Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 623 | 624 | (Page 625) | 626 | 627 | .... | 1896 | newer

  0 0

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi inatarajia kuweka Wazi Daftari la Awali la Wapiga Kura katika Mikoa yote ya Unguja na Pemba kuanzia tarehe 03/09/2015 hadi tarehe 07/09/2015 ili Umma uweze kupata nafasi ya kulikagua Daftari la Awali na kutoa taarifa za kufanyiwa marekebisho pale inapostahili.

  0 0

   Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia, akiwahutubia wananchi katika mkutano huo leo
   Umati wa wananchi ukimsikiliza Mgombea ubunge wa jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, alipohutubia katika mkutano wa kampeni wa mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia, katika eneo la Msange, Singida Kaskazini, leo.
   Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimnadi Mgombea Ubunge Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, katika mkutano uliofanyika katika jimbo hilo leo. 
   Umati wa wananchi ukimsikiliza Mgombea Mwenza kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu alipohutubia mkutano wa kampeni katika eneo la Msange, Singida Kaskazini, leo.   Baadhi ya viongozi na wananchi wakijimwayamwaya kwa furaha  wakati wa mkutano wa kampeni wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan
   Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwasalimiabaadhi ya viongozi, baada ya kuwasili  katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hilo leo.
   Wananchi waliojawa na furaha wakimkimbilia kumlaki, Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu, alipowasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo, katika viwanja vya Kyengege, Iramba mkoani Singida leo
   "Baba hakimbii nyumba" Kijana akiwa na bango linalowasema wanaaokimbia  kutoka CCM kwenda upinzani kutokana na kutochaguliwa katika nafasi za uongozi, kijana huyo alipokuwa kwenye mkutano wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu, uliofanyika leo Iramba mkoani Singida.
   Mgombea Ubunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba akiselebuka na baadhi ya viongozi na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo, katika eneo la Kyengege, Iramba mkoani Singida, leo.
   Mgombea Ubunge jimbo la Iramba Magharibu, Mwigulu Nchemba akiomba kura, wakati wa mkutano wa kampeni za CCM wa mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, uliofanyika leo katika jimbo hilo.
   Wananchi wakimsikiliza Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia wakati wa mkutano wa kampeni za CCM wa mgombea Mwenza huyo, uliofanyika leo katika jimbo hilo.
   Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba katika mkutano uliofanyika katika jimbo hilo leo. Kushoto ni Mgombea wa Ubunge jimbo la Mkalamo, Allan Kiula
   Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la Mkalamo, Allan Kiula, katika mkutano uliofanyika katika jimbo hilo leo.
  Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni, wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan uliofanyika leo, kwenye Ofisi ya CCM mkoa wa Singida. Picha na Bashir Nkoromo).

  0 0

   Vijana wanaunda kundi  la  Timu Makorokoro  wa  wilaya ya Temeke  jijijini Dar es Salaam, wakikongo nyoyo za mashabiki waliojitokeza kwenye onyesho la robof wa shininali ya shindano la Dance100%2015,lililofanyika kwenye viwanja vya Don bosco Oysterbay mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania,Makundi 10 kati ya 15 yalifanikiwa kuingia nusu fainali zitakazofanyika hivi karibuni.
   Vijana wanaaunda kundi la  timu ya Shamba kutoka Temeke wakionyesha umahiri wa  kusakata dansi wakati wa robo fainali ya shindano la Dance 100% lililofanyika kwenye viwanja vya Donbosco Oysterbay jijini Dar es Salaam ,mwishoni mwa wiki.Shindano hilo  iliandaliwa  na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania. Makundi 10 kati ya 15 yalifanikiwa kuingia nusu fainali zitakazofanyika hivi karibuni.


   Vijana wanaounda kundi la The Winner Crews kutoka Kiwalani  jijini  Dar es Salaam, wakikongo nyoyo za mashabiki waliojitokeza kwenye onyesho la robofainali ya  shindano la Dance100%2015,lililofanyika kwenye viwanja vya Donbosco  Oysterbay jijini Da res Salaam  ambapo makundi 10 yalitinga nusu fainali zitakazofanyika hivi karibuni. Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.

   Kundi la wasichana pekee la Cute Babies  kutoka Keko  wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam wakionyesha umahiri wao  wa kudansi wakati wa robo fainali ya shindano la Dance 100% lililofanyika katika viwanja Don bosco Oysterbay  jijini ambapo makundi 10 yalitinga nusu fainali zitakazofanyika hivi karibuni, Shindano hilo liliandaliwa na  EATV na kudhaminiwa  na Vodacom Tanzania.
  Mashabiki wakifuatilia mashindano hayo.   Makundi kumi kati ya makundi 15 yaliyoshiriki katika kinyang’anyiro cha kuingia katika nusu fainali ya mashindano yanayokuwa kwa kasi hapa nchini ya Dance 100% yanayoandaliwa na kituo cha televisheni cha East Africa(EATV) chini ya udhamini wa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania,yanaendelea ambapo mwishoni mwa wiki tulishuhudia hatua ya robo fainali kufanyika katika uwanja wa Don Bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam na kushirikisha makundi 15 kutoka wilaya 3 za mkoa wa Dar es Salaam. 

   Makundi yaliyofanikiwa kuingia nusu fainali ni Wazawa Crew,Majokeri,Quality boys,The best,The best boys kaka zao,Team Makorokocho,The winners, The W.D, Cute babies na Team ya shamba. Mratibu wa mashindano hayo,Happy Shame,alisema kuwa katika kinyang’anyiro cha robo fainali hiyo walipata makundi 10 hayo ambayo yameingia moja kwa moja katika ngazi ya nusu fainali. 

  “Huu ni mwaka wa nne East Africa Televisheni tunaandaa mashindano haya chini ya udhamini wa Vodacom Tanzania na mwaka hadi mwaka mashindano haya yamekuwa yakiongezeka kupata umaarufu na kuwavutia vijana wengi kila kona ya nchi yetu ambao wamekuwa wakijitokeza kushiriki”Alisema Shame. 

   Shame, aliongeza kwamba kundi litakaloibuka na ushindi katika mashindano haya ambayo pia yamekuwa yakionyeshwa na kituo cha televisheni cha East Afrika kila jumatano saa moja kamili usiku,litajishindia kitita cha shilingi milioni 5. 

  Naye Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania ambao ni wadhamini wakuu wa mashindano haya,Matina Nkurlu alisema kuwa Vodacom inatoa udhamini kwa kutambua kuwa muziki na michezo ni maeneo ambao yanaweza kutoa ajira kwa vijana na kuweza kuwakwamua kimaisha.

   Alisema kuwa Vodacom inatambua kuwa jukumu la kukabiliana na tatizo la ajira hapa nchini sio la serikali peke yake bali pia ni la watu wote ikiwemo makampuni,taasisi za umma na za binafsi na ndio maana siku zote imekuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono jitihada za kupambana na tatizo la ajira kupitia nyanja mbalimbali ikiwemo michezo , burudani na huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo. 

  “Vodacom tunaamini kuwa vijana wanaweza kuleta mapinduzi makubwa katika sekta mbalimbali iwapo watawezeshwa,hivyo tunadhamini mashindano haya tukiamini kuwa vijana wenye vipaji wanaoshiriki wataweza kujitangaza na kujulikana ambapo katika siku za usoni ni rahisi kujiajiri kupitia katika sanaa”Anasema Nkurlu. 

   Aliwataka vijana waamke hususani wasichana wasibaki nyuma na watumie fursa kama hizi ili waweze kujikomboa kiuchumi 
  “Suala la ajira sio kufanya kazi ofisini tu bali kuna njia nyingi za kujiajiri na kujipatia mapato mojawapo ikiwa ni kupitia michezo,muziki na sanaa nyingine na Vodacom siku zote tutakuwa mstari wa mbele kuunga mkono jitihada za vijana kujikwamua kiuchumi”Alisisitiza Nkurlu.

  0 0

   Mwigulu Nchemba  akisalimiana na wananchi  Bukombe Mkoa wa Singida wakati wa mkutano wa kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa Chama cha Mapinduzi.
   Mwigulu Nchemba akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita Ndg.Msukuma "KING"
   Mshindi wa nafasi ya Ubunge wa Viti Maalum Mkoa wa Geita Bi.Vick Kamata akiwashukuru na kuomba kura kwa Wananchi wa Bukombe wampigie J.P.Magufuli ifikapo tar.25.10.2015
   Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita Ndg.Joseph Msukuma akizungumza na Wananchi wa Bukombe kuwa yupo tayari kuzunguka Nchi nzima kuinadi Ilani ya CCM, Pia kumnadi Mgombea Urais wa CCM Dk.John Pombe Magufuli kwasababu ndiye Mgombea pekee mwenye dhamira ya dhati yakuwatumikia watanzania tangu akiwa Naibu Waziri.
   Sehemu ya Mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye Mkutano wa kampeni uliofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Bukombe.
   Mwigulu Nchemba akizungumza na wananchi wa Bukombe Mkoa wa Singida wakati wa mkutano wa kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa Chama cha Mapinduzi.

