Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 624 | 625 | (Page 626) | 627 | 628 | .... | 1898 | newer

  0 0

  - Naye akabidhi nakala ya kitabu chake kipya kiitwacho; ‘KAMWE SI MBALI TENA’
   Profesa Said Ahmed Muhammed (aliyevaa miwani) akimpa nasaha mwandishi wa ‘Paka wa Binti Hatibu’ Bwana Yussuf Shoka Hamad.
   Profesa Said Ahmed Muhammed akipokea nakala ya ‘Paka wa Binti Hatibu’ kutoka kwa mwandishi wa kitabu hicho Bwana Yussuf Shoka Hamad.
    Profesa Said Ahmed akimkabidhi Bwana Yussuf Shoka Hamad nakala ya kitabu chake kipya kiitwacho; ‘Kamwe si Mbali Tena’ nyumbani kwake Limbani, Wete.


  Profesa Said Ahmed na Bwana Yussuf Shoka wakionesha nakala za vitabu vyao walivyoandika na kukabidhiana leo hii.

  Na: Salum Msellem

  Mwandishi mashuhuri wa kazi za fasihi ya Kiswahili nchini na mwalimu mzoefu katika midani ya lugha na fasihi ya Kiswahili, Profesa Said Ahmed Muhammed amepokea nakala adhimu ya kitabu cha ‘Paka wa Binti Hatibu’ kutoka kwa mwandishi chipukizi wa tasnia hiyo Bwana Yussuf Shoka Hamad .  Tukio hilo lilifanyika leo huko nyumbani kwa Profesa Said, Limbani Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba wakati mwandishi huyo chipukizi alipomtembelea mwandishi huyo nguli wa Afrika Mashariki na kujadili mambo mbali mbali yahususyo uandishi na taaluma.

  Katika makabidhiano hayo, Profesa Said alimshukuru sana Bwana Yussuf  Shoka kwa juhudi zake na ujasiri alioonyesha wa kuandika kitabu hicho ambacho kwa sasa kimejinyakulia umaarufu mkubwa katika ulimwengu wa Kiswahili duniani.


  Akizungumza kuhusu mapokezi ya kazi yake hiyo Bwana Yussuf alisema, kwa hakika kitabu kimeuza na kupokelewa kwa kasi kubwa ambapo kwa sasa ameuza nakala nyingi za kitabu hicho na bado kuna mahitaji makubwa ya kazi hiyo hasa hasa visiwani Zanzibar.


  ‘Kwa hakika nimeshangazwa sana na jinsi jamii ilivyompokea Paka wa Binti Hatibu. Juzi juzi tu nilikuja na nakala hamsini (50) lakini kwa muda usiozidi siku tatu niliuza  nakala hizo zote. Na hadi sasa kuna orodha ndefu ya wasomaji wanataka kitabu hicho. Kwa kweli nashukuru sana na nimeemewa sana na mapokezi ya kazi yangu hii!’ Alisema Bwana Yussuf.


  Akizungumza kuhusu washabiki wake wakubwa na wasomaji wa kazi yake hiyo Bwana Yussuf alisema;

  ‘Nimefurahishwa sana kuona jinsi gani jamii yetu inathamini kazi za waandishi wazawa. Tena hata kwa wasomaji wasiokuwa wa fani ya fasihi. Kwa mfano, nimeuza nusu ya nakala zote kwa wafanyakazi wa PBZ, Pemba na zilziobaki kwa wanafunzi na walimu wa Chuo kikuu Huria cha Tanzania, tawi la Pemba. Kwa kweli nashukuru sana kwa kuungwa mkono kiasi hiki!’


  Pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana kwa kitabu hicho, Profesa Said alimnasihi mwandishi huyo chipukizi nchini kutovunjika moyo na changamoto nyingi zinazomkabili kwa sasa na kumtaka aendelee kuandika na kuielemisha jamii kwa kadiri ya vile anavyoimulika na kuiakisi kwa minajili ya kuleta mabadiliko na maendeleo katika jamii ya Tanzania, Afrika Mashariki na Ulimwengu kwa ujumla.


  Profesa pia alimtaka mwandishi huyo anayejulikana zaidi kwa kazi yake ya ‘Paka wa Binti Hatibu’ kuongeza kasi ya uandishi na kumtaka aisivunjike moyo hata kidogo katika kukabiliana na shida zilizopo katika tasnia ya uandishi hasa hasa za uchapishaji.

  ‘Nasaha zangu ni kukutaka tu uendelee kuandika kwa kasi hiyo hiyo. Usivunjike moyo kwani naona unaenda na kasi nzuri kwa sasa.’

  Mwandishi Yussuf Shoka Hamad hadi sasa ameshakamilisha kazi yake ya ‘Paka wa Binti Hatibu’ na sasa anatarajia kuchapisha vitabu vyengine vitano mwaka huu pindipo kazi hizo zitachapishwa kwa wakati unaofaa.

  ‘Kwa kweli kuna msoyoyo mkubwa katika kuchapisha kazi siku hizi. Mchapishaji anaweza kuchukua mua mrefu sana kukupatia majibu ya muswada wako na hata kuuchapisha. Hii inarudisha nyuma kidogo kwa kweli’ Alisema Bwana Yussuf Shoka kumwambia Profesa Said.

  Kuhusiana na kadhia hiyo, Profesa alimtaka Bwana Yussuf kujaribu kuwasiliana na wachapishaji wengine ili kuharakisha juhudi zake za uchapishaji wa vitabu.

  Wakati huo huo, Profesa Said alimweleza  Bwana Yussuf kuwa hadi sasa ameshaandika vitabu takribani 57 na moja ya kati ya kitabu chake kinachotamba kwa sasa ni riwaya yake  inayokwenda kwa jina la ‘Kamwe Si Mbali Tena’ ambacho pia alimkabidhi Bwana Yussuf Shoka nakala ya kitabu hicho.

  Katika mazungumzo yao, Profesa aligusia nukta mbali mbali zinazohusiana na Elimu na maendeleo ya taifa pia sambamba nay ale ya uandishi wa vitabu na kupanuka kwa kiwango cha taaluma nchini.

  ‘Jamii ya Watanzania kwa sasa imepanuka kifikra na kimawazo. Ninaposema hivi sikusudii wasomi tu, bali hata Watanzania wasiosoma wametanuka sana kiupeo kiasi ambacho kasi ya maendeleo nchini inakuwa kubwa. Hivyo, ni busara kabisa kwa wasomi kurejea nchini na kushirikiana na wenzao wengine katika kuharakisha maendeleo hayo!’ Alisema Profesa Said.


  Profesa Said ni mwalimu mstaafu kwa sasa aliyeamua kwa makusudi kurejea nchini kujiunga na wazalendo wengine katika kusukuma mbele maendeleo ya Taifa ambapo kwa sasa na kwa nyakati tafauti amekuwa akifundisha katika chuo kikuu cha Taifa (SUZA) na chuo kikuu kishiriki cha Elimu Chukwani.


  Naye Bwana Yussuf Shoka ambaye  ni mzaliwa wa Wingwi, Wilaya ya Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba ni mhadhiri wa Kiswahili na Fasihi katika chuo kikuu cha London (SOAS) na pia anafundisha Kiswahili katika chuo kikuu cha Cambridge nchini Uingereza.

  0 0


   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Qatar Nchini Tanzania Mhe. Abdulla Jassim Al Maadadi wakati Balozi huyo alipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Agosti 31, 2015 kwa ajili ya kujitambulisha.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Qatar Nchini Tanzania Mhe. Abdulla Jassim Al Maadadi wakati Mabalozi huyo alipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Agosti 31, 2015 .
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na kumkaribisha Balozi wa Burundi Nchini Tanzania Mhe. Issa Ntambuka wakati Balozi huyo alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu    Dar es salaam leo Agosti 31,2015 kwa ajili ya kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa Nchini. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Burundi Nchini Tanzania Mhe. Issa Ntambuka wakati Balozi huyo alipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Agosti 31, 2015, kwa ajili ya kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa Nchini.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Burundi Nchini Tanzania Mhe. Issa Ntambuka wakati Mabalozi huyo alipomtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu Dar es salaam leo Agosti 31, 2015, kwa ajili ya kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa Nchini. (Picha na OMR) 

