke wa Waziri Mkuu wa Tanzania, Mama Tunu Pinda akizungumza na akinamama wa UWT Mkoa wa Dodoma.  '...Na wapigwe tu maana hamna namna nyingine..' Mke wa Waziri Mkuu wa Tanzania, Mama Tunu Pinda akizungumza na akinamama wa UWT Mkoa wa Dodoma.

   Na Mwandishi Wetu, Dodoma
  MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa ameweka kando msimamo aliyokuwa nao awali na kuanza kumnadi kwa nguvu mgombea wa nafasi ya Urais kwa tiketi ya CCM, John Pombe Magufuli huku akiahidi atafanya hivyo nyumba kwa nyumba, kitanda kwa kitanda na shuka hadi shuka. 

  Kimbisa alitoa kauli hiyo jana mjini Dodoma alipokuwa kwenye mkutano na akinamama wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) walipokuwa wakizungumza na mgombea mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM, Bi. Samia Suluhu katika ukumbi wa NEC Makao Makuu ya Chama hicho mjini Dodoma. 

  Tukio la Kimbisa kumnadi mgombea urais wa CCM, Dk. John Pombe Magufuli pamoja na mgombea mwenza Bi. Suluhu linaonesha tayari kimbisa amefunga ukurasa wa kutokubaliana ambao aliuonesha mapema mjini hapo wakati wa mchakato wa chama hicho kutafuta mgombea mmoja wa urais atakaye peperusha bendera ya CCM. 

  Awali mara baada ya Magufuli kuchaguliwa kupeperusha bendera ya CCM, Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa wa Dodoma, Kimbisa pamoja na wajumbe wenzake wawili, yaani Sophia Simba na Dk. Emmanuel Nchimbi walizungumza na vyombo vya habari mjini Dodoma huku wakionesha kupinga uteuzi huo huku wakidai haukwenda sawia jambo ambalo ni tofauti na sasa. Akizungumza katika mkutano huo aliwataka akinamama wa UWT kuhakikisha wanashirikiana kuhamasisha kampeni za CCM na kutembea nyumba hadi nyumba mtu kwa mtu ili kuinadi ilaya ya Chama Cha Mapinduzi na hatimaye ushindi upatikane.

   Hata hivyo tayari Dk. Nchimbi naye ameungana na kuanza kumnadi mgombea huyo wa CCM ikiwa ni ishara ya kuvunja makundi. Mapema akizungumza katika mkutano huo, mke wa Waziri Mkuu wa Tanzania, Mama Tunu Pinda alisema yeye pamoja na mumewe hawawezi kuihama CCM kwa kuwa ndiyo chama pekee chenye sera za kueleweka na zinazotekelezeka ukilinganisha na vyama vingine.

   Aliwashauri wanachama waliogombea na kushindwa kutokata tamaa na kujaribu kukihama chama hicho kwani asiyekubali kushindwa si mshindani. "...Napendekeza wanao hama vyama wapigwe tu, maana hamna namna nyingine na wapigwe tu, lakini naomba tuwapige kwa kuwanyima kura huko wanapokwenda lakini si vinginevyo," alisema Mama Tunu Pinda alipokuwa akiwasalimu wanachama wa UWT.

   Katika mkutano huo mgombea mwenza wa CCM, Bi. Suluhu alitaja vipaumbele kwa akinamama endapo watafanikiwa kuunda Serikali, ikiwemo vile vya afya bora kwa mama na mtoto, ujasiliamali kuinua uchumi wa akinamama katika vikundi, uwezeshaji kipembejeo na zana za kisasa kwa akinamama wakulima, na hivyo kuwaomba wanaUWT kumchagua ili aweze kutimiza ndoto za ahadi zake. *Imeandaliwa na www.thehabari.com .

  0 0

  EAST African Community Secretariat, Kampala, Uganda, 1st September, 2015: 

  The President of the Republic of Uganda, H.E. President Yoweri Kaguta Museveni has said that Africa and many developing countries face the challenge of high and growing youth unemployment, which if not addressed can potentially be a source of instability as has been the case in North Africa.