   "Tunahitaji Rais Mchapa kazi,sio Rais aliyezungukwa na Genge la wapiga Dili"Mwigulu.   Mwigulu Nchemba akiwapungia Mkono wananchi waliofurika kusikiliza Ilani ya chama cha Mapinduzi hii leo Bukombe.


  "CCM ni Ile Ile"

   Wanabukombe wakifurahia Mkutano wa Chama cha Mapinduzi,Wameahidi kuwa Miaka 5 walioyokuwa na Prof.Kahidi wa CHADEMA imekuwa yauchungu sana kwao,Hivyo kwa Uchaguzi huu kura zote kwa Dotto wa CCM. 
   Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa mwaka2015 ambayo Madiwani,Wabunge na Mgombea Urais wa CCM ataitumia kutekeleza Shughuli za Maendeleo Nchini Tanzania.

  Mwigulu Nchemba akimnadi Mgombea wa Ubunge Jimbo la Bukombe Ndg.Dotto Mashaka.
   Sehemu ya Wananchi waliojitokeza kwenye Mkutano huo.

  Picha na Sanga Jr.

  0 0

   Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anna Makinda akiwa  katika Mkutano wa Kumi wa  Maspika  Wanawake uliofanyika kwa siku mbili  hapa  Umoja wa Mataifa, Mkutano wa Maspika Wanawake, umetangulia Mkutano wa Nne wa Maspika zaidi ya 180 unaoza leo jumatatu hapa Umoja wa Mataifa.
  Sehemu ya  Wajumbe wa Mkutano wa Kumi wa Maspika  wanawake,   mkutano  uliojadili mbinu za kuchagiza  usawa wa kijinsia, miaka 20 baada ya Beijing pamoja na  kuhakikisha utekelezaji  wa malengo 17  ya Maendeleo Endelevu Baada ya 2015.
    Maspika  Wanawake wakiwa  katika picha ya pamoja  na Rais wa IPU Bw.  Choedhury Saber na  Katibu Mkuu wa IPU Bw. Martin Chungong wakati wa mkutano wao wa siku mbili uliofanyika  jumamosi na jumapili, ukitangulia  mkutano wa nne wa Maspika  wa  Mabunge.


  Na Mwandishi Maalum, New York
  MKUTANO wa Nne  unaowakutanisha Maspika  180 na Manaibu Spika 35 kutoka nchi 140,  unaanza leo ( jumatatu) hapa Makao Mkuu ya Umoja wa Mataifa.


  Mkutano  huu wa siku tatu na  ambao umeandaliwa  na  Chama cha Mabunge Duniani ( IPU), utafunguliwa na Rais wa  IPU  Bw. Chowdhury Saber na Katibu Mkuu wa Umoja wa Matafa,  Ban Ki Moon.


  Spika wa Bunge  la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe. Ann Makinda  anaongoza  ujumbe wa Tanzania katika mkutano huu.

   Mkutano ambao  Maspika wanatarajiwa kujadiliana kwa kina namna ya kukabiliana na changamoto za Amani, Demokrasia na Maendeleo kwa  maono ya Kibunge.


  Mkutano wa Nne wa Maspika,  ulitanguliwa na   Mkutano wa Kumi   wa  Maspika wanawake,  mkutano  uliofanyika kwa siku mbili ( jumamosi na Jumapili). Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe. Ann Makinda ameshiriki kikamilifu na  kuongoza baadhi ya  mikutano.


  Mkutano wa  Nne wa Maspika ni sehemu ya  mfululizo wa mikutano ya Maspika hao  na ambayo imekuwa  ikifanyika kuelekea Mkutano wa Kilele wa Viongozi wakuu wa Nchi na Serikali utakaofanyika wiki chache zijazo ambapo watapokea na kupitisha  Ajenda Mpya za  Maendeleo Endelevu  baada ya 2015.
  0 0  0 0

   Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Ismail Juma(kushoto) akikabidhi jezi kwa kapteni wa timu ya G Unity Fc kwa ajili ya mchezo wa fainali uliofanyika katika kiwanja cha Kipunguni B katika kata ya Kipunguni manispaa ya Ilala jijini Dar. Ambapo timu ya G Unity FC waliibuka washindi baada ya kuichapa timu ya Sukuma Land Fc bao 5 kwa 2.
    Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Ismail Juma(kushoto) akikabidhi jezi kwa kapteni wa timu ya Sukuma Land FC wakati wa mchezo wa fainali wa kombe la Madereva bodaboda wa kata ya Kipunguni.Wa pili kushoto ni ASP Mbunja Matibu kutoka Traffic Makao Makuu.
  Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Eliaichi Remmy(kushoto) akitoa somo kwa madereva bodaboda kuhusu Mfuko wa Pensheni wa PSPF hasa katika uchangiaji wa Hiari(PSS) waliofika katika mchezo wa fainali katika uwanja wa Kipunguni B

  Mmoja wa Madereva Bodaboda akiendelea kupewa faida za mfuko wa Uchangiaji wa Hiari(PSS) kutoka kwa Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Ismail Juma(kushoto)
  Mmoja wa madereva wa Bodaboda akijisajili kwenye mfuko wa (PSPF) kupitia (PSS) kwa ajili ya kuendelea kupata huduma zilizobora na  zenye uhakika kulia ni Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Eliaichi Remmy 
  Mmoja wa madereva wa Bodaboda akijiunga kwenye mfuko wa (PSPF) kupitia (PSS) ambapo kila mtu anaweza kujiwekea akiba kupitia kwenye mfuko huo wa hiari wakati wa mchezo wa fainali.
  Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Eliaichi Remmy(kushoto) akiwasajili madereva wa Bodaboda kwenye mfiko wa Uchangiaji wa Hiari(PSS)  wakati wa mchezo wa fainali wa Madereva bodaboda ambapo G Unity aliibuka mshindi kwa kumchapa Sukuma Land bao 5-2
  Vijana waliofika katika mchezo wa fainali wakisoma vipeperushi vya mfuko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF ambapo mfuko huo ulidhamini ligi hiyo iliyoendeshwa kwa wiki nzima
  Mmoja wa Madereva Bodaboda akisoma maelekezo ya jinsi ya kutuma pesa kwenye akaunti kwenye mfuko wa Uchangiaji wa Hiari(PSS) mara baada ya kupatiwa kitambulisho cha uanachama wa mfuko wa PSPF.
  Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Eliaichi Remmy(kushoto) akimjazia fomu ya mfuko wa Uchangiaji wa Hiari(PSS) mama aliyekuja kushabikia timu yake wakati wa fainali ya Kombe la Madereva bodaboda
  Maafisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF,waratibu wa michezo hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja na Timu ya Sukuma Land ambapo katika mchezo huo timu hiyo iliibuka mshindi wa pili baada ya kufungwa na timu ya G Unity Fc kwa mambao 5-2.
   
  Maafisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF wakiwa kwenye picha ya pamoja na waratibu wa michezo hiyo pamoja na Timu ya G Unity Fc walioibuka washindi wa wa kwanza baada ya kufunga timu ya Sukuma Land Fc mabao 5 -2, mchezo huo uliofanyika katika kiwanja cha Kipunguni B.


  Mchezaji wa Timu ya Sukuma Land Fc akiwatoka mabeki wa G Unity Fc ambapo katika mchezo huo timu ya G Unity Fc iliibuka mchindi wa mashindano hayo
  Ilikuwa ni burudani katika mchezo wa fainali kati ya Timu ya G Unity Fc na Sukuma Land Fc
  Gori kipa wa timu ya G Unity FC akijifunga gori wakati wa mchezo wa fainali uliopigwa kwenye uwanhja wa Kipunguni B
  Wachezaji wa Timu ya G Unity Fc wakishangilia baada ya kupata bao wakati wa mchezo wa fainali

  Mbwembwe za mashabiki katika fainali hizo
  Hizi ndizo zawadi zilizotolewa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF kwa mshindi wa kwanza mpaka wa nne katika mashindano ya mpira wa miguu kwa madereva bodaboda wa kata ya Kipunguni amabapo mshindiwa kwanza aliondoka na Mbuzi wawili na seti moja ya jezi, mshindi wa pili aliondoka na mbuzi mmoja na seti moja ya jezi, mshindi wa tatu aliondoka na seti moja ya jezi na mshindi wa nne aliodoka na mpira mmoja.
  Mkurugenzi mtendaji wa kata ya Kipunguni na Kivule Dr. Kadry Pinde ambaye alikuwa ni Mgeni rasmi katika mchezo wa fainali akikabidhi mpira kwa kapteni wa timu ya Kilimani Fc walioibuka washindi wa wa nne katika mashindano ya mpira wa miguu kwa madereva Bodaboda wa kata ya Kipunguni. Wa kwanza kushoto ni Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Ismail Juma.
  Mkurugenzi mtendaji wa kata ya Kipunguni na Kivule Dr. Kadry Pinde akiwakabidhi zawadi ya seti ya jezi timu ya Loliondo Fc baada ya kuibuka mshindi wa Tatu katika mashindano hayo.
  Kapteni wa timu ya Sikuma Land Fc akipokea seti ya jezi mmoja na Mbuzi mmoja baada ya kuibuka washindi wa pili katika mashindano ya mpira wa miguu kwa madereva bodaboda kutoka kwa Mkurugenzi mtendaji wa kata ya Kipunguni na Kivule Dr. Kadry Pinde ambaye alikuwa mgeni rasmi katika fainali hiyo. Wa kwanza kushoto ni ASP Mbunja Matibu kutoka Traffic Makao Makuu, wa pili kushoto ni Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Eliaichi Remmy
  Washindi wa mashindano ya mashindano ya mpira wa miguu kwa madereva Bodaboda wa kata ya Kipunguni wakisalimiana mgeni rasimi wakati wa kukabidhiwa zawadi zao
  Mkurugenzi mtendaji wa kata ya Kipunguni na Kivule Dr. Kadry Pinde akikabidhi seti ya jezi na mbuzi wawili wa kapteni wa timu ya G Unity Fc ambao waliibuka washindi wa mashindano ya mpira wa miguu kwa madereva Bodaboda wa kata ya Kipunguni baada ya kuichakaza timu ya Sukuma Land Fc bao 5-2
  Mashabiki wakiendelea kufuatia kinachijiri uwanjani