  0 0
 • 08/31/15--05:13: STARS YAMALIZA KAMBI UTURUKI
 • Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro chini ya Kocha wake Mkuu Charles Boniface Mkwasa imefanya mazoezi yake ya mwisho leo asubuhi katika viwanja vya hoteli ya Green Park Kartepe – Kocaeli nchini Uturuki.
  Taifa Stars ambayo imeweka kambi nchini Uturuki kwa takribani wiki moja, inajiwinda na mchezo wake dhidi ya Nigeria siku ya Jumamosi Septemba 5, 2015 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika mwaka 2017.
  Kocha Mkuu wa Stars Charles Mkwasa akiongea na tovuti rasmi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) www.tff.or.tz amesema anashukuru kambi imekua na mafanikio makubwa kwani vijana wanaonyesha mabadiliko makubwa sana.
  “Ukiondoa mchezaji moja tu ambaye ni majeruhi Abdi Banda, Mkwasa amesema wachezaji wengine wote wapo fit na kila mmoja atakayepata nafasi katika mchezo wa sikuya jumamosi atafanya vizuri” amesema Mkwasa.
  Mkwasa amesema mazingira ya kambi yamekua mazuri, na katika mechi ya maozezi dhidi ya Libya iliyochezwa siku ya ijumaa, vijana wake walicheza vizuri kwa nguvu na kufuata maelekezo yake, makosa machache yaliyojitokeza katika mchezo huo wameyafanyia kazi na sasa anaamini wako tayari kuwakabili Nigeria.
  Mwisho Mkwasa amewaomba watanzania kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa siku ya jumamosi  kuishangilia timu ya Taifa, kwani uwepo wa washabiki wengi uwanjani utawaongeza morali zaidi wachezaji na kujiona wapo nyumbani wanapambana kwa ajili ya Taifa lao.
  Naye nahodha wa Taifa Stars, Nadir Haroub “Cannavaro” amesema maandalizi waliyopata ni mazuri na yamewajenga vilivyo kuelekea kwenye mchezo dhidi ya Nigeria siku ya jumamosi na kuwaomba watanzania kuja kwa wingi kuwasapoti.
  Nadir amesema wao kama wachezaji kila mmoja yupo fit na anahitaji  kucheza mechi hiyo, hivyo yeyote atakayepata nafasi ya kucheza ana imani atafanya vizuri katika kuipeperusha bendera ya Tanzania.
  Stars ambayo iliweka kambi ya takribani siku nane katika milima ya Katrepe - Kocaeli, inatarajiwa kuodoka kesho jumanne saa 1 jioni nchini Uturuki kurejea nyumbani kwa usafiri wa shirika la Ndege la Uturuki (Turkish Airlines) na kuwasili uwanja wa JK Nyerere majira ya saa 9 kasoro usiku.
  Mara baada ya kuwasili Dar es salaam timu itaendelea na kambi kwa kufanya mazoezi mepesi siku ya jumatano pamoja wa wachezaji wa kimataifa Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu na Mrisho Ngasa katika uwanja wa Taifa kujiandaa na mchezo wa siku ya jumamosi dhidi ya Nigeria.


  0 0

   Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dares Salaam leo.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kazini jijini Dar es Salaam leo.

  Na Magreth Kinabo 
  SHERIA mpya   ya Makosa ya Mtandao ya mwaka   2015 na Sheria ya Miamala ya Kielektroniki ya mwaka 2015 zitaanza kutumika rasmi kesho Septemba Mosi mwaka huu, hivyo watumiaji   na watoa huduma waaswa kuzingatia sheria hizi ili kuepuka mkondo wa sheria.

   Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dares Salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo.

  “Sheria hizi ni nzuri zitaanza kutumika Septemba Mosi mwaka huu,kuanzia saa 6.00 usiku . zina maslahi katika nchi yetu. Ninatoa wito kwa wananchi kuzingatia matumizi salama ya mtandao kwa manufaa yako na maendeleo ya Taifa letu,” alisema Profesa Mbarawa.

   Aliongeza kuwa sheria hiyo ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015 hazihitaji utungaji wa kanuni kwa kuwa iko wazi.

   Alisema tayari wizara imeanza kuelimisha watu kuhusu sheria hiyo na itendelea kuwajengea uwezo wadau mbalimbali.


  Profesa Mbarawa alisema sheria ya makosa ya mtando ya mwaka 2015 na Tanzania sio nchi ya kwanza kuwa nayo, bali nchi mbalimbali zina sheria kama hiyo ,ambapo alitolea mfano Uingereza,India,Malaysia, Uganda na Korea ya Kusini.

   Akizungumzia kuhusu  madai sheria hiyo kuhusika na suala la Uchaguzi Mkuu, alisema si kweli, bali imekamilika katika kipindi hicho ndio maana baadhi ya watu wanadai hivyo.Aliongeza kwamba sheria hiyo imetunga ili kudhibiti matumizi ambayo  si mazuri. 

  “ Mtu akitumiwa ujumbe akiupokea hapaswi kuisambaza  kwani atakapousambaza atakuwa na amefanya kosa,”alisisitiza.

  Aliyataja baadhi ya makosa kuwa ni usiri, usalama wa upatikanaji wa taarifa za kompyuta na mifumo  kama vilekuingilia mawasiliano ya kompyuta au mifumo ya kompyuta kinyume cha sheria na wizi wa taarifa kimtandao.

  Makosa  dhidi ya kompyuta ikiwa ni pamoja na,udanganyifu kwa kutumia kompyuta,kugushi kwa kutumia kompyuta wizi wa utambulisho wa mtu binafsi  mtandaoni, matumizi ya vifaa kinyume cha sheria.

  Makosa yanayohusiana kimaudhui kama vile usambazaji wa ponografia, ponografia za watoto makosa dhidi ya ubaguzi wa rangi na chuki, michezo ya kmari mtanadaoni kiunyume cha sheria, kashfa na habari za uongo na makosa dhidi ya haki na hati miliki.

  Pia inatambua muungano wa makosa inajumuisha kama vile utakatishaji wa fedha haramu na ugaidi kwa kutumia mtandao.

  Kwa upande wa sheria ya miamala ya kieletroniki ya mwaka 2015, baadhi ya makosa likiwemo la wajibu wa watoa huduma kwa walaji, bidhaa ,huduma au mawasiliano ambayo hayajaombwa na uhalali wa Muamala wa elektroniki.

  Aliongeza kuwa kanuni za sheria hiyo zinatayarishwa zikiwa tayari zitangazwa  na zitaanza kutumika wakati wowote.

  0 0

   Waziri wa Uchukuzi Samwel Sitta akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya kuchukua hatua kubwa kuanza  kufufua reli ya kati muda wowote, ujenzi wa reli hiyo utaanza ili kuongeza kasi ya maendeleo  hapa nchini leo Jiji Dar es Salaam.
  Waandishi wa habari walio hudhulia  katika mkutano na Waziri wa Uchukuzi Samwel Sitta, wakimsikiliza kwa makini.
   (Picha na Emmanuel Mssaka.

  Na JenikisaNdile –Maelezo

  SERIKALI  kwa kushirikiana na kampuni ya reli Asset holding imejizatiti kuimarisha miundo mbinu ya reli itakayogharimu Tsh. Trilioni 16 katika kuleta maendeleo endelevu hapa nchini.


  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam waziri wa uchukuzi Mhe. Samweli sitta amesema kuwa  mkakati ni kuimarisha  reli  katika maeneo mbalimbali hapa nchini.


  Aliongeza kuwa maeneo yatakayonufaika na uboreshwaji wa miundo mbinu hiyo ni pamoja na Songa Mpiji. Mtwara hadi Mbambabay, Songea hadi Mchuchuma na mradi mpya wa reli ya kutoka Dar es Salaam hadi Bagamoyo.


  “Lengo  la miradi hii ni kuhakikisha kuwa tunaleta maendeleo ya kiuchumi  kwa kujipatia fedha za kigeni ambazo  zitatokana na usafirishaji wa mizigo nje ya nchi “ amesema Mhe. Sitta.


  Aliongeza kuwa miradi hiyo inatarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi wa tisa  ambapo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Jakaya Kikwete ataweka jiwe la msingi tayari kwa utekelezaji.


  Aidha alibainisha kuwa kwa kuimarisha miundo mbinu ya reli kutasaidia katika kurahisisha usafirishaji wa mizigo yenye uzito mkubwa kama mafuta, makaa ya mawe na chuma ndani na nje ya nchi.

  0 0

  Kamishna wa Bima nchini Bw. Israel Kamuzora.

  Jovina Bujulu-MAELEZO
  WATANZANIA theluthi mbili hawana ufahamu wa kutosha kuhusu namna Bima inavyofanya kazi nchini hasa Bima ya Maisha na Mali.

  Hayo yamesemwa na Kamishna wa Bima nchini Bw. Israel Kamuzora alipokuwa akifunga mafunzo ya wiki ya huduma kifedha na uwekezaji mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.