  The President, who was this afternoon officiating at the official opening of the 1st East African Manufacturing Business Summit and Exhibition 2015 (EAMBS'15) at the Speke Resort, Munyonyo in Kampala, Uganda said many African youth had lost lives as they attempted to cross the Mediterranean Sea in search of employment opportunities in Europe.

  In a speech read on his behalf by the Prime Minister, Rt. Hon. Dr. Ruhakana Rugunda, President Museveni said "this is a painful lesson and we as leaders must think of a collective regional strategy to respond to unemployment including expanding the manufacturing sector capacity, promoting micro, small and medium enterprises (MSMEs) and youth entrepreneurs.


  President Museveni urged the private sector to invest sufficient funds in research, technology and innovation and called on both the public and private sectors to come up with a regional research, technology and innovation network to serve as a vehicle for fostering collaborative research and transfer of technology into the sector.

  The President noted that EAC Partner States were giving high priority to the development of infrastructure and energy, which were critical for efficient operations of the manufacturing sector in particular, and facilitating business, and cross-border investment. He said the regional target was to eliminate electricity supply deficits and achieve full interconnectivity of the region by 2017, making it (EAC) attractive for investment in heavy industries such as steel mills, petrochemicals, paper, cement etc.

  "East Africa is on its way to become a regional hub for manufacturing and a gate-way to investing in Africa," said the President.


  Uganda's Minister of Trade, Industry and Cooperatives, Hon. Amelia Kyambadde hailed the EAC Secretariat, East African Business Council and the private sector for initiating the Manufacturing Business Summit. She said the Summit creates a relevant regional platform for building partnerships for growth of cross-border businesses and also facilitate advocacy on the need to improve business environment for a competitive manufacturing sector.

  Uganda's Minister urged the private sector in the region to bring on board the youth as part of the aggressive apprenticeships, internships and other skills development programmes. She also urged the region not to forget Political Federation as the ultimate goal of the East African Community, as well as peace and stability, which will be able to consolidate the gains that are were being made in the regional integration process.

  The Secretary General of the EAC, Amb. Dr. Richard Sezibera urged Partner States' governments to take some tough decisions so as to turn the region into one viable economic entity by eliminating all barriers to the factors of production in the bloc; active involvement and commitment to industrialization, and; financing of technology transfer and innovation.

  "Governments in the region should also be bold enough to undertake investments in those areas where the private sector are afraid to venture into, as well as use of public preferential treatment to support locally manufactured goods, and the labour mobility by freeing labour market in the region," said the Secretary General.

  Amb. Sezibera said improving the business environment was critical, adding that the recent Kenya-Uganda sugar saga was the most unfortunate thing in the recent years of the integration process.

  "Sugar produced in Uganda or in any of the Partner States is EAC sugar, there is no such a thing like Burundi avocado, Rwanda pineapple, Tanzania Rice, Kenya beef or Uganda sugar. These are all products produced within the EAC and are bound by the EAC Customs Union and Common Market protocols," said Dr Sezibera.

  The Secretary General of the United Nations Conference on Trade and Development (UNCTAD), Dr. Mukhisa Kituyi, called for sustainable investment in an integrated manner in the region and noted that EAC was the gateway for Africa.  Dr Kituyi said the region needs to model itself to the realities of the market otherwise it will be left behind on the global market.


  The Chair of the East African Business Council, Mr. Dennis Karera, called for fast-tracking the harmonization of domestic taxes, work permits and residence regimes within the bloc in order to improve on the business environment.
  "In addition, governments need to improve road networks, do away with non-tariff barriers, and use the procurement system to promote local industries by providing opportunities for local sourcing so as to enhance the business environment and make the region competitive," said Karera.

  The Chief Executive Officer of Bidco Africa, Mr. Vimal Shah said this was an exciting moment for region and Partner States should start thinking of removing all the borders in readiness for rapid transformational change.  


  The two-day summit is running under the theme "Unleashing the Manufacturing Potential for Accelerated Development and Employment Creation in East Africa."

older | 1 | .... | 625 | 626 | (Page 627) | 628 | 629 | .... | 1897 | newer