  MASHINDANO ya ligi wa mpira wa miguu kwa madereva bodaboda yahitimishwa na wadhamini wa mashindano hayo ambao ni mfuko wa Pensheni wa PSPF kwa kuweza kuwasajiri wachezaji katoka mfuko wa hiari wa PSS. Ligi hiyo iliyodumu ndani ya siku saba (7) ambapo alikuwa akitafutwa mshindi atakayeweza kuwa balozi mzuri wa mfuko wa penshenI wa PSPF yamemalizika kwa timu 32 kumenyana vikali na timu  ya G Unity kuibuka kinara ambapo timu hiyo ndiyo iliyotawazwa na kuwa balozi wa PSPF katika kata ya Kipunguni  mara baada ya fainali iliyohusisha timu ya Sukuma Land FC na G Unity Fc na hatimaye timu yaG Unity kuibuka kinara kwa bao 5 kwa2 katika fainali iliyopigwa katika kiwanja cha Kipunguni B.


  Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Ismail Juma alikabidhi jezi za kuchezea fainali kwa timu mbili zilizo fuzu kuingia katika fainali hizo ambazo ni G Unity Fc na Sukuma Land FC alisisitiza wachezaji wote kuweza kijiunga na mfuko wa pensheni wa PSPF fainali hizo za mashindano hayo ya ligi ya madereva bodaboda wa Kipunguni ambayo yaliweza kuhitimishwa na Mkurugenzi mtendaji wa kata ya Kipunguni na Kivule Dr. Kadry Pinde ambapo aliweza kuwaasa vijana waweze kujihusisha na kufanya kazi kwa bidii na kuweza kuhifadhi mafao yao katika mfuko wa pensheni wa PSPF.


  Msaidizi wa Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Josephat Sylvery Tirumanywa naye alitoa neno kuhusu usalama barabarani na kuwashukuru wachezaji kwa kucheza ligi hiyo kwa usalama na kumalizika kwa amani na hata hivyo aliwasisitizakuwa watu wote wanaotumia vyombo vya moto kuwa makini pindi wawapo barabarani.
  0 0

  IMG_5298
  Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema (katikati) kabla ya kuanza zoezi la usafi katika soko la Temeke Stereo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
  (Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

  Na Mwandishi wetu
  KATIKA kuadhimisho miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa (UN) wafanyakazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Kimataifa walijumuika na wakazi wa Temeke katika kufanya usafi kwenye soko la Temeke Stereo.

  Shughuli hiyo wameifanya baada ya wiki iliyopita kufanya shughuli za upandaji miti katika miteremko ya mlima Kilimanjaro, wakiwa katika miteremko ya milima Kilimanjaro walipanda miti 2,000.

  Shughuli hizo za kufanya usafi ambazo ziliongozwa na Mratibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez, zilifanyika katika juhudi za kuleta uhalisia wa utunzaji wa mazingira kama umoja huo unavyofanya.

  Akizungumza katika shughuli hizo Mkuu wa wilaya ya Temeke, Sophia Mjema, ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa aliupongeza Umoja wa Mataifa kwa kusherehekea miaka 70.

  “Nachukua nafasi hii kupongeza watu wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kwa kufanya shughuli mbalimbali kuelekea maadhimisho ya miaka 70 kwa kupanda miti 2,070 kwenye miteremko ya Mlima Kilimanjaro na hili tendo la leo la usafi kama mwendelezo wa kaulimbiu inayohimiza utunzaji wa mazingira ya“ Sayari moja, watu bilioni 7, Ulinzi wa mazingira ni wajibu wetu,” alisema.

  Akisisitiza umuhimu wa kutunza mazingira na usafi, Mkuu huyo wa wilaya alisema wajibu wa kutunza mazingira ni wa kila mtu.
  IMG_5365
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akitoa salamu za Umoja wa Mataifa katika kuadhimisha miaka 70 ya Umoja wa Mataifa ikiwemo kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii kwa wananchi na wafanyabiashara wa soko la Temeke Stereo mwishoni mwa juma. Kushoto ni Kaimu Mwakilishi Mkazi wa FAO nchini, Patric Otto. Wa tatu kulia ni mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya Temeke, Sophia Mjema, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (wa pili kulia) na Mkuu wa Idara ya Usafi na Mazingira manispaa ya Temeke, Ally Hatibu.

  “Kutunza mazingira si wajibu wa mtu mmoja. Ni wajibu wako kama ilivyo kwa jirani yako. Kunapokuwepo na watu wengi mara nyingi hutokea watu ambao hawajali wala kuona umuhimu wa kutunza mazingira, umuhimu wa kufanya haya.

  “ Nawaomba wote mlioshiriki katika shughuli hii leo kuwa watu wa kuchunga mazingira katika maeneo yenu mnayofanyia kazi na majumbani kwenu.Hakikisheni mnafundishana na majirani zako katika suala hili na kuhakikisha kwamba kila mmoja anayekuzunguka anawajibika katika kutunza mazingira.”

  Akisisitiza menejimenti ya mazingira, Rodriguez, alizungumza kwamba mabadiliko ya tabia nchi na mazingira endelevu ndio ajenda kuu katika malengo endelevu ya maendeleo (SDG’s).

  “Mwaka huu jumuiya ya kimataifa itakubaliana kuhusu SDGs na kukamilishwa kwa malengo ya milenia (MDGs). Malengo ya milenia yamewezesha kupatikana kwa mabadiliko makubwa katika kukabiliana na umaskini, afya bora na kiwango kikubwa cha watu wanaojiunga na shule. Mataifa ya Umoja wa Mataifa kwa kupendezwa na mafanikio ya MDGs sasa wanataka kukubaliana kuhusu SDGs.

  “ SDG itakuwa na vipengele 17 kikiwamo cha mabadiliko ya tabia nchi. Umoja wa Mataifa umechagua suala la mabadiliko ya tabia nchi kuwa ndio kipaumbele cha mwanzo kwani imebaini kwamba ni tishio kwa maendeleo endelevu. Hii inatokana na ukweli kuwa mabadiliko ya tabia nchi ni ya kweli na ni vyema kila mtu kuwajibika ili kuhakikisha mazingira yetu yanaendelea kuwa mazuri-tukianzia na mazingira yetu yanayotuzunguka” alisisitiza.

  Rodriguez alizitaka jamii mbalimbali kutoa kiipaumbele katika kusafisha mazingira na usafi binafsi hasa kipindi hiki ambapo kumezuka ugonjwa wa Kipindupindu kwa mikoa ya Dar es salaam na Morogoro.

  “Usafi wa soko hili ni muhimu kwa ajili ya afya yako na uhai mrefu. Afya njema inatuwezesha kuendelea kufanya shughuli zetu mbalimbali za kuchangia ukuaji wa uchumi.Hebu angalia pembeni mwako imetuchukua saa chache kusafisha soko la Temeke na je hamuoni tofauti? Nawaomba wakazi wa Temeke na wafanyakazi wa soko hili kufanya shughuli hizi kila siku kwani maisha yao, afya yao na uchumi unategemea soko hili.”
  Pia aliwaalika wananchi wote katika sherehe za miaka 70 za Umoja wa Mataifa zitakazofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja Oktoba 13 ili kushiriki kikamilifu katika kuadhimisha siku hiyo ya Umoja wa Mataifa.
  Pia alihimiza serikali kuendelea kuelimisha wananchi juu ya utunzaji wa mazingira na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
  IMG_5475
  Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya Temeke, Sophia Mjema akitoa nasaha zake kwa wananchi na wafanyabiashara wa soko la Temeke Stereo, ambapo aliwataka kuzingatia usafi wa maeneo yao ya biashara pamoja na majumbani ili kuepeukana na mlipuko wa Kipundupindu.

  Katika hafla hiyo ya kusafisha soko la Temeke, Umoja wa Mataifa na serikali ya Tanzania kwa pamoja walitoa vifaa vya kufanyia usafi vyenye thamani ya shilingi milioni 10. Vifaa hivyo vilikabidhiwa kwa menejimenti ya soko la Temeke.

  Watu wengine walioshiriki katika shughuli hiyo ni pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy; mkuu wa wilaya ya Temeke Mheshimiwa Sophia Mjema, akimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam na maofisa wengine wa serikali na wakazi wa Temeke.