  Kamuzora aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kueneza ujuzi na ufahamu waliopata ili wananchi walio wengi waweze kunufaika na huduma za bima nchini.

  “Ninawaomba muwe mabalozi wazuri wa kueneza ufahamu juu ya faida za Bima kwa ndugu, jamaa na marafiki ambayo ni mojawapo ya mbinu za kujilinda kimaisha na kujikwamua katika umasikini”. Alisema Kamuzora.

  Kamuzora alisema kuwa kwa upande wao kama waratibu wa huduma za Bima nchini wanao wajibu wa kuendelea kujenga mazingira ambayo ni rafiki na wezeshi kwa watoa huduma  ya Bima ili waendelee kuwa wabunifu katika kufikisha huduma hiyo kwa Watanzania wenye uwezo mkubwa na mdogo.

  Aidha, Bw. Kamuzora alisema kuwa mpango wa Taifa wa huduma Jumuishi za kifedha nchini unalenga kuwafikia watu wazima asilimia 50 wanaotumia huduma rasmi za kifedha ifikapo mwaka 2016.

  Ili kufanikisha mpango huo, Bw. Kamuzora alitoa wito kwa taasisi za kifedha na za utafiti wa sayansi kuendelea kushirikiana na mamlaka ya Bima kuona namna ya kuendeleaza matumizi ya simu za mkononi kwa ajili ya kuwapatia wananchi fursa ya kupata huduma za Bima ili kulinda mali na maisha ya Watanzania waliowengi.

  Hadi sasa nchini, takwimu zinaonyesha kuwa karibu asilimia 90 ya wenye simu za mkononi nchini wanatumia huduma za fedha za simu ziliongeza ndugu Kamuzora.

  Mafunzo ya wiki ya huduma za kifedha na uwekezaji yalipambwa kwa kauli mbiu inayosema “Maisha ni Duni Bila Bima” yaliwahusisha wajariamali, benki, na kampuni za Bima yalidhaminiwa na kampuni ya NUEBRAND na Shirika la PESCODE.

  0 0

   Mgombea wa nafasi ya udiwani katika kata ya Kilungule Said Fella (kushoto) akiteta jambo  na mgombea wa nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Mbagala Issa Mangungu, wakati wa uzinduzi wa kampeni za udiwani ambazo zimezinduliwa jana.
  Msanii Richard  Maviko, (katikati) akiwa na wasanii wenzake  wakitoa salamu maalum ya kumuunga mkono mgombea wa udiwani katika Kata ya Kilungule Said Fella, ambaye  amezindua rasmi kampeni katika kata hiyo.
  Msanii wa muziki wa kizazi kipya Lameck Ditto akiongea kwa niaba ya wasanii wenzake  ambao walikuwepo katika uzinduzi wa mgombea wa udiwani kata ya Kilungule iliyopo.

  Asha Kigundula
  WASANII mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya juzi walimuunga mkono Mkurugenzi wa  Kituo cha Mkubwa na Wanawe, Yamoto Band na meneja wa Wanaume Family Said Fella, katika uzinduzi wa kampeni za kuwania Udiwani katika kata ya Kilungule, iliyopo  Mbagala Dar es Salaam.

  Katika mkutano huo ambao ulifurika vilivyo kwa Wanachama wa Chama cha Mapinduzi  (CCM) na wakazi wa kata hioyo kujitokeza kwa wiki kumsikiliza mgombea huyo, ambaye  alifanyika uzinduzi wake kwenye uwanja wa njia panda ya Chasimba Majimatitu B.

  Baadhi wasanii hao ni Siti Almas, Amin Mwinyimkuu, Lameck Ditto, Rich Mavoko,  Queen  Darleen na meneja wa msanii Nassib Abdul Hamis Taletale  'Babu Tale'.  Akizungumza kwa niaba ya wasanii wenzake   Ditto aliwataka wakazi wa Maji matitu  kutofanya makosa kwa kumpa mpinzani, wampe Said Fella ili awe diwani wao.

  Alisema kila mtu atambue kuwa ukimchagua mtu wa CCM utakuwa umefanya jambo la  muhimu kwa sababu ndiyo anayeweza kutelekeza ilani ya chama hicho.

  Ditto alisema atamfahamu Fella ni mchapakazi hivyo kumpa kwake kata hiyo lazima iwe  na mafanikio makubwa.

  Alisema sehemu yoyote anayokuwepo Fella lazima iwe na mafanikio hivyo hata kama hiyo  itakuwa moja ya kata zenye mafanikio makubwa.

  "Naomba msifanye makosa kuchagua upinzani mchagueni Fella kuwa diwani wenu na  mchagueni Issa Makungu kuwa mbunge wenu wa Mbagala na John Magufuli kuwa Rais wa  Tanzania"alisema Ditto.

  Akizungumza kwa upande wake Fella alisema anaitambua Kata hiyo ina matatizo mengi,  hivyo akipata nafasi atahakikisha anaziofanyia kazi.

  Fella alisema yeye ni mkazi wa eneo hilo ana amini kupata kwake nafasi kutatua mambo  mengi kwa kuwa yupo karibu na viongozi wakubwa ambao atakuwa akikutana nao.

  "Nitaweza kukutana na viongozi wakubwa na kutatua matatizo yetu ya huku Kilungule  ambayo ninayofahamu vizuri kwa sababu nami ndiyo mkazi wa eneo hilo"alisema Fella.

  0 0

   Baadhi ya wanajeshi wakiwa wamebeba jeneza la Marehemu Kanali Mstaafu Ayub Kimbau aliyewahi kuwa mbunge wa Mafia wakati wa Mazishi yake huko Kilwa leo jioni.
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la aliyewahi kuwa Mbunge wa Mafia Kanali Mstaafu Marehemu Ayub Kimbau huko Mafia leo jioni.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,mkuu wa Mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo na watoto wa marehemu Kanali Mstaafu Marehemu Ayub Kimbau wakiomba dua wakati wa mazishi ya Mbunge huyo wa Zamani wa Mafia yaliyofanyika huko Mafia leo jioni.
  Rais Dkt.Jakaya Kikwete na Mkewe Mama Salma(aliyeketi na mke wa Marehemu kushoto) wakimfariji mke wa Marehemu Kanali Mstaafu Nyumbani Kwake Mafia wakati wa mazishi ya Mbunge huyo wa zamani wa Mafia leo jioni.
  (picha na Freddy Maro)

  0 0

  Mgombea Ubunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh aziz Abood Pamoja na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini wakiwaasa wakazi wa Jimbo la Morogoro Mjini Kumchagua MH John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mgombea Ubunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh aziz Abood Akiwahutubia wananchi na wakazi wa Jimbo la Morogoro Mjini waliojitokeza kwenye uzinduzi wa Kampeni za  Ubunge za Jimboni humo.
  Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini Fikiri Juma akimnadi Mgombea Ubunge Wa Jimbo hilo Mh Aziz Abood wakati wa Uzinduzi wa Kampeni za Jimbo hilo, ikumbukwe Mh aziz Abood anatetea Kiti cha Ubunge wa Jimbo hilo Mara baada ya Kuongoza Jimbo hilo kwa Miaka 5 Kwa mafanikio ya Hali ya Juu.  Wakazi wa Jimbo la Morogoro Mjini waliojitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi wa Kampeni za Ubunge na Madiwani wa Jimbo hilo.

  0 0


  Mkuu wa Wilaya Kinondoni Mh.Paul Makonda alipokuwa akizungumza baada ya kuzindua vitabu. 
  Mh.Paul Makonda akizindua vitabu 
   Mh.Paul Makonda alipokuwa akionesha vitabu baada ya kuzindua
  Apostle Ndegi akimlisha keki Mwl Lilian Ndegi ambaye ni mke wake ikiwa ni ishara ya kupongezana.
  Mh.Paul Makonda akilishwa keki Mwl Lilian Ndegi mwandishi wa vitabu vilivyozinduliwa.