  Balozi Mushy katika risala yake ya kumkaribisha mgeni rasmi kufanya usafi aliitaka jamii kutambua kwamba usafi ni jukumu la kila mmoja wetu kwani bila usafi madhara yake ni makubwa ikiwamo ya kutunzwa kwa mazingira.

  Alilitaka jiji la Dare s salaam ambalo linalinganishwa na majiji mengine duniani kama Nairobi, Kenya; Pretoria Afrika Kusini, Washinton DC na Paris kujifunza kuwa wasafi kwani hata mlipuko wa sasa wa Kipindupindu ni dalili tosha ya kukosekana kwa usafi.

  Aidha alisema kwamba suala la usafi si lazima kwenda kujifunza nje kwani ipo miji na mikoa misafi ambayo inaweza kuulizwa wamefanikishaje jambo hilo. Aliitaja miji hiyo ni Moshi, Iringa na Mwanza.

  Alisema katika kuadhimisha miaka 70 ya Umoja wa Mataifa, wameamua kufanya usafi wa mazingira katika soko la Temeke kuonesha kwamba inawezekana kufanya usafi kwa kuwajibika kwa lengo la kufanya mazingira yawe masafi na ya uhakika.

  Kwa kutekeleza usafi kwa maana nyingine kutasaidia kuondoa gharama zinazoambatana na uchafu wa mazingira.
  Alitaka kila mmoja katika soko hilo kuanzia wakulima hadi wachuuzi kuwajibika kwa usafi ili mazingira yawe salama.
  IMG_5301
  Pichani juu na chini ni wafanyabiashara wa Soko la Temeke Stereo, wananchi na wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na wa Wziara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakifuatilia kwa umakini hotuba ya mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Temeke (hayupo pichani).


  IMG_5471
  IMG_5299
  IMG_5285
  IMG_5554
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati) akikambidhi Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema (kushoto) vifaa vya kufanyia usafi katika Soko la Temeke Stereo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa. Anayeshuhudia tukio hilo kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy.
  IMG_5558
  Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akivaa 'gloves' tayari kushiriki zoezi la usafi katika soko la Temeke Stereo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
  IMG_5569
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy wakifanya usafi katika maeneo ya wafanyabiashara katika soko la Temeke Stereo.
  IMG_5575
  Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akibeba taka katika soko la Temeke Stereo.
  IMG_5604
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema wakishiriki zoezi la usafi katika soko la Temeke Stereo ikiwa ni sehemu ya kusheherekea maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
  IMG_5649
  Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wakijumuika na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema pamoja na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez wakiendelea na zoezi la usafi.
  IMG_5643
  IMG_5633
  IMG_5787
  Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Titus Osundina (kulia), Beatrice Mkiramweni pamoja na Jacqueline Namfua wakifanya usafi kwenye maeneo ya soko la Temeke Stereo.
  IMG_5789
  Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Titus Osundina akishiriki zoezi la kuzoa taka katika soko la Temeke Stereo.
  IMG_5801
  IMG_5678
  Umoja ni Nguvu: Wafanyabiashara wa soko la Temeke Stereo, wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na Wizara ya Mambo ya Nje wakishirikiana kwa pamoja kufanya usafi katika soko hilo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
  IMG_5695
  Petra Karamagi na Nasser Ngenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa wakishikishiriki zoezi la usafi katika soko la Temeke Stereo.
  IMG_5704
  Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano alipomulikwa na kamera ya Modewjiblog
  IMG_5683
  IMG_5716
  Zoezi likiendelea.
  IMG_5721
  Zoe Glorious katika ubora wake.
  IMG_5723
  #HapaKaziTu ......Usia Nkhoma Ledama akiwajibika katika zoezi la usafi soko la Temeke Stereo.
  IMG_5726
  Wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na wafanyabiashara wakishirikiana katika zoezi hilo.
  IMG_5741
  IMG_5756
  IMG_5290
  Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu (kulia) akiteta jambo na na baadhi ya maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa walioshiriki kwenye zoezi la kufanya usafi wa mazingira katika soko la Temeke Stereo.

  0 0

  Meneja Mauzo wa Airtel Kagera , Mohamed Kabeke (kushoto) akimkabithi
  pesa taslimu  bwana Mwahamadi Katula (24) mfanyabiashara na mkazi wa
  mkoa wa Kagera , mara baada ya kuibuka mshindi wa shilingi milioni 3
  katika droo ya wiki ya tano ya promosheni ya Jiongeze na Mshiko
  inayoendeshwa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel.
  Afisa uhusiano na matukio, Dangio Kaniki akiongea na mshindi
  aliyepatikana wakati wa kuchezesha droo ya sita ya wiki ya promosheni
  ya "Jiongeze na Mshiko" ambapo wateja wawili wa Airtel kutoka mikoa ya
  Mbeya na Dar es Salaam walipatikana akichukua taarifa za mshindi
  (kushoto) ni mkaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha bwana
  Bakari Majid na Afisa huduma za ziada Airtel bwana Fabian
  Felician.(kulia) droo hii imechezwa jana katika makao makuu ya Airtel
  Moroco jijini Dar es saalam,.


  KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel imeendelea kuchezesha droo za
  kila wiki na kuwazawadia  wateja wake jumla ya pesa taslimu shilingi
  milioni 4 kila wiki baada ya kuibuka washindi katika droo za wiki za
  promosheni hiyo.

  Akizungumza wakati wa kuchezesha droo ya wiki ya sita ya promosheni hiyo
  Meneja Uhusiano na Matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki alisema “ Tanga
  tuanze promosheni hii mwenzi wa Julai mwaka huu tumeshuhudia wateja
  wengi wakijishindia mamilioni ya fedha kila wiki na leo tumechezesha
  droo ya wiki ya sita na kuweza kupata washindi wawili ambao nao
  wamejishindia pesa taslimu akiwataja washindi hao Kaniki alisema” ninayo furaha kumtangaza Rajabu Mwanalipanga (19) Mwanafunzi na mkazi wa Dar es Salaam kuwa mshindi wa shilingi milioni 3 na mshindi wetu wa pili ni Bwana Frank Kapesa (22) mkulima na mkazi wa Mbeya amejishindia shilingi milioni 1 promosheni hii bado inaendelea tukiwa tumebakiwa na takribani wiki 10 za kuchezesha droo.  

  Mpaka sasa shilingi milioni 25,000 zimeshatolewa
  kwa washindi waliopatikana kutoka katika mikoa mbalimbali.  

  Washindihao ni pamoja na John Luu na Josephat Mahinda wakazi wa Manyara, Mwahamadi Katula  Mkazi wa Kagera, Daudi Aliki na Agrisius Kapinga wakazi wa Dar es saalam, Rogers Shangali Mkazi wa Tanga, Gabriel
  Ferdnandi  mkazi wa Musoma Mara, Hamisi Rashid mkazi wa Tabore, Rashid Hassani Mkazi wa Mtwara na Plasis Gabriel mkazi wa Geita.

  Ili kushiriki mteja anatakiwa kutuma ujumbe wenye neno “BURE” kwenda
  namba 15470, na kisha kuanza kupokea maswali kwenye simu zao na kujibu
  maswali bure bila gharama yoyote na kujikusanyia pointi.

  “ Jiongeze na Mshiko”  inamwezesha mteja kujiunga na kushiriki bure
  kwa kujibu maswali na kujishinda shilingi milioni 1 kila wiki na
  mwisho wa promosheni kujishindia milioni  2. 

   Na pia kumwezesha mteja
  kujishindia zawadi kubwa zaidi  kwa kujiunga na ngazi ya Premium  kwa
  kuchajiwa  shilingi 300 kwa siku na kupata nafasi ya kujishindia
  shilingi milion 3 kila wiki na mwisho wa promosheni kujishindia

  shilingi milioni 50.

  0 0

   Makamu Rais wa kampuni ya StarTimes, Bw. Michael Dearham (kushoto) akisalimiana na Jokate Mwegelo (kulia) atakae kuwa mtangazaji wa kipindi cha Mashariki Max kitakacho onyeshwa na StarTimes kupitia chaneli ya ST Swahili, wakati wa uzinduzi wa kipindi hicho uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katikati ni mtangazaji wa kipindi hicho nchini Kenya, Sarah Hassan. Picha na mpiga picha wetu. 
   Makamu Rais wa kampuni ya StarTimes, Bw. Michael Dearham (kushoto) akiwapungia mkono wageni pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes, Bw. Lanfang Liao (kulia) wakati wa uzinduzi wa kipindi cha Mashariki Max kitakacho onyeshwa na StarTimes kupitia chaneli ya ST Swahili. Uzinduzi huo uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Picha na mpiga picha wetu.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes, Bw. Lanfang Liao (katikati) katika picha ya pamoja na watangazaji wa kipindi cha Mashariki Max Jokate Mwegelo (kulia) na Sarah Hassan (kushoto) wakati wa uzinduzi wa kipindi cha Mashariki Max kitakachoonyeshwa na StarTimes kupitia chaneli ya ST Swahili. Uzinduzi huo uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Picha na mpiga picha wetu. 

  Na Mwandishi Wetu
  STARTIMES  Tanzania kupitia chaneli yake mahususi ya vipindi vya kishwahili, StarTimes Swahili imezindua kipindi cha Mashariki Max ambacho kitakuwa kinaangazia mitindo na maisha ya watu mbalimbali maarufu nchini.

  Kipindi hicho kilichozinduliwa jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Serena mwishoni mwa wiki kitakuwa kikitangazwa na mrembo Jokate Mwegelo ambaye licha ya kuwa alishawahi kuwa mshindi wa pili wa shindano la Miss Tanzania, pia ni mwanamuziki, mcheza filamu na pia mjasiriamali.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mgeni rasmi ambaye ni Makamu wa Rais wa StarTimes Africa, Bw. Michael Dearham amesema kuwa, “Tunayo furaha siku ya leo kuzindua kipindi cha Mashariki Max kwani kitaongeza uhondo wa vipindi veytu vya kuvutia tulivyonavyo,Kuongezewa kwa kipindi hiki katika chaneli ya StarTimes Swahili kuna maana kubwa katika kujenga, kukuza na kuithamini lugha ya Kiswahili ambayo inatumika sehemu kubwa ya Afrika Mashariki na Kati.”

  Bw. Dearham aliendelea kwa kusema, “Kipindi hiki cha Msahriki Max kitaanza kuruka siku ya Jumamosi ya Septemba 5 kuanzia saa 12:30 jioni na kila, tunaamini kuwa kwa kuzidi kuongeza vipindi ambavyo vina maudhui mengi ya Kiswahili wateja wetu wataburudika. Kipindi hiki tunaamini kuwa hakitaonekana ukanda wa Afrika ya Mashariki au Afrika nzima bali hata sehemu zingine za dunia.”

  Aliongezea kuwa licha ya StarTimes kuwekeza nguvu katika kuongeza na kuboresha vipindi vya nyumbani pia inajitahidi kadiri ya uwezo wake kuongeza zaidi chaneli na vipindi vya michezo nchini hususani vya mpira wa miguu.

  “Mbali na kuongeza na kuboresha vipindi vyenye maudhui ya nyumbani pia tunafuta fursa za kuboresha vipindi na chaneli za michezo, tuna mipango ya kuboresha na kukuza michezo nchini kama vile kudhamini mashindano na timu za soka nchini ili kuinua sekta hii,” alisema na kuongezea Bw. Dearham kuwa, “Licha ya vipindi vingine sasa hivi wateja wetu wanayo fursa ya kufurahia ligi mbalimbali bora za mpira wa miguu duniani kama vile ya Ujerumani (Bundesliga) na  Italia (Serie A) ambazo zipo mahususi kupitia visimbuzi vyetu vya StarTimes.”

  “Tunayo furaha sana kuona watejea wetu wanafurahia vipindi vyite hivi ambavyo tunazidi kuvitambulisha kwenu kila kukicha, napenda kuwaambia kuwa StarTimes itazidi kuwaletea huduma na bidhaa nzuri na vipindi bor ana vya kusisimua zaidi.” Alihitimisha bosi huyo wa StarTimes

  Naye kwa upande wake mtangazaji wa kipindi hicho mrembo Jokate Mwegelo alibainisha kuwa kwake hii ni heshima na fursa kubwa sana kwake kwani StarTimes imesambaza huduma zake sehemu kubwa ya bara la Afrika.

  “Nimekwisha tangaza vipindi mbalimbali vya luninga lakini hiki cha Mashariki Max kupitia chaneli ya StarTimes Swahili kitanipa fursa kubwa ya kukua kwani nitakuwa nikionekana sehemu kubwa ya Afrika ya Mashariki na Afrika nzima kwa ujumla.”

  Aliongezea kwa kusema kuwa wateja wote wa StarTimes wakae mkao wa kula na kutegemea mambo mazuri kwani kipindi hiki kitakuwa na maudhui bomba yanayohusu mitindo, maisha ya watu maarufu wa tasnia mbalimbali pamoja na tamaduni kwa ujumla.

  “Ninategemea watazamaji licha ya kuburudika kupitia kipindi cha Mashariki Max pia wataweza kujifunza na kujua mambo mbalimbali watu wanayopitia mpaka kufanikiwa katika maisha yao. Nina hakika hii ni fursa kwa kujifunza kupitia simulizi tamu za maisha ya watu wengine.” Alihitimisha mrembo huyo.

  0 0

   Baadhi ya viongozi wa vyuo vya ualimu nchini wakibadirishana mawazo nje ya ukumbi.
   Baadhi ya washiriki katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.
   Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF , Crescentius Magori akitoa ufafanuzi wa masuala muhimu ya Mfuko wa NSSF kwa waandishi wa habari.
   Washiriki wa warsha kuhusu mfuko wa NSSF ambao ni viongozi wa vyuo vya ualimu nchini wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi .
    Washiriki wa warsha ya NSSF kubadirishana mawazo.

  Washiriki wakisililiza jambo kutoka kwa mmoja wa watoa mada za NSSF.

  Na John Nditi, Morogoro.
  SHIRIKA  la Taifa la Hifadhi ya Jamii ( NSSF), limewataka  waajiri wa sekta mbalimbali  nchini wanaodaiwa madeni ya makato kutoka kwa  waajiriwa wao  ambao ni wanchama wa mfuko  huo kulipa madeni yao  ndani ya mwezi mmoja kuanzia Septemba mwaka huu .

  Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF , Crescentius Magori, alisema hayo Augosti 29, Mmwaka huu mjini Morogoro  wakati alipokuwaakizungumza na waandishi wa habari  baaada ya kufungua warsha ya siku moja ya  kutoa  elimu  kwa viongozi wakuu wa vyuo vya ualimu nchini juu ya namna mfuko huo unavyofanya kazi ya kutoa huduma  zake kwa wanachama.


  Magori alisema wale ambao watashindwa kulipa madeni yao katika muda huo ,uongozi wa NSSF  utawafikisha  mahakamani kwa mujibu wa sheria na watalazimika kulipa na adhabu iliyowekwa.


  Alisema , zoezi la kufuatilia madeni kutoka kwa waajiri sugu walioshindwa kuwasilisha  kwa wakati makato litaanzia  mkoa wa Dar es Salaam na baadaye litaendelea katika  nchi nzima. 

  “ Kuanzia wiki hii ‘ Augosti 31’ NSSF itafuatilia wadaiwa wote ambao wameshindwa kulipa madeni ya makato ya michango ya wanachama wa NSSF na tunaanzia na mkoa wa Dar es Salaam na baada ya hapo zoezi litaendelea nchini kote” alisema Magori.

  Alisema ,baada ya kipindi hicho  kumalizika, waajiri ambao watakuwa wameshindwa kulipa madeni yao, NSSF utatumia sheria ilizopo kuwafikisha mahakamani  ambapo watalazimika kulipa na adhabu . 

  Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF alitolea mfano kwa kusema  katika waajiri 100 kati yao 20 hawaleti michango baada ya kuwakata waajiri wao , wengine ni kwa sababu za kiuchumi na baadhi ni wakorofi .

  “ NSSF itatumia njia zote za kukutana na waajiri hawa na kuzungumza nao na endapo  utaratibu wote ukishindikana tutawapeleka mahakamani “ alisema Magori.

  Alitumia fursa hiyo kutoa  rai kwa waajiri wote wa mkoa wa Dar es Salaam  kulipa madeni yao ndani ya mwezi mmoja  ,ambapo pia  zoezi hilo maalumu litafanyika katika nchi nzima baada ya kukailika kwa mkoani humo.

  Pia aliwataka wanachama kuhakikisha wanakuwa na taarifa sahihi za ajira zao na kufuatilia michango yao kama inawasilishwa kwa wakati kupitia Ofisi za NSSF ili kuwaondolea usubufu wakati wa muda wa kulipwa mafao hayo ya pensheni.

  Magori  alisema, NSSF inatarajia kusogeza huduma zake kwa kuwatumia mawakala katika maeneo mbalimbali watakaokuwa na jukumu la kuingiza wanachama nchini.

  Alisema  warsha hiyo kwa viongozi wa vyuo vya ualimzu nchini ni mkakati endelevu wa kutoa elimu pana zaidi kwa makudi mbalimbali ili wajiunge na mfuko huo wakiwa na uelewa mpana badala ya kuwavizia wakati wa wanapoajiriwa .

  Mkurugenzi  wa Uendeshaji wa NSSF Alisema , tayari warsha kama hiyo imefanyika kwa Mahakimu na Majaji kwa mkoa wa Dar es Salaam  iliyolenga wao kuweza  kuzijua sheria za mfuko huo hasa wanapokuwa  wakiendesha mashauri yanaohusiana na waajiri dhidi ya NSSF.

  Nao baadhi ya washiriki  Baraka Mwakyeja , ambaye ni Ofisa Utawala wa Chuo Kikuu Mkwawa , pamoja na Maria Mdee , Ofisa Rasilimali watu wa Chuo Kikuu Kishiriki Elimu (DUCE), kwa nyakati tofauti walisema,  elimu waliyoipata itawasaidia wao  na wanachuo ambao ni waajiriwa watarajiwa serikalini  kuwa na ufahamu na umakini wa kuchagua  mifuko ya kujiunga nayo.