  Baadhi ya wageni waliokuwa wamealikwa katika uzinduzi huo wa vitabu wa kwanza kush Mchungaji Deborah Ntepa,Mama Mchungaji Tumwidike koka Mbeya na Mwl. Lilian ndegi mwenyeji
  Mh.Paul Makonda alipokuwa akiwakabidhi vitabu baadhi ya watu walionunua baada ya kuvizindua
  Mh.Paul Makonda alipokuwa akiwakabidhi Mzee wa Kanisa vitabu baadhi ya watu walionunua baada ya kuvizindua
  Mh.Paul Makonda alipokuwa akiwakabidhi Kiongozi wa mabinti Kanisani hapo Magreth vitabu baada ya kuvizindua

  Mama Mchungaji Tumwidike kutoka mbeya alikuwepo katika uzinduzi huo
  Mchungaji Deborah Ntepa kutoka Oasis Healing Ministry alikuwepo katika uzinduzi huo
  Upendo Nkone alipokuwa akihudumu katika ibada ya uzinduzi wa vitabu iliyoongozwa na Mh. Makonda

  Mwl Lilian Ndegi na Upendo Nkone wakicheza mbele za Bwana ilikuwa full shangwe
  Mh.Paul Makonda wa kwanza kushoto,katikati ni Apostle Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Center na wa mwisho ni Mwandishi wa vitabu Mwl. Lilian Ndegi 
  Mh.Paul Makonda na Mwandishi wa vitabu Mwl. Lilian Ndegi katika picha ya pamoja baadhi ya mabinti  wa kanisani hapo.
  Mwandishi wa vitabu Mwl. Lilian Ndegi katika picha ya pamoja baadhi ya wakina mama wa  kanisani hapo.
  MKUU wa Wilaya Kinondoni Mh.Paul Makonda siku ya jana katika kanisa la Living Water Center chini ya mtumishi wa Mungu Apostle Onesmo Ndegi alikuwa mgeni wa heshima katika uzinduzi wa vitabu vitatu  "MJUE MWANAMKE,USIIPE HOFU NAFASI na RAFIKI ANAYEKUFAA vilivyoandikwa na Mwl Lilian Ndegi wa Kanisa la Living Water Center Kawe.

  Ibada hiyo ya uzinduzi wa vitabu ilipambwa na vikundi vya uimbaji sifa kama Living Waters wenyeji Upendo Nkone,GUG Dancers na More Than Enough Band.

  Mkuu huyo wa wilaya ndiye aliyezindua vitabu hivyo na kuendesha zoezi zima la uuzaji wa vitabu hvyo,kwa kuanza alinunua vitabu hivyo vitatu kwa shiling Milioni 5 ikiwa ni kuchangia na kusapoti huduma hiyo ya uandishi wa vitabu vya Mwl Lilian Ndegi ambaye ni Mama yake kwa malezi ya kiroho kanisani hapo Living Water Center Kawe.

  Katika uzinduzi huo uliambatana na kukata keki ikiwa ni ishara ya kufurahia mafanikio ya kazi ya uandishi wa Mwl Lilian Ndegi na ugawaji wa zawadi katika tukio hilo ulifanyika kwa watu ambao wamekuwa wakihusika katika ufanikishaji kwa namna moja au nyingine au kumuwezesha Mwl Lilian kufanikisha uandishi wake wa vitabu.

  Mh Paul Makonda aliwasihi washirika wa Kanisa la Living Water Center Kawe kusapoti kazi ya Mwl Lilian ikiwa ni kwa kununua na kuvisambaza vitabu vyake ili viwafikie wasomaji wengi ikiwa vitaleta matokeo mazuri katika maisha yao kutokana na ujumbe ulio ndani ya vitabu hivyo.

  Apostle Onesmo Ndegi kiongozi wa Kanisa la Living Water Center na mme wa mwandishi wa vitabu Mwl Lilian Ndegi katika kuzungumza kwake alikuwa akijivunia Mkuu huyo wa Wilaya na kusema ni kijana wake anamfahamu vizuri siku nyingi tangu bado anasoma na kusema amelelewa hapo na kusema kuwa alikuwa msikivu,na mpaka Mh Rais kumteua kwa nafasi hiyo ya kuwa Kiongozi wa Wilaya hakukosea.

  0 0


  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

  JESHI LA POLISI TANZANIA  RPC.                                                                                              Ofisi ya Kamanda wa Polisi,                                                                                                                                                                                                                                                                                                   Mkoa  wa  Mbeya,                                                                                    

  Namba ya simu 2502572                                                                                              S. L. P. 260,

  Fax - +255252503734                                                                                            MBEYA.             

                tanpol.mbeya@gmail.com

                  

  TANGAZO KWA UMMA.

  JESHI LA POLISI TANZANIA LINAWAITA KWENYE USAILI WAHITIMU WALIOORODHESHWA WA SHAHADA, STASHAHADA NA ASTASHAHADA. USAILI UTAFANYIKA KUANZIA TAREHE 03.09.2015 HADI TAREHE 04.09.2015 KUANZIA SAA MBILI ASUBUHI HADI SAA KUMI JIONI KATIKA MAENEO YAFUATAYO:-

  ·         FANI YA UTAWALA, UCHUMI, USIMAMIZI WA SHERIA NA UTEKELEZAJI [BALE], UALIMU, UANDISHI HABARI, UHANDISI MADINI [MINING ENGINEERING], UGAVI, LUGHA, USHAURI NASIHI, KATIBU MUKTASI, LAND SURVEY CATHOGRAPHER NA GEOMATICS WATAFANYA USAILI KATIKA CHUO CHA TAALUMA YA POLISI DAR ES SALAAM [DPA] KILICHOPO KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI JIJINI DAR ES SALAAM.


  ·         MAFUNDI MAGARI, MATENGENEZO YA PIKIPIKI, MAFUNDI MATENGENEZO YA UMEME WA MAGARI [AUTO ELECTRICAL], MAFUNDI RANGI ZA MAGARI, MAFUNDI MAGARI, MAFUNDI USHONAJI,MAFUNDI BODY ZA MAGARI NA MADEREVA. USAILI WA KADA HIZI UTAFANYIKA KIKOSI CHA POLISI UFUNDI KILICHOPO KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI DAR ES SALAAM.  ·         MATENGENEZO YA KOMPYUTA, FAX & PHOTOCOPY MACHINES NA MAWASILIANO YA REDIO [DIPLOMA IN RADIO COMMUNICATION], USAILI WAO UTAFANYIKA NYUMA YA KIKOSI CHA UFUNDI YAANI TEHAMA KEKO CHINI.


  ·         WAKEMIA, BAILOJIA [MOLECULAR BIOLOGY] USAILI UTAFANYIKA MAKAO MAKUU YA POLISI YALIYOPO MAKUTANO YA BARABARA YA OHIO NA GHANA JENGO LINALOTAZAMANA NA POSTA HOUSE.  ·         KADA ZA AFYA USAILI WAO UTAFANYIKA KATIKA KIKOSI CHA AFYA KILICHOPO KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI DAR ES SALAAM.


  ·         MANAHODHA NA MAFUNDI MITAMBO WA MELI, USAILI WAO UTAFANYIKA KATIKA KIKOSI CHA WANAMAJI KILICHOPO KARIBU NA JENGO LA MAHAKAMA YA RUFAA.


  ·         DAKTARI WA WANYAMA, USAILI WAO UTAFANYIKA KATIKA KIKOSI CHA MBWA NA FARASI KILICHOPO KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI DAR ES SALAAM.


  ·         MAFUNDI AC ZA MAJUMBANI, ARCHITECTURE DRAFTMAN, QUANTITY SURVEYORS, CIVIL ENGINEER, WELDING & FABRICATION, UMEME WA MAJUMBANI, PAINTING, ALUMINIUM & GLASS WORK, PLUMBING, MOSONRY, MOTOR REWINDING, HYDRO GEOLOGY DRILLING WELL, REFRIGERATION & AIR CONDITIONING. USAILI WA KADA HIZI UTAFANYIKA KIKOSI CHA POLISI UJENZI NDANI YA KAMBI YA POLISI BARRACKS KURASINI KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI DAR ES SALAAM.


  ·         FANI ZA BENDI, BRASS BENDI, WOODWIND, STRING JAZZ NA PERCUSSIVE, USAILI WAO UTAFANYIKA KIKOSI CHA BENDI KILICHOPO KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI DAR ES SALAAM.


  ·         FANI YA URUBANI,USAILI  UTAFANYIKA  KIKOSI CHA ANGA KILICHOPO UWANJA WA NDEGE NDOGO WA ZAMANI WA J.K.NYERERE DSM.

  MUHIMU:

  1.      MWOMBAJI AFIKE KWENYE USAILI AKIWA NA NAKALA HALISI YA VYETI VYOTE VYA MASOMO/TAALUMA [ACADEMIC TRANSCRIPT (S)/CERTIFICATE (S) YAANI KIDATO CHA NNE, SITA, CHUO NA CHETI CHA KUZALIWA. KIAPO CHA KUZALIWA HAITAKUBALIWA.

  2.      MWOMBAJI ALIYEITWA KWENYE USAILI ATALIPIA GHARAMA ZA UPIMAJI AFYA SHILINGI ELFU KUMI (10,000/=), USAFIRI, CHAKULA NA MALAZI KWA MUDA WOTE WA ZOEZI LA USAILI.