  Walisema NSSF imeweka utaratibu mzuri wa kutoa kwanza elimu juu ya faida anazozipata mwanachama anayejiunga na mfuko huo tofauti na mingine ambayo inasubiri tu pale mwajiriwa akiwa tayari katika ajira na hivyo kukosa umakini  katika maamuzi yake ya kuchangua mfuko huliosahihi.

  0 0

  JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA

  KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO


  Simu ya Upepo   : “N G O M E”        Makao Makuu ya Jeshi,

  Simu ya Mdomo : DSM  22150463     Sanduku la Posta 9203,

  Telex                     : 41051                      DAR ES SALAAM,  31 Agosti, 2015,

  Tele Fax                : 2153426

  Barua pepe               : ulinzimagazine@yahoo.co.uk

  Tovuti                  : www.tpdf.mil.tz

                      


       Taarifa kwa Vyombo vya Habari
            Vyombo vya Ulinzi na Usalama vinaandaa sherehe ya kumuaga Amiri Jeshi Mkuu tarehe 01 Septemba 2015 kwa gwaride rasmi litakalofanyika katika viwanja vya Uhuru, kuanzia saa 2.00 Asubuhi hadi saa 6.30 mchana.

  Waandishi wa Habari mnakaribishwa katika uwanja wa Taifa kwa ajili ya Coverage ya tukio hilo la kihistoria.   


  Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Mahusiano

  Makao Makuu ya Jeshi, Upanga

  S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.

  Kwa Mawasiliano zaidi: 0756 - 342279

                                           0783- 309963.

  0 0

  Na Woinde Shizza,Arusha
   Mkuu wa mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda, amevitaka vyombo vya habari nchini kusaidia uchaguzi mkuu mwaka huu umalizike kwa amani na utulivu ili Tanzania iendelee kuwa na sifa ya amani Barani Afrika.

  Akizungumza katika tamasha la 10 la vyombo vya habari mkoani hapa, lililowashirikisha wanahabari kutoka mkoa wa Arusha, Manyara na jijini Dar es Salaam, Ntibenda, alisema vyombo vya habari ni wadau wakubwa wa amani na utulivu.

  Alisema kama wanahabari wote watafanyakazi kwa weledi, wanaweza kusaidia Taifa kupita salama katika uchaguzi Mkuu wa mwezi Octoba mwaka huu.
  Ntibenda alisema kwa mkoa wa Arusha, suala la amani ni la kipekee hivyo ni muhimu kila mdau kuhakikisha amani inakuwepo, kwani Arusha ndio kitovu cha utalii nchini.Alisema anaunga mkono kauli mbiu za Tamasha hilo, kuwa Uchaguzi mkuu bila vurugu inawezekana.

  Hata hivyo, alisema kama wa wanahabari wakifanya kazi kwa ushabiki wa vyama bila kujali maadili wanaweza kuchangia kulitumbukiza taifa katika vurugu.

  Awali Mkuu wa Idara ya Matukio ya kampuni ya Bia nchini(TBL), Chris Sarakana aliwataka wanahabari kutumia vyema kalamu zao kuhamasisha amani na utulivu nchini.Naye mmoja wa waandaaji wa Tamasha hilo, Mussa Juma alisema waliamua kauli mbiu katika tamasha hilo la 10, kuwa ni uchaguzi bila vurugu inawezekana, ili kuweza kuhamasisha amani na utulivu kuelekea uchaguzi mkuu.


  Katika kuhamaisha amani na kukuza utalii wa ndani, wanahabari kutoka Jijini Dar es Salaam walipata fursa kutembelea hifadhi ya Taifa ya Arusha na wanahabari wa mkoa wa Arusha, walitembelea kiwanda cha bia nchini TBL

  0 0

   Ngoma Africa band
   Ngoma Africa Band aka FFU katika gwaride jukwaani nchini Latvia
   Ngoma Africa band thrilling fans.
   ngoma africa wordpress-1
  ngoma-africa_Band Live

  BENDI maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU-ughaibuni ukipenda waiite viumbe wa ajabu Anunnaki Alien's yenye makao kule Ujerumani inatarajiwa kutingisha jukwaa katika maonyesho ya Vechelde Festival nchini Ujerumani Jumamosi 5. September 2015 saa 2:00 Usiku katika eneo la Bürgerzentrum Vechelde liliopo mtaa Hildesheimer Straße 5 mjini Vechelde jirani mji wa Braunschweig,Ujerumani.

  Bendi hiyo maarufu Ngoma Africa yenye sifa za kuwatia kiwewe washabiki wa muzikikatika maonyesho ya kimataifa kwa kutumia mdundo wao "Bongo Dansi" made in Uswahilini ndio bendi pekee ya kiafrika barani ulaya iliyoweza kudumu kwa miaka 22 na kufanikiwa kukama soko la kutumbuiza katika maonyesho ya kimataifa.

  Kwa sasa bendi hiyo inatamba na CD yake mpya ya "LA MGAMBO" yenye nyimbo mbili za kumuaga rais Jakaya Kikwete na CD hiyo utunzi wake Kiongozi wa bendi Ebrahim makunja aka Kamanda Ras Makunja imeshatua nchini Tanzania tayari kwa kutingisha anga katika vituo vya redio mbali mbali.
  wasikilize ffu-ughaibuni at www.reverbnation.com/ngomaafricaband  0 0  Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba (katikati mbele), akisindikizwa na wanachama wa chama hicho, alipowasili katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati CCM ilipozindua kampeni kwaajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, katika jimbo hilo, jijini Dar es Salaam jana. 
  PICHA/JOHN BADI WA DAILY MITIKASI BLOG
  Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge (kulia) akimtambulisha Mgombea Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya CCM, Kippi Warioba mbele ya umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi wa kampeni kwaajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, katika jimbo hilo, jijini Dar es Salaam jana.
  Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba ‘Gadafi’ (kulia) akimpongeza Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya CCM, Kippi Warioba baada ya kumkabidhi Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015, mbele ya umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi wa kampeni jimboni humo, jijini Dar es Salaam jana.
  Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba ‘Gadafi’ (kushoto) akimtambulisha Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya CCM, Kippi Warioba baada ya kumkadhi Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015, mbele ya umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi wa kampeni jimboni humo, jijini Dar es Salaam jana.


  Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba (kulia), akiusalimia umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, baada ya kutambulishwa na kukabidhiwa Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015, wakati wa uzinduzi wa kampeni jimboni humo, jijini Dar es Salaam jana. Kulia kwake ni Katibu Mwenezi wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba ‘Gadafi’.
  Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba akizungumza umati wa wanachama wa CCM na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi wa kampeni kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, katika jimbo hilo, jijini Dar es Salaam jana.
  Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba akiinadi Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015, mbele ya umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi wa kampeni jimboni humo, jijini Dar es Salaam jana.
  MAMA MZAA CHEMA … Mama Evelyne Warioba ambaye ni mama mzazi wa Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba akiusalimia umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi huo. 
  Sehemu ya umati wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi huo. 
  Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Salum Londa akimwaga sera za CCM mbele ya umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi huo. 
  Mhamasishaji maarufu kwa jina la ‘Msaga Sumu’ naye alikuwepo. 
  0 0  Watanzania wametakiwa kutafakari kwa kina kauli iliyotolewa na mgombea wa kiti cha urais kupitia UKAWA Mh Edward Lowassa ya kuwaachia huru baadhi ya watuhumiwa wa makosa ya kigaidi yaliyosababisha vifo na ulemavu wa kudumu kwa baadhi ya viongozi wa dini wa kiislamu na kikristo pamoja na wageni kutoka nje ya nchi sambamba na watuhumiwa wengine wa makosa ya kijinai bila kujali athari zinazosababishwa na matukio ya kigaidi ulimwenguni.


  Tahadhari hiyo imetolewa mjini Ludewa mkoani Njombe Bwana Amoni Mpanju wakati akizungumza na mamia ya wananchi waliojitokeza kusikiliza sera za Dr Magufuli na kuongeza kuwa wakati dunia ikihaha kupambana na janga la matukio ya kigaidi yanayosababisha vifo na ulemavu wa kudumu kwa binadamu bila ya kujali imani zao za kidini na mataifa yao baadhi ya viongozi wanaowania kuliongoza taifa la Tanzania wanatangaza hadharani kuwaachia huru watuhumiwa wa ugaidi waliosababisha vifo na majeruhi kwa viongozi wa dini za kikristo na kiislamu na wageni wa mataifa mengine na kuwataka watanzania kutafakari kauli hiyo ya Mh Lowassa.
  Dr John Pombe Magufuli akiwa katika ubora wake amefanya mikutano zaidi ya mitano akiwa njiani kutoka mkoano Njombe kuelekea Ludewa Songea kwa njia ya barabara ambapo amekuwa pia akisikiliza kero za walemavu alioonana nao na kuongeza kuwa uongozi ni msalaba na si kila mtu anaweza kuwatumikia kwa dhati wananchi na kwamba kiongozi anapaswa kuzifahamu kero za wananchi na kuziishi na kwamba ili Tanzania iwe na amani ni lazima majeshi yetu yaendeshwe kisayansi na kuahidi kuayaboresha.
  Aidha Dr Magufuli ambaye amekuwa akishangiliwa na umati mkubwa wa wananchi waliokuwa wanaziba barabara kwa lengo la kutaka kumsikia amewataka wananchi kumchagua yeye kupitia CCM kwa kuwa ndio chama chenye ilani bora na ahadi za ukweli huku akiwazodoa UKAWA kwa kutokuwa na ilani ambayo ni mkataba kati ya watawala na watawaliwa.

  Dr Magufuli anatarajiwa kuendelea na ziara yake ya kusaka ridhaa ya watanzania kuliongoza taifa la Tanzania ambapo jumatatu ya Septemba mosi anatarajiwa kuendelea na kampeni zake mkoani Ruvuma

  0 0   Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua kitambaa wakati wa uwekaji jiwe la msingi la Ujenzi wa National Defence Headquarters huko Lugalo jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Mkuu wa majeshi ya Ulinzi  Jenerali Davis Mwamunyange,Watatu Kushoto ni Waziri wa Ulinzi Dkt.Huessein Ali Mwinyi na kulia ni Bwana Hu mwakiklkishi wa kampuni ya ujenzi kutoka China.
   Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange akimuonyesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mchoro wa majengo ya Makao Makuu ya Ulinzi yatakayojengwa eneo la Lugalo jijini Dar es Salaam leo.Wapili kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange wakati wa Uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa National Defence Headquarters Lugalo jijini Dar es Salaam leo.
  (Picha na Freddy Maro).

  0 0

   kikosi cha timu ya mchezo wa mpira wa pete ya Taswa Dar mara baada ya mechi kuisha.  Siku moja kabla ya bonanza waandishi wa habari wa mkoa wa Arusha walipata fursa ya kutembelea kiwanda cha bia ya TBL Arusha hapa mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo akiwa anawapa maelekezo ya jinsi kiwanda hicho kinavyoweza kufanya kazi  ya kutengeneza beer kwa kutumia mashine na komputa
   nikiwa na waandishi wa habari wakogwe mara baada tu ya kuwasili ndani ya kiwanda cha bia cha Tbl Arushawa kwanza kushoto ni Gwandu  akifuatiwa na Woinde shizza,Mr mchau wakwanza kulia ni Salma Mchovu pamoja na Yasinta..


   waandishi wahabari wa mkoa wa Arusha wakifurahia wakati tamasha likiendelea


   Na Woinde shizza,Arusha
  TIMU  ya soka ya chuo cha uandishi wa habari   Arusha(AJTC) juzi walitwaa ubingwa katika bonanza la 10 vyombo vya habari mkoani Arusha huku Timu ya wanahabahari wa Dar es Salaam TASWA FC wakishindwa kutamba.

  Katika Bonanza hilo, ambalo lilishirikisha jumla ya timu nane, TASWA FC) alishindwa kutamba na kushika nafasi ya nne, Hata hivyo timu ya wanahabari wasichana kutoka Dar es Salaam(TASWA Qeen) iliweza kutwaa ubingwa wa mpira wa pete.


  Katika bonanza hilo, lililofanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda  ,AJTC walitwaa ubingwa baada ya kujikusanyia alama saba huku nafasi ya pili, ikichukuliwa na timu ya wanahabari kutoka mkoa wa Manyara wa kituo cha radio ORS.

  Chuo cha habari cha IMS kilishika nafasi ya tatu ,kikifuatiwa na TASWA Dar, TASWA Arusha, MJ Radio,Arusha One radio na radio  Habari Maalum.
  Mkuu wa mkoa wa Arusha, Filex Ntibenda aliwakabidhi mabingwa wa soka kikombe na fedha taslim Tsh 250,000, huku washindi wa pili wakipata fedha taslimu 150,000 na kikombe.

  Katika Tamasha hilo, timu ya TASWA Qeen ilikabidhiwa kikombe na Tsh 150,000, huku timu ya pili AJTC Qeen ikipata fedha taslim 10000 na kikombe.
  TASWA FC ilipata zawadi ya timu yenye nidhamu katika michuano hiyo na kupokea zawadi na fedha taslimu 50,000.

  Akizungumza wakati akifunga bonanza hilo, Ntibenda alipongeza TASWA Arusha na kampuni ya Arusha media kwa kuandaa Bonanza hilo.
  Aliwataka wanahabari kuwa na tabia ya kushiriki katika michezo kwani michezo hujenga, Afya na ni ajira.

  Mkuu wa mkoa wa Arusha, pia alikabidhi vyeti vya udhani Bonanza hilo  , kampuni ya bia nchini(TBL), Shirika la hifadhi ya Taifa TANAPA, kampuni ya Mega Trade.

  Shirika la nyumba la Taifa(NHC),Kampuni ya Tanzanite One, Big Expedition, Taasisi ya Faidika, Kampuni ya Pepsi na Coca cola.

  0 0

  Mwenyekiti wa Chama cha Walimu mkoa wa Arusha ,Mwalimu Jovin  Kuyenga akizungumza na waandishi wa habari jana Ofisini kwake  juu ya deni la shilingi bilioni 4 wanalodai  kwa serikali, kushoto ni Katibu wa Chama cha Walimu mkoa wa Arusha, Mwalimu Hassan Saidi.

  Na Woinde Shizza,Arusha
  CHAMA cha Walimu mkoa wa Arusha CWT wamelalamikia serikali na kuitaka kutekeleza kwa wakati madeni yao la zaidi ya billioni 4 kwani yamekuwa kikwazo katika ufanisi wa kazi hali ambayo inapelekea walimu wengi kushindwa kuendelea kufanya kazi kwa moyo na kujituma jambo ambalo linaweza kushusha kiwango cha elimu nchini.

  Akizungumza na Waandishi wa habari, Mwenyekiti wa chama cha walimu mkoa waArusha Mwalimu Juvin Kuyenga amesema, kumekuwa na  chanagamoto kubwa ambazo zinakwamisha ufanisi wa kazi kwa walimu kwani wanazidai halmashauri zilizopo mkoani zarusha zaidi ya billioni nne ,amabapo katika jiji la arusha wanadai millioni  987,689,00,Arumeru billioni
  2,996,607,848.21,Karatu  millioni 423,983,820,Longido millioni 171,112,680,
  Ngorongoro million 169,000,000, na Monduli 135,832,000.

  Mwalimu Kuyenga ameendelea kusema kuwa,madeni haya yanatokana na madai mbalimbali ikiwa ni pamoja na malimbikizo ya mishahara
  ,mafunzo,uhamisho,matibabu na likizo pamoja na mapunjo ya mshahara na
  madeni haya yamekuwa ni kero kubwa  na kusababisha wakati mwingine walimu kuzichukia kazi zao.

  Alisema kuwa Walimu wamekuwa wakigota madaraja bila kupanda kwa muda mrefu kati ya walimu 12,319 waliopo mkoani arusha walimu 5,364 wamegota kwenye madaraja yao na bado hawajafunguliwa  pamoja na serikali ilishatoa waraka wa kufungua madaraja tangu julai 2014 hivyo wametaka seriakali kuhakikisha inapandisha madaraja kwa wakati.

  ‘Posho ya madaraka kwa viongozi wa elimu, wakuu wa shule,wakuu wa vyuo
  kutokana na waraka wa seriakali uliotolewa mwaka jana posho hiyo alitakiwa ianze kutolewa kuanzia julai mwaka huu 2015 lakini hadi sasa bado pesa hiyo haijanza kutolewa hii inakuwa kama danganya toto kwa viongozi wetu” alisema mwalimu Juvin Kuyenga.

  Hivyo  wameilalamikia serikali juu ya kuchelewesha kwa malipo kwa wastaafu, sababu kuna walimuwaliostaafu toka january  zaidi ya walimu 67 huku wakiishi katika mateso ilihali wameshastaafu kazi na mpaka leo hawajapata viiinua mgongo vyao

  “Tunaidai serikali sababu tunapowasiliana na hawa wa mifuko ya hifadhi za
  jamii inasema serikali bado haijawarejesha michango ya walimu inayotakiwa kupelekwa hivyo na danadana hizi zinawafanya walimu kuona haki zao zinanyonywa kwani utasababisha ufanisi kuwa mdogo makazini” Alisema

  Sababui swala hili laweza kupelekea malumbano kati ya walimu na serikali
  ukizingatia katika kipindi cha kueleka katika uchaguzi ,mitihani ya darasa
  la saba na kidato cha nne kwani kukataa huku tamaa kunaweza kupelekea vitu hivyo vya taifa kushindwa kufanikiwa.

  Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Walimu mkoa wa Arusha, Mwalimu Hassan Saidi amesema chama hicho kimetoa wiki mbili kwa  waajiri wa halmashauri zilizopo mkoa wa arusha kuwarudisha majumbani walimu waliostaafu na wanaostaafu na wasipofanya hivyo watawachukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwashtaki mahakamani kwani wamekuwa wakiteseka sana baada ya kustaafu na ni kinyume cha sheria .

  Mwalimu Saidi , amewataka wagombea wa Uraisi kutazama vipaumbele vya walimu walivyovitoa likiwemo la kuwapatia walimu  kompyuta mpakato (laptop)  wakati wanamahitaji mengi na ya  msingi zaidi ya hayo ikiwa ni pamoja na mishahara isiyokidhi mahitaji ya walimu na kurejeshwa na kwa posho ya kufundishia kwa walimu.