  3.      AMBAYE HATAHUDHURIA USAILI KUANZIA SIKU YA KWANZA HATAPOKELEWA.

  ILI KUPATA/KUONA ORODHA YA MAJINA, TEMBELEA www.policeforce.go.tz

  Imetolewa na:

  [AHMED Z. MSANGI – SACP]


  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

  0 0


  Ms Martha Nghambi, the Country Director for Global Peace Foundation Tanzania (GPFTZ), addressing a press conference in Dar es Salaam during the official launch of the peaceful awareness national campaign named Amani Kwanza” on Monday, August 31, 2015. On the right is Reverend Thomas Ngoda, Director for the Inter Religious Council for Peace in Tanzania (IRCPT) and left is GPFTZ Administration Officer, Ms Hilda Ngaja. 
  Director for the Inter Religious Council for Peace in Tanzania (IRCPT), Reverend Thomas Ngoda, speaking during the press conference. Others in the picture are GPFTZ Administration Officer, Ms Hilda Ngaja, and GPFTZ Country Director, Martha Nghambi.

  GPFTZ Country Director, Martha Nghambi (right), addressing a press conference in Dar es Salaam on Monday, August 31, 2015. On the left is GPFTZ’s Projects and Youth Officer, Mr Dixon Kamala.

  Global Peace Foundation Tanzania (GPFTZ) Country Director, Martha Nghambi (left) and Director for the Inter Religious Council for Peace in Tanzania (IRCPT), Rev. Thomas Goda, showing a flyer with peace awareness message.

  Members of the press at the conference.


  GPFTZ Administration Officer, Hilda Ngaja (left) and Ambassador of Peace for GPF, Dr. Ulimwengu, showing a flyer with peace awareness message.


  By Daniel Mbega

  Dare es Salaam, Tanzania

  Monday, August 31, 2015: Tanzanians have been urged to observe peace through common spiritual aspirations, principles, values and the universal truth during the upcoming general election.

  The call was made today during the official launch of a peacefulawarenessnationalcampaignnamedAmaniKwanza” by the Global Peace Foundation Tanzania (GPFTZ) with its partner, Inter Religious Council for Peace in Tanzania (IRCPT).

  Speaking during the launch in Dar es Salaam, GPFTZ’s Country Director Ms Martha Nghambi, said the campaign seeks to inspire and encourage all Tanzanians towards a peaceful participation at the upcoming General election on 25thOctober 2015.

  This campaign is not intending to support or oppose any candidate, and has no political affiliations and it works on the sloganKURA YANGU UZALENDO WANGU, AMANI YA NCHI YANGU NI JUKUMU LANGU” (My vote my patriotism, my country’s peace my role),” she said.

  Tanzania had recently become one of the few African countries that had continued to mobilise other countries to maintain peace.

  According to her, the campaign – which will be promoted on all media outlets (mainstream and online) – is designed to promote and influence peace throughout the country, with particular focus on women and youths because they are the majority of voters and are also the most vulnerable groups in the event of election upheavals.

  Ms Nghambi added: “The campaign aims to make women and youths good ambassadors in maintaining and promoting peace during the election season as well as to curb unnecessary events and actions that have potential to interrupt peace in Tanzania.”

  IRCPT director, Rev. Thomas Goda, said everyone has the responsibility to maintain peace in the country especially towards this year’s general elections.

  “African region has witnessed an alarming rise of intra-state and interstate conflicts in recent decades, most of them caused by politics especially pre and post elections. These conflicts have taken a huge toll in terms of human lives lost, the suffering of refugees and internally displaced people, and the destruction of the social fabric, physical infrastructure, and natural resources, we need join hands to protect peace,” he was quoted as saying.

  GPFTZ is the Tanzanian Chapter of Global Peace Foundation (GPF), an international non-sectarian, non-partisan and nonprofit making organization with its headquarters in Washington DC which promotes an innovative and values-based approach to peace building that is guided by the vision of OneFamilyunderGod.

  GPF engages and organizes a global network of public and private sector partners who develop community, national, and regional peace building models as the foundation for ethical and cohesive societies.

  GPF’s records of effectiveness are seen in hot spots in Africa, Asia and other parts of the world.

  The peace campaign launch comes hardly two months before the general elections and one month since the 21st Global Peace Leadership Conference took place in Zanzibar that attracted eight former African presidents, top government, religious and business leaders, entrepreneurs, women and youth leaders and other influential public figures from over 20 countries.

  The conference, held at the Melia Hotel in the Spice Island from July 21-25, 2015, was aimed at promoting peace, security and sustainable development in East Africa.

  The four-day conference was attended by former Zambia President Rupiah Banda and former presidents Amani Abeid Karume (Zanzibar), Olusegun Obasanjo (Nigeria), GirmaWolde- Giorgis (Ethiopia) and James Mancham (Seychelles) as well as former Kenya Prime Minister Raila Amoro Odinga.  0 0

   Waziri wa Fedha wa Zanzibar, Mheshimiwa Omari Yusuf Mzee, akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa huduma ya Benki yako Kiganjani ya Zantel pamoja na benki ya PBZ. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Zantel, Pratap Ghose, akifuatiwa na Mwenyekiti wa bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Salmin Senga, na mwisho kulia ni Mkurugenzi wa benki ya PBZ, Juma Mohammed.
   Mkurugenzi wa Zantel, Pratap Ghose akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma mpya kati ya kampuni yake na benki ya PBZ, Benki Yako Kiganjani.
   Mkurugenzi wa Huduma ya Kifedha za simu za mtandao, Hashim Mkudi akielezea namna ya kutumia huduma ya Benki Kiganjani Mwako iliyozinduliwa kwa ushirikiano wa kampuni yake na benki ya PBZ.


  Mkurugenzi wa benki ya PBZ, Juma Mohammed akizungumza wakati wa kuzindua huduma ya Benki Kiganjani Mwako, inayoendeshwa na kwa ushirikiano wa benki yake na kampuni ya Zantel.

  Zantel yaingia ubia na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kutoa huduma za kibenki kupitia simu za mkononi

  Zanzibar, 31/8/2015: Kampuni ya simu ya Zantel leo imeingia ubia na Benki ya Watu wa Zanzibar, kwa ajili ya kutoa huduma za kibenki kwa wateja wao kupitia huduma ya simu ya Ezypesa.

  Makubaliano haya yatawawezesha wateja wa Ezypesa wenye akaunti za PBZ kufanya miamalakupitia simu zao za mkononi, kujua salio katika akaunti zao pamoja na kupata taarifa fupi za akaunti zao.
                                               
  Akizungumza wakati wa kuzindua ushirikiano huo, Waziri wa Fedha wa Serikali ya Zanzibar, Mheshimiwa Omari Yusuf Mzee, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo amesema ushirikiano kati ya Zantel na Benki ya Watu wa Zanzibar ni faraja kubwa kwa wananchi kwani itaongeza wigo na kurahisisha huduma za kibenki.

  ‘Ushirikiano kati ya benki ya PBZ na Zantel ni wa muda mrefu, na kwa uzinduzi wa huduma hii leo ambao umekuwa ukisubiriwa na Wazanzibari kwa muda mrefu wameweka historia’ alisema Mheshimiwa Mzee.

  Mheshimiwa Mzee pia alisema huduma hii imekuja kwa wakati muafaka, kwani asilimia kubwa ya Wazanzibar wana simu za Zantel na akaunti katika benki ya PBZ huku akiwachagiza makampuni kuoungeza huduma zaidi za kijamii kwa watu wa Zanzibar.

  Naye Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Pratap Ghose alisema ushirikiano baina ya PBZ na Zantel utawezesha ukuaji wa huduma ya EzyPesa ambayo imekuwa ni sehemu ya maisha ya watu wa Zanzibar

  “Ubia huu baina ya Zantel na PBZ utawarahishia wateja wetu katika kutumia huduma za benki katika kufanya miamala ya kifedha kutoka katika akaunti zao za PBZ kwenda kwenye akaunti zao za EzyPesa kwa njia rahisi na salama” alisema Ghose.

  Ghose aliongeza kwa kusema kuwa wateja wa Zantel sasa wataweza kutumia simu zao kufanya shughuli za kibenki na hivyo kuondoa usumbufu wa upatikanaji wa huduma za PBZ kwa mwananchi wa kawaida.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa PBZ, Juma Mohammed, alisema kwamba ubia huo utawawezesha wateja kutoa na kuweka fedha kwenye akaunti zao, kulipia huduma, kujua salio, kufanya miamala kutoka akaunti moja kwenda nyingine pamoja na kununua muda wa maongezi.

  ‘Huduma hii itafanya huduma za kifedha zipatikane kwa urahisi zaidi kwa wateja wetu kuliko ilivyokuwa awali, na pia itaboresha ubora wa huduma pamoja na kupunguza msongamano wa wateja hasa kipindi cha mwisho wa mwezi’ alisema Mohammed.

  Uzinduzi wa huduma hii kwa kushirikiana na PBZ inakuja kama ongezeko baada ya huduma ya awali ya TUKUZA inayotolewa na Ezypesa kwa wateja wote wa Zanzibar, wateja wanaweza kuanza kufurahia huduma hii moja kwa moja kwa kubonyeza namba *150*02#.

  ‘Zantel ina miundombinu ya kisasa na imara kuwezesha kufanya kazi sawasawa na kwa viwango vya dunia, hivyo wizara ya miundombinu inawahakikishia wazanzibar waipokee huduma hii kwa mikono miwili’ alisema Mkurugenzi wa Mawasiliano Zanzibar, Dkt Mzee Suleiman Mndewa.

  0 0


  0 0

  DSC01579

  Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kibaoni mjini Singida, Sundi Samike, akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi choo bora chenye matundu nane chenye thamani ya zaidi ya shilingi 16 milioni zilizotolewa na MO Dewji Foundation (shilingi 14 milioni) na Doris Mollel Foundation shilingi 2.3 milioni).
  DSC01583
  Mwakilishi wa Mo Dewji Foundation mkoani Singida, Duda Mughenyi, akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi choo bora chenye matundu nane shule ya msingi Kibaoni mjini Singida, chenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 16. Duda amewataka wakazi wa manispaa ya Singida, kujenga utamaduni wa kuchangia kwa hali na mali, uboreshaji wa mazingira ya shule, ili kuvutia wanafunzi kupenda shule.
  DSC01592
  Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundation ya jijini Dar-es-sa-laam, Doris Mollel, akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi choo bora chenye matundu nane ya shule ya msingi Kibaoni mjini Singida chenye thamani ya zaidi ya shilingi 16 milioni, kati ya fedha hizo, Mo Dewji Foundation imetoa shilingi 14 milioni na Doris Foundation shilingi 2.3 milioni.


  DSC01596
  Mwakilishi wa Mo Dewji Foundation mkoani Singida, Duda Mughenyi, (wa tatu kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundation, Doris Mollel (wa pili kulia) wakielekea kuzindua choo bora kipya cha shule ya msingi Kibaoni.
  DSC01600
  Mwakilishi wa MO Dewji mkoani Singida, Duda Mughenyi, (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundatin, Doris Mollel (wa tatu kushoto) kwa pamoja wakizindua choo bora kipya cha shule ya msingi Kibaoni chenye thamani ya zaidi ya shilingi 16 milioni. MO Dweji Foundation imechangia shilingi 14 milioni na Doris Mollel, shilingi 2.3 milioni.
  DSC01603
  Jengo la choo bora chenye matundu nane kilichojengwa kwa thamani ya zaidi ya shilingi 16 milioni kwa ushirikiano wa MO Dewji Foundation na Doris Mollel Foundation kitakachotumiwa na wanafunzi 842 wa shule ya msingi Kibaoni mjini Singida. (Picha na Nathaniel Limu).

  Na Nathaniel Limu, Singida
  WAZAZI/WALEZI wakazi wa halmashauri ya manispaa ya Singida, wamehimizwa kujenga utamaduni wa kuchangia kwa hali na mali uboreshaji wa mazingira ya shule, kama njia moja wapo ya kuwavutia wanafunzi kuhudhuria shule.

  Wito huo umetolewa na Mwakilishi wa MO Dewji Foundation mkoa wa Singida, Duda Mughenyi, wakati akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi choo bora chenye matundu nane chenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 16 kwa shule ya msingi Kibaoni mjini hapa, yenye jumla ya wanafunzi 842, kati yao wavulana ni 377 na wasichana ni 465.

  Alisema uzoefu unaonyesha kwamba mazingira ya shule yakiwa safi, vifaa vya kufundishia na kujifunzia viwepo vya kutosha , maji safi na salama yawepo na vyoo bora vinavyokidhi mahitaji, hatua hiyo huwajengea mazingira mazuri wanafunzi , kujiendeleza kielimu.

  Akifafanua, alisema shule ya msingi ya Kibaoni ilikaribia kufungwa kutokana na kukosa vyoo kwa ajili ya wanafunzi na wanafunzi,lakini Dewji Foundation na Doris Mollel Foundation, ilinusuru shule hiyo isifungwe baada ya MO Dewji Foundation kutoa shilingi 14 milioni na Doris Mollel kutoa shilingi 2,300,000.

  Duda alitumia nafasi hiyo kuwataka wanafunzi wakitunze na kudumisha usafi wa choo hicho ili kiweze kutumika kwa muda mrefu.

  Kwa upande wake Doris Mollel (Miss Singida 2014), alisema Foundation yake itaendelea kufadhili sekta ya elimu mkoani Singida kama njia ya kuwashukuru wakazi mkoani hapa kwa kumsapoti na kufanikisha kushinda nafasi ya Miss Singida mwaka jana.

  Awali Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kindai tarafa ya Mungumaji iliyoanzishwa mwaka 1975,Sundi Samike,alishukuru uongozi wa Mo Dweji Foundation na Doris Mollel Foundation, kwa kuifadhili shule hiyo ujenzi wa choo na kuinusuru kufungiwa.

  “Nitumie nafasi hii pia kulipongeza shirika la WaterAid Tanzania kwa uamuzi wake wa kufadhili ujenzi wa vyoo bora ambao ujenzi wake tayari umeishaanza.Aidha,nitoe wito kwa wazazi,wasaidie kwa hali na mali kuharakisha ujenzi huu”,alisema.

  0 0

  Mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu akizungumza na akinamama wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) na kuwaomba kushirikiana na kuhakikisha wanashinda na kupata heshima hiyo.Mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu akizungumza na akinamama wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) na kuwaomba kushirikiana na kuhakikisha wanashinda na kupata heshima hiyo.Baadhi ya wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) wakiwa katika mkutano na mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu jana katika Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu ya CCM Dodoma.Baadhi ya wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) wakiwa katika mkutano na mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu jana katika Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu ya CCM Dodoma.Mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu akizungumza na akinamama wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) na kuwaomba kushirikiana na kuhakikisha wanashinda na kupata heshima hiyo.Mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu akizungumza na akinamama wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) na kuwaomba kushirikiana na kuhakikisha wanashinda na kupata heshima hiyo.Mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu akizungumza na akinamama wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) na kuwaomba kushirikiana na kuhakikisha wanashinda na kupata heshima hiyo.Mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu akizungumza na akinamama wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) na kuwaomba kushirikiana na kuhakikisha wanashinda na kupata heshima hiyo.Mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu akizungumza na akinamama wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) na kuwaomba kushirikiana na kuhakikisha wanashinda na kupata heshima hiyo.Mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu akizungumza na akinamama wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) na kuwaomba kushirikiana na kuhakikisha wanashinda na kupata heshima hiyo.Baadhi ya wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) wakiwa katika mkutano na mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu jana katika Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu ya CCM Dodoma.Baadhi ya wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) wakiwa katika mkutano na mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu jana katika Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu ya CCM Dodoma.    MGOMBEA mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu amefanya mazungumzo na wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) na kuwaomba kuitumia vema heshima na nafasi waliopewa akinamama nchini ya kushika nafasi ya makamu wa rais kwa mara ya kwanza, hivyo kuhakikisha wanahamasisha wenzao ili CCM iweze kushinda na wanawake kutwaa heshima hiyo. Bi. Suluhu amesema hayo alipokuwa akizungumza na akinamama wa UWT mkoani Dodoma ikiwa pamoja na kutaja kipaumbele ambapo kimewekwa kwa akinamama katika ilani mpya ya CCM katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25, 2015. 

  Alisema atatumia nafasi yake kushawishi akinamama kipata vifaa na mazingira rafiki ya kuendesha kilimo cha kisasa ili waweze kukuza uchumi wao, pia kuwawezesha katika vikundi vya ujasiliamali ikiwa ni pamoja na kukomesha usumbufu ambao akinamama wafanyabiashara wamekuwa wakibughuziwa na mgambo wa jiji.

   Mgombea huyo alisema kupitia vikundi akinamama watawezeshwa na fungu la fedha shilingi milioni hamsini fedha ambazo zitatolewa kila kijiji maalumu kwa ajili ya kuwawezesha akinamama pamoja na vijana ili waweze kukuza mitaji yao. 