  Kwa taarifa tulizozipata kutoka kwa vyanzo vyetu kuwa baraza la kuu la
  walimu tanzania  wanatarajiwa kukutani mkoani dodoma  Agosti  31 hadi
  Septemba 8 mwaka huu kwa ajili ya kutoa matamko ya kitaifa juu ya kero hizi nyingi wanazozipata walimu.

  0 0

  TAARIFA  YA UMOJA WA VIJANA WA CCM  ( UVCCM) MAKAO MAKUU  DAR ES  SAALAM  KWA VYOMBO VYA HABARI JUMAPILI 30 AUGUST 2015.
   CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Agosti 29 kimezindua kampeni zake katika viwanja vya Jangwani Jijini Dar es Salaam. Katika uzinduzi huo viongozi kadhaa wa Chama  hicho wakiwemo na waliokuwa Mawaziri waandamizi katika Setikali ya CCM, Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye, Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Ufisadi, Edward Lowassa pamoja na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Lawrance Masha wakihutubia mkutano huo.

  Ni jambo la kushangaza kumsikia mgombea wa nafasi ya  Urais kupitia CHADEMA, Edward Lowassa akihemewa na Kujikuta  akishindwa kuikabili hadhira ya Watanzania wanaofikia milioni 45  kuwaelezea ana malengo gani ya urais, Chama chake kina dira na sera zipi za msingi, pia akizungumza bila kuonyesha mtiririko  wa sera kusudiwa  kama muongozo wa uendeshaji Serikali ukikosa kuainishwa kwenye kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho.

  Kwa msingi huo, CHADEMA/UKAWA wameonesha jinsi gani wasivyo na maandalizi ya mkakati wa kitaalam na mipango endelevu kwa maendeleo ya kisekta katika dhamira ya kujenga uchumi imara utakaoimarisha huduma za jamii, kuheshimu misingi ya utawala bora wa sheria huku akionesha kukosa dira makini ikiwemo  mipango ya muda mfupi na muda mrefu ya Serikali yao ikiwa itatokea muujizq wa wa kushinda na kujikuta  wakitaja  changamoto zinazozikabili nchi nyingi zinazoendelea.

  Mgombea wa CHADEMA Lowassa ni dhahiri ameshindwa uchaguzi mkuu mapema, amebakia akilalama, kupiga soga na kujenga matumaini hewa kwa Watanzania huku akishindwa kujua ni changamoto zipi za msingi zinazowakabili wananchi katika maisha ya kila siku na hatimaye atoe majawabu mbadala ya utatuzi wa msingi unaoweza kuaminiwa na wananchi wanaoishi aidha mijini au  vijijini.

  Lowassa ameshindwa kabisa kukonga nyoyo na kugusa hisia za Watanzania katika mambo ya msingi kwa sababu ya kuandamwa kwake na pupa, kiherehere na kukurupuka toka Chama kimoja hadi kingine huku akiwa hana maandalizi yanayoweza kutoa majibu halisi yanayowakabili wafanyakazi, wakulima, wavuvi, wafugaji, walimu, madaktari, wauguzi pia wasanii na wanamichezo.

  Lowassa na CHADEMA, wameshindwa kubainisha dhamira na maandalizi ya kuleta chachu ya maendeleo mbadala kwa sababu sehemu kubwa ya changamoto zilizokuwepo zimetatuliwa hatua kwa hatua kwa kipindi cha miaka kumi iliopita chini  uongozi wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambapo sasa mashirika ya Kimataifa ya kusimamia uchumi na fedha ikiitaja Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo uchumi wake unakua kwa kasi kuelekea uchumi wa kati.

  Sisi UVCCM, tulitegemea sana kuona labda  ile shauku , mikiki , hamu na kiu alionayo Lowassa ya kutamani Urais kwa gharama yoyote huenda angekuwaa na mikakati. , sera au mipango mipya ya kushughulikia matatizo yaliyobaki ambayo aidha yamekawia kiutekekezaji kwa ukosefu wa fedha  au utatuzi wa matatizo hayo miradi husika imeanzishwa na kutofikiwa suluhisho kwa wakati au baadhi ya viongozi waliopewa dhamana hizo kushindwa kutekeleza kwa muda na wakati muafaka.

  Hotuba ya Lowassa kuhusu azma na dhamira yake katika kukuza uchumi, UVCCM tunaifananisha na orodha ya manunuzi (shop list) maana haioneshi viashiria , njia au vyanzo vya mapato ya kukuza uchumi kwa mwendo haraka wa kisera na kujikuta akipiga porojo akifanana na kasuku aliyekariri maneno aliyofundishwa  akiyatumia bila kujuwa tija , faida, hasara na maana ya jambo analolikusudia.

  Tumeshangaa kumuona akishindwa kuzungumzia masuala ya ufisadi na kutowataja wezi waliopora rasilimali za umma na maliasili za nchi, waliofuja uchumi, wala rushwa watu waliokosa kuwajibika  na kutochukuliwa  hatua za kisheria kwa masuala mazima ya kukiuka maadili ya uongozi ikiwemo sakata zito za mradi wa kufua umeme wa dharura kupitia kampuni hewa ya RICHMOND ambayo ilimsababishia Lowassa kulazimishwa na Bunge ajiuzulu Uwaziri Mkuu akiwa ni Waziri Mkuu aliyekaa muda mfupi zaidi kuliko yeyote katika historia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  UVCCM tunachukua nafasi hii kuwaasa na kuwaomba sana Watanzania wenzetu kwamba mabadiliko au mageuzi ya kiuchumi na kisiasa hayahitaji pupa na papara kama iliyotokea kwa  wananchi wa Taifa la Libya ambao sasa wako katika dimbwi la majuto.

  Viongozi wa Upinzani akiwemo Lowassa na kundi la UKAWA hawana dhamira njema kwa nchi yetu na UVCCM  tunawafanisha sawa na manahodha ambao muda mfupi ujao toka sasa watagombea sukani wakiwa katika kina kirefu cha bahari jambo ambalo ni hatarishi kwa maisha na mustakabali wa wasafri waliomo kwenye chombo chenye amani, utulivu, umoja, upendo na mshikamano wa kitaifa kinachoitwa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Lowassa ameonyesha dalili za kuwa kiongozi dikteta asiyeheshimu hata misingi ya utawala bora hasa pale aliporejea kwa mara ya pili akisisitiza msimamo wake wa kuwaachia huru Masheikh wanaokabiliwa na tuhuma za makosa ya ugaidi ambapo suala hilo sasa lipo mbele ya mahakama na hatutakiwi kuingilia mwenendo wa kesi kulingana na matakwa ya mgawanyo wa madaraka kati ya mihimili ya dola.

  Mbali na suala hilo, pia ameonekana  kulizungumzia suala ambalo tayari mahakama ya juu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limekwisha litolea hukumu kesi ya Mwanamuziki Nguza Viking na mwanawe Papii Kocha waliohukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya ubakaji kana kwamba Lowassa anaona vyombo vya sheria vimewaonea na kuwakandamiza.

  Ifahamike kati ya makosa ambayo yameainishwa katika sheria za Tanzania, kosa la ubakaji halina msamaha.

  Aidha, Lowassa na UKAWA wameonekana kuzungumzia sana dhana ya uzalendo wakati mfumo utokanao na itikadi ya Chama chao imejiegemea katika uliberali usiojali wala  uzalendo zaidi ya kuthamini utajiri binafsi, kujilimbikizia mali zisizo na vyanzo na uvukaji wa mipaka isiyozingatia mila, desturi na utamaduni.

  UVCCM tumeshangazwa sana na ujasiri uchwara ulionyeshwa na Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye anapothubutu kuzungumzia ufisadi wakati yeye mwenyewe ni miongoni mwa viongozi wanaotuhumiwa kwa kashfa ya uanzishaji wa Televesheni ya Taifa {TVT} na ufufuaji wa fedha za umma , soko la Kibaigwa, tuhuma ya uporaji  ardhi huko Tondoloni akitumia madaraka yake vibaya pia chini ya  usimamizi wake akiwa mtendaji mkuu wa Serikali, halmamshauri nyingi za wilaya nchini ziliongoza kupata hati chafu kutokana na  matumizi holela ya ruzuku toka serikali kuu kama ilivyofichuliwa  na ofisi ya CAG kufuatia upotevu wa fedha za miradi ya maendeleo ya jamii.

  Sumaye kinywa chake wakati mmoja kikitoa moto na baridi ndiye aliyekitaka Chama cha Mapinduzi kutompitisha Lowassa kuwa mgombea  urais kwa madai ya kuhusika kwake na tuhuma za ufisadi huku akitishia kuhama CCM. Matamshi ya Sumaye yameushangaza ulimwengu na sasa anapopania kumsafisha Lowasa kwa kutumia maji taka akifikiri atasafika  ili aaminiwe na watanzania  werevu na wazalendo ajijue fika anatwanga maji kwenye kinu. 
   
  SHAKA HAMDU SHAKA (MNEC)
  KAIMU KATIBU MKUU UVCCM TANZANIA

older | 1 | .... | 623 | 624 | (Page 625) | 626 | 627 | .... | 1896 | newer