  Pamoja na hayo Bi. Suluhu alisema Serikali watakayoiunda itashughulikiwa changamoto anuai wanazokumbana nazo walemavu hasa akinamama ili kuwawezesha na wao katika ushindani. "...Kwa upande wa kilimo nitahakikisha nachochea kidogo kidogo ili wanawake wapate vitu kama pembejeo na vifaa vingine kuwawezesha kuendesha kilimo cha kisasa," alisema.Mmoja wa wajumbe wa kamati ya taifa ya kampeni za CCM, Bi. Ummy Mwalimu akitoa neno katika mkutano na wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) kwenye Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu ya CCM Dodoma.Mmoja wa wajumbe wa kamati ya taifa ya kampeni za CCM, Bi. Ummy Mwalimu akitoa neno katika mkutano na wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) kwenye Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu ya CCM Dodoma.Baadhi ya wajumbe wa kamati ya taifa ya kampeni za CCM (mbele) walioambatana na mgombea mwenza, Bi. Samia Suluhu wakiwa katika mkutano na wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) katika Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu ya CCM Dodoma.Baadhi ya wajumbe wa kamati ya taifa ya kampeni za CCM (mbele) walioambatana na mgombea mwenza, Bi. Samia Suluhu wakiwa katika mkutano na wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) katika Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu ya CCM Dodoma.Mke wa waziri Mkuu wa Tanzania, Mama Tunu Pinda akizungumza na wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) kabla ya mkutano huo na mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu jana kuanza katika Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu ya CCM Dodoma. Mke wa waziri Mkuu wa Tanzania, Mama Tunu Pinda akizungumza na wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) kabla ya mkutano huo na mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu jana kuanza katika Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu ya CCM Dodoma.Mmoja wa wajumbe wa kamati ya taifa ya kampeni za CCM, Bi. Asumpta Mshana akitoa neno katika mkutano na wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) kwenye Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu ya CCM Dodoma.Mmoja wa wajumbe wa kamati ya taifa ya kampeni za CCM, Bi. Asumpta Mshana akitoa neno katika mkutano na wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) kwenye Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu ya CCM Dodoma.Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) mkoani Dodoma, Bi. Salome Kiwaya akizungumza kabla ya mkutano huo na mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu jana kuanza katika Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu ya CCM Dodoma.Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) mkoani Dodoma, Bi. Salome Kiwaya akizungumza kabla ya mkutano huo na mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu jana kuanza katika Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu ya CCM Dodoma.Baadhi ya wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) wakiwa katika mkutano na mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu jana katika Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu ya CCM Dodoma.Baadhi ya wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) wakiwa katika mkutano na mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu jana katika Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu ya CCM Dodoma.Baadhi ya wawakilishi wa makundi anuai katika wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) wakitoa neno kuwawakilisha wajumbe wenzao katika mkutano huo na mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu jana katika Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu ya CCM Dodoma.Baadhi ya wawakilishi wa makundi anuai katika wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) wakitoa neno kuwawakilisha wajumbe wenzao katika mkutano huo na mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu jana katika Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu ya CCM Dodoma.Makundi ambalimbali ya akinamama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) mkoani Dodoma, wakimpa zawadi mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu katika Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu ya CCM Dodoma. 
  Makundi ambalimbali ya akinamama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) mkoani Dodoma, wakimpa zawadi mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu katika Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu ya CCM Dodoma.

   Alisema ilani ya CCM imetoa kipaumbele kwa huduma za afya hasa huduma za mama na mtoto ikiwa ni kutambua changamoto na matatizo wanayokumbana nayo akinamama eneo hilo.

   Alisema atadhibiti rushwa na matumizi mabaya ya dawa zinazopelekwa wizara ya afya kuhakikisha zinafanya kazi kama ilivyokusudiwa na kudhibiti urasimu. Aliongeza kuwa baada ya ujenzi wa shule za kata kufanikiwa akiingia madarakani anaongeza nguvu katika ujenzi wa mabweni ya wasichana ili kukabiliana na changamoto ya mimba kwa wanafunzi wasichana ambazo zimekuwa zikichangiwa na wao kutembea umbali mrefu na kupata changamoto njiani.

   Aidha aliongeza kuwa ili kuonesha Serikali ya CCM inawajali walimu itaunda chombo maalumu ambacho kitakuwa na kazi ya kushughulikia matatizo ya walimu pamoja na kukiwezesha kuhakikisha kinatimiza majukumu yake kiufasaha. 

   Aliwaomba akinamama kushirikiana kufanya kampeni na kuhakikisha CCM inashinda hivyo akinamama kupata fursa hiyo waliyopewa na CCM kwa sasa. "...Naombeni tushirikiane wote kufanya kampeni nyumba kwa nyumba, kitanda kwa kitanda na shuka kwa shuka ili kuhakikisha tunashinda maana hii ni zawadi kwa akinamama tujitahidi tuweze kushinda nafasi hii," alisema Bi. Suluhu.Baadhi ya wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) wakiwa katika mkutano na mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu jana katika Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu ya CCM Dodoma.Baadhi ya wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) wakiwa katika mkutano na mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu jana katika Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu ya CCM Dodoma.Baadhi ya wawakilishi wa makundi anuai katika wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) wakitoa neno kuwawakilisha wajumbe wenzao katika mkutano huo na mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu jana katika Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu ya CCM Dodoma.Baadhi ya wawakilishi wa makundi anuai katika wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) wakitoa neno kuwawakilisha wajumbe wenzao katika mkutano huo na mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu jana katika Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu ya CCM Dodoma.Baadhi ya wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) wakiwa katika mkutano na mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu jana katika Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu ya CCM Dodoma.Baadhi ya wanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) wakiwa katika mkutano na mgombea mwenza wa nafasi ya urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu jana katika Ukumbi wa NEC ofisi za makao Makuu ya CCM Dodoma.
   *Imeandaliwa na www.thehabari.com

  0 0

  bty
  Modewjiblog Operations Manager, Zainul Mzige taking a 'selfie' with the Nigerian Artist Mr. Flavour at Sir Seerwoosagur Ramgoolan International Airport upon our arrival in Mauritius.
  IMG_5901
  Head of delegation from Tanzania, Public Relations Manager at MultiChoice Tanzania Ltd, Barbara Kambogi pose for a photo with Tanzanian Journalists who have been invited to Mauritius to experience the biggest week in Africa's video entertainment, hosted by MultiChoice Africa.
  IMG_5906
  Invited guests from Botswana poses for a group photo.
  IMG_5912
  Comedian from Nigeria, Basket Mouth (left) pose for a photo with award winning singer and songwriter Mr.Flavour
  IMG_5913  
  The Guardian Newspaper Senior Reporter Sylivester Domasa with Nigerian Comedian Basket-Mouth (right) and award wining singer and song writer Mr.Flavour
  dav
  Invited guests mingle at the VIP Lounge upon their arrival.
  Dear readers.

  We are in Mauritius to experience the biggest week in Africa’s video entertainment, hosted by MultiChoice Africa.

  We have arrived at Sir Seerwoosagur Ramgoolan International Airport just some hours ago and the fun has already started.
  For the next five days, we will be treated to ‘ONLY THE BEST’ in video entertainment on the DStv and GOtv.

  We are here, and the only thing we have been encouraged, is to open our mind to experience television like we had never before and also to grab the opportunity to interact with various exciting channels that will engage with us and give an exclusive, in-depth and VIP experience of their content.
  I trust that throughout this event, I will have plenty of material to share with you.

  I look forward to give you an amazing Africa-inspired content live-in action.
  While am here definitely I will touch and rubbed shoulders with the stars of Hollywood, Nollywood, Bollywood and so much more. I am truly looking forward to sharing with you this exciting journey of television content discovery.

  0 0

    Msanii wa Reggae Princes Delyla akiongea na wadau wa Sanaa kwenye Jukwaa la Sanaa la Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) mapema wiki hii kwenye makao makuu ya Baraza hilo Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Msanii Mwasiti Almas na Afisa Sanaa kutoka BASATA Augustino Makame.
    Msanii wa kizazi kipya Mwasiti Almas(katikati) akisisitiza jambo wakati akiongea na wadau wa Sanaa kwenye programu ya Jukwaa la Sanaa la Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) linalofanyika makao makuu ya Baraza hilo Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Msanii wa reggare Princes Dalyla na Afisa Sanaa kutoka BASATA Augustino Makame.
    Mtafiti na Msanii wa Reggae Innoncent Nganyagwa akifafanua jambo kwenye Jukwaa la Sanaa la Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) mapema wiki hii. Kulia kwake ni Msanii mwenzake wa Reggae Princes Delyla. 
   Msanii Mwasiti akisakata muziki sambamba na mashabiki wake kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA.


   Msanii Princes Dalyla akitoa burudani kwa wadau wa Jukwaa la Sanaa la BASATA mapema wiki hii
    Sehemu wa wadau wa Sanaa waliohudhuria Jukwaa la Sanaa wiki hii wakifuatilia kwa makini burudani.


  NEWS RELEASE
  MSANII mahiri wa muziki wa kizazi kipya Mwasiti Almas amewataka wasanii wenzake kuwa wabunifu katika kutanua mianya ya kujiingizia kipato na kuhakikisha wanazingatia maadili wawapo jukwaani ili kulinda hadhi zao.


  Mwasiti ameyasema hayo mapema wiki hii wakati akijibu maswali ya wadau wa Jukwaa la Sanaa linalofanyika kwa mwezi mara mbili ziku za Jumatatu makao ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Ilala Sharif Shamba.


  Wadau hao wa Sanaa walitaka kujua ni kwa nini wasanii wengi hufilisika mara wanaposimama kufanya shughuli za Sanaa na wengine wamekosa ubunifu wawapo kwenye maonesho au wanapozalisha kazi zao hali ambayo inawafanya watumie sehemu za siri za miili yao katika kutafuta mvuto kwa mashabiki.


  “Wasanii wengi wanang’ang’ania kwenye sanaa pekee. Hawawekezi kwenye miradi mingine. Kuwa na umaarufu si kuwa na fedha bali umaarufu ni njia tu inayokusaidia kuingia kwenye sekta na miradi mbalimbali kwa ajili ya kujiimarisha kimapato” alisema Mwasiti wakati akifafanua suala la wasanii kufilisika mara wanapochuja kwenye Sanaa.


  Alizidi kueleza kwamba wasanii waliopo sasa hawana budi kutambua kwamba hawatakuwepo muda wote bali kuna leo na kesho hivyo lazima kuiandaa kesho sasa.


  “Umri wa wasanii unaenda, waliopo sasa hawawezi kuwepo kesho kwani kuna wasanii wengi wanaibuka na lazima wapate nafasi. Ni muhimu sana kwa wasanii kuliona hili. Huko nyuma kaka na dada zetu walipata shida ilikuwa ngumu lakini kwa sasa wasanii tunapata kipato na baadhi wanajitahidi kuwekeza” alisema Mwasiti.


  Kuhusu wasanii kufanya maonesho yasiyo na maadili, Mwasiti alisema kwamba inasikitisha sana kwani katika hali ya kawaida msanii anayejitambua na kuthamini utu na hadhi yake hawezi akafanya maonesho ya uchi kwani matendo ya wasanii huathiri sana jamii inayowazunguka.


  “Matendo yetu wasanii huathiri sana jamii inayotuzunguka. Sisi ni binadamu na tuna leo na kesho. Sipendi siku zijazo watoto wetu waje kuuliza na kushangaa yale tuyafanyayo sasa maana yataendelea kuonekana” alisema Mwasiti.


  Katika Jukwaa hilo BASATA lilimwalika Mwasiti na wa msanii mwenzake wa kike Princes Dalyna anayefanya muziki wa reggae ili kueleza historia, changamoto na mafanikio waliyoyapata katika kazi zao za Sanaa.   

  0 0

   Mwenyekiti wa Elimu Saccos Ahmedi mohd akitoa hotuba ya makaribisho kwa mgeni Rasmi katika Mkutano maalum wa Elimu Saccos uliofanyika Amaan Judo Zanzibar.
   Mgeni Rasmi Mrajisi wa vyama vya Ushirika Hamis Daudi Simba akitoa hotuba ya ufunguzi katika mkutano wa maalum wa Elimu Saccos uliofanyika Amaan Judo Zanziobar,kulia yake ni Mwenyekiti wa Elimu Saccos Ahmed Mohd na kushoto yake ni Katibu wa Elimu Saccos Salma Simai.
  Baadhi ya Wanachama wa Elimu Saccos waliohudhuria katika Mkutano maalum wa Elimu Saccos uliofanyika Amaan Judo Zanzibar.

  PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

  0 0

    picha no:1 Dokta Gao Yun Lai akimpima presha na sukari bwana Mohd Ali mkazi wa Kisauni upimaji huo ulifanyika katika kijiji  cha kisauni Zanzibar. 
    Dokta Fadhil Mohd ambae ni dokta dhamana kanda ya Unguja akitoa maelezo kwa waandishi wa habari hawapo pichani.
  Wananchi mbalimbali wakipatawa  huduma za matibabu katika kijiji cha Kisauni zanzibar.
  Picha na Abdalla Omar habari maelezo zanzibar.

  Mwashungi Tahir,     Maelezo-Zanzibar  01-09-2015
  JUMLA ya madaktari bingwa tisa  kutoka nchini  china wakishirikiyana na madaktari wa hapa Zanzibar  wameweza kutoa huduma za afyakwa wananchi wa shehia ya Kisauni  kwa kuwapima  na kuweza kujua afya zao na kuwapatia huduma za matibabu.

  Akizungumza na mwandishi wa  habari hizi huko katika shehia ya Kisauni wilaya ya Magharibi B Dr Fadhil Mohammed ambae ni dhamana ya kanda ya Unguja  amesema madaktari hao wamekuja kutoa huduma za afya za jamii  hapa Zanzibar.

  Amesema madaktari hao wanatoa huduma hizo vijijini kwa kila baada ya miezi mitatu wanakwenda katika kijiji chengine kwa lengo la kuwarahisishia huduma hiyo watu hao na kuwapelekea huduma hiyo katika maeneo yao.

  “Lengo ni kuwapelekea wananchi huduma hiyo karibu na maeneo yao ili waweze kupata urahisi wa kuweza kujua afya zao” alisema daktari huyo.
  Sambamba na hayo Fadhil amesema jitihada hizi ambazo zinafanywa na madaktari hao na kwa kushirikiana na Wizara ya Afya  ni kuweza kuimarisha huduma hiyo kupitia vijijini ili kuweza kuwapa muamko wananchi na kuweza kujitokeza kupima afya zao kwa urahisi.

  Madaktari hao bingwa ambao ni maspeshalisti wa maradhi mbalimbali wameweza kuwapima wananchi  maradhi mbali mbali na kuweza kuwapatia matibabu hapo hapo bila ya usumbufu wowote.

  Maradhi wanayopima na kutoa huduma ni pamoja na ukimwi, koo, pua, meno, presha magonjwa ya moyo , ganzi, sukari na matatizo ya mkojo na maradhi mengineyo.

  Pia wanatoa huduma za akinamama za uzazi wa mpango kwa njia salama na huduma za watoto ambapo akinamama wengi wameweza kujitokeza  kwa kujipatia huduma hiyo.

  Nae mratibu wa afya wa mama na mtoto Bi Fatma Ussi Yahya amesema amefurahishwa sana na akinamama wa kijiji hicho pamoja na majirani kwa kuweza kufika kwa wingi katika kujipatia na huduma hiyo.

  Pia kati ya madaktari hao bingwa Dr GAO YUNLAI amesema amefarijika sana kuona wananchi wameweza kujitokeza kwa wingi na kupima vipimo vya aina ya maradhi mbali mbali ikiwemo maradhi yasiyoambukuza ya kisuari na presha.

  Sheha wa shehia hiyo ya Kisauni Hija Suleiman Othman amewataka wananchi wake wasiidharau huduma hizi zinapofika vijijini kwani hiyo ni bahati adhimu kwa wananchi wa visiwa hivi.

  “Nimefurahi kuona wananchi wangu wameweza kuhamasika kwa kujitokeza kwa wingi kwenye huduma hizi ambazo wameletewa hapa hapa na pia huduma hizi zinatolewa bure kupitia Wizara ya Afya.” Alisema sheha huyo.

  Kwa upande wa wananchi Bi M wanajuma Omar kutoka mitondooni amesema ameweza kushiriki vizuri katika kujipatia vipimo na kuweza kujifahamu afya yake ambayo vipimo vyote alivyoima ameweza kujigundua kuwa yuko salama.

  Amewataka akinamama na akinababa kuweza kujitokeza kwa wingi kupima afya zao na kuweza kujitambua na kupatiwa matibabu ambapo matibabu hayo yanatolewa kwa wingi  hapo hapo na kuweza kuwaambia kuwa kinga bora kuliko tiba.

  Madakatari hao ni maalum Chinese medical team  wapo hapa visiwani kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi na kuweza kuwapa matibabu watu wote.

older | 1 | .... | 624 | 625 | (Page 626) | 627 | 628 | .... | 1898 | newer